Simulizi : Let Me Die
Sehemu Ya Tano (5)
Alilia sana kiasi cha kuwaliza mpaka wazazi wake. Baba yake akanyanyuka pale alipo na kumsogelea. Alipomfikia, alimshika bega la kulia. Hali iliyomfanya Abdul ageuke na kukurtana na sura ya baba yake iliyojaa imani na upendo juu yake. Hakusita kumkumbatia kwa uchungu huku akimuita baba kwa mara ya kwanza toka anapata akili timamu.
Mama yake nae hakua mbali, aliwasogelea na na kuwakumbatia wote kwa pamoja. Hakika kilio cha faraja ndicho kilichoendelea kati yao.
Furaha ya kukutana na wazazi wake ilimfanya Abdul kuandaa sherehe kubwa ya utambulisho wa wazazi wake. Media zote zilitangaza tukio hilo la kihistoria lililofanywa na msanii mkubwa hapa nchini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Taarifa hizo zilifika mpaka kijijini kwao walipotokea wazazi wake. Walifurahi sana kwa wazee hao kufanikiwa kuonana na mtoto wao.
Wazee hao hawakupendelea sana kukaa mjini kutokana na mazoea ya mazingira waliyokuwepo. Hivyo walimuomba mtoto wao awarudishe tu kijijini.
Wazo hilo lilkubaliwa na Abdul ila alihakikisha kua inajengwa nyumba nzuri na kijijini kulichimbwa kisima kikubwa kilichokua na maji ya bomba na kuwaruhusu wanakijiji kuchota maji bure.
Aliwanunulia wazazi wake matrekta yapatayo kumi kwa ajili ya kuwakodishia wanakijiji wenzao ili waachane na kilimo cha jembe.
Matunda hayo yaliwafanya wazazi wake wamshukuru sana mungu kwa kuwajali na kukisikiliza kilio chao.
*************************
Baada ya ratiba za chuo kukamilika, Diana alirudi tena Tanzania akiwa na mchumba wake huyo mpya wa kizungu waliyevishana mpaka pete. Mr .Zungu alifurahi sana kuwapokea wageni wake hao na kuandaa sherehe ya ukaribisho kama afanyavyo miaka yote pindi mtoto wake arudipo kutoka katika masomo yake.
Safari hii sherehe iliboa kwa kutokua na Live band. Hata Diana mwenyewe hakuifurahia sana kama kipindi kile alipokuja na kukutana na bend ya Dreams iliyomburudishwa vya kutosha.
Sherehe hiyo iliwatambulisha wapenzi hao waliokua mbioni kufunga pingu za maisha. Baada ya wiki mbili, msafara mkubwa kutoka marekani uliingia Tanzania. Hiyo ilikua familia ya mchumba wake Diana ambao waliingia Tanzania kwa ajili ya harusi ya mtoto wao na Diana.
Harusi hiyo ya kukata na shoka ilitangazwa kila kona ya jiji. Hakuna mtu ambaye alikua hafahamu kuwa mtoto wa Mr.Zungu alikua anaolewa.
Muonekano wa nje, Diana alionekana kuwa na furaha kwakua harusi yake imekua gumzo hapa nchini, ila ndani ya moyo wake bado kulikua na nafasi kubwa ya Abdul ambayo anaamini hakuna mwanaume yeyote anayeweza kukaa na kuziba pengo la Abdul.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kinachomshinda na furaha tu ya baba yake. Maana mwanaume anayempenda, baba yake hataki hata kumuona. Aliwaza sana bila kupata majibu.
“Diana, bado hujajiandaa tu… leo ndio siku ya harusi yako mwanangu. Unatakiwa usiiharibu siku hii kwa kuhuzunika hata kidogo. Fanya haraka basi maana unasubiriwa wewe tu.” Aliongea mama yake Diana huku akimfunga mtoto wake kamba za shela alililolivaa.
Diana alijikuta ameganda kwenye kioo kwa muda mrefu sana mpaka mama yake aliporudi kumfuta tena kwa mara ya pili. Alimtoa na kumpeleka kwenye gari tayari kwa msafara huo wa kuelekea kanisani tayari kwa ndoa hiyo ya kihistoria kwa mtoto wa tajiri wa hapa Tanzania kuolewa na mtoto wa Tajiri kutoka Marekani.
Msafara ulianza kwa gari hiyo aina ya benz nyeusi ikiwa imembeba bibi harusi huyo mtarajiwa akielekea maeneo ya tukio.
Msafara huo uliokua na gari zipatazo tano zilizofanana kila kitu ulianza taratibu na baadae kuongeza mwendo ulipokua kwenye njia kuu.
Walipokua njiani, Diana alikua amejawa mawazo juu ya kipenzi chake Abdul. Alitamani asimamishe gari na kukataa kuolewa na huyo mzungu aliyekubali kuolewa nae ili azibe nafasi ya Abdul.
Hata hivyo bado hakuweza kumfikia hata robo. Ukijumlisha na ukweli juu ya maisha ya Abdul aliuanika katika documentary ya maisha yake ndio kabisaa. Alujua ukweli kua Abdul ni mtu mwema sema hila za baba yake ndio zilizomfanya achafuke kwa kipindi Fulani.
Gari liliendelea kukata mitaa kuelekea katika kanisa lao ambalo ndio ndoa hiyo inafungwa hapo.
“MAMAAAAAAAAAAAA”
Ilikua ni sauti moja tu iliyoweza kusikika baada gari aliyopanda Diana kugongwa na fuso lililokua spidi likitokea kushoto kwao likiwa linataka kuwa over take.
Gari yao ilipinduka mara tatu na kutolewa kabisa nje ya barabra huku ikiwa haitamaniki. Watu wote walishuhudia tukio hilo walibaki midomo wazi. Mama yake Diana aliyekua gari ya pili alitoka huku akiwa kama amechanganyikiwa na kwenda kuishuhudia gari hiyo ambayo ilitapakaa damu.
Wengine walipiga simu emergency na haikuchukua muda, ambulance ilifika na kuchukua watu wote waliokua kwenye ile ajali.
Diana alionekana akiwa kafumba macho huku akiwa na majeraha sehemu chache hususani sehemu za miguu kwa sababu ilikandamizwa na gari hiyo.
Mama yake Diana nae alipakizwa kwenye Ambulance hiyo kutokana na kupoteza fahamu baada ya kuona tu hali ilivyokua mbaya kwa watu waliopanda gari ile.
“hakuna aliyefanikiwa ku note sehemu namba za hilo fuso?” yalikua maneno ya askari ambao walifika sambamba na hiyo gari ya kubebea wagonjwa
“kwa jinsi tulivyopigwa na butwaa, hakuna aliyekua na wazo la kuandika hizo namba.” Aliongea mmoja wa madereva wa magari yaliyosalimika katika ajali hiyo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Askari walichukua maelezo ya kila mmoja wapo na kuchukua mawasiliano yao na kuiripoti ajali hiyo kwenye vyombo vya habari.
Taarifa zilifika kanisani juu ya ajali mbaya iliyompata bibi harusi. Kanisa lote lilitetema na kujawa na huzuni ghafla juu ya taarifa hiyo ya kusikitisha.
Mr. Zungu alikua kama amechanganyikiwa baada ya kupokea taarifa hizo za mtoto wake na juu ya kupotea fahamu kwa mke wake. Hakuna kilichoendelea hapo zaidi ya mchungaji kuhairisha hiyo misa ya ndoa iliyotakiwa kusomwa baada ya bibi harusi kuwasili hapo kanisani.
Safari ya kuelekea hospitali ilianza huku Mr. Zungu akiwa amechanganyikiwa kiasi cha kushindwa hata kuendesha gari na kupewa msaada na mkwe wake huyo mtarajiwa na safari ya kuelekea hospitali waliyo elekezwa ikaanza huku wakiwa kwepa mapararazi waliomiminika kanisani hapo.
Walifika hospitali na kukutana na waandishi wa habari wakiwa wamejazana wakimsubiri Mr. Zungu ili wapate mapokeo ya taarifa za ajali iliyompata mtoto wake wa pekee na aliyekua anampenda kuliko kitu chochote.
Hakuweza kuongea chochote zaidi ya kulia tu na kusaidiwa na wafanyakazi wake kumuingiza hospitalini hapo kutokana na adha aliyokua anayoipata juu ya maswali mfululizo ya waandishi hao huku akiwa hataki kujibu swali lolote.
Alipelekwa chumba cha mapumziko na kutulizwa huko kwa muda baada ya kupewa maagizo hayo na daktari aliyekua anawahudumia wahanga hao wa ajali.
“watu wawili waliokua katika gari hiyo wamepoteza maisha tayari. Na binti yako amesagika miguu kabisa kiasi cha kwamba haifai. Hivyo nakupa taarifa tu kua miguu tumeikata ili tuendelee na tiba nyingine.” Aliongea Daktari nakuwaambia Mr.Zungu na mkwe wake waliokua wote muda huo.
“kwa hiyo dokta mmeshindwa kutumia njia nyingine mpaka kumkata miguu mwanangu?” aliongea kwa Uchungu Mr.Zungu.
“kwa hali ailyokua nayo, hakukua na njia nyengine kwakua ilisagika sana hivyo alistahili kukatwa miguu haraka ili tuzuie damu na kumlinda na bacteria mbali mbali kwa usalama wake.” Aliongea daktari na kuondoka baada ya kuona kuwa hakutakua na maelewano juu yake na mzee huyo aliyechanganyikiwa huku akiwa mwekundu kwa jinsi alivyokua analia kwa muda mrefu.
Baada ya nusu saa, alipelekwa chumba alicholazwa mke wake na kumkuta amesharejewa na fahamu.
Mama yake Diana alianza kulia baada ya kumuona mume wake analia huku kamasi jepesi likimtoka mzee huyo.
“usiniambie mwanangu amekufa!!!!.” Aliongea mama yake Diana huku akilia kwa uchungu.
“hajafa mke wangu…. Ila amekatwa miguu.” Aliongea Mr.Zungu na kumsogelea mke wake na kuungana nae kwenye kilio hicho cha wazazi wenye uchungu na mtoto wao.
“masikini mwanangu…. Ningejua nisingemfuta. Mwenyewe alikua anasita kwenda kanisani… kumbe ndio mambo kama haya yalikua yanataka kumtokea mwananguuuuuu.”
Aliongea kwa uchungu mama yake Diana huku akiongeza sauti ya kilio kilichomchoma zaidi Mr.zungu na yeye akaanza kulia kwa kwikwi huku akionyesha wazi kua sauti ilianza kum kauka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya muda, Diana alirejewa na fahamu baada ya kuisha kwa nusu kaputi aliyopewa kwa ajili ya operation hiyo. Wazazi wake pamoja na mchumba wake akiongozana na mama yake wakaruhusiwa kuingia ndani kumuona Diana.
Wote walishika midomo baada ya kumuona Diana akiwa na antenna mikono yote huku bandeji ikiwa imefunika kichwa chake. Hawakuweza kuona miguu iliyokatwa kwakua alifunikwa shuka.
Kilio kikatawala kwa watazamaji waliokua wanamuona, lakini muhusika alikua kimya tu akiwaangalia huku macho yake akiwa ameyatuliza kwa baba yake ambaye wakati huo hakuwa na uwezo wa kuona vizuri kutokana na ukungu ulojaa machoni kwake kutokana na utawala wa machozi ambayo hakuwahi kulia toka utotoni mwake.
“Mom….. marriage is over, I can`t marry her for this situation.” Aliongea maneno hayo bwana harusi huyo baada ya kumfunua Diana shuka na kugundua kua ni kweli alikatwa miguu yote miwili.
Maneno hayo yaliendana na vitendo baada ya wazungu hao kuondoka na kufanya wazee hao kutomini kiichotokea hapo.
Hapo ndio machozi ya Diana yalipoanza kudondoka bila ya kutoa sauti yake, ila ishara za machungu yatokayo moyoni yalijichora usoni na kuyaruhusu machozi yatiririke kama maji katika mashavu yake.
Mama yake alimfuata huku analia na kumkumbatia kwa uangalifu huku akimfuta machozi mwanae kwa mikono yake.
Mr. Zungu alikubali kuanguka kwa magoti baada ya kuliagalia jicho la mtoto wake na kujikuta ana hatia kubwa ya kumkatili mwanae kuolewa na mtu ampendaye na kumfanya kukubali kuolewa na huyo mzungu kwa ajili ya kumfanya yeye awe na furaha.
Alilia sana Mr.Zungu huku Diana akiwa hataki hata kumuona baba yake kwa jinsi alivyotokea kumchukia.
“nipo tayari kufanya lolote mwanangu ili mradi unisamehe.” Aliongea Mr. Zungu huku akiwa amepiga magoti kwenye kitanda cha Diana.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“umeshachelewa baba….. unafikiri huyo Abdul anaweza kunipenda nikiwa katika hali hii…. Nakuchukia sana na sihitaji hata kukuona tena baba. Umeyatia doa maisha yangu.”
Aliongea Diana huku analia na kusababisha mzee huyo kushikilia nguzo ya kitanda hicho na kuzidi kulia huku mke wake akimbembeleza.
“nipe adhabu yoyote mwanangu kwa sababu nastahili adhabu, ila msamaha wako nauhitaji kuliko kitu chochote. Naumia unaponiambia kuwa unanichukia.” Aliongea Mr. Zungu huku machozi yanamtoka.
“msamaha wangu ni pale utakapoweza kumleta Abdul hapa hosptalini…. Hapo ndio naweza kukusamehe.” Aliongea Diana na baba yake akaitikia kwa kichwa na kutoka hapo hospitalini kama amechanganyikiwa.
Aliingia kwenye gari yake na kuelekea nyumbani kwa Abdul. Alipofika, alikutana na ulinzi mkali. Aliulizwa shida yake na taarifa zikafikishwa kwa Abdul aliyekua ndani kupitia mitambo maalum iliyokua inamuonyesha huyo mtu aliyekua anamuulizia huko nje.
“mwambie kuwa Abdul hayupo.”
Abdul alitoa oda hiyo baada ya kumuona Mr Zungu pale nje.
“hayupo, unaweza kwenda mzee.” Aliongea mlinzi huyo mwenye mwili mkubwa.
“huwa anarudi saa ngapi?” aliuliza Mr. Zungu.
“nimesha kuambia hayupo… hivyo unatakiwa kuondoka eneo hili.” Alikaripia yule mlinzi na Mr.Zungu akatii amri na kuondoka. Alipiga hatua kadhaa na kukaa mbali kidogo na pale ili amsubiri Abdul arudi.
Aliganda mpaka saa tatu usiku bila kuona hata dalili za gari kupita pale. Alinyanyuka na kurudi tena getini.
“mzee… huwezi kuonana na Abdul kwa leo.” Aliongea yule minzi baada ya kumuona Mr. Zungu amerudi tena pale getini.
“mruhusu aingie, lakini hakiksheni mmemkagua vizuri.”
Ilisikika sauti ya Abdul kupitia kifaa maalum kilichokua masikioni mwa yule mlinzi.
Walimkagua na baada ya kuridhika kuwa hakua na kitu chochote kinachoweza kumdhuru bosi wao, wakaamua kumpeleka mpaka ofisini kwa Abdul ambapo alimkuta abdul akiwa amejaa tele ofisini wake.
“unaweza kuongea shida yako iliyokuleta.” Aliongea Abdul baada ya kumuona Mr. Zungu akishindwa aanzie wapi kuongea nae.
“mwanangu wa pekee amepata ajali mbaya.” Aliongea Mr. Zungu huku uso wake ukwa umejaa huzuni huku akimuangalia Abdul kama mtu anayehitaji huruma yake au kupewa pole kwa matatizo yaliyomkuta.
“nimeisikia hiyo habari.” Alijibu Abdul na kumkazia macho Mr. Zungu.
“amekatwa miguu yote miwili… na ameniambia kuwa hawezi kunisamehe mpaka nianze kukuomba msamaha wewe kwa niliyokutendea Abdul.” Aliongea kwa uchungu Mr. Zungu na hapo hapo machozi yakaanza kumwagika upya.
“sorry for her… na kuhusu wewe nilishakusamehe kitambo sana.” Aliongea kwa huzuni kidogo Abdul japokua alijikaza na kuichukulia taarifa ile kikawaida sana.
“pia ana hitaji kukuona leo hii.” Aliongea mze huyo huku akiyafuta machozi yake yaliyomfanya avimbe macho na kuwa mekundu sana.
“swala la kuonana na mim litakua gumu sana.” Aliongea Abdul na kunyanuka kwenye kiti chake. Jambo hilo lilimfanya Mr. Zungu kumpigia magoti Adul na kumshika miguu yake huku akilia kwa sauti iliyokwisha kauka huku akimbembeleza Abdul akubaline na
yeye.
Roho ya imani ilimuingia Abdul na kumnyanyua mzee huyo na kumfuta machozi. Safari ya kuelekea hospitalini usiku huo ilianza huku kila mtu akiwa amependa gari lake na kuongozana mpaka hospitali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Abdul alishindwa kujizuia na kujikuta anaangusha machozi baada ya kumuona Diana akiwa katika hali mbaya sana. Alimfuata na wote wakajikta wanakumbatiana pale kitandani huku wanalia na kuamsha kilio kwa Mr. Zungu na mke wake.
“ I think you know that i`m in love with you at all…. But now you can LET ME DIE because you can`t be mine forever.”
Aliongea Diana kwa sauti ya kulia huku akiwa ameendelea kumkumbatia Abdul ambaye nae muda huo alikua analia kwa uchungu.
“usiseme hivyo Diana… I love you so much.” Aliongea Abdul huku analia na kumpapasa Diana mashavu yake huku akiyafuta machozi ya Diana kwa viganja vyake.
Wakati huo huo, Sapna nae anaingia kumuangalia Diana, hakuamini kumuona Abdul pale. Alijikuta ameganda mlangoni kwa dakika kadhaa. Alipiga moyo konde na kuungana na Abdul pale chini na kumpa pole Diana.
“huyu ndio mwanamke wa maisha yako Abdul. Hata kule hotel tulipokua siku ile ulikua unalitaja jina la Sapna na kujiapiza kuwa ndio mwanamke wa maisha yako… usijali kuhusu mimi Abdul, najua kua huna upendo wa dhati kwangu ila nilikua nakulazimisha. Na hata ukiniambia unanipenda hivi sasa, si kweli ila utakua unanionea huruma tu kwa haya maswahibu yaliyonikuta… huyu ndio yupo moyoni mwako Abdul… nadhani unasubiri jibu kutoka kwake…. Sapna, unampenda Abdul???”
Diana alingea maneno yaliyowachoma wote waliokua pale na kujikuta wanatokwa na machozi. Hatimaye aliuliza swali liliwabaksha midomo wazi
“sio mahala pake hapa Diana kuniuliza swali kama hilo.” Aliongea Sapna kwa sauti ya upole huku akiangalia chini.
“kuwa huru Sapna…. Unampenda Abdul au humpendi?” aliuliza tena Diana.
Sapna alitulia kwa muda huku akiwa hajiamini kwa kile alichoulizwa. Alimtazama usoni Abdul na kujkuta ana angukia kifuani na hilo ndio likawa jibu tosha kwa Swali hilo.
Diana alitabasamu na kuwashika vichwani Abdul na Sapna.
“leo ni siku ya ajabu kwetu. Ilikua huzuni mwanzo ila kwa sasa imekua nzuri kwa kuwakutanisha wapendanao na kumsameha baba yangu kwa dhati ya moyo wangu. Ni furaha pia kwa baba yangu kutambua makosa yake na kujuta kwa kile alichokitenda juu yetu…. Mungu awape maisha marefu.” Aliongea Diana na kutabasamu.
Wote walijikuta huzuni inwapungua baada ya kumuona mlengwa akiwa anatabasamu.
Baada ya mwezi mmoja Diana alitolewa hospitalini na kupewa ratiba za kuhudhuria kiliniki mpaka atakapo pona kabisa.
Mipango ya harusi ya Abdul na Sapna ilipangwa na ulimwengu ulitangaziwa juu ya harusi hiyo ya ina yake.
Siku ya harusi ilifika kwa kuhudhuriwa na watu mbali mbali wenye nyadhifa zao. Wasanii mashuhuri kutoka pande zote za dunia walihudhuria pia.
Meza kuu walikaa wazazi wake Abdul, Mr. Zungu, mke wake na mtoto wao mpendwa Diana.
Ilifungika ndoa hiyo baada ya sheikh kupitisha ubani na watu wakaanza kuisheherekea harusi hiyo iliyogharimu mamilioni ya fedha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zawadi ya mshangao kwa mashabiki ni pale mkusanyiko wa watu sita ulipotimia na kuipandisha bendera ya bendi ya Dreams..
Ufufuo huo wa bendi uliwarudisha tena katika ramani wasanii wa bendi hiyo waliopotea kwa muda mrefu.
Waliopoteza maisha kwa hila za Mr. Zungu walifanya kundi hilo kutotimia idadi ya watu walikuwepo hapo mwanzo.
Na huo ndio ukawa ukurasa wa mafanikio kwa kila aliyeitumikia bendi hiyo chini ya bosi wao mpya ABDUL.
******************** MWISHO****************
0 comments:
Post a Comment