Search This Blog

Friday, July 15, 2022

KIFO CHA MARRY - 5

 







    Simulizi : Kifo Cha Marry

    Sehemu Ya Tano (5)



    Bahati iliyo waangukia wazazi wa Shabani ndiyo iliyowabadilishia maisha baada ya mtoto wao kupasua vizuri elimu ya juu na kujiunga na jeshi la polisi kwakua ndio kazi aliyokua anaipenda .

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kutokana na kujituma sana katika kupeleleza mpaka kwenye kesi zilizohatarisha maisha yake, ndio sababu iliyomfanya kupelekwa kwenye mafunzo ya juu ya upelelezi huko nchini Quba na kukutana na Mtazania mwenzake Zuberi.



    Urafiki wao ulidumu kipindi chote cha mafunzo yao. Kwakua zuberi alikuja nyuma, Shabani alimaliza wa kwanza na kumuacha chuoni Zuberi.



    Aliporudi Tanzania, alipata taarifa juu ya kifo cha wazazi wake waliowawa na wauzaji wa madawa ya kulevya. Taarifa hizo zilimuhuzunisha na kuwalaumu kwa kumficha kwa sababu alikuta tayari wazazi wake wameshazikwa na serikali.



    Alipelekwa kwenye makabuli ya wazizi wake na kupewa picha za wahusika wa kifo cha wzazi wake.



    Akiwa kama Inspector Shabani, alikabidhiwa jukumu hilo alilolikubali kwa mikono miwili.



    Kwa utaalamu wa uchunguzi na umahiri katika mapambano. Akishirikiana na maaskari wengine alifanikiwa kuwakamata wauaji wa wazazi wake na kuhakikisha wanahukumiwa kunyongwa.



    Kazi ya kujitolea kuwasaidia watu wanaoonewa na kunyanyaswa na wenye hila ndio ilimfanya Shabani kupendwa na raia wema.



    Wakati mwingine alitumika kama Police in counter kwa kuruhusiwa kuua kwa jambazi yoyote sugu kwakua walikuwa wanatoka kila wakikamatwa kutokana na baadhi ya maofisa wa polisi kutokuwa waaminifu.



    Jina la Inspector Shabani lilizagaa na kuwa tishio kwa wahalifu na kuwa msaada kwa wanyonge waliokuwa wana muombea maisha marefu kila siku iendayo kwa mungu.



    ***********************



    “vipi daktari?” aliuliza Rojas aliyekuwa anambembeleza mchumba wake aliyekuwa akilia muda wote. Hii ilikua baada ya kumuona daktari akitoka kwenye kile chumba alicholazwa Anna.



    “wewe ni mwanaume, unatakiwa kuwa na moyo na koo la kumezea na kustahimili mambo yote. Yawe mabaya au mazuri. Kiukweli nimejitahidi kwa uwezo wangu kama daktari kuokoa maisha ya mgonjwa wenu. Lakini ahadi yake imeshafikia. Hatunaye tena duniani.” Aliongea Daktari na kumshika bega Rojas ambaye alikua yupo katika dimbwi la huzuni.



    “ooh my god”



    Alisema Rojas kwa uchungu huku akishindwa kuzizuia hisia zake . kilio kilianza na kumfanya Marry atambue kinachoendelea.

    Kwa uchungu mkubwa, Marry aliingia kwenye hicho chumba na kumkuta mama yake amefunikwa gubi gubi.



    “hapana … mama yangu kalala tu Rojas,..mama hawezi kufa kabla ya kushuhudia harusi yangu.. mama.. mama amka… mama mimi mwanao wa pekee nakaribia kuolewa mama. Mama fumbua macho japo kidogo.. mamama… MAMAMAAMMAAAAA”



    Alilia kwa uchungu Marry huku akimtingisha Anna. Alizuiwa na Rojas akishirikiana na Daktari.

    Wote waliguswa na msiba huo mkubwa kwa Marry aliyempoteza baba yake kabla hata ya kumtia machoni na mama yake ndio huyo nae anatangulia mbele za haki.

    Marry alilia sana mpaka akapoteza fahamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kilio klidumu mpaka siku ya mazishi ya Anna. Marry alikuwa mtu wa kulia tu japokuwa marafiki zake walikuwa msitari wa mbele kumfariji.



    Baada ya arobaini ya mama yake Marry kupita, zoezi la maandalizi ya ndao liliendelea.



    “haiwezekani, nasema haiwezekani…. Atamuoaje yeye wakati mimi ndio ninayestahili kuwa mume wake?.. haiwezekani.” Aliongea peke yake Zuberi huku machozi yakimtoka. Hakuamini kuwa Rojas atampiku kwa kumuoa Marry wakati yeye alienda kusoma kwa ajili ya Marry,



    Siku zilizidi kukatika na hatimaye siku ya harusi ilifika. Watu wengi kutoka sehemu mbali mbali walihudhuria harusi hiyo ya aina yake kwa mtoto wa tajiri mkubwa hapa Tanzania Rojas kumuoa Marry aliyekuwa mtoto wa mjasilia mali mwenye viwanda kadhaa ndani na nje ya nchi, Anna.



    Ndoa ilipita bila kipingamizi huku Zuberi akiwa hajaifurahia hata kidogo ile harusi. Alistahimili na kushiriki sherehe zote kama mwana kundi la Seven heroes lakini moyoni hakuwa na amani hata kidogo. Moyo wake ulimuuma sana kumkosa Marry tena akishuhudia kwa macho yake.



    Baada ya mwezi mmoja kupita toka Rojas amuoe Marry, ndio walikuwa wanarudi baada ya kwenda kula honeymoon huko London uingereza na kumalizia mapumziko yao Cape town Afrika kusini.



    Walipokelewa na kundi zima la Seven heroes waliowaacha hapa Tanzania. Hata zuberi alikuwepo na yeye katika zoezi hilo la kuwapokea.



    Siku mbili baadae Zuberi aliwatembelea nyumbani kwao mida ya saa kumi na mbili jioni. Rojas na Marry walipiga story na Zuberi mpaka saa tu usiku.

    Walikula pamoja na kucheka pamoja huku wakikumbushiana mambo kadhaa wakati walipokua chuoni.



    Mara wakasikia kama kuna kitu kimegonga kwenye dirisha lao la sebuleni.

    “sijui nani katupa kitu kama jiwe dirishani!” aliongea Rojas baada ya kisikia mlio wa kioo baada ya kugongwa na kitu kizito ambacho hakikuvunja kioo.



    Kabla hajafanya lolote, mlio kama huo ukasikika tena. Hapo maamuzi ya kwenda kuangalia ni nani ambaye alikua mle ndani wakati kulikua na geti na electronic security ndio ilikua inalinda pale pote.



    Baada ya Rojas kufungua dirisha, alikutana na mshale uliompiga sawia kifuani na kuchomoza mgongoni.



    Mshtuko mkubwa uliwapata Zubery na Marry waliokuwa wakimshuhudia Rojas akidondoka.

    Kilio cha haja kilisikika baada ya Marry kumuona mume wake akitokwa na damu huku akihema kwa tabu. Zuberi alitoka nje na kuangalia watu waliofanya lile tukio na alipowakosa alirudi ndani na kusaidiana na Marry kumnyanua Rojas ili wamuwahishe hospitali. Lakini Rojas aliaga dunia hata kabla hawajamnyanyua.



    Kifo hicho cha utata cha mume wake Marry kilizua utata mkubwa. Hakuna aliyejua ukweli juu ya kifo hicho.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya maiti ya Rojas kufanyiwa uchunguzi, alizikwa kwa majonzi makubwa na marafiki zake.

    Hata mke wake alishindwa kula kwa siku kadhaa na kumlalamikia mungu kwa kumpa mitihani mfululizo.

    Mwezi uliopita tu aliwapoteza wazazi wake wote waili na hivi sasa anamkosa mume wake waliodumu katika ndoa mwezi mmoja tu.



    Inspekta Shabani na inspekta Zuberi walipewa kazi ya kupeleleza kifo cha Rojas.

    Kwa kutumia vifaa maalumu ambavyo viliwapa ripoti nzuri juu ya wauaji.

    Alama za vidole vilivyochukuliwa kwenye ule mshale, waliweza kumbaini muuaji na kuanza kumsaka usiku na mchana.



    Baada ya miezi miwili, mtuhumiwa wa mauaji alikamatwa na Inspector Shaban. Kazi hiyo ilifanywa vizuri na zuberi akiwa mstari wa mbele katika kutoa ripoti kwa kila hatua aliyofikia.



    “naomba mleteni mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano.” Aliongea Inspector Shaban na kumuamuru mmoja wa maafande anao watumia katika kazi yake hiyo ya upelelezi.



    “Inspector, mbona mtuhumia mwenyewe ameshafariki?” aliongea huyo afande na kumfanya Inspector Shaban aende kumuangalia.



    “ooh my god”



    Alichoka Inspector shaaban baada ya kukuta muuja wa Rojas naye ameshafariki.

    Baada ya vipimo vya maiti ile, iligundulika kuwa alikunywa sumu kabla ya kifo chake.



    Baada ya miezi miwili kupita, taarifa ya habari kutoka kituo cha habari BBC kiliripoti kifo cha Mtanzania mmoja huko visiwa vya Commoro aliyeokotwa na wavuvi akiwa anaelea kwenye bahari.



    Picha za maiti hiyo iliwashtusha wengi sana kwakua alikua mtu maarufu sana. Si Tanzania tu, bali Afrika nzima ilisikitika baada ya kumuona mshindi wa African chalange pekee wa kike wa mwaka uliopita.



    Kundi zima la Seven heroes akiwemo Inspector Shaban walipatwa na mshituka baada ya kumuona MARRY ndio aliyekutwa amekufa.



    Msiba mzito uliikumba kundi hilo, lakini zuberi ndio alikuwa anaonekana kuumia sana. Alilia kupita watu wote na kuonyesha wazi ni jinsi gani alikua anampenda sana Marry abaye sasa na marehemu..



    Uchunguzi wa kina ulianza kwa kufanya utafiti kwenye shirika lililotoa boti baada ya mtu aliyemuona Marry akiwa na mtu mwingine ambaye maiti yake haikuonekana kuripoti taraarifa hizo police.

    “unasema kuwa marehemu alikuja na mtu hapo ofisini kwenu walipokuja kukodi hiyo boti?” aliongea Inspekta Shabani baada ya kuipokea simu ya mtu huyo.

    “ndio. Tena ni mawnaume maji ya kunde hivi. Yaani ikitokea namuona tena kwa mara nyingine, basi lazima nimtambue.” Aliongea yule mtu na kumfanya Inspekta Shabani kuona kuwa amepata mwanga kidogo katika upelelezi wake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “unaweza kuja kituoni kwetu. Maana kuna mchoraji hapa. Kwa maelezo yako tunaweza kuipata sura halisi ya muuaji wa Marry.” Aliongea Inspector Shabani.

    “sawa.”

    Aliomgea yule mtu na kukata simu. Ilipita saa nzima bila yule mtu kufika pale kituoni. Mara akapigiwa simu na mkuu wake kuwa kuna tukio lingine limetokea maeneo ya mwananyamala koma koma.



    Alifika eneo la tukio haraka na kukuta gari likiwa limepaki na kuzungukwa na umati mkubwa wa watu waliokuja kushuhudia tukio lile.

    Baadhi ya maaskari walikuwepo kwa ajili ya kuwazuia raia walikuwa wakisogolea kabisa eneo hilo. Alilifikia lile gari. Na alipochungulia ndani, aliuona mwili wa mwanaume aliyeuwawa kwa kupigwa risasi ya kichwa. Alijaribu kuangalia leseni ya huyo maiti na kukuta jina linalofanana na yule mtu aliyekuwa anaongea nae kwenye simu. Wazo la kupiga simu likamjia. Alipopiga alisikia mlio wa simu ukiita kwenye suruali ya yule maiti aliyekuwa pale.



    Iinspekta Shabani alizidi kuchanganyikiwa baada ya kugundua kuwa muuaji alikua na mtandao mkubwa.



    Siku mbili baadae ile boti ilipatikana ikiwa imetelekezwa msasani beach. Taarifa zilimfikia inspector Shabani na kuamua kwenda kupeleleza huko.



    Aliambulia baadhi ya nguo za kike ambazo zilimjulisha kuwa muuaji atakuwa alibaka kwanza kabla hajaua. Maana zilikuwa zimechanika na upande mwengine kuwa na damu. Alizichukua ili zimsaidie kwenye upelelezi wake.



    Usiku wa manane, inspector Shabani alipigiwa simu na mtu asiyejulikana

    “kaka hii game ni ya kifo. Hivyo kaa mbali na mchezo huu maana muda si mrefu watu wataiokota maiti yako kama waliotangulia.”

    Hayo maneno aliyasikia Inspector Shabani baada tu ya kupokea simu. Kabla inspector Shabani hajaongea lolote, simu ilikatwa na yule mtu. Alijaribu kupiga lakini haikupatikana.



    Kabla hajafanya lolote. Alianza kusikia harufu nzito kama ya moshi hivi ikitawala kwenye chumba chake. Aliopotoka sebuleni, aliona moto mkubwa uliokuwa ukisambaa kwa kasi.



    Alikimbia chumbani kwake na kuchukua nyaraka muhimu na kupita mlango wa dharula na kuondoka. Dakika moja baadae nyumba nzima ya Inspector Shabani ilishika moto.



    Wakati akikimbia kunusuru maisha yake, alimuona mtu aliyevalia koti jeusi akiwa kwenye piki piki na pembeni yake kulikua na madumu kadhaa ya mafuta.

    Yule mtu machale yakamcheza na kuwasha piki piki yake na kutimua mbio. Japokuwa kulikua na mwanga hafifu, lakini Inspector Shaabani alizinakili namba za ile pikipiki na kuwapigia maafande wengine waliokuwa doria eneo hilo kwa radio call yake aliyofanikiwa kutoka nayo.



    “tumefankiwa kumkamata mtuhumiwa wako over”

    Taarifa hizo zilimfanya inspector Shaban kupanda moja kati ya magari ya maaskari waliofika pale kwake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alifanikiwa kumkuta mtuhumiwa wake akiwa hai. Alimuangalia na kugundua kuwa ile sura ilikuwa ngeni kwake.



    Kutokana na mafunzo aliyoyapata nchini Quba. Dakika mbili zilitosha kabisa kumfanya yule mtu kumtaja aliyemtuma.



    “una uhakika na unachokisema!!!” aliuliza inspector Shaban hukua akionyesha kuzishangaa zile taarifa.

    “yeye ndio kanituma mimi. Nisamehe mkuu” aliongea yule mtu huku akilia kwa maumivu kutokana na kibano alichokipata.



    “tusilaze damu. Twendeni kwa inspector Zuberi muda huu huu.”

    Aliongea Inspector Shaabani na wote wakatii.



    “upo chini ya ulinzi Inspector Zuberi”

    Aliongea inspector Shaban baada tu ya zuberi kufungua mlango wake.

    “acha utani bwana. Matani gani hayo rafiki yangu.” Aliongea Zuberi huku akitweta baada ya kumuona inspector Shabani nyumbani kwake.



    “mkamateni, maelezo zaidi kituoni,” aliamuru Inspector Shabani na wale maaskari wengine wakamfuata Zuberi na kumfunga pingu.



    Kesi ya mauaji ya Rojas,Marry na Amini mfanya kazi wa bandari ndio kesi iliyokuwa inamkabili Zuberi. Pia alitajiwa kosa la kutaka kumuua Inspector Shabani kwa makusudi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kukiwa na waandishi wa habari kutoka vituo mbali mbali nchini na nchi jirani, wote walikuja kusikiliza kesi hiyo iliyounguruma kwenye mahakama kuu.



    Yule tuhumiwa namba mbili, alimwaga kila kitu na kufanya kesi kuwa ngumu kwa Zuberi ambaye alikua kimya wakati wote ambao kesi ilikua inaendelea.



    “kutokana na ushahidi uliopatikana. Unakutia hatiani Zuberi kwa kuhusika na mauaji. Unakubali au unakataa?” aliuliza hakimu baada ya ushahidi kukamilika.



    “siwezi kukata ndugu hakimu, mimi nilimpenda sana Marry. Nimepoteza muda wangu kwenda kusoma kwa ajili yake. Yote hayo kwangu nilikua najisumbua. Hiyo ndio sababu iliyonifanya nimuue Rojas kwa kua alimuoa mwanamke niliyompenda kwa kuwaingiza watu wangu walionisaidia kufanya hilo tukio…. Marry niliamua kumuua kwa kumpiga na kumzamisha baharini baada ya kukubali vizuri kunipa company katika safari yangu kwenye visiwa vya Comoro. Lakini alinibadilikia njiani baada ya kumuelezea hisia zangu na kunikataa. Nikamuulia mbali. Na huyu mwingine nilimpiga risasi kwa kimbele mbele chake mwenyewe. Kila simu iliyokuwa inaingia kwa Inspector Shabani nilikua naisikia baada ya kudivet namba yake. Pia nilitaka kumuu Inspector Shabani kwakua alikua anaifatilia sana kesi hii. Sikuwa na lengo la kuua kabisa ndugu hakimu. Ila ni mapenzi tu ndio yaliyosababisha.”



    Zuberi aliamua kuongea kila kitu kwakua hakuona thamani ya maisha bila kipenzi chake Marry. Ingawaje ni yeye mwenyewe aliamua kumuua baada ya kukataliwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na kuwaachia wenzake huzuni kubwa ambao kwa sasa wamebaki wanne tu badala ya saba kama walivyokuwa chuoni na kujiita SEVEN HEROES

    **************** MWISHO*****************

0 comments:

Post a Comment

Blog