Simulizi : Plastic Tears
Sehemu Ya Tatu (3)
“kwanini unasema hivyo.” Aliongea Joakim na kukaa vizuri na kuanza kumsikiliza Maheer.
“mdogo wake Ahlam bwana ndio aliyekua amepiga simu jana na leo toka asubuhi amekazana na sms. Sijui kitu gani kilichomfanya mpaka achukue namba yangu na kunitafuta hivi toka jana.” Aliongea Maheer na kumuangalia Joakim ambaye wakati huo alikua anamsikiliza kwa umakini mkubwa.
“kwani wewe umeshawahi kumuona?” aliuliza Joakim huku akiwa na shauku ya kutaka kujua.
“hatujawahi kuonana kabisa, yaani hata mimi mwenyewe nashangaa.” Aliongea Maheer na kumfanya Joakim kujitupa kitandani na kujifunika shuka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ameshapenda huyo… itakua Ahlam kakumwagia sifa wee ndio maana huyo mdogo wake anataka kujiweka kwako.” Aliongea Joakim na kumfanya Maheer atabasamu.
“we unaonaje kama kesho tukimualika sehemu yoyote ili tuonane nae…. Inaweza ikawa bahati yako brother.” Aliongea Maheer kiutani na kumungalia Joakim.
“mimi bado macho yangu hayajaona bwana.” Aliongea Joakim na kugeukia upande wa pili kuonyesha kuwa alikata mawasiliano yalikuwepo kati yao kwa muda ule na kuunganisha mawasiliano ya usingizi na ndoto.
Kama kawaida yake toka siku iliyopita, ujumbe mfupi uliingia kwenye simu ya Maheer iliyokuwa ikimtakia asubuhi njema. Maheer, hakuwa na ajizi. Alirudisha ujumbe huo huku anatabasamu.
Mawazo ya kuangalia kama namba hiyo ilikua imeunganishwa whatsapp yalimjia na kuanza ku refresh account name yake ya mtandao huo wa jamii. Alipoipata account hiyo. Alimchokoza kwa kutuma picha yake.
Dakika mbili baadae zikaingia picha tano matata katika account hiyo. Maheer alitoka mbio na kwendas kumuonyesha Joakim huyo mdogo wake Ahlam alivyo.
“wooooooh”
Alijikuta Joakim akimnyang`anya simu Maheer na kuziangalia zile picha kwa ukaribu. Mwili mzima ulimsisimka baada kuona ni jinsi gani Asphaa alivyokuwa mzuri.
“tunaenda saa ngapi mwanangu?”
Alijikuta anaulizia muda wa kwenda kuonana na Asphaa wakati jana yake tu alikataa na kumwambia mwenzake kua macho yake yalikua bado hayajaona.
Maheer alimuangalia Joakim na kutabasamu.
“ tukimaliza kula chakula cha mchana ndio nita mcheki.” Aliongea Maheer na Joakim akaonyesha hali ya kukubaliana naye.
Walipomaliza kula chakuala cha mchana, Joakim akamkumbusha Maheer ahadi yake. Maheer nae hakufanya ajizi, alichukua simu yake na kuangalia kama mafuta yata mruhusu kuongea kwa muda mrefu. Baada ya kuridhika na salio lililokuwemo kwenye simu yake. Alibonyeza namba za Asphaa na kuiruhusu simu yake kupelekwa kwenye mawimbi ya satellite. Muito wa simu ulioashiria kua simu inapatikana uliwafanya Joakim na Maheer kuangaliana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“weka loud speaker.” Aliongea Joakim kwa sauti ndogo ya kunong`oneza
Baada ya sekunde mbili, simu hiyo ilipokelewa na Asphaa na wote wakatulia na kuanza kuongea nae kwa utaratibu kabisa.
“nimejikuta leo hii ghafla tu natamani kukuona.” Aliongea Maheer baada ya salamu na matani ya hapa na pale. Kauli hiyo ndio alikua anaisubiri Joakim toka walipoanza kuongea na simu.
“oooh.. realy?, wapi sasa?” aliongea Asphaa na kuwafanya wote watabasamu.
“wewe tu… sijui tukutane pande zipi?” aliongea Maheer na kujikuta amempa majukumu hayo Asphaa.
“now natoka home naenda shooping mlimani city.” Aliongea Asphaa na kumfanya Maheer amuangalie Joakim ambaye alimpa ishara ya kukubali kukutana nae huko.
“basi sio mbaya kama tukikutana huko, maana hata sisi tulikua na mpango wa kwenda shooping.” Aliongea Maheer na kumuangalia Joakim ambaye alimuonyeshea dole gumba kama ishara ya kumpongeza.
“poa, msichelewe sana basi.” Aliongea Asphaa
“poa,”
Alijibu Maheer na kukata simu.
Baada ya kukata simu. Wote walinyanyuka na kwenda kujiandaa. Maheer alitoka simple tu, ila Joakim aliripuka sana. Si kwa mabomu, Bali viwalo alivyojitupia mwilini.
Walipanda kwenye gari yao na kuelekea maeneo ya mlimani city.
Walipofika walitafuta parking, kwa mbali wakaiona gari ndogo aina ya Starlet iliyokua na namba zilizokua zinafanana kabisa na gari ya Ahlam. Wakajua kua bila shaka Asphaa alikua ameshawasili maeneo hayo.
Maheer alichukua simu yake na kumpigia Asphaa.
“bila shaka umefika.” Aliongea Maheer.
“yeah.” Alijibu Asphaa.
“hata sisi ndio tunaingia muda huu, upo upande gani?” aliuliza Maheer
“huku kwenye tangazo la gari la promotion . njoo huku game mlango wa pili kutokea kushoto.” Alielekeza Asphaa na kumfanya Maheer akate simu baada ya kuelewa.
Joakim na Maheer wakaenda mpeka walipoelekezwa, walianza kuangaza macho yao huku na huko ili mradi waweze kumuona mlengwa wao.
Joakim alipoinua macho yake mbele kutazama waelekeapo, alikua wa kwanza kumuona Asphaa akiwa na umbo lake halisi lililo fanana kabisa na kwenye picha alizoziona kwenye simu ya Maheer kupitia mtandao wa whatsApp.
Alitoa macho sana na kuanza kumshtua Maheer aliyekua bize na simu. Maheer alipomuangalia Asphaa, macho yake yakagongana na macho ya Aspaa na kumfanya binti huyo mdogo kushika mdomo wake kwa mshangao baada ya kuwaona.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asphaa aliwasogelea na kuwapa salamu kwa kuwashika mikono. Ulaini na uteke wa mikono ya binti huyo, ilikua ni silaha tosha kwa Joakim ambaye alionyesha wazi kufurahia kukutana na Asphaa huyo kuliko hata Maheer. Joakim alidata baada ya kuziona picha zake tu. Leo amepata nafasi mpaka ya kushikana nae mikona, aliona ni bahati iliyoje.
Baada ya salamu na maongezi ya hapa na pale. Joakim alitambulishwa na Maheer kwa Asphaa na kupata nafasi ya kushikana mikono tena kwa mara ya pili.
Salamu hiyo iliwafanya wote watabasamu na kuangaliana vizuri usoni huku Asphaa akionyesha wazi kua alikua na aibu baada ya kuinamisha kichwa chake chini.
Baada ya maongezi hayo ya utambulisho, waliingia kwenye restaurant ya hapo mlimani city na kupata chakula ambacho kiliandaliwa kwa siku hiyo. Baada ya hapo walipata nafasi ya kuingia kwenye ukumbi wa sinema na kuangalia filamu moja.
Asphaa alipitiwa na usingizi na kujikuta amemlalia Joakim. Kwakua walimuweka katikati, upande wa kushoto alikaa Maheer na kulia alikaa Joakim ambaye alipata bahati ya mtende kulaliwa na mrembo huyo.
Joakim alimuangalia Maheer na kumkonyeza. Maheer alicheka na kumlipizia kwa kupandisha kidogo na kushusha nyusi za jicho la kulia na kama ishara ya kulipokea konyezo lake.
Baada ya kuangalia filamu hiyo, walimuamsha Asphaa na kutoka naye nje. Waliagana huku Joakim akiomba ruhusa ya kuchukua namba ya simu ya Asphaa. Walibadilishana namba zao na wote wakaachana kwa furaha.
Furaha ilikua mara mbili yake kwa Joakim ambaye alijikuta amefurahia sana mtoko huo ambao aliamini ulikua special kwa ajili yake.
Siku hiyo alikua na furaha kuliko kawaida. Hata usingizi haukupata nafasi haraka.
Baada ya siku mbili kupita toka waonane na Asphaa, wote walikua bize na whatsApp na kutumiana picha na video mbali mbali ikiwemo sauti ambazo zilikua kama vile kumbu kumbu katika memory card ya Joakim.
Urafiki wao uliongezeka kutoka team ya watu watatu na kuwa wanne baada ya kumjumlisha na Asphaa aliyekuja kuleta mapinduzi na kuwa rafiki pendwa kwa Joakim kuliko Ahlam aliesoma nae chuo kimoja.
Maisha ya familia mbili zilizokua kama ndugu kwa wakati huo yaliendelea huku kila mmoja akiwa na lake moyoni.
“vipi mshikaji.” Aliuliza Maheer alipomuona Joakim akiwa amepooza kwa siku hizo mbili.
“safi tu brother.” Alijibu Joakim na kujiinamia.
“nakujua Joakim, ukiwa hivyo ni dhahiri kabisa kuwa una tatizo. Kuwa huru hata kama tatizo lako linasababishwa na mimi.” Aliongea Maheer huku akimuangalia Joakim ambaye muda huo aliacha kujiinamia na kumtazama yeye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“nahisi nina malaria.” Aliongea Joakim ma kumfanya Maheer aliridhike na jibu hilo.
“malaria si ya kupuuzia hata kidogo, twende hospitali .” aliongea Maheer na kumfuata Joakim na kumnyanyua pale alipokaa.
Walienda mpaka hospital. alipopimwa Joakim, aligundulika kuwa alikua na wadudu wawili wa malaria.
Aliandikiwa dozi ya sindano na akaanza hapo hapo kupatiwa tiba kwa muda walioenda.
Waliporudi nyumbani, Maheer alichukua simu yake na kupiga namba moja katika kitabu cha majina ya simu yake.
“haloow” aliitikia mtu aliyekua upande wa pili baada ya kuipokea simu yake.
“hallow”Maheer alijibu haraka.
“habari yako” alisalimia dada aliyekua upande wa pili.
“safu tu Ahlam, nilikua nakupa taarifa tu kua Joakim anaumwa.” Aliongea Maheer na kumsikiliza kitendo atakacho kitenda mrembo huyo baada ya kusikia kutokea taarifa zile juu ya Joakim.
“jamani… anasumbulliwa na nini wangu?” aliuliza Ahlam huku akionyesha wzi kuwa alikua anajali afya ya Joakim
“malaria.” Aliongea Maheer
“poa, tutakuja nyumbani kwenu jioni.” Aliongea ahlam na kukata simu yake.
Ilipofika jioni, Ahlam na mdogo wake walienda nyumbani kwa kina Maheer huku wakiwa wamebeba mfuko uliokua na matunda kadhaa kwa ajili ya kumuona mgonjwa huyo.
Walipofika, walifunguliwa na Maheer na kuingia ndani mpaka sebuleni, kisha Maheer akaingia ndani na kumuamsha Joakim aliyekua chumbani kwake amelala.
“wameshakuja wageni ambao niliokuambia watakuja.” Aliongea Maheer na kumuambia Joakim ambaye aliamka huku sura yake ikionyesha wazi kabisa kua alikua ni mgonjwa.
“nakuja.” Aliongea Joakim.
Maheer alitoka nje na kwenda kuwatoa upweke wageni wao.
Joakim alikaa na kuanza kuikarabati sura yake kutokana na hali ya usingizi aliyokuwa nayo. Kisha akavaa shati laini na kutoka nje.
“pole wangu.” Aliongea Asphaa baada ya kumuona Joakim akikaa pale karibu na sofa alilokaa yeye.
“ahsante.” Aliitikia Joakim huku akijilazimisha kutabasamu.
Walimkabidhi zawadi zake na kuanza kupiga stori za hapa na pale katika kumliwaza mgonjwa wao.
Ilipotimia saa moja usiku. Walimsindikiza Joakim kwenda kuchoma sindano. Waliporudi waliachana juu kwa juu na wao wakarudi kwao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ukaribu wao uliwapendeza mpaka wazazi wa Maheer kutokana na kusaidiana kimawazo na kila mmoja alikua anamjali mwenzake.
Baada ya wiki moja, Joakim alirudi katika hali yake ya kawaida. Siku hiyo aliamua kwenda salon kupunguza nywele zake, alipokua huko alipigiwa simu na Asphaa na kumuomba akutane nae siku hiyo akiwa peke yake. Alishangaa na kujikuta anafurahi hata kabla hajaambiwa kitu alichokiitiwa.
“umependeza sana mwana… unaenda wapi?” aliuliza Maheer baada ya kuona mchomoko wa Joakim aliotoka nao haukuwa wa kawaida.
“kuna sehemu naenda tu mara moja… nakuja sasa hivi.” Aluiongea na kumuacha mwenzake kwenye mataa.
Aliondoka na gari yao na kumfanya Maheer asijue ni kipi kilichomfanya mwenzake awe vile siku ile.
Alifika eneo walilokubaliana mapema kabisa na kukaa eneo ambalo lilikua tulivu na kumsubiri Asphaa aliyemuhitaji mwenywe kwa siku hiyo.
Dakika kumi baadae, gari ya Ahlam ilifika na kupaki sehemu yake. Alishuka Asphaa akiwa amependeza sana.
Alichukua simu yake na kumpigia Joakim. Baada ya maelekezo, alifuata njia na kwenda kukutana na Joakim alipo na yeye akachukua siti ya karibu kabisa na Jaokim alipo.
“umenisubiria sana eeh?” aliongea Asphaa huku akivuta kiti chake na kukaa.
“hapana… kama dakika Tano tu.” Aliongea Joakim na kuachia tabasamu.
Baada ya salamu na utani wa hapa na pale, hatimaye Asphaa aliamua kufunguka kitu alichumuitia pale Joakim.
“samahani sana kama utahisi chochote labda cha kukukosea heshima kwa hiki nitakachokuambia Joakim.” Alitanguliza kuomba radhi Asphaa kabla hata hajaanza kuongea kitu alichotaka kumuambia Jaokim.
“bila samahani.. tena kuwa huru kuongea chochote juu yangu.” Aliongea Joakim na kuamua kukaa vizuri kumsikiliza Asphaa kitu kilichomfanya asuesue kumueleza.
“unajua kila binaadamu ameumbwa na hisia, na kila mwanamke ameumbwa na siha. Ila siha ya mtu inaweza kufilisika baada tu ya kuzidiwa na hisia juu ya kitu Fulani. Siku fichi Joakim, hivi sasa nimezidiwa na hili jinamizi la mapenzi. Linanisumbua sana. Linanifanya nikose hamu ya kula na usingizi wangu unakua wa mashaka sana kwa ajili ya hii kitu mapenzi. Nimevumilia sana na hivi sasa nimeamua kukuambia wewe kama rafiki yangu wa karibu. Nina amini kabisa kuwa utanitoa katika jamga hili linalonikabili na unaweza kuirudisha furaha yangu inayopotea kila siku na kujawa na hisia za simanzi juu ya penzi langu kila siku isafiriyo kwa mungu. Hakika naamini kua muda umefika na wewe ndio utanisaidia kwa asilimia zote katika kufanikisha ndoto zangu. ………..NAMPENDA SANA MAHEER…. Nakuomba unifikishie huo ujumbe.. nateseka sana juu yake.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliongea maneno hayo Asphaa bila kujua kua alikua ana mchoma moyo zaidi Joakim. Kiukweli Joakim alijua kua macho yake yamefumbuka kwa msichana huyo wa kwanza kumtia moyoni kabla ya kuongea. Alijikuta jasho linamtoka na kushindwa kuongea lolote na kubaki akimtazama Asphaa ambaye alionyesha sura yenye uhitaji wa msaada wake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment