Simulizi : Machozi Ya Baraka
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku iliyofuata Bi.Mwasi aliamka Asubuhi na mapema ili kumuandaa Baraka Kwenda shuleni.Tausi alimsaidia mama yake kuandaa chai kisha wakapata kifungua kinywa,walipomaliza wakaongozana kuelekea shuleni.Baada ya muda walifika shuleni,Tausi alimsukumu kaka yake na kumpeleka darasani.Siku hiyo waliwakuta wanafunzi na waalimu wote wameshafika ,Baraka Ghafla aliisi mtu akija nyuma yake,alipogeuka alikutana uso kwa uso na Juma,walisalimiana kisha haraka Juma alimtaka Tausi amuachie yeye kumsukuma Baraka kuelekea darasani,Tausi alimuachia kisha Juma akamchukua Baraka na kumsukuma kuelekea darasani.“Juma ana huruma jamani”Tausi alijisemea moyoni kisha akaondoka kuelekea darasani mwake, ambapo alikuwa anasoma darasa la sita katika shule hiyo.Wakati Bi.Mwasi akiondoka nyumbani, wakati yupo njiani alikuwa mtu mwenye mawazo Sana alionekana muda mwingi akiwa anaongea peke yake.Baadhi ya watu waliokuwepo maeneo hayo walidhani amechanganyikiwa,hawakumsemesha walimuacha akaendelea na safari zake.
Baada ya wanafunzi kumaliza kusafisha mazingira ya shule yao, waliingia darasani kama kawaida na kipindi cha kwanza kikaanza waalimu wakaingia madarasani.Katika darasa analosoma Baraka na rafiki yake Juma aliingia mwalimu Njaidi na kuanza kufundisha.Ambapo mwalimu huyo alifundisha kwa vitendo tena kwa upendo wa hali ya juu kwa wanafunzi.Wakati mwalimu Njaidi akiendelea kufundisha mwanafunzi aitwaye Benson alitembea kwa kunyata na kumsogelea Baraka alipokaa kisha akamfinya.Baraka alishtuka mithili ya mtu aliyeumwa na Nge,alipiga ukemi mkubwa uliowashtua darasa zima,Mwalimu Njaidi aligeuka ghafla na kumuona Baraka akilia kwa uchungu kisha akamfuata na kumwuliza
“Umefanya nini Baraka?
“Nimefinywa Mwalimu”Baraka alijibu huku akilia
“Ni nani aliyekufanya kitendo kicho?”Mwalimu Njaidi alimwulizaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baraka hakumjibu badala yake aliendelea kulia tena safari hii kwa sauti kubwa Mwalimu Njaidi alivyoona hivyo alimsogerea karibu Baraka na k umtaka anyamaze, amwambie aliyemfinya ni nani?.Mwalimu Njaidi alipoona Baraka hamjibu aliwageukia wanafunzi na kuwauliza,”Ninawauliza wanafunzi wote ni nani aliyemfinya Baraka? Ukimya wa ajabu ulitawala darasani, kila mwanafunzi alitulia tuli kama maji mtungini.”Iwapo hakuna atakayejibu, basi kila mmoja wenu atakwenda kuchimba shimo la taka.”Mwalimu Njaidi alisema .Wakati Benson akimfinya Baraka, Mwajuma ambaye ni mlemavu wa miguu aliyekuwa amekaa karibu na Baraka alimwona hivyo alipoona adhabu ikimkabili aliinua mkono kisha akasema.
“Mwalimu, mimi nimemwona aliyemfinya Baraka”Mwajuma alisema
“Ni nani mtaje haraka!”Mwalimu Njaidi aliwaambia
“Ni Bensoni mwalimu”Mwajuma alisema
“Benson simama”mwalimu Njaidi alisema
“Kwanini umemfinya Baraka?”
“Nimemjalibu mwalimu nilitaka nione hisia zake”Benson alijibu
“Ulitaka uone hisia zake, kivipi? Mwalimu Njaidi alimwuliza kwa ukali
“Nilitaka kujua kama mpole au mkolofi”Benson alijibu
“Kwahiyo umepata jibu gani?”Mwalimu Njaidi alimwuliza
“Mpole mwalimu tena mjinga sana huyu”Benson alijibu kwa dharau
“Wewe Benson ni mwanafunzi mtundu sana tena mkorofi mno,sasa leo utapata adhabu”
Mwalimu Njaidi alimpa adhabu Benson ya kuchimba shimo ili iwe fundisho kwa wanafunzi wengine wenye tabia kama hiyo.muda huo ilifika mwisho wa kipindi cha mwalimu Njaidi kufundisha aliwaanga wanafunzi na kutoka.Juma alifurahi sana kuona Benson akipewa adhabu na mwalimu Njaidi,alisogea karibu na Baraka kisha akamwambia anyamaze na kumtaka ajifute machozi,kwani Bensoni ni mwanafunzi mtundu sana katika darasa hilo,kuna kipindi alimchokoza na kumpiga ngumi ya usoni mwanafunzi mmoja kipofu.Baraka alinyamaza na kuendelea kuandika huku Juma alienda sehemu anapokaa na kuchukua vifuniko vya soda na kumletea Baraka ili ahesabu nambari kwa kufuatilia vifuniko hivyo.Baraka alifurahi kuletewa vifuniko hivyo akahesabu kwa makini huku akiandika.
Siku zilikatika miezi ikayoyoma hatimaye Baraka akafikisha miezi miwili Shuleni.Ndani ya miezi hiyo aliweza kusoma na kuandika japokuwa sio sana, Siku moja Majira ya mchana Baraka akiwa msalani kujisaidia, walitokea wanafunzi wenzake Benson na Sadiki, walimfuata na kumwagia maji walimlowanisha mwili mzima kisha wakakimbia. Baraka akajiisi baridi akaanza kutetemeka na mwili ukaanza kunyongonyea na kuonekana kama kifaranga cha kuku.Baada ya kumwagia maji mwenzao Benson na Sadik walikimbilia darasani na kutulia tuli kama sio wao wakajifanya kulala huku wakinong’onezana,
“Tumemuweza leo Albino Yule”Benson alisema
“Sijui kaja kufanya nini shuleni, mtu mwenyewe Albino macho aoni alafu kutembea ndio kabisa anachechemea”Sadiki alisikika
“Yaani shida tupu pale na atakoma mwaka huu”Benson alisema
“Namshangaa Juma ana urafiki nae”Sadiki alidakia
“Yaani Rafiki Albino, hasiyeweza kutembea mimi siwezi kabisa”Benson alisema.
Wote wakaachia kicheko kikali mno huku wakigonganisha viganja wa mikono yao juu.Wakati Benson na Sadiki wanamwagia maji Baraka Juma aliwaona aliwaacha mpaka pale walipomaliza kufanya tendo hilo na kutoka. Juma aliingia chooni maana alijua fika kama Benson na rafiki yake watakuwa wamemfanyia kitu Baraka kisicho cha kawaida,Maana yeye wakati anampeleka Baraka chooni alimsubili nje ,hivyo wakati kina Benson na mwenzake wanatoka aliwaona wakiwa wanacheka cheka.Juma alimsubili Baraka pale nje bila mafanikio akajua mwenzake amepata tatizo akaamua kwenda kumwangalia,Alipoingia tu alimkuta Baraka akiwa amelowana maji huku akilia,Juma hakutaka kumwuliza kilichomtokea,moja kwa moja akajua kina Benson na Sadiki ndio waliofanya kitendo hicho,alimnyanyua Baraka na kumpeleka Ofisini.
Juma na Bahati waliingia moja kwa moja mpaka ndani ya ofisi hiyo,Baadhi ya waalimu walipowaona hawakuuliza chochote kilichompata mpaka akawa katika hali hiyo,waliendelea na shughuli zao hawakumjali wala kumthamini mtoto huyo.Juma alisogea karibu kabisa na meza zao,kisha akawaelezea kilichomkuta Baraka,Mwalimu Gama alikasilika sana kile kitendo alichofanyiwa Barakakilikuwa cha ubaguzi tena kwa watoto ,je wakiwa wakubwa wakiiendeleza tabia hii si itakuwa matatizo kwa jamii yetu aliwaza mwalimu Gama kisha akainuka na kuelekea Darasani,
“Ben…. Simama haraka.Kwanini umemwagia na kumlowesha Baraka?”Mwalimu Gama aliuliza
“Sio Mimi mwalimu”Benson alijibu
“Kumbe ni nani aliyefanya kitendo hicho?”Mwalimu Gama akauliza
“Ni Sadiki mwalimu”Benson alijitetea
“Nyie watoto, kwanini mnapenda kumwonea mwenzenu? Mwalimu Gama alisema kwa ukali kisha akaendelea “Huyu ni mtoto kama ninyi, lazima mpendane ili kuikomesha na kuikemea tabia hii ya unyanyasaji kwa walemavu.Kengele ya kuondoka nyumbani itakaposikika nataka mnifuate ofisini”Mwalimu gama aliwaambia kwa ukali.......
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa siku ya jumatano majira ya asubuhi na mapema siku hiyo ilionekana kama mkosi kwa Baraka kwani alipofika shuleni,alikuta wanafunzi wote wapo kimya wametulia,hata wale wanafunzi watundu wote wametulia yaana darasa lilikuwa kimya kabisa.Baraka aliingia darasani huku mwili ukimtetemeka, hofu ikamjaa tele na moyo unakwenda mbio.Akajongea sehemu yake akaangaza macho yake huku na kule alimuona Juma akiwa ametulia tu naye akakaa kimya akiwa na wasiwasi.Taratibu mlango ulifunguliwa mwanga wa jua ukapenya mpaka darasani na kuwasumbua wanafunzi Albino waliokuwepo maeneo hayo. Je nani aliyefungua mlango huo?
Kipindi cha hesabu kilipofika mwalimu Aisha aliingia darasani ,siku hiyo wanafunzi wote waliokumo darasani mle walinywea kutokana na kumuogopa mwalimu hiyo.Walemavu wote walikuwa wametulia kama wafungwa gerezani,ilikuwa kawaida kwa Mwalimu Aisha kufundisha somo la hesabu katika darasa ilo, lililokuwa limechanganywa wanafunzi walemavu na wasio walemavu.Mwalimu Aisha ana kawaida yake anapoingia darasani wanafunzi wote usimama kisha uanza kuwauliza maswali,yule ambaye atakayepata kujibu kwa usahihi swali atakalouliza ndiye atakayeruhusiwa kukaa chini.Siku hiyo alipoingia Darasani aliuliza maswali,Baadhi ya wanafunzi wakajibu akauliza tena safari hii aliwageukia walemavu na kuwataka kulijibu swali lakini,hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyediliki kulijibu swali hilo.Mwalimu Aisha alihamaki kisha akawasogelea na kuwaambia,
“Yaani walemavu hamna akili ata kidogo, naomba mtoke mbele mkae nyuma ya darasa”Mwalimu Aisha akawaamuru kwa ukali kisha akaendelea “Mimi ninafundisha ninyi kazi yenu mnanikodolea macho tu.Wewe Albino mdomo unao, wewe usiyeona masikio unayo, lakini nyote mnaniangalia.Wanafunzi hao walemavu walitii amri ya mwalimu wao, waliinuka na kukaa nyuma kabisa ya darasa hilo.Tendo hilo halikumpendeza Juma, alikasilika kusikia maneno yale kutoka kwa mwalimu Aisha. Akaamua kuvunja ukimya na kuzungumza,
“Hee! Mwalimu sio vizuri kuwakalipia wanafunzi wenye ulemavu”Juma alisema
“Wanakela mpaka wakati mwingina najisikia vibaya”
“Kila siku tunafundishwa na kuwekwa wazi kuwa walemavu ni wenzetu tuwapende”Juma aliongea
Juma alipoongea hivyo mwalimu Aisha alistuka Sana, akakumbuka kuwa kauri ya Juma ilikuwa ni ukweli mtupu kwani muda mwingi wataalamu wa elimu ya walemavu walikuwa wakifika mara kwa mara pale shuleni hapo kisha walitoa nasaha na elimu ya watoto wenye ulemavu juu ya namna na kuwasaidia.
Muda huo Mwalimu Aisha alikuwa amesimama karibu kabisa na dawati analokaa Juma, macho yake yakiwaangalia watoto walemavu, ambao walikuwa wamekaa kimya huku wengine walikuwa wameshika tama.Licha ya Juma kukwazika na tendo hilo, mwanafuzi Shamila pia alionekana kukasilika pia kwa kitendo cha mwalimu Aisha ila hakutaka kuongea kitu alikaa kimya na lake rohoni.
“Haya tuendelee kusoma jamani, nimeshaamua wakae nyuma kwa leo, kesho watakuwa wameshashika adabu”Mwalimu Aisha alisikika.Mara ghafla Shamila aliinua mkono ili kusema kitu,
“Haya unasemaje na wewe? Mwalimu Aisha aliuliza kwa fedhea
“Mwalimu naomba kuuliza swali”Shamila alisema
“Ehee! Uliza”
“Kwanini unawafanyia hivyo watoto wenye ulemavu, si wanasema tusiwatenge na kuwanyanyasa, sasa wewe mbona unawanyanyasa? Shamila aliuliza
Mwalimu Aisha hakujibu swali hilo kutoka kwa mwanafunzi wake .Hasira zilimshika kutokana na kujisikia vibaya ,alijiona kama amechomwa mkuki moyoni mwake,kwani hakutegemea kusikia swali kama hilo kutoka kwa mwanafunzi wake.Alijisikia aibu iliyotukuka ndani yake,alijiona kama amevuliwa nguo adhalani,alistaamili na kuvumilia aliyoyaisi ndani ya moyo wake.”Wewe Shamila, kwanini unaniuliza hivyo? Wanafunzi wa siku hizi hamna hata heshima kazi kulopoka lopoka tu”Mwalimu Aisha aligutuka na hasira zikampanda akachukua mkoba wake na kutoka darasani bila kupindi chake kumalizika.
Baada ya nusu saa kupita tangu mwalimu Aisha kutoka katika darasa hilo, Mwalimu Gama aliingia darasani aliwakuta watoto wenye ulemavu wote wakiwa nyuma ya darasa.Aliona hali hisiyo ya kawaida kwa darasa hilo, wanafunzi wengi walionekana wakiwa kwenye majonzi, mwalimu Gama akuelewa kilichowasibu wanafunzi hao.Japokuwa yeye ndio mwalimu wa darasa hilo, upendelea kila siku wanafunzi walemavu kukaa mbele ya darasa ili wapate kuelewa na kumsikiliza vizuri kinachofundishwa.Lakini leo ndani ya darasa hilo amekuta sivyo ndivyo alivyowapanga.Mwalimu Gama aliwaza na kuwazua ili kutaka kujua nani aliyefanya kitendo kile cha kuwaamisha wanafunzi wale,akafikiria ratiba ya vipindi siku hiyo mara moja akapata jibu kwa mtu aliyefanya tendo hicho.Mwalimu Gama akaamua kuwaamuru wanafunzi hao kurudi katika nafasi zao,wanafunzi hao walirejea kila mmoja sehemu yake kisha wakakaa kimya kumsikiliza Mwalimu wao.Baada ya dakika kadhaa Mwalimu Gama akaanza kufundisha kwa upole na kuwaelewesha wote.Wanafunzi hao walifurahi sana wakapata fursa ya kuuliza na wao maswali Kwa Mwalimu huyo,walifurahi wamepata mlezi bora.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya miaka kadhaa Baraka akiwa darasa la saba alikuwa tayari ameshazoea na kuyajua mazingira ya shuleni,alicheza michezo mbali mbali kwa ajiri ya kuunyoosha mwili wake Michezo hii ilimfanya Bahati aonekane Kijana mtanashati,Mwalimu Njaidi aliwataka wanafunzi wajifunze kuchora,kurusha mpira wa kikapo,Baraka alifanya yote hayo kucheza na wenzake.Utaratibu huo wa mazoezi ulimsaidia sana Baraka.Baada muda kupita aliyazoea sana maisha ya shuleni na nyumbani,hakuitaji kushikwa wala kusaidiwa anapotoka nyumbani kwenda shuleni na kurudi tena nyumbani.Mwalimu Njaidi alitokea kumpenda sana Baraka kutokana na juhudi zake katika masomo na michezo.Kila mara alimchagu a ili kuwaongoza wanafunzi wenzake katika michezo,jambo hilo liliwakasilisha sana wanafunzi wenzake hasa Benson na Sadiki,walikuwa na chuki ya ajabu kwa Baraka.Walimfanyia kila aina ya visa ili kumkosesha amani walimuona analinga kupendwa na mwalimu ,walikuwa hawaishi kumuonea na kumkebei Baraka kuwa karibu na mwalimu Njaidi kama mtoto wake.....
Siku moja wanafunzi wote walikuwa katika kipindi cha michezo walicheza na kuimba michezo mbalimbali huku wakiwa na mwalimu wao wa michezo Bwana Kundakombe.Wapo waliocheza mpira wa miguu, vollball, basketball.Baraka alikuwa anacheza mchezo wa vollball na wenzake akiwemo Juma, alikuwa akizunguka vema ndani ya uwanja mdogo mpaka Benson akawa anamuonea gere.Baada ya muda kipindi hicho kikaisha kengele iligongwa, wanafunzi wote wakaanza kutawanyika kurejea nyumbani. Baraka akiwa anamsubili Juma ili waondoke pamoja, Ghafla alisikia mtu akishika bega la mkono wa kulia na kumsukumiza moja kwa moja alirushwa mpaka chini, alijisikia maumivu ndani ya kifua chake akajikaza na kujizoa zoa pale chini ili amwangalie aliyemsukuma ni nani.Bahati alimuona Bensoni na Sadiki wakiwa wameshikilia begi lake huku wakicheka kwa kejeli, akashindwa kuvumilia akaanza kulia nao wakazidi kumcheka na kulizungusha begi lake na kulitupilia pembeni.
Kilio cha Baraka kilikuwa kikubwa kwa wakati huo wanafunzi walikuwa wameshaanza kutawanyika,hakuna aliyekuwa akimuona Baraka kwenye masaibu hayo.Baada ya muda kilio kikawafikia baadhi ya walimu waliokuwepo ofisini kwao.Mwalimu Njaidi aliposikia sauti hiyo akaifahamu moja kwa moja kuwa ni Baraka,alitoka na kuelekea upande ilipotokea sauti hiyo.Alipofika pale alipigwa na bumbuwazi kumuona Baraka yupo chini katikati ya dimbwi la maji machafu,mwili wake umetapakaa chapachapa kwa matope na begi lake limetupwa kando ya dimbwi hilo.Mwalimu Njaidi alishangaa zaidi alipomuona damu zikimtoka puani mithili ya bomba la maji,aliamua kumsogerea karibu zaidi kishachukua kitambaa chake cha mkononi na kumfuta, kisha akachukua begi na kulifutafuta vizuri maana baadhi ya madaftari yalikuwa yamechafuka.Alipoakikisha vitu vyake vyote vipo vizuri ndani ya begi akamwinua na kumsaidia kukaa,baada ya muda Mwalimu Njaidi alimwuliza Barakakilichomsibu.
“Baraka embu niambie, umefanya nini?”
“Bensoni mwalimu”Baraka alijibu
“Amekufanya nini?’Mwalimu Njaidi alimwuliza
“Amenisukuma mpaka nikaanguka, alafu wamechukua begi langu na kulitupa kwenye matope?”Baraka alijibu huku akilia
“Pole! Jamani wanafunzi hawa hawaishi kwa utundu kesho lazima niwape adhabu”Mwalimu Njaidi alimwambia
Baada ya kujilidhisha na kuelewa kilichomsibu Baraka, mwalimu Njaidi alimchukua Baraka na kumpeleka hospitali iliyopo ndani ya shule hiyo.Walipofika daktari alimchunguza Baraka kisha akampatia matibabu. Muda huo huo Juma naye alipata taarifa za kuumia kwa Baraka akaelekea ndani ya hospitali,Baada ya kukamilisha taratibu za shuleni hapo Mwalimu Njaidi alimtaka Juma kumpeleka Baraka nyumbani kwao,Juma alikubali kisha akamchukua Baraka na kumpeleka.Baaada ya mwendo wa kinyonga kwa sababu ya maumivu aliyokuwa nayo ,walichukua takribani dakika ishirini kufika nyumbani kwa Bi.Mwasi,walimkuta mwenyeji wao akiwa jikoni akiandaa chakula cha mchana,Juma alibisha hodi kisha wakaingia ndani.Walipoingia tu Bi.Mwasi alishangaa kumuona mwanae akiwa na majeraha usoni huku akikosa furaha,aliacha kupika na kumsogelea Baraka na kumwuliza kilichomsibu
“Hee! Vipi tena Baba?”
“Nimepigwa na kutupiwa kutupiwa begi langu kwenye matope mama”Baraka alimjibu mamaye huku akilia
“Ni nani aliyekupiga mwanangu?”Mamaye alimwuliza
“Bensoni na Sadiki!”Baraka alijibu
“Pole mwanangu! Ndio faida ya shule hiyo”Bi.Mwasi alimwambia mwanae
“Ahsante mama!”Baraka alijibuCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mi nilisema watakuonea wenzako umeona sasa!”Mwasi alimwambia kwa uchungu
Juma aliaga na kuondoka huku nyuma mama yake alimtaka kunyamaza na kusamehe maana yeye ni mlemavu uwezo wa kupambana na wenzake hakuwa nao, Baraka alimsikiliza mamaye na kufuta machozi yaliyokuwa yakiendelea kumtoka kisha akanyamaza,aliongoza moja kwa moja chumbani kwake kisha alibadilisha nguo na kisha akaenda kuoga kwani alichafuka mwili mzima .alipomaliza kukoga akaingia ndani na kujitupa kitandani usingizi ukampitia.
Siku iliyofuata Baraka aliamka asubuhi na mapema kuliko siku zote, alijitayarisha kama kawaida kisha akachukua begi lake na taratibu kuelekea shuleni, alipofika shuleni aliingia darasani .Baada ya muda Mwalimu akaingia, siku hiyo kipindi cha kwanza kilikuwa kipindi cha Hesabu, hivyo kilipogonga Mwalimu Aisha aliingiakama kawaida yake akaanza kuuliza maswali kwa wanafunzi wa darasa hilo.Swali lake la kwanza alimwuliza Baraka “Nitajie milango mitano ya fahamu?”Maskini Baraka hakuweza kulijibu swali haraka haraka, alikuwa akitafakari jinsi ya majibu ya swali hilo.
“Mbona hujibu wewe?”Mwalimu Aisha akamwuliza
“Najibu mwalimu”Baraka alijitetea
“Nipe jibu sasa hivi!
“Milango ya fahamu ni macho, pua….sikio….”Baraka alijibu kwa kujiuma huma
“Hivi wewe unajiona kabisa ni Albino alafu mlemavu wa miguu tena uliozaliwa nao, unakuja kufanya nini shuleni wenye uzima wapo majumbani mwao hawasomi, je ninyi mnaojifanya kusoma sana mtaweza? Mimi huwa sipendi kabisa walemavu”Mwalim Aisha alimshushia maneno makali.
Baada ya muda mfupi kilio kilisikika kutoka kwa Baraka, kilikuwa kilio kilichosababishwa na mwalimu huyo aliyemkalipia darasani kutokana na kutokujibu swali lake.Baraka alijisikia vibaya mno, alijuta kwanini alikwenda shule, badala ya kubaki nyumbani. Juma pia hakuvipenda vitendo hivyo vya mwalimu huyo, aliona kabisa mwalimu Aisha hakuonesha tabia nzuri katika kazi yake.Siku hiyo Baraka alirudi nyumbani akiwa hana furaha alipofika alikuwa amekasilika sana ata mama yake aliona hali hiyo akamwuliza Baraka hakuficha kitu aliamua kuongea ukweli huku akianza kulia....
“Shuleni kuna mwalimu ananionea mama”
“Amekufanya nini”mamaye aliuliza
“Amenitukana na kuninyanyasa kwa muda mrefu bila sababu”Baraka alimwambia mama yake yote yaliyotokea tangu alipomfahamu mwalimu Aisha.
“Pole sana mwanangu, unatakiwa kuwa mvumilivu kwani mvumilivu ula mbivu”Bi.Mwasi alimsihi
*******
Ilikuwa asubuhi na mapema siku hiyo Bi.mwasi aliwai kuamka ili kumtengenezea kifungua kinywa mwanae.
Chai ilikuwa jikoni ikifuka moshi na baada ya muda ilikuwa tayari, aliwaita watoto wake ili kupata kifungua kinywa mapema na kuwai suleni.Baraka na Tausi walitoka ndani ili kujumuika pamoja na wazazi wao kupata kifungua kimywa.Siku hiyo Bwana Ahmed hakwenda kazini, alikuwa pamoja na familia yake nyumbani. Walipofika mezani Bi.Mwasi alishangaa alipomuona Baraka akiwa hakuvaa nguo za shule kama inavyokuwaga uvaa kabisa kisha unywa chai na kuelekea shuleni lakini siku hiyo hakuvaa nguo hizo yeye alikuwa amevaa nguo za nyumbani,Mama yake alimwuliza kilicho msibu ili apate kumsaidia lakini Baraka alikataa kumweleza kilicho moyoni mwake kuhusu mwalimu aisha lakini baadae akaamua kumwambia mzazi wake
“Mama mimi leo siendi shule”
“Kwanini mwanangu?
“Mwalimu Njaidi yeye anatupenda sana, lakini mwalimu Aisha hatupendi, kwa hiyo nimeamua kubaki nyumbani”Baraka alisema
Mama Yake aliposikia maneno hayo, alijisikia vibaya Sana akaisi kuna jambo zito mbele ya mwanae, akaona nuru sasa inafifia mbele ya ndoto za mwanae,chai yote ilimshinda kuinywa akashusha kikombe chini na kumtazama.Alitaka kujua zaidi habari za huyo Mwalimu Aisha.Bwana Ahmed alisikia maneno hayo kutoka kwa mtoto wake hivyo akasogea karibu kutaka kujua kulikoni mpaka Baraka hataki kwenda shuleni.Bi mwasi nae Alimsogelea karibu mwanae kisha akamwuliza
“Ehee! Niambie mwanangu huyo mwalimu Aisha anakufanyaga nini?”
“Mwalimu Aisha anatunyanyasa hasa watoto walemavu, pia amesema hapendi kutuona”Baraka alimjibu mama yake
“Aisee! Pole sana mwanangu”Bi.Mwasi alisema
“Pia kuna wanafunzi wasiokuwa na ulemavu utunyanyasa na kutupiga mama”Baraka aliendelea kumwambia mama yakeCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mmmh! Hapana mwanangu hiyo pia isiwe sababu ya kukufanya ukatae kwenda shule”Mama yake alimwambia
“Sitaki mama mimi namuogopa mwalimu Aisha”Baraka alisema
“Baba Tausi unamsikia mwanao?”Bi.Mwasi alimuuliza mumewe
“Eeeh! Unataka nini sasa”
“Sitaki kwenda shule”Baraka alisema
“Hutaki kwenda shule? Baba yake aliuliza
“Ndio baba”
“Haya mke wangu umemsikia mtoto, tufanye nini sasa maana ameshagoma kwenda shule”Ahmed alimwuliza mkewe
"Yaani baada ya kunijibu nawe unaniuliza jamani"
"Ndio tujadiliane mke wangu kuhusu mtoto huyu"
“Labda tumwulize kisha tumsikilize rafiki yake Juma, kama aliyotuambia Baraka ni kweli au sio kweli.Bi.Mwasi alitoa wazo.
Bwana Ahmed na mkewe walihisi kama kuna jambo baya amefanyiwa mtoto wao.Wakanywea tuli hawakutaka tena kumhoji kwani waliona kabisa anapoelekea mtoto wao hapakakuwa sahihi.Lakini sasa hawakujua watafanya nini ili kumshawishi kwenda shuleni kwani yupo katika kipindi cha mwisho kuingia katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.
Wazazi wake hawakupenda Baraka kuacha shule, walijifikiria njia gani ambayo ingeweza kumrejesha Baraka Shuleni.Haikupita muda mrefu wakiwa pale sebuleni walisikia sauti ya Juma akibisha hodi Bwana Ahmed alimkaribisha,Juma alipoingia tu ndani aliwakuta Baraka na wazazi wake wote wawili wakiwa wamekaa sebuleni.Akawasalimia kisha akamwuliza Baraka kwanini hakuonekana shule siku hiyo,Baraka hakujibu badala yake Bi.Mwasi akawai kumuelezea yote aliyosema Baraka kama kuna Mwalimu anayewachukia wanafunzi wenye ulemavu.Juma alijibu ni kweli tena wapo mpaka wanafunzi wenye roho mbaya pia kuna wanafunzi ambao wana upendo kwa wenzao kama yeye anavyompenda Baraka kama ndugu yake. Juma aliwaeleza kwamba Benson na Sadiki umpiga Baraka kutokana na utundu wao, hivyo wapo wanafunzi wenye uwelewa na nidhamu kwa kuwaonyesha upendo kwa wanafunzi wenye ulemavu...
Wakiwa kwenye maongezi hayo Juma alimsogelea karibu Baraka na kumtaka aende shule,alimshawishi na kumtaka kupuuza mambo yote anayofanyiwa,lakini Baraka hakutaka kumsikiliza.Badala yake alishikilia msimamo ule ule kwamba hatokwenda shule,hakutaka kabisa kusikiliza habari za shule hakufikiria kabisa yupo mbioni kufanya mitihani.Aliwaza sana adhabu alizokuwa anazipata shuleni aliona hakuna haja ya kuendelea kuteseka wakati njia ya kunusurika ipo wazi.Bora kubaki tu nyumbani.Juma alipoona Baraka kashikiria msimamo wake kukataa kwenda shuleni,akaamua kuaga na kuondoka.
Baada ya mwendo wa kuzunguka hapa na pale hatimaye Juma alifika nyumbani kwao na kumkuta mama yake anapika cha mchana,alimsalimia kisha akaingia ndani na kubadili nguo.Juma alipotoka akutaka kupoteza muda alimsogerea mamaye na kumsimulia habari za Baraka kukataa kwenda Shule.Mama yake alimsikiliza kwa umakini mkubwa kisha akamtaka Juma kuondoa wasiwasi kwani yeye atalifuatilia na kuhakikisha Baraka anarejea shuleni.Juma alimshukuru mamaye kisha alifuatilie na tabia hiyo ikomeshwe mara moja. Mama Juma alipomaliza kupika alivaa kanga yake kisha akatoka na kuongoza njia kuelekea nyumbani kwa Bi.Mwasi.
“Hodo hodi nyumba hii! Wenyewe mmelala”Mama Juma alibisha hodi
“Hatujalala jirani karibu”Bi.Mwasi alijibu
“Ahsante jarani”Mama Juma aliingia ndani
“Vipi Jirani kwema huko? Bi.Mwasi aliuliza
“Salama tu, ila nimekuja jirani kujua kamajambo kuhusu Baraka”Mama Juma alisema huku akikaa kwenye jamvu
“Eehee! “Bi.Mwasi alishangaa
“Juma amekuja na kuniambia kwamba Baraka amekataa kwenda shuleni, naomba kujua jirani kwa sababu gani?”Mama Juma aliuliza
“Ni kweli jirani mtoto hataki kwenda shuleni, amesema kwamba kuna mwalimu na wanafunzi wanaompiga bila kosa, kwa hiyo amechoka kuvumilia ameamua kupumzika nyumbani”Bi.Mwasi alijibu
“Si unajua Baraka yupo mbioni kumaliza shule”Mama Juma alisema
“Ndio hivyo tena watoto wenye ulemavu wanateseka shuleni”Bi.Mwasi alisema
“Basi mlazimisheni Baraka kwenda shule siku mbili hizi, maana wiki zijazo mitihani inaanza”Mama Juma alishauriCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tumejaribu kumbembeleza Baraka ili akubali kwenda shuleni, lakini amegoma”Bi.Mwasi alijibu
“Sasa jamii lazima ipate elimu ili itambue haki za watoto wenye ulemavu,”Mama Juma alisema.
Baada ya Maongezi hayo, Mama juma alimtaka Baraka kurejea shuleni kwani mambo hayo yote watayazungumza na kuyamaliza na walimu wake.Baraka alikubali kwa shingo upande kwamba siku inayofuata atakwenda shuleni.
**********
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment