IMEANDIKWA NA : NYEMO CHILONGANI
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ukali wa jua tayari ulikuwa umeanza kupungua katika kipindi hicho cha jioni. Njia ambazo hazikuwa na wapitaji wengi katika kipindi cha mchana, katika kipindi hicho zikaanza kujaa watu wengi kutoka na ukali wa jua kupungua kwa asilimia kubwa. Vijana ambao walikuwa wakisubiria jua lianze kuzama na kisha kuendelea na shughuli zao tayari walikuwa wamekwishaanza kufanya shughuli hizo.
Watu walikuwa wakiendelea na pilikapilika zao za hapa na pale huku watu wengine wakitembea kwa mwendo wa haraka kuelekea majumbani kwao kutokana na mihangaiko ya hapa na pale ambayo walikuwa wameifanya katika kipindi kirefu cha mchana wa siku hiyo. Maustadhi ambao walikuwa na vyeo vya Uimamu nao hawakuwa mbali, walikuwa wakijiandaa kwa ajili ya kwenda kutoa adhana kwa ajili ya kuwakumbusha watu kwamba walikuwa wakihitajika katika misikiti ya ibada kwa ajili ya kumuabudu Allah.
Katika kipindi hiki cha jioni ambacho kilihitajika kuwa na utulivu mkubwa ndio kikawa kipindi ambacho mwanamke mmoja, Bi Agnes alikuwa akigonga kwa fujo ndani ya nyumba moja kubwa ya kifahari. Ugongaji ambao alikuwa akiutumia Bi Agnes katika ugongaji wa mlango ule haukuonekana kuwa na amani hata kidogo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bi Agnes hakuwa peke yake mahali hapo, alikuwa amekuja na kijana wake ambaye alikuwa akimpenda sana na kumthamini, Kelvin. Sekunde ziliendelea zaidi na zaidi lakini wala hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuja kuufungua mlango. Bi Agnes hakuacha, aliendelea kugonga zaidi na zaidi na hatimae mlango kufunguliwa na Brian, kijana ambaye alikuwa akiishi ndani ya nyumba hiyo.
“Karibuni” Brian aliwakaribisha huku Bi Agnes akionekana kuwa katika uso uliokuwa na hasira.
“Huyu malaya yupo?” Lilikuwa swali la kwanza ambalo Bi Agnes alimuuliza Brian hata kabla ya salamu.
“Malaya! Nani?” Brian aliuliza huku akionekana kushtuka.
“Nimeuliza huyo malaya Albertina yupo?” Bi Agnes aliuliza huku akionekana kukasirika zaidi.
Sauti yake ya juu na ya ukali ndio ambayo iliwafanya mzee Rutaba na mkewe, Bi Janeth kufika mahali hapo. Bi Agnes alipowaona tu, maneno yake yaliyojaa matusi yakaongezeka zaidi na zaidi jambo ambalo lilimfanya kila mmoja kumshangaa. Bi Agnes hakuonekana kujishtukia, uso wake haukuwa hata na chembe ya aibu, bado alikuwa akiendelea kuropoka zaidi na zaidi huku wote wakiwa wamekaa kimya.
Wala hazikupita sekunde nyingi, Albertina akatokea mlangoni hapo huku macho yake yakiwa mekundu kama mtu ambaye alikuwa ametoka kulia kipindi kichache kilichopita. Mara baada ya Bi Agnes kumuona Albertina, matusi yake yakaongezeka zaidi na zaidi.
“Kuanzia leo wewe malaya nikikuona katika nyumba yangu, nitakuua” Bi Agnes alimwambia Albertina ambaye alikuwa kimya tu mahali pale.
Kelvin hakuongea kitu, muda wote uso wake alikuwa ameuinamisha chini. Mama yake, Bi Agnes alikuwa akiendelea kuongea maneno mengi, Kelvin alikuwa akijisikia aibu moyoni mwake jambo ambalo alitamani sana kuondoka mahali hapo.
“Kwanza hebu jiangalie jinsi ulivyo halafu mwangale mtoto wangu Kelvin, hivi una hadhi ya kutembea na mwanaume kama huyu? Msichana mwenyewe mbaya utafikiri katuni gani sijui. Yaani kuanzia leo hii sitaki uje nyumbani kwangu na wala sitaki umpigie simu mtoto wangu na kumsumbuasumbua” Bi Agnes alisema huku akionekana kuwa na hasira zaidi.
Bi Agnes ndiye ambaye alikuwa akiongea mahali hapo, hakukuwa na mtu ambaye alithubutu kumnyamazisha, aliongea kiasi ambacho ilionekana kama alikuwa amewekewa mota mdomoni. Albertina akashindwa kuvumilia, machozi yakaanza kutiririka mashavuni mwake. Moyoni aliumia kupita kawaida, jina la ‘malaya’ ambalo alikuwa ameitwa mahali hapo lilionekana kumuumiza kupita kawaida.
Kelvin hakutakiwa kuongea kitu chochote kile kwa sababu tayari makubaliano yalikuwa yamekubaliwa toka nyumbani. Bi Agnes aliongea kwa nguvu zote, mpaka katika kipindi ambacho aliamua kukaa kimya, tayari zilikuwa zimepita zaidi ya dakika tano. Alipoona amemaliza, akamshika mkono mtoto wake, Kelvin na kisha kuondoka mahali hapo.
Hali ilionekana kuwa kama msiba kwa Albertina, alilia kwa maumivu makali moyoni mwake. Hakuamini kama mwanamke yule ambaye alitarajia kumuita mkwe ndiye ambaye alikuwa ametoka mahali hapo na kuongea maneno mengi ambayo yalijaa kejeli na matusi katika maisha yake. Moja kwa moja Albertina akaelekea chumbani kwake na kisha kujilaza kitadani.
Mito juu ya kitanda chake ilionekana kuwa michache, alikuwa akilia sana huku akiwa ameikumbatia. Mama yake, Bi Janeth akaingia chumbani humo na kisha kuanza kumbembeleza Albertina. Hali haikuwa rahisi kwa Albertina kunyamaza, alikuwa akiendelea kulia kwa maumivu makali moyoni mwake.
Moyo wake bado ulikuwa ukimpenda sana Kelvin ambaye alionekana dhahiri kuyafuata maamuzi ya mama yake, Bi Agnes. Kwa kadri Bi Janeth alivyokuwa akizidi kumbembeleza Albertina na ndivyo ambavyo alivyozidi kulia zaidi na zaidi. Maumivu ndani ya moyo wake yalikuwa ni zaidi ya kuchomwa na msumali wa moto.
Dakika ziliendelea kwenda mbele lakini Albertina hakutaka kunyamaza kabisa kitendo ambacho kilimpelekea baba yake, mzee Rutaba kuingia ndani ya chumba kile. Wala hazikupita sekunde nyingi nae Brian akaingia chumbani pale na wote kuaza kumbembeleza Albertin ambaye alikuwa akilia kama mtoto huku akiwa katika maumivu makali.
Siku hiyo ndio ilikuwa siku ya huzuni kuliko siku zote katika maisha ya Albertina, siku hiyo ndio ilikuwa siku ambayo ilikuja kukaa katika kichwa cha Albertina. Maumivu ambayo aliyapata katika siku hiyo yalikuwa ni makubwa sana ambayo hayakuwa na mfano.
Siku ya kwanza ikapita, wiki ikafika na kutokomea, mwezi ukaingia, mawasiliano kati yake na Kelvin hayakuwepo tena. Albertina akashindwa kuvumilia kabisa, hali ambayo alikuwa akiishi nayo ilikuwa ikimuumiza. Hapo ndipo ambapo akaanza kumpigia simu Kelvin. Simu haikuwa ikipatikana kabisa, alijaribu kupiga kila siku lakini hali ilikuwa ile ile, ilionyesha kwamba Kelvin alikuwa amebadilisha namba yake ya simu.
Mawazo yakaonekana kumtesa sana Albertina ambaye alionekana kuwa kama chizi. Akili yake ikaonekana kuanza kuchanganyikiwa, muda mwingi alikuwa akiongea peke yake. Mapenzi ambayo alikuwa akiyatumia kumpenda Kelvin yalikuwa makubwa sana, mapezi hayo hayo kwa sasa ndio ambayo yalionekana kutaka kumpa uchizi maishani mwake.
Baada ya miezi sita kupita, kidogo Albertina akaonekana kurudi katika hali yake. Mawazo juu ya Kelvin yakaonekana kuanza kupungua na si kama siku za kwanza. Hapo ndipo ambapo akaamua kuyasahau mapenzi, hakutaka tena kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi. Katika kila hatua za mahusiano ya kimapenzi ambazo alizipitia aliona kwamba aliteleza mara moja. Kwa sasa hivi alijiona kuinuka na kuendelea na safari yake ya kusonga mbele. Hakutaka kukumbuka kitu chochote juu ya Kelvin japokuwa hali ilikuwa ngumu sana. Katika kila hatua ambayo alipita pamoja na Kelvin, katika kila kitu ambacho alikifanya pamoja na Kelvin kikaonekana kuwa kama historia ambayo milele isingeweza kujirudia tena.
“Sitopenda…..sitopenda na sipendi tena mapenzi” Albertina alimwambia mama yake huku akionekana kumaanisha yale ambayo alikuwa akiyaongea.
“Usiseme hivyo Tina”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Haiwezekani mama. Mapenzi hayanipendi kabisa. Hebu kumbuka ni siku ngapi zimepita tangu Kelvin anivishe pete ya uchumba? Amenisaliti, Kelvin amenisaliti kwa kuniona mimi sifai. Hanitaki tena, simpendi tena Kelvin na wala siyapendi tena mapenzi” Albertina alimwambia mama yake, Bi Janeth.
Huo ndio uamuzi ambao aliuchukua Albertina, hakutaka tena kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi tena. Miezi ikaendelea kukatika mpaka mwaka mzima kupita, bado Albertina alikuwa katika msimamo wake ule ule wa kutotaka kujiingiza tena katika mahusiano ya kimapenzi.
Moyoni alidhamiria sana kutokuingia katika mahusiano ya kimapenzi, ila mbaya zaidi hakuwa na uwezo wa kujua maisha ya baadae yangekuwa vipi, hakujua kama kulikuwa na kitu kigeni ambacho kingeweza kutokea baadae, kitu ambacho kingeyabadilisha maisha yake na uamuzi ambao alikuwa amejiwekea maishani mwake. Kitu ambacho kingekuwa vigumu sana kuepukika hasa kwa msichana wa Kitanzania kama yeye.
*****
Uhusiano kati ya Kelvin na Albertina ulikuwa mkubwa sana kiasi ambacho kila mtu alikuwa akiona mafanikio makubwa ya mahusiano yao katika siku za mbele. Mara kwa mara walikuwa pamoja wakifurahia maisha ya uhusiano wao ambao kila siku ulikuwa ukizidi kwenda mbele. Uhusiano huo ndio ambao ulipelekea wawili hao kutambulishana kwa wazazi wao.
Pande zote mbili walionekana kuwa na furaha kupita kawaida juu ya uhusino huo ambao ulionekana kutokuwa na tamati mpaka pale ambapo wangeamua kuoana na kuwa pamoja. Siku ziliendelea kwenda mbele mpaka pale ambapo msichana Lucy alipokuja kujitokeza katikati yao na kuwa kidudumtu.
Lucy alionekana kuwa balaa katika uhusiano huo katika kipindi ambacho alikuwa ametoka nchini Australia kusoma. Lucy akaonekana kuanza kuangukia kwenye mapenzi ya Kelvin na hivyo kuanza kufanya harakati kwa haraka sana. Kitu alichokifanya kwa wakati huo ni kuongea na Bi Agnes ambaye akamuahidi kila kitu kumuwekea sawa.
Kitu ambacho alikuwa akikifikiria Bi Agnes kwa wakati huo kilikuwa fedha, katika kipindi hicho ambacho Lucy alikuwa amerudi kutoka nchini Australia, alikuwa amepata kiasi kikubwa cha fedha kwa sababu huko alikuwa akifanya kazi. Pamoja na fedha pia kulikuwa na kitu ambacho kilikuwa kinaendelea. Bi Agnes alikuwa rafiki mkubwa sana na mama yake Lucy, Bi Stella huku ukaribu huo ukisababishwa na biashara ya vitenge ambayo walikuwa wakiifanya pamoja kwa kuchukua vitenge kutoka nchini Kongo na kuvileta nchini Tanzania.
Hizo ndizo zilikuwa sababu kubwa ambazo zilimfanya Bi Agnes kumfanyia mipango Lucy kuwa na uhusiano pamoja na Kelvin. Kwa mara ya kwanza halikuwa jambo rahisi kutokea, Kelvin alionekana kuwa na mapenzi ya dhati kwa Albertina lakini kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo ushawishi mkubwa ukaendelea kufanyika na baada ya wiki mbili Kelvin akaanza kulegeza kamba.
Kitendo cha Lucy kufika ndani ya nyumba ile mara kwa mara na kuongea sana na Kelvin kilionekana kuwa chachu kubwa kwake kufanikiwa kuzikamata hisia za Kelvin. Pamoja na kufanya mambo mengi kama sababu za kuchochoea kwa Kelvin kuachana na Albertina, Bi Agnes alikuwa ametoa mikwara mingi na mizito kwamba kama Kelvin angeendelea kuwa na msichana huo basi asingemuhesabia kama alikuwa mtoto wake.
Ingawa Bi Agnes aliongea maneno ya kirahisi sana lakini ndani ya moyo wa Kelvin yalikuwa ni maneno mazito sana kwa sababu mzazi ambaye alikuwa amebaki nae duniani alikuwa ni Bi Agnes tu. Kwa kuhofia kumwagiwa radhi au kulaaniwa na mama yake, hatua aliyoichukua ni kuanza kufanya harakati za kuachana na Albertina.
Kitu alichoanza nacho kukifanya Kelvin kilikuwa ni kutotaka kuwasiliana na Albertina, kila alipokuwa akipigiwa simu na msichana huyo, Kelvin alikuwa akiikata simu na alipoona kwamba anazidi kupiga simu, alikuwa akiikata.
Bi Agnes hakuonekana kumuamini mtoto wake jambo ambalo likamfanya kumshawishi kwenda nyumbani alipokaa anakaa Albertina na kisha kumwambia ukweli ili asimsumbue tena. Ingawa hiyo ilikuwa ngumu kuingilika akilini mwake lakini mwisho wa siku Thoma akajikuta akikubaliana nae na hivyo kupanga siku ya kwenda huko.
“Nimefanikiwa kumlaghai. Nilikwambia kwamba kila kitu niachie mimi” Bi Agnes alimwambia Lucy simuni.
“Mmmh! Siamini! Kweli umefanikiwa?”
“Ndio hivyo. Mimi ndiye mzazi bwana. Mzazi atabaki kuwa mzazi milele” Bi Agnes alisema.
Siku iliyofuata ndio safari ya kuelekea huko ikaanza na yale yote kutokea huku wakimuachana Albertina kuwa katika maumivu makali moyoni mwake.
*****
“Kuna rafiki yangu atakuja kutoka Marekani wiki ijayo” Brian aliwaambia wazazi wake, mzee Rutaba na Bi Janeth.
“Ndiye nani huyo?” Mzee Rutaba aliuliza.
“Anaitwa Alan. Huyu alikuwa rafiki yangu toka tulipokuwa tukisoma chuo cha Mississippi pale nchini Marekani.
“Sawa. Tunamkaribisha” Mzee Rutaba alisema.
Muda mwingi Brian alionekana kuwa na furaha, mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na Alan simuni jambo ambalo lilimfanya kumtia hamasa ya mtu huyo kufika nchini Tanzania na kuangalia vivutio vingi kama mbuga za wanyama, mlima mzuri wa Kilimanjaro pamoja na mambo mengine mengi.
Wiki moja ilipokatika, Alan akafika nchini Tanzania na kuchukua chumba katika hoteli ya Serena iliyokuwa jijini Dar es Salaam. Brian alikuwa na furaha kupita kawaida, kilikuwa kimepita kipindi cha mwaka mzima pasipo kumiona rafiki yake huyo ambaye alionekana kuwa rafiki yake wa karibu kuliko marafiki wote ambao alikuwa nao chuoni Mississippi nchi Marekani.
Mara baada ya kukaa siku moja hotelini, alichokifanya Brian ni kwenda huko na kisha kumchukua na kumpeleka nyumbani kwao. Muda wote Brian alionekana kuwa na furaha, kuwa karibu na rafiki yake katika kipindi hicho kulimfurahisha kupita kawaida.
“Nice to see you guys (Nimefurahi kuwaona)” Alan aliwaambia Mzee Rutaba na Bi Janeth.
Siku hiyo ilikuwa siku ya furaha sana, katika kipindi chote hicho Albertina alikuwa jikoni akiandaa chakula pamoja na mama yake huku Albertina akiwa hajaonana na mgeni huyo ambaye alifika ndani ya nyumba hiyo. Stori zikaanza mahali hapo, walikumbushiana mambo mengi ambayo yalipita katika kipindi ambacho walikuwa chuoni nchini Marekani huku mzee Rutaba akichangia kila kitu kilichokuwa kikiongelewa mahali hapo.
Mara baada ya chakula kuwa tayari, Albertina akachukua vyombo na kuvipeleka katika sehemu ya chakula. Alan hakumuona Albertina kwa mbele, alipata bahati ya kuliona umbo lake kwa nyumba tu. Muonekano wake wa nyuma, kwa jinsi hipsi zilivyokuwa zikionekana kwa nyuma zilionekana kumchaganya sana. Mara baada ya Albertina kugeuka nyuma na kukutanisha macho yao, kila mmoja akaonekana kushtuka.
Alan alionekana kama kuchanganyikiwa, alibaki akimwangalia Albertina mara mbili mbili, alionekana kutokuamini kama angeweza kukutana na msichana wa namna ile katika bara la Afrika. Albertina alionekana kuwa msichana mrembo ambaye alikuwa ameumbika vizuri katika kila kona, macho yake yalikuwa madogo, alikuwa na hipsi za wastani huku uso wake ukiwa kama uso wa mtoto.
Kadri Alan alivyokuwa akimwangalia Albertina ndivyo ambavyo alivyozidi kuchanganyikiwa zaidi na zaidi, Albertina alionekana kama malaika ambaye alikuwa ameshushwa duniani kwa ajili yake tu. Alan hakuonekana kutulia, muda mwingi alikuwa akiutumia kumwangalia Albertina. Urembo wa Albertina ulionekana kuwa juu sana katika macho yake, alibadilisha mikao tu, mara alikuwa akikaa mkao huu na mara alikuwa akikaa mkao ule.
Ni kweli kwamba alikuwa ameona wanawake wengi nchini Marekani, wanawake ambao walikuwa na kila sifa za urembo machoni mwake lakini katika kipindi ambacho macho yake yalipotua usoni mwa Albertina, aliona fika kwamba katika maisha yake hakuwahi kumuona msichana ambaye alikuwa mrembo kama alivyokuwa Albertina.
Muda wote Alan alionekana kuwa na furaha, alifurahia kuwa ndani ya nyumba hiyo na kuonana na rafiki yake ambaye alikuwa amepotezana nae katika kipindi kirefu kilichopita lakini kitu ambacho kilikuwa kimempa furaha zaidi kilikuwa ni kile kitendo cha kumuona Albertina machoni mwake. Alan alichanganyikiwa, mapigo ya moyo wake yalikuwa yakidunda kwa kasi tofauti na udundaji wake wa kawaida.
Kwa wakati huo kila kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuona kila mtu akiinuka kutoka mezani na kuondoka na kisha yeye kubaki na Albertina ambapo moja kwa moja bila kuhofia kitu chochote kile angemwambia jinsi alivyokuwa akijisikia juu yake. Ingawa sala yake ilikuwa ikiendelea moyoni mwake lakini hakukuonekana kubadilika kitu, bado kila mtu alikuwa mezani pale akila huku ukimya ukiwa umetawala mahali hapo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kichwa cha Alan bado kilikuwa kikifikiria mambo ya mbali kabisa. Alikuwa akijiona kuwa na Albertina katika kisiwa cha Hawaii huku wakila fungate, alijiona akiwa amemkumbatia Albertina na kisha kuanza kupeana malavidavi ya nguvu. Kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo aliomba kiweze kutokea ili aweze kuyafurahia maisha yake pamoja na msichana huyo ambaye kwa wakati huo alionekana kuwa msichana wa ndoto ambaye alikuwa ameletwa katika maisha yake.
“Thank you for everything (Asanteni kwa kila kitu)” Alan aliwaambia mara baada ya kumaliza kula chakula.
“Don’t worry (Usijali)” Brian alimwambia Alan.
Baada ya chakula hicho, wote wakakaa na kuanza kuongea. Wakaanza kuongea mambo mengi sana lakini katika kila wakati Alan alikuwa akimfikiria Albertina tu. Kitendo cha Albertina kuonekana mara kwa mara mbele ya macho yake kilikuwa kikimpa hamasa kubwa sana ya kutaka kuwa na msichana huyo ambaye alionekana kuwa kila kitu katika maisha yake.
Ilipofika saa moja usiku, Alan akaaga mahali hapo huku akionekana kutokuridhika kabisa kwani hakutaka kuondoka kurudi hotelini bila kuongea na Albertina na kumwambia hali ambayo ilikuwa ikiendelea ndani ya moyo wake kwa wakati huo.
“It seems you are not the same Alan (Inaonekana haupo sawa Alan)” Brian alimwambia Alan.
“I think we have to talk right now (Nafikiri yatupasa kuongea sasa hivi)” Alan alimwambia Brian.
“About what? (Kuhusu nini?)
“Albertina” Alan alimwambia Brian.
Brian akaonekana kushtuka, hakuamini kama Alan angeweza kuongea kitu chochote kile kuhusu Albertina, kwanza akabaki kimya, akaanza kumwangalia Alan vizuri machoni mwake huku maneno yale yakianza kujirudia kichwani mwake. Maswali mengi yakaanza kumiminika kichwani mwake juu ya Alan, alikuwa akiendelea kujiuliza juu ya mambo ambayo Alan alikuwa akitaka kuzungumza kuhusiana na dada yake, Albertina.
“What has she done? (Amefanya nini?)” Brian alimuuliza Alan huku akiendesha gari kuelekea hotelini.
“I real need her (Ninamhitaji)”
“How? (Kivipi?)
“I want her to marry me (Nataka kumuoa)” Alan alimwambia Brian ambaye akaonekana kushtuka.
“Are you serious (Upo siriasi?)
“Yeah!
Brian hakuongea kitu, akaonekana kuingia kwenye mawazo, kasi ya uendeshaji gari ikapungua, maneno ambayo aliyazungumza Alan yalionekana kuanza kumchanganya kichwani mwake, alichokifanya ni kulisimamisha gari lile pembezoni mwa barabara na kisha kuanza kumwangalia Alan usoni.
“Rudia tena. Umesemaje?” Brian alimuuliza Alan.
“Ninamhitaji Albertina. Ninataka kumuoa” Alan alimwambia Brian.
“Itakuwa ngumu sana”
“Kwa nini? Hautaki nimuoe dada yako?”
“Si kwamba sitaki umuoe”
“Sasa tatizo nini?”
“Ni miezi sita imepita tangu Albertina aumizwe na mwanaume aliyekuwa akimpenda sana, kutokana na maumivu hayo, alijiapiza kwamba kamwe asingeweza kuingia katika mahusiano ya kimapenzi tena” Brian alimwambia Alan.
“Mara nyingi binadamu tunasema hivyo hivyo lakini mwisho wa siku hubadilika” Alan alimwambia Brian.
“Nadhani Albertina alimaanisha sana”
“Sidhani. Unamkumbuka Profesa Edward alivyotuambia kuhusu mahusiano?” Alan alimuuliza Brian.
“Nakumbuka”
“Basi amini hivyo. Amini kwamba hakuna mtu asiyependa kuingia katika mahusiano mara anapompata mtu ambaye atakuwa tayari kumpenda kwa moyo mmoja” Alan alimwambia Brian.
“Sawa. Kwa hiyo nini kinafuata?” Brian alimuuliza Alan.
“Kumwambia ukweli. Akikubali, namuoa” Alan alimwamia Brian.
“Sawa”
“Kwa hiyo turudi sasa hivi?”
“Hapana. Tufanye kesho mchana wakati wazazi hawapo. Nitakuachia nafasi” Brian alimwambia Alan na kisha kuendelea na safari yao.
Ndani ya chumba cha hoteli Alan alionekana kuwa mgumu kupata usingizi, muda wote mawazo yake yalikuwa kwa msichana Albertina ambaye mpaka katika kipindi hicho moyo wake ulikuwa hoi bin taaban. Alikuwa akijilaza kitandani chali lakini usingizi wala haukupatikana, akaona hiyo haitoshi, akaipeleka miguu yake ukutani lakini bado hali ilikuwa ile ile.
Alan hakuonekana kuishia hapo, alijaribu hata kujifunika shuka mwili mzima lakini bado hali iliendelea kuwa vile vile, usingizi haukumpata hata kidogo. Bado alikuwa akimfikiria msichana Albertina, kila alipokuwa akijaribu kulala, picha ya Albertina ilikuwa kichwani mwake. Usingizi haukumjia kabisa, mawazo yalikuwa yakimtesa huku moyo wake ukiwa na hamu ya kumuona Albertina kwa mara nyingine tena. Ilipofika saa tisa na nusu, usingizi ukampitia.
******
Mwanga wa jua ambao ulikuwa ukipenya kupitia dirishani ndio ambao ulimshtua kutoka usingizini. Alan akasimama kutoka kitandani na kisha kuanza kuiangalia sehemu alipokuwa kwa wakati huo, baada ya sekunde chache akaonekana kukumbuka alikuwa wapi. Kitendo cha kukumbuka ndicho kilichomfanya kumkumbuka Albertina, akaikumbuka vizuri sura ya msichana yule mrembo, sura ya kitoto ambayo ilikuwa na mvuto mkubwa mbele ya macho ya kila mwanaume ambaye angebahatika kumwangalia.
“Nitamfuata tu na kumwambia ukweli. Siwezi kuteseka namna hii. Ila akinikubalia, itakuwaje kuhusu Stacie? Nitawaambia nini wazazi kuhusu Stacie? Mmmh! Ila kwanza hebu ngoja nimalizane na huyu Albertina, kuhusu Stacie nitalizungumzia nikifika Marekani” Alan alijisemea katika kipindi ambacho alikuwa akielekea bafuni kuoga.
Mawazo juu ya Albertina yaliendelea kumjia kama kawaida, kila hatua ambayo alikuwa akipiga sura ya Albertina ilikuwa imeutawala moyo wake. Albertina alionekana kuwa msichana sahihi katika maisha yake japokuwa kwa mbali jina la Stacie lilikuwa likimjia kichwani. Alan akaonekana kubadailika kabisa, hakuamini kama safari yake ya kuja Tanzania ndio ambayo ingemfanya kuangukia katika mapenzi ya msichana ambaye wala hakuwa akimfahamu zaidi ya kumsikia kutoka kwa rafiki yake, Brian.
Japokuwa alikuwa na uhakika kwamba Albertina asingeweza kutoka katika mikono yake lakini moyo wake ukaanza kuingiwa na wasiwasi, akaanza kuhisi kwamba kungekuwa na tatizo jingine ambalo lingetokea huko mbeleni katika kipindi kile ambacho angemwambia Albertina jinsi alivyokuwa akijisikia.
Kama alivyokuwa ameambiwa ndivyo ambavyo alitakiwa kuamini kwamba kilikuwa kimepita kipindi cha miezi sita tangu Albertina afuatwe na Bi Agnes ambaye alikuwa akimtaka kuachana na mwanaume ambaye alikuwa akimpenda sana, Kelvin. Tukio lile lilikuwa ni moja ya matukio ambayo yalimuumiza sana moyoni mwake. Alijua fika kwamba Kelvin hakutaka kabisa kufanya kitu kama kile bali alishinikizwa na mama yake kukifanya kitu kile.
Bado Albertina alionekana kuwa na kidonda moyoni, tena kidonda kibichi kabisa ambacho hakikuonekana kuwa na dalili ya kupona kabisa. Katika kipindi hicho ambacho Albertina alikuwa na kidonda kibichi cha mapenzi moyoni mwake ndicho kilikuwa kipindi ambacho Alan alitakiwa kufanya kitu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Albertina anakuwa mikononi mwake.
Japokuwa baba yake alikuwa miongoni mwa matajiri watatu wakubwa duniani lakini hiyo haikuonekana kuwa sababu ambayo ingemfanya kufanikisha kile ambacho alikuwa akitaka kufanikisha kwa wakati huo. Alijua fika kwamba fedha hazikuwa mapenzi, kama Albertina hakuwa akifahamu kwamba alitoka katika familia ya kitajiri, alitaka hali iendelee hivyo hivyo mpaka pale ambapo msichana huyo angeamua kuwa pamoja nae.
“Nitampata tu. Ila sitotaka afahamu kuhusu familia yangu. Au Brian atakuwa amemwambia? Mmh! Kama amemwambia atakuwa amekosea sana” Alan alisema katika kipindi ambcho alikuwa akivaa nguo zake. Alipoona kila kitu kimekamilika, akampigia simu Brian ambaye baada ya dakika ishirini akafika hotelini hapo na kumchukua Alan.
“Anaendelea vipi?” Alan alimuuliza Brian.
“Nani?”
“Mke wangu mtarajiwa” Alan alijibu huku akitoa tabasamu pana.
“Hahaha! Usije kuwachukia tu wanawake wa kitanzania. Huwa hawana huruma hao wanapoamua kufanya maamuzi yao” Brian alimwambia Alan.
“Kwa hiyo atanikataa?”
“Sijajua”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huwa nyie watanzania mnaanza vipi kuongea na wanawake kuhusu mahusiano?” Alan aliuliza.
“Kawaida tu. Kwani kule kwenu huwa mnafanyaje? Hebu nikumbushe”
“Kama unampenda msichana, unamfuata, unamuomba kula chakula cha usiku pamoja nae huku gharama zikiwa zako au wakati mwingine mnagharamia kila kitu. Mkifika huko, kila kitu kinakuwa tayari. Hakatai. Ni lazima akubali” Alan alimwambia Brian.
“Hahaha! Ni lazima kukubali?”
“Yeah! Yaani kitendo cha kukubali kwenda kula nawe chakula cha usiku, tayari kashakubali. Safari ya pili inakuwa ni safari kama wapenzi” Alan alimwambia Brian.
“Kwenu ni tofauti na kwetu. Unamfuata msichana, unaongea nae na kisha kumwambia ukweli” Brian alimwambia Alan.
“Kwa hiyo hakuna masuala ya kumwambia kwenda kula chakula cha usiku?”
“Huku hatuna utamaduni huo”
“Basi sawa”
Safari bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida. Katika kipindi chote hicho Alan alikuwa akitetemeka kwa woga. Moyo wake ulikuwa ukimuogopa sana Albertina, kwake alionekana kuwa msichana wa tofauti sana katika maisha yake, kadri gari lilivyokuwa likizidi kusogea mbele na ndivyo ambavyo alizidi kuwa na wasiwasi zaidi moyoni mwake.
Alan hakutaka kujiamini, alijua fika kwamba Albertina angeweza kumkubalia na hatimae kuwa wapenzi lakini hakujua ni nini kingetokea endapo msichana huyo angekataa kuwa nae. Alijua fika kwamba angeumia sana moyoni mwake, alijua fika kwamba moyo wake ungemchoma sana na kuhisi maumivu makali kupita kawaida. Alijitolea maisha yake kwa Albertina, hakutaka kumkosa msichana huyo, alikuwa radhi kukosa kila kitu katika maisha yake lakini si kumkosa Albertina.
“Vipi?” Brian alimuuliza Alan mara baada ya kufika nyumbani.
“Ngoja kwanza” Alan alimwambia Brian, akateremka ndani ya gari na kisha kuanza kujifunga vizuri shati lake. Akajiangalia katika kitoo cha pembeni ya gari, akajiona kuwa tayari.
“Hapa vipi?”
“Hapo safi. Jiamini sasa! Mbona unakuwa na wasiwasi?” Brian alimwambia Alan.
“Usijali. Twende ndani. Kwanza una uhakika yupo?” Alan alimuuliza Brian.
“Nina uhakika kwani nilimuacha na huwa hatoki ndani ya nyumba” Brian alijibu huku akitoa tabasamu, kila alivyokuwa akimwangalia Alan ambaye alikuwa akijiweka sawa, alijihisi kutaka kucheka.
“Daah! Mbona leo sijiamini?” Alan alijiuliza, hapo hapo akaanza kujipiga vibao mashavuni mwake.
“Hata mimi nakushangaa. Upo tayari?”
“Yeah!” Alan alijibu na wote kuanza kupiga hatua kuelekea ndani.
Wamarekani bado walionekana kuwa juu kwa kuwa na watu wengi katika orodha ndefu ya matajiri ambao walikuwa wakimiliki kiasi kikubwa cha fedha duniani. Japokuwa katika orodha hiyo ndefu kulikuwa na matajiri mbalimbali duniani lakini katika orodha ya watu kumi matajiri duniani, watu saba walikuwa ni raia kutoka nchini Marekani.
Orodha hiyo ndefu ya matajiri duniani ambayo ilikuwa ikiongozwa na Carlos Slim huku nafasi ya pili ikishikiliwa na mmarekani Bill Gates, nafasi ya tatu ilikuwa ikishikwa na mzee ambaye alikuwa akimiliki visima vya mafuta katika nchi mbalimbali za uarabuni, alikuwa akimiliki kampuni kubwa ya ndege za Mapple Airline kampuni ambayo ilikuwa na ndege zilizokuwa zikisafiri katika nchi zaidi ya mia na kumi duniani, alikuwa akimiliki kampuni ya magari ya kifahari ya McLloyd, alikuwa akimiliki timu mbalimbali za mpira wa kikapu, NFL pamoja na ile kampuni ya Pelvin ambayo ilikuwa ikitengeneza simu, televisheni, redio pamoja na vifaa mbalimbali vya umeme. Vitega uchumi hivi na vingine vingi vilikuwa vikimilikiwa na Bwana Thomson Kurt, tajiri aliyekuwa na miaka hamsini na tano huku akionekana kuwa na utajiri uliokuwa na zaidi ya dola bilioni sitini.
Kama ilivyokuwa kwa matajiri wengine, Bwana Kurt alikuwa akiheshimika na watu wengi duniani, kila alipokuwa akipita watu walikuwa wakimpa heshima yake ambayo alistahili kupewa. Utajiri wake ulikuwa mkubwa sana lakini katika maisha yake alikuwa mtu asiyekuwa na makuu kabisa. Yeye ndiye alikuwa tajiri pekee kati ya matajiri waliokuwa katika ishirini bora ambaye alikuwa akitembelea gari la bei rahisi kuliko wote.
Pamoja na utajiri wote huo, Bwana Kurt alikuwa akiendesha gari lililokuwa na thamani ya dola milioni moja na nusu tofauti na matajiri wengine ambao walikuwa wakitembelea magari ya kifahari. Kuhusu usafiri, Bwana Kurt hakutaka kabisa kuwa na gari la thamani kubwa ila katika masuala ya nyumba za kuishi, Bwana Kurt alikuwa na nyumba nyingi za kifahari ambazo zote alikuwa amezijenga katika fukwe mbalimbali nchini Marekani.
Fedha zilikuwepo, alikuwa na uwezo wa kubadilisha kila mwanamke aliyetaka au kukaa bila ya kuwa na mke kama walivyokuwa matajiri wengi wa Marekani. Kwa Bwana Kurt hali ilionekana kuwa tofauti, katika maisha yake alikuwa na mke mmoja ambaye allimpenda sana kuliko mwanamke yeyote katika dunia hii. Alimthamini mwanamke huyu, kwake alimchukulia kuwa kila kitu katika maisha yake, Bertha.
Bertha ndio lilikuwa jina la mke wake ambaye alikuwa akimpenda sana. Katika kipindi chote cha maisha ya ndoa, Bwana Kurt alijitahidi kuonyesha uaminifu wa hali ya juu kwa mke wake huyo ambaye alikutana nae mara ya kwanza katika kipindi ambacho alikuwa grade la sita katika shule ya wanafunzi masikini ya St’ McBerth ambayo ilikuwa katika mji wa Manhattan uliokuwa Kaskazini mwa jiji la New York
Japokuwa katika kipindi hicho alikuwa miongoni mwa wanafunzi masikini sana shuleni hapo lakini msichana Bertha alionekana kumkubali kwa kila kitu. Walianza kama marafiki, waliendelea kuwa pamoja zaidi na zaidi huku kila mmoja akiuchukulia urafiki wao kuwa wa kawaida sana. Wazazi wao wakaufahamu urafiki huo, wazazi nao wakafahamiana kwa sababu watoto wao walikuwa karibu sana.
Walipotakiwa kuingia High School, hapo ndipo walipotengana kitu ambacho kilionekana kuwaletea majonzi sana mioyoni mwao. Msichana Bertha akawa amekwenda kusoma St’ Mathew High School iliyokuwa katika mji wa Brooklyn Kusini mwa jiji la New York huku Kurt akienda kusoma Martin Luther King High School iliyokuwa katika jiji la Washington.
Wawili hao wakawa wametengana, kila siku wakawa wakiongea katika simu tu huku kila mmoja akionekana kumkumbuka sana mwenzake. Hicho ndicho kikawa kipindi ambacho kila mmoja akahisi kwamba alikuwa na kitu cha tofauti moyoni mwake, kitu ambacho kilikuwa ni zaidi ya urafiki ambao walikuwa nao, wakagundua kwamba mapenzi ndio ambayo yalikuwa yameitawala mioyo yao.
Hilo ndilo ambalo lilionekana kuwapa hamu kubwa ya kukutana tena na kuanza kuongea kama wapenzi, kubusiana kama wapenzi na hata kushikana mikono kama wapenzi. Kutokana na maisha ya kimasikini ambayo alikuwa akiishi Kurt, hakupata hata nauli ambayo ingemuwezesha kufika New York ili kuonana na mpenzi wake ambaye alikuwa akimthamini sana, Bertha.
“How can I live without you Bertha? (Nitaishi vipi bila wewe Bertha?)” Lilikuwa moja ya swali ambalo mara kwa mara lilikuwa likisikika masikioni mwa Bertha kutoka mdomoni mwa Kurt.
“I don’t know baby, I love you, I love you baby (Sijui mpenzi, ninakupenda, ninakupenda mpenzi)” Sauti ya Bertha ilisikika kama mtu ambaye alianza kushikwa na kwikwi tayari kwa kuanza kulia.
“I have no money, Bertha (Sina fedha, Bertha)”
“But you have true love on me, that’s enough Kurt. Don’t tell me anything about money, I love you the way you are my love, money comes and goes away but remember my love stays with you forever (Lakini una mapenzi juu yangu, hilo linatosha Kurt. Usiniambie kitu chochote kuhusu fedha, ninakupenda kwa hivyo ulivyo, fedha zinakuja na kuondoka lakini kumbuka penzi langu litakaa nawe milele)” Bertha alimwambia Kurt.
Ni kweli Kurt hakuwa na fedha na alitamani sana kuwa na fedha kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wake lakini maneno ambayo mara kwa mara Bertha alikuwa akiyaongea masikioni mwake yakamfanya kubadilika kabisa na kuanza kufikiria kitu kingine kabisa. Hapo ndipo akagundua kwamba fedha hazikuwa na nafasi katika mapenzi, fedha zilionekana kuwa kitu cha kuja na kuondoka lakini mapenzi hubaki moyoni milele.
Mapenzi yake kwa mpenzi wake, Bertha yakaongezeka zaidi, kila siku akawa mtu wa kumpigia simu na kuongea mambo mbalimbali. Mwaka wa kwanza ukapita na wa pili kuingia, watu hawa hawakuwa wameonana zaidi ya kuwasiliana kwa njia ya simu tu. Mwaka wa tatu ukaingia, wakamaliza shule na bila kutarajia wakajikuta wakiipelekwa katika chuo Washington State kilichokuwa katika mji wa Vancouver ndani ya jiji la Washington.
Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwao. Hapo ndipo ambapo wakaonana na kisha kuanza kufanya kama vile walivyokuwa wakitaka kuvifanya kwa mara ya kwanza kama wapenzi. Katika kipindi cha nyuma walikuwa wakishikana mikono kama marafiki, walikuwa wakitembea barabarani kama marafiki na hata kubusiana kama marafiki lakini katika kipindi hiki hali ikaonekana kuwa tofauti kabisa, wakaanza kuvifanya vitu hivyo vyote kama wapenzi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha ya chuoni hapo yaliendelea zaidi. Walikuwa wakionyesheana mapenzi ya dhati kiasi ambacho mapenzi yale yakaonekana kuwa mfano wa kuigwa kwa wanachuo wengine ambao walikuwepo chuoni pale. Siku zilisonga mpaka pale ambapo bahati kubwa ya kuwa milionea ilipomwangukia Kurt kwa kupitia mchezo ambao ndio kwanza ulikuwa umeanzishwa katika kipindi hicho, mchezo wa kujibu maswali ambao uliitwa WHO WANTS TO BE MILLIONAIRE.
Kwa sababu Kurt alikuwa mtu wa kujaribu kila kitu kilichokuwa kikihusiana na fedha, akanunua tiketi ya kushiriki katika mchezo huo ambapo moja kwa moja akapita na kisha kuanza kuulizwa maswali. Ulikuwa mchezo mrefu ambao ulikuwa ukichukua mwaka mzima mpaka kumpata yule mtu ambaye atakuwa amejinyakulia kiasi kikubwa cha fedha.
Kutokana na umahiri wake wa kujibu maswali, Kurt alijikuta akizidi kusonga mbele zaidi na zaidi. Kila siku machoni mwa watu alionekana msindikizaji lakini kadri alivyokuwa akizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo watu wakaanza kumuwekea umakini kwa kugundua kwamba Kurt hakuwa msindikizaji kama watu wengine bali alikuwa mshiriki ambaye nae alitakiwa kujishindia kitika cha dola milioni mia moja ambacho kilikuwa kimetangazwa.
Baada ya mzunguko wa mwaka mzima kumalizika na ndipo mtu mmoja akapatikana na kutangazwa kuwa mshindi, huyu alikuwa Kurt. Hiyo ikaonekana kuwa furaha kwake, kwa wazazi wake na hata kwa mpenzi wake, Bertha ambaye alikuwa amekubali kuwa nae kwa kila hatua ambayo angepiga katika maisha yake. Dunia nzima ikamtambua mshindi huyo ambaye maisha yake yalionekana kubadilishwa na fedha za mchezo ambao kwa mara ya kwanza ulikuwa umeanzishwa nchini Marekani.
Magazeti mbalimbali ya nchini Marekani kama New York Times, Daily News, Morning News na magazeti mengine pamoja na majarida kama Forbes, Playboy yalikuwa yakiamuandika sana Kurt kama miongoni mwa mamilionea ambao kama wangezifanyia biashara fedha ambazo walikuwa nazo basi fedha zile zingeweza kubadilisha maisha yao. Kwa sababu mchezo wa WHO WANTS TO BE MILLIONAIRE ndio kwanza ulikuwa umeanza huku ukivuma sana duniani hasa nchini Marekani na Uingereza, watu wengi wakaonekana kuanza kumfuatilia Kurt na baada ya siku chache nae kuanza kuwa miongoni mwa watu maarufu duniani.
“Tumbo linauma” Bertha alimwambia Kurt.
“Kwa nini linauma? Hebu sogea kwangu, nadhani litakuwa linahitaji mguso wangu” Kurt alimwambia Bertha na kisha kumsogeza karibu yake na kulishika tumbo lile.
“Nina mimba” Bertha alimwambia Kurt ambaye alionekana kushtuka.
“Unasemaje?”
“Nina mimba”
“Kweli?”
“Ndio”
“Unamaanisha ninakwenda kuitwa baba?”
“Ndio”
“Mungu wangu! Siamini!” Kurt alisema, akamuinua Bertha na kisha kumkumbatia.
Hapo wakawa kama wameanza upya. Mapenzi ambayo walikuwa nayo yakaongezeka zaidi na zaidi, kila mmoja akajiona kuwa na uhitaji wa kuwa karibu na mwenzake. Fedha ambazo alikuwa amezipata Kurt hakutaka kucheza nazo, alichokifanya ni kuanza kufanya biashara mbalimbali.
Baada ya miezi tisa kukamilika, Bertha akajifungua mtoto wa kiume na wote kukubaliana kumpa jina la Alan. Mtoto huyo ndiye alikuwa furaha yao katika maisha yao, wakampenda kuliko mtu yeyote yule, Alan ndiye ambaye alikuwa amewaunganisha kama wazazi na kuwafanya kuwa karibu zaidi.
Mwaka wa kwanza ukakatika na wa pili kuingia. Alan alikuwa akilelewa katika maisha ya kitajiri, alikuwa akipewa kila kitu ambacho kilihitajika kupewa mikononi mwake. Utajiri wa Kurt ulizidi kuongezeka zaidi na zaidi. Akaanza kununua hisa katika kampuni mbalimbali nchini Marekani pamoja na kuongeza biashara nyingine nyingi. Kadri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo alivyozidi kupata utajiri zaidi na zaidi na kuwapa taarifa matajiri wengine kwamba nae alikuwa akija kwa kasi sana.
Baada ya mwaka wa tatu kuingia, Kurt akajikuta akiingia katika orodha ya matajiri wakubwa mia moja duniani. Kurt hakutaka kuishia hapo, lengo lake kubwa katika kipindi hicho lilikuwa ni kuwa tajiri mkubwa kuliko matajiri wote duniani. Aliendelea kufanya biashara zake na kuwekeza sehemu mbalimbali. Faida zilizidi kuongezeka na kujikuta akizidi kupanda juu zaidi na zaidi tena kwa kasi kupita kawaida mpaka pale jarida la Forbel lilipomtangaza kwamba alikuwa ameingia katika orodha ya matajiri wakubwa thelathini duniani.
Japokuwa alikuwa akiendelea kufanya biashara zake lakini kamwe hakuweza kumsahau mke wake kipenzi, alikuwa akimpenda zaidi na zaidi huku akijitahidi sana kutafuta muda na kukaa pamoja na familia yake. Mapenzi kwa mkewe na mtoto wake hayakuisha hata kidogo, kila siku alikuwa akiwapenda kama alivyokuwa akijipenda.
Baada ya kupita miaka mitano, Bwana Kurt akatamani kuwa na mtoto mwingine kitu ambacho akamwambia mkewe kuhusiana na suala hilo ambapo moja kwa moja shughuli ya kuanza kumtafuta kuanza. Kila siku walikuwa kitandani huku wakijitahidi kuiridhisha miili yao lakini hakukuwa na kitu ambacho kiliendelea kabisa. Walifanya kama kawaida tena kwa nguvu zote lakini hakukuwa na kitu chochote ambacho kilitokea kabisa, mtoto hakuweza kupatikana.
“Tatizo nini?” Bwana Kurt alimuuliza mkewe kwa mshangao.
“Sijui tatizo ni ni mpenzi”
“Yaani mwaka mzima huu patupu utafikiri natumia mpira. Au tuna tatizo?” Bwana Kurt alimuuliza mkewe.
“Sijui”
“Hebu ngoja nimpigie simu daktari” Bwana Kurt alimwambia mkewe na kisha kumpigia simu daktari wa familia, Dokta Paul ambaye baada ya dakika kadhaa akafika nyumbani hapo.
Hakukuwa na muda wa kupoteza hata mara moja, moja kwa moja vipimo vikachukuliwa na kisha Dokta Paul kuvifanyia kazi. Dokta hakutaka kuchelewa, alichokifanya ni kuvipeleka vipimo vile maabara na kisha kuanza kazi yake. Alichukua muda wa dakika thelathini na ndipo hapo alipowarudia huku uso wake ukionekana kuwa na majonzi.
“Vipi Dokta?” Bwana Kurt aliuliza huku akionekana kuwa na wasiwasi.
“Kuna tatizo”
“Tatizo gani?” Bertha aliuliza.
“Mbegu zako hazina nguvu ya kutengeneza mtoto katika yai la mkeo” Dokta Paul alimwambia Bwana Kurt.
“Kwa nini tena?”
“Nahisi una kansa ya korodani, kansa ambayo kazi yake kubwa ni kuzishambulia mbegu zako” Dokta Paul alimwambia Bwana Kurt ambaye alionekana kuchoka.
“Lakini mbona kipindi cha nyuma niliweza kupata mtoto?” Bwana Kurt aliuliza.
“Hata mimi nashangaa. Ila nadhani tatizo hili limeanza hivi karibuni, kama mwaka mmoja hivi” Dokta Paul alimwambia Bwana Kurt.
“Kwa hiyo nifanye nini?”
“Nitakupatia dawa ambazo utatakiwa kuzitumia. Kwanza zitaua hiyo kansa na kuipoteza kabisa” Dokta Paul alimwambia Bwana Kurt.
“Nitapona?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Utapona ila bado sijajua kama mbegu zitakuwa na nguvu” Dokta Paul alimwambia Bwana Kurt.
Huo ndio ukawa mwisho wa kila kitu, wote wawili wakaonekana kukubaliana na matokeo ya vipimo vyao. Alan ndiye akawa mtoto wao pekee katika maisha yao. Wote wakaweka nguvu zao kwa Alan ambaye aliendelea kukua zaidi na zaidi.
Baada ya miaka ishirini, Alan akawa kijana mkubwa. Japokuwa Alan alikuwa mtoto wa tajiri lakini maisha yake yalionekana kuwa tofauti kabisa. Marafiki zake wengi ambao alikuwa akiwapata walikuwa wale ambao waliishi katika maisha ya kimasikini. Hakuwa mtu wa kuchangamana na watoto wa matajiri kama walivyokuwa wazazi wake. Kila gari la kifahari ambalo alikuwa akinunuliwa hakutaka kulitumia kabisa, gari ambalo alikuwa akilitumia katika kipindi hicho lilikuwa na thamani ya dola milioni milioni mbili tu na alionekana kuridhika nalo.
Wazazi wakahuzunika lakini mwisho wa siku wakaona kwamba Alan alikuwa akifanya jambo ambalo lilikuwa sahihi sana katika maisha yake, walichokifanya ni kukubaliana nae tu. Katika muda wa kujiunga na chuo ulipofika, Alan akajiunga na chuo cha wanafunzi wa kawaida cha Mississippi kilichokuwa katika jiji hilo la Mississippi ambapo huko akakutana na watu wawili ambao wakatokea kuwa marafiki zake wakubwa sana, wa kwanza alikuwa Brian Ruttaba ambaye alikuwa ametoka nchini Tanzania na wa pili alikuwa Antonio Sanchez, kijana kutoka nchini Mexico, nae maisha yake yalikuwa kama ya Alan, japokuwa baba yake alikuwa tajiri mkubwa nchini Mexico lakini Antonio hakutaka kuishi maisha ya kifahari kabisa.
Alan akajitahidi kujivika ujasiri moyoni mwake. Hakuonekana kuwa na amani kabisa, alionekana kuwa na wasiwasi mwingi kupita kawaida. Hakuamini kama kitendo cha kuwa mahali hapo kwa ajili ya kumuona Albertina na kuongea nae ndicho ambacho kilikuwa kimeanza kumpa hofu kiasi hicho. Mwili wake ukaanza kutetemeka, amani ikatoweka moyoni mwake kiasi ambacho wakati mwingine akaonekana kujuta kwa kuamua kutaka kufanya kile alichikuwa akitaka kukifanya mahali pale.
Wakaingia ndani na kisha kukaa kochini. Kila wakati Alan akawa mtu wa kujiangalia kama alikuwa sawa au la. Muda wote huo Brian alikuwa akimwangalia tu, Alan alionekana kutokujiamini kabisa, uso wake ulionekana kuwa na hofu kubwa kupita kawaida. Alichokifanya Brian ni kuondoka sebuleni hapo, aliporudi baada ya dakika moja, alirudi akiwa na Albertina kitu ambacho kilimfanya Alan kuusikia moyo wake ukipata mshtuko mmoja mkubwa, mzunguko wa damu mwilini mwake ukaongezeka zaidi.
Kwa siku hiyo, Albertina alionekana kuwa mrembo zaidi usoni mwa Alan, alibaki akimwangalia Albertina usoni, bado hakuonekana kuamini kama msichana aliyekuwa na urembo mkubwa namna ile angekuwa barani Afrika tena katika nchi kama Tanzania. Albertina akamsalimia Alan huku akiachia tabasamu pana usoni mwake, tabasamu ambalo lilionekana kumchanganya zaidi Alan.
Kama walichokipanga ndicho ambacho kilitakiwa kufanyika mahali hapo. Alichokifanya Brian ni kuaga kwamba alikuwa akielekea katika kituo cha mafuta kwa ajili ya kununua mafuta ya gari na angeweza kurudi baada ya dakika kadhaa huku akimtaka Albertina kubaki na Alan ili asijisikie upweke mahali hapo.
Hiyo ndio ilionekana kuwa njia nyepesi lakini kwa Alan ukaonekana kuwa mtihani mkubwa sana katika kufanikisha kile alichokuwa akitaka kukifanikisha kwa wakati huo. Msichana ambaye alikuwa akimtaka sana kwa wakati huo alikuwa mbele yake tena huku wakiwa wawili tu pale sebuleni. Alan akabaki akimwangalia Albertina huku kila wakati akimeza fundo la mate. Kwa muonekano ambao alikuwa nao mahali hapo alionekana kutokufahamu ni mahali gani ambapo alitakiwa kuanzia ili apate kueleweka moyoni mwa Albertina.
“Unaonekana tofauti sana” Alan alimwambia Albertina, kwa sababu hakujua aanzie wapi, yeye akaanza kuyatamka maneno ambayo yalimjia mdomoni wakati huo.
“Kivipi?”
“Unaonekana mnyonge sana, mwenye mawazo mengi na wakati uso wako unaonyesha kwamba hautakiwi kuwa katika hali hiyo” Alan alimwambia Albertina ambaye akaanza kumtilia umakini Alna.
“Uso wangu unatakiwa kuonekana vipi?” Albertina alimuuliza Alan.
“Unatakiwa kuonekana kuwa na furaha. Tabasamu ndicho kitu pekee ambacho ninaamini kinaweza kuupendezesha zaidi uso wako” Alan alimwambia Albertina.
“Huwa ninatabasamu kila siku na kila wakati”
“Labda katika kipindi ambacho sipo mahali hapa”
“Kila wakati ninatabasamu Alan”
“Hivi ni muda gani ambao nilikuwa ndani ya nyumba hii na ukatabasamu?” Alan alimuuliza Albertina.
“Muda wote”
“Unanidanganya. Ninatamani sana kukuona ukitabasamu. Hata kama una shida, wakati mwingine yakupasa kusahau shida zako” Alan alimwambia Albertina.
“Najua na ndio maana najitahidi kutabasamu kila wakati” Albertina alimwambia Alan.
Huo ndio ukaonekana kuwa mwanzo wa Alan kuanza kuongea na Albertina. Alijua fika kwamba moyoni alikuwa akihofia sana na hivyo alitakiwa kwanza kumzoea Albertina hata kabla hajamwambia jinsi alivyokuwa akijihisi ndani ya moyo wake juu yake. Muda ukazidi kusonga mbele, dakika zikazidi kukatika huku mazungumzo ya hapa na pale yakizidi kuongezeka zaidi na zaidi mpaka kufikia kipindi ambacho Alan akaonekana kumzoea Albertina.
“Kuna mengi ninatamani sana kukwambia, ila nadhani moja ni la umuhimu kuliko yote” Alan alimwambia Albertina ambaye kwa mbali akaonyesha mshtuko.
“Kama lipi?”
“Kuhusu uzuri wako, mvuto wako na mengine mengi yanayokuhusu wewe” Alan alimwambia Albertina ambaye akaanza kujiangalia.
“Kati ya wazuri mimi ni mzuri?”
“Unajionaje?”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Wa kawaida sana”
“Hapana. U mzuri sana. Nimekuwa nikiutafakari uzuri wako katika usiku mzima uliopita. Taswira ya sura yako imekuwa ikinijia kila wakati mawazoni mwangu Albertina” Alan alimwambia Albertina.
“Umekuwa ukinifikira?” Albertina alimuuliza Alan huku akionekana kushtuka.
“Huo ndio ukweli. Nimekuwa nikikufikiria sana. Nadhani ni kwa sababu ya jinsi ulivyo, nina uhakika” Alan alimwambia Albertina ambaye akabaki kimya, ukimya ambao ukampa ujasiri Alan na kuendelea kuongea.
“Nimesafiri umbali mrefu sana kuja kumtembelea Brian, katika safari yangu hii nadhani Mungu alikuwa ameniandalia kitu kwa ajili ya maisha yangu. Katika kipindi ambacho ninaianza safari sikuwa nikifahamu ni kitu gani ambacho Mungu alikuwa ameniandalia ila kwa sasa nimeanza kugundua, safari yangu haikuwa ya bure, baada ya kukaa kwa kipindi kirefu, nadhani Mungu amejibu maombi yangu, ameyajibu kupitia safari yangu” Alan alimwambia Albertina ambaye alikuwa kimya, alionekana kufahamu Alan alimaanisha nini.
“Najua unataka kuniambia nini. Tafadhali, naomba usiniambie unachotaka kuniambia” Albertina alimwambia Alan huku akionekana kuanza kubadilika.
“Kwa nini nisikwambie? Kuna ubaya kama nikikwambia wewe ni msichana mzuri ambaye umetokea kuuteka moyo wangu na kukuhitaji katika maisha yangu? Kuna ubaya kama nitasema kwamba baada ya kukuona wewe moyo wangu umekuwa radhi kukupenda kwa moyo mmoja? Sidhani kama kuna ubaya Albertina” Alan alimwambia Albertina. Maneno ya mbalimbali yakaonekana kutokuwa na uwezekano wa kuubadilisha msimamo wa Albertina, alichokifanya ni kumsogelea na kukaa karibu yake.
“Albertina….!” Alan alimuita Albertina ambaye alikuwa ameuinamisha uso wake chini, alipouinua, machozi yalikuwa yakimtoka.
“Kuna nini tena? Mbona unalia?” Alan alimuuliza Albertina.
“Naomba usiendelee zaidi” Albertina alimwambia Alan.
“Kuna tatizo Albertina?”
“Nakuomba usiendelee”
“Najua nimekukumbusha mbali na kukuumiza, najua una maumivu makubwa moyoni mwako, naomba unipe nafasi moyoni mwako, si nafasi ya kukuumiza zaidi, ninahitaji nafasi ya kuyaondoa maumivu ambayo umekuwa nayo moyoni. Ninaomba unipe nafasi hiyo Albertina, ninakuahidi kukutunza na kukupenda kwa mapenzi ya dhati, zaidi ya hayo, ninakuahidi kukuoa, uwe mke wangu wa ndoa” Alan alimwambia Albertina.
Maneno mengi ambayo alikuwa akiyaongea Alan ndio ambayo yalikuwa yakimfanya Albertina kuanza kumfikiria Kelvin. Kila neno ambalo lilikuwa likimtoka Alan yaliyafanya mawazo juu ya Kelvin kichwani mwa Albertina kujirudia zaidi na zaidi. Kama ni kidonda kilichokuwa kikitaka kupona, Alan alikuwa amekitonesha na kukifanya kuwa kibichi tena moyoni mwa Albertina.
Maisha yamapenzi ambayo alikuwa ameyapitia yalionekana kumuumiza kupita kawaida, hakujiona kuwa na uhitaji wa kuwa na mwanaume yeyote katika maisha yake, mapenzi yalikuwa yamemuumiza, mwanaume mmoja ndiye ambaye alimfanya kuyachukia mapenzi na kuchukia kila kitu ambacho kilikuwa kikihusu mapenzi.
Ni miezi sita tayari ilikuwa umepita tangu Albertina aachane na Kelvin ambaye alimsababishia maumivu makali moyoni mwake. Leo hii mbele yake kulikuwa na mwanaume mwingine ambaye alikuwa akiongea maneno mengi ambayo yalikuwa yakifanana na maneno yale aliyoyaongea Kelvin katika kipindi cha nyuma. Maneno yale hayakuonekana kubadilisha kitu chochote kile moyoni mwa Albertina, hata Alan nae alionekana kufanana na Kelvin, ili kuyaepuka maumivu mengine moyoni mwake, njia nyepesi ambayo alikuwa akiiona ni kutojihusisha na mapenzi katika maisha yake.
“Albertina….” Alan alimuita Albertina huku akimshika mkono kitu ambacho kilimshtua Albertina na kumletea msisimko mkubwa mwilini mwake.
“Nakuomba Alan. Unaniumizaaaaa…..!!”
“Najua. Nahitaji nafasi moyoni mwako. Nahitaji kuwa nawe, ninahitaji uwe mke wangu wa ndoa. Nadhani Mungu kanileta Afrika kwa ajili yako. Nakuomba uwe mke wangu wa ndoa” Alan alimwambia Albertina ambaye alibaki kimya.
Kila ukimya ambao ulikuwa ukitokea mahali hapo ukaonekana kuwa kusudi la kumtaka kufanya jambo jingine zaidi, jambo la maendeleo ambalo lingemfanya kumuweka Albertina katika hali ya tofauti kabisa. Alichokifanya Alan ni kumsogelea zaidi Albertina na kisha kuupitisha mkono wake mabegani mwa Albertina na kisha kumwangalia usoni. Machozi yalikuwa yakitiririka mashavuni mwa Albertina jambo ambalo lilimpelekea Alan kutoa kitambaa chake kilichokuwa mfukoni na kuanza kumfuta machozi Albertina.
“Ninahitaji nafasi kutoka kwako. Ninaomba unifanye nijione kuwa mwanaume mwenye bahati katika maisha yangu” Alan alimwambia Albertina ambaye alibaki kimya, Alan hakunyamaza, akaendelea kutoa maneno mazito ya mapenzi.
“Ninachokihitaji kutoka kwako ni kuweka uaminifu wako juu yangu, sitaki kuonekana mtu nisiyekuwa na msimamo kwa kila ahadi ninayokupa katika kipindi hiki, ninahitaji kusimama imara katika kila ahadi ambayo nimekwambia siku ya leo. Ninachokihitaji ni kuwa nawe tu, ninachokihitaji ni kukuoa tu, sipendi kukuona uso wako ukiwa kwenye maumivu makali, sipendi kuyaona machozi ya uchungu yakitiririka mashavuni mwako, ninachokihitaji ni kukuona ukiwa na furaha, ukitabasamu na kukufanya uvutie zaidi” Alan alimwambia Albertina ambaye alibaki kimya, maneno ya Alan bado yalikuwa yakiendelea kumuingia na kumkaa moyoni mwake.
“Ninakuhitaji. Popote utakapokwenda jua kwamba ninakuhitaji, utakapokuwa ukitembea, ukilala, ukikaa au hata ukipika jua kwamba ninakuhitaji, jua kwamba kuna mwanaume anakuhitaji sana katika maisha yake, jua kwamba kuna mwanaume ambaye yupo tayari kujitolea maisha yake kwa ajili yako, jua kwamba kuna mwanaume ambaye yupo radhi kukuoa na kuwa mke wake wa ndoa” Alan alimwambia Albertina ambaye akasimama na kisha kuanza kuelekea chumbani kwake.
Alan hakusema kitu kingine, hakumzuia Albertina, akamuacha aondoke mahali hapo. Albertina akaanza kulia tena kwa kwikwi, Alan akabaki kochini akimwangalia Albertina ambaye akapotea machoni mwake. Alan akajiona kuutua mzigo mkubwa ambao ulikuwa ndani ya moyo wake, hakuamini kama alikuwa amefanikisha kumwambia Albertina jinsi alivyokuwa akijisikia moyoni mwake. Ingawa alikuwa ameongea maneno mengi ya mapenzi lakini hakuwa na uhakika kama Albertina angeweza kumkubalia au la.
“Akinikataa itakuwaje?” Alan alijiuliza lakini akakosa jibu kabisa.
*****
Alan hakutaka kuchoka, alijua fika kwamba kulikuwa na kazi kubwa mbele yake ambayo alitakiwa kuifanya kwa mikono yake, alijua fika kwamba Albertina alikuwa ametoka katika maumivu makali ya mapenzi, maumivu ambayo yalimfanya kutokuyatamani tena mapenzi. Alan hakujiona kuwa na ulazima wa kufanya haraka, aliona kwamba kwa jinsi hali ilivyokuwa ilikuwa ni lazima afanye mambo kwa taratibu tena hatua kwa hatua.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakuishi hapo, siku iliyofuata kama kawaida akaelekea nyumbani hapo na kuendelea kupigilia misumali ya moto moyoni mwa Albertina ambaye muda mwingi alikuwa akibaki kimya tu. Maneno mengi matamu ambayo alikuwa akiyaongea Alan yakaonekana kuingia moyoni mwa Albertina na kueleweka zaidi na zaidi lakini maneno hayo hayakumfanya Albertina kuwa mwepesi, bado aliendelea na msimamo wake kwamba hakutaka kujiingiza tena katika mahusian ya kimapenzi.
Alan hakukoma, leo aliishia hapa na kesho kuendelea kwa kuamini kwamba kungetokea siku ambayo Albertina angeweza kukubaliana nae na hatimae kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na hatimae kumuoa lakini hali ikaonekana kuwa tofauti kabisa, Albertina alionekana kuwa mgumu sana.
“What should I do Brian? (Natakiwa kufanya nini Brian)” Alan alimuuliza Brian mara baada ya kuona kwamba kila maneno matamu ambayo aliyaongea kwa Albertina hayakuwa yakieleweka.
“Just keep going Alan (Endelea Alan)” Brian alimwambia Alan.
“We always fight Brian and sometime we have to give up, maybe God prepares someone for me (Mara kwa mara tunapigana Brian na wakati mwingine yatupasa kusalimu amri, inawezekana Mungu kaandaa mtu mwingine kwa ajili yangu)” Alan alimwambia Brian huku akionekana kukata tamaa.
“Do you real want to marry Alby? (Ni kweli unataka kumuoa Alby?)” Brian alimuuliza Aan.
“I do….I always do (Ninataka…kila wakati ninataka)”
“Then ask her for dinner (Muombe uende nae kula chakula cha jioni)” Brian alimwambia Alan.
Brian shauku yake ilikuwa ni kuona Alan akimchukua Albertina na kisha kumuoa. Alijua fika kwamba Albertina hakuwa katika hali nzuri hata kidogo, muda mwingi alikuwa akionekana kuwa katika mawazo, hakupenda kumuona katika hali ile, kila siku alitamani kumuona dada yake akitabasamu tena na kuwa na furaha kama zamani na hiyo ndio ilikuwa sababu pekee ambayo ilimfanya kufanya kila kilichowezekana kuhakikisha kwamba Alan anakuwa na Albertina.
Kitu alichokisema Brian kikaonekana kuwa na msingi sana, alichokifanya Alan ni kumuomba Albertina kwenda nae kula chakula cha usiku. Albertina hakukataa, kwa sababu Alan alionekana kuwa muelewa, akakubaliana nae. Mpaka kufikia hatua hiyo Alan akaona kwamba alikuwa anakwenda kufanikiwa kwa kile kitu ambacho kila wakati alikuwa akikihitaji kutoka kwa Albertina, kwa sababu hakuwa akizifahamu sehemu nyingi ndani ya jiji la Dar Es Salaam, akamchukua Albertina na kwenda nae katika hoteli ya Kilimanjrao ambapo hapo wakaanza kula chakula cha usiku.
Kidogo mtoko ule ukaonekana kuanza kumbadilisha Albertina, tabasamu lake likaanza kuonekana mara kwa mara usoni mwake, alionekana kufurahia kwa kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea lakini bado msimamo wake ulikuwa ni ule ule kwamba hakutaka kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na Alan.
Huo ukaonekana kuwa mwanzo tu, katika kipindi cha siku tano zilizokuwa zimebakia kabla ya kurudi Marekani Alan alitaka kuhakikisha kwamba msichana Albertina anakuwa wake na mwisho wa siku kumuoa na kuwa mke wake wa ndoa. Hakunyamaza, kila siku alikuwa akimwambia Albertina kuhusiana na jinsi alivyokuwa akiendelea kujisikia moyoni mwake. Tabasamu pamoja na muonekano wake wa tofauti usoni mwake ukaonekana kama kuulegeza msimamo wake lakini kila alipokuwa akiulizwa kama alikuwa tayari, jibu lake lilikuwa lile lile, hakuwa tayari.
Kikafika kipindi ambacho Alan alionekana dhahiri kukata tamaa, kama ni maneno matamu alijiona kumaliza kila neno ambalo alitakiwa kulizungumza mbele ya msichana huyo lakini katika kila neno bado Albertina alionekana kuwa mgumu kumuelewa, yaani alionekana kuwa kama kiziwi. Siku hazikumsubiri, bado ziliendelea kukatika mpaka kufikia siku moja kabla ya kuanza safari ya kurudi nchini Marekani.
Katika siku hiyo alishinda siku nzima nyumbani kwa mzee Ruttaba huku akiongea na Albertina tu. Alan alijitahidi kumfurahisha na kumuonyeshea mapenzi ya dhati lakini kwa Albertina alionekana kama kutokuyaona matendo ya kimapenzi ambayo alikuwa akimuonyeshea. Tayari Alan alijiona kuwa na mkosi, alijona kutokuweza kukamilisha kile ambacho alikuwa akitaka kukikamilisha kwa wakati huo, aliona kila dalili kwamba alikuwa akitakiwa kurudi nchini Marekani huku akiwa hajakamilisha kitu chochote kile kwa Albertina.
Katika kipindi ambacho alikuwa akiendelea kuongea na Albertina hapo ndipo jina la msichana mwingine likaanza kujirudia kichwani mwake. Stacie, lilikuwa jina la mtu pekee ambaye alionekana kuwa na pingamizi kubwa la yeye kuwa na Albertina. Historia ya kimapenzi ambayo alikuwa nayo pamoja na Stacie ikaonekana kuanza kumchanganya kabisa kichwa chake. Wazazi wake walikuwa wakimfahamu sana Stacie na kila siku walikuwa wakitamani sana mtoto wao, Alan awe pamoja na msichana Stacie lakini kwa Alan katika kipindi hicho hakuonekana kuwa tayari kuwa na Stacie.
Ni kweli alimchukulia Stacie kuwa kama mpenzi wake, walikuwa wakifanya mengi isipokuwa mapenzi tu. Stacie akawa amekufa na kuoza kwa Alan lakini kwa Alan mambo yalionekana kuwa tofauti kabisa. Alimpenda Stacie lakini hakuwa akimpenda kama vile alivyotakiwa kumpenda. Hakutaka kuwaambia wazazi wake kwamba Stacie hakuwa chaguo lake kwa sababu tu katika kipindi kile hakukutana na msichana ambaye alitokea kumpenda zaidi ya Stacie.
Barani Afrika ndani ya nchi ya Tanzania katika jiji la Dar es Salaam ndipo ambapo Alan alikuwa amekutana na msichana ambaye alikuwa ametokea kumpenda kuliko msicha ayeyote yule, msichana huyu alikuwa Albertina. Albertina ndiye alionekana kuwa msichana wake sahihi ambaye alikuwa amezaliwa kwa ajili yake na si Stacie kama wazazi wake walivyokuwa wakifikiria. Alikuwa tayari kufanya lolote juu ya Albertina, hakutaka kumkosa msichana huyo, hata kama wazazi wake walikuwa wakitaka amuoe Stacie, kwake kitu hicho kisingeweza kukubalika kabisa, yeye alikuwa akimtaka Albertina tu.
“Why are you doing this to me? (Kwa nini unajifanyia hivi?)” Alan alimuuliza Albertina.
“How am I suppose to love you, Alan? I know that you real love me, but I can’t go back ( Natakiwa kukupenda vipi Alan? Najua kwamba unanipenda lakini siwezi kurudi nyuma)” Albertina alimwambia Alan.
“Pleaseee (Tafadhaliiii)”
“I CAN’T (SIWEZI)” Albertina alimwambia Alan na kisha kusimama na kuondoka mahali hapo.
Huo kama ukaonekana kuwa msimamo wake wa mwisho ambao alikuwa amejiwekea, akaelekea chumbani kwake na kujilaza kitandani. Kila wakati Alan alipokuwa akiongea maneno ya kimapenzi yalimfanya kumkumbuka Kelvin. Hakujiona kama aliruhusiwa kupenda ndani ya dunia hii, kwa jinsi alivyokuwa amempenda Kelvin hakuamini kama ingetokea siku ambayo mwanaume huyo angeweza kumkataa kwa sababu ya mama yake.
“Wanaume wote hawafanani Albertina. Inawezekana ulikuwa ukiyalazimisha mapenzi kwa Kelvin na wakati hakuwa mwanaume sahihi katika maisha yako. Kwa jinsi ulivyonielezea, nadhani Alan ni mwanaume sahihi katika maisha yako” Bi Janeth alimwambia Albertina.
“Mama! Wanaume wanafanana mama” Albertina alimwambia mama yake.
“ Sidhani kama Alan yupo hivyo. Amekuja kwako moja kwa moja na kukwambia kwamba anataka kukuoa, kwa nini usimpe nafasi ya kumsikiliza na kukubaliana nae? Hii inaweza kuwa nafasi yako Albertina, nafasi hii inaweza isijirudie tena katika maisha yako, inawezekana kamwe usimpate mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kwako endapo utamuacha Alan aondoke bila kukubaliana nawe” Bi Janeth alimwambia Albertina.
*****CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila kitu alichokuwa amejaribu kukifanya kikaonekana kuwa si kitu chochote kwani bado Albertina alikuwa akiendelea kukataa kuwa nae. Alan akaonekana kuwa mnyonge, moyo wake ukakosa amani mpaka kufikia kipindi ambacho akaanza kujuta. Alijuta sababu iliyomfanya kuja nchini Tanzania ambapo ndipo alipokutana na Albertina na kujikuta akiingia katika mzigo mzito wa mapenzi huku msichana huyo akionekana kutokujali kitu chochote kile.
Hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kuishi mara atakaporudi nchini Marekani siku inayofuatia. Hakupenda kurudi nchini Marekani huku moyo wake ukiwa katika mzigo mzito wa mapenzi juu ya msichana ambaye hakuwa akimhitaji, alikuwa akitamani sana kukamilisha kila kitu lakini tatizo lilikuwa lile lile kwamba Albertina alikuwa amemkataa.
Usiku hakulala, alikesha huku akimfikiria Albertina, alishindwa kabisa kumtoa moyoni msichana huyo, alipogeuka huku, alikuwa akimfikiria Albertina na hata alipogeukia upande mwingine bado alikuwa akimfikiria Albertina tu. Alan alijua kwamba nchini Marekani kulikuwa na msichana aliyeitwa Stacie, msichana ambaye wazazi wake walikuwa wakimtaka kuwa nae kwa sababu nae alikuwa mtoto wa tajiri lakini Alan hakuonekana kuwa na muda wa kumfikiria Stacie tena.
Moyo wake ukazama kwa msichana wa kitanzania, msichana ambaye alikuwa na kila sifa ya kuitwa mrembo mbele ya macho yake. Kitendo cha kumkosa Albertina kikaonekana kumuumiza sana, hakutarajia kama ingetokea siku ambayo angekuja kukataliwa na msichana ambaye alitokea kumpenda kwa mapenzi yote moyoni mwake, kwake aliamini kwamba kama Mungu alikuwa amempangia msichana fulani basi ilikuwa ni lazima ampate.
“Au kuna jambo Mungu anajaribu kuniepushia?” Alan alijiuliza.
“Inawezekana” Alijijibu.
Siku ya safari ya kurudi nchini Marekani ikaingia, kwa sababu siku hiyo ndege ya shirika la American Airlines ilikuwa ikiondoka saa tano asubuhi tofauti na siku nyingine ambapo huwa inaondoka usiku wa manane, saa mbili asubuhi Alan tayari alikuwa amekwishajiandaa na ni Brian ndiye ambaye alikuwa akimsikilizia kwa ajili ya kuondoka hotelini hapo na kuelekea uwanja wa ndege.
Saa tatu kasoro asubuhi Brian akaingia ndani ya eneo la hoteli hiyo huku akiwa ndani ya gari lake, akamtaka Alan kuingia garini kwa ajili ya kuondoka mahali hapo. Alan hakuonekana kuwa na furaha, bado alionekana kuwa mnyonge kupita kawaida, alipoingia ndani ya gari na macho yake kukutana na macho ya Albertina ambaye alikaa kiti cha nyuma, Alan akaonekana kushtuka.
“Karibu” Albertina alimkaribisha Alan huku uso wake ukiwa na tabasamu pana.
Alan hakuonekana kuamini, wakati mwingine alijiona kama alikuwa katika usingizi mzito ambapo baada ya muda fulani angeshtuka na kujikuta akiwa kitandani. Hakuamini kama Brian alikuwa amekuja pamoja na Albertina kwa ajili ya kumsindikiza kuelekea uwanja wa ndege. Albertina alikuwa katika kiti cha nyuma huku Brian na Alan wakiwa katika viti vya mbele, muda wote Alan alionekana kuwa na furaha tele, uwepo wa Albertina ndani ya gari lile ukaonekana kumpa furaha kupita kawaida.
Hawakuchukua muda mrefu wakawa wamekwishafika uwanja wa ndege. Alichokifanya Brian ni kuteremka kutoka garini na kuwaacha wawili hao ndani ya gari. Alan akaonekana kutokuridhika, akatoka pale katika kiti cha mbele na kuelekea katika kiti cha nyuma, wakabaki wakiangaliana tu.
“Ujio wako unamaanisha nini?” Alan alimuuliza Albertina huku akionekana kutabasamu.
“Unahisi unamaanisha nini?” Albertina nae akauliza.
“Umeniacha njia panda” Alan alimwambia Albertina.
Alichokifanya Albertina ni kumsogelea, akahakikisha kwamba uso wake upo karibu na uso wa Alan na kisha kumbusu shavuni. Alan akashtuka, kila kilichokuwa kikiendelea mahali hapo kilionekana kama ndoto moja nzuri ambayo alikuwa akiitamani katika maisha yake yote. Albertina hakuishia hapo, akaupeleka mkdomo wake katika mdomo wa Alan na kisha kuanza kubadilishana mate. Kwa kile kitendo kilichokuwa kimetokea, tayari kilionyesha kwamba ukurasa wa mapenzi kati ya watu hao wawili ulikuwa umekwishafunguliwa.
“Umekuwa wangu hatimae” Alan alimwambia Albertina.
“Naomba usiniumize” Albertina alimwambia Alan huku akiwa amekiinamisha kichwa chake kifuani mwa Alan.
“Nakuahidi kutokukuumiza” Alan alimwambia Albertina.
Hilo ndio lilionekana kuwa tukio la kwanza la furaha ambalo lilikuwa limetokea katika maisha yake yote. Moyo wake ukalipuka kwa furaha, hakuamini kwamba msichana ambaye alikuwa akimhitaji siku zote hatimae alikuwa amekuwa mpenzi wake na alionekana kuwa tayari kufunga nae ndoa. Alan akateremka kutoka garini, akamsogelea Brian na kisha kumkumbatia huku wote wawili wakionekana kuwa na furaha.
“Nashukuru kwa kila kitu. Nakuahidi kutokumuumiza Albertina” Alan alimwambia Brian.
“Hakikisha unafanya hivyo. Nakuamini” Brian alimwambia Alan.
Wakaagana mahali hapo na kisha Alan kuanza kupiga hatua kuufuata mlango wa kuingilia ndani ya jengo la uwanja wa ndege. Majonzi aliyokuwa nayo, mawazo ya maumivu aliyokuwa nayo katika kipindi hicho kila kitu kikaonekana kubadilika kabisa. Majonzi yakawa furaha huku maumivu yale ya moyo yakiwa yamebadilika na kuwa faraja yake.
“STACIE…!” Lilikuwa ni jina ambalo lilijirudia kichwani mwa Alan, tayari akaona kulikuwa na kitu kikubwa kingetokea endapo angewaambia wazazi wake kwamba alikuwa amempata msichana ambaye aliamini kwamba aliletwa duniani kwa ajili yake, ila pamoja na hayo, hakujua Stacie angelichukuliaje suala hilo.
Stacie Bruce alikuwa miongoni mwa wasichana warembo ambao walikuwa wakisoma katika chuo cha Cornell kilichokuwa katikati ya jiji kubwa la New York. Stacie alikuwa na kila sifa za kuitwa msichana mrembo kati ya wasichana wote ambao walikuwa wakisoma katika chuo hicho namba moja kwa kutoa elimu bora ndani ya jiji la New York huku kikifuatiwa na chuo cha Columbia kilichokuwa kusini mwa jiji hilo.
Stacie alikuwa mtoto wa tajiri mkubwa nchini Marekani, tajiri ambaye alikuwa na utajiri uliomfanya kununua magari ya kifahari, nyumba kubwa pamoja na kufungua biashara nyingi, Bwana Bruce Thomson. Stacie alikuwa msichana mrembo aliyejitambua. Chuoni hapo alikuwa akiishi kifahari, alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha fedha kila siku chuoni hapo kitu ambacho mpaka wakati mwingine marafiki zake walikuwa wakimshangaa.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Stacie hakuzionea huruma fedha za baba yake, kwa sababu alizaliwa katika familia iliyokuwa na fedha, kichwa chake kila wakati kilikuwa kikifikiria kutumia fedha tu. Alibadilisha magari aliyotaka, kila mwisho wa wiki alikuwa na mazoea ya kwenda katika maduka makubwa ya nguo za wanawake na vipodozi kwa ajili ya kufanya shopping tu huku akiwa na marafiki zake.
Stacie aliringia fedha za baba yake, kila siku alikuwa akitumia fedha alivyotaka. Chuoni alikuwa akiishi kitajiri zaidi ya mwanachuo yeyote yule kitu ambacho kwa wanachuo wengine hali hiyo ikaonekana kuwa kama kero. Japokuwa alikuwa na fedha, alikuwa akipata kila alichokuwa akikitaka, kuna kitu ambacho Stacie hakuonekana kubarikiwa kuwa nacho, hiki kilikuwa ni mwanaume.
Wanaume wengi chuoni hapo walikuwa wakimuogopa Stacie. Ni kweli alionekana kuwa msichana mrembo ambaye alivutia mbele ya macho ya kila mwanaume lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa radhi kumfuata Stacie. Matumizi yake ya yalikuwa makubwa kupita kawaida, wanaume walikuwa wakiiangalia mifuko yao. Walijua fika kwamba kuwa na msichana kama Stacie ilikuwa ni kujitoa mhanga kwani alizaliwa katika sehemu iliyokuwa na fedha hivyo starehe ilikuwa sehemu ya maisha yake.
Kama wasichana wengine, Stacie alikuwa akitamani sana kufuatwa na mwanaume na kuambiwa maneno ya mapenzi. Hiyo ndio ilikuwa kiu katika maisha yake lakini hakukuwa na mwanaume ambaye alikuwa radhi kumfuata Stacie. Mara nyingi alikuwa akiwaona wanaume ambao kwa moyo mmoja alikuwa ametokea kuwapenda lakini hakujua angeanzia wapi, hakutaka kumfuata mwanaume na kumwambia kwamba anampenda kwa sababu uso wake ulikuwa umejawa na aibu.
Mapenzi yakamtesa, moyo wake ukatamani kuwa na mwanaume lakini hiyo kwake ikaonekana kuwa kama ndoto, ndoto ambayo kamwe aliiona isingeweza kutokea katika maisha yake. Kila alipokuwa akimuona msichana akiwa na mpenzi wake moyoni mwake Stacie alikuwa akijisikia wivu kupita kawaida, alitamani nae itokee siku ambayo ingemfanya kuwa na mwanaume, ambusu kama wapenzi wengine walivyokuwa wakibusiana na hata kutembea pamoja lakini jambo hilo likaonekana kama ndoto kutokea.
“Ninatamani kupenda” Stacie alimwambia rafiki yake, Esther.
“Kwani haupendi?” Esther alimuuliza.
“Pamoja na hayo, ninapenda kupendwa pia, ninataka kupenda pale nitakapopendwa” Stacie alimwambia Esther.
“Umetokea kumpenda nani hapa chuoni?” Esther alimuuliza.
“Nimetokea kuwapenda wengi lakini naona hakuna hata mwenye wazo na mimi. Mapenzi yananitesa sana moyoni” Stacie alimwambia Esther.
“Pole sana. Ila jaribu kumfuata mwanaume na kumwambia kuhusu hisia zako” Esther alimwambia.
“Hapana. Ninaogopa”
“Unaogopa nini?”
“Nitaanzia wapi?”
“Mbona rahisi tu. Unamfuata na kumwambia. Wewe unampenda nani nikusaidie kumwambia?” Esther alimuuliza Stacie
“Raymond”
“Sawa. Nitafanya hivyo. Sitaki kukuona ukiwa na mawazo kila siku. Nitahakikisha unampata Raymond na kuwa na furaha maishani mwako” Esther alimwambia Stacie.
Raymond Robert alikuwa miongoni mwa wavulana ambao walikuwa wakichukua masomo ya sanaa chuoni hapo. Raymond alikuwa kijana mtanashati ambaye muda mwingi alionekana kuwa na furaha huku akipenda sana kuongea na watu. Ucheshi wake ambao alikuwa akiuonyesha kwa kila mtu chuoni hapo ndio ambao uliwafanya wanachuo wengi kumpenda huku wasichana wengi wakitamani kuwa nae.
Pamoja na ucheshi wake wote huo, Raymond alikuwa na ndoto kubwa ndani ya moyo wake ndoto ambayo ilikuwa ikimtesa kila siku katika maisha yake. Toka katika kipindi ambacho alikuwa mdogo, moyo wake ulikuwa ukitamani sana kuwa muigizaji. Aliweza kushiriki katika mashindano mbalimbali ya uigizaji yaliyokuwa yakiandaliwa na kampuni mbalimbali za Hollywood kama Columbia Pictures, Marvel, 20 Century na mengine mengi lakini huko kote hakuwa akipata nafasi jambo ambalo lilikuwa likimuumiza sana moyoni mwake.
Ndoto zake zilikuwa ni kutamani kuwa kama mchekeshaji Jimmy Carey. Mara kwa mara alikuwa akiziangalia filamu za muigizaji huyo kitu ambacho kilimpa shauku kubwa ya kuwa kama Jimmy Carey lakini aliona dhahiri kwamba waandaaji wa mashindano ya uigizaji walikuwa wakimnyima nafasi ya kutimiza ndoto hiyo ambayo kila siku alikuwa akitamani sana itokee katika maisha yake.
Siku ziliendelea kwenda mbele lakini ndoto yake haikuweza kutimia. Mara kwa mara alikuwa akienda katika usaili wa uigizaji lakini bado alionekana kutokuwa tayari kusaini mkataba wa kuanza kuonekana katika filamu mbalimbali ambazo zilikuwa zikitengenezwa na kampuni hizo katika jiji la Hollywood. Raymond hakukata tamaa mpaka katika kipindi kile ambacho alifanikiwa kupitishwa na kuwa muigizaji kama mhudumu wa hotelini katika filamu iliyotamba sana miaka hiyo, filamu ya Coming to America.
Kwa kiasi fulani akaona kwamba ndoto yake ilikuwa ikienda kutimia, Kila siku akawa mtu wa kujifungia chumbani na kuanza kuigiza mbele ya kioo huku chumba chake kikiwa kimetawaliwa na picha za Jimmy Carey ambazo alikuwa amezibandika ukutani. Maisha yaliendelea zaidi, baada ya kusaini mkataba wa kuonekana japo kidogo katika filamu hiyo, hakuitwa tena kuigiza filamu yoyote ile jambo ambalo lilimuonyeshea kwamba inawezekana hakuwa amefanya vizuri katika filamu ile.
Leo hii, huyu Raymond ambaye alikuwa na ndoto za kuwa muigizaji mkubwa duniani alikuwa ametokea kupendwa na msichana mrembo, Stacie ambaye alikuwa mtoto wa tajiri mkubwa nchini Marekani, Thomson Bruce. Raymond hakuwa akifahamu kitu chochote kile, ishara zote ambazo msichana Stacie alikuwa akijaribu kumuonyeshea wala hakuwa akizitambua, alionekana kuzipuuzia kabisa.
Hakutaka kuwa na msichana yeyote yule, alikuwa akitaka kukamilisha malengo yake ambayo alikuwa amejiwekea na ndipo hapo ambapo angekuwa na uhitaji wa kuwa na msichana yeyote yule. Alijiona kuwa mbali na malengo yake, alikuwa na uhitaji wa kukamilisha kila alichokuwa akikihitaji na ndipo ambapo angeamua kwa moyo mmoja kuingia katika mapenzi.
“Does she love me? (Ananipenda?)” Raymond alimuuliza Esther huku akionekana kushtuka.
“Yes. She loves you. She has been telling me about you everyday (Ndio. Anakupenda sana. Amekuwa akiniambia kuhusu wewe kila siku)” Esther alimwambia Raymond.
“Impossible (Haiwezekani)”
“Why? (Kwa nini?)”
“I don’t know what to say (Sijui niseme nini)” Raymond alisema huku akikishika kiuno chake kwa mikono miwili na uso wake kuuinamisha chini.
“She real loves you. She wants to be with you (Anakupenda. Anataka kuwa na wewe)”
“Why didn’t she come and tell me? (Kwa nini hakuja kuniambia?)”
“She feels shame (Anajisikia aibu)”
“Are you sure (Una uhakika)?”
“Yes”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“How do I look? Do I look like Jimmy Carey (Kwani naonekana vipi? Kama Jimmy Carey)?”
“I don’t know (Sijui)”
“No. I cant be with her (Hapana. Siwezi kuwa nae)”
“Why (Kwa nini)?”
“I can’t date her right now. I have nothing Esther, just look at me, what do I have? Just tell her to wait, I don’t deserve her right now (Siwezi kutoka nae kimapenzi kwa sasa. Sina chochote kile Esther, hebu niangalie, nina nini? mwambie asubiri, simstahili kwa sasa)” Raymond alimwambia Esther.
“Raymond, Stacie loves you (Raymond, Stacie anakupenda)”
“Go and tell her that I am not ready, or until I become great actor (Kamwambie sipo tayari, au mpaka niwe muigizaji mkubwa)” Raymond alimwambia Esther.
Maisha ambayo alikuwa akiyaishi Stacie chuoni hapo yalionekana kuwaogopesha wanaume mbalimbali. Kila mwanaume alikuwa akimuogopa Stacie. Maisha yake yalionekana kuwa ya gharama kubwa sana jambo ambalo lilionekana kuwa kizuizi kikubwa kwa wanaume kumfuata na kutaka mahusiano ya kimapenzi pamoja nae.
Mara baada ya kuambiwa kile ambacho Raymond alichokuwa amekisema, hapo ndipo ambapo Stacie akaamua kubadilika, maisha ya gharama ambayo alikuwa akiyaishi akaamua kuyaacha na kuishi kama wanachuo wengine chuoni hapo. Gari yake ambayo alikuwa amenunua dola laki mbili akaachana nalo na kununua gari la kawaida la dola elfu tano na kuanza kutembea nalo. Wanachuo wakaonekana kumshangaa sana Stacie lakini yeye hakuonekana kujali, kitu alichokuwa akikihitaji ni kuwa na mwanaume tu.
Hali ile ilihitaji muda mrefu mpaka kuzoeleka na si mara moja tena kwa haraka sana. Stacie akavumilia, akawa mtu wa maisha ya kawaida. Japokuwa yalikuwa ni maisha magumu lakini aliona ni bora kupigana nayo kila siku. Hakuwa mtu wa kwenda kufanya shopping kila mwisho wa wiki kwa kununua nguo za gharama pamoja na marafiki zake. Wakati huo akawa amebadilika, akawa mtu wa kwenda shopping kila baada ya miezi mitatu tena huko akienda kununua nguo za kawaida kwa gharama ya chini kabisa.
Hayo ndio maisha ambayo alikuwa ameyaingia, aliamua kuishi maisha hayo kwa sababu tu alikuwa akihitaji mwanaume ambaye angeamua kuwa nae. Kwa wale ambao walikuwa wamemzoea waliona dhahiri alikuwa akiigiza bila kufahamu lengo lake la kufanya vile lakini kwa wale ambao walikuwa wakiendelea kujiunga na chuo kile walimuona kuwa msichana wa chini ambaye hakuwa na maisha mazuri sana.
****
Vyuo vingi nchini Marekani vilikuwa na utaratibu wa kukutana kila baada ya miezi sita kwa ajili ya kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusiana na masomo huku lengo jingine likiwa ni kuanzisha urafiki mpya kutoka kwa wanachuo wengine ambao hawakuwa wakifahamiana. Tukio hili huwa hufanyika mara moja kila baada ya miezi sita na hufanyika katika uwanja mkubwa wa FedEx Field ambao unaingiza zaidi ya watazamaji elfu tisini na moja na unaomilikiwa na timu inayoshiriki ligi ya NFL, timu ya Washington Redskins.
Katika mwaka huu, kama kawaida wanachuo wengi walikuwa wamejiandaa kwa ajili ya kwenda katika uwanja huo ambapo huko wangekaa pamoja kuanzia asubuhi mpaka jioni huku kila mmoja akiwa na lengo la kukutana na marafiki wapya na kuanzisha urafiki na hata wengine kuanzisha mahusiano. Japokuwa katika vipindi vyote tukio kama hili linapotokea huwa Stacie si mtu wa kwenda huko, katika kipindi hiki nae akaamua kuelekea huko kwa ajili ya kuangalia kama kulikuwa na uwezekano wa kumpata mtu ambaye angeweza kuanzisha nae mahusiano.
Lengo lake ambalo lilimpeleka katika uwanja huo likaonekana kutimia mara baada ya kukutana na Alan Kurt, mtoto wa tajiri Kurt ambaye mara ya mwisho alionana nae miaka miwili iliyopita. Kuonana kwao kukamfanya kila mmoja kuwa na furaha, wakakumbatiana na kuanza kuzungumza mambo mengi kuhusiana na maisha pamoja na masomo.
Kwa jinsi muonekano aliokuwa nao Stacie ulivyoonekana, tayari alionyesha kuwa na kila dalili za kuvutiwa na Alan ambapo akamtaka kuwasiliana nae mara kwa mara jambo ambalo kwa Alan wala halikuwa na tatizo lolote lile. Hapo ndipo mawasiliano yao yalipoanza. Walianza kama marafiki huku Stacie akiwa na wazo lake kichwani mwake. Kila alipokuwa akijaribu kuingizia hisia zake kupitia mazungumzo, Alan alikuwa akimtoa na kumuweka katika njia nyingine kabisa.
Stacie hakuwa akiipenda hali hiyo, alikuwa akitamani kuchiwa nafasi ya kuzungumza mambo mengi kuhusiana na mahusiano. Kitendo cha Alan kumtoa katika maongezi ya mahusiano na kumpeleka katika maongezi mengine kikaonekana kumkosesha raha mpaka pale alipoamua kulitoa dukuduku lake la moyoni.
“Unanitania” Alan alimwambia Stacie kupitia simu.
“Huo ndio ukweli. Nimetokea kukupenda Alan, nimejaribu kuzificha hisia zangu lakini naona kwamba nimeshindwa. Naomba uwe wangu Alan” Stacie alimwambia Alan kwa sauti ya kinyonge iliyojaa mahaba.
“Mbona bado mapema mno Stacie”
“Hapana. Kwangu naona huu ni muda muafaka, nahisi utachukuliwa na mimi kukukosa maishani mwangu. Ninakuhitaji Alan” Stacie alimwambia Alan.
“Unajua kwamba mapenzi yanaumiza?” Alan alimuuliza Stacie.
“Najua”
“Una uhakika kwamba mimi ni chaguo lako?”
“Nina uhakika”
“Mbona moyo wangu unakataa hilo Stacie?”
“Nina uhakika Alan. Najua moyo wako unakataa lakini kuna siku utakuja kukubaliana na moyo wangu. Wewe ni chaguo langu na ninatumaini mimi ni chaguo lako pia” Stacie alimwambia Alan.
“Sipendi kukumiza Stacie. Wasiwasi wangu ni pale ambapo nitahisi kitu cha tofauti kwa msichana mwingine Stacie” Alan alimwambia Stacie.
“Alan. Tafadhali, kuwa wangu, ninakupenda sana”
“Najua Stacie lakini…..”
“Alan naomba uniambie ukweli. Una mwanamke?”
“Hapana”
“Sasa tatizo lipo wapi?”
“Hakuna tatizo”
“Ninakuhitaji. Nimeshindwa kuvumilia, moyo wangu umekuwa mgumu kuvumilia zaidi. Ninahitaji kukuona hata kesho” Stacie alimwambia Alan.
“Siwezi kuja New York kwa kesho. Au uje Mississippi” Alan alimwambia Stacie.
“Nitakuja. Kwa ajili yako, nitakuja”
“Sawa. Ukija tutaongea vizuri” Alan alimwambia Stacie na kisha kukata simu.
Huo ukaonekana kuwa mwanzo wa kila kitu. Siku iliyofuatia Stacie akajipanga na kisha kuelekea jijini Mississippi. Huko akaonana na Alan ambapo mapenzi yakaanza japokuwa moyo wa Alan ulionekana kuwa mgumu kukubaliana na Stacie. Stacie hakuonekana kujali, kitu ambacho alikuwa akikifahamu ni kwamba mwanzo moyo wa kila mtu huwa mgumu lakini mara baada ya kuzoeana kila kitu huwa kawaida na mapenzi kuchipuka.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwaka wa kwanza wa mapenzi yao ukapita na kuingia mwaka wa pili. Wote wakatambulishana kwa wazazi wao kwamba walikuwa wapenzi walioshibana ambao walikuwa na lengo la kufunga ndoa hapo baadae. Wazazi wakaonekana kufurahi kwa sababu wote wawili walikuwa ni watoto wa matajiri hivyo wala hakukuonekana kuwa na tatizo lolote lile.
Kwa Alan alijiona kuwa tofauti sana. Alijua fika kwamba kwa wakati huo Stacie alikuwa msichana wake lakini wala hakuonekana kuwa na furaha ile inayotakiwa mara mtu anapokuwa na mpenzi. Walifanya mambo mengi kama wapenzi lakini bado moyo wa Alan haukuonekana kuridhika kabisa kitu ambacho kilimfanya kuona kwamba Stacie hakuwa msichana ambaye alipangwa kuwa pamoja nae.
Mwaka wa pili wa mahusiano yao ukaingia, bado waliendelea kuwa pamoja huku moyo wa Alan ukiwa kama ulivyokuwa. Furaha haikuwepo moyoni mwake japokuwa kila alipokuwa na Stacie uso wake ulikuwa ukionyesha tabasamu pana. Kila siku wakawa watu wa kutoka na kuelekea sehemu mbalimbali kwa ajili ya starehe tu. Walikwenda katika kisiwa cha Hawaii kula raha huku wakati mwingine wakielekea mpaka katika visiwa vilivyokuwa na hewa safi kuliko sehemu zote duniani, visiwa vya Tasmania vilivyokuwa nchini Australia lakini huko bado hakukuonekana kumpa furaha Alan kama ambayo alitakiwa kuwa nayo kila mwanaume hasa anapokuwa na mpenzi wake.
“Kuna kitu nimekosa moyoni, najiona kutokuwa sawa. Hiki ni kitu gani? Ina maana Stacie si mwanamke ambaye ninatakiwa kuishi nae?” Alan alijiuliza lakini hakupata jibu lolote lile.
Mwaka wa tatu ukaingia, hali ilikuwa vile vile. Mwaka wa nne ulipoingia ndipo hapo ambapo walipanga kufunga ndoa. Hilo halikuonekana kuwa tatizo, wakakubaliana na siku ya ndoa kupangwa, ilikuwa miezi kumi na mbili mbele. Bado moyo wa Alan ulikuwa vile vile, hakuonekana kuyafurahia mapenzi kama alivyopaswa kuyafurahia.
Kama ilivyokuwa kwa wapenzi wengi ndivyo ilivyokuwa hata kwao pia. Kugombana mara kwa mara ilikuwa ni sehemu ya maisha yao. Leo walikuwa wakigombana kwa ajili ya hili na siku nyingine walikuwa wakigombana kwa ajili ya lile. Ugomvi huo wa mara kwa mara ndio ambao ulimhakikishia Alan kwamba Stacie hakuwa mwanamke sahihi katika maisha yake.
Kila alipokuwa akigombana na Stacie, Alan alikuwa akisafiri na kuelekea sehemu yoyote ile duniani kwa ajili ya kupumzisha akili. Huko alikuwa akikaa kwa wiki mbili na kisha kurudi nchini Marekani. Hivyo ndivyo alivyokuwa akifanya kila alipokuwa akigombana na Stacie.
Katika kipindi hiki ambacho alikuwa amegombana na Stacie, Alan aliamua kuelekea nchini Tanzania kwa ajili ya kuipumzisha akili yake kwa kumtembelea rafiki yake wa siku nyingi, Brian. Katika safari yake ya nchini Tanzania ndipo ambapo akakutana na Albertina. Siku ya kwanza ambayo alimtia machoni msichana huyo, akauhisi moyo wake kuingiwa na kitu ambacho alikuwa amekikosa katika maisha yake ya nyuma, alikiona kile kitu ambacho Stacie alishindwa kumuwekea kikiwa kimeingizwa moyoni na msichana huyu ambaye alikuwa amemtia machoni siku hiyo.
Mapenzi yakamtawala moyoni, furaha kubwa ikampata na kuona kwamba huyo ndiye alikuwa mtu ambaye alipangiwa kuishi nae katika maisha yake. Alan akajikuta akiangukia katika mikono ya Albertina ambaye alimfanya kumsahau Stacie, msichana ambaye alitarajia kumuoa baada ya mieizi kumi na mbili huku wazazi wao wakiwa wanafahamu kila kitu kuhusiana na mahusiano yao. Alan hakuonekana kujali sana, kitu ambacho alikuwa akikitafuta kwa muda mrefu, leo kilikuwa kimeingia moyoni mwake na kujiona mtu wa tofauti sana.
Msichana Albertina akawa amekiweka kitu hicho moyoni mwake, furaha ikampata, amani ikamuingia, moyo wake ukaburudika na kuona kwamba piga ua, ilikuwa ni lazima kuwa pamoja na Albertina, hata kama wazazi wangesema nini au Stacie kuamua uamuzi gani, yeye moyo wake ulikuwa kwa Albertina tu, yaani piga ua, angehakikisha kwamba anamuoa Albertina kwani ndiye msichana ambaye alimini kwamba angempa furaha ile ambayo alikuwa akiitaka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndani ya ndege Alan alionekana kufarijika, muda mwingi alionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Kitendo cha Albertina kukubali kuwa wake kikimpa furaha isiyo kawaida. Kwa miaka mingi ambayo alikuwa ameishi, katika kipindi hicho ndicho ambacho alikuwa amekipata kile kitu alichokuwa akikitafuta, kitu ambacho kilihitajika kuwa moyoni mwa kila mtu ambaye alikuwa na mpenzi aliyekuwa akimpenda.
Moyo ukafarijika, akajiona kuwa katika hali ya tofauti kabisa. Akili yake kwa wakati huo ilikuwa ikifikiria ndoa tu. Hakutaka kumuoa Stacie, alikuwa akitaka kumuoa Albertina ambaye alikuwa msichana pekee ambaye moyo wake ulikuwa umemchagua kwa asilimia zote. Kichwa chake bado kilikuwa kikiendelea kufikiria maneno ambayo angekwenda kuwaambia wazazi wake na hata Stacie mwenyewe ili apate kueleweka. Hakujua ni maneno gani ambayo alipaswa kuwaambia kuhusiana na Albertina, hakutaka kujua kama Stacie angeumia au la, yeye alichokuwa akikitaka ni kuwaambia ukweli tu.
“Lakini nampenda sana Albertina, siwezi kumuoa Stacie, acha niwe na Albertina tu” Alan alijisemea katika kipindi ambacho safari ilikuwa ikiendelea.
Hayo ndio maisha ambayo alikuwa akiyataka kila siku. Alan hakutaka kujionyesha kwamba alikuwa mtoto wa tajiri, japokuwa baba yake alikuwa amemnunulia ndege binafsi ya kutembelea kwenda sehemu mbalimbali duniani lakini Alan hakutaka kuitumia. Ndege ilikuwa imenunuliwa toka miaka mitano iliyopita lakini alikuwa ameitumia mara moja tu kwa kwenda Dubai kutembea na baada ya hapo hakuwahi kuitumia tena.
Kila siku alikuwa akitaka kuishi kama watu wengine walivyokuwa wakiishi, hakutaka kuishi maisha ya kujiachia na kula bata kama walivyokuwa wakifanya watoto wengine wa watu wenye fedha. Hayo ndio yalikuwa maisha yake ya kila siku, ndani ya ndege, kila mtu alimuona kuwa mtu wa kawaida aliyekuwa na fedha za kawaida na wakati ukweli ulikuwa ni kwamba alimiliki kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yake, kiasi ambacho alikuwa akiwekewa kila siku na baba yake.
Baada ya masaa ishirini na mbili, ndege ya American Airlines ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa King County uliokuwa katika jiji la Washington. Abiria wakateremka na kuanza kuelekea katika jengo la uwanja huo na baada ya mizigo kuchunguzwa Alan akatoka nje ambapo akachukua teksi na kisha kuelekea nyumbani.
“Ni maisha gani unayoishi Alan?” Lilikuwa ni swali la kwanza mara baada ya Bwana Kurt kummtia machoni Alan, alionekana kukasirika sana.
“Mbona naishi kawaida baba”
“Unaishi kawaida? Hebu jiangalie, unaishi tofauti, unayahatarisha maisha yako. Unataka niingie gharama kama ikatokea ukatekwa na watu wabaya. Nimekununulia ndege utumie, hautaki kutumia, nimekununulia magari yanayostahili kutumiwa na wewe tena yakiwa na uwezo wa kuzuia risasi, hautaki kuyatumia, unaishi vipi mtoto wangu? Unataka niingie gharama mara utakapotekwa na wabaya wangu?” Bwana Kurt alimuuliza Alan.
“Kwani ni lazima baba kuyatumia magari hayo? Kwa ni lazima kuitumia ndege hiyo baba? Najisikia raha kuishi kama ninavyoishi baba” Alan alimwambia baba yake huku begi likiwa mkononi mwake.
“Nahofia kuhusu maisha yako, nahofia kunaweza kukatokea watu wabaya watakaokuteka na kisha mimi kuingia gharama mtoto wangu. Nayapenda maisha yako, sitaki jambo baya litokee kwako na ndio maana najitahidi kufanya mengi kwa ajili yako kama kuyalinda maisha yako” Bwana Kurt alimwambia Alan.
“Najua baba”
“Hebu uridhishe moyo wangu, usitake niishi kwa presha muda wote. Ninakuhitaji sana mtoto wangu, sitaki kukupoteza maishani mwangu” Bwana Kurt alimwambia Alan.
Bwana Kurt aliongea maneno mengi wakati huo lakini maneno yale yalionekana kuingia katika sikio hili na kutokea katika sikio jingine. Bado kuishi katika maisha ya kifahari hakutaka kabisa kuishi, maisha ambayo alikuwa akipenda kuishi ni maisha ya kawaida na kuonekana kama watoto wengine wa kimasikini, hakutaka kuishi maisha kama aliyokuwa akiishi Paris Hilton.
Alan akatoka mahali hapo na kuelekea chumbani kwake. Kila siku Alan alikuwa akitamani kuhama nyumbani hapo lakini wazazi wake walikuwa wakimzuia. Hawakutaka Alan aishi mbali na macho yao, walikuwa wakitaka kumuona kila wakati ambao walikuwa na uhitaji wa kumuona. Kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo kulionekana kuwa na usalama zaidi wa maisha yake tofauti na jinsi ambavyo angekwenda kuishi katika nyumba yake mbali na wao walipo. Alan kwao alionekana kuwa kama dhahabu ambayo haikutakiwa kuwekwa mbali na macho yao.
Alan akafika chumbani kwake na kisha kukaa kitandani. Kitu cha kwanza alichokifanya ni kuelekea bafuni kuoga na kisha kutulia. Katika kipindi chote alikuwa akimfikiria mpenzi wake, Albertina. Aliuona huo ndio wakati pekee wa kuwaambia wazazi wake juu ya kile kilichokuwa kimetokea nchini Tanzania, Angeanzia wapi ili kueleweka? Hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima kuwaambia tu.
Alipojifikiria vya kutosha, akatoka chumbani hapo na kurudi sebuleni. Akakaa katika kochi kubwa na kuwaangalia wazazi wake machoni mwao. Alan akaonekana kuwa na jambo kubwa ambalo alikuwa akitaka kulizungumza mahali hapo. Bwana Kurt na Bi Bertha wakabaki kimya wakimwangalia Alan.
“I have found a girl of my life (Nimempata msichana wa maisha yangu)” Alan aliwaambia.
“What do you say? (Unasemaje?)” Bwana Kurt aliuliza huku akionekana kutokusikia vizuri.
“I have found a girl of my life (Nimempata msichana wa maisha yangu)” Alan alirudia maneno yake na kisha kubaki kimya.
“We know and that’s why we we continue to plan your wedding (Tunajua na ndio maana tunaendelea na mipango ya harusi yenu)” Bwana Kurt alimwambia Alan.
“I am not talking about Stacie , I am talking about Albertina, a girl I met in Tanzania (Simzungumzii Stacie, ninamzungumzia Albertina, msichana niliyekutana nae nchini Tanzania)” Alan aliwaambia wazazi wake, wote wakaonekana kushtuka.
“What do you say? (Unasemaje?)” Bi Bertha aliuliza kwa mshtuko.
“I am talking about Albertina. I love her (Hapa ninamzungumzia Albertina. NInampenda. Ameonekana kuwa msichana pekee mwenye kitu nilichokuwa nikikihitaji moyoni mwangu” Alan aliwaambia wazazi wake ambao wakabaki huku wakiangaliana.
“Who is Albertina? (Albertina ndiye nani?)”
“A girl I met in Tanzania (Msichana niliyekutana nae Tanzania)”
“Alan, are you out of your mind? (Alan, umechanganyikiwa)”
“No (Hapana)”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sit down and tell us what you said (Hebu kaa utuambie vizuri hicho unachokisema)”
“For a long time I’ve missed something in my heart. Although I was with Stacie but there was something that I hve missed in my heart. Its true that we loved each other but still there was something that missing in my heart. We used to walk together, we kissed each other and we did many things but I did not feel anything that a anyone who has girlfriend has to feel. After meeting with Albertina, I am feeling what I missed in my heart (Katika kipindi kirefu nimekuwa nikikosa kitu fulani moyoni mwangu. Japokuwa nilikuwa na Stacie lakini kulikuwa na kitu ambacho hakikuwepo ndani ya moyo wangu. Ni kweli Stacie alikuwa akinipenda na mimi kumpenda lakini kulikuwa na kitu ambacho kilikosekana moyoni mwangu. Tulikuwa tukitembea pamoja, tukibusiana na kufanya mambo mengi lakini sikuwa nikijisikia furaha kama ambavyo mtu alitakiwa kujisikia. Baada ya kukutana na Albertina, kitu hicho nimeanza kukisikia moyoni mwangu)” Alan aliwaambia wazazi wake ambao wakashusha pumzi ndefu.
“I think you have a problem Alan, its impossible to speak such words. Have a rest and tell us later because you are not okey right now (Nahisi una tatizo Alan, haiwezekani kuongea maneno kama hayo. Hebu kapumzike kwanza na kisha baadae utuambie vizuri kwa sababu naona haupo sawa kwa sasa)” Bwana Kurt alimwambia Alan ambaye akaamua kuondoka mahali hapo, hakutaka kubaki zaidi kwani tayari alikuwa amekwishawagusia wazazi wake juu ya kile kilichokuwa kikiendelea.
Bwana Kurt akabaki na mke wake, Bertha sebuleni pale, maneno ambayo aliyaongea Alan yalionekana kumshtua kila mmoja, hawakuelewa kama kijana wao alikuwa amemaanisha kile alichokuwa amekisema au alikuwa ameongea kiutani utani. Wakabaki wakijadiliana hasa kile ambacho walitakiwa kukizungumza mbele ya macho ya wazazi wa Stacie.
Hawakujua ni wapi wangetakiwa kuanzia, walijadiliana zaidi na zaidi na mwisho wa siku wakaona ni bora kuwaita wazazi hao pamoja na binti yao, Stacie na kisha kuwaambia kile alichokuwa amekizungumza Alan. Hivyo ndivyo walivyokubaliana wote wawili lakini kwanza kabla ya kuwaita wazazi hao pamoja na Stacie na kuongea nao ilitakiwa wamkalishe chini Alan na kuwaambia zaidi kile alichokuwa amewaambia.
Siku hiyo hawakutaka kumsumbua, wakamuacha apumzike mpaka siku iliyofuata ambapo saa tatu asubuhi wakamuita Alan na kisha kuanza kumuuliza maswali kadhaa kuhusu huyo Albertina ambaye alikuwa amemzungumzia siku iliyopita. Kila alichokuwa akiulizwa kuhusiana na Albertina, Alan hakutaka kuficha, alikuwa akiwaambia kila kitu huku wakati mwingine akizungumzia kila kitu kilichokuwa kimetokea nchini Tanzania.
“Kwa hiyo wewe na Stacie ndio basi tena?” Bwana Kurt alimuuliza Alan.
“Ndio. Sioni sababu ya kuwa na Stacie na wakati nimekutana na msichana ambaye ameufanya moyo wangu kukamilika” Alan alimjibu baba yake.
“Ila hiki ni kitu ulichokuwa umekipanga kabla kumuumiza Stacie?” Bi Bertha alimuuliza Alan.
“Hapana mama. Hiki ni kitu ambacho kimetokea ghafla na wala sikukitegemea kabisa. Kama nilivyowaambia kabla kwamba kwa Stacie kulikuwa na kitu ambacho nilikikosa moyoni mwangu, niliyahisi mapenzi yangu kwake kutokukamilika. Ila nilipokutana na Albertina, kiukweli moyo wangu umekamilika kwa asilimia mia moja” Alan aliwaambia wazazi wake.
Hilo ndio alilolisema Alan siku hiyo. Wazazi walimsikiliza kwa makini na kumuelewa na ni jambo moja tu ndio ambalo lilikuwa limebakia kwa wakati huo, kumuita Stacie na wazazi wake na kisha kuwaambia kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
Ilipofika saa saba mchana, Stacie na wazazi wake, Bwana Bruce na Bi Susie walikuwa ndani ya nyumba hiyo. Bwana Kurt, Bi Bertha na Alan nao walikuwa mahali hapo. Kila mmoja alikuwa kimya kwa muda, walikuwa wakiangaliana tu. Muda wote, Stacie alionekana kuwa mwenye furaha tele, alikuwa akimwangalia mpenzi wake, Alan huku akiachia tabasamu pana, alionekana kummisi sana mpenzi wake.
“Tumefika” Bwana Bruce aliwaambia.
Hapo ndipo ambapo Bwana Kurt alipoanza kuelezea baadhi ya mambo ambayo alitakiwa kuyaelezea mahali hapo. Kila mmoja alionekana kuwa kimya kumsikiliza. Alielezea kwa karibu dakika tano na ndipo alipomuachia Alan aendelee. Alan akaanza kuelezea toka siku ambayo alikuwa ameanza safari kuelekea nchini Tanzania kwa ajili ya mapumziko ya muda mchache mara baada ya kugombana na mpenzi wake, Stacie.
Alan aliendelea zaidi na zaidi, akaelezea kuhusu Albertina ambaye alikutana nae nchini Tanzania na kujikuta akianzisha mahusiano pamoja nae. Maneno yote ambayo aliyaongea Alan yakaonekana kuwa kama msumali wa moto uliokuwa na ncha kali moyoni mwa Stacie. Tabasamu ambalo alikuwa akilitoa, ghafla likapotea usoni mwake, mwili wake ukampigwa ganzi, japokuwa kulikuwa na kijibaridi, mwili wake ukaanza kutokwa na kijasho chembemba.
“Hicho ndicho kilichotokea nchini Tanzania” Alan aliwaambia na kisha kutulia.
Bwana Bruce na mkewe, Susie walibaki wakiangaliana, walionekana kutokuyaamini maneno ambayo aliyaongea Alan mahali hapo. Ni kweli alikuwa amekaa na binti yao kwa kipindi fulani kirefu lakini kwa wakati huo alikuwa amempata msichana mwingine ambaye alikuwa amempa furaha na kitu ambacho alikuwa amekikosa moyoni mwake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Stacie akabaki akitokwa na machozi na mwisho wa siku kuanza kulia kwa sauti kubwa. Hiyo ilionekana kuwa kama taarifa ya msiba moyoni mwake, hakuamini kwamba yule Alan ambaye alikuwa amempa mapenzi yake yote leo hii alikuwa ameamua kumuacha na kuangukia katika mapenzi ya msichana mwingine.
Alichokifanya Alan ni kusimama mahali hapo, akaanza kumfuata Stacie na kisha kumuinua na kutoka nae nje. Stacie alionekana kuumia lakini hakuwa na jinsi, kwa wakati huo alitakiwa kukubaliana na ukweli kwamba mtu ambaye alikuwa akimpenda, Alan alikuwa amempata msichana mwingine na hivyo alitakiwa kusahau kila kitu kuhusu Alan.
“Samahani Stacie, haina jinsi, ni lazima ukubaliane na ukweli kwamba wewe haukuwa mwanamke wangu sahihi” Alan alimwambia Stacie mara baada ya kutoka nje.
“Alan….Alan….” Stacie alijikuta akiita lakini hakuongea kitu chochote kile.
“Nadhani hata mimi si mwanaume wako sahihi, nakuomba umtafute mwanaume sahihi wa maisha yao. Tumekuwa tukigombana sana, hii ni moja ya dalili kubwa kwamba sisi hatutakiwi kukaa sehemu moja. Najua nimekuumiza sana lakini kukuumiza huku tegemea kwamba utakuja kupata furaha zaidi ya uliyokuwa ukiipata kutoka kwangu. Huu ni uamuzi mzito ambao nimeufanya lakini wakati mwingine haina jinsi, yatupasa kufanya uamuzi mgumu kwa ajili ya kupata furaha ndani ya maisha yetu” Alan alimwambia Stacie.
“Usiniache Alan….”
“Haina jinsi. Imekwishatokea Stacie. Wewe ni msichana mzuri, kuachwa na mimi haimaanishi kwamba wewe ni msichana mbaya. Kuna wanaume wengi wenye mapenzi ya dhati ambao wanataka kuwa na mwanamke mzuri kama wewe, amini kwamba kuna mwanaume sahihi wa maisha yako atakuja. Naomba uniache nianze mahusiano na Albertina, najua unaumia lakini haina jinsi, samahani sana Stacie” Alan alimwambia Stacie.
Katika kila neno ambalo alikuwa akiliongea mahali hapo liliendelea kuwa msumali wa moto moyoni mwa Stacie ambaye alibaki akilia tu. Kila alipokuwa akimwangalia Stacie, hata yeye moyo wake ulikuwa ukimuuma sana lakini hiyo haikuwa sababu ya kubadilisha uamuzi ambao alikuwa ameuamua katika kipindi hicho. Alijua kabisa kwamba Stacie hakuwa msichana wake sahihi na ndio maana alikuwa akikikosa kile alichokuwa akikihitaji sana moyoni mwake.
Alichokifanya Alan mahali hapo ni kuingia ndani ya gari lake na kisha kuondoka mahali hapo. Safari ambayo alikuwa ameipanga kwa wakati huo ni kwenda nchini Mexico kwa rafiki yake, Antonio. Yeye kama yeye alikuwa amedhamiria kwenda nchini Mexico kwa kutumia usafiri wa gari. Kitu ambacho alikuwa akikihitaji mahali hapo ni kwenda kuchukua ndege yake ambayo ilikuwa imepakiwa katika uwanja wa ndege wa King County.
Katika kipindi cha miaka ishirini na tatu, siku hiyo ndio ilikuwa siku yake ya kwanza kuelekea nchini Mexico. Alijua fika kwamba baba yake alikuwa akimkaza sana kwenda nchini Mexico huku akiwa hajui sababu ambayo ilimfanya kumzuia kwenda katika nchi hiyo. Siku hiyo ndio alikuwa amepanga safari ya kwenda nchini Mexico kisiri, hakutaka baba yake afahamu kama alikuwa akielekea katika nchi hiyo.
Alichokifanya ni kumpigia simu rubani wake na kumpa taarifa kwamba alikuwa akimhitaji katika uwanja huo wa ndege ndani ya dakika kumi kwa ajili ya safari fupi ya kuelekea Texas. Alan akamuonya rubani wake kwamba hakutakiwa kumpa taarifa baba yake kwamba alikuwa njiani kuelekea uwanja wa ndege na kuchukua ndege yake kwa ajili ya kuelekea katika jiji la Texas huku akitaka kuingia nchini Mexico kwa kutumia gari, kwani alijua fika endapo angetumia ndege, baba yake angeweza kumzuia uwanjani nchini Mexico kwani huko napo aliweka ulinzi, endapo Alan angeonekana basi arushwe, ilikuwa ni amri.
Moyo wake ulikuwa na hamu ya kumtembelea Antonio ambaye mpaka katika siku hiyo ilikuwa imepita miaka miwili hakuwa ameonana nae, alitaka kwenda kumtembelea huku ikiwa njia mojawapo ya kujiweka mbali na Stacie. Moyo wake uliamini kwamba endapo angeendelea kubaki nchini Marekani basi kuna siku ambayo ingemfanya kumuonea huruma Stacie na kubadilisha uamuzi wa kuendelea kuwa nae na hivyo kumuumiza Albertina.
“Ni bora kwenda Mexico, niwe mbali na nyumbani tu” Alan alisema katika kipindi ambacho alikuwa ameingia katika barabara kubwa ya St’ Barnabas, barabara kubwa ambayo ilikuwa ikielekea moja kwa moja mpaka katika uwanja wa ndege wa King County uliokuwa hapo hapo jijini Washington tayari kwa kuelekea Texas, jiji lililokuwa na asilimia arobaini ya jangwa huku watu wa huko usafiri wao mkubwa ukiwa farasi, watu ambao walikuwa wakifahamika vizuri kwa jina la Cowboys.
Kampuni nyingi zile kubwa zilikuwa zikizidi kufunguliwa duniani huku watu wakifanya biashara ambazo kila siku zilikuwa zikiwaingizia mamilioni ya fedha. Kampuni nyingi za magari ya kisasa zilikuwa zikifunguliwa huku biashara nyingine ambazo kila siku zilikuwa zikiingiza fedha nyingi zikiendelea kuongezeka kila ilipoitwa leo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upinzani ulikuwa mkubwa sana, leo kampuni fulani ya magari ilipokuwa ikitoa aina fulani ya magari, kesho kampuni nyingine ya magari ilikuwa ikitoa aina nyingine za magari. Katika kampuni zote hasa katika nchi za Ulaya na Marekani kulikuwa na mashindano makubwa ambayo yalikuwa yakizihusisha kampuni ambazo zilikuwa zikifanya bishara za aina moja.
Bwana Kurt alikuwa miongoni mwa matajiri ambao walikuwa wakimiliki kampuni za magari huku kampuni yake akiita McLloyd ambayo ilikuwa ikitengeneza magari ya kisasa aliyoyapa jina la McLloyd. Kampuni hiyo ya magari ilikuwa ikizalisha magari mengi kila wiki, magari ambayo yalikuwa yakitengenezwa ndani ya kampuni hiyo yalikuwa yakitolewa katika ngazi tatu tofauti ambazo zilimgusa kila mtu.
Ngazi ya kwanza kabisa ilikuwa inahusika na utengenezaji wa magari hayo ambayo kwa gharama yake ya chini kabisa ilikuwa ni dola milioni moja. Katika ngazi hiyo ni matajiri tu ndio ambao walikuwa wakihusika zaidi katika ununuzi wa magari hayo ambayo mara zote yalikuwa yakitengenezwa kwa oda maalumu, oda ambazo zilikuwa zikitoka kwa matajiri wakubwa Uarabuni au hata masupastaa ambao katika maisha yao walikuwa wakitaka kuonekana na magari ambayo hayakuwa yakipatikana sehemu yoyote ile.
Ukiachana na aina hiyo ya magari, pia ngazi ya pili ilikuwa ni ile aina ya magari ambayo gharama yake ilikuwa ikianzia dola laki saba mpaka dola laki mbili. Aina ya magari ambayo yalikuwa yakitengenezwa katika ngazi hii yalikuwa yakitumiwa zaidi na wasanii mbalimbali pamoja na waigizaji wa filamu ambao hawakuwa na fedha nyingi zaidi ya matajiri wengine.
Ukiachana na ngazi zote hizo, kulikuwa na ngazi ya tatu na ya mwisho ambayo ilikuwa ikitengeneza magari ambayo yalikuwa yakiuzwa kwa watu ambao hawakuwa na fedha nyingi kiasi ambacho magari mengine yalifika mpaka dola elfu kumi. Hiyo ndio ngazi ambayo ilikuwa na wanunuzi wengi na ndio ngazi ambayo ilikuwa ikiingizia kampuni ya Mc Lloyd kiasi kikubwa cha fedha kila siku.
Magari ya McLloyd yalikuwa yakinunuliwa na watu wengi duniani kiasi ambacho kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, magari hayo yakawa yakijulikana zaidi duniani. Muonekano wa magari hayo pamoja na uimara ndivyo vitu ambavyo vilimfanya kila mtu kuvutiwa zaidi kitu ambacho kilizidi kuongeza wanunuaji wa magari hayo katika kampuni hiyo.
Ukiachana na kampuni ya magari ya McLloyd iliyokuwa ikimilikiwa na Bwana Kurt pia kulikuwa na kampuni nyingine iliyokuwa ikijihusisha na utengenezaji wa magari, kampni hii iliitwa kwa jina la Nacho na ilikuwa ikipatikana nchini Mexico. Hii ilikuwa ni moja ya kampuni ambayo ilikuwa ikitengeneza magari yake na kuyasambaza sana katika bara la Marekani.
Watu wengi wa Brazil, Mexico, Paraguay na Colombia ndio walikuwa wanunuaji wazuri wa magari haya ambayo kwao yalionekana kuwa na mvuto. Mmiliki wa kampuni hiyo, tajiri Sanchez kila siku alikuwa na kazi ya kukaa na watu wake wa kuchora michoro mbalimbali na kuwapa kazi ya kuwachorea picha za magari ambayo yalionekana kumvutia kwa kuziangalia tu. Vijana wake hao walikuwa wakifanya sana kazi hiyo kwa malipo makubwa huku nae akiwa anaendelea kuyatangaza magari yake duniani.
Japokuwa mzee Sanchez alikuwa akijitahidi kila siku kuyatangaza magari yake duniani lakini mbele ya magari ya kampuni ya Mc Lloyd, magari yake ya Nacho hayakuonekana kuwa na thamani. Hapo ndipo mzee Sanchez alipoonekana kukasirika na hasira kuanza kumuingia, wivu ukamtawala moyoni mwake, akaanza kumchukiwa Bwana Kurt.
Bwana Kurt alikuwa akiharibu soko la magari yake katika bara la Marekani, magari ya Mc Lloyd yalikuwa yakitumika kwa wingi katika bara la Marekani kuliko magari ambayo yalikuwa yakitengenezwa katika kampuni yake ya Nacho. Moyo wake ukamvimba, japokuwa kila alipokuwa akikutana na Bwana Kurt katika mikutano mbalimbali ya matajiri alikuwa akimuonyeshea tabasamu lakini tabasamu lake halikuwa la kweli kabisa.
“Lo mataré (Nitamuua)” Mzee Sanchez alimwambia mke wake katika lugha ya Kiispaniola huku akionekana kuwa na hasira.
“Quién (Nani?)” Mkewe, Bi Shakira.
“Él destruyó mi negocio (Anaharibu biashara yangu)”
“Quién (Nani?)” Bi Shakira alimuuliza mumewe.
“Kurt. Lo mataré (Kurt. Nitamuua)” Mzee Sanchez alimwambia mke wake.
“Esto no le ayudará a (Unafikiri hii itakusaidia?)” Bi Shakira aliuliza.
“Espero que sí (Nadhani)”
Mzee Sanchez alikuwa amekasirika hasa, kitendo cha Bwana Kurt kuwa juu zaidi yake katika mambo yote kuhusiana na biashara ilionekana kumkasirisha kupita kawaida, moyo wake ulikuwa na chuki kubwa, hakumpenda hata kidogo kitu ambacho kwa wakati huo kikamfanya kufikiria mauaji tu, alitaka kumuangamiza kwani aliamini hilo lingeweza kumpa furaha maishani mwake.
Siku zikaendelea kukatika, hasira yake ilikuwa ikiongezeka moyoni mwake kila alipokuwa akimuona Mmexico akiendesha gari aina ya McLloyd. Alitamani kama angekuwa na sauti ya juu kwa kuamua magari yote yaliyokuwa yakitengenezwa katika kampuni ile yalipuliwe na kuchwa magari ya kampuni yake ya Nacho tu.
Aliishi akiwa na manung’uniko moyoni mwake kila siku, hakutaka watu wafahamu kama moyo wake ulikuwa kwenye hasira kali juu ya Bwana Kurt. Kitendo cha Bwana Kurt kusaini mkataba na kuwapa wachina kibali cha kutengeneza magari ya McLloyd na kuyasambaza duniani kote ndicho ambacho ambacho kilimuuma zaidi mzee Sanchez. Aliwafahamu vilivyo wachina, aliwajua kwa undani sana hasa katika masuala mazima ya utengenezaji na usambazaji wa bidhaa duniani.
Kwa kitendo kile cha kusaini mkataba na wachina kilimfanya mzee Sanchez kuona kwamba Bwana Kurt alikuwa akienda kujulikana zaidi na zaidi kutoka na magari yake hali ambayo ingeyafunika kabisa magari kutoka katika kampuni yake ya Nacho. Hicho alichokiona ndicho ambacho kikaanza kutokea. Miezi sita baada ya wachina kusaini mkataba na kampuni ya McLloyd, mkataba ambao ulikuwa na fedha nyingi mno Bwana Kurt, magari yakaanza kuachiwa na kusambazwa duniani kote zaidi na zaidi tena kwa bei nafuu.
Wachina wakaonekana kama kuchanganyikiwa kwa jinsi fedha zilivyokuwa zikiingia, mkataba wa miaka mitano wa kutengeneza magari ambaco walikuwa wamesaini na Bwana Kurt ulionekana kuwa na mafanikio sana kwao, magari yakasambazwa zaidi na zaidi na watu kununua wengi. Magari zaidi ya milioni tano yakaletwa barani Afrika ambapo yakagombaniwa kupita kawaida. Wachina wakaingiza fedha zaidi ya zile ambazo walikuwa wamemlipa Bwana Kurt.
Huo ndio ulikuwa mchakato mzima wa biashara. Mkataba ambao alikuwa amesaini na wachina ulikuwa mkataba uliokuwa na fedha nyingi sana ambazo zilimuongezea utajiri zaidi na zaidi. Baada ya kipindi cha miezi kadhaa Bwana Kurt akaanza kusikia tetesi kwamba hakuwa akipendwa na mzee Sanchez na mzee huyo alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile hata kama kumtoa roho yake, alikuwa tayari.
Maneno yale hayakuonekana kuwa mazuri kwake, hakupenda kuishi katika mafarakano na mtu fulani, alichokifanya ni kutafuta njia ya kuonana na mzee Sanchez lakini jambo hilo likaonekana kuwa gumu kutokea. Akamtumia rais wa nchini Mexico, Puto Mendez lakini napo jambo hilo lilikuwa gumu kutokea. Bwana Kurt hakuogopa hata mara moja, kila alipokuwa kulikuwa na ulinzi mkubwa ila kitu ambacho alikuwa akikitaka ni kuishi kwa amani na kila mtu.
Huku wakiwa katika hali hiyo, watoto wao ambao walikuwa wakiishi katika aina moja ya maisha wakakutana chuoni Mississippi na kuwa marafiki jambo ambalo liliwashangaza sana. Mzee Sanchez hakutaka kumuona mtoto wake akiwa na urafiki na mtoto wa Bwana Kurt, Alan lakini jambo hilo akashindwa kulizuia kutokea kwani hata pale alipotaka kumuamisha chuo, Antonio alikataa katakata.
“Promoción ha cambiado (Mpango umebadilika)” Mzee Sanchez alimwambia mke wake.
“Cómo (Kivipi?)CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Voy a matar a su hijo (Nitamuua mtoto wake)
Hicho ndicho ambacho mzee Sanchez alikuwa ameamua, hakuonekana kuwa na raha kwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea kutokea katika maisha yake. Alikuwa ameachwa mbali kifedha na Bwana Kurt kitu ambacho kilimuumiza sana. Ukiachana na mambo ya fedha, biashara za magari ambazo wote wawili walikuwa wakizifanya ndizo ambazo zilichochea chuki kubwa moyoni mwa mzee Sanchez.
Kila siku akawa mtu wa kulalamika tu, kila siku alikuwa akimuona Bwana Kurt kuwa na makosa kwa kuyaruhusu magari yake kuingia ndani ya nchi ya Mexico. Kila siku alikuwa na kiu ya kutaka kumuua Bwana Kurt lakini kwa wakati huu alikuwa amebadilisha mpango wake, akataka kumuua Alan.
Kitendo cha mtoto wake, Antonio kuwa rafiki wa Alan chuoni kilimkasirisha sana lakini kwa namna moja au nyingine akaona jambo hilo lilikuwa jema sana kwake kwani angeweza kumtumia mtoto wake katika kukamilisha kila kitu alichokuwa akikihitaji. Hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kumshawishi Antonio katika kufanikisha kile alichokuwa amekipanga chumbani kwake.
Antonio hakuonekana kuwa radhi kuukubali mpango wa baba yake, japokuwa hakuwa amemwambia lakini muonekano ambao aliuonyesha Antonio ulionyesha wazi kwamba hakuwa tayari kukubaliana na kitu kile. Muonekano ule ukaonekana kuwa sahihi, katika kipindi ambacho mzee Sanchez alipomgusia Antonio kuhusu mpango wake, Antonio akaja juu, akaonekana kukasirika, siku hiyo ikaonekana kuwa kama vita, nyumbani hakutaka kula wala kulala, akaondoka zake kuelekea nchini Colombia kulala.
Mzee Sanchez akajiona kufanya kosa kubwa, hakutaka kumkasirisha mtoto wake, Antonio kitu ambacho kilimfanya kumpigia sana simu na kumuomba msamaha lakini Antonio hakuonekana kukubali. Mzee Sanchez hakukoma, kitendo cha mtoto wake kuondoka nyumbani na kuelekea nchini Colombia huku akitumia muda wa wiki nzima kuwa nchini humo kilimkosesha raha. Alichoamua kukifanya kama mzazi anayemjali mtoto wake ni kusafiri kuelekea nchini Colombia.
Akaonana na kijana wake na kisha kuongea nae huku akitumia muda mwingi kumuomba msamaha. Antonio hakuwa na jinsi, kwa sababu baba yake alikuwa amekwishajirudi, akaamua kumsamehe na kurudi nyumbani. Hapo ndipo mzee Sanchez alipoona kwamba kitu ambacho alitakiwa kukifanya ni kufanya vitu vyake kimya kimya bila kumshirikisha mtoto wake.
“Nitamuua tu mtoto wake” Mzee Sanchez alisema huku akionekana kuwa na hasira, kitendo cha kuzidiwa wateja katika biashara ya magari kilianza kusababishia kuingiwa na roho ya uuaji moyoni mwake.
*****
Mara baada ya Alan kutoka nje pamoja na Stacie, wazazi walibaki sebuleni pale huku wakiangaliana, kila mmoja alibaki kimya, hali ambayo aliionyesha Alan ilionekana kuwashangaza kupita kawaida. Alan alikuwa amebadilika kabisa, hakutaka kuambiwa lolote lile, moyo wake katika kipindi hicho ulikuwa kwa msichana ambaye alikutana nae nchini Tanzania, Albertina.
Stacie hakuonekana kuwa na chake ndani ya moyo wake, Alan alikuwa ameamua kwa moyo mmoja kwamba ni lazima awe na Albertina na hivyo Stacie alitakiwa kusahau kila kitu kilichokuwa kimeendelea katika maisha yao. Alan alikuwa amebadilika kwa haraka sana, safari yake ya kuelekea nchini Tanzania ndio ambayo ilikuwa imebadilisha kila kitu katika maisha yake ya uhusiano.
Bwana Bruce na mkewe, Susie hawakuonekana kuwa na raha, kitendo ambacho alikuwa amekifanya Alan cha kumkataa mtoto wao kiliwakasirisha lakini hawakuonekana kuwa na jinsi, walitakiwa kukubaliana na kila kitu. Hayo ndio yalikuwa mapenzi, leo mtu anaweza kuwa hivi lakini kesho mtu akawa tofauti na siku iliyopita.
Baada ya kukaa nje kwa muda wa dakika kadhaa, Stacie akarudi sebuleni, macho yake yalikuwa mekundu huku machozi yakiendelea kutiririka mashavuni mwake. Kwa muonekano wa nje tu Stacie alionekana kuumizwa kupita kawaida, akapiga hatua na kwenda kukaa karibu na mama yake na kisha kukilaza kichwa chake mapajani mwa mama yake.
Kila mmoja mahali hapo alionekana kuhuzunika lakini huzuni zao hazikuweza kubadilisha kitu chochote kile mioyoni mwao. Walitakiwa kukubaliana na kila kitu kwamba Alan hakuwa mtu wa Stacie tena, alikuwa mpenzi mpya wa msichana Albertina ambaye alikuwa nchini Tanzania. Bwana Bruce na familia yake wakaondoka mahali hapo.
“Alan yupo wapi?” Bwana Kurt aliuliza, ilikuwa ni saa tatu usiku, Alan hakuwa amerudi nyumbani toka katika kipindi ambacho alitoka nje na Stacie.
“Bado hajarudi” Bi Bertha alijibu.
Bwana Kurt akainuka toka kitandani, siku hiyo moyo wake ulikuwa mzito sana, usingizi haukumjia kabisa, kila wakati alikuwa akimfikiria mtoto wake, alionekana kutokuwa na raha kabisa. Alichokifanya ni kuchukua simu yake na kisha kuanza kumpigia Alan. Simu ilikuwa ikiita, iliiita zaidi na zaidi lakini wala haikuwa ikipokelewa.
Hali ile ikamshangaza sana Bwana Kurt, haikuonekana kuwa hali ya kawaida kabisa. Akaendelea kumpigia simu zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa ni yale yale, simu iliita sana lakini wala haikupokelewa kabisa. Moyo wake ukasinyaa, tayari akajua kwamba kulikuwa na tatizo ambalo lilikuwa limetokea, hakujua mahali ambapo kijana wake alipokuwa kwa wakati huo, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kumpata Alan kwani kuondoka nyumbani bila kuaga na kukaa nje kwa kipindi kile kirefu kulimtia wasiwasi.
“Jaribu kumpigia simu Christopher” Bi Bertha alimwambia mumewe.
“Unafikiri Christopher atakuwa akifahamu chochote? Alan hapendi kutumia ndege yake katika safari zake” Bwana Kurt alimwambia mke wake.
“Jaribu tu mume wangu. Wakati mwingine yakupasa kujaribu kufanya kitu hata kile ambacho moyo wako unaamini kwamba hakiwezi kutokea” Bi Bertha alimwambia mume wake, Bwana Kurt.
Hapo ndipo ambapo Bwana Kurt alipoamua kumpigia simu Christopher, rubani wa ndege aliyomnunulia Alan. Simu ikaanza kuita, iliita kwa muda mchache na kisha kupokelewa, sauti ya Christopher ilisikika upande wa pili.
“Upo wapi?” Bwana Kurt aliuliza.
“Nipo Texas” Sauti ya Christopher ilisikika simuni.
“Umekwenda kufanya nini huko?”
“Nimemleta Alan”
“Alan! Kaenda kufanya nini huko?”
“Sijui”
“Upo nae hapo jirani?”
“Hapana. Aliondoka huku akinitaka nirudi Washington, ndio najiandaa kuja huko kesho asubuhi” Christopher alimwambia Bwana Kurt.
Bwana Kurt hakutaka kuendelea kumsikiliza Christopher, alichokifanya huku akionekana kuchanganyikiwa ni kukata simu ile na kupiga simu huduma kwa wateja na kisha kuhitaji kupatiwa namba ya kituo kikubwa cha polisi cha huko Texas huku lengo lake kubwa likiwa ni kuongea na mkuu wa kituo hicho. Wala haukupita muda mrefu, simu ikaonganishwa na simu ya kituo hicho. Simu ikapokelewa na polisi ambaye alikuwa mapokezini.
“Nataka kuongea na mkuu wa kituo hicho” Bwana Kurt alisema huku akionekana kuchanganyikiwa. Mtu aliyepokea simu wala hakutaka kuuliza, alijua kabisa kwamba mtu ambaye alikuwa upande wa pili hakuwa mtu wa kawaida, kauli yake ya kulazimisha ilionyesha kwamba alijiamini, simu ikaonganishwa mpaka katika simu ya mkuu wa kituo hicho, Michael MaxwellCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nikusaidie nini?” Mkuu wa kituo hicho cha polisi cha hapo Texas alimuuliza Bwana Kurt.
“Ninamtaka mtoto wangu” Bwana Kurt alimwambia Maxwell.
“Naongea na nani?” Maxwell aliuliza.
“Thomson Kurt. Ninamtaka mtoto wangu, Alan. Amekuja huko, ninahitaji mumtafute na kumpata. Nina uhakika anataka kwenda nchini Mexico, ninahitaji mumzuie na mumlete Washington” Bwana Kurt alisikika.
“Atakuwa wapi kwa sasa?”
“Nitakutumia namba ya rubani wake, huyu atakuwa anafahamu wapi pa kuanzia mpaka apatikane. Namhitaji, naomba muhakikishe aingii nchini Mexico” Bwana Kurt alisema kwa kumaanisha.
“Usijali”
Alichokifanya Bwana Kurt ni kumpa Maxwell namba ya Christopher kwa ajili ya kuwapa taarifa ni mahali gani ambapo walitakiwa kuanzia kwa wakati huo kuhakikisha kwamba Alan anapatikana. Bwana Kurt akakaa kitandani huku akionekana kuwa na mawazo mengi, akaiangalia saa yake, ilikuwa ni saa tatu kasioro usiku. Kichwa chake hakikuwa sawa kabisa, alijua dhahiri kwamba Alan alikuwa safarini kuelekea nchini Mexico.
Bwana Kurt akaanza kujilaumu kwa kufanya kosa moja kubwa, kila siku alikuwa akijitahidi sana kumzuia Alan kuingia nchini Mexico lakini hakuwahi kumwambia sababu iliyomfanya kutokumtaka kuingia nchini Mexico. Alan hakuwa akijua kitu chochote kile, japokuwa baba yake alikuwa akimzuia, kichwa chake kilimwambia kitu tofauti kabisa kwa kudhani kwamba baba yake alimzuia kwa sababu tu Mexico ilikuwa moja ya nchi iliyobarikiwa kuwa na wanawake wazuri, hivyo hakumtaka kwenda huko kwani alijua kwamba angeweza kumsaliti mpenzi wake, Stacie.
“Atamuua tu. Najua atamuua tu mtoto wangu” Bwana Kurt alimwambia mke wake.
“Nani?”
“Sanchez. Alan anataka kuelekea nchini Mexico, bila shaka anakwenda kumtembelea Antonio, mtoto wa Sanchez. Mungu wangu! Huyu mtu anaweza kumuua mtoto wangu” Bwana Kurt alisema huku akionekana kuchanganyikiwa.
Kitendo cha Alan kuelekea katika jiji la Texas ilionyesha dhahiri kwamba alikuwa safarini kuingia nchini Mexico. Bwana Kurt hakuwa akitulia, muda mwingi alikuwa akisimama na kuanza kutembea huku na kule, alionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida, kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo, aliona dhahiri kwamba mtoto wake alikuwa akienda kuuawa, kitu pekee ambacho alikuwa akitakiwa kukifanya ni kumzuia Alan kuingia ndani ya nchi ya Mexico.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Je nini kitaendelea?
Je Alan atafanikiwa kuingia nchini Mexico kama alivyopanga?
Je Bwana Kurt ataweza kumzuia Alan kuingia nchini Mexico?
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment