Simulizi : Upendo Wangu
Sehemu Ya Pili (2)
Baada ya muda mzee rashid aliwasiliana na Yohana ili amsindikize, sehemu waliyopanga kukutana na mzee muba,yohana alikubali na kumtaka ampe nusu saa atakua ameshafika pale. Yohana alipofika pale hawakupoteza muda wakaanza safar, Mzee Rashidi na Yohana walienda sehemu walio panga kukutana na Mzee muba,baadaya robo saa waliwasili, walipofika Yohana alikaa mbali kidogo na walipokaa wao Mzee muba alimkaribisha mzee rashidi na kumtaka hasiwe na wasiwasi kuhusu wito wake. waliposalimiana Mzee Muba alianza kivunja ukimya na kumuuliza mzee rashidi,
"Nakuona una mashaka?
"Hapana bwana,mi nipo kawaida,
"sijui unajua nini nimekuitia ?" “alijibu sijui “Mzee rashidi alimjibu uku akiwa na wasiwasi alichoitiwa,
" sawa nashukur umekuja!"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" nakusikiliza!"
Mzee muba alianza kwa kumwambia
"sisi ni marafiki wa siku nyingi toka tuanze biashara, kwahiyo niko hapa kama Rafiki, nataka kukusaidia!" Mzee Rashidi alifurahi kusikia hivyo,Mzee Mubaaliendelea
" sitafanya ivyo bure kwa sababu kuna kitu nataka unifanyie "Mzee muba alimwambia.
"kitu gani icho? Niambie tu kama ikiwa ndani ya uwezo wangu nitakusaidia?” mzee rashidi alijitetea,
" mtoto wangu manase nadhani unamfahamu vizuri?"
"Ndio namfahamu vizuri yule kijana" mzee rashidi alimjibu
"anataka kumuoa mtoto wako!"MzeeRashidi aliposikia hivyo akacheka kidogo,kisha akamjibu,
"ilo ni jambo dogo sana,nitaongea na Amina kisha nitawapa jibu, Amina ananikiliza sana mimi baba yake!"
Mzee muba alimwangalia mzee Rashidi kisha akamwambia
" sio amina,anayemtaka dada yake Amina.
"Sawa nimekuelewa"
Semeni na manase walipokuwa watoto walicheza pamoja,walisoma shule moja,walikuwa wamezoeana kuwa karibu walipokuwa wadogo,mpaka pale walipokuja kutengana, semeni alipokuja kuchukuliwa na mama yake kwenda kuishi uko akiwa mdogo sasa yafikia miaka kumi na tano tangu kutengana kwako.
Mzee Rashidi alishusha pumzi ndefu kisha kumwambia Mzee Muba
" kwa nini asimuoe amina?"
" semeni ndio chaguo la mwanangu na sio amina!" Mzee muba alimjibu. Mzee Rashidi hakuwa na jinsi alikubali kwa shingo upande, na kumtaka Mzee Muba,ampe mda kwani Semeni yupo mbali na mji wa Arusha anaishi Morogoro kwa mama yake, atamjulisha baada ya wiki mbili, Mzee Muba alimwambia kuwa ondoa shaka yeye atalimaliza pia awe huru muda wowote atamjulisha, mzee rashidi alimshukuru na kumtaka haraka kwani atalifuatilia taratibu kisha atampa jibu kama amekubaliwa au amekataliwa na kumuhaidi hatomwangusha.
Baada ya maongezi hayo wazee hao wawili waliagana na kila mmoja kuondoka kivyake.
Walipofika njiani Mzee Rashidi alimtaka Yohana asimamishe gari pembeni ili waongee,Yohana alisimamisha gari pembeni ya barabara na kumuliza bosi wake kama kuna tatizo,mzee Rashidi alimwambia hakuna tatizo ila kuna jambo gumu japo si sana, Yohana alimuliza bosi wake
" jambo gani ilo?"
" mtoto wa Mzee Muba anataka kumuoa mwanangu?"
"Kumuoa Amina ?" Yohana akadakia
"Hapana,wanataka kumwoa Semeni" mzee rashidi alimjibu Yohana,
"una mtoto mwingine anaitwa Semeni aliuliza uku akiwa katika mshangao kwani hakuwai kumsikia bosi wake akimuongelea mtoto mwingine zaidi ya amina na ndie anayemjua,
"Ndio! najua kuwa hujawai kusikia,
" hata picha sijawai kuiona!"yohana alimjibu uku akimdadisi,
" sawa utamuona sasa! mzee Rashidi alimwambia yohana na kisha kumtaka warudi nyumbani Wakapumzike ili kesho waongee vizuri.
Siku iliyofuata mzee rashidi alikutana na wenzake nyumbani kwake, kila mmoja alimkabidhi mzigo wake na kuwataka wasameheane kwa yote yaliyotokea,na kila mmoja alikubali yameisha na kumpongea mzee rashidi kwa ujasili aliokukuwa nao.baadae walikubaliana na kuagana wakaondoka wakiwa na fedha zao mikononi.
Ilikuwa ni jumapili tulivu kama wengi wanavyopendelea, siku hii kupumzika na familia zao nyumbani.ikiwa inatimia saa sita mchana yohana alifika nyumbani kwa mzee rashidi na kumkuta mzee rashidi akiwa amekaa na mkewe pamoja na binti yake amina,pale sebuleni. yohana aliwasalimia kisha mzee rashidi akamwambia waongee pembeni, yohana alikubali na kisha wakatoka nje na kukaa kwenye bustani nzuri iliyokuwa mle ndani, bila kupoteza muda,mzee rashidi akaanza kumsimuliaYohana, kwa kifupi ,jinsi alivyokua anakaa na mwanae walielewana sana,alimwambia hakuondoka pale kwake kwa mapenzi yake,Bali
walikuwa wanakosana na hawakua na mausiano mazuri na mama yake wa kufikia,ambaye ndiye anayeishi nae sasa, baada ya kuacha na mama yake Semeni , mzee rashidi aliendelea kumwambia Yohana hakuwa na mawasiliano yoyote wala hajui ata namba zao za simu tangu semeni mama yake walipoondoka.
Mzee Rashidi alimsimulia yote yohana kisha akamtaka kesho ajiandae kwa safari, kwenda mkoani morogoro kata ya morogoro vijijini ndipo walipo semeni na mama yake. Mzee rashidi akamtaka yohana kwa maelezo zaidi wakutane kesho take ofisini pale,Yohana hakuwa na jinsi alimkubalia bosi wake kwa shingo upande na kuanza safari ya kurudi nyumbani kujiandaa kwa safari .
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kesho yake asubuhi ikiwa siku ya jumatatu, Yohana alikwenda ofisini kwa mzee Rashidi ,alipofika alimkuta mzee amekaa kwenye kiti cha kuzunguka ofisini kwake baada ya salamu, Mzee alimpa maelezo yote na kumwambia ataanzia kufika kwa mjomba yake Semeni anayeitwa mgalu,ambaye ni mjumbe pale kijijini,pia alimwambia atampa kiasi cha pesa za matumizi katika safari yake.
Mzee rashidi anamjua sana mgalu alivyo mpenda pesa,ndio maana akamuelekeza yohana kuanzia hapo anajua mara moja anaweza kuwasaidia, mgalu anaweza kufanya lolote ilimradi wampate Semeni.
Mzee rashidi alimkabidhi yohana pesa za nauli na matumizi ya siku atakayokua katika safari yake na kumtaka atakapoishiwa basi amjulishe ili aweze kumsaidia.
Yohana aliagana na bosi wake kisha mzee rashidi kumtakia yohana safari njema. Yohana hakutaka kupoteza muda alianza safari ya kumfuata semeni morogoro.Yohana akaanza safari hadi stendi ya kuu ya arusha akafanikiwa kupata tiketi ,bahati nzuri alipata gari inayotoka saa sita mchana ule, akapanda gari linalokwenda dar es salaam, muda ulipofika mara moja gari ikaanza safari.
Baada ya safari ndefu, gari lilifika chalinze ,yohana alishuka kama alivyoelekezwa na bosi wake akavuka barabara na kwenda upande wa pili, pale bahati nzuri alikuta gari likipakia abiria wanaokwenda morogoro nae akapanda na kukaa siti ya nyuma ,baada ya kama dakika tano safari ikaendelea.
Njia nzima yohana alikuwa mtu mwenye mawazo sana,akiwaza jinsi ya kufika na namna ya kumpata semeni, ambaye yeye hamjui nawa hajawai kumuona.
Safari iliendelea ,gari likichanja mbuga na hatimaye baada ya mwendo wa masaa matatu,gari kuwasili stend ya msamvu morogoro .
Yohana alishuka na kwenda kituo cha daladala zinazokwenda vijijini kwa kina semeni alipanda gari na kumwambia konda anapokwenda,
"Oyaaah ! Mwanangu utaniacha njia panda,mbele yake hapo"
" wapi,unashuka?
" nimekisahau kituo,ila naenda kijiji cha matombo"
" usijali basi,nitakujulisha tukifika "poa mwanangu,
"Haina noma,ila ukishuka njia panda utapanda gari lingine "
"Kwani ili linaenda wapi, si uko uko matombo?
" hapana ili halifiki matombo linaishia njiani"
" sasa mimi nitafikaje? Yohana alimuuliza konda wa daladala ile bila kujali kelele zake zinazowaudhi abiria wengine
"Utapanda gari nyingine ipo nyuma inakuja!"konda alimjibu yohana kwa mbwembwe kubwa uku akimwambia atamshusha njia panda sababu ya gari kutofika matombo,Yohana hakuwa na shaka sababu maelezo ya mzee yalilingana na konda.
Baada ya mwendo mfupi walipofika mwisho Wa gari lile konda alimwambia Yohana wamefika mwisho wa safari yao hivyo kushuka ili kusubili gari linalofuata atapanda na kuendelea na safari.
Yohana aliposhuka alisogea pembeni ya barabara akisubili gari, wakati yohana akiwa anasubiri gari kuna msichana mrembo alikuja na kusimama karibu na Yohana,wote wakiwa wanasubili gari,Yohana alishindwa kuvumilia kutokana na uzuri aliokuwa nao Yule msichana alimsogelea kisha akamsalimia,
"Habari yako dada?"
"Salama!"yule msichana aliitikia na kuelekeza shingo yake mbeni,
"Samahani dada,sijui unaitwa nani?"yohana aliendelea kumuuliza yule msichana, lakini yule msichana akujali, hakujibu maswali ya Yohana, hata Yohana alipompa Business cad yake msichana alikataa na kusogea mbali na pale walipokuwa wamesimama,yohana kuona vile akaamua kuachana nae yule dada.
Muda ukiwa unazidi kwenda huku abiria wengine nao waliongezeka,baada ya muda si mrefu gari lilifika na kusimama karibu na alipokuwa Yohana, bila kucherewa abiria nao wakaanza kuingia, kwa bahati nzuri Yohana aliwahi kupanda na kubahatika kupata siti, waliingia abiria wote mpaka wengine wakakosa siti na kusimama. Baada ya konda kuakikisha abilia wote wameingia,akamuru dereva kuwasha gari na safari ikaanza ,kuelekea kijiji cha matombo.
Wakiwa hatua chache kutoka pale kituoni waendelea na safari, Yohana alimuona yule msichana aliyekutana nae pale stand akiwa amesimama ndani ya gari ile,Yohana hakukubali kushindwa akaona atangaze wema kwa kumuachia siti akae, yohana aliinuka na kumshtua yule Msichana bila kusita akakaa, abiria wote ndani ya gari walimwangalia yohana.Yohana bila kujali alisimama na kushikilia juu kulipokua na chuma ndani ya gari lile, watu waliendelea kumshangaa yohana kwa kumuachia siti yule dada na kusimama.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
walipofika katika kijiji cha matombo Yohana alikuwa wa kwanza kushuka,aliposhuka aliingiza mkono mfukoni mwake na kutoa kikalatasi chenye maandishi juu yake,kisha kukisoma kuangalia upande gani anatakiwa kwenda...... .
Yohana akiwa hajui wapi ataanzia ili apate mwenyeji amwelekeze nyumbani kwa mgalu,mara alimwona Yule msichana mrembo akielekea upande wa kulia wa barabara,yohana alimfuata na kumuomba amuwelekeze kwa mjumbe wa kijiji kile kama anamfahamu, yule Msichana alimwambia anamfahamu nae anaelekea huko.
Yohana alimuomba amfuate huko anapokwenda kwani safari yao ni moja,yule msichana wala hakuwa na kinyongo alimkubalia, Wakati wakiwa njiani Yohana alimuuliza yule msichana
"Samahani dada"
"Bila ya samani "yule mdada alimjibu,
"Jina langu naitwa yohana,Sijui wewe unaitwa nani mwezangu?" Yohana alizidi kumdadisi yule dada,
"Asia!"
"Ooh! Asia,jina zuri sana"
"Asante!
"Wewe ni mrembo sana vipi,shemeji yupo? Yohana alizidi kutupa ndoano kwa yule dada,
"Utakapouliza maswali yako tena,na kuongea ujinga wako,nitakuacha hapa sitakupeleka!"alimuambia yohana uku akiwa amekunja uso wake kwa fedhea.
Yohana akaanza kulalamika kukuambia kuwa we mzuri au kukupa sifa unazositahili ndio ujinga basi mi siongei ila nipeleke tu dada.
Baada ya mabishano ya wawili hao , hatimaye waliendelea na safari ila Yohana alionekana kumtamani sana yule dada aliyejitambulisha kama asia.Baada ya mwendo mrefu, uliochukua nusu saa nzima hatimaye walifika njia panda na yule msichana akamuelekeza Yohana njia ya kupita nyingine ,mbele akikuta nyumba yenye bendera ya ccm,ndio hapo kwa mjumbe, Yohana alimshukuru Yule msichana kisha waliagaliana na kila mmoja kuondoka njia yake, Yohana alifuata maelezo ya yule msichana,hakutembea umbali mrefu akaiona nyumba moja ya miti iliyotengenezwa undogo juu ikiwa imeezekwa kwa nyasi zilizokauka,yohana alizidi kusogea zaidi, aliwana wazee kwa vijana wamekaa ubavuni mwa nyumba ile, yohana alienda moja kwa moja mpaka pale walipokaa wale watu na kuwasalimia, wanakijiji wale walimuitikia salamu yake kisha walimkaribisha,yohana hakusita,Mara moja akamuulizia mjumbe na kutaja jina la mjumbe anayemuulizia jina lake ni mgalu, aliitikia mzee wa makamo kidogo, Yohana alitoa kikaratasi kidogo kilichokua na maneno machache ndani yake na kumpa Yule mgalu. ,baada ya kukisoma kwa muda,mgalu alinyanyuka pale nje na kumtaka Yohana wakaongee ndani.
Mgalu ni Mjomba wa semeni,anayeishi na familia yake yenye watoto wawili,mgalu na mama semeni wamechangia baba ila mama tofauti,pia ndugu hao hawana maelewano mazuri kutokana na mgalu kuwa mlevi kupindukia.
Siku hiyo mgalu alipoona ujumbe ule kutoka kwa mzee rashidi alifurahi sana akacheka mpaka meno yote 32 kuonekana ,akajisemea moyoni ama kweli baada ya dhiki faraja,sasa leo nimepata faraja,alimkalibisha ndani.
Walipoingia ndani,yona wala hakuwa na papala alishajua alichopelekewa ndani na mzee yule,hakuna la zaidi ya pesa,mgalu alimtaka yona hasiwe na wasiwasi semeni yupo na ataakikisha anaondoka nae,baada ya kuelewana yona hakuona sababu ya kukaana zile pesa akaamua kumpa kabisa mgalu pesa zake na kumwambia atapata nyingine,pale semeni atakapopatikana.
Mgalu hakuona sababu ya kuchelewa alimtaka yona waelekee kwa mama semeni mara moja ili wakaelewane,yona alikubaliana na mgalu kwenda kwa mama semeni,walipotoka nje waliwakuta wale wazee waliokuwa wanacheza bao wameondoka,nao bila kuchelewa mgalu alifunga mlango wa nyumba yake na kumtaka yohana amfuate kwa mama semeni ambapo hapakuwa mbali na pale kwa mgalu.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada mwendo wa miguu kama dakika kumi walifika , walipofika nyumbani kwa mama semeni walikuta nyumba imefungwa kufuri likiwa linaning'inia mlangoni, kabla hawajaamua lolote ,walimuona mama semeni anakuja akitokea shamba mkononi akiwa ameshikilia kikapu kidogo kilichosukwa kwa kutumia miyaa mikavu, Mara moja yohana akajua yule mama anayekuja pale ndiye mhusika Wa nyumba ile aliyofikia.
Alikuwa mrefu kiasi ,sio mwembamba wala mnene ,mwenye sura nzuri iliyokunjana sababu ya umri kumtupa lakini bado alionekana mwanamke mwenye nguvu anayepambana na maisha, ni kweli kwani mama semeni alikuwa na uwezo wa kulima na kuvuna mazao mbalimbali.
Bi ramla ndio jina lake halisi alilopewa baada ya kuzaliwa na wazazi wake miaka hamsini iliyopita, majirani zake wengi upenda kumuita mama semeni, kama yeye anavyopenda kuitwa hivyo,sababu semeni ndio mtoto pekee kwake...
Siku hiyo mama semeni alikuwa anatoka shamba,akiwa amechoka kama mtu aliyekimbia mbio za maradhoni,uku mkononi wa kulia akiwa ameshikilia kikapu kidogo kulichokuwa na mihongo ndani yake,mama semeni alipofika pale alimkuta kaka yake akiwa na yona ,lakini yeye wala hakumjua yule mgeni aliyekuwa na kaka yake, aliwakaribisha kisha akaingia ndani na kutoka mkononi akiwa ameushika mkeka. Mama semeni akasalimiana na kaka yake,yona nae akawai kumsalimia mama semeni kwa unyenyekevu, akionyesha kuwa ni kijana mstarabu na mwenye heshima .wakati wote huo mama semeni alikuwa wakitaniana kiluguru na kaka yake. Yona akawa anawaangalia na kucheka uku akiwa hajui wanachoongea wanandugu wale. Na kisha mgalu akamtambulisha Yona kwa mama Semeni,na kumwambia kila kitu yona alivyotumwa na mzee rashidi kumchukua semeni.mama semeni alishtuka gafla kama mtu aliyepokea taatifa za msiba, alibadilika ghafla na kutaka yona aondoke nyumbani kwake,mgalu akamtuliza dada yake na kumtaka wakaongee ndani,Mama Semeni akakubali,alinyanyuka pale kwenye mkeka na kuingia ndani mgalu nae akamfuata, kisha kumtaka yohana hasiwe na wasiwasi wao wanaongea na kuyamaliza.
Yona akiwa amekaa pale nje peke yake alimwona yule msichana aliyekutana nae njiani anakuja pale,yona hakusita akamkalibisha na kujifanya mwenyeji ,
"Karibu dada!"
"Asante,kumbe ulikua unakuja hapa? Yule mdada akamuuliza
"Hapana nilikuwa nakwenda kwa mjumbe,nilipofika pale nikaletwa huku,
"Sawa ,nashukuru wenyewe nimewakuta hapa"yule msichana aliendelea kuuliza
"Ndio wapo, karibu ukae! Yona aliendelea kumkaribisha yule dada
"Asante,
Yule binti alikaa kwenye mkeka,uku akimwangalia yona kwa macho ya kuibia,yona alikaa uku macho yake yenye umbo kubwa kama goroli yakimwangalia yule binti mrembo mwenye sura nzuri ya duara,macho madogo yaliyokolezwa wanja, mashavuni vishimo vinavyooneka achekapo, hakika alikuwa msichana mrembo wa sura na umbo la kuvutia kila mwanaume lijali atakayemtokea mbele yake lazima achanganyikiwe.
Wakati wakiwa wamekaa peke yao pale nje ,yohana alimuuliza yule binti shida iliyomleta pale,
"Nikusaidie mimi binti?''
"Namuitaji kuonana na mama" yule Dada Alimwambia"
"Ata mimi pia unaweza kumwambia"
"Hapana namsubili mwenyewe"
"Kwani mimi ukiniambia kuna tatizo"yohana aliendelea kumhoji
" Mimi nimetumwa kwa mama kumpa mzigo wake,hivyo basi namsubili mpaka atakapokuja nitaongea nae mwenyewe!"
Yule dada alimwambia yohana na kadai kuwa anamhitaji mama mwenye nyumba na shida yake atamweleza mama mwenye nyumba na sio yeye yona hakuwa na jinsi akaamua kukaa kimya huku akimuangalia yule binti. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mjumbe na dada yake walikuwa
kwenye maongezi ya kina,dada alipingana na Kaka yake,hakutaka semeni kwenda kwa baba yake sababu anamjua vizuri mzee rashidi,
"Kaka ,semeni kwenda kwa baba yake haiwezekani!"
"Kwanini Dada angu,muache mtoto akamsikilize baba yake"mgalu alimuambia dada yake
" unajua semeni nimepata nae shida sana,eti leo aje kumchukua kilaisi hivi" mama semeni alibwata
" sikia dada angu,mzee rashidi hatujua anachomuitia mtoto wake,hivyo basi muache akamsikilize"
muachie mtoto aende kumsikiliza baba yake,hatujui anachomuitia mtoto wake muache tu aende Dada" mgalu alimsihi dada yake, huku akimwambia mara mbilimbili amruhusu yohana kuondoka na semeni.baada ya mabishano ya wanandugu hao,mwishowe mgalu alifanikiwa kumshawishi dada yake, kwani mama semeni hakuwa na neno juu ya kaka yake huyo,kwa sababu mgalu alikua ameshalewa kwa ahadi kibao na pesa alizopewa na kuahidiwa zilimchanganya.....
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment