Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

ADHABU YA PENZI LAKO - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ROSE MACHA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Adhabu Ya Penzi Lako

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    "kwann unanikatili kiasi hiki victo, nimekukosea nini?" kwa uchungu nililia sana, sikuruhusu mdomo wangu unyamaze, niliendelea kulalama huku machozi yakinitirika kama mvua za manyunyu zikitokea angani kuangukia ardhini, Cha ajabu ni kwamba machozi yangu wala sauti yangu Ile ya huzuni havikuweza kumshawishi Victor walau anisikilize. Aliendelea kunisakama na kunitolea maneno ya kashfa sana kwangu, "Rose kiukwel nimekuchoka Huna mvuto wa kuwa na mimi, tambua wewe si hadhi yangu sijui ilikuaje hata nikawa na wewe" Ni kwel maneno ya Victor yalikuwa makali ila sababu ya upendo ule wa dhati niliyokuwa nao niliyaona ya kawaida. Nilizidisha machozi na kumbembeleza anisamehe kama Kuna kosa nililolifanya. "Victor kumbuka tulipo toka kumbuka maneno yako kwangu kwamba hutoniacha, kwamba mimi ndo mwanamke pekee unaenipenda, tafadhal usinitende haya," Nilizidi kulia huku kwikwi ikinishika, muda huo wote nilikuwa mlangoni mwa nyumba yake sabab alikataa nisiingie ndan, "Victor basi naomba niingie ndani walau nipumzike kidogo sababu sijihisi vizur" , Nilipomaliza kusema hayo nilimtazama Victor machoni nikitegemea angenipisha niingie, Lakin ghafla kabla hata Victor hajatoa jibu lolote nilisikia sauti ya mtu aliyetoa msonyo wa dharau tena msonyo ule ulikuwa mkali hata kupenya kwenye masikio yangu kwa upesi, "Nani yumo humo ndani" Niliuliza kwa tahamaki huku nikitaka kumjua aliyeko humo ndani, kwa nguvu nilimsukuma Victor na Kuingia ndani "Mungu wangu wa mbinguni" bila kificho nilijikuta nikimwita Mungu wangu huenda angenisaidia pale pale, sikuweza kuamini macho yangu kwa yule niliyemwona mle ndani, Mary rafiki yangu wa damu, aliyekuwa kama ndugu yangu, aliyenijua kuliko ndugu yangu yeyote yule ndiye aliyekuwa mle ndani kwa Victor, Lakin yeye aliponiona hakuonekana kuniogopa wala kushtuka, alisimama kwa kujibaraguza huku akibinua midomo yake iliyopakwa lipstick ya pink akionekana kujiamin zaidi ya neno lenyewe, pale pale na mimi uso wangu ulibadilika, nikaanza kuvuta nyusi ya kulia imfate ya kushoto Ili kitokee kitu kinachoitwa ndita usoni, midomo ilianza kuumana sababu ya hasira, mapigo ya moyo nayo yalianza kwenda mbio sana, "unashangaa nini kipi kigeni kwako au kipi hakijielezi" Mary alitamka hayo

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wakat mimi niko busy kumtazama Kwan hata alichovaa kilikuwa ni jibu tosha ya maswali niliyokuwa nayo. Kwa hasira nilimrukia na kuuvamia mwili wake, kabla ya Victor kuingilia kati tayar nilishauvaa uso wake na kumkwaruza vibaya sana, "Rose sitaki balaa kwangu" kwa ukali Victor alitamka huku akionekana kuwa upande wa rafiki yangu Mary, "ebu nisikilize kwanza, Mary ndie chaguo langu na hiki unachokiona naomba ukielewe na utambue ya kwamba sikuhitaj tena" Nilipo sikia hayo nilichoka akili na mawazo, "Victor leo unanikana mbele ya Mary, hapana Victor usiwe mnyama kwangu tafadhal," nililia mara dufu ya mwanzo nilidiriki hadi kupiga magoti sababu nampenda sana Victor wangu, ndiye mwanaume niliyemweka moyoni na kuamini kuwa ndiye mume wangu kipenz. "Victor nakupenda jaman siwezi bila ya wewe na unalijua hilo" Nilizidi kulia kwa uchungu sana ila Mary alikuwa akicheka sana alikuwa akichochea maneno kwa Victor. "naomba utoke humu ndani sitaki kukuona" Victor alisema, nilipo ona Victor hawezi nisikiliza nilifuta machozi yangu na kuweka Sawa sauti yangu Ili niongee neno La mwisho kwake, "Sawa naondoka ila Mungu atanilipia" nilivuta pumzi yangu na kumtazama Victor Ili nimueleze jambo La msingi, "Victor kilichonileta hapa ni kutaka kukueleza kuwa Nina..... Nina mi..." kabla sijamaliza kusema shetan alimvaa Mary Ili kunitenda unyama ambao si kutegemea kama angediriki kunitenda, alimsogeza Victor pembeni na kunikamata kwa nguvu na kunisukuma, kwa kuwa sikujiandaa nilikosa balance na kujikwaa kisha mguu wa kushoto ukautega mguu wa kulia nikaanguka kwa kishindo puuuuu!! hatimae nikaangukia kiuno, "ebu toka nje husikii" Mary hakujua kama nimepata maumivu makali sana kiunoni, nilitoa sauti ya uchungu nikiomba msaada ambapo Victor aligundua nimeumia ila hakuweza kunisaidia sababu alimwogopa Mary, nilichoambulia ni kusikia mlango mkifungwa kwa nguvu. Nikiwa pale chini nilijisikia kama roho inatoka ila nilijitahidi kujiinua na hatimae nilisimama japo kwa shida. Nilijifuta machozi yangu na kuanza safari ya kurudi kwangu. Kiukwel niliumia sana kiuno ila sikuwa na jinsi. Nikawa natembea kwa shida huku nilijitahidi mtu asije chochote kinachoendelea, nikiwa njian naelekea mahali taxi zilipo nilianza kuhisi maumivu ya kizidi huku macho yangu yakikosa nguvu za kutazama vizuri mbele, na masikio yangu yakiwa hayasikii tena, kumbe nilikuwa katikati ya barabara. Hatimae nilidondoka chini na kupoteza fahamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Nilizinduka kutoka katika usingizi ule mzito ambao ni nusu ya kufa, nilipo fungua macho yangu sikuweza kujielewa niko wapi, nilianza kupepesa macho yangu huku na kule nikijiuliza niko wapi, chumba kilikuwa kikubwa chenye mwanga wa kutosha, hewa Safi pia palikuwa patulivu sana, bado sikuweza kubaini mapema niko wapi, nilipotaka kusogeza mkono wangu nilishindwa nikalazimika kutazama kipi kinachozuia mkono wangu usijisogeze, ilikuwa drip imechomekwa kwenye mikono yangu, "ooh niko hospitali" nilijisemea japo sikujua nimefikaje, wakat bado nawaza hayo mlango ulifunguliwa Kwan kwenye chumba kile nilikuwa mwenyewe, "heeyyi habari Dada yangu" alikuwa ni kijana ambae sijawahi muona awali japo yeye alionesha kunifahamu, sikumjibu kitu zaid ya kumtazama kwa makini, "usiogope upo salama, ila pole sana" alinikarimu sana Kaka huyo Lakin nilitaka kujua nimefikaje mle ndan, "usijali ukipona utajua tu, usiwe na haraka," majibu ya yule Kaka yalikuwa yakinikera sana sababu sikuwa namjua hivyo nilitaka kumjua. "mimi naitwa Gabriel, ndiye niliyekuleta hospitali sababu ulidondoka ghafla njiani ukiwa unatembea" kwa upole na ukarimu Gabriel alijieleza kwangu."tangu lini niko humu ndan " niliuza" hii ni siku ya nne tangu upoteze fahamu" Niliguna tu na kugeukia upande mwingine. Ghafla sura ya Victor na ya Mary ziliniijia kichwani kwangu, maneno Yale machafu ya Mary yalianza kunitawala kichwan kwa kasi, nilianza kuweweseka huku mikono ikikakamaa kwa hasira, "noo Victor, usiniache tafadhal, nakuhitaji" nilianza kulia tena hali iliyomtisha Gabriel wa watu, alikimbia haraka kumwita doctor ambae nae hakukawia kufika mle ndani, alinikuta nikikakamaa hasa mikononi, kwa haraka niliona akiinua bomba La sindano na kunichoma, ndani ya sekunde chache nilijihisi kuishiwa nguvu, Gabriel alinisogelea na kunishika mkono wangu na kuubusu ishara ya kunifariji japo nae hofu Ilimtawaka, ghafla usingizi mzito ulinivaa.

    Gabriel hakuonesha kuwa na hofu za mimi kuendelea kukaa pale hospital. Alizidi kuwa karibu yangu na kunihudumia kwa chochote nilichohitaji. "Nina mdogo wangu anaitwa Jackline naishi nae, nahisi atakuwa ananitafuta sana" nilianza kumpa maelezo na mwongozo wa kumpata Ili aje pale hospital, "naomba unisaidie kumtafuta Kwan najua atakuwa ananitafuta sana" nilimsisitiza afanye ivo nae aliondoka kumtafuta Jackline, akiwa njian alijitahidi kukumbuka mtaa alioelekezwa. Alipofika alianza kuuliza bila ya mafanikio kila mtu anadai hamjui, alihisi kukata tamaa hatimae alijisogeza kwenye duka Linalouza mahitaji ya nyumban na kununua maji walau apunguze kiu huku akitafuta mbinu mpya za kumpata huyo Jackline. Akiwa pale dukani alikuja binti mmoja amevaa kanga Safi iliyochora umbo lake na kiblauzi chepesi sana kilichoendana na maua ya kanga Ile, "aisee yani hapo ndo huwa nakupendea binti mapozi" muuza duka alianza kumpamba kwa maneno matamu, "ivi mapozi wewe una roho gani tangu uje huu mtaa sijawahi kukuona na mwanaume mhh ujue unatutesa sana" habari za muuza duka zilimvutia sana Gabriel aliyeanza kumkagua huyo anaeitwa mapozi, "haki ya Mungu nitaenda kwa babu Ili nikupate niweke historia mtaani kwa kummiliki mtoto mzuri kama wewe" muuzaji alikuwa akichekesha sana jambo ambalo hata Gabriel alianza kucheka, "Yan we na Dada yako mnatupa matatizo mtaani yani tukiwaona hatupumui, looh Victor anafaidi sana vitu adimu kwa Rose," maneno ya muuza duka yalimshtua sana Gabriel ambae alisimama wima kutoka pale alipokuwa amekaa. "kwanza Nina siku kama Tatu nne ivi sijamuona amesafiri nini?" muuza duka bila kujua alikuwa akinirahisishia kazi alizid kuhoji "eee we na wewe maneno yamezidi utadhan unaimba taarabu ebu nipatie sabuni me niondoke zangu" binti mapozi kama anavojulikana mtaani alichukua sabuni na kuondoka, pale pale nae Gabriel alimfuata kwa nyuma, "samahan dada, wewe unaitwa Jackline?" Gabriel aliuliza huku akiwa na furaha kazi yake imefanikiwa, Jackline alikubali ndipo Gabriel pale pale aliamua kumweleza yaliyojiri, "nilijua tu haya yatatokea" Jackline alianza kutoa machozi sababu alifahamu fika kinachoendelea pia kwa sabab ya mimi kulazwa "Sasa anajijua ni mjamzito Lakin bado anaenda kufanya fujo kwa watu" aliendelea kulia kwa uchungu huku akilaani kabisa kitendo cha Mary kunigeuka. Gabriel alitaman kujua kilichonipata ndipo Jackline alianza kumhadithia Gabriel

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "unajua Dada yangu alikuwa akihudumu kwenye supermarket moja iko maeneo ya mjini, alikutana na kijana mmoja anaitwa Victor ambae ni mmiliki wa hiyo supermarket, kiukwel Victor alimpenda sana Dada yangu, alimwachisha hiyo kazi na kumfungulia duka La nguo zuri tu. Waliishi kama mke na mume kwa kipindi kirefu sana, hakuna asiyejua kama Dada yangu ni mke wa Victor, mapenzi yao yalikuwa yakiwavutia wengi sabab ya kusikilizana kwao pia waliendana sana. Siku zilivokuwa zikisogea na upendo wao ulidumu, siku moja tukiwa dukani aliingia mdada mmoja mzuri kwel, Rose alipomwona alimwita jina Lake ishara anamfahamu, nae alipogeuka na kubaini ni Rose alifurahi sana na wote wawili walisogeleana na kukumbatiana mkumbatio ambao naamin haukuwa wakinafki ndani yake na kila mmoja alionekana kufurahia kitendo cha wao kuonana. Walisalimia huku nyuso zao zikionesha tabasamu zito. Walianza story nying za maisha kila mmoja akimweleza mwenzie changamoto za maisha wanazokumbana nazo, Rose alisahau kabisa kazi sikuiyo sabab ya Mary. Story zilizidi hadi Victor aliwakuta, Dada Rose alimtambulisha Mary kwa Victor. Basi ikawa ndo ratiba za Mary Kuja dukani na kukaa pamoja nasi. Mary alionekana mcheshi, mpole na mstaarabu sana, wakat mwingine Dada alikuwa akiongea mengi na mengine hata me hakuwahi hata kunieleza ila alimweleza Mary sababu ya uaminifu waliokuwa nao tangu Zaman, wakati mwingine Mary alimsifia Dada kwa kumpata mwanaume aliyekuwa akimjali na kumhudumia, huwezi amini katika maneno yao kumi wanayoongea basi ya Victor ni maneno saba, siku moja Mary alifanya utani kwa Dada kuwa akizubaa ataibiwa kwa Dada Rose ilikuwa kawaida sana ila mimi nilianza kuingiwa na mashaka, nilianza kuingiwa na wasiwasi juu ya uhusiano ule baina yao, Mary alianza vituko ambavo kwa Rose vilikuwa vya kawaida ila kwangu nilianza kuhoji, siku moja alimwomba Dada amwombe Victor awapeleke outing nae Dada hakuona hiyana aliomba na kukubaliwa, tulipelekwa wote na tulikunywa sana japo mimi sikunywa sana sikuiyo. Mary alianza vihoja akijisifu na kujitapa, aliongea mengi sana hasa yahusuyo mapenzi huku kila alichoongea alikuwa akimshika shika Victor ambae alivutiwa na habari za Mary. Looh! Nilimtazama Dada yangu ambae hakuwa na wasiwasi na rafiki yake kama vile mimi nilivo. Muda wa kurudi nyumban uliwadia sababu sisi tulikuwa jirani na tulipokuwa tumekaa ilimbidi Victor atufikishe nyumbani kisha amsindikize Mary kwake. Kutoka tunapokaa na anapokaa Mary ni nusu saa tu. Nilipoangalia saa ilikuwa kama saa sita usiku, basi Victor alipomsindikiza alichelewa kurudi Rose alikuwa amelewa sana kiasi kwamba alipojilaza hakujitambua nikabaki mimi namwesabia masaa Victor. Tangu saa sita mpaka saa tisa kama na nusu ivi ndipo aliporudi nyumban na kunikuta sebuleni naangalia TV. Aliponiona alishtuka sana



    Victor alishtuka sana kuniona mpaka saa tisa Ile niko macho, Nami nilipomwona nilitabasamu kuficha sababu zilizonifanya nikae mpaka muda ule kwamba nilitaka kuhakikisha anarudi muda gani. Alianza kunihoji kwanini mpaka muda ule sijalala Nami nilimjibu kuwa sikuwa na usingizi, aliitika kwa kichwa na kuniuliza tena kama hata Dada Rose yupo macho, nikamjibu kwamba alilala tangu saa sita Ile aliyoturudisha nyumban na kumpa uhakika zaidi kuwa hakumuulizia, baada ya maelezo hayo nilianza kuona sura Ile ya hofu na wasiwasi aliyokuja nayo ikipotea usoni na hali ya kujiamin ikimvaa, alipitiliza hadi chumban bila ya hofu yoyote ndipo nilipopata uhakika asilimia zote kuwa Victor alimsaliti Dada Rose Kwan harufu ya manukato ya Mary ilisikika baada ya Victor kupita mbele yangu. Muda huo huo nilimchukia Mary kiasi kwamba sikutaka hata kumuona.

    Palipokucha tulielekea dukani nae Mary alikuja, siku hiyo alionekana kutokujiamin kama siku zote, muda wote alikuwa busy na simu yake, japo Dada Rose alijitahidi kuongea kama sikuzote Ile Mary alikuwa mkimya kigezo ni uchovu wa Jana, sikutaka kumwonesha kuwa najua machafu yake sababu sikutaka kuwa mwepesi wa kuvunja aman baina yetu. Mary alizidi kuwa mkimya alaf ghafla akaibuka na maswali mengi kwa Rose. Alianza kudadisi ujio wa Victor usiku ule, "shost me najua hata alipanda kitandani muda gani? Yani hata sijui" kwa madaha Dada alijibu huku akionesha kutokujali muda aliorudi Victor, nahisi hakujali sababu alimwamini mume wake kipenz, nilishindwa kuvumilia nikabidi niropoke, "mhh yatawashinda mwaka huu" wote wawili walinitazama na kucheka bila ya kuhoji kauli yangu.

    Siku zilipozidi kusonga ndo na mambo yalianza kunipa uhakika zaidi kwamba Kuna usaliti unaoendelea baina ya Victor na Mary, kasi za Mary Kuja dukani zikianza kupungua, na hata akiwa dukani muda mwingi alijitenga tenga na rafiki yake mkubwa akawa simu, pia hakupenda tena simu yake ishikwe hasa na Rose. "Mary yani Nina matatizo mwenzio" Dada alianza kumsimulia shost wake huyo habar za Victor yakuwa amebadilika sana, "sikuiz nisipopiga simu hanipigii, amekuwa mkali sana kwangu, najitahidi kumhoji tatizo nini ndo kabisa nazidisha matatizo" Dada Rose alimweleza huku akiwa mnyonge sana, "pole sana shost ameanza lini hiyo tabia yani Hawa wanaume wabaya sana" Mary alisema kumfariji Dada Rose, nilihisi kama sumu imepanda hadi mdomoni, nilitaman kusema ukwel ila nilishindwa sababu sikuwa na uhakika wowote japo najua kila kitu, Rose alizidi kumweleza shida zake naye Mary akiwa busy kumsikiliza na kuishia kumpa pole, wanaongea huku Mary akiendelea kuchat na simu, ghafla sms iliingia kwenye simu ya Rose, "NIAMIN MIMI KUWA NAKUPENDA USIOGOPE" Rose alipoisoma alitabasamu na kumwonesha Mary "mhh alijuaje kuwa Nina mawazo hata akanitumia huu ujumbe" baada ya Rose kusema Yale Mary alibadilika sura, aliguna tu bila ya kumjibu Rose, kwa kuwa mimi ndo nilikuwa nafatilia huo mchezo mchafu wa Mary, nilibaini Ile sms haikuwa ya Rose ila Victor alikosea, nilianza kujifanya nataka kutumia simu ya Mary kumpigia mtu, kwa kuwa Mary alinidharau na kuamin sijui chochote zaidi ya kuuza nguo alinipa simu tena bila masharti, nilijidai napiga kisha nikatoka nje ya duka na kuanza kusoma sms zake, "SAMAHANI USICHUKIE NILIKUWA NAKUTUMIA WEWE" mara "MARY WEWE NI FUNDI SANA UMENIPA VITU ADIMU MPAKA NATAMAN TENA" nyingine "FALA HUYO ACHANA NAE KWANZA NAMVUTIA UPEPO WA KUMTEMA" looo sikuamini kabisa kama kweli Mary ni mnyama kiasi kile, chuki yangu ilizidi mara dufu kwake na niliapa kumlipiza japo hakunitenda mimi ila nikifikiri wema aliotendewa na Rose ndo hasira zinanipanda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku moja tukiwa dukani mida ya saa nne asubuhi, Mary aliaga kuwa anatoka ila ndan ya lisaa atarudi, kila nikimtazama Dada roho ya huruma inanijia ila sikutaka kusema mapema nikihofia fujo zinaweza kuzua madhara ila niliamin ipo siku tu atajua mwenyewe, tuliendelea na kazi bila ya tatizo, "Jackline ebu nenda nyumban kuniletea kadi ya bank sijui nimeisahau vipi leo" Rose aliniagiza na mimi niliita pikipik nikapanda kuelekea nyumban, nilipofika nikabaini mlango upo wazi, nilishtuka sababu wakat tunatoka asubuhi mimi ndo niliufunga basi nikaingia kwa haraka kujua Nani yupo mle ndani, nilipofika kwenye chumba cha Rose niliingia kwa kuparamia bila kubisha hodi "mama yangu mzazi" kwa tahamaki nilitamka bila kutarajia niliufunga ule mlango kisha nikaenda kuketi kwenye sofa nikiwa siamin macho yangu, taswira ya Dada yangu kipenz ilinijia nikifikiria jinsi Dada yangu alivo mpole, mcheshi na mtaratibu, nikiliwaza tabasamu lake analopenda kulitoa pindi awapo na Victor, roho ya huruma ilinijia na nikaamua kunyanyua simu yangu na kutaka kumweleza niliyoyaona, Ile nataka kumweleza nilishtukia Victor amenipokonya simu na kuikata, "Sasa unampigia Ili afanyanye, au unataka afe kwa presha na ivi unajua kwangu hajiwezi" tangu namfahamu Victor kwa mara ya kwanza ndo namsikia akimkashfu Dada yangu, "ila sikukatazi kumweleza, ukitaka mwambie simu hii apa" alinirushia simu yangu huku akifunga zipu ya suruali, "ila kiherehere chako kitakuponza kwani akijua nitawafukuza dukani na hapa nilipowapangia sababu mnaishi kwa pesa zangu" aliposema hayo alimvuta Mary mkono kisha waliondoka zao, Mimi nilibaki pale sofani sijielewi pia nilisahau nilichoagizwa nikajikuta napeleka kingine, sikuamini kabisa kile nilichokiona, Lakin kubwa zaid ni kauli za Victor. Nikifikiria ni kweli tunamtegemea yeye hivyo Sina budi kuwa mpole. Nilirudi dukani na kumkuta Mary amekaa na rose wa nacheka kama ilivokawaida yao, nilishindwa kumtazama Mary machoni ila Dada yangu kila nikimwona nataman kulia kwani hajui adui yake yuko mbele yake. Niliamua kukaa kimya kama nilivoonywa.

    Baada ya siku kama tano ivi tangu niwafume, Victor aliaga anasafiri, "tunaenda wote?" Dada aliuliza sababu safari yoyote ya Victor walikuwa wakienda pamoja, "hapana we utabaki" alimjibu kwa mkato na kuondoka zake, Mimi sikutaka kuamin kama amesafiri nilijua wazi yupo na Mary, siku mbili baada ya Victor kusafir Rose alianza kujisikia vibaya mara tumbo, kutapika n.k, alienda kupima na kubainika Ana mimba ya miezi mitatu, Rose alifurahi sana kiasi kwamba alijua hata Victor akijua atazidi kumpenda sababu awali Victor alitaman kupata mtoto kwa Rose, kitendo tunatoka hospital sms iliingia kwenye simu ya Rose "KILA KITU KILICHOPO DUKANI NA NYUMBAN NIMEKUACHIA NAOMBA USINITAFUTE WALA USINIJUE. MIMI NA WEWE BASI" alipomaliza kusoma machozi yalianza kumtoka huku akinipa na me nisome, niliposoma si kuona ajabu wala kushangaa kama Rose alivofanya, nilipuuza na kumtaka asilie njiani ila tukifika nyumban tuongee na me nimweleze niyajuayo. Kabla hatujafika nyumban Rose aliita taxi na kuniambia Kuna mahali anakwenda ila hataki tuende wote... ..... Tangu sikuiyo mpaka leo hakurudi nyumban, sikutaman kumtafuta Victor Ili nimweleze kuwa Rose huonekana sababu asingenisaidia, yani ndo leo unanieleza kuwa Dada yangu yuko hospital

    **************

    Jackline alimaliza kumweleza Gabriel mkasa ulionipata huku Gabriel akionesha kutokuami kile kisa sababu kilikuwa chakusikitisha sana... "anyway twende ukamwone Dada yako" Gabriel alisema na wote walianza safiri ya Kuja hospital

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya Jackline kueleza Yale yote, kwa Gabriel ilionekana kuwa kama ni story isiyokuwa rahisi kuaminika ila ilimlazimu kuamini.

    Niliendelea kukaa pale hospital kwa siku kadhaa, madaktari wakiendelea kunipa huduma stahiki Kwan niliumia sana kiuno ambacho kilipelekea kuumiza na kusumbua uterus, jitihada zao zilinisaidia na kwa kiasi kikubwa waliyaokoa maisha ya mwanangu aliyeko tumboni pia maisha yangu binafsi.

    Haikuwa kazi rahisi kwa Gabriel na Jackline kunihudumia hasa nikiwa pale hospitalini, wakat mwingine Gabriel alilazimika kuachana shughuli zake na kushinda na me pale hospitalini, alijitahid sana kuwa karibu yangu, kunifariji na kunipa moyo juu ya yote yaliyonipata, maneno yake wakat mwingine yalinipa nafasi ya kutabasamu na kufurahia uwepo wake

    Baada ya kundi kubwa La madaktari walikuwa wakinihudumia kuhakikisha afya yangu iko Sawa na inaridhisha kwa mimi kiruhusiwa basi niliruhusiwa na kurudi nyumba ila kwa masharti kwamba nisifanye kazi ngumu, nisitembee kwa miguu kwa muda mrefu ila kubwa kuliko lote nisiishi kwa mawazo, hasira wala nisipewe taarifa zitakazo nishtua sana. Wote kwa pamoja walihakikisha hayo hayataweza kutokea kwani wakinihudumia kwa umakini mkubwa.

    ***

    Kiukwel pamoja na ndugu zangu hao kuwa karibu yangu kwa kiwango kikubwa lakini bado haikuwa rahisi kumsahau Victor. Nitawezaje kumsahau mtu niliyempenda kwa dhati? Nitawezaje kumsahau mwanaume aliyenipenda kwa dhat kwa kipindi kirefu? Sikutaka kuamini kabisa kama kwel Victor alimpenda Mary kwa ridhaa yake ila nilijua Mary ndo aliyekusudia hayo, Mary nilikuwa namfahamu tangu tunasoma, alikuwa ni binti aliyevuruga mapenzi ya watu wengi ambao nilikuwa nawafahamu na wengine ni marafiki zetu tuliosoma nao, ila kwa upande wangu sikuwahi kudhania kama angethubutu kunigeuka kutokana na ukaribu wetu tangu awali, kutokana na undugu wa kiukabila tuliokuwa nao, kilichoniponza kutokumfikiria ni kwamba nilipotezana nae miaka karibia tisa iliyopita na tulipoonana aliniambia ana mpenzi wake ambae yuko masomoni, hayo ndo yalinipumbaza akili nikamwamini kuliko hata Jackline ambae ni mdogo wangu. Nilijitahidi sana kumsahau yaliyopita ila haikuwa rahisi, kila ifikapo usiku kwangu ni mateso sababu nilikuwa nikilalia kitanda nilichokuwa nikilalia na Victor wangu, najikaza nisilie ila wakat nazuia chozi lisitoke jicho La kulia basi lakushoto hutiririsha machozi. Kile chumba kilijaa kumbukumbu nyingi za vitu vyangu na Victor, maumivu yangu sikutaka kumuhusisha mtu yeyote yule, sikuhitaji kumkwaza yeyote yule hasa Gabriel aliyekuwa akijitahidi kunisahaulisha yaliyopita. Wakat mwingine nilikuwa nikiamini Victor bado ananipenda "labda hanitafuti sababu Mary kambana sana" kila mara nilikuwa nikijifariji na kuamini kuwa ipo siku atarudi tena.

    Siku zilizidi kusogea, Lakin kwenye moyo wangu niliendelea kuamin ipo siku atarudi wala masaa hayasogei sana. Siku moja nikiwa chumbani pekee yangu wazo lilinijia kuwa niende kwa Victor, "huenda akijua au akiona Nina mimba basi atanirudia na tutaendelea na mapenzi yetu, nilijiandaa vizuri, nikavaa dera langu Safi na kujiweka Sawa kama mama mjamzito kisha niliondoka bila ya kumtaarifu mtu yeyote yule, nikiwa njian nilikuwa nikificha shauku yangu ya kumwona Victor kwa kutabasamu, wakat nakaribia kwake niliona msafara kubwa wa magari ya kisasa na ya kifahari ishara kuwa kulikuwa na harusi maeneo hayo, sikujali sana sababu anapokaa Victor Kuna majumba mengine ya kifahari. Lakin kadiri nilivokuwa nikisogea ndivo ninavobaini kuwa magari Yale yanatokea kwenye nyumba ya Victor. Ghafla mapigo ya moyo yalianza kwenda taratibu kama vile mtu ambae amelewa na kileo kikali, nilijikaza Ili nisogee karibu kwa ajili ya kuuliza, "leo ni harusi ya Victor na Mary" nilipewa jibu ambalo sikuamini kabisa macho yangu. Sikuweza kuongea lolote zaid nilimwomba dereva taxi anirudishe nyumbani. Nilipofika tu ndan, nilimkuta Gabriel na Jackline wakinisubiri, wote kwa pamoja walinilaki kwa mshangao, nilipowatazama kwa kuwakazia macho nilibaini wanajua taarifa za harusi ya Victor na Mary. "tangu lini mnajua taarifa hizi" niliuliza kwa ukali huku macho mekundu, waliogopa sana sababu wanajua hali yangu, "tangu zaman ila......" kabla Jackline hajasema zaidi nilidondoka chini na kupoteza fahamu.....



    Nilizinduka nikajikuta tena hospitalini hata sijielewi, maumivu ya tumbo pamoja na kiuno yalirudi tena kwa kasi ya ajabu, nilipotazama kulia nilimwona Gabriel, kushoto ni Jackline, wote kwa pamoja walikuwa kimya hakuna aliyeongea chochote, awamu hii nilitambua mapema kuwa niko hospitalini. Nilipowatazama nyuso zao nilibaini wote wanaduku duku juu yangu, "ulipoteza fahamu tangu Jana mchana mpaka leo" Jackline aliniambia huku Gabriel akiwa kimya haongei chochote, "hutoweza tena kutembea kwenda popote mpaka utakapo jifungua" Jackline aliniambia nikiwa niko kitandani siwezi hata kujisogeza, "mfuko wako wa uzazi umelegea hauwezi tena kustahimili misukosuko yote iwe ya kutembea au kufanya kazi yoyote" aliendelea kunieleza habari zilizonihuzunisha, nikiwa pale pale kitandani Jackline alianza kunigombeza, "siwezi kuvumilia mpaka upone acha nikueleze makosa yako" kwa ukali alisema, "ivi kabla hujaonana na huyo Victor ulikuwa hauli, hulali, wala kupungukiwa na chochote" alisema kwa ukali, "Ana kipi haswa chakukufanya uhangaike hadi kutuhangaisha na sisi?" alizidi "Victor! Victor! Victor! Ni Nani hasa kama angekupenda asingemuoa

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mary" maneno yake yalikuwa makali na machungu, "sitaki kujua kama utakufa saiv au laa Iwapo utasikia kauli hizi ila sihitaji kusumbuliwa na wewe kisa huyo Victor." aliposema vile Gabriel alitoa sauti ya ukali ikimtaka Jackline anyamaze, "Gabby niache nimwambie bora afe kwa maneno yangu kuliko huyo Victor wake" alifoka macho yakiwa yamemtoka nayo mishipa ya kichwa ikiwa imesimama kwa hasira. "unajua ni shida gani uliyoileta Sasa? Maana yake saiv Lazima niwe na wewe muda wote, OK niambie Nani asimamie duka, Rose kwa nini hutumii akili lakini" aliposema tu ivo Gabriel alimtazama Jackline kwa ukali "nimesema nyamaza" Jackline alitoka nje na kuondoka zake akiwa ameniacha na Gabriel pale chumbani, Gabriel alinitazama na kunisogelea kisha akakaa karibu yangu kitandani, "unaendeleaje Rose" alinishika mkono wangu na kuupapasa, "usijali utapona tu mama sawa ee" huwez amini pale pale machozi yalianza kutoka, "shiiiiiii basi Rose usilie, ebu nitazame mimi" kwa sauti ya ukarimu Gabriel alitamka, "nipo nawe na nitakuwa nawe milele, sijakuacha, Jackline nae anakupenda, sote tu nakupenda" aliyatamka hayo huku akinifuta machozi yaliyokuwa yakitoka machoni, "naomba usilie kwani utazidisha tatizo" Gabriel alinibembeleza sana ila sikuweza kuvumilia maumivu, nikifikiria Kuhusu ndoa ya Victor ndo kabisa natamani kufa, bado kauli za Jackline za kukatisha tamaa ndo ziliufedhehesha moyo wangu sana, kibaya zaidi mapenzi yamesababisha mimi kuishi kwa masharti kama hayo niliyopewa na madaktari, Japo kuwa machoni hapakuwa na chozi lolote ila asikwambie mtu moyon nilikuwa nikitiririsha machozi yaliyochanganyikana na maumivu makali sana ndan mwangu. Maneno ya Jackline alianza kuzunguka akilini mwangu, "haina sababu ya mimi kuendelea kumuwaza mtu ambae ni tayar ni mume wa mtu. Nilivuta pumzi kwa nguvu kisha niliitoa kwa nguvu tena, hii ilikuwa ishara ya kumtoa Victor maishani mwangu. Sikutaka kumkwaza yeyote Kati ya ndugu zangu hao.

    Baada ya siku kadhaa niliruhusiwa kutoka hospitalini, Gabriel alikataa nisirudi tena kwenye Ile nyumba, "nataka ubadili mazingira utarudi ukijifungua" alisema hayo siyo kwamba alitaka msimamo wangu ila alitoa taarifa tu. Sikupinga chochote, nilichukua vitu vyangu na na Jackline pia hatimae tulianza maisha mapya katika jumba kubwa la kifahari La Gabriel, "mhh humu ndan unaishi mwenyewe?" kwa tahamaki niliuliza sababu ni jumba kubwa, magar mawili yapo parking huku bustani nzurii ikiwa imeipamba Ile nyumba, "maua uliyokuwa unaniletea ulitoa humu bustanini?" niliuliza kwa taratibu nae alitabasamu na kuniambia nikwel aliyatoa hapo bustanini. Nilitabasamu na kumshukuru. "Haya karibuni ndani" alitukaribisha na kutupeleka kila mmoja chumbani kwake, "woow! Jaman una nyumba mzuri sana Gabriel" sikusita kumpongeza kwa utajiri ule ambapo muda wote yeye alikuwa akicheka tu, siku hiyo ilikuwa furaha kwetu sote hasa kwa Gabriel ambae alidiriki kusema huo ni mwaka wa Tatu Sasa hakuwahi kumkaribisha rafiki yeyote wa kike me ndani, "sijui kwa nini ila naamini ni mpango wa Mungu nyie Kuja kuishi na mimi kwani ni muda mrefu sijawahi tembelewa na jinsia yoyote ya kike. Wote tulitabasamu kila mmoja akionekana kuvutiwa na uwepo wa mwenzie,

    Kiukwel ukarimu wa Gabriel ulizidi mara dufu na dufu, Kuna wakat mpaka namzuia kufanya baadhi ya vitu kwangu ila haikuwa rahisi kwa yeye kunisikia, "usinizuie kufanya kitu ambacho kinanipa furaha na aman" zilikuwa kauli zake hasa pale nitakapo mzuia kufanya jambo. Hakuwahi kunisikia na aliahidi kutokunisikia, Gabriel alidiriki kutenga muda wake wa kila ifikapo saa tano hurudi nyumbani na kunipikia chakula cha mchana, akishamaliza kupiga huniandalia vizuri na kunikaribisha chakula, baada ya chakula, hunipeleka bustanini na kuanza kunikanda miguu yangu huku akinipigia stori nyingi sana na nyingi hizo zilikuwa zikinichekesha sana kiasi kwamba huzifanya siku zangu kuwa zilizobarikiwa, upendo wa Gabriel kwangu ulizidi hata upendo wa wa wapenzi waliopendana kwa dhati, niliamini kuwa mwenye bahati ya kupendwa na rafiki dunia nzima nilikuwa mimi, upendo ule hata mwanangu aliyekuwa tumboni aliutambua, alikuwa akisikia tu sauti ya Gabriel basi huruka ruka na kunipiga mateke ya furaha sana, wazungu husema "I didn't experience that love before I haven't met Gabriel" basi ilifika kipindi nikawa sitaki Gabriel aondoke aende kazini akae tu na mimi, Kuna wakati haikuwezekana basi nitalia mpaka anaamua kurudi nyumbani, maisha yetu yalikuwa ya Amani, furaha, na kusikilizana, Yale maisha yalinifanya nisikumbuke maisha niliyopitia pia yalinifanya hata ujauzito wangu pamoja na masharti Yale niishi maisha ya kawaida wala sikuwahi kupata tatizo

    Muda wa kujifungua uliwadia, nilipoenda clinic nilimshukuru Mungu kuwa vipimo vinaonesha nitajifungua salama bila shida Iwapo Mungu ataweka mkono wake kama ilivo kawaida ya wajawazito wote wakati wa kujifungua huwa wakijikabidhi kwa Mungu wao.....



    Ilikuwa jumapili ya katikati ya mwezi, siku hiyo watu wote tuliokuwa tunaishi mle ndani tulienda kanisani kama ilivo kawaida yetu ya kwenda kanisani, sikuiyo niliamka mchangamfu kuliko watu wote ila kila muda nilihisi njaa, sikujali kama niko kanisani, niliinuka na kuondoka zangu kuelekea hotelini kula, niliagiza ugali na dagaa nikaanza kula, wakat nakula niliona kama sijaridhika nikaagiza na juice, siku jiuliza mara mbili mbili kwa nini siku hiyo niliagiza vyakula ambavo tangu mimba ikiwa ndogo nilivichukia vyakula ivo, juice ndo sikutaka kabisa kuiona ila jumapili hiyo nilivila na kuvifurahia sana. Nilipomaliza kula niligairi kurudi ndan ya kanisa ndipo nilipoamua kukaa nje nikisubiri ibada imalizike kwani ilibaki kama dakika kumi tu. Nikiwa pale nje nilianza kuhisi mwili ukibadilika kutoka katika hali niliyoizoea hadi hali ambayo sikuielewa, mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi, jasho jembamba na maumivu makali ya kiuno, niliogopa sana kiasi cha kuwajulisha wenzangu waliopo mle kanisani, Gabriel alitoka haraka na kunipakiza garini kisha aliniwahisha hospitalini kwa msaada zaidi. Masikini Gabriel alijawa na huzuni uliochanganyikana na wasiwasi juu yangu, "Ni vema mmemuwahisha, kaka upo makini sana na afya ya mkeo" nesi alisema hayo bila ya kujua kuwa hata upenzi tu baina yao haukuwepo nae bila kujieleza chochote alitabasamu kwa yule nesi, hakujali kauli ya nesi hivyo aliendelea kusubiri, "ila kweli unajua wewe na Dada Rose mnafanania kuwa wapenzi na wengi wanajua nyie wanandoa" Jackline alikazia maneno ya nesi ambapo yalimfanya Gabriel acheke sana, "yani hata kazini wanaamini kuwa Rose ni mke wangu" nae Gabriel aliyesema yaliyo moyoni mwake, "eti si rahisi kuhudumia mimba isiyo yangu" waliendelea kupiga stori za hapa na pale wakicheka Kuhusu maneno ya marafiki zao, "ila kweli hata mimi kama nisingekuwa najua ukweli, nahisi nisingeamini" Jackline alimweleza Gabriel ambae alipatwa na mshangao "yani wewe ni kama Malaika katika maisha ya Dada Rose" Jackline alizidi kueleza ya moyoni "mwanamke utakae muoa anabahati sana" Jackline alieleza Yale maneno ambayo ghafla yalibadilisha sura ya Gabriel, alionekana mnyonge na mtu kama aliyekumbushwa jambo lenye kuumiza sababu aliinamisha kichwa chini na kufikiria kama sekunde ivi. "Jackline sikuzote mwamini Mungu alaf shukuru kwa kila jambo hata kama una maumivu moyon" maneno ya Gabriel yalijaa mafumbo kwa Jackline sababu hakumwelewa kabisa. Kitendo anataka kuhoji, alimwona nesi akija kwa mwendo wa haraka kumfuata Gabriel "Rose anakuhitaji, amesema akikuona atajifungua" Gabriel kusikia hayo aliogopa sana "hapana usiwe na hofu hii huwa kawaida, mara nyingi hutokea, tumejitahidi kumsaidia ila mtoto amekataa kutoka, hatuna uhakika kuwa ukifika pale atajifungua ila Rose amekuhitaji tu uende" nesi alizidi kumchanganya Gabriel ila kwa ushawishi wa nesi yule Gabriel alikubali kwenda, alipofika tu chumbani na kunitaja jina, nilianza kuhisi mtoto akicheza tumboni yani akijigusa, "unajua leo mtoto amekasirika sababu asubuhi huku msalimu, uliamka ukamsahau" maneno yangu yalijaa imani kiasi kwamba niliamini Gabriel ndo msaada, baadhi ya madaktari walikasirishwa na ucheleweshwaji niliokuwa naufanya "hakuna msaada

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wowote hapo zaidi ya upasuaji" daktari mmoja alisema, Lakin wengine walitaka kuona nini kitatokea, muda huo machozi yalinitiririka, sababu sijui hatma yangu. Gabriel alinisogelea na kunibusu usoni, alinisogelea na kuweka mdomo wake karibu na tumbo langu, "mwanangu Anthony nisamehe sana kama nimekuudhi, unajua tulichelewa ibadani ndo maana ila niko na wewe kila siku, nataka nikuone mwanangu njoo basi Ili nikubebe.........." masikini Gabriel alishindwa kuendelea kuongea sababu machozi yalimjaa machoni, alishindwa kuvumilia kukaa pale hivyo alinyanyuka Ili atoke nje, ghafla alinisikia nikipiga kelele na hatimae alisikia sauti ya mtoto akilia, aligeuka na kushuhudia kwa macho yake, cha kwanza kutazama ilikuwa ni mtoto gani kazaliwa, "eeh tangia nianze hii kazi sijawahi kuona mtoto anatoka kwa kuombwa msamaha" daktari mmoja alisema "heee na ametoka kwel mtoto wa kiume au mlishajua kabla?" nesi nae alidakia. Lile tukio si tu kushangaza ila liliibua maswali hasa walipojua mtoto yule si wa Gabriel "sitaki kuamini, ebu ona kuchat na vidole aah anyway tusihoji sana" nesi alisema huku akimhudumia mtoto wangu. Gabriel nae alitoka nje ya chumba machozi yakimtoka "Kuna nini Rose mzima mtoto je" Jackline alidadisi ila Gabriel alitoka nje kabisa ya hospital kupunga hewa, Lakin bado hakuacha kulia, "Gabriel mbona unalia, siku ya leo si ya majonzi Bali furaha" Jackline alimshika bega Gabriel akimpooza, "laiti ungefungua moyo wangu ungejua Nina furaha kiasi gani" Gabriel alijitetea "mbona Sasa unalia?" Jackline alihoji "ipo siku utajua ila usimwambie Dada yako kama nalia" alijitetea "Sawa japo unanipa wasiwasi" Jackline alisema huku akimpapasa mgongoni ishara ya kumliwaza......



    Nilimshukuru sana Mungu wangu kwa kunipa wepesi katika kujifungua kwangu. Niliishukuru pia imani yangu iliyoamini kwamba Gabriel ndie mkombozi wangu na hatimae kwel ilikuwa vile nilivoamini. Furaha yangu ilizidi zaidi nilipomwona Gabriel akiwa karibu yangu akitimiza ahadi yake ya kuwa na mimi milele. Nilipomtazama machoni, niliona tabasamu na furaha iliyozidisha amani moyoni mwangu.

    Ni wiki mbili Sasa tangu nijifungue, Jackline na Gabriel walinihudumia na kuhakikisha hakuna kasoro yoyote inayojitokeza, Gabriel alikuwa akanileta mahitaji mengi sana ya mtoto na mimi, "Gabriel mbona unasumbuka sana Kuhusu mtoto, usinunue vitu vya gharama kisa mtoto, huoni unaharibu pesa" nilijaribu kumkataza ila yeye hakutaka kusikia, kila akirudi nyumbani huleta mifuko mingi yenye nguo, vifaa vya michezo na mahitaji ya mtoto, kibaya zaidi alimwita fundi kisha akamwonesha chumba ambacho Gabriel alikitenga kwa ajili ya mtoto, "nadhan unajua vyumba vya watoto vinatakiwa vikae mkao gani" alimweleza ndipo fundi alipoanza kupaka rangi upya kile chumba, picha picha za katuni, maua na mapambo mengi yalizidi kwenye kile chumba, kitanda chake kilikuwa kizuri na cha gharama, midoli iliyokuwa ikitoa milio mbalimbali ilikuwemo mle ndan, hakika kile chumba kilikuwa zaidi ya chumba cha mtoto ambae baba yake ni tajiri na maarufu kuliko, hakuna aliyekiona kile chumba asikitaman, mtoto yule kwa Gabriel alikuwa ni zaidi ya almasi au kitu cha thaman ambacho hayuko radhi kukipoteza, upendo wa Gabriel ulizidi hata mimi mama wa mtoto,

    Afya ya mtoto iliridhisha na kuboreka kila mwez, kila nikimpeleka clinic manesi hawachoki kumbeba na kumsifia, "jaman Anthony, kasura kama cha baba yake, mhh mwone alivolala yani nataman ungekuwa wangu" hayo ni maneno ambayo manesi hupenda kuyasema, sikuwahi kwenda clinic pekee yangu, huwa naongozana na Gabriel ambae yeye hupenda kumbeba mtoto huku mimi nikiwa nimebeba mkoba wangu, "yani maisha ya hawa wateja huwa nayataman sana, ebu ona baba na mama Anthony wanavopendana" wengi walivutiwa na maisha yetu japo hakuna anaejua kama mimi na Gabriel si wapenzi.

    Sikumoja wakati tunatoka clinic nilimwomba anipeleke supermarket kununua mahitaji ya mtoto sababu Kuna baadhi ya mahitaji nilimaliza, alikubal na kunipeleka. Tuliingia wote na kuanza kukusanya mahitaji yetu, Gabriel alikuwa amembeba Anthony me kama kawaida yangu sikuwa na kitu nimebeba zaidi ya mkoba wangu. Wakati naendelea kukusanya ghafla nikikutana uso kwa uso na Mary mle ndani, aliponiona alishtuka sana, alinitazama juu mpaka chini akiwa haamini, nahisi hakutegemea kuniona katika hali Ile, nadhan alijua amenitoa kwenye raman ya uzuri na urembo kama niliyokuwa awali, aliponitazama alibaini uzuri wangu umeongezeka mara dufu, shingoni nina mkufu mzuri wa dhahabu, gauni langu La thaman, hereni na mkoba nikioubeba wa gharama kuliko hata mikoba niliyokuwa nikiitumia enzi niko na Victor. Nilipomwona sikukunja uso sababu nilimsamehe tangu zaman. "mambo Mary, jaman ndoa imekupendeza" kiukwel nilimweleza hayo kiunafki sababu kabla ya ndoa alikuwa na shape acha kabisa, rangi yake haikuwa nyeupe kama yangu ila yenye mvuto ila baada ya ndoa yote hayo yaliporomoka. "nzur tu Rose naona unapendeza sana, yani siamin kama ni wewe" Maneno yake dhahiri hayakuwa na unafiki sababu kile asemacho ndicho cha ukweli, "ulidhani baada ya yote ningepauka?" nilimjibu kwa dharau lililofichwa na tabasamu. Wakat bado tunashangaana Gabriel alikuja "mami vipi nimeona huu unga ni mzuri kwa mtoto ebu tukaujaribu" nilishukuru sana kitendo cha Gabriel kuniita jina La mvuto "mami" Nami nilitabasamu na kuitikia "yes darling huo unafaa weka huku" nilimjibu nae aliweka, Gabriel huwa si mwepesi kuhoji kila kitu alimsalimu tu Mary kikawaida sana kisha alitaka kuondoka "baba Anthony, huyu anaitwa Mary mke wa Victor, yule aliyekuwa mpenzi wangu" kwa mtu mwenye akili timamu Lazima angetambua wazi nilikuwa najitapa kwa Mary. Nilihisi mimi Nina dharau ila Gabriel alizidi, alipomtazama alisunya na kunishika mkono tuondoke bila ya kusema chochote, naamin Mary alijisikia vibaya sana, alijiona ovyo na mtu asiye na thaman kwetu.

    Tulipo fika nyumban tulimweleza Jackline "yani mmekosea mngemzaba kibao ila najua ataenda kuoga baharini kuondoa mkosi maana hiyo ni zaidi ya fedheha mliyomfanyia" wote kwa pamoja tulicheka na kuendelea na stori za kawaida huku Gabriel akituchekesha

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku Tatu baada ya kuonana na Mary, wakat Jackline anaelekea dukani alimkuta mwenye nyumba pamoja na Mary wakimsubiri Jackline. Nae Jackline alipowaona alishtuka mno, "kuanzia leo naomba utoe vitu humu ndani sababu hili duka Victor ndo alikuja kuomba hivyo mimi namtambua yeye si nyie" Jackline kusikia vile alimpigia simu Gabriel nae alikuja kuwasikiliza "ahaaa basi Sawa mzee tupe siku mbili Ili tutoe vitu vyetu" Gabriel aliomba ila tulikataliwa, Gabriel alitafakari kama sekunde ivi kisha alinyanyua simu yake na kumpigia mtu aje, kama roho saa gari La mizigo lilikuja na watu walianza kutoa vitu "Gabriel mbona mnatoka tena" mmoja wa vibarua anaemfahamu Gabriel alisema "wenye nguvu wameamua kutunyanyasa" alijibu "nguvu wapi ujinga tu ngoja nimpigie simu mzee mmoja ana fremu kubwa na nzur tu" yule kijana alisema na kufanya ivo "tena una bahati vimebaki viwil ebu twende maana ni mtaa unaofata" Gabriel na huyo Kaka walienda, akabaki Jackline na Mary pale wenyewe, Mary alianza kumwonesha dharau Jackline. "hahahaa watu wanaoishi kwa misaada" Mary alijishaua bila ya kujua Jackline si Kama mimj, yeye hasubiri kesho hulipa muda huo huo. "ebu rudia ulichosema" kwa jazba Jackline alisema. "eeh ebu niondolee mikosi" masikini Mary hakujua anachana na nyoka aina ya kifutu. Jackline hakumchelewesha alimkamata na kumpa kichapo cha maana, aliiharibu sura yake ndan ya dakika moja, watu Kuja kuwaamua tayar Mary kaona rangi zote, Gabriel kurudi hakuamini alichokiona. "nahuu ni mwanzo kila unionapo uwe unakimbia" Jackline alijitanua mabavu kwa Mary ambae hakuamini kama kupokea kile kichapo, alimpigia simu Victor nae ndan ya dakika kadhaa aliwasili na kumkuta mke wake kavimba uso..



    Victor alimsogelea mke wake na kubaini alipokea kichapo cha maana, uso umevimba kama vile mtu aliyeshambuliwa na nyuki. Mbali na Victor, kila mtu alishangaa ni kichapo gani kile cha sekunde kiliweza kumuumusha Mary vile, kwa jazba Victor aligeuka kumfuata Jackline Ili akishushe kichapo kwa Jackline, alipomkaribia bila kutarajia alishtukia Gabriel yuko mbele ya Jackline. Mhhh midume mawili ilijikuta ikitazamana kama majogoo yanayotaka kupigana, wanaume hao waliolingana urefu, yenye miili Sawa, wote walionekana wamejawa hasira huku kila mmoja akimtazama mwenzie kwa makini na wote walikuwa tayari kwa lolote. Lakini Gabriel alionesha kujiamini zaidi ya mwenzie sababu sura yake haikuwa na jazba kama ya Victor, "nadhan ingekuwa busara ukawaacha wanawake Hawa wapigani sababu ni ugomvi wa kike wewe mwanaume unataka kupigana na Jackline Ili iweje" Gabriel alimweleza Victor ambae hakutaka kusikia, "kwaiyo wewe ndo ulimtuma ampige si ndio?" alihoji kwa ukali ambao haukumbabaisha Gabriel aliyezidisha kujiamini, muda huo wote Jackline alijificha kwenye mgongo wa Gabriel . Victor alimsukuma Gabriel Ili amkabili Jackline, looh hapo Victor alikosea sana kwa kitendo cha kumshika Gabriel na kumsukuma, kwa hasira ambazo hakuna mtu aliyeweza kuamini Gabriel angekuwa nazo alimvuta Victor na kumgeuza kama vile mtu ageuzavo chapati, bila kuchelewesha Gabriel aliinua mkono wake uliokunjwa ngumi tayari kwa kushushwa kwenye mwili wa Victor, ashukuriwe mmoja wa vijana wale vibarua alibahatika kumuwahi Gabriel na kumtoa pale, "usije ukajaribu maisha yako yote kumshika Jackline wala Rose naahidi nitakufuta kwenye list ya watu hapa mjini" alisema kwa ukali huku akiwa amejaa sumu ambazo hakuna aliyetegemea. Alimvuta Jackline akamfungulia mlango wa gari kisha waliondoka kurudi nyumban. Walipofika walinikuta nanyonyesha mtoto wangu. Nilishtuka kuona Gabriel anaingia ndan bila ya salamu na alipitiliza hadi chumban kwake, niliogopa sana ikabid nihoji yaliyotokea, "ivi Mary ananitafuta nini si nimeshamwachia Victor" nilisema kwa hasira na jazba, niliinuka na kumfata Gabriel mle ndani, alinieleza kila kitu huku akiwa amejilaza kitandani, "najua nakosea nakitetea na kukipigania kitu ambacho si mali yangu" Gabriel alisema "wewe si mpenzi wangu wala si ndugu yangu, huyu mtoto si wangu ni wa huyo Victor" aliguna kidogo kisha aliendelea "muda wowote atamhitaji mtoto wake na wakat mwingine hata wewe unaweza kurudi kwake" aliendelea "umeniingiza kwenye ugomvi na watu, Sina uadui na mtu yeyote hapa mjini kwa mara ya kwanza nimeanza leo" maneno yake yalikuwa machungu kwangu "ila sijakulaumu Rose ahadi yangu ya kuwa na wewe siku zote bado ipo moyon mwangu". Niliinamisha kichwa chini machozi yakibubujika, "Rose usilie sababu kila kitu duniani kina sababu, ebu tusubiri tuione hiyo sababu" Gabriel aliniambia huku amenilaza kwenye kifua chake, muda huo nae Jackline alisimama mlangoni kutusikiliza. "nawapenda sana wote hasa mwanangu Anthony" Gabriel alisema hayo akinibusu kichwan kama faraja. Jackline nae alitusogelea na kukupapasa migongoni "namwomba sana tuendelee kuishi ivi milele" Jackline alisema

    Gabriel alifanikiwa kupata kile chumba cha biashara, aliniita mimi na Jackline, akatukalisha kikao, "nahitaji kujua malengo yenu Sasa maana naona wewe Rose mtoto amekuwa na Hana usumbufu alaf Jackline upo upo tu hivyo kila mmoja aniambie anataka nini nimfanyie" Nilipo sikia hayo sikuamini kabisa nilitabasamu na kufurahi "ehee Jackline nakusikiliza" Gabriel alisema "kiukwel Kaka ndoto zangu mimi ni kuwa mwanamitindo, napenda sana ivo kama utaweza nisaidia nifikie malengo nitashukuru" Jackline alisema hayo kwa kiu na hamu ya kusikia Gabriel atamjibu nini. Gabriel alimtazama Jackline na kuguna tu "haya wewe mama Anthony" ilipofika zamu yangu, nlijiweka Sawa na kuanza kujieleza "mimi umri ushasogea na tayari Nina mtoto, nachoomba ni kuwa tu na biashara hasa maduka ya urembo ikiwezekana na saloni sababu ndiyo ninayoweza" Nami nilijieleza yaliyo moyon mwangu, "Jackline unauhakika na ulichoomba siyo napoteza pesa bure" Gabriel alimweleza Jackline ambae kwa mara ya kwanza nilishuhudia akipiga magoti kwa Gabriel "Iwapo nitaenda kinyume na malengo yangu, Kaka Gabriel naomba Mungu anihukumu" looh hadi Gabriel alipumua kwa nguvu, "OK ngoja tuone itakuaje ila Rose kesho utaniandikia mahitaji yako Ili nilianze lakwako wakat nafatilia La Jackline" alisema

    Zilipita siku kama Tatu ivi nikiwa nyumbani, ghafla simu yangu Iliita "Kuna mtu atakuja kukuchukua hapo nyumbani" ilikuwa sauti ya Gabriel. Gari Hilo lilifika kisha nilienda kule aliko Gabriel, "woow pazuri" nilijikuta nikitamka hayo huku macho yangu yakikagua kwenye kile chumba, ilikuwa salon ya kike bora, nzur, yakisasa na yenye kuvutia kwa mandhari yake, chumba kilikuwa kikubwa na chenye hewa, mle mle ndani kulikuwa na duka kubwa la nguo za wanawake na vipodozi, nikikadiria nadhani ni pesa nyingi sana na gharama nyingi ambazo hata ningekuwa vipi nisingeweza kupata biashara kama Ile. Kikubwa zaidi kulikuwa hadi na wafanya kazi mle ndani,. Sikuamini macho yangu, machozi yalinitoka sikuamini pale aliponiambia hiyo ndo biashara yangu, nililia siku nzima nilimkumbatia Gabriel kwa huba na msisismko nikimshukuru kwa moyo wake, "utaanza kazi kuanzia kesho binti wa kukusaidia mtoto atakuja leo jioni, basi we nenda nyumbani " Gabriel alisema huku akikataa kunipeleka yeye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku iyo Gabriel alichelewa Kuja nyumbani ila alipokuja tuliona magari yakiongozana, moja lakwake alilokuwa nalo, lingine ni dogo lenye rangi jekundu. Wote tulitoka kutizama," supriseeeeeeee! "Gabriel alisema " Rose ebu njoo mama" Gabriel aliniita "sitaki kuingia ndani mpaka ujibu maswali yangu" alizidi kusema "Rose wewe ni mwanamke wa pekee sana ambae nimekuzoea na kukukubali sana" aliendelea "tangu siku ya kwanza kukuona nisijihisi kitu ila sikuwa mwepesi kukisema" aliguna na kunitazama machoni "Rose nakupenda sana na naomba uwe mchumba wangu hatimae mke wangu" Gabriel aliyasema maneno Yale huku akiwa amepiga goti moja na Pete ikiwa mikonon akisubiri majibu yangu. Nililia sana, nikikumbuka nilikotoka sikuwa na haja ya kufikiria mara mbili, na mimi nilipiga magoti na kumkumbatia Gabriel, sikuweza kuongea zaidi ya kulia kwa kwikwi, macho yangu yalitoa machozi kiasi cha kuloanisha kifua changu "nakupenda sana Gabriel niko tayar kuwa mkeo" nilisema hayo ndipo nilipovalishwa Pete ya uchumba na wote walifurahi sana hasa Jackline. "mpenz wangu Nina zawadi yako ya gari" Gabriel alinipa ufunguo wa gari langu lile, sikuamini macho yangu jaman nilihisi kama ndoto, nikiwa ktk furaha zile Gabriel aliniacha na kumsogelea Jackline, "ehee jack wangu unasemaje hapo" alimweleza Jackline huku akitabasamu "mambo yako yametimia, utaenda Italy kujifunza mitindo kama ulivotaka," Jackline hakuamini kabisa alirukaruka kama mwanakondoo aliyeshiba maziwa ya mama yake. "kila kitu kipo Sawa ni wewe kujiandaa" Gabriel alisema

    Sikuamini kile nilichokiona Kati yangu na Jackline . Jackline alituaga hatimae alikwea ndege na kuelekea Italy kwa muda wa miaka mitatu. Ndipo maisha yangu na Gabriel yalianza upya bila ya Jackline kuwepo. ....



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog