Search This Blog

Friday, July 15, 2022

NILIVYOMLIZA MKE WANGU KWA SIKU 366 - 3

 







    Simulizi : Nilivyomliza Mke Wangu Kwa Siku 366

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilichokifanya ni kuwasiliana na bosi wangu ofisini, nilimwambia kwamba sikuwa mzima kiafya hivyo anipe ruhusa niende hospitali na nipumzike, nikaruhusiwa huku nikiwa na lengo la siku hiyo kumtafuta Isabela tu.

    Kumbuka kwamba sikuwa nikifanya kazi serikalini, ilikuwa ni kampuni ya mtu binafsi so siku kama hiyo ilikuwa ni lazima kwenda ofisini japokuwa si lazima kukaa mpaka jioni, unapomaliza kazi zako, unaruhusiwa kuondoka.

    Mimi: Ni lazima nimtafute Isabela, nataka niongee naye, sina raha, sina furaha (nilijisemea)

    Nilipanga kumtafuta Isabela siku hiyo, nikaingia bafuni na kujiandaa, nilipomaliza, nikatoka na kuelekea sebuleni. Nikamkuta Salama akiwa amekwishaamka kitambo sana, tena akiwa amefanya usafi na kuniandalia chai.

    Salama: Karibu, chai tayari.... (aliniambia kwa sauti ya upole sana)

    Mimi: Chai na nini?

    Salama: Chai na chapati, nimejitahidi kupika asubuhi sana, sijui utazipenda..... (aliniambia huku uso wake ukiwa kwenye tabasamu pana, hakuamini kama siku hiyo ningemsemesha kiupendo)

    Nikaelekea mezani kwa ajili ya kunywa chai. Siku hiyo sikuwa na jinsi, njaa ilikuwa ikiniuma sana hivyo ilikuwa ni lazima nile kwani usiku uliopita, sikula kabisa. Aliponiona nimekaa mezani, naye akasogea mezani pale na kuanza kunywa chai.

    Salama: Nikuandalie nini mchana? (aliniuliza)

    Mimi: Hapana! Sitokuja kula...

    Salama: Na usiku je?

    Mimi: Bado sijajua!

    Salama: Halafu na h....(kabla hajamalizia, nikamuwahi)

    Mimi: Salama, hebu naomba uniache kwanza, kichwa changu hakipo sawa kabisa. Unaweza kunyamaza?

    Salama: Sawa...naomba unisamehe....(alisema huku akisogea kwa lengo la kunipigia magoti, nikasimama zangu)

    Sikutaka kukaa nyumbani, siku hiyo nilikuwa na kazi moja ya kumtafuta huyu Isabela na kuongea naye. Ujinga ambao niliufanya ni kwamba sikuwa nikipafahamu alipokuwa akiishi, niliujua mtaa ambao mara kwa mara nilikuwa namfikisha na kisha kutimua zangu, sasa siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza kwangu kwenda nyumbani kwao.

    Njiani, kama kawaida mawazo hayakunitoka hata kidogo, bado niliendelea kumfikiria, wala sikuchukua muda mrefu nikafika kwenye mtaa huo, harakaharaka nikasimamisha gari na kuteremka, nikawafuata kwa lengo la kuwauliza mawili-matatu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Samahanini, kuna msichana namtafuta, sijui anaishi sehemu gani, ila ni huuhuu mtaa..(niliwaambia mara baada ya salamu)

    Jamaa 1: Msichana gani?

    Mimi: Anaitwa Isabela! (nikamjibu, wote wakaonekana kushtuka, wakaangaliana)

    Jamaa 2: Wewe nani?

    Mimi: Naitwa Denis.

    Jamaa 3: Ni nani wake?

    Mimi: Rafiki yake!

    Jamaa 1: Sisi wala hatumjui! (aliniambia kwa kujiamini kabisa, sijui aliniona mimi mjinga)

    Mimi: Kweli? Hapana, mbona hata sura zenu zinaonyesha kabisa mnamfahamu...(niliwaambia huku nikiachia tabasamu pana)

    Nilikuwa na uhakika kwamba washikaji walikuwa wakimfahamu sana Isabela ila walitaka kunizingua tu. Mara kwa mara walikuwa wakiangaliana tu, nilijiuliza ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, je Isabela alikufa au kulikuwa na tatizo gani.

    Wakati najiuliza hivyo, kuna gari likafika mahali hapo, ilikuwa ni Land Cruiser mpya, nyeusi iliyokuwa tinted vioo vyote. Nikamuona jamaa mmoja akitoka pale alipokuwa na kulifuata gari lile, kioo kikashushwa kidogo na kuzungumza na dereva.

    Sikujua walizungumza nini lakini kilichoendelea ni kwamba hakukuwa na mtu yeyote aliyeshuka kutoka ndani ya gari lile, liliendelea kusimama na hata baada ya hapo nilipoendelea kuwauliza wale vijana kuhusu Isabela, hawakunijibu chochote kile.

    Kiukweli nilikasirika na kutatizwa, sikujua kabisa kilichokuwa kikiendelea, sikutaka kujali sana, nilichokifanya ni kuondoka, si kurudi nyumbani, bali kuendelea mbele ile njia ambayo Isabela alikuwa akienda kila nilipomshusha.

    Majumba yalikuwa mengi, tena ya kifahari, nilichanganyikiwa kujua wapi ni wapi, nikawa naendesha gari kwa mwendo wa taratibu sana huku nikipepesa macho huku na kule.

    Nilipofika katika nyumba moja ambapo nje kulikuwa na watu wawili, nikateremka na kuwafuata huku nikiwa na uhakika kwamba inawezekana watu hao wanamfahamu.

    Mimi: Samahani, kuna msichana namtafuta anaitwa Isabela.

    Jamaa 1: Isabela?

    Mimi: Ndiyo! Mnamfahamu?

    Jamaa 2: Kuna asiyemfahamu Isabela mtaa huu? (alijibu jamaa mmoja, hapo nikaanza kushikwa na hofu)

    Mimi: Anaishi wapi?



    Jamaa 1: Nyumba hiyo hapo mbele! Kwani wewe ni nani? (aliniuliza, kilichojengeka akilini mwangu ni kwamba inaelekea msichana huyo hakuwa ametulia, hivyo na mimi nikajifanya waruwaru)

    Mimi: Mimi bwana wake. Jana kanikimbia baa baada ya kunywa bia zangu....

    Jamaa 2: Hahaha! Nilijua tu, huyu demu sijui atajirekebisha lini...kila siku kesi na ana bahati buzi lake halipo, lingekuwepo, angepigwa risasi (alisema jamaa huyo tena huku akiachia tabasamu lenye masikitiko, maneno yake yakaifanya damu yangu kuzunguka kwa kasi mwilini)

    Mimi: Kwa hiyo mimi siyo wa kwanza?

    Jamaa 1: Wewe kama wa nane hivi kuja kulalamika. Unajua hawa mademu zetu wa siku hizi wanapenda sana pesa, sasa mcheki mtu kama Isabela, anaishi na mzee mwenye pesa ndefu, mzee mwenye migodi na anapata anachokitaka, lakini hatulii.....

    Kiukweli maneno yao yalinichanganya sana, nikabaki nikiwaangalia mara mbili-mbili, sikuamini kama kweli maneno hayo yalimhusu yule Isabela demu wangu au mwingine. Uso wangu ukajawa na tabasamu pana lakini moyo wangu ulikuwa kwenye maumivu makali, iweje yule Isabela, mwenye sura nzuri kama vile, mpole awe na mabwana lukuki, halafu eti aishi na bwana na wakati aliniambia anaishi kwao, tena na wazazi wake?

    Nilichanganyikiwa, kama kupagawa, basi siku hiyo nilipagawa haswa. Nguvu zikaniisha, kwa kuwa kulikuwa na kibenchi pale nje, kwanza nikayakalisha makalio yangu.

    Jamaa 2: Kama unataka kwenda anapoishi, nyumba hiyo hapo, ila muulizie kwanza kwa mlinzi, unaweza kuingia ukakutana na bwana wake mwingine ikawa msala. Bwana wake babu hayupo sasa hivi watu wanajilia vitu humohumo ndani....

    Sikutaka kubaki mahali hapo, nilichokifanya ni kuondoka kuelekea kulekule waliposema anaishi. Nilipofika, nikakutana na mlinzi.



    Mlinzi: Bila shaka unamtaka Isabela (aliniambia bila hata salamu)

    Mimi: (Huku nikionyesha tabasamu la kinafiki) Umejuaje mwana?

    Mlinzi: Si ndiyo kawaida yenu. Sasa hivi dau limepanda, kumuona ndani kwake ni shilingi elfu kumi.

    Mimi: Poa, ila yupo?

    Mlinzi: Hayupo, kuna jamaa alikuja kumchukua na Land Cruser...

    Mimi: Nyeusi, si ndiyo?

    Mlinzi: Ndiyo?

    Mimi: Tena ina tinted, si ndiyo?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mlinzi: Ndiyo hiyohiyo...umeiona sehemu nini?

    Sikutaka kujibu swali hilo, nilichokigundua ndiyo ileile Land Cruiser niliyoiona kule kona karibu na wale washikaji waliokataa kunijibu zaidi. Sikutaka kubaki hapo, nikarudi garini na kuanza kurudi kule nilipoiona, kiukweli nilikasirika sana, hasira zikanikaba kooni, moyo wangu uliamini kwamba bado Isabela alikuwa demu wangu, hata kupigana kwa ajili yake, nilikuwa tayari ila si kuona nanyang’anywa manzi kizembe kama vile.

    Nikakunja mikono ya shati langu, nikajiandaa kwa ajili ya kupambana hukohuko kwenye ile gari, ila kwanza ningeanza na wale washikaji kwani nilipowaangalia, mbona walikuwa wadogo tu na ningewaweza wote. Eti nilitaka kupigana kisa huyu malaya Isabela.



    Kwa kweli nilikasirika mno, sikutaka kukubali hata kidogo, niliamini kwamba Isabela alikuwa wangu na sikutakiwa kupokonywa na mtu yeyote yule. Nilipofika katika njia ile na kukata kona, cha kushangaza sikumuona mtu yeyote yule, yaani hawakuwepo wale wanaume wala lile gari, hakika ilinichanganya sana.

    Nilibaki nikizunguka huku na kule, niliangalia kila kona, sikumuona mtu yeyote hivyo kuamua kuondoka zangu kurudi nyumbani huku nikiwa na mawazo tele. Nilipofika, kama kawaida ya Salama, alinipokea kwa mbwembwe, heshima kubwa na kunipelekea viatu chumbani.

    Salama: Mbona upo hivyo? Kuna nini?

    Mimi: Hakuna kitu...naomba uniache...(nilisema kwa hasira)

    Salama: Jamani! Haupo sawa, sasa mimi nitakuachaje? Sipendi kukuona ukiwa hivyo, unanihuzunisha mume wangu.....

    Mimi: Nani mumeo? Mimi mumeo? Nilikuoa lini? Una pete ya ndoa? Wewe mwanamke jichunge sana, yaani jichunge, usitake kuniletea za kuleta, kwanza nakurudisha kijijini, naona unanijazia nzi nyumbani kwangu (nilimwambia maneno yaliyoonekana kumuumiza mno)

    Salama hakuzungumza kitu, maneno yale yalimuumiza mno, alibaki akiniangalia tu, niliyaona machozi yakijikusanya machoni mwake, yalijaa na hatimaye kutiririka mashavuni mwake.

    Sikujali, sikuwahi kuishi naye, sikuwahi kumpenda, hivyo sikutaka kufuatilia sana. Mawazo yangu yalikuwa kwa Isabela tu. Kichwa changu kilivurugwa na penzi la Isabela, halafu huku nyumbani mtu anaanza kuniita mume wangu, ningemuelewaje?

    Salama akainuka na kuelekea jikoni, kwa mbali nilisikia sauti yake, alikuwa akilia kwa kilio cha kwikwi, sikutaka kujali, kwani kulia kwake kulinihusu nini? Acha alie, akimaliza atanyamaza.

    Zilipita dakika kumi, Salama akarudi sebuleni hapo, nilipouangalia uso wake, alionekana kuwa kwenye tabasamu pana. Akaenda mezani, akaweka chakula kisha kunifuata na kunikaribisha, tena kwa kupiga magoti.

    Salama: Karibu mume wangu!



    Mimi: Hivi wewe mwanamke, nani kakwambia nina njaa, yaani unaleta shobo, nikuone mpishi bora, nimesema hivi, kama niliwahi kula chakula chako, nilikula kwa bahati mbaya sana, sasa hivi nimejanjaruka, siwezi kula chakula chako kabisa, kwanza SIKUPENDI, ninakuchukia, mwanamke mchafu, hujui kuvaa, ngozi mbaya, hata kuoga hujui, halafu unakuja mjini kijingajinga, yaani wewe si wa kuishi mjini, wewe ni wa kijijini tu, tena uishi hukohuko mpaka kifo chako, mwanaizaya wewe.....

    Salama: Denis, nashukuru sana, ila wewe ni mume wangu, nitavumilia yote uyafanyayo. Kamwe huwezi kuona thamani ya kitu hasa unapokuwa nacho mikononi, kikipotea, utaiona thamani yake. Nashukuru sana mume wangu!

    Mimi: Hivi wewe mwanamke nimekwambia kuniita hilo jina? Mimi mumeo tangu lini? Mbona unanidhalilisha hivyo? Nilikuoa lini? Pete ya ndoa iko wapi? Cheti cha ndoa kipo wapi?

    Salama hakuzungumza kitu. Alibaki kimya tu. Ngoja nikwambie kitu rafiki yangu, mimi ni mtu mmoja mwenye upole wa ajabu, huwa ninakuwa na huruma sana, kwa kile nilichokifanya kilikuwa ni cha kumuonea huruma Salama lakini sikufanya hivyo, yote ni kwa sababu ya penzi la Isabela lilivyonichanganya kichwa changu.

    Siku hiyo sikutaka kula chakula chake, nilikwenda chumbani na kuanza kumuwaza Isabela tu.

    Wakati nikiendelea kumuwaza Isabela, mara nikasikia mlio wa meseji katika simu yangu kuashiria kwamba kulikuwa na meseji imeingia, ki chovu kabisa nikaichukua simu yangu na kuangalia jina la mtumaji wa meseji hiyo, huwezi amini, alikuwa Isabela, harakaharaka nikaifungua.

    Isabela: Mambo!

    Mimi: Poa, nimekumiss Isabela wangu!

    Isabela: Sawa...nashukuru, ila sikia sasa...sitaki unifuatiliefuatilie, umenisikia?

    Mimi: Eeh! Kuna nini tena?

    Isabela: Nimesema sitaki unifuatiliefuatilie, umesikia?

    Mimi: Sikuelewi, kuna nini?

    Isabela: Hivi wewe mwanaume una akili kweli?

    Mimi: Hebu subiri nikupigie.....

    Nilichokifanya ni kumpigia, simu ikakatwa na meseji ikatumwa.

    Isabela: Naomba usinisumbue...yaani usinisumbue kabisaaaaaa

    Mimi: Jamani mpenzi, tatizo nini?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Isabela: Nani mpenzi wako? Tangu lini?



    Haya mapenzi wakati mwingine yanakuwa kigeugeu sana, eti yuleyule Isabela ananiambia kwamba yeye si mpenzi wangu! Kwa jinsi majibu yake yalivyokuwa, yalinifanya nimchukie zaidi Salama kwa kuwa ndani ya nyumba ile.

    Hakukuwa na siku ambayo kwangu ilikuwa ngumu kama siku hiyo, niliumia mno lakini sikuwa na jinsi, mpenzi wangu, niliyempenda, Isabela eti leo alikuwa akinichamba namna hiyo.

    Usiku mzima sikulala, nikaanza kukumbuka tangu siku ya kwanza nilipokutana naye, alivyonipenda na mpaka siku hiyo ambayo aliamua kunipa vidonge vyangu. Kiukweli niliumia mno lakini sikuwa na jinsi, nilitakiwa kukubaliana na matokeo kwamba mtu mzima nilikuwa nimemwagwa.

    Huku nyumbani, Salama hakukoma, huyu mwanamke alining’ang’ania kama ruba, kwa kuwa baba ndiye aliyeniolewa, sikuwa na jinsi, sikuwa na ujanja wa kumuacha, niliendelea kuwa naye hivyohivyo.

    Salama: Mume wangu!

    Mimi: Nini?

    Salama: Nina ombi kwako!

    Mimi: Ombi gani? Unataka kurudi kwenu, rudi tu wala usiombe....

    Salama: (akanyamaza, akameza mate na kuniambia) Nina kiu, nina hamu.

    Mimi: Hamu ya nini?

    Salama: Ya kuwa nawe kitandani....tafadhali naomba unisaidie, kiu imenikaba.

    Mimi: Hahaha! Hivi wewe mwanamke huishiwi vituko? Yaani mimi nilale na wewe! Nilale na wewe kweli? Hahaha! Hivi hujisikii aibu, eti unaniambia kilainilaini, nilale na wewe...hahaha! Hebu acha kuchekesha waliofiwa....(nilimwambia kwa kejeli huku nikicheka kidharau)

    Salama: Nakuomba mume wangu....

    Hapohapo nikamfuata, nikamzaba kibao cha haja, kilimuingia mpaka kikatoa alama ya kiganja shavuni mwake.

    Mimi: Nilikwambiaje kuniita jina hilo?

    Salama: Naomba unisamehe mume wangu...naomba unisamehe (aliniambia huku akipiga magoti, akaona haitoshi, hapohapo chini akaanza kuishika mpaka miguu yangu.

    Mimi: Hebu niache kwanza....unanichafua...(nilisema huku nikisogea nyuma, sikutaka aniguse)

    Yaani sikutaka kusikia lolote lile, eti Salama afanye tendo la ndoa na mimi? Anichafue, sikutaka kabisa kusikia kitu kama hicho. Nilichokifanya ni kuelekea chumbani, nilipotoka nilitoka na chupa ya soda na kumpa.

    Mimi: Kafanye na hiyo hapo......

    Salama: Nashukuru....(akaichukua chupa hiyo na kwenda nayo jikoni)



    Rafiki yangu, hayo ndiyo maisha niliyokuwa nikiishi na huyu mwanamke ambaye wazazi wangu waliamua kuniolea kijijini. Maisha hayakuwa mazuri hata kidogo, kila siku nilimtesa na kumpa maneno ya kejeli kisa tu alikuwa akiishi nyumbani kwangu.

    Kichwa changu kiliendelea kumfikiria Isabela lakini sikutaka kwenda kule kwake tena kwani niliamini kuwa ningeuumiza moyo wangu. Nikajitahidi sana kufanya kazi zangu kama kawaida.

    Kumbuka kwamba sikuwa na mapenzi kwa Salama na muda mwingi nilijiona kama mtu aliye singo hivyo nilikuwa na uhuru wa kufanya lolote nililotaka kufanya.

    Wakati mwezi wa nne unaingia, nikaamua kutoka na kuelekea ufukweni kula bata kidogo. Nikiwa huko ndipo macho yangu yakatua kwa msichana fulani hivi, alikuwa mrembo, amejaajaa kwa nyuma, alivalia kinguo cha kuogelea, sikutaka kumuacha hivihivi, nikaamua kumfuata.

    Wakati nikimfuata, kama kawaida watu wengine walikuwa wakimwangalia, alionekana kuwa mrembo hasa, alipendeza machoni kwa kila mwanaume aliyemwangalia, nilipomfikia tu, nikaachia tabasamu.

    Mimi: Mambo mrembo.....

    Irene: Safi tu.

    Mimi: Naomba unifundishe kuogelea!

    Irene: Nikufundishe kuogelea jamani?

    Mimi: Ndiyo! Naogopa maji, nahitaji mwalimu kama wewe....(nilimwambia huku nikitoa tabasamu)

    Irene: Hahaha! Mimi mwenyewe sijui kuogelea....

    Mimi: Kweli?

    Irene: Ndiyo!

    Mimi: Basi naomba kampani yako, nataka tu niwe nawe kwa muda huu hapa ufukweni.

    Irene: Weeee...unataka wifi anipige....

    Mimi: Hahah! Wifi gani tena jamaniiii? Mbona unanitabiria hivyo? Au unaninyima kijanja kuungana nawe?

    Irene: Mmmh! Wanaume nyie wala hamueleweki kabisa...

    Mimi: Sawa! Hatueleweki, ila kwa leo naomba mimi nieleweke, pleasee...nielewe kidogo tu, yaani kidogo tu.

    Irene: (Kimyaaa)

    Wakati nazungumza hivyo, macho yangu yalikuwa yakitalii mwili wake vilivyo kabisa, alionekana kuwa mwanamke fulani hivi ambapo baada ya kumchukua mawazoni na kumpeleka chumbani, alikuwa balaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Basi nikakaa pale huku nikizungumza naye, lengo langu lilikuwa ni kumzoea tu kabla ya kumchombeza kwa vineno vya hapa na pale. Kwa nilichokigundua ni kwamba msichana yule hakuwa mgumu kivile japokuwa pale ufukweni kila mmoja alionekana kumuogopa. Kabla sijaanza kuishi na yule Salama, nilikuwa mkali kwa totozi hasa ‘loose ball’ kama zile, hivyo nilichokifanya ni kuonyesha umwamba wangu.

    Mimi: Ningependa kupata muda wa kuzungumza na wewe...

    Irene: Kuzungumza na mimi? Kuhusu nini?

    Mimi: Mambo ya kawaida tu....

    Irene: Sina muda....

    Mimi: Najua muda unao ila hutaki tu.

    Irene: Nitachelewa nyumbani...

    Mimi: Usijali! Nina usafiri wangu, nitakurudisha.....tena nitakuwahisha....

    Kitendo cha kumwambia nina usafiri wangu tu, mtoto akapagawa. Hapa ndiyo maana ninasema kwamba ukiona demu wako anachukuliwa na mtu mwenye gari, wewe kuwa mpole tu au tafuta lako uwachukulie washikaji wengine. Hawa wanawake wanapagawa sana na magari kana kwamba wamebatizwa kwa petroli.

    Nilipomwambia hivyo tu Irene, akachanganyikiwa, uso ukawa na tabasamu pana, nikaona ni lazima nimchukue na kufanya mambo yangu! Basi akaogeleaogelea kwa muda, alipomaliza, akaenda sehemu ya kuvaa nguo zake, nikamchukua na kuelekea naye kwenye gari, ile kuingia tu, akajiachia, sketi yake ikapanda juu, mapaja yakawa wazi, nikabaki nayatolea macho, nikasahau kama nyumbani kulikuwa na Salama ambaye nilimnyima haki yake ya ndoa, mtoto akanikonyeza kisiri hivi, akanionyeshea bonge moja la tabasamu. LIKANIPAGAWISHA NA BABA JOHN KUAMKA.

    Utulivu wangu ulikuwa sifuri kabisa ndani ya gari, macho yangu hayakutulia kuangalia mbele kule tulipokuwa tukiangalia, muda wote nilikuwa nikiyaangalia mapaja yake kwa macho ya kuibia. Huyu mtoto alikuwa balaa, kila nilipomwangalia, nilijua tu mambo yangeharibika.

    Japokuwa kichwa changu kilikuwa kikimfikiria sana Isabela, huwezi amini muda huo mtu huyo hakuwepo kabisa kichwani mwangu, mawazo yangu yalikuwa na huyu mtoto, nifanye mikakati gani ili nimchukue kama ilivyokuwa kwa Isabela.

    Sasa naye alivyokuwa na mapozi na miguu yake, mara aikunje kidogo, mara apandishe sketi, mara aitanue kidogo, yaani naye kama alijua vile kwamba ananipagawisha, nikawa naendelea kuyaangalia tu.

    Mimi: Nimefanya kosa sana kutokujua jina lako, hivi unaitwa nani?

    Irene: Naitwa Irene Godfrey.

    Mimi: Waooh! Jina zuri! Mimi naitwa Denis, na unaishi wapi?

    Irene: Naishi hapo Magomeni Mapipa.

    Mimi: Sawa!

    Wakati naendelea kupiga naye stori, akaipandisha miguu yake mpaka kwenye dashboard, hapo sketi ikaenda mpaka karibu na kiuno na kuifanya pichu kuonekana kwa kuibia.

    Nikazidi kuwehuka, yaani ni kama nilizaliwa siku hiyo. Nikapagawa, tulipofika Mkwajuni Kinondoni, bado nusu nigonge basi la shule kutokana na muda mwingi kuwa bize katika miguu yake.

    Irene: Jamani kuwa makini mpenzi....

    Aliniambia bila soni. Hebu fikiria, mtoto nilimuweka kwenye tageti zangu, sikuwa nimemtokea mara mwisho wa siku anaanza kuniita mpenzi. Jamani jamani! Haya magari kuna kitu Mzungu kaweka humu, haiwezekani eti from nowhere nishaanza kuwa bebi, basi nikaona siyo kesi, yeye si kajibebisha, na mimi nikakubaliana naye.

    Mimi: Mpenzi una miguu mizuriiiiiCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Irene: Kweli?

    Mimi: Ndiyo! Unantia hamu mwenzako (nilisema huku nikitoa kicheko cha chini, naye akakipokea)

    Irene: Jamani! Yaani miguu tu ndiyo uwe hivyo?

    Mimi: Ndiyo! Hebu subiri nipaki gari pembeni.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog