Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NOTHING WITHOUT YOU (SI KITU BILA WEWE) - 5

 





    Simulizi : Nothing Without You (Si Kitu Bila Wewe)

    Sehemu Ya Tano (5)





    Ilipoishia



    Wakaangalia katika eneo lile, nguo za Patick zilikuwa zipo chini huku damu zikiwa zimetapakaa katika nguo zile. Kila mmoja akaonekana kushtuka kupita kiasi. Kila walipokuwa wakiangalia katika kila upande, hakukuwa na mtu yeyote zaidi ya zile nguo za Patrick zilizokuwa na damu ambayo iliwafanya kuona kwamba Patrick alikuwa ameliwa na wanyama wakali.



    Songa nayo sasa...







    Siku zilikuwa zimekatika na siku ya shindano la uchoraji kufikia. Watu walikuwa wamekusanyika kwa wingi katika ukumbi wa chuo cha Emden kilichokuwa katika jiji hilo la Humberg. Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari walikuwa wamekusanyika katika ukumbi wa chuo hicho kwa ajili ya kuangalia ni nani ambaye alikuwa akienda kuibuka mshindi katika shindano hilo ambalo liliteka hisia za watu duniani.

    Majaji zaidi ya ishirini walikuwa wamekaa katika viti vyao mbele kabisa ya ukumbi ule wakiwa tayari kwa ajili ya kumchagua mshiriki ambaye alikuwa na picha nzuri kuliko washindani wengine.

    Benard, mchoraji bora wa bara la Ulaya alikuwa amekaa pamoja na watu ambao alikuwa amekuja nao nchini humo. Muda wote uso wake ulikuwa ukionyesha tabasamu pana kama kawaida yake kwa kuona kwamba ni lazima angechukua ushindi huo kama kawaida yake.

    Benard hakuonekana kumuogopa mtu yeyote katika kinyang’anyiro hicho, alijua fika kwamba kulikuwa na wachoraji wengi mbalimbali ambao walikuwa wazuri, lakini kila alipokuwa akijiangalia yeye, alijiona kuwa bora zaidi ya wachoraji wote duniani.

    Picha ambazo alikuwa akizichora katika mashindano yote zilionekana kukubalika na kila aliyekuwa akiziangalia, Benard hakuonekana kuwa na mpinzani katika kipindi chote cha nyuma kilichopita, lakini katika kipindi hiki, hali ilionekana kuwa tofauti kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jina la Patrick lilikuwa likisikika katika midomo ya watu wengi nchini Ujerumani jambo ambalo wengi wao wakaamua kuanza kuzifuatilia picha mbalimbali ambazo alikuwa amezichora, hakukuwa na picha ambayo ilionekana katika mitandao katika kipindi hicho kutokana na watu waliohusika kuzitoa kutokana na muda wake kupita.

    Watu wengi walitaka kuona ni nani angeibuka kuwa mshindi kati ya Patrick kutoka katika bara la Marekani ya Kaskazini na Kati na Benard kutoka katika bara la Uaya. Si kwamba wachoraji wengine kutoka katika mabara mengine hawakuwepo, walikuwepo lakini hawakuonekana kuwa bora zaidi ya watu hao wawili, wao walionekana kuwa kama wasindikizaji tu.

    Muda ulizidi kusogea mbele huku watu wakizidi kuongezeka katika ukumbi huo mpaka kufikia hatua ambayo hakuhitajika mtu yeyote ukumbini kutokana na watu kuwa wengi. Wale ambao walikuwa wamekosa nafasi, walikuwa nje wakifuatilia kila kitu katika televisheni kubwa ambazo zilikuwa zimewekwa ukutani.

    Picha za washirika wote zikaletwa kwa majaji, majaji wakaanza kuzipitia moja baada ya nyingine huku wakiwapa watu waliokuwa wakihusika na komputa kuziingiza katika mitandao.

    Picha ziliendelea kuingizwa katika mitandao huku kila mtu akiwa na simu yake tayari kwa kupiga kura ambazo zingemuwezesha mshindi kujinyakulia kiasi cha dola milion thelathini pamoja na kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa ambaye angetembelea nchi mbalimbali kuwaona watoto na watu ambao walikuwa wagonjwa mahospitalini.

    “Mmmmh!” Jaji mmoja alisikika akiguna.

    Jaji yule hakuishia kuguna tu, alipoangaliwa na wenzake, akawagawia picha zile ambazo zilimfanya kuguna. Kila jaji akaonekana kushtuka, hawakuamini kama michoro ambayo walikuwa wakiiangalia iliwafanya kushangaa kuita kiasi.

    “Vipi kuhusu hii michoro? Hivi hii imechorwa au kupigwa picha?” Jaji mmoja aliwauliza wenzake kwa sauti ya chini.

    “Nilisikia kuhusu michoro ya kijana huyu ambayo alikuwa akiichora. Nilitamani sana kuziona picha zake. Kweli inashangaza” Jaji mwingine alisema.

    Hawakuta kuedelea kuizungumzia michoro ile. Kitu walichokifanya ni moja kwa moja kuipeleka kwa watu ambao walikuwa wakihusika na mitambo ya kompyuta. Watu ambao walikuwa wakiziweka picha zile wakaonekana kushangaa, picha ambazo walikuwa wakiziangalia, zilionekana kuwashangaza.

    Muda wa kuanza kuzipigia kura pcha zile ukafika. Kila mtu akachukua simu yake na kuanza kubonyeza namba fulani fulani kwa ajili ya kuzichagua picha bora.

    Muda wote Benard alibaki akishangaa, picha za Patrick ambazo alikuwa akiziangalia katika simu yake zilionekana kumshangaa kupita kawaida. Hakuonekana kuamini kitu ambacho kilimfanya kufungua begi lake na kulifungua na kisha kuchukua komputa yake ndogo.

    Akaiunganisha na internet na kisha kuanza kuziangalia picha zile kwa ukubwa zaidi. Muda wote alibaki akishangaa tu, hakuamini hata mara moja kama picha zile zilikuwa zimechorwa kwa mkono wa binadamu. Ni kweli alikuwa amechora picha nyingi lakini kwa zile picha ambazo alikuwa akiziangalia, zilionekana kuwa bora zaidi.

    Dakika thelathini za kupiga kura ambazo zilikuwa zimtolewa zilionekana kutosha kabisa, zaidi ya kura milioni mia nne themanini na tano zilikuwa zimepigwa kwa wakati huo mpaka katika muda ambao mitambo ilifungwa.

    Benard alikuwa akitetemeka kwa hofu, hakuona dalili zozote ambazo zilionyesha kuchukua ubingwa ule ambao ulikuwa na zawadi nyingi kuliko vinyang’anyiro vyote vilivyopita. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka japokuwa kulikuta na viyoyozi ukumbini mule.

    Tayari mambo yakaonekana kubadilika, watu ambao walikuwa wamekuja nae walikuwa wakimwangalia kwa nyuso zilizojaa aibu, hawakuona kama mtu wao angekwenda kuibuka na usindi kama miaka mingine.

    Jaji akainuka huku kompyuta yake ikiwa mkononi tayari kwa kumtaja mtu ambaye alikuwa amejinyakulia kiasi kikubwa cha fedha pamoja na ubalozi wa Umoja wa Mataifa. Jaji akauangalia umati wa watu, hakuwa na lolote la kuongea zaidi ya kumtangaza mtu ambaye aliibuka kuwa bingwa wa kuchora duniani.





    *****





    Wapelelezi wakazichukua nguo zile za Patrick ambazo zilikuwa zimeloana damu na kisha kuanza kuondoka nazo mpaka pale ambapo waliiacha boti yao. Kila mmoja alibaki akishangaa, boti ya watu wale ambao walikuwa wamekuja na Patrick ilikuwa mahali pale ikielea.

    Hawakujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea, hawakujua kama wanyama wakali kama dubu na mbwa mwitu walikuwa wamewatafuna na wao pia au la. Wakaingia katika boti yao na kisha mashine kuwashwa na safari ya kurudi mjini kuanza.

    Mara baada ya kufika katika chumba cha hoteli ile moja kwa moja wakachukua simu na kuwapigia makao makuu kuwaeleza kile ambacho kilikuwa kimetokea kisiwani Rogen.

    Habari ile ilipokelewa kwa masikitiko makubwa, hakukuwa na mtu aliyeamini kama mwisho wa Patrick ungekuwa ni kuliwa na wanyama wakali porini. Serikali ya Ujerumani ndio ambayo ilikuwa imebeba lawama zote hali iliyopelekea kwa kiasi fulani urafiki kati ya Marekani na Ujerumani kuanza kuyumba.

    Tarifa ile ikatangazwa katika vyombo vya habari. Dunia ikatikisika huku watu wakihuzunika kupita kawaida mitaani. Kifo cha Patrick kilionekana kuwahuzunisha kupita kiasi. Alionekana kuwa kijana mdogo ambaye wala hakutakiwa kufa kwa wakati ule, alionekana kuhitajika kula matunda ya kipaji chake ambacho kilikuwa kimeushangaza dunia.

    Wamarekani wakalia sana, wanafunzi wa shule ya Vanguard wakaonekana kushtushwa sana na taarifa zile, wanafunzi wengine wakazimia. Mgogoro mkubwa katika ya Marekani na Ujerumani ukaanza upya.

    Hakukuwa na kitu chochote ambacho kilikuwa kikiongelewa na Ujerumani ambacho kilikuwa kikieleweka kwa Wamarekani. Nchi ya Ujerumani ikaonekana kuwa nchi iliyojaa vitisho ambayo haikutakiwa kukaliwa na watu waliokuwa na ngozi nyeusi.









    *****





    Bwana Mayemba alisimama pembeni ya kitanda alicholalia mkewe, muda wote uso wake ulikuwa ukionyesha majonzi mazito. Hakuonekana kuamini kama Patrick yule ambaye alikuwa amejizolea umaarufu mkubwa duniani ndiye ambaye alikuwa mtoto wa mkewe ambaye alikuwa akizisikia habari zake mara kwa mara.

    Muda wote alikuwa na majonzi, alitamani sana mkewe azinduke kutoka katika usingizi mzito na kuanza kuongea nae mambo mbalimbali. Madaktari walikuwa wakiingia na kutoka ndani ya chumba kile huku wengine wakiendelea kutoa huduma ambayo ilikuwa sahihi kupewa Bi Anna.

    Sindano moja ya dripu ilikuwa imeingia katika mshipa wake huku maji yakimiminika taratibu katika mshipa wake. BI Anna alikuwa kimya kitandani, toka kule hotelini mpaka hapo kitandani kwa wakati huo, hakuwa ameongea kitu chochote kile.

    Yalipita masaa kadhaa, Bi Anna akafumbua macho yake na kuanza kuangali huku na kule. Hakuonekana kupafahamu sehemu ambayo alikuwepo mahali hapo. Akaanza kuangalia huku na kule, akaonekana kushtuka mara baada ya kuona dripu ikining’inia.

    Acho yake yakagongana na macho ya mumewe ambaye kwa mbali alionekana kuonyesha tabasamu. Bi Anna akarudisha tabasamu, mara tukio la kila kitu kilichotokea hospitalini likaanza kujirudia kichwani mwake. Uso wak ukabadilika na kuanza kulia.

    “Mtoto wangu...mtoto wangu Patrick...” Bi Anna alimwambia mumewe.

    “Usijali. Yuko salama” Bwana Mayemba alimwambia mkewe, Bi Anna.

    Bi Anna alikaa hospitalini hapo kwa masaa mawili zaidi na ndipo akaruhusiwa kutoka. Muda wote akawa mnyonge huku akianza kufuatilia kwa karibu vyombo vya habari ambavyo mara kwa mara viikuwa vikitoa taarifa kuhusiana na Patrick nchini Ujerumani.





    *****

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Hali ilionekana kuwa tofauti kabisa mara baada ya Patrick kutangazwa kuwa mshindi katika kinyang’anyiro kile. Badala ya watu washangilie kwa shangwe, idadi kubwa ya watu walikuwa wakilia. Mioyo yao iliumia kupita kawaida kwani kila mmoja alijua kwamba Patrick alikuwa ameuawa katika kisiwa cha Rogen baada ya kuliwa na wanyama wakali.

    Mwalimu Simon akasimama na kuanza kuelekea mbele ya ukumbi ule ambapo alikuwa akihitajika. Makofi yakaanza kusikika, uso wa mwalimu Simon haukuonyesha furaha yoyote, macho yake yalikuwa mekundu na baada ya muda machozi yakaanza kumtoka.

    Ni kweli kitu ambacho kilikuwa kikihitajika na Wamarekani wengi kilikuwa kimepatikana lakini tatizo lilikuwa kwa mtu ambaye alikuwa amesaidia kwa asilimia zote kitu hicho kupatikana. Alisimama mbele ya ukumbi huku watu wakipiga picha mbalimbali.

    Vanessa hakuwa na nguvu na tayari alikuwa amelia mpaka kupoteza fahamu. Muda huo hakuwa ukumbini hapo, alikuwa amekimbizwa katika hospitali ya Humberg ambako matibabu yalikuwa yakiendelea.

    Ndoto ya Patrick ilikuwa imetimia japokuwa hakuwa hai katika kipindi hicho. Dunia nzima likuwa imemtambua zaidi kuwa kama mchoraji ambaye ameutikisa ulimwengu kwa kupata kura zaidi ya miaka yote iliyopita.

    Siku mbili zilizouata, Vanessa ambaye alikuwa amepata nafuu pamoja na mwalimu Simon wakarudi nchini Marekani huku wakitangulizana na jeneza la Patrick ambalo lilikuwa na zile nguo zake.

    Uwanja wa ndege watu walikuwa wakilia kupita kawaida. Vipeperushi vilivyokuwa na jina lake viikuwa vikipeperushwa hewani. Hakukuwa na mtu ambaye uliufurahia ushindi ule vilivyo, kifo cha Patrick kiliwafanya kuwa na huzuni kupita kawaida





    *****





    Ilikuwa ni siri kubwa sana ambayo ilikuwa ikiendelea katika maisha ya Bruno Deutcsher. Mara kwa mara alikuwa akielekea katika kisiwa Rogen kwa ajili ya kuwawinda wanyama wadogo wadogo ambao alikuwa akiwatumia kutengenezea gundi iliyokuwa ikitumiwa sana nchini Ujerumani.

    Biashara hiyo ikaonekana kumuingizia fedha nyingi kiasi ambacho alinunua nyumba kubwa za kifahari pamoja na magari kadhalika. Ingawa jina lake halikuwa kubwa kama majina ya wafanyabiashara wengine lakini Bruno alikuwa akiheshimika sana.

    Mara kwa mara alikuwa akielekea katika kisiwa cha Rogen ambako huko alikuwa akiendelea kuwauwa wanyama mbalimbali na kisha ngozi zao kutengenezea gundi. Miaka yote hiyo ndio ilikuwa kazi yake kubwa, kuwauawa wanyama na kisha kutengeneza gundi.

    Kitu kilichomfanya kufanya kila kitu kisiri ilitokana na serikali ya Ujerumani kuweka ulinzi mkubwa sana katika kisiwa cha Rogen. Hakutakiwa mtu yeyote kuingia katika kisiwa hicho kwani kilikuwa kisiwa chenye wanyama wakali ambao hata wengine hawakupatikana katika sehemu yoyote ya Ulaya.

    Bruno hakuonekana kuogopa, bado alikuwa akielekea katika kisiwa kile huku mikononi mwake akiwa na bunduki pamoja na mikuki iliyokuwa na sumu kali. Kila mnayama ambaye alikuwa akimuona mbele yake, alikuwa halali yake.

    Sauti za watu zilikuwa zikisikika kutoka katika sehemu ambayo wala haikuwa na miti mingi. Bruno akaonekana kushtuka kupita kawaida. Hakuamini kama katika kisiwa kile kungekuwa na watu wengine ambao walikuwa wakija porini pale. Maswali kibao yalikuwa yakimiminika kichwani mwake juu ya watu wae ambao walikuwa wamefika katika kisiwa kile.

    Hofu ya kudhani kuwa watu wale walikuwa walinzi ikaanza kumuingia, alitamani kukimbia ili kuepuka kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. Kila alipotaka kukimbia, akajikuta akisimama na kusonga mbele kuangalia ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea.

    Wanaume wawili walikuwa wakionekana vizuri machoni mwake huku kijana mmoja akiwa chini akilia. Mara mlio wa bunduki ukasikika, Patrick akushika mguu wake na kuanza kulia. Risasi ilikuwa imezama mguuni mwake na kuutoboa mfupa wa ugoko wake.

    Kilio kikubwa kilikuwa kikisikika kutoka kwa Patrick, kilio kile kilimfanya Bruno kushikwa na huruma kupita kawaida. Vijana wale walikuwa wakiendelea kufurahia, kilio ambacho alikuwa akilia Patrick kilionekana kuwapa furaha kupita kawaida.

    “Tutaendelea kupanda juu” Sauti ya kijana mmoja ilisikika.

    Akaikoki tena bunduki yake na kisha kujiandaa kumpiga tena na risasi. Mara akashtukia mkuki ukiwa umezama shingoni mwake. Kijana mwingine, hata kabla hajapata wazo la nini alitakiwa kufanya, nae akashtukia mkuki mwingine ukizama shingoni mwake.

    Kutokana na sumu kali iliyokuwa imepakwa katiika mikuki ile, wakajiukuta wakianguka chini. Bruno akaanza kupiga hatua za haraka haraka kumfuata Patrick mahali pale alipokuwa. Bado Patrick alikuwa akilia kwa maumivu makali huku akiwa ameushika mguu wake, mfupa wake wa mguu wake ulikuwa umevunjika.

    Kitu alichokifanya Bruno ni kuzichukua nguzo za Patrick na kuzipaka damu ambazo zilikuwa zikiendelea kuwatoka vijana wale ambao alikuwa amewapiga mikuki ya shingoni. Alipomaliza kuwapaka, akaibeba miili ile na kwenda kuificha porini zaidi.

    Alipomaliza akarudi pale alipokuwa Patrick na kisha kuanza kumbeba huku akiwa mtupu. Bruno alifanya vile makusudi huku akiwa na lengo la kutaka kuwapiga changa la macho watu ambao wangefika mahali pale kwa kutaka kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeendelea kwa kuamini kwamba watu wale walikuwa wamekuja na wenzao ambao waliwaacha katika boti yao.

    Patrick alikuwa katika hali mbaya sana, mguu wake ulikuwa umejeruhiwa vibaya na risasi ile ambayo ilimuingia. Akapakiwa botini na safari ya kuelekea mjini kuanza.

    Bruno alikuwa akiendesha boti kwa kasi, alitaka kufika ufukweni haraka ambako hapo angechukua gari lake na kisha kuelekea nyumbani kwake. Ndani ya dakika kumi, akawa amekwishafika ufukweni. Ukimya ulikuwa umetawala mahali hapo kutokana na njia ile ambayo mara kwa mara alikuwa akiitumia kuwa njia ya panya.

    Akambeba Patrick mgongoni na kisha kumuingiza garini na safari ya kuelekea nyumbani kwake kuanza. Maswali kibao yalikuwa yakimiminika kichwani mwake, alitamani sana kumfahamu mtu ambaye alikuwa amembeba lakini kutokana na giza kuwa kubwa, wala hakuweza kumfahamu japokuwa alijua kwamba mtu yule alikuwa mweusi.

    Mara baada ya geti la nyumba yake kufunguliwa, moja kwa moja akaliingiza gari lake na kisha kumshusha Patrick garini na kuanza kuelekea nae ndani ya nyumba yake huku aiwa amembeba begani mwake. Alipomfikisha katika chumba kimoja ambacho kilionekana kuwa kama zahanati ndogo, akamlaza katika kitanda.

    Akachukua simu yake na kumpigia daktari wake ambaye alimtaka afike mahali hapo haraka iwezekanavyo. Ni ndani ya dakika kumi, daktari akawa amefika mahali hapo ambapo akaanza kukiosha kidonda cha Patrick na kisha kuanza kuitoa risasi ambayo ilikuwa ndani ya mfupa wake ugokoni.

    “Kweli mguu utarudi katika hali ya kawaida kweli?” Bruno alimuuliza Dokta Paul.

    “Utarudi, ila atachukua muda mrefu kidogo kitandani. Baada ya hapo tutampa kibaiskeli cha kutembelea huku mguu wake ukiwa kwenye P.O.P” Dokta Paul alisema.

    Maisha ya Patrick yalikuwa juu ya kitanda ndani ya nyumba hiyo, hakutakiwa kutoka kwenda sehemu yoyote ile. Kila siku dokta Paul alikuwa akifika nyumbani hapo kwa ajili ya kuhakikisha matibabu kwa Patrick. Wote walikwishajua kwamba mtu ambaye walikuwa wakimtibia alikuwa yule Patrick ambaye alikuwa amechaguliwa kuwa mchoraji bora na ndiye ambaye alikuwa ametangazwa kuuawa porini kwa kuliwa na wanyama wakali.

    Waliendelea kukaa na Patrick kwa muda mrefu mpaka pale alipopata nguvu ya kukaa juu ya kibaskeli na kukifanya kuwa miguu yake. Kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea ndani ya nyumba ile kilioekana kuwa siri kubwa kwani waliamini kama siri ingetoka basi mtu ambaye aliwatuma vijana wale kumuua Patrick wangefika mahali pale na kumuua.

    Miezi mitatu ikakatika na Patrick kuanza kujisikia nafu, kutokana na dawa kali ambazo alikuwa amepewa, akaanza kutembea kwa kuchechemea mpaka pale ambapo akaanza kutembea kamakawaida.

    Kitu ambacho alikuwa akikitaka kukifanya mahali hapo ni kumpigia simu mchungaji Smith pamoja na familia yake na kuwaambia kuwa yeye ni mzima na alitarajiwa kurudi nchini Marekani siku yoyote ile.

    “Unajisikia vizuri kabisa?” Bruno alimuuliza.

    “Ndio. Ninajisikia vizuri” Patrick alijibu.

    “Ila kuna kitu ningependa usikiseme kwa mtu yeyote yule” Bruno alimwambia Patrick.

    “Kitu gani?”

    “Jinsi nilivyokuokoa kisiwani. Unajua kama utasema kila kitu, utaniweka katika wakati mgumu sana kwani serikali itanikamata kwa kuingia ndani ya kisiwa kile” Bruno alimwambia Patrick.

    “Usijali Bruno. Kwa kuwa umeniokoa katika mdomo wa kifo, amini kuwa sitoongea kitu chochote kile” Patrick alimwambia Bruno na kisha kuchukua simu kumpigia mchungaji Smith pamoja na Vanessa kuwataharifu juu ya uwepo wake.



    **************************







    Furaha haikupatikana kwa Vanessa, kila siku alikuwa mtu wa majonzi. Moyo wake ulikuwa umeumia kupita kiasi. Maisha kwake pasipo Patrick yalionekana kuwa ya kinyonge kupita kiasi. Vanessa alikuwa katika wakati mgumu kupita kawaida, machozi ndio ilikuwa sehemu ya maisha yake.

    Furaha yote ambayo alikuwa nayo katika kipindi alichokuwa na Patrick ikaonekana kupotea. Afya yake ikaanza kuonekana kudhoofika kutokana na mawazo aliyokuwa nayo juu ya Patrick ambaye hadi katika kipindi hicho, kila mtu alikuwa akijua kwamba alikufa kisiwani.

    Siku nyingine Vanessa hakuwa akielekea shuleni, kila alipokuwa akiziangalia sehemu ambazo mara kwa mara alikuwa akipenda kukaa pamoja na Patrick, alionekana kuumia kupita kawaida. Maisha yake yakaonekana kubadilika, Vanessa yule ambaye alikuwa katika kipindi kile cha nyuma pamoja na Patrick alionekana kuwa tofauti na Vanessa huyu ambaye alikuwa katika kipindi hiki.

    Kila wakati Vanessa alikuwa akiangalia simu yake, jina la Patrick lilikuwa likionekana vizuri simuni mwake. Bado maumivu makali yalikuwa yakiendelea kuwepo moyoni mwake.

    Miezi miwili ilikuwa imepita tangu wamazike Patrick katika makaburi ya Louis ambayo palikuwa pakizikwa watu waliokuwa maarufu. Vanessa aliyatamani maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa na furaha lakini kila kitu kikaonekana kubadilika.

    Vanessa akashtuka kutoka katika lindi la mawazo mara baada ya kuisikia simu yake ikianza kuita. Simu iliendelea kuita, Vanessa akaichukua na kuanza kuiangalia. Namba ikaonekana kuwa ngeni machoni machoni mwake, alichokifanya ni kuikata ili kumuondolea usumbufu.

    Akasimama katika kiti ambacho alikuwa amekalia na moja kwa moja kuelekea katika kiti kingine darasani pale alipokuwa. Simu ile ikaanza kuita tena, wanafunzi wote wakaanza kumuangalia. Vanessa akaichukua simu ile na kuangalia tena kioo, namba ile ngeni ndio ambayo ilikuwa ikipiga tena, alichokifanya ni kuikata tena.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vanessa alionekana kuchanganyikiwa na hali ambayo alikuwa amekutana nayo katika kipindi hicho. Hakuonekana kuhitaji usumbufu wowote ule. Alionekana kuhitaji muda mwingi wa kupumzika kuliko kuongea ovyo na watu. Kuna kipindi alikuwa akiichukia sana simu yake kwani muda mwingi ilimfanya kutokutulia kutokana na watu wengi kumpigia simu na kumpa pole kwa kile kilichotokea.

    Simu ile ikaanza kuita kwa mara ya tatu, Vanessa akaiangalia simu ile na kuikuta namba ile ile ambayo ilikuwa ngeni simuni mwake. Kama kawaida yake, akaikata na kuizima kabisa simu yake. Vanessa akailalia meza yake ya kusomea na kutulia.

    Mara mwalimu Kerri akaingia darasani hapo na macho yake kuanza kuangalia huku na kule hali iliyoonyesha kwamba alikuwa akimtafuta mtu fulani. Alipomuona Vanessa, akaanza kupiga hatua kumfuata huku wanafunzi wengine wakimwangalia.

    Alipomfikia, akamuinua na kisha kumwambia kwamba amfuate ofisini. Vanessa akainuka na moja kwa moja kuanza kumfuata mwalimu Kerri. Vanessa hakuonekana kuelewa sababu ambayo ilimfanya mwalimu Kerri kuja kumuita na kwenda nae ofisini pasipo kuongea kitu chochote kile.

    Macho yake yakatua kwa mchungaji Smith pamoja na mkewe, Rachel ambao macho yao yalikuwa yamejawa na tabasamu pana. Vanessa akaonekana kushtuka, akaanza kujiuliza maswali kibao kuhusiana na tabasamu yale lakini hakupata jibu.

    “Kuna nini?” Vanessa aliuliza huku akionekana kushangaa.

    “Habari njema” Mchungaji Smith alijibu.

    Vanessa akaonekana kushtuka, hakujua habari njema hizo zilizozungumziwa na mchungaji Smith zilimaanisha nini kwake. Akajiona kuwa na hamu ya kutaka kuzisikia habari hizo njema ambazo mchungaji Smith pamoja na mkewe, Rachel walikuwa wamekuja nazo mahali hapo.

    “Habari njema kuhusu nini” Vanessa aliuliza.

    “Patrick....” Mchungaji alijibu.

    Vanessa akanyong’onyea, akamuona mchungaji kumtonesha kidonda ambacho kilikuwa kimeanza kupona. Akaanza kumkumbuka zaidi Patrick ambaye walikuwa wamemzika miezi miwili iliyopita. Akayapeleka macho yake kwa walimu wengine ambao walikuwa ndani ya ofisi ile, walimu wote walikuwa wakionyesha nyuso zilizojaa tabasamu.

    “Patrick anakuja. Patrick hakufa kama ilivyotangazwa. Nimeongea nae simu na amesema kwamba anakuja. Ninafikiri kwa sasa atakuwa ndani ya ndege” Mchungaji alimwambia Vanessa.

    Vanessa akaonekana kushtuka, hakuamini kama kweli kitu alichokuwa akikisikia masikioni mwake kilikuwa kweli au si kweli. Alijiona kuwa ndotoni ambako baada ya muda angeamka kutoka katika usingizi mzito. Akajaribu kuyafikicha macho yake kuona kwamba alikuwa ndotoni au katika uhalisia.

    “Unasemaje?” Vanessa aliuliza huku akionekana kutokuamini.

    “Patrick anakuja. Kwani hakukupigia simu nusu saa iliyopita?” Mchungaji alimuuliza Vanessa.

    Mawazo ya Vanessa yakarudi katika simu ambayo alikuwa amepigiwa katika kipindi kichache kilichopita. Akaanza kujuta kwa kitendo chake cha kutokuipokea simu ile ambayo ilikuwa ikiingia katika simu yake. Vanessa akaonekana kuumia kupita kawaida.

    Akaichukua simu yake kutoka mfukoni, akaiwasha na kuanza kuitafuta namba ile ambayo ilikuwa imeingia katika kipindi kichache kilichopita. Alipoipata, akaanza kuipiga. Simu ile ikaanza kuita, iliendelea kuita zaidi na zaidi, ikapokelewa na sauti nzito kusikika.

    “Patrick......” Vanessa aliita.

    “Wewe ni nani?” Sauti ya Bruno ilisikika.

    “Rafiki yake, Vanessa. Alinipigia simu muda mchache uliopita. Naomba kuongea nae” Vanessa alimwambia Bruno.

    “Hayupo. Amepanda ndege kuja huko Marekani. Nafikiri kesho asubuhi ataingia” Bruno alimwambia Vanessa ambaye akakata simu.

    Vanessa akashindwa kujizuia, machozi ya furaha yakaanza kumtoka. Hakuamini kama kweli Patrick yule ambaye alikuwa ameambiwa taarifa zake ndiye alikuwa Patrick yule ambaye alikuwa akija na ndege kutoka nchini Ujerumani.

    Mwalimu mkuu akaanza kuelekea katika ofisi yake ambako akakichukua kipaza sauti kidogo na kuanza kuongea. Kutokana na vispika vidogo vilivyokuwa viemchomekwa katika kila pembe shuleni hapo, sauti yake ilikuwa ikisikika vizuri.

    Taarifa juu ya Patrick ikatolewa, hakukuwa na mtu ambaye alionekana kuamini. Wanafunzi wa shule ya Vinguard waliona tukio hilo kuwa kama muujiza mkubwa ambao wala haukutarajiwa kutokea katika maisha yao. Kila mmoja akawa na kiu ya kutaka kumpokea Patrick ambaye alitarajiwa kuongia asubuhi ya siku inayofuatia.

    Ni ndani ya dakika sabini tu, waandishi wa habari wakaanza kufika shuleni pale na kutaa kupata ukweli wa mambo. Kile ambacho walikuwa wamekisikia ndicho ambacho waliambiwa shuleni hapo. Taarifa ikatangazwa katika vyombo vyote vya habari nchini Marekani.

    Kila mtu ambaye alizisikia habari zile alionekana kutokuamini kabisa. Watu wakajiandaa vilivyo kumpokea Patrick, watoto ambao kazi yao ilikuwa ni kubeba maua wakatafutwa. Serikali ya Marekani ikamuzandaa Waziri wa Mambo ya Ndani Bwana Thomson kwa ajili ya kusimamia mapokezi uwanjani hapo.





    *****





    Ndege ilikuwa ikitarajiwa kuingia katika uwanja wa JFK saa tatu asubuhi lakini saa moja asubuhi tayari watu walikuwa wamekusanyika uwanjani hapo. Muda ulikuwa ukizidi kwenda lakini watu waliyaona masaa kwenda taratibu sana.

    Mabango yalikuwa yametapakaa katika umati huo wa watu ambao walikuwa wakimsubiri Patrick huku idadi kubwa ya watu wakiwa wamevalia fulana zilizokuwa na picha ya Patrick. Watoto wawili ambao walikuwa na maua mikononi walikuwa wamewekwa tayari kwa ajili ya kumkabishi Patrick maua hayo.

    Waandishi wa habari hawakuwa mbali, walikuwa uwanjani hapo huku kamera zao zikiwa zinaendelea kufanya kazi ya kuwapiga picha watu mbalimbali ambao walikuwa mahali hapo. Eneo kubwa la uwanja ule ulionekana kujaa watu ambao walikuwa wamefika mahali pale kwa ajili ya kumpokea Patrick ambaye alitarajiwa kuingia muda mchache ujao.

    Huku zikiwa zimesalia dakika kumi na tano kabla ya ndege hiyo kufika uwanjani hapo, gari la kifahari ambalo lilikuwa likiongozwa na pikipiki kadhaa pamoja na mgari mengine ya kifahari yakaanza kuingia mahali hapo. Watu wakaombwa kuachia nafasi. Magari yale yakasimama na Waziri wa Mambo ya Ndani, Bwana Thomson akateremka na kuanza kupiga hatua kule ambapo alielekezwa kwenda.

    Saa tatu kasoro tano ndege ya shirika la American Airways ilikuwa ikionekana angani, watu wakajiandaa vilivyo, wale ambao walikuwa wamesimama kwa mbali wakaanza kusogea karibu na uwanja ule, mapolisi ambao walikuwa mahali pale wakaanza kuwazuia watu kutokusogea karibu zaidi.

    Waandishi wa habari wakaanza kuipiga picha ndege ile mpaka inatua bado zoezi lao wa upigaji picha lilikuwa likiendelea. Ndege ikasimama na abiria kuanza kuteremka, kila mtu macho yake yalikuwa makini kumtafuta Patrick.

    Abiria waliendelea kuteremka zaidi na zaidi. Vanessa alikuwa amesimama huku akionekana kutokuamini kama siku hiyo ingekuwa siku yake ya kwenda kumuona Patrick ambaye alisadikiwa kufa kisiwani. Abiria wakamalizika, watu wakasimama vizuri, Patrick akaanza kuteremka.

    Umati wote wa watu ukaanza kuripuka kwa furaha huku maua yakirushwa angani. Hakukuwa na mtu aliyeamini kwamba Patrick, mshindi wao ndiye ambaye alikuwa akiteremka ngazi za ndege ile huku akiwa na kofia kubwa.

    Watoto ambao walikuwa na maua mikononi mwao wakaanza kupiga hatua kumfuata Patrick huku wakiwa pamoja na Bwana Thomson. Patrick hakuonekana kuamini, akabaki akipunga mikono yake hewani huku kelele za shangwe zikiendelea kusikika mahali pale.

    Patirick akakabidhiwa maua yae na watoto wale huku waandishi wa habari wakiendelea kupiga picha na kuchukua kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea mahali pale. Kila mtu alikuwa akitaka kumgusa Patrick lakini mapolisi ambao walikuwa mahali pale walikuwa wakiwazuia watu hao.

    Vanessa akapiga hatua zaidi, kutokana na mapolisi kumfahamu vilivyo, wakamuachia. Vanessa akamsogelea Patrick na kumkumbatia. Machozi yalikuwa yakimtoka Vanessa, hakuamini kama alikuwa amemuona Patrick kwa mara nyingine tena.

    “I cant believe...I cant believe..(Siamini...siamini...)” Vanessa alimwambia Patrick hku akimwangalia usoni na mikono yake ikiwa begani.

    Bwana Thomson akampa mkono Patrick na wote kusalimiana kwa furaha na kisha kuingia garini na safafri ya kuelekea katika hoteli ya Huddlesfield kuanza mara moja. Ndani ya gari ilikuwa ni furaha tupu, muda wote Vanessa alikuwa akimwangalia Patrick huku akionekana kutokuamni kama yule ambaye alikuwa pembeni yake alikuwa Patrick.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sherehe kubwa ikafanyika katika ukumbi wa hoteli hiyo huku viongozi wengi wa Serikali wakiwa wamehudhuria huku baadhi ya wanafunzi na walimu wa Vanguard wakiwa katika ukumbi huo. Ilionekana kuwa siku ya shangwe ambayo kwa Patrick ilionekana kuwa historia ambayo hakuwa akiamini.

    Katika sherehe hiyo, Patrick akakabidhiwa ubalozi kutoka katika shirika la Umoja wa Mataifa. Kitu ambacho alitakwa kukifanya baada ya wiki kumalizika ni kutembelea katika nchi mbalimbali kwa lengo la kuwaangalia wagonjwa pamoja na watoto ambao walikuwa katika matatizo mbalimbali.

    Mchungaji Smith na familia yake muda wote walikuwa wakijisikia furaha, kitendo cha Patrick kuwa mmoja wa familia yao kilionekana kuwafurahisha kupita kawaida. Muda wote Patrick alipokuwa akiongea alikuwa akimtaja mchungaji Smith na familia yake kwa kuwapa ushirikiano mkubwa katika maisha yake.

    Patrick alipoulizwa kuhusu historia ya maisha yake, akaanza kueleza kuanzia mwanzao hadi katika kipindi ambacho alisafiri na kuelekea nchini Marekani. Hakukuwa na mtu aliyeamini kama duniani kulikuwa na mtu ambaye alikuwa amepitia matatizo kiasi kile. Watu ambao walikuwa na mioyo dhahifu, walikuwa wamelia kupita kawaida.

    Sherehe ilichukua masaa matano, ikaisha na kisha Patrick kubaki hotelini hapo akipumzika huku ulinzi ukiwa umeimarishwa mahali hapo.

    Usiku, Patrick hakulala, muda wote alikuwa akimfikiria Siwema, bado alijiona kuwa na uhitaji mkubwa wa kumuona msichana huyo ambaye alikuwa kila kitu maishani mwake. Alikumbuka mambo mengi ambayo alifanya na msichana huyo katika kipindi ambaco alikuwa nchini Tanzania.

    Patrick akapania kuja nchini Tanzania ambapo angepata nafasi ya kuelekea katika kijiji cha Wami na kuonana na msichana ambaye alikuwa akimpenda kwa moyo wote, Siwema.



    ************************************





    Wiki ikakatika, maandalizi ya Patrick kama balozi kutembelea nchi mbalimbali zilizokuwa na watu wengi waliokuwa na matatizo mbalimbali yakaanza. Muda wote Patrick alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida, akili yake ilikuwa ikifikiria kwenda nchini Tanzania tu.

    Katika kipindi cha mwezi huo, Patrick alitakiwa kutembelea nchi tatu za Afrika, ratiba ambayo aliletewa ilikuwa ni nchi ya Misri, Namibia na Sudan.

    Patrick hakutaka kwenda peke yake barani Afrika, alitaka kwenda pamoja na Vanessa ili kumuonyeshea sehemu ambayo alikuwa ametokea. Umoja wa Mataifa haukuwa na kipingamizi, wakakubali ombi la Patrick. Bado Patrick alionekana kuhitaji uangalizi mkubwa jambo ambalo liliifanya Umoja wa Mataifa kuwaandaa vijana wawili, msichana Matilda pamoja na mvulana Simpson kwenda pamoja na Patrick barani Afrika.

    Ndani ya ndege Patrick alionekana kuwa na furaha, hakuamini kama muda huo alikuwa ndani ya ndege kurudi barani Afrika. Muda wote alikuwa akijiona kuwa kama ndotoni ambako baada ya muda angeshtuka na kujikuta yuko kijijini kwao, Chibe.

    Baada ya masaa kumi na mbili, ndege ikaanza kutua katika uwanja wa kimataifa wa Kairo. Watu wengi walikuwa wamesimama huku wakiwa na fulana zilizokuwa na picha za Patrick. Muda wote nyimbo mbalimbali za kiarabu zilikuwa zikiimbwa mahali hapo.

    Patrick hakuonekana kuamini, idadi ya watu zaidi ya elfu tatu ambayo ilikuwa uwanjani hapo ilionekana kumshangaza kupita kawaida. Ndege ikakanyaga ardhi na baada ya muda kusimama. Patrick hakutaka kuchelewa ndani ya ndege, moja kwa moja akaanza kuteremka pamoja na Vanessa.

    Watu wote wakaanza kupiga kelele za shangwe, Patrick akapiga magoti chini, akaipeleka mikono yake hewani na kumshukuru Mungu kwa kurudi Afrika kwa mara nyingine. Akaanza kushuka ngazi za ndege. Waziri Mkuu wa Misri, Abdurahiman Raziffa akaanza kupiga hatua kumfuata Patrick, alipomfikia, akamkumbatia na kisha kumbusu shavuni.

    Waandishi wa habari walikuwa wakiendelea kupiga picha huku kelele za shangwe zikiwa zimetawala mahali hapo. Watu hawakuamini kama kweli wangeweza kumuona Patrick macho kwa macho maishani mwao. Kitendo cha kumuona Patrick kilionekana kuwa kama tukio la kukumbukwa maishani mwao.

    Mara baada ya Patrick kuwasalimia watu waliokuwa mahali pale, safari ya kuelekea katika hospitali kuu ya hapo Misri kuanza. Garini, Patrick alikuwa amepakizwa katika gari ambalo lilikuwa wazi kwa juu, watu walikuwa wamezunguka barabara nzima kuanzia uwanja wa ndege mpaka hospitalini.

    Muda wote Patrick alikuwa akiwapungia watu mikono, watu wengine walikuwa wakilia, hawakutarajia katika maisha yao kwamba siku moja wangeweza kumuona Patrick. Safari ile iliendelea zaidi mpaka katika kipindi ambacho msafara ule unaingia katika eneo la hospitali ile.

    Patrick akateremka kutoka katika gari ambalo alikuwa yeye pamoja na dereva na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo la hospitali ile huku pembeni yake akiwepo Bwana Raziffa. Wote wakaanza kutembea katika chumba kimoja baada ya kingine, wagonjwa wakaonekana kupata nafuu, kitendo cha kumuona Patrick hospitalini pale kulionekana kuwafariji kupita kawaida.

    Patrick aliendelea kutembea katika kila chumba hospitalini mule huku ulinzi ukiendelea kuwekwa kila alipokuwa. Kila alipokuwa akipita, waandishi wa habari walikuwa wakiendelea kupiga picha kwa ajili ya kuzionyesha katika televisheni pamoja na kuzitoa katika magazeti mbalimbali.

    Patrick aliangalia wagonjwa kwa takribani masaa mawili, baada ya hapo akaanza kuelekea nje ambako baada ya muda safari ya kuelekea katika Ikulu ya nchi hiyo kuanza.

    Watu wakazidi kushangilia kupita kawaida katika kipindi ambacho Patrick alikuwa akipiga hatua kuelekea nje ya jengo lile la hospitali ile huku pembeni yake akiwepo Vanessa. Bado alikuwa akiendelea kupuga mikono hewani huku tabasamu pana likionekana usoni mwake. Patrick, Vanessa, Matilda na Simpson wakaanza kupiga hatua kulifuata gari lile, walipolifikia, wakaingia ndani.

    Wala hazikupita sekunde nyingi, mara mlipuko ukasikika mahali hapo, gari lilionekana kulipuka. Watu wakapiga kelele huku wakikimbia huku na kule.

    “Patrick....Patrick....” Watu walisikika wakiita.







    *****







    Bwana Khan alionekana kukasirika, kitendo cha vijana wake kutoweza kumuua Patrick kilionekana kumuudhi kupita kawaida. Wasiwasi ukaonekana kumshika kwamba ni lazima Patrick angesema kile ambacho kilikuwa kimeendelea nchini Ujerumani, hasa mambo yake.

    Kitu alichokitaka kwa wakati huo ni kumnyamazisha milele, aufunge mdomo wake na aiongee tena. Alichokifanya ni kuandaa vijana wawili ambao alikuwa akiwaamini sana katika kufanya kazi za uuaji. Akawapa pesa za kutosha na kisha kuwatuma kuelekea nchini Marekani.

    Bwana Khan alitaka kumuangamiza Patrick kwa haraka sana, hakutaka kujiharibia kabisa juu ya kitu ambacho kilikuwa kinaendelea maishani mwake, alitaka siri ya kuwaua watu weusi iendelee kudumu maishani mwake.

    Vijana wake, Biholf na Maxwell wakasafiri mpaka nchini Marekani. Walijitahidi kwa nguvu zao zote lakini wala hawakufanikiwa jambo ambalo lilioekana kumuongezea wasiwasi Bwana Khan. Hakuwataka vijana hao warudi nchini Ujerumani, aliwataka waendelee kubaki nchini Marekani mpaka kazi yake itakapokamilika. Aliwatumia kiasi cha fedha chochote ambacho walikuwa wakikihitaji pamoja na malupulupu mengine ili mladi tu kazi yake ikamilike.

    “Anasafiri na kwenda barani Afrika” Biholf alimwambia Bwana Khan.

    “Safi sana. Hiyo ndio nafasi nzuri. Ngoja niwatumie fedha za kutosha na ninyi msafiri kuelekea huko. Hakikisheni mnamuulia huko” Bwana Khan aliwaambia.

    “Sawa bosi”

    “Ninataka mmuue hata kwa kumpiga risasi” Bwana Khan aliwaambia.

    “Hiyo naona haitowezekana bosi, naona kama atanusurika kwa kuwaishwa hospitalini” Biholf alimwambia Bwana Khan.

    “Kwa hiyo ninyi mmeonaje?”

    “Tumlipue na bomu”

    “Itawezekana vipi?”

    “Hiyo tuachie sisi. Kila kitu kitakuwa kama kilivyopangwa”

    “Lakini inabidi mniambie mtafanyaje”

    “Tutatega bomu katika gari atakalopanda, baada ya hapo, puuuuuuuuu...kwisha habari yake” Biholf alimwambia.

    Huo ndio mpango ambao ulikuwa umepangwa. Walikuwa wakifuatilia kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea. Ratiba yote ya Patrick ilikuwa mikononi mwao. Siku mbili kabla ya Patrick kusafiri kuelekea barani Afrika nchini Misri, wakaanza kusafiri wao huku lengo lao likiwa ni kulizoea jiji la Kairo.

    Baada ya kufika katika jiji hilo, wakachukua chumba katika hoteli ya Pharaoh na kisha kuanza kupanga mipango yao. Wakajadiliana kuhusu kutengeneza bomu, kutokana na mafunzo makubwa waliyokuwa nayo, wakatengeneza bomu ambalo lingelipuka mara baada ya gari kwenda chini kutokana na uzito tofauti na ule ambao ulikuwa kabla.

    Siku ambayo Patrick alikuwa akiingia katika hospitali ya Taifa ya Misri, Biholf na Maxwell walikuwa wamekwishaingia. Katika kipindi ambacho Patrick alikuwa akiingia ndani ya jengo la Hospitali hiyo, Biholf akaanza kupiga hatua kulifuata gari lile ambalo alikuwa amekuja nalo Patrick, alipolifikia akalitegesha bomu ambalo lilikuwa limetegeshwa kwa mtindo wa uzito, kwamba lingelipuka mara baada ya gari kuongezeka uzito hasa baada ya mtu kuingia.

    Kutokana na maaskari wa pale kuwa bize kumuangalia Patrick, hawakuona kabisa kama Biholf alikuwa amekwenda katika gari lile alilokuja nalo Patrick na kutegesha bomu. Biholf na Maxwell wakatulia ndani ya gari walilokodi huku wakifuatilia kila kitu.

    Walipomuona Patrick akitoka nje ya jengo la Hospitali ile, wakaanza kuondoka mahali hapo. Wala hazikupita sekunde zaidi ya ishirini, sauti ya mlipuko mkubwa ukasikika nyuma yao kutoka hospitalini.

    “Kazi nzuri” Maxwell alimwambia Biholf huku akikenua.







    *****





    Kila siku Siwema alikuwa mtu wa kwenda kazini, kutokwenda kazini lilionekana kuwa suala gumu katika maisha yake. Kila siku alikuwa akipata usumbufu kutoka kwa wafanyakazi mpaka kwa bosi wake ambaye bado alikuwa akimlaghai kwa fedha alizokuwa nazo.

    Siwema alionekana kuwa tofauti na wasichana wengine, ingawa katika kipindi hicho alikuwa na uhitaji mkubwa wa fedha lakini hakutaka kujirahisisha kwa ajili ya fedha. Bado alikuwa na msimamo mkali katika maisha yake, msimamo wa kutomkumkubalia mwanaume yeyote zaidi ya Patrick.

    Patrick bado alikuwa kichwani mwake, siku zote alikuwa akimkumbuka kupita kawaida, majonzi ya kutokumuona Patrick ndio yalikuwa sehemu ya maisha yake. Hakujua ni kitu gani ambacho kiliendelea katika maisha ya Patrick mara baada ya kuondoka pale porini na kuelekea asipopafahamu.

    Siwema alkuwa ametoka kazini huku akionekana kuchoka kupita kawaida, kazi ambazo alikuwa amezifanya kwa siku hiyo zilionekana kumchosha. Alionekana mpweke huku akitembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea nyumbani alipokuwa akiishi na nesi Getrude.

    Watu zaidi ya mia moja walikuwa wamesimama nje ya nyumba yao kwa mtindo wa duara. Siwema akaonekana kushtuka kupita kawaida, akaanza kupiga hatua kuelekea kule ambako umati wa watu ulipokuwa umesimama. Kitu cha kwanza mara baada ya kuufikia umati ule, akaanza kupenya penya mpaka mbele kabisa.

    Macho yake yakatua kwa nesi Getrude ambaye alikuwa amelala chini huku mapovu yakimtoka mdomoni. Siwema akaonekana kushtuka kupita kiasi, akapiga magoti chini na kumshika Getrude. Tayari macho yake ambayo yalikuwa makavu yakaanza kutoa machozi.

    Siwema hakuelewa ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea mahali hapo. Wasiwasi ukaanza kumshika, akayapaleka macho yake kwa watu ambao walikuwa wamesimama kuwazunguka, macho yake tu yalionyesha kwamba alikuwa akitaka kufahamu ni kitu gani ambacho kilitokea mahali hapo.

    “Alianguka ghafla, nafikiri kama ana kifafa” Mwanaume mmoja alimwambia Siwema.

    Siwema akapigwa na mshtuko, hakuwa na taarifa yoyote kama Getrude alikuwa na kifafa cha aina yoyote ile. Hakutaka kuyapuuzia maneno yale, akasaidiana na watu waliokuwa mahali pale na moja kwa moja kuanza kumpeleka hospitalini.

    “Haitowezekana kumtibia mahali hapa. Alipoanguka, aliangukia uti wa mgongo, kwa vyovyote vile ni lazima asafirishwe na kupelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam” Dokta alimwambia.

    Siwema akaonekana kuishiwa nguvu, maneno aliyoambiwa na dokta yalionekana kumsikitisha. Hakuwa na fedha za kutosha na hata nauli tu ya kumsafirisha Getrude kwenda Dar es Salaam pamoja nae hkuwa nayo kabisa. Akajiona kuwa na uhitaji wa kupata fedha.

    “Sisi kama wafanyakazi wenzie hospitalini hapa, tutamsaidia fedha za matibabu. Cha msingi wewe tafuta fedha za nauli tu” Dokta alimwambia Siwema.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siwema akajiona kushushiwa mzigo mkubwa, ingawa hakuwa na fedha za kutosha za kukata tiketi ya treni lakini akaona ahueni. Kitu alichokifanya ni kuondoka hospitalini hapo na moja kwa moja kuelekea kazini kwake. Lengo lake kubwa lilikuwa ni kuonana na bosi wake, Bwana Mayayu ambaye kila siku alikuwa akimtaka Siwema.

    “Nitakusaidia Siwema...” Bwana Mayayu alimwambia Siwema huku akimwangalia kwa macho yaliyojaa mahaba.

    Bosi Mayayu akasimama kutoka katika kiti chake na kisha kuanza kupiga hatua za taratibu zilizojaa mapozi kumfuata Siwema, kabla hajaongea kitu chochote kile, akaupeleka mkono wake begani kwa Siwema na kuanza kumpapasa papasa Siwema.

    Siwema akaonekana kukasirika, akasimama na kumwangalia bosi Mayayu kwa macho yaliyojaa hasira. Mayayu akaachia tabasamu pana ambalo aliamini lingemlegeza kabisa Siwema. Siwema akageuka kwa lengo la kutoka ofisini mule, Bwana Mayuya akamshika mkono.

    Siwema alipogeuka, akageuka na kofi zito ambalo lilimuingia hasa Bwana Mayuya ambaye akayumba. Siwema akaufungua mlango na kutoka nje ya ofisi ile. Bwana Mayuya akaonekana kukasirika kupita kiasi, kitendo cha kupigwa kofi na mtu kama Siwema ambaye alikuwa mfanyakazi wake aliyeishi kwa kutumia fedha zake kilionekan kuwa dharau katika maisha yake.

    Akaanza kupiga hatua kumfuata secretari wake ambaye alikuwa amebaki na mshangao baada ya kumuona Siwema akiwa ametoka ofisini kwa bosi wao huku akioekana kuwa na hasira.

    “Huyu mbuzi sitaki kumuona tena akija mahali hapa.....umesikia?” Bwana Mayuya alimwambia sekretari wake.

    “Ndio bosi. Tatizo nini?”

    “Nimekwambia asije...ebo...haunielewi?”

    “Nimekuelewa” Secretari aliitikia.

    Njia nzima Siwema alikuwa akilia, hakuamini kama kule ambako alitakiwa kupata msaada ilishindikana. Alipofika nyumbani, akaanza kuelekea katika nyumba za majirani zake na kisha kuanza kuwaomba msaada wa fedha za nauli.

    Kutokana na kila mtu kujua kila kilichotokea, wakaamua kumsaidia kwa moyo mmoja. Siwema akapata kiasi cha shilingi elfu thelathini na tano ambacho alikiona kumfaa kwa kusafiri kutoa Tabora mpaka Dar es Salaam. Siwema hakutaka kuchelewa, siku iliyofuata akaanza safari kutoka Tabora kwenda Dar es Salaam.



    *************************************************





    Mawasiliano kati ya hospitali ya Nzega na Muhimbili yakafanyika kiasi ambacho wala haikuwa shida kwa Siwema. Alipofika katika stesheni ya Railways iliyokuwa jijini Dar es Salaam, gari la wagonjwa lilikuwa mahali pale likiwasubiri.

    Siwema hakuonekana kuwa na fahamu, muda wote alikuwa kimya. Siwema hakuonekana kuwa na furaha kabisa, alijiona kupitia katika kipindi kigumu sana maishani mwake. Kila wakati aipokuwa akimwangalia Getrude, sala ya kimoyo moyo ilikuwa ikiendelea moyoni mwake.

    Gari ile la wagonjwa lilifika katika hospitali ya Muhimbili baada ya dakika nne kutoka Railways. Moja kwa moja akateremshwa na kuwekwa juu ya machela ambayo ikaanza kusukumwa kuelekea katika jengo la hospitali ile.

    Huduma ya kumuhudumia Getrude ikaanza mara moja. Kila kitu kilikuwa kimefika katika ofisi ya dokta mkuu juu ya hali ambayo alikuwa nayo Siwema. Akaruhusiwa kulala hospitalini hapo mpaka katika kipindi ambacho Getrude atapata nafuu na kuruhusiwa.

    Siku ya kwanza ikapita, siku ya pili, ya tatu mpaka wiki, bado Getrude hakuwa amefumbua macho yake, alikuwa amelala katika usingizi wa kifo. Siwema bado alikuwa akiendelea kulala hospitalini pale huku dokta mkuu akitumia kiasi cha fedha katika kumnunulia chakula cha kila siku.

    “Kuna nini? Mbona mnaonekana tofauti sana leo?” Siwema aliwauliza manesi ambao walionekana kuwa haraka haraka.

    “Mmarekani amekuja. Yule Mtanzania aliyeshinda shindano la uchoraji” Nesi mmoja, Fatuma ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Siwema toka afike hapo, alimwambia.

    “Mbona mimi simfahamu” Siwema alimwambia

    “Utamuona tu”

    “Sasa nyie mnaelekea wapi?”

    “Nje. Tunakwenda kumpokea, si kila siku kumuona kwenye televisheni” Nesi Fatuma alisema na kuondoka.

    Siwema alijikuta akibaki peke yake mahali pale alipokuwa amekaa benchini. Ukimya ndani ya hospitai ile ulikuwa mkubwa huku kwa mbali kelele za watu zikiwa zinasikika kwa nje. Siwema hakutaka kutoka nje kumuona mtu huyo ambaye hadi kufikia hatua hiyo, aliona mtu huyo kuwa maarufu ambaye kila mtu alitamani kumuona na hata kumgusa.

    Siwema alibaki benchini huku akiangalia chini. Mawazo yake yalikuwa juu ya Getrude ambaye bado hakuwa na fahamu kabisa. Mara kelele zile zilizokuwa zikisikika nje zikaanza kuhamia ndani. Mtu huyo ambaye alikuwa amepokelewa na manesi pamoja na madaktari alikuwa ameingia ndani ya jengo lile. Kwa haraka haraka daktari mmoja akaanza kupiga hatua kumfuata Siwema pale alipokuwa amekaa benchini.

    “Binti. Ungekwenda kidogo hapo nje...kuna kazi inaanyika mara moja” Dokta yule alimwambia Siwema ambaye akasimama na kuanza kuondoka kuelekea kule ambako watu wale walikuwa wamepitia.

    Uso wake ulikuwa ukiangalia chini huku kwa mbali machozi yakianza kumlenga. Hakutarajiwa kama angeweza kutolewa mahali pale kwa ajili ya kumpisha mtu ambaye alikuwa ametoka nchini Marekani. Siwema akapishana na watu wale ambao walikuwa zaidi ya ishirini pamoja na waandishi wa habari.

    Siwema alikuwa akipiga hatua za haraka haraka kuelekea nje huku uso wake ukiangalia chini, hakutaka kumwangalia mtu yeyote usoni kwa wakati huo kutokana na kuonekana kwamba alikuwa akilia. Aliendelea zaidi na zaidi kupiga hatua kuelekea nje, mara akashtuka baada ya kusikia akiitwa kwa nyuma.

    “Siwema.....Siwema....Siwema...” Alisikia vilivyo akiitwa.

    Mara ya kwanza Siwema alipuuza, aliendelea kupiga hatua kuelekea nje. Bado sauti ile ilikuwa ikiendela kumuita. Siwema akapigwa na mshangao, hakujua kama kulikuwa na mtu yeyote Dar es Salaam ambaye alikuwa akimfahamu zaidi ya baadhi ya madaktari waliokuwepo hospitalini pale.

    Aliisikiliza vizuri sauti ile ambayo ilikuwa ikimuita, haikufanana na sauti ya daktari yeyote yule hospitalini pale lakini sauti ile wala haikuwa ngeni masikioni mwake, akajaribu kukumbuka mahali ambapo alikwishawahi kuisikia sauti ile. Siwema akashtuka kupita kawaida mara baada ya kuikumbuka sauti ile, mwili wake ukapigwa ganzi, kijasho chembamba kikaanza kumtoka.

    Akasimama huku kwa mbali akionekana kutetemeka kupita kawaida. Akauinua uso wake. Kila alipotaka kugeuka nyuma kumuangalia muitaji, alisita kufanya hivyo japokuwa sauti ile alionekana kuikumbuka vlivyo ingawa miaka miwili ilikuwa imepita tangu aisikia.

    “Ni mimi, Siwema. Naomba ugeuke nyuma mpenzi” Sauti ile ilisikika.

    “Patrick........” Siwema alijisemea moyoni hata kabla hajageuka na kumuangalia muitaji.





    ******





    Maisha ya Patrick yalikuwa hatarini, hakuonekana kumuaini mtu yeyote katika kipindi hicho. Kila wakati alikuwa akiishi kwa wasiwasi. Alimfahamu vilivyo muuaji yule ambaye alikuwa amefanya mauaji mengi kwa watu weusi. Alikuwa akimuogopa sana mtu huyo kuliko kitu chochote.

    Aliamini kwamba huo haukuwa mwisho wake wa kumtafuta, alijua fika kwamba ni lazima agemtafuta tena. Maisha yake yalikuwa yakfanya kila kitu mara moja moja tu mpaka pale ambapo angerudi nchini Marekani na kuwaeleza mapolisi juu ya mtu ambaye alikuwa amemteka nchini Ujerumani.

    Baadhi ya vitu ambavyo alikuwa akivifanya hakuwa akififanya mara mbili mbili. Njia ambayo alikuwa akipita wakati anaondoka basi wakati wa kurudi alikuwa akipita njia nyingine. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake siku zote, hakutaka kuyabadilisha staili ya maisha yake mpaka pale ambapo mtu yule angetiwa nguvuni.

    Gari ambalo alikuwa akilitumia katika kipindi ambacho alikuwa akiingia katika katika sehemu fulani, basi alikuwa akiondoka na gari jingine. Hayo ndio yalikuwa maisha yake kila siku, hakutaka kuyakatisha maisha yake hasa katika nchi ya kigeni.

    “Siwezi kuingia katika gari lile” Patrick alimwambia Vanessa.

    “Kwa nini?” Vanessa aliuliza.

    “Haya ndio maisha yanguniliojiwekea katika maisha yangu ya sasa. Haukumbuki nilivyokuwa nikifanya nchini Marekani Vanessa?” Patrick alimuuliza Vanessa.

    “Nakumbuka”

    “Safi sana. Hayo ndio maisha yangu. Nitaingia ndani ya gari lenu” Patrick alimwambia Vanessa.

    Kila mmoja alionekana kushangaa utaratibu ambao Patrick alikuwa amejiwekea juu ya maisha yake. Patrick pamoja na Vanessa wakaanza kupiga hatua kulifuata gari ambao alikuwa amepakizwa Vanessa katika kipindi ambacho walikuwa wameingia katika hospitali ile.

    Mara mlio wa bomu ukasikika, gari lile ambalo alitakiwa kuingia Patrick lilikuwa limelipuka. Watu wakaanza kutawanyika huku wengine wakiita jina la Patrick kwa kudhani kwamba Patrick alikuwa amelipuliwa katika lile gari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mungu wangu! Patrick! Umejuaje?”

    “Kila siku Mungu yupo pamoja nami” Patrick alimwambia Vanessa.

    Safari ya kuelekea Ikulu ikaanza mara moja ambako huko wakakaribishwa chakula cha usiku. Ilikuwa ni furaha kubwa kwa rais wa Misri Bwana Mahomoud kula chakula pamoja na Patrick ambaye alikuwa mtu maarufu sana duniani.

    Siku iliyofuata, safari ya kuelekea nchini Tanzania ikaanza. Safari ya kuelekea nchini Tanzania haikuwa katika ratiba ila iliingia ghafla baada ya Patrick kutaka iwe hivyo. Tayari akaonekana kuwa na wasiwasi mkubwa. Alitamani kwanza afike nchini Tanzania hata kabla ya kuelekea katika nchi mbili zilizobakia.

    Safari kutoka nchini Misri iliwachukua masaa manne, wakaanza kuingia katika nchi ya Tanzania. Watu wengi walikuwa wamesimama uwanja wa ndege. Ingawa taarifa zilikuwa zimefika kwa kuchelewa sana kuingia kwa Patrick nchini Tanzania lakini watu wakajitoa vilivyo, masaa sita ambayo walipewa kwa kujiandaa yalikuwa yametosha kabisa kwa wao kufika uwanja wa ndege kwa ajili ya kumpokea mtu wao, ndugu yao na mtoto wao, Patrick.

    Patrick akayapeleka macho yake chini, fuaha kubwa ikamtawala, machozi yakaanza kumtoka, hakuamini kama kweli kwa wakati huo alikuwa akitarajiwa kutua katika ardhi ya nchi ya Tanzania, nchi ambayo alikuwa amezaliwa na kukulia.

    Ndege ikatua na kuanza kutembea kwa mwendo fulani na kisha kusimama. Mlango ukafunguliwa. Patrick hakutaka kuwa wa mwisho kama ambavyo alifanya katika sehemu nyingine, alikuwa wa kwanza kufika mlangoni. Kelele za shangwe zikaanza kusikika mahali hapo, Patrick akaanza kupiga hatua kushuka ngazi huku akijifuta machozi ambayo yalikuwa yakimtoka.

    Vanessa, Matilda na Simpson ndio ambao walikuwa wamefuatia kwa nyuma. Patrick akajiona akishuka ngazi taratibu, alichokifanya ni kuanza kupiga hatua za haraka haraka mpaka alipofika chini ambako akapiga magoti chini.

    Tayari shati lake ambalo alikuwa amelivaa lilikuwa limeloanishwa na machozi ambayo yalikuwa yakimtoka. Waandishi wa habari wakaanza kumpiga picha Patrick ambaye bado alikuwa akiendelea kulia mahali pale. Baada ya muda, akasimama na kuanza kumpa mkono Mheshimiwa Peter Charles, ambaye alikuwa Waziri wa Mkuu.

    Watoto waliokuwa na maua wakafika mahali hapo na kumgawia Patrick maua ambayo walikuwa nayo mikononi. Muda wote Patrick alikuwa akionekana kuwa na furaha kupita kawaida..

    Patrick pamoja na wakina Vanessa wakaingia ndani ya gari ambalo likaanza safari ya kuelekea katika jengo la uwanja wa Taifa ambako Watanzania zaidi ya elfu themanini walikuwa wamekusanyika wakimsubiri yeye. Patrick alikuwa akipunga mikono kwa Watanzania ambao walikuwa wamekusanyika barabarani.

    Muda wote Patrick alikuwa akilia, kila alipokuwa akiliangalia jiji la Dar es Salaam alikuwa akizikumbuka siku zile ambazo alikuwa akiishi kwa Gibson.

    Safari ile ikaishia katika eneo la uwanja wa ndege. Ulinzi ulikuwa mkubwa kwa kila mtu ambaye alitaka kumgusa patrick. Patrick na wenzake wakaanza kupiga hatua kuelekea ndani ya uwanja ule. Mara baada ya kuonekana tu, uwanja mzima ukaanza kupiga kelele za shangwe.

    Patrick hakutakiwa kukaa zaidi ya dakika thelathini uwanjani hapo kitu ambacho kilimfanya kupelekwa mpaka katika jukwaa mbele kabisa na kuanza kuongea. Kitu cha kwanza ambacho alikuwa amekiongea mahali hapo ni kuhusu maisha yake.

    Alieleza kila kitu ambacho kilitokea katika maisha yake. Kila mtu mahali pale alionekana kusikitika. Historia ya Patrick ilionekana kumgusa kila aliyekuwa akiisikiliza mahali pale.

    “Wazazi wangu waliuawa kwa kuteketezwa na moto. Jambo hilo liliniuma na kila siku litaendelea kuniuma” Patrick alisema huku umati wote ukiwa umegubikwa na huzuni.





    ******





    Bi Anna hakutaka kuendelea kukaa kisiwani Madagaska hali iliyompelekea mumewe kurudi nae nchini Marekani. Muda wote Bi Anna alikuwa akionekana kuwa na huzuni, hakuamini kama mtoto wake alikuwa ameauwa katika nchi ya kigeni.

    Kila siku alikuwa na majonzi kupita kawaida, alitamani kumuona tena mtoto wake na kuongea nae tena. Kila siku maisha ya kinyonge ndio ambayo yalikuwa yakiendelea maishani mwake.Kila siku alikuwa akilia katika kipini ambacho Patrick alikuwa amesemekana kuuawa porini.

    Baada ya miezi kadhaa kupita, Bi Anna akaonekana kuwa na furaha tena mara baada ya kusikia kwamba Patrick alikuwa hai na hivyo alikuwa nchini Marekani. Kila siku ndoto zake zilikuwa ni kuonana na mtoto wake huyo ili kujua ni kitu gani ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake ya nyuma.

    Katika kipindi ambacho Patrick alianza ziara, Bi Anna akaonekana kuwa na furaha zaidi kwani aliamini kwa kitendo cha Patrick kuja barani Afrika basi ni lazima pia angefika nchini Tanzania, nchi ambayo alizaliwa na kukulia.

    Mlipuko wa Misri ulimfanya Bi Anna kuwa na wasiwasi kwa kuona kuwa maisha ya kijana wake yalikuwa matatani. Safari ya Patrick ilipotangazwa kwamba alikuwa akitarajiwa kuingia nchini Tanzania masaa machache yajayo, Bi Anna alionekana kuwa na furaha zaid kwa kuamini kwamba ni lazima angeweza kuonana na kijana wake huyo.

    Bi Anna alikuwa miongozi mwa watu ambao walikuwa wamekusanyia uwanja wa ndege wakimsubiria Patrick. Alikuwa amevalia fulana nyeupe ambayo ilikuwa na picha ya mtoto wake huyo. Kila alipokuwa akiiangalia picha ile, alifarijika kupita kiasi.

    Wakati Patrick anashusha ngazi, Bi Anna alibaki akimwangalia mtoto wake, alishindwa kabisa kujizuia, akabaki akilia tu. Kila alipokuwa akimwangalia mtoto wake, maisha ya nyuma katika kipindi ambacho alikuwa kijijini yalikuwa yakijirudia kichwani mwake kama mkanda wa filamu.

    Bi Anna alijitahidi kupenya penya kumfuata Patrick lakini alishindwa kabisa, hiyo ilitokana na wingi wa watu pamoja na mapolisi ambao walikuwa wakiwazuia watu hao. Mara baada ya kuwapungia watu mikono mahali hapo, moja kwa moja Patrick na wenzake wakaingia garini.

    Bi Anna akalifuata gari lake na kuingia. Akaanza kuufuatlia msafara ule ambao uliishia uwanja wa Taifa. Akateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika uwanja ule. Maneno yote ambayo alikuwa akiyaongea Patrick yalikuwa yakimgusa kupita kiasi. Alitamani aondoke mahali hapo na kumfuata Patrick na kumwambia kwamba hakuwa ameuawa bali alikuwa hai.

    Patrick bado alikuwa akiendelea kuongea mambo mbalimbali ambayo yalikuwa yametokea maishani mwake. Bi Anna akashindwa kuvumilia, kwa haraka haraka akatoka mahali hapo na kuufuata mlango wa kutokea nje. Akatoka na kuanza kuufuata mlango wa kuingilia katika uwanja wa kuchezea mpira kabisa ambao kulikuwa na majukwaa kadhaa.

    “Nikusaidie nini mama?” Polisi mmoja ambaye alisimama mlangoni alimuuliza Bi Anna.

    “Nataka kuongea na mwanangu”

    “Kuongea na mwanao? Mwanao yupi?” Polisi yule aliuliza huku akionekana kumshangaa Bi Anna.

    “Patrick” Bi Anna alijibu. Polisi yule hakuongea kitu chochote kile zaidi ya kuanza kucheka kwani alikwishamuona Bi Anna kuwa kama kichaa.

    Bi Anna akaonekana kukasirika, akaanza kumfuata polisi yule. Polisi akamuwahi Bi Anna kwa kumdhibiti vilivyo. Polisi mwingine akafika mahali pale, Bi Anna alikuwa pembeni huku akiendelea kumuomba polisi yule amuachie.

    “Kuna nini?”

    “Huyu mwanamke. Eti anataka kuonana na mtoto wake, Patrick” Yule polisi alimwambia.

    Maneno yale yalionekana kumshangaza kila mtu, wakamwangalia Bi Anna kwa macho ya mshangao huku akilia kwa kung’ang’ania kuongea na Patrick.

    “Haiwezekani kabisa”

    Bi Anna akaonekana kukumbuka kitu, akatoka mahali hapo na kuelekea pembeni, akachukua kipande cha karatasi pamoja na kalamu na kisha kuandika kitu fulani, akawarudia na kuwakabishi.

    “Naomba mumpe hii karatasi. Naomba mumpatie” Bi Anna aliwaambia na kuondoka mahali hapo.

    “Yule mwanamke unajua kama namkumbuka” polisi mmoja alisema.

    “Hata mimi mwenyewe namkumbuka. Nafikiri ni yule mke wa Mheshimiwa Mayemba”

    “Sawa sawa. Sasa kwa nini tumemzuia, hauoni kama inaweza kuwa tatizo hata kupoteza kazi?”

    “Inawezekana. Ila tufanye kama alivyotaka. Tumfikishie karatasi hii mhusika, Patrick”

    “Itawezekana vipi?”

    “Hata mpambe wa Waziri tutampa ili mladi tu Patrick aipate”

    “Wazo zuri”





    ********************************





    Patrick alikuwa ametulia ndani ya chumba kimoja katika hoteli ya Moven Pick. Mawazo yake katika kipindi kile yalikuwa yakimfikiria Siwema tu. Kitu alichokitaka kukifanya ni kuanza safari ya kuelekea katika kijiji cha Wami kwa ajili ya kuonanan na Siwema tu.

    Huyo ndiye amsichana ambaye alikuwa kichwani mwake, alikuwa akimpenda kuliko msichana yeyote yule. Alikuwa kila kitu katika maisha yake, hakuwa radhi kumpoteza maishani mwake. Ingawa masaa yalikuwa yamekatika lakini Patrick hakuonekana kuwa na usingizi, muda wote alikuwa akijigeuza geuza tu kitandani.

    Mara simu ya mezani kwake ikaanza kuita, akainuka na kuanza kuifuata, alipoifikia, akaunyanyua mkonga wa simu na kuupleka sikioni. Sauti ya Vanessa ilikuwa ikisikika vizuri masikioni mwake.

    “A piece of paper? (Kipande cha karatasi?)” Patrick aliuliza kwa mshangao.

    “Yeah”

    “What does it say? (Kinasemaje?)” Patrick aliuliza.

    “It is written in Swahili language, I dont know this language (Imeandikwa katika lugha ya Kiswahili, siifahamu lugha hii)” Vanessa alimwambia Patrick.

    Patrick akakata simu, akaifuata suruali yake ya jinzi, akaivaa na kuanza kuelekea katika chumba cha Vanessa. Alipoufikia mlango, akagonga na Vanessa kumfungulia.

    “Where is it? (Iko wapi?)” Patrick aliuliza.

    Vanessa akakichukua kipande kie cha karatasi na kisha kumkabidhi Patrick. Patick akakaa kitandani na kuanza kuisoma karatasi ile, ghafla kama mtu aliyechanganyikiwa akasimama juu na kuana kuruka ruka kwa furaha kama mtu ambaye alishinda Bingo.

    “My mother...my mother, Vanessa (Mama yangu....mama yangu, Vanessa)” Parick alimwambia Vanessa huku akiendelea kuruka ruka juu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “You told me she died (Uliniambia alifariki)

    “I think she didn’t, she is the one who wrote this (Nafikiri hakufariki, yeye ndiye aliyeandika hii)” Patrick alimwambia Vanessa.

    “What does a piece of paper say? (Karatasi inasemaje?)

    “I see you my son at last. You’ve grown up now. I love you more than anyone in this world. I survived from the murderers though your dad was murdered (Hatimae ninakuona kijana wangu. Umekua sasa. Ninakupenda kuliko mtu yeyote katika ulimwengu huu. Nilinusurika kutoka kwa wauaji ingawa baba yako aliuawa)” Patrick alimsomea Vanessa.

    Usingizi haukupatikana tena. Patrick alibaki chumbani kwa Vanessa wakipiga stori tu mpaka alfajiri. Wote wakaanza kujiandaa kwa ajili ya safari ya kuelekea katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuwaona wagonjwa ambao walikuwa wakisumbuliwa na magonjwa tofauti tofauti.

    Saa mbili asubuhi, magari saba yakafika mahali hapo huku gari a Waziri Mkuu, Bwana Peter Charles akiwa amefika hotelini hapo na gari lake. Moja kwa moja Patrick na Vanessa wakatoka. Wakaingia garini na moja kwa moja safari ya kuelekea katika hospitali ya Muhimbili kuanza.

    Mawazo ya Patrick kwa wakati huo yalikuwa juu ya watu wawili tu, alikuwa akimfikiria sana mama yake pamoja na Siwema, alijua fika kwamba mama yake alikuwa ndani ya jiji la Dar es Salaam. Hakujua ni kwa jinsi gani alikuwa amefika ndani ya jiji hilo na wakati hawakuwa na ndugu yeyote mahali hapo.

    Mawazo juu ya Siwema yalikuwa ni kutaka kumuona tu. Alimpenda sana binti huyo kuliko msichana yeyote yule katika dunia hii. Alihitaji kwenda kijijini Wami na kwenda kumchukua Siwema kama ambavyo alimuahidi katika kipindi ambacho alimuacha porini.

    Idadi kubwa ya wauguzi walikuwa nje, tayari walikuwa wamekwishapewa taarifa kwamba Patrick angekuwa katika hospitali hiyo muda wowote. Kelele zikaanza kusikika japokuwa walijua sheria mojawapo hospitalini hapo ilikuwa ni kutopiga kelele.

    Wananchi ambao walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kuwaona wagonjwa wao, wakaanza kumpiga picha Patrick ambaye aliteremka garini na kuungana na wenzake pamoja na waziri mkuu, Bwana Peter Charles. Wakaanza kuangalia sehemu mbalimbali katika hospitali hiyo huku Patrick akipata muda wa kuwaona wagonjwa mbalimbali na kuwafariji.

    Kila mgonjwa alijiona kufarijika, uwepo wa Patrick mbele ya macho yake ulionekana kumfariji sana. Patrick akaendelea kupiga hatua mpaka katika wodi ambayo wagonjwa waliokuwa wakiugua Upungufu wa Kinga mwilini walipokuwa.

    Patrick akajikuta akitokwa na machozi, hakuamini kama kweli katika dunia hii kulikuwa na watu waliokuwa wakiteseka namna ile. Akatumia muda wa dakika thelathini, akatoka ndani ya wodi ile huku moyo wake ukiwa umeumia kupita kiasi.

    “Kuna wodi ya watu ambao wanasumbuliwa na uti wa mgongo. Kila siku idadi ya wagonjwa hao inaonekana kuongezeka” Dokta Humphrey alimwambia Patrick.

    “Naomba mnipeleke huko, ninahitaji kuwaona pia” Patrick alimwambia Dokta Humphrey ambaye wala hakuleta pingamizi lolote lile.

    Katika kila hatua ambayo Patrick alikuwa akiendelea kuwaona wagonjwa, waandishi wa habari bado walikuwa wakiendelea kupiga picha kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea mahali hapo. Watu wote ishirini na mbili waliokuwa pamoja na Patrick wakaanza kuelekea katika wodi ambayo kulikuwa na wagonjwa waliokuwa wakisumbuliwa na uti wa mgongo.

    Binti mmoja alionekana kukaa benchini huku uso wake akiwa ameuinamisha chini. Kwa haraka haraka dokta Humphrey akaanza kumfuata binti yule, alipomfikia, akaanza kuongea nae, mara binti yule akasimama na kuanza kupiga hatua kuelekea kule Patrick, wenzake na waandishi wa habari walipokuwa.

    Mara baada ya kupishana na binti yule, Patrick akasimama. Uso wake haukuonekana kuwa wa kawaida, akageuka nyuma na kuanza kumwangalia binti yule. Kila mtu akaanza kumshangaa Patrick kutokana na kusimama kwa muda akimwangalia binti yule ambaye alikuwa amepishana nao.

    Mawazo ya Patrick yakarudi nyuma kabisa, tena kwa haraka haraka kwa kasi ambayo wala haikuwa ya kawaida. Alimfahamu Siwema vilivyo, alijua ni kwa mwendo gani binti huyo alikuwa akitembea, alijua mambo mengi kuhusu Siwema kiasi ambacho hata kama angekuwa mbali kiasi gani, basi ni lazima angejua kama ni yeye.

    “Siwema....Siwema...” Patrick alijikuta akiita.

    Hakuwa na wasiwasi hata kidogo, alikuwa na uhakika asilimia mia moja kwamba mtu ambaye alikuwa akimuita alikuwa Siwema. Siwema akasimama lakini hakugeuka nyuma hali iliyoonekana kama mtu ambaye alikuwa akijifikiria kugeuka au kutokugeuka.

    Kwa taratibu Patrick akaanza kupiga hatua kumfuata Siwema ambaye bado alikuwa amesimama. Patrick alijihisi kutetemeka huku kijasho chembamba kikimtoka. Bado alikuwa akiendelea kupiga hatua kumfuata Siwema.

    Kila mtu mahali pale alibaki akiwa amesimama huku akimwangalia Patrick ambaye bado alikuwa akipiga hatua za taratibu kumfuata Siwema. Vanessa alibaki kimya akmwangalia Patrick, jina ambalo alilisikia kutoka kwa Patrick wala halikuwa geni masikioni mwake, alikuwa na uhakika kwamba yule ndiye Siwema ambaye mara kwa mara Patrick alikuwa akipenda kumzungumzia nchini Marekani.

    “Ni mimi, Siwema. Naomba ugeuke nyuma mpenzi” Patrick aliendelea kumwambia Siwema.

    Siwema akaanza kugeuka nyuma kwa taratibu sana. Macho yake yakagongana na macho ya Patrick, Siwema akashtuka kupita kawaida, alijiona kukosa nguvu. Akabaki akiwa amesimama akimwangalia Patrick. Nae akaanza kumsogelea Patrick na wote kukumbatiana.

    Kila mmoja alikuwa akitokwa na machozi. Hakuna aliyeamini kama angemuona mwenzake mahali hapo. Walikumbatiana mpaka wote kuanguka chini huku wote wakilia kama watoto wadogo. Tukio lile likaonekana kuwa tukio kubwa, waandishi wa habari wakaanza kuwapiga picha.

    “Siamini. Hatimae nimekutana nawe” Patrick alimwambia Siwema huku wakiwa chini.

    “Nimekukumbuka mpenzi. Nimekaa kipindi chote huku nikiamini kwamba ni lazima ningekuona tena” Siwema alimwambia Patrick.

    Siku hiyo ikaonekana kuwa siku ya furaha kwa wote wawili. Kila wakati walikuwa na furaha. Patrick hakujali kama muonekano wa Siwema ulikuwa si mzuri hasa kutembea pamoja nae, kitu ambacho alikuwa akikifurahia ni kukutana na Siwema mahali hapo.

    Muda wote alikuwa akiuzunguusha mkono wake mabegani mwa Siwema. Alijisikia furaha sana kukutana na msichana ambaye alikuwa akimkumbuka siku zote. Akayaona maisha yake yakianza kutawaliwa na furaha katika kipindi hicho.

    Mara baada ya kumaliza kuwaona wagonjwa, Patrick hakutaka kupoteza muda, wakapanda ndege na kuanza safari ya kuelekea Shinyanga. Taarifa ya habari ikatangazwa kwamba Patrick alikuwa njiani kuelekea mkoani Shinyanga.

    Ingawa habari ile ilikuwa ni ya kushtukiza lakini watu waliokuwa wakiishi mkoani Shinyanga wakakusanyika katika uwanja wa ndege wakiisubiria ndege hiyo. Saa nane kasoro kumi na mbili, ndege ile ikaanza kutua katika uwanja wa ndege wa mkoani Shinyanga.

    Ndege ikatua na Patick kuanza kuteremka huku akiwa amemshika Siwema mkono. Watu wakaanza kupiga kelele za shangwe katika kipindi ambacho Patrick alikuwa akishuka ngazi. Vigelegele vikaanza kusikika, wakinamama wakaanza kuimba nyimbo za lugha yao.

    Patrick akaanza kutembea kumfuata mkuu wa mkoa, Bwana Wambura. Wote wakasalimiana na kisha kuwapungia mkono wananchi ambao walikuwa wamkusanyika uwanjani hapo na kisha kuanza kuongea nao kama mtu aliyekuwa akiuhutubia mkutano.

    Patrick alitumia dakika tano kuongea na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga ambao walikuwa wamefika mahali hapo na kisha kuingia garini na safari ya kuelekea katika kijiji chao cha Chibe kuanza. Safari ilichukua dakika arobaini na tano, wakaanza kuingia katika kijiji hicho.

    Wote wakateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea kule nyumba ya mwenyekiti wa kijiji, Bwana Msumari. Kila mtu kijijini alikuwa akiwashangaa wazungu wale ambao walikuwa wametangulizana na mkuu wa mkoa pamoja na Patrick.

    Patrick alionekana kuwa tofauti na kipindi ambacho alikuwa nyuma, alionekana kubadilika katika kila kitu. Mara baada ya mwendo mdogo, wakafika katika eneo la nyumba ya mwenyekiti wa kijiji huku watu wakiwa wanawafuatilia kwa nyuma.

    Bwana Msumari akaitwa, alipotoka, macho yake yakatua kwa wazungu ambao walikuwa mbele yake. Akaonekana kushtuka, akaanza kujiuliza maswali mengi kuhusu wazungu wale, mara alipmuona Patrick, moyo wake ukatulia.

    “Karibu Patrick” Bwana Msumari alimkaribisha Patrick.

    “Asante” Patick aliitikia huku akiachia tabasamu pana.

    Wakaongea mambo mengi mahali hapo na kisha wote kuanza kupiga hatua kuelekea kule katika nyumba ambayo Patrick alikuwa akiish na wazazi wake. Moyo wake ukaanza kumuuma na kumkumbusaha mambo ya nyuma ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yake.

    Nyumba ilikuwa imeteketezwa kwa moto na wala hakukuwa na kitu chochote ambacho kilikuwa kimebakia. Eneo la nyumba ile ikaonekana kujaa majani. Patrick aliumia zaidi mara baada ya kupaangalia sehemu ambayo baba yake, mzee Christopher alipokuwa amelazwa na kushambuliwa.

    Patick akaingia ndani, machozi yalikuwa yakimtoka kama mtoto mdogo. Moyo wake uliendelea kumuuma zaidi, kila alipokuwa akiyaangalia maisha yake ambayo alikuwa akiyaishi zamani na yale aliyokuwa akiyaishi katika kipindi hiki, aliona utofauti mkubwa sana.

    “Kaburi la baba yangu liko wapi?” Patick aliuliza.

    “Nifuate” Bwana Msumari alimwambia Patrick na kisha kuanza kumfuata.

    Safari yao ikaishia nyuma ya nyumba ile. Patrick akaanza kuangalia katika sehemu ile, sehemu ambayo ilionekana kufukiwa kitu ilikuwa ikionekana vizuri machoni mwake.

    “Hili ni kaburi la baba yako. Nilimzika peke yangu baada ya wanakijiji wote kukataa kumzika” Bwana Msumari alimwambia Patrick ambaye machozi yakaongezeka zaidi.

    “Nitakichukia kijiji hiki katika maisha yangu yote” Patrick alimwambia Bwana Msumari huku akionekana kuwa na hasira.

    “Usifanye hivyo mpenzi. Haitosaidia” Siwema alimwambia Patrick.

    “Inaniuma Siwema. Moyo wangu unaniuma. Baba yangu niliyekuwa nampenda kwa moyo wote, amezikwa kama mnyama” Patrick alimwambia Siwema huku akiendelea kuwa na hasira.

    “Kumbuka kuwa hiki ni kijiji chako na kila siku kitaendelea kuwa kiji chako. Haitosaidi kama utaendeleza chuki kwao” Siwema alimwambia Patick.

    “Lak...”

    “Usiseme hivyo mpenzi. Naomba uwasamehe” Siwema alimwambia Patrick.

    “Nimekuelewa”

    Patrick hakutaka kuendelea kukaa kijijini hapo. Alichokifanya ni kuchangia mfuko wa kijiji kwa kutoa shilingi milioni tano na kumpati Bwana Msumari kiasi cha shilingi miioni moja kama shukrani kwake na kisha safari ya kuelekea katika kijiji cha Wami kuanza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waliingia katika kijiji cha Wami baada ya dakika thelathini. Watu wote ambao walikuwa wakimuona Siwema walikuwa wameshtuka kupita kiasi. Siwema alionekana kuwa tofauti na Siwema yule ambaye alitoroka kijijini pale. Mavazi aliyokuwa ameyavaa, nywele zake alivyokuwa amezitengeneza zilionekana kumpendezesha sana.

    Mara baada ya kumuona mama yake ambaye alikuwa nje ya nyumba yao, Siwema akaanza kumkimbilia na kumkumbatia kwa furaha. Wote walikuwa wakilia kwa furaha. Mzee Abdallah akatoka ndani na kuja mahali hapo. Macho yake yakatua kwa binti yake, Siwema, uso wake ukaonyesha tabasamu pana.

    “Shikamoo baba”

    “Marahaba binti yangu”

    Wote wakakaa chini na kuanza kuongea mambo mengi. Patrick na Siwema wakatumia muda huo kuelezea historia za maisha yaliyotokea katika maisha yao. Kila mmoja alibaki akistaajabu. Patric alionekana kuwa na bahati kupita kawaida.

    “Nimeona ni bora kuja kuomba ruhusa kwenu. Ninahitaji kukaa na binti yenu hata kabla sijamuoa” patrick aliwaambia.

    “Hilo hakuna tatizo. Sisi kama wazazi tunakuruhusu kwa moyo mmoja” Mzee Abdallah alimwambia Patrick hali iliyowafanya kufurahia.

    Walikaaa kwa takribani masaa matat na ndipo wakaondoka na moja kwa moja kupanda ndege. Safari iliyofuata ilikuwa ni kuelekea jijini Mwanza. Lengo lake kubwa lilikuwa ni kwenda katika kisiwa cha Ukerewe ili kuwaona watu ambao alikuwa amewaacha mahali huko.

    Kama kawaida, taarifa ikatangazwa na watu wengi kukusanyika uwanja wa ndege. Patrick akaanza kuteremka kutoka katika ndege huku Siwema akiwa pembeni yake. Akawapungia miko watu waliokuwa mahali hapo na kisha kusalmiana na mkuu wa mkoa huo, Bwana Yusuph Kandoro na kisha kuanza kuelekea pembezoni mwa ziwa Viktoria ambapo boti nzuri ikaandaliwa na kisha kuanza kuelekea kisiwani Ukerewe.

    Kutokana na mwendo wa boti ile kuwa mkubwa, ni ndani ya dakika kumi tu wakawa wamekwishafika. Wote wakateremka na kuanza kuelekea kule kulipokuwa na nyumba kadhaa za wavuvi.

    “Mungu wangu! Patrick!” Fikiri alisema mara baada ya kumuona Patrick.

    Wote wakaanza kumkimbilia na kukumbatiana. Kila mmoja akaonekana kuwa na furaha. Mzee Mshana akatokea mahali hapo, Patrick akamsalimia na kisha kukaa mahali hapo kwa dakika kadhaa huku akiwasimulia kila kitu kilichotokea katika maisha yake mara baada ya kutoroka na mtumbwi wao.

    “Kweli Mungu alikuwa pamoja nawe” Fikiri alimwambia Patrick.

    Patrick hakutaka kuondoka mahali hapo hivi hivi. Alichokifanya ni kuwaachia milioni saba kama shukrani zake kwao na kuwaaahidi kuwanunulia mitumbwi ya kisasa ya uvuaji pamoja na boti ambayo itawasaidi kuwasafirisha kutoka Ukerewe mpaka Mwanza mjini na fedha ambazo zingepatikana basi zingeyaendesha maisha yao.

    “Ni msaada mkubwa sana ambao wala hatukuutarajia maishani mwetu. Tunashukuru sana” Bwana Mshana alimwambia Patrick.

    “Msijali. Ninafanya hivi kwa kuwa mlinionyeshea moyo wa kunijali. Ndani ya wiki moja, kila nilichokiahidi kitakuwa kimewafikia” Patrick aliwaambia.

    Patrick akaagana nao na kupanda boti na kisha kuelekea Mwanza mjini. Alionekana kuchoka sana lakini akataka kumaliza kila kitu kwa wakati huo ili hata kama angerudi Dar es Salaam basi kazi ingekuwa ni kumtafuta mama yake tu.

    Watu walikuwa wamekusanyika pembezoni mwa ziwa Viktoria wakimsubiri Patrick. Kila mtu alikuwa akitaka kumuona Patrick ambaye alikuwa akitangazwa sana na vyombo vya habari. Patrick na wenzake wakateremka kutoka mtumbwini na kisha kuanza kuongea na watu waliokusanyika mahali hapo.

    “Patrick...Patrick...Patrick...” Sauti ilisikika ikiita.

    Ingawa Patrick alikuwa akiitwa na watu wengi tofauti mahali hapo lakini sauti hii ilionekana kuwa si ngeni masikioni mwake. Akageuka na kuanza kuangalia angalia ni nani ambaye alikuwa amemuita mahali hapo. Macho yake yakatua kwa mtu ambaye nae alikuwa muhimu katika maisha yake, katika siku zote alikuwa akifikiri kwamba mtu huyu alikuwa amefariki dunia, Azizi.

    Patrick akaanza kumfuata Azizi huku akionekana kuchanganyikiwa kwa furaha, alipomfikia, akamkumbatia. Kila mtu akamuona Azizi kuwa na bahati ya kukumbatiana na Patrick. Wote walikuwa wakilia kwa furaha, hawakuamini kama kweli wangeweza kukutana.

    “Ni wewe Azizi?” Patrick aliuliza.

    “Ni mimi...ni mimi...” Azizi alimwambia Patrick.

    “Kumbe haukufa ziwani! Au hawakukutosa majini?”

    “Walinitosa. Nilipoteza fahamu. Niliokolewa na wavuvi kutoka nchini Uganda. Kipindi chote nilikuwa nikiishi Uganda. Niliposikia kuhusu wewe, nikapanga kuja kukuona. Hivi hapa unaponiona nilikuwa na safari ya kuelekea Dar es Salaam kutaka kuonana na wewe tu” Azizi alimwambia Patrick.

    Ni lazima tuondoke Patrick. Siwezi kukuacha peke yako, ni lazima niwe pamoja nawe tena. Ni lazima uishi nami nchini Marekani” Patrick alimwambia Azizi.

    “Haitowezekana Patrick. Nina mchumba ambaye ni mjauzito. Ni lazima nikae nae na kumtunza” Azizi alimwambia Patrick.

    “Utamtunzi nchini Marekani. Wewe ni rafiki yangu. Sitokuwa tayari kukuacha uendelee kuishi huku. Sitaki upate shida yoyote ile” Patick alimwambia Azizi.

    “Sawa. Tutakwenda lakini kwanza ni lazima niende nikamchukue nchini Uganda” Azizi alimwambia Patrick.

    “Panda ndege. Nenda kamchukue na kisha uje nae Dar es Salaam. Sitoweza kuondoka bila wewe” Patrick alimwambia Azizi

    “Kupanda ndege! Sina nauliza Patrick”

    “Hilo si tatizo. Kila kitu nitagharamia mimi” Patrick alimwambia Azizi.







    ****





    Ndege ilikuwa ikitua katika ardhi ya jiji la Dar es Salaam. Patrick akaanza kuteremka na kisha kuanza kuyafuata magari yaliyokuwa mahali pale huku akiwa na wenzake. Muda ulikuwa umekwenda sana na hakutakiwa kwenda sehemu yoyote ile zaidi ya kwenda Ikulu ambako huko chakula cha usiku kilikuwa kimeandaliwa.

    Alihitajika kwenda kula pamoja na viongozi kadhaa wa nchi hii akiwepo raisi na mawaziri wote. Mara baada ya gari kusimama katika eneo la Ikulu, wote wakateremka na kuanza kuelekea sehemu iliyokuwa na viti na kutulia.

    “Patrick...” Patrick alisikia akiitwa.

    Akageuka nyuma, macho yake yakagongana na macho ya mama yake. Katika hali iliyoonyesha kuchanganyikiwa, akasimama na kuanza kumsogelea mama yake, Bi Anna na kumkumbatia. Wote walikuwa wakilia, familia ikaonekana kuungana mara bada ya mtawanyiko wa muda mrefu maishani mwao.

    “Siamni kama ningekutana nawe mwanangu” Bi Anna alimwambia Patrick.

    “Umekua mwanangu. Umekua” Bi Anna alimwambia Patrick na kumkumbatia tena.

    Patrick akasimama na kuwaeleza watu kwamba yule ndiye ambaye alikuwa mama yake. Kutokana na kuwaelezea kabla historia ya maisha yake, kila mmoja alimtambua.

    “Nimeolewa Patrick. Yule pale ni baba yako” Bi Anna alimwambia Patrick huku akimuonyeshea Bwana Mayemba. Patrick akamsogelea, akamsalimia na kumkumbatia.





    *****







    Patrick akajisikia kuwa na amani. Staili ya maisha yake ya kubadilisha magari kila anapokwenda, haikutokea nchini Tanzania kwani aliona hata kama angeuawa nchini Tanzania, ilikuwa ni sawa kwani angeuawa ndani ya nchi yake mwenyewe.

    “Tunakwenda kuanza maisha mapya Marekani” Patrick alimwambia Siwema huku akionekana kuwa na furaha.

    “Sitoweza kwenda huko mpaka utakaponifanyia kitu kimoja” Siwema alimwambia Patrick.

    “Kitu gani mpenzi?”

    “Nataka usafirishe dada yangu akatibiwe huko. Sitaki kumpoteza katika maisha yangu. Yeye ni muhimu, kila siku nilikuwa nae akinilinda na kunilea kama mama yangu” Siwema alimwambia Patrick.

    “Dada yupi?”

    “Getrude ambaye nilikuwa nikiishi nae mkoani Tabora”

    “Usijali. Ni hilo tu au kuna jingine?”

    “Ni hilo tu”

    “Tutaondoka nae. Ila ninyi inabidi mtangulie. Ninamsubiri Azizi, mfanyiwe mambo yote kuhusu hati za kusafiria, baada ya hapo mtaondoka, nami nitawakuta huko” Patrick alimwambia Siwema.

    “Kwa nini hautaki kwenda nasi?”

    “Si kwamba sitaki. Ila kuna nchi mbili zimebakia kwenda kuzitembelea kama balozi. Naanza nchini Namibia kisha Zimbabwe. Nitakapomaliza, nitakuja kuendelea kuishi nawe mpenzi” Patrick alimwambia Siwema.

    “Utachukua muda gani?”

    “Siku tano”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sawa”

    Kila kitu ambacho kilikuwa kimepangwa ndicho ambacho kilikuwa kimetokea. Mara baada ya hati za kusafiria kupatikana, Siwema, Azizi, Getrude na mchumba wa Azizi, Mariamu wakasafiri kuelekea nchini Marekani. Getrude akapelekwa katika hospitali kubwa jijini New York na kisha kuanza kupatiwa matibabu.

    Patrick hakutakiwa kuishi kwa wasiwasi tena kwani tayari aliwaambia mapolisi kwamba Bwana Khan ndiye ambae alikuwa akihusika na mauaji yote ya watu waliokuwa na ngozi nyeusi nchini Ujerumani. Hukumu ya kifo ikatolewa na mzee huyo kuuliwa kwa kuchomwa sindano iliyokuwa na sumu kali.

    Ilichukua miaka mitano Patrick na Azizi wakaoa pamoja katika kanisa la kilutheri nchini Marekani huku Azizi na mkewe wakiwa wamebadilisha dini zao na kuwa wakristo. Maisha mapya kama familia yakaanza nchini Marekani.

    Azizi akatafutiwa kazi nzuri ambayo ilikuwa ikimuingizia kiasi kikubwa cha fedha ambazo akaaanzisha miladi mingi na baada ya miaka miwili akawa akimiliki televisheni zake mbili zlizokuwa zikirusha vipindi vyake nchini Marekani.

    Bado Patrick alikuwa akiendelea kuingiza fedha kila siku katika maisha yake. Kamwe hakumsahau mama yake ambaye mara kwa mara alikuwa akielekea nchini Marekani. Patick akaingia katika orodha ya matajiri mia moja ambao walikuwa wakimiliki kiasi kikubwa cha fedha.

    Miladi mbalimbali ambayo alikuwa ameianzisha ndio ambayo ilikuwa ikiendelea kumuingizia fedha kiasi ambacho alikuwa akimiliki ndege, boti kubwa, magari ya kifahari pamoja na vitu vingine vingi. Baada ya miaka miwili, akainunua klabu ya mpira wa kikapu ya Chicago Bulls na kumnunua mchezaji mdogo, Michael Jordan ambaye baadae akaja kuwa mchezaji mahili katika klabu hiyo.

    Getrude hakutakiwa kurudi nchini Tanzania, alitakiwa kuanza maisha yake nchini Marekani huku akipelekwa katika chuo kimojawapo kusomea uuguzi ambako baada ya mwaka, akawa dokta katika hospitali ya jijini Los Angels.

    Miaka miwili ikapita, Siwema akajifungua watoto mapacha ambao majina yao yalikuwa Octavia na Octaviana. Patrick na mkewe, Siwema walikuwa wakiishi maisha ya furaha, kila kitu ambacho kilipita katika maisha yao, walikichukulia kuwa kama historia.





    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog