Simulizi : First Year
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati nikijitahidi kushindana na bughudha za stendi hapo kama jina tu lake lilitosha kusaliwili kero za mule ndani "Msavu" nilimsikia moja ya abilia akilitaja jina la mahali pale. Kikwetu Msavu nikama bughudha saa sijui hapa wanamaana gani? Nilijiuliza huku nikijaribu kujikwatu kutoka wakati huo bado macho yangu yalikuwa yakimuangalia tu yule dada kule alipokuwa akienda
Mmh!, sikuamini nikichokiona kumbe lile gari la kifahari nilikuwa nikilishangaa kabla sijashuka lilikuja kwa niaba ya dada yule.
"Mmh", Niliguna, ngoja niwaambie kitu Waandishi ukweli dunia hapa vizuri uenda sambamba na vizuri vyenzao kabisa. Na mimi naamini kabisa katika dunia hii kama ukiumbwa mwanamke hakikisha unakuwa mzuri hautoteseka ,na kama ukijujua wewe si mzuri namaanisha wa kawaida. Basi soma sana la sivyo jua litakuwakia na maisha utayaona machungu kabisa kwa upande wako.
Uzuri wa Shufaa ulitosha kabisa kuishi maisha mazuri kabisa hilo halijipingi. Mimi nikiwa nashangaa gari mwenzangu analipanda kila siku hapo ndio kuna utofauti. Ndugu Waandishi kati yangu na yule mdada si utofuti wa kijinsia tu bali kila kitu nazani hapo mnanielewa kabisa.
Nilitazama ndugu Salimu namna alivyokuwa akiongea aliongea kwa hisia kali sana kabisa wazi niliweza kubaini tu bwana yule kuna jambo zito lilimkuta kwenye maisha yake. Dakika kadhaa ndugu Salimu alitulia huku akiwa kama anatafakari jambo kwa sekunde kadhaa. Alivuta pumzi ndefu mithili ya punda aliyetuwa mzigo. Pumzi ile iliambatana na miguno ya kuugulia maumivu aliyekuwa akiyapata iiii! Agggggh….. Uuuuuu.
Moyo wangu ulighadhabika sana niliumia mno si mimi hata mwandishi mwenzangu hakuwa katika hali ya kawaida
Baada ya yote yale muda kidogo niliweza kuingia ndani ya Mzumbe kwa maelekezo aliyonipatia Shufaa yalitosha vyema kufika mahali pale. Punde tu baada ya lisa limoja na nusu tangia ni shuke ndani ya basi lile. Ugeni nilikuwa nao machoni tu mwa wenyeji wa chuo kile uliwafanya kubaini mimi ni moja kati ya wanafunzi wageni ndani ya chuo kile.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilikata mitaa taratibu nikiwa na mabegi yangu huku nikipishana na wanafunzi wachache ndani ya mitaa ile ya chuo kile. Hata sikujua nianzie wapi niliendelea tu kupiga hatua nilizunguka vya kutosha na majengo yalikuwa yakifanana mno. Basi ilikuwa na zunguka mule mule sasa nilipoona mambo yatanichachia ilinibidi nitafute msaada. Lakini msaada nao ulichelewa maana kila niliyopishana nae alikuwa mtoto wa kike. Hivyo nilikuwa nikiona soo hata kuwauliza ijapokuwa nilishaanza kutoa uoga wa kuongea na viumbe hivyo ila bado ile roho ya kushindwa ilikuwa ikinitawala. Niliendelea kuangalia huku na huku hatimaye nilimwona boy moja nilichepua hatua zangu na kumfata mahali alipo.
“Kaka samahani ndugu mimi mgeni hapa taratibu zinakuwaje kwa upande wetu” aliniangalia kwa muda kidogo hatimaye aliniambia nimfuate. Tukaaza kupiga hatua mdogo mdogo nikiwa na mtupia maswali kaka yule alionekana akiringa dhahiri. Ujibuji wake ulikuwa wa kujishauwa shauwa ila mimi sikulijali nilizidi kuongoza mahali kule. Tulipokuwa tukielekea njiani tulikuwa tukipishana na wanafunzi wengine haki walikuwa wakinitazama sana sijui kwa sababu ya ule ugeni wangu au la.
Tulikata hatua mpaka tuliiingia ndani ya ofisi moja hivi kwa bahati hakukuwa na mtu nje hivyo aliniacha ningie mule ndani. Nilibisha hodi hatimaye niliruhusiwa kuingia taswira yangu. Ilikutana vyema na taswira ya mtu yule wa makamo nikiwa kimya baada ya kutoa salamu kujielezea kilichonipeleka pale. Grafla simu yangu iliinza kuita nilijibinya kwa nguvu iliniikate ilikuepusha usumbufu mule ofisini lakini ilikataa. Macho yangu yakiwa sambamba na mtu yule ilionesha kuchukizwa na hali ile haraka tu alinipachika swali.“Kijana unaonekana dhahiri kabisa ujawahi kuingia sehemu zenye hadhi? Alinyamaza kidogo huku akiwa bado ananitumbulia macho wakati huo simu yangu ilikuwa tiyari imeacha kuita.
Nilikaa kimya hata cha kujibu nilikuwa sina nilijikuta tu napoteza kujihamini mbele ya yule mbaba na weza kumwita hivyo ndugu Waandishi. Kwa sababu ya umri wake kutokana na muonekano wake ilifaaa mimi kumwita hivyo.Hata mdomo nilishindwa kunyanyua , aliendelea kuongea kile alichotaka kuzungumza kama kichwa chake kilivyo muhamuru kufanya vile mbele ya macho yangu
“Wewe kijana” kwa ukali sana aliendelea “maishani mwako…. kabisa sisi tunawaanda nyinyi katika misingi iliyobora jifunze kokote kule mahali kwenye ofisi za watu hutakiwi kuleta mambo ya ajabu ajabu kama hayo kwani ?nani ana simu jifunze umesikia kijana siku nyingine usifanye hivyo si umenisikia”
SURA YA NNE
Nilitulia kidogo huku nikitikisa kichwa changu kuashiria kuwa nimemuelewa mbaba yule namna alivyokuwa anaongea. Ilitosha tu kubaini tabia yake muda mfupi tu kiukweli alikuwa mnoko hata sikujua jambo la kawaida vile analichukulia jambo kubwa hivyo. Lakini sikuona ajabu ndugu Waandishi labda niseme kitu kabla sijaendelea.
Nilibadili mkao maana tiyari makalio yangu yalikuwa yamechoka sikuwa peke yangu hata mwaandishi mwenzangu. Nilimwona akijivuta huku akionekana anashuku dhahiri kufahamu kile ambacho ndugu Salimu anakiongea. “Kwa sauti ya upole nilimjibu ndugu Salimu tupo makini endelea tu”
Hizi tabia za namna hizi zipo sana kwenye maofisi mengi kuna watu wanajifanya kama wamezaliwa na kila kitu hapa duniani. Na kuwaona wenzao si kitu kabisa ,haswa wale wenye vyeo kwenye maofisi mengi. Hivyo ndugu Waandishi japokuwa kitu kile kilikuwa kigeni kwangu ndani ya ofisi ile ila hivi vitu vipo na vinisikitisha sana katika hii dunia.
Nilipewa maelekezo yote kama mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ndani ya chuo kile yaani First year.Hapo sasa ndio maisha yalianza rasmi ndani ya chuo kile. Hakika sitakuja kuhisahau siku ile na kama muda ungekuwa unarudi nyuma nilitamani ile siku ingerudi nyuma. Na hata nisingekubali yatokee yale aahhh !,kwanini? ilikuwa hivi maisha haya yana mambo sana nawaomba haswa vijana wajifunze kutokana na hichi ninachokisema First year umeniponza mimi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huo tiyari nilishaoneshwa hostel ambapo ndio ilikuwa mahali husika kwa jili ya makazi yangu. Muda wote ndani ya chuo kile, taratibu nilibeba mizigo yangu kuelekea mahali hosteli zilipo. Nilikatiza mitaa ndani ya chuo kile huku nikiendelea kupishana na watu wa aina tofauti. Kiukweli maisha ya chuo ni tofauti kabisa na maisha ya sekondali , kuanzi rika hata mavazi ilikuwa tofauti kabisa.Yaani macho yangu siku ile yalionana na vitu vya tofauti sana naweza kusema. Maana kila niliyepishana nae alikuwa akijenga utofauti ndani ya kichwa changu si mavazi tu umri na kila kitu vili leta utofauti sana kwangu.
Niliingia ndani ya hosteli kwa vile nilishapewa hadi chumba nilichotakiwa kulala.Hapo pia nilikumbana tena na kizaazaa, cha kukisaka chumba nilichopangiwa.Nilizunguka kidogo na hatimaye nilipata msaada mule ndani kutoka kwa wanafunzi wachache niliwakuta. Na wao walionekana wageni kama mimi siunajua mgeni kama mgeni ukimwangalia tu lazima utamjua. Hajifichi machoni hata kidogo walinielekeza mahali ninapotakiwa kukaa na kwa bahati nilikuta kuna mwanafunzi mwingine. Kidogo ilikuwa njema kwa upande wangu kupata mtu ambaye naweza kusema mwenyeji ijapokuwa yeye alikuwa kama mimi ni mwaka wa kwanza. Ila alitangulia kuja hivyo ilikuwa rahisi kunionesha mazingira ya pale chuo.
Kizuri zaidi tulikuwa tunachukua kozi moja nilitambua hilo baada kuzungumza nae. Alionekana mtu wa starehe maana stori zake tu zilikuwa zikiwazungumzia wanawake. Hazikuwa zikinivutia sana kwa wakati ule na sikumbuki lini nilianza kuvutiwa na stori zile. Ninachokumbuka ni maumivu haya ninayopata kutokana First year ndugu Waandishi. Naomba mjifunze mazoea yanajenga tabia ila tabia haijengi mazoea ndugu Waandishi nazani tupo pamoja.
Uwiii ! alivuta pumzi kubwa ndugu Salimu hali yake, ilikuwa dhaifu mno muonekano wake ulitisha sana. Ijapokuwa mgonjwa unatakiwa umpe moyo atapona ila kwenye macho yangu ulifuta kabisa uwezekano wa kijana yule kupona. Sijui ndugu Arifu aziz upande wake mwandishi mwenzangu alikuwa akiona nini? ila taswira yake ilionekana ya kukata tamaa tu.
Aliendelea kuzungumza maneno yale yalikuwa yakitoka ndani ya kinywa chake.
Siku tatu tu niliweza kuelewa mazingira ya chuo kile, sikuwa na rafiki zaidi ya yule mwana room wangu. Kila sehemu tulikuwa tukienda tulikuwa pamoja na hata hapo tulianza kuelewana sana. Tulikuwa kama mapacha wiki , ndani ya chuo tabia yangu ilianza kufana naye. Kiukweli alikuwa ana ushawishi sana nilijikuta tu na mimi napenda kufanya vitu anavyofanya yeye muda mfupi. Kila mtu alituelewa darasani haswa mimi nilichaguliwa kuwa class representative. karibia member wote walikuwa namba za kwangu sio boyz sio girls.
Hapo sasa ndio usumbufu ulipokuwa umeanza kuja upande wangu. Visichana vilinipa kelo sana mpaka nilikuwa naogopa kupokea namba ngeni. Nilikuwa nikizifikiria sana na muda mwengine nilikuwa nikimpatia Izack apokee.
Maisha muda mfupi tu yalikuwa hivyo maeneo yote tulikuwa tumeyazoea.
Wakati huo nilishasahau maisha ya kubanwa tena niliamini niko sahihi sana kila nilichokuwa nafanya upande wangu. Niliona yale ndio maisha kumbe nilikuwa na kosea yote ilikuwa First year kwanini? ilikuwa hivi.
Mwenzi moja ulitosha mambo yangu kubadilika sasa akili za ki sekondali ziliondoka kabisa. Nikawa mwanachuo kamili na hata mwenendo wangu sasa ulibadilika. Nilikuwa nikipendeza sana ijapokuwa nilikuwa nikipata usumbufu kutoka kwa watoto wakike ila nilikuwa bado nikiogopa sana. Nilimkumbuka Baba alikuwa akiniambia sana ukitaka kufanikiwa maishani basi kaa mbali sana na watoto wakike. Yaani nisijihusishe kwenye mapenzi kabisa si jambo vyema,sauti ile ilikuwa bado inajirudia kichwani mwangu. Jambo hilo mwanzoni lilikuwa gumu licha ya ushawishi mkubwa kutoka kwa marafiki zangu haswa Izack. Ila nilikuwa mgumu kweli sikutaka suala lile liniingie kwenye damu yangu kabisa. Kwa muda ule naweza kusema kitu hapa ndugu Waandishi katika hii dunia haswa dunia ya uwanafunzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ogopa sana marafiki, vikundi mbali mbali mashuleni hatari sana kila mtu anabeba tabia tofauti sana. Kitendo cha mimi kuwa na marafiki wa aina ile ,hata sikujua ilikuwaje nilijikuta tu nadumbukia kwenye mapenzi. Jambo ambalo lilikuwa gumu mwanzoni kwenye kichwa changu.
Namkumbuka sana yule msichana wangu wa kwanza ndani ya chuo kile na si chuo tu mule ilikuwa ndio mara ya kwanza mimi kuingia kwenye Dunia ya mapenzi. Hakika sitasahau siku ile ni mwenzi miwili tu tangia nijiunge na chuo kile. Ndipo nilipoanza michezo ile ambayo wazazi haswa wa kwangu naweza kusema hawakukosea kuita michezo mibaya wanakoseaje?kuita hivyo wakati ndugu Waandishi mnaona wenyewe kwa macho yenu ubaya wa michezo ile. Hii si stori ndugu bali ni mkasa ulionitokea kwenye maisha yangu mimi Salimu punde tu nilipoanza kulifahamu jina naweza kusema la First year.
Namna ambavyo ndugu salimu alivyokuwa anaongea hakika jambo lile halikuwa la kawaida kabisa. Nilitulia kwa makini kabisa kusikiliza kile ambacho kijana yule anacho kizungumza. Sasa nilianza kupata mwanga wa kile kilichomkuta kijana Salimu. Wakati huo mwandishi mwenzangu bwana Arifu Aziz simu yake iliianza kuita kitendo kile kilimfanya ndugu Salimu atulie kidogo kusitisha kile alichokuwa anakiongea.
Alitoa macho kidogo ndugu yule punde tu bwana Arifu alipomaliza kuikata yake simu. Alikohoa khoo! khoo!, na kuachia tabasamu hafifu mbele ya mboni zetu. Alafu aliunua kinywa chake kuonesha kuendelea kutupatia kile kilichomo ndani ya kichwa chake.
Baada ya usumbufu wa muda mrefu kutoka kwa dada yule hatimaye nilikubali wake wito. Naikumbuka vyema jioni ile nilipokubali kupokea wito wa dada yule. Ilikuwa ndani ya hoteli nzuri ndani ya Morogoro mjini nje kidogo na Mzumbe chuoni kwetu .Ni umbali wa dakika arobaini hivi na kitu kutokea pale mahali chuo kilipo. Nikiwa nimependeza kuonesha ushababi wangu taratibu niliingia ndani ya hoteli ile. Kwa maelekezo aliyonipatia ilitosha kufahamu haswa mahali ambapo alikuwa amekaa nilijivuta hatimaye nilifika eneo lile.
Kiukweli ndugu Waandishi katika hii dunia wanawake wanaushawishi mkubwa sana. Kinguo alichovaa yule dada kiukweli kilikuwa kinaonesha sehemu kubwa ya mwili wake wazi wazi. Mbele ya macho yangu hata nilipojaribu kukwepesha yangu macho ilikuwa ngumu kukwepa mautamu yale kwenye mboni zangu. Meza moja tu ilitosha ikiwa inaviti viwili ambavyo nilijuwa tu ilikuwa mahususi kwa jili yangu. Nilinyongea hatimaye nilifika na kuketi mahali pale huku nikaribishwa na tabasamu mwanana na dada yule.
Recho ndio lilikuwa lake jina kiukweli mungu alimuumba kabisa hakumkosea hata kidogo. Alibalikiwa kila kitu sura nzuri macho yenye mvuto yalikuwa ni kivutio kikubwa kwa msichana yule. Pindi nilipoweza kukaa nae karibu muda mfupi niliweza kubaini hayo yote.
Sikuwa najua dhamira ya mimi kufika eneo lile nilikubali tu kufika pale baada ya kunisumbua sana. Izack ndio alichangia mimi kwenda pale niya na madhumuni tu kwenda kusikiliza wito ule. Ambao nilikuwa tu nahisi ndani ya fikra zangu tu shida na dhamira yake ila sikutaka moja kwa moja nitoe suluhisho ya kile ambacho nilikuwa nakiwaza juu ya wito ule.
Niliagiza kinywaji baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Recho huku tukiendelea kuongea maongezi ya kawaida.Kwa kuwa nilikuwa situmii bia niliagiza soda taratibu ilikuwa ikiendelea kusindikiza maongezi yetu. Tuliendelea kuongea kama nusu saa hivi nilihisi uwepo wa haja ndogo ulikuwa unakaribia kuja kwenye mwili wangu . Niliomba kuoneshwa mahali pakwenda kuitoa aaah... raiti ningejua basi ile haja isingekuja kwa muda ule Ihiiiiiiiiiiiiiiiiiii!, ishiiiiiiiiiiii!
SURA YA TANO
Hapa kuwa mbali na mahali ambapo tulikuwa tumeketi , baada ya kupewa maelekezo na Mhudumu aliyekuwepo karibu ndani ya hoteli ile. Mara moja nilienda kumaliza haja yangu nilipiga hatua chache na kuingia mahali mule. Dakika kadhaa nililejea mahali pale nikaribishwa tena na tabasamu nzito la Resho. Taratibu tukiendelea na maongezi ,nikisindikizwa na kinywaji changu kama nilivyokiagiza.
Hapa Waandishi mambo ndipo yalipoharibika kwa sababu kadiri nilivyokuwa na kunywa kile kinywaji hali yangu ilianza kubadilika. Nilihisi kichwa kizito sana na hata sikufahamu hali ile kwanini? ilikuwa ikinitokea. Ila baada ya yote yalitokea siku ile niliweza kubaini kuwa kitendo cha mimi kutoka kwenda chooni. Ilikuwa kama mwanya aliotumia Recho kumaliza alichokuwa amekizamilia, kwasababu naweza kusema uwenda kama akili yangu ingekuwa mwenyewe nisinge fanya yote yale.
Muda ulikuwa umeenda huku tukiendelea kuongea na Recho hapo sikuwa hata nawazo tena la kurudi chuoni. Kama nilivyokuwa nimepanga baada punde tu kusikiliza wito wa Recho. Haikuwa hivyo tena tuliendelea tu kuongea, nikitokwa na maneno ambayo hata sikujua yalikuwa ya natoka wapi? Nahisi hakikuwa kinywa changu kilichokuwa kikitoa maneno yale kabisa.
Kigiza nacho kiliingia hatimaye mboni zangu zilipoteza nuru sikuweza tena kuona kile nilichokuwa nakiona. Miguu ulikuwa mizito sikujua kiliendelea nini? kutokea hapo ninachokumbuka nilijikuta nipo kitandani. Punde mboni zangu zilipoipokea nuru tena haikuwa kawaida kabisa nilijigeuza huku na huku sikuona mtu kitandani pale. Niliendelea tena kutazama huku na kule ndani ya chumba kile. Cha ajabu nilichokiona hata sikuwa na niamini kwa sababu sikujua kile ninachokiona nikweli au naota. Nilifikicha macho yangu kuangalia tena nguo!,nguo! zangu zile nilijikuta nalopoka hapo sasa akili ikanicheza ina maana kuwa nipo uchi nilifunua shuka Mama wee!...CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilichokiona ndugu Waandishi kilinifanya nijiulize mara mbili mbili inamaana Recho amenifanyia yote bila ridhaa yangu na kwanini? Amenifanyia hivi na kama tumefanya ilikuwa salama au nilijikuta na jilaamu sana kwanini? nilikubali wito ule nilijiona mjinga sana.
Kabla hata sijajua cha kufanya nilisikia mlango unafunguliwa wa chumba kile niligeuka kuangalia nani? Hakuwa mwingine Recho macho yangu yaligongana ana kwa ana macho ya mdada huyo. Hata uwezo wa kunyanyua mdomo wangu nilishindwa nilijikuta nimeshikwa na hasira mbaya.
Taratibu Recho alijisogeza mahali pale kwenye kitanda huku akinisogelea mahali nilipo mimi. Kuniacha nisijue cha kumfanya taratibu alifunua shuka moja kwa moja na kuanza kunipapasa maeneo ya ikuru yangu. Sikuelewa nimekumbwa nanini? nilishiwa nguvu kwa kweli nikabaki tu nimemuachia mwili wangu afanye kile alichokuwa anakifanya. Ambacho kwangu mimi kilikuwa kigeni ndugu Waandishi namna ambavyo alivyokuwa akicheza na maeneo yale nilijikuta najisikia raha. Sikutamani tena Recho aache kile alichokuwa anakifanya nikiwa mshamba wa mapenzi. Kiukweli Recho aliendelea kunifanyia mchezo ule haki mchezo ulikuwa mtamu balaha. Sikujua utamu ule wote unatokea wapi ?nilijikuta tu natoa miguno tu mara hiiiiiiiiiiiii!, shiiiiiiii!.. ahahhhhh! sikuelewa inatokea wapi? si mimi hata mwenyewe Recho naye ilikuwa akitoa sauti fulani ambazo zilikuwa zikiniongezea raha sana upande wangu.
Tuliendelea kufanya ule mchezo kama masaa mawili hivi hatimaye tulichoka.Na hata sikujua saa ngapi? tulipatwa na usingizi ! usingizi mzito sana nakumbuka mwisho tu nilikuwa nipo juu ya mwili wa Recho. Tukiendelea kufanya mchezo ule basi ilikuwa hivyo hivyo nilistuka nipo juu ya mwili wa Recho. Nilijitoa haraka sikutaka tena jambo lile liindelee kwa wakati huo Recho alikuwa bado yu usinginzini. Haraka niliingia bafuni ndani ya chumba kile cha hoteli nakujimwagia maji. Akili yangu haikuwepo kabisa pale nilijikuta nimechukizwa na mahali pale sikutaka hata kukaaa.
Nilirudi mahali pale nakuanza kuvaa nguo zangu wakati na maliza kuvaa tu kabla hata sijanyanyua mguu wangu. Kutoka mahali pale nilisikia sauti ya Recho ikiniuliza kile nilichokuwa nataka kufanya punde tu nilipogeuza yangu shingo. Kuelekea mahali sauti ile ilipokuwa inatokea pale kitandani. Kwa hasira sana na sauti ya kadhabu nilimjibu Recho aniache kabisa. Nikiwa naelekea mahali mlango ulipo kwa haraka na kuufungua , nikiwa sijali kile alichokuwa anakisema Recho.
Nilipiga hatua kuutafuta mlango ulipo wa kutokea ndani ya hoteli ile dakika moja nilifahamu mahali pakutokea. Nilipiga hatua na hatimaye nilikuwa nje ya hoteli sikuwa na cha kufanya moja kwa moja nilitafuta magari ya kurudi chuoni. Na baada ya muda kidogo nilifika ndani ya chuo kukiwa kumetulia tofauti na jumapili zote. Bahati Izack nilimkuta kwenye room letu nilingia na kujitupa kitandani baada ya kupokea yake salamu. Muonekano wangu ulitosha kujua kuwa sipo sawa hata kabla hajaniuliza kitu. Simu ya Izack ilianza kuita sekunde tu wakati nimejibwaga kitandani pale niliweza kusikia kile Izack alichokuwa anakiongea. Ndugu Waandishi maongezi yale yalikuwa ni kama msumali kwangu.
Kwanini? Izack azungumze na mtu yule alafu anazungumza kikawaida, kana kwamba kitendo alichonifanyia Recho kilikuwa kawaida. Haki nilishikwa na gadhabu pale kwenye kitanda niling'ata meno kuashilia nilikuwa sikubaliane na jambo lile. Nikiwa tiyari nimetumbulia macho Izack yeye alikuwa yuko kawaida sikutaka kuzungumza chochote nilitulia kimya. Nilijuwa wazi uwenda mipango ile Recho alimtumia Izack na si kwahivi hivi uwenda hata alimpatia pesa ili kuukamilisha adhima yake.
Nilijitupa tena kitandani hata usingizi uliponichukua sikujua kutokana na kuchoka sana .Na yale yalitokea usiku na asubuhi mwili wangu ulikuwa hauna nguvu , hali ya kulala nisingiweza kuizuia. Nililala kweli hata nilipokuja kustuka sikuamini na sikuelewa kama ilikuwa ni kigiza cha kuikaribisha asubuhi au usiku. Baada ya muda nilifahamu kuwa ni saa moja ya usiku , hapa kuwa na mtu ndani nikilikuwa mimi mwenye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kumkaa kule ilinibidi nitafute maji ilikuweza kuoga kuondoa uchovu ule. Ijapokuwa nilitoka kiuvivu uvivu hatimaye niliweza kuekea bafuni na kuoga. muda mfupi tu nilipokuwa navaa zangu nguo mlango wa chumbani ulifunguliwa. Hakuwa mwingine Izack macho yangu yalimwona vyema hapo sikutaka kukaa kimya tena. Nilianza kubwabwaja juu yale aliyonifanyia Recho nilibwabwaja vya kutosha ,kuna muda nilimtupia lawama Izack. Kwanini? ilikuwa vile, kutokana Izack alikuwa ananielewa sana aliishia tu kujitetea mbele yangu. Sikuona shida tena niliamua kunyamaza wakati huu njaa ilikuwa ikigonga kwenye tumbo langu. Nilimwwmbia Izack anisindikize maeneo ya cafe area nikapate chakula.
Izack hakuwa na hiyana aliamua kunisindikiza, tukiendele kupiga stori na kwa vile Izack alikuwa mzee wa mastori. Muda tu nilianza kusahau kile kilichotokea ,tulipiga hatua mpaka maeneo yale tuliingia na kuagiza chakula. Kwa upande wangu ila Izack yeye aliagiza soda alidahi ameshiba hivyo hana mpango wa kula tena. Tulikaa kwenye moja ya meza punde tu mhudumu alituletea kile tulichoagiza.
Naweza kusema kitu Waandishi siku ile nilikula vibaya mara nyingi chakula ambacho nilikuwa nikiagiza mahali pale nilikuwa si malizi hata kidogo. Sikujua siku ile tumbo langu lilipakia kweli hata Izack alishaanga jambo lile ila alilimezea. Tulimaliza na kufanya malipo na kulejea hostel hatukuwa na mpango wa kutoka kama jumapili nyingi.
Soga zilifatia baada ya kufika ndani ya chumba chetu tulipiga domo hadi mida tulipo ona sasa muda wa kulala. Kila moja alisogelea kitanda chake na kujitupia kwa upande wangu usingizi ulichelewa na hata pale ulipokuja kuja. Nilijikuta nayakumbuka yale yote nilikuwa nimeyafanya na Recho hapo sasa nilikumbuka utamu ule japo kitendo kile. Nilifanya bila ridhaa yangu ila ilikuwa kama kuchovya kidole kwenye mzinga wa asali. Ndugu Waandishi naweza sema jambo lile kiasi lilinipeleka puta sana mpaka nilipozea michezo ile sikutaka kuikosa tena.
Nakumbuka vyema baada ya wiki moja tangia tukio lile litokea nilikuwa sijaonana na Recho tena wala kupokea simu kutoka kwake. Hali ile ilileta ukinzani kwenye kichwa changu Recho alikuwa akinirudi nilivumila vya kutosha. Ila niliona wacha nimtafute kweli nilimtafuta Recho kitendo kile kilinifanya nijue kuwa sikuwa mimi tu niliyeteseka na kitendo kile.
SURA YA SITA
Hata yeye alikuwa akiteswa na mchezo ule sema alipoteza simu yake alipokwenda kwenye msiba.
Kitendo cha kunitajia habari za msiba kidogo nilistuka, nilimpa pole kwa msiba ule. Ambao nilifahamu kuwa alifiwa na Bibi yake baada ya mazungumzo yale. Sauti yake namna alivyokuwa anaongea ilitosha kufahamu vyema alikuwa anafuraha isiyoelezeka.
Hapo sasa mchezo ule nilianza kuuzoea na raiti ningejua nisingekubali kuuzoea mchezo ule ndugu Waandishi yote ilikuwa First Year.
Kikubwa tu ambacho Recho alifanikiwa ni kulinew line ndomana tuliweza kupata mawasiliano. Alikuwa anafuraha sana na mimi kidogo moyo wangu ulifalijika, sikujuwa kwanini? nakuwa vile ndugu Waandishi. Sasa dunia ya mapenzi ilianza kutawala kwenye maisha yangu , tulitumia muda mwingi kuzungumza. Na Recho hakusita kunikumbushia yale yalitokea tulijikuta tunacheka wote, hapo sasa mapenzi yangu na Recho ndipo yalipoanza rasmi.
Recho alikuwa ndio mwanamke wangu wa kwanza tangia nipozaliwa , upendo wangu ulikuwa mkubwa sana na sijui kwanini? Ilitokea vile ndugu Waandishi na kama ningeweza kuzuia jambo basi lile lingekuwa la kwanza katika yangu maisha. Nakili lile lilikuwa kosa kubwa sana ndugu Waandishi katika maisha haya na omba mjifunze kitu kamwe usiwamini viumbe vinavyoitwa wanawake kabisa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hapo ndugu Salimu alinyamaza kidogo akitutumbulia macho kuonesha msisitizo wa jambo lile. Kiukweli namna alivyokuwa akisimulia lile jambo wazi lilikuwa likimchoma sana. Ndani ya moyo wake na sijambo dogo kabisa ndugu msomaji wa mkasa huu naomba uelewe kitu. Katika maisha haswa maisha ya kawaida kabisa, hakuna jambo ambalo linaweza kubadili mfumo mzima wa maisha kama mapenzi. Ni jambo ambalo linaharibu sana maisha ya watu haswa vijana.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment