Search This Blog

Friday, July 15, 2022

NILIVYOMLIZA MKE WANGU KWA SIKU 366 - 5

 







    Simulizi : Nilivyomliza Mke Wangu Kwa Siku 366

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Unalijua hilo?

    Isabela: Mpenzi! Naomba turudi kama zamani, nimekukumbuka, hata kuwa mchepuko wako, nipo tayari, nakuomba sana.

    Wakati nikizungumza naye, mara simu ya Halima ikaanza kuingia. Nilipogundua kwamba alikuwa Halima, hapohapo nikamuweka Isabela kwenye HOLD na kisha kupokea simu ya mtoto Halima, si unajua Kipya Kinyemi.

    Halima: Mambo mpenzi?

    Mimi: Poa, niambie umeamkaje?

    Halima: Salama tu.

    Mimi: Umeniota?

    Halima: Sana tu..nimekukumbuka mpenzi, yaani sijuti kukupenda, hata Irene akigundua, nipo radhi kugombana naye, hata kutafutana na mapanga mitaani lakini si kumuona akiwa na wewe tena.

    Mimi: Ya kweli hayo?

    Halima: Ndiyo!

    Mimi: Basi naomba leo tuonane, unaonaje?

    Halima: Sawa...nije kwako?

    Mimi: Wewe njoo, niambie utakuwa na ya rangi gani ndani.

    Halima: Nitaangalia, kama ni pinki, nyeupe au nyekundu...wewe unataka ya rangi gani?

    Mimi: Chukua pinki...nadhani that colour is killing me wallah....

    Nilizungumza naye kwa kipindi kirefu, tukakubaliana tuonane ili tufanye yetu. Kumbuka kwamba huo ndiyo ulikuwa mwezi wa tano mwanzoni. Nilimwambia kwamba ningekwenda kazini hivyo baada ya kurudi ningempitia njiani na kuelekea naye nyumbani kwangu. Basi tukaagana.

    Kazini sikuwa nikifanya kazi vizuri, kila wakati nilikuwa nikimpigia simu, alikichanganya sana kichwa changu, yaani ni kama sikuwa na mke. Muda ulizidi, kazi hazikufanyika kwa ufasaha, kila nilipokuwa nikiandika hiki, jina lake lilinijia kichwani.

    Ilipofika jioni, sikutaka kukaa ofisini, haraka sana nikaondoka. Nikaamua kumpitia sehemu tulipokubaliana. Nilipomuona siku hiyo, Halima alikuwa balaa, sikukosea kumpenda wallahi! Alikuwa bomba ile mbaya. Alivalia kigauni kifupi kilichoishia mapajani, alikuwa mweupe peee...nilipomwangalia, alinipagawisha kinoma.

    Akafika na kuingia ndani ya gari, kitu cha kwanza kabisa, nikakamatia kiuno na kumbusu. Pale kiunoni nilipomshika, kwa mbali nikaihisi cheni aliyokuwa ameivaa, basi hapo ndipo nikachanganyikiwa zaidi.

    Mimi: Nimeipenda cheni yako...

    Halima: Hahaha! Umeiona?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Si kuiona, nimeigusa jamaniii, kwani kama kuiona si nitaiona sana tu leo, sina presha.

    Halima: Kwanza niambie nyumbani kwako unaishi na nani?



    Mimi: Mfanyakazi wangu, nilimtoa kijijini.

    Halima: Wawili tu?

    Mimi: Ndiyo! Unamuogopa?

    Halima: Hapana! Ni msichana au mvulana?

    Mimi: Msichana!

    Halima: Mmh! Kuna amani kweli humo?

    Mimi: Ipo, tena imejaa tele mpaka inamwagika, wala usijali.

    Nikaondoka naye, njiani, yeye alikuwa mzungumzaji sana lakini sikuwa mzungumzaji sana kwani akili yangu niliipeleka chumbani tu. Umbo lake murua nikaona leo kazi ipo.

    Nilipofika nyumbani, Salama sikumkuta, sikujua alikwenda wapi, nikapita moja kwa moja pamoja naye, tulipofika chumbani, akalala kifudifudi kitandani, gauni lake likapanda, mapaja yake yakawa wazi, uchu ukanipanda.

    Hapa ndipo ninapoona hasira sana kumnunulia msichana nguo yake ya ndani. Mwanaume unajitoa kumnunulia, tena kwa mapenzi motomoto, mwenyewe unamvalisha kwa mahaba yote na kujiona mwanaume wa shoka.

    Mbaya zaidi, umemvarisha wewe lakini kuna boya fulani hivi, anakuja na kuivua, wewe umemvarisha, yeye anamvua, tena kirahisi sana na ndiyo maana sipendi kumnunulia manzi nguo ya ndani kwani kila nikifikiria kuna boya atamvua, huwa nashikwa na hasira.

    Basi akalala...kilichotokea usiku huo, WALA HAKIANDIKIKI HAPA...tulipomaliza, tukalala kwani kila mmoja alichoka mno, uzuri wake na kile alichokifanya, haki ya Mungu alikuwa na haki.

    Wakati tumetulia huku ikiwa ni saa moja usiku, nikasikia mtu akigonga mlango. Unajua nilihisi ni nani? Salama, na kweli alikuwa yeye. Nikaufungua mlango na kumwangalia kwa macho ya hasira.

    Salama: Chakula tayari....karibu.

    Mimi: Nimekwishakwambia sitaki kula chakula, husikii?

    Salama: Sawa.... (aliitikia kinyonge)



    Halima aliposikia sauti ya Isabela, harakaharaka akaja na kusimama pale mlangoni huku akiwa na shuka alilolifunga mwilini mwake, uso wake ulikuwa kwenye tabasamu kubwa, alimwangalia Isabela.

    Halima: Kama yeye hataki, mimi nakuja kula....

    Halima hakujua kilichokuwa kikiendelea mule ndani, hakujua ni kwa jinsi gani Salama aliumia moyoni mwake, huyo alikuwa msichana mwingine, si yule Irene niliyekuja naye siku ile, alikuwa mwingine kabisa.

    Hapo ndipo alipojua kwamba mimi ni malaya, ila pamoja na hayo, eti hakutaka kuniacha. Halima alipoondoka, kama kawaida mapenzi yake yalikuwa makubwa mno kwangu, hakuacha kunijali, alinithamini na kuanza kujiuliza alikuwa na moyo gani juu yangu? Yaani kila nilichojiuliza, nikakosa jibu kabisa.



    Kuruka na Halima haikuwa mwisho, huo ulikuwa mwanzo tu, niliruka naye sana, tulifanya siri na hata Irene alishangaa kwa nini nimepunguza mapenzi kwake. Kwanza sikuwa nikimpigia simu, sikumtumia meseji, kilichoniudhi, sawa, inawezekana hakujua kusoma, ila hata picha hakuiona?

    Mwisho wa siku, nikaachana naye kabisa na hivyo kutulia kwa mtoto Halima. Nilispend naye sana, ilipofika mwezi wa nane, si ndiyo nikaanza kumtafuta na yule Rosemary.

    Nilikuwa na namba yake, nikamcheki, kwanza dizaini kama hakuamini kama ndiye nilimpigia, akabaki akichekacheka tuuuu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Mbona unanicheka?

    Rose: Noo! Nimefurahi kupokea simu yako my ex shemeji...

    Mimi: Hahaha! Upo wapi?

    Rose: Nipo saluni naseti nywele.

    Mimi: Hivi naweza kukuona?

    Rose: Leo?

    Mimi: Yaaap! Inawezekana?

    Rose: Sawa....hakuna shida my ex shemeji.

    Japokuwa kuitwa hivyo nilikasirika lakini nikajifanya kufurahi tu. Nilitaka kuonana naye, nimalizane naye kabisa. Ngoja nikwambie kitu, kwa sisi tunaofuatilia mpira kuna kitu kinaitwa hat trick, yaani ni pale mchezaji anapofunga magoli matatu kwenda juu.

    Sasa tayari nilishafanikiwa kulala na marafiki wawili, sasa nikawa namtaka huyu wa tatu, nilitaka kupiga hat trick na kisha kuondoka zangu, na hicho ndicho nilichotakiwa kukifanya kwani mechi yangu na Rose, niliiona nyepesi sana kiasi kwamba hat trick ilikuwa ikinukia.

    Nikamfuata zangu huko saluni, nikamchukua na kumpeleka Toroka Uje kule Kinondoni na kula chakula cha jioni. Mwenyewe akafurahi wee, akanirembulia tu bila kujua kwamba yeye alikuwa beki na alikuwa akimchekea fowadi hatari zaidi ya Pele.

    Rose: Naomba uninunulie pombe shemu.

    Mimi: Unakunywa pombe?

    Rose: Yaaap!

    Daah! Unajua sisi wengine tunazaliwa na mazali tu, nilikuwa nikijifikiria ni jinsi gani ningeweza kumshawishi kulala nami usiku wa siku hiyo, mwenyewe kajilainisha, anataka pombe, akilewa je? Kwao sipajui kwa maana hiyo ningemchukua na kumpeleka ninapotaka kumpeleka mimi, nyumbaniiiiiiii.

    Nikamnunulia pombe, John Walker baridiiiii na kumtaka anywe mdogo mdogo na si kwa pupa kwani wote hatukuwa na haraka. Akaanza kunywa, akanywa na kunywa, akanywa



    Nikamnunulia pombe, John Walker baridiiiii na kumtaka anywe mdogo mdogo na si kwa pupa kwani wote hatukuwa na haraka. Akaanza kunywa, akanywa na kunywa, akanywa weee...akanywaaaaaa......baada ya dakika kama arobaini, akaanza kuzungumza kwa kuingiza Kingereza kingiiiii, nikajua tayari huyu.

    Nikamsogelea, kila alichokuwa akiongea, nilimuuliza, unasemaje shemu, tena huku nikimvuta karibu yangu.

    Rose: Nataka kwenda kulala...nimechoka (aliniambia kwa sauti ya kilevi)

    Mimi: Kwangu au kwako?

    Rose: Popote pale mpenzi....

    Hapohapo nikashangilia moyoni...nikajisemea...yes! Mzee wa hat trick nikambeba na kuondoka naye.

    ***** Sikusimulii haya kama kuhamasisha ngono, sikusimulii haya kama kujisifia kwamba mimi mkali wa watoto wazuri, sikusimulii haya kama kujiaibisha, nakusimulia haya kwa kuwa nataka ujifunze, pale ambapo mimi nilikosea, wewe usikosee.

    Hakika mke ni mtu wa thamani sana, ni bora kuoa mwanamke mbaya, asiyekuwa na mvuto lakini heshima yake uendelee kumpa kuliko kuoa mwanamke mzuri ili majirani wakusifie na mwisho wa siku ujutie uamuzi wako wa kumuoa huyo mke mzuri kama staa wa filamu.

    Nilikuwa na uhakika siku hiyo kwamba Rose amekwisha. Ndivyo ilivyotokea. Ngoja nikwambie kitu kimoja. Miongoni mwa watu bahili katika dunia ya sasa, mimi huwa sikosi, kwanza sipendi kwenda lodge au gesti na mwanamke.

    Huwa ninafikiria gharama, ukienda kule, kitu cha kwanza ni lazima ulipie chumba, mle, hivyo unaweza kutumia zaidi ya laki moja kitu ambacho kwa mtu mwenye maisha ya kawaida kama mimi, ni gharama kubwa.

    Ili nisitumie kiasi hicho cha fedha, sina budi kwenda nao nyumbani kwangu, kwanza kwangu ilikuwa sehemu salama lakini kubwa kuliko zote, sikuweza kutumia kiasi kikubwa cha fedha.

    Nikamuingiza Rose ndani ya ndinga na kuanza kwenda naye nyumbani. Pale kitini alipokuwa, alikuwa hoi, hata kuzungumza kwake ilikuwa ni kama mtu aliyelewa sana ambaye alihitaji kulala muda huo.



    Sikuchukua muda mrefu nikafika nyumbani. Nikamtoa ndani ya gari na kuanza kwenda ndani. Kama kawaida, muda ulikuwa umekwenda sana na pale sebuleni nilimkuta Salama akiwa kajilalia kochini, wala sikutaka kujali, nilimshika Rose kiuno huku akiyumbayumba mpaka chumbani ambapo nikamtupa kitandani.

    Mimi: Leo kazi ipo, kama kawa hakuna kuremba.

    Nilijisemea kisifa huku nikivua nguo zangu, hakukuwa na kilichoendelea zaidi ya kufanya kile kilichotuleta mule ndani. Hatukuja kupiga stori, humo tulikuja kwa kazi moja tu ambayo ilifanyika kikamilifu.

    Asubuhi ilipofika, tukaamka, kwa kuwa nilijiona nikiwa kwenye mahaba niue na huyu Rose, nikaamka na kwenda kumchemshia chai kwani Salama hakuwa akipika tena kutokana na mimi kumkatalia kila siku kula chakula chake.

    Nilipomaliza, nikampelekea chumbani huku kukiwa na mikate ambayo mara kwa mara ninainunua kama dharura. Nilipoweka kitandani tu, nikamuamsha.

    Mimi: Amka mpenzi! Amka amka....

    Rose: Waoooo...asante sana.

    Mimi: Kunywa kwanza, maliza tukanywe supu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Rose: Nashukuru kwa upendo wako. Ningekuwa napendwa hivi tangu utotoni, haki ya Mungu ningenenepa.

    Hayo yalikuwa kama maandalizi mapya kwani baada ya hapo, kilichondelea ni kurudi kitandani na kufanya kile kilichotakiwa kufanywa. Rose alikuwa msichana wa kawaida, hakuwa mtundumtundu kama wenzake ila mwili wake ulionyesha matamanio makubwa na kumwacha lilikuwa jambo gumu.

    Rose: Ninakupenda sana Denis wangu, naomba unioe...

    Mimi: Usijali, nitakuoa tu mpenzi, hakika umeniteka sana....

    Rose: Kweli?

    Mimi: Ndiyo! Hakuna zaidi yako.

    Asubuhi hiyo nilikaa naye sana, tulifanya mambo mengi na baadaye kuondoka kumpeleka nyumbani kwao. Sikumfikisha kwa kuogopa kuonana na Irene lakini mwenyewe wala hakujali, akaniambia kwamba Irene hawezi kumfanya kitu kwani mpaka yeye kunipata mimi, ilionyesha kwamba msichana huyo hakuwa na uwezo wowote ule kitandani.

    Tulipofika, nikamteremsha na kurudi zangu nyumbani. Kabla sijafika, nikaona bora nipitie supermarket kuchukua chakula kwani sikuwa na mpango wa kula chakula cha Salama hata kidogo.



    Nilipofanikiwa kununua, nikakichukua na kurudi nyumbani. Wakati nimefika nyumbani, nikaona gari ndogo ikiwa imepaki pembeni. Kwanza nikashtuka, haikuwa kawaida kabisa, nilichokifanya ni kusogea karibu, nilitaka kujua huyo alikuwa nani na kwa nini alipaki gari lake karibu na geti langu!

    Wakati nimeanza kulifikia, mlango ukafunguliwa na mtu mmoja kuteremka, huwezi kuamini, alikuwa Isabela. Kwanza nilipomuona, nikashtuka, nikaanza kujiuliza kwa nini alikuwa hapo, alihitaji nini? Alisahau nini kutoka kwangu? Wakati nikiwa na maswali lukuki, nikaanza kumsogelea huku nikiwa na hamu ya kusikia amesahau nini.

    Isabela: Ooh! My baby boy!

    Wakati ananiita hivyo, tayari aliipanua mikono yake ili anikumbatie. Kwanza nikamzuia, sikutaka anisogelee kabisa.

    Mimi: Umefuata nini?

    Isabela: Nimekufuata wewe...

    Mimi: Hebu niondolee upuuzi, kuna kitu umesahau?

    Isabela: Jamani! Zilikuwa ni hasira tu.

    Mimi: Hivi wewe mwanamke, tangu lini ukaona mwanamke anamg’ang’ania mume wa mtu?

    Nikamuona akiwa mnyonge, hapohapo akainamisha kichwa chini, alianza kujisikia sana aibu lakini sikunyamaza, nikaendelea kumpa vidonge vyake. Kwa kweli hakukuwa na mtu niliyekuwa nikimchukia kama yeye, sikumpenda,

    Nilimchukia sana msichana huyu, kiukweli sikutaka hata kumuona kwani ilikuwa ni afadhali ulale na malaya aliyekuwa akijiuza kuliko kulala na msichana kama huyu. Nilimwangalia huku nikiongea mpaka povu likinitoka, mara, Salama huyo akatoka nje.

    Salama: Kuna nini tena mume wangu?

    Mimi: Si huyu malaya kanifuata, sijui anataka nini! Hebu mwambie mke wangu unataka nini!

    Niliziona hasira zake waziwazi, najua alikasirika sana lakini sikuwa na jinsi, sikuwa na namna nyingine ya kumkataa zaidi ya kumwambia hivyo. Ila wakati huo, nilibaki nikijishangaa, nilitoa wapi ujasiri wa kumuita Salama mke wangu? Kila nilipojiuliza, nikakosa jibu.

    Muda wote Salama alikuwa akifurahi tu, alionekana kuwa na furaha ya ajabu, inawezekana hata yeye mwenyewe hakuamini kama ningemuita kwa jina hilo. Tabasamu lake pana likanifanya nimuone mtu aliyehitaji sana faraja kutoka kwangu.





    Kutokana na kupewa mashuti, Isabela akaamua kuingia ndani ya gari, huyo akaondoka zake. Sasa kazi ikabaki kwangu na Salama tu. Niliona anaanza kunizoea, anajichekeshachekesha tu, nikajua kabisa kwamba sasa aliona kwamba kuna uwezekano wa kunichukua.

    Tuliondoka na kuelekea ndani, tulipofika huko, kwanza nikampa mikausho mikali, sikutaka aniambie kitu chochote kile, alinionyeshea tabasamu lakini sikumpa ushirikiano.

    Salama: Nikuandalie chakula mume wangu?

    Mimi: Hapana! Usiniandalie chakula chochote kile, kwani umesahau? Nilishasema kwamba sitokula chakula chako.

    Salama: Sawa...

    Siku zikaendelea kukatika, maisha yetu hayakubadilika, kazi yangu kubwa ilikuwa ni kubadilisha wanawake, mara Maria, mara Mwajuma, Fatuma, Asha na wote hao nilikuwa nikilala nao hapohapo nyumbani. Siku zilikwenda, nikaanza kugundua kwamba ninapoteza hela sana, yaani matumizi yangu yanakuwa makubwa hivyo ilikuwa ni lazima niyapunguze.

    Mimi: Kwanza nipunguze mademu...

    Hilo ndilo lililokuja kichwani mwangu, ilikuwa ni lazima nipunguze mademu kwani nilikuwa nikitoa sana zaidi ya kuingiza. Wakati imefika mwezi wa kumi na mbili kwenye tarehe ishirini, ndipo nilipoanza kuhisi hali ya tofauti mwilini mwangu.

    Kwanza mwili ukaanza kuuma sana, kizunguzungu na kuanza kulala kila wakati. Kiukweli nilikuwa na hofu kubwa, moyo wangu ukaniambia kwamba nilikuwa naumwa UKIMWI ila upande mwingine ukaniambia kwamba nilikuwa naumwa malaria.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikutaka Salama ajue, nilikuwa chumbani kimya, nikatoa taarifa ofisini kwamba nilikuwa naumwa sana. Nahisi Salama alishangaa kwa nini sikuwa nikitoa ndani, mara nyingi alikuja mlangoni na kugonga, sikufungua ila baadaye nikaona ujinga huu, ningeweza kufa, hivyo nikamkaribisha.

    Salama: Tatizo nini mume wangu?

    Mimi: Nahisi naumwa sana, nasikia sana kizunguzungu...

    Salama: Twende hospitalini... (Aliniambia huku akinishika kupima joto la mwili wangu, ulikuwa wa moto mno)

    Mimi: Naogopa sindano.

    Salama: Sasa kama unaogopa itakuwaje? Twende kwanza...

    Hakukuwa na jinsi, bado nilikuwa kwenye hali mbaya mno, muda wote nilikuwa mnyonge huku mwili ukiniuma sana. Hakika kipindi hicho nilikiona kuwa kigumu kwangu na muda mwingi nilikuwa nikihisi kwamba ningeweza kufa.



    Salama akaninyanyua na kunipeleka sebuleni, akaniambia nisubiri, akaenda nje ambapo akaita bajaj na kunipakia, safari ya kuelekea hospitalini ikaanza.

    Ndani ya bajaji hiyo sikuwa na nguvu, nilibaki nikiwa nimemlalia mapajani tu, nilideka sana kwake, mpaka leo nikikumbuka jinsi nilivyodeka kwa mwanamke ambaye sikuwa nikimpenda, niliyemtesa, hakika ninajishangaa sana.

    Tulipofika hospitalini, akanitoa na kunipeleka ndani. Huko, kulikuwa na watu wengi, alichokifanya ni kuniweka kwenye benchi na kunitaka nitulie hapo. Muda wote Salama alikuwa pembeni yangu akinidekeza, nilijisikia vibaya sana na nilijisemea kwamba bila msaada kutoka kwake, hakika ningeweza hata kufa.

    Daktari: Mgonjwa Denis njoo ndani.

    Mimi: Nakuja.

    Nikatoka mapajani mwa Salama na kwenda ndani, nilipofika huko, daktari akaniangalia kwa umakini, tayari alikuwa amekwishanifanyia vipimo na aliniita hapo kwa ajili ya majibu yangu.

    Mimi: Nina vidudu vingapi vya maralia?

    Daktari: Huna maralia, unaumwa UTI.

    Mimi: UTI?

    Daktari: Ndiyo!

    Mimi: Haiwezekani, huo ni ugonjwa wa wanawake.

    Daktari: Kakudanganya nani? Huu ugonjwa ni wa wote lakini unawapata zaidi wanawake.

    Mimi: Sasa mbona umenipata mimi? Choo changu kisafi, tatizo nini?

    Daktari: Kama choo chako kisafi, basi jua kuna njia ulitumbukiza ambayo ina huu ugonjwa, tena haukutumia kinga! Uongo?

    Mimi: Ni kweli (nilijibu baada ya kujifikiria sana, siku tatu zilizopita, nilifanya na msichana Lucy, tena pekupeku, nikajua hapo ndipo nilipopata ugonjwa huo)

    Tukaondoka hospitalini hapo huku nikiwa nimepewa dawa. Nilitembea huku nikiyumbayumba kama kawaida yangu, sikuwa na nguvu kabisa na mtu ambaye alinilea kipindi hicho alikuwa Salama tu.

    Tulipofika nyumbani, kitu cha kwanza akanipeleka chumbani na kuniambia anakwenda kuniandalia uji na juisi, akaenda huko na aliporudi, akaanza kuninywesha uji kwanza.

    Haukuwa na ladha mdomoni lakini alinisisitiza ninywe tena kwa kunibembeleza kama mtoto mdogo. Mapenzi yake aliyonionyeshea kipindi hicho yakaniacha hoi, sikuamini kama angeweza kunifanyia kitu kama hicho.

    Salama: Kunywa uji jamani, bado kidogo tu, malizia mpenzi.... (aliniambia huku akininywesha)

    Mimi: Siwezi, uji mwingi sana...



    Salama: Jamani malizia, mara moja tu, naomba umalizieeeeeee

    Nilijitahidi kunywa, nilifanikiwa kumaliza, akaondoka na kwenda kuniletea juisi ya maembe aliyokuwa ameitengeneza. Nilipenda sana juisi hiyo lakini huwezi kuamini kwamba siku hiyo ilikuwa chungu mno.

    Nilikataa kula lakini Salama bwana, akawa ananing’ang’aniza na kuniambia kwamba hiyo ndiyo ilikuwa salama ya afya yangu. Hebu fikiria, ugonjwa kakupa mwanamke mwingine halafu unakuja kumsumbua mwanamke ambaye wala hausiki, kila nikifikiria namna ilivyokuwa siku hizo, nilibaki na kujiambia kwamba huyu Salama ndiye alikuwa mtu sahihi, mwenye mapenzi ya dhati zaidi ya wale wengine.

    Nilipomaliza kula, akaniambia nipumzike na yeye anakwenda kuandaa chakula. Kitandani nilikuwa na mawazo mengi juu ya Salama, moyo wangu ukapiga konde na kusema LAZIMA NIWE NA SALAMA.

    Mchana huo, marafiki zangu na wafanyakazi wenzangu wakafika hapo nyumbani, walipokelewa vizuri, nikaitwa kwenda kuwasalimia. Nikaenda huko, Salama akaenda jikoni kuandaa chakula.

    Mudi: Huyu ni mfanyakazi wako?

    Mimi: Hapana! Huyu si ndiye yule mwanamke aliyeniolea baba!

    Issa: Mmh! Huyu mwanamke ni noma, ana mapokezi mazuri sana, mchangamfu mno! Haki ya Mungu, Denis, huyu mke, sikufichi, huyu mke kaka! Nimewahi kwenda kwa watu wengi wanaoumwa, mapokezi tunayoyapata huko ni tofauti na huyu mwanamke.

    Michael: Isaa anasema kweli! Unajua mpaka na mimi nikashangaa...

    Maneno waliyokuwa wakiyazungumza, yakaingia kichwani mwangu. Niliwalewa sana, baada ya chakula kuiva, Salama akawaletea, tena kwa heshima kubwa na kuanza kula. Wote wakabaki wakimshangaa, alikuwa msichana wa kipekee kabisa.

    Issa: Kaka umekubali kuwa naye au?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Kama sijakubali.

    Issa: Niachie mimi! Natafuta mke wa namna hii...

    Wote: Hahaha!

    Issa: Sasa kama unaona dodo unafikiri inakuwaje? Kama wewe kibogoyo huwezi kula, tuachie wenye meno tutafune.

    Sifa walizokuwa wakimmwagia Salama zilinishangaza sana na kujiona kumbe nilikuwa mjinga tu, nilikuwa na kitu cha thamani ndani ila sikuwa nimeiona thamani yake.



    Hebu fikiria, nimetembea na wanawake wote unaowajua wewe! Weupe, weusi, wanene, wafupi, wembamba, warefu, wenye wowowo, vipotabo lakini kote huko, sikupata kitu chochote zaidi ya kumaliza pesa zangu na kukaribia kupata magonjwa.

    Walipoondoka, nikamuita Salama na kumshukuru kwa ukarimu wake kwangu na kwa wageni wangu, akaniambia huo ulikuwa wajibu wake na wala hakutakiwa kushukuriwa, yaani ni sawa na daktari kumponya mgonjwa halafu umshukuru, hapana, ule ni wajibu wake, wapo hapo kwa ajili ya kazi ya kuwaponya wagonjwa.

    Sikuwa na nafuu, niliendelea kuumwa lakini Salama alikuwa bega kwa bega. Wakati nikiwa naumwa hivyo, wanawake wangu, yaani michepuko ikawa inanitumia meseji kwamba walikuwa wakitaka pesa, yaani hata kunijulia hali walishindwa, hivyo nikaachana nao.

    Mimi: Mke wangu! Siwezi kulala peke yangu, naogopa nitakufa.

    Salama: Unatakaje?

    Mimi: Tulale wote.

    Salama: Kweli?

    Mimi: Ndiyo!

    Salama: Hapana, nimepazoea sebuleni mume wangu, kunanifanya nijisikie amani, huru, naomba niendelee kulala sebuleni.

    Mimi: Hapana! Hautakiwi kulala sebuleni tena, wewe ni mke wangu! Nimekutesa kwa mwaka mzima, siwezi kukubali kukutesa tena, naomba tulale wote.

    Salama: Ila kumbuka wewe ni mgonjwa.

    Mimi: Najua ila naomba tulale wote.

    Kweli usiku wa siku hiyo, kwa mara ya kwanza nikalala na Salama. Sikutaka kufanya kitu, si unajua nilikuwa mgonjwa hoi, nilikuwa mpole tu. Salama hakunifanyia utundu wowote, muda wote alikuwa kimya, hakulala, aliuchukua mto, akauweka nyuma, akauegemea na kisha kunilaza katika mapaja yake.

    Hata nilipokuwa nikishtuka usiku wa manane, nilipomwangalia, alikuwa macho akiniangalia tu.

    Mimi: Mbona hulali? Saa nane hii?

    Salama: Nakulinda, sitaki kulala kwa kuwa unahitaji ulinzi wangu mume wangu! Nisipokulinda mimi, nani atakulinda? Naomba nifanye wajibu wangu!

    Nilibaki nikimshangaa, alikuwa mwanamke wa ajabu kabisa. Kama alivyosema, kweli alimaanisha, hakulala, alibaki akinilinda usiku kucha, nilimuonea huruma, alipoamka, kama kawaida akawa ananipetipeti mpaka hali yangu ilipoanza kutengemaa.



    Tarehe mbili Januari ndipo nilipopona kabisa, nilimshukuru sana Salama kwa kile alichonifanyia, sikuamini kama kweli, kwa jinsi nilivyomtesa angeweza kunifanyia mambo kama yale, ndiyo kwanza angenikatili na hata kuniulia mbali, ila yeye, walaa hakufanya hivyo!

    Mimi: Naomba unisamehe, sasa nipo tayari kuanza maisha na wewe!

    Salama: Kweli?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mimi: Ndiyo! Hakika umefanya kitu nisichokitarajia kabisa, nashukuru sana.

    Salama: Asante sana kipenzi....

    Huo ndiyo ukawa mwanzo wa maisha mapya, baada ya hapo, tulikwenda kijijini kuwashukuru wazazi kwa kunipatia mke mwema, wenyewe waliniambia kwamba walihakikisha wananipa mwanamke mzuri, mwenye tabia njema na ndiyo maana walinichagulia huyo.

    Basi baada ya mwezi mzima, Salama mke wangu akaniambia ana dalili zote za mimba, sikuamini, tukaenda kupima, kweli akaonekana kuwa mjauzito! Hivi ninavyoongea na wewe, tayari mimi ni baba wa mapacha wawili, wa kike aitwaye Claire na wa kiume aitwaye Clarence.



    MWISHO



    Ahsanteni kwa kuifuatilia simulizi hii tangu mwanzo mpaka hapa ilipoishia. Bila shaka kuna mengi mmejifunza. Kwa yale mazuri, yachukueni na yawe msaada katika maisha yenu ila kwa yale mabaya, yaacheni.



0 comments:

Post a Comment

Blog