Search This Blog

Friday, July 15, 2022

MASSACRE (MAUAJI YA HALAIKI) - 5

 







    Simulizi : Massacre (Mauaji Ya Halaiki)

    Sehemu Ya Tano (5)



    “Vua kofia” Ilisikika sauti ya kijana mmoja akimwambia Benedict.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mapigo ya moyo yakazidi kumdunda Benedict, wasiwasi ukazidi kumuingia huku mwili wake ukizidi kumtetemeka. Aliliangalia kundi lile la watu na kuziangalia silaha zile ambazo walikuwa wamezishika, hofu ikazidi kuingia zaidi. Kauli aliyopewa ya kuvua kofia yake ilisikika vizuri masikioni mwake lakini alionekana kutokuwa tayari kuivua kofia ile.



    “Vua kofia” Mwanaume yule ambaye alionekana kuwa kiongozi wa undi lila alirudia kauli yake huku akionekana kuwa na hasira zaidi.







    Benedict hakutaka kuleta ubishi tena, akaivua kofia yake pamoja na miwani ambayo alikuwa ameivaa. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kustuka mara baada ya kuuona uso wa Benedict hali iliyoonyesha kwamba hakuwa akijulikana na watu wale. Jamaa yule ambaye alionekana kuwa kiongozi akaanza kupiga hatua kumfuata Benedict, alipomfikia akaanza kumwangali vizuri usoni mwake.



    “Umetoka wapi?” Mwanaume yule alimuuliza huku akimwangalia vizuri.



    “Bunju” Benedict alijibu.



    “Unaelekea wapi?”



    “Bagamoyo”



    Jamaa yule akaanza kupiga hatua kuwafuata wenzake, alipowafikia akaanza kuongea nao kwa sauati ya chini ambayo Benedict hakuisikia. Mara baada ya kuongea nao, akaanza kumfuata Benedict ambaye bado alikuwa akionekana kuwa na wasiwasi. Alipomfikia, hakutaka kuongea nae kwanza, alichokifanya ni kuanza kumwangalia vizuri hali ambayo ilionekana kumkasirisha Benedict.



    “Unafanya nini shambani kwetu?” Jamaa yule alimuuliza Benedict swali jingine.



    “Nilikuwa napita njia”



    Jamaa alibaki kimyahuku akiendelea kumwangalia Benedict na kisha kuwageukia wenzake na kuanza kucheka. Vicheko vile viliendelea kwa sekunde kadhaa, wakanyamaza. Wasiwasi ukazidi kukaa ndani ya moyo wa Benedict, amani ambayo alikuwa moyoni mwake ilikuwa imetoweka kabisa.



    “Nadhani u mgeni maeneo haya”



    “Ndio”



    Yule jamaa hakutaka kuendelea kumuuliza maswali zaidi, alichokifanya ni kuanza kumuelekeza Benedict njia ya kuelekea Bagamoyo Mjini. Benedict alitulia huku akionekana kuyafuatilia maelekezo yale kwa makini. Alitumia sekunde kadhaa kutoa maelekezo yale, alipomaliza akawageukia wenzake na kuanza kucheka tena.



    “Unamjua Bi Mwenda?” Kijana yule alimuuliza Benedict.



    “Hapana”



    “Sawa”



    “Naomba uniambie kuhusu huyo Bi Mwenda” Benedict alimwambia kijana yule.



    “Sikiliza kijana, hautakiwi kujua kitu chochote kile kuhusu huyu bibi. Kumbuka tu kwamba hautakiwi kupita katika mashamba yake: Jamaa yule alimwambia Benedict maneno ambayo yalionekana kumuogopesha zaidi kuhusu Bi Mwenda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nitayajua vipi mashamba yake?”



    “Makubwa sana. Yamezungukwa na miti mingi mirefu” Kijana yule alimwambia Benedict.



    “Sawa”



    Safari ya kuelekea Bagamoyo ikaendelea zaidi na zaidi. Jua lilikuwa kali lakini Benedict hakutaka kupumzika sehemu yoyote ile. Alipita katikati ya miti na sehemu zilizokuwa na nyasi ndefu ndefu lakini hakutaka kusimama. Kichwa katika kipindi hicho kikaanza kumfikia Bi Mwenda ambaye alionekana kuogopwa na vijana ambao alikuwa amekutana nao.







    Kutokana na mwanga mkali wa jua, joto mwilini mwake likazidi kuongezeka jambo ambalo lilimpelekea kuivua fulana yake na kisha kuiweka begani na kuendelea na safari yake. Jasho lilikuwa likizidi kumtiririka mwilini mwake lakini Benedict hakuonekana kujali kitu chochote kile. Safari yake ya kuelekea Bagamoyo Mjini ilikuwa ikiendelea zaidi na zaidi. Benedict alitembea kwa muda wa dakika kadhaa na kufika katika eneo ambao lilikuwa na shamba moja kubwa ambalo lilikuwa limezungukwa na miti mingi mirefu.







    Benedict akasimama na kisha kuanza kuliangalia shamba lile. Tayari akili yake ikamwambia kwamba shamba lile lilikuwa ni shamba la Bi Mwenda, Bibi ambaye alikuwa ametahadharishwa na vijana wale kutokupita katika shamba lake. Benedict akaangalia pembeni mwa shamba lile na kuona kama kulikuwa na njia nyingine ya kupita lakini hakukuwa na njia yoyote ile, njia ambayo ilikuwepo mahali hapo ilikuwa katikati ya shamba lile.







    Hakujua sababu ambazo ziliwapelekea vijana wale kumkataza kupita katika njia ya shamba lile. Benedict akapiga moyo konde na kisha kuanza kupita katika njia iliyokuwa katika shamba lile lenye ukubwa wa hekali zadi ya thelathini. Ghafla huku akiwa amepiga hatua kadhaa, mwili wake ukaanza kusisimka, jasho likaanza kuongezeka mwilini mwake.







    Benedict hakusimama, alizidi kupiga hatua zaidi na zaidi. Huku akiwa amekwishapiga hatua zaidi ya themanini, ghafla akaanza kusikia milio tofauti tofauti nyuma yake. Kwa haraka akageuka, kundi kubwa la nyui lilionekana angani. Benedict hakutaka kutembea, akaanza kukimbia kusonga mbele. Kundi lile kubwa la nyuki likaanza kumkimbiza, Benedictalizidi kukimbia aidi na zaidi, ghafla katika hali ambayo hakuifahamu ilisababishwa na nini, akaanza kukosa nguvu na kuanguka chini na kundi lile kubwa la nyuki kumfuata na kuanza kumuuma hali ambayo ilimpelekea kupoteza fahamu shambani pale.







    Benedict alikuja kupata fahamu baada ya masaa matatu kupita. Akayafumbua macho yake na kuanza kuangalia kila kona mahali pale alipokuwa. Akabaki akishangaa tu, sehemu ambayo alikuwepo katika kipindi hicho ilikuwa tofauti na sehemu ambayo alikuwepo katika kipindi kilichopita. Alikumbuka vizuri kwamba alipoteza fahamu kakiwa shambani katika kipindi ambacho alishambuliwa na nyuki, lakini katika kipindi hiki, hakuwa shambini .



    Benedict akainuka pale kitandani na kuanza kujaribu kutembea chumbani mule, alijua fika kwamba alikuwa ameumwa na nyuki mwili mzima, cha ajabu katika kipindi hicho, hakuwa akisikia maumivu hata mara moja, na kitu ambacho kilikuwa kimemshangaza kuliko vyote, mwili wake wala haukuwa umevimba. Benedict alibaki kwa muda huku akiuangalia mwili wake, hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona, hakukuwa na uvimbe wowote ule, hapo ndipo alipokuja kugundua kwamba inawezekana kulikuwa na kitu cha ajabu kilikuwa kimetokea.



    Huku akifikiria hayo, hapo ndipo ambapo jina la Bi mwenda likaanza kumjia kichwani hasa mara baada ya vijana wale kumwambia kwamba sehemu ya shamba ambalo alikuwa akitaka kuvuka kilikuwa ni sehemu ya shamba la Bi Mwenda, Bibi ambaye alikuwa akiogopeka sana na vijana wa hapo, tena inawezekana na sehemu yote. Benedict akalifuata dirisha lililokuwepo chumbani pale na kisha kuanza kuchungulia nje, macho yake yakatua kwa mwanamke ambaye alikuwa akitwanga mpunga, moja kwa moja Benedict akajua kwamba yule ndiye alikuwa yule mwanamke ambaye alikuwa akizungumziwa na vijana wale.



    Benedict akaamua kurudi kitandani pale huku uso wake ukiwa bado kwenye wasiwasi mwingi. Hakutaka kumuamini kabisa mwanamke yule kwani kwa jinsi ambavyo alikuwa akitafutwa ndani ya jiji la Dar es Salaam, aliamini kwamba kulikuwa na uwezekano kuwa hata Bi Mwenda nae angeweza kumsaliti kama alivyofanya hamidu. Mara baada ya kukaa kwa dakika chache, Bi Mwenda akaingia ndani ya chumba kile, macho yake yalipotua kwa Benedct ambaye alikuwa amekaa kitandani, akatoa tabasamu pana.



    Ingawa Bi Mwenda alikuwa ametoa tabasamu pana ambalo aliamini lingemfanya Benedict kuwa na amani ndani ya chumba kile, lakini bado Benedict hakuonekana kuwa na amani. Moyo wake ulikuwa ukimuogopa sana Bi Mwenda, kwake, hakuonekana kuwa mwanamke mzuri. Be mwenda akaonekana kuigundua hali ambayo alikuwa nayo Benedict katika kipindi hicho, alichokifanya ni kuanza kumtoa wasiwasi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usiogope Benedict” Bi Mwenda alimwambia Benedict huku akimsogelea.



    Benedict akaonekana kuogopa zaidi, hakujua ni kwa jinsi gani Bi Mwenda alikuwa amelifahamu jina lake. Kwa haraka haraka Benedict akaanza kuyapitisha macho yake katika kila kona ndani ya chumba kile kuona kama kulikuwa na gazeti lililokuwa na picha yake au hata picha zake zenyewe, hakuona picha wala gazeti lolote lile jambo ambalo likazidi kumuongezea hofu zaidi.



    Unaendeleaje?” Bi Mwenda alimuuliza Benedict ambaye wala hakujibu kitu chochote kile zaidi ya kuendelea kuwa na wasiwasi mwingi moyoni mwake



    Bi Mwenda hakuonekana kujali sana, alichokifanya ni kutoka ndani ya chumba kile na kisha kuelekea nje. Benedict akabaki kimya huku akiangalia katika kila kona ndani ya chumba kile. Wazo ambalo lilikuwa limemjia katika kipindi hicho lilikuwa ni kutoroka tu.



    Hakuwa radhi kujiona akiendelea kuwa ndani ya chumba kile, sehemu ambayo wala hakuwa nayo huru kabisa. Katika kila njia za kutorokea ambazo alikuwa akizifikiria, akaosa kabisa jibu ni kwa namna gani angeweza kutoroka ndani ya chumba kile ambacho kwake wala hakikuonekana kuwa na usalama.



    Huku akiwa akifikiria hili na lile, mlango ukafunguliwa na Bi Mwenda kurudi tena ndani ya chumba kile. Benedict akabaki kimya kwa muda huku akimwangalia Bi Mwenda ambaye alikuja na maji na kisha kumpa. Mara ya kwanza Benedict akataka kuogopa kuyanywa maji yale, akapiga moyo konde na kuyanywa kwani alijua fika kwamba mwanamke yule angekuwa na nia mbaya kwake, basi angeweza kufanya chochote kile katika kipindi ambacho alikuwa amepoteza fahamu.



    “Najisikia vizuri sasa” Benedict alimwambia Bi mwenda.



    “Nashukuru Mungu kwa hilo” Bi Mwenda alimwambia Benedict.



    “Kuna kitu ningeomba kukuuliza kama hautojali” Benedict alimwambia Bi Mwenda.



    “Uliza tu”



    “Hivi umenijua vipi? Uliniona katika magazeti au?”



    “Hapana. Nimekujua kipindi kirefu sana kilichopita japokuwa baadae nilikuja kukujua zaidi kupitia magazeti. Najua kwamba umefanya mambo mengi ambayo yameiumiza mioyo ya Watanzania. Mwili wako kwa sasa umekuwa lulu, kila mtu anakutafuta kwa kuamini kwamba kama mtu yeyote atafanikiwa kukupata basi atakuwa amepata utajiri katika maisha yake” Bi mwenda alimwambia Benedict.



    “Kwa nini umeamua kunisaidia?” Lilikuwa swali jingine lililotoka kwa Benedict.



    “Kwa sababu nataka umpeleke mtoto wangu kwa mama yake mkubwa aishie Mombasa” Bi Mwenda alimjibu Benedict ambaye akaonekana kushtuka.



    “Nimpeleke mtoto wako! Hauoni kama nitakamatwa kirahisi na kufikishwa mbele ya sheria?” Benedict alimwambia Bi Mwenda.



    “Usijali. Mtoto wangu ni mdogo sana, najua kuna uwezekano asionekane kwa watu wengine zaidi yako. Nitahitaji sana umfiche mtoto wangu asiweze kuonekana katika maisha yako yote ya huko uendapo” Bi Mwenda alimwambia Benedict.



    “Na vipi kama ataonekana?”



    “Utakufa papo hapo” Bi Mwenda alimwambia Benedict ambaye akaonekana kushtuka zaidi.



    “Sasa nitaweza kumficha vipi asionekane kwa watu? Hauoni kama hilo ni jambo gumu sana?” Benedict alimuuliza bi mwenda huku dhahiri akionekana kushtuka.



    “Nisubiri” Bi Mwenda alimwambia Benedict.



    Bi mwenda akainuka mahali hapo na kuanza kuelekea katika chumba kingine, Benedict alibaki kimya ndani ya chumba kile, tayari akili yake kwa wakati huo ilionekana kuchanganyikiwa kupita kawaida. Maneno ambayo aliyaongea Bi Mwenda yalionekana kumchanganya kupita kawaida. Ingewezekana vipi kumchukua mtoto na kumpeleka mpaka Mombasa bila kuonekana na macho ya watu? Katika kila kitu ambacho Benedict alikuwa akijiuliza mahali hapo, alikuwa akikosa jibu kabisa.



    Bi Mwenda wala hakuchukua muda mrefu sana akarudi mahali hapo huku akiwa na tunguli moja ambayo alikuwa ameishika. Benedict akaonekana kushtuka kupita kawaida. Tayari hapo kukaonekana kuwa na matatizo makubwa. Alijua fika kwamba alizaliwa katika familia ya mchungaji, familia ambayo ilimjua Mungu haswa, sasa ilikuwa vipi siku ya leo akubali kwa moyo mmoja kubebeshwa tunguli ile. Alichoamua ni kukaa kimya na kumsikiliza kitu alichokuwa akikitaka Bi Mwenda.



    Bi Mwenda akakaa chini na kisha kuanza kuiangalia tunguli ile. Alichokifanya ni kuingiza mikono ndani na kisha kuitoa hirizi moja iliyofungwa katika kitambaa chekundu na kisha kuanza kuiangalia. Mapigo ya moyo ya Benedict kwa wakati huo yalikuwa yakimdunda kupita kiasi, hakuamini kama siku hiyo alikuwa akiiona hirizi na hicho ndicho kitu ambacho alitakiwa kupewa kwa wakati huo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Huyu ndiye mtoto wangu. Mtoto huyu anaitwa Zubeda na ningependa mpelekea kwa mama yake mkubwa aishie mjini Mombasa” Bi Mwenda alimwambia Benedict.



    Benedict akashusha pumzi ndefu, akaanza kuiangalia hirizi ile ambayo aliishika Bi mwenda. Mapigo ya moyo wa Benedict bado yalikuwa yakidunda kwa kasi kupita kawaida, kila alipokuwa akiiangalia hirizi ile ilionekana kumuogopesha kupita kawaida.



    “Mtoto wangu ana nguvu sana. Najua utakapotoka nae mahali hapa utaweza kuona mambo mengi ya ajabu. Kila mtu anamtaka huyu mtoto wangu ambaye anaonekana kuwa wa thamani sana katika maisha ya ulimwengu ambao ninautumikia. Najua utaweza kukutana na mambo mengi ya ajabu ila hautakiwi kuogopa, kitu ninachokitaka ni kumfikisha Zubeda kwa mama yake mdogo na kila kitu kitakuwa safi kama unavyotaka kiwe” Bi Mwenda alimwambia Benedict.



    “Kwa hiyo itabidi niiweke mfukoni?”



    “Hapana. Ukimuweka mfukoni utakuwa unamvunjia heshima, atatakiwa kuwa katika mikono yako tu” Bi mwenda alimwambia Benedict.



    “Nitawezaje kumshika mpaka naingia Mombasa? Naona mtihani mkubwa sana” Benedict alisema.



    “Usijali. Nitamfunga mkononi mwako” Bi Mwenda alimwambia Benedict.



    Alichokifanya Bi Mwenda ni kusimama na kisha kuuchukua mkono wa Benedict na kisha kuanza kumfunga hirizi ile ambayo alimwambia kwamba yule alikuwa ni mtoto wake ambaye alikuwa akimpenda na kumthamini, Zubeda. Muda mwingi Benedict alikuwa akitetemeka kupita kiasi, alikuwa na woga mwingi kwa kuona kwamba alikuwa akishirikishwa kufanya mambo ya kishirikina kinguvu.



    Mara alipofungwa hirizi ile katika mkono wake wa kushoto, hapo hapo Bi Mwenda akaondoka na kisha kuelekea chumbani, aliporudi, alikuwa na kipochi mkoni ambacho akakifungua na kutoa kiasi cha shuilingi laki mbili na kumkabidhi Benedict.



    “Hii kwa ajili ya chakula pamoja na nauli” Bi Mwenda alimwambia Benedict.



    “Nashukuru sana”



    “Ila kumbuka kwamba hatakiwi mtu yeyote kumuona”



    “Nimekuelewa. Sasa nitajuaje huko anapokaa huyo mwanamke ambaye nitatakiwa nimfikishie huyu mtoto wako?” Benedict aliuliza.



    “Utapajua tu. Yaani nyumba ya kwanza ambayo utaingia ndio itakuwa nyumba yenyewe. Utakapomfikisha hapo, mwambie kitu chochote utakacho nae atakufanyia” Bi Mwenda alimwambia Benedict a,baye alionekana kutokuelewa vizuri.



    “Kwa hiyo nyumba ya kwanza nitakayoingia ndio yenyewe?”



    “Ndio”



    “Ipo mtaa gani?”



    “Mtaa wa Tangana”



    “Na huyo mwanamke anaitwa nani?”



    “Swaumu” Bi Mwenda alimwambia Benedict.



    Benedict hakutaka kuendelea kukaa mahali hapo, kwa sababu alikuwa amekwishapatiwa kila kitu cha muhimu ambacho alikuwa akikihitaji, akaanza safari ya kuelekea mjini Mombasa ambapo huko angepitia Tanga. Katika kipindi chote hicho ambacho Benedict alikuwa ameanza safari, bado hakuwa akijisikia uhuru kabisa. Hakuamini kama yeye, mtoto wa mchungaji siku hiyo alikuwa amebebeshwa hirizi mkononi mwake.



    Njia nzima Benedict alikuwa akiangalia huku na huko, bado hofu ya kutafutwa na polisi pamoja na wananchi ilikuwa ikimsumbua moyoni mwake. Kila wakati alikuwa akiiweka vizuri kofia yake ambayo wala hakutaka imvuke kabisa pamoja na miwani ya jua ambayo alikuwa nayo usoni.



    Safari yake bado ilikuwa ikiendelea, tena kwa miguu, hakutaka kupanda basi kwa kuhofia kukamatwa. Alikuwa akipita porini porini huku akikatiza maboda mpaka pale ambapo akaanza kuachana na pori na kutokea katika sehemu ambazo zilikuwa na nyumba mbalimbali. Benedict akawa na uhakika kwamba kwa wakati huo alikuwa ameanza kukaribia Bagamoyo mjini, sehemu ambayo angepanda daladala na kuelekea Tanga kabla ya kuingia Mombasa.



    Njiani, picha zake bado zilikuwa zikionekana zimebandikwa katika kila kona huku kiasi cha shilingi milioni ishirini kikiwa bado kimeahidiwa kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa kwake. Japokuwa alikuwa amevaa kofia na miwani lakini bado hakuwa na amani hata kidogo, alikuwa akihofia kupita kawaida. Katika kipindi hicho, tayari akajiona kuwa na sababu ya kupata kuelekea Mombasa. Kipindi cha nyuma alifikiria sana kuelekea Mombasa lakini wala hakujua ni mahali gani ambapo angefikia na kuanzisha maisha yake upya.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kipindi hiki, tayari alikuwa amekwishapata sababu na mahali pa kufikia, sehemu ambayo aliamini kwamba angekaribishwa na kuishi hapo. Ila kichwani mwake bado kuna jambo moja ambalo lilikuwa likimtatiza sana. Maneno aliyoambiwa na Bi Mwenda kwamba katika nyumba yoyote ile ambayo angeingia ndani ya mji wa Mombasa basi ndio ingekuwa nyumba hiyo hiyo ambayo alitakiwa kufika mahali hapo na kisha kuiacha ile hirizi ambayo alikuwa amepewa.



    Benedict hakuchoka kujiuliza maswali juu ya jambo hilo ambalo kwake likaonekana kumtatiza kupita kawaida. Ingekuwa vipi jambo hilo liwezekane na wakati kila alipokuwa akilifikiria, lilionekana kuwa jambo moja gumu ambalo halikuwa likiwezekana kabisa. Angejua vipi kama nyumba fulani ndiyo ambayo alitakiwa kuingia? Angejua fipi kama nyumba fulani ndio ambayo ilikuwa nyumba ya Bi Swaumu ambayo alikuwa ametumwa? Katika kila kitu ambacho alikuwa akijifikiria katika kipindi hicho, Benedict hakuwa na jibu lolote lile.



    “Ngoja nione ili nijue kitu gani kitatokea” Benedict alijisemea katika kipindi ambacho alianza kupiga hatua kuifuata daldala ambayo ilikuwa ikielekea Tanga.



    Benedict akatulia ndani ya daladala ile mpaka pale ilipowashwa na kisha kuanza safari ya kuelekea Tanga. Ndani ya daladala ile bado stori kuhusiana na tukio la kulichoma moto kanisa zilikuwa zikiendelea kuzungumzwa, bado tukio lile lilionekana kuiumiza mioyo ya Watanzania ambao walikuwa wamezoea kuishi kwa amani na upendo bila hata kuumizana mioyo yao.



    Kadri alivyokuwa akiendelea kuzisikia stori zile na ndivyo ambavyo akaanza kukumbuka kitu kimoja ambacho alikiona kuwa cha umuhimu sana kufanyika. Hapo akaanza kumkumbuka msichana Judith ambaye alisema kwamba alitaka kubakwa na mchungaji Matimya ndani ya ofisi yake. Bado Benedict alikuwa na uhakika kwamba jambo lile wala halikuwa la kweli kabisa bali kulikuwa na mtu ambaye alikuwa amesababisha yale yotye kutokea. Moyoni mwake, kuanzia wakati huo akajiona akiwa na mzigo mkubwa sana wa kumpata mtu ambaye alikuwa nyuma ya tukio zima.



    “Wa kwanza Judith. Lazima nimtafute Judith. Yeye nae si mhusika! Nae kwanza lazima nimuue kama hajafa katika kanisa lile” Benedict alijisemea huku gari likiendelea na safari ya kuelekea Tanga.



    Walichukua masaa mawili wakawa wamekwishafika Tanga ambapo Benedict akateremka na kisha kuanza kuelekea katika mghahawa fulani mdogo wa mama ntilie na kisha kuanza kuagiza chakula. Alipoletewa chakula kile, akaanza kula kwa fujo kuashiria kwamba katika kipindi hicho alikuwa na njaa kali sana.



    Benedict alikula haraka haraka mpaka katika kipindi ambacho akaanza kuliona kundi la watu kumi na moja likianza kuja ndani ya mghahawa ule huku wakiwa wameshika karatasi kadhaa mikononi mwao, tena wakiwa wanakuja huku wakiwa na utingo wa daladala ile ambayo alikuwa amepanda katika kipindi kichache kuja mahali hapo.



    Mara baada ya Benedict kuuparamia ukuta ule akafanikiwa kuingia katika eneo la hoteli ile ya Casanova. Akaanza kupiga hatua kuelekea katika upade mwingine ambao ulikuwa na geti. Hata kabla hajapiga hatua zaidi kuelekea kule getini, akapigwa na mshtuko mara baada ya kuliona gari moja likiingia ndani ya eneo la hoteli ile.



    Benedict akajificha huku wasiwasi ukianza kumkamata. Milango ya gari lile ikafunguliwa na vijana watatu kuteremka na kisha kuanza kuongea na mlinzi. Wasiwasi zaidi ukaonekana kumshika, alichokifanya ni kuanza kuuangalia ukuta ambao ulikuwa ukitenganisha hoteli ile na ukumbi na kisha kuuparamia huku akionekana kutokuziogopa seng’enge zilizokuwa ukutani pale.



    Akayapeleka macho yake katika upande ule wa ukumbi, watu zaidi ya ishirini walikuwa wamekaa vitini huku wengine wakitengeneza jukwaa la burudani. Hakuonekana kujali ncha za seng’enge zile, akarukia upande wa pili. Mwili wake ulichomwachomwa na ncha za seng’enge zile, damu zikaanza kumtoka.



    Benedict akaanza kupiga hatua kukifuata kiti kimoja kilichokuwa ndani ya ukumbi ule huku kofia yake aina ya Malboro bado ikiwa kichwani mwake. Sehemu ile ikaanza kuonekana kuwa ulinzi mkubwa kwake. Baada ya dakika thelathini kupita, akageuka nyuma na kuanza kuangalia pale ukutani alipokuwa amepandia kuingilia ukumbini hapo.



    Benedict akapigwa na mshtuko hasa mara baada ya macho yake kugongana na macho ya mtu ambaye alionekana kumtilia mashaka. Wala hazikupita hata sekunde kumi, yule mtu akaacha kuchungulia. Wasiwasi ukamshika Benedict, akajiona kuwa karibu kukamatwa, alijua ni lazima mtu yule angezunguka upande wa pili na kuingilia kupitia mlango wa mbele. Akili yake haikufikiri kitu kingine zaidi ya kitu kimoja tu ambacho kingemfanya kutoka salama mahali pale.



    Kwa haraka haraka Martin akashuka ukutani na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea kule wenzake walipokuwa. Mlinzi hakuonekana kuelewa kitu chochote ambacho kilikuwa kinaendelea, alichokifanya ni kuanza kumfuata Martin mpaka kule lilipokuwa gari walilokuja nalo mahali hapo.



    “Mbona haraka hivyo?” Sabrina aliuliza huku akionekana kumshangaa Martin



    “Shukeni……Twendeni”



    “Wapi?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kule. Benedict yupo kule” Martin alijibu.



    “Unasemaje?”



    “Twendeni”



    Martin hakutaka kupoteza muda mahali hapo, alichokifanya ni kuanza kuelekea nje ya hoteli ile huku akiwa kwenye mwendo wa kasi. Sabrina na Moody hawakutaka kubaki mahali pale, walichokifanya ni kuanza kumfuata Martin



    Mara baada ya kufika katika geti la kuingilia katika eneo la ukumbi ule, wakajitambulisha kwa mlinzi huku wakimuonyeshea vitambulisho vyao. Mlinzi hakuonekana kuamini kabisa, moyo wake ulikuwa mgumu kuamini kama kweli mpelelezi kama mpelelezi angeweza kujitangaza wa mtu kwamba alikuwa akifanya kazi hiyo.



    “Kuna mtu tumekuja kumchukua” Martin alimwambia mlinzi.



    “Sitowaruhusu hadi mtoe viingilio” Mlinzi aliwaambia.



    Kila mmoja akaonekana kumshangaa mlinzi, maneno ambayo aliongea yalionekana kuwashangaza. Hawakutegemewa kudaiwa viingilio katika geti lile kwani walijua fika kwamba viingilio vilikuwa vikichukuliwa katika mlango wa mwisho kuingilia ukumbini mule kwani baadhi a magari yalikuwa yamepaki katika eneo kubwa la ukumbi ule.



    “Lakini sisi ni map……” Martin alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, mlinzi akaingilia.



    “Sogeeni kwanza nifungue geti” Mlinzi aliwaambia.



    Geti likafunguliwa na teksi iliyokuwa na vioo vilivyokuwa na tinted kutoka. Wapelelezi wakazidi kuchanganyikiwa zaidi, walichokifanya ni kuacha kuongea kwa kauli za kulazimisha, wakaanza kuongea na mlinzi kinyenyekevu. Walimbembeleza mlinzi kwa dakika tatu na ndipo akawaruhusu kuingia.



    Wakaanza kupiga hatua za haraka haraka kuufuata mlango mkuu wa kuingilia ndani ya ukumbi ule. Mlangoni wala hakukuwa na mtu yeyote yule jambo lililowafanya kuingia hadi ndani. Bado watu walikuwa wakiendelea kulipamba jukwaa ukumbini mule kwa ajili ya muziki ambao ulitarajiwa kupigwa na bendi ya Twanga Pepeta usiku wa saa nne.



    Walichokifanya ni kuanza kumtafuta Benedict ndani ya ukumbi ule, kitu cha kushangaza, Benedict hakuonekana. Hawakutaka kuridhika, walichokifanya ni kuelekea mpaka chooni lakini napo huko wala Benedict hakuonekana hali ambayo ilianza kuwachanganya.



    “Lakini si ulisema ulimuona! Mbona hayupo?” Moody alimuuliza Martin.



    “Hata mimi mwenyewe na shangaa. Nilipochungulia mwanzao, alikuwa amekaa hapa” Martin alijibu.



    “Ulipomuona alikuona?”



    “Ndio”



    “Basi atakuwa ametoroka” Moody alisema.



    Hawakutaka kuendelea kubaki ndani ya ukumbi ule, walichokifanya ni kuanza kuelekea nje ya ukumbi ule hali iliyowafanya watu waliokuwa mule ukimbini kuanza kuwashangaa. Walichokifanya ni kuanza kumtafuta katika kila eneo ndani ya eneo la ukumbi ule lakini napo Benedict hakuonekana. Hawakuwa na jinsi tena, walichokifanya ni kuanza kupiga hatua kumfuata baunsa ambaye alikuwa akiongea na rafiki yake.



    “Tunamtafuta Benedict Matimya. Mmemuona maeneo haya?” Martin aliuliza.



    “Benedict!”



    “Ndio”



    “Yule anayetafutwa?”



    “Ndio”



    “Acheni utani bwana. Mnajua kwamba mnazizungumzia milioni ishirini hapo?”



    “Tunalijua hilo. Nilimuona hapa muda mchache uliopita. Alikuwa amevaa kofia ya Malboro yeye rangi nyekundu” Martin aliwaambia.



    Maneno aliyoongea Martin yakaonekana kuwashtua, mtu ambaye alikuwa amevaa kofia aina ya Malboro ambayo ilikuwa na rangi nyekundu wala hakuwa mgeni machoni mwao, walimuona kipindi kichache kilichopita. Baunsa alibaki akiwaangalia mara mbili mbili walinzi wale huku akinekana kutokuamini kile ambacho kilikuwa kikizungumziwa.



    “Kumbe yule alikuwa Benedict?”



    “Ndio”



    “Mna uhakika?”



    “Ndio”



    “Nendeni Blue Diamond hoteli pale Magomeni. Alichukua teksi hapa” Baunsa aliwaambia.



    Unamaanisha ile teksi ambayo iliondoka muda mchache uliopita”



    “Ndio hiyo hiyo. Yeye ndiye aliyeikodi kumpeleka hotelini” Baunsa aliwaambia.



    Martin na wenzake wakaanza kupiga hatua kulifuata gari lao huku kila mmoja akionekana kuzidi kuchanganyikiwa. Tayari Benedict kwao akaonekana kuwa mgumu kupatikana tofauti na jinsi ya walivyokuwa wakidhani mwanzoni. Moody akashikilia usukani kama kawaida yake na safari ya kuelekea katika hoteli ya Blue Diamond kuanza.



    “Ni lazima tumkamate” Martin alisema huku akionekana kukasirika.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Benedict hakutaka kuwa macho tena, macho yake yalikuwa na usingizi mwingi, alichokifanya kwa wakati huo ni kulala tu. Daladala ile iliendelea na safari zaidi na zaidi huku barabara yote ikiwa ni lami. Walikwenda zaidi na zaidi na baada ya dakika arobaini na tano wakaanza kuingia mpakani, mpaka wa Tanzania na Kenya upande wa mashariki. Hapo ndipo kulikuwa mwisho wa safari ile, abiria walitakiwa kuteremka.



    Benedict akashtuka, alipoangalia nje, akaona watu wakianza kuteremka na hivyo nae pia kuteremka. Akasimama nje ya daladala ile na kisha kuanza kuangalia huku na kule. Idadi ya watu mpakani pale ilikuwa kubwa huku wanajeshi wakiwa wanatembea huku na kule kama kuhakikisha usalama mahali pale. Benedict hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya, ni kweli kwamba alikuwa akitamani sana kuvuka mpakani pale na kisha kuingia upande wa Kenya ambapo huko angeendelea na safari yake mpaka kufika Mombasa mjini ambapo huko angeangali ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya.



    Alichokifanya Benedict ni kuanza kuwatafuta wenyeji wa mahali pale ambao aliamini kwamba wangekuwa wanafahamu mambo mengi kuhusiana na mahali pale ili hata kama kungekuwa na njia za panya basi angeweza kupita kutokana na kutokuwa na kibari chochote kile mkononi mwake. Mara baada ya kukaa kwa kipindi kirefu akiangalia huku na kule kwa lengo la kuwatafuta wenyeji, akaamua kuwafuata vijana wawili ambao walikuwa wamekaa katika sehemu moja pembezoni mwa ukuta wa nyumba moja wakila maembe.



    “Mambo vipi!” Benedict aliwasalimia mara baada ya kuwafikia.



    “Poa. Inakuwaje?”



    “Kama kawa. Samahanini kidogo” Benedict aliwaambia.



    “Bila ya samahani”



    “Nataka kuingia nchini Kenya kwa njia za panya” Benedict aliwaambia.



    “Kwa nini utumie njia za panya?”



    “Kwa sababu sina vibali vya kuniruhusu kuingia”



    “Umetokea wapi?”



    “Dar es salaam”



    “Sasa umetokea Dar es Salaam halafu sio mjanja!” Kijana mmoja alisema na wote kuanza kucheka.



    “Si unajua huu ni uwanja wa ugenini”



    “Sikiliza bro. Kuvuka hapa hata bila kibali unavuka tu” Kijana mmoja alimwambia Benedict.



    “Kivipi?”



    “Una karatasi jekundu?”



    “Ndio nini hilo?” Benedict aliuliza swali ambalo liliwafanya vijana wale kuanza kucheka huku wakiangaliana.



    “Umetoka Bongo hata karatasi jekundu hulijui! Okey! Una Msimbazi hapo?”



    “Kumbe umemaanisha hivyo? Ninalo”



    “Tupe moja tukufanyie mishe ya fasta fasta” Kijana yule alimwambia Benedict ambaye bila kuchelewa akaingiza mkono mfukoni na kutoa shilingi elfu kumi na kumgawia yule kijana ambaye akaanza kuondoka mahali hapo kuelekea katika sehemu ambayo ilionekana kuwa na wanajeshi kadhaa. Alipofika pale, akaanza kuongea na mwanajeshi mmoja na kisha kumuita Benedict.



    “Una shilingi ngapi hapo?” Mwanajeshi yule alimuuliza Benedict.



    “Numekwishampa mshikaji elfu kumi” Benedict alimwambia.



    “Hiyo yake. Nataka yangu ya kukufanyia mishemishe”



    “Kwani wewe unahitaji kiasi gani?”



    “Nahitaji elfu sitini”



    “Mbona nyingi hivyo?”



    “Si unataka kibali cha kuingia kwa Kibaki?”



    “Ndio”



    “Basi fanya elfu sitini. Fanya fasta fasta hata kabla wazushi hawajajaa” Mwanajeshi yule alimwambia Benedict.



    Alichokifanya mwanajeshi yule ni kumchukua Benedict na kisha kuanza kuelekea nae nyuma ya nyumba moja ambayo ilikuwa mahali pale na kisha kukabidhiwa zile fedha. Benedict akatakiwa kusubiri mahali hapo kwa ajili ya kibali ambacho mwanajeshi yule alikuwa amekwenda kumchukulia. Benedict alisubiri mahali pale kwa takribani dakika kumi, mwanajeshi yule akarudi huku akiwa na karatasi.



    “Kibali hicho cha kuvukia Kenya” Mwanajeshi yule alimwambia Benedict ambaye akaichukua karatasi ile na kuanza kuiangalia.



    “Hawatonisumbua?”



    “Hakuna kitu kama hicho. Nenda nacho, ukifika kwa wanajeshi wa Tanzania, waonyehsee halafu ukisogea kule kwa wanajeshi wa Kenya, waonyeshee pia” Mwanajeshi yule alimwambia Benedict.



    Benedict hakutaka kusbiri, alichokifanya ni kuanza kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na mabasi ambayo yalikuwa yakivuka mpakani pale. Alipofika mlangoni, mwanajeshi mmoja akamfuata na kisha kutaka kumuonteshea kibali cha kuingia nchini Kenya. Benedtct akaitoa ile karatasi huku akionekana kuwa na wasiwasi. Mwanajeshi yule alipoichukua tu na kuiangalia, hakuwa na swali, akamuachia na kumruhusu kuingia ndani ya basi lile huku akijiandaa kumpta utingo nauli yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hili basi linakwenda Nairobi. Wewe unaelekea wapi?”



    “Naelekea Mombasa”



    “Poa. Elfu kumi na nane”



    Benedict hakutaka kuchelewa, hapo hapo akaingiza mkono mfukoni na kisha kumgawia utingo yule kiasi kile ambacho kilikuwa kikihitajika. Baada ya basi lile kujaa, likaanza kuondoka mahali hapo na kuuvuka mpaka ule. Bado moyo wa Benedict haukuwa ukijisikia kuwa na furaha, alijua fika kwamba mbele kidogo kulikuwa na wanajeshi wa nchi ya Kenya ambao walikuwa na kazi ya kuhakiki vibali vyao.



    Kama alivyofikiria ndivyo ambavyo ilitokea, mara baada ya kufika kule mbele, wanajeshi wanne wakaingia ndani ya basi lile na kisha kuwaomba abiria kuwaonyeshea vibali vyao vya kuingia nchini Kenya. Benedict akatoa ile karatasi ambayo alikuwa amepewa na mwanajeshi yule wa Tanzania na kisha kumuonyeshea mwanajeshi mmoja ambaye alionekana kuridhika. Huo ukaonekana ndio mchezo mmoja mzuri ambao ulifanyika kwa Benedict kuingia nchini Kenya kinyemela, kwa njia ambazo wala hazikuwa na uhalali wowote ule.



    Aliingia nchini Kenya kirahisi sana lakini hakuwa akijua kwamba kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea mahali hapo, Bi Mwenda alikuwa akifanya mambo yake na kumpa urahisi wa kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea katika maisha yake. Basi likaanza safari ya kuelekea Mombasa mjini, muda wote Benedict alionekana kuwa mwenye furaha kupita kawaida. Alijiona kuwa na uhakika wa kuishi nchini Kenya bila matatizo yoyote yale.



    Hapo ndipo kichwa chake kilipoanza kufikiria namna ambayo angeweza kuipata nyumba ya Bi Swaumu ambayo ilikuwa hapo Mombasa katika mtaa wa Tangana. Benedict hakujua ni kwa namba gani angeweza kuipata sehemu hiyo, nchini kenya, hiyo ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia na wala hakuwa na ndugu yeyote yule jambo ambalo aliona kama ingekuwa ngumu sana kuipata sehemu yenyewe.



    Safari bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida mpaka wakaingia Changamwe, sehemu ambayo ilikuwa na njia ya kuingia Mombasa mjini. Majengo mengi ya kale ambayo yalikuwa yakionekana katika sehemu zile walizokuwa wakipita zilionekana kumkumbusha Benedict katika kipindi kile ambacho alikuwa darasani akisoma somo la Historia.



    Basi likaanza kuingia Mombasa mjini na kuchukua barabara ya Shimanzi ambayo ilikuwa ikielekea mpaka katika eneo la viwanda. Kila mmoja ndani ya gari alikuwa akijisikia uchovu mwingi kwa wakati huo, safari ile ya masaa sita ikaonekana kuwachosha kupita kawaida.



    Macho ya Benedict hayakuweza kutulia, yalikuwa yakiangalia katika kila kona kila sehemu ambapo basi lile lilikuwa likipita. Basi lilitembea zaidi na zaidi katika hiyo barabara ya Shimanzi mpaka pale walipoachana nayo na kuchukua barabara ya Beira ambayo wakaonganisha nayo mpaka kufika Tangana.



    Hapo ndipo palikuwa mwisho wa safari ya Benedict ambapo alikuwa ametumwa kuipeleka hirizi ambayo muda wote alikuwa nayo katika mkono wake huku ikiwa imefungwa vilivyo. Benedict akaanza kuangalia mazingira ya mtaa ule, vijana wengi walikuwa mahali hapo huku wakicheza karata huku wanawake wakifanya biashara mbalimbali. Benedict akabaki akiwa amesimama, hakujua ni upande gani ambao alitakiwa kuelekea katika kipindi hicho.



    Kwa sababu alikuwa katika nchi ngeni ambayo hakukuwa akimfahamu mtu yeyote, hakutaka kujisumbua tena kuvaa kofia yake ya malboro pamoja na miwani yake. Alichokifanya ni kuviacha vitu vile ndani ya basi lile na yeye kushuka bila kuwa navyo. Benedict hakujua afanye nini, alichokifanya ni kumuita kijana mmoja ambaye alikuwa akipita mbele yake.



    “Do you speak English? (Unaoongea Kingereza?)” Benedict alimuuliza kijana yule.



    “Yeah! What can I help you? (Ndio,! Unataka nikusaidie nini?)” Kijana yule alimuuliza.



    “I want to change my money from Tanzanian shillings to Kenyan shillings (Nataka kubadilisha fedha zangu kutoka shilingi ya Tanzania na kuziweka katika shilingi ya Tanzania)” Benedict alimwambia kijana yule.



    “So you want me to show you the place where you can change your money? (Kwa hiyo unataka nikuonyeshee sehemu ambayo utaweza kubadilisha fedha zako?)”



    “Yes (Ndio)”



    Kijana yule akaanza kumuelekeza Benedict sehemu ambayo ilikuwa na sehemu ambayo ingemuwezesha kubadilisha fedha zake. Benedict alikuwa makini kupokea maelekezo, alipoona kwamba ameelewa, akaanza kuelekea huko.



    Muda ulikuwa umekwenda sana, saa yake ilimuonyesha kwamba ilikuwa ni saa 9:25 alasiri. Benedict alikuwa akitembea kwa haraka haraka sana, hakutaka jioni imkute akiwa bado hajaingia ndani ya nyumba hiyo kwa ajili ya kumkabidhi Bi Swaumu kile ambacho alikuwa ameagizwa na Bi Mwenda kukifikisha.



    Baada ya dakika mbili, macho ya Benedict yakatua katika fremu ambayo iliandikwa ‘Bureau De Change’ kwa nje. Benedict akakenua meno yake na moja kwa moja kuanza kuifuata fremu ile ambapo nje kulikuwa na askari wawili ambao walikuwa wameshika bunduki. Mara baada ya kuufikia mlango wa kuingilia ndani ya fremu ile, akaufungua na kisha kuingia ndani.



    Benedict akaanza kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na kidirisha kidogo na kisha kuanza kuongea na mtu ambaye alikuwa ndani ya chumba kidogo. Mara baada ya mtu yule kuongea sana na Benedict, akaamua kutoka nje na kuanza kumwangalia vizuri Benedict usoni hali ambayo ilimfanya Benedict kuanza kuwa na wasiwasi mwingi.



    “Mmmh!” Mtu yule ambaye alikuwa na asili ya Kiarabu aliguna huku akiangalia ukutani.



    Benedict akayageuza macho yake na kuangalia katika ukuta ambao mtu yule alikuwa akiangalia, macho ya Benedict yakatua katika picha yake kubwa ambayo ilikuwa imebandikwa ndani ya fremu ile. Benedict akashtuka, mwili wake ukawa kama umepigwa ganzi, akaanza kutetemeka huku kijasho chembamba kikianza kumtoka.



    Tayari mambo yakaonekana kuharibika mahali hapo, taratibu, Benedict akaanza kupiga hatua za nyuma nyuma na kisha kuufungua mlango ule. Mzee yule hakutaka kukaa kimya, akaanza kupiga kelele. Benedict akatoka nje na kuanza kukimbia. Kelele zile ambazo zilikuwa zimesikika kutoka ndani zikawashtua askari wale ambao walikuwa nje, na kitendo cha Benedict kutoka ndani ya fremu ile huku akikimbia kikawafanya kufikiria kwamba alikuwa mwizi ambaye aliingia ndani ya fremu ile na kuiba fedha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bila kuuliza kitu chochote kile, askari wale wakaanza kumkimbiza Benedict ambaye alikuwa akikimbia kwa mwendo wa kasi. Muda wote walikuwa wakipiga kelele za kumtaka Benedict asimame lakini wala Benedcit hakutaka kusimama. Hapo ndipo wakaamua kutumia bunduki ambazo walikuwa nazo. Wakaanza kumfyatulia risasi, watu wote ambao walikuwa wakiisikia milio ya bunduki ile, wakaanza kukimbia ovyo.



    Benedict alikuwa akikimbia kwa mwendo wa kasi, hakutaka kukamatwa kijinga, ilikuwa ni bora hata apigwe risasi lakini si kujisalimisha. Kukamatwa nchini kenya kingekuwa kitu kibaya sana kwake ambacho kingemfanya kushangawa na watu wote kwamba alikuwa amefanikiwa kuikimbia tanzania na kukamatwa kizembe nchini Kenya.



    Benedict akazidi kukimbia zaidi huku akikata katika vichochoro ambavyo wala hakuwa akijua vilikuwa vikitokea sehemu ipi. Benedict alikimbia mpaka akachoka. Hakujua ni mahali gani ambapo alitakiwa kukimbilia kwa wakati huo.



    Huku akiendelea kukimbia, mara adhana ikaanza kusikika masikioni mwake kutoka katika msikiti mkubwa wa hapo Tangana. Benedict akajiona akipata nguvu za ziada, akaanza kukimbia kwa kukata vichochoro kadhaa huku mpaka pale ambapo alitokea katika msikiti huo, akavua viatu haraka haraka na kisha kuingia ndani ya msikiti ule.



    Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwake kuingia msikitini. Akaanza kupiga hatua kuelekea katika sehemu ambayo watu walikuwa wakitawaza na kisha kuanza kujiosha. Hakuwa akielewa kitu chochote kile zaidi ya kuwaiga watu kile ambacho walikuwa wakikifanya katika kipindi hicho. Mara baada ya kumaliza kutawaza, moja kwa moja nae akaingia msikitini na kuanza kuswali huku mwendo ukiwa ni ule ule wa kuiga.



    Askari wale waliendelea kumkimbiza Benedict huku wakiendelea kupiga risasi ambazo ziliwafanya watu kukimbia huku na kule. Kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba wangeweza kumkamata Benedict ambaye kwao alionekana kuwa mwizi aliyeiba ndani ya fremu ya mzee yule wa Kiarabu.



    Kitendo cha Benedict kuanza kuingia vichochoroni kikaonekana kuanza kuwachanganya, Benedict akaanza kupotea machoni mwao. Hawakutaka kukata tamaa, walichokifanya ni kuendelea kumkimbiza japokuwa hawakuwa na uhakika kama wangeweza kumpata.



    Benedict, kwao akaonekana kuwa mwenyeji wa vichochoro vile, walikimbia zaidi na zaidi lakini hawakuwa wamemuona. Walichoamua kukifanya ni kuanza kutembea kwa tahadhari, walikwishaona kwamba mtu ambaye walikuwa wakimkimbiza alikuwa amepotea machoni mwao.



    Askari wale wakatokea katika eneo ambalo lilikuwa na msikiti. Watu wengi walikuwa wakielekea ndani ya msikiti ule, idadi kubwa ya watu waliokuwa wakielekea katika msikiti ule ilitokana na siku hiyo kuwa ya Ijumaa, siku ambayo ilikuwa ikijulikana sana kwa Waislamu kwamba ilikuwa ni lazima kwenda msikitini kumuabudu Allah hata kama ulikuwa bize na mambo yako.



    Askari wale hawakutaka kuelekea sehemu yoyote ile, wakasimama mahali pale huku wakionekana kuchoka kupita kawaida. Waliendelea kuwaangalia watu ambao walikuwa wakiendelea kuingia ndani ya msikiti ule. Tayari wakaonekana kuwa na wasiwasi kwamba inawezekana kwamba mtu ambaye walikuwa wakimtafuta alikuwa ndani ya msikiti ule kutokana na kutokuwa na dalili za mtu yeyote kupita kuelekea katika njia nyingine mahali pale.



    Walichokifanya mahali hapo ni kuelekea katika kiambaza cha ukuta wa nyumba moja na kisha kutulia. Macho yao yalikuwa yakiangalia ndani ya msikiti ambpo waumini wa dini ya Kiislamu walikuwa wakiendelea kusujudu kama ishara ya kumuabudu Allah.



    Askari wale waliendelea kusubiri nje ya msikiti ule mpaka katika kipindi ambacho ibada ikamalizika na hivyo waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa msikitini kuanza kutoka nje. Kwa mbali, macho yao yakatua kusoni mwa Benedict ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakitoka huku uso wake ukionekana kuwa na wasiwasi.



    Macho yake yalipotua nyusoni mwa watu wale, Benedict akaonekana kushtuka, akarudi ndani ya msikiti ule. Askari wale hawakuonekana kukubali, walichokifanya ni kuanza kuelekea kule kulipokuwa na mlango wa kuingilia ndani ya msikiti ule. Walipofika, wakataka kuingia, wakazuiliwa mpaka pale ambapo wangevua viatu vyao, wakafanya hivyo na kisha kutaka kuingia tena.



    “Mbona mnatuzuia?” Waliwauliza wazee ambao walikuwa wakiwazuia.



    “Nyumba ya kumwabudu Allah. Hautakiwi kuingia na bunduki,. Hii ni nyumba ya amani, nyumba ya kuabudu na sio uwanja wa vita” Mzee mmoja aliyeonekana kuwa na busara aliwaambia. Hawakuwa na jinsi, wakaziacha bunduki zao nje na kisha kuingia ndani ya msikiti ule.



    Idadi ndogo ya watu bado walikuwepo ndani ya msikiti ule wakiwa wamejipumzisha huku wengine wakisoma koran na wengine wakiwa wameshika misaafu. Askari wale wakaangalia huku na kule, Benedict hakuwa akionekana machoni mwao.



    Hawakutaka kuishia hapo, wakaendelea kuangalia zaidi mpaka katika vyoo pamoja na sehemu za kutawazia lakini Benedict wala hakuonekana jambo ambalo likawafanya kujua kwamba mtu huyo alikuwa amekwishaondoka mahali hapo.



    Walichokifanya ni kutoka ndani ya msikiti ule, wakaanza kuvaa viatu vyao na kuchukua bunduki zao huku wazee wale waliokuwa pale nje wakionekana kuwashangaa. Nyuso za wazee wale zilionyesha kuwa na kitu fulani, walionekana kutaka kuongea jambo fulani.



    “Kuna nini?” Askari mmoja aliwauliza.



    “Kuna mtu mnamtafuta?”



    “Ndio”



    “Amevaa vipi?”



    “Suruali ya jinsi pamoja na fulana ya bluu”



    “Ameondoka sasa hivi. Ametoka katika ile sehemu ya kutawazia, amekimbia mara baada ya kuja hapa na kuvaa viatu vyake haraka haraka” Mzee mmoja aliwaambia.



    “Ameelekea wapi?”



    “Kule” Mzee yule alisema huku akinyoosha kidole katika upande wa Kaskazini.



    Hakukuwa na kitu cha kusubiria mahali hapo, tayari wakajiona kwamba walikuwa wameachwa kwenye mataa, walichoifanya, nao ni kuanza kukimbia kuelekea upande wa Kaskazini. Kila mmoja alikuwa na presha kwa wakati huo, walijua fika kwamba bosi wao alikuwa ameibiwa, hivyo walijitahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba mtu yule ambaye kwao walimuona kuwa mwizi wanamkamata.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Waliendelea kukimbia zaidi na zaidi mpaka kufika katika sehemu ambayo kwa mbali wakaweza kumuona Benedict akitembea kwa mwendo wa kasi. Walichokifanya ni kuongeza kasi zaidi ambayo ilimfanya Benedict kuanza kukimbia. Askari wale wakajiona wakipata nguvu zaidi na zaidi za kumkimbiza, wakaongeza kasi na kuanza kupiga tena risasi ambazo ziliwatawanyisha watu waliokuwa pembeni yao.



    Walimkimbiza Benedict zaidi mpaka pale ambapo wakamuona akiingia katika nyumba fulani. Askari wale walizidi kuelekea kule mpaka kuifikia nyumba ile na kisha kusimama nje ya nyumba ile. Wasiwasi ukaanza kuwashika, mioyo yao wakaihisi kama ikianza kuungua moto kila walivyokuwa wakiiangalia nyumba ile, wakaanza kutetemeka bila sababu huku mapigo ya mioyo yao ikidunda kupita kawaida.



    “Vipi tena?” Askari mmoja alimuuliza mwenzake.



    “Hata mimi sifahamu”



    “Mmmh! Hali hii si ya kawaida kabisa. Tuondoke” Askari mwingine alimwambia mwenzake.



    Watu wakaanza kutokea mahali pale na kisha kuanza kuwaangalia askari wale ambao walikuwa wamesimama nje ya nyumba ile. Kila mtu akaonekana kushtuka, hawakuamini kama askari wale walikuwa na uwezo wa kusimama nje ya nyumba ile, nyumba ya mtu ambaye alikuwa akiogopwa na kila mtu katika sehemu yote ya Mombasa.



    “Najisikia kufa kufa” Askari mmoja alimwambia mwenzake na baada ya muda wakajikuta wote wakianguka chini kama mizigo.



    “Hawakuwa wakimjua mmiliki wa nyumba hii nini?” mwanamke mmoja aliwauliza wenzake.



    “Hata mimi nashangaa. Ila kama nilimuona mtu fulani akiingia ndani ya nyumba hii” Mwanamke mwingine alisema.



    “Hakuna kitu kama hicho, utakuwa umeona vibaya, nyumba hii ni hatari tupu”



    “Sasa hawa askari kwa nini walisimama nje ya nyumba hii?”



    “Hata mimi mwenyewe sijui”



    Benedict alijikuta akianza kuishiwa nguvu hali ambayo aliona kwamba askari wale ambao walikuwa wakimkimbiza wangeweza kumfikia na hatimae kumata na kuanza kumpeleka katika kituo cha polisi ambapo simu ingepigwa nchini Tanzania na kisha kusafirishwa ambapo angefikia moja kwa moja mahakamani. Moyoni mwake hakujua kama watu wale walikuwa wakimkimbiza kwa kumdhania kwamba alikuwa mwizi ambaye alikuwa amemuibia bosi wao katika fremu ile ya kubadilishia fedha.



    Alichokifanya Benedict ni kuifuata nyumba moja ambayo ilikuwa imeachwa mlango wazi na kuingia ndani. Hakumjua mmiliki wa nyumba ile, alichokiona yeye ni kwamba endapo angefanuikiwa kuingia ndani ya nyumba ile basio maisha yake yangekuwa salama kabisa. Mara baada ya kuingia ndani ya nyumba ile, Benedict akaufuata mlango na kisha kuufunga.



    Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakimdunda kupita kawaida, alikuwa amejawa na hofu kwa kuona kwamba alikuwa akienda kukamatwa kama askari wale wangeamua kuingia ndani ya nyumba ile. Benedict akaanza kutembea katika kila sehemu ndani ya nyumba ile huku akiangalia sehemu ambayo angeweza kujificha kwa wakati huo. Alizunguka katika nyumba nzima, hakuona sehemu ambayo ingemfaa kujificha.



    Benedict akaonekana kuchanganyikiwa, akaona dhahiri kwamba angeweza kukamatwa na askari wale kama wangeamua kuingia ndani ya nyumba ile. Benedict hakutulia, kila wakati alikuwa akiangaika huku na kule tena akihema kwa nguvu hali iliyoonyesha kwamba alikuwa amechoka kupita kawaida.



    Ghafla Benedict akausikia mlango wa uani ukifunguliwa, moyo wake ukajawa na wasiwasi zaidi kwa kuona kwamba alikuwa akienda kuonekana na mwenyeji na hatimae kumtoa nje ya nyumba ile ambapo alijua fika kwamba askari walikuwa wakimsubiri atokea nje ya nyumba ile. Mwenyeji alipotokea mbele yake, alikuwa mwanamke mzee.



    Benedict akaanza kumsogelea mwanamke yule na kisha kuanza kumuomba amfiche kwani kulikuwa na watu wabaya ambao walikuwa wakimsubiri nje ya nyumba ile, watyu ambao walikuwa wakitaka kumkamata.



    “naomba unisaidie bibi” Benedict alimwambia mwanamke yule ambaye alikuwa akimwangalia tu.



    “Kuna nini?”



    “Kuna watu wananikimbiza” Benedict alijibu huku akiuangali angalia mlango.



    “Watu gani?”



    “Askari”



    “Wewe ni mharifu?”



    “Hapana”



    “Sasa kwa nini wanakukimbiza?”



    “Sijui kwa nini?”



    “Kwa hiyo wanakukimbiza bila sababu?”



    “Inawezekana”



    “Kwa hiyo mimi nikusaidie nini?”



    “Naomba unifiche”



    “Huwa siwafichi wadanganyaji” Mwanamke yule alimwambia Benedict.



    “Naomba unisaidi bibi yangu. Nitakupa chochote utakacho” Benedict alimwambia mwanamke yule.



    “Hahaha” Utanipa nini? Unafikiri una cha kunipa Benedict?” Mwanamke yule alimuuliza.



    Benedict akaonekana kushtuka kupita kawaida, hakuamini kwamba hata mwanamke yule alikuwa akimfahamu. Moyo wake ukaogopa zaidi kwa kuona kwamba alikuwa ameruka haja ndogo na kukanyaga haja kubwa. Moyo wake ukaongeza mapigo zaidi ya udundaji huku kijasho chembamba kikianza kumtoka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwili ukaanza kumtetemeka, alijiona kwamba hakuwa na sababu yoyote ya kuendelea kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuanza kuufuata mlango wa uani kwa ajili ya kuufungua na hatimae kuondopka ndani ya nyumba hiyo kupitia mlango wa nyuma. Mara baada ya kuufungua mlango ule, macho yake yakakutana na giza kubwa, giza ambalo hakuwahi kuliona katika maisha yake.



    Jambo lile likaonekana kuwa kama muujiza katika maisha yake, kwa haraka haraka akaufunga mlango ule. Benedict alikuwa akitembea huku na kule huku bibi yule akiendelea kumwangalia tu. Tayari kwake hali ambayo ilionekana nje ya nyumba ile ikaonekana kumchanganya.



    Alijua fika kwamba katika kipindi hicho ilikuwa ni jioni, sasa ilikuwaje kule nje kuwe na giza kubwa nambna ile. Hapo ndipo alipokata shauri la kwenda nje kupitia ule mlango wa mbele ambao alikuwa ameingilia. Hakuonekana kujali kama nje kulikuwa na askari, tayari alijiona kuwa kwenye hatari kubwa ya kukamatwa kwa hiyo aliona bora kama angetoka nje na kisha kuanza kukimbizana tena na askari wale.



    Mara baada ya kuufikia mlango ule, Benedict akaufungua. Hakuamini macho yake, akakutana na giza kubwa. Benedict akachanganyikiwa zaidi, ni muda mchache uliopita alikuwa ameingia ndani ya nyumba hiyo huku ikiwa ni jioni, iliwezekana vipi kwa wakati huo tayari usiku ulikuwa umeingia? Kila alipokuwa akijiuliza, alikuwa akiendelea kuchanganyikiwa zaidi.



    “Zubeda yupo wapi?” Mwanamke yule alimuuliza Benedict swali ambalo likaonekana kumshtua.



    Benedict akayageuza macho yake na kuanza kumwangalia mwanamke yule. Swali lake likaanza kumkumbusha toka kipindi kile ambacho alikuwa amepewa hirizi na Bi Mwenda kwa ajili ya kuileta Mombasa. Akaanza kumsogelea mwanamke yule huku akiiangalia nyumba ile kwa makini, tayari akaonekana kufahamu kwamba mwanamke yule ndiye alikuwa Bi swaumu ambaye alikuwa akihitajika kumpeleka hirizi ile ambayo alikuwa amepewa.



    “Hii ndio nyumba ya kwanza nilioingia” Benedict alijisemea.



    “Zubeda yupo wapi?” Bi Swaumu alimuuliza.



    Hapo hapo bila kuchelewa, Benedict akaikunja fulana yake na kisha kuanza kuifungua hirizi ile ambayo alikuwa ameifunga katika mkono wake kwa juu. Bi Swaumu alibaki akimwangalia benedcit ambaye aliifungua hirizi ile na kisha kumgawia. Uso wa Bi Swaumu ukaonyesha tabasamu pana, kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa muda mrefu tayari kilikuwa katika mikono yake katika kipindi hicho. Akamwangalia Benedict machoni na kisha kumshukuru.



    “Asante sana. Unataka nikupe zawadi gani?” Bi Swaumu alimuuliza Benedict.



    “Hapana. Nimesaidia tu kukuletea” Benedict alimwambia Bi Swaumu.



    “Najua umenisaidia. Kuna watu zaidi ya watatu walijaribu kumleta Zubeda lakini walishindwa kumfikisha. Wakawaruhusu watu wamuone na hatimae walikufa njiani na Zubeda kumrudia mdogo wa Mwenda” Bi Swaumu alimwambia Benedict.



    “Usijali mama. Nimekusaidia tu”



    “Sawa nashukuru. Ila nauona moyo wako una kiu ya kitu kimoja” Bi Swaumu alimwambia Benedict.



    “Kitu gani?”



    “Kufanya mauaji juu ya aliyehusika na kifo cha baba yako” Bi Swaumu alimwambia Benedict.



    “Upo sahihi. Ninataka kujua ni nani amehusika” Benedcit alimwambia Bi Swaumu.



    “Cha msingi fanya kitu kimoja”



    “Kipi?”



    “Mtafute Judith. Anajua kila kitu”



    “Sawa. Ila inawezekana kwamba nae alikufa kwenye kanisa lile”



    “Hajafa. Yupo hai. Mtafute, atakwambia kila kitu” Bi Swaumu alimwambia Benedict.



    “Kwa hiyo unamaanisha nirudi nchini Tanzania?”



    “Ndio”



    “Ila natafutwa sana”



    “Kuna kitu nitakufanyia”



    “Kitu gani?”



    “Nitakupa ulinzi. Utakwenda bila kujificha. Utakapofika Tanzania, hakuna atakayekujua. Ila hautotakiwa kuingia msikitini wala kanisani, ukiingia sehemu hizo, ulinzi wangu utapotea na hivyo kujulikana” Bi Swaumu alimwambia Benedict.



    Siku hiyo, siku nzima Benedict akabaki ndani ya nyumba hiyo, Bi Swaumu alikuwa na kazi ya kumuwekea dawa zake Benedict kuwa kama ulinzi katika maisha yake. Zoezi la kumuwekea ulinzi katika maisha yake ulichukua kwa zaidi ya masaa matano na ndipo aliporuhusiwa kulala ndani ya nyuma hiyo.



    Siku iliyofuata, Benedict hakutaka kukaa ndani ya nyumba hiyo, alichokifanya ni kuaga na kisha kuondoka ndani ya nyumba hiyo. Japokuwa beneidtc alikuwa amepewa ulinzi wa kishirikina wa kumlinda lakini bado alikuwa na wasiwasi mwingi moyoni mwake, hakuamini kama agefanikiwa kumfikia Judith bila kujulikana na mtu yeyote yule.



    Benedcit akachukua gari mahali hapo na kisha kuanza kwenda Changamwe, sehemu ambayo ulikuwa ukivuka na kutokea katika upande mwingine. Ndani ya gari, Benedict alikuwa na wasiwasi mwingi, hakuamini kama katika kipindi hicho alikuwa akielekea nchini Tanzania kwa ajili ya kukamilisha kitu kimoja ambacho kilikuwa kimebaki katika maisha yake.



    Hakutaka kumuacha Judith, alijua kwamba msichana yule ndiye alikuwa chanzo cha kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha ya baba yake katika kipindi ambacho alikuwa hai mpaka mauti uilipomkuta. Kadri gari lilivyokuwa likizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo hasira zake zilivyozidi kuongezeka zaidi na zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walichukua muda wa masaa saba mpaka kuuvuka mpaka wa Kenya na Tanzania na kisha kuingia Tanga. Hapo ndipo wasiwasi ulipoanza kumshika Benedict kwa kuona kwamba angeweza kujulikana na watu ambao walikuwa hapo tanga. Kama ambavyo Bi Swaumu alivyokuwa amemwambia ndivyo ambavyo ilivyotokea, hakukuwa na mtu ambaye alionekana kumfahamu Benedict.



    Ulinzi wa dawa za kishirikina ambao alikuwa amepewa kutoka kwa Bi Swaumu ulionekana kumfanya kuwa huru maishani mwke katika kipindi hicho. Alipofika tanga, hakutaka kuendelea na safari yake, alichokifanya ni kwenda katika nyumba ya wageni ya MGOSI iliyokuwa katika barabara ya kumi na tatu na kisha kujipumzisha huku ikiwa imetimia saa kumi na moja jioni.



    Kichwa cha Benedict kwa wakati huo kikaanza kufikiria mambo mbalimbali ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yake ya nyuma. Alikaa na kuanza kuifikiria siku ambayo alilichoma moto katika la Praise And Worship lililokuwa Mwenge jijini Dar es Salaam. Benedict hakuishia hapo, aliendelea kufikiria mambo mengi mpaka katika kile kipindi ambacho alikuwa akitafutwa na wapelelezi ambao walikuwa wakibakiza hatua chache kumkamata lakini alikuwa akiwatoroka kirahisi sana.



    Mawazo yake hayakuishia hapo, akaanza kumfikiria mama yake pamoja na dada yake, Angelina ambao mpaka katika kipindi hicho hakuwa amewasiliana nao kabisa. Usiku huo ndani ya nyumba hiyo ya wageni ndio ulikuwa usiku wa kukumbuka mambo yake mengi ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yake ya nyuma.



    Mbele yake aliona kuna mlima mrefu wa kuupanda katika kufanikisha kila kitu ambacho alikuwa akitakiwa kukifanya katika kipindi hicho. Ilimchukua masaa zaidi ya manne kukumbuka kila kilichotokea katika maisha yake ya nyuma na kisha kupitiwa na usingizi, usingizi mzuri ambao aliupata toka katika kipindi alipolichoma moto kanisa lile.



    Asubuhi ya saa kumi na mbili, Benedict akaamka na kisha kuelekea bafuni ambapo akaoga na kisha kujiandaa kwa ajili ya safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam. Ilipofika saa moja kamili asubuhi, Benedict akatoka katika chumba kile na kisha kuanza kuelekea katika kituo cha mabasi na kisha kukata tiketi ya basi la Shabib na kisha kuanza safari ya kuelekea katika jiji la dare es salaam.



    Benedict akaonekana kuwa katika hali ya furaha, hakuamini kama dawa ya kishirikina ambayo alikuwa amefanyiwa na Bi Swaumu ilikuwa ikifanya kazi kama kawaida kwa kutokutambulika na watu kwamba yeye alikuwa Benedict, mtu ambaye alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba ndani ya nchi ya Tanzania.



    Basi lile lilitumia masaa sita na ndipo likaanza kuingia ndani ya jiji la Dar es salaam. Basi liliposimama ndani ya kituo cha mabasi cha Ubungo, Benedict akateremka na kisha kuanza kuelekea nje ya kituo kile cha mabasi. Hakukuwa na mtu ambaye alionekana kumtambua Benedict ambaye alikuwa akitembea katika njia za watu wengi ambao walikuwa wakiendelea na harakati zao kama kawaida.



    Kwa sababu siku hiyo ilikuwa ni siku ya Jumapili, Benedict akaanza kupiga hatua kuelekea katika kituo cha daldala ambacho kilikuwa na daladala kadhaa na kuingia katika daladala iliyokuwa ikielekea Magomeni. Katika kipindi hicho, Benedict hakutaka kuchelewa kufanya mambo yake, alikuwa akitaka kumuona Judith na kisha kumtaka amwambie juu ya mtu ambaye alikuwa nyuma ya mchezo ule mchafu ambao alikuwa amechezewa baba yake.



    Kwa sababu alikuwa akimjua vizuri Judith na sehemu ambayo alikuwa akiishi, akaanza kuelekea huko. Alitumia dakika kumi kutoka Ubungo mpaka Magomeni Usalama na kisha kuteremka. Katika kipindi hicho, Benendict alikuwa bize, hakutaka kuchelewa kuifanya kazi yake ambao ilikuwa ikitarajiwa kukamilika muda mchache ujao.



    “Nakumbuka alikuwa akiishi magomeni Mikumi, nyuma ya kanisa la T.A.G” Benedict alijisema moyoni.



    Hapo hapo akaanza kupiga hatua kuelekea magomeni Mikumi, sehemu ambayo kulikuwa na kanisa la T.A.G. Alipofika katika kanisa hilo, akapitiliza mpaka katika mtaa wa nyuma ambapo akaingia katika kichochoro kimoja kidogo, alipokimaliza, alikuwa akiangaliana na nyumba aliyokuwa akiishi Judith.



    “Hatojua kama ni mimi. Dawa zinamficha. Atanijua kama nitajitambulisha kwake” Benedict alijisemea na kuanza kupiga hatua kuelekea katika nyumba ile ambapo akaanza kupiga hodi katika mlango wa nyumba ile.



    “Karibu” Mwanamke mmoja aliitikia huku akija katika mlango ule na kuufungua mlango.



    “Samahani mama. Nimemkuta Judith?” Benedict alimuuliza mwanamke yule.



    “Hapana. Ametoka kuelekea kanisani” Mwanamke yule alijibu.



    “Mmmh! Hajarudi tu mpaka muda huu?” Beneedict aliuliza huku akiangalia saa yake na kuona ilikuwa ni saa nane kasoro mchana.



    “Bado”



    “Naweza kumsubiri?”



    “Hakuna tatizo. Karibu” Mwanamke yule alimwambia Benedict.



    Benedict akaanza kuingia ndani ya nyumba ile na kisha kutulia kochini. Macho yake hayakuwa yakitulia sehemu moja, yalikuwa yakiangalia katika kila kona ndani ya sebule ile. Japokuwa halikuwa jambo la kawaida kwa mwenyeji kumuamini sana mgeni kumkaribisha ndani huku akimpa uhuru, lakini dawa za kishirikina ambazo alikuwa amewekewa Benedict mwilini mwake zilimfanya mwanamke yule kumuamini moja kwa moja na kujisikia huru moyoni mwake juu ya Benedict.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Benedict alikaa ndani ya nyumba ile kwa zaidi ya saa moja na ndipo Judith alipoingia ndani ya nyumba ile. Macho yake yalipotua usoni mwa Benedict, hakuwa akimtambua, alionekana kuwa mtu wa kawaida ambaye wala hakuwa akimfahamu kabisa. Judith akamsalimia Benedict na kisha kuelekea chumbani kwake.



    “Umemuona mgeni wako?” mwanamke yule alimuuliza Judith.



    “Hapana. Mgeni gani?”



    “Huyo hapo sebuleni”



    “Mmmh! Mgeni wangu?” Judith aliuliza huku akionekana kushtuka.



    “Ndio”



    Judith akaanza kuelekea sebuleni, kichwa chake kikaanza kujawa na maswali mengi juu ya mgeni yule ambaye alikuwa amekuja ndani ya nyumba yao na kumuulizia huku akijitambulisha kwamba alikuwa mgeni wake. Alipofika sebuleni, akaanza kumwangalia Benedict, hakujua kama alikwishawahi kumuona sehemu yoyote ile.



    “Karibu mgeni wangu” Judith alimwambia Benedict.



    “Asante. Sijui naweza kupata muda wa kuongea nawe mchana wa leo?” Benedict alimuuliza Judith.



    “Hakuna tatizo. Hapa hapa au?”



    “Hapana. Itabidi tutoke”



    “Sawa. Sasa hivi au baadae?”



    “Sasa hivi kama itawezekana”



    “Poa. Ngoja nijiandae” Judith alimwambia Benedict.



    Benedict alibaki akishangaa, kitendo cha Judith kutokumtambua na pia kukubaliana na kila kitu ambacho alikuwa akiongea nae kilionekana kumshangaza kupita kawaida. Dawa za kishirikina za Bi Swaumu zilimfanya kuwa na ushawishi mkubwa sana wa kukubalika na kila mtu kwa kile kitu ambacho alikuwa akitaka kukiongea. Moyoni mwake akafarijika, kwa mara ya kwanza akaanza kukubali kwamba uchawi upo na pia ulikuwa ukiendelea kufanya kazi katika maisha ya watu.



    Msichana Judith ambaye alikuwa akifahamiana nae sana kanisani siku hiyo hakuwa amemtambua, dawa zile za kishirikina zilionekana kufanya kazi sana katika mwili wake. Benedict akafurahi zaidi, akajiona kuwa mshindi katika kundi la washindi. Akatamani kuinuka na kuanza kuruka ruka kwa furaha lakini akashindwa kufanya hivyo.



    Akili yake kwa wakati huo ikabadilika kabisa, japokuwa alikuwa na kiu kubwa ya kutaka kumuua Judith lakini akaona lisingekuwa jambo jema kama angemuua Judith kwa kuamini kwamba kulikuwa na uwezekano wa binti yule kutumiwa kwa sababu alikuwa ameahidiwa kiasi kikubwa cha fedha kama malipo. Kitu ambacho alikuwa akikitaka yeye ni kumuuliza maswali kadhaa Judith, maswali ambayo yangemfanya kujua ni nani alikuwa nyuma ya kila lililotokea.



    Judith alichukua dakika arobaini na ndipo alipomaliza kujiandaa na kutoka chumbani kwake. Hawakutaka kukaa mahali hapo, walichokifanya ni kuondoka na kuelekea Magomeni Mapipa kwenye kiosk kimoja na kisha kugiza vyakula na kuanza kula. Muda wote walikuwa wakiongea kama marafiki, walicheka na hata kutaniani kwa utani wa hapa na pale. Benedict hakutaka kupoteza muda wake, alichokifanya ni kuanza kumuuliza Judith maswali yale ambayo alikuwa amepanga kumuuliza.



    “Unamkumbuka mchungaji Matimya?” Benedict alimuuliza Judith.



    “Mungu wangu! Mchungaji wa watu aliuawa wiki kadhaa zilizopita. Namkumbuka sana” Judith alimjibu Benedict.



    “Ni nani alimuua mtumishi yule wa Mungu?” Benedict alimuuliza Judith.



    “Sijui. Ila nadhani kwamba kuna mtu amehusika”



    “Mtu gani?”



    “Mchungaji mwenzake”



    “Yupi?”



    “Ngoja kwanza. Mbona unaniuliza maswali mengi? Wewe ni nani?” Judith alimuuliza Benedict.



    “Mimi ni rafiki yako”



    “Una maswali mengi sana rafiki”



    “Usijali. Unakumbuka kwamba ulisema kwamba mchungaji yule alitaka kukubaka ofisini?” Benedict alimuuliza Judith.



    “Ulikuwa ni mchezo tu, mchezo ambao ulinipatia kiasi kikubwa cha fedha”



    “Nani walicheza mchezo huo?”



    “Mchungaji mwenzake”



    “Nani?”



    “Mwakipesile”



    “Unamaanisha yule mchungaji ambaye anagombania uaskofu?”



    “Ndio. Tena baadae atasimikwa kuwa Askofu pale makao makuu ya dhehebu la Praise And Worship yaliyopo Sinza” Jidith alimwambia Benedict.



    “Una namba yake ya simu?”



    “Yeah! Unataka nikupe?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kama itawezekana”



    “Usijali. Ila usimwambie kama nipo hai. Ananitafuta sana mpaka nimebadilisha dhehebu nasali hapo T.A.G”



    “Usijali. Hii ni siri yangu na wewe tu”



    “Sawa” Judith alimwambia Benedict na kisha kuanza kumpa namba za simu za mchungaji Mwakipesile.



    Judith alikuwa akiongea mambo mengi bila ridhaa yake, dawa za kishirikina ambazo alikuwa nazo Benedict zilimfanya kumuweka huru na kuongea kila kitu ambacho Benedict alikuwa akitaka kukisikia kwa wakati huo. Waliongea mengi mpaka kumwambia Benedict kwamba katika kipindi hicho mchungaji yule alikuwa akikaribishwa kusimikwa na kuwa askofu mkuu wa tanzania mara baada ya kushinda uchaguzi ule.



    “Nashukuru kwa msaada wako. Ukweli wako, umeokoa maisha yako” Benedict alimwambia Judith na kisha kuinuka kitini hapo na kuanza kuondoka huku akionekana kuwa mwenye hasira nyingi.



    Hapo ndipo akili ya Judith ikamrudia, akaanza kukumbuka jinsi alivyokuwa ameongea maneno mengi katika kipindi kilichopita, maneno ambayo hakutakiwa kuyaongea kwa mtu yeyote yule. Ufahamu wake ukafunguka na kugundua kwamba mtu ambaye alikuwa akimwambia maneno yale alikuwa Benedict jambo ambalo lilionekana kumshtua sana.



    “Benedict!!!” Judith alisema kwa mshtuko lakini akawa amekwishachelewa kwani Benedict alikuwa amekwishapotea machoni mwake.



    Wachungaji wa makanisa mbalimbali wa dhehebu la Praise And Worship walikuwa wamekusanyika katika makao makuu ya dhehebu hilo yaliyokuwa Sinza Africa Sana, nyuma ya shule ya Sekondari ya Kenton. Wachungaji wengi pamoja na wazee wa makanisa walikuwa wamekusanyika katika makao makuu ya kanisa hilo huku wakiwa tayati kuangalia kusimikwa kwa mchungaji Mwakipesile ambaye alikuwa akitarajiwa kuwa askofu wa dhehebu hilo.



    Kwaya mbalimbali zilikuwa zimeitwa mahali hapo kwa ajili ya kumsifu Mungu katika ibada hiyo fupi ambayo ilikuwa ikihudhuria na viongozi mbalimbali wa dhehebu hilo. Kila kitu ambacho kilikuwa kinafanyika mahali hapo, watu walionekana kuwa na furaha kupita kawaida. Mara kwa mara walikuwa wakimpongeza mchungaji Mwakipesile ambaye alikuwa akikenua muda wote.



    Ubaya wote ambao alikuwa ameufanya wa kumuua mchungaji Matimya wala haukuwa ukikumbukwa kichwani mwake, wakati huo alikuwa akifikiria cheo kile ambacho alikuwa akienda kukipokea muda mchache ujao.



    Mishemishe za hapa na pale wala hazikupungua, kila wakati watu walikuwa bize wakifanya mambo yao huku wakizunguka huku na kule mahali hapo. Pambio zilikuwa zikiimbwa mahali hapo, kila mmoja kwa wakati huo alikuwa akionekana kuwa na furaha. Nyimbo za kumsifu Mungu ziliendelea kwa dakika kadhaa na ndipo askofu ambaye alikuwa akienda kumaliza muda wake, askofu Lugakingira kusimama mahali hapo.



    Wahudumu ambao walikuwa wakigawa maji katika sehemu hiyo walikuwa wakiendelea na huduma zao kama kawaida. Ibada hiyo fupi ilikuwa imeandaliwa kama sherehe fulani ya kumpongeza mchungaji ilikuwa ikisindikizwa na vinywaji kadhaa pamoja na chakula ambacho kingeliwa muda ambao sherehe hiyo ingekwisha.



    “Bwana Yesu Asifiwe” Askofu Lugakingira aliwasalimia watu waliohudhuria mahali hapo.



    “Amen” Watu waliitikia huku nyuso zao zikiwa kwenye furaha.



    Askofu akaanza kuongea mambo mengi mahali hapo huku kila alilokuwa akiliongea lilikuwa la kumpa Mungu utukufu. Askofu hakuweza kuishia hapo tu, pia akaanza kumsifia Mchungaji Mwakipesile ambaye alikuwa ameshinda uchaguzi huo na siku hiyo alikuwa akisimikwa na kuwa Askofu mkuu wa dhehebu hilo la Praise And Worship nchini Tanzania.



    Askofu aliongea kwa muda wa dakika tano, mara mhudumu mmoja akaanza kutembea kwa mwendo wa haraka haraka kuelekea kule kulipokuwa na madhabau. Watu wote wakaanza kumwangalia mhudumu yule huku Askofu akinyamaza na kumwangalia mhudumu yule ambaye alikuwa akitembea kwa mwendo wa haraka haraka. Mhudumu yule alipofika katika madhabau ile, akamkabidhi Askofu kikaratasi ambacho akakifungua na kuanza kukisoma.



    Watu wote walikuwa kimya, Askofu alikuwa akikisoma kikaratasi kile huku kadri muda ulivyokuwa ukienda mbele na ndivyo ambavyo alikuwa akionekana kubadilika na kuwa na wasiwasi. Uso wake ambao kipindi cha nyuma ulikuwa na tabasamu pana, ukabadilika na kuanza kuingia na hali ya tofauti. Alipomaliza kukisoma, akasikika akihusha pumzi ndefu.



    “Nakuomba Makamu Askofu, Mchungaji Marko na Katibu, Mchungaji Steven mje mbele mara moja” Askofu alisema hali ambayo ikawafanya viongozi wale kufika pale mbele na kisha kuanza kupelekana pembeni kidogo. Askofu akaanza kuwaonyeshea kikaratasi kile ambacho wote wakaanza kukisoma, hata wao walianza kubadilika pia.



    “Ni kweli hii ndivyo ilivyo?” Askofu Lugakingira aliuliza.



    “Kwanza inabidi tumuone mwenyewe yupo wapi”



    “Ila mbona hataki kuja? Kwa nini amtume mtu kukileta kikaratasi hiki na si yeye?” Mchungaji Marko aliuliza.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Si anatafutwa na polisi”



    “Inawezekana. Ila tutaamini vipi?”



    “Hapa napo ni mtihani” Askofu mkuu alisema.



    Huku wakiendelea kuongea hili na lile kuhusiana na kikaratasi kile, mara mwanaume mmoja akaanza kupiga hatua kuelekea katika madhabau ile. Kila mmoja akaanza kumwangalia, tayari mioyo yao ilijua kwamba mtu yule ambaye alikuwa akipiga hatua kuelekea mbele ya kanisa, alikuwa Benedict.



    Hakukuwa na mtu ambaye alimfahamu mpaka pale alipoifikia madhabau na kisha kuchukua kipaza sauti. Uso wake, alikuwa ameuinamisha chini kana kwamba hakutaka mtu yeyote amuone. Alipoona kwamba alikuwa amekishika kipaza sauti, akayainua macho yake. Alikuwa Benedict jambo ambalo lilimshtusha kila mtu mahali pale.







    Benedict alikuwa akipiga hatua za haraka haraka kuelekea kituoni. Kwa wakati huo alikuwa akitaka kuwahi hata kabla mchungaji Mwakipesile hajasimikwa na kuwa Askofu mkuu Tanzania. Mara baada ya kufika katika kituo cha daladala cha Mikumi, akachukua gari ambalo lilikuwa likielekea Sinza.



    Ndani ya gari, Benedict alikuwa akiliona gari lile likitembea kwa mwendo wa taratibu kiasi ambacho wakati mwingine alikuwa akitamani daladala ile ipate mbawa, ipae na kisha kutua katika uwanja wa eneo la makao makuu ya dhehebu lile. Muda wote Benedict alikuwa akionekana kuwa na hasira, alitamani dereva aendeshe haraka haraka.



    “Au nishuke nianze kukimbia?” Benedict alikuwa akijiuliza swali hilo kila wakati.



    Kutokana na foleni ya magomeni, walitumia muda wa dakika arobaini na tano mpaka kufika Sinza Africa Sana ambapo Benedict akateremka na kisha kuanza kukimbia. Kwa wakati huo alijiona kuwa nyuma ya muda, alikuwa akikimbia haraka haraka kuwahi katika sehemu ya tukio.



    Wala hakuchukua muda mrefu akawa amekwishafika katika sehemu ya tukio hilo na kisha kuanza kulifuata geti na kuingia ndani. Watu bado walikuwa wakiendelea kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, Benedict akaanza kuwaza ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya katika kipindi hicho. Hapo ndipo akapata akili ya kuifanya kitu, kuandika kitu katika kikaratasi na kisha kumgawia Askofu mkuu.



    “Naomba karatasi” Benedict alimwambia mwanaume mmoja ambaye alionekana kuwa kama shemasi mahali hapo.



    “Chukua kwenye ile Biblia kitini” mwanaume yule alimwambia Benedict ambaye akaifuata Biblia hiyo na kuchukua kikaratasi hicho alichokihitaji na kisha kukaa kwenye kiti kingine na kuanza kuandika kile alichotaka kukiandika.



    “Yanatosha” Benedict alisema mara baada ya kumaliza kukiandika kikaratasi kile na kisha kuanza kukirudia kukisoma. Kikaratasi hicho kiliandikwa hivi.



    ‘Mioyo yenu imejaa dhambi, mnashangilia kwa kuona kwamba mchungaji Mwakipesile alifanya kitu kilicho sahihi kabisa katika maisha yake. Alimtumia msichana Judith kusema kwamba alitaka kubakwa na baba yangu, alipoona mmemtenga hakuridhika, akaamua kuwatuma watu na kisha kumuua ili awe Askofu. Leo hii anajiona ameshinda, nguvu zake za kufanya mauaji zimeonekana kuwa na nguvu zaidi. Leo mnamsifu Mungu pamoja nae, nae analitaja jina la BWANA. Hiki ni kichefu chefu machoni mwa Mungu wetu aliye hai. Japokuwa hamfahamu chochote kilichotokea, jueni kwamba mchungaji Mwakipesile kalitia doa kanisa, doa ambalo halitokuja kufutika mpaka hatua za kinidhamu na sheria za nchi zichukue mkondo wake. ACHENI KUPIGA KELELE MBELE ZA BWANA ENYI MNAOKUMBATIA DHAMBI’



    Alipoona kwamba ujumbe ule ulikuwa mfupi na unaoeleweka, akamgawia kijana mmoja ambaye alikuwa mhudumu mahali pale kwa ajili ya kwenda kumgawia Askofu ambaye alikuwa amesimama huku akiongea. Kijana yule hakuonekana kukubali.



    “Unaogopa nini?” Benedict alimuuliza kijana yule.



    “Si heshima”



    “Kivipi?”



    “Mpaka amalize kuongea”



    “Sawa. Ila kumbuka kwamba mtoto wake amekamatwa kwa ishu ya madawa ya kulevya na mchungaji anahitajika kituoni sasa hivi” Benedict alimwambia kijana yule.



    “Unasemaje?”



    “Nadhani umenisikia. Mimi naondoka zangu” Benedict alimwambia kijana yule huku akijifanya kuondoka.



    Kijana yule akaonekana kushtuka, tayari wasiwasi ukamjaa kwamba kama asingefanya kile ambacho Benedict alikuwa amemwambia na kumcheleweshe kikaratasi kile askofu yule basi matatizo yangekuwa makubwa zaidi. Kwa haraka haraka bila kupoteza muda, kijana yule akaanza kupiga hatua kuelekea kule mbele ambapo akamgawia Askofu kikaratasi kile huku Benedict akifuatilia.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Askofu alikisoma mpaka alipowaita viongozi wengine pembeni na kisha kuanza kuongea nao. Benedict alipoona kwamba wanachelewa sana kumaliza kile walichokuwa wakikiongea, hapo hapo akaanza kupiga hatua kuelekea katika madhabau ya kanisa lile huku akiwa amekiinamisha kichwa chake chini.



    Alipofika katika madhabau ile, akakichukua kipaza sauti na kisha kuuinua uso wake, watu wote wakamgundua Benedict, nguvu za kishirikina ambazo alikuwa nazo mwilini mwake, mahali pale hazikuonekana kumsaidia.



    “Umeua” Ilisikika sauuti ya Benedict katika kipaza sauti huku akimnyooshea kidole mchungaji Mwakipesile.



    “Moyo wako umejaa hila. Umemuua baba yangu kwa tamaa yako ya madaraka. Umenifanya mpaka mimi mwenyewe kuua watu wasiokuwa na hatia. Umemuua baba yangu kwa tamaa zako. Umemuua baba yangu kwa kumnyonga” Benedict aliendelea kusema huku akiwa amemnyooshea kidole Mchungaji Mwakipesile ambaye alibaki kitini pale kama kamwagiwa maji.



    Japokuwa Benedict alionekana kuwa mtu hatari ambaye alikuwa akitafutwa na polisi kwa udi na uvumba lakin katika kipindi hicho kila mtu alikuwa akimwangalia tu. Maneno ambayo alikuwa akiyaongea yalionekana kumshtua kila mtu mahali pale, wote wakaanza kumwangalia mchungaji Mwakipesile.



    “Ungejisikiaje kama ningekuja na kumuua mmoja wa watu unawaopenda. Baba yangu alikuwa kila kitu kwangu, alinifundisha kumjua Mungu toka nilipokuwa mtoto mdogo. Umeamua kuyakatisha maisha yake. Umemuua baba yangu. Wewe ni muuaji mchungaji Mwakipesile” Benedict aliendelea kuongea.



    Benedict hakutaka tena kuongea, akaanza kulia kama mtoto. Maneno ambayo alikuwa ameyaongea mahali hapo yalionekana kumuumiza kupita kawaida. Askofu mkuu akaanza kupiga hatua kumfuata Benedict ambaye alikuwa akilia huku akiwa amepiga magoti na kisha kumuinua huku akijaribu kumnyamazisha.



    “Usilie”



    “Inaniuma Askofu. Mikono yangu imejaa damu kwa ajili yake” Benedict alimwambia Askofu.



    “Nimekuelewa. Naomba unyamaze” Askofu alimwambia Benedict.



    Mchungaji Mwakipesile, Askofu mtarajia alitulia kitini, mwili wake aliuhisi ukiwa umepigwa shoti ya umeme, akaanza kuangalia huku na kule, kila mtu alikuwa akimwangalia kwa macho yalioonyesha kwamba kama si kweli ilibidi aongee kitu chochote kile.



    Mchungaji Mwakipesile hakuendelea kukaa katika sehemu hiyo, akainuka na kisha kuanza kuondoka huku akiwa ameuweka mkono wake sehemu iliyokuwa na moyo wake. Kila mtu mahali pale alikuwa akimwangalia kwa macho ya mshtuko.



    “Kumbe yeye ndiye aliyemuua mchungaji Matimya?” Mwanamke mmoja aliuliza.



    “Itakuwa hivyo tu, si unamuona alivyo. Kanyong’onyeaa” Mwanaume mmoja alimwambia mwanamke yule.



    Japokuwa alikuwa amemtaja mtu ambaye alikuwa nyuma ya kila kitu lakini hiyo wala haikuwa sababu ya kutokuwekwa chini ya ulinzi. Kwa sababu ilikuwa ni sheria kufikishwa mbele ya sheria, Benedict akakamatwa na kisha kupelekwa katika kituo cha polisi huku akiwa pamoja na viongozi wengine. Sherehe za kumsimika mchungaji Mwakipesile na kuwa Askofu zikaishia hapo.



    Polisi walipomuona Benedict akiletwa mahali pale, wakaanza kumsogelea, hata kabla hawajauliza kitu chochote kile, akapigwa kofi moja zito la shavuni ambalo lilimfanya kuyumba.



    “Mpumbavu wewe” Polisi yule aaliyepiga alimwambia Benedict hata kabla ya kuuliza chochote.



    “Mbona unampiga?” Askofu alimuuliza.



    “Kaisumbua sana Serikali muuaji huyu”



    “Hiyo ni sheria kumpiga mtuhumiwa?” Askofu aliuliza lakini polisi yule hakujibu kitu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hiyo ndio ilikuwa siku ambayo Benedict alikamatwa. Taarifa zilivyotolewa kwenye vyombo vya habari, kila mtu alionekana kuwa na furaha kwani hatimae yule mtu ambaye alilichoma kanisa wiki iliyopita alikuwa amekamatwa.



    Taarifa ya kukamatwa kwake ikawa kama msumali wa moto kwa mama yake pamoja na dada yake ambaye walifika mahali hapo kwa ajili ya kumuona lakini hawakuruhusiwa. Baada ya masaa mawili, taarifa zikasambazwa kwa washirika wa dhehebu la Praise And Worship kwamba mchungaji Mwakipesile alikuwa amejiua ndani ya chumba cha hoteli ambacho alikuwa amefikia.



    “Hata nikihukumiwa kifo, sitokuwa na wasiwasi tena” Benedict alijisemea katika siku ambayo alikuwa akipelekwa mahakamani katika siku ya nne ya kesi ile, siku ambayo hukumu ilikuwa ikienda kutolewa juu yake.



    “Utanyongwa mpaka ufe” Ilisikika sauti ya hakimu ambaye alikuwa amemhukumu Benedict kifo.



    “Benedict..Benedict...” Iliskika sauti ya Bi Meriana.



    Benedict akaamka kutoka usingizini huku akitokwa na jasho kupita kawaida japokuwa feni lilikuwa likiendelea kupepea chumba kizima.



    Bi Meriana akaonekana kushangaa, hakuwahi kumuona Benedict akiwa kwenye hali ile, alichokifanya ni kukaa kitandani na kisha kuanza kumuuliza maswali juu ya hali iliyomfanya mpaka kuwa katika hali ile ambayo ilikuwa ikitia hofu.



    “Kuna nini?”



    “Kumbe nilikuwa naota mama. Kumbe matukio yote yalikuwa ndoto” Benedict alimwambia mama yake, Bi Meriana.



    “Ulikuwa ukiota nini?”



    “Ndoto moja ndefu sana. Baba yupo wapi?” Benedict aliuliza huku akiangalia huku na kule.



    “Yupo sebuleni. Ndio anajiandaa kwenda kusimikwa na kuwa Askofu mkuu wa Tanzania” Bi Meriana alimwambia Benedict.



    “Kumbe ilikuwa ndoto mama”



    “Kwani umeota nini?”



    “Nitakwambia. Judith yupo wapi?”



    “Alinipigia simu na kusema kwamba atakuja. Amejaribu kukupigia simu lakini haukuwa ukipatikana. Amesema atapitia hapa ili muelekee Kariakoo kununua pete kwa ajili ya uchumba wenu ambao utatangazwa kanisa Jumapili Ijayo” Bi Meriana alimwambia Benedict.



    “Afadhali imekuwa ndoto. Afadhali imekuwa ndoto mama” Benedict alimwambia mama yake.



    “Kwani umeota nini?”



    “Ndoto ndefu sana mama. Ila nashukuru imekuwa ndoto. Nitawahadithia baadae” Benedict alimwambia mama yake ambaye akatoka chumbani mule.



    Benedict akabaki kimya kwa muda, akashika tama. Moyo wake ukaanza kumshukuru Mungu kwa kuona kwamba kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea kilikuwa ndoto, ndoto mbaya ambayo ilionekana kutisha sana. Benedict akaichukua simu yake na kuiwasha ambapo akakutana na meseji mbili kutoka kwa mpenzi wake, Judith Simon.



    “Nilikuwa nimekupoteza ndotoni baby” Ilikuwa meseji ambayo Benedict aliamua kumuandikia Judith.



    “Kwa nini?” meseji ya Judith ilisomeka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Utakapokuja nitakwambia kwa sababu gani nimekwambia hivyo. Nakupenda mpenzi” Benedict aliandika meseji hiyo na kisha kuamka kuelekea bafuni kuoga.



    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog