Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

UPENDO WANGU - 1

 







    IMEANDIKWA NA : TATU KIONDO



    *********************************************************************************





    Simulizi : Upendo Wangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa jumatatu moja tulivu majira ya jioni, mzee rashidi akiwa sebuleni na familia yake wakipata vinywaji huku wakiwa wanaangalia televisheni iliyokuwa pale ukutani upande wa kushoto mwa nyumba ile ya kifahari!



    Mzee Rashidi kingstone  ni mtu tajiri sana mjini Arusha ni mtu mwenye kumiliki Kampuni mbalimbali na nyumba za kifahari ndani na nje ya nchi, pia kumiliki vituo mbalimbali vya watoto yatima. Nje ya utajiri wake , Mzee Rashid ni baba wa watoto wawili wa kike, aliyozaa na wanawake tofauti, mkubwa ni Semeni ambae hajazoeleka sana mjini arusha hata mtaani kwao hapendi  kuzungumza na watu akiwa kwa baba yake,pia hana maelewano mazuri na mama yake wa kufikia hivyo mzee rashid akaamua kumrudisha kwa mama yake mzazi huko palaka kisarawe mkoa wa pwani. Hivyo sababu muda mrefu sana, miaka mingi aliishi  kwa mama yake ambaye mtalaka wa Mzee Rashidi walitalakiana sababu ya tabia isiyoeleweka ya mzee huyo kutokuwa mwaminifu. baadae alioa mwanamke mwingine  anayeitwa Bi moza ndiye aliyenaye mpaka sasa. Katika maisha yao ya ndoa mzee rashidi na bi moza wamejaaliwa mtoto mmoja ambaye ndie mtoto wake wa  pili anayeitwa Amina, Amina ni  mdogo wa Semeni japo tumbo tofauti lakini wao  wanapendana sana , Amina alikuwa ni mtoto kama nembo ya familia sababu ndie anaishi na wazazi wake yaani baba yake na mama yake pamoja.

    Siku nyingi Mzee Rashidi alijulikana kama ni mtu mwenye heshima zake sababu ya ucheshi na ukalimu wake kwa ndugu jamaa na marafiki zake, japo alikua tajiri ila ni mtu aliejihusisha na biashara haramu, alikua mmoja wa kiongozi kwa vijana wanaojiusisha na biashara haramu ya kuuza na kusambambaza madawa ya kulevya ndani na nje ya nchini, alifanya biashara yake kwa usiri mkubwa sana bila kujulikana.

     Mzee Rashidi alikua na vijana watatu  anaowatumia kwenye kazi  zake za kusambaza madawa hayo kwa siri,katika vijana hao mmoja wapo alikuwa kama msimamizi wake katika kazi hiyo aitwaye Yohana, Kijana yohana alikua ni mtu wake wa karibu hakuna jambo la mzee rashid bila kumshirikisha yohana, ukaribu wao yapata miaka mitatu sasa wapo pamoja kwenye kazi hiyo, Yohana alijulikana sana  nyumbani kwa Mzee Rashidi alikuwa na mazoea ya kutaniana na kila mtu nyumbani hapo na aliishi kama mtoto wa Mzee Rashidi.

    Siku mmoja Mzee Rashidi alikuwa amekaa na familia yake sebuleni yohana pia alikuwepo, ilikuwa sebule kubwa iliyonakshiwa kwa rangi ya kijani yenye kila thamani inayojulikana pale sebleni pembeni yake kulikuwa na meza kubwa iliyojaa vinywaji vikali.

    Huku mziki mkubwa ukiwaburudisha, Gafla mzee rashid alimwambia,

    "Yohana punguza sauti"

    "Sawa bosi!

    Yohana alinyanyuka na kuelekea sehemu ilipo meza ya radio ile akazima kabisa

    " bora ulivyozima kabisa najiisikia kuumwa leo

    " unajisikiaje mzee wangu" yohana alimuuliza mzee rashidi.

    " Nina jambo zito sana linanitatiza" mzee rashidi alimjibu yahana.

    " niambie mzee wangu labda naweza kukusaidia" yohana aliinuka akipokua amekaa na kumsogelea mzee rashidi alipokaa,

    "Kuna jambo naomba unisaidie yohana.................

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mzee rashid Aliamua kumuomba Yohana na kumtaka ampe ushauri wafanye nini kwani kuna kazi ambazo zilimchanganya. alizofanya na wahusika wenzake iliyohusika na mzigo ule aliowatuma. mzee Rashid akamtaka yohana amsimulie ilivyokuwa ili ajue jinsi gani atampata huyo mtu aliyetumwa kuufikisha kwake mzigo huo .ikabidi amwambie ilivyokuwa kwani yeye hajui chochote kinachoendelea,

    Mzee rashid na wenzake wamejikuta wapo kwenye matatizo makubwa kwani kuna uwezekano Mkubwa kukamatwa sababu ya mtu kupotea na mzigo ule. Wakati mzee rashidi anaongea yohana alikaa kimya kumsikilza bosi wake kwa makini.mzee rashid alipomaliza kuongea uku akimwangalia yohana.Yohana alishusha pumzi ndefu huku akiwaza jinsi gani atampata muhusika aliyetoloka na kupotea na mzigo ule.



    Ilikuwa siku ya jumapili majira ya jioni tulivu katika mtaa wa chasimba kulikuwa na nyumba mmoja ya matofali ya kuchoma ni nyumba ya kupangisha wapangaji ni nyumba mbovu mbovu ilijulikana kama jumba la maisha plus sababu ilijengwa kwa mtindo wa kipekee.

    yohana kilale ndio jina lake halisi kama yeye anavyopenda kuitwa, ndio alilopewa na wazazi wake, pia katika nyumba hiyo yahana alipanga chumba kimoja kikiwa na sebule ndogo, sebule ile ikiwa na thamani chache zinazovutia.

    ikiwa imetimia saa kumi na moja za jioni yohana amepumzika chumbani kwake akiwa ameshikilia simu yake ndogo aina ya nokia huku akibofya vitufe vya simu ile, yohana alikumbuka kitu aliamua kuwapigia simu wenzake ili wakutana.

    baadaye walikubaliana kukutana ubungo mataa ili kuelekea uwanja wa ndege, kupokea mzigo waliotumwa na mzee wao. katika upande wa watendaji yeye yohana na wenzake walihusika kupokea mzigo unaotoka nchini congo kuja Tanzania. Baada ya makubaliano na wenzake yohana alijiandaa na kutoka kuelekea ubungo kukutana na wenzake. Baada ya nusu saa walikutana,yohana akawapakia wenzake kwenye gari alilopewa na mzee rashidi kwa kazi hiyo. Ilipotimia mishale ya saa moja jioni yohana na wenzake waliwasili uwanja wa ndege yohana aliegesha gari pembeni na wenzake kuteremka garini na kuelekea sehemu ya  kupokelea wageni.

    Walikaa na kumsubili mgeni wao,walisubili sana bila mafanikio

    baadaye wakachoka ila wakaendelea kumsubiri, alichanganyikiwa zaidi walipowaona abiria wengine bila kumuona muhusika waliyeagizwa kukutana nae ili awapatie mzigo huo. Walisubiria bila mafanikio, waliamua kumpigia simu lakini hakupatikana hewani, ikabidi yohana kuwataka  wenzake wakaongee pembeni, yohana aliwaambia wenzake

     "sasa tutamwambia nini mzee maana mtu mwenyewe hatumuoni ! Mwenzake alimjibu,

    "Mimi hata sijui itakuwaje? Mwengine akadakia,

    "Mzee anaweza akajua sisi tumemuibia kumbe sio!" Yohana akawajibu,

    " kweli kabisa yaani mzee hatatuelewa kabisa

    "Kwa hiyo tufanye nini jamani?

    "Mi naona tumwambie kama ilivyokuwa tu !

    " sawa tumwambieni ukweli tu.

    Baada ya maongezi hayo yohana na wenzake walikubaliana kumueleza mzee rashidi hali halisi ilivyokua.nao hawakua na maamuzi waliochukua zaidi ya kukubaliana kukwambia mzee rashidi ukweli...............



              Baada ya kusubili bila mafanikio hatimaye yohana na wenzake wakaamua kurudi majumbani mwao,uku wakimjulisha kwa njia ya mawasiliano bosi wao.

    Sasa siku hiyo mzee rashid alitaka kujua jinsi ilivyokuwa mpaka wakamkosa huyo muhusika wa mzigo huo.baada ya kutafakari kwa muda yohana alimueleza kila kitu jinsi ilivyokuwa walivyofatilia abilia wote walioshuka katika ndege hiyo bila mafanikio, na kumueleza mpaka wana usalama wa uwanjani pale walivyokuwa na mashaka nao mzee rashidi alichoka zaidi kwani alishajua tayari amepoteza mzigo.

            Mzee Rashidi alikubaliana na Yohana na kumwambia, hakuwa na njia ya kufanya wakati ule kwani yote watamalizana na wenzake. Yohana na bosi wake wakiwa katika mazungumzo ara simu ya Mzee Rashidi ikaita,aliiangali kisha akaipokea na kuiweka sikioni.wakati mzee rashidi akiipokea simu ile   alionekana kuongea kwa upole uku akiwa mtu mwenye wasiwasi mkubwa,yote hayo alijua fika kama mambo yameshaiva uko.mzee rashid  alipomaliza kuongea alimgeukia na  kumwambia Yohana

    "wakubwa wanataka tukutane usiku"

    " sawa bosi" yohana alimjibu bosi wake"

    Mzee rashidi alijiinamia na kumwambia yohana

    " lakini sijui  kama watanielewa wale,mzee rashidi aliongea maneno mfululizo

    " twende tu mzee tutajua cha kufanya uko.yohana alimjibu bosi wake na kumtaka ajiandae kwani muda umeshaienda wakati huo ilikuwa yapata kufikia saa mbili za usiku.

    Mzee rashidi alijiandaa alipomaliza kumtaka yohana waondoke, mzee rashidi alimkabidhi yohana funguo ya gari kisha yohana akaielekea gari mojawapo kisha wakajipakia na kuondoka kuelekea hotel ya syret iliyopo mita chache kutoka nyumbani kwa mzee rashidi. Baada ya ya mwendo wa talatibu kama nusu saa hivi walifika katika hotel ya syret walipotakiwa kukutana na wanzake, Mzee Rashidi aliingia ndani aliwakuta  wakubwa na mabosi wezie na Yohana alibaki nje na vijana wenzake.

         Mzee Rashidi alikuwa kiongozi katika mkutano ule lakini wenzie walimlaumu kwa kusababisha hali ile na kumtaka awalipe fidia sababu alitia hasara na kusababisha wengine kupoteza pesa nyingi kwa mzigo ule,Mzee Rashidi alilaumiwa sana  na wenzake na kumtaka awalipe pesa zao kisha ajitoe uongozi kama hawezi kusimamia kazi hiyo kuuza na kusambaza madawa ya kulevya la sivyo watamgeuka,Mzee Rashidi aliupinga uwamzi huo nakutaka wampatie mda mfupi wa kuwalipa pesa zao wote na kufuatilia mzigo uliopotea. Mzee Rashidi alijitetea na kuwaambia walipata hasara wote ata yeye pia alilipia pesa nyingi kuufanikisha mzigi huo.wenzake walimwambia ajalibu kumpigia simu king aliyemtuma kijana ambaye amepotea katika mazingira ya kutatanisha sana lakini yeye alitaka wamuache atalifuatilia mwenyewe ila wampe muda wa kuwalipa.

           Siku hiyo hakuna hata mtu mmoja mule ndani aliyesikiliza maongezi ya mzee rashidi, wakati huo kila mtu alikuwa anafikilia pesa zake tu hakuna kingine Wanachokitaka kutoka kwake, kwani walishalipia pesa kabisa wao walichokuwa wanakiitaji mzigo ufike na wagawane basi, ila yote hayo yalishindikana Kutokana mzigo kupotea.baada ya kuelewana hawakuwa na jinsi wakaamua kumsamehe mzee rashidi na kumwambia watamvumilia na kumpa muda wa mwezi mmoja  ili afuatilie mizigo iliyopote uwanja Wa ndege. waliagana na kila mmoja kuondoka kivyake,mzee rashidi alipotoka nje alimkuta yohana ameshaingi ndani ya gari ameketi nyuma ya usukani ikimsubili.mzee rashidi nae alijipakia na kumtaka yohana aendeshe kwa spidi kubwa mara moja safari ya kuelekea nyumbani ikaanza.baada ya mwendo wa kasi walitumia kama dakika ishirini kufika nyumbani kwa mzee rashidi,safar hii yohana alimuomba mzee rashidi akifika nyumbani amuache ila yeye aende na gari ile nyumbani kwake, mzee rashid hakuwa na pingamizi kwani alishazoea muda mwingi kumuachia yohana gari ili afanyie safar zake kisha urudisha nyumbani kwake.hivyo ndivyo ilivyokua,walipofika mzee rashidi alishuka na kuingia ndani,muda huo yohana aligeuza gari na kufuata balabala inayoelekea nyumbani kwake mtaa Wa Yombo..........

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ilikuwa yafikia saa sita za usiku,wakati huo mzee rashidi aliwasili nyumbani na kumuacha yohana akiendelea na safari ya kurudi kwake. Uku mzee rashidi akipofungua geti na mlinzi aliingia ndani moja kwa moja mpaka chumbani kwake, alimkuta mkewe ameshalala, aliamua kwenda kujimwagia maji ili kuondoa uchovu wa hali hile aliyekua nayo.alifuata kabati kisha alibadili nguo alizokua amevaa na kuchukua taulo kuelekea maliwatoni,baada ya dakika kadhaa alitoka na kuelekea kitandani ili kuungana na mkewe,mzee rashidi alipanda kitandani uku akimkumbatia mkwe na kumbusu mkewe nae alipomuona mumewe akimkumbatia alitoa ushirikiano,baada ya purukushani za hapa na pale, kila mmoja akapitiwa na usingizi .

    Ilikuwa yapata saa kumi na mbili za asubuhi, mzee rashid akiwa bado pale kitandani, alisikika honi kubwa ya gari nje ya nyumba yake ,mzee rashidi alikukurupuka gafla uku akitweta midhili ya mtu aliyekimbizwa na simba polini, alisogelea dirisha na kufungua panzia ili ahangalie nje na kujiuliza ninani anayekuja muda huo nyumbani kwangu?,akawa anajiuliza mwenyewe pale kitandani ,mzee rashid akiwa pale dirishani alimshuhudia kijana akishuka gar7ini na kuanza kugonga mlango mkubwa geti la kuingilia nyumbani kwake. Nyumba ya mzee rashid ilijengwa kwa mtindo wa kisasa iyolikuwa na vyumba vitatu na sebule kubwa iliyopendeza kwa thamani za kisasa zilizopangwa kwa mtindo wa kipekee, nje kukiwa na ukuta mlefu uliozungushiwa nyaya maalum kwa usalama wa nyumba ile.

    Mzee rashidi alipomuona yule kijana alimtambua mara moja kuwa ni kijana wake manase,alijifikilia na kujiuliza maswali kibao kuhusu ujio wa kijana yule, bila kupata majibu mwishowe aliamua kutoka na kwenda kumsikiliza kijana yule. manase ni mtoto wa rafiki yake mzee rashid anayeitwa mubarak,huyu mzee upendelea sana kumtuma mwanae kwa mzee rashidi kumpa taarifa au mzigo aliotumwa na baba yake. Siku hiyo mzee rashidi akajua hapa kuna kitu maana sio kawaida kwa muda huu manase kufika nyumbani kwake tena akiwa na gari.mzee rashidi aliamka na kuelekea maliwatoni kujiswafi,alipotoka alijiandaa na kutoka kueleke sebuleni, ambapo alimkuta manase anamsubili kwani mkewe alishampatia taariza za ugeni ule.mzee rashid alimsabahi manase na alisogea karibu kabisa na kiti alichokaa manase na kuanzisha mazungumzo ,

    " haya niambie kijana, habar za ulipotoka?"

    " salama tu mzee wangu" manase alimjibu ,

    " vipi kuna kipya kilichotoke "mzee rashid aliendelea uku akimsikiliza kwa making

    " ni njema kwamba baba amepokea simu kutoka kwa king!

    " unasema kweli kijana? Mzee rashid hakuamini anachokisikia"

    " ndio hivyo mzee amenituma nije kukupa taarifa mzigo haujapotea kama mnavyofikili!

    " aisee! Kumbe uko wapi kijana?" Mzee rashidi aliendea kuuliza maswali mfululizo, uku akiwa na shauku ya kutaka kujua ulipo mzigo"

    " king amesema mzigo haujapotea kwani kijana aliyemtuma alipata matatizo makubwa njiani! Manase alimjibu kwa kifupi "

    "Kwa hiyo mzigo umefikia wapi kwa sasa maana kila nikimpigia king simu yake haipo hewani!

    " ndio anesema simu alizima kutokana na kijana wake aliyemtuma kupata matatizo"

    " sawa nimekuelewa manase " mzee rashid alimjibu huku akitabasamu.

    " sasa nimetumwa nije nikupe taarifa kwamba mzigo unawasili leo saa nane mchana hivyo mjiandae kumpokea, anakuja nao yeye mwenyewe kingi akitokea kinshasa.

    Baada ya kumjulisha mzee rashid jinsi alivyotumwa na baba yake ,manase aliaga na kuondoka.uku nyuma alimuacha mzee rashidi akiwa na amani ndani ya moyo uku akimshukuru mungu wake kwa kumnusuru kwa fedheha hile iliyompata usiku uliopita.mzee rashidi aliinuka na kuiendea meza iliyokuwa pembeni pale sebuleni uku akijisemea moyoni ama kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa giza,uku akivuta kiti na kukaa tayari kwa kupata kifungua kinywa..........



    Siku hiyo mzee rashid hakutoka kabisa nyumbani,alikaa tu nyumbani akisubilia muda ufike ili wakutanane na mwenzake, akiwa anatafakari jinsi ya kuupokea mzigo huo,mara yohana nae alifika nyumbani pale kwa mzee rashid. Alipongia ndani alimkuta bosi wake akiwa mtu mwenye mawazo sana,yohana alimsabahi na kukaa kwenye sofa lililokuwa karibu na mzee rashid.baada ya salamu mzee rashidi alimueleza yohana jinsi hali ilivyokuwa na hapo alipo anasubili muda ufike waende uwanja wa ndege kuupokea mzigo wao,yohana hakua na jinsi alikubaliana na bosi wake kwa safari.

    ilipofika saa nane na dakika zake mchana mzee rashid alijiandaa kisha alimtaka yohana waondoke, kuelekea uwanja wa ndege ili kuupokea mzigo ambao wao walijua umepotea.

    Baada ya mwendo wa nusu saa waliwasili uwanjani hapo na kuwakuta baadhi ya marafiki zake mzee rashidi wameshafika,miongoni mwao akiwepo mzee mubaraka au kwa jina wanamkatisha muba, ambaye ndiye aliyemtuma mwanae akamjulishe mzee rashid kupatikana kwa mzigo huo.walisalimiana kisha akaungana nao kumsubili mgeni huyo.

    Baada ya muda mchache kupita tangu walipifika, mzee rashid akiwa amekaa na wenzake sehemu maalum ya kusubilia wageni,Mara moja wakaiona ndege ikiwasili.ilikuwa ndege ya shirika la ndege emirate,baada ya muda ndege kutua, abilia wakashuka kutoka kwenye ndege hiyo, alishuka abilia mmoja baada ya mwingine uku macho ya mzee rashidi na mwenzake yakiwa kwenye mlango wa ndege hiyo,mara wakamuona kijana mfupi mwenye milaba minne akishuka kutoka kwenye ndege ile,akiwa na begi kubwa mgongoni mwake mwake.

    Baada ya kushuka kijana yule akawa anaangaza macho yake uku na kule kama mtu aliyekua anatafuta kitu,mzee rashidi akili ikacheza fasta na kumtaka yohana amfuate yule kijana,yohana akafanya alivyoagizwa na bosi wake.kwa kua mtu aliyekuja na mzigo ule hawakumfahamu ndio maana mzee rashidi akaamua kumfuatilia.

    Yohana àlimsogelea yule kijana na kumsabahi

    " habari yako?"

    "Salama, habari ya ww?"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Safi kabisa,karibu"

    "Asante bwana mdogo"yohana alikasilika kwa kuitwa bwana mdogo alimwangalia na kisha akamuuliza

    "Sijui unaitwa nani,maana kuna mgeni namsubili hapa akitokea congo"yule kijana mwenye milàba nne alimwangalia yohana kisha akamwambia

    " Mimi natokea kinshasa nchini Congo naitaji kuonana na mzee rashid mwinyimkuu sijui kama ndio wewe au unamfahamu?"

    " namfahamu! Karibu sana" baada ya kutambulishana,yohana alimjulisha kama mzee rashid ndio aliyemtuma na yupo hapo kwa ajiri ya kumpokea yeye, baada ya maongezi machache hatimaye walielewana na yohana akampokea begi lake dogo na kumtaka mtu yule amfuate.yule kijana alimfuata mpaka pale sehemu waliyokaa kina mzee rashid.

    Wakati ule mzee rashid na wenzake alimuona yohana akiwa ameongoza na yule kijana moja kwa moja wakajua ndio yeye,walimkaribisha na kuanza kusalimiana.ilikuwa siku tulivyu kabisa,kulikuwa na vinyunyu vya mvua kwa mbali.wakati ule maeneo yale yalionekana kutulia, mzee rashid aliamuakuvunja ukimya na kumuuliza kijana yule jinsi ilivyokua mpaka mzigo ukachelewa kufika mikononi mwao.

    " haya kijana embu tuambie kitu gani kilisababisha mpaka mzigo kuchelewa kufika?"

    " ni matatizo tu mzee,wakati natoka kule kuja uku"

    "Ebu tueleze basi maana hapa sielewani kabisa na hawa wenzàngu".

    Baadae yule kijana akaanza kuwaekeza kilichotoke uwanja Wa ndege Kinshasa wakati anauleta tanzania.......



     Ilikuwa saa kumi na moja alfajiri ilikuwa ndio kwanza naingia uwanja wa ndege na tiketi yangu mkononi,nikapita kukaguliwa bila matatizo,nikapita karibu kabisa na ndege ile, akatokea kijana mfanyakazi wa pale na kunikabidhi begi dogo lenye mzigo ule nikaupokea,ila kabla sijaingia kwenye ndege ndio wakatokea polisi wa usalama pale wakaniweka chini ya ulinzi,hapo sasa ndio nikajua tayari nimekamatwa, nikajua hapa tena siwezi kitoka mikonini mwao.wakati nikitafuta mbinu za kuwatoloka polisi wale,mara nikaisi mkono Wa mtu begani kwangu,nikageuka ili nimwangalie aliyenishika,nikakutana uso kwa uso na askari wa kike, akinitaka nimpe begi nililokua nalo,lakini nilikataa kuwapa uku nikijitetea kama begi lile limeshakaguliwa bila matatizo,lakini hawakunielewa walinipokonya kwa nguvu nami niling'ang'ania sikuliachia, hapo ndio ikawa tatizo na ata walipotaka kuchukuwa kwanguvu ndio mapambano na polisi hao yalipoanza.

    wakati yule kijana anasimulia mkasa uliomkuta mzee na wenzake walimsikiza kwa makini, Mzee Rashidi akamuuliza "uliwezaje kupambana nao polisi wale wakati inaonekana hukua na ujanja nao,mpaka mzigo ukapona?", yule kijana king akaendelea kuwasimulia,nilipambana nao kwa kurushiana risasi huku nikiwa nakimbia na lile begi, lenye mzigo mpaka nikawa mbali nao. wale askari wawili walinikimbiza bila , bila wao kunipata,nikakimbilia katikati ya watu wengi na kujichanganya nao uku nikifanya harakati za mawasiliano na wenzangu,niliwapata na kuwajulisha nilipojificha,baada ya muda kidogo wakanifuata bila kuchekewa,nilipowaona nikajitokeza na kisha walinipakua kwenye gari na safar ya kuludi nilipotoka ikaanza,nikiwa nimeshawatoloka polisi hivyo ndivyo ilivyokua ndugu zangu.

    king alipomaliza kusimulia, mzee rashidi na wenzake walimpa pole na kumtaka siku nyingine kuwa makini na safari zake,kwani ni kazi hisiyokubalika katika jamii.

    mzee rashid na wenzake walielewana wao wakutane kesho yake kwa ajiri ya mzigo ule na kisha kila mmoja aliondoka kivyake, king akiongozana na mzee rashidi kumkabidhi mzigo huo nyumbani kwake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku iliyofuata mzee rashidi alionekana kuwa na mawazo sana hata nyumbani familia yake walijuwa kutokana na kuonekana si kawaida yake, ata mke wake alipomuuliza alikataa na kumwambia anajisikia vibaya wala hakuna tatizo lingine,wakati huo huo mzee rashidi akamalizana na king kisha wakaagana na king kuondoka zake, mzee rashid akiwa amekaa simu yake ikaita alipoangalia mpigaji aliona mzee muba alipokea, na aliongea nae na kutaka wakutane, sehemu mzee muba alimwambia kuna kitu anataka kumsaidia Mzee Rashidi alikubali na kukata simu.........





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog