Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

MPENZI WANGU SARAFINA - 3

 







    Simulizi : Mpenzi Wangu Sarafina

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kubakwa ndiyo yalikuwa sehemu ya maisha ya msichana Malaika. Kila siku Ibrahim ilikuwa ni lazima amuingilie, alifanya naye mapenzi kinguvu na mwisho wa siku msichana huyo mdogo akazoea.

    Wakawa wapenzi, kila walipokuwa wakienda kuomba, walikuwa pamoja, usiku ulipoingia, walitafuta sehemu nzuri na kulala. Malaika alipokuwa na shida, mtu pekee aliyekuwa akimwambia shida zake alikuwa Ibrahim ambaye alimsaidia kama mpenzi wake.

    Mbali na kuwa ombaomba mitaani, lakini Ibrahim alikuwa mwizi, alijua kufungua vioo vya gari na kuiba kitu chochote alichokiona kufaa garini. Hakukaukiwa pesa ndogondogo, hizo ndizo zilizomfanya Malaika kumpenda kwani alipokuwa na shida, kijana huyo alimsaidia pasipo matatizo yoyote yale.

    Wakawa kama mume na mke, hakukumbuka ukatili aliowahi kufanyiwa na kijana huyo, kwake, moyo wake ukampenda, hakulazimishwa kufanya mapenzi, wakati mwingine kila ilipofika usiku, yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumpapasa Ibrahim kifuani na mwisho wa siku kujikuta wakikumbatiana kimahaba katika vibaraza vya watu.

    Siku ziliendelea kukatika, mambo hayo yote yalikuwa yakifanyika wakati Malaika akiwa hajavunja ungo, alikuwa binti mdogo lakini aliijua michezo yote ya kiutu uzima. Alikuwa na miaka saba tu lakini umbo lake lilibadilika na kuonekana kama msichana aliyekuwa na miaka kumi na tano.

    Moyo wake haukuacha kumkumbuka mama yake, kila picha ya mwanamke huyo ilipokuwa ikimjia kichwani, alilia, alihuzunika na kitu pekee kilichokuwa kikimuumiza ni kwamba hakuwahi kumuona baba yake.

    Alitamani kumtia machoni, hakujua angemuona vipi, hakuwahi kuonyeshewa picha zake, alichosaidiwa na mama yake ni kwamba mwanaume huyo huyo aliitwa David Kimario. Aliambiwa kwamba alifariki dunia, na mara nyingi alipokuwa akimuuliza mama yake kuhusu mwanaume huyo, alikuwa akilia kitu kilichomfanya kuamini kwamba alifariki dunia kitu kilichouumiza moyo wake mno.

    “Nataka tutafute nyumba tukaishi wote,” alisema Ibrahim huku akimwangalia Malaika.

    “Una hela?”

    “Ninayo kidogo. Ila kuna sehemu nakwenda, nataka nikifika huko niibe kitu kwenye gari moja hivi, tukauze halafu tukipata hela, tukapange chumba mpenzi,” alisema Ibrahim huku akimwangalia Malaika.

    “Ukaibe wapi?”

    “Kuna magari mengi mjini. Nitakwenda Posta kufanya mishemishe halafu nitakwambia,” alisema Ibrahim.

    Hiyo ndiyo ilikuwa kazi yake, alikwenda kwenye magari mengi na kuiba huko kwa kufungua vioo vya gari huku akijifanya kuokota chupa za plastiki za maji. Aliwaliza watu wengi wenye magari mjini na wengi walimtafuta lakini hawakumuona kwani alikuwa mjanja mno.

    Ibrahim akaelekea Posta Mpya huku akiwa na kiroba cha chupa za maji. Huko ndipo alipokuwa akifanya uhalifu wake. Alipofika maeneo hayo, hakutaka kuchelewa, akaelekea katika sehemu ya kuegeshea magari katika Ghorofa la Benjamin Mkapa kwa ajili ya kufanya uhalifu huo.

    Alipofika, kulikuwa na magari mengine, asilimia kubwa yalikuwa ni magari ya kifahari. Hapo, akaweka kiroba chake pembeni na kutoa waya, akalifua gari moja la kifahari, Range SUV jekundu na kama kawaida yake akaangalia huku na kule, alipoona hakuna mtu anayemuona, akaanza kukifungua kioo cha gari hilo kwa kutumia waya huo aliokuwanao.

    Alikuwa mzoefu, alijua jinsi ya kufungua vioo vya magari, alipofanikiwa, akatoa loki, akaufungua mlango na haraka sana kuanza kupekua ndani. Macho yake yakatua katika laptop moja, bahasha kubwa ya kaki ambapo alipoifungua, macho yake yakatua katika mabunda ya mengi ya noti za elfu kumi.

    “Dili hili,” alisema na kisha kuchukua bahasha hiyo na laptop kisha kutokomea zake na vitu hivyo pasipo kujua gari hilo lilikuwa la nani.

    ****

    Mzee Mpobela akampanga David na kumwambia jinsi biashara hiyo ilivyokuwa ikifanywa na hata jinsi usafirishaji ulivyokuwa mwepesi. Kutoa mzigo mkubwa kutoka Tanzania kupeleka nchi kama Brazil hakukuwa na ugumu wowote ule.

    Kitu ambacho kilitakiwa kufanywa ni kufanya mawasiliano uwanja wa ndege wa Tanzania na Brazil kwa kutoa kiasi kikubwa cha pesa na kazi kufanyika kwa haraka sana na wepesi mno.

    Kwa wafanyakazi ambao walikuwa na tamaa ndiyo waliokuwa wakiingizwa kwenye mkenge na kufanya kazi hiyo kwa ajili ya kuingiza kiasi fulani cha pesa. Akapewa michongo yote na kisha kupewa mzigo wenye gharama ya shilingi bilioni mbili na kuupeleka nchini Brazil kwa mfanyabiashara Marcos Bebe.

    Kwa Tanzania hakukuwa na tatizo, tayari wafanyakazi hao wenye tamaa walipewa taarifa na hivyo kazi kuachwa kwa Bebe ambaye naye akafanya kwa sehemu yake kwa kuhonga wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Rio De Janeiro uliokuwa katika jiji hilo hilo.

    Alipofika, akachukua mabegi yake, akateremka na kuanza kuelekea nje ya uwanja huo. Hakukuwa na mtu yeyote aliyembughudhi, kitu cha kushangaza kabisa ni kwamba hakupekuliwa, akapitishwa katika mlango mwingine na kuelekea nje kabisa.

    Huko, akakutana na vijana watatu wakiwa nje ya gari moja la kifahari. Akakaribishwa na kuingia ndani ya gari hilo. Alipokuwa ndani ya ndege alikuwa na hofu ya kukamatwa lakini baada ya kuingia ndani ya gari hilo akajiona akiwa salama kabisa.

    Hakuzungumza kitu garini, macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule kulitalii jiji hilo kubwa la Rio. Safari iliendelea huku wanaume wale wakipiga stori kwa Lugha ya Kireno, hakuelewa walizungumza nini, alikaa kimya tu.

    Baada ya dakika kadhaa gari hilo likaanza kuingia katika jumba moja kubwa na la kifahari. David alibaki akishangaa, katika maisha yake aliwahi kuyaona majumba makubwa ya kifahari lakini halikuwa kama hilo.

    Lilipendeza machoni mwake, gari likajifungua na gari kuingia ndani. Kulikuwa na walinzi wengi humo waliokuwa wameshika bunduki picha iliyoonyesha kwamba mtu aliyekuwa akimiliki jumba hilo alikuwa na nguvu kubwa, ulinzi uliokuwepo humo hakuwahi kuuona kabla.

    Akapelekwa sebuleni na kutulia kwenye kochi kubwa. Baada ya dakika chache, mwanaume mmoja aliyekuwa na mwili wenye misuli mingi akatokea mahali hapo, akamsalimia na kujitambulisha kwamba yeye ndiye alikuwa Marcos Bebe.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimefurahi kukuona,” alisema David mazungumzo waliyotumia lugha ya Kiingereza.

    Akampa mzigo wake, ulikuwa ni wa madawa ya kulevya, mzigo huo ukaenda kuangaliwa na kupimwa, haukupungua, ujazo alioambiwa ndiyo aliokutana nao hivyo kumpatia David kiasi fulani cha fedha kwa matumizi yake na shukrani ya kumpelekea mzigo na kuufikisha salama kabisa.

    Huo ndiyo ukawa mwanzo wa safari yake ya kuuza madawa ya kulevya. Alipoufikisha mzigo huo Brazil, akapewa kiasi cha dola elfu kumi, zaidi ya shilingi milioni ishirini kwa kazi kubwa ya kuufikisha huko.

    Maisha yake yakabadilika, akaanza kununua magari na kujenga jumba kubwa Mbezi Beach. Maisha yake yalikuwa mazuri, hakuamini kama angepata zali kubwa kama hilo. Akawa na pesa, shughuli zake zikawa ni kusafiri, mara Afrika Kusini, Brazil, Uarabuni na sehemu nyingine.

    Gloria hakuhisi kitu chochote kibaya kwa kuwa baba yake ndiye aliyekuwa msimamizi wa biashara hiyo. Alimwambia kwamba aliamua kumfungulia biashara mbalimbali David kwa kuwa hakutaka kuona mkwewe akipata shida ya maisha.

    Msichana huyo aliridhika na kumshukuru sana baba yake kwa kazi hiyo aliyokuwa amempa David. Waliendelea kuishi kama wachumba na baada ya miezi kadhaa wakafunga ndoa na hatimaye kuwa mume na mke.

    Kila mmoja alikuwa na furaha tele, David alikuwa akiendelea na kazi zake za kusafirisha madawa ya kulevya kama kawaida. Akajuana na watu wengi wakubwa, akaingiza kiasi kikubwa cha fedha japokuwa alikuwa mbebaji tu.

    “Nataka twende Dubai kula bata! Utakuwa tayari?” aliuliza David huku akimwangalia mke wake, Gloaria.

    “Nipo tayari!”

    Hilo ndilo lililobakia, alikuwa na kila kitu, maisha mazuri na ili kuizuga serikali isifahamu kile kilichokuwa kikiendelea, akaanzisha maduka ya mengi ya nguo nchini Tanzania. Utajiri wake ukakua, akawa na wapambe wengi, akajipanga, kila mtu alikuwa akishangaa kwani kati ya matajiri waliokuwa wakichipukia huku wakiwa na umri mdogo wa kwanza alikuwa yeye.

    Kila alipokuwa akitembea, alikuwa akitembea na kiasi kikubwa cha fedha, zaidi ya milioni tano ilikuwa ni lazima kiwe ndani ya gari lake pamoja na laptop yake ambayo ilikuwa na ratiba za safari zake zote. Alikuwa tayari kupoteza kitu chochote lakini si laptop hiyo.

    Baada ya miaka kadhaa, wakati mke wake akiwa na mimba ndipo akaamua kwenda katika ofisi yake iliyokuwa katika ghorofa la Benjamin Mkapa na bahati mbaya kwake wakati anatoka ofisini na kuelekea kwenye gari lake, akapigwa na mshtuko baada ya kukuta gari lake likiwa limefunguliwa mlango, alipoingia ndani, pesa, zaidi ya milioni sita na laptop vyote havikuwepo.

    Alichanganyikiwa, alipiga gari kwa hasira, akawafuata walinzi na kuwaambia kilichotokea. Wao wenyewe walishangaa, hawakuamini kama kweli kulikuwa na mtu aliyeingia na kuiba vitu hivyo.

    “Nimesema hivi! Nisikilizeni, nimesema hivi nisipompata mtu aliyeiba laptop na pesa zangu, nitawaueni wote,” alisema David huku akionekana kuwa na hasira nyingi.

    “Sawa bosi!”

    Walichokifanya ni kwenda katika chumba kilichounganishwa na kamera za CCTV na kuanza kuangalia kila kitu kilichotokea. Wakati huo David alikuwa ndani ya gari lake, hakuondoka, alibaki garini na kutaka kujua kamera hizo zilionyesha nini.

    Baada ya dakika kadhaa, walinzi wakarudi na kumwambia kwamba mtu aliyekuwa ameiba vitu hivyo alikuwa muokota makopo ambaye alifungua gari lake na kuondoka zake.

    “Ninamtaka mtu huyo,” alisema david huku akichukua simu yake.

    Akapiga upande wa pili, simu ikapokelewa na mwanaume mmoja aliyekuwa na sauti nzito, akampa maagizo kwamba alitaka kumuona muda huo akiwa na mwenzake. Ndani ya dakika kumi wanaume wawili waliokuwa na miili mikubwa wakafika mahali hapo, akawaambia kwamba kulikuwa na mtu alitakiwa kuuawa haraka sana.

    “Nani mkuu?”

    “Nendeni watawaonyeshea video na picha ya mtu huyo,” alisema David.

    Wanaume hao wakachukuana na walinzi, wakarudi katika chumba kile, wakaonyeshewa kilichokuwa kimetokea, kumpata mtoto wa mitaani, aliyekuwa akiokota chupa wala halikuwa jambo gumu, wakaiprinti picha yake na kuwa nayo kisha kuanza kumtafuta. Agizo moja walilopewa ni kuipata laptop, na ikiwezekana, kijana huyo auawe mara moja.





    Bianca aliendelea kumfuatilia Richard, hakuwa radhi kuona akimkosa mwanaume huyo ambaye kwake alikuwa kama mwanaume wa maisha yake. Alikuwa mgumu lakini kila siku alijitahidi kumfikishia ujumbe kwamba alikuwa akimpenda sana.

    Richard alikuwa akikataa, aliyaogopa mapenzi, hakutaka kuwa na msichana yeyote kwani kumbukumbu kuhusu Sarafina zilimjia kichwani mwake na kuyachukia mapenzi hayo. Hakutaka kuyapa nafasi, alitaka kubaki peke yake kwa kuamini kwamba kungekuwa na siku moja ambayo angefurahi kwa kumpata mwanamke wa maisha yake lakini si Bianca.

    Siku zikakatika, ukaribu wa Bianca kwa Richard ukazidi kushamiri. Wakati mwingine mwanaume huyo alikuwa akichukia sana, hakutaka kuwa karibu na msichana huyo lakini alishindwa, kila alichokuwa akikifanya, Bianca alikuwa pembeni yake.

    Bianca akawa hakwepeki, alimtawala kila sehemu, ndiye alikuwa mtu ambaye alimpigia kumpigia simu huku akiwa wa mwisho kuzungumza naye kwa njia ya simu. Hakutaka ukaribu na msichana huyo lakini kikafika kipindi akawa hana jinsi, akakubaliana na ukweli uliokuwepo kwamba awe tu na msichana huyo.

    Akamkubalia kuwa mpenzi wake, wakawa pamoja na mapenzi kuanza kama ambavyo msichana huyo alivyotaka. Kila siku ilikuwa ni lazima wawili hao kugandana kama ruba. Uhusiano huo wala haukuwa siri kwani baada ya siku tatu tu chuo kizima kikagundua kwamba wawili hao walikuwa kwenye uhusiano mzima wa mapenzi.

    Siku zikakatika, mwaka wa kwanza ukaondoka, Richard hakutaka kurudi nchini Tanzania, moyo wake ulikuwa na chembechembe za maumivu kutoka kwa msichana Sarafina ambaye alimuumiza sana, msichana ambaye alimtesa usiku na mchana.

    Hakutaka kuonana naye, alitamani kuona akiendelea na maisha yake akiwa na Bianca, msichana ambaye alijitolea kwa asilimia mia moja kuwa naye katika maisha yake yote. Richard na Bianca walichukua miaka mitatu kusoma nchini Marekani na ndipo wakarudi nchini Tanzania.

    Kitu cha kwanza kabisa walichokifanya kilikuwa ni kutambulishana kwa wazazi kwamba walikuwa wapenzi, wazazi wakakubaliana nao, wakawapa baraka zao na kisha wawili hao kuvalishana pete na hatimaye kuingia kwenye uchumba.

    “Nitataka nikuoe, uwe mke wangu wa ndoa,” alisema Richard, alikuwa akimwambia mchumba wake Bianca aliyeonekana kuwa na furaha tele, kwake, kuwa na msichana huyo ndani ya nyumba yake ndicho kitu alichokuwa akikihitaji kuliko vyote katika maisha yao.

    Hilo halikuwa la kusubiri, kilichotokea baada ya miezi kadhaa ni kufunga ndoa na hatimaye kuwa mume na mke kitu ambacho kilimpa furaha kila mmoja.

    Maisha yao yakabadilika kabisa, kila mmoja alionekana kuwa na furaha, katika maisha yao, wote walitamaniana, ukaribu ukaongezeka, wakazoeana kupita kawaida kiasi kwamba kuna kipindi wakawa wakiishi kama marafiki hali iliyoyafanya mapenzi yao kudumu zaidi.

    Wakapanga kuwa na watoto na baada ya miaka miwili ya ndoa ndipo wakaamua kumtafuta mtoto huku tayari wakiwa na miaka mitano tangu walipokutana chuoni. Kupata mimba kwa Bianca hakukuwa tatizo lolote, kwani tangu waamue, ndani ya miezi miwili akaanza kuhisi dalili zote za kuwa na mtoto tumboni mwake.

    Hilo lilimpa furaha kila mmoja, wakasubiri na baada ya miezi michache kwenda hospitali ambapo daktari aliwaambia kwamba walitegemea kupata mtoto wa kike kitu kilichomfanya kila mmoja kufurahi.

    “Unasemaje?” aliuliza Richard huku akiwa haamini.

    “Mtoto wa kike.”

    “Ataitwa Claire! Mke wangu naomba usinipinge katika hili,” alisema Richard huku akiachia tabasamu pana usoni mwake.

    “Wewe tu!”

    Wakaanza kupanga mipango juu ya mtoto huyo, walikuwa wakimpenda hata kabla hajazaliwa hospitalini. Wakafanya sana shopping, wakanunua vitu vingi kwa ajili ya mtoto huyo. Wakawaambia marafiki zao kwamba hatimaye walikuwa wakienda kupata mtoto wa kike hivyo wangefanya sherehe moja kubwa ambayo ingewafanya waandishi kuiandika sana na kutawala mno katika mitandao ya kijamii.

    Siku zikaenda mbele, miezi ikakatika na hatimaye miezi tisa kutimia, siku ambayo Bianca alitakiwa kujisikia uchungu akaanza kujisikia hivyo. Alipiga kelele chumbani na kwa sababu kulikuwa na mfanyakazi wa ndani, akamsaidia na mtunza bustani na kumuingiza ndani ya gari huku damu zikivuja.

    Aliogopesha, kwa jinsi alivyokuwa akilia, wakajua kulikuwa na tatizo kubwa, haikuwa kawaida kwa mwanamke kulia kama alivyofanya, huku Mrisho, kijana wa bustani akiendesha gari, dada wa kazi akampigia simu Richard na kumweleza kilichokuwa kikiendelea.

    “Mpo wapi?”

    “Tupo njiani tunakwenda Ocean Road,” alijibu dada wa kazi.

    “Nakuja!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hakutaka kuchelewa, alikuwa na kazi nyingi ofisini lakini hazikuonekana kuwa na umuhimu wowote ule, kitu alichokuwa akikifikiria kilikuwa ni mke wake, akaacha kila kitu na kwenda hospitalini huko.

    Siku hiyo alionekana kuwa tofauti, moyo wake ulikuwa na majonzi kuliko siku nyingine, alijitahidi kujifurahisha kwamba alikuwa akienda kupata mtoto lakini moyo wake haukuwa na furaha hata kidogo.

    Aliendesha gari kwa hofu kubwa, alipofika katika hospitali hiyo, akateremka na kwenda ndani ambapo huko akawakuta dada wa kazi na kaka wa bustani ambapo alipowauliza, akaambiwa kwamba hali ya Bianca haikuwa nzuri.

    “Imekuwaje?” aliuliza huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Alipoteza damu nyingi mno,” alijibu Mrisho.

    “Unasemaje? Mungu wangu! Amejifungua?” aliuliza Richard huku akitembeatembea, hata kukaa kwenye kiti alicshindwa.

    “Bado! Madaktari ndiyo wanafanya kazi yao ndani,” alijibu Mrisha.

    Alikaa mahali hapo huku akiwa na hofu tele, bado moyo wake ulikuwa na hofu, alihisi kabisa kwamba kulikuwa na tatizo lililokuwa njiani kutokea, akapiga magoti na kuanza kumuomba Mungu huku kijasho chembamba kikimtoka.

    “Mungu! Ninahitaji mtoto! Mungu naomba umuongoze mke wangu ajifungue salama,” alisema Richard huku akipiga kelele. Kadiri dakika zilivyozidi kwenda mbele ndivyo ambavyo moyo wake ulikosa amani zaidi.

    ****

    Vijana wa David waliogopa, walimfahamu bosi wao, hakuwa mtu wa mchezo, aliposema kwamba alihitaji kitu fulani, haraka sana alitaka kupata majibu ya kitu hicho. Alichukia kufanyiwa uhuni wa kuibiwa laptop yake na pesa zake, alikasirika, hakutaka kuona mwizi huyo akiendelea kuishi, alichokitaka ni kumuua kama malipo kwa kile alichokuwa amekifanya.

    Vijana wakaingia mitaani, kwa kuwa Ibrahim alikuwa akijulikana sana kama muokota chupa, hata walipoanza kumtafuta hakukuwa na ugumu wowote ule, ilikuwa ni kumuulizia kijana aliyekuwa akiokota chupa na hivyo kuonyeshewa mahali alipokuwa akiishi.

    “Ni mtoto wa mitaani?” aliuliza Jumanne, mmoja wa wanaume waliotumwa na David.

    “Ndiyo!”

    “Anauza chupa wapi?”

    “Ilala Mabondeni!”

    “Twende!”

    Hawakutaka kubaki mahali hapo, ilikuwa ni lazima waende kumtafuta, waliamini kwamba kama kweli alikuwa ameelekea huko ilikuwa ni lazima wampate. Njiani walikuwa wakizungumza, walimuona mkuu wao alivyokuwa na hasira, siku hiyo hasira zake zilikuwa tofauti na siku nyingine, alivimba, aliwaka, alichokuwa akikihitaji ni vitu vyake tu.

    Jumanne na mwenzake, Fred wakafika mpaka Ilala Mabondeni, hapo, kulikuwa na sehemu iliyokuwa na milima mikubwa ya chupa, wakawafuata vijana fulani waliokuwa mahali hapo na kuwauliza kuhusu Ibrahim, kijana aliyekuwa akiokota chupa maeneo ya Posta.

    “Huko Posta hawaruhusu watu kwenda kuokota, sasa iweje huyo aende huko?” aliuliza kijana aliyekuwa mahali hapo.

    “Hatujui, ila alikwenda huko. Unamjua?” aliuliza Jumanne.

    “Hapana! Wapo wengi sana, au labda mngenionyeshea picha zake,” alisema kijana huyo.

    Hawakutaka kumficha, waliona kwamba huyo ndiye angekuwa msaada wao mkubwa. Wakamwambia kilichokuwa kimetokea, jinsi kijana huyo alivyotumia nafasi ya kuokota chupa na kuwaibia kiasi kikubwa cha pesa.

    “Huyo atakuwa Ibra!” alisema kijana huyo.

    “Kwa nini?”

    “Alikuja hapa na kusema kwamba haokoti tena chupa! Maisha yake yanakwenda kuwa ya kitajiri,” alisema kijana huyo.

    “Tutampata wapi?”

    “Nendeni Ilala Bungoni, kule kulipokuwa na Chuo cha DSJ, kuna nyumba ina rangi ya Bluu, hapo kuna watoto wengi wa mitaani, yupo hapohapo,” alisema kijana huyo.

    Jumanne na Fred hawakutaka kupoteza muda, wakaingia ndani ya gari na kisha kuanza kuelekea huko walipoelekezwa. Njiani walikuwa na presha kubwa, waliambiwa kwamba kama itawezekana wamuue mtu huyo kwani hakutakiwa kabisa kuishi kutokana na kile alichokuwa amekifanya.

    Hawakuchukua muda mrefu wakafika mahali hapo, kama walivyoambiwa kulikuwa na watoto wengi wa mitaani, wakaanza kuangalia huku na kule, hawakujua Ibrahim alikuwa yupi kwani hata kamera za CCTV walizoonyeshwa hawakumuona vizuri.

    Wakamuita msichana mmoja na kumuuliza, huyo ndiye aliyewaambia kwamba Ibrahim alikuwa ameondoka na demu wake kuelekea Magomeni kwa lengo la kupanga chumba na muda huo hawakuwa mbali, kama wangekimbia kuelekea Ilala Boma wangekutana nao njiani.

    Wakarudi garini na kuanza kuelekea huko Ilala Boma, njiani walikuwa wakiangalia huku na kule, walipofika Amana, kwa mbele wakawaona watoto wawili, walikuwa wachafuwachafu na walikuwa wakitembea kwa mwendo wa kasi, hivyo kuanza kuwafuata.



    Ibrahim alirudi mpaka kule alipokuwa akilala na Malaika, alipofika, hakumwambia kitu kwa kuwa alikuwa na watoto wengine, akamvutia pembeni na kwenda naye kukaa sehemu, Malaika alishangaa, haikuwa kawaida, alimwangalia Ibrahim, jinsi alivyokuwa siku hiyo alionekana kabisa kuwa na kitu alichotaka kumwambia.

    Kabla ya kuzungumza kitu akamwangalia Malaika, alitamani kumwambia ukweli lakini moyo wake ulikuwa mzito kufunguka. Mkononi alishikilia mfuko wa nailoni ambao ndani yake kulikuwa na laptop aliyokuwa ameiba na ile bahasha iliyojaa pesa.

    “Kuna nini?” aliuliza Malaika huku akimwangalia Ibrahim.

    “Tuondoke!”

    “Tuondoke! Kwenda wapi?” aliuliza Malaika.

    “Popote! Hapa si salama kwetu,” alisema Ibrahim huku akimwangalia Malaika.

    Malaika hakutaka kukubaliana naye, kwanza alitaka kufahamu ni kitu gani kilikuwa kimetokea, halikuwa suala la kuondoka mahali hapo pasipo kujua kulikuwa na nini. Alimuuliza Ibrahim lakini kijana huyo hakutaka kumjibu kitu chochote kile.

    “Kuna nini?”

    “Hakuna kitu!”

    “Sasa tutaondokaje? Mimi siwezi kuondoka,” alijibu Malaika.

    Alimaanisna alichokizungumza, asingeweza kuondoka kuelekea sehemu yoyote ile. Hapo ndipo palikuwa nyumbani kwake, hakuwa na ndugu, watu pekee aliokuwa amewazoea walikuwa watoto wenzake hao tu.

    Ibrahim hakutaka kumwambia Malaika ukweli, hakumwamini msichana, alijua kwa namna moja au nyingine kama ungeamua kumwambia ukweli, hata kama ungemwambia hiyo ni siri asingeweza kuitunza.

    Alipoona Malaika amekataa kuondoka naye, kwa hasira akaondoka zake. Kwanza alitaka kwenda kutafuta chumba Magomeni ili pale atakapomwambia Malaika kwamba wanaondoka, basi ajue ni mahali gani walipokuwa wakienda.

    Alizunguka Magomeni huku akiwaulizia madalali ambapo baada ya kumpata akaambiwa kwamba chumba kilikuwepo kwa mzee Masharubu hivyo kwenda kukiona. Kilikuwa chumba kizuri, akakipenda na hivyo na hivyo kulipia, akaacha kila kitu humo na kurudi Ilala mikono mitupu kwa ajili ya kumchukua Malaika na kuondoka naye.

    “Nimesema siondoki mpaka uniambie kwanza,” alisema Malaika.

    “Sawa. Ngoja nikwambie,” alisema Ibrahim.

    Hakutaka kumficha, alimpenda, alikuwa msichana wake ambaye alimchukulia kama mke wake, akamwambia jinsi hali ilivyokuwa tangu hatua ya kwanza mpaka alipokuja kuiba kiasi kile cha fedha na kuondoka nacho.

    Malaika aliogopa, alitetemeka, hakujua vitu hivyo aliibiwa nani, hakujua mwenyewe angechukua hatua gani kama angemgundua kwamba yeye ndiye aliyeiba vitu hivyo.

    “Posta kubwa mpenzi! Hawawezi kunijua. Tuondoke,” alisema Ibrahim huku akionekana kuwa na uhakika kwamba kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angemgundua.

    Malaika akakubaliana naye na kuondoka mahali hapo. Walikuwa wakitembea kwa mwendo wa taratibu, walikuwa wakizungumza mambo mengi, walipanga biashara zao ambazo walitakiwa kuzifanya wakiwa huko. Walipigwa na maisha na waliamini kwamba pesa zile zingeweza kuyabadilisha maisha yao.

    Huku wakiwa wamefika Ilala, ghafla gari moja likafunga breki pembeni yao, hawakujua walikuwa wakina nani, waliduwaa, walilishangaa gari hilo ambalo ghafla likafunguliwa milango, wanaume wawili wakatoka, wakawafuata na kuwakamata wote wawili, hawakutaka kuwauliza maswali yoyote yale, wakawapakiza ndani ya gari.

    Watu waliokuwa njiani walikuwa wakishangaa, hawakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Mara ya kwanza walihisi ni watu waliokuwa wakiigiza, lakini baada kupakizwa ndani ya gari na kuondoka mahali hapo wakagundua kwamba watu hao hawakuwa wakiigiza bali lilikuwa tukio la utekaji lililokuwa likitokea mahali hapo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Malaika alikuwa akilia, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alipiga kelele lakini ghafla akashtukia akizabwa vibao vitatu mfululizo, damu zikaanza kumtoka mdomoni kwani vibao vile vya shavu viliuchana mdomo wake kwa ndani.

    “Nyamaza nguruwe weee,” alisema Jumanne huku akimwangalia Malaika kwa macho ya hasira.

    “Tumefanya nini bro?” aliuliza Ibrahim lakini badala ya kujibiwa swali hilo, akaanza kupigwa ngumi za mbavu mfululizo.

    Wote wakaamriwa kunyamaza, hawakutakiwa kuzungumza kitu chochote ndani ya gari. Watu hao walionekana kuwa na hasira mno, viunoni mwao walikuwa na bastola, walikuwa tayari kufanya kitu chochote kile kama tu wangeambiwa na David wakifanye.

    “Mkuu! Tumempata mtuhumiwa!” alisema Jumanne wakati akizungumza na David kwenye simu.

    “Safi sana! Kompyuta mmeipata?”

    “Bado! Ndiyo tunataka atupeleke ilipo. Tukiipata tufanye nini bosi?” aliuliza Jumanne.

    “Muueni!”

    “Ila tumemkuta na demu wake, itakuwaje?” aliuliza Jumanne.

    “Waueni wote wawili na miili yao muende mkaitupe,” alisema David na kukata simu.

    Hayo ndiyo yalikuwa maagizo waliyokuwa wamepewa, wakamuuliza Ibrahim mahali kompyuta ilipokuwa, akawaambia kwamba aliiweka katika chumba kimoja kilichokuwa Magomeni. Wakamwambia waende huko na hivyo safari ya kwenda huko ikaanza.

    Hawakuchukua muda mrefu wakafika Magomeni Mapipa ambapo wakaenda mpaka katika nyumba aliyopanga Ibrahim na kisha kumwambia apige hodi. Mlango ulipofunguliwa, wakabadilika, wakajifanya kuwa marafiki wa David na hivyo kuelekea chumbani.

    Ilikuwa ni vigumu kugundua kwamba Jumanne alikuwa adui mkubwa wa Ibrahim kwani walikuwa wakizungumza kwa furaha kana kwamba hakukuwa na jambo baya lililokuwa nyuma yao.

    Wakaingia mpaka chumbani, kulikuwa na mfuko uliokuwa na kompyuta hiyo lakini pia kulikuwa na bahasha. Hakutaka pesa, kitu muhimu kilikuwa ni ile kompyuta. Akaichukua na kisha kutoka ndani ya chumba kile na kurudi garini ambapo Fred alibaki na Malaika.

    “Jamani! Si mmekwishapata mnachokitaka. Naomba mtuache,” alisema Ibrahim huku akilia kama mtoto.

    “Bado kuna kazi! Tunaelekea msitu wa Pande kwenda kufundishana adabu kidogo ili iwe fundisho,” alisema Jumanne huku akijigusa kiunoni kuona kama bastola yake ilikuwepo.

    Safari ya kuelekea katika msitu wa Pande ikaanza. Ibrahim na Malaika hawakujua kulikuwa na kitu gani lakini mioyo yao ilihisi kabisa kwamba walikuwa wakienda kuuawa. Walijitahidi kuomba msamaha lakini hawakusamehewa, watu hao walitaka kutekeleza maagizo waliyopewa na bosi wao kwamba ni lazima wawaue.

    “We have to kill them both, that is an order from the big boss,” (Inabidi tuwaue, hiyo ni amri kutoka kwa bosi mkuu) alisema Jumanne kwa Kiingereza kwa kuamini kwamba mateka wao hawakuwa wakielewa.

    “No problem,” (hakuna tatizo) alijibu Fred huku safari ikiendelea kama kawaida, na muda huo tayari walikuwa wanakaribia Mbezi kwa Msuguri.

    ****

    David alikuwa kimya sebuleni kwake, masikio yake aliyategesha katika simu yake, alikuwa akisikilizia ni kitu gani kingetokea baada ya kuwatuma vijana wake kwa ajili ya kumuua kijana ambaye alimuibia pesa zake na laptop yake ambayo ilikuwa muhimu kuliko kitu chochote kile.

    Alitaka kusikia kwamba kijana huyo amekufa kwani hakutaka kuona akiendelea kuishi kutokana na kile alichokuwa amekifanya ambacho kwake kilionekana kama kumpotezea muda na baya zaidi kumpotezea marafiki zake ambao mambo yao mengi alikuwa ameyahifadhi katika kompyuta ile.

    Japokuwa aliambiwa kwamba angepigiwa simu lakini aliona kama vijana hao wanachelewa na hivyo kuwa na kimuhemuhe cha kutaka kuwapigia na kusikia ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea huko.

    Akaichukua simu yake na kumpigia Jumanne ambapo baada ya kupokea akamwambia kwamba kila kitu kilikuwa tayari na kijana huyo alitekwa akiwa na msichana, akaagiza kwamba wote hao ilikuwa ni lazima wauawe.

    “Haina shida,” alisema Jumanne.

    Akarudi kwenye kiti chake, akashusha pumzi ndefu na kukunja nne, hatimaye kile alichokuwa amekihitaji kilifanyika na hivyo kilichokuwa kikisubiriwa ni kitu kimoja tu, kuwaua watu hao na maisha yake kuendelea.

    Akaendelea kusubiri zaidi, baada ya saa moja akaona simu yake ikianza kuita, kwa haraka sana akaichukua na kuangalia namba, simu ilikuwa ikitoka kwa Jumanne, haraka sana akaipokea.

    “Imekuwaje?” aliuliza huku akiwa na presha ya kutaka kujua kilichotokea.

    “Tumemaliza, hakukuwa na ugumu wowote ule, tumefumua vichwa vyao,” alisikika Jumanne kutoka upande wa pili.

    “Safi sana.”

    “Hakikisha unakaa kwenye televisheni bosi kuangalia, manake kwa tulivyofanya, vyombo vya habari vitatangaza sana mwaka mzima,” alitamba Jumanne.

    “Safi sana. Hiyo ndiyo adhabu yao wote wawili japokuwa hako kasichana hakakuhusika ila kaache nako kafe,” alisema David, akafurahi sana na kisha kukata simu.

    ****

    Richard alibaki akiwa anatetemeka pale kitini alipokuwa amekaa, hakuamini kama kweli mke wake angejifungua salama au la, muda wote alionekana kuwa na hofu tele na wakati mwingine aliikutanisha mikono yake na kumuomba Mungu amfanyie muujiza ili mkewe ajifungue salama salimini.

    Alimwangalia dada wa kazi, kwa jinsi alivyoonekana, alionekana kuwa na hofu kubwa, alihisi kwamba wakati mkewe akifikishwa katika hospitali hiyo hakuwa mzima kiafya, hakuwa na dalili za kupona kama ilivyokuwa kwa wanawake wengine.

    Wakati akiwa amekwishakata tamaa, mara mlango ukafunguliwa na daktari kutoka ndani ya chumba kile. Haraka sana Richard akasimama na kumsogelea, alitaka kujua ukweli juu ya kile kilichokuwa kikiendelea mule ndani.

    Uso wa daktari huyo ulimpa majibu yaliyomvunja moyo, hakuonekana kuwa na furaha, amani, na hata mlango ulivyokuwa wazi, kama mkewe alijifungua salama ilikuwa ni lazima angesikia sauti ya mtoto akilia, cha ajabu kabisa, chumba kilikuwa kimya.

    “Nini kimetokea? Mke wangu amejifungua salama?” aliuliza David huku akimwangalia daktari huyo.

    “Njoo ofisini kwangu!”

    Richard hakuwa na la kufanya zaidi ya kumfuata daktari huyo. Moyo wake ulikuwa na hofu kubwa, hakuamini kama mke wake alijifungua salama, alijua kulikuwa na tatizo kubwa na ndiyo maana daktari hakutaka kumwambia akiwa nje ya chumba kile.

    Hakumfuata peke yake bali hata mtunza bustani na dada wa kazi wote walisimama na kumfuata daktari huyo ambapo baada ya kuingia ndani ya ofisi hiyo, wakakaribishwa katika viti na kutulia, wakabaki wakimwangalia daktari huyo.

    “Kwanza pole sana,” alisema daktari huyo.

    Hakutaka kumficha kitu chochote kile, alimwambia ukweli kwamba yeye na madaktari wenzake walijitahidi sana kuokoa maisha ya mke wake na mtoto lakini wakafika kipindi ambacho walitakiwa kumuokoa mtu mmoja na mwingine afe kwani Bianca alikuwa amepoteza damu nyingi na alipata tatizo kidogo katika mfumo wake wa uzazi.

    “Tukaona ni bora kuyaokoa maisha ya mama,” alisema daktari huku akimwangalia Richard.

    “Kwa hiyo mtoto wangu amekufa? Mtoto wangu amekufa?” aliuliza Richard huku akilia kama mtoto, machozi yalitiririka mashavuni mwake.

    “Pole sana,” alisema daktari huyo.

    Richard hakuacha kulia, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kile kilichokuwa kimetokea, alimpenda sana mke wake na alikuwa akijiandaa kupata mtoto wake wa kwanza. Walikuwa wamekwishamfanyia shopping hata kabla ya kuzaliwa. Moyoni mwake tayari alitengeneza upendo mkubwa kwa mtoto wake huyo ambaye kwa bahati mbaya sana, alifariki dunia japokuwa madaktari walijaribu kwa nguvu zao zote.

    Hakubembelezeka, kitu alichokuwa akikizubiria kwa hamu muda huo kilikuwa ni mtoto tu. Alilia na kulia huku akilitaja jina la mtoto wake ambalo tayari alikuwa amelipanga. Baada ya kubembelezwa kwa nusu saa nzima, akatolewa ndani ya chumba kile na kuelekea kule kulipokuwa na benchi ambapo alikaa na kujiinamia chini huku akilia kwa kugugumia.

    Hakutaka kumuona mtu yeyote zaidi mke wake, Bianca ambaye hakujua alikuwa kwenye hali gani kipindi hicho. Baada ya saa moja, Bianca akatolewa ndani ya chumba kile na kupelekwa katika chumba kingine.

    Alikuwa kimya kitandani, dripu ya maji ilikuwa ikining’inia juu ya kitanda chake. Hakuwa na fahamu, hakujua kitu gani kilikuwa kikiendelea. Richard alipomuona mke wake, akasimama na kuanza kukisogelea kitanda kile. Alikuwa akilia kwa uchungu, hakuamini kile alichokuwa akikiona.

    Mlango wa chumba kingine ukafunguliwa na yeye kutakiwa kubaki nje, alibaki akiwa amesimama nje ya mlango wa chumba hicho. Alikuwa akilia, kila kitu alichokuwa akikipitia wakati huo alihisi kama alikuwa katika njozi fulani ya kusisimua ambapo baada ya muda angeshtuka na kujikuta akiwa kitandani.

    “Bianca mke wangu!” aliita Richard kwa sauti ya chini, machozi yaliendelea kumtiririka mashavuni mwake.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari ilikuwa ikiendelea kuelekea katika Msitu wa Pande, kitu kilichokuwa kichwani mwao ni kufanya mauaji kwa watoto hao bila kuwaonea huruma. Mawingu yalijikusanya angani na baada ya dakika chache, manyunyu yakaanza kudondoka na hatimaye mvua kubwa kuanza kunyesha.

    Hilo halikuwazuia kusonga mbele, ilikuwa ni lazima kuhakikisha kwamba wanafanya kile walichotakiwa kufanya. Safari iliendelea na walipofika sehemu ambayo ilionekana kuwa nzuri kuingia upande wa wa msitu huo, gari likakatwa kona na kuingia humo.

    Ibrahim alikuwa kimya, kipigo alichokuwa amepewa kilimchosha kupita kawaida. Alivimba, aliamua kunyamaza kwani kama kuomba msamaha, alijitahidi sana kufanya hivyo lakini hakukuwa na mtu aliyejali chochote kile.

    Wakati wakiwa wameingia msituni, ghafla hali ya ajabu ikaanza kumshika Malaika, akaanza kutetemeka pale alipokuwa na ndani ya sekund chache akaanza kupiga kelele za maumivu makali.

    Kila mmoja alishangaa, kabla walihisi kwamba alikuwa akijifanyisha lakini walivyomwangalia, alionekana kuhisi maumivu makali. Mwili wake ukaanza kuvimba, akazidi kutetemeka kama mtu aliyekuwa akisikia baridi kali.

    Damu zikaanza kumtoka puani. Hali ilionekana kutisha, japokuwa Fredi na Jumanne walikuwa na roho za kinyama lakini wakaanza kumuonea huruma msichana huyo ambaye hapohapo akaanguka na kuanza kukakamaa mwili.

    “Kuna nini?” aliuliza Fredi huku akiendesha gari.

    “Hata mimi sijui! Wewe, mwenzio mgonjwa huyu?” aliuliza Jumanne.

    “Sijui! Nashangaa! Sikuwahi kumkuta kwenye hali hii hata siku moja,” alisema Ibrahim huku akionekana kuogopa, akamsogelea Malaika pale chini, msichana huyo aliendelea kukakamaa huku damu zikimtoka na macho yake kuanza kuwa mekundu kama yaliyokuwa yakikusanya damu nyingi.

    “Malaika! Malaika! Malaika!” aliita Ibrahim huku akianza kulia.

    Hakukuwa na safari ya kuingia zaidi msituni, Fredi akalisimamisha gari lake na kuanza kurudi walipotoka. Walikuwa wakienda kuwaua watu hao, japokuwa naye alitakiwa kuuliwa lakini hali aliyokuwa nayo ilimuumiza kila mtu.

    Wakarudi barabarani, wakasimisha gari na kumwambia Ibrahim ateremke na Malaika huku mvua kubwa ikipiga nje. Ibrahim hakuwa na jinsi, akamchukua Malaika wake, akamshusha kutoka garini na kumuweka kwenye lami.

    “Bro! Mbona mnataka kutuacha! Mbona mnanichia majanga?” aliuliza Ibrahim huku akilia, kila alipomwangalia mpenzi wake, Malaika moyo ulimuuma mno.

    “Baki naye, utaomba msaada! Msaada pekee tuliowapa ni kuwaacheni hai!” alisema Jumanne na Fredi kuliondoa gari mahali hapo ambapo baadaye akampigia simu David na kumwambia kwamba tayari waliwaua watu hao kwa kuamini kwamba wasingeonana tena katika maisha yao.

    Ibrahim akabaki na Malaika wake, aliangalia kila upande, hakukuwa na magari mengi yaliyokuwa yakipita na hata yale machache yaliyokuwa yakipita mahali hapo hayakuwa yakisimama hata kidogo.

    Alishindwa kujua afanye nini, kila alipomwangalia Malaika, moyo wake ulimwambia kwamba hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho za uhai wa msichana huyo mdogo ambaye tangu kuzaliwa kwake, alikuwa mtu wa kuteseka tu.

    “Malaika usiniache! Usiniache Malaika subiri niendelee kusimamisha magari,” alisema Ibrahim huku akiwa amemuinamia msichana huyo na mvua kali ikiendelea kunyesha.

    Ibrahim hakutaka kuacha, bado alihitaji msaada mkubwa kutoka kwenye gari lolote lile, alimwangalia msichana Malaika, alionyesha kabisa kwamba alikuwa akienda kufa kwani kwa jinsi mwili wake ulivyokuwa, alionekana kutokuwa na muda mwingi wa kuendelea kuishi.

    Magari hayakusimama, yaliendelea kuwapita. Uamuzi wa mwisho kabisa alioufanya Ibrahim ni kumbeba Malaika na kumuweka katikati ya barabara na kusimama karibu yake, alitaka kuona gari lolote ambalo lingepita alisimamishe.

    Wala hazikupita dakika nyingi, gari ndogo aina ya Spacio likaonekana mbele yake. Ibrahim akapunga mikono juu kama kulisimamisha gari hilo. Alikuwa akipiga kelele ili aonekane kwani kama asingelisimamisha na gari hilo kupita, ilimaanisha lingemgonga yeye na msichana Malaika aliyelala chini.

    Ilikuwa ni kama bahati, dereva wa gari hilo akamuona, akafunga breki kwa nguvu na gari kusimama kama mita tatu kutoka pale aliposimama Ibrahim. Hakutaka kusikia lolote, akambeba Malaika na kulifuata gari hilo ambapo dereva akafungua kioo.

    “Vipi?” aliuliza dereva huyo.

    “Naomba mtusaidie! Malaika anakufa,” alisema Ibrahim, hapokuwa alikuwa na moyo wa kushujaa lakini alishindwa kujizuia, akaanza kulia, machozi yake hayakuonekana kutokana na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.

    Dereva huyo mwanaume akamwangalia Malaika, kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa kama mfu. Alitaka kumwambia Ibrahim asijisumbue sana kwa kuwa rafiki yake alikuwa amekufa lakini hakutaka kumuumiza.

    Akamfungulia mlango na kuingia ndani, akabaki akimshangaa Malaika, alionekana kuwa binti mdogo lakini hali aliyokuwa nayo ilimtisha mno.

    “Imekuwaje?” aliuliza dereva huyo.

    “Naomba utupeleke hospitali! Malaika wangu atakufa,” alisema Ibrahim huku akilia kama mtoto.

    Kwa hali aliyokuwanayo Malaika hakukuwa na la kupoteza mahali hapo, kwa haraka sana akapiga moto na kuondoka mahali hapo kwa kasi. Alikuwa na jukumu la kuyaokoa maisha ya msichana huyo mdogo, mvua kubwa iliendelea kunyesha lakini hilo halikumfanya kupunguza mwendo, aliendelea kusonga mbele kwa mwendo wa kasi.

    Akafika Kibamba katika Hospitali ya Dk. Faroukh, akaliingiza gari ndani ya hospitali hiyo ambapo machela ikaletwa haraka sana na msichana huyo kuwekwa juu yake na kusukumwa kuelekea ndani ya jengo la hospitali hiyo.

    “Mmh! Jamani! Kuna nini tena?” aliuliza nesi mmoja, alivyokuwa akimwangalia Malaika katika machela ile, aliogopa kwani kwa jinsi alivyokuwa, alionekana kama tayari alikuwa mfu.

    “Hali ni mbaya! Naomba muokoe afya ya binti huyu,” alisema dereva.

    Malaika akapelekwa mpaka katika chumba cha upasuaji na kuingizwa humo. Hawakuangalia pesa, kitu cha kwanza kabisa walichokijali kwa wakati huo ni hali ya msichana huyo mdogo.

    Alipofikishwa ndani, madaktari wawili wakaingia, waliguswa kumuhudumia msichana huyo mdogo ambaye alionekana kuhitaji msaada hasa. Ibrahim na dereva yule hawakutakiwa kuingia ndani, wakabaki nje kwenye benchi huku wakisikilizia ni kitu gani kingeendelea huko.

    Ibrahim alikuwa akilia mno, kwake, kila alipoangalia hakuona kabisa kama kulikuwa na dalili za mpenzi wake kupona. Alikata tamaa na aliona kabisa huo ndiyo ulikuwa mwisho wa msichana huyo mrembo.

    “Mungu naomba umsaidie! Naomba umponye Malaika wangu,” alisema Ibrahim huku akiwa amejiinamia.

    Muda ulizidi kwenda mbele, dakika zikakatika na mlango wa chumba kile haukufunguliwa. Kila mmoja akahisi kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wa msichana yule ila baada ya saa moja, ukafunguliwa na daktari kutoka.

    Uso wake tu ukaonyesha kile kilichokuwa kimeendelea ndani ya chumba kile hakikuwa kizuri, alionekana kukata tamaa, alionekana kama mtu ambaye alijitolea sana lakini mwisho wa siku hakufanikiwa kwa kile alichokuwa amekikusudia.

    Akawaangalia Ibrahim na dereva waliokuwa nje ya chumba kile kwenye benchi na kuwaomba kumfuata. Wakamfuata mpaka taika ofisi yake ambapo huko hakutaka kuwaficha, aliwaambia ukweli kwamba Malaika alikuwa kwenye hali mbaya, alikuwa akiumwa ugonjwa ambao kama angevuka salama miaka kumi na nane, angepona kabisa kwani asilimia tisini na tano walikuwa wakifa kabla ya kuvuka umri huo.

    “Anaumwa nini?” aliuliza dereva.

    “Sickle cell!”

    “Sickle cell?”

    “Ndiyo!”

    Dereva akashusha pumzi nzito, akamwangalia Ibrahim ambaye hata ugonjwa huo hakuwa akiufahamu, na mbaya zaidi hakuwahi hata kuusikia. Hakujua ulikuwa ugonjwa wa nini, hakujua ni kwa jinsi gani ugonjwa huo ulikuwa ukiathiri mwili wa mgonjwa.

    Sickle Cell ulikuwa ni miongoni mwa magonjwa mabaya yaliyokuwa yakiua watu wengi duniani hasa watoto. Mtu aliyekuwa na ugonjwa huu, mara nyingi ilikuwa ni lazima afe kama tu hatofikisha umri wa miaka kumi na nane na kuvuka salama.

    Ugonjwa huu ambao husababisha damu kupungua kwa kiwango kikubwa, tena mara kwa mara mwilini mwa mgonjwa, ulikuwa gumzo nchini Tanzania kipindi hicho. Ugonjwa huo unapokomaa, mwili wa mgonjwa hudhoofika na kusikia maumivu makali.

    Ni ugonjwa unaohitaji damu nyingi kwani mgonjwa anaweza kuwa na damu ya kutosha leo hii asubuhi na jioni akaonekana kutokuwa na damu ya kutosha kutokana na seli hai nyekundu kuzishambulia seli ambazo hupeleka damu katika mifupa.

    “Atapona?” lilikuwa swali la kwanza alilouliza Ibrahim.

    “Kupona atapona ila….”

    “Ila nini daktari!”

    “Sijajua kama atafikisha umri wa miaka kumi na nane. Kwa kifupi, katika kipindi hiki cha maisha yake kitakuwa ni kipindi chenye mateso sana. Atahitajika kula sana vyakula vya kuongeza damu lakini pia vilevile atatakiwa kwenda hospitali kuongeza damu mara kwa mara, hata kwa wiki mara kumi, vinginevyo, atakufa,” alisema daktari huyo ambaye hakutaka kuficha chochote kile.

    “Hivyo tu halafu atapona moja kwa moja.”

    “Kama atavuka miaka kumi na nane akiwa hai, ugonjwa utapona na ataishi ila kama hatovuka basi atakufa kwani ugonjwa huu huwa haumruhusu mtu kuvuka miaka hiyo, kwa bahati akivuka, na ugonjwa unapona moja kwa moja,” alisema daktari huyo maneno yaliyomfanya Ibrahim kushusha pumzi nzito.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/





    Malaika alikuwa kitandani, mwili wake haukuwa na nguvu, kwa juu, dripu ya damu ilikuwa ikining’inia. Aliyafumba macho yake, wakati mwingine aliyafumbua na kuangalia huku na kule.

    Alikuwa kwenye maumivu makali mno, pale kitandani alipokuwa, hakuacha kulia, aliumia na alihisi maumivu makali katika mifupa yake. Ugonjwa huo ulikuwa ukimtesa kupita kawaida, alionekana kukata tamaa na kila alipoangalia maisha yake ya mbele, alihisi kabisa kwamba alikuwa akiend kufa.

    Ibrahim ambaye alikuwa akiingia ndani ya wodi ile, alipokuwa akimwangalia msichana wake, moyo wake ulichoma kupita kawaida. Hakuamini kama hizo ndizo zilikuwa hatua za mwisho za msichana huyo.

    Wakati mwingine alikataa kabisa kukaa karibu naye kwani kwa jinsi msichana huyo alivyokuwa akilalamikia maumivu makali ya mifupa ilimfanya kutamani kulia, ili kupusha uchungu mkubwa moyoni mwake, wakati mwingine alikuwa akiondoka kabisa.

    Kipindi hicho kilikuwa ni cha mateso makali, aliendelea kukaa hospitalini hapo kwa siku mbili ndipo akaruhusiwa huku akiwa amekwishawekewa damu ya kutosha. Kitu kimoja alichokuwa akihitaji kukifahamu sana ni sababu iliyowafanya kutokuuawa na watu wale.

    Hakukumbuka kitu chochote ambacho kilitokea msituni. Alichokikumbuka ni kwamba walikuwa ndani ya gari, wanaume wale walisema kwamba walikuwa wakienda kuwaua ila cha ajabu kabisa mpaka muda huo wote walikuwa hai.

    “Nini kilitokea?” aliuliza Malaika.

    “Walituacha baada ya kuona upo hoi,” alijibu Ibrahim huku akimwangalia Malaika.

    “Kweli?”

    “Ndiyo! Unajisikiaje lakini?” aliuliza Ibrahim.

    “Kidogo nafuu! Ila wakati mwingine mifupa inauma mno,” alisema Malaika.

    Ibrahim aliumia, muda mwingi maneno ya daktari yalikuwa yakimjia kichwani mwake, akakosa amani, akakosa furaha na kujua kwamba mpenzi wake huyo kuna siku angekufa, na hata kwa jinsi walivyokuwa wakifurahia maisha, kuna siku msichana huyo asingekuwa mikononi mwake.

    Hakutaka kumwambia, alijua ni kwa namna gani msichana huyo angeumia kama tu angemwambia ukweli juu ya kile kilichokuwa kimetokea. Hakuishi kwa furaha tena, hata msichana huyo alipokuwa akimwambia maneno mazuri ya matumaini lakini bado kumbukumbu zake zilikuwa palepale kwamba ilikuwa ni lazima msichana huyo afariki dunia.

    Hawakuwa na maisha ya kitajiri, zile pesa alizokuwa ameziiba Ibrahim ndizo ambazo ziliyaendesha maisha yao. Alikuwa na akili ya biashara, alijua kabisa kwamba kwa kiasi alichokuwa nacho ingekuwa kazi nyepesi kabisa kama angeanzisha biashara na kufanikiwa.

    Hakuwa na umri mkubwa, wakati Malaika akiwa na miaka saba, yeye alikuwa na miaka kumi na sabab hivyo kidogo akili yake ilikuwa imepanuka vya kutosha. Akafungua genge la kuuza mbogamboga za majani, hakuishia hapo, akaamua kununua toroli na madumu na kuanza kuuza maji.

    Aliamini kwamba kupitia biashara hizo zingeweza kumsaidia. Ndani alibakiza kiasi cha milioni tano na alitaka kuona kiasi hicho kikiendelea kukua na si kupungua kwani kama kuyahatarisha maisha yake kwa ajili ya pesa hizo aliyahatarisha hivyo hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuzitumbua pesa hizo.

    “Ibrahim, naomba uniambie kitu kimoja,” alisema Malaika huku akimwangalia Ibrahim.

    “Kitu gani?”

    “Kwa nini huna furaha siku hizi?” aliuliza Malaika.

    “Nani? Mimi?”

    “Kwani kuna nani mwingine hapa?”

    “Malaika! Nafikiria zaidi maisha, ni kwa jinsi gani maisha yetu yataendelea kwenda mbele. Hivi huoni jinsi tunavyoishi kwa shida kidogo? Tuna pesa, nafikiria ni kwa jinsi gani nitaweza kufungua biashara nyingi,” alisema Ibrahim, alitoa maelezo mengi ambayo hayakuwa na maana.

    “Bado hujanipa jibu ninalolitaka,” alisema Malaika.

    Moyoni mwake alianza kuhisi kitu, akajua kwamba kulikuwa na kitu ambacho mwanaume huyo hakutaka kumwambia. Aliyahofia maisha yake, alijua kwamba kulikuwa na uwezekano wa kufa na ndiyo maana mwanaume huyo hakutaka kumwambia ukweli.

    Ibrahim alijikaza kiume, wakati ameulizwa swali hilo, hakutaka kuonyesha majonzi yoyote yale japokuwa bado kumbukumbu za maneno aliyoyasema daktari zilikuwa zikijirudia kichwani mwake.

    Hali ya Malaika haikubadilika, katika kipindi cha mvua ambacho kilikuwa na baridi kali alikuwa akilalamika maumivu ya mifupa hasa katika uti wa mgongo, alihisi kabisa pingili za uti wa mgongo zilikuwa zikiachia.

    Yalikuwa ni maumivu makubwa, akawa akipelekwa hospitalini ambapo huko, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuongezewa damu kwani ilikuwa ikipungua kwa kasi kubwa mno.

    Hayo yalikuwa ni maisha ya mateso, ugonjwa wa sickle cell uliendelea kuyatesa maisha yake kiasi kwamba kuna wakati aliomba kufa kwani mauamivu aliyokuwa akiyasikia hayakuwa yakielezeka.

    “Hizi Folic Acid zitaweza kumsaidia, cha msingi awe anakunywa kidonge kimoja kwa siku,” alisema daktari, alikuwa akimwambia Ibrahim.

    Folic Acid zilikuwa moja ya dawa zenye nguvu ambazo alitakiwa kunywa mgonjwa aliyekuwa akiumwa ugonjwa huo. Wakati seli hai nyekundu za damu zinapokuwa zikipambana kuhakikisha damu haipungui, dawa hiyo ndiyo inayozisaidia seli hizo katika mapambano hayo.

    Ilikuwa kazi kubwa, mwili ulikiwa kuwa na damu ya kutosha. Kila siku kazi ya Malaika ilikuwa ni kunywa vidonge hivyo ambavyo viliuzwa kwa bei ya juu lakini kwa kuwa Ibrahim alikuwa na pesa, hilo halikuonekana kuwa tatizo.

    “Kuna siku utapona tu!” alisema Ibrahim huku akimwangalia Malaika aliyeonekana kukata tamaa kabisa.

    “Kweli?”

    “Ndiyo!”

    “Ila nimesikia huu ugonjwa mbaya sana!”

    “Hakuna. Si ugonjwa mbaya! Ni ugonjwa wa kawaida ambao unaweza kupona kabisa,” alisema Ibrahim huku akimwangalia Malaika.

    Hiyo ndiyo ilikuwa kazi kubwa aliyokuwa nayo. Kila siku ilikuwa ni lazima amtie moyo kwani pasipo kufanya hivyo ilimaanisha kwamba binti huyo angekufa kwa kuwa tu angekata tamaa mbele yake alingeona giza.

    Kidogo Malaika akafarijika, kwake, kitu kilichompa tumaini la kuishi kwa kipindi kirefu kilikuwa ni maneno ya mwanaume huyo. Alimpenda kutoka moyoni mwake, na kila siku alimwambia kwamba hakuogopa kufa bali kitu pekee alichokuwa akikiogopa moyoni mwake ni kumpoteza tu.

    “Kweli?”

    “Ndiyo! Siogopi kufa tena! Kitu pekee ninachokiogopa ni kukupoteza mpenzi,” alisema Malaika huku akimwangalia mpenzi wake huyo aliyeonekana kuwa kwenye mapenzi ya dhati.

    ****CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha ya David yalikuwa ni kula bata tu, kila siku alikuwa mtu wa kusafiri kusafirisha madawa ya kulevya. Aliingiza kiasi kikubwa cha pesa na Bwana Mpobela alikuwa akimtegemea kwani mbali na kusafirisha huko, David alikuwa mjanja, viwanja vya ndege kulipoonekana kuna noma, alitumia kila ujanja hata kusafirisha kwa meli ya mizigo lakini mwisho wa siku mzigo ufike salama.

    Mpaka katika kipindi hicho, mke wake, Gloria hakujua kitu chochote kile, alidanganywa vya kutosha na kuona kwamba mume wake huyo alikuwa mfanyabiashara ambaye alikuwa akisafiri safiri.

    Biashara ilikuwa, watumiaji wa madawa ya kulevya wakaongezeka. David akatanua utajiri wake, akaanza kuvuma jijini Dar es Salaam kwamba alikuwa bilionea aliyekuwa akichipukia.

    Baada ya miaka miwili kufanya biashara hiyo, David akaanza kuvutika na utumiaji wa madawa ya kulevya. Alikuwa akishangaa, vijana wengi walikuwa wakitumia madawa hayo na kuyasifia, mzigo mkubwa aliokuwa akiupeleka Tanzania ulikuwa ukimalizika kwa kipindi kifupi sana hali iliyomfanya kugundua kwamba kulikuwa na watumiaji wengi waliokuwa wameongezeka.

    Alitaka kujua kuhusu madawa hayo, kama kuna wengi walikuwa wakivuta na kuendelea kuishi, kwa nini na yeye asijaribu kufanya hivyo? Hapo ndipo alipoanza kujiingiza katika utumiaji wa madawa hayo.

    Hakutaka kumwambia mkewe, alifanya kificho, siku za kwanza zilionekana kuwa za mateso lakini baada ya wiki moja ya kutumia, akavutiwa mno na madawa hayo. Kila alipokuwa akivuta, akili yake ilihama, alijiona kuwa na nguvu kubwa, alijiamini na alihisi kuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote lile.

    Hiyo ilikuwa ndiyo stimu yenyewe. Alipokuwa akivuta, alijifungia hotelini na kuanza kubwia unga mdogomdogo kitu kilichomfanya kujisikia hali ya tofauti kuliko kipindi cha nyuma.

    Taratibu akawa anaingia katika mkumbo wa matumizi ya madawa hayo, wakati mwingine hakuwa akifanya kazi nyingine zaidi ya kujifungia hotelini na kuanza kuvuta madawa hayo ambayo kwake yalionekana kuwa kitu bora na muhimu kuliko vyote katika dunia hii.

    “Nilichelewa sana kujua 

0 comments:

Post a Comment

Blog