IMEANDIKWA NA : YONA FUNDI
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Pole ndugu Salimu utapona kuugua si mwisho wa maisha hichi nikipindi cha mpito tu ndugu. Yakupaswa uwe mvumilivu usijikatie tamaa utapona hakuna kinachoshindikana mbele ya Mungu yupo, pamoja nasi hayupo mbali na mahali hapa”. Alinyamaza kidogo mtu yule aliyekuwa akiyazungumza yale mavazi yake tosha yalionesha yu mfanyakazi wa hospitali ile ambayo ndugu Salimu alipokuwa anapatiwa matibabu.
“Ndugu Salimu” kwa upole daktari yule aliendelea kuzungumza.“Unawaona watu hawa wamekuja kama ulivyotuagiza ombi lako tumelifanyia kazi. Unao waona mbele yako ni Waandishi wamekuja kusikiliza kama ulivyotuagiza unajambo unataka kuawambia ili Jamii iweze kutambua ulicho nacho ndani ya kichwa chako”.
Nilijisogeza vyema baada ya maneno ya yule Daktari kuelekea karibu na kitanda ambacho ndugu Salimu alipokuwa amejilaza.
Kiukweli muonekano wake tu ulitosha vyema kufahamu hakuwa katika hali ya nzuri hata kidogo mwili ulikuwa umepungua sana, si kawaida kama binadamu wengine. Hali ile ilitisha machoni mwangu si mimi tu hata Mwandishi mwenzangu bwana Arifu. Hali ile ilimtisha niliona wazi wazi. Taratibu huku macho yangu ya kikodoa kwenye kitanda kile katika chumba kile cha hospitali ile ya Bombo.
Kwa mboni yangu niliweza kukadiria umri wa ndugu yule miaka ishirini na miwili ndio ilikuwa nikiona halali yake. Kiukweli alikuwa bado kijana haswa lakini alibaki kichwa tu. Tofauti na hivyo mboni zangu ziliweza kubaini uzuri wa kijana yule, hakika ugonjwa ule ndio ulipoteza naskhi na urembo wa kijana yule. "Masikini Mungu kijana yule alikuwa amekosa nini" Nilijikuta maneno yale yanapita ndani ya kichwa changu huku uchungu ukiwa umenishika kuona kizazi kama kile kinapotea hivi hivi.
Kimya kilitawala eneo lile ambapo pembeni ya kitanda cha ndugu yule kulikuwa na kiredio kidogo ambacho kilikuwa kinapitisha sauti ya mziki wa taratibu kumliwaza ndugu yule.
Ni kiwa pamoja na ndugu Arifu Azizi Shebe moja kati ya Waandishi ambao wanafanya vizuri kwenye chombo chetu cha habari. Hapo tuliweka vifaa vyetu sawa kwa jili ya kupata kile ambacho ndugu Salimu alikuwa anataka kutupatia sisi kama, Waandishi wa habari ili tukifikishe katika Jamiii. Maana ndio kazi yetu kuijuza Jamii juu ya mambo mbali mbali ikiwemo mikasa kama hii ya ki maisha.
"Hali yako ndugu Salimu" kwa unyonge na sauti ya chini ndugu yule aliitikia lakini alionekana kupata shida sana hata kuzungumza kwake kulikuwa kwa shida shida tu.
Punde tu ilifatiwa na sauti ya bwana Arifu Azizi "pole sana ndugu" Wakati huo tiyari tulishaweka vyema vinasa sauti pamoja na note book zetu. Kupata vyema kile alichopanga kuzungumza na nasi ndugu Salimu kwa faida ya Jamii nzima. Kiukweli haukuwa mkasa wa kawaida ndugu msomaji wa mkasa huu jaribu kuwa makini mwanzo hadi mwisho na kuvuta taswira ya jambo hili si mzaa hata kidogo ya kupaswa ujue.
Ndani ya mkasa huu maana ulikuwa ni zaidi ya mkasa niliyowahi kuisikia tangia nianze kazi hii ya uwaandishi.
Mwanzoni tulipata tabu sana kuisikia sauti ya ndugu Salimu ila baada ya muda kidogo tuliweza kumsikia vyema kile alichokuwa anakitoa ndani ya kinywa chake.
"Naomba mnisikilize kwa makini ndugu zangu haya ninayoongea ni muhimu sana ni vyema mkaya chukua kwa makini nisemavyo ili Jamii na haswa vijana kama mimi watambue" ndio yalikuwa maneno ya ndugu yule. Yaliyo tufanya tuvute umakini juu ya jambo.
Naikumbuka vizuri siku ile maisha yangu yalipoanza kubadilika hakika sitoisahau katika hii Dunia siku ile.
Nakumbuka Usiku wa siku ule ulikuwa mrefu sana sikuamini kama kesho itafika kama siku zingine. Nililala kwa kustuka stuka usiku kucha. Hakika usiku ule ulikuwa mrefu sikujua sababu au ndio siku pekee ya kwenda kuanza maisha mpya ya chuo, ambayo kwangu yalikuwa mageni nilizoea tu kuyasikia tu.
Kuwa maisha ya chuo bwana ya na raha asikuambie mtu muda wote huko huru mambo yale yalikuwa ni kivutio kikubwa kwangu.
Kwa sababu nilikuwa nikibanwa kama mtoto wa kike nakumbuka siku moja nilivyochelewa kurudi shule balaha nilikutana nalo Nyumbani lilikuwa si dogo Mzee aliongea sana huku nikinusurika kipigo. Kama asingekuwa Mama sijui ingekuwaje hivyo Mzee hakuwa na masihara hata kidogo afadhari ya Mama lakini Mzee alikuwa kavu sana. Kwa ujumla maisha yangu ndani ya jii la Tanga ambapo nilikuwa ni kiishi yalikuwa ya namna ile, hakuna ujinga hata kidogo hata sikukuu si kuwa naruhusiwa kutoka mimi na kitabu, kitabu na mimi mpaka kieleweke.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hivyo kufaulu kwangu katika masomo yangu ya mwisho katika elimu ya sekondari niliamini sasa uhuru wangu nitakuwa nimeupata kutoka ndani ya kifungo hiko.Tangia hapo nilikuwa na pambana sana ili na mimi ni faulu na sikupenda kabisa kusoma pale ndani ya jiji la Tanga ndoto yangu ilikuwa kusoma Mzumbe ndani ya mkoa wa Morogoro. Mji ambao kwa mara ya kwanza niliufahamu tulivyoendaga kisafari cha utalii pindi nilipokuwa kidato cha pili katika mbuga ya mikumi. Kiukweli nilivutiwa sana tamaa ya kutaka kurudi tena ndani ya mkoa ule ilikuwa inaishi kwenye kichwa changu.
Lakini ndoto ile hatimaye ilitimia hapo ndipo maisha yangu yalipoanza kuingia dosari.
First year ndio chanzo cha yote haya ndugu Waandishi tupo sawa mnanisikiliza kwa makini alitupia swali ndugu yule.
Hatukutia neno tulichofanya mimi na mwenzangu kuitikia tu kwa vichwa huku ndugu Salimu akiendelea kusimulia.,
Hivyo hata pale nilipopata usingizi nilijikuta ni kiamka mapema kuliko kawaida safari yenyewe ilikuwa ni saa mbili. Nilivyonyanyua vyema saa yangu ambayo nilikuwa nimeiweka pembeni kidogo ya kitanda changu ilionesha vizuri kumi na moja kasoro mishale ile ndani ya saa niliona ikitoa taarifa juu ya muda haswa loo!. Hata hamu ya kulala tena ilipotea niliamka na kuanza kujiandaa taratibu mpaka kigiza kilianza kupotea hatimaye kumi na mbili ilitimia. Wakati bado naendelea kuweka mambo sawa nilisikia mlango wa chumbani kwangu unagogwa ngo! Ngo! Ngo! kwa sekunde kadhaa nilienda kufungua mlango.
Kufungua kule kuliendana sambamba na taswira ya Baba "za asubuhi Salimu mwanangu" maneno yale yalipita vyema ndani ya masikio yangu nilimjibu "safi tu" na kufatiwa na "shikamoo" na upande wake, Baba alitikia vizuri salamu ile na kumtaka nimsikilize kidogo kabla yeye ajaenda kazini kama kawaida yake.
"Sikia mwanangu Salimu unajua wazi leo ni siku yako ambayo unaenda kuanza maisha mpya mwanangu japo hapo nyuma kidogo nilizungumza na wewe ila leo nataka nikukumbushie tu. Mwanangu maisha unayoyaenda kuyaanza yana changamoto kubwa unatakiwa upambane nayo unaenda chuo kusoma si vingine ilo Baba tambua hivyo kuwa makini kaa mbali na makundi kila mtu anatabia yake huko mwanangu unapoenda akili kichwani mwako".
Mzee alifumba funda moja la mate nakuendelea "haswa kaa mbali na marafiki wabaya tafuta mtu mtakuwa mnaendana kiitikadi nataka utukomboe wewe ndio mkombozi wetu katika maisha yetu ya baadae". Niliendelea kumsikiliza Mzee kwa makini sana alichokuwa anakiongea sikutaka kutia neno mpaka pale nilipoona amemaliza kuongea". Baba nimekuelewa sana Mzee wangu nakuahidi nitaenda kufanya vyema nitasoma nalitambiua hilo, nahitaji siku moja na mimi niwe moja ya viongozi katika nchi hii sitoweza kwenda kinyume na hicho Mzee wangu ondoa shaka kabisa naomba unipe baraka zote Mzee wangu.
Maneno yale yalimwingia vizuri Mzee niliona vyema kupitia mboni za macho yangu. Hivyo kutokana Mzee kuniamini hakuwa na hiyana wala akutaka kuongeza neno zaidi ya kunitakia safari njema na yeye kuondoka kuelekea kazini kama kawaida yake.
Muda mfupi baada Baba kuondoka nilisikia sauti ya Mama akiniita
"Salimu!!! Salimu!!! mwanangu jiandae unywe chai kabisa kabla haujaondoka si unajua tena safari hatua mwanangu”. Maneno yale ya Mama yalipenya vizuri kwenye ngome za masikio yangu kunifanya nimwitikie Mama. Kabla ya dakika chache kutoka chumbani kwangu na kwenda jikoni bahati nzuri chai ilikuwepo kwenye chupa hivyo nikachukua mikate kabatini nikaanza kupata kifungua kinywa wakati huo Mama alikuwa yu chumbani kwake akijiandaa kwa jili ya kunisindikiza stendi. Nilikunywa chai haraka haraka hata sikula vizuri nilijihisi nimeshiba.
Hapo tiyari Mama nilimkuta yupo sebuleni akinisubili nilimpa salamu kama kawaida nikaelekea chumbani kwangu kuchukua mizigo yangu,ambayo ilikuwa ya kawaida tu begi la nguo na vifaa vichache tu si kuwa na mizigo mikubwa kihivyo.
Safari ya kwenda stendi ilianza ikiwa saa moja na dakika kumi tu saa yangu ilionyesha kama baada ya nusu saa tulifika maeneo ya stendi. Hatukuchelewa sana kwa sababu basi lilikuwa linatoka pale stendi sa mbili na nusu. Hivyo kufika tu Mama alienda kunikatia tiketi haraka katika kampuni ya mabasi ya Simba Mtoto.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni moja kati ya mabasi maarufu katika safari za Morogoro na Tanga. Nikiwa hapo nilishuhudia kituko kimoja jamani stendi kuna mambo ya ajabu sana.
Sijui wale wahuni walivyokuwa wakimgombania yule Mzee. Ambaye alionekana kama mshamba hivi karibu kutaka kimwangusha Mzee wa watu tukio lile lilinistajabisha sana nikabaki tu nacheka mwenyewe. Kabla Mama kurudi eneo lile ambalo hakuchukua muda sana hatimaye alirudi mahali pale nilipo huku akiwa ameshika karatasi ambayo ndio ilikuwa tiketi na kunikabidhi. Niliangalia ilionesha kuwa natakiwa kukaa siti namba kumi hivyo kitendo cha Mama kunikabidhi tiketi ile kilifatiwa na Maneno ya kunitakia safari njema. "Mwanangu Salimu nakutakia safari njema Baba uwende salama mwanangu” Maneno ya Mama yaliningia kiukweli roho iliniuma licha ya kufurahia safari ile ila kuachana na Mama nalo lilikuwa tatizo kiukweli nilimzoea vibaya kibaya zaidi maneno yale ya Mama yalionekana wazi kuwa yalibeba hisia kali ndani yake.
Nilimwitikia Mama wakati huo tiyari nishaanza kupandisha ngazi kuelekea mahali nilipotakiwa kukaa kwa jili ya safari ile ndani ya basi lile niliangalia vizuri tiketi yangu kujilizisha namba ile ya siti hivyo taratibu nilianza kukatiza huku nikihesabu siti zile. Nilijua wazi haikuwa mbali kutoka mwanzoni mwa basi lile hatimaye nilifahamu mahali nilipotakiwa kukaa kwa bahati nzuri upande ule ambapo ulikuwa unasiti mbili.Yani namba kumi na moja na namba kumi, ambayo nilitakiwa nikae mimi hakukuwa na mtu hivyo nilifika na kuweka mizigo yangu vizuri nikasogea upande ule wa dirishani kwenye moja ya siti zile niliona panapo nifaa.
Wakati huo muda ulikuwa umebaki mchache tuweze kutoka pale nikiangalia upande zote zilikuwa zimekaliwa watu upande wangu tu kulikuwa hakuna abiria ambaye alitakiwa akae pamoja na mimi, kama zilivyo siti zingine ndani ya basi lile. Nikatulia tuli huku nikiwa nimeinamisha kichwa changu nikifikiria jambo mara nilisikia sauti kali ikipenya kwenye masikio yangu ilikuwa ni sauti ya kike kabisa hata kabla si jainua macho yangu niliweza kufahamu.
"Samahani kaka naomba nikae siti yangu ya dirishani tiketi yangu inaonesha natakiwa nikae dirishani kaka ila samahani kwa hilo." Hata kujibu nilishindwa nikibaki nashangaa tu uzuri wa yule dada. Haki Mungu alimpatia kila kitu si sauti bali kila kitu sura nzuri iliyosanifiwa na rangi yake yake ilitosha vyema kusadifu uzuri wa dada yule.
Macho yalibaki tu yakitumbua niliona kama nipo kwenye maonesho ya fashion la hasha nilikuwa kwenye siti ile ya basi. Hivyo nilipisha taratibu hata mdomo wangu ulikuwa mzito kufumbua mbele ya yule mdada. Nilishindwa hata kutamka kitu nilikuwa kama nimepigwa ganzi ganzi gani kwenye changu kinywa.
Uwiii .. aiseehe!, Ilikuwa balaha kabisa maisha yangu yote nilikuwa mbali sana na wasichana niliwaogopa japo nilikuwa nikisikia wakinisifia mimi mzuri tena handsome. Ila nilikuwa sina mazoea nao hata kidogo hivyo ule kwangu ulikuwa mtihani tena mkubwa katika safari ile.
Nilitulia kimya huku hata sikujua nitaanzaje? hata kumpa salamu yule dada. Wakati mimi nikiwa nafikiria nilisikia sauti ya yule dada ikipenya tena kwa mara nyingine masikioni mwangu." Kaka mambo vipi” huku nikiwa natetemeka nilishangaa tu na mimi baada ya kujibu “powa au fresh” nilijikuta najibu “mambo.” Ila kwa bahati nzuri yule dada hakusikia vizuri maana aliendelea, kuniongelesha nilishanga tu akiniangalia sana usoni kadiri alivyokuwa akitoa neno kwenye kinywa chake. Kwasababu nilikuwa muoga hivyo yeye alikuwa muongeaji tu mimi nikiwa natingisha tu kichwa huku nikijibu kwa kifupi. Maswali aliyekuwa akinitupia ndani ya mazungumzo yake.
Wakati huo tulishaanza kuaviacha vijiji mbali mbali vya mkoa wa Tanga huku mwendo wa dereva ukionekana kuwa wa kistarabu. Kwasababu alikuwa yuko vizuri kufatiria taratibu zote za uendeshaji barabarani, kwenye kutakiwa kukimbia alikuwa ana kimbia kwenye kutakiwa kutembea kwa mwendo wa kawaida pia alifanya hivyo. Kiukweli kwa upande wangu nilipenda namna dereva yule alivyokuwa akiliendesha basi lile.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulizidi kuviacha vijiji vya mkoa wa Tanga huko namna muda ulivyokuwa unaenda na hatimaye mimi nilianza kumzoea yule dada. Ukweli alikuwa mcheshi usheshi ule nilitamani muda wote ni msikie akizungumza na mimi nilikuwa nikiona raha ajabu mithiri uwapo kwenye bembea. Unafanya mtindo ule wa juu chini ilimradi ulete radha tu ndani ya mwili wako. Basi kwangu hata sikujua hali ile inatokea wapi? bali moyo wangu ulikuwa ukifalijika kila yule dada akinitupia swali. Hata pale muda alipokuwa akisinzia nilitamani nimwamshe tu aendelee kuzungumza na mimi. Sauti yake ilikuwa kama kinanda ndani ya masikio yangu muda wote nilitamani hata safari tusifike haraka niendele tu kukaa na yule mdada.
Sijui kwanini? si kuwa na mazoea na watoto wa kike lakini siku ile nilihisi kuwa nilikuwa nikikosa vingi kutoka kwa watu wa jinsia ile. Hata nilianza kumkumbuka Aziza msichana ambaye alikuwa akinipenda ila hata si kuwa na habari naye. Japo shule nzima yeye alikuwa anakikimbiza kwa uzuri mbele ya wasichana wote. Wavulana wengi walikuwa wakimshoboke ila kwangu haikuwahi kutokea kiukweli nakumbuka vyema nilivyomsemea mbovu kwa ile tabia yake ya kunigusa gusa.
Nilihisi nilikuwa na kosa kitu “kumbe wasichana wana maneno matamu kama hivi” nilijisemea mwenyewe kimoyo moyo tu.
Basi lilizidi kuchanja mbuga na hatimaye tuliingia mkoa wa Pwani na kuacha mkoa wa Tanga. Hapo kidogo dereva alipunguza mwendo na gari liliacha njia ile kubwa na kuingia kwenye hoteli moja. Nilifahamu vyema kuwa tulitakiwa tupate vyakula kidogo kabla hatujaendelea na safari. Wakati huo tiyari nilifahamu jina la yule dada, kutokana alikuwa amepitiwa na usingizi nilimgusa na kumtingisha ili amke “Shufaa! Shufaa! amka sister” Maneno yale yalinitoka huku yakifatiwa na mguso wa mikono yangu kwenye mwili wake.
Mmh!, ule mguso nilijisikia raha nikitamani hata kumgusa tena ila alikuwa yu tayari ameshamka na kufahamu. Tulikuwa tunatakaiwa kufanya nini? abiria wote wa basi lile hivyo tulishuka wote na hata tulielekea wote mule hotelini. Muda mfupi tu nilikuwa tiyari nimezoea hali sikuwa na muogopa tena kama mwanzoni. Tulingia ndani mule na kuagiza chakula taratibu tuliendelea kula namna tulivyokuwa tunakula yule dada alikuwa akiniangalia vibaya hata sikujua anawaza nini?. Niliendelea kula sikuwa na wasi wasi wakati tunaendele kula yule dada alinuliza swali. Haki lile swali lilikuwa geni masikoni mwangu na sikutegemea kama hataniuliza swali kama lile. Sikujua nini? kimemsukuma kuniuliza kitu kama kile.
“Salimu unaonekana handsome sana vipi una mchumba wewe yaani na maanisha girl friend hivi.” Swali lile liniingia vyema nilibaki nikimtazama tu sikutegemea kabisa ndugu Waandishi. Labda niwaambie kitu maisha yangu yote sikuwahi kusikia habari za wachumba sijui? girl friend.Masuala hayo kwangu yalikuwa mbali sana na hata mtu akiwa anaongelea mambo hayo kwa upande wangu namchukulia mtu wa ajabu. Tena mtu aliyekosa busara mbele yangu kwa umri wangu mambo yale yalikuwa hayanihusu. Sistahili kabisa kuyazunguza kutokana tu na misingi ambayo niliyokuwa nikilelewa na wazazi wangu. Na hata hivyo umri wangu nilikuwa na ona bado kabisa kufaa kuzungumza jambo lile.
Hivyo nilipigwa na butwaa hata cha kujibu sikuwa nacho namna ambavyo nilivyokuwa tu yule dada aliweza kunisoma. Grafla tu niliona mdomo wake ukinyanyuka na kuzungumza jambo “Usijali Salimu nafikiri hukutegemea kuulizwa swali kama hilo any way fanya tumalize haraka naona muda umebaki mchache. Abiria wenzetu wanarudi kwenye basi hata hivyo mimi nimeshiba nakusubili umalize tuondoke|”
Nilishangaa hata sikujua tulivyozoena grafla vile kiukweli dada yule alikuwa mchechi sana ndugu Waandishi. Niliona kama tumekutana siku nyingi zilizopita la hasha kumbe siku ile ya safari. Nilikula haraka haraka kutokana na njaa niliyokuwa nayo, nalikumbuka asubuhi sikunywa chai vizuri kutokana na kihoro cha safari. Hivyo fursa ile sikutaka kuichezea kabisa nilipakia tumbo langu ndindi na kuhakisha nimetosheka. Baada ya kumaliza chakula mfanyakazi wa hoteli ile alikuja kuchukua malipo ila kabla hata sijatoa pesa kulipia yule dada alilipia. Alikuwa anapesa nyingi, vile alivyokuwa anatoa kwenye pochi nyekundu nyekundu tu zilikuwa zimejaa. Alitoa nyekundu mbili na kulipia nilisikia tu akimwambia muhudumu eti "keep change "
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo mimi tiyari nilikuwa nimenyanyuka, nikimshukuru yule dada sikutegemea hali ile niliyiona. “Yaani duniani kuna watu wanatabia nzuri na kama ninge pata fursa ya kuongea na Mungu basi ningemwambia angeumba viumbe vyote mithili ya huyu dada. Mwenye jina la Shufaa” nilijikuta nikijiseme kabla ya kumwongezea sifa zingine. Alibalikiwa kila kitu roho nzuri mchechi mshangamfu anavutia mbele ya macho ya kila amtazamaye hata sita kugeuza shingo yake kuungalia mara mbili mbili. Uzuri wa yule dada kiukweli licha ya uzuri wangu nilikuwa najiona sifanani kabisa kuongozana nae kabisa huyo ndio alikuwa Shufaa.
Tulipiga hatua kuelekea kwenye basi ambapo baadhi ya abiria walikuwa tiyari wamesharudi. Ilikuweza kuendelea na safari yetu. Dakika kadhaa tulifika kwenye siti zetu muda mchache tu baada ya kukaa dereva aliwasha gari kuendelea na safari. Hapo tiyari hata usingizi haukuwepo tena si mimi wala Shufaa mazungumzo tu yalitawala. Kwa upande wangu mimi sikuwa mzungumzaji mkubwa maswali yalikuwa kama njugu yanakuja upande wangu.Huku macho ya yule dada ya kiwa yameganda kuniangalia mimi kila anapo niswalika swali.
Naweza kusema kitu ndugu Waandishi hapa maswali ya yule mdada kiukweli yalionekana wazi wazi kunakitu alikuwa anakitafuta kutoka kwangu kabisa.
SURA YA TATU
Maana hayakuwa maswali ya kawaida yalikuwa yamejengwa kujua undani wangu kabisa. Wakati huo mimi nilikuwa muwazi tu kwake sikuwa na mficha chochote alichokuwa anakiuliza kwangu niliona kawaida. Na hata hivyo swali lake la kuwa eti mimi handsome ninamchumba, muda fulani alirudia tena nikaona isiwe tabu nilimjibu. Hakujua mwenzake mimi nilikuwa "bikra" wakiume ya kwamba siwajui Wanawake hata kidogo. Na kama angelijua hilo sidhani kama angeniuliza ndani ya kinywa chake. Tuliendelea kuzungumza ,nalo basi ilizidi kupunguza umbali wa kutoka Tanga kuelekea Morogoro. Ijapo kuwa Morogoro nilikuwa mgeni ila nilifahamu vyema ya kuwa karibia tunafika katika mkoa huo. Nilitazama saa yangu kwa mara nyingine saa saba na dakika sita ilinionesha kwenye mboni za macho yangu, hapo sasa nilijua wazi tunakaribia kufika ndani ya
Morogoro.
Huku mazungumzo yale yalionekana kunogea na dada yule na alisha anza kunimbia maisha ya Mzumbe yalivyo. Yaani kwa upande wangu nilijiona kama nina bahati sana kukaa na mtu ambaye anapafahamu vizuri kule ninapotakiwa kwenda. Alinipa maelekezo jinsi gani ya kufika kule kiukweli nilimshukuru sana. Kwa upande wake aliniambia kuwa sasa yeye anakaa kihonda pale pale mjini na ameolewa na mfanya biashara maarufu ndani ya mkoa wa ule. Punde tu alipomaliza chuo, na Tanga ni kwa wazazi wake. Hivyo alienda mara moja kuwa salimu. Mazungumzo hayakuishia hapo hadi tunaingia ndani ya mkoa wa Morogoro. Tulikuwa tunaongea sisi tu na hata alinipatia namba yake na kuchukua ya kwangu. Kwa jili ya mawasiliano alisitiza nimtafute maana tumeshakuwa ndugu muda mfupi tu alieleza hivyo.
Nilingalia saa yangu tena saa nane na nusu tu ilinionesha kwa mara nyingine wakati huo tiyari tulikuwa tumeshaingia ndani ya mkoa wa Morogoro.Wakati dereva akiweka sawa basi lake ilituweze kushuka macho yangu yalikuwa yakishangaa shangaa bughudha za watu wa stendi ile. Ndani ya mkoa wa Morogoro, nikiendelea kushaanga mahali pale haki niliona kitu kilichonifanya nisiamini kama dunia kuna watu nyie hiiiii!.Wamebalikiwa na Mungu sikuwahi kuona gari kama lile “live live”(ana kwa ana) nishazoea kuona kwenye tv tu leo live live mkoani Morogoro. Hakika kumbe Tanzania hii watu wana pesa namna hii.
Wakati na shangaa kabla hata sijasema neno tiari abilia walishaanza kunyanyuka kwenye siti zao. Hivyo kwa upande wangu mimi sikuwa na haraka kabisa. Ugeni wangu ulinifanya niwe mpole tu huku nikiendelea kusaficha macho katika kila pembe mbele ya lile gari ambalo lilikuwa la kifahari haswa. Simu ya yule dada ilianza kuita tena dakika tu alipokea na kuanza kuzungumza kwa sekunde kadhaa alafu alikata na kunigeukia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Salimu nakutakia safari njema ufike salama huko. Hapa na mzumbe kama nilivyokueleza mwanzo si mbali nusu saa tu utakuwa umefika naimani Mungu atakuongoza. Ila cha msingi usisahau kunitafuta Salimu. Nimekupenda sana kaka wewe ni mkalimu sana “ Shufaa aliongea yale maneno huku akiniachia tabasamu mwanana ndani ya taswira ya uso wake.
Kiukweli alikuwa hakipendeza sana sura yake ilikuwa ikivutia nilitamani niendelee kumwangalia tu ila haikuwa hivyo. Taratibu alianza kushuka huku mimi nikiwa nyuma na mizigo yangu mpaka chini ya basi. Alinipungia tu mkono kuonesha ishara ya kuniaga macho yangu yalikuwa yakimsindikiza.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment