Simulizi : Machozi Ya Baraka
Sehemu Ya Pili (2)
Bwana Ahmed hakuwa na hisia yoyote kutokana na ulemavu aliokuwa nao mtoto wake,hakumjali kabisa Baraka,fikra na upeo wake ulikuwa mdogo mno.Hakuelewa umuhimu wa kumtunza na kumlea mtoto akufikiria kama kukaa ndani kwa Baraka kulitokana na Mama yake kumzuia kucheza na watoto wenzake.Baada ya muda Mwasi alimaliza kusafisha chumba cha Baraka na kujumuika sebuleni na mumewe.Wakati walipokuwa wamekaa pale sebuleni mara ukimya ukatawala kati yao kila mmoja akiwaza lake, hakuna aliyedhubutu kuongea chochote.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baadae Mwasi aliamua kumuwekea mumewe chai kisha akaelekea chumbani alipokuwa amefungiwa Baraka.Mle ndani alimkabili vilivyo mtoto wake na kumsema maneno makali akaiona haitoshi alitoka mpaka nje na akachukua fimbo na kurudi nayo ndani na kuanza kumchapa nayo Baraka.
“Mama Nionee huruma, unaniumiza” Baraka alilia
“Nikuonee huruma nini, nani kakutuma ujisaidie ndani? Mama yake alizidi kumchapa
“Umenifungia mama, mwenyewe naweza kujikokota mpaka Msalani” Baraka alilia huku akijifuta machozi yake kwa kutumia shati lake alilovaa,
“Ninyi watoto walemavu mna matatizo sana.Unajisaidia haja kubwa ndani?”Mama yake alilalamika.
“Mama muache dada Tausi aniudumie, ata hasipokuwepo basi naweza nikajiudumia mwenyewe” Baraka alilalamika,
Maneno ya Baraka yaliingia pima kwenye akili ya mama yeke akaamua kumchukua na kwenda kumsafisha huku akiendelea kumfokea na kumtolea maneno makali.Baada ya kumalizwa kusafishwa alirudi sebuleni na kumuomba mama yake chakula, kwani tangu alipopata kifungua kimywa asubuhi alikuwa hajatia chochote mdomoni wala hajala kitu kingine zaidi ya chai hiyo.“Mama naomba chakula” Baraka alimwambia mama yake tena kwa msisitizo“Heti mama naomba chakula! yaani baada ya kusambaza kinyesi ndani lakini bado unataka tena chakula”mama yake alimjibu kwa ukali.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwasi hakujali ombi la mtoto wake kwa wakati huo,aliingia huku na kutokea kule,mara ashike hiki mara kile,afanye hili mara lile,wala hakujali kwamba aliyeomba chakula alikuwa mtoto wake wa kumza.Bi.Mwasi aliendelea na shughuli zake nyingine mpaka pale alipojilidhisha kumaliza kwa kazi hizo akampatia Baraka chakula.Kilichomfanya Mwasi kutokutulia maanani ombi la chakula ni kitendo cha Baraka kujisaidia chumbani alipofungiwa.Baada ya kukabidhiwa chakula haraka haraka Baraka alipokea na kuanza kula kwa fujo tena kwa pupa kama kuku aliyetolewa bandani alfajiri.Baada ya kumaliza kula Baraka alinawa mikono yake kisha akamshukuru mamaye na kusukuma mlango ili kutoka nje......
“Weee! Wewe! mtoto unataka kwenda wapi”Bi.Mwasi alimuwai na kumwuliza
“Nakwenda nje kucheza mama” Baraka alijibu
“Unakwenda kucheza, mwangalie unataka mambo yanayokushinda mtoto mwenyewe Albino usiyekuwa na ili wala lile rudi ndani ukalale”Bi.Mwasi alimkalipia.
“Naweza mama, nitacheza vizuri na wenzangu” Baraka alimjibu mama yake
“Nimekwambia ingia ndani ulale upesi”
Mwasi alimtaka Baraka kurudi ndani, Baraka alitii amri ya mama yake na kurudi ndani huku akilia.Aliingia moja kwa moja katika chumba chake mpaka karibu kabisa na kilipo kitanda kisha akashikilia mbao za kitanda hicho na kupanda akalala, huku akiwa na duku duku moyoni mwake.
Miaka ilisogea na Baraka akakuwa sasa akafikia umri wa miaka tisa,katika umri huo akatamani kwenda shule,yeye mwenye aliona kabisa muda wa kuanza shule umempita sana.Mawazo na fikra za kwenda shule ziliibuliwa tena na dada yake Tausi,kwani muda mwingi dada yake umsimulia habari za shuleni.Kila anaporejea kutoka shuleni Dada yake uzungumzia habari za shule mara moja moja Mama yake alimruhusu Tausi kuingia chumbani alipokuwa amemfungia Baraka.Kuna wakati Tausi alimsimulia Baraka Hadithi nzuri alizofundishwa shuleni,alimsimulia jinsi anavyosoma vitabu vya watoto.Tausi alikuwa anamsomea hadithi bila kuzimaliza mpaka mwisho kwa umuogopa sana mama yake.pindi amkutapo anamsomea hadithi kakaye Baraka basi mama yake mfokea na kumtaka atoke katika chumba hicho.Maskini Baraka aliendelea kutamani kwenda shule ila hakuweza maana alikuwa amefungiwa kama ndege tunduni hakika hakuweza kutoka nje.
Siku moja majira ya asubuhi na mapema Ahmed na familia yake walikuwa mezani wakipata kifungua kinywa, hakuna mtu aliyemuongelesha mwenzake mpaka pale walipomaliza kunywa chai. Baraka aliona huo ndio muda mwafaka kwake kueleza kinaga ubaga kinachosumbua akili yake, akaamua kukaa vizuri na kuanzisha Mazungumazo
“Mama Natamani kwenda shule” Baraka alisema
“Unasemaje? Rudia tena maneno yako sijakusikia vizuri”mama yake akamwuliza
“Natamani kwenda shule, kama dada Tausi” Baraka alisema
“Mume wangu unamsikia mwanao anavyoleta kejeli eti anataka kwenda shule”Mama yake alisema
“Akafanye nini shule, mwache hapa hapa Kama alivyo”Ahmed alimjibu mkewe
Wakati Baba yake anaongea maneno hayo Baraka akaanza kulia,Machozi yalimtililika na kulowanisha shati lake,mama yake akaaanza kumkemea na kuanza kumpa vitisho vya shuleni, Baraka hakujali aliendelea kushikilia msimamo wake na kuwaomba wazazi wake wamkubalie ili aweze kusoma na kuandika kama dada yake Tausi.Lakini wazazi wake waliendelea kumkejeli kwa maneno hasa mama yake,
“Tafadhali usinichulie hatujafiwa sie”Bi.Mwasi alisema
“Mama nataka kwenda shule kama dada Tausi” Baraka alimwomba tena mama yake
“Sawa nimekuelewa, unataka nikupeleke shule utasomaje na hali yako hiyo?”Mamaye alimwuliza
“Dada Tausi ameniambia Shuleni wapo watoto wenye ulemavu kama mimi”
“Tausi anakudanganya huyo na ndiye anayekushawishi uende shule, nitampiga marufuku hasiingie tena chumbani kwako”Mama yake alisema
“Mama, Dada Tausi ananisimulia na kunisomea hadithi nzuri nami nataka nisome mwenyewe” Baraka alisema
“Usinipigie kelele hapa”Mama yake alimwambia kwa ukali.
Baraka hakuongeza neno alinyamaza huku akiendelea kulia,Maskini Baraka kilio kiliongezeka mara dufu hadi majirani wakasikia jinsi alivyokuwa analia akiwemo Mama Juma.alikimbilia katika nyumba ya Bi.Mwasi kilipotokea kilio hicho.Mama Juma alikuwa nje ya nyumba yake akiosha vyomba wakati akiendelea na kazi zake alisikia sauti ya kulia kwa sauti ya juu,Ghafla aliaacha vyombo na kujifunga kanga yake vizuri kisha akafunga mlango wa nyumba yake na kushika njia kuelekea nyumbani kwa Mama Tausi.Maana ameshajua kwamba sauti huyo ina tokea moja kwa moja kwa mama Tausi.....
“Jamani kuna nini kimetokea humu ndani, nasikia kilio kikubwa “Mama Juma aliuliza baada ya,
“Ni h uyu kikalagosi yaani ananikela sana ila yeye hajui tu”Bi.Mwasi alijibu
“Anataka nini kwani?”Mama Juma aliuliza
“Heti anataka kwenda shule!”Bi.Mwasi alijibu
“Hee! Jamani kwanini msimpeleke mtoto akasome? Shule ni muhimu sana, ataweza kusoma na kushirikiana na watoto wenzake pia ataweza kupata mazoezi ya viungo”Mama Shamila alisema
“Mama Juma tafadhali sana jirani, usitake kunichanganya tangu lini mtoto mlemavu tena Albino akasoma?”Bi.Mwasi aliuliza kwa jazba
“Haya mambo ya kizamani shoga na yameshapitwa na wakati, sasa hivi watoto walemavu wote wanapata haki zao za msingi kama watoto wengine”Mama Juma alimjibu
“Sasa ndio unataka kuniambia Baraka atasoma kama watoto wengine?”Bi.Mwasi aliuliza
“Siku hizi kuna Haki sawa kwa kila mtanzania,kuna vitengo maalum kwa ajiri ya kushughulikia matatizo ya watoto walemavu”
“Heee! Mlemavu anaweza kusoma na kuandika kweli”Bi.Mwasi aliuliza
“Shoga sio ya kushangaza hayo, vitengo hivyo vipo tangu zamani ila wewe hujui tu”Mama Shamila alimwambia kisha akaendelea
“Unajua shoga Baraka nae ukimpeleka shule anaweza kusoma na kuandika kama dada yake”
“Hivyo kweli hee! “Bi.Mwasi aliuliza kwa mshangao
“Usiwe na wasiwasi ataweza kusoma hatokuwa na tofauti na watoto wenzake, Tausi, Juma na wengineo”Mama Jama alimwambia kwa uwakikaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maelezo ya Mama Juma yalimwingia vilivyo Bi.Mwasi, akilini mwake akaanza kuweka msimamo na fikra mpya kuhusu mtoto wake Bi.Mwasi akaona taswira mbele ya macho yake jinsi mtoto wake anavyokwenda na kurudi kutoka shuleni,akawaza na kuwazoa kuhusu maelezo aliyoyapata.Vitengo maalumu alijiuliza mara mbili mbili kuhusu vitengo hivyo vitawezaje kumsaidia mtoto mlemavu hasa akiwa Albino asiyeona vema ubaoni,alijiuliza sana mwishowe akaamua kumgeukia na kumwambia Mama Huma “Sawa nimekuelewa jirani wewe ni mtu mwema kwangu nakushukuru kwa kunitoa gizani sasa naona nuru mbele yangu kuhusu hatma ya Baraka.Sasa namsubiri baba yake ili niongee nae,nimsikilize mwenzangu nae atasemaje”Mama Juma alifurahi sana kuona tayari jirani yake ameelewa na kuwa na fikra imara kupata mwelekeo kuhusu mtoto Baraka kupata elimu.Baada ya muda Mama Juma aliaga na kuondoka hukua akiwa na furaha ya ushindi.
Ilikuwa majira ya Mchana, mishale ya Saa Saba kamili .Jua lilikuwa kali mno Pilika pilika za watu na wakazi zilikuwa zinaendelea, watoto nao walikuwa wakirudi kutoka shuleni.Tausi alikuwa miongoni mwa watoto hao aliongoza moja kwa moja mpaka nyumbani kwao, alipofika alibisha hodi na kuingia ndani akamkuta Mama yake amekaa sebuleni akichambua mboga za majani ya mchicha.Siku hiyo Bi.Mwasi alikuwa sebuleni akichambua mboga.Muda huo alikuwa yupo peke yake sebuleni hapo,Baada ya kuingia na kumsalimia Mama yake aliingia chumbani mwake na kubadilisha nguo kisha alichukua kitabu chake na kuelekea chumba alichokuwa kaka yake Baraka huku ameshikilia kitabu cha watoto.Alipita kwa tahadhali ya hali ya juu,hakutaka kumkurupusha na kumshtua mama yake,maana anajua fika akimuona akiingia chumbani humo akiwa anamsomea hadithi Baraka atampiga na kumfukuza kwa viboko juu.Ndio maana akaamua kwenda kimya kimya bila mama yake kumwona.Tausi akafanikiwa kuingia chumbani humo na kumkuta Baraka amelala kitandani,akamwita na kumwambia
“Baraka! Baraka amka?Tausi aliita
“Naam dada! “Baraka aliitika
“Amka nimekuletea kitabu”
“Sawa leo tutasoma kama kawaida”
”sawa….”
Wakati huo tayari Tausi alikuwa ameshazama ndani kabisa,wakasalimiana na kakaye kisha akamwambia nduguye kwamba leo amempelekea kitabu cha hadithi, Baraka alifurahi na kumtaka amwoneshe hicho kitaba kilichokuwa kimeandikwa Tola mla kizani.Tausi bila kubisha alikitoa kitabu hicho na kumwonesha nduguye,Baraka alikiangalia kitabu hicho na kumwambia dada yake amsomee ,Tausi akaanza kumsomea kakaye hadithi ndani ya kitabu hicho.Tausi akiwa anaendelea kumsomea Baraka Hadithi mara wakasikia mlango unafunguliwa ,walitahamaki kumuona mama yao akiingia katika chumba hicho,Tausi aliduwaa kitabu kikiwa mikononi mwake hakuna na jinsi, ataanzia wapi kukificha maana alikuwa ameshachelewa kufanya maamuzi hayo ,kwani Mama yake alikuwa ameshakiona kitabu hicho.Bi. Mwasi alipoingia ndani alimkuta Tausi akimsomea hadithi Kakaye naye akaamua kukaa ili kusikiliza hadithi hiyo.Tausi akiwa ameduwaa pale chini alipokuwa amekaa, akasikia sauti kutoka kwa mama yake akimtaka aendelee kusoma hadithi hiyo.Tausi alifunua kitabu hicho na kuendelea huku mama yake akiwa amekaa juu ya kiti kilichopo ndani ya chumba hicho.
Tausi alisoma mpaka mwisho na wa hadithi hiyo akafunga kitabu na kumgeukia mamaye na kumwambia “Nimefikia mwisho wa hadithi hii ya Tola mla gizani.
‘Dada ningejua kusoma na mimi ningemsomea mama hadithi”Baraka alisikika
“Wapo wenzako kama wewe, wanajua kusoma na kuandika”Tausi alimwambia nduguye
“Mama Unamsikia Dada, nipeleke na mimi shule”Baraka alimwambia mama yake
“Subiri Baba yako arudi niongee nae”Mama yake alimjibu
Wakati Bi.Mwasi anaongea na watoto wake ,punde Mbwana Ahmed akarudi kutoka kazini,alipoingia tu ndani alimkuta Mke wake pamoja na Watoto wake wakiwa sebuleni.Alipotupa jicho lake vizuri alimuona Mke wake akiwa hana furaha,akajua labda mkewe anaumwa akaamua kumwuliza kisa na mkasa kilichomsibu mpaka hakawa katika ali hiyo,
“Vipi mke wangu unaumwa?”
“Siumwi chochote hisipokuwa masuala ya bahati yananitatiza”Bi.Mwasi alimjibu
“Masaibu gani tena mke wangu”Bwana Ahmed alimjibu
“Leo Baraka ameleta majanga”
“Ehee! Majanga gani tena mke wangu”Bwana Ahmed alishangaa
“Bado anang’ang’ania kwenda shule”
“Bado anaendelea kushikilia msimamo wake?”Bwana Ahmed aliuliza
“Ndio, leo dada yake Tausi amemsomea hadithi,basi imekuwa tatizo ”
“Sasa tufanye nini?”Ahmed aliulizaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa kweli hatuna budi kumpeleka Baraka shule, ikimsinda atarudi,maana pale alipokuwa anasomewa hadithi na dada yake basi yeye anataka asome mwenyewe,Pia nasikia shuleni kwao kuna watoto walemavu wa kila aina wanasoma nay eye tumpelekea ataweza kusoma pia”Bi.Mwasi alimwambia mumewe
“Jamani mtoto mwenye mlemavu tena Albino, viungo vyake havifanyi kazi miguu hana, macho haoni vizuri atasoma vipi huyu”Bwana Ahmed alimwambia mkewe
“Sawa nasikia watoto walemavu wote wapo wanasoma pamoja”Bi.Mwasi alisisitiza
“Basi tutampeleka tu na yeye akasome”Ahmed alijibu mkewe
Wakati Mama na Baba yao wakiafikiana kuhusu kumpeleka shuleni, Baraka na Tausi walifurahi sana kusikia neno “Tutampeleka” hakika liliwafurahisa sana ndugu hao.Walijikuta wakikumbatiana kwa furaha huku Baraka akilia kwa furaha ya kwenda shuleni akaona kuwa ndoto iliyokuwa inamsumbua siku nyingi sasa imekuwa kweli .Baada ya maongezi ya Bi.Mwasi na Mumewe Ahmed waliafikiana kwamba Mtoto wao Baraka kumpeleka shuleni.kila mmoja akatoka pale sebuleni na kuendelea na shughuli zake.
Ilikuwa mnamo tarehe tatu mwezi wa pili majira ya Asubuhi na mapema,Bi.Mwasi aliandaa kifungua kinywa kisha wakajumuika mezani na familia yake ili kupata kifungua kinywa,walipomaliza Bwana Ahmed na mkewe wakiwa na mtoto wao Baraka walifuatana na Tausi kuelekea shule ya msingi uhuru mchanganyiko.Walifika mapema sana kuliko watu wote shuleni hapo,walitafuta sehemu na kukaa kuwasubiri waalimu wa shule hiyo.Bi.Mwasi na mumewe walikaa pembezoni mwa madarasa ya shule hiyo huku wakiwa wenye mawazo tele kuhusu mtoto wao Baraka.Baadae kama nusu saa kupita tangu kufika kwao,wakawaona wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wanaingia mmoja baada ya mwingine ,wakati Bwana Ahmed na mkewe walipokuwa wamekaa waliwaona wanafunzi wakiwa wameshikana mikono na wenzao,wengine wakiwa na fimbo nyeupe mikononi mwao wakigonga mbele,kushoto na kulia huku wakiwa wanatembea kufuatilia fimbo hiyo,wengine wakiwa wanawasukuma wenzao wakiwa kwenye baiskeli za walemavu.
“Aaah! Maskini wee! wale wapo kwenye baiskeli wanasukumwa”Ahmed alisema
“Ndio, Mimi nimeambiwa wapo watoto wanaosoma wenye ulemavu Kama alivyo Baraka”Bi.Mwasi alisema
“Dada Tausi ameniambia wapo wengi Albino pia kama Mimi”Baraka alisema kwa furaha baada ya kuwaona wenzake wakipita kwa wingi.
“Itapendeza naye Baraka akasoma na kuwa pamoja na watoto wenzake atafarijika”Tausi alisema
“Ni kweli Dada nitafurahi sana nikianza kusoma”Baraka alidakia kwa furaha
Ilipofika saa mbili kamili kengele iliita Tausi akaaga na kuelekea dalasani, Bwana Ahmed na mkewe waliendelea kusubili waalimu wa shule hiyo kufika.Wakiwa bado wapo nje ya shule hiyo walimuona Mwalimu mmoja wa kike akipita mbele yao, Alikuwa mrefu mwembamba mwenye sura pana ya kuvutia.Mwalimu huyo mkononi alikuwa ameshika mkoba wake wa ngozi na mfuko mkubwa auliojaa vitabu.Mwalimu huyo alikuwa anaitwa Njaidi.Mwalimu Njaidi ni Mama wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Hidaya.Mwalimu Njaidi upendelea sana kuwasaidia wanafuzi wenye ulemavu, yeye ndio kiongozi wa umoja wa watoto wenye ulemavu wilaya ya Ilala, pia kazi yake kubwa ni kuwaamasisha na kushirikiana na wazazi kupinga unyanyasaji kwa watoto wenye ulemavu.Mwalimu Njaidi Mumewe ni mlemavu wa macho yaani kipofu, ndio maana ameamua kuthubutu kutenda na kuweka haki sawa kwa watu wenye ulemavu......
Wakati Mwalimu Njaidi anapita maeneo hayo aliwaona Bwana Ahmed na Mkewe pamoja na mtoto wao Baraka wakiwa wamekaa katika kigogo cha mnazi kilichopo kandokando ya njia hiyo, walionekana wakiwa wameshika tama jinsi walivyokuwa wamekaa moja kwa moja mwalimu Njaidi akajua lazima watakuwa na shida shuleni, aliamua kuwafuata kisha alipowasogelea kuwasalimia na akawauliza
“Habari zenu ndugu zangu?”
“Nzuri tu!”Bwana Ahmed alijibu kwa wasi wasi
“Niwasaidie nini ndugu zangu, naona mmekaa mbali na shule”Mwalimu Njaidi alisema
Tumekuja kuulizia watoto Kama hawa wenye ulemavu wanapokelewa shuleni hapa?”
“Mtoto wenu ni Albino tu au ana matatizo mengine?”
“Ni mlemavu wa ngozi na miguu yake imepinda yaani atembei vizuri huku akimwonesha miguu ya Baraka ilivyokuwa
“Mbona mmemchelewesha kuanza shule watoto wenzake wapo wengi wanasoma”Mwalimu Njaidi alisema
“Sisi tulikuwa hatufahamu watoto kama hawa wanapokelewa shuleni”Bi.Mwasi alijitetea
“Watoto wenye ulemavu wapo wa kila aina hapa shuleni”Mwalimu Njaidi aliwaambia
“Sawa basi tunaomba utuelekeze ili tumpeleke mtoto wetu”Bwana Ahmed alisema
“Nifuateni ofisini nikamwandikishe mtoto”Mwalimu Njaidi alisema CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwalimu Njaidi aliwaomba waongozane kuelekea Ofisi wakampatie majina ya mtoto wao na kuwapa utaratibu wa shuleni hapo, Bi mwasi na Mumewe waliinuka walipokuwa wamekaa na kumfuata Mwalimu Njaidi ofisini mwake. Baada ya mwendo wa taratibu uliochukua dakika tano walipofika, Mwalimu Njaidi akafungua mlango wa ofisi hiyo na kuingia ndani.Bwana Ahmed na mkewe nao walijitoma ndani.Baada ya kuketi katika viti vilivyokuwa ndani ya ofisi hiyo, Mwalimu Njaidi akaanza kuwauliza maswali juu ya mtoto wao.
“Mtoto anaitwa nani?”
“Jina lake ni BarakaAhmed,”Bi.Mwasi alijibu
“Ana miaka mingapi? Vipi kuhusu mtoto huyu je alizaliwa akiwa na ulemavu wa miguu au umemkuta ukubwani?”Mwalimu Njaidi aliuliza
“Ndio ana miaka kumi na moja, lakini tuligundua hasa baada ya kumpeleka hospitali na kupata uchunguzi”
“Mtoto wenu tumempokea, itawalazimu kumleta na kumrudisha nyumbani kwa kuwa mlemavu ni lazima aletwe na wazazi mpaka pale atakapo changamka na kuyafahamu mazingira ya Shule” Mwalimu Njaidi alisisitiza.
“Sawa tunashukuru sana Mwalimu “Bi. Mwasi alishukuru
“Haina shida mmefanya vizuri sana kumleta mtoto wenu shuleni”Mwalimu Njaidi alisema
“Ahsante Mwalimu”Bwana Ahmed alishukuru kwa pamoja walimpa mkono mwalimu Njaidi kisha wakaagana na kuondoka Kwa kuwa mwalimu waliyeonana naye ndio hasa aliyehusika na masuala hayo ya watoto wenye ulemavu ,walijisikia furaha sana kupokelewa kwa amani na upendo.Mwalimu Njaidi ni muongoni mwa walimu ambao waliopata elimu ya kuhusiana na ulemavu wa aina zote.Baadhi ya walemavu waliokuwepo katika shule hiyo ya Uhuru mchanganyiko ni walemavu wa aina nyingi,wapo walemavu wa usikivu,viziwi,kuna walemavu wa akili,hawa wanajulikana kama mataahila,kuna walemavu wa uoni hawa hujulikana kama vipofu,pia kuna walemavu wa ngozi huitwa Albino na wengine wengi.
Mwalimu Njaidi ni mtaalamu wa aina zote za walemavu,siku hiyo alifurahi sana kuwaona,wazazi wa Bahati wameamua kumpeleka mtoto wao shuleni hapo.Pamoja na kuwa muda wa uandikishaji ulikuwa umekwishapita ila waalimu walikubaliana Baraka kuanza kusoma,walimu wengine wa shule ya Uhuru waliwapongeza sana kwa uwamuzi wao waliochukua kumpeleka Bahati shuleni.Baada ya makubaliano yaliyofanyika kati yao,Bwana Ahmed na mkewe Mwasi walirejea nyumbani na Bahati kubaki shuleni,Muda si mrefu Mwalimu Njaidi alimtaka mtoto Baraka amfuate ili ampeleke darasani.Katika darasa alipopelekwa Baraka walikuwepo wanafunzi wenye ulemavu mchanganyiko, isipokuwa viziwi na vipofu ndio hawakuwepo.Darasa ilo walikuwepo walemavu wa viungokama miguu, mikono na Albino pamoja na wenye vichwa vikubwa.Mwalimu Njaidi aliingia darasani akiwa na Baraka, huku wanafunzi wote wakasalimia kwa heshima baada ya kumuona mwalimu wao ameingi.
“Heshima kwa Mwalimu “Kiongozi wa darasa alisema
“Shkamoo Mwalimu!”Wanafunzi wote wakasalimia
“Marahaba, wanafunzi.Hamjambo? Mwalimu Njaidi aliitikia
“Hatujambo Mwalimu”wanafunzi waliitikia kwa sauti kubwa
Baada ya salamu hiyo kutoka kwa wanafunzi hao,mwalimu Njaidi alianza kuwatambulisha wanafunzi kwa Baraka .Leo wanafunzi wa darasa la kwanza ‘A’mmepata mwanafunzi mwenzenu mpya anayeitwa Baraka Ahmed.Anaishi Buguruni sheri ni Albino mwenye ulemavu wa miguu,naomba mshirikiane nae kwa shida na raha”wanafunzi wote walifurahi na kumkaribisha kwa furaha Baraka.Juma ambaye alikuwa jirani wa Bi.Mwasi alikuwepo ndani ya darasa hilo la kwanza,alifurahi kumuona Baraka ameletwa shule na kuanza darasa la kwanza .Siku zote Juma alikuwa anampenda sana Baraka,Japo nyumbani hakuwa na uhuru wa kumsogelea na kucheza nae,Sasa leo hii Baraka ameletwa shuleni tena katika darasa yupo naye katika darasa moja furaha iliyoje kwake,akaona sasa anaweza kucheza na kuwa rafiki yake Baraka na si mwengine tena.
Baada ya utambulisho huo mwalimu Njaidi aliaga na kutoka darasani huku akimuacha Bahati akiwa ameketi pembeni juu ya kiti chake.Juma alipoona mwalimu ametoka darasani aliinuka na kumfuata Baraka, alipofika alimsabahi na kumkaribisha shuleni, Baraka alifurahi sana kumuona Juma katika darasa ilo alimkumbatia na kumshukuru.Wakati huo Baraka na Juma wanaongea mara ghafla mwalimu wa Hesabu aliingia darasani , Mwalimu huyo alishangaa kumuona Albino Mwenye ulemavu,akasikika akisema“Hee!leo tumepata mgeni?darasa hili litasomeka kweli maana kila mlemavu yumo humu,utafikiri madarasa mengine hakuna”.Mwalimu Aisha alilalamika “darasa linachukiza sasa wanafunzi wenyewe hawajui kusoma wamekaa tu humu mibichwa mikubwa lakini haina akili”.mwalimu Aisha alilalama vilivyo mpaka wanafunzi waliokuwepo ambao ni walemavu kaanza kujisikia vibaya na kuinamisha vichwa vyao chini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya malalamiko mengi kutokwa kwa mwalimu Aisha ,hatimaye alifundisha hivyo hivyo kisha akatoka darasani bila kujali kumsalimia mwanafunzi Yule mgeni.Juma alimfuata Baraka na kumtaka hasiwe na wasi wasi kwa mwalimu Aisha kwani ndio tabia yake kuwachukia wanafunzi wenye ulemavu kama yeye.Baraka alikubali kwa shingo upande huku akiwa mtu mwenye mawazo kutokana na kauli mbaya kutoka kwa mwalimu Aisha.Saa nne ilipofika kengere ikasikika ya wanafunzi kutoka mapumziko mafupi wote walitoka na kuelekea kujitafutia chochote cha kuingiza mdomoni kwa wakati huo.Juma alimfuata Baraka na kutoka nae nje mpaka wanapouza vitu,Juma alinunua mihogo na vitumbua kisha wakala na kurejea tena darasani.Muda wa saa sita ulipofika kengere ilisikika tena, safari hii ilikuwa muda wa kurejea nyumbani umewadia,kama kawaida Juma alimsaidia kusukuma baiskeli ya Baraka na kumtoa nje.Walipofika nje walimkuta Bi.Mwasi akimsuburi mwanae.Juma na Baraka walifurahi kumuona Bi.Mwasi.Juma aliagana na Baraka kisha akaondoka na Bi.mwasi alimchukua Baraka na kurejea nae nyumbani.Bi.Mwasi alifika nyumbani akiwa na furaha tele moyoni mwake, furaha ya Baraka kuanza shule bila matatizo, alimshukuru sana jirani yake Mama Juma kumtoa kwenye mawazo na fikra potofu na kumuonyesha mwanga.Kuanzia siku hiyo Bi.Mwasi na Mama Juma ujirani wao ulibadilika kuwa ndugu wa kushibana,kila jambo husaidiana kwenye shida na raha wapo pamoja,kwani akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki....
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment