Simulizi : Sipendi Ujinga Mimi
Sehemu Ya Nne (4)
BAADA YA MIEZI 3
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Siku za kujifungua zimekaribia safari hii usifanye makosa kama uliyofanya kipindi kile,” alisema binti Shomvi.
“Sawa naahidi kulitimiza ata kama itagharimu uhai wangu,” alisema mama Amina.
Hali ya Mlali haikuwa nzuri kwani tayari alishaanza kusikia uchungu, mumewe akafanya kila awezalo ili kumuwaisha hospitali, kwa kuwa Sharifu Shamba ni karibu sana na hospitali ya Amana ivyo iliwachukua dakika 10 kwa mwendo wa gari kufika.
Mama Amina akawa akiwafatilia kwa karibu mno, masharti ya dawa aliyopewa safari hii ilimlazimu aipulize kuelekea upande alipo Mlali. Wauguzi wakampokea na kumpeleka wodini baada ya daktari kumuangalia na kugundia kuwa bado anasiku moja kabla hajajifungua. Baba Aida ikabidi arudi nyumbani kwa ajili ya kwenda kutoa taarifa kwa ndugu wakaribu ili waweze kumsaidia walau kuandaa chakula pindi awapo kazini.
Usiku wa siku iyo mama Amina akasogea hadi eneo la hospitali kisha akaongea maneno yasiyoeleweka na ghafla akageuka na kuwa paka mweusi na kuingia hadi wodi aliyopo Mlali na kwa bahati nzuri akakuta amelala ivyo ikawa nafasi nzuri ya kutimiza azma yake. Akatazama huku na huko akiwa bado katika umbile la paka alipojiridhisha na usalama wake akabadirika na kuwa mtu, akachukua dawa aliyopewa na binti Shomvi na kuipuliza kwa Mlali na papo hapo Mlali akawa anaweweseka alipo ona dawa yake inamatokeo chanya akajibadili katika umbo la paka na kuondoka.
Asubuhi ya siku iliyofata Mlali akaamka na homa kali sana, mabadiliko yale yaliwashtua sana madaktari ikabidi wamfanyie vipimo vya haraka, lakini hawakuweza kugundua tatizo. Ilipotimia saa 3 asubuhi Mlali akaanza kusikia uchungu, manesi wakamchukua na kumpeleka leba, wakamuandaa tayari kwa kujifungua lakini akajikuta anaishiwa nguvu na kupoteza nguvu ya kusukuma,
“Jitahidi kusukuma, utamuua mtoto,” aliongea muuguzi mmoja.
“Kweli jitahidi bado kidogo mtoto yupo karibu,” alidakia muuguzi mwingine.
Mlali akajitahidi sana hatimaye akafanikiwa kujifungua ila mtoto akawa amekunywa maji machafu, muuguzi alipoona hali ile ikabidi amyanyue kichanga Yule kichwa chini miguu yuu na kuanza kumpiga piga ili ayatapike yale maji. Mlali alipoona hali ile akajikuta anapoteza fahamu kwa kukata tamaa kwasababu alisikia kwa wengi kuwa mtoto aliyekunywa maji machafu uhai wake si mrefu.
Siku zikaenda lakini afya ya mtoto Yule ilikuwa dhaifu ndani ya wiki mbili akaanza kushikwa na magonjwa ya ajabu ajabu, Mlali akaanza kuangaika kwenda hospitali. Maisha ya mtoto Yule yalitegemea zaidi sindano na madawa. Wazazi wake hawakuweza kufurahi hata kidogo sababu ya matatizo yanayomsibu mtoto wao,
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“eenh! Mungu kama kweli mtoto huyu atakuwa ni nuru katika familia yangu sasa kwanini anateseka angali mdogo hivi?”
Mtoto akazidi kukua kwa kimo na akili akaonekana ni mtoto mwenye utofauti mkubwa na wengine, mtoto Yule alipewa jina la Mdidi na akiwa na miaka miwili tuu, maisha yao yakabadirika sana. Ile nuru iliyokuwa ikizungumwa angali yu tumboni ikaonekana, baba yake alipata kazi katika kampuni moja ya serikali ambayo ni maarufu kwa utengenezaji wa mablanketi kwenye miaka hiyo ya 90. Juhudi na kujituma katika kazi kukamfanya baba Aida kupanda cheo kazini kwake iyo ilienda sambamba na kuongezwa mshahara pamoja na posho nyingine, ndani ya muda mfupi alifanikiwa kujenga nyumba na huo ndio ukawa mwisho wa kuishi kwenye nyumba za kupanga.
Miaka 7 baadae Mdidi akaendelea kusumbua kiafya, safari hii hali yake ilikuwa mbaya zaidi ya alivyokuwa mtoto mdogo, wazazi wake walihangaika kila hospitali kuhakikisha afya yake inarudi katika hali ya kawaida lakini haikuweza kusaidia kitu.
Ilikuwa siku ya Alhamisi majira ya saa 1 jioni, familia nzima ilikuwa sebuleni wakiongea, huku Mdidi akiwa pembeni amelala kwenye kiti, hali yake ikabadirika ghafla akakosa nguvu hata ya kuongea, wazazi wake waliogopa mno, jitihada za haraka zikafanyika kumuwahisha zahanati iliyo karibu, lakini kabla hawajafika zahanati Mdidi akawa amepoteza fahamu asielewe chochote kinachoendelea. Baada ya vipimo kufanyika daktari akagundua kuwa anaupungufu wa maji, ivyo ikalazimu aongezewe maji.
“Mama Aida! Mimi ni mwanamke mwenzako hali aliyokuwa nayo Mdidi si ya kawaida, umeangaika sana hospitali sasa kwanini usijaribu upande wa pili?”
“Upande wa pili upi?”
“Kwenye tiba za jadi”
“Unamaanisha nini kusema hivyo”
“Mimi ninavyoona Mdidi amechezewa sio bure, kwa hiyo lazima uende kwa mtaalamu akamkague la sivyo utampoteza mtoto bure”
“Mhmhmh! Dada unahisi mganga anaweza kuwa suluhisho kwa tatizo la mwanangu”
“Ndio mama Aida! Si unamkumbuka mtoto wa mpwa wake na mama Yassini naye alikuwa anaumwa hivi hivi ila toka nilivyompeleka kwa mtaalamu, tatizo lote likaisha”
“Sawa dada nimekuelewa ngoja nishauriane na baba yake, alafu tutakapofikia tutakwambia maana mwanangu anateseka sana,” alisema Mlali huku machozi yakimtoka.
Kiukweli aliumizwa sana na mateso anayopata mtoto wake, kuna wakati hadi alitamani kumwambia Mungu kwanini asiugue yeye na mwanae awe huru na mwenye furaha kama watoto wengine.
Siku iliyofuata Mdidi bado aliamka na hali mbaya ikabidi awaishe hospitali ya Amana na baada ya vipimo, akaonekana ana damu ndogo sana ivyo ilikuwa ngumu kwao kuendelea na matibabu wakampa uhamisho hadi hospitali ya rufaa Muhimbili ambako huko nako alifanyiwa vipimo na kugundulika ana moyo mkubwa.
Hali ya simanzi ilikuwa kubwa miongoni mwa wanafamilia kila mmoja alishangaa majibu waliyopewa na daktari,
“Hapana baba Aida, mwanangu hawezi kuwa na tatizo hilo mbona nilimzaa akiwa sawa tuu!”
“Tumuachie Mungu mke wangu, yeye ndiye muamuzi wa mwisho juu ya hatima ya mwanadamu”
“Mimi nahisi mwanangu watu wamemfanyia vibaya, twende kwa mtaalamu tukamkague”
“Nini?” aliuliza baba Aida kwa hasira sana.
“Toka lini umekuwa na imani hizo, nani aliyekutia huo ujinga? Vipimo vinaonesha mwanetu anatatizo la moyo wewe unaongea upumbavu gani! Sasa nisikilize kwa makini na unielewe mimi kama baba wa mtoto huyu sitaki mwanangu apelekwe kwa mganga.”
“Lakini baba Mdidi huoni kama mtoto wetu anateseka sana”
“Mungu pekee ndiye anauwezo wa kumponya mwanetu, kumbuka ata maandiko matakatifu yanavyotuonya juu ya kuweka tumaini kwa mwanadamu ambaye hata yeye atakufa kama sisi, tuombe Mungu mwanetu atapona tuu,” alisema baba Aida au Mdidi.
************************
“Mungu pekee ndiye atakayeweza kumuondoa mdogo wangu katika balaa hili,” alisema Aida baada ya kukumbuka matukio kadhaa ya nyuma toka kuzaliwa kwa mdogo wake Mdidi hadi kufikia umri huo, ambapo sasa amelala kitandani hakiwa hajitambui baada ya kuteleza na kuanguka pindi alipotoka msalani.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huu si ugonjwa wa kawaida,” alisema mzee Kobelo baba mwenye nyumba ambayo Mdidi amepanga.
Watu wengi waliguswa na tukio lile, wakajitokeza kwa wingi kuja kumjulia hali Mdidi huku kila mmoja akiwa na Lake Moyoni.
“Daah! Maskini Mdidi amejifanya shujaa kuchimba mambo yasiyo muhusu, ona sasa amelala hamtambui anayeingia wala anayetoka, ama hakika kuna watu hawapendi ujinga,” alisema mama mmoja ambaye anaishi jirani na Mdidi.
“Sasa dada! Ulivyoenda hospitali wamesema ndugu yako anatatizo gani?” akauliza Yahaya machipsi.
“Hamna ugonjwa wowote ulioonekana,” Aida akajibu.
“Mhmhmh! Mambo hayooo”
“Ila naamini mdogo wangu atapona”
“Atapona vipi bila kujiongeza dada, alafu ujue mdogo wako mwanaharakati sana, yaani kitaa kilikuwa kishaanza kuwa raha mustarehe ila daah naona kuna mjinga kamuotea, alafu wewe dada unavyokaa kizembe hivyo naona kama haufanyi poa,” aliendelea kuongea Yahaya kwa hisia sana, huku akionekana kuumizwa kwa tukio lile.
“Njia za Mungu si za mwanadamu na kila litokealo hutokea kwa sababu, japo huyu ni mdogo wangu wa damu lakini moyoni mwangu kuna tumaini kubwa kwamba ipo siku Mdidi atakuwa sawa”
Wakati hayo yanazungumzwa mama Salehe hakuwa mbali, alisikiliza kila linaloongelewa kwa makini zaidi, huku akizidi kushangaa moyo ule alionao dada yake na Mdidi. Ni watu wachache sana wenye imani kama ile na wasiokubali kuyumbishwa kwenye misimamo yao.
“Mhmhm! Shoga yaani kila nikimuangalia huyo Mdidi hadi najisikia vibaya”
“Kwanini?”
“Huyo dada ake nilijua atatangaza vita ila ndio kwanza anasema anamuachia Mungu, sijui ni mlokole Yule mimi nlijua vita ndiyo itakuwa mbichi nijipange kwa mashambulizi zaidi lakini sivyo”
“Sasa mama Salehe nawe, kazi si umeifanya tena vizuri tuu sasa yupo kitandani”
“Ila mbona mtaalamu alisema hatochukua muda mrefu ataamka na kuanza kuonesha tabia ya ushoga ila leo siku ya 5 bado mambo yako vile vile”
“Mhmh! Usijali shoga yangu mambo yatajipa tuu, tusubili kidogo”
Taarifa ya kuugua kwa Mdidi zikamfikia mzee Kilonda, kwa hakika alihuzunika sana alishindwa kujizuia akafunga safari akiwa na mjukuu wake Cathy hadi alipo Mdidi. Watu walishangaa sana kumuona mzee Yule katika nyumba ile, taarifa zilisambaa kwa haraka kama upepo na kutua moja kwa moja kwa mama Salehe. Naye hakuweza vumilia ikabidi aende kwa shoga yake mama Ashura kwa haraka sana,
“Vipi tena mbona haihai?”
“Shoga nilijua walokole kumbe nao sio watu wazuri?”
“Wamaanisha nini?”
“Unamkumbuka Yule mzee wa kipindi kile wakati nagombana na mama Juma?”
“Ndiyo namkumbuka”
“Sasa huyo mzee kaja tena hivi ninavyozungumza yupo chumbani kwa Mdidi”
“Duuh!”
“Hakuna cha Duuh! Shosti hapa nilipo nimevurugwa hata sielewi nifanyaje na Yule mzee alivyokuwa mwanga puuuuuu!” aliongea mama Salehe huku akikaa kwenye kiti.
“Mhmhm! Shoga yangu punguza munkari mboni mzee yule cha mtoto mimi nammudu!”
“Weeeh! Sema kweli mama Ashura”
“Mie sio wakispoti spoti, akiyachokoza lazima naye aonje maumivu”
Waliendelea kupanga mipango yao ya kiovu, huku wote wakiamini kuwa mzee Kilonda sio mtu mzuri, kama alikufa Salehe kipindi kile sasa hivi itakuwa zamu ya nani.
********************
“Dada pole sana! Mdidi ni mtu mwema na mwenye upendo kwa kila mtu, ila hali hii yahuzunisha sana,” alisema Cathy huku akiwa amekaa karibu Zaidi na Mdidi.
“Nimeshapoa! Tumuombee tuu na Mungu atamponya”
“Nimependa sana msimamo wako mjukuu wangu, huyu kijana ni mfano wa kuigwa katika jamii, naamini atapona na kazi ambayo aliianza lazima itatimia,” alisema mzee Kilonda.
Mzee kilonda baada ya kuongea machache na Aida ikabidi aage ili aweze kuendelea na shughuli nyingine, Cathy alikumbuka vizuri hisani aliyofanyiwa na Mdidi kipindi anaumwa hivyo akaamua abaki walau kumfariji na kumtia nguvu dada yake na Mdidi ambaye alionekana kumuhudumia mdogo wake kwa kila kitu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hivi dada, katika familia yenu umezaliwa wewe na Mdidi tu?”
“Hapana tupo wanne, wakike wawili na wakiume wawili, ila tuliopo hapa ni mimi na yeye”
“Wengine wako wapi?”
“Mdogo wetu wa mwisho yupo nje ya nchi kimasomo, na anayenifatia mimi kuzaliwa ambaye ni wakiume yeye yupo Afrika kusini kikazi”
“Na wazazi je?”
“Wazazi wapo ila sijawaambia mama anasumbuliwa na presha ivyo akisikia hali ya mwanae anaweza pata tatizo Zaidi maana alihangaika na Mdidi sana toka akiwa mdogo”
Maongezi ya hapa na pale yakaendelea huku wakiendelea kumuomba Mungu ampe nafuu Mdidi, walau aweze hata kuinuka kitandani.
*******************
Ni saa 8 kamili usiku, hali ya hewa ikiwa tulivu huku watu wengi wakiwa wamelala. Hali ilikuwa tofauti katika msitu mmoja uliopo pembezoni kabisa mwa jiji la Dar es Salaam, kikao cha dhalura kilikuwa kinafanyika siku iyo huku wachawi wote wakitakiwa kutoa taarifa juu ya kazi walizopewa. Wingu zito likatawala eneo hilo na watu waliokuwa eneo hilo wakaacha kuimba na kusikiliza maelekezo waliyopewa,
“Leo ni siku ambayo kila mmoja atatoa taarifa ya kile alichoagizwa kufanya katika kitongoji chake kulingana na uwezo aliopewa,” alisikika sauti moja kali na iliyojawa na mitetemo ikitamka maneno hayo.
Watu wote wakainama mtindo wa kusujudu walifanya ivyo mara saba, kisha wakanyanyua vichwa vyao na sauti ile ikaendelea kuzungumza,
“Kwa yeyote aliyeshindwa kutimiza maagizo ataadhibiwa hapa hapa”
Watu wakainama na kusudu kama ilivyokuwa kwa mara ya kwanza, kisha mwanaume mmoja aliyejaa aliyejazia vizuri kama wale wanyanyua vyuma akasogea mbele na kukaa upande wa kulia, kisha majina yakaanza kutajwa mmoja baada ya mwingine.
“Tukae Khamisi! Wewe ulipewa roho ya kufunga vizazi katika mtaa wako, tupe taarifa umefanyaje,” alisema mtu mmoja ambaye hakuwa anaonekana vizuri, alijifunika kuanzia juu hadi chini ila sauti tuu iliweza kutambulika kuwa ni ya kike.
“Mtukufu mwenye enzi katika dunia hii utukuke!” akainama kutoa heshima zake.
“Kazi imefanyika vizuri, wanawake wengi waliokuwa wajawazito nimesababisha mimba zao kuharibika na wale ambao bado, nimefanikiwa kuwafunga vizazi,” alijibu mama yule kwa kujiamini.
Watu wakampigia makofi kisha akainama na kusujudu mara saba akasogea na kukaa upande wa kushoto huku akitazama wenzake.
“Shabani Mahoka! Tulikupa roho ya uchochezi wa ngono, tupe taarifa umefanyaje”
“Mtukufu mwenye enzi katika dunia hii utukuke, nimefanikiwa kupuliza roho hiyo katika kitongoji changu sasa hivi, si vijana si watoto, wala si watu wazima ashki ya ngono imewaamka, sio ajabu baba kuzini na binti yake na wala si ajabu kwa kijana wa kiume kufanya mapenzi na mtu mwenye umri sawa na mama yake”
Naye akapigiwa makofi ya nguvu, vicheko na nderemo zilitawala eneo hilo, mkuu alioneshwa kufurahishwa na tukio hilo.
”Mama Ashura! Tulikumba roho ya malumbano na mauaji kwa ajili ya sadaka zetu, je umefikia wapi?”
“Mtukufu mwenye enzi katika dunia hii utukuke, nimefanikiwa kuleta malumbano na hata vifo katika kitongoji changu, nilimuua mtoto wa rafiki yangu, nikamuua mpangaji mwingine aliyetambulika kwa jina la Upendo, pia nikaua vijana 10 kwa wakati mmoja,” alijibu mama Ashura huku akiwa na hofu kuu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kweli kikulacho kinguoni mwako siku zote izo hakuna aliyejua kuwa mama Ashura ni mtu mbaya sana na asiyefaa kwenye jamii, kazi yake ilikuwa kuleta malumbano baina ya watu na hata kuua huku lawama akiwabebesha wengine wasiohusika.
“Mama Ashura! Kazi yako hadi sasa inaendelea?”
“Hapana mkuu! Kuna kidudu mtu anayeitwa Mdidi huyu amekuja kuharibu mipango yangu yote, watu wameanza kusikilizana na kama sikufanya la ziada basi hataanika kila kitu wazi”
“Huo ni uzembe usiovumilika, tunamuona Mdidi kitandani akiwa na hali mbaya ila shambulio lenu halijafanya kazi yeyote, tunamuhitaji mama Salehe katika dunia yetu anatakiwa apate mafunzo hili msaidiane kazi ya kummaliza hakikisha Mdidi aamki hadi mauti yake”.
Mama Ashura akainamisha kichwa kutoa heshima zake kwa mkuu huyo na kuashiria kukubali kile alichoambiwa.
*******************
Ni asubuhi na mapema mama Ashura hakuwa na raha hata kidogo, akawaza jinsi gani ataanza kumwambia shoga yake kuhusu na dunia ile ya kichawi hili ajiunge waweze kupambana na Mdidi, alihofu Zaidi itakuaje endapo mama Salehe atagundua kuwa yeye ndiye aliyehusika na kifo cha Salehe na si mama Juma kama alivyodhani awali, akawaza Zaidi vipi itakuwa endapo atagundua yeye ndiye aliyechochea kifo cha upendo na vijana wale 10.
Baada ya muda mfupi mama Salehe akaenda kwa shoga yake mbio mbio, bila hata salamu akafika na kukaa kwenye kiti,
“Shoga yangu huko nilipotoka si kwema kabisaa!” alisema mama Salehe.
“Vipi Mdidi amefariki nini?”
“Bora angefariki, ningeshangilia”
“Ila ni nini sasa?”
“Huwezi amini shoga yangu Mdidi leo kaamka na kutembea anaweza kama vile hakuwa anaumwa”
“Mama Salehe kweli…!”
“Ndio shoga yangu”
“Mungu wangu nitafanyaje sasa”
“Kuhusu nini tena?”
“Mdidi hakutakiwa kuamka sasa”
“Unamaana gani?”
Swali lilikuwa gumu sana kwa mama Ashura akawaza jinsi gani aanze kumwambia kuhusu yeye kuingia katika ulimwengu wakichawi,
“Mama Salehe, itabidi nikupeleke kwa wataalamu Zaidi hili uweze kumdhibiti Mdidi”
“Kwanini tena! Mtaalamu si alisema Mdidi akiamka tuu ataanza zile tabia za Ushoga na kisasi changu ndio kitakuwa kimetimia”
“Mama Salehe umemdharau Mdidi sana, yeye pia ni mchawi kuliko, zile dawa hazikufanya kazi yeyote”
“Mhmhm! Wewe umejuaje?
“Mama Salehe umemdharau Mdidi sana, yeye pia ni mchawi kuliko, zile dawa hazikufanya kazi yeyote”
“Mhmhm! Wewe umejuaje?
Swali lilikuwa gumu sana kwa mama Ashura akawaza jinsi gani aanze kumwambia kuhusu yeye kuingia katika ulimwengu wakichawi,
“Mama Salehe, itabidi nikupeleke kwa wataalamu Zaidi hili uweze kumdhibiti Mdidi”
“Kwanini tena! Mtaalamu si alisema Mdidi akiamka tuu ataanza zile tabia za Ushoga na kisasi change ndio kitakuwa kimetimia”
“Mama Salehe umemdharau Mdidi sana, yeye pia ni mchawi kuliko, zile dawa hazikufanya kazi yeyote”
“Mhmhm! Wewe umejuaje?
“Shoga hatuna muda wa kupoteza Zaidi kwa maswali, hali si shwari kubaliana nami hili tuweze kumuangamiza kabisa Mdidi kabla mambo hayajaaribika”
“Sawa mimi nimekubali kwa iyo tutaenda saa ngapi?”
“Leo usiku”
“Usiku?”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo nitakupitia mimi usiku”
“Sasa tutaenda vipi usiku uoni kama ni hatari kwa usalama wetu, tunaweza tukavamiwa hata na vibaka”
“Mhmhm! Mama Salehe mbona mgumu hivyo kuelewa, hatutotumia usafiri wa kibinadamu”
“Sikuelewi ujue mama Ashura”
“Wewe niamini mimi shoga! Muda ukifika nitakupitia tutaenda zetu ila kwa sasa kuwa makini sana na Mdidi”
“Sawa shoga,” aliitikia mama Salehe japo hakuelewa lengo hasa la mama Ashura.
Afya ya Mdidi ikazidi kuimarika hatimaye kurudi katika hali ya kawaida, kwa namna ya pekee alijikuta akifarijika sana hasa baada ya dada yake kumpa habari juu ya watu wengi waliokuja kumjalia hali kipindi ambacho alikuwa hajitambui. Jioni ya siku iyo Mdidi akaamua kufanya mazoezi mepesi ya kutembea walau kwa wale wachache ambao waliweza kuja kumjulia hali mtu wa kwanza akawa ni Yahaya machipsi, alipofika tuu Yahaya alishangaa sana,
“Duuh! Wewe jamaa hufi leo wala kesho,” alisema Yahaya kwa mshangao sana.
“Na iwe kama ulivyotamka,” alijibu Mdidi.
“Ila jamaa uliumwa vibaya mpaka nikaanza kusikia harufu ya jeneza, kila ukiitwa hautiki, chakula hakipandi nikasema daah kweli wamekufanyia kitu mbaya”
“Kwa Mungu kila kitu kinawezekana kikubwa ni kuweka Imani yako kwako, hamna lolote baya la kutisha litakalokushinda, nilisimamia kweli na kweli hiyo ndiyo itakayefungua vifungo vya wengi katika mtaa huu”
“Aah! Ushaanza Falsafa zako nawee, karibu kwenye benchi kwanza nikupe walau viazi vya ofa leo”
“Hahahah! Sasa si nitakupa hasara”
“Hasara wapi ndugu yangu sadaka yenyewe sitoi, sasa nikikupa mtu kama wewe naamini mambo yangu yatakuwa shwari,” alisema Yahaya huku akiweka viazi kwenye sahani na kumkabidhi Mdidi.
“Vikolombwezo vingine jipimie mwenyewe”
“Asante sana ndugu yangu”
Mdidi akaanza kula huku akiendelea kupiga soga za hapa na pale na Yahaya, ukweli watu wengi hupenda sana kumsikiliza Mdidi akiongea mara nyingi huongea maneno yenye kujenga na kutia moyo sana. Amekuwa msaada mkubwa katika kukomboa fikra za wengi.
“Eeenh! Mdidi nimekumbuka!”
“Nini teena?”
“Kipindi unaumwa nilikuja kukuangalia siku moja nikakuta, mtoto mmoja mkali sana, yaani mzungu si mzungu, mwarabu si mwarabu, mswahili si mswahili kilichonichanganya Zaidi muda wote yeye mtu wa yes na no mara ok yaani zee zee nyingi, vipi ndiyo shemeji nini?”
“Mhmhmh! Wewe acha vituko sijui hata unamzungumzia yupi!”
“Duuuh! Braza uko vizuri inaonekana wale wanaoongea lugha ya weupe unao wengi hadi hujui yupi,” alisema Yahaya kiutani Zaidi.
“Sasa mimi katika hali ile ningetambuaje”
“Unamtambua sana, tena siku iyo alikuja na yule mzee nuksi”
“Aah! Wamzungumzia yule mjukuu wa mzee Kilonda! Yule ni rafiki yangu tuu”
“Rafiki wapi braza wee si useme tuu!”
Waliendelea kuzungumza kwa kirefu mno hadi jua likazama Zaidi na giza likashika nafasi yake. Mdidi akarudi nyumbani kujipumzisha.
**************************
Ni saa 6:00 usiku mama Salehe akiwa amepitiwa na usingizi ghafla anashtushwa na kundi la watu wapatao watano walioingia chumbani kwake huku wakiwa watupu na nyuso zao zikiwa zimepakwa kitu cheupe mithili ya poda. Mama Salehe akaogopa sana, hakashindwa kuelewa alikuwa ndotoni au ni kitu ambacho anakishuhudia katika ufahamu wake wa kawaida.
“Mama Salehe muda unakimbia mno, nyanyuka twende,” aliongea mwanamama mmoja.
“Mbo-na- si-e-le-wi!,” alijibu huku hofu kubwa ikimtawala.
“Hahahaha! Shoga umesahau kile tulichokubaliana mchana?” yule mama akajibu.
Daah! Mama Salehe kutazama vizuri ndiyo akaja kutambua kuwa alikuwa anaongea na shoga yake kipenzi mama ashura, hakuamini kile alichokishuhudia moyoni alizidi kuomba mungu hii iendelee kuwa ndoto na akiamka asahau kila kitu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Leo ni siku rasmi ya kukukaribisha katika chama chetu, kwani kwa muda mrefu umekuwa mshirika wetu, umefanya vingi kama tulivyokuwa tukivifanya sisi na umetumia nguvu ulizopewa na mkuu kama tulivyotumia sisi,” alisema mama Ashura.
“Nini! Yaani mama Ashura kumbe wewe ni mcha…..” kabla hajamalizia kusema akajikuta akinyanyuka kitandani na kumfata mama Ashura kisha kwa pamoja wakasogea hadi katika pembe ya kushoto ya chumba wakainama na kutoweka.
Wakatokea katika eneo ambalo mama Salehe hakulifahamu, akabaki katika hali ya mshangao huku akili yake ikikataa kuamini kwamba yale ayaonayo ni ukweli mtupu. Akajipa moyo kwamba ikifika asubuhi ataamka na yote yale atayasahau.
“Safi sana mama Salehe kwa kutuletea pacha wako,” mkuu wa dunia ya kichawi alimpongeza mama Salehe baada ya watu wote kufika na kukaa katika sehemu zao.
“Ndugu zangu leo tunakwenda kumuadhibu vilivyo Tukae khamisi ambaye alidiriki kusema uongo na kutoifanya vilivyo kazi yake”
Watu wote wakainamisha vichwa vyao kwa utii kabisa, Tukae akasogea sehemu ya mbele upande wa kushoto.
“Jamani huyu atakuwa chakula chetu siku ya mwezi mpevu, ila usiku huu wa leo hatoweza kurudi katika dunia ya kawaida na mama Ashura utahusika kusababisha kifo chake kwakuwa umepanda cheo sasa,” alisema mkuu yule huku macho yake yaking’aa mithiri ya paka.
Mama Ashura akanyanyuka sehemu aliyokaa na watu wote wakaanza kuimba na kucheza nyimbo ambazo hazikuwa rahisi kueleweka masikioni mwa mtu yeyote ambaye angepata bahati ya kusikia. Akasogea hadi alipo Tukae kisha akamtazama na papo hapo macho ya mama Ashura yakabadirika na kuwa mekundu kama yamevilia damu. Taratibu Tukae akaanza kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu. Baada ya zoezi hilo watu wote walifurahi na kuzunguka moto ambao katikati kulikuwa na vipande vya nyama vikichomwa.
“Sasa ni wakati wa kumkaribisha mgeni kwa kumpa Mvinyo na mkate wa dunia yetu,” alisema yule mkuu ambaye sura yake haikuonekana vizuri.
Mama Ashura akatoka alipokuwa na kumfata mama Salehe, hofu kuu ilimtanda mwanamama yule hakuwahi kumuona shoga yake akiwa katika hali ya kutisha kama ile,
“Mama Ashura! Mimi si-nywi po-mbe, sitaki mvi-nyo wenu,” alisema mama Salehe huku akitetemeka mwili mzima.
“Hahahahahahahahaha!,” mama Ashura alitoa kicheko kikali kilichomtisha Zaidi mama Salehe na watu wote wakaanza kucheka kama mama Ashura alivyofanya.
“Si umeona adhabu aliyopewa mwenzio sasa jitie kiburi uone,” alisema mama Ashura kwa ukali Zaidi.
Mama Salehe hakuwa na ujanja ikamlazimu atii kila alichoambiwa, ikafika wakati wa kunywa mvinyo na mkate. Hakuamini macho yake alipokabidhiwa kibuyu kilichokuwa na damu na kipande cha nyama ya binadamu.
“Aaah! Mama Ashura hii si ni damu ya mtu!” alisema mama Salehe kwa mshangao.
Kauli ile ikamkela sana mama Ashura akanyanyua mkono wake na akakunja ngumi mfano wa kukiminya kitu kwa mkono, hapo hapo mama Salehe akahisi kukabwa koo, macho yakaanza kutoka huku akikohoa kwa mfululizo. Mama Ashura aliporidhika na adhabu aliyompa shoga yake akaachia mkono na bila shuruti mama Salehe akainywa ile damu na kula kile kipande cha nyama. Watu wakampongeza kwa kumpigia makofi.
“Kazi yako ya sasa ni kushirikiana na mama Ashura katika kutokomeza kile kikwazo kilichopo katika kitongoji chenu”
“Kikwazo kipi?” akauliza mama Salehe.
“Mdidi”
Asubuhi nyingine tena iliyotawaliwa na hali ya utulivu kabisa, huku watu wengi wakizidi kuishangaa nyumba ya mzee Kobelo kuwa na hali ya utulivu kiasi kile. Mdidi akaamka na kuanza kufanya usafi wa nyumba na ndani ya muda mfupi akawa amemaliza kufagia na kudeki sehemu ya uwani na chooni, baada ya kumaliza akaingia kuoga wakati anatoka akakutana uso kwa uso na mama Salehe ambaye naye kwa muda huo alitoka kuamka. Mama Salehe alipomuona Mdidi akashtuka sana, akahisi aibu na kutazama chini. Mdidi hakulijali ilo akasogea na kumsalimia.
“Shikamoo mama Salehe!”
“Kua upate yako! Mfyuuuu!”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwani ni dhambi mimi kukusabahi mama”
“Mtoto mdogo kutaka kushindana na wakubwa, tutaona mwisho wake”
“Mhmhm! Mbona sielewi unachokizungumza”
“Utaelewa siku ya mwisho, nyooooooo!” alisema mama Salehe na kurudi chumbani kwake.
Mdidi akafikiri kidogo kisha akaamue aendelee na mambo yake, hakuhitaji kuumiza akili kwa mtu kama yule.
*******************
Mama Salehe akaa kitandani na kuanza kufikiri yale yaliyotokea usiku uliopita, hakuwa na uhakika kama ilikuwa ndoto au kweli.
“Mhmhmh! Inamaana kweli ndio nimeshakuwa mchawi au ilikuwa ndoto tuu ile, daah! Kweli shoga yangu naye ni mchawi tena mwenye cheo kikubwa. Aah Siamini!”
Wakati akiendelea kuwaza hayo mara akasikia mtu anabisha hodi mlangoni pake, alipofungua akakuta ni shoga yake mama Ashura,
“Za muda shoga yangu!”
“Mhmhm! Mama Ashura kwani mimi na wewe toka jana tumeonana?” aliuliza mama Salehe ilia pate uhakika kama yale aliyoyaona yalikuwa ndotoni au la.
“Shoga! Sijayajia hayo, nimekuja kwa lengo moja tuu la kuifanya ile kazi tulioagizwa jana”
“Nini..! ina maana kweli nimeshakuwa mchawi”
“Sasa shoga kuna kipi cha kushangaa ushirikina uliuanza kitambo toka enzi za mama Juma, ukamuua na Upendo leo unashangaa nini wewe mchawi”
“Umeniingiza pabaya mama Ashura, ulijifanya rafiki mwema kumbe ulikuwa unanihadaa niingie katika ushetani wenu”
“Mama Salehe umekosea sana leo na utajuta, hata siku moja uwezi ukatukana chama na ukaachwa hivi hivi”
“Mtanifanya nini? Mtaniua au mtanila nyama kama Tukae?” mama Salehe alijikuta akiwaka kwa hasira na kumtoa mama Ashura nje.
“Mama Salehe chunga mdomo wako nakuheshimu sana ujue usitake nikuabishe hapa”
“Huna cha kuniaibisha wewe baradhuli mkubwa! Mfyuuu nilikuona mwema sana mama Ashura kumbe ni chui. Sasa sikia mimi sitaki tena ushoga na wewe naomba uniache fanya mambo yako”
“Mama Salehe umesahau kama ulishaingia agano! Nakuhurumia sana shoga yangu”
“Huna haja ya kunihurumia shetani wewe! Umenifanya nijenge chuki kwa watu wasio na hatia,” aliongea mama Salehe kwa hasira sana.
Mama Ashura alivyoona mama Salehe anaendelea kuropoka na watu washaanza kusogea eneo la tukio kushuhudia kile ambacho mashosti hao wa muda mrefu wanagombania, ikabidi aanze kucheka sana,
“Huhuhuhu! Tumewaweza mtaa huu kwa kupenda ubuyu mfyuuu,” alisema mama Ashura.
“Sio ubuyu ila nakwambia kweli shoga yangu sikutegemea kama wewe mcha…….” Mama Salehe alijikuta akisita kuendelea kuongea hasa baada ya kuona majirani wengi wamejaa.
“Hahahahahah! Msiopenda ujinga leo kulikoni”
“Wanajifanya wanapendana na kugandana kama kupe leo kushinei”
“Mwaga mchele mama Salehe tumeyamiss mambo yako”
Zilikuwa kauli za majirani na watu wengine waliofika eneo hilo kushuhudia ugomvi wa marafiki hao ambao walishibana na kuwa kama ndugu.
“Tumeshawateka akili mazezeta ya mtaa tuendelee na shughuli zetu shoga yangu,” alisema mama Ashura.
“Aah! Kumbe mlikuwa mnatafuta kiki”
“Khaaa! Mmetuweza walah!”
“Hatupendi ujinga sisi,” alijibu mama Ashura huku akishika njia ya kurudi kwake moyoni akiwa na ghazabu kuu juu ya shoga yake hakujua afanye nini kwani akizembea anaweza jikuta naye akiingia kwenye adhabu kama ya Tukae.
Kila mtu alierejea kwake huku mama Salehe akibaki katika hali ya hofu kwani alishauona uwezo mkubwa wa shoga yake kwenye mambo ya kichawi. Alihisi lolote laweza kutokea na hata maisha yake yanaweza kupotea kabisa.
“Mama Ashura nakutangazia vita rasmi mimi ni mwanamke wa kidigo nimezaliwa Tanga nimekulia Tanga, hamtoniweza kwa lolote lile mfyuuuu!” alisema mama Salehe na kuingia ndani.
Wakati akiwa ndani ghafla akaanza kuhisi maumivu ya kichwa, kizunguzungu kikafata akaona moshi mkubwa ukifuka ndani ya chumba chake na ndani ya dakika chache mama Ashura akatokea,
“Kimaneno sikuwezi ila kivitendo hunipati,” alisema mama Ashura.
“Unataka kufanya nini?” alijibu mama Salehe huku akishika kichwa ambacho kinamuuama.
“Hii ni rasha rasha mvua inakuja”
Mama Ashura akakunja mkono wake akawa kama anaminya kitu apo apo mama Salehe akahisi kama anakabwa koo, pumzi ikawa ndogo kwake akahisi macho yanakuwa mazito.
“Ni-u-e tuu! Sistahili kubaki duniani,” alisema mama Salehe.
“Kufa haufi ila cha moto utakiona”
“Hu-hu-hu-hu! Niue maana utaijutia hii siku kama utaniacha nikiwa napumua,” alisema mama Salehe kwa kiburi mno.
Mama Ashura akazidisha kuuminya mkono wake na papo hapo mama Salehe akaanza kukohoa damu. Akafanya hivyo kwa muda kama wa dakika tano kisha akauachia na mama Salehe akatulia.
“Hii inakutosha kwa matusi uliyonitolea, sasa tuungane tumuangamize Mdidi,” alisema mama Ashura.
“Ni-me-kwambia niu-e si-ko tayari kufanya ushetani huo”
Kauli ile ilimghadhabisha sana mama Ashura akajikuta akifanya maamuzi magumu ya kumuua kabisa mama Salehe lakini kabla hajalikamilisha ilo akasikia mlango wa mama Salehe ukigongwa. Akasonya kisha akatoweka.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mlango uliendelea kugongwa kwa muda bila majibu, ndipo yule aliyeugonga alipoamua kuingia ndani. Alijikuta akipiga kelele hasa baaada ya kukuta hali ya mama Salehe ikiwa mbaya. Alikuwa ni Nasra mdogo wake na mama Salehe ambaye aliamua kuja kumtembelea dada yake na kwa bahati mbaya akamkuta katika hali hiyo. Kelele zile zikawafanya wapangaji wengine watoke na kuja kuangalia kilichojili, kila mmoja alishangaa sana kwani muda mfupi uliopita mama Salehe alikuwa mzima na hakuwa na dalili yeyote ya ugonjwa. Mdidi akiwa miongoni mwa wapangaji walioenda kutoa msaada kwa mama Salehe akawahimiza wenzake wamuwaishe hospitali na wote wakakubaliana na wazo hilo lakini kabla hawajamtoa chumbani kwake, shoga yake mama Ashura akawa amefika,
“Jamani shoga yangu nini kimekukuta mboni ulikuwa mzima muda si mrefu,” alilalama mama Ashura huku akioneshwa kuumizwa Zaidi na hali ya mama Salehe.
“Tumuwaishe hospitali bajaji imeshafika,” alisema Mdidi.
“Sawa tusaidiane basi kumbeba,” mpangaji mwingine alishauri.
Mdidi akawa wa kwanza kumbeba mama Salehe huku akishirikiana na wengine hadi ilipo bajaji, kisha akaingia na kumhimiza dereva aongeze mwendo ili wawahi kufika hospitali. Hamna mtu aliyejitokeza kuongozana na Mdidi hospitali wengi walichoshwa na tabia za mama Salehe hivyo kuugua kwake ghafla ilikuwa taarifa njema kwao. Mdidi akawastaajabisha wengi kwani ni mengi maovu aliyofanyiwa na mama Salehe lakini hakujali hayo na akawa mstari wa mbele katika kuhakikisha mwanamama yule anakuwa salama.
Wakafika hospitali na kila aliyemuona mama Salehe alimuonea huruma hivyo akapewa kipaumbele, hakukaa foleni akaingia moja kwa moja kwa daktari. Daktari alivyomuona tuu alishtuka sana kwani damu zilikuwa zikivuja masikioni na nyingine puani akahisi uenda mshipa wa damu umepasuka. Ikabidi kwa haraka amuandikie kisha apelekwe mahabara kwa ajili ya vipimo.
“Kweli rafiki utamjua siku ya dhiki, mhmhmh kujifanya ooh! Shoga yangu kila sehemu tupo wote leo kapata tatizo hata kumsindikiza hospitali kashindwa,” alisema mama Chande ambaye anaishi jirani na nyumba ya mzee Kobelo ambapo mama Salehe na Mdidi wamepanga.
“Ubinadamu kazi shogaa! Wanacheka usoni ukiwapa kisogo wanakung’ong’a,” aliitikia Asha ambaye pia anaishi nyumba moja na Mdidi.
Baada ya kusubili kwa muda majibu yakatoka na Mdidi akaitwa chumba cha daktari, akaingia na kukaa kwenye kiti kilichopo pembeni. Kisha daktari akakohoa kidogo kulegeza koo lake na kuanza kuongea.
“Sasa bwana Mdidi, vipimo vinaonesha kuwa mgonjwa hana ugonjwa wowote ule, isipokuwa alipata mshtuko kidogo na kufanya presha ipande na hii ndio ikasababisha hadi atokwe na damu puani na masikioni. Japo mara ya kwanza nilikuwa na hofu kuwa uenda mshipa wa damu umepasuka ila Mungu bado yupo upande wake, mshipa uko salama kabisa”
“Kwa hiyo dokta mgonjwa atakuwa sawa?”
“Yeah! Ondoa wasiwasi kabisa jitihada za makusudi zimekwisha fanyika na kwa sasa tutamuweka mapumziko hili kuruhusu dawa zifanye kazi vizuri na tutamuangalia hadi jioni hali ikiwa sawa tutamruhusu arudi nyumbani ila kikubwa mgonjwa hatakiwi kupata taarifa za kumshtua kwa hivi sasa”.
“Sawa daktari nimekuelewa na nashukuru sana kwa msaada wako”
“Usijali ni wajibu wangu”
Mdidi akatoka chumba cha daktari na kuelekea kwenye mabenchi yaliyo eneo hilo la hospitali kisha akakaa huku akiendelea kutafakari juu ya matukio yale yanayotokea katika nyumba ile na mtaa kwa ujumla.
Taarifa za kuugua kwa mama Salehe zikasambaa kwa haraka mno lakini hamna hata jirani mmoja aliyejitokeza kuja kumuona. Mdidi alifanya jitihada za kumtafuta baba Salehe ambaye aliamua kuachana na mkewe huyo miezi kadhaa iliyopita kutokana na tabia zake mbovu lakini hakufanikiwa kumpata kwani hata namba zake hazikupatikana.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mdidi dada anakuita,” alisema Nasra ambaye alikuja hospitali muda mfupi baada ya Mdidi kumuwahisha hospitali mama Salehe.
“Vipi hali yake! Ameamka na je ana nguvu?” aliuliza mfululizo.
“Twende ukamsikilize,” alijibu Nasra.
Wakati wakiongozana kuelekea sehemu alipo mama Salehe wakakutana na mama Juma, Nasra hakuamini hata kidogo kumuona mwanamke yule eneo lile.
“Poleni na kuuguza jamani,” alisema mama Juma baada ya kutoa salamu.
“Akhsante! Karibu” alijibu Nasra.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment