Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

A DAY TOO LONG (SIKU NDEFU MNO) - 5

 





    Simulizi : A Day Too Long (Siku Ndefu Mno)

    Sehemu Ya Tano (5)





    Ilipoishia



    Pokwane na vijana wake wakabaki wakicheka tu, hawakuonekana kuyajali maumivu aliyoyasikia Selemani. Alipoona kwamba ile haikutosha, akachukua ndoo ile, akaibeba na kisha kummwagia Selemani asidi yote mwili mzima. Ule ukaonekana kuwa mwisho wa Selemani.   



    Songa nayo sasa….

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Selemani akashtuka kutoka usingizini. Alikuwa akitetemeka kupita kawaida huku mwili wake ukiwa umeloanishwa na jasho. Akaanza kumwangalia Tandi ambaye alionekana kushtuka kipindi kirefu na wote kuangalia. Selemani hakuonekana kujiamini, akaanza kujipapasa mwili mzima.

    “Vipi tena?” Tandi alimuuliza Selemani.

    “Ndoto. Nilikuwa naota ndoto mbaya” Selemani alimwambia tandi.

    “Ndoto gani?”

    “Eti! Pokwane alitukamata na kisha kutuua. Ilikuwa ndoto mbaya sana” Selemani alimwambia Tandi na kisha wote kuanza kucheka.

    “Usiogope mpenzi. Tumekwishafika Mutare” Tandi alimwambia Selemani mara baada ya basi kufika Mutare na kisha kuangaliwa vibali vyao na kisha kuruhusiwa kuingia nchini Mozambique.





    *****





    Safari bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida, hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuwa na wasiwasi katika kipindi hicho, kila mmoja alikuwa akijua kwamba walikuwa wakienda kufika salama nchini Tanzania bila kukamatwa na mtu yeyote yule. Mara baada ya kufika mpakani Mutare, wakaonyesha vibali vyao na kisha kuruhusiwa kuingia kabisa katika nchi ya Mozambique.

    Kila mmoja alionekana kuwa na furaha, kitendo cha kuingia ndani ya nchi hiyo kiliwapa uhakika kwamba walikuwa wakielekea kufanikiwa katika mchakato mzima wa kuingia nchini Tanzania. Safari haikuishia hapo, waliendelea na safari zaidi mpaka walipofika Chimoio, hapo wakaamua kuweka kambi kwani sehemu ambayo walikuwa wakielekea ilikuwa ikizidi kuwa pori.

    Kama kawaida yao, hawakutaka kulala ndani ya gari, wakaelekea katika moja ya hoteli iliyokuwa katika mji huo mdogo hapo Mozambique na kisha kuchukua chumba. Kilichofanyika usiku kucha ni ngono tu. Mchezo huo ndio ambao ulikuwa ukiendelea kufanyika kila siku katika safari yao.

    Mpaka wanaingia nchini Tanzania, tayari walikuwa wametumia siku nne. Basi lilipofika Songea kutokea Malawi, hapo wakachukua hoteli kwani basi lilitakiwa kulala katika mkoa huo. Usiku ulikuwa ni wa furaha sana kwao, hawakuamini kama walikuwa wamekamiliasha asilimia tisini ya safari yao ndefu kutoka nchini Afrika Kusini. Ngono ndio ambayo ilikuwa imetawala katika maisha yao kipindi hicho.

    Asubuhi na mapema siku iliyofuata wakaendelea na safari yao ambapo baada ya siku moja, wakaingia ndani ya jiji la Dar es Salaam. Selemani alionekana kuwa mwingi wa furaha, hakuamini kama katika kipindi hicho alikuwa ndani ya jiji ambalo alikuwa amezaliwa, jiji la Dar es Salaam.

    Kwa sababu alikuwa mwenyeji sana jijini Dar es Salaam, hapo ndipo walipoamua kupanga chumba na hatimae kuishi pamoja. Kiasi cha fedha ambacho walikuwa nacho kilikuwa kikubwa sana, zaidi ya shilingi milioni thelathini, kilichofanyika ni kuanzisha biashara mbalimbali ambazo ziliwaingizia fedha za kutosha sana.

    Kwa kutumia fedha ambazo alikuwa nazo katika kipindi hicho, Selemani akaanza mishemishe zake za kumtafutia Tandi kibali cha kuishi nchini Tanzania huku lengo kubwa likiwa ni kuishi kwa miaka mitano na kisha kuchukua uraia wa Tanzania kwani hakutaka kurudi nchini Afrika Kusini.

    Katika kila hatua ambayo alikuwa akipitia Selemani, fedha ilikuwa ikiongea, alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha fedha mpaka pale kila kitu kilipokuwa sawa. Akampa taarifa Tandi kwamba kwa sasa alikuwa na vibali vyote vya kuishi nchini Tanzania na wala hakutakiwa kuwa na wasiwasi wowote ule.

    “Ila nimebadilisha jina” Selemani alimwambia Tandi.

    “Jina gani?”

    “Badala ya Tandi, utaitwa Siwema. Nimetaka uwe na jina la kiTanzania mpenzi” Selemani alimwambia Tandi.

    Hilo wala halikuonekana kuwa tatizo kwa Tandi, kitu ambacho alikuwa akiktaka kwa wakati huo ni kuishi nchini Tanzania tu. Jina kwake halikuwa tatizo hata kidogo, kwa macho ya haraka haraka, nchi ya Tanzania ilionekana kumvutia kupita kawaida.

    Maisha yalikuwa yamebadilika kwa Selemani, japokuwa alikuwa amepitia maisha magumu ambayo yalikuwa yamemuwekia roho mkononi lakini kwa wakati huo wala hakutaka kujali, alikisahau kila kitu ambacho kilitokea katika maisha yake.

    Hakumkumbuka tena Jamala, miaka saba iliyopita ambayo alikuwa amempa ujauzito ilikuwa mingi sana kiasi ambacho hakutaka kukumbuka kitu chochote kile na wala hakutaka kukumbuka kama katika maisha yake alikuwa amekwishawahi kuwa na msichana mwenye jina hilo.

    Katika moyo wake, katika kipindi hicho alikuwa akimfikiria mpenzi wake tu, Tandi au kwa jina la Siwema ambaye alionekana kuwa kila kitu katika maisha yake kipindi hicho. Ugonjwa wa kifua haukumuisha, mara kwa mara alikuwa akinunua dawa mbalimbali ambazo alikuwa akizitumia kila siku.

    Kutokana na kuwa na fedha za kutosha kutokana na biashara mbalimbali ambazo alikuwa akizifanya, hapo ndipo alipoamua kumuajiri dokta ambaye kila siku alitakiwa kufika nyumbani kwake na kisha kumtibia. Ushauri ambao alipewa wa kupenda kula vitu vyenye sukari ndio kidogo vikaonekana kumpa uafadhali juu ya ugonjwa wa kifua ambao ulikuwa ukimsumbua.

    Selemani akaamua kupigana kufa na kupona kutaka kuchana na uvutaji sigara ambao ulikuwa umemuathiri kupita kawaida. Kuacha kuvuta sigara halikuwa jambo jepesi kwake, ilimpasa kuingia vitani hasa. Alichoanza kukifanya ni kupunguza idadi ya sigara ambazo alikuwa akizivuta. Bada ya kuvuta sigara kumi na mbili kwa siku, akaanza kuvuta sigara saba.

    Zoezi lake hilo liliendelea kwa mwaka mzima mpaka kufikia hatua ya kuvuta sigara mbili kwa siku. Bado Selemani aliendelea kupigana vita katika uvutaji wa sigara na baada ya miezi sita, akaacha kabisa kuvuta sigara. Selemani alijiona kuwa mfungwa wa kifungo kikubwa, kitendo cha kuacha kuvuta sigara kilikuwa kikimtesa sana lakini hakuwa na jinsi. Mara kwa mara alikuwa na kiu kubwa ya kuvuta sigara lakini wala hakutaka kuanza upya kuvuta sigara.

    Kifua chake kilikuwa kimeharibika, kila wakati alikuwa akitibiwa, kwa muda fulani alikuwa akipata nafuu na katika kipindi fulani tatizo lilikuwa likirudi tena. Mwaka mwingine ukakatika na hapo ndipo Selemani alipoamua kumuoa Siwema, hakutaka kuishi nae kama mpenzi tu, aliamua kumuoa na kuishi kama mume na mke.

    Harusi ikafungwa katika nyumba nzima aliyopanga huku ustadhi Ramadhani Koba wa Tandale ndiye ambaye aliifungisha ndoa hiyo ambayo ilionekana kuwa ya furaha sana. Watu wakala na kunywa mpaka kusaza lakini hawakuweza kumaliza vyakula wala vinywaji.

    Selemani yule ambaye alikuwa mpiga debe akawa amebadilika, kwa sasa hivi hakuwa mpiga debe bali alikuwa bosi ambaye alikuwa akimiliki fedha nyingi pamoja na biashara nyingi tena zilizo kubwa nchini Tanzania.

    “Inatupasa tupate watoto kwa sasa. Au unaonaje mpenzi?” Selemani alimuuliza mkewe, Siwema.

    “Nilitaka kukwambia hivyo hivyo. Nikasahau. Afadhali umenikumbusha” Siwema alimwambia Selemani.

    Kwa jinsi mipango yao ilivyopangwa na ndivyo ilivyopangika. Wakaingia katika mchakato mzima wa kutafuta mtoto, hilo wala halikuweza kuwa tabu kwao, ndani ya miezi tisa, mambo yakajipa na hatimae mtoto wa kiume kuzaliwa na kumpa jina la Rahman.

    Rahman, kwao akaonekana kuwapa furaha kupita kawaida, mtoto huyo kwao akaonekana kuwa kila kitu katika maisha yao. Macho yao kwa wakati huo yalikuwa yakimwangalia mtoto huyo ambaye alikuwa amefanana sana na Selemani.

    “Hii ndio mboni yangu. Atakayemgusa kwa ubaya. Nitamuua” Selemani alimwambia mke wake.

    Bado maisha yaliendelea mbele. Baada ya miaka miwili, Siwema akaanza kujisikia tena tofauti tumboni mwake ambapo baada ya siku kadhaa akagundua kwamba alikuwa mjauzito. Hiyo ikaonekana kuwa furaha yao, hawakuamini kwamba walikuwa wakitarajia kupata mtoto mwingine katika kipindi hicho.

    “Hii yote ni mipango ya Mungu. Mungu wetu anaweza sana” Selemani alimwambia Siwema.

    Biashara bado zilikuwa zikiendelea kuingiza fedha, maisha yao yalikuwa yakizidi kubadilika kila siku. Fedha zikawa nyingi, wakaamua kununua nyumba maeneo ya Mbezi beach, nyumba iliyokuwa kubwa na ya thamani kupita kawaida.

    Baada ya miezi tisa, Siwema akajifungua mtoto mzuri wa kike ambaye alifuata uzuri wa mama yake. Mtoto huyo akapewa jina la Latifa, jina ambalo lilikuwa likifikirika katika kichwa cha Siwema kila siku. Watoto hao wawili wakaonekana kutosha katika kipindi hicho, wakaamua kupumzika.

    Walitumia kiasi kikubwa cha fedha katika kuhakikisha kwamba watoto hao wanapata malezi bora kuliko watoto wote nchini Tanzania. Maisha yakasonga zaidi na zaidi, miaka ikakatika mpaka inakatika miaka kumi, tayari walikuwa wamekwishashafanya mengi kwa watoto wao.

    “Kuna habari imenishtua sana” Siwema alimwambia mumewe.

    “Habari gani?”

    “Shule ya St’ Lucas wanayosoma Rahman na mdogo wake, Latifa imeteketezwa kwa moto. Ila ni vyumba viwili ndivyo ambavyo vimeteketezwa kwa moto huo” Siwema aliongea huku akionekana kuwa na wasiwasi.

    “Hiyo habari umeiona wapi?”

    “Nimeona kuna mtu kaandika kwenye mtandao wa facebook” Siwema alijibu.

    “Walimu hawajakupigia simu kukwambia chochote kile?”

    “Bado ila nil…….” Siwema alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, simu yake ikaanza kuita.

    Moyo wa siwema ukaripuka, hofu ikaanza kumuingia moyoni. Akaichukua simu yake na kisha kuangalia kwenye kioo. Jina la ‘mwalimu’ ndilo ambalo lilikuwa likionekana simuni mwake. Hata kabla hajaipokea simu ile, akayapeleka macho yake usoni mwa mume wake.

    “Nani huyo?” Selemani aliuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mwalimu wa St Lucas”

    “Hebu nipe niongee nae” Selemani alimwambia mkewe na kisha kupewa simu ile.

    Selemani aliongea na mwalimu huyo huku kila sekunde zilivyozidi kwenda mbele ndivyo ambavyo alikuwa akizidi kuwa na wasiwasi, kijasho kikawa kikimtoka, kila kitu ambacho alikisikia hakuwa akikiamini mpaka pale alipokata simu.

    “Vipi tena mume wangu?” Siwema aliuliza.

    “Mabweni yamechomwa moto. Bweni la wavulana na wasichana. Mbaya zaidi ni vyumba viwili ndivyo ambavyo vilichomwa moto. Kuna chumba ambacho alikuwa akikitumia Rahman na Latifa. Mbaya zaidi, vyumba hivyo ni watoto wawili ndio ambao wameteketezwa na moto” Selemani alimwambia mke wake, Siwema.

    Maneno yale yakaonekana kuwa kama msumali mkubwa moyoni mwa Siwema. Hawakutaka kukaa mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka mahali hapo na kuelekea katika shule hiyo ya bweni iliyokuwa Masaki huku kila mmoja akifikiria lake kichwani.

    Baada ya kufika katika shule hiyo, moja kwa moja wakapelekwa katika vyumba vile ambavyo vilikuwa vimeteketezwa kwa moto. Vyumba vilikuwa vimeteketea kupita kawaida.

    “Ilikuwaje kwanza?” Selemani aliuliza huku akilengwa na machozi.

    “Hata sisi hatujui” Mwalimu mkuu alijibu.

    “Hamjui na wakati hii ni sh…..” Hata kabla Selemani hajamaliza sentensi yake, hapo hapo akaanza kulia.

    Polisi ambao walikuwa wamefika shuleni pale wakaanza kuwanyamazisha Selemani na mkewe ambao walikuwa na uhakika kwamba watoto wao walikuwa wameteketezwa na moto vyumbani humo.

    Polisi kadhaa wakaingia ndani ya vyumba hivyo na kisha kuanza kuviangalia na baada ya dakika kadhaa kutoka huku kila mmoja akionekana kuwa na majonzi.

    “Miili yao si imekwishapelekwa hospitalini?” Polisi mmoja alimuuliza mwalimu mkuu.

    “Ndio”

    “Sawa sawa. Kwa hiyo nini kilitokea?”

    “Hatujui. Saa kumi alfajiri tulipigiwa simu kwamba shule ilikuwa ikiteketea kwa moto”

    “Mlinzi alikuwa wapi?”

    “Alikuwa getini akiendelea na ulinzi” Mwalimu mkuu alijibu.

    “Sasa mbona watoto wengine walitolewa vyumbani na kuachwa mmoja kila chumba?” Mkuu wa polisi aliuliza.

    “Hata sisi hatujui. Tumeshangaa sana hali hiyo”

    “Vyumba vyenu vimendikwa maneno yoyote ukutani?” Polisi yule aliuliza.

    “Hapana. Huwa haturuhusu mtu yeyote kuandika ukutani” Mwalimu mkuu alijibu.

    “Sasa mbona tumeona vyumba hivyo vikiwa vimeandikwa maneno?”

    “Vimeandikwa maneno! Maneno gani?”

    “POKWANE” Mkuu wa polisi alitoa jibu ambalo liliwashtua Selemani na Siwema na kuwafanya kuangaliana.



    ********************************************





    Selemani na Siwema hawakuonekana kuamini kile ambacho walikuwa wamekisikia kutoka mdomoni mwa polisi yule. Jina ambalo lilitajwa mahali hapo likaonekana kuwachanganya, wote wakajikuta wakianza kumsogelea polisi yule huku wakionekana kutaka kusikia tena jina lile likitajwa.

    “Umesema umekuta wameandika nini?” Selemani aliuliza.

    “Pokwane. Kuna kitu chochote mnafahamu kuhusiana na neno hili?” Polisi yule aliuliza.

    Wakaanza kuangaliana tena. Jina la Pokwane lilikuwa likijulikana vizuri sana katika maisha yao. Walijua fika kwamba mtu ambaye alitajwa mahali pale ndiye yule mtu ambaye alikuwa akiishi nchini Afrika Kusini. Hapo ndipo akili zao zilipofunguka na kuona kwamba japokuwa ilikuwa imepita miaka zaidi kumi lakini bado mtu huyo alikuwa na kisasi moyoni mwake, kisasi ambacho alikuwa akitamani sana kukilipiza siku moja.

    “Mnaonekana kuna jambo mioyoni mwenu. Kuna nini?” Polisi yule aliwauliza.

    Swali lile ndilo ambalo likamfanya Selemani kuanza kuelezea kila kitu ambacho kilitokea nchini Afrika Kusini bila kuficha kitu chochote kile. Stori yake ambayo alikuwa amewahadithia ikaonekana kumgusa kila aliyekuwa ameisikiliza, hata mwalimu mkuu.

    Hiyo ndio ilikuwa stori yake ambayo iliwagusa wote walioisikia. Hawakutaka kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka na kuelekea katika hospitali ya Muhimbili kwa lengo la kuangalia maiti za watoto wao ambao walikuwa wameteketezwa kwa moto ndani ya vyumba vile.

    Njiani, kila mmoja alikuwa na majonzi kupita kawaida, hawakuamini kama watoto wao, Latifa na Rahman walikuwa wameuawa kwa kuteketezwa kwa moto. Moyoni mwa Selemani, hasira ilikuwa imemjaa kupita kawaida, alionekana kukasirika kuliko siku zote katika maisha yake, kitendo cha kuona watoto wake wakiwa wamechomwa moto na mtu ambaye alikuwa akimsikia tu kilionekana kumuuma kupita kawaida.

    “Ni lazima nimuue Pokwane. Ni lazima nimuue. Hata kama nitatumia utajiri wangu wote. Ni lazima nimuue” Selemani alimwambia mke wake huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida.

    Mara baada ya kufika katika eneo la hospitali ya Muhimbili, wakateremka na kisha kuanza kuelekea katika chumba cha maiti ambapo huko wakaruhusiwa kuziona maiti za watoto ambazo zililetwa mahali saa moja lililopita. Majokofu yakafunguliwa na kisha maiti kutolewa.

    Maumivu yakaongezeka mioyoni mwao, maiti zile za watoto wale zilionekana kuwaumiza kupita kawaida. Hapo ndipo mawazo ya Selemani yakaanza kurudi nyuma toka katika kipindi ambacho alikuwa na mke wake, kipindi ambacho waliamua kupata watoto.

    Wale watoto ambao walikuwa wamewapata, leo hii walikuwa wameteketezwa kwa moto katika vyumba vya bweni shuleni kwao, St Luka, wale watoto ambao waliahidiana kuwatunza na kuwajali katika maisha yao, leo hii walikuwa wameteketezwa kwa moto, katika maisha yao yote, tukio lile likaonekana kuwauma kupita kawaida.

    “Nitaua” Selemani alisema huku akimkumbatia mke wake, Siwema.

    Mara baada ya kuziangalia maiti zile, milango ya majokofu yale yakaanza kufungwa tena na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea nje. Hata kabla hawajafika nje, ghafla Selemani akasimama na kisha kuanza kuangalia kule kulipokuwa na majokofu yale ya kuhifadhia maiti.

    “Hebu nizione tena zile maiti” Selemani alimwambia mwanaume ambaye alikuwa akihusika na uangalizi wa maiti ndani ya chumba kile.

    Kila mmoja akaonekana kumshangaa, Selemani hakuonekana kujali kitu chochote kile, kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuziona tena maiti zile. Mwanaume yule akafungua milango ya jokofu na kisha kuzitoa tena maiti zile na kuanza kuwaonyeshea.

    “Hizi ndizo maiti zilizoletwa leo?” Selemani aliuliza.

    “Ndio hizi” Mwanaume yule alijibu huku kila polisi akimsikiliza.

    “Ndio zile zilizotoka katika shule ya St’ Luka ambayo iliteketezwa alfajiri ya leo?” Selemani aliendelea kuuliza.

    “Ndio zenyewe” Mwanaume yule alijibu.

    “Hawa si watoto wangu” Selemani alisema maneno ambayo yakaonekana kumshtua Siwema.

    “Unasemaje?” Mkuu wa polisi aliuliza.

    “Hawa si watoto wangu mkuu. Hizi si maiti za watoto wangu” Selemani alisema huku akiziangalia maiti zile.

    “Una uhakika?”

    “Ndio. Hizi si maiti za watoto wangu” Selemani alimwambia.

    “Umeona nini?”

    “Watoto wangu niliwanunulia saa za chuma katika siku ambayo walikuwa wakijiunga na shule ile. Saa zao ziko wapi?” Selemani alijibu na kuuliza.

    “Inawezekana nazo zikawa zimeungua” Mkuu wa polisi alijibu.

    “Haiwezekani. Chuma kinaweza kuuangua lakini hakiwezi kuyeyuka hasa kutokana na moto ule. Hizi si maiti za watoto wangu” Selemani alisema.

    “Una uhakika hawa si watoto wako?” Mkuu wa polisi aliuliza.

    “Nina uhakika mkuu. Halafu kila nikiziangalia maiti hizi, naona vimo vimetofautiana, hawa warefu zaidi” Selemani aliwaambia huku akiziangalia maiti zile.

    “Mmmh! Wewe unaonaje?” Mkuu wa polisi alimuuliza Siwema.

    “Hata na mimi nakubaliana nae. Inawezakana hawa si watoto wetu” Siwema alitoa jibu.

    Hakukuwa na cha kufanya kwa wakati huo zaidi ya mkuu wa polisi kuchukua simu na kisha kupiga makao makuu ambapo akawataka mapolisi wa mikoa yote kuanza kufanya upekuzi katika kila magari ambayo yalikuwa yakielekea nje ya mkoa husika kwani kulikuwa na watu ambao walikuwa wamewateka watoto wawili ambao walikuwa na miaka si chini ya kumi na si juu ya kumi na tano.

    Polisi hawakutaka kuzubaa, hapo hapo msako ukaanza kufanyika. Kauli ambayo aliitoa mkuu wa polisi, Bwana Iqram Maduro ilionekana kuwa na kitisho zaidi, polisi wakaanza kufanya kama vile ambavyo walikuwa wameagizwa kufanya mahali hapo.

    “Sasa itawezekana kweli kuwakamata wahusika?” Siwema aliuliza huku akiendelea kutokwa na machozi.

    “Inawezekana kama mapolisi wataamua iwezekane” Selemani alijibu.

    “Hawawezi kuwaua?”

    “Hawawezi. Kama wangetaka kuwaua, wangewaua ndani ya kile chumba. Kama unaona hawajawaua, basi wanataka kuwateka tu. Ila huyu Pokwane, ninae. Ni lazima nimuue” Selemani aliwambia mke wake, Siwema.

    Hawakuendelea kukaa ndani ya chumba kile, walichokifanya ni kuondoka na kuambiwa kuelekea nyumbani kwao huku wakitakiwa kuwa watulivu na kama kungekuwa na taarifa yoyote ile basi wangeweza kupewa.

    “Nikae nyumbani! Hivi inawezekana kukaa nyumbani kwa amani kama watoto wangu wametekwa na sijui walipo?” Selemani alimuuliza Iqram.

    “Yeah! Fanya hivyo. Tunajua kwamba unajisikia vib……” Mkuu wa polisi, Bwana Iqram Maduro alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, simu yake ikaanza kuita, akaipokea.

    “Halllow….wapi?......Kibiti….Sawa sawa. Tupo njiani tunakuja….” Iqram alisema na kisha kukata simu.

    “Vipi?” Selemani aliuliza.

    “Polisi wa Kibiti wamesema alfajiri waliliona gari aina ya Mark II ikiwa na watoto wawili, pamoja na wanaume watatu maeneo ya Kibiti” Iqram aliwaambia.

    “Nimekwishajua”

    “Umejua nini?”

    “Watakuwa wanaelekea Afrika Kusini kupitia kusini. Safari yao itakuwa ni kwenda Lindi, Masasi mpaka Tunduru ambapo wanaweza kuingia nchini Mozambique na kisha kuingia Afrika Kusini” Selemani alimwambia Iqram.

    “Unazifahamu njia hizo?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Si hizo tu. Kutokana na maisha niliyopitia na kusumbuka kipindi cha nyuma. Ramani yote ya Tanzania iko kichwani mwangu” Selemani alijibu.

    Hawakutaka kubaki tena hospitalini hapo, walichokifanya ni kuondoka na kisha kumpeleka Siwema nyumbani.

    Selemani akateremka na kisha kuelekea ndani ya nyumba yake ambapo akachukua bunduki yake na kisha kuiweka kiunoni huku akiifunika na shati na kisha kutoka nje kwenda kwenye gari lake kulipokuwa na mapolisi wawili pamoja na mkuu wa polisi, Bwana Iqram Maduro na kisha kuanza kuondoka kuelekea Tunduru, sehemu ambayo waliamini kwamba watu wale wangeweza kuingia nchini Mozambique kwa kupitia njia za panya.

    “Naliamini Prado. Hawawezi kutuzidi” Selemani alisema huku akiliwasha gari lake aina ya Prado na kisha safari kuanza huku polisi wote wakiwa na bunduki.







    ****









    Maisha bado yalikuwa yakiendelea Afrika Kusini. Pokwane bado alikuwa akiendelea kupanga mipango ya harusi yake pamoja na Tandi ambayo ilikuwa imebakiza miezi michache kabla ya kufanyika na hatimae kuishi kama mume na mke.

    Kadri siku zilivyokuwa zikizidi kwenda mbele, mapenzi yakaonekana kuanza kubadilika, thamani ambayo alikuwa nayo kwa Tandi akaiona ikianza kushuka. Katika kipindi ambacho hawakuwa pamoja, hawakuwa akitafutwa kama ilivyokuwa zamani. Pamoja na hayo yote, katika kipindi ambacho walikuwa wakiongea, Tandi alionekana kuwa wa tofauti sana.

    Jambo lile likamuumiza sana Pokwane, hakujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea kwa mpenzi wake ambaye baada ya miezi michache angeweza kuwa mke wake wa ndoa. Kitu ambacho aliamua kukifanya Pokwane, ni kuanzisha upelelezi wa chini chini kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa nyuma ya pazia.

    Akamtuma kijana wake awe anashinda katika maeneo ya jengo lile huku akimwambia ampelelezee kila kilichokuwa kikiendelea. Ndani ya mwezi mmoja tu, akagundua kwamba Tandi alikuwa akitoka kimapenzi na mwanaume mwingine, tena alikuwa Mtanzania.

    Katika maisha yake alikwishawahi kuumizwa moyoni kwa matukio mbalimbali lakini kwa siku hiyo, aliuhisi moyo wake kuumia kupita kawaida. Kwanza hakuamini, hakuamini kabisa kama yule msichana ambaye alikuwa akimthamini sana, Tandi alikuwa ameamua kumfanyia kitendo kama kile ambacho kwake yeye alikiona kuwa cha dharau sana.

    Usiku hakuwa akilala kwa amani, mawazo yake yalikuwa yakimfikiria Tandi tu. Hata siku ambayo Tandi alikwenda kumuomba fedha kwa ajili ya kwenda kuangalia maporomoko ya maji pamoja na marafiki zake nchini Swaziland, Pokwane akaonekana kuwa na wasiwasi lakini akaamua kumpa kiasi kikubwa tu cha fedha.

    Pokwane hakuwa akifikiria fedha zake hata kidogo, kitu ambacho alikuwa akifikiria ni kuhusiana na mapenzi ambayo mpaka kufikia hatua hiyo akayaona kama kuanza kumpiga kikumbo. Kikafika kipindi, kipindi ambacho Pokwane hakutaka kuendelea kuishi na maumivu ambayo yalikuwepo moyoni mwake, alichokiamua katika kipindi hicho ni kuufanya uamuzi ambao ulikuwa mwepesi sana kwake, kumuua Selemani.

    Alichokifanya baada ya wiki moja kupita ni kuwaandaa vijana wake na kisha kuwapanga vilivyo juu ya kwenda katika vyumba alivyopanga mpenzi wake na kisha kumkamata mwanaume huyo ambaye aliamini kwamba alikuwa akiishi nae na kisha kuondoka nae na kwenda kumuua nje ya mtaa huo.

    Mipango ikapangwa na kukamilika, katika siku iliyofuata, vijana wake wanne ambao walikuwa na bunduki wakaanza kuelekea katika eneo la maghorofa ya kupanga ya serikali. Walipofika, wakaanza kulifuata ghorofa moja na kisha kupanda juu mpaka katika mlango wa vyumba alivyokuwa akiishi Tandi.

    Muda kwa wakati huo ilikuwa ni saa nne usiku, muda ambao ukimya ulikuwa umetawala sana. Wakajaribu kuufungua mlango lakini mlango ulikuwa umefungwa jambo ambalo liliwafanya kuchukua bisi bisi na kisha kuanza kufungua nati za kitasa cha mlango ule.

    Nati zote zikatoka na kisha kuendelea kufanya mautundu mengine mpaka mlango kufunguka. Wakaingia ndani huku bunduki zikiwa tayari mikononi mwao na kisha kuanza kuangalia ndani ya vyumba vile. Waliangalia katika kila kona, hakukuwa na mtu yeyote, wakafungua makabati, yalikuwa wazi bila nguo.

    Hali ile ikaonekana kuwachanganya kupita kawaida, walichokifanya ni kutoka na kisha kuanza kuelekea chini. Walipokutana na baadhi ya watu waliopanga ndani ya ghorofa lile wakaanza kuwauliza maswali.

    “Hata mimi mwenyewe leo sijamuona Tandi” Jamaa mmoja alijibu mara baada ya kuulizwa.

    “Ina maana toka asubuhi?”

    “Ndio. Au labda umuulize rafiki wa jamaa aliyekuwa akiishi nae” Jamaa mwingine aliwaambia.

    “Nani?”

    “Kuna Mtanzania ambaye anaishi ghorofa ya chini yake. Anaweza akawa anajua” Jamaa huyo alisema.

    Hawakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, walichokifanya ni kuanza kupanda ghorofani ambapo wakagonga katika chumba walichokuwa wameelekezwa na kisha Nyerere kuja kufungua mlango.

    Nyerere akauhisi moyo wake umeongeza kasi ya udundaji, akaihisi haja ndogo ikianza kumtoka. Japokuwa alikuwa akiishi Afrika Kusini, sehemu iliyokuwa na matumizi ya wazi tena ya ovyo ya bunduki lakini hakuwahi kunyooshewa bunduki.

    “Rafiki yako yupo wapi?” Jamaa mmoja aliuliza huku akionekana kukasirika.

    “Nani?” Nyerere aliuliza huku akitetemeka.

    “Korokochoocho” Risasi ikakokiwa hali iliyomfanya Nyerere kuogopa.

    “Ameondoka”

    “Kuelekea wapi?”

    “Tanzania”

    “Na nani?”

    “Na Tandi”

    “Lini?”

    “Leo asubuhi”

    “Asante kwa msaada wako. Ila haukutakiwa kutuuliza swali lolote. Kumbuka ulituchelewesha kwa kutuuliza swali moja. Chukua zawadi yako” Jamaa yule alisema na kisha kumpiga Nyerere risasi ya mguu na kisha kuondoka mahali hapo.

    Kwa haraka bila kupoteza muda wowote ule, kijana mmoja akachukua simu yake na kisha kumpigia Pokwane na kumwambia kwamba Tandi na jamaa yake walikuwa wameondoka kuelekea nchini Tanzania. Pokwane akaonekana kuchanganyikiwa kupita kawaida.

    “Nitaondoka kuelekea Mozambique. Najua nitawawahi tu” Pokwane alimwambia kijana yule na kisha kuwataka vijana wake wajiandae kwani wangeweza kuafiri kuelekea Mozambique siku inayofuata kwani vibali vingi vya kughushi walikuwa navyo.

    “Haina noma mkuu”

    “Ila anadaeni na mzigo wa kila nne. Nataka tupitie sokoni pia” Pokwane aliwaammbia akizungumzia madawa ya kulevya.

    “Hakuna neno mkuu. Mpaka kesho asubuhi kila kitu kitakuwa mzuka” Kijana yule, Mkwabi alimwambia Pokwane.

    Alichokifanya Pokwane asubuhi iliyofuata ni kwenda katika sehemu ya kituo kikubwa cha mabasi yaliyokuwa yakielekea nje ya nchi hasa Afrika Mashariki kwa ajili ya kuambiwa ratiba ya masabi yaliyoondoka juzi asubuhi na kuambiwa ni basi moja tu la scandinavia ambalo lilikuwa limeondoka kuelekea katika nchi za Afrika Mashariki siku hiyo aliyoiulizia.







    ********************************************





    Asubuhi ya siku hiyo hiyo Pokwane pamoja na vijana wake wakaanza safari ya kuelekea Mozambique kwa kutumia ndege ya shirika la Gulf Air ambalo lilikuwa likifanya safari zake katika nchi mbalimbali za Afrika na Asia. Kwa sababu mipango ya kufanya safari zake huku mizigo ya madawa ya kulevya ikiwa ndani ya ndege kuwa ndio kawaida yake tena akisafirisha bila kukatwa wala mizigo yake kupekuliwa kwa sababu alikuwa akiipitisha kiwizi, uwanjani pale aliweza kupita nayo salama kabisa.

    Ndani ya ndege, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Tandi ambaye alikuwa amelisaliti penzi lake kwa kijana wa KiTanzania ambaye aliamini kwamba alikuwa amefika nchini pale kwa ajili ya kutafuta maisha tu. Hasira zake zilikuwa zimemkaba kooni, hakutaka kuyahisi mapenzi ambayo alikuwa nayo juu ya Tandi, katika kipindi hicho, mapenzi yale yakaanza kubadilika na kuwa maumivu makali.

    Wakati mwingine Pokwane alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa, hakuamini kama Tandi, msichana ambaye alikuwa akimuamini sana ndiye ambaye alikuwa amefanya jambo lile katika siku ile. Kila wakati alikuwa akijipiga ngumi pajani kuonyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na hasira.

    Mara baada ya kufika Mozambique, kama kawaida yake mizigo yake ikapitishwa katika upande mwingine kabisa kutokana na kufanya madili ya kuuza madawa yale pamoja na baadhi ya viongozi katika nchi ile ambao walikuwa wakimuonyeshea ushirikiano mkubwa na kumlinda.

    Mara baada ya mizigo yake kufikishwa salama nje ya jengo la uwanja wa ndege kwa kupitia milango ya dharura, hapo ndipo walipokodi teksi moja ambayo waliomba iwapeleke katika moja ya hoteli kubwa hapo Mozambique.

    Hilo halikuwa tatizo, dereva akapiga gia na baada ya dakika kadhaa akapaki teksi yake nje ya hoteli moja kubwa na ya kifahari ambayo nje iliandikwa Georgia na kisha kuteremka na kuanza kuelekea katika sehemu ya mapokezi ambapo wakalipia na kupelekwa vyumbani.

    “Nataka leo hii hii uondoke mahali hapa Tseseko” Pokwane alimwambia mmoja wa vijana wake.

    “Kwenda wapi?” Tseseko aliuliza.

    “Nataka uende mpaka Lichinga, sehemu ambayo ninaamini basi lile litapita kuelekea nchini Tanzania” Pokwane alimwambia Tseseko.

    “Baada ya hapo?”

    “Utatakiwa kupanda ndani ya basi hilo” Pokwane alimwambia.

    “Basi gani sasa?”

    “Scandinavia”

    “Hayo si yapo mengi mkuu? Nitajuaje kama hili ndilo?”

    “Utajua tu. Hakuna basi lililoondoka nchini Afrika Kusini kuelekea Afrika Masharini zaidi ya basi hilo tu” Pokwane alimwambia.

    “Sawa” Tseseko aliitikia.

    “Nitakachotaka ufanye ni kitu kimoja”

    “Kitu gani bosi?”

    “Nataka ukishaingia ndani ya basi hilo, ingia nalo nchini Tanzania huku ukimfuatilia Tandi na huyo masikini wake mpaka watakapofikia na kisha njoo unipe taarifa” Pokwane alimwambia Tseseko.

    “Na kama watafikia hotelini?”

    “Hilo usijali. Nawe fikia humo hotelini. Asubuhi wakiwa wanaondoka kama kuhama, utatakiwa kuwafuata” Pokwane alimwambia Tseseko.

    “Mmmh! Nitaweza kweli bosi?”

    “Kwa nini usiweze? Kama tunaweza kuipitisha mizigo ya dawa za kulevya katika viwanja mbalimbali vya ndege utashindwa kuwafuatilia hao?” Pokwane aliuliza.

    “Sawa bosi. Nitafanya hivyo. Ila niwaue moja kwa moja au?”

    “Hiyo si kazi yako. Wewe utawaonea huruma. Niachie mimi. Ukishapajua wanapokaa, niachie mimi kila kitu” Pokwane alimwambia Tseseko.

    Mipango ikapangwa na kupangika vilivyo. Tseseko alikuwa na uhakika wa kukamilisha kazi ambayo alikuwa ameambiwa aifanye katika kipindi hicho. Alichokifanya ni kuondoka ndani ya hoteli ile kwa lengo la kuelekea Lichinga ambapo kabla ya kitu chochote kile akaelekea katika moja ya maduka ya kubadilishia fedha na kuzibadilisha fedha zake.

    Kutoka jiji la Beira mpaka Lichinga haukuwa umbali mdogo, kulikuwa na umbali wa zaidi ya kilometa elfu moja na mia tano jambo ambalo lilimchukua siku mbili tu njiani tena kwa sababu barabara haikuwa nzima kama barabara nyingine. Mpaka wanaingia Lichinga, Tseseko alikuwa amechoka kupita kawaida.

    Hakutaka kwenda kulala hotelini kwa kuhofia kwamba basi lile lingeweza kupita mahali hapo bila kufahamu, alichokifanya ni kulala hapo hapo kituoni pamoja na abiria kadhaa ambao walikuwa wakisubiri mabasi ya kwenda mikoani na nje ya nchi.

    Saa nne kamili basi la Scandinavia likaanza kuingia ndani ya kituo cha Lichinga ambapo abiria wakateremka kwa ajili ya kwenda uani. Tseseko alikuwa makini akiwaangalia abiria wote ambao walikuwa wakiteremka katika basi lile. Hakuonekana kuridhika ila baada ya kumuona Tandi akiwa pamoja na Selemani, kwake ikaonekana kuwa amani kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaanza kuwafuata mpaka katika kipindi ambacho wakaingia katika moja ya hoteli ndogo zilizokuwa mahali hapo na kisha yeye kuanza kuelekea kule kulipokuwa na basi lile. Kitu cha kwanza ambacho alikifanya ni kuanza kuongea na utingo kwamba uhitaji wake mkubwa ni kuvuka mpaka na kuingia nchini Tanzania.

    Hata utingo alipohitaji fedha, Tseseko akamgawia kiasi hicho cha fedha ambacho kilihitajika na kuruhusiwa kuingia ndani ya gari na kulala. Vibali vyote vya kizushi alikuwa navyo mifukoni mwake na vibali hivyo ndivyo ambavyo vingemfanya kuuvuka mpaka wa hapo Lichinga na kisha kuingia nchini Tanzania.

    Alfajiri ilipofika, abiria wote wakarudi ndani ya basi lile na kisha safari kuendelea zaidi na katika kipindi hicho walikuwa wakiutafuta mpaka wenyewe hasa kuanza huku katika kila kilichokuwa kikifanyika kwa Selemani na Tandi ndani ya basi lile, Tseseko alikuwa akifuatilia kwa makini.





    ****







    Pokwane alikuwa ametulia chumbani mule pamoja na kijana wake ambaye alikuwa amebakia nae, Tolxosa. Muda wote walikuwa wakipiga stori za hapa na pale japokuwa kwa Pokwane hakuonekana kuwa na furaha yoyote ile. Akili yake katika kipindi hicho bado haikuwa imetulia, alikuwa akifikiria mara nyingi kwamba Tandi alikuwa amekosa nini katika maisha yake kutoka kwake lakini hakupata jibu lolote lile.

    Walicheza karata, wakacheza kamari mpaka kuchoka na kuamua kulala huku wakiwa wamejiachia kwa kuuacha mzigo wa madawa ya kulevya chini ya meza. Saa kumi alfajiri mlango ukaanza kugonhwa, kivivu, Pokwane akaamka na kwenda kuufungua mlango, alichokutana nacho, ilikuwa ni midomo mitano ya bunduki ikimuangalia.

    Polisi wale wakamtaka watulie na wao kuingia ndani na kumuweka Tolxosa chini ya ulinzi na kisha kuanza kufanya upekuzi. Kitu ambacho walikuwa wakikitafuta mahali hapo wala hakikuwa kimefichwa, kilikuwa chini ya meza tu. Pokwane na Tolxosa wakafungwa pingu na kisha kutolewa ndani ya chumba kile huku polisi wale wakiwa wameshika mzigo ule uliokuwa na madawa ya kulevya.

    Pokwane hakutaka kujiuliza juu ya mtu ambaye alikuwa amehusika katika lile, akili yake ilimwambia kwamba kuna watu ambao alikuwa akifanya nao kazi walikuwa wamemgeuka katika kipindi hico. Maumivu ya kukimbiwa na Tandi pamoja na kuchomwa kwa polisi kwamba alikuwa na mzigo wa madawa ya kulevya vikaonekana kumchanganya akili kabisa.

    Baada ya siku kadhaa, Pokwane na Tolxosa wakapelekwa mahakamani ambapo baada ya kesi kusikilizwa vya kutosha, wakahukumiwa kwenda jela miaka kumi kila mmoja.

    Hapo ndipo machungu yalivyozidi kumkamata moyoni mwake, alijua kwamba bila Tandi kumfanyia ule mchezo mchafu basi katika kipindi hicho asingekuwa nchini Mozambique na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi. Chuki yake juu ya Tandi na Selemani ikaongezeka zaidi, alikuwa tayari kulipiza kisasi hata katika kipindi ambacho angetoka jela lakini ili mladi tu awaue Tandi na Selemani au hata kuwawekea vidonda ambavyo visingekuja kupona katika maisha yao yote.

    “Nitaua. Ni lazima niue nitakapotoka. Niombe Mungu Tseseko apafahamu watakapokuwa wanaishi” Pokwane alijisemea katika kipindi ambacho alikuwa akiingia katika mlango wa gereza kubwa ambalo lilijengwa karibu na mpaka wa Palma, sehemu ya kuingia nchini Tanzania na kufikia Mtwara.





    *****





    Maisha ya gerezani hayakuwa ya kawaida kabisa kwa watu wengine lakini kwa Pokwane yalikuwa ni ya kawaida sana ila kitu ambacho alikuwa akinyimwa ni uhuru tu. Viongozi mbalimbali wa nchi walikuwa nae kwa sababu yeye ndiye alikuwa mzizi wa uuzwaji wa madawa ya kulevya ambayo yalikuwa yakifanyika sana katika nchi za Kusini mwa Afrika.

    Kila siku alikuwa akiletewa magazeti, alikuwa akiangalia televisheni pamoja na kupata vitu vingine katika maisha yake ya gerezani. Jina lake lilikuwa kubwa, wafungwa wengi walikuwa wakimuogopa kwani walijua fika kwamba mtu huyo alikuwa na nguvu nyingi.

    Kila siku mawazo ya Pokwane yalikuwa ni kumfikiria Tandi ambaye alikuwa amemuacha katika kipindi kibaya sana, kipindi ambacho wangeweza kuoana na hatimae kuwa mume na mke. Bado moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, alijua fika kwamba Tandi ndiye ambaye alikuwa amesababisha yale yote mpaka kuwa ndani ya gereza hilo siku hiyo.

    Katika kipindi chake cha miezi mitatu ndani ya gereza lile ndipo ambapo alipokea ugeni wa Tseseko ambaye alifika mahali hapo na kumwambia kwamba alikuwa amekwishapafahamu mahali ambapo Tandi na Selemani walipokuwa wamehamia nchini Tanzania.

    Kwa Pokwane ikawa kama faraja kwa kuona kwamba jambo ambalo alitakiwa kulifanya mbele ya safari yake wala halikuwa kubwa, alichokuwa akimuomba Mungu ni amlinde mpaka katika kipindi ambacho angetoka gerezani.

    Mwaka wa kwanza ukakatika, wa pili ukaingia, mwaka wa tatu mpaka miaka mitano ikakatika, bado Pokwane alikuwa gerezani akikitumikia kifungo chake cha miaka kumi.

    Miaka iliendelea kukatika mpaka katika kipindi ambacho miaka kumi ilipotimia na ndipo alipotolewa gerezani. Mazingira mengi ya nchi ya Afrika kusini yalikuwa yamebadilika jambo ambalo lilikuwa likimshangaza sana. Muda mwingi alikuwa akiyaangalia majengo makubwa ambayo yalikuwa yamejengwa huku barabara zikiwa ni za kisasa tofauti na kipindi kile.

    Katika sehemu hiyo, Pokwane alikuwa amefuatwa na mwanaume mmoja aliyekuwa na ndevu nyingi ambaye alikuwa katika gari la kifahari. Mara baada ya macho yake kutua usoni mwa Pokwane, mwanaume yule akateremka kutoka garini na kisha kumfuata na kumkumbatia.

    Walipomaliza kusalimiana kwa furaha, wakaelekea katika gari lile la kifahari na kisha kuanza safari ya kuelekea nchini Afrika Kusini kutoka hapo nchini Mozambique. Ndani ya gari, kila mtu alikuwa muongeaji kupita kawaida huku Pokwane akiuliza maswali kadhaa kuhusiana hali ambayo ilikuwa ikiendelea nchini Afrika kusini.

    Walichukua muda wa siku moja na ndipo wakaingia katika nchi ya Afrika Kusini. Pokwane akabaki na mshangao mkubwa, hakuamini kama nchi ya Afrika Kusini ilikuwa imejengeka namna ile ndani ya kipindi cha miaka kumi kukaa gerezani.

    “Jamaa amechukua fomu bwana nae anataka kugombea urais” Mwanaume yule aliyakuwa akijiita Nebu alimwambia Pokwane.

    “Jamaa gani?”

    “Zuma”

    “Acha utani bwana”

    “Ndio hivyo. Na sisi tunataka tumsimamishe mtu wetu ashindane nae” Nebu alimwambia Pokwane.

    “Tutashinda kweli?”

    “Kwa nini tusishinde? Tutatumia kila aina ya wizi wa kura mpaka tunashinda” Nebu alimwambia Pokwane.

    Japokuwa walikuwa wakiongea mambo mbaliimbali lakini Pokwane hakuacha kuyaangalia majengo makubwa na marefu ambayo yalikuwa yamejengwa katika kipindi alichokuwa gerezani. Mambo mengi yalionekana kubadilika, nchi ya Afrika kusini ilikuwa na muonekano mwingine kabisa.

    Nebu na wazee wenzake ndio ambao wakaamua kuwa pamoja na Pokwane katika kila kitu ambacho alikuwa akikihitaji. Alichokifanya Pokwane mara baada ya wiki kadhaa ni kuwasiliana na Tseseko na kisha kumwambia juu ya mpango wake ambao alikuwa akitaka kuufanya, mpango ambao ulikuwa umedumu katika moyo wake kwa muda wa miaka kumi.

    “Inatupasa twende. Bado nina hasira na wale watu” Pokwane alimwambia Tseseko.

    Baada ya wiki kupita, wakaanza safari ya kuelekea nchini Tanzania. Katika kipindi hicho walikuwa wakitumia ndege ambayo baada ya kutua katika uwanja wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere wakaanza kutoka katika ndege ile na kisha kuingia ndani ya jengo la uwanja huo ambapo mizigo yao ikachunguzwa na kisha kuruhusiwa.

    Katika kipindi hicho mawazo ya Pokwane yalikuwa juu ya Tandi, mwanamke ambaye alikuwa amemuachia jeraha kubwa la mapenzi ndani ya mwili wake. Wakachukua teksi ambayo iliwapeleka mpaka katika hoteli ya New Africa na kisha kuchukua chumba.

    “Unapajua wanapoishi?” Pokwane alimuuliza Tsetseko.

    “Nadhani naweza kupakumbuka. Hatuwezi kupata huduma ya internet sehemu?” Tseseko alimuuliza Pokwane.

    “Nadhani hapa kuna uhitaji wa kompyuta ya mapajani. Kuna huduma ya internet ambayo haitumii waya” Pokwane alijibu.

    “Sawa. Ngoja nikaongee na wahudumu kama tunaweza kupata kompyuta hiyo” Tseseko alimwambia Pokwane na kisha kuinuka na kuanza kwenda nje.

    “Unaelekea wapi?”

    “Kwa mhudumu”

    “Achana nae. Tutatumia hata simu yangu” Pokwane alisema.

    Alichokifanya Pokwane ni kuionganisha simu ile na huduma ya internet bila kutumia waya (wireless) na kisha kumgawia Tseseko simu ile ambayo akaanza kufungua katika akaunti yake ya Yahoo.

    “Kuna nini humo”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Niliyahifadhi majina katika akaunti yangu ya Yahoo” Tsese alijibu.

    “Majina ya nini?”

    “Ya sehemu wanapoishi”

    Pokwane akabaki kimya na kumwangalia Tseseko ambaye alikuwa akiendelea kufanya kile ambacho alikuwa akitaka kukifanya katika simu ile. Alikaa nayo huku akiendelea na kazi yake kwa muda wa dakika kumi na ndipo uso wake ukaanza kuonyesha tabasamu. Akasimama na kuelekea katika meza ndogo ambayo ilikuwa ndani ya chumba kile na kisha kuchukua kalamu na karatasi na kurudi kitandani.

    “Hapa. Ni sehemu hii inayoitwa Magomeni Mapipa nyumba namba 788” Tseseko alimwambia Pokwane huku akiwa ameandika sehemu ile katika karatasi yake.

    Siku iliyofuata, wakampigia simu dereva ambaye alikuwa amewaleta hotelini hapo na kisha kuja kuwachukua na kumtaka kuwapeleka Magomeni Mapipa. Tofauti na kipindi kile cha nyuma, katika kipindi hiki nyumba zilikuwa nyingi kupita kawaida, ila kwa sababu walikuwa na namba ya nyumba hiyo, dereva akawasaidia kuitafuta mpaka pale walipoipata na kisha dereva kwenda kuanza kuongea na wanawake waliokuwa kibarazani huku wao wakiwa garini.

    “Samahanini” Dereva aliwaambia wanawake waliokuwa kibarazani mara baada ya kuwasalimia.

    “Bila samahani”

    “Kuna mtu namtafuta anaitwa Tandi, sijui mnamfahamu?” Dereva yule aliwauliza.

    “Tandi! Ndiye nani?” Mwanamke mmoja aliuliza.

    “Mwanamke mmoja aliishi mahali hapa miaka kumi iliyopita na mwanaume wake” Dereva yule, Salum alisema.

    “Mmmh! Sisi unaotuona hapa wote ni wa juzi juzi tu, labda uongee na mwenye nyumba” Mwanamke mmoja alimwambia Salumu.

    “Mwenye nyumba yupo?”

    “Amejaa tele. Pita ndani kwenye chumba cha nne mkono wa kushoto” Mwanamke huyo alimwambia Salumu ambaye akapita ndani mpaka kwenye mlango wa chumba kile na kisha kuanza kugonga.

    Wala hazikupita sekunde nyingi, mwanaume mmoja mwenye ndevu nyingi nyeupe akatokea mlangoni hapo na kisha kuannza kumwangalia Salumu ambaye alikuwa akionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa.

    “Nikusaidie nini?” Mzee huyo aliuliza mara baada ya salamu.

    “Namuulizia dada yangu”

    “Dada yako! Nani?”

    “Anaitwa Tandi. Aliwahi kuishi ndani ya nyumba hii miaka kumi iliyopita” Salum alimwambia mzee yule ambaye akainamisha kichwa chake chini.

    “Alikuwa akiishi na nani?”

    “Na mwanaume wake”

    “Anaitwa nani?”

    “Wala simfahamu”

    “Itakuwaje haumjui mwanaume aliyekuwa akiishi na dada yako?”

    “Alitoroka nyumbani kwetu”

    “Nyumbani kwenu wapi?”

    “Musoma”

    “Sawa. Miaka kumi iliyopita ndani ya nyumba hii kulikuwa na mpangaji mmoja tu, aliitwa Selemani na mke wake, Siwema. Huyo Tandi wala simfahamu” Mwanaume yule alimwambia Salumu.

    “Hapana. Yeye anaitwa Tandi”

    “Huyo simfahamu”

    “Na huyo Siwema ndiye nani? Yule mke wa tajiri Selemani?” Dereva yule aliuliza.

    “Ndiye huyo huyo”

    “Nashukuru. Asante sana” Salumu alisema na kisha kuanza kutoka ndani ya nyumba ile. Alipofika nje, akawaaga wale wanawake ambao walikuwa wamekaa kibarazani na kisha kuingia garini.

    “Kumbe mlikuwa mnamuulizia Siwema?” Salumu aliuliza huku akionekana kutabasamu.

    “Hapana. Hatukusema Siwema. Tulikwambia Tandi” Pokwane alimwambia Salumu.

    “Sikilizeni. Huyo Tandi mnayemuulizia ni mwanamke ambaye ana asili ya Afrika Kusini, ana kidoti hapa juu ya pua yake. Si ndio?” Salumu aliuliza.

    “Ndiye huyo huyo”

    “Huyo ni Siwema na si Tandi kama mlivyosema” Salumu aliwaambia.

    “Mmmh!” Tseseko aliguna.

    “Inawezekana akawa amebadilisha jina. Kama unamjua naomba utupeleke anapoishi” Pokwane alimwambia Salumu.

    “Huwezi kuonana nae. Mwanaume wake ana pesa hatari. Nyumba yake haisogelewi hata mara moja”

    “Sawa. Ila unaweza kutupeleka?”

    “Hakuna noma”

    “Anaishi wapi?

    “Mbezi Beach” Salumu alisema na kisha kuwasha gari na safari ya kuelekea Mbezi Beach kuanza.





    ******************************************







    Safari ya kuelekea Mbezi Beach bado ilikuwa ikiendelea. Pokwane na Tseseko walionekana kufurahi kupita kawaida kwani tayari walikwishaona kwamba kwa wakati huo hakukuwa na tatizo lolote lile kwani dereva yule, Salum alikuwa akiifahamu sehemu ambayo alikuwa akiishi Tandi, msichana ambaye walikuwa wamekuja nchini Tanzania kwa ajili ya kumuua tu.

    Dereva taksi, Salum alikuwa na uhakika kwamba kwa wakati huo angeweza kupata kiasi kikubwa cha fedha kutokana na wateja wake hao ambao walikuwa wanaendelea kumtumia katika safari za hapa na pale. Kwa Salumu, katika kichwa chake alikuwa akifikiria fedha tu, tayari alijiona kuingiza kiasi kikubwa cha fedha endapo angekamilisha kile ambacho watu wale walikuwa wakikihitaji.

    Kwake, watu wale walionekana kuwa wema, hakufikiria hata mara moja kama watu wale walikuwa ni watu wabaya, watu ambao walikuwa wakimtafuta Tandi kwa lengo la kumuua pamoja na mume wake, Selemani ambaye alionekana kuwa ndio chanzo cha Tandi kuhamia nchini Tanzania baada ya kutoroka nchini Afrika Kusini.

    Safari iliendelea zaidi mpaka kufika katika mtaa ambao alikuwa akiishi Tandi, hata kabla ya kuisogelea nyumba ile, tayari walikwishaona tangazo kwamba hakukuwa na gari lolote lile ambalo lilikuwa likiruhusiwa kuegeshwa karibu na nyumba ile. Salumu hakuonekana kuwa na wasiwasi, alichokifanya ni kuwaonyeshea kwa kidole nyumba ile.

    Pokwane na Tseseko wakataka kupita karibu na nyumba ile, Salumu akafanya kama vile ambavyo alitakiwa kufanya. Moyoni mwa Pokwane kukawa na maumivu makubwa, tayari akili yake ilikwishamwambia kwamba kiasi cha fedha ambacho alimgawia Tandi ndicho ambacho kilikuwa kimemfanya kuwa na maisha yale ambayo alikuwa nayo katika kipindi kile.

    Katika kipindi ambacho teksi ile ilipokuwa ikipita karibu na nyumba ile, Pokwane akaonekana kuumia kupita kawaida, moto ukaonekana kuwaka moyoni mwake huku maumivu hayo yakisindikizwa na msumali uliokuwa na ncha kali ambao uliuchoma moyo huo. Mpaka wanaipita nyumba ile ambayo ilionekana kuwa na walinzi wawili waliokuwa na bunduki mikononi mwao, Pokwane alikuwa amekwishaumia vya kutosha.

    Salumu akakata kona na kuingia katika mtaa mwingine, huko, Pokwane akaanza kumuuliza maswali juu ya Tandi ambaye alionekana kubadilisha jina kwa wakati huo na kuitwa Siwema.

    “Mume wake ni tajiri mkubwa sana. Ana biashara nyingi za mitaji mikubwa kupita kawaida. Serikali inameshimu sana kwani amekuwa mtu wa kutoa sana misaada” Salumu aliwaambia huku akiwa hajui lengo walilokuwa nalo watu hao ambao alikuwa akiwaambia.

    “Sasa jamaa utajiri aliupata vipi?” Pokwane alimuuliza Salumu.

    “Jamaa alikuwa amezamia Afrika Kusini. Huko ndipo alipoupata utajiri wenyewe. Kwanza ile kushuka Tanzania, akashuka na demu mkaliiiiii…hiyo ilikuwa enzi hizo. Maisha yake yamebadilika bwana, huwezi kuamini kama ndiye yule jamaa ambaye zamani alikuwa mpiga debe barabarani” Salumu aliwaambia.

    “Dah!” Sasa tunaweza kumpata mke wake kweli?” Pokwane aliuliza.

    “Utamuona wapi? Utampata muda gani? Ni rahisi sana kuonana na rais wa nchi hii kuliko watu wa familia ile. Hawaonekani ovyo” Salumu aliwaambia.

    “Kwa hiyo haitowezekana kabisa?”

    “Haiwezekani hata kwa asilimia moja. Matajiri nchini hapa wamekuwa watu adimu sana kuonekana machoni mwa watu” Salumu aliwaambia.

    “Kwa hiyo hilo ni gumu sana?”

    “Kiukweli hilo ni gumu sana” Salumu aliwaambia.

    Hiyo ikaonekana kuwa habari mbaya katika masikio yao. Hawakuamini kama kweli safari ile ya kuelekea nchini Tanzania ingewafanya kutokukamilisha kile ambacho kiliwapasa kukamilisha. Wote wakakaa kimya kwa muda huku wakijifikiria ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya.

    Hakukuwa na kitu ambacho walitakiwa kukifanya zaidi ya kumwambia ukweli Salumu juu ya kile ambacho kilikuwa kimewaleta nchini Tanzania. Habari ile ambayo aliambiwa Salumu ikaonekana kumshtua sana lakini kwa sababu aliwaambia kwamba angeifanya siri huku akilipwa kiasi cha shilingi milioni moja na nusu katika kila siku ambayo angekuwa pamoja nao, hakuwa na jinsi, aliahidi kuwa siri moyoni mwake.

    “Kwa hiyo wewe utatusaidia vipi?” Pokwane alimuuliza Salumu.

    “Mmmh! Kuwapata wao ni ngumu sana” Salumu aliwaambia.

    “Hakuna njia yoyoyte ile ambayo itatufanya tuwapate hata kwa njia za magendo?” Tseseko aliuliza.

    “Labda mfanye kitu kimoja”

    “Kitu gani?”

    “Mnaonaje kama mtawateka watoto wao?” Salumu aliuliza.

    “Kumbe wana watoto?” Pokwane aliuliza huku akionekana kutokuamini.

    “Kumbe mlikuwa hamjui! Wana watoto wawili, mmoja wa kike na mwingine wa kiume” Salumu aliwaambia.

    “Hapo safi sana. Wapo wapi hao watoto wao?”

    “Wanasoma”

    “Wapi?”

    “Shule fulani ya matajiri ipo Msasani”

    “Kama ni hivyo hebu tupeleke tukawaone”

    Salumu ambaye alikuwa akionekana kufahamu mambo ya matajiri wengi kutokana na kuwa dereva wa teksi akaanza kuwapeleka Pokwane na Tseseko katika shule ya St Luke ambayo ilikuwa Msasani hapo hapo jijini dar es Salaam. Vichwani mwa Pokwane na Tseseko katika kipindi hicho walikuwa wakifikiria kuhusu kufanya mauaji tu.

    Kwa wakati huo wakaanza kujadili juu ya namna ambayo walitakiwa kuifanya mahali hapo. Lugha ambayo walikuwa wakiitumia ilikuwa ni Kizulu, lugha ambayo Salumu hakuwa akiielewa. Mipango ikapangwa na kupangika kwamba watoto wale ilibidi wawateke na baada ya hapo kumhitaji Tandi na mumewe waende kuwachukua watoto wao na kisha kuwaua wote wawili.

    Kuhusu dereva Salumu, hilo wala hawakuwa na wasiwasi nalo kwani waliamini kwamba mtu huyo alikuwa amejitolea kuwasaidia lakini mwisho wa siku ilikuwa ni lazima wamuue. Hiyo ndio mipango ambayo walikuwa wamekubaliana na ambayo walitakiwa kuifanya katika kipindi cha ndani ya siku tatu.

    Hata kabla ya kuelekea shuleni huko, walichokifanya ni kuelekea madukani na kisha kununua kila kitu ambacho walikuwa wakikihitaji ikiwepo kamera ambayo ingewafanya kuzuga kama wanawapiga picha watoto hao. Wakajikamilisha katika safari hiyo na kisha kuelekea shuleni hapo.

    Walitumia muda wa saa zima mpaka kufika katika geti kuu la kuingilia katika shule ya St Luke na kisha Salumu kuteremka na kuomba ruhusa kwa mlinzi kwamba walikuwa wamefika shuleni hapo kwa ajili ya kuwaona watoto ambao wajomba zao walikuwa ndani ya gari lile.

    Kwa mbali mlinzi akaonekana kuwa na wasiwasi, Salumu alilitambua hilo, alichokifanya ni kuanza kumzubaisha na kisha kumtolea kiasi cha shilingi elfu kumi na tano na kumpa, mlinzi hakuwa na kinyongo, akawaruhusu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara baada ya kuingia katika eneo la shule ile moja kwa moja wakaelekea katika ofisi ya mwalimu mkuu na kisha kuanza kuongea nae. Salumu aliongea kwa kujiamini kwamba watu ambao walikuwa mahali pale walikuwa ni watu ambao walitoka Afrika Kusini huku wakiwa na lengo la kuwaona watoto ambao walikuwa katika shule hiyo.

    “Kwa hiyo wana lengo gani?” Mwalimu mkuu alimuuliza Salumu.

    “Hawa ni marafiki zangu, wanataka kuonana na watoto wa KiTanzania, kwani wamesikia sana sifa zao. Wakishawaona na kuongea nao, basi waondoke na kwenda St Marrys na St’ Peter” Salumu alimwambia mwalimu mkuu.

    Mwalimu mkuu hakuongea kitu chochot kile, alikuwa kimya huku akionekana kufikiria kitu. Alichokifanya Pokwane ni kumbinya Salumu miguuni, Salumu akaonekana kufahamu ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, akajidai kukohoa na kisha kuingiza mkono mfukoni, alipoutoa, alikuwa na noti kumu za shilingi elfu kumi na kuziweka mezani.

    “Laki moja kwa kukubaliana na ombi letu. Hatuna muda mwingi wa kuwa mahali hapa. Kesho tu wanatakiwa kuondoka kurudi kwao” Salumu alimwambia mwalimu mkuu ambaye aliziangalia zile fedha na bila ya kuzihesabu akazichukua kutoka pale mezani na kuziingiza ndani ya mfuko wa suruali yake huku akitoa tabasamu pana.

    “Kijana unajua sana kucheza na akili za watu. Kungekuwa na vijana laki moja kama wewe. Nyumba yangu ya kule Chamazi ingekuwa imekwishakamilika” Mwalimu mkuu yule alisema na kisha kuwaomba kuwafuata.

    Mwalimu yule hakuonekana kuwa na wasiwasi na watu ambao walikuja shuleni hapo, alichokifanya ni kuongea na walimu wengine wa shule hiyo na kisha kuwaomba wanafunzi wote mia tatu wa darasa la kwanza hadi la saba kutolewa nje na kisha Pokwane na Tseseko kuanza kupiga nao picha huku wakiwauliza maswali machache ya Kingereza.

    Kwa sababu walimu walikuwa wameshaonyesha uaminifu wao kwao, kwa uzembe wa hali ya juu wakawaacha Pokwane na Tseseko wakiwa na watoto wale ambao waliendelea kuwauliza maswali. Hata pale walipowataka Rahman na Latifa waje mbele yao, watoto hao wakatoka na kisha kusimama mbele yao.

    Pokwane akashindwa kujizuia, machozi yakaanza kumlenga na kisha kuanza kumtoka. Kwa haraka haraka akachukua kitambaa na kuanza kujifuta. Sura ya Latifa ilikuwa imemkumbusha mbali sana, kwa jinsi ambavyo alivyokuwa amefanana na Tandi, mawazo yake yakaanza kurudi nyuma kabisa toka katika kipindi alichokuwa na mwanamke huyo Afrika Kusini.

    Walichokifanya ni kutoa kamba ya kupimia urefu ambao walikuwa wakiutumia mafundi nguo na kisha kisha kuanza kuwapima Rahman na Latifa mahali hapo na walipoona kwamba wameridhika,wakaendelea na mambo mengine.

    Walitumia dakika ishirini kukaa na watoto wale na ndipo walipowaruhusu kuondoka kuelekea madarasani. Kazi ambayo ilikuwa imebakia kwao wala haikuwa kubwa sana, kitu ambacho walichokuwa wakikitaka ni kufahamu vyumba ambavyo watoto wale walivyokuwa wakivitumia bwenini. Wangefanya nini? Hilo walimuachia Salumu ambaye akaanza kuelekea katika ofisi ya mwalimu mkuu.

    “Hapa kuna dili kubwa sana mwalimu” Salumu alimwambia mwalimu mkuu.

    “Dili gani” Mwalimu mkuu aliuliza huku akiwa ametoa macho.

    “Hawa jamaa ni matajiri sana. Wamekuja hapa kwa ajili ya kutoa misaada ya fedha, si unajua fedha zinawawasha!”

    “Ndio”

    “Sasa wanataka kutoa msaada wa shilingi milioni ishirini kwa ajili ya shule hii:”

    “Sawasawa”

    “Au achana na hilo. Kwanza shule hii ina fedha nyingi. Shule ya vibosile hii” Salumu alisema huku akijifanya kughailisha.

    “Sasa hicho unachosema utakuwa unakosea. Kama ishu ya fedha imekuja, wewe una wasiwasi gani?”

    “Kwanza niahidi kitu kimoja”

    “Kitu gani?”

    “Kwamba na mimi nitakuwa na fungu langu hapo” Salumu alimwambia.

    “Hilo usijali. Katika milioni ishirini utataka kiasi gani?”

    “Pasu kwa Pasu, yaani kumi kwa kumi” Salumu alijibu huku maneno yote hayo yakiwa ni kumteka mwalimu mkuu akili.

    “Mbona unataka kuchukua nyingi?”

    “Sasa si pasu kwa pasu!”

    “Sasa wewe unafikiri nikipata fedha hizo zitakuwa zangu peke yangu? Kuna walimu wengine wanoko nao inabidi niwapoze” Mwalimu mkuu alimwambia Salumu.

    “Kwa hiyo mimi nitapata kiasi gani?”

    “Milioni tano”

    “Poa. Hilo si tatizo”

    “Kama ni hivyo sawa. Kuna jingine?”

    “Yeah! Jamaa wamekwishapiga picha, wanataka kutembelea na mabweni” Salumu alimwambia mwalimu mkuu.

    ”Hilo si tatizo”

    Fedha hewa ambazo aliahidiwa mwalimu mkuu zikaonekana kumlevya, alikuwa tayari kufanya kitu chochote kwa wakati huo ili mladi tu ahakikishe kwamba anapata kiasi hicho cha fedha. Kwa moyo mweupe akawaruhusu Pokwane na Tseseko kutembelea mabweni. Kitu ambacho kilionekana kuwa kama bahati kwao, katika kila kitanda, jina la mtoto aliyekuwa akikitumia kitanda hicho lilikuwa limeandikwa katika vikaratasi vilivyobandikwa kitandani hapo.

    Katika bweni la wasichana chumba namba nne kitanda cha chini ndicho alichokuwa akilala Latifa na katika chumba namba saba katika bweni la wavulana kitanda cha juu ndicho alichokuwa akilala Rahman. Hiyo ikawafanya kukariri namba zile na vyumba vile kwa haraka sana tayari kwa kufanya kazi ambayo walikuwa wamepanga kuifanya siku mbili zijazo.

    “Kwa hiyo inakuwaje kuhusu hizo fedha?” Mwalimu mkuu alimuuliza Salumu.

    “Si wamesema kesho wanarudi tena?” Salumu aliuliza.

    “Ndio”

    “Basi poa. Wameniambia kesho wanakuja na mzigo kamili. Ila wamesema usiwaambie viongozi wa serikali” Salumu alimwambia mwalimu mkuu.

    “Hilo si tatizo”

    “Basi sawa. Kesho tutakuja asubuhi ya saa mbili kwani saa saba inatakiwa wawe ndani ya ndege kurudi kwao” Salumu alidanganya.

    “Hakuna tatizo” Mwalimu mkuu aliitikia.

    Siku iliyofuata, Salumu akapewa kazi ambayo kwake aliiona kuwa ngumu japokuwa kiasi cha fedha cha shilingi milioni tatu ambacho alipewa kilimfanya kukamilisha kile ambacho aliambiwa. Maiti mbili za watoto zilikuwa zikihitajika sehemu hizo kwa ajili ya kukamilisha kile ambacho kilitakiwa kufanyika.

    Alichotakiwa kukifanya ni kwenda katika hospitali yoyote kubwa kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kupata maiti za watoto ambao walikuwa na urefu ambao walikuwa wamemuandikia. Hiyo ikaonekana kuwa ngumu kwa Salumu lakini alichokifanya, mpaka ilipofika saa kumi jioni, tayari alikuwa amekwishapata kile walichomtuma.

    “Kuna dokta alisema hilo si tatizo. Tumfuate katika hospitali yake usiku ili atuambie atatuletea wapi” Salumu aliwaambia.

    “Sawa”

    Usiku wakaanza kuelekea katika hospitali ya dokta huyo ambaye akawaambia kwamba jambo lile halikuwa gunu sana. Alichokifanya ni kuanza kuwasiliana na mtu wa mochwari ambaye huyo alihakikisha kila kitu kinakaa sawa na kisha kuanza kutafuta maiti zilizokuwa zimekaa siku nyingi hospitalini hapo, tena zile maiti za watoto wa mitaani waliokufa na kisha kuziweka tayari.

    “Urefu upo sawa?” Dokta alimuuliza jamaa wa mochwari.

    “Hapana. Hawa wamezidi kidogo” Jamaa wa mochwari alijibu.

    “Hilo si tatizo. Kwa hiyo ngoja niongee nao ili nijue tunazifuata lini” Dokta alimwambia.

    “Hakuna tatizo”

    Alichokifanya dokta ni kuanza kuongea na Salumu juu ya siku ambayo walitakiwa kuja kuzifuata maiti zile, ilikuwa baada ya siku mbili. Hilo halikuonekana kuwa tatizo kwa dokta yule, kitu ambacho nae alikuwa akikijali ni fedha tu na wala si maiti.

    Baada ya siku mbili, salumu akamfuata dokta yule hospitalini na kisha kuanza kuongea na jamaa wa mochwari ambaye tayari alikuwa amekwishaziandaa maiti zile na kisha kutakiwa kuzitoa jambo ambalo wala halikuwa tatizo kwani ndani ya dakika arobaini, kila kitu kilikuwa sawa, wakawalipa fedha ambazo walikuwa wameahidi na kisha kuondoka na maiti zile kuelekea katika shule ya St Luke huku wakiwa na kidumu cha petroli pamoja na kiberiti, muda ulikuwa umekwishafika saa tisa na robo usiku.





    ******************************************





    Kila kitu kilipangwa kufanyika kwa haraka sana, Salumu akaanza kuendesha gari kwa mwendo wa kawaida kuelekea Msasani ambapo kulikuwa na shule hiyo ya St’ Luke. Wala hawakuchukua dakika nyingi, wakawa wamekwishafika katika eneo ambalo ukiangalia kwa mali shule ya St’ Luke ilikuwa ikionekana vizuri.

    Walichokifanya ni kuteremka na moja kwa moja kuanza kuelekea katika uzio wa shule hiyo huku Pokwane na Tseseko wakiwa wamebeba maiti zile na Salumu kuwaongoza mbele yao. Uzio haukuwa mkubwa sana, walichokifanya ni kuziweka maiti zile chini na kisha Salumu kuuparamia ukuta na kuanza kuchungulia.

    Ukimya mkubwa ulikuwa umetawala katika sehemu hiyo, sauti za majenereta tu ndio ambazo zilikuwa zikisikika kutoka katika baadhi ya nyumba ambazo zilikuwa zipo karibu na shule hiyo. Mara baada ya kuona kwamba hali ilikuwa ni ya usalama mkubwa, Salumu akapanda juu ya ukuta na kisha kuanza kupewa maiti moja baada ya nyingine na kuingia ndani ya eneo la shule hiyo.

    Katika kipindi cha nyuma walifikiri kwamba kazi ingekuwa kubwa sana lakini hali ilikuwa tofauti na jinsi walivyokuwa wamefikiria kabla. Kazi haikuwa na ugumu wowote ule. Maiti zilipofikishwa chini katika upande wa shule ile, wakazichukua na kisha kuanza kuelekea katika mabweni yale huku wakiwa katika upande wa nyuma.

    Mlinzi wa shule hiyo hakuonekana kuwa katika upande ambao walikuwa wakitokea hivyo kuwapa urahisi katika kila kitu ambacho walikuwa wakikifanya. Pamoja na hayo yote, giza ambalo lilisababishwa na umeme kukatika lilikuwa limewapata urahisi wa kutaka kukamilisha jambo lile ambalo walikuwa wakikaribia kulifanya kwa wakati huo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara baada ya kutokea katika upande wa pili wa mbele ya mabweni yale, wakajigawanya, Tseseko akaelekea katika bweni la wasichana na Pokwane kuelekea katika bweni la wavulana. Wote kwa pamoja wakaingia ndani ya mabweni yale huku kila mmoja akiwa na maiti yake pamoja na kidumu cha lita tano cha mafuta.

    Kwa kuwa ndani ya shule hiyo chumba kimoja walikuwa wakivitumia watoto wawili, walipoingia katika vyumba hivyo wakawaamsha watoto wale waliokuwa ndani ya vyumba hivyo na kisha kuanza kuangaliana nao usoni.

    “Mkipiga kelele tu, nawaua” Pokwane alimwambia Rahman na mtoto mwingine ambaye alikuwa akilala nae chumbani, wote wakajikuta wakibaki kimya.

    Kilichotokea, yule mtoto mwingine akafungwa kamba miguu na mikononi pamoja na mdomo wake kuufunga na kundi ngumu na kubwa ya karatasi kisha kutolewa kwenye korido na kulazwa chali huku akiamriwa kutokujigeuza kwa sababu angempiga risasi na wakati Pokwane hakuwa na bunduki yoyote ile. Pokwane alipoona kwamba mtoto yule asingeweza kuleta usumbufu wowote ule, akarudi chumbani mule na kumgeuzia Rahman ukutani na kisha kumpiga ngumi kali ya shingo, ngumi ambayo ikampeleka chini Rahman na kupoteza fahamu.

    Alichokifanya Pokwane ni kuelekea katika korido ile ambapo alikuwa ameilaza maiti ile aliyoichukua kutoka hospitalini na kisha kuja nayo ndani ya chumba kile. Hakutaka kuchelewa, hapo hapo akaanza kuimwagia mafuta ya petroli. Hata kabla hajaichoma moto, akashtukia kuona mwanga mkali dirishani, alipochungulia, akagundua kwamba tayari Tseseko alikuwa amekwishafanya kile kilichowapeleka shuleni pale. Hata kabla ya kufanya kitu chochote kile, akachukua marker pen na kisha kuliandika jina lake ukutani ili mara Selemani na Tandi watakapoliona wajue ni nani ambaye alikuwa amefanya hayo na alifanya kwa sababu ipi.

    Hakutaka kuchelewa, nae akafanya kile kilichompelaka ndani ya chumba kile. Akaichoma moto maiti ile pamoja na baadhi ya vitu vilivyokuwa ndani nya chumba kile na kisha kutoka nje ambapo akambeba Rahman na kisha kutoka nae nje. Akaanza kukimbia nae huku akiwa amembeba begani alipofika kwenye ukuta ule, tayari Tseseko alikuwa amekwishafika ambapo wakawapandisha Rahman na Latifa ukutani na kisha kuondoka nao mpaka garini.

    “Wapi sasa?” Salumu aliwauliza.

    “Mozambique” Pokwane alijibu.

    Hakukuwa na muda wa kupoteza mahali hapo, kilichofanyika ni Salumu kuwasha gari lake na kisha kuondoka mahali hapo na kuelekea barabarani. Safari ya kuelekea Mbagala ikaanza huku Rahman na Latifa wakiwa katika viti vya nyuma ya gari lile huku wakiwa wamepoteza fahamu. Mwendo haukuwa mdogo, Salumu alikuwa akiendesha kwa kasi kubwa kupita kawaida kutokana na kutokuwa na magari mengi barabarani.

    Kutokana na kasi kubwa ambayo alikuwa akiitumia Salumu, iliwachukua dakika arobaini na tano tu mpaka kufika Kipara ambapo bado alikuwa akiendelea mbele katika barabara hiyo ya Kilwa. Safari bado ilikuwa ikiendelea tena kwa kasi ya ajabu kiasi ambacho kiliwachukua masaa matano wakawa wamekwishafika Mkuranga.

    Kwa mahesabu ambayo alikuwa akiyapiga Salumu kichwani mwake kwa wakati huo, alitaka sana mpaka inafika jioni wawe wamekwishafika Ikwiriri na kisha kulala mahali hapo kabla ya siku inayofuatia kuendelea na safari mpaka kufika Kilwa kivinje ambapo hapo wangelala na siku inayofuatia kuingia nchini Mozambique.

    Ndani ya masaa mengine matatu wakawa wamekwishafika Kibiti, sehemu ambayo gari lao likasimamishwa na askari wa barabarani na kumgawia kiasi kidogo na kisha kuendelea na safari zaidi huku kila mmoja akijua kwamba piga ua ilikuwa ni lazima kuingia nchini Mozambique ambapo huko wangeonganisha mpaka Afrika kusini.

    *****

    Selemani alikuwa amechanganyikiwa kupita kawaida, alikuwa akiendesha gari lile kwa mwendo wa kasi sana huku lengo lake likiwa ni kuwafikia watu wale ambao aliambiwa kwamba walikuwa wameonekana njiani huku wakiwa na watoto ambao bila shaka walikuwa ni watoto wake.

    Alichokifanya Iqram ni kuwapigia simu polisi wa hapo Kibiti na kisha kuwaambia kwamba walifuatiliie gari hilo, walisimamishe na kisha kuwaweka chini ya ulinzi watu wote ambao walikuwa ndani ya gari hilo na hawakutakiwa kuwaruhusu kuondopka mpaka wao watakafikika katika sehemu hiyo.

    Mwendo wa gari lile ulikuwa ni wa kasi kupita kawaida jambo ambalo liliwafanya hata polisi kuogopa kwa kuona kwamba wangeweza kupata ajali muda wowote ule. Kwa Selemani wala hakuonekana kujali, kitu ambacho alikuwa akikitaka mahali hapo ni kufika kule ambapo walikuwa wakielekea.

    “Punguza mwendo Sele” Mkuu wa polisi, Iqram Maduro alimwambia Selemani.

    “Nikipunguza tutawakosa”

    Badala ya kupumzika mwendo kasi wa gari lile, Selemani akaongeza zaidi mpaka sehemu ya kuonyesha kasi ya gari ikaanza kupiga kelele. Selemani hakuonekana kuelewa chochote kile katika kipindi hicho, kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuwapata watoto wake tu.

    Walitembea kwa mwendo wa kasi mpaka walipoingia Bungu hasa mara baada ya masaa matano kukatika. Mpaka wanafika mahali hapo salama, wakaanza kumshukuru Mungu, sehemu ambayo mabasi makubwa yalikuwa yakitumia masaa zaidi ya kumi, wao walikuwa wametumia masaa matano tu kuonyesha ni kwa namna gani walikuwa wametumia mwendo mkali mpaka kuingia hapo.

    “Kinachofuata ni kupumzika” Iqram aliwaambia.

    “Siwezi kupumzika na wakati watoto wangu wapo mikononi mwa adui. Ni lazima tuendelee na safari” Selemani aliwaambia.

    Hakukuwa na jinsi. Walichokifanya ni kuendelea na safari zaidi. Katika kipindi hicho kila mmoja alionekana kuchoka kupita kawaida lakini kwa Selemani hakuonekana kujali kabisa. Bado alikuwa akiwahitaji watoto wake wakiwa hai, hakutaka watoto hao wawe mikononi mwa adui ambaye wala hakuonekana kuwa mtu wa amani.

    Mara simu ya Iqram ikaanza kuita, alipoichukua na kuongea, alikuwa mkuu wa polisi Kibiti ambaye alikuwa akiwaambia kwamba watu ambao waliwaambia wawafukuze tayari walikuwa wamekwishawakamata na walikuwa chini ya ulinzi wao. Hiyo kidogo ikaonekana kuwa nafuu kwa Selemani, akaanza kupunguza mwendo wa gari kwa kuona kwamba kazi ilikuwa imekwisha.







    ****





    Polisi wa Kibiti wakaingia kwenye magari yao na kisha kuanza kuelekea kule ambapo gari lile walilokuwepo watu wale ambao walikuwa na watoto walipoelekea. Dereva alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi kupita kawaida mpaka kufika sehemu ambapo kwa mbali wakafanikiwa kuliona gari lile likiendelea na safari.

    Alichokifanya dereva ni kuongeza kasi zaidi mpaka kufika umbali wa hatua hamsini kutoka katika gari lile ambalo walikuwa wakilifukuzia. Alichokifanya polisi mkuu wa Kibiti ni kupiga risasi hewani kama kuwataka watu wale kusimama lakini gari halikusimamishwa zaidi ya dakika chache mbele kumuona dereva, Salumu akiwa amesukumwa nje ya gari na kuburuzika barabarani mpaka kuchunika mwili mzima na kufariki papo hapo.

    Tayari polisi walikwishaona kwamba watu wale hawakuwa na nia njema, walichokifanya ni kumuhimiza dereva kuendesha gari kwa kasi zaidi mpaka kuanza kulifikia zaidi lile gari ambapo wala halikusogea sana, likaanza kupunguza mwendo na kusimama jambo ambalo mapolisi wakajirusha kwenye gari lao na kwenda kulizunguka.

    Polisi wakalisogelea lile gari na kisha kuwaweka Pokwane na Tseseko chini ya ulinzi. Polisi wawili wakawasogelea na kisha kuanza kuwapekua, hawakuwa na bunduki yoyote ile jambo ambalo likaonekana kuwa nafuu kwao.

    Hawakutaka kupoteza muda, wakafungua mlango wa nyuma wa gari lile, Rahman na Latifa walikuwa wamekumbatiana huku wakilia, kile kitendo ambacho kilikuwa kikiendelea kilionekana kuwatia hofu kupita kawaida.

    Polisi mmoja akaelekea katika usukuni kwa ajili ya kuliwahs gari lile, lilikuwa limeishiwa mafuta na ndio maana Pokwane hakuweza kusonga nalo zaidi. Polisi wale wakawatoa ndani ya gari lile na kisha kuwapandisha ndani ya gari lao na kisha safari ya kuelekea katika kituo cha polis cha Kibiti kuanza huku wakiwa na Pokwane, Tseseko, Latifa na Rahman.





    ******************************************





    Mara baada ya kufika Kibiti moja kwa moja wakaanza kuelekea katika kituo cha polisi cha hapo Kibiti ambapo mara baada ya kufika wakaruhusiwa kuwaona watoto hao ambao walikuwa wamefungiwa katika chumba kimoja cha usalama zaidi. Selemani alipowaona watoto wake, Rahman na Latifa, machozi yakaanza kumtoka, alijisikia furaha kupita kawaida.

    “Kuna kitu nataka kifanyike” Selemani alimwambia Iqram.

    “Kitu gani?”

    “Hii nataka iwe siri kati yangu na wewe”

    “Usiwe na wasiwasi. Wewe unataka nini kifanyike?”

    “Nataka hawa watu wapotee. Yaani wapotee hata miili yao isipatikane katika uso wa dunia hii” Selemani alimwambia Iqram.

    “Ila si unajua hawa watu lazima wafikishwe Dar es Salaam”

    “Nafahamu. Ila si pesa inaweza kuweka mambo sawa. Kama milioni kumi na tano haiwezi kuweka mambo sawa?” Selemani alimuuliza Iqram.

    “Mmmh!”

    “Usigune. Fanya hivyo kisha nipe taarifa. Nitakuletea cheki ya siri ya kiasi jhicho cha fedha” Selemani alimwambia Iqram.

    “Lakini kwa nini unataka kufanya hivyo?”

    “Hawa ni watu wabaya kwangu tena mbaya zaidi wa Waafrika Kusini, ni watu wabaya kwa familia yangu. Naomba ufanye hivyo” Selami alimwambia Iqram.

    “Usijali. Nitajaribu”

    “Sawa. Kama ukifanikiwa. Nitakuongeza fedha zaidi” Selemani alimwambia Iqram.

    Selemani hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuwachukua watoto wake na kisha kuondoka nao mahali hapo huku akimwacha Iqram na wenzake wakiwa katika mishemishe ya kukamilisha kile ambacho aiikuwa amewaambia. Katika safari nzima, Selemani alikuwa na furaha ya kuwaona watoto wake kwa mara nyingine tena.

    “Nitawalinda popote mtakapokuwa. Nyie ndio watoto wangu wa pekee katika dunia hii” Selemani aliwaambia watoto wake, Rahman na Latiofa.

    ****

    Miaka ikaendelea kukatika. Baada ya miaka ishirini kupita toka atoke Afrika Kusini, Selemani akaanza kujisikia hali ya tofauti katika kifua chake. Muda mwingi alikuwa akikohoa sana hali ambayo ikaanza kumuwekea wasiwasi mkubwa kwamba iliwezekana kwamba ilikuwa ugonjwa wa TB.

    Katika miaka yote kipindi cha nyuma alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua lakini katika kipindi hicho ugonjwa huo ulionekana kuwa mkubwa zaidi. Muda mwingi Selemani likuwa akikohoa sana jambo ambalo wakati mwingine lilimfanya kutokwa na damu.

    Hapo ndipo alipoamua kwenda hospitalini kuona tatizo lilikuwa ni nini. Selemani hakuamini mara baada ya kuambiwa kwamba ugonjwa ambao ulimfanya kuwa katika hali ile ilikuwa ni kansa ya kifua. Kwa Selemani ikaonekana kuwa habari mbaya sana kwake, kifua chake kilikuwa kimeoza sana, kansa ilikuwa ikimtafuna kupita kawaida.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika kipindi hicho akaonekana kuwa na bahati kwani tangu alipoanza kuugua zaidi ugonjwa ule na ndicho kilikuwa kipindi ambacho kukatokea mtu ambaye alikuwa amegundua dawa ya kansa, tena akiwa ni Mtanzania aliyekuwa akisoma nchini India, Abuu. Dawa zile zilipoanza kusambazwa dunia, zilikuwa ngumu sana kufika barani Afrika lakini mara baada ya kusikia kwamba mtu huyo aliyetengeneza dawa hizo alikuwa akitarajiwa kufika nchini Tanzania, hakuwa na jinsi, nae akaelekea hospitalini.

    Kwa wakati huo alikuwa na miaka arobaini na tano, mwili wake ulionekana kuanza kuingia katika uzee, nguvu ambazo alikuwa nazo katika kipindi cha nyuma hakuwa nazo tena katika kipindi hicho. Mara baada ya kufika katika hospitali ya Muhimbili, akataka kuwekwa katika chumba cha wagonjwa waliokuwa wakiugua ugonjwa wa kansa.

    Alijua fika kwamba kwa fedha ambazo alikuwa nazo alikuwa na uwezo wa kwenda katika hospitali bora zaidi lakini kwa sababu lengo lake lilikuwa ni kutaka kuonana na mtu huyo, Abuu, hakuwa na budi kwenda katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kulazwa.

    Katika siku ambayo mtu huyo, Abuu alipokuwa akiingia katika hospitali hiyo, Selemani alikuwa pamoja na mkewe, Siwema huku moyo wake ukiwa na uhakika kwamba tatizo lake hilo lilikuwa linaelekea kwisha kutokana na ujio wa dokta huyo ambaye alikuwa akijulikana dunia nzima kwa wakati huo.

    Mara baada ya Abuu kuingia ndani ya chumba kile na Selemani kumuona, moyo wake ukafarijika, alijiona kama kupona ugonjwa ule ambao ulikuwa ukimsumbua. Abuu alipokwenda kumwangalia na kisha kupiga nae picha, alizidi kupata uhakika zaidi kwamba ule ndio ulikuwa mwisho wa ugonjwa ule kukaa ndani ya mwili wake.

    “Hatutoweza kupata dawa?” Selemani alimuuliza dokta ambaye alikuwa akitembea na Abuu pamoja na madaktari wengine chumbani hapo.

    “Bado hatujajua. Ila tutawapa taarifa” Dokta huyo alimwambia Selemani.

    “Sawa baba. Jitahidi mnamzuia asirudi huko anapoishi bila kutuachia dawa. WaTanzania wenzake tunakufa baba” Selemani alimwambia dokta yule.

    “Usijali. Tutamwambia hilo” Dokta yule alimwambia mzee Selemani katika kipindi ambacho Abuu alipokuwa akitoka ndani ya chumba kile.

    “Mmmh! Umefanana nae” Bi Siwema alimwambia mumewe, Selemani.

    “Nani?” Selemani aliuliza.

    “Yule dokta”

    “Huyu niliyekuwa nikiongea nae?”

    “Hapana. Yule dokta wa kansa, Abuu. Umefanana nae kama mapacha” Bi Siwema alisema.

    “Hapa duniani watu tupo wawili wawili mke wangu” Selemani alimwambia mke wake

    “Kuanzia leo, nimeamini huo msemo” Bi Siwema alimwambia mumewe, Selemani.







    ****





    Mara baada ya kutoka katika chumba kile ambacho kilikuwa na wagonjwa wengi wa kansa, Abuu akaanza kuelekea katika ofisi ya dokta mkuu wa hospitali ile ya Muhimbili, dokta Mwamboka na kuongea nae mawili matatu huku akiahidi dawa za kutibu magonjwa ya kansa zingeingia nchini Tanzania ndani ya wiki moja.

    Siku iliyofuata Abuu akakaa sana na bibi yake huku wakiongea mengi ambayo yalikuwa yamejiri katika maisha yao ya nyuma pamoja na kumuaga kwamba ilikuwa ni lazima arudi nchini Marekani kuendelea na shughuli zake pamoja na mpenzi wake, Jasmin na mtoto wao, Zubeda. Maandalizi ya safari yaliendelea kufanyika mpaka katika kipindi ambacho akaanza safari ya kurudi nchini Marekani huku akiwa na mpenzi wake, Jasmin.

    Kwa Abuu hiyo ilikuwa furaha kubwa sana kwake, hakuamini kama katika kipindi hicho nae alikuwa akiitwa baba, alionekana kuwa katika mapenzi mazito na mtoto wake aliyetoka katika kiuno chake.

    Ndege ilichukua masaa kadhaa na ndipo ikatua katika ardhi ya nchi ya Marekani. Katika kipindi hicho baridi lilikuwa kali sana ambalo kwa kiasi fulani likaonekana kumpa wakati mgumu Jasimn ambaye alikuwa hajazoea hali ya hewa kama ile. Dokta Mickey alikuwa uwanjani hapo kwa ajili ya kumpokea rafiki yake mkubwa, Abuu ambaye alikuwa akiingia pamoja na mpenzi wake ambaye alikuwa na mtoto wake.

    “Umewahi…safi sana” Dokta Mickey alimwambia Abuu katika kipindi ambacho walikuwa ndani ya gari wakielekea nyumbani.

    “Kuna nini?”

    “Kuna mkutano wa madaktari wiki ijayo. Kuna madaktari kutoka nchi mbalimbali wanataka kuongea nawe pamoja na kuwaonyeshea kile ambacho ulikuwa ukikifanya” Dokta Mickey alimwambia Abuu.

    “Nimekuelewa. Ila ninahitaji muda wa kupumzika”

    “Hilo si tatizo kabisa”

    Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kuchezacheza na mpenzi waike, Jasmin kitandani. Walikuwa wakishikana hapa na pale kiasi ambacho kikawapelekea kuvunja amri ya sita kitandani pale. Kila mmoja alionekana kumhitaji mwenzake katika kipindi hicho, miili yao ilikuwa katika hamu kubwa ya kufanya kile ambacho walikuwa wakifanya katika kitanda kile.

    Wiki iliyofuata ndio ilikuwa wiki ambayo Abuu alihitajika katika mkutano wa madaktari wakubwa duniani kwa ajili ya kuongea mambo mengi ambayo yalikuwa yakihusu juu ya tiba ya magonjwa sugu ukiwepo kansa. Kila dokta ambaye alikuwa akishiriki katika mkutano huo alikuwa akitaka kumuona Abuu, alikuwa ni mtu gani, alifananaje kwani kila mmoja alikuwa akifikiri dhahiri kwamba picha za magazetini na kwenye luninga zilikuwa zinadanganya.

    Saa 4:00 asubuhi siku ya jumatatu mkutano huo ukaanza katika chumba kikubwa cha mkutano kilichokuwa katika hoteli kubwa kuliko zote duniani, hoteli ya MGM ambayo ilikuwa ikipatikana katika jiji la wacheza kamari kuliko majiji yote duniani, Las Vegas. Kila dokta ambaye alimuona Abuu alishindwa kuamini kwamba yule ndiye alikuwa mtu ambaye alileta mafanikio katika dunia hii juu ya ugonjwa wa kansa ambao ulikuwa ukiwamaliza sana watu ambao wengi walikuwa wakila vyakula vya kisasa. Alionekana kijana mdogo sana.

    Mkutano ulipoanza na kuendelea, mwisho wa siku Abuu akaitwa mbele ya ukumbi ule na kuanza kuzungumza mengi kuhusiana na ugonjwa wa kansa ambao bado ulikuwa ukiendelea kuwa tishio kubwa duniani. Abuu aliongea mengi sana ambayo yalionekana kuwa faida kwa kila dokta ambaye alikuwa akiyasikia mahali pale huku akielezea hali ambayo alikutana nayo juu ya wagonjwa wa kansa ambao aliwakuta nchini Tanzania.

    Akaona hiyo kutokutosha kabisa, hapo ndipo alipoamua kuwaonyeshea picha mbalimbali katika kitambaa kikubwa cha projector juu ya picha ambazo alikuwa amepiga pamoja na wagonjwa mbalimbali nchini Tanzania. Picha zilitia huruma sana, wagonjwa walionekana kuteseka kupita kawaida.

    Picha zaidi ya mia mbili ambazo alikuwa amezipiga nchini Tanzania alikuwa amewaonyeshea madaktari ambao walikuwa ndani ya ukumbi ule. Mpaka inafika saa 5:02 asubuhi, mkutano ukaingia katika kipindi cha mapumziko, kipindi ambacho watu walitakiwa kula na kunywa na kisha kuendelea na mkutano ule.

    “Zile picha ulizipiga nchini Tanzania?” Dokta Mickey alimuuliza Abuu.

    “Ndio. Katika kipindi ambacho nilikwenda kutembelea wagonjwa wa kansa katika hospitali ya Taifa” Abuu alijibu.

    “Mbona kuna mgonjwa mmoja nimeona umefanana nae sana!” Dokta Mickey alimwambia.

    “Mgonjwa yupi?”

    “Hebu lete kamera nikuonyeshee” Dokta Mickey alimwambia Abuu ambaye akampa kamera ile na kisha kuanza kuitafuta picha ambayo alipiga na mzee Selemani, alipoipata, akamuonyeshea.

    “Itazame hii, tazama mlivyofanana” Dokta Mickey alimwambia Abuu.

    “Kawaida tu. Binadamu huwa wawili wawili duniani” Abuu alimwambia dokta Mickey.

    “Haiwezekani. Hata kama wawili wawili kwa huyu mtu, nina wasiwasi” Dokta Mickey alimwambia Abuu.

    “Wasiwasi wa nini?”

    “Inawezekana akawa baba yako”

    “Kuwa baba yangu! Haiwezekani. Baba yangu amekufa kitambo sana” Abuu alimwambia Dokta Mickey.

    “Ulikwishawahi kumuona?”

    “Hapana”

    “Hata picha yake?”

    “Yeah! Siwahi kuiona” Abuu alijibu.

    “Sawa. Hata kaburi lake haujawahi kuliona?”

    “Sijaliona”

    “Kwa nini sasa?”

    “Halafu wala sijauliza swali hilo. Mama hakutaka kunionyeshea” Abuu alijibu.

    “Kwa nini?”

    “Kila nilipomuuliza kuhusu baba yangu, alikuwa akilia tu” Abuu alijibu.

    ”Kwa hiyo haumjui kabisa baba yako?”

    “Ndio”

    “Na hauna uhakika kama amekufa au la?”

    “Kutokana na maelezo ya mama, amekufa”

    “Wewe unaonaje?”

    “Kama mama alivyoniambia”

    “Ila nina wasiwasi na huyu mzee Abuu” Dokta Mickey alimwambia Abuu.

    “Kwa nini?”

    “Umefanana nae mno. Yaani kama mapacha”

    “Ni kawaida tu”

    “Hapana. SIo kawaida. Uliongea nae japo kidogo?”

    “Ndio. Niliongea nae”

    “Ulimuuliza anaitwa nani?”

    “Anaitwa Sele…..Mungu wangu! Subiri kwanza” Abuu alisema.

    Abuu akaonekana kushtuka kupita kawaida, hakuamini kile ambacho alikuwa amekifikiria kwa kipindi hicho. Hapo hapo bila kupoteza muda, akatoka kutoka katika ukumbi ule huku akionekana kufikiria kitu. Dokta Mickey alibaki akimshangaa tu Abuu ambaye alitoka nje na kuchukua teksi ambayo ilimpeleka mpaka uwanja wa ndege akachukua ndege na kurudi New York.

    Kutokana na umbali uliokuwepo kutoka jimbo la Nevada ambapo kulikuwa kukipatikana jiji la Las Vegas mpaka New York, ilimchukua saa zima kusubiria ndege mpaka pale alipoingia na kuanza safari ya kurudi New york. Ndani ya ndege, alikuwa akiiangalia picha ile ambayo nae ikaanza kumtia wasiwasi fulani kwamba kulikuwa na uhakika kwamba mzee yule alikuwa ndugu yake, kuhusu kuwa baba yake, hakulifikiria hilo.

    Ndege ikachukua masaa matatu angani na ndipo ilipoingia katika jiji la New York. Huku akionekana kuwa na haraka, Abuu akaanza kutoka ndani ya jengo la uwanja ule na kisha kuchukua taksi ambayo ilimpeleka mpaka Manhattan alipokuwa akiishi.

    “Mbona upo hivyo mpenzi?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo lilitoka kwa Jasmin.

    “Hebu angalia hii picha” Abuu alimwambia Jasmin huku akimpa picha ile.

    “Mmmh! Huyu nani tena? Mbona umefanana nae?” Jasmin aliuliza.

    “Ni mgonjwa tu nilimkuta hospitalini. Dokta Mickey aliniambia anaweza kuwa baba yangu” Abuu alijibu huku akivaa nguo zake haraka haraka.

    “Baba yako! Baba yako si amekwishafariki!”

    “Hivyo ndivyo mama alivyoniambia”

    “Sasa iweje huyu awe baba yako?”

    “Hata mimi nashangaa. Mbaya zaidi sasa ambalo linaweza kukushangaza hata wewe”

    “Lipi”

    “Anaitwa Selemani. Jina la baba yangu”

    “Unasemaje?”

    “Ndio hivyo mpenzi” Abuu alijibu.

    “Sasa mbona unavaa! Unataka kwenda wapi?” Jasmin alimuuliza.

    “Tanzania”

    “Kufanya nini tena?”

    “Kumuona huyu mzee”

    “Utafanikiwa kweli kuondoka leo?”

    “Yeah! Sitopata usumbufu kwa sababu narudi nyumbani. Siwezi kuangaikia viza” Abuu alijibu.

    “Sawa”

    Abuu akachukua simu na kisha kumwambia dereva wake amkatie tiketi ya ndege kwenda nchini Tanzania, baada ya saa moja kila kittu kilikuwa tayari hivyo kuchukuliwa na kisha kupelekwa na gari mpaka uwanja wa ndege huku dereva wake akiwa anamshangaa Abuu katika kipindi chote.

    Hawakuchukua muda mrefu sana wakawa wamekwishafika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F kennedy ambapo Abuu akateremka na kisha kuanza kuelekea ndani ya jengo la uwanja ule huku akiendelea kutembelea gongo. Kwa watu ambao walimfahamu, hawakutaka kumuacha, wakaanza kupiga nae picha huku wengine wakitaka kusainiwa vitabu vyao na fulana zao kwani kwao kukutana na mtu mkubwa kama yule lilionekana kuwa jambo gumu kutokea, hasa katika nchi kubwa kama ya Marekani.

    Baada ya saa moja, abiria ambao walikuwa wakitakiwa kusafiri kwa ndege ya American Airlines wakaitwa ndani ya ndege hiyo na moja kwa moja safari ya kurudi nchini Tanzania kuanza huku kila wakati Abuu akiiangalia picha ile, bado ilionekana kumchanganya kupita kawaida.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******************************************





    Baada ya masaa ishirini na tatu Abuu akaingia ndani ya nchi ya Tanzania. Hakutaka kuchelewa, katika kipindi hicho alijiona kuwa nyuma ya muda, alichokifanya ni kutoka ndani ya jengo la uwanja ule wa ndege na kisha kuchukua teksi na kumpeleka mpaka katika nyumba kubwa aliyomnunulia bibi yake, Bi Asha ambayo ilikuwa Mbezi beach.

    Bi Asha akaonekana kushangaa kupita kawaida, hakuamini kumuona Abuu akifika nyumbani hapo bila taarifa, kwa siku hiyo, Abuu alionekana kuwa tofauti sana na siku nyingine ambazo aliwahi kuonekana machoni mwa Bi Asha.

    “Mbona upo hivyo! Kuna nini tena mjukuu wangu?” Bi Asha alimuuliza Abuu mara baada ya salamu na maongezi ya hapa na pale.

    “Mama aliniambia kwamba baba yangu alifariki. Ni kweli?” Abuu aliuliza.

    “Ndio. Ni kweli”

    “Naomba uniambie ukweli bibi. Naomba uniambie ukweli juu ya baba yangu. Ni kweli alifariki?” Abuu akauliza tena swali lile.

    Tayari macho yake yakaanza kutoka machozi ambayo yakawa yanatiririka mashavuni mwake. Moyoni alijisikia uchungu sana, aliumia zaidi ya siku nyingine, kitendo cha kuambiwa kwamba baba yake alikuwa amefariki kilionekana kumuuma.

    “Ni kweli Bibi?” Abuu alilirudia swali lake.

    “Hapana” Bi Asha alijibu na Abuu kuzidi kutokwa na machozi.

    “Sasa kwa nini mama aliniambia kwamba alifariki?” Abuu aliuluza.

    “Baba yako alikukataa toka ukiwa tumboni”

    “Kwa nini alifanya hivyo?”

    Hapo ndipo Bi Asha alipoanza kumuelezea Abuu kila kitu ambacho kilitokea katika maisha ya nyuma, maisha ambayo mama yake alipewa mimba na baba yake na kisha kukataa mimba ile. Kwa Abuu historia ile ikaonekana kumuumiza kupita kawaida, hakuamini kama kweli alikuwa amekataliwa na baba yake.

    “Kumbe baba alinikataa?”

    “Ndio. Alikukataa”

    “Kwa nini alinikataa?”

    “Alisema kwamba mimba haikuwa yake”

    “Kwani mama yangu alikuwa akitembea na wanaume wengi?”

    “Hapana”

    “Sasa kwa nini alikataa?”

    “Anajua yeye mwenyewe” Bi Asha alimwambia Abuu.

    Abuu akaumia zaidi, kukataliwa na baba yake kukaonekana kumuumiza kupita kawaida. Hapo ndipo ambapo akachukua picha ile na kisha kumuonyeshea bibi yake. Bi Asha akaiangalia kwa makini, sura ya Selemani ikaanza kuja kichwani mwake, akaikumbuka sura ile, japokuwa ilikuwa imezeeka, lakini akaonekana kumkumbuka.

    “Ndiye yeye. Ndiye baba yako huyu. Namkumbuka vilivyo Selemani. Mbona upo nae hapa?” Bi Asha alisema na kuuliza kwa mshangao.

    “Nilikutana nae nilipokuja. Anaumwa na amelazwa hospitalini” Abuu alijibu.

    “Naikumbia sura ya baba yako. Ndiye mwenyewe” Bi Asha alisema.

    Abuu hakuona sababu ya kuendelea kukaa mahali hapo, alichokifanya ni kumtaka Bi Asha waelekee hospitalini ambapo walifanikiwa kuonana na dokta mkuu, dokta Mwamboka na kumtaka kuonana na wagonjwa wale waliokuwa wakiugua ugonjwa wa kansa.

    Mara baada ya macho ya Abuu kutua usoni mwa mzee Selemani, machozi yakaanza kumtoka, hakuamini kama kweli alikuwa amekutana na baba yake mahali hapo huku akiwa katika hali yenye maumivu kupita kawaida. Alichokifanya Abuu ni kumsalimia Bi Siwema pamoja na watoto wao, Rahman na Latifa ambao walikuwa mahali hapo.

    “Selemani….!” Bi Asha aliita huku akimwangalia mzee Selamani.

    Selemani akayapeleka macho yake kwa Bi Asha, akaonekana kumtambua vilivyo, alikuwa mama wa mpenzi wake wa zamani, jamala ambaye alikuwa ameikataa mimba aliyokuwa amempa.

    “Bi Asha” Selemani alijikuta akiita.

    “Ugua pole kijana wangu. Sikujua kama unaumwa” Bi Asha alimwambia Selemani.

    “Naomba unisamehe kwa kile kilichotokea. Jamala yupo wapi, ninataka kumuomba msamaha kwanza” Mzaee Selemani alimwambia Bi Asha.

    “Jamala alifariki toka kitambo”

    “Naomba anisamehe huko alipo kwa kila kilichotokea. Ni kweli mimba ile ilikuwa yangu” Selemani alimwambia Bi Asha.

    “Sasa kwa nini uliikataa?”

    “Maisha. Maisha yangu yalikuwa magumu sana, sikuona kama ningeweza kuitunza mimba ile” Mzee Selemani alimwambia Bi Asha huku uso wake ukionekana dhahiri kujutia kile alichokuwa amekifanya katika kipindi cha nyuma.

    Bi Siwema na watoto wake wakabaki wakishangaa, hawakuelewa kile ambacho kilikuwa kikizungumziwa mahali hapo. Hapo ndipo mzee Selemani akaanza kuelezea kila kitu ambacho alikuwa amepitia katika maisha yake toka siku ya kwanza alipokutana na Jamala katika muziki wa rusha roho usiku na kuanzisha mahusiano.

    Hakuishia hapo, alielezea mpaka siku ile ambayo aliikataa mimba ambayo alikuwa amempa. Akaendelea zaidi mpaka alipoanza maisha na msichana mwingine, Farida na kisha kuachana na kuwa mpiga debe ambaye aliamua kuzamia kwenda nchini Marekani au barani Ulaya. Kila kitu ambacho kilitokea katika maisha yake, alikiweka wazi huku akimwambia Bi Asha amsamehe kwa kila kitu.

    “Nimekwishakusamehe toka zamani Selemani. Nimemleta huyu mgeni wako. Unamjua?” Bi Asha alimwambia mzee Selemani na kumuuliza.

    “Namjua. Ni dokta kutoka nchini Marekani. Dokta wa magonjwa ya kansa ambaye nilipiga nae picha wiki iliyopita” Mzee Selemani alisema.

    “Ndio. Huyu ni dokta Abuu. Ni mtoto wa Jamala ambaye alijifungua baada ya wewe kuikataa mimba ile” Bi Asha alisema mamneno ambayo yalimshtua kila mtu mahali pale.

    “Kwa hiyo huyu ni mtoto wangu?” Mzee Selemani aliuliza kwa mshtuko.

    “Ndio. Ni mtoto wako”

    “Siamini” Mzee Selamni akainuka kutoka pale kitandani huku akisaidiwa na mtoto wake, Rahman na kisha kumsogelea Abuu na kuanza kumwangalia. Mfanano wao ukazidi kuonekana zaidi na zaidi, bila kutarajia na kwa furaha kubwa, wakajikuta wakikumbatiana. Wote wawili wakaanza kulia, Abuu hakuamini kama angeweza kukutana na baba yake ambaye aliukataa ujauzito wake.

    “NIsamehe Abuu. Nisamehe kwa kila kitu” Mzee Selemani alimwambia Abuu huku akilia kwa uchungu.

    “Usijali baba. Yaliyopita, tuyaache yapite. Nimefurahi sana kukutana na baba yangu” Abuu alimwambia baba yake, mzee Selemani.

    Hapo ndipo mzee Selemani akaanza kutoa utambulisho juu ya Bi Siwema na watoto wake wengine, Rahman na Latifa. Abuu akaonekana kuwa mwingi wa furaha, hakuamini kama kweli katika kipindi hicho alikuwa amekutana na wadogo zake. Siku hiyo ikaonekana kuwa furaha kwa wote waliokuwa mahali hapo, kwa Abuu, hakutaka kuchelewa, akahitaji likizo ya mwezi mzima kukaa nchini Tanzania ambapo akatengeneza dawa za magonjwa ya kansa na kisha kuanza kuzisambaza katika hospitali zote kubwa nchini Tanzania.

    Hiyo ikaonekana kuwa faraja kwa Waanzania, hawakuamini kama kweli Abuu alikuwa amekuja kisiri nchini Tanzania na kuwatengenezea dawa zile wagonjwa ambao walikuwa wakiwasumbuliwa na magonjwa ya kansa. Mzee Selemani akaanza kutumia dawa zile ambazo zilionekana kumsaidia kupita kawaida.

    Waafrika wengine kutoka atika nchi mbalimbali barani Afrika wakaanza kuja nchini Tanzania ambapo nao wakaanza kutibiwa magonjwa ya kansa kwa kutumia dawa ile ambayo Abuu alikuwa ameitengeneza.

    Katika kipindi hicho, Abuu hakutaka kuwa na kinyongo au hasira, kitendo cha kukutana na baba yake kilionekana kumpa faraja kupita kawaida. Mara baada ya kipindi cha siku kadhaa wakaelekea katika makaburi ya Bi Mtumwa yaliyokuwa Tandale ambapo wakaliangalia kaburi la mama yake, Jamala. Kwa mzee Selemani alionekana kuumia kupita kawaida, hakuamini kama yule mpenzi wake, Jamala ambaye alikuwa akimpenda kupita kawaida katika kipindi hicho alikuwa tayari kaburini.

    “Nisamehe jamala” Mzee Selamni alisema huku akiwa amepiga magoti katika kaburi lile.

    Baada ya siku kadhaa kukatika, jasmin akatakiwa kurudi nchini Tanzania ambapo harusi ikafungwa huku mzee Selemani akipata nafasi ya kukaa kwa muda mrefu na mjukuu wake, mtoto wa Abuu, Zubeda.

    “Kuna lolote mngependa nifanye kwa ajili yenu wadogo zangu?” Abuu aliwauliza Rahman na Latifa mara baada ya siku tano baada ya harusi.

    “Nataka kuja kusoma Marekani” Rahman alisema.

    “Na wewe Latifa?”

    “Nataka kuja Marekani kuishi huko pia” Latifa alijibu.

    “Sawa. Hilo si tatizo. Ila wazazi watakaa na nani kama ninyi wote mkija kuishi Marekani?” Abuu aliuliza.

    “Usijali Abuu. Tuna wafanyakazi wawili ambao watakuwa wakitusaidia. Wafanyie wadogo zako kile wanachotaka uwafanyie” Mzee Selamani alimwambia Abuu.

    “Sawa hakuna tatizo. Ndani ya miezi mitatu mtakuwa mkiishi nchini Marekani na kuwatafutia vyuo vya kusoma. Cha msingi, kuweni makini kwa kila mnachokifanya” Abuu aliwaambia.

    “Usijali kaka. Tutafanya kama ulivyotuambia”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya siku kumi na tano, Abuu na mke wake pamoja na mtoto wake wakarudi nchini Marekani, hiyo ikaonekana kuwa faraja katika maisha yao, katika kipindi hicho walikuwa huru wa kufanya kila walichotaka kukifanya kwa sababu tu walikuwa wamekwishaoana na kuwa mume na mke.

    Kitendo cha kukutana na baba yake kilimpa furaha sana Abuu, hakuamini kama baba yake huyo alikuwa hai nchini Tanzania. Kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha ya nyuma, alikuwa amekwishasahau na kumsamehe na kuangalia maisha ya mbele.

    Kwa sababu Abuu aliendelea kufanya kazi nchini Marekani, nchi hiyo ikatoa madaktari watano ambao walitakiwa kuja kufanya kazi katika hospitali kubwa nchini Tanzania huku kuhusu malipo, nchi hiyop ikiwa inawalipa. Hiyo ikaonekana kuwa shukrani kwa nchi ya Marekani kwa Tanzania kwa kitendo cha kumuacha Abuu kufanya kazi katika nchi yao, hasa katika hospitali kubwa ya Medical centre iliyokuwa jijini new York.

    “Chora picha ya maisha yako mume wangu” Jasmin alimwambia Abuu.

    “Mimi si mchoraji mke wangu. Ila kama ningekuwa mchoraji na ninatakiwa kuchora picha kuhusu maisha yangu basi ningechora saa iliyojifukia nusu katika mchanga huku mawingu yakionekana, tena picha yenyewe iwe imepauka. Kupauka kwa picha hiyo kutakuwa kukimaanisha huzuni katika maisha yangu, saa ile itakuwa ikionyesha majira kwamba mara nyingi maisha hubadilika. Leo unajikuta upo hapa, kesho upo pale. Ila vyote kwa pamoja, SIKU YANGU IMEKUWA NDEFU MNO katika maisha yangu ya nyuma. Shida nilizokuwa nikizipata, manyanyaso niliyokuwa nikiyapata, kutengwa kwangu, vilikuwa ni vitu ambavyo nilikuwa naona siku kuwa ndefu sana kupita kawaida” Abuu alimwambia mke wake.

    “Yote ni maisha. Hatutakiwi kukata tamaa. Leo tunapokuwa hapa, haimaanishi tutakuwa hapa milele. Hapana. Kuna siku kila kitu kitakuja kubadilika, tutatoka katika maisha ya shida tuliyo nayo na kuingia katika maisha ya faraja, maisha ambayo yatatufanya kusahau shida katika maisha yetu. Picha ya maisha yako nimeipenda, ni moja ya picha bora katika maisha yangu. Nakupenda mpenzi” Jasmin alimwambia Abuu.

    “Nakupenda pia” Abuu aliitikia na kisha kujifunika shuka. Kutokana na baridi ambalo lilikuwepo katika usiku huo jijini New York, wakakumbatiana huku wakiwa watupu.





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO.





    *** toa maoni yako kuhusiana na Riwaya hii kali na kufundisha.. Kipi kimekugusa??

0 comments:

Post a Comment

Blog