Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

A DAY TOO LONG (SIKU NDEFU MNO) - 3

 





    Simulizi : A Day Too Long (Siku Ndefu Mno)

    Sehemu Ya Tatu (3)







    Ilipoishia



    “Sikuamini. Sikuamini hata kidogo, huo utakuwa mchezo mchafu mnaotaka kutufanyia” Rais Kyomo alisikika simuni.

    “Ndio ukweli. Nilimtuma waziri wa Afya kwenda kumchukua chuo ili tumsafirishe lakini akakuta Wamarekani wamemchukua” Rais Ranjit alimwambia .

    “Huo ni mchezo tu. TUNAMTAKA ABUU WETU” Iliskika sauti ya rais Kyomo na kisha kukata simu.







    Songa nayo sasa….



    Dokta Mickey alikuwa na presha ya kufika nchini Marekani na kueleza kile ambacho alikuwa amekiona nchini India. Moyo wake ulikuwa kama umebeba mzigo mzito, mzigo ambao alitamani kuushusha katika kipindi ambacho angefika nchini Marekani.

    Muda wote uso wake ulionekana kuwa na furaha kupita kawaida kwa kuona kwamba wakati wa kulipatia sifa zaidi taifa lake la Marekani ulikuwa umefika. Muda wote alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Mara baada ya ndege kushuka katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Baltimore, au Washington kama ulivyokuwa ukijulikana Dokta Mickey pamoja na abiria wengine wakateremka kutoka katika ndege ile na kisha kuanza kupiga hatua kulifuata jengo la uwanja huo na kuanza kuchukua mabegi yao ambayo yalikuwa yamekwishachunguzwa na kuondoka mahali hapo.

    Alipofika nje ya jengo la uwanja wa ndege ule, akakodi teksi na kisha kumwambia dereva ampeleke West Mall, sehemu ambayo ilikuwa ikipatikana Ikulu ya Marekani. Japokuwa dereva alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kawaida lakini dokta Mickey akamuona kama akiendesha kwa mwendo wa taratibu jambo ambalo kila wakati alikuwa akimsisitizia mara kwa mara kwamba aendeshe kwa kasi zaidi.

    Hapo ndipo alipokumbuka kitu, akaichukua simu yake na kisha kuiwasha na kuanza kupiga namba za rais wa Marekani, Obama na kuanza kuongea nae kwamba alikuwa na jambo muhimu sana ambalo alikuwa akitaka kumwambia kwa wakati huo. Aliongea nae kwa dakika kadhaa na hivyo rais kumtaka kufika katika Ikulu ile kwa ajili ya mazungumzo zaidi kwa kile ambacho alikuwa amemuelezea kwa kifupi.

    Mara baada ya kufika umbali wa kilometa moja kabla ya kulifikia geti la kuingilia eneo la Ikulu, dereva akasimamisha gari na kisha Dokta Mickey kuteremka na polisi kadhaa kumfuata na kisha kujitambulisha kwao. Kutokana na rais kutoa taarifa za haraka haraka juu ya dokta huyo, akaruhusiwa kuingia ndani ya eneo la Ikulu ile na kisha kuanza kupiga hatua kulifuata jengo lile huku kila kona kukionekana kuwa na kamera pamoja na polisi kadhaa.

    “Just tell me about it (Hebu niambie kuhusu hilo jambo)” Rais Obama alimwambia dokta Mickey.

    “I saw a young man (Nimemuona kijana)” Dokta Mickey alimwambia rais.

    “Which boy? (Kijana yupi?)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hapo hapo Dokta Mickey akaanza kuelezea kile ambacho kilikuwa kimetokea nchini India juu ya kijana ambaye alikuwa ameonyeshewa pamoja na dawa ya kansa ambayo alikuwa ameitengeneza kijana yule, Abuu. Muda wote rais Obama alikuwa ametegesha masikio akimsikiliza Dokta Mickey ambaye alikuwa akiongea huku akiwa haamini kama kweli kile ambacho alikuwa amekiona nchini India kilikuwa kweli.

    Maongezi yao yalichukua dakika thelathini na ndipo ambapo Dokta Mickey akaamua kuwasiliana na Bwana Thomas, mtu ambaye alikuwa bosi mkuu wa shirika la upelelezi la F.B.I. Maneno ambayo aliongea Dokta Mickey tayari yalikuwa yamemchanganya kupita kawaida, hakuamini kama duniani kungekuwa na mtu ambaye angeweza kutengeneza dawa ya magonjwa ya kansa.

    Aliongea na Bwana Thomas kwa muda wa dakika moja tu na kumtaka kuelekea katika Ikulu ile kwa maongezi kadhaa. Muda wote rais Obama alionekana kuwa na furaha, tayari aliziona sifa nyingi zikianza kumiminika katika nchi ya Marekani, aliamini kabisa kama angeweza kufanikisha kumleta kijana huyo, Abuu ndani ya nchi yake basi kusingekuwa na ugumu wa kukipigania kiti cha urais kwa chama chake kushinda katika uchaguzi ujao, kwani kile kingeonekana kuwa sababu.

    “We have to kidnap him, How do you see that? (Inatubidi tumteke. Unalionaje hilo?)” Rais Obama aliuliza.

    “Good idea (Wazo zuri)” Dokta Mickey alisema huku wote nyuso zao zikiwa zimetawaliwa na tabasamu.

    Ndani ya dakika ishirini, Bwana Thom akawa amekwishaingia ndani ya Ikulu hiyo na moja kwa moja kukutana na rais pamoja na Dokta Mickey na kisha kuanza kuelezwa kile ambacho kilitakiwa kufanyika katika muda huo. Kilichoelezwa ni kwamba Abuu alitakiwa kuchukuliwa kutoka nchini India na kuletwa nchini Marekani kisiri, na hakukuwa na watu ambao wangeweza kufanya hivyo zaidi ya FBI ambao walikuwa na uwezo mkubwa sana katika mambo mengi hasa utekaji.

    Hilo likaonekana kuwa wazo zuri ambalo liliungwa mkono na kila mtu, Abuu ndiye ambaye alikuwa akihitajika nchini Marekani kwa wakati huo na ilikuwa ni lazima kutekwa kwani bila kufanya hivyo, Waindi wasingekubali mtu huyo aondoke mikononi mwao.

    “We are doing this for Americans (Tunafanya hili kwa ajili ya Wamarekani)” Rais Obama alisema huku akiinyanyua glasi yake iliyokuwa na pombe hewani.

    “For Americans (Kwa ajili ya Wamarekani)” Dokta Mickey na Bwana Thomas walisema.



    ****



    Wapelelezi watatu, Jackson, Brian na Shedrack ndio ambao wakaandaliwa kwa ajili ya kufanya kazi moja kubwa ambayo ilikuwa mbele yao, kuhakikisha kwamba kijana Abuu analetwa nchini Marekani kwa njia ambazo wala hazikuwa za uhalali hata kidogo.

    Kazi ile hasa kwa wapelelezi wale ikaonekana kuwa rahisi sana ambayo wala haikuonekana kuwa na ugumu wowote ile. Walichokifanya ni kujiandaa na kisha baada ya siku mbili kuanza safari huku wakiwa na vifaa vyote ambavyo waliona kwamba wangevitumia katika utekaji huo.

    Saa saba mchana, ndege ya shirika la ndege la Alliance Airways ilikuwa ikitua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mumbai ambapo wapelelezi wale wakateremka na kisha kuanza kuelekea katika jengo la uwanjani pale huku wakitangulizana pamoja na abiria wengine ambao walikuwa wamefika nchini hapo kwa kutumia ndege hiyo.

    Wakatoka katika jengo lile na kisha kuelekea nje ambapo wakakodi teksi na kutaka wapelekwe katika hoteli kubwa na ya nyota tano na kisha dereva kuanza kuwapeleka katika hoteli ya Dhabi ambayo ilikuwa katikati ya jiji la Mumbai. Kila mmoja macho yake yalikuwa yakiwaangalia watu ambao walikuwa wakipita huku na kule na huku wengine wakiwa wanaabudu masanamu ya Buddha ambayo yalikuwa yakionekana kuwa kama mungu wao mkubwa katika nchi hiyo.

    Baada ya dakika ishirini, teksi ile ikasimama nje ya hoteli ya Dhabi na kisha kuanza kuelekea katika sehemu ya mapokezi na kuchukua vyumba vitatu na kuanza kuelekea huko. Kwa wakati huo, kila mmoja alikuwa akifikiria kazi ambayo ilikuwepo mbele yao, kazi ile wala haikuonekana kuwa kubwa, walitegemea kuifanya bila kugundulika na mtu yeyote yule.

    Mara baada ya kuweka mabegi yao katika vyumba vya, wakakutana katika chumba cha Shedrack na kisha kutoa ramani kubwa ya dunia na kisha kuanza kuangalia nchi ya India. Kitu cha kwanza walichokifanya mahali hapo ni kuangalia ramani nzima ya India na kisha kuangalia mipaka na sehemu nyingine.

    “Tukimteka, tutaanza kuelekea Bhopal ambapo tutatumia mwendo wa saa moja. Tukifika hapo, tutaendelea na safari yetu ya kuelekea Guna. Kwa sababu tukifika huko kutakuwa tayari ni jioni, hivyo tutaendelea na safari yetu kidogo na kuelekea Udaipul. Tukifanikiwa kufika hapo, tutalala na kisha kesho yake asubuhi na mapema kuanza safari ya kuelekea Jaisalmer ambapo kupitia mpaka huo tutafanikiwa kuingia katika nchi ya Pakistan” Shedrack aliwaambia wenzake huku akiwaonyeshea ramani ile.

    “Ni mwendo gani kutoka hapa mpaka Jaisalmer?” Jackson aliuliza.

    “Ni mwendo wa siku moja mbili. Ila kwa sababu mimi ndiye nitakuwa dereva, tutatumia siku moja na nusu” Shedrack aliwaambia.

    “Mmh! Tutafanikiwa kufika muda muafaka?”

    “Sana tu. Hilo wala hautakiwi kuhofia kabisa”

    “Sawa. Baada ya hapo nini kitaendelea? Unafikiri mpakani tutaruhusiwa kuvuka pamoja nae?” Brian aliuliza.

    “Hilo si tatizo kabisa. Tukifika hapo, tunatelekeza gari na kisha kuanza kuingia porini, tutatumia njia za porini tu” Shedrack aliwaambia.

    “Mbona naona zoezi kama litakuwa gumu”

    “Hapana. Sio zoezi humu kabisa. Hili ni zoezi rahisi sana. Au unavyofikiri ugumu wake upo wapi?” Shedrack aliuliza.

    “Porini”

    “Kumbuka kwamba tuna bunduki”

    “Sawa”

    “Sasa tatizo lipo wapi?”

    “Huyu mtu ataweza kwenda na sisi kwa mwendo tunaoutaka na wakati nimesikia kwamba ni kilema?”

    “Usijali. Hata kubebwa atabebwa ili mladi afike salama”

    “Sawa. Hapo nimekuelewa. Ila bado nina swali” Jackson alimwambia Shedrack.

    “Swali gani tena?”

    “Tukifika Pakistan, nini kitaendelea? Au tutakwenda mpaka Karachi?”

    “Hapana. Karachi ni mbali sana. Kama tungetaka kutumia boti basi tungekwenda huko” Shedrack alimjibu.

    “Sasa tutaelekea wapi? Islamabad?”

    “Napo mbali sana. Kama tungekuwa tunataka kuelekea Afighanistan tungekwenda Islamabad”

    “Sasa sisi tutapitia wapi?”

    “Hapa tutaelekea Raymar na kisha kuchukua ndege ya kivita itakayokuwa kwenye kambi ya Kimarekani iliyokuwa hapo”

    “Mmmh! Lakini kabla ya kufika hapo si itatubidi tupitie Sukkur, sehemu yenye wanajeshi wa kigaidi wa kundi la Maashi?”

    “Hatutopitia huko. Tutachukua njia mojawapo ambayo inapita porini sana na kutokea Raymar. Usijali. Tutafika salama na mtu wetu” Shedrack alimwambia.

    “Kama ni hivyo, sawa”

    Mipango yote ilitakiwa kupangwa katika mchana huo, walikaa na kupanga mpaka namna ya kupata gari ambapo wangemtumia mtu yeyote kuwakodishia gari na kisha kulitumia katika kazi yao. Hawakuwa na tatizo la fedha, serikali ya Marekani ilikuwa imetoa kiasi kikubwa sana kwa ajili yao, kilichotakiwa ni kufanyika kwa kazi ambayo ilitakiwa kufanyika..

    Siku hiyo hiyo wakaamua kumtafuta kijana mmoja ambaye alikuwa tayari kuingiza kiasi cha dola elfu saba kwa kukodisha gari tu. Wala hawakupta tabu kumpata kijana huyo ambaye moja kwa moja akaelekea katika sehemu za kukodisha magari na kuchukua gari moja na kwenda nalo na kuwagawia huku wakiahidi kumrudishia baada ya saa sita.

    Usiku wa siku hiyo wakaamua kuhama hoteli na kuhamia katika hoteli nyingine ambayo ilikuwa pembezoni kidogo mwa jiji la Mumbai ili kuepuka usumbufu kutoka kwa kijana ambaye walikuwa wamemtumia kwa ajili ya kukodisha gari lile.

    “Tusipofanikiwa kumteka mtu huyu, nitaacha kazi” Mpelelezi Shedrack alisema huku akiwa na uhakika wa kumteka Abuu ambaye kwa wakati huo alionekana kuwa lulu duniani.



    *********************



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Selemani alionekana kukata tamaa baharini pale, tayari alijiona kwamba ilikuwa ni heri kufa kuliko kuendelea kupata shida baharini pale. Mikono yake ilikuwa imekosa nguvu kabisa na kwa kipindi hicho, tayari alikuwa ameuruhusu mwili wake uzame kama ambavyo wenzake walivyoamua kuzama na kufa pale baharini.

    Huku kifua kikianza kuzama chini, na hatimae mdomo nao kuanza kuzama, ghafla kwa mbali akaanza kusikia honi za meli ambayo wala hakuwa ameiona katika kipindi hicho. Selemani akashtuka, akajiona akipata nguvu na kuurudisha mwili wake juu na kulishikilia pipa lile. Akaanza kuangalia huku na kule, kwa mbali kama mita mia moja, macho yake yakaanza kuiona boti ndogo nyeupe ikielekea katika upande ambao alikuwepo.

    Selemani akaendelea kupata nguvu, tayari aliuona huo ndio kuwa ukombozi wake kutoka katika bahari ile ambayo ilikuwa imemtesa kwa siku tano. Akaanza kupunga mkono wake juu ili aonekane kwani bila kufanya hivyo, hakuona kama angeweza kuonekana na kuokolewa baharini pale.

    Boti ile ikazidi kusogea kule alipokuwa huku Selemani akiendelea kupunga mkono wake. Baada ya dakika kumi, boti ile ikafika mahali. Selemani akatupiwa boya kwa ajili ya kujivarisha makwapani na hatimae kuvutwa lakini hata nguvu za kulisogelea boya lile hakuwa nazo kwa kipindi kile.

    Ikambidi kijana mmoja miongoni mwa watu ambao walikuwa katika boti ile kujitosa majini huku akiwa amevaa boya na kisha kumshika Selemani na kuanza kuvutwa kuelekea katika boti ile ambayo iliandikwa WEST AFRICA CHRIST AMBASSADORS kwa ubavuni.

    Selemani akavutwa mpaka ndani ya boti ile na kisha kulazwa chini. Kila mmoja alibaki akimwangalia Selamani ambaye mwili wake ulikuwa ukitisha kupita kawaida. Mwili ulionekana kudhoofika kupita kawaida lakini tumbo lake lilikuwa kubwa kutokana na kunywa maji ya baharini pale. Ngozi yake ilionekana kuanza kubadilika, ukijani fulani ulikuwa umeinyemelea ngozi yake ile ambayo hali ile ilisababishwa na kukaa baharini kwa kipindi kirefu.

    Maji ya baharini yalionekana kumbadilisha kupita kawaida, mikono, miguu, kichwa na uso ndio ambao ungekufanya kugundua kwamba alikuwa binadamu. Hapo hapo wakamlaza kifudifudi na kisha kuanza kumtoa maji kwa kumkandamiza mgongoni na kisha kumpeleka bafuni na kumuogesha.

    Katika kipindi chote hicho, Selamani hakuwa na nguvu za kutosha jambo ambalo kila alipoplekwa huku, alikuwa akielekea bila kizuizi chochote kile. Baada ya kuona kwamba Selamani alikuwa salama na hivyo kupumzishwa, watu waliokuwa katika boti ile wakaanza kushikana mikono na kuanza kumshukuru Mungu kwa kila kitu.

    Huo ndio ukawa usalama wake katika kipindi hicho, kuokolewa baharini pale na watu wale ambao walionekana kuwa watumishi wa Mungu ambao walikuwa wakisafiri huku na kule kwa ajili ya kuhubiri kulimfanya kumshukuru Mungu kwa kila kitu kwani kama si wao, tayari katika kipindi hicho alikuwa amekwishakufa kama ilivyokuwa kwa wengine.









    ****











    WEST AFRICA CHRIST AMBASSADOR lilikuwa ni moja ya kundi kubwa la watu ambao walikuwa wakitoka katika makanisa mbalimbali nchi za ukanda wa Magharibi mwa Afrika kama Nigeria, Ghana, Cameruni na nchi nyingine. Kundi hili ambalo lilikuwa likiwakusanya watu wa dini ya Kikristo lilikuwa na kazi kubwa la kuhubiri katika sehemu mbalimba katika nchi za Afrika.

    Kazi ya kuhubiri kwao haikuonekana kuwa ndogo, walikuwa wakikutana na matatizo mbalimbali lakini kamwe hawakutaka kurudi nyuma. Ni kweli mara kwa mara vijana ambao walikuwa wakiingia katika kundi hilo walikuwa wakiuawa na watu wasiojulikana lakini bado watu wengi walikuwa wakiomba kujiunga na kundi hilo ambalo wala halikuwa likitulia katika nchi moja.

    Kazi yao ya kuhubiri sehemu mbalimbali ilianza kufanyika toka mwaka 1995 katika kipindi ambacho mzungu, Partrick McBeth kutoka nchini Marekani alipoamua kuanzisha kundi hilo huku akisema kwamba alikuwa ameonyeshwa maono makubwa kuhusu bara la Afrika ambalo lilikuwa limechafuka sana kwa vita hasa vya wenyewe kwa wenyewe.

    Mara baada ya Patrick kuanzisha kundi hilo ambalo lilijishughurisha na mahubiri pamoja na maombezi, msaada wa magari ukaanza kutolewa kutoka katika makanisa mbalimbali nchini Marekani pamoja na nchi nyingine ambazo zilikuwa zikitia moyo kazi ile ambayo ilikuwa ikifanyika.

    Mpaka Patrick anaufa kwa ugonjwa wa kansa mwaka 2000, tayari kundi lile lilikuwa na wanachama zaidi ya elfu saba ambao walikuwa wamegawanyika katika sehemu mbalimbali. Kundi hili ambalo lilikuwa likizidi kukua zaidi na zaidi ndilo ambalo lilikuwa likiwafanya waasi wengi kuacha mapigano yao dhidi ya serikali kama wale waasi wa Cameruni, Niger na nchi nyingine ambao waliamua kwa moyo mmoja kuweka silaha chini na kuanza kwenda kanisa.

    Kila siku kundi hili la dini lilikuwa likiendelea kufanya kazi yake kama kawaida, walisaidia watu mbalimbali kama watoto yatima na wajane ambao walikuwa wameachwa na waume zao au wazazi wao kutokana na vita ambavyo vilikuwa vikiendelea katika nchi mbalimbali barani Afrika.

    Katika kipindi hiki ambacho walikuwa ndani ya boti yao kuelekea nchini Afrika Kusini ndicho kipindi ambacho waliweza kuyaona mapipa kadhaa yakiwa umbali fulani kutoka pale walipokuwa. Kutokana na kipindi hicho vijana wengi ambao walikuwa wakitaka kuzamia kwenda nchini Marekani au katika nchi za Ulaya kushamili kwa kasi, moja kwa moja wakajua kwamba mapipa yale walikuwa wametupiwa watu ambao walikuwa wametoswa baharini.

    Hapo ndipo Keth, mkuu wa msafara ule alipoamua kuchukua darubini yake na kisha kuanza kuangalia kule kulipokuwa mapipa yale. Keth aliangalia kwa zaidi ya dakika moja, hakumuona mtu yeyote zaidi ya mapipa tu ambayo yalikuwa yakiendelea kuelea katika bahari ile.

    Kila walipotaka kuendelea na safari yao zaidi na zaidi, moyo wa Keth ukaonekana kuwa mzito kuondoka mahali pale ambapo akamtaka nahodha kupiga honi. Honi ilipopigwa, Keth akaanza kuangalia tena kwa kutumia darubini yake na kisha kumuona mtu mmoja akiwa anapunga mkono hewani jambo ambalo liliwafanya kujua kwamba kulikuwa na mtu ambaye alikuwa katika mapipa yake na hivyo kuanza kumsogelea.

    Walipofika mahali pale na ndipo wakakutana na Selamani ambaye wakamchukua na kisha kumuingiza ndani ya boti yao na safari kuendelea mbele huku wakiona kwamba katika kipindi ambacho angepata nafuu ndicho kingekuwa kipindi ambacho wangemuuliza maswali mengi zaidi juu ya kipi ambacho kilikuwa kimetokea mahali pale mpaka yeye kuwa baharini pale.











    ****









    Mipango yote ilikuwa imesukwa na kukamilika. Katika kipindi hiki ni Abuu tu ndiye ambaye alikuwa akihitajika hata kabla ya kuanza safari ya kurudi nchini Marekani. Kila kitu tayari walikuwa wamekiandaa kama kilivyotakiwa kuwa na asubuhi ya siku inayofuata ndio ilikuwa siku ambayo walitakiwa kufanya kila kitu walichotakiwa kukifanya kwa wakati huo.

    Mikono walikuwa na picha za Abuu lakini kwa kitendo cha televisheni mbalimbali duniani kumtangaza sana, picha zake zikawa zinaonekana mpaka kufikia kipindi ambacho waliona kwamba kulikuwa hakuna umuhimu wa kuwa na picha zile tena.

    Usiku wa siku hiyo, walikuwa wamekaa na kupanga mipango kabambe, walijua fika kwamba bosi wao alikuwa amewaamini sana katika kufanya kazi ile ambayo ilikuwa imeagizwa na rais wa nchi kufanyika, tena kwa haraka sana, hivyo waliona kwamba ilikuwa ni lazima kazi ifanye kwa haraka sana tena kwa umakini mkubwa kabisa.

    Asubuhi ilipoingia, moja kwa moja wakachukua kila kilichokuwa chao ndani ya hoteli ile na kisha kuanza kuelekea katika chuo cha Mumbai ambacho kilikuwa katika jiji hilo hilo. Mara baada ya kukamilisha kazi yao, hawakutakiwa kurudi hotelini, walitakiwa kuonganisha moja kwa moja na safari ya kwenda Pakistan kuanza huku wakiwa pamoja na Abuu.

    Mara baada ya kufika chuo, wakaliingiza gari lao katika eneo la chuo kile na kisha kuanza kuangalia huku na kule. Walipoona kwamba Abuu hakuwa akionekana kutoka na idadi kubwa ya watu chuoni pale kuwa wengi sana, wakaamua kumuita kijana mmoja ambaye wakamuagiza kuwaitia Abuu huku wakimkabidhi dola mia moja, kiasi cha fedha ambacho kilionekana kuwa kikubwa kwa mwanachuo yule.

    Moja kwa moja akaondoka mahali hapo na kuelekea katika majengo ya chuo ambapo baada ya dakika kumi, akawa akirudi huku akiwa pamoja na Abuu. Shedrack pamoja na Jackson wakatoka kutoka garini na kisha kuanza kumwangalia Abuu huku nyuso zao zikionyesha tabasamu pana.

    Wakaanza kuongea na Abuu ambaye alikuwa makini kuwasikiliza. Kutokana na kupata mafunzo mengi ya ushawishaji, Abuu alipoambiwa kwamba ujio wao ule ulikuwa umetoka kwa rais wa Marekani, Obama, Abuu hakuonekana kuamini kwamba kuna siku rais wa Marekani angeweza kumhitaji.

    “He wants to see you right now (Anataka kukuona sasa hivi)” Shedrack alimwambia Abuu.

    “Where is he? (Yupo wapi?)”

    “America (Marekani)” Shedrack alimjibu Abuu huku akionekana kujiamini.

    Hata walipomtaka Abuu aingie ndani ya gari wala hakubisha, akaingia garini na kisha Brian kulitoa gari lile katika mazingira ya chuo kile. Hapo ndipo ambapo safari ya kuelekea nchini Marekani kwa kupitia nchini Pakistan ilipoanza, hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuwa na wasiwasi hata kidogo, kwao, kazi ile ilikuwa ni nyepesi kupita kawaida.

    “Utakaa kiti chumba kimoja pamoja na rais wa Marekani, nafasi ambayo hata rais wa nchi yako anatamani kuipata” Shedrack alimwambia Abuu.

    “Nimefurahi kuipata nafasi hiyo. Nilikuwa na ndoto za kwenda Marekani siku moja. Naamini nitatangazwa sana na hatimae dawa yangu kumfikia kila mlengwa” Abuu alisema huku akionekana kuwa mwenye furaha, kitendo cha kuchukuliwa na kupelekwa nchini Marekani, wala hakuwa na wasiwasi nacho, moyo wake ulikuwa kwenye mapenzi ya dhati na nchi ya Marekani, hakuijutia safari hiyo.

    Safari ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Walipokuwa mjini, Brian alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida lakini mara baada ya kutoka nje ya mji, hapo ndipo kasi ya gari ile ilipoongezwa zaidi. Brian alikuwa makini barabarani, mwendo wake ulionekana kuwa wa kasi lakini kwa Shedrack, mwendo ule ulionekana kuwa mdogo sana.

    Hapo ndipo Shedrack alipomtaka Brian asogee pembeni na kisha yeye kushikilia usukukani na kuanza kuendesha gari lile. Kama alichokuwa akikisema kwamba angetumia muda mchache mpaka kufika Pakistan na ndicho ambacho kilianza kuonekana, Shedrack alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi kupita kawaida.

    Kutoka hapo Mumbai mpaka Bhopal walitumia dakika arobaini na tano wakaweza kuingia katika mji huo ambao ulikuwa na watu wengi ambao walikuwa wakiabudu sana masanamu ya Bhuddha kuliko sehemu yoyote ile nchini India, katika mji huo ndio sehemu ambayo ilikuwa ikikumbwa sana na maafa kama mafuriko na matetemeko ya ardhi.

    “Tukitoka hapa tunaingia Gandhinagal na kisha kuendelea na safari yetu kama kawaida” Shedrack aliwaambia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Umbali wa kutoka Bhopla mpaka Gandhinagal haukuwa umbali mdogo, ulikuwa ni zaidi ya kilometa elfu moja ambazo zote walitakiwa kutembea kwa mwendo wa kasi kupita kawaida. Hapo ndipo walipoamua kufanya kitu kimoja, wakawasha redio na kuanza kusikiliza kile ambacho kilikuwa kinaendelea.

    Wakapigwa na mshtuko mara baada ya kugundua kwamba Waindi walikuwa wamekwishashtuka kile kilichotokea na hivyo mipaka ilitakiwa kufungwa huku kila gari likipekuliwa kuhakikisha kwamba watu ambao walikuwa wamemteka Abuu hawavuki mipaka ya nchi hiyo.

    “Hawa wanashindwa kuelewa. Hivi tumekuteka au tunaondoka na wewe?” Brian aliuliza huku akicheka.

    “Wala hamjaniteka” Abuu alijibu.

    “Sasa mbona wanasema tumekuteka? Kama wao wangepata nafasi ya kukaa sehemu moja na rais wa Marekani wangekataa? Ebu zima redio, tusijisumbue kusikiliza siasi zao” Brian alisema huku Shedrack akizima redio ile.

    Kila mmoja alikuwa akifahamu kwamba walikuwa wakitafutwa sana na watu wa India kwa kile ambacho walikuwa wamekifanya kwa wakati huo cha kumchukua Abuu. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifahamu kwamba zaidi ya mapolisi hamsini walikuwa wakiendelea kuyapekua magari ambayo yalikuwa yakiingia Gandhinagal, mji ambao walikuwa wakiuendea kwa wakati huo.



    *******************************************-**





    Bado safari ya kuelekea Gandhnagal ilikuwa ikiendelea kwa kasi sana, Shedrack alionekana kuwa makini kupita kawaida huku kila mmoja ndani ya gari akiwa na uhakika kwamba safari ile wangefika salama nchini Marekani na kisha kumkabidhisha Abuu katika mikono ya rais wao, Obama.

    Ndani ya gari, stori za hapa na pale zilikuwa zikiendelea huku muda mwingi wakichukua nafasi ya kuisifia nchi yao kama lengo la kumfanya Abuu azidi kuvutiwa kuingia katika nchi hiyo. Moyoni mwa Abuu, hakukuwa na haja ya kuisifia nchi hiyo, kwake ilionekana kuwa kama nchi ya ndoto ambayo siku zote alikuwa akitamani kuiingia.

    Waliendelea na safari mpaka kuingia katika kijiji cha Vadodola, sehemu ambayo ilikuwa na ukame mkubwa wa maji. Baada ya kufika katika kijiji hicho ambacho wala hakikuonekana kuwa na umeme, Shedrack akalipaki gari pembeni na kisha wote kuteremka na kwenda kununua maji katika kiduka kidogo kijijini hapo na kisha kuyaweka katika sehemu ya kuwekea maji katika gari lile ambalo lilikuwa limeishiwa maji.

    Baada ya kila kitu kumalizika, wakaingia ndani ya gari na kisha safari kuendelea kama kawaida. Kila mmoja alionekana kuwa mwenye furaha, kitendo cha kutumwa kazi na raisi wa nchi halafu ukaifanikisha kilionekana kuwafurahisha kupita kawaida. Walichukua dakika hamsini kutoka hapo Vadodola mpaka kuanza kuingia katika mji wa Gandhinagal.

    Kwa mbali mbele yao, macho yao yakatua katika magari kadhaa ambayo yalikuwa yamesimama pembezoni mwa barabara huku magari zaidi ya ishirini yakiwa yamepakiwa pembeni na madereva kuhojiwa na polisi wale. Kila mmoja akashtuka, hawakuonekana kujua kama katika kipindi kile tayari polisi walikuwa katika kila kona.

    Alichokifanya Shedrack ni kulisimamisha gari lile katika foleni ya magari ambayo yalikuwa yakitembea kwa mwendo wa taratibu na kisha kuanza kufanya kile walichokuwa wakitaka kukifanya kwa wakati huo. Kitu cha kwanza, Jackson akachukua begi na kisha kulifungua, akatoa nguo kadhaa ambazo zilikuwa zikivaliwa sana na Waindi matajiri, nguo ndefu ambazo zilikuwa zikionekana kuwa kama majoho.

    Jackson hakuishia hapo, kitu kingine ambacho alikifanya mahali hapo ni kutoa ndevu za bandia pamoja na vilemba na kisha kuwagawia wenzake ambao wakaanza kuvivaa kwa pamoja tena kwa haraka haraka na kisha kutulia vitini.

    “Kuna kitu umesahau” Shedrack alimwambia jackson.

    Jackson akaonekana kuelewa Shedrack alimaanisha nini, hapo hapo akaingiza mko wake katika mfuko wa surali yake na kutoa kiasi kikubwa cha fedha na kisha kukiweka karibu kabisa na sehemu ilipokuwa usukani wa gari lile. Alipoona kwamba amekwishafanya jambo hilo, hapo hapo akachukua manukato ya bei mbaya, manukato ambayo yalikuwa yakinunuliwa na matajiri pekee nchini India kutokana na gharama yake kuwa kubwa na kisha kuanza kupulizia ndani ya gari lile.

    Abuu hakuachwa hivi hivi, kwanza gongo lake likaingizwa chini ya viti vilivyokuwa ndani ya gari lile na kisha na yeye kupewa joho moja kubwa, kilemba, ndevu za bandia na kitabu ambacho alitakiwa muda wote kukiangalia kana kwamba alikuwa akikisoma huku akiuficha uso wake.

    Wote wakaonekana kukamilika, kizuizi kikubwa ambacho kilikuwa mbele yao kikaonekana kuwa si kitu, walijiona kwamba ilikuwa ni lazima kupita katika kizuizi kile japokuwa kulikuwa na polisi wengi ambao walikuwa wakiyakagua magari yale kwa zamu.

    Foleni ikazidi kusogea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo gari lao lilipofikia zamu yake. Polisi mmoja mwanamke akaanza kulisogelea, alipolifikia tu, kioo kikashtushwa na pua yake kukutana na harufu ya manukato yale ya bei mbaya. Mpaka kufikia hatua hiyo, tayari polisi yule alijua moja kwa moja kwamba watu ambao walikuwa ndani ya gari lile walikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa na fedha nyingi nchini India.

    Hata kabla hajaongea kitu chochote kile, akaanza kumwangalia kila mtu ndani ya gari lile. Walijua kabisa kwamba macho yake yangefika katika viti vya nyuma basi angeweza kumuona Abuu, kwa kutumia akili alizokuwa nazo, kwa haraka haraka Shedrack akamuita polisi yule ambaye aliyapeleka macho yake usoni mwake.

    Shedrack akaanza kuongea kiindi kana kwamba alikuwa amezaliwa ndani ya nchi hiyo. Uwezo wake wa kuongea Kiindi ulikuwa mkubwa sana kwani lugha mbalimbali, kwake kama mpelelezi wa Kimataifa alikuwa akizifahamu kabisa tena kwa ufasaha mkubwa sana.

    Ile ikaonekana kuwa ngumu sana kwa polisi yule kujua kitu chochote kile, maneno mengi ya mfululizo ambayo alikuwa akiongeleshwa na Shedrack yakaonekana kumsahaulisha juu ya kile ambacho alikuwa amekifuata katika gari lile. Shedrack hakutaka kuishia hapo tu, alichokifanya ni kuanza kuzishika zile fedha ambazo zilikuwa karibu na usukani ule.

    Mpaka katika kipindi hicho tayari alikuwa amecheza na akili ya polisi yule kwa kiasi kikubwa sana, kila polisi alipokuwa akiongea hili, Shedrack alikuwa akiongea hili na lile tena kwa haraka haraka sana. Fedha zikaonekana kumdanganya polisi yule kwa kuamini kwamba watu ambao walikuwa ndani ya gari lile walikuwa na fedha nyingi kupita kawaida.

    Alichokifanya Shedrack ni kuchukua noti saba kati ya zile fedha ambazo alikuwa nazo mahali pale na kisha kumgawia polisi yule ambaye alizipokea kisiri, akavua kofia yake na kisha kuzitumbukiza kofiani na kisha kuivaa. Kwa sababu tayari alikuwa amechukua kiasi kikubwa cha fedha, akaona kwamba kama gari lile lingeendelea kuwa mahali pale basi polisi wengine wangekuja na hatimae kumharibia, alichokifanya ni kuwaruhusu bila kujua kwamba mtu ambaye alikuwa akitafutwa na wananchi wa India alikuwa ndani ya gari lile.

    “Kuna Afrika na Asia, maisha magumu sana. Fedha imekuwa kila kitu maishani mwao” Shedrack aliwaambia wenzake huku akicheka.

    Safari bado ilikuwa ikiendelea zaidi na zaidi na sasa hivi walikuwa wakielekea Bhilwala, Magharibi mwa nchi ya India, sehemu ambayo maisha yalikuwa ni ya shida kupita kawaida. Mwendo wao ulikuwa ni wa kasi kama kawaida, hawakutaka kupumzika sehemu yoyote ile au pale ambapo mafuta yalikuwa yakiisha na kisha kuongeza.

    Safari ile iliendelea kwa zaidi ya masaa nane na ndipo wakaanza kuingia katika mji wa Bhilwala uliokuwa katika jiji kubwa la Rajasthan. Walipofika katika mji huo, hawakutaka kuendelea na safari, walichokifanya ni kutafuta vyumba vya hoteli ambayo wala haikuonekana kuwa na hadhi kubwa na kisha kupumzika.

    Kama kawaida yao, usiku wala hawakulala, bado walikuwa wakiendelea kupanga mipango yao juu ya namna ambayo ingewawezesha kutoka ndani ya nchi ya India na kuingia Pakistan bila kukamatwa. Katika kila mpango ambao walikuwa wakiupanga katika kipindi hiki, Abuu alikuwa pamoja nao kwani hawakutaka kuacha kumshilikisha katika mambo yao, hiyo yote ilikuwa ni kuiteka saikolojia yake iikubali zaidi nchi ya Marekani.

    Mipango ikapangwa zaidi siku hiyo, njia ambazo walipanga kuzitumia zikabadilka katika kipindi hicho, kwa sasa walitaka kupitia katika miji Jodhpur na Paroj hata kabla ya kuingia nchini Pakistan. Usiku mzima walikuwa wakipanga mipango yao huku wakiwasiliana na wapelelezi wenzao ambao walikuwa nchini Marekani ambapo wakawataka wanajeshi waliokuwa katika kambi ya vita pakistan waweke ndege tayari kwa kumsafirisha Abuu kuelekea nchini Marekani, kama walivyosema, ndege ilikuwa imewekwa tayari.

    Asubuhi na mapema, safari ikaanza upya, siku hiyo walitakiwa kutembea kwa mwendo mrefu zaidi kusonga mbele mpaka kufika katika mji wa Paroj, mji ambao ulikuwa karibu na mpaka wa India na Pakistan katika upande wa Magharibi.

    “Kwa nini tusipitie New Delhi, tukaingia Punjab na kisha kuelekea katika ule mpaka ndani ya mji wa Amritsa na kisha kuingia Pakistan?” Jackson aliuliza.

    “Kule ni hatari sana. Katika mpaka ule kunakuwa na ulinzi mkubwa sana kwa sababu pako karibu na miji ya New Delhi na Punjab, sehemu ambazo zimekuwa kichocheo cha maendeleao ya India. Twendeni huku huku ambapo hakuna ulinzi wa kutosha” Shedrack alimjibu huku akiendesha gari kwa kasi kubwa.

    Safari ilendelea zaidi na zaidi, walitumia masaa kumi na saba na ndipo walipoingia katika mji wa Jodhpur ambapo wakaamua kuchukua chumba na kisha kupumzika huku kila mmoja akionekana kuchoka kupita kawaida, safari kwao ilionekana kuwa ndefu.

    Japokuwa nchini India walikuwa wametangaza kuhusiana na kutekwa kwa Abuu lakini watu ambao walikuwa wakiishi mbali na mji wa Mumbai walionekana kutokujali kabisa, kwao, kuangaikia maisha ndio ilikuwa sehemu ya maisha yao, jambo la kutaka kumwangalia barabarani kila mtu ambaye alikuwa akipita halikuonekana kuwa la maana sana, hiyo ndio sababu ambayo iliwapa urahisi Shedrack na wenzake kufika Jodhpur pamoja na Abuu kwa usalama.

    Siku ya tatu ikaingia, siku ambayo ilitakiwa kuuvuka mpaka uliokuwa katika mji wa Paroj na kisha kuingia nchini pakistan ambapo huko wangekwenda moja kwa moja mpaka katika sehemu iliyokuwa na kambi ya kijeshi ya Kimarekani na kisha kuchukua ndege ambayo ingewapeleka pamoja na Abuu mpaka nchini Marekani.

    Saa 4:09 asubuhi safari ikaanza upya. Kila mmoja akaonekana kuwa na nguvu kuendelea na safari hiyo ambayo kwao ikaonekana kuwa nzito sana. Shedrack hakutaka kuachia usukani, kila siku alikuwa akiamini kwamba yeye ndiye alikuwa dereva mkongwe na asiyekuwa na woga wowote ule katika uendeshaji wake.

    Umbali wa kutoka Jodhpur mpaka Pajor kulikuwa na umbali wa zaidi ya kilometa mia sita njiani. Ingawa hizo zilionekana kuwa kilometa nyingi lakini kwa Shedrack akataka kutumia masaa machache sana mpaka kuingia katika mji huo na kisha kuelekea sehemu ilipokuwa na mpaka. Kila mmoja ndani ya gari alikuwa akiamini kwamba Shedrack angeweza kuendesha kwa masaa chini ya saba na kuingia ndani ya mji huo.

    Barabara ilikuwa lami tupu hali iliyomfanya Shedrack kuendesha kwa mwendo wa kasi kupita kawaida kiasi ambacho mpaka wengine wakaanza kuogopa garini. Kutokana na mwendo wake kuwa mkali sana huku barabara ikionekana kunyooka, walitumia masaa matano tu wakawa wamekwishaanza kuingia ndani ya mji huo huku ikiwa ni saa tisa alasiri.

    “Tuondokeani au?”Jackson aliuliza.

    “Acha tupumzike. Tunaondoka kesho usiku kuuvuka mpaka” Shedrack alijibu.

    Wote wakakubaliana kwamba usiku wa siku hiyo ndio ambayo wangeuvuka mpaka huo na kisha kuingia nchini Pakistan. Njia ambayo walikuwa wakitaka kuuvuka mpaka huo haikuwa njia halali, wasingeweza kutumia njia halali kutokana na Abuu kutafutwa kupita kawaida, njia ambayo walikuwa wakitaka kutumia ni njia za panya tu.

    Hakukuwa na aliyebisha, kila mmoja akilini mwake akaweka kwamba ilikuwa ni lazima kupitia njia za panya na kisha kuingia nchini Pakistan huku wakiwa salama kabisa. Usiku wa siku hiyo waliendelea kuwa macho mpaka pale ilipofika saa saba na nusu usiku, muda ambao Shedrack akaliwasha gari na kisha kuondoka mahali hapo. Walitumia zaidi ya dakika arobaini na tano, kwa kutumia ramani ambayo walikuwa nayo, wakaanza kuingia porini, sehemu ambayo ilikuwa mbali na mpaka kwa zaidi ya kilometa mia mbili.

    Walikuwa garini, baadae wakaona kwamba gari halikustaili kutumika katika safari ile jambo ambalo wakaamua kuachana nalo kwani kuonekana kwa mwanga wa taa za gari lile kulionekana kuwaletea hatari kubwa. Wakaanza kutembea huku Abuu akiwa pamoja nae, wakati mwingine walikuwa wakimmbeba kwa zamu mpaka kufika katika sehemu ambayo wala hawakujua wangepita njia gani, sehemu ilionekana kuchanganya, kulikuwa na njia sita zikiwa zimejigawanya, sehemu ambayo ilikuwa ikiitwa Kurnool kwa Kihindi huku kwa kiswahili ikimaanisha Njia Panda, hasa kuanzia nne na kuendelea.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *********************************************





    Dunia ilikuwa imetetemeka kwa mara nyingine tena hasa ukiachilia kipindi kile ambacho maghorofa mawili ya biashara ya WTC yaliyokuwa nchini Marekani yalivyokuwa yamelipuka mara baada ya ndege mbili kuyagonga maghorofa hayo ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekufa mwezi wa tisa mwaka 2001.

    Tukio kama lile lilikuwa limetokea tena nchini Marekani. Moja ya daraja kubwa ambalo walikuwa wakuwa wakijivunia nalo, daraja la Brooklyn lilikuwa limegongwa na ndege ya shirika la Fly Emirates ambayo ilikuwa ikifanya safari yake ya kwenda nchini Canada.

    Mlipuko wa daraja hilo ulisababisha majonzi makubwa, magari zaidi ya elfu tatu yalikuwa yamelipuka huku mengine yakidondokea ndani ya maji jambo ambalo lilisababisha mauaji ya watu wengi. Daraja lilikuwa liwaka moto, shoti za umeme zilikuwa zikitokea katika jiji zima la New York jambo ambalo liliwafanya watu kuwa na mashaka makubwa.

    Hilo lilikuwa ni tukio la pili kutokea ndani ya miaka mitano, kilikuwa ni kilio kikubwa ambacho kilionekana kuwatonesha Wamarekani juu ya kile ambacho kilikuwa kimetokea. Serikali ya Marekani ilionekana kuchanganyikiwa, vilio vile ambavyo vilikuwa vikisikika kutoka kwao, baadhi ya nchi hasa za Kiarabu watu walikuwa wakisherekea.

    Kundi la Al Qaida lilikuwa limekwishasambaratishwa, tukio jingine na la hatari lilikuwa limetokea kwa mara nyingine nchini Marekani. Vyombo mbalimbali vya habari duniani vilikuwa vikitangaza kuhusiana na tukio lile ambalo lilionekana kuitetemeasha dunia.

    Hata kabla upelelezi haujafanyika kujua ni nani alikuwa amehusika, kundi jingine la Kigaidi la Bidar ambalo lilikuwa likipatikana nchini Afghanistan likajitokeza na kutangaza kwamba ndio lilikuwa limehusika katika mlipuko ule ambao ulikuwa ukiendeleza kuwaliza Wamarekani muda wote.

    *****

    Walibaki wakiziangalia njia zile ambazo walikuwa wamezifikia mahali hapo. Hawakuwa wakijua njia zile sita ambazo zilikuwa zikionekana mbele yao zilikuwa zikiishia mahali gani. Mioyoni mwao tayari wakahisi kwamba baadhi ya njia zile zilikuwa zinaishia sehemu mbaya na ya hatari, sehemu ambayo ingewafanya kujutia uamuzi wao wa kuzifuata njia zile.

    Hata kabla hawajaendelea mbele, wakatulia na kisha kuanza kuziangalia njia zile kwa umakini sana mpaka pale ambapo wakaamua kuifuata njia moja ambayo ilionekana kuwa nyembamba. Waliendelea kuifuata njia ile mpaka walipoliingia tena pori huku tayari ikiwa ni saa saba usiku.

    Mwendo wao ulikuwa ni wa makini sana kutaka kuvuka sehemu hiyo na hatimae kuingia katika nchi ya Pakistan. Jackson alikuwa amembeba Abuu huku Shedrack akiwa amelishika gongo lake. Sehemu ilikuwa ni ya pori kubwa huku giza likiwa kubwa mahali hapo, walikuwa wakitembea kwa tahadhali sana.

    Walitembea kwa muda wa dakika arobaini kutoka katika njia zile sita ambazo hawakuwa wakifahamu waichukue njia ipi na ndipo walipofika katika sehemu ambayo ilikuwa na eneo kama uwanja wa mpira wa miguu huku ikiwa imezungukwa na miti mingi. Kabla ya kuendelea na safari yao, wakasimama na kisha kuanza kujishauri kama ilikuwa ni salama kuvuka katika eneo lile au la. Walijifikiria kwa dakika kadhaa, Shedrack akachukua simu yake ambayo ilikuwa na uwezo mkubwa na kisha kuanza kuangalia sehemu walipo na umbali ambao walikuwa wameubakiza hata kabla ya kuingia katika nchi ya Pakistan, zilikuwa zimebakia kilometa mbili.

    “Tuvukeni” Shedrack aliwaambia.

    Hakukuwa na cha kusubiria mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kuingia katika uwanja ule na kisha kupiga hatua zaidi. Hawakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea, mara ghafla mlio wa risasi ukasikika, Brian akaanguka chini, risasi tatu zilikuwa zimeingia kifuani mwake. Milio ya risasi zile zikaonekana kuwashtua, wakachukua bunduki zao na kisha kulala chini. Walikuwa wakiangalia katika kila kona mahali pale, giza lilikuwa kubwa, hawakufanikiwa kumuona mtu yeyote yule hata kujua risasi ile ilipigwa kutoka eneo gani.

    Macho yao yalikuwa yakiangalia kwa makini katika kila eneo katikati ya miti ile, mara mianga ya bunduki ambazo zilikuwa zikitoa risasi ikaanza kuonekana machoni mwao. Kila risasi ambayo ilikuwa ikipigwa na watu hao ambao walikuwa wamejificha zilikuwa zikipiga ardhini. Shedrack na Jackson hawakutaka kukaa kimya, nao wakaanza kupiga risasi kuelekea katika sehemu zile ambazo walijua fika kwamba kulikuwa na maadui wao.

    Sehemu hiyo ikabadilika na kuwa uwanja wa vita, milio ya risasi ilikuwa ikiendelea kusikika zaidi na zaidi. Kutokana na mafunzo ya shabaha ambayo walikuwa wamepewa, Shedrack na jackson wakafanikiwa kuwaua watu kadhaa katika sehemu ambazo walilenga lakini mwisho wa kila kitu, risasi zikawaishia jambo ambalo likaonekana kuwakasirisha kupita kawaida.

    Bunduki hazikuwa na risasi, wasingeweza kuendelea kubaki mahali pale, walichokifanya ni kusimama na kisha kuanza kukimbia. Lile likaonekana kuwa kama kosa kubwa kwao, milio ya risasi ikaanza kusikika tena, risasi zile ambazo zilikuwa zikipigwa zikawaingia migongoni mwao na kujikuta wakianguka chini.

    Huo ndio ulikuwa mwisho wa kila kitu. Abuu alikuwa amebaki peke yake chini huku akitetemeka, hakujua ni wakina nani ambao walikuwa wakipiga risasi. Macho yake yakaanza kutokwa na machozi, alikuwa akitetemeka kupita kawaida.

    Ndani ya ukimya wa dakika tano, watu zaidi ya mia moja wakatoka porini kule na kisha kuanza kuelekea kule ambapo alikuwepo Abuu. Hapo akauona ule kuwa mwisho wake, alijiona kwamba zamu yake ya kuuawa ilikuwa imekwishafika mahali hapo.

    Watu wale walisogea mpaka kuile ambapo alikuwepo, walikuwa Waarabu. Bado Abuu alikuwa akitetemeka kwa hofu kubwa, katika kipindi hicho aliona kwamba muda wowote ule nae alikuwa akienda kuuawa kama ilivyokuwa kwa Shedrack na wenzake. Mara baada ya Waarabu wale kumfikia, wakavua vilemba vyao na kisha kuanza kumwangalia.

    Wakaanza kuongea kiarabu, lugha ambayo Abuu wala hakuwa akiielewa hata kidogo na kisha kumbeba mahali hapo na kuanza kuondoka nae. Maswali mengi yalikuwa yakimiminika kichwani mwa Abuu sababu ambayo ilikuwa imewapelekea Waarabu wale kumbeba na kisha kuanza kondoka nae na si kumuua kama ilivyokuwa. Hakuuliza swali lolote lile, alikuwa kimya huku akiendelea kufuatilia kuona ni kitu gani ambacho kingeendelea mahali hapo, lakini pamoja na hayo yote, woga ulikuwa umemkamata kupita kiasi.









    ****





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Al Qaida ilikuwa imekwishasahaulika katika vichwa vya watu mbalimbali duniani na sasa kundi la kigaidi la Bidar ndilo ambalo lilikuwa limeshika hatamu. Milipuko mingi ilikuwa ikitokea katika sehemu nyingi ndani ya nchi za Ulaya pamoja na watu kujitoa mhanga, kundi hili la kigaidi la Bidar likaonekana kuwa hatari hata zaidi ya kundi la kigaidi la Al Qaida.

    Kundi hili lilikuwepo toka mwaka 1988 katika kipindi ambacho kijana wa kiarabu, kijana ambaye alionekana kuwa na akili nyingi, Idrisa Mansoor alipoona kwamba alitakiwa kuanzisha kundi la kigaidi kwa ajili ya kupambana na Marekani.

    Katika miaka ya nyuma, Mansoor alikuwa amepewa mafunzo ya kijasusi na wanajeshi wa Marekani kwa lengo moja tu la kumtumia hapo baadae katika nchi zake za Kiarabu. Mipango mingi ya Marekani ilikuwa ni kwa Mansoor ambaye tayari alijiona kuwa miongoni mwa wananchi wa Marekani.

    Mansoor alikuwa akipewa kila kitu ambacho alikuwa akikihitaji kutoka kwa Wamarekani huku akiendelea kuwafanyia kazi zao kama ambavyo walikuwa wakitaka. Kwa viongozi wote wa nchi mbalimbali za Kiarabu ambao Marekani walitaka wauawe, Mansoor ndiye ambaye alikuwa akifanya kazi hiyo ambayo ilikuwa ikimlipa kupita kawaida.

    Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea katika ya Mansoor na Wamarekani kikaonekana kuwa siri kubwa mpaka pale ambapo Waarabu walipokuja kumgundua. Walichokifanya, hawakumuua bali ni kumchukua na kisha kumuweka katika chumba maalumu huku wakimtumia mwanasaikolojia mmoja ambaye alikuwa akisifika sana nchini Afghanistan na kisha kuanza kuongea na Mansoor.

    Mwanasaikolojia yule aliongea nae mambo mengi, Mansoor alikuwa makini kumsikiliza mwanasaikolojia yule ambaye alikuwa na maneno mengi yenye kuumiza ambayo yalimfanya Mansoor kuumia kila alipokuwa akimsikiliza. Maongezi yake na Mwanasaikolojia yule hayakuisha ndani ya siku moja, yalikuwa yakiendelea kila siku.

    “Kwa sababu ya Wamarekani, umeamua kumsaliti baba yako na mama yako, umeamua kuisaliti familia yao ya Kiarabu, haukutosheka, ukaanza kuwaua, unaua ndugu zako, unaiua damu yako ya kweli kwa sababu ya Wamarekani. Hebu jifikirie adhabu yako kwa Allah itakuwa ni kubwa kiasi gani kwa kuua viumbe wake ambao hawana kosa lolote, kuua uzao wa Mtume wetu Mohammad. Kama unaua uzao wako ambao ulisaidiana na Mtume wetu Mohammad kueneza dini yetu Takatifu ya Kiisalmu, nani ataeneza dini yetu? Nani ambaye atawaonea huruma watu wanaoishi katika mazingira magumu? Ni nani ambaye ataweza kuwasaidia wanawake ambao ni wajawazito? Mikono yako imejaa damu, kwa ajili ya fedha haramu, fedha zilizotoka katika mikono ya watu wasiomjua Allah. Unapolipua majengo, unasababisha moto mkubwa na mwisho wa siku kuchoma moto kitabu chetu Kitakatifu cha Koran, unapozichoma moto Koran zote, ndugu zako watasoma nini, watapata wapi muongozo ulio bora wa kumuabudu Mungu wetu na kuyasoma mafundisho aliyotugawia Mtume wetu Mohammad? Badilika, watu ambao upo nao si watu wazuri, ni watu ambao wanataka kukutumia na kisha baadae kukumaliza wewe mwenyewe” Mwanasaikolojia huyo alimwambia Mansoor.

    Hayo ndio yalikuwa maneno yake ya kila siku, mara kwa mara alikuwa akitumia muda wake kumfanya Mansoor ajutie kile ambacho alikuwa akikifanya kuwaua Waarabu na kisha kuwasaidia Wamarekani ambao walionekana kuwa maadui wakubwa wa Wamarekani. Maneno yale ambayo alikuwa akiambiwa kila siku ndio ambayo yakasababisha chuki kubwa dhidi ya Wamarekani na mataifa yote ya Ulaya.

    Tarehe 12/7/1988 ndio ilikuwa siku ambayo Mansoor akaanzisha kundi lake la Kigaidi la Badir ambalo lengo lao lilikuwa ni moja tu, kuteketeza mataifa ya Ulaya pamoja na taifa la Marekani ambalo lilionekana kuwa kwenye nguvu kubwa kipindi hicho.

    Alichokifanya Mansoor ni kutoa mafunzo kwa vijana wa Kiarabu na kisha kuwajazia hasira huku akiwatoa hofu mioyoni mwao kwamba kila kitu ambacho walikuwa wakitakiwa kukifanya, wakifanye kwa ajili ya ndugu zao, Waarabu. Vijana wa Kiarabu waliendelea kumiminika ndani ya kundi hilo ambapo baada ya mwaka mmoja, lilikuwa na vijana zaidi ya elfu kumi, vijana ambao walionekana kuwa na hasira kupita kawaida.

    “Tunaanza na kulipua kituo kikubwa cha reli nchini Uholanzi kwa kujitoa mhanga. Unapojitoa mhanga, tutaisaidia familia yako baada ya wewe kwenda kwa Allah na kisha kufarijiwa kwa kazi yako kubwa ya kuutetea uzao wa Mitume yake ambayo ilitenda miujiza hapa duniani, utafutwa jasho kwa sababu utakuwa umefanya kazi kubwa ya kujitolea katika maisha yako” Mansoor aliwaambia vijana ambao walikuwa wamepokea mafunzo ya kutosha.

    Kila kitu ambacho kilikuwa kimepangwa na ndicho ambacho kilifanyika, nchi nyingi za Ulaya zilikuwa zikizidi kulipuliwa, upelelezi ulikuwa ukifanyika lakini mwisho wa siku wakaona kwamba kundi la kigaidi la Al Quida ndilo ambalo lilikuwa limehusika katika milipuko mbalimbali japokuwa Osama alikuwa akijitetea lakini hakuweze kueleweka.

    Baada ya miaka mitano, ndipo ambapo waligundua kwamba kulikuwa na kundi jingine, kundi ambalo lilikuwa likiongozwa na Mansoor, kijana ambaye alikuwa amepewa mafunzo ya kutosha na jeshi la Marekani katika mambo yote ya ujasusi. Ile ilikuwa ni taarifa mbaya kwa Wamarekani japokuwa hawakuwahi kulipuliwa na kundi hilo la Badir.

    “Ni lazima tufanye kitu kabla mambo hayajawa makubwa zaidi” Ilisikika sauti ya Obama, rais wa Marekani ambaye alikuwa na kiu ya kulimaliza kundi hilo la kigaidi la Badir mwaka 2010.

    Wamarekani walijua fika kwamba Mansoor ndiye ambaye alikuwa akilipa nguvu kundi hilo ambalo lilikuwa likizidi kukua kila siku, walichoamua kukifanya ni kitu kimoja tu, kummaliza Mansoor. Tutammalizaje? Tutaanzia wapi? Hayo yalikuwa maswali ambayo yalikuwa yakimiminika vichwani mwa viongozi wa Kimarekani.

    Wamarekani hawakujiona kushindwa kitu kwa wakati huo, walichokifanya ni kutaka kumnyong’onyeza Mansoor kwa kumgawia ugonjwa wa kansa ambao ungemshambulia mpaka kifo chake. Walichokifanya kwa wakati huo ni kuandaa barua ambayo ilionekana kama kutumwa kutoka kwa kiongozi wa kundi la Al Qaida, Osama Bin Laden.

    Huo ulikuwa ni mwaka 1999, barua ikaandikwa na kisha kupelekwa katika chumba cha maabara ambapo ikapandikizwa virusi pamoja na bakteria wadogo ambao wote kwa pamoja wangeweza kumsababishia msomaji ugonjwa wa kansa na kisha kuandika jina la Osama na nchi aliyokuwa ametokea, Saudi Arabia na kisha kumtumia Mansoor.

    Barua ile ilipofika mikononi mwa Mansoor, akaonekana kuwa na wasiwasi mwingi kuifungua, lakini alipoona kwamba ilikuwa imetoka kwa swahiba wake wa karibu, akaamua kuifungua na kisha kuanza kuisoma. Kwake, tukio la kuifungua barua ile likaonekana kuwa tukio moja la hatari sana kulifanya kwa wakati huo, alianza kuosoma barua ile mpaka mwisho ambayo ilikuwa imeansikwa kwa lugha ya Kiarabu, katika maneno ya mwisho kabisa, yalisomeka kwa lugha ya Kingereza ‘THIS IS HOW WE KILL YOU (HIVI NDIVYO TUNAVYOKUUA) na kisha kumalizikia na jina la USA.

    Mansoor hakuonekana kuelewa maana halisi ya barua ile na maneno yale, kila alipokuwa akijifikiria yalimaanisha nini, hakuwa akijua. Alichoamua kukifanya ni kuichana barua ile huku akicheka kidharau bila kujua kwamba virusi na bakteria wenye nguvu ambao walikuwa wakiishi katika mazingira magumu walikuwa wakekwishaingia kupitia hewa na vidole vyake ambavyo alikuwa amevitumia kushika barua ile. Japokuwa alikuwa akicheka na kujiona mjanja, hakujua kwamba nchini Marekani kulikuwa na wajanja zaidi yake, wajanja ambao walikuwa wakitaka kummaliza huku akijiona..



    **********************************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Japokuwa alikuwa Muislamu ambaye alikuwa akiipenda sana dini yake lakini katika kipindi hicho Selamani hakuwa na jinsi, alikuwa akitangulizana na kundi la Kikristo la West Africa Christ Ambassador katika kila sehemu ambayo walikuwa wakielekea katika kufanya Injili barani Afrika.

    Katika kipindi hiki, mwili wake ulionekana kuwa na unafuu kutokana na kupewa dawa ambazo alikuwa amezitumia katika kipindi chote alichokuwa amekitumia kuwa pamoja na watu wale. Selemani alijua fika kwamba safari ile ya boti ile ilikuwa ikiishia katika nchi ya Afrika Kusini, nchi ambayo wala haikuwa mbali sana kutoka nchini Tanzania, alichoamua kukifanya kwa wakati huo ni kuwa bubu tu.

    Hilo lilikuwa kusudi lake, alijua kwamba kama angekuwa akiongea na kuambiwa alitoka wapi na kusema kwamba alikuwa akitokea nchini Tanzania basi angeweza kurudishwa huko lakini kama angekjifanya bubu wala asingeulizwa maswali mengi na wala asingejuliakana kama yeye alikuwa Mtanzania.

    Huo ndio ujanja ambao alikuwa ameufanya katika kipindi hicho. Selemani hakuongea, muda wote alikuwa akijifanya kuwa ni bubu. Japokuwa hali ile ilikuwa nggumu huku muda mwingine akitaka kujisahau lakini kwa asilimia mia moja aliweza kufanikiwa.

    Selemani hakuongea, kila mtu ndani ya boti ile alijua kwamba mtu ambaye walikuwa wamemuokoa katika bahari alikuwa bubu, bubu ambaye alikuwa akitaka kuzamia kwenda katika nchi za Ulaya. Ujanja huo ukaonekana kumsaidia kupita kawaida na hata meli ilipofika nchini Afrika Kusini, akawatoroka na kuanza kuingia mitaani.

    Nchi ya Afrika Kusini ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo watu wengi walikuwa wakiingia kwa ajili ya kutafuta maisha, Selemani alijua fika kwamba kama asingeweza kutorokea ndani ya nchi hiyo basi kusingekuwa na nafasi ya kuingia katika nchi nyingine Afrika ambayo ingekuwa na ajira nyingi kama nchi hiyo ambayo kwa watoto wa Kibongo walizoea kuiita kwa jina la ‘Bondeni’

    “Siondoki nchini hapa mpaka nifanikiwe. Nimekwishafika Bondeni, kuna nini tena zaidi ya kurudi nchini Tanzania nikiwa tajiri na kuwamega wakina dada kadri niwezavyo” Selemani alijisemea huku akiwa amejisahau kwamba hapo Afrika Kusini, bado kulikuwa ni Afrika kama Tanzania.









    ****









    Mishemishe za hapa na pale bado zilikuwa zikiendelea kama kawaida. Vijana wa kundi la kigaidi la Bidar bado walikuwa wakiendelea na mazoezi mazito ya kijeshi huku Mansoor akiwasimamia vilivyo. Kulipua sehemu mbalimbali za nchi za Ulaya ndio ilikuwa kazi yao kubwa mahali hapo huku matukio hayo yote yakiwa kama kuwatumia salamu Wamarekani kwamba walikuwa njiani katika kutekeleza kile walichokuwa wakitaka kukifanya.

    Katika kila tukio ambalo Bidar hawakuwa wamehusika, walikuwa wakisema wazi kwamba hawakuwa wamehusika lakini katika matukio ambayo walikuwa wamehusika, walikuwa wakisema wazi kwamba walikuwa wamehusika kwa asilimia mia moja.

    Mmarekani hakuwa ameguswa katika matukio yote ya milipuko au ya kujitoa mihanga ya vijana wa kundi la kigaidi la Bidar ila akilini mwake alijua kabisa kwamba watu hao wangeweza kuja na kuishambulia Marekani, hivyo walitakiwa kujiwekea ulinzi wa kutosha.

    Katika kipindi ambacho rais wa Marekani, Bill Clinton alipoachia madaraka kutokana na kashfa nzito ya kufanya ngono na mwanamke Monica Lewis, hapo ndipo George Bush akachukua madaraka na kukabidhiwa jukumu zito la kuweza kukabiliana na kundi la kigaidi la Bidar ambalo lilikuwa likiendelea kulipua sehemu mbalimbali katika nchi za Ulaya.

    Kazi ile haikuonekana kuwa nzito kwa rais Bush ila mara baada ya majengo ya kibiashara ya WTC (World Trade Centre) yalipogongwa na ndege za abiria ndipo ambapo masikio yake yakafunguka na kuanza kufanya kazi juu ya kile ambacho alikuwa ameambiwa kukifanya na rais aliyepita, Bill Clinton.

    Akili yake kwa wakati huo ilikuwa ikilifikiria kundi la kigaidi la Bidar ambalo bado mchakato wake mzito ulikuwa ukiendelea katika mataifa mbalimbali barani Ulaya. Magazeti yakaandika kwamba ni kundi hilo ndilo ambalo lilikuwa limefanya tukio lile lakini kiongozi wao, Mansoor akaonekana kupinga sana.

    “Hatuwezi kufanya kitu kama hicho. Zamu yenu bado” Mansoor alisikika akiongea katika vyombo mbalimbali vya habari.

    Wala hazikupita siku nyingi ndipo kundi kongwe la Al Qaida lilipojulikana kwamba lilikuwa nyuma ya kila kitu kilichokuwa kimeendelea mahali hapo huku likiwa chini ya kiongozi wao, Osama Bin Laden. Nchi ya Marekani ikaonekana kuchanganyikiwa, tayari kukawa na makundi mawili ambayo yalikuwa yameanza kuwachanganya kwa wakati huo, huku kulikuwa na Al Qaida lililokuwa likiongozwa na Osama Bin Laden na huku kukawa na kundi la Bidar ambalo lilikuwa likiongozwa na Mansoor. Mpaka katika kipindi ambacho rais Bush anaachia madaraka na kuingia Obama, bado Mansoor hakuwa amepatikana.

    Katika kipindi hicho kwa upande wa pili, hali ya Mansoor haikuwa nzuri hata mara moja. Muda mwingi alikuwa akionekana kuwa katika maumivu makali mwilini mwake. Vidole vyake tayari vilikuwa vimeanza kuharibiwa na kanza pamoja na uso wake ambao ukaanza kutafunwa na kansa iliyosababishwa na virusi pamoja na bakteria ambao walikuwa wamepandikizwa katika barua ambayo alikuwa ameandikiwa na Wamarekani.

    Hali yake ikaonekana kuwa mbaya sana kwake, vijana wake wakaanza kutafuta dawa hospitalini lakini wala hakukuwa na dawa ambayo ilikuwa imepatikana. Kansa haikuonekana kumtafuna kwa haraka sana, ilikuwa ikila taratibu sana kitu ambacho watengenezaji virusi na bakteria wale walivyotaka, walitaka kumuua huku akijiona.

    Walichokifanya ni kuanza kuwateka madaktari mbalimbali ambao walikuwa na uwezo mkubwa lakini napo haikuonekana kuwa msaada kwa Mansoor ambaye alikuwa akiteseka sana. Mateso kwake yakazidi kuongezeka kila siku, hakuwa na afadhali, kila siku alikuwa akilala kitandani kama mtu ambaye alikuwa akisubiri kifo tu.

    Mwaka wa kwanza kitandani ukapita na kuingia mwaka wa pili, hali bado ilikuwa ile ile, hakupata nafuu hata kidogo. Aliendelea kukaa kitandani kwa zaidi ya miaka kumi na ndipo hapo lilipoonekana tangazo kwamba dawa ya kansa ilikuwa imegundulika na mwanachuo mmoja ambaye alikuwa akisoma katika chuo Kikuu cha Mumbai nchini India.

    Hiyo ikaonekana kuwa taarifa nzuri kwa kila mwanakundi wa kundi la kigaidi la Bidar ambaye aliisikia, wakaonekana kurudiwa na matumani yao kwa kuona kwamba hali ya kiongozi wao ambaye walikuwa wakimpenda ingerudi na kuwa kama zamani. Kitu kilichoamuliwa ni kimoja tu, kwamba mtu huyo, Abuu alikuwa akihitajika haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kumtibia kiongozi wao, Mansoor,

    Mipango Ikapangwa rasmi kwamba kijana huyo ilikuwa ni lazima atekwe na kuletwa katika handaki ambalo kiongozi wao alikuwa akiishi katika kipindi hicho kwa ajili ya kumfanyia matibabu mpaka pale ambapo angepona na kuwa kama zamani. Walijua fika kwamba dawa zilikuwa zikiendelea kugaiwa bure lakini wao hawakutaka kwenda huko kuonana na dokta yeyote kwani sharti kubwa lilikuwa ni mgonjwa kuangaliwa na daktari ambaye alikuwa akigawa dawa hiyo.

    Mipango iliposukwa, vijana wanne wakatumwa nchini India kwa ajili ya kupeleleza juu ya Abuu. Walipofika nchini India wala hawakutaka kupoteza muda, walichokifanya ni kuanza kuelekea katika chuo hicho. Kama bahati kwao, katika kipindi ambacho walifika chuoni hapo na kuonyeshewa Abuu alipokuwa, alikuwa akiongea na wazungu ambao walikuwa wamesimama nje ya gari na kisha kuingia nao garini.

    Tukio lile likaonekana kuwashtua kupita kawaida, tayari wakaona kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo na walikuwa na uhakika kwamba watu wale walikuwa ni Wamarekani ambao walionekana kuhitaji kitu fulani kutoka kwa kijana huyo.

    Walichokifanya vijana wale ni kuanza kulifuatilia gari lile kisiri siri bila kugundulika. Hawakuishi hapo Mumbai tu, hata gari lile lilipokwenda katika miji mingine walikuwa wakiendelea kulifuatilia kama kawaida. Mpaka katika kipindi hicho walijua fika kwamba lengo la Wamarekani wale lilikuwa ni kuelekea nchini Pakistan, hiyo ilitokana na njia ambazo walikuwa wakizitumia katika wakati huo.

    Mawasiliano baina yao na vijana wengine wa kundi lao yakaanza kufanyika kwamba ilikuwa ni lazima vijana wengine watumwe kuelekea nchini Pakistan kwani kama wangewaruhusu kuingia ndani ya nchi hiyo ni lazima wangeelekea katika kambi yao ya kijeshi na hivyo kuwapa wakati mgumu na hata kumkosa mtu wao ambaye walikuwa wakimhitaji kwa kipindi hicho.

    Hakukuwa na kitu cha kuchelewa katika kipindi hicho, vijana zaidi ya mia tatu wakaanza kuelekea nchini Pakistan na kisha kukaa karibu na mipaka miwili ya kuingilia katika nchi hiyo kutokea nchini India. Mara ya kwanza walikuwa na uhakika kwamba watu hao wangeweza kupitia katika moja ya mipaka ile lakini walipoambiwa kwamba walikuwa wamekwishafika Pajor, wakajua kwamba watu hao wangetumia njia za panya kuingia nchini Pakistan.

    Hakukuwa na cha kusubiri mahali hapo, safari ya kuelekea Meerut, mji mmoja wa Pakistan ambao ulikuwa ukipakana na Pajor na kisha kuanza kusubiria mahali hapo. Wote walikuwa na uhakika kwamba watu wale wangeweza kuingia ndani ya sehemu hiyo muda wa mchana, ila walipoambiwa kwamba saa nne usiku watu hao walikuwa wameanza safari ya kuelekea katika njia za panya, watu zaidi ya mia moja wakaanza kuingia porini mule.

    “Tunachokitana ni kitu kimoja tu. Mtu wetu”

    Kwa sababu njia nyingi za panya zilikuwa zikijulikana sana, wakatafuta njia ambayo ilikuwa ikitumiwa na wafanyabiashara za magendo kutoka nchini India na kisha kujificha huku wakiona kwamba ni lazima watu hao wangepitia katika moja ya njia ambazo walikuwa wamezizingira kwa wakati huo.

    Hisia zao zilionekana kufanya kazi kwa ufasaha kabisa, saa saba usiku, kwa mbali wakawaona watu wakija, mwanga wa mbalamwezi ukaonekana kuwasaidia sana. Hawakutaka kujifikiria, wakajua moja kwa moja kwamba hao ndio wale watu ambao waliwafanya kutembea mwendo mrefu sana mpaka kufika mahali hapo kwa ajili yao, walichokifanya ni kumpiga risasi mtu mmoja na kisha mapigano ya kurushiana risasi kuanza mahali hapo.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/







    ****





    Abuu alikuwa amebebwa juu juu na kisha watu wale kuanza tena kuingia porini pamoja nae. Tayari kwa wakati huo wakajiona kuwa washindi, kitendo cha kumpata Abuu kilionekana kuwafurahisha kupita kawaida. Waliendelea kutembea mule porini mpaka pale ambapo walipoyafikia magari yao na kisha kuingia na kuanza safari ya kuelekea nchini Afghanistan.

    Serikali ya Pakistan ilikuwa ikitambua kila kitu, walikuwa wakitoa ushirikiano wa asilimia mia moja kwa kundi hilo la kigaidi kiasi ambacho iliwafanya kuchukiana na Wamarekani ambao walionekana kuwa binadamu wenye roho mbaya katika maisha yao.

    Safari kutoka nchini Pakistani mpaka nchini Afghanistan wala haikuwa safari ndefu sana, ndani ya masaa ishirini na saba wakawa wamekwishafika na hivyo kuanza kuelekea katika mji wa Qalat, sehemu ambayo ilikuwa na makazi yao, sehemu ambayo kiongozi wao, Mansoor alikuwa amejificha katika moja ya mahandaki ambayo yalikuwa yakipatiokana katika mji huo.

    Muda wote Abuu alikuwa akitetemeka kutokana na kufungwa kitambaa machoni mwake kwa kutokutakiwa kuona kitu chochote kile ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo na wala kutokupafahamu sehemu ambayo alikuwa akipelekwa katika kipindi hicho.

    Alipokuja kufunguliwa kitambaa kile, alikuwa ndani ya handaki ambalo lilionekana kutisha kupita kawaida kutokana na mwanga hafifu uliokuwa mahali pale huku mbele yake kukiwa na kitanda ambapo mwanaume mmoja mwenye ndevu nyingi alikuwa amelala, alikuwa Mansoor.





    *********************************









    Selemani alikuwa akitembea huku na huko katika jiji la Pretoria huku akiwa hafahamu aelekee wapi katika kipindi hicho. Alionekana dhahiri kuwa mgeni katika nchi hiyo, macho yake alikuwa akiyapeleka huku na kule kana kwamba alikuwa akitafuta kitu fulani kutoka mahali fulani.

    Katika kipindi hicho, kilikuwa ni kipindi cha jua kali, kipindi ambacho kilikuwa kikichukiwa sana na watu wengi wa nchi hiyo ya Afrika Kusini. Jua kali ambalo lilikuwa likiwaka ndilo ambalo likamfanya Selemani kutokwa na jasho na hivyo kuhitaji maji ya kunywa.

    Angeomba wapi maji ya kunywa na wakati asilimia themanini za nyumba ambazo zilikuwa zikipatikana katika jiji hilo zilikuwa zimezungushiwa ukuta? Selemani hakuwa na jinsi, alijitahidi kutembea zaidi na zaidi kana kwamba alikuwa akitafuta sehemu fulani ya kwenda kupumzika na kisha siku iliyofuata kuanza safari ya kwenda mahali fulani.

    Bado akili yake ilikuwa ikifikiria utajiri tu, aliamini kwamba kama angetulia ndani ya nchi hiyo basi ilikuwa ni lazima kupata fedha na hatimae kurudi nchini Tanzania akiwa tajiri mkubwa. Siku hiyo alishinda huku akitembea ndani ya jiji hilo zuri la Pretoria, hakuwa na pa kwenda wala kulala jambo ambalo lilimfanya kulala nyuma ya ukumbi wa Savannah, ukumbi ambao ulikuwa na wanawake wengi waliokuwa wakifanya biashara ya kujiuza usiku.

    Usiku kwake ulikuwa ni wa shida, midundo ya muziki ilionekana kuwa kama kero masikioni mwake ila kutokana na kuwa na usingizi mwingi machoni mwake, akalala mahali hapo.

    Saa kumi na moja alfajiri Selamani akaamka kutoka usingizini kutokana na kelele za wanawake ambao walikuwa wakigombana karibu na ukumbi huo. Selemani akasimama na kisha kuanza kuelekea katika msehemu ambayo wanawake wale walikuwa wamesimama na kisha kuanza kuwaangalia.

    Mavazi yao mafupi ambayo yaliyaacha mapaja yao wazi yakamfanya kushikwa na tamaa ya kuzidi kuwaangalia huku moyoni akijuta sababu ambayo ilimpelekea kutokuwa na fedha katika kipindi hicho. Uzuri wa wanawake wa Kizulu ambao alikuwa akiambiwa na marafiki zake ambao walikuwa wamefika nchini Afrika Kusini ndio ambao alikuwa akiuona mahali hapo.

    Wanawake wale walionekana kuvutia sana machoni mwake kiasi ambacho alibaki akiwa amesimama tu akiwaangalia. Mpaka pale ambapo mwanga unaanza kuchomoza, Selamani bado alikuwa akiwaangalia wanawake wale ambao walianza kuondoka mahali hapo.

    Selemani hakutaka kubaki katika jiji hilo, akili yake tayari ilimwambia kwamba mahali hapo hakukuwa na kazi yoyote ile hasa kwa mtu kama yeye, alihitaji kuelekea katika jiji kuu la Johannesburg. Mfukoni hakuwa na fedha za kutosha, fedha ambazo alikuwa nazo alizopewa na kundi lile la West Africa Christ Ambassador hazikuwa zikimtosha kwa sana kufanya mambo yake yote, alichoona kufaa kufanywa kwa wakati huo ni kuelekea kituoni ambapo akapanda basi na kisha kuanza kuelekea katika jiji hilo ambalo lilikuwa gumzo katika masikio ya Waafrika kutokana na uzuri wake.

    Huku akiwa ndani ya basi lile, mawazo yake yakaanza kurudi katika kipindi ambacho alikuwa nchini Tanzania hasa katika kipindi kile ambacho alikuwa pamoja na mpenzi wake, Jamala ambaye hakuwa ameonana nae toka mara ya mwisho alipoachana nae miaka saba iliyopita. Katika kipindi hicho, Selemani alikumbuka mambo mengi, kuanzia mwanzo wa mahusiano yao mpaka katika kipindi kile ambacho alikuja kukorofishana nae sababu ya ujauzito.

    Jambo lile likaonekana kumuumiza sana Selemani lakini akajiona kutokuwa na jinsi kwani hata kama angekubali kwamba ujauzito ule ulikuwa wake bado tu kungekuwa na tatizo kubwa, angeweza vipi kumtunza Jamala na wakati hakuwa na fedha zozote zile.

    Basi lilikuwa likiendelea na safari kama kawaida mpaka pale ambapo lilisimama katika kituo kimoja cha Xosario ambapo abiria kadhaa wakapanda na kisha msichana mmoja kuja kukaa katika kiti ambacho alikuwa amekaa Selemani. Mawazo ya Selemani hayakuonekana kuwa mahali hapo, alionekana kufikiria mbali kutokana na jinsi muonekano wake ulivyokuwa. Msichana yule alibaki kimya, ila baada ya kwenda kwa umbali fulani, akaanzisha mazungumzo.

    “How are you (Habari yako)” Msichana yule alimsalimia Selamani.

    Selemani akashtuka kutoka katika lindi la mawazo na kisha kuanza kumwangalia msichana yule huku akimshangaa. Msichana yule alikuwa ameachia tabasamu pana ambalo liliufanya uzuri wake kama msichana kutoka katika kabila la Xhosa kuonekana usoni mwake.

    “Sifahamu Kingereza” Selemani alimwambia msichana yule ambaye wala hakuwa akielewa kuzungumza Kiswahili japokuwa alikuwa akiielewa lugha hiyo kila ilipokuwa ikizungumzwa.

    Msichana yule akaonekana kushtuka, mshtuko wake haukuwa wa kawaida hata kidogo, hakuamini kama kweli katika kipindi hicho alikuwa amekaa kiti kimoja pamoja na Mtanzania. Akaanza kumwangalia Selemani mara mbili mbili huku akionekana kutokuamini hata kidogo.

    WaTanzania walionekana kuwa na thamani kubwa sana nchini Afrika Kusini hasa kwa wasichana kutoka katika nchi hiyo. Thamani hiyo ilikuja mara baada ya kugundua kwamba WaTanzania wengi walikuwa watu wanyenyekevu ambao katika mahusiano walikuwa wakijali huku wakionekana kuwa wazi kuwasaidia wapenzi wao na si kama ilivyokuwa kwa wanaume wa Afrika Kusini.

    Wanaume wa Afrika Kusini walikuwa wakiwategemea sana wanawake katika mambo mengi, hawakutaka kufanya kazi hata mara moja, mwanamke ndiye alikuwa kila kitu katika maisha yao. Katika mahusiano, wanaume wa Afrika Kusini walikuwa wagumu kununua zawadi kwa wanawake wao na hata kuwaonyeshea moyo wa kujali katika mapenzi hali ambayo ilikuwa tofauti sana na WaTanzania.

    Hali hiyo ndio ambayo iliwafanya wanawake wa Afrika Kusini kutamani sana kuwa pamoja na wanaume wa KiTanzania ambao katika kipindi hicho walikuwa wakimiminika ndani ya nchi hiyo kwa njia za panya. Kila msichana wa Afrika Kusini alikuwa akipenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume wa KiTanzania, mapenzi mazito pamoja na kujaliwa kwa wasichana wengine kutoka kwa wanaume wa KiTanzania ndio lilikuwa jambo ambalo liliwavutia sana wanawake wengine.

    Hapo ndipo ulipozuka uhasama mkubwa ambao umeonekana kudumu mpaka leo hii. Wanaume wengi wa Afrika Kusini wakaonekana kuchukizwa na hali ile, kitendo cha WaTanzania kusifiwa na wanawake wa Afrika Kusini kwamba walikuwa na mapenzi ya dhati kilionekana kuwakasirisha sana hali ambayo iliwapelekea kuanza kuwaua.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waafrika Kusini walitaka kubaki wao kama wao, hawakutaka mtu kutoka katika taifa jingine hapa Afrika afike katika nchi yao na kisha kuchukua wanawake wao, kwa kila Mtanzania ambaye alikuwa akijulikana kuishi na mwanamke wa Afrika Kusini, alikuwa akiuawa kinyama.

    Pamoja na mambo hayo yote, wanawake wa Afrika Kusini walikuwa na wivu mkubwa mioyoni mwao hasa pale ambapo wanafanikiwa kuwa na wanaume kutoka nchini Tanzania. Kamwe hawapendi kusalitiwa na WaTanzania, hicho kilikuwa kitu cha pili ambacho kilikuwa kikiwafanya WaTanzania wengi kuuawa nchini Afrika Kusini.

    Japokuwa WaTanzania walikuwa wakiwaonyeshea thamani na mapenzi ya dhati wanawake wa Afrika Kusini lakini bado tatizo kubwa lilikuwa pale pale, walikuwa na tamaa za kupenda kila msichana mzuri ambaye alikuwa akipita mbele ya macho yao. Hilo nalo lilionekana kuwa kosa kubwa, kwa wanawake wa Afrika Kusini walikuwa na wivu kupindukia lakini kwa wanaume wa KiTanzania kulikuwa na tamaa ya kutaka kuwa na kila msichana mrembo aliyekuwa akipita mbele yao.

    “What is your name? (Unaitwa nani?)” Msichana yule alimuuliza Selemani.

    Japokuwa lugha ya kingereza hakuwa akiifahamu lakini neno’name’ alikuwa akilifahamu vizuri hivyo akagundua kwamba mmsichana yule alikuwa akimuuliza jina lake.

    “Selemani” Selemani alijibu.

    Baada ya hapo, kila alichokuwa akiongea msichana yule hakikupewa majibu kabisa jambo ambalo likamfanya Selemani kujuta sababu ambayo ilimfanya kutokwenda shule katika kipindi cha nyuma. Msichana yule alikuwa akiongea peke yake bila kujibiwa kitu chochote kile mpaka pale ambapo wakaingia ndani ya jiji la Johannesburg.

    Selemani hakujua ni mahali gani ambapo alitakiwa kwenda kwa wakati huo, alikaa chini kwa muda mpaka pale ambapo wazo lilipomjia na kuona kwamba ilikuwa ni lazima aelekee Soweto, sehemu ambayo ilikuwa ikionekna kuwa ya uswalini kuliko sehemu yoyote nchini Afrika Kusini.

    Selamani hakujua Soweto ilikuwa upande gani na alitakiwa kupanda gari la wapi ambalo lingempeleka mpaka katika sehemu hiyo. Hakujua ni mtu gani ambaye alitakiwa kumuuliza, hakujua ni mtu gani ambaye alikuwa akiifahamu lugha ya Kiswahili.

    “Can I help you? (Naweza kukusaidia?)” Lilikuwa swali ambalo lilitoka kwa msichana yule ambaye mpaka katika kipindi hicho alionekana kuvutiwa na Selemani.

    Selemani akabaki kimya huku akimwangalia msichana yule ambaye alikuwa akiendelea kumwangalia huku akitabasamu. Selemani hakujua msichana yule alikuwa amemwambia maneno gani na hivyo alitakiwa kujibu nini, alikaa kimya kwa muda mpaka pale alipoona kwamba alitakiwa kutaja sehemu moja tu.

    “Soweto’ Selemani alimwambia msichana yule.

    Msichana yule hakuongea kitu chochote kile, alibaki akimwangalia Selemani tu ambaye alionekana kutokuwa na msaada wowote ule, alichokifanya msichana yule ni kumtaka Selemani amfuate mpaka katika sehemu iliyokuwa na kituo cha daladala na kisha kuingia ndani ya daldala ile ambayo ilionekana kuwa tofauti na hizi ambazo tunatumia Tanzania.

    Muda wote wa safari Selemani alikuwa akiangalia huku na kule, majengo marefu na mazuri ambayo yalikuwa yakionekana katika macho yake yalionekana kuyapendezesha sana mitaa ya jiji hilo ambalo lilionekana kuwa kama dhahabu kwa kila mtu aliyekuwa akiliona kwa mara ya kwanza.

    Daladala ile ilipofika katika kituo cha Metropelian, sehemu ambayo ilikuwa na nyumba nyingi za serikali ambazo zilitengenezwa katika mtindo wa ghorofa, milango ikajifungua na kisha kuteremka. Selemani bado alikuwa akiendelea kuangalia huku na kule, kila kitu ambacho alikuwa akikiona kwa wakati huo alikuwa akikishangaa.

    Bado alikuwa akizidi kumfuata msichana yule ambaye akaanza kupandisha ghorofani mpaka katika ghorofa ya nne na kisha kuufuata mlango wa chumba kimoja na kuufungua. Selemani akaingia ndani ya chumba kile. Chumba kilikuwa kwenye mpangilio mzuri ambao ulikuwa ukimfurahisha hata yeye mwenyewe, kila kitu cha muhimu ambacho kilikuwa kikihitajia ndani ya chumba kizuri kilikuwa kikipatikana ndani ya chumba kile.

    Msichana yule wala hakutaka kukaa sana, akatoka chumbani hapo na aliporudi baada ya dakika tano, alikuwa ameongozana na mwanaume mmoja ambaye akaanza kupiga hatua kumfuata Selemani.

    “Mambo vipi mwana!” Mwanaume yule alimsalimia Selemani ambaye akaonekana kushtuka.

    “Poa” Selemani aliitikia.

    “Mimi ni Mtanzania mwenzako. Huyu malaya alikuja kuniita nije nizungumze nawe” Mwanaume yule alimwambia Selemani.

    “Malaya!”

    “Yeah! Kwangu, mademu wote wa Afrika Kusini huwa ninawaita hivyo” Mwanaume yule alimwambia Selemani.

    “Amesemaje sasa?”

    “Amesema ametokea kukupenda, anataka kuishi na wewe, sijui upo tayari?” Mwanaume yule alimwambia Selamani na kumuuliza.

    “Hilo shavu mwana. Mwambie nipo tayari. Tena nipo tayari hata kuzaa nae” Selamani alimwambia mwanaume yule.

    “Poa. Wewe unaitwa nani?”

    “Naitwa Selamni”

    “Aminia mwana. Mimi naitwa Juma, ila hapa Afrika Kusini najiita Nyerere, na kila mtu anajua kwamba naitwa Nyerere, usiniite Juma hata siku moja” Nyerere alimwambia Selemani.

    “Usijali. Na wewe umepanga hapa au?”

    “Hapana. Ninaishi na malaya fulani hivi wa hapa hapa Afrika Kusini”

    “Poa mwana. Ila hilo jina sio zuri kabisa kulitumia”

    “Usikonde. Kwa hiyo demu ndio hivyo kafagilia mziki, unachotakiwa ni kumfanyia maujanja”

    “Maujanja! Kama yapi?”

    “Full kumuonyeshea unamjali, yaani kama swaga zetu za Kibongo tunazowadanganya watoto wa kike, si unazijua?”

    “Yeah!”

    “Sasa hizo ndizo wanazozipenda. Ila kuwa makini, usithubutu kuzaa nae”

    “Kwa nini?”

    “Selikali ya hapa haikuruhusu kuondoka na mtoto, anakuwa ni mali yao na anakuwa ni Mwafrika Kusini” Nyerere alimwambia Selemani.

    “Nimekuelewa kaka”

    “Poa poa. Kwa hiyo nimwambie hakuna noma?”

    “Ndio maana yake”

    “Mia mia mzeiya. Ila kuwa makini, usijidai una tamaa ya kupenda kila demu wa huku, utauawa”

    “Usiwaze mwana”

    “Poa. Ngoja nimfikishie habari. Karibu sana hapa bondeni”

    “Mia mia”

    Hapo ndipo ambapo Selamni akaanza maisha pamoja na msichana Tandi, msichana mrembo kutoka katika kabila la Xhosa. Kila wakati Tandi alionekana kuwa mwenye furaha kupita kawaida, kitendo cha kumpata mwanaume wa KiTanzania, Selemani kilionekana kumfurahisha kupita kawaida.

    Ingawa walikuwa wakiendelea kuishi pamoja kila siku kama wapenzi au mke na mume, kuna kitu kimoja Tandi hakuonekana kuwa mkweli kwa Selemani, kilikuwa ni kitu kibaya, kitu ambacho kama angeendelea kukifumbua macho basi kuna siku ambayo Selemani angeuawa ndani ya nchi ya Afrika Kusini.

    Kila siku Tandi akawa msichana wa kujifkiria kama alikuwa akitakiwa kumwambia Selemani au la ili kuyaokoa maisha yake, alipoona kwamba hakutakiwa kumwambia, akaachana nalo huku akisubiri kuona ni kitu gani kingetokea, kama Selemani kuuawa au kuendelea kuishi pamoja kwa raha na mahaba moto moto.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ********************************************



    ***** Je nini kitaendelea..??



    *****ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog