Search This Blog

Friday, July 15, 2022

NILIVYOMLIZA MKE WANGU KWA SIKU 366 - 4

 







    Simulizi : Nilivyomliza Mke Wangu Kwa Siku 366

    Sehemu Ya Nne (4)



    Hapo tulikuwa tumefika Magomeni Hospitali, kipindi kile kabla barabara za mabasi yaendayo kasi hazijaanza kutengenezwa. Kigiza kilianza kuingia, nikawa namwangalia kwa macho yale ya ‘Nikiomba utanipa?’ naye bila soni akawa ananiangalia kwa macho yale ya ‘Sasa mbona huombi? Au unaogopa?’

    Mimi: Irene, umetokea kunivutia sana na sijui kama nikihitaji niwe nawe itawezekana!

    Irene: Kuwa nami kivipi?

    Mimi: Kimapenzi, unadhani kuna kingine zaidi ya hicho? Ninahitaji faraja kutoka kwa msichana mrembo kama wewe, unayejitambua na kujiheshimu. Nahisi nikiwa nawe, nitakuwa miongoni mwa wanaume wenye bahati kubwa.

    Irene: Hahaha! Una manenooooo

    Mimi: Kweli tena! Mara ya kwanza nilipokuona, nilihisi kabisa moyo wangu ukikupenda, nikakufuata huku nikihisi kwamba usingenionyeshea mapokezi mazuri, kumbe upo simpo sana, umenivutia na umenifanya nikupende Irene.

    Irene: Ya kweli hayo?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Nadhani hakuna sifa kukudanganya na ndiyo maana nimeamua kukwambia ukweli....

    Irene: Asante sana.

    Mimi: Kwa hiyo?

    Irene: Kuhusu nini laaziz?

    Mimi: Nataka baadaye nije nikuchukue.

    Irene: (akajifanya kushtuka) Unipeleke wapi?

    Mimi: Tukatembee sehemu, ninajisikia amani nikiwa karibu nawe, najisikia furaha sana mpenzi...naomba nije nikufuate baadaye!

    Irene: Mmh!

    Nilichokifanya ni kumsogelea pale alipokuwa na kuanza kuhema kwa chini karibu kabisa na yeye. Sikiliza ndugu yangu, mimi nilikuwa mhuni tu uswahili, najua njia zote za kumpagawisha mwanamke, najua jinsi ya kuzungumza naye na ndiyo maana hata kama msichana alikuwa mgumu, kuna tekniki nilikuwa nazitumia mwisho wa siku anajikuta akiwa ndani na mimi.

    Ndiyo ilivyokuwa kwa Irene! Kwanza nikagundua kwamba hakuwa mgumu, kama angekuwa mgumu, asingekubali kuingiandani ya gari langu! Wewe toka lini unamtokea demu mgumu, unataka kumpa lifti anakuchomolea? Ipo, lakini kwa Irene, nikaona piga ua lazima mtu mzima ning’oe.

    Wakati nazungumza naye kwa sauti ya kunong’oneza, nikaona kama nikibaki hivihivi kama sanamu noma nisingefanikiwa, nikauchukua mkono wangu na kuupeleka begani kwake na kuanza kushuka chini, nikashangaa kuona pumzi zake zinabadilika. Nikaona haiwezekani, nikavua shati langu.



    Irene: Mbona unavua shati! Unataka kufanya nini jamani?

    Mimi: Kukupepea....

    Irene: Kunipepea na wakati AC inafanya kazi.

    Mimi: Sasa unaona kabisa navua shati, unaniuliza nataka kufanya nini tena jamani! Jamani, kwani haujui kwamba ukitaka kula lazima uandae sahani!

    Irene: Hahaha!

    Nikaona kwisha kazi yake, wakati namsogelea zaidi, nikashtuka baada ya kusikia kioo cha gari kikigongwa, kuangalia, alikuwa msela ambaye sikumuelewaelewa. Nikashusha kioo.

    Mimi: Nikusaidie nini? (niliuliza kwa hasira)

    Jamaa: Umepaki vibaya gari, si unasikia unapigiwa honi wewe tu!

    Aliponiambia hivyo ndipo nikasikia honi nyingi nyuma yangu. Wakati nilipokuwa nikimwangalia Irene ndani ya gari lile, wala sikusikia hizo honi zote mpaka nilipoambiwa na kutuliza masikio yangu.

    Sikuwa na neno, nikapiga gia na kuondoka mahali hapo mpaka katika kituo cha Magomeni Mapipa ambapo Irene akataka ateremke.

    Mimi: Kwa hiyo?

    Irene: Si una namba yangu! Utanicheki lovie....

    Mimi: Poa.

    Huyu Irene akaanza kunichanganya, safari nzima nilikuwa nikimuwaza yeye tu, kiukweli sikumpenda ila nilimtamani kutokana na mazingira niliyomkuta nayo na hata yale mapozi yake aliyokuwa akiniwekea.

    Sikuchukua muda mrefu nikafika nyumbani, nikalipeleka gari katika sehemu ya maegesho na kuelekea ndani. Kama kawaida nikamkuta mke wangu Salama akiwa sebuleni akiangalia televisheni, sikumsalimia japokuwa nilimuona, nikapitiliza mpaka chumbani na kutulia kitandani.

    Kichwa changu kilimpa nafasi kubwa msichana Irene, nikachukua simu yangu na kuangalia namba yake, hakika niliiona namba yake kuwa nzuri kweli, rahisi kukariri japokuwa ilikuwa 739284.

    Wakati nikiwa kwenye feelings zangu, nikasikia mlango ukigongwa, nilijua alikuwa Salama, nikataka kujua alikuwa akitaka nini, nilipomkaribisha, akaingia huku akiwa amebeba sahani zilizokuwa na chakula na kunifuata kitandani.

    Salama: Pole na kazi mume wangu!

    Mimi: (Sikujibu)



    Akaweka chakula kitandani, akatoka na kwenda kuchukua juisi, akarudi na kuniwekea chini kisha akatoka chumbani humo kiheshima kweli. Nikabaki nikiangalia chakula kile, eti nikile, kama kaniwekea limbwata je? Nimpende ghaflaghafla kwa mapenzi ya kubebana mpaka chooni? Sikutaka kukubali, ndiyo kwanza nikakitoa kitandani na kukiweka pembeni kabisa, nikaanza kuchati na mtoto Irene.

    Mimi: Yaani bado wewe mtoto unazunguka kichwani mwangu!

    Irene: Kweli jamani?

    Mimi: Ndiyo! Umeniwekea dawa nini?

    Irene: Jamaniiiii! Unanionea tu...mimi dawa niitoe wapi?

    Mimi: Hahaha!

    Irene: Nikuulize swali mpenzi?

    Mimi: Niulize tu.

    Irene: Nyumbani unaishi na nani?

    Mimi: Mfanyakazi wangu wa kike....

    Irene: Mmhhh!

    Mimi: Nini sasa?

    Irene: Mpo wawili tu?

    Mimi: Ndiyo!

    Irene: Nyumba nzima?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Ndiyo!

    Irene: Mmh!

    Mimi: Najiiamini bwana, wala usijali, kwanza lini utakuja kunitembelea kwangu?

    Irene: Wewe tu, siku yoyote na muda wowote ukitaka nije, nitakuja.

    Mimi: Kwa hiyo hata sasa hivi?

    Irene: Niruhusu uone.....

    Mimi: Basi njoo!

    Irene: Nipe dakika ishirini za kujiandaa, nakuja kukuonyeshea kwa nini watu wanasema mapenzi yamezaliwa Tanga.....

    Mimi: Utawezaaaaaaaa?

    Irene: Utaona mwenyewe....si unamjua nyigu lakini alivyo na kiuno chake?

    Mimi: Namjua.....

    Irene: Basi leo umekutana na nyigu mtu...nakuja.....

    Nikapagawa, nikachanganyikiwa, sikuamini kile nilichokuwa nikikisoma. Yaani mimi nilimchukulia demu mguuuumu, nilikuwa namvutia kasi kumbe wapi! Mtoto mwepesi mno, nikasema poa, ngoja nimsikilizie.



    Baada ya dakika ishirini, akaniambia nimuelekeze achukua bajaj lakini hela ningelipia mimi, nikasema poa, nikamuelekeza, ndani ya dakika kumi na tano, nikasikia bajaj ikiwa imepaki nje.

    Harakaharaka nikatoka chumbani, sebuleni nilipopita, alikuwepo Salama, alikuwa amelala kwenye kochi, akashtuka na kuniangalia, alitaka kujua kuna nini kwani haikuwa kawaida yangu kabisa kutoka nje usiku namna hiyo.

    Akasimama na kuniangalia, wala sikujali, nikafungua geti na kutoka nje, nilipomuona Irene tu, nikamfuata, nikamkumbatia na kumpa mahaba mazito, mabusu mfululizo mpaka dereva bajaj akatushangaa. Nikamlipa hela yake.

    Nikaingia ndani pamoja naye. Inawezekana Salama alipoona naingia na demu akapigwa na mshangao, akaumia lakini wala sikujali. Nilipofika sebuleni, nikamtambulisha kama mfanyakazi wa ndani.

    Mimi: Irene, huyu ndiye dada wa kazi anayenisaidia kazi hapa ndani. Salama, huyu ni wifi yako! (nilimwambia bila soni usoni)

    Irene: Mambo wifi!

    Salama: Safi tu, karibu wifi yangu.....

    Sikutaka kubaki naye sebuleni hapo, nilichokifanya ni kumchukua na kumpeleka chumbani. Huku nyuma sikujua kama niliacha maumivu makali kwa Salama. Usiku huo, wakati mimi napata raha ndani, mwenzangu alikuwa akilia. Aliomboleza kupita kawaida. Aliiona dunia chungu, akakubali kuolewa, alichanganyikiwa sana, hakuamini kama muda huo mume wake alikuwa chumbani akifanya ngono na mwanamke.

    Nadhani alihisi msumari wa moto ukiuchoma moyo wake. Taaaap...damu chururuchururu.



    Tuliingia chumbani na kutulia kitandani. Kwa jinsi nilivyomchukia Salama, sijui kama nilijuta kuwa chumbani na mwanamke mwingine zaidi yake. Nilimwangalia msichana Irene, nilimtamani sana msichana huyo ila wakati mwingine nilikuwa na wasiwasi mno.

    Yaani msichana nilikutana naye siku hiyo, tena jioni, hata kulala hatujalala, eti nilikuwa naye chumbani. Hakika ilinishangaza, sisemi kwamba yeye ni malaya, hapana ila inakuwaje aniamini kwa harakaharaka sana, wakati najiuliza maswali yote, nikapata jibu kwamba gari ndilo lililomfanya kuwa hivyo.

    Irene: Nataka unikate kiu yangu...

    Mimi: Hakuna tatizo, usije ukaomba poo.

    Hakukuwa na stori, sikumuita humo ndani kwa kuwa nilitaka kupiga naye stori, humo kulikuwa na kazi moja tu iliyotakiwa kufanyika. Kiukweli nilifanya na Irene, japokuwa alitamba kabla kwamba alikuwa mtoto wa Tanga, anajua mapenzi lakini hakukuwa na kitu, alikuwa mzito, kama gogo, mimi ndiye nilikuwa masta, yaani nikimwambia, anafanya bila tatizo, nikaona watoto wa mjini bwana, wanajulia wapi michezo hii!

    Asubuhi ilipofika, saa kumi na mbili nikamuamsha kwa ajili ya kuondoka. Ndiyo! Alitakiwa kuondoka haraka sana, hivyo alitakiwa kujiandaa.

    Irene: Nataka tena, sijawahi kukutana na mtu kama wewe, please Denis, nataka tena.

    Mimi: Hahaha! Usijali, siku nyingine bhana.

    Irene: Jamaniiiiiii! Naomba, nikate kiu mwenzio nateseka....

    Sikuwa na jinsi, japokuwa nilijua kwamba ningechelewa kazini lakini nikakubaliana naye na hatimaye kuingia tena mzigoni. Sikutaka kucheza sana, nikamaliza na kuhakikisha kwamba alikuwa ameridhika, nikatoka chumbani na kwenda sebuleni.

    Pale, nilimkuta Salama amelala, hakuwa ameamka, alilala kwenye kochi kama kawaida yake, nilipomfikia, nikamuasha, akaamka huku macho yake yakiwa mekundu mno, ilionyesha kwamba alilia sana usiku kucha, na hata muda wa kulala, sidhani kama alikuwa amelala.

    Mimi: Wewe mwanamke mbona mvivu hivyo? Yaani unalala mpaka sasa hivi! Hivi una akili kweli? (nilianza kumlalamikia kwa sauti)

    Salama: Naomba unisamehe mume wangu! Ninajisikia vibaya, ninaumwa.

    Mimi: Pole (sikutaka kusikia anaumwa nini, huyo nikaelekea zangu bafuni)



    Nilipomaliza kujiandaa, huyo nikaondoka na Irene wangu kumpeleka kwao na mimi kuelekea kazini. Huko, muda wote Irene alikuwa akinitumia meseji, eti alipagawa na mimi na nilikuwa mwanaume wa kipekee kukutana naye.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sifa zote hizo zilikuwa ni halali yake kwani ukweli ni kwamba kwa wasichana wote niliokuwa nao, sifa zilikuwa hizohizo, eti nilikuwa fundi. Siku hiyo sikutaka kuonana naye kwani nilitumia nguvu nyingi sana hivyo ilikuwa ni lazima nipate chakula bora siku hiyo.

    Jioni ilipofika nikarudi nyumbani, siku hiyo nilikuwa nimechoka sana na nilihitaji muda wa kupumzika. Nilipofika nyumbani, huyu mke wangu, Salama hakubadilika, alikuwa vilevile, yaani kunipokea kwa mahaba kana kwamba nilimuoa jana.

    Nilishangazwa sana, mwanamke gani alikuwa haelewi, matukio yote niliyokuwa nikimfanyia, bado tu alikuwa akining’ang’ania, alinikera sana, nilimchukia mno ila sikuwa na jinsi, niliamua kumpotezea na mimi kufanya mambo yangu.

    Kama kawaida aliandaa chakula, eti nile na wakati kitambo sana nilimwambia kwamba chakula chake sitokula, labda alifikiri ni utani, nilimaanisha atii...kweli sikula chakula chake, mimi nikazama ndani na kufanya mambo yangu, hasa kuchati na mtoto Irene.

    Irene: Nimewaambia marafiki zangu kuhusu wewe...wanatamani sana kukuona....

    Mimi: Kweli jamani?

    Irene: Ndiyo! Eti wananilalamikia ooh! Mbona shemeji yetu hujamleta aje kutuona.

    Mimi: Hahaha! Aya bwana, wapo wapi hao mashemeji?

    Irene: Nipo nao hapa nyumbani.

    Mimi: Kwa hiyo nije niwaone?

    Irene: Watafurahi sana.

    Sikutaka kuendelea kuchati, nilichokifanya ni kuinuka kitandani na moja kwa moja kuelekea huko kwao. Wakati nikiwa njiani, nikapokea meseji kutoka kwa mtu ambaye huwezi kuamini, alikuwa Isabela.

    Isabela: Mambo kipenzi!

    Kwanza nikashtuka, nilichokifanya ni kulipaki gari pembeni na kuangalia meseji ile, kweli ilitoka kwa Isabela ninayemfahamu au alikuwa mwingine? Nilipoangalia, alikuwa yeye.

    Kwanza nikatulia, nikaanza kujiuliza alikuwa akitaka nini, nakumbuka kwamba nilipata maneno mengi kwamba alikuwa demu fulani hivi mwenye mabwana wengi, sasa mimi nimsaidie nini?

    Mimi: Poa.

    Isabela: Jamani umenitengaaaa...



    Kwa kawaida yangu mtu akishaanza kutuma meseji kama hizo huwa ninauchuna, sikuona sababu ya kumjibu meseji yake zaidi ya kupiga gia na kuondoka zangu, kwanza mtoto Irene alikuwa akiisubiri kwa hamu.

    Baada ya kuona sikumjibu meseji kwa dakika kadhaa, akatuma nyingine, nikaisoma, kama kawaida nikailia bati. Baada ya dakika chache, nikafika Magomeni Mapipa, Irene akaja na kuingia garini na kuanza kwenda huko kwake. Tulipofika, tukaingia ndani.

    Haki ya Mungu kile nilichokutana nacho humo ndani, sikuamini wallahi. Kulikuwa na mademu wawili, walikuwa weupe sana kana kwamba wamekunywa sana mapipa ya maji, walikuwa wamepozi kitandani huku wakiwa na uzuri wa ajabu.

    Kwa wanaume kama mimi wanaelewa unapokutana na kitu kama hicho cha kwanza huwa nini. Majuto! Nikajuta kuwa na msichana kama Irene kwani nilipokuwa nikiwaangalia wanawake wale, kweli walikuwa mademu, kweli walistahili kukesha ukizungumza nao, waliniangalia kwa macho yaliyoniambia “Jamani shemeji na wewe mzuri”.

    Kwanza nikatoa tabasamu pana, ilikuwa ni lazima iwe hivyo, huwezi kununa wakati mbele yako wamekaa watoto wazuri kama wao. Wakanisalimia kwa kunipa mikono, ile kuishika mikono yao tu, ilikuwa lainiiiii.

    Mimi: (Kimoyomoyo) Wewe Irene una balaa sana, yaani umejiamini vipi kunitambulisha kwa mashoga zako wakali zaidi yako? Hunijui eeeeh! Unaniona mimi mshambamshamba...sasa umekula wa chuya!

    Irene akaanza kunitambulisha. Wa kwanza alikuwa mweupe kama kawaida, alivalia kisketi kifupi kilichojaacha wazi mapaja yake, kifuani alisimama haswa, japokuwa alikuwa amekaa, ila niligundua kwamba alikuwa na hipsi kubwa, nikamcheki kwa jicho la matamanio, lililosema “Ipo siku utalala nami mpaka asubuhi”. Huyo aliitwa Rose.

    Nilipomaliza kumwangalia yeye, nikalipeleka jicho langu kwa mwingine, huyo alikuwa kama mmanga fulani hivi. Alikuwa amejaajaa kidogo, kama kawa alivalia kigauni kifupi, transparent ambacho kilionyesha mpaka maungo yake ya ndani, kila kitu, hasa kifuani niliona vizuri kabisa. Huyo aliitwa Halima.



    Irene: Karibu sana mpenzi...huyu ni shoga yangu anaitwa Rose na huyu Halima! Jamani, huyu ni shemeji yenu anaitwa Denis (alinitambulisha)

    Wote: Wakaachia tabasamu.

    Sasa kichwani nikawa na hesabu zangu, itakuwaje huyu Irene nimtoke niweze kula sahani moja na marafiki zake? Kila nilipojiuliza, nikakosa jibu kabisa, nikasema sawa, piga ua ni lazima nikamilishe michakato na hawa marafiki zake.

    Basi siku hiyo, kila nilipokuwa nikizungumza, walibaki wakiniangalia, wakabaki wakinisifia kwamba ninaongea pointi sana hivyo wakataka kujua kama nina PhD au vipi manake pointi zangu zilikuwa si mchezo.

    Wakati nikiwa nazungumza nao, kuna kitu niligundua, macho yao waliyotumia kuniangalia, yalinipa uhakika kwamba walikuwa wakinitaka ila walishindwa kuniambia. Basi ndivyo ilivyokuwa, nikapiga nao stori, ili kuwapagawisha, niliposimama na kuondoka, nikawaachia laki moja wagawane ili iwasaidie kwa kesho...

    Hahahah...mimi najua kuendana na kasi ya mchezo, niliamini kitendo cha kutoa fedha hiyo basi kingewachanganya, na ndivyo ilivyokuwa. Walinishukuru sana, sikutaka kujali, huyo nikaondoka zangu kuelekea nyumbani.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipofika, nikatulia kitandani. Ilipofika saa tano usiku, meseji ikaingia, ilitoka katika namba nisiyoifahamu, iliniambia Mambo! Nikaitikia, Poa. Nikaulizwa unajua unachati na nani? Nikajibu sijui, basi akaniambia yeye ni Halima, rafiki yake Irene, nikashtuka, nikaachia tabasamu, hapohapo nikamuendea hewani.

    Mimi: Hujambo lakini?

    Halima: Sijambo tu shemu, nimekumisi...

    Mimi: Umenimisi?

    Halima: Ndiyo! Au vibaya mtu kummisi shemu wake?

    Mimi: Hakuna ubaya, na si ubaya kama kwenda kumuona mtu uliyemmisi.

    Halima: Hahaha! Kwa hiyo kama nimekumisi nije kukuona?

    Mimi: Ndiyo! Kwani kuna ubaya? Ila ukija, huyo mzushi asijue.

    Halima: Hawezi kujua.....labda wewe umwambie. Basi nitakuja kesho shemu.

    Mimi: Sawa, ila si unajua naitwa nani?

    Halima: Yeah! Kwani nikiita shemeji tatizo?

    Mimi: Ndio! Tatizo hilo. Nitakuwaje shem wako bhana na wakati wewe ushaingia kwa moyo wangu?

    Halima: Hahaha! Una vituko wewe...kwanza hongera...

    Mimi: Hongera ya nini?

    Halima: Si Irene kasema wewe simbaaaaaaa

    Mimi: Simba? Kivipi?



    Halima: Unajua sana, kakusifia kupita kawaida...na mimi nataka nijionee, kweli au uongo...

    Mimi: Hahaha! Kujionea ruksa bhana.

    Irene bhana! Eti kisa nilimuonyeshea mambo fulani, basi ndio kaenda kuwaambia marafiki zake, hakujua kama ndio alikuwa akiuwasha moto na kujiwekea kichwani mwake.

    Nilizungumza sana na Halima, baada ya kumaliza nikakata simu huku ikiwa ni saa sita usiku. Wakati ndio nimegeuka ili nilale, mara nikasikia kama sauti ya kilio, sikujua ni nini, nikatoka chumbani na kwenda sebuleni. Nilipofika, nikamkuta mke wangu Salama akilia, alijifunika shuka ila sauti niliisikia vilivyo.

    Mimi: Kuna nini? Umepokea taarifa za msiba uende nyumbani kwenye mazishi? (nilimuuliza huku nikiwa nimemsogelea)

    Salama: Unaniumiza Denis, kwa nini unanifanyia hivi? Nimefanya kosa kuolewa na wewe?

    Mimi: Kwani nani kakuoa Salama? Nimekuoa lini?

    Salama: Denis, naomba usinifanyie hivi, unaniumiza mno, haujui ni jinsi gani ninakupenda na jinsi gani ninavyoumia kwa ajili yako! Kumbuka mimi ni mwanamke, binadamu mwenye moyo wa nyama kama wewe, unauma, unaniumiza sana, kama hutaki nikae kwako, niambie, sijafukuzwa nyumbani kwetu, nitawaambia tu wazazi wako kwamba nimeshindwa, hakuna kingine.....

    Mimi: Salama...hebu lala bwana...tatizo unaongea sana kama mwanasiasa...hebu acha nipumzike, nimesikia kilio, nilifikiri kuna msiba, kumbe una uendawazimu wako unakusumbua kichwani...hebu acha ujinga, lala huko..... (nilimwambia, nikamwangalia kidharau, halafu mimi huyo nikaondoka zangu kwenda kulala huku nikimuacha akilia kwa nguvu, sikujali wala nini)



    Kesho asubuhi ilipofika, nikaamka na kukaa kitandani. Ilikuwa saa kumi na mbili asubuhi, Kitu cha kwanza kabisa kugusa kilikuwa ni simu yangu, nikaichukua na kuanza kuiangalia.

    Nilikuta kukiwa na meseji mbili, kwa haraka sana nikazifungua na kuangalia mtumaji alikuwa nani, alikuwa msichana Isabela. Nikajikuta nikikunja sura kwani mawazo yangu yote yalifikiri kwamba mtumaji alikuwa msichana Halima.

    Isabela: Mambo mpenzi...nahitaji kukuona....

    Mimi: Haiwezekani!

    Nikaiweka simu pembeni na kutulia. Kichwa changu kikaanza kumkumbuka msichana Halima, huwezi kuamini, muda huo hata kumkumbuka Irene sikumkumbuka, kichwani mwangu alinitoka baada ya kukutana na rafiki yake mrembo. Wakati nikiwa na mawazo yangu, simu ikaanza kuita, nilipoangalia mpigaji alikuwa nani, nikakutana na jina la Isabela.

    Kwanza nilichukia zaidi na nikawa najiuliza kama ni busara kupokea simu yake au niachane naye kwani kila nilipokuwa naliangalia jina lake, mawazo yangu yalirudi nyuma kabisa, siku ile alipokuwa ndani ya Land Cruiser. Nikaamua kuipokea nione ataniambiaje.

    Isabela: Naomba unisamehe mpenzi...

    Mimi: Nikusamehe kuhusu nini?

    Isabela: Kuhusu siku ile ulipokuja nyumbani!

    Mimi: Ngoja nikuulize swali moja tu. Ulikuwepo ndani ya ile Cruiser?

    Isabela: Naomba unisamehe.

    Mimi: Nijibu kwanza.

    Isabela: Ndiyo nilikuwepo.

    Mimi: Na bwana gani tena manake wewe ni shiiiida sana huko mtaani kwenu. Ulikuwa na mwenye ndege, muuza madini au mmiliki wa hoteli?

    Isabela: Denis, naomba unisamehe.

    Mimi: Ok! Niambie unahitaji nini kutoka kwangu.

    Isabela: Nionane nawe.

    Mimi: Ili?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Isabela: Nizungumze nawe.

    Mimi: Isabela unajua mimi ni nani?

    Isabela: Denis mpenzi wangu!

    Mimi: Hapana! Umekosea, mimi ni mume wa mtu...au umesahau?

    Kwanza akabaki kimya kwa muda, aligundua kwamba nilimwambia hivyo kwa kuwa siku ya mwisho mimi kuzungumza naye aliniambia kwamba siwezi kuwa naye kwa kuwa nilikuwa mume wa mtu.

    Sasa siku hiyo na mimi nikamwambia hivyohivyo kwamba alitakiwa kukumbuka kwamba nilikuwa mume wa mtu. Nahisi alikumbuka vile alivyoniambia na ndio maana akabaki kimya tu.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog