Simulizi : Massacre (Mauaji Ya Halaiki)
Sehemu Ya Nne (4)
Mara baada ya Benedict kuuparamia ukuta ule akafanikiwa kuingia katika eneo la hoteli ile ya Casanova. Akaanza kupiga hatua kuelekea katika upade mwingine ambao ulikuwa na geti. Hata kabla hajapiga hatua zaidi kuelekea kule getini, akapigwa na mshtuko mara baada ya kuliona gari moja likiingia ndani ya eneo la hoteli ile.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Benedict akajificha huku wasiwasi ukianza kumkamata. Milango ya gari lile ikafunguliwa na vijana watatu kuteremka na kisha kuanza kuongea na mlinzi. Wasiwasi zaidi ukaonekana kumshika, alichokifanya ni kuanza kuuangalia ukuta ambao ulikuwa ukitenganisha hoteli ile na ukumbi na kisha kuuparamia huku akionekana kutokuziogopa seng’enge zilizokuwa ukutani pale.
Akayapeleka macho yake katika upande ule wa ukumbi, watu zaidi ya ishirini walikuwa wamekaa vitini huku wengine wakitengeneza jukwaa la burudani. Hakuonekana kujali ncha za seng’enge zile, akarukia upande wa pili. Mwili wake ulichomwachomwa na ncha za seng’enge zile, damu zikaanza kumtoka.
Benedict akaanza kupiga hatua kukifuata kiti kimoja kilichokuwa ndani ya ukumbi ule huku kofia yake aina ya Malboro bado ikiwa kichwani mwake. Sehemu ile ikaanza kuonekana kuwa ulinzi mkubwa kwake. Baada ya dakika thelathini kupita, akageuka nyuma na kuanza kuangalia pale ukutani alipokuwa amepandia kuingilia ukumbini hapo.
Benedict akapigwa na mshtuko hasa mara baada ya macho yake kugongana na macho ya mtu ambaye alionekana kumtilia mashaka. Wala hazikupita hata sekunde kumi, yule mtu akaacha kuchungulia. Wasiwasi ukamshika Benedict, akajiona kuwa karibu kukamatwa, alijua ni lazima mtu yule angezunguka upande wa pili na kuingilia kupitia mlango wa mbele. Akili yake haikufikiri kitu kingine zaidi ya kitu kimoja tu ambacho kingemfanya kutoka salama mahali pale.
Kwa haraka haraka Martin akashuka ukutani na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea kule wenzake walipokuwa. Mlinzi hakuonekana kuelewa kitu chochote ambacho kilikuwa kinaendelea, alichokifanya ni kuanza kumfuata Martin mpaka kule lilipokuwa gari walilokuja nalo mahali hapo.
“Mbona haraka hivyo?” Sabrina aliuliza huku akionekana kumshangaa Martin
“Shukeni……Twendeni”
“Wapi?”
“Kule. Benedict yupo kule” Martin alijibu.
“Unasemaje?”
“Twendeni”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Martin hakutaka kupoteza muda mahali hapo, alichokifanya ni kuanza kuelekea nje ya hoteli ile huku akiwa kwenye mwendo wa kasi. Sabrina na Moody hawakutaka kubaki mahali pale, walichokifanya ni kuanza kumfuata Martin
Mara baada ya kufika katika geti la kuingilia katika eneo la ukumbi ule, wakajitambulisha kwa mlinzi huku wakimuonyeshea vitambulisho vyao. Mlinzi hakuonekana kuamini kabisa, moyo wake ulikuwa mgumu kuamini kama kweli mpelelezi kama mpelelezi angeweza kujitangaza wa mtu kwamba alikuwa akifanya kazi hiyo.
“Kuna mtu tumekuja kumchukua” Martin alimwambia mlinzi.
“Sitowaruhusu hadi mtoe viingilio” Mlinzi aliwaambia.
Kila mmoja akaonekana kumshangaa mlinzi, maneno ambayo aliongea yalionekana kuwashangaza. Hawakutegemewa kudaiwa viingilio katika geti lile kwani walijua fika kwamba viingilio vilikuwa vikichukuliwa katika mlango wa mwisho kuingilia ukumbini mule kwani baadhi a magari yalikuwa yamepaki katika eneo kubwa la ukumbi ule.
“Lakini sisi ni map……” Martin alisema lakini hata kabla hajamalizia sentensi yake, mlinzi akaingilia.
“Sogeeni kwanza nifungue geti” Mlinzi aliwaambia.
Geti likafunguliwa na teksi iliyokuwa na vioo vilivyokuwa na tinted kutoka. Wapelelezi wakazidi kuchanganyikiwa zaidi, walichokifanya ni kuacha kuongea kwa kauli za kulazimisha, wakaanza kuongea na mlinzi kinyenyekevu. Walimbembeleza mlinzi kwa dakika tatu na ndipo akawaruhusu kuingia.
Wakaanza kupiga hatua za haraka haraka kuufuata mlango mkuu wa kuingilia ndani ya ukumbi ule. Mlangoni wala hakukuwa na mtu yeyote yule jambo lililowafanya kuingia hadi ndani. Bado watu walikuwa wakiendelea kulipamba jukwaa ukumbini mule kwa ajili ya muziki ambao ulitarajiwa kupigwa na bendi ya Twanga Pepeta usiku wa saa nne.
Walichokifanya ni kuanza kumtafuta Benedict ndani ya ukumbi ule, kitu cha kushangaza, Benedict hakuonekana. Hawakutaka kuridhika, walichokifanya ni kuelekea mpaka chooni lakini napo huko wala Benedict hakuonekana hali ambayo ilianza kuwachanganya.
“Lakini si ulisema ulimuona! Mbona hayupo?” Moody alimuuliza Martin.
“Hata mimi mwenyewe na shangaa. Nilipochungulia mwanzao, alikuwa amekaa hapa” Martin alijibu.
“Ulipomuona alikuona?”
“Ndio”
“Basi atakuwa ametoroka” Moody alisema.
Hawakutaka kuendelea kubaki ndani ya ukumbi ule, walichokifanya ni kuanza kuelekea nje ya ukumbi ule hali iliyowafanya watu waliokuwa mule ukimbini kuanza kuwashangaa. Walichokifanya ni kuanza kumtafuta katika kila eneo ndani ya eneo la ukumbi ule lakini napo Benedict hakuonekana. Hawakuwa na jinsi tena, walichokifanya ni kuanza kupiga hatua kumfuata baunsa ambaye alikuwa akiongea na rafiki yake.
“Tunamtafuta Benedict Matimya. Mmemuona maeneo haya?” Martin aliuliza.
“Benedict!”
“Ndio”
“Yule anayetafutwa?”
“Ndio”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Acheni utani bwana. Mnajua kwamba mnazizungumzia milioni ishirini hapo?”
“Tunalijua hilo. Nilimuona hapa muda mchache uliopita. Alikuwa amevaa kofia ya Malboro yeye rangi nyekundu” Martin aliwaambia.
Maneno aliyoongea Martin yakaonekana kuwashtua, mtu ambaye alikuwa amevaa kofia aina ya Malboro ambayo ilikuwa na rangi nyekundu wala hakuwa mgeni machoni mwao, walimuona kipindi kichache kilichopita. Baunsa alibaki akiwaangalia mara mbili mbili walinzi wale huku akinekana kutokuamini kile ambacho kilikuwa kikizungumziwa.
“Kumbe yule alikuwa Benedict?”
“Ndio”
“Mna uhakika?”
“Ndio”
“Nendeni Blue Diamond hoteli pale Magomeni. Alichukua teksi hapa” Baunsa aliwaambia.
Unamaanisha ile teksi ambayo iliondoka muda mchache uliopita”
“Ndio hiyo hiyo. Yeye ndiye aliyeikodi kumpeleka hotelini” Baunsa aliwaambia.
Martin na wenzake wakaanza kupiga hatua kulifuata gari lao huku kila mmoja akionekana kuzidi kuchanganyikiwa. Tayari Benedict kwao akaonekana kuwa mgumu kupatikana tofauti na jinsi ya walivyokuwa wakidhani mwanzoni. Moody akashikilia usukani kama kawaida yake na safari ya kuelekea katika hoteli ya Blue Diamond kuanza.
“Ni lazima tumkamate” Martin alisema huku akionekana kukasirika.
Benedict hakutaka tena kuendelea kubaki mahali pale, mtu ambaye alikuwa amechunglia juu ya ukuta ule tayari alikwishaanza kumtia wasiwasi. Alichokifanya muda huo ni kusimama na kuanza kuufuata mlango mkuu wa kuingilia ukumbini pale. Macho yake yakapigwa na mshtuko mara baada ya kuliona gari dogo likiwa limesimama pembeni huku vijana watatu wakiongea na mlinzi.
Benedict hakuona uwezekano wa kutoka ndani ya ukumbi ule. Macho yake yakapigwa na mshtuko wa furaha mara baada ya kuiona teksi ya biashara ikiwa katika eneo la ukumbi ule. Kwa haraka haraka akaanza kuisogelea taksi ile, alipoifikia, kijana mmoja akafika mahali hapo huku akiwa ameongozana na baunsa wa ukumbi ule.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Karibu” Dereva alimwambia Benedict bila kumtambua huku akimfungulia mlango.
“Nipelekee Blue Diamond Hotel”
“Elfu saba”
“Haina tatizo” Benedict alijibu.
Dereva akawasha gari na kumuaga baunsa. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alikuwa akifahamu kwamba kijana yule ambaye alikodi teksi ile alikuwa ni Benedict ambaye alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba nchini Tanzania. Dereva akaanza kuliondoa gari lile mahali pale.
Mlinzi akafungua geti, gari likatoka. Macho ya Benedict yalikuwa yakiwaangalia vijana watatu ambao bado walikuwa wakiendelea kuongea na mlinzi. Moyo wa Benedict ukamlipuka kwa furaha hasa mara baada ya kujiona ametoka salama katika ukumbi ule. Mara baada ya teksi kufika maeneo ya Kijitonyama, akamtaka dereva asimamishe gari pembeni, akateremka na kwenda katika mashine ya ATM. Akatoa kadi yake, akachukua kiasi chote cha fedha kilichobaki na kurudi garini.
Safari iliendelea. Gari lilichukua dakika arobaini likafika katika eneo la hoteli ya Blue Diamond. Akateremka, akamgawia dereva kiasi cha fedha alichokuwa akidaiwa na moja kwa moja kuanza kuelekea katika sehemu ya mapokezi. Alipojiandikisha, akapewa ufunguona kuanza kwenda katika chumba namba themanini kilichokuwa katika ghorofa ya tatu.
Benedict alitulia kwa dakika hamsini, ghafla akashtukia kitasa cha mlango wa chumba kile kikianza kutekenywa. Kwa haraka akainuka pale kitandani, akaanza kupiga hatua kuufuata mlango ule. Alipoufikia, akachungulia kupitia kitundu kidogo cha mlangoni. Jicho lake likatua katika uso wa kijana ambaye alichungulia katika ukuta uliotenganisha hoteli ya Casanova na ukumbi wa muziki wa Hill Top.
Foleni ndefu ya magari ilikuwepo barabarani. Magari yalikuwa yakitumia muda mwingi kusimama kuliko kutembea. Kila mmoja akaonekana kukasirika kutokana na foleni ile kuwakera kupita kiasi. Kila mmoja aliona ilikuwa ni afadhali kushuka garini na kuanza kutembea kutokana na foleni ile kuwachelewesha kupita kiasi.
Walitumia dakika arobaini hadi kufika maeneo ya Morocco. Foleni bado ilionekana kuwakera. Walikaa katika foleni hiyo ya mataa ya Morocco kwa muda wa dakika saba na ndipo wakaruhusiwa. Moody hakutaka kuendesha gari kwa kasi ndogo tena, akaingiza gia na kuanza kuendesha kwa mwendo wa kasi.
Watu walibaki wakilishanga gari lile ambalo lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi kiasi ambacho kila mmoja akaona kwamba lilikuwa limeibwa na hivyo lilikuwa likikimbizwa na polisi. Walitumia dakika mbili mpaka kufika katika maeneo ya Magomeni hospitalini, hapo wakakutana na foleni nyingine ambayo iliwaweka hapo kwa muda wa dakika tano.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Waliporuhusiwa, walitumia muda wa dakika mbili tu wakawa wamekwishafika katika eneo la hoteli kubwa ya Blue Diamond ambayo ilikuwa imezungushwa ukuta mkubwa. Walipoingia ndani ya eneo la hoteli hiyo, wakateremka na moja kwa moja kuanza kuelekea mapokezini huku macho yao yakiangalia kila upande.
“Tunahitaji kumuona Benedict” Martin alimwambia dada wa mapokezi.
“Benedict nani?”
“Matimya” Martin alitoa jibu lililoonekana kumshtua dada wa mapokezini.
“Umesema nani? Benedict Matimya?”
“Ndiye huyo huyo”
“Hapana. Sijawahi kumuona uso kwa uso toka nizaliwe zaidi ya kuziona picha zake tu” Dada yule alijibu.
“Kuna mtu yeyote kachukua chumba katika hoteli hii dakika kadhaa zilizopita ambaye alivalia kofia aina ya Malboro iliyokuwa na rangi nyekundu?” Martin aliuliza.
“Ndio”
“Ulimpa chumba?”
“Ndio”
“Namba ngapi?”
“Themanini”
Hawakuwa na sababu ya kuendelea kuchelewa mahali hapo, walichokifanya ni kutoa vitambulisho vyao na kumuonyeshea yule dada ambaye akaonekana kugundua kwamba wale walikuwa polisi waliotoka katika kitengo cha upelelezi, alichokifanya ni kuanza kwenda nao katika chumba hicho kilichokuwa katika ghorofa ya tatu.
Wakapandisha ngazi mpaka kuifikia ghorofa ya tatu ambapo moja kwa moja wakaanza kuziangalia namba zilizokuwa katika milango kadhaa, walipoufikia mlango uliokuwa na namba themanini, Martin akaanza kukitekenya kitasa cha mlango ule ambao ulionekana kufungwa.
“Naomba funguo za akiba za mlango huu” Martin alimwambia yule dada.
“Nimeziacha kaunta. Subiri nikakuletee”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa haraka haraka dada yule, Mariamu akaanza kuelekea kaunta kuzichukua funguo zile huku wapelelezi wakiwa wamebaki mlangoni pale. Mwendo wake ulikuwa wa haraka haraka huku moyoni akijilaumu kwa kutokujua kwamba mtu ambaye alichukua chumba alikuwa Benedict ambaye alikuwa akitafutwa na polisi. Alipofika kaunta, akazichukua funguo zile za akiba na kuanza kurudi ghorofani.
“Hizi hapa” Mariamu alisema huku akimkabidhi funguo zile Martin.
Martin akaingiza ufunguo katika kitasa kile, bahati ilionekana kuwa yake kutokana na kutokuwa na ufunguo wowote kwa ndani. Wakaufungua mlango na kuingia ndani. Chumba kilikuwa kitupu, wakaanza kumtafuta Benedict katika kila kona ndani ya chumba kile lakini wala hakuweza kuonekana.
“Yupo wapi?” Martin aliuliza.
“Hatujui. Chumba kitupu”
“Hadi chooni kutupu?”
“Nd…….” Sabrina alijibu lakini hata kabla hajamalizia jibu lake, wakasikia Mariamu akianza kupiga kelele kutoka chooni. Kwa haraka haraka wakaanza kumfuata.
“Kuna nini?”
“Angalieniiiiii…….”
“Mungu wangu! Twendeni chini” Martin aliwaambia wenzake na kuanza kuelekea chini huku wakiamini kwamba Benedict alikuwa ameshuka chini kwa kutumia bomba kubwa la chooni.
Benedict alitulia kwa muda na kuyapeleka macho yake kila kona ndani ya chumba kile. Hakuona kama kulikuwa na dalili zozote za kuondoka ndani ya chumba kile bila kupitia mlangoni. Kwa haraka haraka akaanza kulifuata dirisha la chumba kile na kufungua kioo, hakukuonekana kuwa na bomba lolote ambalo lingemuwezesha kushukia chini.
Benedict hakutaka kupoteza muda, kwa haraka haraka akaanza kuelekea chooni ambako akaufungua mlango na kisha kulifuata dirisha la choo kile na kuchungulia. Moyo wake ukamlipuka kwa furaha mara baada ya kuliona bomba kubwa likiwa limeelekea chini.
Kwa haraka haraka Benedict akatoka nje ya choo kile kwa kupitia dirishani, akalidandia bomba lile na kuanza kuteremka chini. Moyo wake haukuwa na wasiwasi wowote kwani alijua ni vigumu kuonekana na mtu yeyote kutokana na upande ule kuwa nyuma ya hoteli ile. Kutokana na haraka aliyokuwa nayo wala hakuchukua muda mrefu kufika chini, ni ndani ya dakika mbili tu, akawa amekwishafika chini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akaanza kupiga hatua kuelekea mbele ya hoteli ile, lakini hata kabla hajafika, akajibanza pembezoni mwa ukuta na kuanza kuchungulia kule mbele ya hoteli ile. Macho yake yakatua kwa mlinzi ambaye alikuwa makini kuangalia kila upande kitu ambacho kilionekana kumpa wasiwasi mkubwa Benedict. Akayatoa macho yake kutoka kwa mlinzi na kuyapeleka katika ghorofa ya tatu hasa katika dirisha la chumba alichokuwa amepanga.
Macho yake yakatua kwa mtu ambaye alikuwa akichungulia nje kupitia katika dirisha la chumba kile na baada ya sekunde chache, watu watatu wakaongezeka dirishani pale. Wasiwasi ukaongezeka zaidi hasa mara baada ya kuwaona watu wale wakichomoka kwa haraka kutoka pale dirishani.
Benedict akaangaza macho yake huku na kule, macho yake yakatua katika choo kidogo kilichojengwa nyuma ya hoteli ile. Benedict hakutaka kujiuliza, hapo hapo akaanza kupiga hatua kukifuata choo kile. Alipokifikia, akaufungua mlango na kuingia ndani. Macho yake yakaanza kuangalia katika kila kona ndani ya choo kile.
Hakukuwa na sehemu yoyote iliyokuwa wazi zaidi ya dirisha dogo lililokuwa katika upande uliokuwa na nyaya nyingi za umeme. Akapanda kwa kukanyaga bomba la maji chooni mule, akaanza kuliangalia dirisha lile.
“Ni lazima niling’oe” Benedict alijisemea.
Martin, wapelelezi wenzake pamoja na Mariam wakaanza kuteremka ngazi kwa haraka haraka kuelekea chini. Kichwa cha kila mtu katika kipindi hicho kilikuwa kikimfikiria Benedict. Kila mtu alikuwa na uhakika kwamba Benedict alikuwa ameteremkia chini kwa kutumia bomba la choo ambalo lilikuwepo nyuma ya hoteli ile.
Mara baada ya kufika chini, moja kwa moja wakaanza kuangalia katika kila eneo la hoteli ile. Wakaelekea hadi katika eneo lililokuwa na bomba lile kubwa la choo, wakaangalia katika maeneo ya karibu na bomba lile lakini napo hakukuwa na mtu yeyote. Hawakutaka kuendelea kubaki kule nyuma ya hoteli, wakaanza kupiga hatua kumfuata mlinzi huku kila mmoja akionekana kuchanganyikiwa.
“Vipi?” Martin alimuuliza mlinzi.
“Sijamuona hapa”
“Na hakuna mtu aliyetoka?”
“Hakuna kabisa”
“Acha utani”
“Huo ndio ukweli”
Wakazidi kuchanganyikiwa zaidi, Benedict akaonekana kuwazidi ujanja kwa mara nyingine tena. Kila mmoja akaonekana kuchoka, wakabaki kimya huku wakiwa hawajui ni kitu gani ambacho walitakiwa kukifanya katika kipindi kile. Martin ndiye ambaye alionekana kuchanganyikiwa zaidi, alibaki katika hali hiyo kwa sekunde kadhaa, akamsogelea mlinzi.
“Hauna wasiwasi na sehemu yoyote nyuma ya hoteli hii” Martin alimuuliza mlinzi.
Swali lile likaonekana kuwa gumu kujibika, mlinzi akabaki kimya kwa muda huku akionekana kufikiria kitu. Kwa haraka haraka katika hali ambayo ilimshangaza kila mtu, mlinzi akachomoka kutoka mahali hapo huku akikimbia kuelekea nyuma ya hoteli ile. Wapelelezi hawakutaka kubaki mahali pale, nao wakachomoka mahali pale kumfuata mlinzi kule nyuma ya hoteli alipokuwa akielekea.
“Kuna nini?” Moody alimuuliza mlinzi mara baada ya kumfikia.
“Mmeangalia chooni?” Mlinzi aliuliza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Chooni! Choo gani?” Martin aliuliza.
“Kile pale” Mlinzi aliwaonyeshea.
Kwa haraka haraka wakaanza kukifuata choo kile. Mara baada ya kuufikia mlango wa choo kile, Moody akashika komeo la mlango wa choo kile na kujaribu kuufungua. Mlango ukaonekana kufungwa, Moody akajaribu zaidi na zaidi lakini mlango haukufunguka kitu ambacho kiliwafanya kuona kuwa Benedict alikuwa ndani ya choo kile.
“Nani hutumia choo hiki?” Martin aliuliza huku akilishika komeo la mlango na kujaribu kuufungua.
“Mimi, mlinzi”
“Unaweza kuturuhusu kuuvunja mlango huu?” Martin alimuuliza mlinzi. Mlinzi akabaki kimya kwa muda huku akiyapitisha macho yake kwa kila mpelelezi ambaye alikuwepo mahali pale.
“Sawa. Uvunjeni”
Martin na Moody hawakutakakupotza muda, hapo hapo wakaanza kuuvunja mlango ule. Kutokana na mlango ule kutokuwa imara, wakafanikiwa kuuvunja. Wakaingia chooni, macho yao yakatua katika dirisha dogo la choo kile. Nyavu ilikuwa chini, Martin akapanda juu ya ndoo iliyokuwa ndani ya choo kile na kuanza kuchungulia kupitia katika kidirisha kile.
“Huyu atakuwa ametuacha kwa mara nyingine tena” Martin aliwaambia wenzake huku akiendela kuchungulia katka kidirisha kile.
“Unaona nini huko?” Moody aliuliza.
“Mitambo kadhaa ya umeme. Nafikiri itakuwa mitambo ya kuendeshea umeme ndani ya hoteli hii” Martin alijibu.
Benedict hakupata tabu sana katika kazi yake ya kutaka kutafuta njia ya kutokea ndani ya choo kile, ni ndani ya sekunde kumi na tano tu, akafanikiwa kuitoa nyavu ya dirisha lile. Mara baada ya kuona kuwa kazi ya kutoa wavu ule imekamilika, hapo hapo akapanda hadi katika kidirisha kile na kuanza kutoka nje kwa kujipindapinda.
Mitambo mbalimbali ya umeme ilikuwa imezagaa katika eneo lile aliloteremkia. Benedict akaanza kupiga hatua kuufuata ukuta mkubwa ambao ulizunguka hoteli ile. Mwendo wake ulikuwa wa makini zaidi kutokana na kuogopa kuigusa mitambo ile ya umeme ambayo ilionekana kuwa na nguvu.
“Asante Mungu” Benedict alisema na kuanza kuuparamia ukuta ule.
Mara baada kuteremkia nje ya eneo la hoteli ile, moja kwa moja akaanza kupiga hatua za haraka haraka kuelekea katika eneo ambalo lilikuwa na nyumba zilizokuwa na vichochoro. Akaanza kupita katika vichochoro vile hadi katika eneo la bustani ya Magomeni. Akaendelea zaidi na safari yake na kutafuta sehemu nzuri ya kupumzikia ndani ya bustani ile na kisha kupumzika.
Idadi kubwa ya miti pamoja na mwanga hafifu ambao ulikuwepo ndani ya bustani ile ilimfanya kutokuonekana na watu ambao walikuwa wakipita bustanini pale. Benedict alitulia kwa muda wa dakika hamsini, akaiweka vizuri kofia yake kichwani na kuondoka katika eneo hilo huku saa yake ikionyesha kwamba tayari ilikuwa saa nne kasoro usiku. Akachukua daladala ambapo akaanza safari ya kuelekea Tandale ambako aliamini ingekuwa vigumu kugundulika.
Daladala ilichukua dakika kumi ikafika katika kituo cha daladala cha Kwa Tumbo ambapo akateremka na kuanza kupiga hatua kukipandisha kilima kidogo. Macho ya Benedict yalikuwa yakiangalia katika kila upande, mwili ulikuwa umechoka, katika kipindi hicho hakutaka kitu kingine chochote zaidi ya nyumba ya wageni tu. Macho yake bado yalikuwa yakitafuta nyumba ya wageni lakini hakufanikiwa kuiona nyumba yoyote ya wageni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Samahani kidogo” Benedict alimwambia kijana mmoja mara baada ya kumsimamisha. Benedict akaiweka vizuri kofia yake na kuendelea.
“Natafuta nyumba yoyote ya wageni” Benedict alimwambia kijana yule.
“Maeneo haya zipo nyingi tu. Kuna Ntahamba, Kieleweke, sijui wewe unataka ipi”
Yoyote iliyo karibu na hapa”
Kijana yule akaanza kutoa maelekezo pasipo kufahamu kwamba yule ambaye alikuwa akimpa maelekezo alikuwa Bendict. Alitumia sekunde ishirini kutoa maelekezo, baada ya hapo, Benedict akaanza kuyafanyia kazi maelekezo yale. Banedict akaanza kupita katika vichochoro kadhaa mpaka alipofika katika nyumba hiyo ya wageni ambayo iliandikwa KIELEWEKE GUEST HOUSE’.
Uso wake ukajawa na tabasamu. Akapiga hatua zaidi kuifuata nyumba ile na kisha kuelekea katika sehemu ya mapokezi. Akapokelewa na tabasamu pana kutoka kwa msichana wa mapokezi. Akaongea nae, akamlipa kiasi cha fedha ambacho kilikuwa kikitakiwa na kisha kupelekwa katika chumba hicho.
“Mna vyumba vizuri sana” Benedict alimwambia msichana yule.
“Utahitaji nini kwa sasa?” Msichana yule alimuuliza.
“Chakula chochote kile”
“Kingine…..”
“Labda jina lako mrembo” Benedict alijibu huku akitabasamu.
“Naitwa Asha” Msichana yule alijibu.
Kamanda mkuu wa jeshi la Polisi, Bwana Idrisa alionekana kuchanganyikiwa zaidi. Hakuamini kama siku saba zilikuwa zimefika lakii Benedict hakuwa amepatikana. Ofisi ikawa moto, mara kwa mara waandishi wa habari walikuwa wakifika mahali hapo huku wakitaka kufahamu ni kitu gani ambacho kilikuwa kinaendelea juu ya upelelezi wa Benedict.
Wapelelezi ambao alikuwa amewapa kazi ya kumtafuta Benedict hawakuwa wamempa jibu lolote lile japokuwa walikuwa wamemuahidi kumapa ndani ya siku chache. Mara kwa mara Kamanda Idrisa alikuwa akiongea peke yake, mbele yake alikuwa akiona giza nene, lawama zote za Watanzania zilikuwa juu yake kwa kushundwa kufanikisha kumkamata Benedict.
Kazi ndani ya ofisi yake haikufanyika sawa sawa, alijiona kuwa na mzigo mkubwa kutoka kwa Watanzania ambao walitamani sana kuona Benedict akikamatwa na kusfikishwa katika vyombo vya sheria na kuhukumiwa kwa kosa la kuua zaidi ya watu mia mbili na hamsini. Mara kwa mara alikuwa akiwasiliana na vituo mbalimbali vya polisi jijini Dar es Salaam kuona kama kulikuwa na uwezekano wa Benedict kuonekana sehemu.
“Kipindi fulani alikuwa Tandale, ndani ya nyumba ya rafiki yake” Mkuu wa kituo cha polisi cha Tandale alimwambia kamanda Idrisa kupitia simu ya mezani.
“Ikawaje sasa! Mlimkamata?”
“Hapana. Alitoroka hata kabla hatujafika katika nyumba hiyo”
Kamanda Idrisa akachanganyikiwa zaidi, haikumuingia akilini kama Benedict alikuwa na uwezo mkubwa wa kuwasumbua namna ile. Kamanda Idrisa akatulia kwa kipindi fulani, ghafla kama mtu aliyeshtushwa na jambo fulani akanyanyua mkonga wa simu na kpiga namba fulani. Alitulia kwa muda akisubiri majibu ya simu ile ambayo ilikuwa ikiita, wala haikuchukua muda mrefu sana, simu ikapokelewa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuna kitu nimefikiria Ibrahim” Kamanda Idrisa alisema hata kabla ya salamu mara baada ya simu kupokelewa.
“Kitu gani?”
“Nafikiri Benedict atakuwa anawasiliana na ndugu zake akiwepo mama yake”
“Hiyo ni kweli kabisa”
“Mlipokwenda kutafuta maelezo kwa mama yake, aliwapa namba yake ya simu?”
“Ndio”
“Mtandao gani?”
“Etisalat Mobile”
“Nipatie namba hiyo” Kamanda Idrisa alisema na kisha kupatiwa namba hiyo.
Kwa haraka haraka akainuka kitinia kisha kuanza kuondoka kuelekea nje kwa mwendo wa haraka haraka huku mkononi akiwa na karatasi iliyokuwa na namba ya simu aliyopewa ya Bi Meriana. Polisi wakaonekana kushangaa mara baada ya kumuona mkuu wao akitembea kwa mwendo wa kasi kuelekea nje ya jengo lile.
Polisi waliokuwa na vyeo vidogo walikuwa wakimpigia saluti mfululizo lakini Kamanda Idrisa hakutoa saluti yoyote ile zaidi ya kuendelea kutembea mwendo wa haraka haraaka kuelekea nje. Macho yake yalikuwa yakiangalia mara mbili mbili karatasi ile kana kwamba hakuamini kile ambacho alikuwa akikiona. Mara baada ya kufika nje ya jengo lile, akaanza kulifuata gari lake, akaingia na kuondoka kwa mwendo wa kasi.
Safari yake haikuchukua muda mrefu akawa amekwishafika katika jengo la mtandao wa simu za mkoni la Etisalat Mobile lililokuwa maeneo ya Upanga. Moja kwa moja akateremka na kuanza kuelekea ndani ya jengo lile na kufikia sehemu ya mapokezi huku akiwa na sare zake za kazi.
“Karibu mkuu” Dada wa mapokezi alimkaribisha mara baada ya salamu.
“Nataka kuonana na bosi wenu” Kamanda Idrisa alisema.
Hakukuwa na mtu yeyote aliyehoji chochote kile, kwa haraka sana dada wa mapokezi akaanza kuelekea ghorofani huku akitaka kamanda Idrisa amfuate. Wafanyakazi wote ndani ya jengo lile walionekana kushtuka, hawakujua sababu ambayo ilimpeleka Kamanda wa jeshi la polisi kufika mahali hapo.
“Hizo namba zenyewe zipo wapi?” Bosi wa kampuni ile, Bwana Nehemiah alimuuliza Kamanda Idrisa mara baada ya kumwambia nia yake.
“Hizi hapa” Kamanda Idrisa alisema huku akimkabidhi kikaratasi kile.
Hawakutaka kubaki ndani ya ofisi ile, moja kwa moja wakatoka na kuelekea katika sehemu moja iliyokuwa na chumba kikubwa ambacho kiliandikwa ‘OPERATOR ROOOM’ mlangoni na kisha kuingia ndani.
Chumba hakikuwa na ukimya kabisa, sauti za watu mbalimbali waliokuwa wakifanya mawasiliano zilikuwa zikisikika chumbani hapo. Bwana Nehemiah pamoja na Kamanda Idrisa wakaanza kupiga hatua kumfuata kijana fulani ambaye alikuwa katika chumba kimoja na kisha kuanza kugonga. Kijana yule akafungua mlango wa chumba kile na wote kuingia ndani.
“Ndio mkuu” Kijana yule alimwambia Bwana Nehemiah.
“Tutahitaji kupata kila taarifa za simu zote ambazo zitaingia katika namba hii. Rekodi namba zote, nitahitaji kupata data zote” Bwana Nehemia alimwambia kijana yule.
“Nitafanya hivyo mkuu” Kijana yule alisema huku akichukua kile kikaratasi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku zilikuwa zinakatika kama kawaida, tetesi za uwepo wa Benedict bado zilikuwa zikiendelea kusikika mitaani. Makanisa mbalimbali nchini Tanzania yalikuwa yakiendelea na maombi kwa kutaka kuona Benedict akikamatwa na kufikishwa katika mikono ya sheria. Vilio vya watanzania bado vilikuwa kwa polisi kwani waliamini kwamba wao ndio walikuwa na uwezo mkubwa wa kuweza kufanikisha kukamatwa kwa Benedict.
Kamanda Idrisa alikuwa ametulia kitini huku macho yake yakiiangalia picha ya Benedict ambayo alikuwa ameipachika ukutani na kuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wakitafutwa na polisi. Akili ya Kamanda Idrisa haikuwa imetulia, muda wote alikuwa akimfikiria Benedict. Akayafungua mafaili ambayo yalikuwa mezani na kisha kuanza kuyasoma.
Kamanda Idrisa akatulia, jina la Benedict lilikuwa likijirudia mara kwa mara kichwani mwake. Hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya kwa wakati huo ili kufaniisha Benedict kutiwa mikononi mwa mikono ya sheria. Huku akiwa katika lundo la mawazo, mara simu ya mezani ikaanza kuita. Kwa haraka haraka akauchukua mkonga wa simu na kisha kuuweka sikioni.
“Nani anaongea?” Kamanda Idrisa aliuliza mara baada ya kuuweka mkoga wa simu sikioni.
“Bwana Nehemiah. Meneja wa Etisalat Mob…..” Mtu wa upande wa pili aliitikia lakini hata kabla hajamalizia, sauti ya mtu wa upande wa pili akaingilia.
“Niambie. Kuna mafanikio yoyote?”
“Kijana kaniletea ripoti na kuniambia kwamba kuna mpigaji alipiga simu ambaye alikuwa akihisi kwamba atakuwa ni Benedict” Bwana Nehemiah alisema.
“Huyo mpigaji alisemaje?”
“Alimpa taarifa mama yake kwamba alikuwa katika chumba cha nyumba ya wageni iitwayo Kieleweke” Bwana Nehemiah alijibu.
“Nyumba hiyo ya wageni ipo wapi?”
“Ipo Tandale. Pia mpigaji alisema kwamba angeondoka kuelekea Bagamoyo saa nne asubuhi” Bwana Nehemiaha alisema.
“Shukrani” Kamanda Idrisa alisema na kukata simu.
Furaha ambayo alikuwa nayo katika kipindi hicho ikaonekana kumchanganya kupita kawaida. Akayapeleka macho yake katika saa yake ya ukutani, akapigwa na mshtuko mara baada ya kuona kwamba zilibakia dakika tano tu hata kabla ya kuingia saa nne asubuhi, hakujua afanye kitu gani kwa wakati huo.
Kwa kipindi hicho, alijiona kufanya mawasiliano na watu wawili tofauti, wa kwanza alikuwa mkubwa wa kituo cha polisi cha Tandale na kumtaarifu juu ya kwenda katika nyumba ya wageni ya Kieleweke kwa ajili ya kumkamata Benedict. Lakini mtu wa pili alikuwa mkuu wa kituo cha polisi cha Mwenge kumtaarifu juu ya kwenda katika kituo cha daladala cha Mwenge.
Kamanda Idrisa hakutaka kupoteza muda, hapo hapo akaanza kubonyeza vitufe vya simu ya mezani huku mkonga wa simu ukiwa sikioni mwake. Simu ikaanza kuita, simu iliita kwa sekunde kadhaa, ikapokelewa.
“Kituo cha polisi Tandale” Sauti ya kike ilisikika.
“Kamanda Idrisa hapa. Nendeni katika nyumba ya wageni ya Kieleweke, Benedict yupo ndani ya nyumba hiyo” Kamanda Idrisa alisema kwa sauti nzito iliyojaa utetemeshi.
“Tayari vijana walikwishakwenda huko. Tulipewa taarifa na binti mmoja toka saa tatu asubuhi” Sauti ya upande wa pili ilisikika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Safi sana” Kamanda Idrisa alisema na kukata simu huku akingoja simu iingie na kumwambia ni kitu gani kiliendelea, kama kulikuwa na mafanikio ya kukamatwa kwa Benedict au la.
Wiki moja tayari ilikuwa imekatika tangu Benedict aanze kuishi katika nyumba ya wageni ya Kieleweke ambayo ilikuwa ndani ya mtaa wa Tandale. Ingawa zilikuwa zimepita siku kadhaa tangu achukue chumba ndani ya nyumba hiyo ya wageni lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye aligundua kwamba mtu yule alikuwa Benedict, mtu ambaye alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba na Watanzania. Mara kwa mara kofia yake aina ya Malboro ilikuwa kichwani mwake huku miwani yake myeusi ikimsaidia kuwaficha watu kumgundua.
Benedict hakuwa na wasiwasi tena, nyumba ile ya wageni ikaonekana kuwa sehemu nzuri kwake kwa kuendelea kujificha zaidi na zaidi. Watu mitaani pamoja na wapelelezi walikuwa wakiendelea kumtafuta mitaani bila kufahamu kwamba mtu ambaye walikuwa wakimtafuta alikuwa akiishi ndani ya nyumba ya wageni ya Kieleweke iliyokuwa katika mtaa wa Tandale. Muda mwingi Benedict alikuwa akiutumia kuwa ndani ya chumba chake, na kama alikuwa akitoka, basi alikuwa akipiga stori na Asha, msichana wa mapokezi.
Mara kwa mara Benedict alikuwa akipiga stori na Asha huku kofia yake pamoja na miwani vikiendelea kuwa mwilini mwake. Japokuwa alikuwa akiongea na Asha katika hali ya kawaida lakini kwa Asha hali ikaonekana kuwa tofauti. Kwanza aliipenda sauti yake, alikuwa akipenda jinsi ambavyo alivyokuwa akiongea kwa mpangilio mzuri lugha ya Kiswahili.
Moyo wa Asha ukaanza kujiingiza katika mapenzi mazito juu ya Benedict, mara kwa mara alikuwa akikaa nae na kupenda kupiga stori na Benedict. Moyo wake ulikuwa ukimsisimka sana kila alipokuwa akiisikia sauti ya Benedict masikioni mwake. Ingawa Benedict alikuwa akivaa kofia yake pamoja na miwani lakini bado Asha alikuwa akivutiwa sana na Benedict ambaye alijitambulisha kwa jina la Peter.
Mara kwa mara Asha alikuwa akimpelekea Benedict chakula, alikuwa akimpatia chakula na kumtandikia kitanda. Asha alitamani kujiweka wazi, moyo wake haukuwa ukijiamini hata mara moja kutokana na muonekano ambao alikuwa akionekana Benedict. Kila siku moyo wa Asha ulikuwa na mawazo juu ya Benedict, hakutaka kabisa kumuona Benedict akiondoka katika nyumba hiyo hata kabla hajamwambia ukweli juu ya moyo wake.
Mara baada ya Asha kuamka kutoka kitandani, akatandika kitanda na kutoka nje ya chumba chake. Siku hiyo aliamua kutaka kumwambia ukweli Benedict juu ya jinsi alivyokuwa akijisikia moyoni mwake. Hakutaka siku hiyo ipite kwa sababu ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa Benedict ambaye alijitambulisha kwa jina la Peter kuwa ndani ya nyumba hiyo.
Asha akaelekea chooni na kuanza kufanya usafi na kukiacha choo pamoja na bafu katika hali ya usafi. Kwa haraka haraka akaelekea nje ya nyumba hiyo na kuendelea na usafi. Mara baada ya kumaliza kila kitu, Asha akayapeleka macho yake katika saa ya ukutani, tayari ilikuwa saa tatu na dakika tano asubuhi.
Asha akaanza kupiga hatua kuufuata mlango wa kuingilia katika chumba alichokuwa akikitumia Benedict, akaanza kuchungulia kupitia katika kitundu cha funguo. Asha akalipeleka sikio lake na kuanza kusikiliza. Sauti ya Benedict bado ilikuwa ikiendelea kumdatisha. Aliisikiliza vizuri, akaanza kuunyonganyonga mwili wake.Kadri alivyozidi kuisikiliza sauti ile na ndivyo ambavyo mwili wake ulizidi kusisimka.
“Nipo ndani ya nyumba ya wageni ya Kieleweke huku Tandale” Sauti ya Benedict ilisikika vyema masikioni mwa Asha katika kipindi ambacho alikuwa akiongea na simu.
“Saa nne nitaondoka kuelekea Bagamoyo” Sauti ya Benedict iliendelea kusikika.
Asha akapigwa na mshtuko mara baada ya kugundua kuwa Benedict angeondoka kuelekea Bagamoyo asubuhi hiyo. Hata kabla hajaamua afanye nini, mara akasikia mlango wa chumba kingine ukifunguliwa, alichokifanya ni kuondoka mahali hapo na kuelekea mapokezini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asha hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kufanya kwa wakati huo. Alibaki akiwa na mawazo huku akifikiria kitu ambacho alitakiwa kukifanya. Mara akasimama, akaonekana kupata wazo fulani. Akasimama na kisha kuelekea chumbani kwake ambako akavua nguo zake zote na kisha kuvaa khanga moja tu.
Alichokifnya Asha ni kuvaa kandambili na kisha kutoka nje ya chumba kile na kuelekea bafuni ambapo akaoga. Lengo lake kubwa kwa wakati huo ni kujiweka katika hali ya usafi na kisha kwenda kugonga mlango wa chumba alichokuwa Benedict ambapo kama angefungua angeingia na kisha kumlazimisha kufanya nae mapenzi.
Alipomaliza kuoga, akatoka na kisha kuanza kuelekea katika mlango wa chumba cha kuingilia kwa Benedict, alipoufikia akaanza kuchungulia kupitia katika tundu la kitasa. Benedict alikuwa amejilaza kitandani mwake, Asha akaonekana kutabsamu. Mara Benedict akainuka na uso wake kuuelekezea katika upande ulipokuwa mlango.
“Mungu wangu!” Asha alisema mara baada ya macho yake kutua usoni mwa Benedict ambaye wala hakuwa amevaa kofia wala miwani.
Moyo ukamlipuka, macho yake hayakuamini juu ya kile ambacho alikuwa akikiona mahali hapo. Akamwangalia Benedict mara mbili mbili, kichwa chake kikaanza kufikiria fedha. Milioni ishirini zilizokuwa ndani ya brifukesi zikaanza kuonekana kichwani mwake. Akili yake ikachanganyikiwa kabisa, hakuamini kama alikuwa akikaa na Benedict pasipo kufahamu.
Mapenzi yote ambayo alikuwa nayo juu ya Benedict yakapotea, tamaa ya fedha ikaanza kumuingia moyoni mwake. Akajiona akipoteza muda kusimama pale mlangoni, kwa kasi ya ajabu akachomoka mlangoni pale na kuelekea chumbani.
Akavaa nguo zake kwa haraka haraka, akatoka chumbani na moja kwa moja kuanza safari ya kuelekea katika kituo cha polisi cha Tandale huku saa yake ikionyesha kwamba tayari ilikuwa ni saa tatu na dakika ishirini na tano asubuhi. Asha alikuwa akitembea kwa mwendo wa haraka haraka, alipoona kama angechelwa, akaanza kukimbia huku kichwa chake kikifikiria fedha tu kiasi cha shilingi milioni ishirini kama zawadi kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa Benedict.
Ingawa Asha alikuwa akitembea kwa mwendo wa haraka haraka lakini alikukuwa akijiona akichelewa kitu ambacho alitamani muujiza utokee, apotee na kutokea katika kituo cha plisi. Asha akaanza kukimbia, kila mtu njiani alikuwaa akimshangaa lakini Asha hakuonekana kujali kitu chochote kile. Kichwa chake kwa wakati huo kilikuwa kikifikiria fedha tu.
Hakutaka tena kuendelea kuwa mhudumu wa nyumba ya wageni, kitu ambacho alikuwa akikifikiria kwa wakati huo ni kuanzisha biashara zake mwenyewe hasa mara baada ya kupokea kiasi hicho cha fedha. Milioni ishirini kwake kilionekana kuwa kiasi kikubwa sana cha fedha ambacho kingemfanya kingemfanya kutatua matataizo ambayo alikuwa nayo. Harufu ya mafanikio ilizidi kusikika zaidi puani mwake.
Asha alitumia muda wa dakika kumi akawa amekwishafika katika kituo hicho cha polisi cha Tandale. Jasho lilikuwa likimtoka mfululizo, Asha akashindwa kuongea kitu chochote kile, akabaki akihema kwa nguvu huku akiwa amesiamama mbele ya kaunta katika kituo kile. Polisi waliokuwa zamu katika kipindi hicho walibaki wakimwangalia Asha ambaye bado alikuwa akiendelea kuhema kwa nguvu. Asha alitumia dakika moja kupumzika.
“Tukusaidie nini?” Polisi mmoja kati ya polisi waiokuwa zamu alimuuliza.
“Nimemuona Benedict” Asha alijibu.
“Benedict! Yupo wapi?” Polisi yule aliuliza huku wenzake wakiwa wamekwishafika mahali pale.
“Guest house”
“Guest ipi?”
“Kieleweke” Asha alijibu.
Kila polisi alionekana kushtuka, walimwangalia Asha mara mbili mbili huku wakionekana kutokuamini kile ambacho walikisikia wakati ule. Mara baada ya kumuuliza mara kadhaa na kuwapa uhakika, polisi wakatoka nje na kupanda ndani ya gari lao aina ya defender na kuanza safari ya kuelekea katika nyumba ya wageni ya Kieleweke.
“Dada..Una uhakika ni yeye?” Polisi mmoja alimuuliza huku akiwa ameshika bunduki.
“Ni yeye…ni yeye kabisa” Asha alijibu.
Dereva hakutaka kuendesha gari kwa mwendo wa taratibu. Gari liliendeshwa kwa mwendo wa kasi ambao ulionekana kumshangaza kila mtu aliyekuwa akiliangalia gari lile. Picha ambayo ilikuwa ikionekana machoni mwa wananchi kilionekana kuwa kama filamu ya mapigano hasa zile za nchini Marekani.
“Ni mbali sana dada?” Polisi mwingine ambaye allikuwa na bunduki aliuliza.
“Walaaa. Ni hapo tu mbele” Asha alijibu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara baada ya kufika katika kona ya kuelekea katika gesti ile, gari likasimamishwa. Kwa staili ya kikomandoo, polisi wakajirusha chini na kuanza kupiga hatua kuelekea katika eneo lililokuwa na gesti ya Kieleweke huku wakiongozwa na Asha. Ni ndani ya sekunde kadhaa tu wakawa wamekwishafika katika eneo la gesti ile na kisha kutawanyika katika staili ya kuizunguka.
Mara baada ya Benedict kumaliza kuongea na simu na mama yake, moja kwa moja akajilaza kitadani. Kichwa chake kikaanza kufikiria juu ya safari ya kuelekea Bagamoyo ambayo angeianza katika kipindi kichache kijacho. Hakutaka tena kuishi ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa kuona kwamba ni lazima angekamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Aliona kuwa na kila sababu za kuondoka ndani ya jiji hilo na kuelekea mbali kabisa. Benedict hakuwa radhi kuona akikamtwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria, kitu ambacho alikuwa akikitaka kwa wakati huo ni kupambana mpaka hatua ya mwisho. Lengo lake kwa wakati huo lilikuwa ni kuondoka kuelekea Bagamoyo ambapo huko safari nyingine ingeanza upya.
Mara baada ya kufikiria kwa kipindi fulani, Benedict akainuka na kuanza kuelekea mlangoni. Akaufungua mlango na kutoka nje. Macho yakatua sakafuni, alama za kandambili ambazo zilikuwa zimeloa maji zilikuwa zikionekana pale karibu na mlango. Benedict alizidi kuziangalia alama za kandambili zile ambazo ziliingia moja kwa moja mpaka ndani ya chumba cha Asha.
“Mmmh!” Benedict akatoa mguno.
Tayari wasiwasi ukaonekana kumshika. Akazidi kuzikodolea macho alama zile za kandambili, maswali kibao yakaanza kumiminika kichwani mwake, hasa sababu ambayo ilimfanya Asha kusogea mpaka pale katika mlango wa chumba kile.
Benedict hakutaka kuendelea kujiuliza maswali mengi ambayo hayakuwa na majibu, alichokifanya tena kwa haraka sana ni kuerudi chumbani ambapo huko akachukua taulo na kisha kuelekea bafuni na kuanza kuoga haraka haraka. Kila kitu ambacho alikifanya katika kipindi hicho, alikuwa akikifanya kwa haraka haraka.
Wananchi ambao walikuwa wakiwawaangalia polisi wale ambao walikuwa wamezunguka gesti ile walibaki wakishagaa tu. Hawakujuani kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea mpaka polisi wale kukusanyika mahali pale na kuizunguka gesti ile huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Wazo la ujambaza likaanza kuwaingi vichwani mwao kwa kudahini kwamba kulikuwa na majambazi walikuwa wamechukua chumba ndani ya gesti hiyo.
Polisi walitulia kwa muda, ulinzi mkali waliuweka katika milango mikuu yote ya kuingilia ndani ya gesti ile. Mara baada ya kuona kuwa hali ilikuwa shwari, mkuu wa kituo cha polisi cha Tandale, Bwana Muniru akaanza kuongozana na Asha kuingia ndani ya gesti ile huku polisi watatu waliokuwa na bunduki mikononi wakiwa pamoja nao.
Wateja wote ambao walikuwa ndani ya gesti ile wakaamriwa kuingia ndani ya vyumba vyao. Bwana Muniru, Asha pamoja na wale polisi watatu wakaanza kupiga hatua kukifuata chumba ambacho alikuwa amepanga Benedict, walipokifikia, Asha akaanza kuchungulia kwa kutumia kitundu cha kitasa sehemu ya kupitishia ufunguo.
Ndani, hasa kitandani hakukuonekana kuwa a mtu yeyote. Asha akaanza kuliita jina la Peter, jina ambalo Benedict alikuwa akilitumia lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliitikia kutoka ndani ya chumba kile.
Asha akakishika kitasa na kisha kuufungua mlango, mlango ukafunguka kutokana na kutokuwa na kutofungwa na ufunguo. Wote watano wakaingia ndani, chumba kilikuwa kitupu. Wakaanza kumtafuta Benedict katika kila kona ndani ya chumba kile lakini Benedict hakuonekana kitu ambacho kilionekana kumchanganya Asha.
“Mbona hayupo sasa?” Bwana Muniru aliuliza huku wakiendelea kumtafuta.
“Nilimuacha humu”
“Kama ulimbuacha mb……..” Bwana Muniru aliuliza lakini hata kabla hajamalizia swali lake, Asha akaingilia.
“Subiri” Asha alisema.
Asha akafungua kabati kwa mara ya pili na kisha kuanza kuangalia tena huku uso wake ukionekana kuhisi kitu. Polisi hawakuongea kitu chochote kile, walibaki wakimwangalia Asha ambaye alikuwa akiendelea kuangalia angalia ndani ya kabati lile huku akionekana kutafuta kitu. Aliporidhika, akayapeleka macho yake usoni mwa Bwana Muniru.
“Kuna kitu umehisi?”
“Ndio”
“Kitu gani? Tueleze”
“Taulo”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Taulo! Limefanya nini tena?”
“Silioni”
“Haulioni! Unamaanisha nini?”
“Atakuwa yupo bafuni anaoga”
Hawakutaka keuendelea kubaki ndani ya chumba kile. Kwa haraka haraka wakatoka na kuanza kuelekea bafuni. Kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba kwa wakati huo Benedict alikuwa bafuni akioga. Kila mmoja akaanza kutabasamu mara baada ya kusikika mtu akioga bafuni. Wakaandaa bunduki zao vizuri, wakasubiri zaidi na zaidi mpaka pale ambapo mlango wa bafu ulipofunguliwa na muogaji kutoka bafuni.
Kamanda Idrisa aliendelea kusubiri zaidi na zaidi. Hakukuwa na simu yoyote ambayo iliingia kutoka katika kituo cha polisi cha Tandale. Hakutaka kuendelea kusubiri zaidi na zaidi, akanyanyua mkonga wa simu na kuanza kupiga katika kituo hicho. Taarifa alizopewa ni kwamba polisi ambao walikwenda katika nyumba ya wageni ya Kieleweke hawakuwa wamerudi kituoni hapo.
Kamanda Idrisa alionekana kuchanganyikiwa, hakujua kama Benedict alikuwa amepatikana au la. Akanyanyua mkonga wa simu na kisha kupiga simu katika kituo cha polisi cha Mwenge. Simu ikaanza kuita, iliendelea kuita kwa sekunde kadhaa, simu ikapokelewa na sauti nzito ya mwanaume kusikika kutoka upande wa pili.
“Kituo cha polisi Mwenge”
“Kamanda Idrisa hapa”
“Ndio mkuu”
“Nendeni kwenye kituo cha daladala cha hapo Mwenge na kisha kagueni daladala zinazokwenda Bagamoyo, nadhani Benedict atakuwa huko. Fanyeni hima” Bwana Idrisa alisema kwa kutilia mkazo.
“Sawa mkuu” Sauti ya upande wa pili ilijibu na Kamanda Idrisa kukata simu.
Kamanda Idrisa akatulia, tayari moyoni alijiona kuwa mshindi. Kwa jinsi hali ilivyoonekana basi ilikuwa ni lazima Benedict akamatwe hapo hapo katika nyumba ya wageni ya Kieleweke au katika kituo cha daladala cha Mwenge.
Kila mmoja akapigwa na mshangao mara baada ya muogaji kutoka nje ya bafu lile. Mategemeo yao yalikuwa tofauti na picha ambayo ilikuwa ikionekana katika kipindi hicho. Mtu huyo ambaye alitoka bafuni katika kipindi hicho hakuwa Benedict kama jinsi ambavyo walifikiria kabla. Kila mmoja akaonekana kuchanganyikiwa. Kila mmoja alikuwa akimwangalia mtu yule mara mbili mbili huku nae akiwaangalia kwa macho yaliyojaa woga.
“Sio Benedict huyu….” Bwana Muniru alisema huku akimwangalia vizuri mwanaume yule.
Hawakutaka kubaki mahali pale, walichokifanya kwa wakati huo ni kuodoka katika sehemu ile na kisha kuanza kumtafuta Benedict katika vyumba vyote ndani ya gesti ile lakini hawakuwaweza kufanikiwa kumuona..
Asha akaanza kuelekea katika sehemu ya mapokezi. Akapigwa na mshtuko mara baada ya kuliona daftari la kuandikia wageni likiwa juu ya meza yake. Asha akalifungua na kisha kuanza kuangalia katika ukurasa ambao ulikuwa na jina la Peter, jina alilokuwa akilitumia Benedict na kisha kuanza kuliangalia.
“Mungu wangu! Kumbe amekwishaondoka leo asubuhi” Asha alisema huku akiwa haamini kile alichokuwa amekiona. Benedict alikuwa ameondoka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila kitu ambacho alikifanya Benedict alikifanya haraka haraka. Mara baada ya kutumia dakika moja katika kuoga, akachukua taulo na kuanza kujifuta. Alipomaliza, akavaa pensi aliyokuwa nayo bafuni na kutoka nje huku akilisahau taulo bafuni. Mara baada ya kufika ndani ya chumba chake akavaa nguo zake, akachukua kila kitu kilichokuwa chake na kisha kutoka ndani ya chumba kile.
Benedict akaanza kupiga hatua huku lengo lake likiwa ni kutoka nje, huku akiwa ameufikia mlango, akasimama, akionekana kukumbuka kitu. Akaelekea sehemu ya mapokezi na kisha kuchukua daftari la wageni waliokuwa wakiingia na kisha kutafuta jina lake bandia alilokuwa akiitumia, Peter na kisha kusaini kwamba alikuwa amekwishaondoka.
Benedict hakutaka kupoteza muda zaidi pale mapokezini, alichokifanya ni kuvaa vizuri kofia yake pamoja na miwani na kisha kuondoka mahali hapo na kuanza kuelekea katika kituo cha daladala cha Yemen huku lengo lake kwa wakati huo likiwa ni kutaka kuelekea Sinza.
Ndani ya gari, Benedict akaelekea katika kiti cha nyuma kabisa na kisha kukaa karibu na dirisha huku macho yake yakiangalia nje tu. Ingawa daladala ilikuwa na abiria kumi na mbili lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alijua kwamba Benedict alikuwa ndani ya gari lile. Mara baada ya kufika Sinza AfrikaSana, Benedict akateremka na kisha kuanza kutembea kuelekea katika kituo cha daladala cha Mwenge.
Benedict alitumia dakika kumi mpaka kufika katika kituo cha daladala cha Mwenge. Macho yake yakatua katika picha zake nyingi ambazo zilikuwa zimebandikwa huku neno kubwa lililosomeka ‘ANATAFUTWA’ likionekana katika kila picha huku kiasi cha shilingi milioni ishirini kikiwa kimewekwa kama zawadi ya atakayefanikisha kukamatwa kwake. Hapo hapo Benedict akaanza kupiga hatua kuzifuata daladala ambazo zilikuwa zikielekea Bagamoyo.
“Kiasi gani mpaka Bagamoyo?’ Benedict alimuuliza jamaa ambaye alikuwa akiita abiria.
“Elfu mbili mia tano”
Benedict akaifuata daladala hiyo ambayo ilikuwa na abiria saba na kisha kuingia na kutulia. Muda ulizidi kusonga mbele. Abiria waliendelea kuongezeka zaidi na zaidi, daladala ilipojaa, dereva akawasha gari na kisha safari ya kuelekea Bagamoyo kuanza. Benedict akapigwa na mshangao mara baada ya daladala kufika nje ya kituo hicho, magari matatu ya polisi yakafika na kuingia ndani ya kituo kile.
Kwa haraka sana polisi wote kumi na tano wakaruka chini huku wakiwa na bunduki mikononi. Kila mtu ambaye alikuwa ndani ya kituo kile alibaki akiwashangaa polisi wale ambao walikuwa wamevamia kwa ghafla sana ndani ya kituo kile. Polisi wakagawanyika, kuna wale ambao walibaki ndani ya kituo kile huku wengine wakiwa wamekizunguka kituo kile na kuanza kumtafuta Benedict.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakukuwa na mtu ambaye aliruhusiwa kutoka ndani ya kituo kile, kila kitu ambacho kilikuwa kikiendelea kilikuwa kimesimamishwa kwa muda. Madeiwaka ambao walikuwa wakipiga deiwaka mahali hapo wakaamriwa kuacha kufanya hivyo, kila kilichokuwa kikiendelea kilisimamishwa mpaka pale kila kitu kitakapokamilika mahali hapo.
Mkuu wa kituo cha polisi cha Mwenge, Bwana Matiku akaanza kupiga hatua kuelekea katika sehemu ambayo ilikuwa na magari yaendayo Bagamoyo. Bwana Matiku pamoja na polisi watano waliokuwa na bunduki wakaanza kuangalia katika magari yote yaendayo Bagamoyo lakini Benedict hakuonekana jambo ambalo liliwashangaza.
“Mkuu alisema Benedict yupo huku?” Polisi mmoja aliuliza.
“Ndio. Ila haonekani” Bwana Matiku alijibu.
“Kwa hiyo tufanye nini mkuu?”
“Ngoja kwanza” Bwana Matiku alijibu.
Hapo hapo Bwana Matiku akachomoa simu yake ya mkoni na kisha kuanza kulitafuta jina la Kamanda Idrisa. Mara baada ya kuliona, akabonyeza kitufe cha kijani na kisha simu kuanza kuita. Wala hazikupita sekunde nyingi, simu ikapokelewa. Maongezi yakaanzia hapo. Bwana Matiku akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilikuwa kimeendelea kituoni hapo.
“Wataarifu polisi wa Mapinga waanze kuangalia magari yaendayo Bagamoyo, nadhani atakuwa amekwishaondoka” Bwana Idrisa alisikika akisema.
Simu ikakatawa. Kwa haraka haraka Bwana Matiku akaanza kupiga simu katika kituo cha Mapinga na kuwaeleza kwamba msako ulitakiwa kufanyika kwa magari yote ambayo yalikuwa yakielekea Bagamoyo, haikujalisa daladala au gari za watu binafsi. Mara baada ya kutoa maelekezo, Bwana Matiku akakata simu na polisi wote kuondoka mahali hapo na kila kitu kuendelea kama kawaida.
Moyo wa Benedict haukutulia, mara kwa mara maswali mfululizo yalikuwa yakiendelea kumiminika kichwani mwake juu ya magari yale ya polisi ambayo yalikuwa yamefika katika kituo kile. Hakuelewa sababu ambazo ziliwafanya polisi kufika katika kituo kile, hakujua kama polisi walikuwa wamefika ndani ya kituo kile cha daladala kwa ajili yake au la.
Benedict hakutaka kuendelea kukisumbua kichwa chake kujiuliza maswali mfululizo ambayo hayakuwa na majibu. Akapuuzia, akayapeleka macho yake dirishani na kuanza kuangalia nje. Kila mtu ndani ya daladala alikuwa akifanya lake, watu wengine walikuwa wakiongea na simu huku wengine wakisoma magazeti ambayo waliyanunua katika kituo cha daladala cha Mwenge.
Dereva alitumia dakika kumi na tano mpaka kufika Bunju. Safari iliendelea zaidi na zaidi huku wakianza kulitafuta daraja la Mapinga.. Hakukuwa na abiria yeyote ambaye alikuwa akijua kama mmoja wa abiria ambao walikuwa ndani ya gari lile alikuwa Benedict, mtu ambaye alikuwa akitafutwa kwa udi na uvumba nchini Tanzania. Benedict alitulia kimya huku kofia yake aina ya Malboro pamoja na miwani yamwanga ikiwa vizuri usoni mwake.
Huku safari ikiendelea zaidi, mara foleni ikaanza kuonekana hata kabla ya kuingia katika daraja la Mapinga. Magari yakaanza kwenda taratibu huku wakati mwingine yakisimama. Kila mmoja alionekana kutokuelewa kitu chochote kile juu ya kilichokuwa kikiendelea ambacho kilikuwa kikisababisha foleni ile. Utingo wa daladala akateremka na kisha kuanza kuelekea mbele kuona ni kitu gani ambacho kilikuwa kikiendelea, baada ya sekunde kadhaa, akarudi.
“Vipi tena! Kuna ajali?” Dereva alimuuliza utingo baada ya kurudi.
“Hakuna ajali yoyote ile”Utingo alijibu.
“Sasa kuna nini?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Polisi wanafanya msako katika kila gari”
“Wanatafuta nini? Milungi au?”
“Kuna mtu wanamtafuta” Utingo alitoa jibu ambalo lilimshtua Benedict.
Polisi a kituo cha Mapinga hawakutaka kupoteza muda. Mara baada ya kupewa taarifa ya kukagua magari yote ambayo yalikuwa yakielekea Bagamoyo, moja kwa moja wakaingia katika magari yao na kisha kuanza safari ya kuelekea katika daraja la Mapinga. Kila polisi ambaye alikuwa ndani ya gari hilo alikuwa na shauku kubwa ya kutaka kumkamata Benedict ambaye alionekana kusumbua.
Mara baada ya kufika katika daraja la Mapinga, wote wakateremka na kisha kujipanga tayari kwa kuanza kazi hiyo. Kila gari ambalo lilikuwa likitaka kuvuka katika daraja hilo lilikuwa likipekuliwa kwa ajili ya kumtafuta Beedict. Upekuzi ulikuwa ukifanyika taratibu sana kiasi ambacho wakasababisha foleni kubwa mahali hapo.
Yalikuwa yamebaki magari ishirini kabla ya kufikia katia daladala ambayo alikuwepo Benedict. Muda wote Benedict alikuwa ameituliza akili yake huku akifikiria ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya mahali hapo. Benedict alitulia kwa muda fulani, akapata wazo la kufanya, tabasamu pana likaonekana usoni mwake.
Akayapitisha macho yake kwa kila abiria ambaye alikuwa ndani ya daladala ile. Kila abiria alionekana kukasirika kutokana na foleni kubwa ambayo ilikuwa imetokea katika eneo lile karibu kabisa na daraja la Mapinga. Benedict alitulia kwa muda, akaisoma hali iliyokuwepo ndani ya daladala ile, akaingiza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha shilingi elfu tano.
Benedict hakuwa radhi kujiona akitiwa katika mikono ya polisi na wakati hakuwa amefika mwisho wa safari yake ile. Alitamani sana kuingia mjini Bagamoyo hata kabla hajapanga ni safari ipi ingeanza baada ya hiyo. Akayapeleka macho yake katika saa yake, foleni bado ilikuwa ikiendelea hadi kufikia magari kumi na tano kabla ya daladala ile kufika darajani.
“Shika hii konda. Nishushe Bunju” Benedict alimwambia konda wa daladala ile huku akimpa kiasi kile cha fedha.
Kila abiria akashtuka, wakaanza kumwangalia Benedict pasipo kumgundua kutokana na kofia pamojana miwani ambayo alikuwa ameivaa. Kauli yake ya kutaka kushusha Bunju ndio ambayo ilionekana kuwashtua wote. Wakashindwa kuelewa kama mtu yule alikuwa mgeni au la. Benedict hakuonekana kujishtukia, maneno ambayo alikuwa ameyaongea yalikuwa sawa na uso wake.
“Ulikuwa umelala nini bro? Mbona Bunju tumekwishapita kitambo” Konda alisema maneno ambayo yalimfanya Benedict kujifanya kushtuka.
“Unasemaje?”
“Bunju tumekwishapita kitambo” Konda alimwambia Benedict.
Benedict hakutaka kuendelea kubaki ndani ya daladala ile, hapo hapo akainuka na kuanza kuufuata mlango. Konda akamgawia kiasi cha nauli ambacho kilibakia na kisha kuteremka. Benedict akaanza kupiga hatua kuelekea kule ambapo walikuwa wametoka. Mwendo wake ulikuwa ni wa haraka haraka, hakuamini kama alikuwa ametoka salama ndani ya daladala ile.
Benedict hakutaka kuendelea kuifuata barabara, alichokifanya ni kuingia katika pori la Mapinga na kuendelea na safari yake kwa miguu. Ingawa wakati huo ulikuwa ni asubuhi, jua lilikuwa kali sana hali ambayo ilimfanya kupumzika chini ya miti mara kwa mara. Benedict hakutaka kurudi tena ndani ya jiji la Dar es Salaam, dhamira yake kwa wakati huo ilikuwa ni kuelekea ndani ya mji wa Bagamoyo tu ambapo baada ya kufika huko angejua ni safari ya wapi ambayo alitakiwa kwenda.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akili yake bado ilikuwa ikiwafikiria ndugu zake, mama yake, Bi Meriana pamoja na dada yake, Angelina. Bado alihitaji kuwaona kwa mara nyingine tena. Hakutaka kuwasiliana nao katika kipindi hicho, alihitaji kupata sehemu ambayo angekaa na kutulia. Safari yake bado ilikuwa ikiendelea kama kawaida, alipita katika sehemu zilizokuwa na nyasi nyingi na miti mirefu hadi kuufikia mto wa Mapinga.
“Nataka kuvuka ng’ambo” Benedict alimwambia jamaa ambaye alikuwa na mtumbwi mdogo.
“Mia tatu tu” Kijana yule alimwambia Benedict.
Benedict hakutaka kupoteza muda, akaingia ndani ya mtumbwi ule na kisha kijana yule kuanza kupiga kasia. Benedict hakutaka kuongea kitu chochote kile na kijana yule, macho yake yalikuwa yakiangalia miti mirefu ambayo ilikuwa imezunguka mto ule. Walitumia dakika mbili wakawa wamekwishafika ng’ambo ya pli ya mto ule na kisha kumlipa kijana yule.
“Dah! Cheji sina bro” Kijana yule alimwambia Benedict mara baada ya kulipwa kiasi cha shilingi mia tano.
“Usijali Chukua yote tu ila nahitaji unisaidie kitu kimoja” Benedict alimwambia kijana yule.
“Kitu gani?”
“Nataka nifike Bagamoyo Mjini. Kuna njia ya kwenda huko?”
“Ndio. Pita njia hii, utatokea katika barabara ya lami na kis………”
“Sihitaji kutumia gari. Nataka kwenda kwa miguu kwa njia za panya” Benedict alimwambia kijana yule na kumpa maelekezo mapya.
Benedict akaendelea na safari yake ya kuelekea bagamoyo. Jua bado lilikuwa kali sana kiasi ambacho mara kwa mara alikuwa akipumzika katika vivuli chini ya miti. Alipita katika njia iliyokuwa na pori zaidi na kisha kuanza kuingia katika mashamba ya watu. Hakutaka kabisa kutumia barabara ya lami, hakutaka kuonekana na mtu yeyote ambaye alikuwa akitoka ndani ya jiji la Dar es Salaam ambalo lilikuwa na picha zake nyingi.
Mara baada ya kumaliza pori, akatokea katika sehemu ambayo ilikuwa na uwazi mkubwa sana. Benedict akaiangalia sehemu ile vizuri, ilikuwa ni eneo kubwa ambalo lilikuwa na shamba la mpunga. Akayapeleka macho yake katika kila kona ndani ya shamba lile, hakukuwa na mtu yeyote yule.
Benedict akaanza kupita katika njia iliyokuwa shambani pale. Machale yakaanza kumcheza, amani ikaanza kutoweka moyoni mwake, akaanza kuangalia vizuri katika kila kona ya shamba lile.. Benedict akapigwa na mshtuko wa hofu mara baada ya kuliona kundi la watu wakiwa wanakimbia kumfuata kule alipokuwa huku mikononi mwao wakiwa na silaha mbalimbali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Benedict alitamani kukimbia lakini miguu yake ikafa ganzi. Mwili mzima ukaanza kumtetemeka huku kijasho chembamba kikianza kumtoka. Benedict akatulia kuona ni kitu gani ambacho kingeendelea baada ya hapo. Watu wale wakamsogelea zaidi, hofu ikazidi kumkamata, hakujua ni kitu gani ambacho alitakiwa kukifanya katika kipindi kile.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment