Search This Blog

Friday, July 15, 2022

KIFO CHA MARRY - 3

 







    Simulizi : Kifo Cha Marry

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Miezi mitatu baadae, maandalizi ya harusi yalianza kushika kasi. Ken alikua na nia ya dhati ya kuishi na Anna. Mpaka Anna aliamini kuwa kuwa hakuna anayempeda zaidi yake.

    Siku zilisogea na hatimaye siku iliyosubiriwa kwa hamu iliwadia. Harusi kubwa ilifungwa na watu wakasheherekea vya kutosha.

    Anna alitunzwa vito vingi vya thamani na mkwe wake. Zawadi kubwa kutoka kwa shemeji yake anayeishi marekani ilikua gari aina ya BMW. Anna alitoa macho na kulia machozi ya furaha. Aliamini mungu ameamua kumpa mitihani ili aishi maisha mazuri na mume ampendaye.



    Nyota aliyokuwa nayo Anna iling`aa. Si kwake tu. Hata kwa mumewe. Ken alipandishwa cheo kazini na kuwa manager katika kampuni kubwa ya Sumsung kwa hapa Tanzania.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku moja Anna akiwa sheli ya pale Bamaga akiweka mafuta kwenye gari yake, kwa mbaali alimuona mtu anayemfahamu akikatisha pale. Alishuka kwenye gari yake na kumkimblia yule mtu ambaye hakua na habari kama anafuatwa. Anna alipoona kuwa hawezi kumfikia, aliamua kuita ili ayakinishe kuwa ndiye kweli yule mtu anayemjua au amemfananisha.

    “SIRAAAAAA”

    Aliita Anna na kwa haraka yule mtu akageuka nyuma kumtafuta mtu anayemuita.

    ”ANNA????”

    Alishangaa Sira baada ya kumuona Anna pale. Alimkimbilia na wote wakakumbatiana kwa furaha.

    Walijikuta wamekumbatiana kwa muda na hakuna hata mmoja aliyeonyesa ishara ya kumuachia mwenzake, walijikuta wametumia dakika zipatazo tatu. Baada ya hapo waliachiana huku kila mmoja wapo macho yake yakisoma tafsiri juu ya muonekana mpya wa mwenzame. Macho yao yalionyesha wazi kumisiana kutokana na kutoonana kwa miaka ipatayo mitano.

    “Za miaka, maana kitambo” aliongea Sira akiutathmini mwili wa Anna ulivyonawiri kutokana na lishe nzuri.

    “safi tu sijui wewe.” Aliongea Anna na kumuangalia Sira huku akiwa haamini kuwa wamekutana tena.

    “umependeza sana Anna, uongo mbaya” alisifia Sira baada ya kushindwa kuficha hali aliyokuwa nayo baada ya kumtazama kwa muda.

    “halafu wewe, haya niambie mwenzangu hajambo?” aliuliza Anna na kumuangalia Sira ambaye alikua anatabasamu wakati wote.

    “nimtoe wapi huyo mwenzako wakati nikupendaye wameninyang`anya tonge mdomoni.” Aliongea Sira na kumfanya Anna acheke.

    “Hujasahau tu, niambie basi una deel na kitu gani?” aliongea Anna na kumuangalia Sira aliyekuwa Smart kiasi aiwa na bahasha ya A4 mkononi.

    “mi ni mtunzi wa riwaya na chombezo na nafanya kazi katika kampuni ya Global Publishers.” Aliongea Sira na kumuelekeza hiyo kampuni inayomilikiwa na Erick Shigongo ambayo haikuwa mbali na pale walipo.



    Basi waliongea mengi na kupeana namba za simu. Baaada ya hapo, kila mmoja akaelekea alipokua anaenda.



    Ilipotimia saa sita usiku, Anna alisikia mlio wa sms kwenye simu yake na alipoifungua, alikuta ni sms ya Sira ikimtakia usiku mwema. Aliifuta ile sms na kumjibu kwa kumtakia usiku mwema na yeye kisha akaamua kuzima simu.



    Asubuhi ya siku ya ijumaa, Anna alilitafuta gazeti la ijumaa na kulisoma. Lengo ni kuisoma hadithi mpya ya Sira aliyomwambia kuwa itaanza kuruka siku hiyo.



    Baada ya kuperuzi kurasa kadhaa, alisuuzika moyo wake baada ya kuona jina la Siraji likiwa limejitokeza kama mtunzi wa riwaya ya MAPIGO YA MOYO.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa ni stori ya mapenzi iliyogusa maisha yake kabisa. Kila kipengele alichokisoma alikua anajihisi mkosaji kumuacha Sira na kuolewa na mwanaume mwengine. Stori ilimuhusu msichana aliyepigania penzi lake na kushinda baada ya wazazi wake kumkataa mtu anayempenda na kumlazimisha amkubali watakao mchagulia wao.

    Utamu wa hadithi uliishia njiani baada ya kutakiwa kuisubiri ijumaa ijayo ili iendelee.



    Umahiri wa kutunga riwaya na chombezo alionao Sira kulimfanya apate umaarufu mkubwa sana kutokana na kuwa na mashabiki wengi waliokuwa wanalinunua gazeti la ijumaa kwa ajili ya hadithi zake. Hali iliyomfanya kupewa magazeti karibu yote atie mkono wake. Pia haikua shida kwake kwani alikua na uwezo wa kuendesha riwaya nne na chombezo tatu bila kuingiliana na zote kubamba katika nafasi yake.



    Ulevi wa kufuatilia hadithi za Sira ulimuingia Anna na kumpigia simu mara kwa mara na kumpongeza kwa kipaji cha ajabu alichonacho.



    Kuna wakati alijisikia raha kuonana na Sira kutokana na kuwa na maneno yaliyokuwa yanamuacha hoi kila akutanapo naye.

    Mazoea ya Sira na Anna yalizidi kila siku iendayo kwa mungu. Mpaka kuna wakati mwengine mume wake alichoka kusikia habari za Sira nyumbani kwake. Maana akiongelewa mtu mashuhuri kwa utunzi basi yeye atamtetea Sira kuliko hata wakina Shaaban Robert.



    Kuna siku zingine alikua anaona kusubiri wiki nyingine ni mbali sana hivyo kumuomba Sira kumtumia riwaya zake hata kwa njia ya e-mail amalizapo tu kutunga. Sira alifanya hivyo na kusababisha Anna kujisikia faraja kuwa karibu naye.



    Siku moja Sira alimualika Anna nyumbani kwake, bila ya kusita. Anna alienda kusikiliza wito. Alikuta Sira kapanga nyumba nzima na anaishi peke yake kama alivyomuambia awali.

    “nashukuru kwa kukubali wito Anna, jisikie upo nyumbani.” Aliongea Sira na kumkaribisha katikaka moja ya sofa zilizokuwa sebuleni.

    “nishakaribia.” Aliongea Anna na kwenda kukaa kwenye sofa lilikua karibu na meza ya kiioo.

    “kuna kitu nimeamua nikwambie Anna, ila usinifikirie vibaya.” Aliongea Sira kwa sauti ya upole huku akimuangalia Anna kwa nukta.

    “kitu gani tena, mbona unanitisha?” aliuliza Anna huku akiwa amejawa na wasiwasi.

    “si kitu kibaya. Ni kizuri upande wangu, ila sijui wewe utakipokeaje.” Aliongea Sira na kumtazama Anna ambaye alikua anamuangalia bila kujibu chochote.

    “haya niambie.” Aliongea Anna kinyonge.



    Kabla Sira hajaongea kitu chochote, simu ya Anna iliita na Sira akamruhusu Anna apokee simu kwanza. Ile simu ilimtaka Anna arudi nyumbani haraka kutokana na matatizo yaliyotokea.

    Kutokana na taarifa zile muhimu, ilibidi waghairishe kikao chao na Anna kwenda kusikiliza wito.



    Aliwasha gari yake kwa spidi na kuanza kukata mitaa kuelekea kwake. Alipofika alishangaa kukuta gari kama nne zikiwa zimepaki karibu na mlango wake. Alishuka kwenye gari baada ya kupaki nje na kuanza kuingia ndani huku taswira ya wasi wasi ikitawala kichwa chake. Alizihesabu hatua zake taratibu kuelekea ndani. Huku alisikia mtu akilia kwa kwiwi. Kengele ya hatari ikagonga kichwani mwake na kumfanya aongeze kasi ya kutembea na kuingia kwake.

    “WIFIII, KAKA KATUTOKAAAA”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikua ni sauti ya dada yake Kenedy aliyeongeza kilio baada tu ya kumuona.Anna.

    Hapo hapo na yeye akaanza kuangua kilio kilichofanya watu kadhaa wliokuwepo humo ndani kuanza kulia na kufanya hiyo nyumba kutawala maombolezo.



    Anna alilia sana baada ya kuuona mwili wa mumewe ukiletwa tayari kwa ajili ya mazishi. Taarifa za kifo kilichomtokea ghafla Kenedy alipokuwa ofisini kilimuumiza sana mkewe na familia yake.



    Hata baada ya uchunguzi kupita, ikagundulika kuwa marehemu alipigwa na kitu kizito kichwani kabla ya kifo chake. Moja kwa moja ikabainika kuwa marehemu aliuwawa.

    Tume ya kuchunguza kifo cha mfanya biashara mkubwa hapa Tanzania iliundwa ili kumtafuta muuaji aliyemuua Kenedy.



    Baada ya mazishi na mirathi, wanandugu walikubaliana kumpa milioni 45 Anna na aache kila kitu na akaanzishe maisha yake kwakua hakuwazalia mtoto.



    Wakati Anna anafikiria ni wapi aende. Ghafla moyo wake unamkumbusha penzi la zamani ambalo lilijaa ukweli na kutokea hitilafu ya kifamilia iliyomfanya ashindwe kuishi nae.



    Sira naye alikua mstari wa mbele kumfariji na kuchombeza maneno ya kumpa tena nafasi nyingine katika moyo wake.

    “najua ni jinsi gani umepata maumivu moyoni, lakini mimi ndio wako uliyepangiwa na mungu. Naomba kumbuka kuwa hakuna kosa nililokutendea. Nipe nafasi nyingine japokuwa sijaharibu nafasi ya kwanza uliyonipa.”

    Alilalamika Sira huku akimshika Anna mikono yake baada ya kukubali wito aliomuita kwenye kile kikao cha watu wawili alichokihairisha mwezi mmoja uliopita baada ya taarifa mbaya alizozipata Anna.

    “naomba niache kwanza nimalize arobaini ya mume wangu, tutaongea Sira.” Aliongea Anna huku akionyesha wazi kuwa hakuwa na raha licha hela alizokuwa nazo.

    “sawa, nipo tayari kukusubiri kwa kipindi chote cha huzuni. Ila ukae ukijua kuwa nakupenda sana.”

    Alimaliza Sira na Anna akaaga na kuondoka zake.



    Baada ya miezi mitatu kupita, Anna na Sira wakasahau maumivu ya nyuma na kufungua ukurasa mpya wa mapenzi. Anna alihamia kabisa kwa Sira na kuwa kama mke wake.



    ********************



    Warda na mumewe Bilal walikuwa na shereha ya siku ya kuzaliwa kwa mtoto wao aliyekua anatimiza mwaka mmoja. Sherehe hiyo fupi waliifanya coco beach. Hakuna mtu aliyehudhuria huko, zaidi ya wao wenyewe kununua keki na kumuimbia mtoto wao huyo kwa furaha. Watu wachache walivutiwa na hiyo sherehe na kujumuika nao japokuwa hawafahamiani.



    Wazungu wawili waliokuwa wakizunguka eneo lile, walivutika na aina ya sherehe hiyo. Walisogea na wao wakalishwa keki kwa niaba ya mtoto huyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kijisherehe hicho, waliendelea kubarizi upepo mwanana uliokuwa unapiga jioni ile.

    “your baby is so cute, what his name?” aliongea yule mzungu wa kike baada ya kupata nafasi ya kumnyanyua na kumtazama usoni.

    “Shaban.” Alijibu Warda kifupi.

    “nice name, give us your baby just five minute, we want to snap some picture with him.” Aliongea yule mzungu wa kike huku akimuangalia yule mtoto na kumbusu busu.

    “worry out, but we haven`t time to stay here. Just be hurry.” Aliongea Bilal na wale wazungu walkaondoka na mtoto wao na kwenda kupiga naye picha.



    Idadi ya watu waliokuwa wakipita kila dakika iliongezeka na kuwafanya Warda na mumewe kushindwa kumuona mtoto wao kwa dakika kadhaa, lakini watu wakipungua waliwaona wale wazungu wakiwa wanapokezana kumbeba yule mtoto huku wakibadilisha mapozi ya kupigia picha.



    Ilipita nusu saa wakimsubiri mtoto wao, lakini kila dakika iendayo walijikuta wanapatwa na wasiwasi. Hata waliposogea pale kwa mpiga picha hawakuwaona wale wazungu.



    “we kaka, wale wazungu uliokua una wapiga picha wapo wapi?” aliongea Warda huku akiwa amejaa wasiwasi mkubwa.

    “wamechukua kamera yao wameondoka sasa hivi, waangalie kule juu.”alijibu yule mtu na Warda akiongozwa na mumewe walielekea haraka walipoelekezwa.

    Hata huko waliambulia patupu. Walitafuta sana mpaka kiza kilipoanza kuingia. Hapo walijua fika kuwa mtoto wao atakuwa kaibwa na wale wazungu. Hapo wote wawili walijikuta wanamwaga machozi hadharani.



    *******************

    “Michael, why” hiyo ilikua sauti ya mzungu wa kike akimlaumu mume wake baada ya kupaki gari yao mita kadhaa na pale coco beach walipokuwepo.

    “don`t ask me like that, u know everything I do.” Alijibu yule mzungu wa kiume kwa ukali.

    “but…....”

    Kabla yule mzungu hajamalizia alichokua anataka kuongea, alikatishwa na sauti kali iliyomfanya akubali matokeo.

    “shut up?... u haven`t able to make someone to call me a daddy…damn you.”

    Aliongea Michael na kumfanya mke wake kujiinamia na kuanza kulia.

    “i`m sorry, “

    Sauti ya upole ilitoka kwa Michael huku akijitahidi kumbembeleza mke wake aliyekua akiumia kwa tatizo lao la kukosa mtoto kwa kipindi kirefu. Mara zote Michael hulitumia tatizo hilo kama fimbo na kumlaumu mkewe japokuwa hakuna aliyekuwa na tatizo kati yao. Baada ya muda, Catherine alinyamaza na kumkumbatia mumewe ambaye alionekana akijutia kauli yake.



    ************************



    Mapenzi matamu ya Sira na Anna yalirudi kwa kasi ya ajabu. Sasa kila mmoja alikiri kuwa kaumbwa kwa ajili ya mwenzake.

    “baby, fanya haraka. Unavaa mawe huko.” Aliongea Sira baada ya kuvumilia kwa dakika kadhaa toka amalize kuvaa na kutoka nje.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “jamani honey, namalizia hereni tu.” Aliongea Anna na kujiangalia kwenye dressing table na kujikagua kagua kwa kujigeuza kila upande. Baada ya kuridhika. Alitoka na cheni ya dhahabu mkononi na kumpelekea Sira.

    “nivalishe wewe, maana una haraka.” Aliongea Anna na kuachia tabasamu.

    “bora umelitambua hilo.” Aliongea Sira na kumvalisha Anna ile cheni.

    “umependeza sana.” Alisifia Sira.

    “wala sishangai mume wangu. Maana hata nikivaa kituko unasema nimependeza.” Aliongea Anna na kumuangalia Sira ambaye alikua anatabasamu wakati wote.

    “yeah, kupendeza ni jina lako la tatu. Baada ya Anna, Mashuhuri linalofuata ni kupendeza.” Aliongea Sira na kumfanya Anna acheke.



    Sira alishuka kwenye gari na kwenda kufungua geti ili kuliruhusu gari

    Kutoka.

    Alipofungua tu mlango, waliingia maaskari wapatao watano na wote wakiwa na silaha.

    “upo chini ya ulinzi kuanzia hivi sasa ninavyoongea.”

    Aliongea askari mmoja mwenye nyota tatu begani na kumuamuru Sira ageuke nyuma na kunyoosha mikono yake juu.





    “Maelezo zaidi tukifika kituoni.” Aliongea yule askari mkuu na kumchukua Sira na kwenda naye kituoni. Anna aliifatilia ile Deffender kwa nyuma hadi kituoni alipopelekwa mpenzi wake na kutaka maelezo yakinifu yaliyofanya Sira akamatwe.



    “mama tumemuweka chini ya ulinzi kutokana na uchunguzi wa kifo cha mumeo ulipofikia. Tunamuhitaji sana katika kukamilisha uchunguzi wetu.” Aliongea askari huyo na kumuangalia Anna kwa umakini.

    “kwani yeye ndiye aliyeua?” aliuliza Anna kwa hasira.

    “uchunguzi bado haujakamilika. Ndio maana tume kwambia tuna muhitaji kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi wetu.” Aliongea yule askari na kumfanya Anna aondoke kwa hasira.



    Baada ya siku mbili, Sira anapandishwa kizimbani kwa kesi ya kumuua Kenedy. Shtaka hilo linalomkabili Sira linamuweka Anna katika mazingira magumu kutokana na kuwa na Sira wakati wa tukio. Anahusika vipi ndio swali lilikoa lina kosa majibu.



    Sira anakanusha na kurudishwa tena ndani. Dhamana yake inafungwa mpaka kesi yake itakaposomwa tena miezi miwili ijayo.



    ***************************



    Baada ya kukamilisha taratibu za kusafiri, Michael na mkewe wanakwea ndege na kurudi kwao marekani. Huko walianza malezi ya mtoto Shaabani kama mtoto wao kutokana na kudanganya kuwa wamemchukua kwenye kituo cha kulelea watoto yatima.



    Maisha yanakuwa mazuri baada ya mfuko wa serikali yao kuwatengea fungu la hela juu ya uchunguzi wa dawa ya kansa ya mapafu ambayo watafiti hao waliamini ilikua katika miti iliyojiotea yenyewe katika hifadhi ya ngorongoro iliyopo nchini Tanzania.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Majani hayo waliyoyachuma kwa wingi kiasi walichanganya na mchanganyiko Fulani hivi uliokuwa katika maabara yao na kupata kitu chenye maji maji ya rangi ya kijani kibichi.

    Experiment ya kwanza waliifanya kwa mgonjwa aliyekaribia kufa kwa ugonjwa huo na kutoa majibu mazuri. Walifurahi sana kwakua utajiri ulikua unanukia upande wao.



    Walianza kufanya kazi usiku na mchana mtu na mke wake. Waligundua kua iliweza kuongeza nguvu za kiume na kuongeza wingi wa mbegu kwa wale ambao hawakuzaliwa na tatizo hilo.



    Dawa hiyo pia ilitoa majibu mazuri kwake yeye mwenyewe baada kufanikiwa kumtia mimba mke wake.



    Furaha isiyokuwa na kifani iliwapata wawili hao. Walijulikana Marekani nzima na kufungua duka kubwa lililouza dawa hizo kwa bei ya juu iliyowafanya kutajirika kwa muda mfupi.



    Majani yalipo karibia kuwaishia, walikubaliana kurudi nchini Tanzania kuchukua mbegu na majani mengine lakini lengo lao lingine ni kumrudisha mtoto wa watu kwakua mungu alishwaangazia kwa kuwapa upeo wa kutengeneza dawa inayowasaidia watu ikiwemo wao wenyewe.



    Michael na mkewe walirudi Tanzania na kwenda hifadhi ya ngorongoro na kuchukua majani hayo na kuyalipia kiasi kidogo cha fedha kwakua watanzania walikua wanautumia huo mti kama dawa ya tumbo tu.

    Baada ya kupata shehena ya kutosha, walitangaza kwenye televisheni na kwenye Radio juu ya kuwatafuta wazazi wa mtoto wanayeishi naye.



    Zawadi ya milioni mia kwa wazazi halisi wa mtoto huyo ndio sababu iliyowachanganya watu wengi kwenda kujaribu bahati zao japo kuwa hawakua na uhakika na mtoto huyo.



    “mwenzangu taarifa za wazungu waliomchukua mtoto na sasa hivi wanawatafuta wazazi wa mtoto huyo umezisikia?”ilikua sauti ya dada mmoja akimwambia Warda.

    “sijasikia, wapo wapi jamani anaweza kuwa mwanangu.” Aliongea Warda na kukimbilia ndani na kuwasha tv baada ya kuambiwa tangazo lilikuwa linarushwa muda huo.



    Hakuamini macho yake baada ya kuona picha za mwanae zikiwa zinapita na tangazo linalomuhusu yeye kabisa. Alimshukuru mungu na kumpigia simu mume wake ambaye alikuja mbio.



    Baada ya mkewe kumpa taarifa muhimu juu ya tukio lile, waliamua kuelekea eneo walilotangaziwa.



    Walishangaa kuona msururu wa watu utafikiri walikua wameenda kwenye audition ya bongo star search kwa jinsi walivyopanga msitari.



    Warda aliona ujinga, hakupanga mstari zaidi ya kuingia moja kwa moja kwenye chumba cha upimaji. Kwa bahati nzuri yule mtu aliyekua amekaa kwenye kiti alikua ni Michael mwenyewe.

    Wote walikumbukana na Michael alitoka nje kwanza na kuutangazia umati uliofika pale kuwa mzazi halisi wa yule mtoto ameshapatikana.



    Michael na mkewe waliwaomba sana msamaha wazazi wa Shabani na baadae waliwapa fedha walizoahidi kuwapa wazazi wa mtoto halisi kama zawadi ya kusamehewa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikua kama ndoto kwa Warda na mumewe, walizipokea milioni mia zao na kwenda kufungua miradi kadhaa ikiwemo kumalizia nyumba yao waliyoitelekeza muda mrefu kutokana na kukata kwa hela.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog