Search This Blog

Friday, July 15, 2022

KIFO CHA MARRY - 4

 







    Simulizi : Kifo Cha Marry

    Sehemu Ya Nne (4)



    Siku illyokuwa inasuburwa kwa hamu iliwadia. Watu wengi walihudhuria kwenye kesi ya mtunzi mashuhuri Sira juu ya kuhusika kwa mauaji ya mfanya biashara mkubwa Kenedy.



    Mashahidi waliletwa na kutoa ushuhuda wao. Alikuwepo kijana mmoja ambaye alikua mtuhumiwa wa mauaji hayo aliyekuja kutoa ushahidi wa kutumwa na Sira kufanya hivyo na kulipwa kiasi cha pesa.



    Mpaka kufikia hapo Sira hakua na la kujitetea zaidi ya kumwaga machozi hadharani hata kabla hajahukumiwa.

    “una lolote la kujitetea kabla ya hukumu?” hilo swali lilimgutusha Sira kutoka kwenye dimbwi la machozi. Alinyanyua sura na kuutazama umati wa watu waliokuwa pale na kumtazama Anna ambaye alikua analia wakati wote wa kesi ile.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “naomba unisamehe Anna, si mimi niliyeamua kutenda haya. Bali ni nguvu ya mapenzi iliyonielemea juu yako. Nilijua kua tunaweza tukawa pamoja kwa kitendo kile tu kwakua nakupenda na tayari kuna mtu mwingine anakumiliki moja kwa moja. Nakupenda Anna ila sheria ndio inatutenganisha. Nitafurahi zaidi kama utanisamehe japokuwa huwezi kunitoa kwenye kesi hii ngumu inayonikabili…ni hayo tu ndugu hakimu.”



    Maelezo hayo yalimfanya Anna na wengine kuamini kuwa ni kweli Sira alihusika kiasi kikubwa na mauaji ya Kenedy kwa sababu ya mapenzi.

    Hakimu aliongea mengi ikiwemo kukumbushia baadhi ya kesi zinzzifanana na hizo na kutoa hukumu iliyowaacha watu vinywa wazi.

    “umehukumiwa kifungo cha maisha.”

    Alimaliza hakimu na kugonga nyundo mezani.



    Baada ya hukumu hiyo, yaliwatoka machozi wengi walihudhuria pale mahakamani. Hadithi zake za kusisimua zilikua zimekomea hapo. Hakutofautiana na mtu aliyekufa kwa jinsi alivyoliliwa na raia wengi waliokuwa mashabiki wake.



    Maisha ya ubachelour yalichukua nafasi yake kwa Anna ambaye starehe yake ilikua club na kumbi mbali mbali za starehe.

    Alianza kunywa pombe kali huku akiwakataa vibopa vilivyojitokeza kuomba hifadhi kwake.



    Siku moja akiwa kwenye hotel kubwa maeneo ya posta, alikuja mzungu mmoja mwenye asili ya kijerumani na kumfata pale alipokaa wakati akimsubiri muhudumu ili ampe oda yake.



    “good evening” alisalimia yule mzungu na kutabasamu baada ya kumuangalia Anna vizuri.

    Anna alimuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akaitikia ile salamu. Baada ya Anna kuitikia ile salamu yule mzungu aliendelea kumsemesha.



    “can I seat with you?” aliuliza yule mzungu huku akiwa ameshikilia kiti kilichokuwepo mbele ya Anna.

    “yes, you can.” Alijibu Anna na yule mzungu akavuta kiti na kukaa. Bila kupoteza muda yule mzungu akajitambulisha.

    “my name is Augustino… and you?” aliuliza yule mzungu baada ya kujitambulisha.

    “ Anna.” Alijibu Anna kifupi huku akimuangalia yule mzungu kwa pozi za kibantu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “good evening”

    Hiyo ilikua salamu ya muhudumu baada ya kuwafikia Anna na yule mzungu pale kwenye meza yao. Waliitikia kwa pamoja na Augustino alikuwa wakwanza kuagiza.

    “bring to us some food as ordered by this lady”

    Aliongea yule mzungu na kumfanya Anna atabasamu.



    “tuletee mzinga wa whisky ya kimarekani na nyama choma, mguu wa mbuzi tafadhali.” Aliagiza Anna na yule mzungu alitabasamu kuashiria alikielewa Kiswahili.



    Baada ya kuhudumiwa, waliendelea kula na kunywa huku maneno yakiendelea kusindikiza chakula chao.



    Saa limoja baadae Anna alianza kukolea kilevi baada ya kukitandika kwa fujo mzinga huo uliokuwa na kileo kingi.

    Augustino alimchora Anna kwa muda kisha akaamua kufunguka baada ya kimya kirefu kupita.

    “upo tayari nikuelezee ninachojisikia hivi sasa juu yako ?” aliongea yule mzungu na kumtazama Anna usoni.

    “ok” alijibu Anna kwa sauti ya kilevi huku macho yake yakionyesha ni kiasi gani kilevi kilichukua nafasi kubwa kwenye mwilini mwake.

    “unaweza kushangaa kwanini imekua haraka hivi, ila huu ndio ukweli ambao siwezi kuusogeza hata kwa dakika tano mbele kwa jinsi nilivyozidiwa.. nakupenda sana Anna.” Aliongea yule mzungu na kumfanya Anna ashtuke na kumuangalia Augustino.



    “what?.. oooh ….but..no Augustino.” Aliongea Anna huku akipatwa na kigugumizi cha ghafla.

    “please Anna, give me a chance in your heart to show how much I love you.” Aliongea Augustino kwa sauti ya chini lakini iliyosikika vizuri kwenye ngoma za masikio ya Anna.



    “umechelewa boy… nina mtu tayari.” aliongea Anna huku akijitahidi kumkazia macho Augustino ambayo hayakutisha. bali yaliongeza uzuri wa sura yake.



    “si kauli sahihi kuniambia kwa muda huu Anna, unaniumiza mimi niliyetokea kukupenda kiukweli “ aliongea Augustino huku machozi yakiashiria kumlengalennga



    “wasichana wote uliowaona hapa nchini hawajakuvutia mpaka niwe mimi tu?” aliuliza Anna huku akiyashuhudia machozi ya yule mzungu yakianza kutiririka na kujifuta na leso aliyokuwa nayo.



    “nimewaona… ila sijavutika nao.” aliongea Augustino huku akijaribu kujiweka sawa kwa kuyafuta machozi yake

    Anna alimuangalia yule mzungu jinsi alivyo,fikira za kuishi nchi tofauti na Tanzania zilimjia. Alitamani kuihama kabisa hii nchi kutokana na kuchoshwa na mikasa inayomuandama.



    Baada ya kuwaza dakika kadhaaa alikata shauri

    “I agree with u but when my boyfriend see us?” aliuliza kimitego Anna kuangalia nini malengo ya yule mzungu kwake.

    “I exept traver to Germany next week, atatuonea wapi??” aliongea Augustino na kumuonyesha Anna passport yake iliyokuwa tayari kwa safari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “kama ni hivyo.. tufanye haraka”

    Maneno hayo yaliendana na vitendo. Kwani siku ya pili yake walienda ubalozi wa ujerumani na kugongewa viza kwa ajili ya passport ya Anna.



    *****************************



    Safari ya ujerumani iliiva na Anna akiambatana na mpenzi wake huyo mpya wa kizungu walikwea ndege na kuiacha Ardhi ya Tanzania na kwenda kuanza maisha mapya Ujerumani.



    Baada ya miezi mitatu, Anna anaonekana na ujauzito wenye miezi hiyo hiyo. Augustino anapata wasi wasi kidogo lakini anaamua kuachilia mbali mawazo potofu.



    Miezi ilikatika kama mvua inyeshayo kwa kasi na hatimaye mimba ya Anna ikafikisha miezi tisa. Uchungu ulipomfika, alipelekwa hospitali kubwa sana huko ujerumani. Alijifungua salama mtoto wa kike ambaye alikua ndota za Anna. Alipenda sana kuwa na mtoto wa kike..



    Japo kuwa tunaamini wazungu huwa wana damu kali sana, lakini mtoto aliyezaliwa alikua maji ya kunde kama mama yake. Augustino hakuhoji chochote kwa kua alikua anampenda sana Anna.

    “our doughter “ aliongea Augustino baada ya kumnyua mtoto wao baada ya kuruhusiwa hospitalini na kurudi nyumbani.

    “beautiful like her mother” aliongea Anna na kumfanya Augustino agune.



    Hakika wote walijawa na furaha lakini Anna alionekana kuwa na wasiwasi juu ya yule mtoto. Moja kwa moja alijua kuwa huyo mtoto ni mali ya mwanaume ampendaye SIRAJI.



    “what the name you deside to give our baby” aliuliza Augustino baada ya kumlaza mtoto wao

    “mh…. MARRY..or DIANA” aliongea Anna na kutaja machaguo yake.

    “Mary..ni jina zuri zaidi.” aliongea Augustino na wote wakakubaliana na jina hilo litumike kama jina halisi la mtoto wao huyo.



    Baada ya mwaka mmoja toka Marry alipozaliwa, Anna alimshauri mume wake juu ya kurudi tena Tanzania. .

    “unaonaje kama tukirudi tu Tanzania mpenzi wangu?.” Aliongea Anna baada ya kumuita Augustino.

    “unaipenda sana nchi yako??” aliuliza kwa utani Augustino.

    “ukumbuke pia kuwa mali nyingi zipo huko pia… hulifikirii hilo?.” Aliongea Anna na kumfanya Augustino kukubaliana na mawazo ya mpenzi wake.



    Wiki moja baadae walikata mawingu na kurudi Tanzania. Walifikia kwenye nyumba ya Augustino aliyoinunua maeneo ya msasani beach.



    Maisha ya furaha ndio ulikuwa wimbo mzuri ulioendelea kudumu kwa Anna. Alikua zaidi ya malikia kwa mzungu huyo.



    Miaka miwili baade, wanaamua kumpeleka Marry shule ya awali nchini Kenya. Hayo yalikua mapendekezo ya Augustino japokuwa Anna hakupenda kuwa mbali na mwanae. Walichagua shule kubwa ya Mac international high school kupitia matandao na walipoipata walimsafirisha mtoto wao kupitia usafiri wa ndege.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati Augustino akiwa safarini kwenda Afrika kusini ambapo kampuni yake ya cement ilikuwepo huko inatokeo ajali ya ndege ambayo hakuna hata mtu mmoja aliyrpona.

    Kilio na huzuni vinarudi tena upyaa kwa Anna. Hata hivyo misingi aliyomuachia Augustino ilimuwezesha Marry kumiliki mali zote baba yake.



    Miaka ilikatika kwa kasi hadi kufikia mtoto wa Anna kumaliza elimu ya shule ya msingi huko Kenya na kuendelea na Secondary huko huko Kenya katika shule ya Mac international High school.



    Akili za Marry zilifanya kuwa na marafiki wengi kutoka nchi mbali mbali kwa sababu shule hiyo ilikuwa ya kimataifa.



    Alipasua vizuri kidato cha nne na cha sita na kuchaguliwa chuo kikuu cha Kenya. Akiwa huko kwa nyakati tofauti anakutana na watanzania wenzake wapatao sita. Utimilifu wa watu saba unawafanya waunge kundi lao la kimasomo Watanzania hao kwa kujiita SEVEN HEROES.



    Jina hilo lilikua gumzo si chuoni kwao tu, bali Afrika nzima baada ya kuibuka kidedea katika mashindano ya African challenge.



    ROJAS, ZUBERI, MAULID, IBRAHIM , KASSIM , PETER wakiongoza na MARRY ndio yalikua majina yaliyoacha historia huko Kenya baada ya kumaliza masomo yao chuoni hapo.

    *****************************



    Watu wenye hela tu ndio walikuwa wanaweza kusoma chuo hicho cha kimataifa ambacho kinamilikiwa na serikali ya marekani kinachohusiana na mambo ya uchumi.



    Rojas , Maulid , Ibrahim , Kassim na Peter familia zao zilikuwa zinajiweza kwakuwa na kipato kikubwa cha Fedha.



    Zuberi alizaliwa kwenye familia ya mvuvi Abdallah. Hali ya kiuchumi kwao ni mbaya sana. Ilikuwa kama bahati pale alipokuwa mtu wa kwanza Tanzania nzima alipokuwa kidato cha sita na kupewa scholarship na chuo hicho na kugharamiwa gharama zote atakapokuwa anasoma hapo.



    Hela nyingi alizopewa alizituma kwa baba yake na kuwawezesha kujenga nyumba ndogo maeneo ya tabata aroma kwenye kiwanja chao cha siku nyingi.



    Waliishi pamoja kama kundi kipindi chote walichokuwa wanasoma. Lakini alikua ana kitu moyoni ambacho kilikua kinamsumbua muda mrefu.

    Kutokana na hali yake kuwa tofauti na wengine alimezea moyoni mwake.



    Kuna wakati alitamani kumuelezea Marry hisia alizonazo juu yake, lakini moyo wa kukata tama ulimjia pale tu alipokumbuka kuwa Marry ni mtoto anayetoka kwenye familia ya kitajiri.



    “nakupenda sana Marry”

    Aliongea maneno hayo kila akiwa peke yake baada tu ya Marry kupotea machoni mwake.



    ************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kumaliza chuo, walikubaliana kupanda ndege moja na wote wakarudi Tanzania pamoja.



    “jamani mawasiliano muhimu, na kundi la Seven heroes lidumu hata kama hatusomi tena, au mnasemaje?” aliongea Marry na kauli hiyo kukubaliwa na kila mmoja wao.



    “ila mimi nitaenda kujiunga na chuo cha upelelezi nchini quba. Naipenda sana hiyo kazi kuliko hii niliyokuwa na vyeti vya kutosha.” Aliongea Zuberi na kuwafanya wenzake washangae.



    “ni uamuzi wake jamani, kila mtu ana malengo yake mwenyewe.” Aliongea Marry baada ya kuzuka mjadala wa wanaompinga na wanaekubaliana nae.



    Hayo maamuzi ya Zuberi yalimaanisha baada ya kupaa na ndege kuelekea nchini Quba katika mafunzo hayo. Azma ya kuendelea kusoma kwa hasira zote ni juu ya kuwa na maisha mazuri ili ampate Marry katika maisha yake.



    Zuberi alitokea kumpenda kupita kiasi Marry na kumfanya asome kwa bidii. Juhudi zake zilizaa matunda baada ya kumaliza mafunzo na kuondoka na shahada ya juu ya upelelezi.



    Aliporudi Tanzania, alipokelewa kwa shangwe na wenzake wa kundi lao la Seven heroes.

    Alifurahi kumuona Marry akiwa katika hali yake ile ile tena kwa muda huo alionekana kunenepa kiasi lakini uzuri wake ulibaki pale pale.



    Waliandaa sherehe fupi ufukwani mwa bahari ya kipepeo beach maeneo ya kigamboni.

    Watu wote waliifurahia siku hiyo hususani Zuberi aliyekuwa mlengwa wa tafrija hiyo.



    Sherehe ilipoisha, kila mtu aliondoka kivyake kasoro Marry aliyepanda gari ya Rojas na kuondoka wote.

    “ umeshamwambia Zuberi juu ya mipango ya harusi yetu?.” Aliuliza Rojas walipokuwa njiani.



    “sijamwambia mie, hata hivyo sikupata muda wa kuzungumzia hayo kwakuwa pale kila mtu alikua ana deal na yake. Ila ni vizuri tukimpa taarifa mapema.” Aliongea Marry.



    Safari yao iligota nyumbani kwa kina Marry. Waliingia ndani wapendanao hao na kuanza kumuita mama yao ambaye alikuwa mtu mzima kidogo kwa wakati huo.



    “sijui mama atakuwa kaenda wapi usiku huu.” Aliongea Marry baada ya kuita kwa muda mrefu.

    “umemuangalia chumbani kwake?” aliongea Rojas huku akimtuliza Marry aliyeanza kuwa na wasi wasi kwakua hayakuwa mazoea ya mama yake kutoka mida hiyo.



    Wazo hilo lilifuatiwa na vitendo . wote walienda chumbani kwa Anna na kukuta mlango wake upo wazi. Walibisha hodi. bila kuitikiwa wakaingia ndani.



    “MAMA…. MAMAAAAAA”



    Alijikuta Marry anaangua kilio baada ya kumuona mama yake kalala chini ya kitanda huku mapovu yakiwa yamemtoka mdomoni. Alipoangalia vizuri, aliona gazeti la uwazi likiwa lina picha ya Sira akiripotiwa kupoteza maisha huko gerezani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bila kupoteza muda, walimchukua Anna na kumuingiza kwenye gari na kumuwahisha hospitali. Huko walipokelewa haraka na Anna kuwahishwa chumba cha wagonjwa mahututi.



    Baada ya masaa mawili alitoka Daktari na kuwashauri warudi nyumbani mpaka siku inayofuata kwa kuwa hawataweza kumuona kwa muda huo.



    Siku ya pili yake asubuhi na mapema, Marry na Rojas walienda hospitalini.



    “vipi doctor, hali ya mgonjwa ipoje?” aliuliza Marry baada ya kuonana na yule daktari waliyemuacha usiku wa kuamkia siku hiyo.



    “hali bado tete, lakini fahamu zimesharudi.” Aliongea Daktari.

    “tunaweza kumuona?.”aliuliza Marry huku akimuangalia yule daktari kwa wasi wasi.

    “sawa, ila msimsumbue sana.” Aliruhusu yule daktari.



    Walipofika, walimkuta Anna akiwa kwenye kitanda huku vifaa kadhaa vikiwa vimepita puani na sehemu nyingine ya mwili. Anna alipomuana mwanae machozi yalianza kumtoka.



    “mwanangu, nakufa kabla sijashuhudia harusi yako,” aliongea Marry huku machozi yanamtoka.



    “mama, usiseme hivyo.” Aliongea Marry huku na yeye akiyaruhusu machozi yake kumtoka kama maji na kutiririka kwenye mashavu yake.



    “ kwa mshtuko nilioupata umesababisha preasure yangu kushuka sana, ukilinganisha na ugonjwa wa shinikizo la damu unaonisumbua ndio kabisaa. Kupona ni maajabu ya mungu.” Aliongea Anna kwa uchungu huku akihema kwa tabu.



    “kwani kuna kitu gani kimetokea mpaka ukawa hivi. Maana nimeliona gazeti likiwa chini na mtunzi wa zamani aliyekuwa gerezani kuripotiwa kuwa amekufa… ni ndugu yako?” aliuliza Marry swali lililozidi kumuumiza Anna moyo wake.



    “nisamehe mwanangu kwa kutokueleza ukweli mpaka umri huo uliofikia. Ukweli ni kwamba yule uliyemuona kwenye gazeti ndio baba yako halisi.” Aliongea Anna na kumfanya Marry apigwe na butwaa.



    “na Augustino je!!?” aliuliza Marry kwa mshangao mkuu.



    Anna aliamua kumpa mkanda mzima kuanzia mwanzo mpaka kufikia pale. Story hiyo ya maisha ya Anna kuanzia mwanzo mpaka kufikia pale iliwatoa machozi na kuwafanya wote kumuonea huruma Anna. Kufiwa na mwanaume aliyempenda kwa dhati toka moyoni mwake ndio sababu iliyomfikisha pale hospitali.



    Si Marry tu aliyekuwa analia, bali hata mkwe wake Rojas alishindwa kuvumilia na kumfanya na yeye kulia.

    Hakuna aliyembembeleza mwenzake kwa uchungu wa maisha na mateso aliyoyapitia Anna.



    Mara hali ilianza kubadilika na kuwa mbaya kwa ANNA. Alianza kuhema juu juu na kutoa macho huku akihangaika. Hali hiyo ikiwafanya Marry na Rojas kutoka mbio kwenda kumuita daktari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Daktari aliwaambia wamsubiri nje wakati yeye akijaribu kumsaidia mgonjwa. Huku machozi yakimtoka, marry alizidi kuomba dua kwa mungu amponye mama yake.



    ********************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog