Search This Blog

Friday, July 15, 2022

KIFO CHA MARRY - 2

 







    Simulizi : Kifo Cha Marry

    Sehemu Ya Pili (2)



    Zikapita siku tatu bila mawasiliano yoyote kati ya sira na Anna kutokana na kuchukuliwa simu ya Anna na wazazi wake.



    Wiki moja baadae walikuja wageni kutoka kijiji cha pili na kuonana na wazazi wa Anna

    “sisi hatuna pingamizi,ni nyie tu pangeni tarehe mje mumchukue mke wenu” aliongea mzee Mashuhuri baada ya kukaa kikao kifupi huku akihesabu burungutu la hela alizoletewa.

    “mtoto wetu hataki kupoteza muda na ana kazi nyingi sana mjini, kwa huyo kwakua hakuna tatizo la hela, mnaonaje ndoa iwe kesho kutwa?” aliongea mshenga aliyekuja kumuwakilisha muoaji.

    “hamna shida, ni nyinyi tu”aliongea mzee mashuhuri huku aktabasamu.

    “basi wapeni taarifa ndugu na jamaa ili wahudhurie harusi ya aina yake, maana mwanetu kajipanga haswa na hahitaji mchango kutoka kwa mtu yeyote.”

    Waliondoka wale wageni na mzee mashuri bila kuchelewa alimuita binti yake na kumueleza kilichojiri kwenye kile kikao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “sikubali baba, huo ni unyanyasaji wa kijinsia!” alihamaki Anna baada ya kuambiwa kuwa wale wageni wana muhusu kwa kiasi kikubwa, kwani wamekuja kuoa siku mbili zijazo.

    “shenzy….. tena ufunge mdomo wako kabla sija kuzabua. Unajua kunyanyaswa wewe?, nishawahi kukunyanyasa?.. mi baba yako nakupenda sana na sitaki mtu yeyote katika familia yangu apate taabu. Mpaka namekubali kuwapa hawa majamaa binti yangu wa pekee basi ujue ni watu wazuri na wana hela. Achana na yule jamaa Muislamu. Hujui hata taratibu za ndoa zao na hujui hata ni nani atakuangalia. Maana utakapobadilisha dini si mimi tu nitakaye kukataa. Bali hata mama yako hatotaka kukuona. Unafikiri ukipata matatizo utakuwa mgeni wa nani?.. na mwanaume akishajua kuwa umemuegemea yeye kama nguzo ya maisha yako, atakachokufanya ni kukunyanyasa na ikiwezekana kukuolea wanawake wengine. Maana waislamu wameruhusiwa kuoa mpaka wanawake wanne. We upo tayari uingie kwenye ndoa za mitala??” aliongea mzee mashuhuri na kumshika mikono binti yake kama ishara ya upendo juu yake.

    “sihitaji baba” alijibu Anna kwa utulivu kuonyesha kuwa maneno ya baba yake yanamuingia sawasawa.

    “ninachosikitika ni muda tu wa kujiandaa umekosekana, ila ndoa yako nitakupa zawadi niliyokuhifadhia toka zamani.” Aliongea mzee mashuhuri kwa sauti ya upole na kuonyesha jinsi gani anavyosikitika.

    “ huyo mwanaume anayenioa mmeshawahi kumuona?” aliuliza Anna na kuwaangalia wazazi wake.

    “hatujawahi kumuona, ila wazazi wake ni watu wazuri sana. Pia unaolewa na msomi.kwa hiyo ile ndoto yako ya kusoma na kufika chuo anaweza kukusomesha mume wako. Ndio maana nikakwambia siwezi kukubali uwe sehemu mbaya. Si unakumbuka nimewatimua wanaume wangapi wasiokuwa na Dira waliokuja kukuchumbia?” aliongea mzee Mashuhuri na kutabasamu.

    “nakumbuka baba” aljiibu Anna na kucheka.



    Siku iliyosubiriwa kwa hamu na Mzee Mashuhuri iliwadia. Anna akiwa kwenye shela la bei mbaya na mumewe akiwa amevalia suti ya thamani, walionekana waking`ara kuliko yeyote pale. Haikua harusi ya kitoto, japo iliandaliwa muda mfupi.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kulichinjwa mbuzi na ng`ombe wengi sana. Gari zima la soda lilikuwa pale kwa ajili ya watu waliohudhuria. Jenereta kubwa liliwashwa na kutapanya umeme na mziki mkubwa uliunguruma na kuwafanya wanakijiji karibu wote kujisogeza kushuhudia harusi hiyo ambayo haijawahi kutokea. Kila mtu alikula na kunywa mpaka aliposaza mwenyewe. Hakuna aliyekua na swali juu ya harusi pekee ya kufunga karne kwao.

    Hata Anna mwenyewe alikubali na kuifurahia ile harusi iliyompa maujiko kijijini kote. Hata mawazo ya Sira kichwani kwake yaliyeyuka kama barafu liyeyukavyo kwenye maji yachemkayo.

    Sira akiwa katika pikipiki yake, alishangaa kuona msafara wa gari karibu nne zikiongozana huku gari ya tano ikiwa na maharusi wakisindikizwa na kundi la watu waliokuwa wakitembea kwa miguu wakiwasindikiza maharusi.

    Alipigwa na butwaa baada ya kumuona Anna akiwa ndani ya shela. Hakutaka kuamini, lakini aligundua kuwa ndie yeye baada ya gari kumpitia karibu.

    “Annaaaaaaaaaaaa”

    Aliita Sira, lakini sauti yake ilimezwa na kelele za shangwe zilizotawala maeneo yale.

    *************************

    Safari ya Anna iligota kwenye kituo cha taksi. Alisimama kwa muda huku akiangalia ataanza vipi kuomba msaada.

    “karibu dada, unaenda wapi?” aliongea dereva taksi mmoja aliyekuwa karibu yake.

    “ siendi popote.” Alijibu Anna.

    “huendi popote?...sasa mbona upo hapa usiku huu, utabakwa bure dada.”

    Alipoongelea swala la kubakwa yule dereva taksi, Alarm nyekundu ililia kwa kasi ubongoni mwake na vipele vya baridi vilimtoka mwili mzima. Aliogopa sana swala lile kutokea.

    “mi nilikua naelekea ubungo kaka yangu” akajikuta ameongea mwenyewe bila kujitambua.

    “twende” aliongea dereva taksi na na kuwasha gari.

    “lakini…”

    Alitaka kuongea kitu, lakini alikatishwa na yule Dereva taksi baada ya kumshika mkono na kumuingiza ndani ya gari na safari ikaanza.

    “ulitaka kusemaje, maana nimekukatiza” aliongea yule dereva taksi huku aikiwa makini na usukani.

    “hivi unajua kuwa sina hela?..hilo ndilo nililolitaka kusema.” Alifunguka Anna

    “umefukuzwa nini?..mbona na mabegi usiku huu?” aliuliza yule Dereva taksi bila kuonyesha kujali kuwa mteja wake hakua na hela.

    “nimefukuzwa na nimepigwa kama mbwa mdokozi kaka yangu.” Aliongea huku akionyesha majeraha yaliyo kwenye mwili wake.

    “pole sana dada.” Aliongea yule dareva taksi baada ya kuyaona majeraha ya Anna.

    “ sasa kama nauli ya kukupeleka ubungo tu huna, hiyo nauli ya kwenda kwenu unayo?” aliuliza yule Dereva taksi.

    “sina kaka yangu?” alijibu haraka Anna.

    “ duh!..sasa kwenu ni mkoa gani?” aliuliza yule Dereva rtaksi.

    “mi ni mwenyeji wa Dodoma, ila kwa sasa nataka kufika morogoro kwa shangazi yangu.” Alijibu Anna na kuondoa hofu aliyokuwa nayo juu ya kupanda taksi ya watu bila ya kuwa na hela.



    gari ilifika ubungo na kuendelea na safari. Anna alishangaa kuuona yule deriva taksi anapapita ubungo.

    “wacha nikupeleke tu morogoro, maana umenishawishi kukusaidia.” Aliongea yule Dereva taksi ili kumuondoa wasi wasi aliokua nao Anna

    .

    Kimya kilipita kama nusu saa. Na usingizi ukaanza kumnyemelea Anna na haikuchukua muda mrefu ukamchukua kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alipokuja kuamka aliona hali tofauti kidogo. Taksi aliyopanda ilikua inazidi kukata pori na kuelekea kusikojulikana. Alichunguza na barabara pia, aligundua alikua anapitishwa kwenye majani tu. Na muelekeo wa gari lilikua linazidi kuzama msituni.

    “ wapi huku kaka??” aliuliza Anna kwa hofu kubwa.

    “usijali dada, hii ni short curt” alijibu yule dereva Taksi bila kumuangalia usoni Anna.

    “geuza gari kaka, huko mi siendi!” aligomba Anna.

    Yule dereva hakumsikiliza. Ndio kwanza alizidi kukanyaga mafuta na kutokomea mbali zaidi. Anna alijaribu kuongea lakini hakujibiwa kitu.

    “hebu tuachie kelele”

    Ilisikia sauti ikitokea nyuma ya siti. Anna alishtuka sana. Aliguza shingo kumuona aliyeongea. Alikutana na sura za watu watatu waliokuwa wakimuangalia bila kupepesa macho. Alipiga kelele lakini hakukua na hata nyumba eneo lile. Zaidi sauti yake ililsikika na miti tu iliyokua ikipulizwa na kiupepo kilichokuwa maeneo yale.

    Kelele zilipozidi, mmoja kati ya watu waliokuwa nyuma ya ile Taksi alimpiga ngumi nzito Anna iliyomfanya apoteze fahamu.





    Alipokuja kushtuka, alijikuta anasikia maumivu maeneo ya katikati ya mapaja. Pia aliona kama ameelemewa na kitu kizito . alipofumbua macho yake. Alikuta pande la mtu likiwa linamuingilia huku mikono na miguu yake ikiwa imechanuliwa na kila mmoja kufungwa kwenye mti wake.



    Alipiga kelele za maumivu lakini hakuna aliyejali. Baada ya yule pande la mtu kumaliza shida zake, akaingia mwengine. Alilia mpaka sauti ilimkauka. Lakini alichoambulia na makofi na mikanda.

    Wakati yanatendeka hayo yote,yule dereva taksi alikua pembeni akishuhudia yote yale.

    “vipi wewe, hutaki kupata raha kutoka kwa Malaya huyu?” aliongea yule kiongozi aliyempiga ngumi Anna.

    “endelea tu mkuu. Mi nina dozi ya malaria na sijisikii vizuri.” Aliongea yule dereva na kuendelea kukaa pembeni.



    Walirudia round nyingi mpaka wallipomuona Anna kazima. Walinyanyuka na kuingia kwenye taksi.

    “kama kafa muache hapo hapo, kitakua chakula cha ndege.”

    Aliongea yule mkuu wao na wakaondoka kwa kasi.



    Masaa mawili baadae, Anna alirejewa na fahamu. Alipojaribu kuinuka alishindwa kutokana na maumivu aliyokuwa nayo. Alijaribu kuiangalia. Alijikuta kama alivyozaliwa na damu nyingi zikimtoka sehemu za siri. Alilia kwa kwikwi na kumuomba mungu amchukue kama uhai wake ni wa mateso kila siku.



    Alimkumbuka Sira. Kipenzi cha moyo wake. Aliwalaumu wazazi wake kumkataa Siraji kwa sababu ya dini na kumkubalia mkiristo mwenzao aliyemsababishia yote yale.



    Kwakua alikua na njaa. Alishindwa kupiga hata hatua moja. Alilala palepale akisubiri mauti

    Alijua kua njaa ilitosha kumuua kwakua hakukua na chakula wala mti wa matunda.



    Mara akasikia mlio wa gari likija upande wake. Alitamani kujificha kwa kua alijua itakua ni wale wale wabakaji wamekuja kummalizia. Lakini alishindwa kutokana na maumivu na hakua na nguvu hata ya kukaa kitako.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Gari ile ilipaki karibu yake na akashuka yule dereva taksi akiwa na kibakuli maalumi cha kuwekea chakula ( take away ) na maji makubwa ya Kilimanjaro.



    Alimsogelea Anna na kumkalisha. Anna hakutaka kumuangalia mara mbili. Alijua yule ndio mbaya wake. Yule ndiye sababu ya yeye kufanyiwa unyama kama ule.

    “naomba kula chakula, mengine yote yatafata baadae.” Aliongea yule dereva taksi kwa upole.

    “kama umekuja kunimalizia we nimalizie tu… sina hamu na haya maisha mie.” Aliongea Anna na kukigomea kile chakula.

    “najua mimi ndio niliyekusababishia yote haya. Lakini sikua na jinsi. Mimi mwenyewe nilitekwa dada na salama ya maisha yangu ilikua ni wewe dada.” Aliongea yule Dereva taksi bila kumuangalia Anna ambaye alikua uchi na ameloa damu sehemu nyingi za mwili wake.

    “kama ningekua dada yako ungekubali kunifanyia hivi?” aliuliza Anna huku machozi yanamtoka.

    “naomba nisamehe dada, sikuwaza kama wangeweza kukudhuru kama hivi.” Aliongea yule Derva taksi na kumvulia koti lake na kumpa Anna ajistiri kidogo.

    “mimi si dereva taksi kama ulivyoniona pale, ila nilimpokea tu Dereva wangu kwakua nimempa likizo aende kuwatembelea wazazi wake. Ndio kikanikuta kisanga cha kutekwa na kuniamrisha kumsubiri mwenzao maeneo yale. Alipoingia tu ndio na wewe ukatokea. Wakanionyeshea bastola na kuniambia wataniua kama nikishindwa kukushawishi kuingia ndani ya gari. Unafikiri ningefanyaje?” alijaribu kumuelezea Anna kwa jinsi hali ilivyikua nzito upande wake.

    “siwezi kukusamehe kwa uliyonitendea” aliongea Anna baada ya kulipokea lile koti na kujifunika.

    “hata kama hutaki kunisamehe. Nakuomba ule ili upate nguvu.” Aliongea yule Dereva taksi na kumfuunulia chakula alichomletea.

    Baada ya kulazimishwa sana na kuombwa sana msamaha na yule Dereva taksi,Anna alikubali kula kile chakula.



    Alikula kama anakimbizwa kutokana na njaa aliyokuwa nayo. Baada ya kushiba alipumzika kwa dakika kadhaa na baadae yule Dereva taksi alimsaidia na kumuingiza kwenye Taksi yake.

    ******************************



    Safari iliishia nyumbani kwa dereva taksi. Kwakua alikua anaishi peke yake. Alimkongoja mpaka sebuleni. Aliingia chumbani kwake na kutoka na bukta na kumvisha Anna. Baada ya hapo alimnyanyua na kumuingiza bafuni na kumuogesha.



    Baada ya hapo alimrudisha ndani na kumpeleka kwenye chumba cha wageni na kumlaza.

    Alitoka na kwenda kununua vitenge na nguo kadhaa za kike. Aliporudi alikuta Anna amepata usingizi.

    Anna alipoamka alikuta ameandaliwa nguo kitandani na chakula kikiwa kimefunikwa kwenye meza ndogo ya kioo iliyokuwa mbele ya kile kitanda.



    Japo alikua na maumivu makali, lakini angalau aliweza kusimama kwa shida na kuvua ile bukta na kuvaa nguo alizoletewa.

    Alifungua darisha na kugundua kuwa usiku ulishaingia. Alipotupa macho yake ukutani, alikutana na saa iliyomjulisha kuwa ilikua saa tano usiku.

    Alikula chakula na kulala tena.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asubuhi alipoamka, alijivuta na kusogea sebuleni ambapo hakukua na mtu yeyote. Aliingia kwenye kijichumba cha kulia chakula. Alikuta kuna kawa limefunika vyakula. Alipofunua alikuta mikate na vitafunwa vingine. Pembeni kulikua na kikaratasi kilichoandikwa ujumbe mfupi.

    “nimeenda kuangalia nyama na mahitaji mengine sokoni, ukiamka we kula na kama hujatosheka, vingine vipo kabatini”

    Ujumbe huo ulimfanya atabasamu kidogo na kukaa chini na kumywa chai.



    Lisaa limoja baadae, yule Dereva alirudi na kumkuta Anna sebuleni akiangalia Movie.

    “nakuona unaangalia Movie, we endelea ngoja mi niingie jikoni kupika.” Aliongea Yule dereva taksi.

    “yaani we mwanaume upike wakati mi nimekaa tu.” Aliongea Anna na kumfanya yule Dereva atabasamu.

    “we si unaumwa, ukipona utapika.” Aliongea na kuondoka zake jiko.



    Zilipita wiki mbili Anna akijiuguza kwa yule Dereva taksi. Baada ya afya yake kutengemaa. Alishauriwa kwenda kupima virusi vya ukimwi na mimba.

    Kwa bahati nzuri hivyo vyote hakua navyo. Anna alifurahi sana.



    Siku zilizidi kukatika na ukaribu wa KENEDY (dereva taksi) na Anna ulizidi kuimarika siku hadi siku. Kuna wakati walitoka out na kwenda wote sehemu mbalimbali za starehe.

    Baadhi ya marafiki wa Ken walianza kumuita Anna shemeji naye aliitikia na hakuona tatizo. Mpaka siku Ken alipofunguka na kumwmbia kuwa anamuhitaji katika maisha yake. Na kwakua miezi mitatu ilipita bila kumuona Ken akiwa na msichana au tabia yoyote iliyokwaza, Anna aliamua kuuweka moyo wake rehani kwa huyu kijana aliyemsababishia matatizo na aliyekuja kumuokoa porini akikaribia kufa kwa njaa.



    Ukurasa mpya wa maisha ya Anna ukafunguka na kuanza maisha upya ya upenndo na amani kwa kijana huyo Ken. Alijitahidi kusahau aliyotendewa na kijana huyo na kusahau mateso ya aliyekua mume wake. Alifuta kumbukumbu za kijana aliyetokea kumpenda kipindi kile kabla hajaolewa. Alimsahau Sira kwakua hakua na uwezo wa kuonana naye tena. Pia alijua kuwa Sira alishapata habari za kuolewa kwake, hivyo nay eye itakua ameamua kuwa na mwanamke mwengine

    Baada ya kufuta mawazo yote kichwani, akaanza kula raha taratibu na mpenzi wake huyu mpya. Alimpenda sana na alimuheshimu kama mumewe. Hakuona haja ya kujificha wala kuwa na aibu kama zamani. Alijiachia na Ken kila sehemu na kusababishia Ken kupata bichwa kila sehemu wanayoingia kutokana na kusifiwa kwa uzuri wa mpenzi wake.



    Hakika Ken alikua tumaini jipya kwa Anna aliyekata tamaa ya maisha kutokana na manyanyaso ya binaadamu. Alijiona kuwa kaumbwa kuja kubeba mikosi yote waliyotakiwa kuwa nayo binaadamu wengine. Ila kwa sasa aliamini kuwa huenda Ken

    ndio mume ambaye mungu kamuandalia. Licha ya kuona anavyobakwa lakini alikubali kuficha aibu yake kwa kuwa tayari kumuoa yeye. Alijua kuwa Ken ni mwanaume mwenye huruma na ana mapenzi ya kweli moyoni mwake.



    Hakuwahi kumfumania wala kusikia mambo ya ajabu kama wanawake wengine wanavyoteseka juu ya wapenzi wao. Lakini msimamo wa Ken ulimtia faraja Anna na kumuamini asilimia zote..

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ken nae kwa upande wake alijitahidi kumuondoa mawazo Anna kwa kumpatia kila anachokihitaji. Cha kwanza alimpeleka chuo kusomea kozi ya kiingereza na computer.

    Anna alipohitimu kozi hizo, tayari alikua na uwezo wa kuongea vizuri kiingereza na mikono ikawa mepesi kuandika kwa kutumia program ya office.



    Alimfungulia stationary kubwa maeneo ya karibu na wanapoishi. Na huo ndio ukawa mwanzo wa maisha ya furaha kwa Anna.



    Uzuri na urembo wa Anna ulijtokeza kwa kasi na kumfanya awe kivutio kwa kila mvulana anayepishana naye. Alinenepa kiasi na kiuno kilichobeba makalio wastani yaliyoongeza uzuri wa shepu ya Anna ndivyo vilivyowadatisha wengi.



    Ken hakutaka kufanya makosa, alimpeleka kwa wazazi wake na kumtambulisha rasmi kama mke wake mtarajiwa.



    Baada ya hapo, walipanda gari yao kwenda nyumbani kwa kina Anna. Walipofika walikuta hali tofauti. Nyumba yao ilikua kama gofu kwa jinsi ilivyokosa usafi wa muda mrefu.

    “shikamoo bibi.” Alisalimia Anna baada ya kufika kwa jirani yao wa karibu.

    “marahaba!” aliitikia yule bibi na kumshangaa Anna kwa jinsi alivyokuwa mkubwa kutokana na kutomuona kwa miaka mitano sasa.

    “mimi Anna bibi.” Alijitambulisha Anna baada ya kumuona yule bibi akimfananisha

    “aaah!.. macho ya uzee tena, niambie mjukuu wangu” aliongea yule bibi baada ya kumtambua Anna.

    “safi tu bibi, hivi mzee mashuhuri na mkewe wamehama?...maana nimeingia nimeona nyumba tupu.” Aliuliza Anna na kumuangalia yule bibi aliyekua amekaa chini ya muembe akisuka ukili.

    “ we mtoto weeh!... ina maana hujui kama wazazi wako wamefariki muda mrefu?” aliongea yule bibi kwa mshangao. Maana ni miaka miwili imepita toka wazazi wa Anna wafariki.

    Bila kuuliza kitu kingine. Anna aliangua kilio na kubembelezwa na Ken. Alilia kwa uchungu kwa kutohudhuria mazishi ya wazazi wake.



    Anna toka aolewe hakukanyaga tena kule kijijini kwao, mumewe hakumpa ruhusa kabisa. Hata wazazi wa Anna waliridhika sana baada ya kutumiwa hela na mkwe wao na kudanganywa kuwa Anna ameajiriwa na serikali hivyo ataenda akipewa likizo.

    Anna alijiona ana mkosi katika dunia. Aliamini labda alitakiwa kuishi muda mfupi kwenye raha na kuishi kipindi kirefu kwenye shida.



    Hakutamani kuishi kutokana na mateso ya moyo wake yanayomsumbua. Aliwapenda wazazi wake japokuwa wao hawakumtendea haki kwa kumchagulia mtu wao na kumkataa Sira eti kwa kua ni muislamu.



    Alilaani kuishi na mume katili kama aliyemuoa, alijua laiti kama wazazi wake wangejua kuwa mateso waliyomsababbishia, basi wangekuja mjini kumchukua.

    Alilia sana na Ken alikua mstari wa mbele kumpooza Anna na kumfariji kwa maneno mazuri.

    Baada ya kubembelezwa sana, alikubali kunyamaza na kumsikiliza mpenzi wake. Anna alimuomba sana Ken asije akamuacha kwa kua hakua na msaada mwengine zaidi yake. Ken alimuhakikishia kuwa hatajaribu hata kumpiga kibao wala kusababisha maumivu yoyote kwake kwa kua anampenda sana.



    Baada ya machungu kupoa, Anna alipelekwa kwenye makaburi ya wazazi wake na kutoa heshima zake za mwisho.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya hapo hawakukaa sana. Walirudi Dar kwa majonzi.

    “usijali Mpenzi wangu, mimi nipo pamoja na wewe.” Aliongea Ken walipofika nyumbani.

    “inauma sana,” aliongea Anna huku analia.

    Ken akachukua nafasi yake kumfariji na kumuhakikishhia kuwa ataishi naye maisha yake yote.

    ************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog