Search This Blog

Friday, July 15, 2022

KIFO CHA MARRY - 1

    IMEANDIKWA NA : HUSSEIN O. MOLITO

    *********************************************************************************

    Simulizi : Kifo Cha Marry

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    Ni majira ya joto hususani hapa kwetu Dar ndio kabisaa. Watu wanadiriki mpaka kulala nje ya nyumba zao kutokana joto linavyowakosesha usingizi. Mbali na adha yote hiyo, lakini bado jiji hili linazidi kuwa maarufu na kila mmoja kwa wakati wake anausifia akilinganisha na alipokuwa kijijini kwao.

    Lakini ni tofauti kabisa na mawazo ya msichana mremba ANNA.

    Yeye hatamani hata kidogo kuendelea kukaa jiji hili na kila siku ilikuwa kilio akidai kuwa anataka kurudi kwao. Hana raha ya kuishi ndani ya jiji hili ambalo kwa mara ya kwanza kulisikia lilikua jiji la ndoto yake kila siku. Alimuomba mungu angalau afike japo kwa siku moja ajionee ayasikiayo kwa watu wanaotoka Dar.

    Yeye ni msichana wa miaka ishirini na tatu. Ameolewa mwaka mmoja uliopita. Lakini mateso anayoyapata katika maisha yake hayafanani na kitu chochote.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vipigo, manyanyaso na kila aina ya hila anayofanyiwa na mumemwe ndio hamu ya ndoa ilivyokuwa inamtumbukia nyongo kila siku.

    Mume aliyemua alikuwa anaitwa Dickson. Alikua ni mlevi mbwa. Hajui nyuma mkewe kala nini na anaishi vipi. Ila arudipo anahitaji chakula na kama hakuna basi mwili wa Anna ndio tulizo la hasira zake.

    Hakika alionewa huruma na kila jirani, lakini hakuna aliyethubutu kuingilia kwa ukorofi wa mume wake.

    Maisha yalizidi kumuendea kombo siku hadi siku. Hata uzuri aliokuwa nao ulichujuka. Hata umbo lake liliowavutia wengi hususani Dick mwenyewe nalo lilitoweka. Alikuwa tofauti na watu wate pale ingawaje mumewe alikuwa na kipato kikubwa.

    Siku moja mumewe alirudi saa tisa usiku. Alipiga honi mara mbili. Kutokana na uchovu na maumivu aliyonayo kutokana na kipigo cha jana yake, hakusikia zile honi alizokuwa anapiga mume wake. Hadi alipopiga kwa mara ya tatu kwa fujo ndipo Anna alipokurupuka na kwenda kufungua geti haraka. Dickson alimkata jicho lake lililokuwa jekundu kutokana na pombe alizokunywa. Aliliingiza gari haraka na Anna kunusurika kugongwa. Alipopaki, alikuja mbio na kumpiga kofi la haja Anna lililompeleka mpaka chini. Damu zilianza kumtoka masikioni kutokana na kuchanwa na pete aliyovaa mume wake. Pia sikio lilinusurika kukatika kutokana na herein aliyovaa kutoka kwa uzito wa kofi alilopigwa.

    Anna alibaki analia tu na hakujua kosa alilolifanya mpaka apewe adhabu kubwa kama ile.

    Dick hakujali chochote. Aliingia ndani na kukaa kwa dakika kadhaa.

    Alipotoka alianza kumtukana Anna na wazazi wake kwa kutomfundisha adabu za mwanamke pindi mumewe arudipo kutoka kwenye shughuli zake

    Hayakuwa maneno matupu. Alitoka na furushi la nguo na kumtupia Anna na kumuamuru aondoke usiku huo huo.

    Anna hakuwa na ndugu wala rafiki kutokana na kuchungwa sana na mumewe. Aliishi katika jumba zuri lakini lilikua kama anaishi katika tanuri la moto.

    Hakuwa na jinsi zaidi ya kummbembeleza mume wake amuachie japo alale usiku mmoja. Lakini maombi hayo yalipingwa vikali na kumwambia kama hataki kuondoka kwa hiyari yake, basi atawafungulia mbwa wakali na kuwaamuru wamtafune. Hapo Anna hakutaka mabishano kwa jinsi anavyomjua mume wake alivyokuwa hana utani aamuapo jambo lake

    Kwa uchungu na maumivu makali aliyoyapata jana yake ukijulisha na kibao alichoopigwa. Ilitosha kuyakubali matokeo na kuamua kuanza safari asiyoijua. Maana kwao ni mbali na hakuwa na hata senti tano nyekundu. Pia usiku una mambo mengi.

    Wezi na wabakaji ni wengi na hiyo mida kupata msaada ni ngumu. Alipiga moyo konde na kunza safari kuelekea mbele bila kujua nini kutakachompata wala ni vipi atafika salama nyumbani kwao.

    **************************CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Anna ni mtoto pekee wa mzee mashuhuri. Alikuwa kama mboni na ndugu yake wa pekee baada ya kumpoteza mtoto wake wa kwanza wa kiume akiwa na umri mdogo wa miaka mitano.

    Ni familia masikini lakini walikuwa na upendo na waliishi kwa furaha. Mzee mashuhuri na mkewe walimlea mtoto wao katika maadili mazuri na mara zote walijitahidi kuhakikisha mtoto wao anakuwa na furaha.

    Siku moja mama yake Anna alishikwa na homa jioni. Homa ilikua kali na hospital pia hazikua karibu.

    Walitakiwa wafunge safari kutoka kijiji cha pahi mpaka kondoa mjini ndio wapate huduma kbora. Wakati wapo nje wanatafakari wafanye nini. Alipita kijana mmoja aliyekuwa na pikipiki yake. Anna aliisimamisha na kumuomba awasaidie.

    Bila kusita yule kaka akawasidia mpaka hospitalini. Ingawaje walifika usiku sana, lakini walipata huduma..

    “sijui kaka utatoza shilingi ngapi..maana hela tuliyokuja nayo ni ndogo sana.” Aliongea Anna huku akumuangalia yule kijana kwa wasiwasi mkubwa.

    “pale nilipowakuta si ndio nyumbani?” aliuliza huku akivaa tena helementi yake ya pikipiki.

    “ndio” alijibu Anna

    “kwa leo tumieni hicho kiasi mlichokuwa nacho kwa ajili ya kumuuguza mama ..mimi nitapita siku yoyote kufuata hhela yangu.”

    Yale maneno yalishusha hofu aliyokuwa nayo na kumuona yule kaka ni waajabu sana. Wakati hajui ajibu nini, yule kaka aliwasha pikipiki yake na kuondoka.

    Hata mzee Mashuhuri mwenyewe alimuona ni kijana wapekee na hakuwahi kukutana na mtu mwenye moyo kiasi kile.

    Kesho yake asubuhi. Madaktari walijitahidi kumpima na kugundua kuwa anauvimbe tumboni. Kwahiyo ilihitajika laki tatu kwa ajili ya kumfanyia upasuaji. Akiba yao yote ya mauzo ya mahindi waliyovuna mwezi uliopita ilikua laki moja. Ambayo waliibeba yote kutokana na kutokujua kinachomsumbua mama yake anna.

    Walitoka nje wakiwa hawana nguvu na hawajui wafanye nini. Mara walipoangalia mbele walimuona yule kijana aliyewasaidia jana akija kwa mbali na pikipiki yake. Walishangaa kuumuona tena na wakahisi labda atakua kapigiwa simu na mteja aje amfate.

    Pikipiki ilisimama karibu ni wao, kasha yule kijana akashuka.

    “shikamoo mzee’aisalimia

    “marahaba, za toka jana?”

    “nzuri tu..sijui nyiyi na mgonjwa pia anaendeleaje?”

    “mh!..hali sio nzuri, mama amegundulika ana uvimbe tumboni, kwa hiyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji.”aliongea Anna .

    Nesi aliyekuwa anamuangalia mama yake Anna. Alitoka nje na kumuita mzee Mashuhuri.

    “kwa hiyo mmechukua hatua gain?” aliuliza yule kijana baada ya baba yake Anna alipoenda kusikiliza wito.

    “inatakiwa laki tatu… na hapa tulipo tuna laki moja tu…na ndio tunaitegemea hiyohiyo.”

    Aliongea Anna na kujiinamia.

    ‘usijali dada..hiyo ni mitihani tu…hata hivyo kwa hali ya mama niliyomuona nayo, nilijua tu matibabu yake yatagharimu. “ aliongea yule kijana na kujisachi mfukoni. Alitoa burungutu la hela bila kuhesabu ni kumkabidha Anna.

    “hizi ni laki mbili na thelathini. …nitarudi mchana kuangalia kama nitapata chochote nijazie.” Aliongea yule kijana na kuaga.

    “utaniagia kwa mzee.” Alimaliza na kupanda pikipiki yake na kuondoka.

    Anna alikuwa kapigwa na bumbuwazi na hajui amtafsiri vipi yule mtu. Wakati mwingine mawazo yalikataa kuwa yule ni mtu na wakati mwingine akafikiri labda ni malaika aliyetumwa na mungu. Alibaki akimsindikiza kwa macho mpaka pikipiki ilpoishia. Hakuamini. Alizihesabu zile hela na kukuta zimetimia. Pia alizikagua na kufahami hazikuwa feki. Alimshukuru mungu kwa miujiza inayozidi kutokea.

    Saa nane juu ya alama, yule kijana alifika hospitali na kuwachukua Anna na baba yake na kwenda nao kwenye mgahawa. Walipokuwa wanakula ndipo maongezi yalishika nafasi yake.

    “kwa hiyo wamesema wanamfanyia lini upasuaji?” aliuliza yule kijana na kuwaangalia kwa zamu Anna na baba yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “ wamesema kesho watamfanyia na ndio tumalizie kiasi kilichobaki.” Aliongea mzee mashuhuri.

    “haya maradhi mabaya sana…tukijifanya mikono mifupi tutampoteza mama. Kwa hiyo ni bora tuonane na daktari kisha mimi nitajua jinsi ya kumpa morali wa kufanya kazi yake kwa haraka na utulivu.” Aliongea yule kijana na kugida juisi yake yote iliyobakia kwenye glass.

    Waalipomaliza kula, mzee mashuhuri akaenda kumtafuta yule daktari anaye muhudumia mke wake na kuwaacha yule kijana na Anna.

    “ ahsante sana kaka yangu kwa yote unayotutendea….yaani nashindwa hata kukutafsiri kilaa nikikuangalia” aliongea Anna na kumuangalia yule kijana .

    “nimemsikia baba yako akikuita Anna. Lakini si vizuri ukiniita tu kaka wakati nina jina langu.” Aliongea yule kaka na kuyapa pumzi maneno yake kisha akaendelea.

    “mimi naitwa Siraji Hussein, ila kwa kuokoa muda wengi huniita Sira.” Aliongea Sira na kumtazama Anna kwa umakini.

    “nashukuru kukufahamu.. ila, ningependa kujua ni kipi kilichokusukuma mpaka kuamua kutusaidia wakati hutujui?? Aliongea Anna na kumuangalia sira aliyekuwa mbele yake wakati huo.

    “mama ni mtu muhimu katika maisha ya kila binaadamu. Hata motto mdogo humuamini mama yake kuliko kiumbe chochote. Hata kuna wakati hutishia kumuita mama yake hata kama mama huyo hana ubavu hata wa kuua panya. Ndio maana siku ile uulipokua unalia na kuniomba nimsaidie mama yako. Moyo ulinichoma sana kwakua mimi sikuwahi kuishi na mama yangu. Pia nilimpoteza kwa ugonjwa huu huu anaoumwwa mama yako…hiyo ndio sababu kubwa inayonifanya niwe karibu na familia hii.” Aliongea sira na kuyaruhusu machozi yamlengelenge. Anna aliingiwa na huruma na kuchukua leso yake na kumfuta machozi yaliyokuwa yanakaribia kudondoka.

    “pole sana Sira.” Aliongea Anna na kumuangalia Sira kwa macho ya huruma.

    Baada ya maongezi hayo machache. Mzee mashuhuri alirudi akiwa na daktari.

    Sira alitoka naye yule daktari chemba na kuongea nae. Walitumia kama nusu saa kasha wakaongungana pamoja na kukubaliana kesho yake ndio wamfanyie operation ya tumbo mama Anna.

    ********************************

    Hatimaye mama yake Anna anafanyiwa operation. Maombi ya kila mmoja wao yalimsaidia mama yake Anna kupata nafuu.

    Baada ya wiki kadhaa, waliruhusuwa na kurudi nyumbani.

    “Ahsante sana mwanangu, mungu atakulipa kwa wema wako wote ulionitendea.” Aliongea mama baada ya kuhadithiwa yale yote alilyoyafanya Sira juu yao.

    “hamna shida mama, wakushukuriwa ni mungu kwa kukupa tena uzima.. maana yeye ndiye mpangaji wa kila kitu.” Alijibu Sira huku akuinyesha ni jinsi gain alivyofarijika kwakua afya ya mama Anna imeimarika tena.

    Baada ya maongezi machache Sira akaaga na kuondoka zake. Anna aliamua kumsindikiza mgeni huyo.

    . “kwa hiyo lini tena…maana nimekuzoea sana.”aliongea Anna walipokuwa njiani.

    “Mungu akipenda nitakuja siku yoyote. Maana kesho kutwa naenda Dar kufunga mzigo. Nitakaa kama wiki moja kasha nitaanza kuusambaza Dodoma. Kwa hiyo itanichukua kama mwezi mmoja hivi.” Alionga sira na kumuangalia Anna ambaye alikuwa na sura yenye bashasha tofauti na alivyomuona kwa mara ya kwanza.

    “safari njema Sira, mungu akutangulie.” Aliongea Anna na kumuangalia Sira huku akitabasamu.

    “na wewe pia….unataka nikuletee zawadi gain kutoka Dar?” aliuliza Sira na kumuangalia Anna ambaye alii ama kwa Aibu.

    “yoyote tu.” Alijibu bila kumtazama Sira, lakini tabasamu likibaki palepale.

    “nimekupa nafasi uchague…kuwa huru Anna.” Aliongea na kumuanggalia Anna usoni.

    “mi nitafurahi kama utaniletea simu…nitafurahi sana.” Aliongea Anna na kumfanya Sira aridhike na kumuaga.

    Siku zilikua hazienda kabisa kwa Anna. Maana zawadi ya Sira ndio iliganda kwenye akili yake. Pia alijikuta amemkumbuka sana Sira kiasi cha kukosa raha wakati Fulani. Aliamini akiletewa simu basi mawasiliano yake na sira yataimarika. Mwanzoni alivutika na wema aliowatendea. Lakini sasa hali ni tofauti. Anamuhitaji Sira kama mwanaume wa maisha yake.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Saa nane juu ya alama, yule kijana alifika hospitali na kuwachukua Anna na baba yake na kwenda nao kwenye mgahawa. Walipokuwa wanakula ndipo maongezi yalishika nafasi yake.

    “kwa hiyo wamesema wanamfanyia lini upasuaji?” aliuliza yule kijana na kuwaangalia kwa zamu Anna na baba yake.

    “ wamesema kesho watamfanyia na ndio tumalizie kiasi kilichobaki.” Aliongea mzee mashuhuri.

    “haya maradhi mabaya sana…tukijifanya mikono mifupi tutampoteza mama. Kwa hiyo ni bora tuonane na daktari kisha mimi nitajua jinsi ya kumpa morali wa kufanya kazi yake kwa haraka na utulivu.” Aliongea yule kijana na kugida juisi yake yote iliyobakia kwenye glass.

    Waalipomaliza kula, mzee mashuhuri akaenda kumtafuta yule daktari anaye muhudumia mke wake na kuwaacha yule kijana na Anna.

    “ ahsante sana kaka yangu kwa yote unayotutendea….yaani nashindwa hata kukutafsiri kilaa nikikuangalia” aliongea Anna na kumuangalia yule kijana .

    “nimemsikia baba yako akikuita Anna. Lakini si vizuri ukiniita tu kaka wakati nina jina langu.” Aliongea yule kaka na kuyapa pumzi maneno yake kisha akaendelea.

    “mimi naitwa Siraji Hussein, ila kwa kuokoa muda wengi huniita Sira.” Aliongea Sira na kumtazama Anna kwa umakini.

    “nashukuru kukufahamu.. ila, ningependa kujua ni kipi kilichokusukuma mpaka kuamua kutusaidia wakati hutujui?? Aliongea Anna na kumuangalia sira aliyekuwa mbele yake wakati huo.

    “mama ni mtu muhimu katika maisha ya kila binaadamu. Hata motto mdogo humuamini mama yake kuliko kiumbe chochote. Hata kuna wakati hutishia kumuita mama yake hata kama mama huyo hana ubavu hata wa kuua panya. Ndio maana siku ile uulipokua unalia na kuniomba nimsaidie mama yako. Moyo ulinichoma sana kwakua mimi sikuwahi kuishi na mama yangu. Pia nilimpoteza kwa ugonjwa huu huu anaoumwwa mama yako…hiyo ndio sababu kubwa inayonifanya niwe karibu na familia hii.” Aliongea sira na kuyaruhusu machozi yamlengelenge. Anna aliingiwa na huruma na kuchukua leso yake na kumfuta machozi yaliyokuwa yanakaribia kudondoka.

    “pole sana Sira.” Aliongea Anna na kumuangalia Sira kwa macho ya huruma.

    Baada ya maongezi hayo machache. Mzee mashuhuri alirudi akiwa na daktari.

    Sira alitoka naye yule daktari chemba na kuongea nae. Walitumia kama nusu saa kasha wakaongungana pamoja na kukubaliana kesho yake ndio wamfanyie operation ya tumbo mama Anna.

    ********************************

    Hatimaye mama yake Anna anafanyiwa operation. Maombi ya kila mmoja wao yalimsaidia mama yake Anna kupata nafuu.

    Baada ya wiki kadhaa, waliruhusuwa na kurudi nyumbani.

    “Ahsante sana mwanangu, mungu atakulipa kwa wema wako wote ulionitendea.” Aliongea mama baada ya kuhadithiwa yale yote alilyoyafanya Sira juu yao.

    “hamna shida mama, wakushukuriwa ni mungu kwa kukupa tena uzima.. maana yeye ndiye mpangaji wa kila kitu.” Alijibu Sira huku akuinyesha ni jinsi gain alivyofarijika kwakua afya ya mama Anna imeimarika tena.

    Baada ya maongezi machache Sira akaaga na kuondoka zake. Anna aliamua kumsindikiza mgeni huyo.

    . “kwa hiyo lini tena…maana nimekuzoea sana.”aliongea Anna walipokuwa njiani.

    “Mungu akipenda nitakuja siku yoyote. Maana kesho kutwa naenda Dar kufunga mzigo. Nitakaa kama wiki moja kasha nitaanza kuusambaza Dodoma. Kwa hiyo itanichukua kama mwezi mmoja hivi.” Alionga sira na kumuangalia Anna ambaye alikuwa na sura yenye bashasha tofauti na alivyomuona kwa mara ya kwanza.

    “safari njema Sira, mungu akutangulie.” Aliongea Anna na kumuangalia Sira huku akitabasamu.

    “na wewe pia….unataka nikuletee zawadi gain kutoka Dar?” aliuliza Sira na kumuangalia Anna ambaye alii ama kwa Aibu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “yoyote tu.” Alijibu bila kumtazama Sira, lakini tabasamu likibaki palepale.

    “nimekupa nafasi uchague…kuwa huru Anna.” Aliongea na kumuanggalia Anna usoni.

    “mi nitafurahi kama utaniletea simu…nitafurahi sana.” Aliongea Anna na kumfanya Sira aridhike na kumuaga.

    Siku zilikua hazienda kabisa kwa Anna. Maana zawadi ya Sira ndio iliganda kwenye akili yake. Pia alijikuta amemkumbuka sana Sira kiasi cha kukosa raha wakati Fulani. Aliamini akiletewa simu basi mawasiliano yake na sira yataimarika. Mwanzoni alivutika na wema aliowatendea. Lakini sasa hali ni tofauti. Anamuhitaji Sira kama mwanaume wa maisha yake.

    Siku zilizidi kuyoyoma hadi kufikia siku aliyoahidi Sra kurudi. Anna alikaa nje siku hiyo akiangalia huku na huko kama Sira atamuona. Baada ya masaa kadhaa, alisikia mlio wa pikipiki kwa mbaali. Moyo ulimshtuka na kujua bila shaka huyo ni Sira. Alitoka mbio kuelekea kule aliposikia huo mlio. Kwa mbaali alimuona Sira akija taratibu. Hakika alifurahi sana kumuona na alimuona ni mtu wa kusema ukweli siku zote.

    “waooo… umejuaje kama ni mimi” aliongea Sira baada ya kushuka na kupaki pikipiki yake pembeni.

    “nimekaa muda mrefu kukusubiri…hivyo nikisikia mlio wa pikipiki, basi huikimbilia kwa kudhani kuwa ni wewe.” Aliongea Anna na kumuonyeshea wazi Sira kuwa amekuwa akimkumbuka sana.

    “unaonyesha wazi kuwa umenikumbuka sana…eti eeh?” aliuliza Sira ili kupata uhakika.

    “zaidi ya sana…siku zilikua haziendi kabisa.” Alijibu Anna na kuachia tabasamu mwanana lililomchengua mpaka Sira aliyekuwa bize kumsoma.

    Baada ya maongezi ya hapa na pale, Sira alitoa mfuko mdogo na kumkabidhi Anna.

    “humo kuna simu, laini na vocha kiasi. Na kuna vizawadi vingine kidogo..nadhani utavifurahia.” Aliongea Sira na kumuacha Anna akiwa na furaha kubwa.

    “basi mi naishia hapa..maana nimechoka sana….kesho nitakuja kwa ajili ya kusalimia kwenu.”

    Aliongea Sira na Anna aliafiki. Sira akapanda pikipiki yake na kuondoka.

    Anna alirudi yumbani kwao na kwenda moja kwa moja chumbani kwake na kujifungia. Huko alikua kama mtu aliyechanganyikiwa au mtu ambaye hajawahi kuletewa zawadi. Alifungua ndani na kukuta kibox ambacho ndani yake kulikua na simu mpya aina ya Nokia, charge na betri ya ziada. Pia alikuta mkanda wa vocha ishirini za mia tano tano. Alikitoa kile kiboksi kwa furaha na kuangalia zawadi nyingine. Alikuta kibahasha cha kaki.

    Alikifungua kwa haraka sana. Ndani alikutana na karatasi iliyoviringishwa kitu Fulani kilichofungwa na rubber band. Alifungua na kukutana na kitita cha shilingi elfu sitini.

    Alitaharuki na kushindwa kabisa kuamini alichokiona. Aliifungua ile karatasi na kuanza kuisoma.

    “ naamini mpaka sasa utakua ushajua kwanini nimeamua kufanya yote haya kwa ajili yako. Sina nia mbaya wala kutaka kulipwa fadhila na wewe, bali ni msukumo tu wa moyo wangu ndio ulionituma nikwambie haya machache. Nakupenda sana Anna kutoka rohoni. Toka siku niliyokuona ndio siku niliyokupenda na sasa naona tabu kuwa mbali na wewe. Nakuahidi kukuoa pindi tu utakaponikubali.

    Nimeandika namba kwenye simu yako. Nakuomba nipe majibu yangu pindi tu utakapoupata ujumbe huu.”

    Anna alijihisi anaota. Maana yeye alitokea kumpenda sana Sira. Alistaajabu kupendwa na mtu anayempenda kutoka moyoni. Bila kuchelewa, aliwasha simu ambayo ilishawekwa chaji kabisa. Alienda upende wa majina na kukuta jina moja tu lililoandikwa Siraji. Alijishauri kama dakika moja hivi. Kisha akaamua kupiga.

    Simu iliita mara kadhaa na baadae kupokelewa na Sira mwenyewe.

    “mambo” alisalimia sira baada ya kuipokea.

    “safi tu, sijui wewe.” Alijibu Anna huku akiwa na woga kidogo.

    “nadhani umeelewa kila kitu Anna. Kwa chochote kibaya usinifikirie. Nakupenda sana .” aliongea Sira na kumfanya Anna azidi kutetemeka. Hakutaka kumpoteza Sira kwakua hata yeye ni chaguo lake. Kwa kuhofia kuonekana rahisi. Aliomba apewe muda wa kufikiria. Maana maamuzi ya kuanzisha mahusiano hayahitaji pupa.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku mbili baadae Sira alienda kwa kina Anna kama alivyomuahidi, kisha akaaondoka na kusindikizwa na Anna kama kawaida.

    “unaweza kuniambia umenipendea nini?” hatimaye Anna alijikuta akimuuliza swali lile Sira wakiwa njiani.

    “imetokea tu na sijui ni kipi kilichonivutia ….unajua moyo ndio kitu pekee chenye kuuridhisha mwili au kuudhoofisha. Sasa moyo wangu umekuhitaji na kukukosa ni sawa na kuninyima maji wakati nina kiu. Na wewe uwezo wa kunipa maji unao.” Alionga Sira na kuumuangalia Anna aliyekua anatabasamu na kuinamisha kichwa chini kwa aibu.

    “una maneno wewe?” aliongea Anna na kuendelea kutabasamu. Kwa haraka na kumshtua Anna, Sira alisimama na kumshika Anna mikononi kwa kutumia nguvu kidogo lakini hakumuumiza. Hali yo ilimshtua kidogo Anna na kumtazama Sira usoni kwa wasiwasi kidogo.

    “hivi na wewe unanipenda??”

    Aliuliza Sira na kumuangalia Anna kwa kumtolea macho kidogo ambayo hayakumtisha Anna.

    “Sira…” aliongea Anna na kumuonyesha Sira kuwa anahitaji kusema kitu ila anashindwa.

    “kuwa huru Anna, kama hunihitaji we niambie, wala haitokuwa mwisho wa kuwa karibu na wewe kama ukipenda.” Aliongea na kumuangalia Anna ambaye alikua amenyamaza kimya bila kujibu kitu.

    “nakulazimisha??” aliongea Sira na kumuachia mikono yake.

    “siku njema” aliongea Sira na kuwasha pikipiki yake.

    “sasa unaenda wapi?” Anna aliongea na kumsogelea Sira karibu.

    “naenda nyumbani..maana mi naongea na wewe lakini mwenzangu haupo kabisa.”

    “unakuwa na presha, kwani aliyekuambia hakupendi ni nani?” alionga Anna huku anatabasamu. Sira alizima pikipiki yake haraka na kumkaribia Anna.

    “kwa hiyo unamaanisha unanipenda pia?” aliuliza Sira huku akitabasamu.

    Anna hakujibu kwa mdomo. Zaidi aliitikia kwa kutikisa kichwa chake kwa ishara ya kukubali. Sira hakuchelewa. Alimrukia Anna na kumkumbatia.

    *******************************

    Penzi matata kati ya Anna na Sira lilikua gumzo kote walik-oonekana. Wengi waliwasifia kwa vile walivyoendana. Hata wao wajisikia furaha na kuamua kuoana. Sira akaandika barua na kumtuma mshenga mpaka nyumbani kwa kina Anna. Barua ilipokelewa na kusomwa.

    “Anna….Anna weeh!” aliita mama yake Anna baada ya kuisoma ile barua.

    Anna alijua kila kinachoendelea. Hivyo alijua wanamuitia ile barua. Lakini alipofika alishangaa kuona nyuso za wazazi wake zikiwa hazina furaha.

    Alifika na kuchukua nafasi yake na kusikiliza alichoitiwa.

    “hivi unaakili kweli?”

    Hilo ndilo swali la kwanza alilokutana nalo Anna baada tu ya kukaa.

    “hivi sisi tumekulea katiika misingi iliyothabiti na unajua dini ni nini….unakubali vipi kutuletea muislamu hapa? “ alifoka mzee mashuhuri na kumuangalia Anna kwa hasira.

    “lakini baba mi sioni kama kuna tatizo..tunapendana baba ndio maana anataka kunioa.” Alijibu Anna bila kumuangalia baba yake usoni

    “Hiyo ndoa inafungika kanisani au bomani?” aliuliza mzee mashuhuri kwa sauti ya ukali.

    “si nakuuliza wewe?” alizidi kufoka mzee mashuhuri.

    “nilimwambia kama mtakubali..nita….nitabadilisha dini!!” aliongea Anna kwa woga.

    “NINI???” hilo swali lilikuja sawia na kofi zito la mkono wa kushoto wa mzee Mashuhuri. Kofi lililomfanya Anna aanze kuangua kilio cha haja.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kilio cha Anna hakikua sababu ya Mzee Mashuhuri kuendelea kumpa kipigo cha nguvu.

    Anna alilia na kwenda kujifungia chumbani kwake na kulia kwa kwikwi.

    “ mi nna..nampe…nda Sira” aliendelea kuliahuku akilitaja jina la mpenzi wake.

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog