Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NOTHING WITHOUT YOU (SI KITU BILA WEWE) - 1

 





    IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI



    *********************************************************************************



    Simulizi : Nothing Without You (Si Kitu Bila Wewe)

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Hali ya hewa tayari ilianza kubadilika mahali hapo, jua ambalo lilikuwa katika kipindi kifupi kilichopita lilianza kupotezwa na mawingu yaliyokuwa na rangi ya kijivu ambayo yalikuwa yametanda angani. Kadri muda ulivyozidi kusonga mbele na ndivyo hali ya hewa ilivyozidi kubadilika hali iliyoonyesha kwamba muda wowote ule mvua ingeanza kunyesha mahali hapo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Upepo ukaanza kuvuma kwa mbali, manyunyu yakaanza kudondoka, watu ambao walikuwa na miamvuli, wakaifungua na kuanza kujikinga nayo katika kipindi hicho ambacho mkutano wa Injili ulikuwa ukiendelea katika uwanja wa mpira wa Makao uliokuwa katika kijiji cha Chibe mkoani Shinyanga.

    Mchungaji Zakayo alikuwa akiendelea kuhubiri; kila wakati alikuwa akijifuta jasho ambalo lilikuwa likimtoka huku mara kwa mara akinywa maji ambayo yalikuwa katika kichupa kidogo. Ingawa manyunyu yalikuwa yameanza kudondoka lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alidiriki kuondoka uwanjani hapo.

    Mzee Innocent alikuwa amesimama pamoja na familia yake, mkewe Anna, alikuwa upande wa kushoto huku mtoto wake Patrick akiwa mkono wake wa kulia. Wote watatu macho yao yalikuwa yakimwangalia mchungaji Zakayo ambaye alikuwa akiendelea kuhubiri katika jukwaa lililokuwa uwanjani hapo.

    Kila mtu ambaye alikuwa katika uwanja ule akaonekana kutikisa kichwa chake juu kwenda chini na chini kwenda juu kwa kila neno ambalo mchungaji Zakayo alikuwa akiliongea katika kipindi hicho. Watu wengine walionekana kuumizwa sana na maneno ambayo yalikuwa yakitoka mdomoni mwa mchungaji kiasi ambacho kiliwafanya baadhi yao kuanza kutokwa na machozi.

    “Bado Yesu anakupenda, hata kama umetengwa na ndugu zako, rafiki zako, na hata majirani zako, amini kwamba atakuwa pamoja nawe katika maisha yako yote.” Mchungaji Zakayo aliendelea kuhubiri.

    “Yesu ndio kimbilio lako katika maisha yako, Yeye hatokutenga kamwe. Kila siku atakuwa pamoja nawe akikufariji na kukutia nguvu katika safari hii ya kwenda Mbinguni.” Mchungaji Zakayo aliendelea kuhubiri.

    Vilio vingi zaidi viliendelea kusikika kutoka katika umati ambao ulikuwa umekusanyika mahali hapo. Kila mtu akaonekana kuguswa na maneno ambayo yaliongewa na mchungaji Zakayo. Mchungaji hakutaka kunyamaza, aliendelea kuongea maneno ya kuwafariji na kuwatia moyo kila wakati.

    Mzee Innocent pamoja na mkewe Anna, walikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wakilia uwanjani hapo. Maneno ambayo aliyaongea mchungaji Zakayo ndiyo yaliyoonekana kuwagusa kupita kiasi. Mioyo yao iliumia sana; kila kitu ambacho alikiongea mchungaji kilikuwa kikilenga maisha yao ya kila siku.

    Mchungaji Zakayo aliendelea kuhubiri zaidi na zaidi mpaka katika kipindi ambacho alimaliza kuhubiri na kisha kuanza kumshukuru Mungu na mkutano kufungwa na kisha watu kuanza kutawanyika kuelekea majumbani mwao. Mzee Innocent pamoja na familia yake wakaanza kupiga hatua za haraka haraka kumfuata mchungaji ambaye alikuwa nyuma ya jukwaa akijiandaa kuondoka uwanjani hapo.

    Tayari giza lilikuwa limeanza kuingia mahali hapo huku yale manyunyu kuacha kudondoka. Mara baada ya kufika nyuma ya jukwaa lile, wakamkuta mchungaji Zakayo akiwafanyia maombi binafsi watu ambao walikuwa wakihitaji kufanyiwa maombi kwa wakati huo.

    “Bwana Yesu Asifiwe.”

    Wote walijikuta wakimsalimia mchungaji.

    “Amen.”

    Mchungaji Zakayo aliitikia huku akiachia tabasamu.

    “Tuna tatizo mchungaji.”

    Mzee Innocent alimwambia mchungaji kwa sauti liyojaa upole huku uso wake ukionyesha tabasamu pana.

    “Tatizo gani tena watumishi wa Mungu?”

    “Kijijini kwetu. Yaani kila siku tumekuwa watu wa kutengwa; hakuna mtu ambaye anataka kuongea na sisi, kila mtu anatuona kuwa sisi ni wabaya.”

    Mzee Innocent alimwambia mchungaji.

    “Ila nilikwishawaambia kwamba hamtakiwi kuwa na wasiwasi kabisa. Hayo ni majaribu ambayo hayana budi kutokea. Itawabidi msimame imara katika Neno la Mungu Naye Atawasaidia.”

    Mchungaji aliwaambia.

    Bado waliendelea kuongea mambo mengi huku mchungaji akiendelea kuwatia moyo hali ambayo ilionekana kurudisha matumaini yao katika mioyo yao. Mchungaji akaona hiyo kutotosha hali ambayo ilimfanya kuwafanyia maombi na kisha kuwaruhusu kwenda nyumbani kwao.

    “Ninampenda mwanaume yule mama. Ni lazima niwe kama yeye.”

    Patrick alimwambia mama yake kuhusu mchungaji Zakayo.

    “Usijali mwanangu. Kuna siku utakuwa kama yeye.”

    Anna alimwambia Patrick ambaye alikuwa na miaka kumi na sita.









    ******************







    Bado mauaji yalikuwa yakiendelea kutokea katika vijiji mbalimbali vya Shinyanga. Wakinamama au wakinababa ambao walikuwa na macho mekundu bado walikuwa wakiendelea kuuawa kwa kusadikiwa kuwa wachawi. Kutokana na hali ngumu ya maisha ambayo ilikuwa imeutawala mkoa wote wa Shinyanga, watu hawakuwa na fedha zozote za kuweza kununua mkaa hali iliyofanya kutumia kuni kupikia.

    Moshi wa kuni hizo ndizo ambazo ziliyafanya macho yao kuwa mekundu. Bado waliendelea kuuawa pasipo kujali kuwa wekundu wa macho hayo ulisababishwa na moshi mwingi katika kipindi cha kuandaa chakula cha familia. Ingawa Serikali ilikuwa imeweka vikwazo na vitisho kwa wote ambao walikuwa na tabia ya kufanya mauaji hayo lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyeonekana kujali.

    Familia ambazo zilikuwa zikionekana kama kujihusisha na mambo ya kichawi zilikuwa zikitengwa ingawa familia nyingine hazikuwa zikifanya mambo hayo ya kishirikina. Kila mwezi idadi ya watu waliokuwa wakiuawa katika vijiji vya mkoani Shinyanga kwa kukisiwa kuwa wachawi ilikuwa ikiongezeka kwa kasi kupita kawaida.

    Familia ya mzee Innocent ndiyo ilikuwa familia pekee ambayo ilikuwa imetengwa katika kijiji cha Chibe. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akilisogelea eneo la nyumba yao, macho yao mekundu ndiyo ambayo yaliwafanya watu kuona kwamba watu hao walikuwa wachawi.

    Ingawa walikuwa wakielekea katika kanisa la kijiji cha Beda lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akiwaamini, kila siku watu waliwaona kuwa wachawi ambao walikuwa wakitumia dini kama mwamvuli wa kufunika maovu ambayo walikuwa wakiyafanya.

    Hawakushirikishwa katika kikao chochote kijijini hapo, na kama ilitokea wakashiriki, basi kila mtu alikuwa akiondoka mahali hapo na kuwaacha peke yao. Tayari maisha yakaonekana kuwa magumu, hawakuonekana kuwa na raha hata kidogo, masengenyo ndiyo ambayo walikuwa wamezoea kuyasikia kutoka kwa wanakijiji wenzao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Roho za chuki zilikuwa zikizidi kuongezeka juu yao. Walikuwa wakichukiwa na wanakijiji wenzao kuliko mtu yeyote yule. Maisha yao yalikuwa ya shida sana kiasi ambacho mara kwa mara walijiona kuwa na kila hali ya kuomba msaada lakini hawakufanya hivyo.

    Hawakuona kama kulikuwa na mtu ambaye angekuwa tayari kuwasaidia kwa msaada wa aina yoyote ile. Walikaa peke yao, hawakutaka shida zao kuwatangazia watu wengine. Kila siku walizidi kumwomba Mungu ili abadilishe kila kitu lakini hakukuwa na kitu chochote kilichobadilika.

    Kila kona walikuwa wakiitwa wachawi huku wakizomewa. Kila mmoja akaonekana kuumia lakini hakukuwa na njia yoyote ya kuepuka maneno hayo. Kumtegemea Mungu na kumwombea Patrick afanikiwe maishani mwake ndivyo vitu walivyokuwa wakivifanya kila siku maishani mwao.

    “Mtoto mchawi anapita.”

    Sauti ya mwanafunzi mmoja wa kike ilisikika akiwaambia wenzake katika kipindi ambacho Patrick alikuwa akipita karibu yao.

    Patrick akaonekana kuumia kupita kawaida. Akageuka nyuma na kuwaangalia wasichana wale, wote walikaa kimya. Alipogeuka na kuendelea kupiga hatua, sauti ya vicheko vya vikaanza kusikika tena kutoka kwa wasichana wale. Patick akashindwa kuvumilia, akapiga hatua za haraka haraka kuelekea nyuma ya darasa alilokuwa akisoma na kuanza kulia.

    Shuleni hakukuwa na raha hata kidogo, kila siku alikuwa mtu wa majonzi tu. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akiongea naye shuleni. Katika darasa lilokuwa akisoma, hakukuwa na mwanafunzi yeyote aliyekuwa akikaa pamoja naye katika dawati alilokuwa akikaa yeye.

    Kutengwa kwake hakukuwa kwa wanafunzi tu, bali hata walimu walikuwa wakimtenga. Darasani hakuwa akichaguliwa kujibu swali lolote hata kama alinyoosha mkono, madaftari yake hayakukusanywa wala kusahishwa. Kila mtu hakuwa akimpenda Patrick, alionekana chukizo mbele yao kutokana na imani ya kishirikina ambayo ilikuwa imejengeka katika vichwa vyao juu ya familia yake.

    Kuchapwa hakuwa akichapwa shuleni, kila mwalimu alikuwa akimuogopa kumchapa kwa kuona kama wangepata matatizo endapo usiku ungeingia. Maisha yake yote, Patrick alikuwa na rafiki mmoja ambaye alikuwa akimpenda sana, huyu alikuwa masomo.

    Kila siku Patrick alikuwa mtu wa kusoma tu kwa kuamini kwamba hapo ndipo yalipokuwa maisha ambayo alikuwa akiyatamani kila siku. Hakupenda kabisa wazazi wake waendelee kuishi katika nyumba ya udongo kama ambayo walikuwa wakiishi, alitamani asome kwa bidii, apate fedha na kuwatengenezea wazazi wake nyumba nzuri iliyokuwa na bati pamoja na umeme.

    Mitihani ya kumaliza elimu ya msingi tayari ilikuwa imemalizika na katika kipindi hicho wanafunzi wote wa vijiji vya karibu na kijiji cha Beda ambacho hakikuwa mbali sana na kijiji chao cha Chibe walikuwa wamekusanyika katika ukumbi mmoja mkubwa uliotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kusherehekea mahafali yao.

    Wanafunzi zaidi ya elfu mbili walikuwa wamekusanyika wakicheza muziki ambao ulikuwa ukisikika ukumbini hapo. Ingawa kila mwanafunzi alikuwa na furaha mahali hapo, Patrick alionekana kuwa tofauti kabisa. Alikuwa amekaa pembeni huku akichora chora chini.

    Wanafunzi ambao alikuwa amemaliza pamoja nao, hawakutaka kabisa kumsogelea, kila mmoja alionekana kumuogopa kupita kiasi. Kadri muda ulivyozidi kwenda na ndivyo ambavyo hali ilivyozidi kubadilika, jua likazama na hatimaye kwa mbali kigiza kuanza kunyemelea.

    Bado Patrick alikuwa amekaa katika jiwe lililokuwa pembeni, mara akashtuka baada ya kuona mtu akiwa amesimama mbele yake. Akaanza kuyapandisha macho yake juu, akakutana na uso wa msichana ambaye hakuamini kama angeweza kukutana naye katika maisha yake.

    Akabaki akimwangalia msichana huyo, machoni mwake alikuwa mgeni kabisa, na alijua fika kwamba msichana huyo alikuwa mwanafunzi kutoka katika shule nyingine ambazo zilikuwa zimekusanyika mahali yapo kwa ajili ya kusherehekea mahafali ya kumaliza darasa la saba.

    Patrick akauhisi moyo wake kufa ganzi, damu ikaanza kuzunguka kwa kasi ya ajabu katika mishipa yake hali iliyopelekea moyo wake kudunda kwa kasi huku kijasho chembamba kuanza kumtoka kwa mbali.

    “Naomba tukacheze muziki.”

    Msichana yule alimwambia Patrick ambaye alibaki akimshangaa tu.







    **************************





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bi Anna akaonekana kuwa na wasiwasi, muda ulikuwa umekwenda sana pasipo Patrick kurudi nyumbani. Hofu ikaanza kumshika kwa kuona kwamba tayari mwanawe alikuwa amepatwa na tatizo. Neno ‘mauaji’ ndilo ambalo lilionekana kumtawala akilini mwake.

    Alijua fika kwamba familia za watu mbalimbali waliokuwa wakihisiwa kuwa wachawi zilikuwa zikiuawa katika sehemu mbalimbali mkoani Shinyanga, hali hiyo ndio ambayo ilionekana kumtia wasiwasi. Akajikuta akianza kulia kwa uchungu.

    “Vipi tena mke wangu?”

    Mzee Innocent alimuuliza mkewe, Bi Anna.

    “Patrick mpenzi.”

    “Patrick! Amefanya nini?”

    “Hajarudi mpaka sasa. Nina wasiwasi mpenzi.”

    Bi Anna alisema huku akionekana dhahiri kuwa na wasiwasi.

    “Wasiwasi wa nini tena?”

    “Wanaweza wakawa wamemuua. Hebu fikiria, saa mbili sasa bado hajarudi. Watakuwa wamemuua mwanangu. Ni bora ...”

    Bi Anna alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake akaanza kulia.

    Moyo wake ulikuwa umeumia kupita kiasi, tayari aliona kuwa Patrick alikuwa ameuawa. Amani yote iliyokuwa moyoni mwake ikawa imepotea kabisa. Akaanza kulia kama mtu ambaye alikuwa akiomboleza. Mzee Innocent akawa na kazi kubwa ya kuanza kumbembeleza. Hakuna kitu kilichosaidia, bado Bi Anna alikuwa akiendelea kulia.

    “Kulia hakutasaidia mke wangu. Patrick bado ni mzima, inatubidi tuanze kumuomba Mungu amlinde huko aliko.”

    Mzee Innocent alimwambia mkewe.

    Akamwinua na kumshika mikono. Hawakuwa na tumaini lolote katika maisha yao zaidi ya kuanza kumkabidhi Patrick mikononi mwa Mungu ili amlinde. Sala ilikuwa ikiendelea zaidi na zaidi. Bado walikuwa wakimwamini Mungu kwamba alikuwa na uweza mkubwa wa kumlinda kule alikokuwa na kumnusuru na mauti yoyote ambayo ilikuwa imepangwa.

    Huku wakiwa katikati ya sala, wakapigwa na mshtuko mara baada ya kuona vitu kama maji vikiwa vimewamwagikia. Kwa kutumia mwanga hafifu wa koroboi, wakaanza kuviangalia vimiminiko vile kwa makini huku wakionekana kutokuamni macho yao.

    “Mungu wangu! Petroli.”

    Mzee Innocent alimwambia mkewe huku petroli ile ikizidi kumwagiwa katika nyumba ile.

    Mara minong’ono ya watu ikaanza kusikika kutoka nje ya nyumba ile hali ambayo ilionekana kuwatia wasiwasi. Huku akionekana kujiamini, mzee Innocent akaufungua mlango na kuchungulia nje, akashtukia akipigwa na kitu kizito usoni ambacho kilimfanya kuangukia ndani huku damu zikianza kumtoka usoni.

    Bi Anna akabaki akiwa na wasiwasi, hata kabla hajajua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, akashtuka alipoona nyumba hiyo ya nyasi ikianza kuteketezwa kwa moto. Bi Anna akabaki akilia huku akimuinua mumewe, tayari waliuona mwisho wa maisha yao ukiwa umekaribia, sala zote ambazo walikuwa wakisali katika kipindi cha nyuma, wakaonekana kusahau.

    “Inuka mume wangu ...tunakufa mume wangu...”

    Bi Anna alimwambia mumewe huku akilia.

    Vicheko na sauti za kushangilia zikaanza kusikika nje ya nyumba yao huku moto ukiendelea kuiteketeza nyumba ile. Mzee Innocent akainuka huku akianza kuyumbayumba kama mtu aliyelewa. Akamwangalia mkewe, akajiweka sawa na kurudiwa na hali yake ya kawaida.

    “Tunakufa mume wangu... tusali sala ya mwisho... wamekuja kutuua...”

    Bi Anna alimwambia mumewe huku akimshika mikono miwili.

    “Hata kama tutakufa... naamini tutakwenda Mbinguni kupumzika”

    Mzee Innocent alimwambia mkewe, Bi Anna.

    “Lakini vipi kuhusu mtoto wetu Patrick?”

    Bi Anna alimuuliza mumewe.

    Taswira ya sura ya Patrick ikaanza kujijenga kichwani mwa mzee Innocent. Ni kweli aliuona mwisho wao kufikia tamati, lakini hakujua kama wangeuawa kwa wakati huo Patrick angebaki katika maisha gani duniani. Akajiona akipata nguvu, alitamani kutoka nje na kupambana na watu ambao walikuwa wamekuja kumvamia nyumbani kwake.

    “Ni lazima nipambane nao...nitapambana nao kwa ajili ya Patrick.”

    Mzee Innocent alimwambia Bi Anna na kisha kutoka nje kwa lengo la kupambana na watu hao.

    Bi Anna akabaki ndani akiwa anatetemeka, mara akaanza kusikia sauti ya mumewe ikilia kutoka nje, Bi Anna akatamani atoke nje na kumsaidia mumewe lakini kila alipotaka kufanya hivyo, aliogopa. Sauti ya mumewe iliendelea kusikika zaidi na zaidi akilia, lakini baada ya sekunde kadhaa, sauti ile ikakatika na wala haikusikika tena. Bi Anna hakujua afanye nini, nyumba bado ilikuwa ikiendelea kuteteketea kwa moto.

    “Bado mkewe na mtoto wake... tuingieni ndani na wao tuwaue”

    Sauti ya mwanaume mmoja ilisikika, Bi Anna akazidi kutetemeka kwa hofu.





    ****************************







    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vijana wa kijiji cha Chibe walionekana kuamua. Hali ambayo ilikuwa ikiwatokea usiku kila siku ilionekana kuwachosha. Mara nyingi walikuwa wakilala vitandani mwao usiku lakini kitu cha ajabu, asubuhi walikuwa wakijikuta wamelala nje huku wakiwa wachafu kupita kiasi. Miili yao ilikuwa ikichoka kupita kiasi kitu ambacho walijua kuwa ni lazima usiku walikuwa wakichukuliwa na kupelekwa mashambani kulima.

    Hali ile ikaonekana kuwachosha kupita kiasi. Msako wa kuwatafuta watu ambao walikuwa wakiwafanya hivyo kuanza. Katika vijiji vingine, watu wengi waliokuwa wakihisiwa kuwa ni wachawi walikuwa wakiuawa kupita kiasi huku dalili zake zikiwa ni kukutwa na macho mekundu.

    Hali hiyo ndio ikawapelekea kuihisi familia ya mzee Innocent, hawakuona sababu yoyote ya familia hiyo kuendelea kuvuta pumzi ya dunia hii na wakati walikuwa wakiwatesa watu usiku. Mashambulizi ya kuwaangamiza watu hawa bado ulikuwa ukiendelea katika vijiji mbalimbali mkoani Shinyanga.

    Vijana zaidi ya ishirini walikuwa wamekusanyika nje ya nyumba ya mwenyekiti wa kijiji hicho mzee Msumari. Vijana hao hawakuwa mikono mitupu, silaha mbalimbali ziikuwa mikononi mwao. Nyuso zao hazikuonekana kuwa na amani hata mara moja, walionekana kukasirika kupita kiasi.

    Nyimbo mbalimbali zilikuwa zikiendelea kuimbwa kwa mbwembwe huku zikimaanisha juu ya hasira kubwa waliokuwa nayo katika kipindi hicho. Mara baada ya dakika kadhaa, mwenyekiti wa kijiji hicho, mzee Msumari akatokea mahali hapo na kuanza kuwaangalia vijana wote aambao walikuwa wamekusanyika katika eneo la nyumba yake.

    “Mbona usiku namna hii?”

    Mzee Msumari aliwauliza huku akionekana kushangaa.

    “Tumekuja mahali hapa kwa kuwa tuna shida na wewe”

    Kijana ambaye alionekana kuwa kiongozi, Manase alimwambia mzee Msumari.

    “Mna shida na mimi huku silaha mkononi! Shida gani hiyo usiku wote huu?” Mzee Msumari aliwauliza huku bado akiendelea kushangaa.

    “Tunataka kukamilisha kila kitu, kila siku familia zetu zinaumizwa, ni lazima tufanye jambo kuziokoa”

    Manase alimwambia mzee Msumari huku vijana wengine wakitikisa vichwa vyao chini na juu.

    “Bado mnanichanganya, sijafahamu hizo silaha zinamaanisha nini juu ya jambo mnalonieleza” Mzee Msumari aliwaambia.

    “Tunataka kuwaondoa wabaya wetu ambao wanatukosesha amani kijijini hapa. Tunataka tuanze na familia ya mzee Innocent”

    Manase alimwambia.

    “Ina maana mnataka kuiteketeza familia ile kama wanavyofanya vijiji vingine?”

    “Ndio. Tena usiku huu huu”

    Manase alimwambia mzee Msumari.

    “Haiwezekani. Haiwezekani hata kidogo. Kama mmekuja kuomba ruhusa.....hapa hakuna ruhusa juu ya jambo kama hilo. Haiwezekani”

    Mzee Msumari aliwaambia.

    Vijana wale wakaonekana kukasirika, wakamuona mwenyekiti wao kuwa miongoni mwa wasaliti wao. Wakaona kwamba wasingepata msaada wowote kutoka kwa mwenyekiti huyo. Wote wakapanga kuondoka mahali hapo na kwenda kujichukulia shera mkononi.

    Waliokuwa na marungu, wakayaandaa vizuri, waliokuwa na mapanga, nao pia wakayaandaa vizuri. Fimbo zikaandaliwa vilivyo na zote zilitakiwa kuisha katika miili ya watu ambao walikuwa wamepanga kuwaangamiza. Moja kwa moja safari ya kuelekea nyumbani kwa mzee Innocent kuanza.

    Vijana wote walikuwa wakiimba kwa shangwe kama wanajeshi ambao walikuwa wakielekea katika uwanja wa vita. Walipofika hatua themanini kabla ya kuifikia nyumba ya mzee Innocent, wakanyamaza na kuanza kutembea kimya kimya.

    Wakaizunguka nyumba ile. Kijana mmoja ambaye alikuwa na dumu lililojaa petroli akaanza kuimwagia nyumba ile na bila kupoteza muda wowote ule, Manase akawasha kiberiti chake na kisha kukitupa katika nyasi za nyumba ile, nymba ikaanza kuteteketea.

    Ghafla, mlango ukafunguliwa na mzee Innocent kuchungulia nje, Manase akachukua rungu ambalo alikuwa nalo mkononi na kumpiga mzee Innocent usoni na kuangukia ndani. Vijana wote wakaanza kushangilia kwa shangwe, nyumba ile ilizidi kuteketea.

    Baada ya dakika chache, mlango ukafunguliwa na mzee Innocent kutoka. Vijana wote wakamvamia na kuanza kumshabulia. Waliokuwa na marungu, walikuwa wakimpiga na marungu waliokuwa nayo. Waliokuwa na mapanga, wakaanza kumkatakata pasipo huruma yoyote ile.

    Damu zikaanza kumtoka mzee Innocent huku akianza kupiga kelele. Fimbo mfululizo zikaanza kumwangukia mwilii mwake kiasi ambacho fimbo zote walizokuwa wamekuja nazo vijana wale zikaishia mwilini mwake. Mzee Innocent bado alikuwa akipiga kelele huku akiomba msaada, wala haukupita muda mrefu, akaanguka chini na kubaki kimya..

    “Tumeua....”

    Kijana mmoja aliwaambia wenzake.

    “Hili ndilo lilikuwa lengo letu”

    Kijana mwingine alimwambia.

    “Bado mkewe na mtoto wake...tuingieni ndani na wao tuwaue”

    Manase aliwaambia wenzake na kisha kuanza kuufuata mlango na kuufungua.

    Ndani hakukuwa na mtu yeyote, kila mmoja akaonekana kuchanganyikiwa, wakaangalia angaliandani ya nyumba ile, kulikuwa na sehemu moja ambayo ilikuwa na tundu kubwa. Hakukuwa na sababu ya kujiuliza, moja kwa moja wakajua kwamba sehemu hiyo ndio waliyoitumia watu waliokuwa wakiwataka kutorokea.

    “Watakuwa hawajafika mbali kuoka mahali hapa....ni lazima tutawanyike na kuwatafuta, tukiwapata...tuwaueni. Mmenielewa?”

    Manase alisema na kuuliza.

    “Tumekuelewa”

    Vijana wale waliitikia na kutawayika mahali hapo kwa lengo la kumtafuta Bi Anna na Patrick.





    **********************************



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Patrick bado alikuwa amemkazia macho msichana yule ambaye alisimama mbele yake akimuomba kucheza nae. Mshangao kubwa ulikuwa umemshika, hakuelewa kwa nini msichana yule hakuwa akimuogopa kutokana na sifa kubwa ya uchawi ambayo alikuwa amepewa.

    Patrick akasimama na kuendelea kumwangalia msichana yule, bado mapigo yake ya moyo yalikuwa yakiendelea kumdunda kupita kawaida, hakueewa msichana yule alikuwa na lengo gani kwake. Wanafunzi wengine ambao walikuwa wamesoma nae shule moja, wakaonekana kumshangaa mschana yule ambaye wala hakuonekana kuogopa kitu chochote kile.

    “Naitwa Siwema. Siwema Abdallah”

    Msichana yule alijitambulisha kwa Patrick huku akijaribu kuupeleka mkono wake katika mkono wa Patrick.

    “Naomba tukacheze muziki”

    Siwema aliendelea kumwambia Abdallah.

    Patrick hakutaka kubaki mahali hapo, akaanza kupiga hatua kurudi nyuma na baada ya kufika umbali fulani, akaanza kukimbia kuelekea porini. Siwema hakutaka kusimama mahali hapo, nae akaanza kukimbia kuelekea kule ambapo Patrick alikuwa amekimbilia. Kutokana na kasi kubwa aliyokuwa akiitumia Patrick, Siwema hakuweza kumuona.

    Tayari giza lilikuwa limeingia. Patrick akazidi kukimbia zaidi na zaidi. Moyo wake ulikuwa na wasiwasi mkubwa kwamba wazazi wake walikuwa wakimsubiri kwani haikuwa kawaida yake kuchelewa kufika nyumbani. Hakutaka kuyasubiri magari ambayo yalikuwa yakiwachukua wanafunzi kuwapeleka katika vijiji mbalimbali kwani aliamini kuwa asingechukuliwa kama ambavyo alifanyiwa kipindi cha kwenda mahali pale.

    Giza lilikuwa limekwishaingia na bado alikuwa akikimbia kwa mwendo wa kasi kuelekea kijijini kwao, Chibe. Ingawa kulikuwa na giza lakini Patrick hakuonekana kuogopa kitu chochote kile, alichokuwa akikitaka kwa wakati huo ni kuingia kijijini na kuelekea nyumbani kwao.

    Kwa mbali Patick akaanza kuuona mwanga wa moto ambao ulikuwa ukiwaka, Patrick akasogea zaidi na zaidi kuelekea kule kulipokuwa na eneo la nyumba yao. Patrick akaonekana kushtuka kupita kiasi, nyumba ambayo ilikuwa ikiyteketea kwa moto ilikuwa nyumba yao.

    Akajificha katika kichaka kimoja na kuanza kuangalia kule kulipokuwa na nyumba yao. Vijana zaidi ya ishirini walikuwa nje ya nyumba ile huku wakishangilia kwa shangwe. Mara akamuona baba yake, mzee Innocent akitoka nje na wale watu kumvamia.

    Kila kitu ambacho kilikuwa kinatokea, Patrick alikuwa akikiangalia, hakujua afanye nini, alimuona baba yake akishambuliwa na vijana wengi ambao walikuwa nje ya nyumba ile. Moyo wake ulimuuma kupita kawaida, akaanza kulia kwa uchungu kichakani pale. Mara baada ya wale vijana kumshambulia baba yake, moja kwa moja wote wakaingia ndani ya nyumba ile.

    Patrick hakutaka kuendelea kubaki mahali pale, tayari alikwishaona sehemu ile kuwa na hatari, alichokifanya ni kuanza kukimbia kuelekea porini huku akilia kupita kawaida. Alishuhudia baba yake akiuawa mbele ya macho yake, hakujua kuhusu mama yake, ila moyo wake ulimwambia kuwa mama yake nae alishambuliwa na vijana wale na kubaki peke yake.

    Alijiona kuanza kuishi maisha ya peke yake, jina ‘Yatima’ ndilo ambalo alikuwa amejipa kwa wakati huo. Hakuona sababu yoyote ya kuwa na amani tena moyoni mwake.

    Patrick aliendelea kukimbia kwa mwendo wa kasi, alikimbia kiasi ambacho akajikuta akichoka. Alipata muda wa kupumzika na kisha kuendelea tena na safari ya kuelekea kule asipopajua. Umbali wa kilometa zaidi ya kumi ndio ambao alikuwa amekimbia. Alijihisi kuchoka sana hali iliyompelekea kutafuta sehemu nzuri na kupumzika chini ya mti.

    Lengo lake kubwa lilikuwa ni kulala hapo chini ya mti. Usingizi ulionekana kuwa mgumu, taswira ya picha ya baba yake ambaye alikuwa akishambuliwa na vijana wale waliokuwa na hasira kali ilikuwa ikimjia kichwani mara kwa mara. Patrick aliumia kupita kiasi, alibaki akilia tu. Patrick alipata usingizi wa mang’amung’amu baada ya saa moja kupita. Ndoto mbaya na za kutisha ndizo ambazo zilikuwa zimemtawala katika usingizi wake.

    Sauti za ndege zilikuwa zikisikika kwa mbali porini hapo hali iliyoashiria tayari asubuhi ya siku nyingine ilikuwa imeingia. Mwanga tayari ukaanza kuonekana. Patrick bado alikuwa amelala usigizi mzito. Mara baada ya mwanga wa jua lililochomoza kumpiga usoni, akashtuka kutoka usingizini. Patrick akaonekana kustuka kupita kiasi, watu zaidi ya watano waliokuwa wameshika silaha mbalimbali walikuwa wamesimama mbele yake wakimwangalia.

    Patrick akaonekana kuogopa, mwili wake wote ukapatwa na ganzi. Tayari hali ya hatari ikaonekana kumpata. Akabaki akilia, tayari alikwishaona watu ambao alikuwa amewakimbia walikuwa wamekwishamfikia kule alipokuwa. Akaanza kulia kwa kuomba msamaha.

    “Naombeni mnisamehe...naombeni mnisamehe”

    Patrick alilia huku akiomba msamaha. Patrick alionekana kuchanganyikiwa mara baada ya kuwaona vijana wale wakiziweka vizuri silaha zao.









    *************************











    Bi Anna alibaki akitetemeka ndani ya nyumba, tayari alikwishaona zamu yake ilikuwa imemfikia. Hakujiona kuwa na zaidi ya dakika tano za kuendelea kuvuta pumzi ya dunia hii. Alibaki pale ndani huku kijasho chembamba kikianza kumtoka.

    Alijiona yeye ndiye ambaye alikuwa akifuatia mara baada ya mumewe kuuawa kwa kushambuliwa na watu hao waliokuwa na silaha mbalimbali. Akabaki kimya kwa muda huku akijifikiria ni kwa njia gani angeweza kutoka salama na kunusurika kutoka katika mikono ya wale vijana.

    Bi Anna akaanza kuangalia huku na kule ndani ya nyumba ile. Akaiona sehemu ambayo ilikuwa imeteketzwa kwa moto, akaanza kuifuata na kuanza kuzitoa nyasi ambazo zilikuwa zimebabikia. Akapata sehemu ya kupenyea na kutorokea kupitia kule nyuma ya nyumba yake.

    Kutokana na vijana wale waliokuwa nyuma ya nyumba kukimbia mbele ya nyumba ile kwa ajili ya kumshambulia mzee Innocent, Bi Anna akaonekana kuwa na bahati kupita kawaida. Hakukuwa na kijana yeyote nyuma ya nyumba. Akaanza kukimbia kwa mwendo wa kasi kuelekea kichakani.

    Akaingia kichakani huku akianza kuangalia kule ilipokuwa nyumba yake ambayo asilimia kubwa ilikuwa imeteketea kwa moto. Bi Anna akaonekana kuumia kupita kiasi, chuki kubwa ikamjaa moyoni mwake juu ya vijana wote waliokuwa katika kijiji kile.

    “Ni lazima nikimbie kuelekea katika kijiji chochote tofauti na hiki”

    Bi Anna allisema huku akijifuta machozi ambayo yalikuwa yakimtomka na kuanza kukimbia.

    Bi Anna alikimbia kwa mwendo wa kasi kubwa, ingawa kulikuwa na giza kubwa lakini wala hakuonekana kujikwaa wala kujichoma na mwiba. Aliruka katika sehemu zote ambazo zilitakiwa kurukwa, macho yake yalikuwa yamepata nguvu kubwa katika uonaji.

    Alikimbia kwa takribani masaa mawili, akatokea katika sehemu ambayo kwa mbali akaanza kuona taa, moyo wake ukaanza kupatwa na furaha kwani tayari aliona kuwa alikuwa amekimbilia sehemu sahihi.





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******************************************





    Kijiji cha Wami kilionekana kuwa tofauti na vijiji vyote ambavyo vilikuwa mkoani Shinyanga. Hakukuwa na tabia ya kufanya mauaji kwa watu ambao walikuwa na macho mekundu kwa kuwahisi kuwa ni wachawi. Kila mtu aliishi kwa amani na upendo huku dini ya Kiislamu ndio ikionekana kuwa nguzo kubwa.

    Mara kwa mara wanakijiji wa kijiji hiki walikuwa wakienda kuwinda na wanyama ambao walikuwa wakipatikana huko, basi kila mwanakiji alikuwa akipewa na kufanya kitoweo cha siku hiyo. Hayo ndio maisha ambayo walikuwa wakiishi wanakijiji wa kijiji cha Wami.

    Ibada ndio ikawa sehemu kubwa ya maisha yao, walimtegemea Mungu katika maisha yao kuliko kitu kingine. Katika vijiji vyote ambavyo vilikuwa vikizidi kuendelea kwa kasi, basi kijiji cha Wami kilikuwa kimojawapo. Hakukuwa na shida kubwa ya maji kama ilivyokuwa katika vijiji vingine.

    Viongozi wa kijiji hiki walikuwa wakikiendeleza kijiji hiki katika maendeleo ambayo yalipaswa kuigwa kama mfano na vijiji vingine. Watu hawakuwa wakipigana, na hata kama kitu kama hicho kilikuwa kinatokea, basi ilikuwa ni lazima wapatanishwe na kuwa marafiki kama kawaida.

    Wanakijiji wa kijiji hiki waliishi kama ndugu huku kila siku wakiomba Mungu aendelee kuwalinda katika uhusiano mkubwa ambao walikuwa nao mioyoni mwao. Kwa kuwa asilimia kubwa ya wanakijiji wa kijij hiki walikuwa wakijihusisha na kilimo, basi mazao mengi ambayo yalikuwa yakipatikana walikuwa wakigawana kijiji kizima.

    Kila mtu ambaye alikulia kijijini hapo, upendo na amani ndio ilikuwa sehemu kubwa katika maisha yake. Mikwaruzano ya hapa na pale haikuwa ikipewa nafasi maishani mwao. Kila siku wanakiji wa kijiji hiki cha Wami walikuwa wakiswali msikitini huku wale wakristo wachache wakielekea kanisani kusali.

    “Usilie...wewe ni nani na unafanya nini mahali hapa?” Sauti ya muindaji mmoja kutoka katika kijiji cha Wami alimuuliza Patrick ambaye alikuwa akilia huku akitetemeka.

    Patrick bado alikuwa akilia huku akionekana kuogopa, hakuamini kama watu wale ambao walikuwa wamesimama walikuwa watu wazuri kwake au watu wale ambao walikuwa wameiteketeza nyumba yao na kumuua baba yake.

    Vijana wale wawindaji wakaanza kumtoa wasiwasi Patrick kwa kutaka kumhakikishia usalama wa maisha yake na kisha kuomba kuelezwa juu ya kile ambacho kilikuwa kimempata.

    Patrick akaanza kuelezea kila kitu pasipo kuacha hata kitu kimoja. Kila alipokuwa akielezea, alikuwa akilia. Moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita kawaida. Kila mtu akaonekana kutokuamini kama kweli mambo yale yalikuwa yakiendelea kutokea ingawa serikali kila siku ilikuwa ikiyapigia kelele.

    Kila mmoja akaonekana kumuonea huruma Patrick ambaye alionekana kuhitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu ambao walikuwa wamesimama mbele yake. Nyuso za huzuni ndizo ambazo zilikuwa zimewatawala. Patrick, kwao alionekana kijana mdogo sana kupitia matatizo ambayo alikuwa amepitia kwa wakati huo.

    “Ni lazima turudi nae kijijini. Maisha yake yanaonekana kutokuwa na usalama wowote ule” Kijana mmoja aliwaambia wenzake ambao wote wakaonekana kukubaliana nae.

    Safari ya kurudi kijijini ikaanza huku wakiwa pamoja na Patrick ambaye alikuwa akimshukuru Mungu kila wakati. Hakuamini kama watu ambao walikuwa wamemchukua walikuwa salama katika maisha yake au la, kitu alichokifanya ni kukubaliana nao kuelekea kijijini.

    Walitumia dakika hamsini hadi kufika kijijini Wami. Kila mtu alikuwa akiwaangalia wawindaji wale pamoja na Patrick ambaye walikuwa wamekuja nae pale kijijini. Safari ikaishia katika eneo la nyumba ya mwenyekiti wa kijiji, mzee Abdallah na kumpa taarifa juu ya kila kilichotokea juu ya Patrick.

    “Ataishi hapa mpaka hapo atakapofikisha miaka kumi na nane na kuamua pa kwenda kuishi” Mzee Abdallah aliwaambia.

    Maisha ya Patrick yakaanza upya katika kiji cha Wami. Amani na upendo ambavyo vilikuwa vikipatikana katika kijiji hicho vilimfanya kujisikia vizuri kuliko kitu kingine. Patrick hakuhitajika kukaa peke yake kutokana na msongo wa mawazo ambao mara kwa mara ulikuwa ukimuandama.

    Vijana watatu wakachaguliwa ambao walitakiwa kuwa na Patrick katika wakati wote kwa ajili ya kuhakikisha kwamba anakuwa katika hali isiyokuwa na mawazo kwa kucheza nae na kufanya mambo mengine. Kwa kiasi fulani hali hii ikaonekana kusaidia, Patrick hakuwa mtu wa mawazo kama ilivyokuwa katika kipindi cha nyuma, mara kwa mara alikuwa akiongea na marafiki zake hao ambao walionekana kuwa karibu nao.

    Hapo ndipo Patrick akakigundua kipaji kikubwa alichokuwa nacho cha uchoraji. Akaanza kuchora picha mbalimbali ambazo kila mtu alionekana kuzikubali. Picha zile hazikuonekana kuchorwa, zilikuwa kama picha ambazo zilipigwa na kamera kubwa iliyokuwa ikichukua picha za kuvutia.

    Kila siku Patrick akawa mtu wa kuchora, kuchora ndio ikawa faraja yake kuliko kitu chochote kile. Kila mwanakijiji wa kijiji hicho cha Wami alitokea kuvutiwa na picha ambazo mara kwa mara zilikuwa zikichorwa na Patrick. Kila mwanakiji alikuwa akikishangaa kipaji ambacho alikuwa nacho Patrick.

    Hapo kabla waliwaona wachoraji mbalimbali ambao walikuwa wamechora picha nyingi tofauti tofauti lakini kwa Patrick ilionekana kuwa tofauti kabisa. Sanaa ya uchoraji ilionekana kuwa kubwa katika maisha yake. Hawakujua huko mbele ingekuwa vipi kama angeweza kukiendeleza kipaji chake.

    Miezi mitatu ilikuwa imepita tangu Patrick ahamie kijijin pale. Kila mtu alipenda sana kuwa karibu na Patrick ambaye mara kwa mara alikuwa akiwachora wanakijiji kijijini hapo picha ambazo zilionekana kuwavutia. Ukaribu wa Patrick na wanakijiji wengine ukawa mkubwa, lakini kwa msichana Siwema, ulionekana kuongezeka.

    Kila alipokuwa Patrick, Siwema alikuwa pembeni yake. Tayari kitu cha tofauti kikaanza kuonekana kwa Siwema, kila siku hakutaka kukaa na wasichana wenzake, mtu ambaye kila siku alikuwa akitaka kukaa nae alikuwa Patrick. Kadri siku zilivyozidi kuongezeka na ndivyo ambavyo ukaribu huo ulivyozidi zaidi na zaidi hadi kufika kipindi ambacho kila mtu akahisi kuna kitu cha siri kilikuwa kikiendelea miongoni mwa vijana hao

    Tayari hisia kali za mapenzi zilikuwa zimeanza kumteka Siwema, kila siku alijiona kuwa mtu wa tofauti hasa kila alipokuwa akikaa na Patrick. Moyo wake ulikuwa na dukuduku kubwa la kumwambia Patrick juu ya kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea moyoni mwake lakini alikuwa akiogopa.

    Alimheshimu sana baba yake ambaye alikwa amemlea katika maisha ya kidini, hakutaka kuzielezea hisia kali za mapenzi ambazo alikuwa nazo juu ya Patrick kwa kuogopa kuuchafua moyo wake kwa kuukaribisha uzinzi moyoni mwake. Akaamua kunyamaza kimya ingawa kila siku moyo wake ulikuwa ukijisikia kumwambia ukweli Patrick.

    Wakati mwingine usingizi kwake ulionekana kuwa mgumu kupatikana, alikuwa akibimbilika huku na kule kwa lengo la kuutafuta lakini wala haukupatikana kirahisi, na hata kama ulikuwa ukipatikana, basi Patrick alikuwa akichukua nafasi kubwa sana katika ndoto zake.

    Alijua fika kwamba alikuwa msichana bikira, aliikumbuka sana ahadi ambayo alikuwa amewawekea wazazi wake juu ya maisha yake kwamba asingeweza kufanya tendo lolote la ndoa mpaka pale atakpoolewa na kuwa mke wa mtu. Tayari alikwishaona dalili zote za ahadi aliyoiweka kuanza kuvunjika.

    Patrick alionekana kuwa mwanaume sahihi ambaye kila siku alikuwa akimfikiria katika maisha yake. Kila siku alikuwa akikumbuka siku ya kwanza ambayo alikutana nae katika kipindi ambacho walikuwa wakisherehekea siku ya mahafari ya kumaliza elimu ya msingi.

    Siwema alikuwa ameamua, Patrick ndiye alikuwa mwanaume ambaye alikuwa akimtaka katika maisha yake. Alikuwa tayari kukosa kitu chochote katika maisha yake lakini si kumkosa Patrick. Alikuwa tayari kugombana na mtu yeyote yule, hata wazazi wake lakini ili mladi awe pamoja na Patrick.

    Moyo wake ulikuwa umekufa kwa Patrick ambaye mara kwa mara alikuwa akionekana kuwa bize akichora picha mbalimbali huku wakati mwingine akitumia muda mwingi kuongea na marafiki zake mbalimbali kijijini hapo. Siwema alikuwa akitumia nafasi ambazo Patrick alikuwa akionekana peke yake na kuanza kuongea nae.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kila siku mdomo wake ulikuwa na kigugumizi katika kila kipindi ambacho alikuwa akitaka kuongea na Patrick juu ya kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea moyoni mwake. Hakuelewa ni kwa jinsi gani Patrick angemchukulia kama tu angediriki kumwambia ukweli

    “Unaonekana kuwa na kitu unataka kuniambia” Patrick alimwambia Siwema ambaye alikuwa akimwangalia kwa jicho ambalo lilimaanisha kile ambacho kilikuwa moyoni mwake.

    “Nani? Mimi?” Siwema aliuliza huku akijifanya kushangaa.

    “Ndio. Niambie ni kitu gani ambacho kinakutatiza moyoni. Au unataka nikuchore na wewe pia?” Patrick alimuuliza Siwema.

    “Nafikiri uko sahihi ila ningependa unisaidie kufanya kitu kimoja” Siwema alimwambia Patrick.

    “Kitu gani?”

    “Nataka unisindikize sehemu fulani”

    “Wapi?”

    “Sehemu fulani”

    “Lakini giza linaingia Siwema”

    “Hata kama. Ninaomba unisindikize Patrick. Nakuombaaaa” Siwema alimwambia Patrick.

    Patrick alimwangalia Siwema mara mbili mbili. Hakuonekana kuelewa kile ambacho Siwema alikuwa akikiongea. Kumsindikiza sehemu fulani kwa wakati huo kulionekana kumtatiza kupita kiasi. Giza lilikuwa likiingia kadri muda ulivyozidi kwenda mbele, hakuelewa ni sehemu gani ambayo alitakiwa kumsindikiza Siwema.

    Kwa kuogopa kumkasirisha, Patrick akainuka. Siwema nae akainuka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika sehemu ambayo kulikuwa na kichaka huku akihakikisha hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akiwaona. Safari ya kuelekea katika sehemu ambayo hakuifahamu kuanza.

    Tayari giza lilikuwa limeanza kuingia, Patrick alionekana kuwa na wasiwasi lakini Siwema hakuonekana kuwa na wasiwasi wowote ule. Wakaingia porini na kuanza kuelekea mbele zaidi, Siwema alionekana kuzifahamu kila kona ambazo alikuwa akizipita katika sehemu hizo japokuwa kulikuwa na giza kubwa.

    Walitembea kwa muda mchache, Siwema akaingia katika kichaka ambacho akamtaka Patrick kumfuata. Siwema akakaa vizuri chini na kisha kukifungua kilemba ambacho alikuwa nacho kichwani. Akaichukua khanga ambayo alikuwa aeivaa na kuitandika chini.

    Patrick alionekana kuchanganyikiwa, tayari alikwishaelewa ni kitu gani ambacho kilitakiwa kutokea mahali hapo lakini kila alipokuwa akimfikiria mzee Abdallah jinsi alivyokuwa na kwa jinsi wanakijiji walivyokuwa, aliona kutokuwa tayari kufanya kile ambacho Siwema alikitaka kifanyike kwa wakati huo.

    “Nakuhitaji Patrick” Tayari sauti ya Siwema ilikuwa imekwishaanza kubadilika, ilisikika kwa chini huku ikiwa imetolewa kwa mtindo ambao Patrick hakuwahi kuusikia kabla.

    Siwema akamsogelea Patrick na kisha kumvutia kwake. Pumzi zilikuwa zikimtoka mfululizo kama mtu ambaye alikuwa amekimbia umbali mrefu. Kwa kasi ya ajabu akaanza kuipandisha sketi yake ambayo alikuwa nayo na kisha kujilaza huku akiendelea kumvutia Patrick pale chini.

    “Siwema. Unafanya nini?” Patrick aliuliza huku akionekana kushangaaa.

    “Ina maana hauelewi kitu Patrick? Naomba unielewe...nakuhitaji..naomba tufanye....nakuomba Patrick...nimezidiwa kwa ajili yako” Siwema alimwambia Patrick.

    Patrick akabaki akitetemeka, hakujua afanye nini kwa wakati huo. Siwema alionekana kuzidiwa kupita kawaida, alionekana kuwa na uhitaji mkubwa wa kupewa kile ambacho alikuwa akikitaka. Patrick alionekana kuogopa, kitabu cha Biblia Takatifu kikaonekana akilini mwake, amri ambazo zilikuwa zimeandikwa katika kitabu hicho zikaanza kumiminika kichwani mwake.

    “USIZINI” Sauti ilisikika kichwani mwa Patrick.

    Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kufanya kwa wakati huo. Bado Siwema alikuwa akiendelea kulalamika kwa sauti iliyojaa mahaba. Patrick hakujua afanye nini, akili yake ikachanganyikiwa kupita kawaida. Moyo wake ulikuwa na msimamo wa kumkatalia Siwema kile ambacho alikuwa akikitaka.

    Patrick akahisi kuona tofauti mwilini mwake, msimamo ambao alikuwa ameuweka ukaonekana kuanza kuyumba hasa mara baada ya mikono ya Siwema kuanza kumpapasa. Mwili wake ukaanza kusisimka, hali ya tofauti ambayo hakuwahi kuihisi toka azaliwe ikaanza kumpata.

    Patrick akaanza kumlalia Siwema ambaye bado alikuwa akiendelea kutoa maneno mbalimbali kwa sauti ambayo ikaonekana kuanza kumchanganya Patrick. Patrick akabaki akimwangalia Siwema ambaye alikuwa akianza kuvua nguo moja hadi nyingine.

    Ingawa katika usiku huo kulikuwa na kibaridi lakini miili yao ilikuwa tofauti kabisa na hali hiyo. Vijasho vilikuwa vikiwatoka huku wakizidi kusisimka kupita kawaida. Patrick hakutaka kubaki kama alivyokuwa, nae akaaanza kuvua nguo zake kwa kasi ambayo hata mwenyewe alionekana kuishangaa.

    Patrick alikuwa juu ya kifua cha Siwema na kufanya kile ambacho kila siku alikuwa akikatazwa kanisani kukifanya. Kwa wakati huo hakukumbuka kitu chochote kile, ngono ndiyo ambayo alikuwa akiifikiria na kuifanya kwa wakati huo.

    Kilio kilikuwa kikisikika kutoka kwa Siwema, maumivu makali yaliyochanganyikana na raha fulani alikuwa akiyasikia. Alipiga kelele za kumtaka Patrick atoke juu yake lakini mikono yake wala haikutaka kumsukuma. Alikuwa akimvutia kwake kila wakati huku akilia kwa maumivu makali. Damu zikaanza kumtoka na kuanza kutapakaa katika mapaja yake.

    “Unaniumiza Patrick.....Unaniumiza...” Siwema alilalamika huku akilia.

    Patrick alitamani kuacha kile ambacho alikuwa akikifanya lakini kwa hali ile ambayo alikuwa akiihisi kwa wakati ule, ilionekana kuwa vigumu kuacha.

    Kitendo kile kilichukua dakika kadhaa, Patrick akaonekana kuchoka kupita kiasi. Siwema alikuwa akiugulia kwa maumivu, damu zilikuwa zimemtoka vya kutosha, bikira hakuwa nayo tena. Siwema alibaki akimwangalia Patrick kwa hasira huku wakati mwingine akionekana kutabasamu.

    “Ndio tumefanya nini Siwema?” Patrick aliuliza huku akionekana kukasirika.

    “Unasemaje?”

    “Ndio tumefanya nini? Angalia Siwema, nimemtenda Mungu wangu dhambi!” Patrick alimwambia Siwema huku akivaa haraka haraka.

    “Nilizidiwa Patrick...naomba unisamehe mpenzi”

    “Nani mpenzi wako. Naomba uniache Siwema....nimemtenda Mungu wangu dhambi” Patrick alisema kwa kulalamika.

    Siwema akaanza kuvaa nguo zake, ghafla wakasikia minong’ono ya watu ambao hawakuwa mbali sana kutoka pale walipokuwa. Mianga ya tochi ikawamulika usoni hali ambayo ilimpekea Patrick kumuinua Siwema na kuanza kukimbia nae kuelekea mbele zaidi.

    Watu wale waliokuwa na tochi wakatoka kutoka vichakani na kuanza kuwakimbiza. Patrick alimshika vilivyo Siwema na kuongeza kasi kukimbia. Tayari waliona hatari ikiwa karibu nao, hawakutaka kusimama, bado waliendelea kukimbia mbele huku wakiomba Mungu awanusuru na hatari ambayo ilikuwa karibu yao.









    *******************************





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Bi Anna akazidi kuisogelea nyumba ile, tayari matumaini yakaanza kuonekana mbele yake. Akazidi kupiga hatua kuifuata nyumba ile. Mlango ulikuwa umefungwa, Bi Anna akaanza kuugonga huku akionekana kuwa na wasiwasi. Wala hazikupita sekunde nyingi, mlango ukafunguliwa na kijana mmoja.

    Bi Anna akakaribishwa, akaingia ndani huku bado akionekana kuwa na wasiwasi. Akakaa kwenye kiti. Mwili ulikuwa ukimtetemeka kwa hofu, machozi yalikuwa yakimtoka huku akilia. Picha ya mumewe alivyokuwa akishambuliwa na vijana wa kijiji cha Chibe ilikuwa ikionekana kichwani mwake.

    Moyo wake ulikuwa ukimuuma, alijiona kuwa katika wakati mgumu kuliko katika nyakati zote ambazo alikuwa amepitia katika maisha yake. Kijana yule akabaki akimwangalia Bi Anna huku koroboi ikiwasaidia kuonana mahali hapo.

    “Karibu. Mbona unalia?” Kjana yule alimuuliza Bi Anna ambaye akaanza kuyafuta machozi yake.

    Hata kabla hajajibu chochote kile, mlango mmoja wa chumba kimoja ukafunguliwa na mzee moja kutokea mahali hapo. Anna akamwangalia mzee yule, hakuwa akimfahamu na wala hakuwahi kumuona hata siku moja. Bi Anna akaaanza kulia tena, machozi yakaanza tena kutiririka mashavuni mwake.

    “Kuna nini tena? Mbona huyu mwanamke yupo hapa ndani akilia?” Mzee Jumanne alimuuliza kijana wake.

    “Nimemkaribisha akiwa katika hali hii. Nimejaribu kumuuliza lakini bado analia, nafikiri tumpe dakika kadhaa” Kijana yule alimwambia mzee Jumanne.

    Anna aliendelea kulia zaidi na zaidi huku mzee Jumanne akimbembeleza kwa kumtaka kumwambia ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha yake. Zilimchukua dakika tano, akanyamaza na kuanza kuelezeka kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea.

    Mzee Jumanne na kijana wake wakaonekana kuhuzunika kupita kawaida. Mambo ambayo aliwaelezea Anna yalionekana kuwasikitisha na kuwatisha, hawakuamini kama katika vijiji vya Shinyanga bado kulikuwa na watu ambao walikuwa na roho ya ukatili kama waliokuwa nayo vijana ambao walikuwa wamemshambulia mzee Innocent.

    “Inasikitisha sana” Mzee Jumanne alimwambia Anna.

    “Naomba mnisaidie...naomba mnisaidie” Anna aliwaambia.

    “Kama tukisema ukae hapa, bado unaweza kuonekana. Si unajua kutoka hapa mpaka kijijini Chibe sio mbali sana. Wanaweza wakaja na kukukamata” Mzee Jumanne alimwambia Bi Anna.

    “Kwani hapa ni wapi?”

    “Hiki ni kijiji cha Usule” Mzee Jumanne alimwambia Bi Anna na kuendelea.

    “Tutakusaidia kwa kukupeleka kwa mdogo wangu katika kijiji cha Itilima, utaishi huko na kuangalia maisha yako ya mbele” Mzee Jumanne alimwambia Bi Anna.

    “Nashukuru sana....asanteni kwa msaada wenu” B Anna aliwashukuru.

    “Kwa hiyo vipi kuhusu kijana wako? Nae walimuua pia?” Mzee Jumanne alimuuliza.

    “Najua watakuwa wamemuua. Alikuwa amechelewa sana kurudi nyumbani, kwa vyovyote vile watakuwa wamemuua. Inaniuma sana kubaki peke yangu katika familia yangu. Nimekuwa mpweke, sijui kama nitapata furaha katika maisha yangu yaliyobakia” Bi Anna aliwaambia.

    Bi Anna akalala ndani ya nyumba ile katika usiku huo. Usingizi kwake haukuwa wa amani, ulikuwa wa mang’amung’mu. Kila wakati alikuwa akishtuka, bado wasiwasi wa vijana wale kumfuata hadi kule ulikuwa umemtawala moyoni.

    Asubuhi ilipofika, Omari akamchukua katika baiskeli yake na kuanza kumpeleka katika kijiji cha Itilima. Njia hazikuwa nzuri sana, wakati mwingine alikuwa akishuka kutoka katika baiskeli na kisha Omari kuibeba. Walipita katika milima na mabonde, kijiji cha Itilima kilionekana kuwa mbali tofauti na jinsi alivyofikiria kabla.

    Walichukua masaa manne, wakaingia katika kijiji cha Itilima na moja kwa moja kuelekea katika nyumba ya mzee Ubuge. Omari akamuelezea mzee Ubuge kila kitu kuhusu Bi Anna. Mzee Ubuge akaonekana kusikitika kupita kiasi, habari ile aliyopewa ilionekana kumuogopesha sana.

    Hakuwa na jinsi, akamkaribisha Bi Anna ndani ya nyumba yake hiyo ambayo alikuwa akiishi pamoja na mkewe. Bi Anna akapewa chumba kimoja na maisha yake kuanza mahali hapo. Kila wakati alikuwa akimshukuru Mungu kwa kumuwezesha kufika mahali hapo ambapo alipaona kuwa na usalama.







    *****************************





    Hakukuwa mwanakijiji katika kijiji cha Wami ambaye hakuwa akimfahamu mzee Jafari Abdallah. Mzee huyu alifahamika vizuri sana kutokana na kuwa mtu wa dini kupita kiasi. Dini ndio ilikuwa muongozo wa maisha yake ya kila siku. Kila mwanakijiji alikuwa akimpenda mzee Abdallah kiasi ambacho kiliwapelekea kumchagua kama mwenyekiti wa kijiji chao.

    Mzee Abdalaha akatengeneza jengo dogo ambalo lilikuwa likitumika kama chuo cha Madrasa kijijini hapo. Watoto zaidi ya arobaini ilikuwa ni lazima waende chuoni hapo kujifunza mambo mbalimbali ya dini ya Kiislamu kila asubuhi na jioni. Mzee Abdallah akajitengenezea jina kubwa sana mpaka katika vijiji vingine vya jirani.

    Mzee Abdallah alikuwa Muislamu wa swala tano, kila siku alikuwa akishinda akiswali pasipo kumwangalia mtu yeyote yule. Msikiti wala haukuwepo kijijini hapo kitu ambacho kilimfanya mzee huyo kutenga sehemu maalumu ndani ya eneo la nyumba yake kwa ajili ya wanakiji kuswalia.

    Aliipenda dini kuliko kitu chochote katika maisha yake. Muda mwingi alikuwa akishika kitabu cha Koran akisoma. Kanzu ndilo likawa vazi lake kuu katika maisha yake. Alikuwa na kanzu tofauti tofauti zaidi ya kumi huku suruali akiwa nazo mbili tu na mashati matatu.

    Kila alipokuwa, alikuwa akivaa kanzu au wakati mwingine kuvaa misuli iliyokuwa na rangi tofauti tofauti. Tangu ajiingize rasmi katika mabo ya dini miaka ishirini na tano iliyopita, hakuwahi kuvaa fulana hata siku moja, na hata mashati ambayo alikuwa akiyavaa, alikuwa akiyavaa mwezi mpaka mwezi.

    Mzee Abdallah alikuwa na watoto wanne ambao alizaa na mwanamke ambaye alikuwa akimpeda sana, Bi Nuru. Mwanamke huyu alionekana kuwa sehemu kubwa sana katika maisha yake, alimthamini kuliko mwanamke yeyote yule katika maisha yake.

    Katika miaka ishirini na mbili ya ndoa yao wakafanikiwa kupata watoto watatu, wa kwanza alikuwa Hamisi, wa pili alikuwa Ramadhani na wa mwisho alikuwa msichana, huyu alikuwa Siwema.

    Mzee Abdallah aliwalea watoto wake katika mazingira ya kidini. Hakutaka waharibikiwe katika maisha yao. Kila siku alikuwa akiwahimiza kuelekea chuoni na kupata elimu ya kidini. Watoto wake hao ndio walionekana kuwa kila kitu katika maisha yake.

    Mzee Abdallah hakutaka binti yake aharibikiwe kama mabinti wengine wa kijiji hicho ambao wengi wao walijiingiza katika matendo ya ngono kabla ya kuolewa. Alisaidiana na Bi Nuru kumlea Siwema katika mazingira ya kidini. Kila siku Siwema alikuwa akivaa ushungi au kitambaa kichwani mwake kama ambavyo alitakiwa kuvaa mwanamke wa Kiislamu.

    Nywele za Siwema hazikuwahi kuonekana na wavulana wa kijiji hicho hata siku moja, kila siku alikuwa msichana wa vilemba au hijabu. Wavulana walikuwa wakimuogopa Siwema, kamwe hawakudiriki kumfuata hata siku moja. Kwa wale wavulana ambao walionekana kuwa wabishi, walimfuata Siwema ambaye mara kwa mara alikuwa akiwaambia kaka zake.

    Siwema akaonekana kuogopwa kuliko msichana yeyote kijijini. Wavulana hawakuwa wakimsogelea kabisa. Mzee Abdallah alionekana kuwa mtata kwa kila mvulana ambaye alipata taarifa alikuwa akmfuatilia binti yake. Mzee Abdallah hakuonekana kumuogopa mtu yeyote kijijini hapo ambaye alikuwa akimfuatilia binti yake.

    Wavulana mbalimbali walikuwa wakijitokeza kwa ajili ya kutoa posa kwa ajili ya Siwema lakini mzee Abdallah alikuwa akiwakatalia. Hakutaka binti yake aolewe katika umri mdogo, aliogopa kumpa majukumu mazito ya ndoa. Kila siku alikuwa akikaa na watoto wake na kuwapa zaidi elimu ya kidini na jinsi ambavyo walitakiwa kuishi.

    Khanga, hijabu na vitenge ndio yalikuwa mavazi pekee ambayo Siwema alikuwa akinunuliwa na wazazi wake, kamwe hawakutaka kumnunulia sketi na kama walikuwa wakinunulia mavazi ya kawaida, walimnunulia magauni marefu ambayo kila alipokuwa akiyavaa, yalikuwa yakifunika hadi unyayo wake.

    “Kuna kitu gani kinaendelea kati yako na Patrick?” Mzee Abdallah alimuuliza Siwema huku akionekana kukasirika.

    “Hakuna kitu baba. Yeye ni rafiki yangu ambaye mara kwa mara ananifundisha hesabu” Siwema alijitetea.

    “Kuwa makini nae, kamwe usitake kufanya kila kitu anachokwambia. Umenisikia?”

    “Ndio baba”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ukaribu kati ya Siwema na Patrick ukaonekana kuwatia wasiwasi Hamisi na Ramadhani. Kila siku walikuwa wakifuatilia kimya kimya, walitaka kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea. Wao ndio ambao walimwambia baba yao juu ya ukaribu mkubwa aliokuwa nao mdogo wao, Siwema na Patrick.

    Kila siku walikwa watu wa kuwafuatlia kila hatua ambayo walikuwa wakipitia. Wakaanza kushikwa na wasiwasi katika kipindi ambacho Siwema alikuwa akiongozana na Patrick kuelekea vichakani. Kwa haraka haraka Hamisi akaelekea ndani na kuchukua tochi mbili na kisha kuanza kuwafuatilia.

    Si Patrick wala Siwema ambaye alijua kama walikuwa wakifuatiliwa. Walitembea kwa kujiamini huku wakizidi kusogea mbele. Hamisi na Ramadhani walikuwa wakizidi kuwasogelea. Kutokana na giza ambalo lilikuwa limetanda, Patrick na Siwema wakaonekana kupotea machoni mwao.

    Wakaanza kuwatafuta katika vichaka mbalimbali porini pale lakini wala hawakuwaona kabisa. Dakika ishirini zilipita, wakaisikia sauti ya Patrick kutoka katika kichaka ambacho hakikuwa mbali kutoka katika sehemu ambayo walikuwa wamesimama wakionekana kukata tamaa.

    Wakaanza kusogea zaidi kule walipokuwa Patrick na Siwema, wakabaki kimya wakiwasikiliza kila kitu ambacho kilikuwa kinaongelewa.

    “Mungu wangu! Wamekwishafanya....! Yaani Siwema amefanya...amefanya porini! Haiwezekani” Hamisi alijikuta akisema kwa uchungu.

    “Kwa hiyo tufanye nini sasa?” Ramadhani aiuliza

    “Tuwakamate na kuwapeleka kijijini. Washenzi sana” Hamisi alisema na kuanza kuwamulika tochi usoni.

    Hata kabla hawajafanya kitu chochote kile, wakashtuka mara baada ya kuwaona Patrick na Siwema wakianza kukimbia. Kwa haraka haraka nao wakatoka pale kichakani walipokuwa wamejificha na kuanza kuwakimbiza huku wakiwamulika kwa tochi.

    Patrick na Siwema walikuwa wakikimbia kwa kasi kuliko hata wao wenyewe kiasi ambacho waliwapotea machoni mwao. Wakaanza kuwatafuta tena, waliwatafuta kwa dakika kadhaa, wakamuona mdogo wao, Siwema akiwa amesimama sehemu ya wazi huku akitetemeka kwa hofu.

    “Firauni mwenzako yuko wapi?” Hamisi alimuuliza Siwema huku akionekana kukasirika.

    “Amekimbia...amekimbia” Siwema alijibu huku akitetemeka kwa hofu na machozi yakimtoka

    “Amekimbia? Tuambie Firauni mwenzako yuko wapi?” Hamisi aliendelea kuuliza kwa hasira huku akimmulika kwa tochi usoni.

    Siwema hakujibu kitu chochote kile, alibaki akitetemeka kwa hofu huku jasho likimtoka. Walichokifanya ni kumshika mkono na kuanza kuelekea nae kijijini huku kila mmoja akionekana kukasirika.

    “Atakuwa amekimbilia kijijini. Ni lazima tumuwahi na kumkamata huko huko. Kwa wewe mshenzi tuliyekukamata, breki ya kwanza kwa baba” Ramadhani alimwambia Siwema ambaye bado alikuwa akilia huku akitetemeka kwa hofu.

    *****

    Patrick na Siwema walikuwa wakikimbia kwa kasi. Kila mmoja aliiona hatari ambayo ilikuwa ikiwakaribia. Tochi bado zilikuwa zikiwamulika hali ambayo iliwafanya kuongeza kasi. Walikimbia kwa mwendo mrefu, hawakujua ni watu gani ambao walikuwa wakiwakimbiza muda huo.

    Baada ya kukimbia kwa mwendo mrefu, wakaingia kichakani na kjificha. Hamisi na Ramadhani wakapita kwa kasi huku wakimulika tochi zao huku na kule. Patrick na Siwema hawakuonekana mahali pale ambako walikuwa wamejificha.

    “Hawa watakuwa watu wa kijijini kwenu Siwema” Patrick alimwambia Siwema na kuendelea.

    “Siwezi kurudi kijijini kwenu tena, ni lazima niondoke. Huu si mwisho wa safari yangu, nitaendelea mbele. Najua hapa sio mwisho” Patrick alimwambia Siwema ambaye muda wote alikuwa akilia.

    “Usiondoke Patrick...usiniache peke yangu” Siwema alimwambia Patrick.

    “Haina jinsi Siwema, ni lazima niondoke na kuendelea na safari yangu” Patrick alimwambia Siwema.

    “Ina maana hautorudi tena? Ina maana huu ndio mwisho wa mimi na wewe kuonana?” Siwema aliuliza.

    “Huu si mwisho. Tutaendelea kuonana Siwema. Nitarudi kijijini kwenu. Nitarudi kwa ajili ya kukuoa tu. Kama kuna mtu atakuja na kutaka kukuoa....kataa, nitarudi kwa ajili yako” Patrick alimwambia Siwema huku akimwangalia usoni.

    “Nimekuelewa. Kamwe sitoolewa na mwanaume mwingine zaidi yako. Nitakusubiri mpaka utakaporudi” Siwema alimwambia Patrick.

    “Ni lazima nitarudi Siwema. Maisha yangu si kitu bila wewe. Yaani SI KITU BILA WEWE. Ni lazima nitakurudia” Patrick alimwambia Siwema na kisha kumbusu mdomoni na kisha kuondoka akimuacha Siwema akilia na kusimama njiani akiwasubiria watu ambao walikuwa wakiwakimbiza.

    *****

    Maisha mapya yakawa yamekwishaanza katika kijiji cha Itilima. Kila siku Bi Anna alionekana kuwa na majonzi, furaha kwake haikuwa sehemu ya maisha yake kabisa. Kichwani mwake, taswira ya marehemu mumewe bado ilikuwa ikimsumbua, kila siku ndoto juu ya mumewe zilikuwa zikimjia.

    Hakujua katika kipindi hicho mtoto wake Patrick alikuwa hai au vipi ingawa moyoni mwake alikuwa na uhakika asilimia mia moja kuwa Patrick alikuwa ameuawa. Kila siku alikuwa akimuomba Mungu juu ya familia yake, kama Patrick alikuwa ameuawa basi Mungu Amlinde Pahala Pema Peponi lakini kama alikuwa hai basi aendelee kumlinda kila siku.

    Miezi miwili ilkapita, Bi Anna alikuwa akifanya kazi kwa juhudi zote katika shamba la mzee Ubuge kiasi ambacho kila mtu alikuwa akishangazwa. Wanawake wengi wa kijiji cha Itilima walikuwa wakielekea shambani kulima huku wanaume wakibaki nyumbani wakipiga soga.

    Bi Anna akaonekana kukasirika hali iliyomfanya kuanzisha kikundi kidogo cha wanawake kumi ambacho kilikuwa kikihusika na haki za wakinamama kijijini hapo. Kila siku alikuwa akiwaita wanawake hao na kuongea nae. Sifa za kikundi kile zikaanza kusambazwa sehemu mbalimbali. Kila mwanamke akawa na hamu ya kutaka kujiunga na kikundi hicho.

    Mpaka mwezi mmoja unakatika baada ya kuanzisha kikundi kile, wanawake zaidi ya hamsini walikuwa wamejiunga. Kila siku walikuwa wakikutana na kuongelea mambo mbalimbali kuhusu maendeleao kijijini hapo. Hawakutaka kabisa kufanyishwa kazi kama punda huku waume zao wakiwa nyumbani wakipiga soga.

    Kila siku kelele zao zilikuwa ni kuwataka waume zao wawasaidie kazi mbalimbali kama kulima na kazi nyingine badala ya kubaki nyumbani na kupiga soga. Jumbe mbalimbali kutoka katika kikundi kile zilikuwa zikipuuzwa na wanaume wote lakini kadri siku zilivyozidi kuongezeka na wanachama kuongezeka, wanaume wakaanza kubadilika.

    Wanachama walizidi kuongezeka zaidi na zaidi huku Bi Anna akiwa mhamasishaji na kupewa uongozi wa kuwa mwenyekiti. Wanawake wengi kutoka katika vijiji mbalimbali wakaanza kujiunga na kikundi hicho ambacho kiliitwa WAMASHI ambayo ilikuwa na maana iliyojulikana WANAWAKE WA MAENDELEO SHINYANGA.

    Kundi lile la wanawake likazidi kuongezeka zaidi na zaidi hadi kufikia idadi ya wanawake mia tano kumi na sita. Mara kwa mara mikutano ilikuwa ikiendelea huku michango mbalimbali ya kuiwezesha kikundi kile ikiendelea kuchangwa. Kila mwanamke alionekana kuhitaji mabadiliko katika jamii, hawakutaka kufanyishwa kazi kama watumwa.

    “Tunahitaji mabadiliko katika jamii zetu....tunahitaji kusaidiwa katika kila kazi ambayo tunaifanya na si kila kazi kufanya sisi huku ninyi wanaume mkipiga soga tu” Bi Anna alisema katika mkutano wa wazi ambao ulifanyika katika kijiji cha Itilima.

    Wanaume walibaki wakiangaliana kwa aibu. Maneno mbalimbali ambayo alikuwa akiyaongea Bi Anna yalionekana kumgusa kila mtu. Kila wakati vigelegele vilikuwa vikisikika kutoka kwa wanawake ambao walikuwa wamekusanyika mahali hapo.

    “Mabadilikoooooo...........” Bi Anna alisema kwa sauti kubwa iliyosikika vizuri katika uwanja ule.

    “Yanawezekanaaaaaaa.....” Wanawake wote waliitikia kwa sauti kubwa.

    *****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Mzee Abdallah alionekana kukasirika kupita kawaida. Alikaa kitini nje huku akiipigapiga chini fimbo ambayo alikuwa ameishika. Moyo wake ulikuwa na hasira kubwa, kitendo alichokifanya Siwema cha kuondoka na Patrick kuelekea porini kilionekana kumkasirisha kupita kiasi.

    Kila wakati alikuwa akiiangalia saa yake ambayo ilionyesha kuwa tayari ilikuwa saa mbili na dakika tano usiku. Muda wote alikuwa akiangalia kule kichakani ambako Siwema na Patrick walikuwa wameelekea, alionekana kukasirika kupita kawaida.

    Patrick alionekana kuuharibu moyo wake vilivyo, akatokea kumchukia kuliko kijana yeyote kijijini hapo. Alitamani kijana yule aletwe mbele yake na kumfanya kile ambacho alikipanga kumfanyia. Mzee Abdallah alijiona kuchafuliwa, kwake, Patrick hakuonekana kustahili msamaha wowote ule.

    Kila wakati alikuwa akiombea Patrick na Siwema waletwe mahali hapo haraka iwezekanavyo, dakika ziliendelea kwenda mbele lakini wala hakukuwa na mtu yeyote aliyefika mahali hapo. Muda ulizidi kusogea, dakika zilizidi kusonga mbele huku nazo sekunde zikizidi kukatika lakini wala hakukuwa na badiliko lolote.

    Ilipotimia saa tatu kasoro, Hamis, Ramadhani pamoja na Siwema wakaanza kuingia kijijini hapo. Mzee Abdallah akasimama na kuanza kuwasogelea huku akionekana kukasirika kupita kawaida. Muda wote Siwema alikuwa akilia. Mzee Abdallah akamshika Siwema mkono na kumsogezea kwake.

    “Mwenzake yuko wapi?” Mzee Abdallah aliwauliza huku akionekana kuwa na hasira.

    “Alikimbia. Hatujui alikimbilia wapi”

    “Niambie.....mmefanya?” Mzee Abdallah aliuliza huku akionekana kukasirika. Siwema hakujibu kitu chochote kile, alibaki akilia tu.

    “Niambie...mmefanya kitu chochote?” Mzee Abdallah alirudia swali lake kwa hasira zaidi.

    “Ndi....” Siwema alijibu akini hata kabla hajamalizia sentensi yake, akashtuka kibao kizito kikishushwa shavuni mwake.

    Siwema akaanguka kama mzigo, kilio kiliendelea kusikika kwa sauti kubwa ambayo iliwakusanya watu kutoka sehemu nyingine na kuzunguka katika eneo la nyumba ile.

    Bado mzee Abdallah alikuwa akionekana kuwa na hasira kupita kawaida, alibaki akimwangalia Siwema huku akiuma meno yake kwa hasira. Akamfuata pale chini alipokuwa amekaa na kumnyanyua. Akampiga kibao kingine cha nguvu, Siwema akaanza kuyumba, tayari akaona kulikuwa na hatari mahali hapo.

    “Mwachie mwanangu” Bi Nuru alimwambia mumewe ambaye alionekana kubadilika na kuwa na hasira kali kupita kawaida.

    Kitendo cha mzee Abdallah kumwachia Siwema kilionekana kuwa kama kosa, hapo hapo Siwema akaanza kukimbia kuelekea porini huku akilia.

    Kila mtu akabaki akimsangaa mzee Abdallah, hawakuonekana kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo. Kila mtu akaonekana kumuonea huruma Siwema ambaye alikuwa amepotea katika pori lililokuwa limezunguka kijiji hicho

    Bi Nuru akaonekana kuwa na wasiwasi, moyoni mwake alimpenda sana binti yake, Siwema ambaye alikuwa mtoto wa mwisho na mtoto pekee wa kike. Kuondoka kwake kulionekana kumkasirisha, akaonekana dhahiri kutofurahishwa na hali ambayo alikuwa nayo mumewe katika kipindi hicho.

    “Mwacheni aende...atarudi tu. Mtoto mpumbavu sana yule” Mzee Abdallah aliwaambia.

    Sekunde ziliendelea kukatika kama kawaida huku dakika zikiendelea kusonga mbele. Masaa yakaendelea kusogea zaidi na zaidi lakini wala Siwema hakurudi mahali hapo. Kila mtu nyumbani hapo akaanza kuingiwa na wasiwasi kwamba Siwema alikuwa ameondoka moja kwa moja.

    Waliendelea kuvuta subira kwa kudhani kwamba Siwema angerudi nyumbani hapo. Muda uliendelea kusogea zaidi lakini bado hali ilikuwa ile ile, Siwema hakurudi nyumbani. Bi Nuru hakuonekana kutulia, kila wakati alikuwa akiangalia porini kuona kama Siwema angeweza kurudi mahali hapo, lakini bado Siwema hakurudi.

    “Mungu wangu! Saa nane” Bi Nuru alisema katika kipindi ambacho bado alikuwa akimsubiria Siwema.

    Hakukuwa na dalili zozote za Siwema kurudi nyumbani, masaa yalizidi kwenda mbele lakini wala hakukuwa na mabadiliko yoyote yale. Bi Nuru hakupata usingizi kabisa, muda wote macho yake yalikuwa wazi yakimsubiri Siwema ambaye mpaka inafika saa kumi na mbili asubuhi, hakuwa amerudi.





    *******************************





    Shughuli za uchimbaji wa almasi bado ulikuwa ukiendelea katika mgodi wa Mwadui. Vijana ambao walikuwa wakifanya kazi ya uchimbaji madini katika mgodi huo walikuwa wakifanya kazi kwa juhudi zote kwani waliamini kama wangetoka mahali hapo, basi mafanikio yalikuwa pamoja nao.

    Kila siku vijana wengi walikuwa wakiongezeka mgodini hapo na kuajiriwa na makampuni mbalimbali ambayo yalikuwa yakizidi kuongezeka mahali hapo. Kila mtu alikuwa akihitaji kupata fedha na ndio kitu ambacho kilionekana kuwafanya kufanya kazi kwa nguvu zote.

    Mji wa Mwadui ukaonekana kuanza kubadilika, huduma zote za kijamii kama maji na umeme vikaletwa mahali hapo. Shule zikajengwa kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi ambao walikuwa wakifanya kazi mchana na usiku. Madini mengi yalikuwa yakipatikana kila siku na kusafirishwa kupelekwa nje ya nchi.

    Makampuni mbalimbali ya uchimbaji madini bado yalikuwa yakizidi kungezeka mgodini hapo hali iliyoonkana kuwavutia zaidi vijana kumiminika mgodini hapo. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuwajali watoto, watoto mbalimbali walikuwa wakiajiriwa mgodini hapo kwa ajili ya kuchekecha mchanga wa almasi ambazo zilikuwa zikichimbwa kila siku.

    Malipo yalikuwa yakifanywa vizuri kiasi ambacho kila mtu alionekana kuridhika. Huduma mbalimbali za kijamii zilizidi kuongezeka katika mji wa Mwadui kiasi ambacho kiliwafanya hadi watu kutoka mikoa mingine ya jirani kutamani kwenda kuishi katika mji huo ambao ulikuwa ukizidi kuendelea kila siku.

    Patrick alikuwa mmoja wa watoto ambao walikuwa wameajiriwa katika kampuni ya uchimbaji madini iliyokuwa mahali hapo ambayo iliitwa MWAGOCO DIAMOND COMPANY LIMITED. Kila siku kazi yake pamoja na watoto wengine ilikuwa ni kuchekecha mchanga ambao ulikuwa umechimbwa katika mashimo mbalimbali.

    Kila siku mashimo ya kampuni ya MWAGOKO yalikuwa yakitoa almasi nyingi kuliko mashimo yote ambayo yalikuwa katika mgodi huo wa Mwadui. Hakukuwa na mtu ambaye alikuwa akifahamu kitu chochote kuhusu siri iliyokuwa imeufunika mgodi huo.

    Kila siku magari mbalimbali makubwa yalikuwa yakifika katika mgodi huo hasa karibu na mashimo ya kampuni ya MWAGOKO na kuchukua mchanga ambao tayari ulikuwa umechekechwa. Kampuni ya MWAGOKO ikawa kampuni pekee iliyokuwa na wafanyakazi wengi ambao walikuwa wakilipwa vizuri kuliko kampuni zote mgodini hapo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa miezi miwili ambayo Patrick alikuwa ameishi mgodini hapo, hakuzoeana na mtu yeyote zaidi ya Aziz, mtoto ambaye alikuwa akifanya kazi pamoja nae. Kila wakati walikuwa pamoja, chakula walikula pamoja na hata sehemu walilala katika hema moja.

    Walizoeana kupita kawaida kiasi ambacho kila mtu alijua watoto hao walikuwa ndugu. Kitu ambacho kilionekana kuwa tofauti kwao ni rangi tu. Aziz alikuwa mchanganyiko wa rangi mbili, kiarabu na mmatumbi huku Patrick akiwa mmatumbi kamili.

    Kila siku walikuwa wakifanya kazi pamoja katika kampuni ya MWAGOKO iliyokuwa chini ya Bwana Mayasa Godfrey, tajiri ambaye alikuwa akimiliki mali zilizokuwa na kiasi cha shilingi Trilioni sabini.

    Hakukuwa na mtu ambaye hakuwa akimfahamu Bwana Mayasa nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla. Kila siku utajiri wake ulikuwa ukiongezeka, alinunua magari ya kifahari pamoja na nyumba kubwa za kifahari. Fedha kwake haikuwa tatizo kabisa, alitumia fedha kwa kadri alivyoweza lakini wala hazikupungua zaidi ya kuongezeka kila siku.

    Siri kubwa ilikuwa nyuma ya kampuni ya MWAGOKO, siri ambayo hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliifahamu. Kila kitu kilikuwa kikifanyika kwa usiri mkubwa ambapo hakukuwa na mtu yeyote ambaye alifahamu kitu chochoe kile.

    Damu za watoto ndizo ambazo zilikuwa zikitumika katika katika mashimo yaliyokuwa yakimilikiwa na kampuni ya MWAGOKO. Kila wiki watoto walikuwa wakichukuliwa kutoka mitaani na kupelekwa katika migodi hiyo ambako walichinjwa na damu zao kunyunyiziwa katika sehemu mbalimbali.

    Majini ndio ambayo yalikuwa yakinywa damu hizo ambazo zilikuwa zikinyunyiziwa na kisha kuruhusu almasi nyingi kupatikana katika mashimo hayo. Ukatili ambao ulikuwa ukifanyika mara kwa mara haukuwa ukijulikana na mtu yeyote zaidi ya Bwana Mayasa na wafanyakazi wake wa karibu ambao alikuwa akiwaamini kupita kiasi.

    Watoto walikuwa wakipotea mitaani, wazazi walikuwa wakiwatafuta katika kila kona lakini hakukuwa na mafanikio yoyote yale. Walikuwa wakiingizwa katika buti za magari na kisha kusafirishwa kupelekwa katika migodi hiyo pamoja na baharini.

    Kila mwaka zaidi ya watoto elfu kumi walikuwa wakipotea mitaani na kupelekwa katika migodi mbalimbali pamoja na baharini kwa ajili ya kutolewa kafara. Kila siku Serikali ilikuwa ikijitahidi kwa nguvu zote kutaka kujua sehemu ambayo watoto hao walipokuwa wakipelekwa lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alipata jibu, kila kitu kilionekana kuwa siri kubwa.

    “Unasemaje?” Bwana Mayasa aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Ndio hivyo mzee. Yaani tumejitahidi sana, hatujafanikiwa” Sauti ya upande wa pili ilisikika.

    “Haiwezekani. Yaani watoto wote huko!”

    “Ndio hivyo mzee. Kila mzazi amekuwa makini na mtoto wake, au kama utatupa wiki moja tujitahidi” Sauti ile iliendelea kusikika.

    “Wiki moja! Acha utani. Tunataka tuanze kazi leo usiku wewe unaniambia baada ya wiki moja! Naona umechoka kazi Stefano” Bwana Mayasa aliongea huku akionekana dhahiri kuchaganyikiwa.

    “Lakini bosi h...” Sauti ya Stefano ilisikika lakini hata kabla hajamaliza sentensi yake, Bwana Mayasa akakata simu kwa hasira.

    Bwana Mayasa akaonekana kuchanganyikiwa. Amani ikatoweka moyoni mwake, tayari aliwaona vijana wake kutofanya kazi ambayo alikuwa akihitaji ifanyikie haraka iwezekanavyo. Watoto walihitajika haraka sana kwa ajili ya kuwachinja na damu zao kutumika kama sadaka katika mashimo yake, kukosekana kwa watoto hao kulimaanisha kwamba sadaka isingetolewa na hivyo basi majini kukasirika na kuyaficha madini

    Kikao cha dharura kikaitishwa ndani ya chumba kimoja kidogo, muda wote Bwana Mayasa alionekana kuwa na hasira. Tayari aliyaona mambo kuanza kwenda kombo, kila wakati alikuwa akipiga meza kwa hasira. Wafanyakazi wake wa siri ambao walikuwa mahali hapo wakaonekana kuogopa, hawakuwahi kumuona mzee huyo akiwa katika hali hiyo hata siku moja.

    “Usikasirike mzee. Ni lazima tufaye kitu fulani” Godwin, mfanyakazi ambaye alikuwa akiaminika sana na Bwana Mayasa alimwambia huku watu wote wakiwa kimya kumsikiliza.

    “Kitu gani? Unafikiri kitu gani ambacho tunatakiwa kufanya?”

    “Kwani si hata hapa Mwadui kuna watoto. Kwa nini tusiwachukue hata hao. Tena wapo watoto wengi kweli” Godwin alimwambia Bwana Mayasa.

    Bwana Mayasa akaonekana kushtuliwa katika lindi fulani la mawazo, akamwangalia Godwin, tabasamu pana likaanza kuonekana usoni mwake. Wazo hilo likapitishwa kwa nguvu zote, vijana watatu ambao walitakiwa kufanikisha kwa kazi hiyo wakaandaliwa kwa ajili ya kazi kufanyika usiku wa siku hiyo.







    *****







    Patrick na Aziz walikuwa wamelala katika hema ambalo mara kwa mara walikuwa wakilitumia kama chumba chao. Usiku ulikuwa umekwenda sana, wadudu wadogo wadogo walikuwa wakisikika wakilia kutoka maeneo tofauti tofauti katika sehemu hiyo.

    Walinzi walikuwa wakiendelea kuhakikisha usalama mahali hapo huku wakiwa na bunduki zao ili hata kama kungekuwa na mtu yeyote ambaye angekuja kufanya uhalifu na bunduki, basi waweze kupambana nae. Hali ya usalama mkubwa ndio ambayo ilikuwa imetawala mgodini hapo ambao idadi kubwa ya watu waliokuwepo mahali hapo walikuwa vijana wa rika mbalimbali.

    Vijana watatu ambao walikuwa wamevalia makoti makubwa myeusi wakaonekana wakianza kulifuata hema ambalo Patrick na Azizi walikuwa wanatumia kama chumba chao. Mara baada ya kulifikia, wakaingia ndani na kisha kuanza kuwafuata.

    Kwa harka sana wakawafumba midomo yao kwa kutumia mikono yao waliyoivarisha grovu. Patrick akataka kupiga kelele, akabaki akinguruma tu, akataka kumwamsha Aziz kwa kumtikisa lakini nae Azizi alikuwa amefumbwa mdomo kama alivyofumbwa yeye.

    Kwa haraka haraka wakatolewa kutoka katika hema lile na moja kwa moja kuanza kupelekwa katika shimo moja kubwa liliokuwa likitumika katika uchimbaji madini. Walinzi hawakusema kitu chochte kile hali iliyoonyesha kwamba hata wao walikuwa wameshirikisha katika tukio lile.

    Watu zaidi ya saba walikuwa wamekusanyika katika shimo lile huku pembeni yao kukiwa na mzee mmoja mchafu ambaye alikuwa ameshika kisu kilichoonekana kuwa kikali. Hakukuwa na swali lolote juu ya mzee yule, kwa kumuangalia mara moja tu na kwa jinsi alivyovaa, alionekana dhahiri kuwa mganga wa kienyeji.

    Patrick na Aziz wakawekwa chini na kufungwa kamba vilivyo. Walijaribu kupiga kelele lakini wala sauti zao hazikuweza kutoka. Watu wote waliokuwa mahali pale wakaanza kumwangalia mganga katika mtazamo uilomaanisha kwamba alikuwa akisubiriwa yeye tu.

    Bwana Mayasa akatoa tabasamu pana ambalo lilionekana kuwa na matumaini makubwa. Kila kitu kwake kikanekana kukamilika, alitarajia kuona madini yakichibwa kwa wingi mara tu kazi ya kuwatoa sadaka Patrick na Azizi kukamilika.

    Mganga akaanza kumwangalia Patrick na Azizi kwa makini kana kwamba alikuwa akiwachunguza. Alipoonekana kuridhika, akachukua kisu kile na kukinyoosha juu. Akaanza kuongea maneno ambayo wala hayakuwa yakieleweka na watu ambao walikuwa wamesimama shimoni pale.

    Muda wote Patrick na Aziz walikuwa wakilia, tayari walikiona kifo kikiwa mbele yao. Patrick akashindwa kujizuia, akaanza kulia, hakuamini kama zilikuwa zimebakia sekunde chache za kuvuta pumzi ya dunia hii na kumfuata baba yake kule alipokuwa.

    Mganga hakuchukua muda mrefu kuwakabidhi Patrick na Azizi kwa miungu yake. Akaagiza chungu ambacho mara kwa mara kilikuwa kikiwekewa dau kisogezwe mbele yake, kwa haraka haraka kikasogezwa. Akainama na kisha kumvuta Patrick karibu nae.

    Muda wote huo Patrick alikuwa akilia, kisu kilichokuwa na makali pande zote kilikuwa kinaonekana vizuri machoni mwake. Tayari alijiona kukaribia kifo, akaanza kusali sala yake ya mwisho katika kasi ambayo ilimshangaza hata yeye mwenyewe.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mganga akaonekana kuridhika na sala yake ambayo alikuwa akisali katika kipindi kichache kilichopita. Alichokifanya ni kumsogeza Patrick karibu na chungu kile na kisha kukisogeza kisu shingoni mwa Patrick ambaye alikuwa akilia huku akikukuruka huku na kule.

    “Majini..miungu yetu...pokeeni damu hii kama chakula chenu cha kila siku” Mganga alisema kwa sauti ndogo lakini iliyosikika vizuri masikioni mwa Patrick.







    *****









    Bi Anna bado alikuwa akiendelea na harakati zake za kuendelea kuwatetea wanawake ambao kila siku wao walikuwa watu wa kufanya kazi nyingi huku waume zao wakiwa wanakunywa kahawa na kupiga soga. Kila siku idadi ya wanawake ilizidi kuongezeka mpaka kufikia wanawake elfu moja.

    Bi Anna akaamua kukipeleka kikundi kile Shinyaga mjini ambako kwa mchango mkubwa wa wanawake, ofisi ikatengenezwa na kuwa kama ofisi kuu ya chama hicho. Idadi ilizidi kuongezeka zaidi mara baada ya wanawake ambao walikuwa wakiishi mjini kujua malengo ya kikundi kile.

    Jina la Bi Anna likaanza kusikika katika kila kona mkoani Shinyanga, kila mwanamke ambaye alikuwa nje ya kikundi kile alitamani kujiunga na kikundi kile. Wanawake kutoka katika mikoa mbalimbali, nao walikuwa wakijiunga katika kikundi hicho ambacho kilikuwa kikishika kasi kadris siku zilivyozidi kwenda mbele.

    Ndani ya miezi sita, kikundi hiki cha wanawake kikaamua kuchangishana michango na kutengeneza nyumba nzuri ambayo wakaamua kumpa mwenyekiti wao, Bi Anna kuitumia katika siku zote ambazo ataendelea kuwa mwenyekiti wao.

    Bi Anna akaona maisha kuanza kubadilika, akaanza kujiona mtu mwenye thamani sana katika maisha yake. Hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuishi katika nyumba ambayo ilikuwa na umeme pamoja na maji. Kila wakati alikuwa akijiona kuwa mwanamke ambaye alikuwa amepangiwa mambo mengi sana katika maisha yake.

    Moyo wake haukuwa sawa, kila wakati alikuwa akiifikiria familia yake. Aliikumbuka vizuri sana siku ambayo mume wake, mzee Innocent aliuawa kwa kushambuliwa na vijana katika kijiji cha Chibe. Bado moyo wake ulikuwa na mamivu kadri alivyokuwa akilikumbuka tukio lile.

    Hakujua kama mwane, Patrick alikuwa ameuwa kama alivyouawa mumewe au alikuwa hai. Kila siku alikuwa akimuomba Mungu amlinde mtoto wake kama alikuwa hai ili baadae waweze kuonana tena.

    Nyumba ile kwake ilikuwa kubwa, kila kitu ambacho kilikuwa kikihitajika katika maisha ya binadamu kilikuwa kikipatikana katika nyumba ile. Maisha yake yalikuwa ya upweke, bado alionekana kuihitaji familia yake iwe pamoja nae.

    Mara kwa mara kikundi chake kilikwa kikifanya mikutano malimbali katika mkoa wa Shinyanga. Wanawake walikuwa wakijaa kwa wingi katika mikutano hiyo ambayo ilionekana kumvutia kila mtu, hata wanaume nao walikuwa wakishiriki katika mikutano hiyo.

    Kikundi kile kikaanza kutembea katika mikoa mbalimbali ya karibu na kuendelea kuongea maneno ambayo yalikuwa yakiwatetea wanawake waliokuwa wakifanyishwa kazi kama punda.

    “Kuna mkutano wa wanawake unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam. Na wewe kama mwenyekiti wetu tumeamua uende ukatushirikishe” Bi Stumai, katibu wa kikundi hicho alimwambia Bi Anna ambaye aaonekana kushtka.

    “Unasema kweli? Taarifa hizo zimekuja lini?” Bi Anna aliuliza.

    “Zilikuja juzi hapa ofisi. Nilikuwa nakusubiri urudi kutoka Mwanza ili nikueleze jambo hili” Bi Stumai alimwambia.

    Bi Anna akashusha pumzi ndefu, hakuonekana kuziamini taarifa zile. Alijiona kuwa kama alikuwa ndotoni ambapo baada ya muda angeamka kutoka katika usingizi mzito. Akaanza kumwangalia Bi Stumai huku akionekana kutokuamini kile ambacho alikuwa amemwambia.

    Kila siku kufika jijini Dar es Salaam ndio ilikuwa ndoto yake.Mara kwa mara alikuwa akisikia sifa mbalimbali kuhusu jiji la Dar es Salaam hali ambayo alitamani sana nae kuingia ndani ya jiji hilo. Taarifa ile ilionekana kumchanganya kupita kiasi.

    Moyo wake uliamini kwamba kitu chochote ambacho kingefanyika ndani ya jiji la Dar es Salaam basi kilikuwa na uwezo mkubwa sana kusikika Tanzania nzima kutokana na kuwa na vyombo vingi vya habari. Alitamani ajitangaze ili Tanzania nzima kumfahamu yeye ni nani na alikuwa na malengo gani katika maisha yake. Muda wote alijisikia kuruka ruka kwa furaha, safari ya kwenda Dar es Saaam ilionekana kumchanganya kupita 

0 comments:

Post a Comment

Blog