Simulizi : Machozi Ya Baraka
Sehemu Ya Nne (4)
Ilikuwa kama vile mwalimu Aisha hakujua kilichokuwa kimetokea hakuyaamini macho yeke, akahisi labda madaktari na manesi wamabadilisha watoto.”Maana siku za mwanzo mtoto wa mama huyu akapewa mama mwengine, lakini siku hizi mambo yamekuwa tofauti.Manesi wapo makini au inawezekana kweli manesi watakuwa wamekosea hawa?”Mwalimu Aisha alikuwa anajiuliza kichwani mwake,Alimkumbuka Baraka ni kiasi gani alivyomnyanyasa kutokana na tatizo la ulemavu.Hakika ilikuwa pigo kubwa kwa Mwalimu Aisha,Pamoja na hayo yote ukweli ulibaki pale pale mtoto aliyekuwa amempakata ,alikuwa mtoto wake aliyemzaa kwa uchungu.Manesi hawakukosea kabisa hata yeye mwenyewe alihisi hivyo kuwa ni mtoto wake ingawa hakupenda kuamini ilibidi amini hivyo.Mtoto alifanana kabisa na Baba yake kuanzia pua,macho na sura kwa ujumla.Kilichomfanya Mwalimu Aisha kutokuyaamini macho yake ni kumwona kwamba mtoto wake alikuwa kipofu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Wakati mwalimu Aisha akimyanyasa na kumuonea Baraka hakuwa mjamzito ata hivyo Baada ya Muda alipata ujauzito,alifurahi sana kwa vile alikuwa hakupata hata mtoto mmoja katika kipindi cha miaka miwili ndani ya ndoa yake na mumewe maulidi.Wakati huo mwalimu Aisha aliilea mimba yake kwa huangalifu mkubwa.Mara kwa mara aliomba mapumziko ya kutokwenda shuleni kufundisha ili mtoto aliyepo tumboni hasipate madhara.Miaka ya nyuma aliomba sana ili kupata mtoto ila hakujua angepata mtoto wa aina gani,ndio maana leo hii anashangaa kupata mtoto kipofu.Alifikiria sana kutokana na aibu atakayoipata kutokana na mkosi huo,aliona kama yupo ndotoni lakini alipochunguza vizuri inaonyesha haikuwa ndoto bali ni ukweli m tupu.Mwalimu Aisha alichoka akajiona sasa ameumbuka tena hadharani mchana kweupe amejifungua mtoto kipofu hasiyeona,hadha iliyoje hiyo.........
Baada ya siku mbili waalimu wenzake walipata taarifa kwamba Mwalimu Aisha amejifungua mtoto wa kike katika hospitali ya temeke, kama kawaida waliambizana na michango kuchangishana kisha wakaamua kwenda kumpa hongera Mwalimu mwenzao. Alikuwa mwalimu Njaidi na mwalimu Rehema ndio waliofika nyumbani kwake siku hiyo, Wakati walimu huo wakiwa mlangoni mwa nyumba hiyo wanabisha hodi walimkuta mwalimu Aisha akiwa amempakata mtoto wake mapajani. Alipowaona walimu mwenzake wakiingia ndani alimfunika haraka mtoto wake kwa kitenge kizito, hakutaka walimu wenzake wamuone kisha akawakalibisha.
“Karibuni waalimu”alisema huku akifungua mlangoCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tushakaribia usijali”Mwalimu Njaidi alijibu kisha wakaingia ndani na kukaa
“Ahsante sana, hongera mwenzetu kwa kupata kimwana”Mwalimu Rehema alimpongeza
“Ahsante ndugu zangu, sijui mnakunywa soda gani niwaletee”Mwalimu Aisha aliwauliza
“Hebu mlete mtoto nimbebe hachana na hizo soda tumeshakunywa tulipotoka”mwalimu Njaidi aliomba kumbeba mtoto
“Unajua amelala na akilala huyu hataki kuguswa”Mwalimu Aisha alijibu kwa wasiwasi
“Mmmh! Kwanini tena maana sie wengine tunapenda kubeba watoto sasa yeye hataki kuguswa kwa nini?”Mwalimu Njaidi aliuliza
“Ndio hivyo tena hataki kusumbuliwa huyo, kidogo tu ukimgusa kilio”Mwalimu Aisha alidanganya
“Basi aina shida muache alale”walimu hao walihafiki
Punde walimu hao wakiwa kwenye maongezi ya hapa na pale, ghafla bila kutarajia ilisikika sauti ya mtoto akilia, hivyo ikawa ishara mtoto ameshtuka kutoka usingizini.”Mlete amekwisha amka huyo”Mwalimu Njaidi alidakia, alikuwa akionyesha kuwa na shauku ya kumuona mtoto huyo.Wakati Mwalimu Njaidi akisema maneno hayo alikuwa ameshapiga hatua kuelekea kitandani alipolala, Kipindi hicho mwalimu Aisha hakuwa na la kufanya ilimbidi kumpa.Mwalimu Njaidi alimbeba kwa furaha huku akimpongeza mwalimu Aisha kumpata mtoto huyo. “Siku nyingi ulikuwa na hamu ya kupata mtoto, leo hii mungu amekujalia kupata mtoto wa kike hongeza zako sasa ulezi ndio huu kazi kwako”Mwalimu Njaidi alimwambia kwa furaha kisha akimsihi kumlea mtoto wake kwa malezi mema.Muda huo mtoto akiwa mikononi mwa Mwalimu Njaidi ameshaanza kulia, alimbembeleza bila mafanikio akaamua kumrejesha kwa mama yake.Mwalimu Aisha aliwashukuru waalimu wenzake, baada ya muda walimu hao waliaga na kuondoka.Wakati wapo njiani kurejea shuleni walimu hawa wakawa mazungumzo yao yote yanalenga kumsema Mwalimu Aisha kwa ubaya wake aliokuwa anawaonyesha watoto walemavu.Mwalimu Aisha hakuwapenda watoto hao kutokana na unyanyapaa kwa walemavu,wakati awapo darasani alikuwa na tabia ya kuwanyanyasa sana wanafunzi hasa walemavu,alionekana dhahili kuwa si mtu wa mchezo mchezo hasiyekuwa na utu hata kidogo,kutokana na tabia yake ya kuwakalipia wanafunzi.Siku hiyo sasa amepata mtoto mlemavu tena aliyezaliwa akiwa kipofu “hama kweli mungu ana ubaguzi umpa kila mtu kwa wakati wake sasa nae amepata kwa wakati wake alisema mwalimu Njaidi.
******
Siku nyingi zilipita, wiki akakatika bila Baraka kwenda shule Juma nae alizidi kumbembeleza ili arejee shuleni, lakini Baraka aligoma hakutaka kabisa kusikia habari za shule aliona hakuna umuhimu shuleni zaidi ya mateso aliyokuwa anayapata.Kila siku anapotoka shuleni Juma upendelea kupita nyumbani kwa Bi.Mwasi kumsalimia Baraka kisha umsimulia jinsi walivyofundishwa shuleni, Baraka nae ufuatilia masomo yaliyompita kwa kusoma madaftari ya Juma.
Hapo mwanzo mwalimu Njaidi alifikiri Baraka anaumwa ndio maana hafiki shuleni,siku zinavyozidi kwenda ndivyo ukimya wa Baraka unavyozidi kuongezeka.Alipata wasi wasi mno kutokumuona Baraka shuleni,alitamani apelekwe nyumbani kwao anapoishi lakini alikosa muda na kumpata mtu wa kumpeleka.Siku moja Mwalimu Njaidi alipanga kwenda nyumbani kwa wazazi wake Baraka alimtafuta mwanafunzi Juma na kumtaka kesho yake ampeleke,Juma alimkubalia mwalimu wake kwa furaha kwani alijua sasa Baraka atarejea tena shuleni na kufanya mitihani yake.Mwalimu Njaidi alikaa na kupata wazo hakutaka kwenda peke yake, aliona haja ya walimu na wanafunzi kuelimishwa juu ya umuhimu wa kuwatunza walemavu,ili kuwasaidia walimu na wazazi wote kuwajali na kuwathamini walemavu wa aina zote.Siku hiyo Mwalimu Njaidi aliandika Barua kwenda kwa Taasisi na kitengo kinachojiusisha na masuala ya walemavu Shuleni hapo.Baada ya kukamilisha Barua hiyo aliituma kwa sanduku la posta kisha baada ya siku mbili Barua ya majibu ilirudi na kusomeka ombi lake limekubaliwa.Mwalimu Njaidi alifurahi sana kuona majibu hayo sasa fikra na mawazo yake yote yakawa kumrejesha Baraka shuleni tena kuacha elimu itakayowanufaisha na kuwasaidia walemavu.....
Siku iliyofuata asubuhi na mapema baada ya kipindi chake kumalizika Mwalimu Njaidi alimfuata mwalimu Aisha na kumtaka waongozane kwenda nyumbani kwa Bi.Mwasi,alikubali bila hiyana aliona ndio waka maalimu kumwomba msamaha Baraka ili arejee shuleni.Mwalimu Njaidi alimfuata Juma na kumwambia awapeleke anapoishi Baraka,Juma alitoka na kuwaongoza waalimu wake nyumbani kwa Bi.Mwasi.Baada ya mwendo wa robo saa walifika katika nyumba hiyo,kwa bahati nzuri walimkuta Baraka amekaa nje na wazazi wake.Baraka alipowaona alishangaa sana,Mwalimu aliyesababisha kusitisha masomo yake amekuja nyumbani kwao kufanya nini kama kumtesa ameshamtesa vya kutosha shuleni,sasa ameamua kumfuata nyumbani ili iweje?,Baraka alijiuliza bila kupata jibu,akaona isiwe tabu kuumiza kichwa chake akawasubiri waseme shida iliyowaleta.Bi.Mwasi alipowaona aliwakaribisha kwa furaha kisha wakakaa kwenye vii vilivyopo pale nje,Juma akakaa chini kwenye mkeka.
“Karibuni walimu”Bi.Mwasi aliwakalibisha
“Habari za hapa”Mwalimu Njaidi alisalimiaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nzuri tu ndugu zanguka ribuni sana”Bi.Mwasi alikaribisha
“Ahsante tumeshakaribia”Mwalimu Njaidi alijibu
“Hujambo Baraka?
“Sijambo shkamoo mwalimu”Baraka alimsalimia mwalimu Njaidi
“Marabaha”Mwalimu Njaidi alisikika.Muda huo huo sauti ya Bwana Ahmed ilisikika
“Niwasaidie nini walimu”Ahmed alisema
“Tumekuja kumwona Baraka siku nyingi hajafika shuleni, Sisi ni waalimu wake tumekuja kumfuata arejee shuleni”Mwalimu Njaidi alisema
“Haya Baraka unawasikia walimu wako? Bi.Mwasi alimwuliza
“Mimi mwalimu siwezi kurudi shule”Baraka alijibu
“Kwa sababu gani”mwalimu Njaidi alimwuliza
“Shuleni kuna walimu na wanafunzi ambao wananionea sana, Benson na Sadiki hao ni maadui zangu sijui kipi nilichowakosea”Baraka alisema
“Sisi tumefika hapa lengo letu kuona unarudi shuleni, kumaliza elimu yako ya msingi ili uweze kuendelea na Sekondari achana na majungu dhidi yao unatakiwa kusahau na kusamehe kwa yote yaliyotokea”Mwalimu Njaidi aliendelea kumbembeleza Baraka.
Mwalimu Aisha aliposikia hivyo alijiinamia kwa aibu kutokana na hisia zilivyomchoma moyoni mwake, aliona kabisa siku ya kufichuliwa maovu yake imefika, alijikaza na kujiinamia chini.Mwalimu Njaidi alimueleza Baraka kuhusu elimu inayotarajiwa kutolewa kutoka kwa wataalamu Mbalimbali watakaofika shuleni siku ya Jumamosi.Bi.Mwasi na Bwana Ahmed walimsikiliza kisha wakamwuliza kama na wao wanaweza kufika,Mwalimu Njaidi akawaeleza kwamba wao ndio muhimu zaidi kwani kutakuwa na shughuli ya kuwaaga wanafunzi wanaomaliza darasa la saba.Baraka alitulia kimya akitafakari,alianza kuona sasa tayari kumekuwa na mwelekeo ili kuweza kufanya mitihani yake,hatimaye Baraka alikubali kurejea tena shuleni ili kumaliza elimu yake ya msingi.
Walimu na wazazi wake walifurahi sana kuona Baraka amekubali kurejea tena shuleni, waliinuka kwa pamoja kisha wakakumbatiana kwa furaha na upendo.Mwalimu Aisha alijisikia furaha moyoni mwake alimsogerea Baraka huku machozi yakiwatoka na kumwambia “Nisamehe sana mwanangu, sahau yote yalipita na sasa tugange yajayo”kisha alitoa zawadi na kumkabidhi Baraka alipokea kwa mikono miwili na kumshukuru mwalimu Aisha machozi yakimtoka akiwa na amani moyoni mwake.Bi.Mwasi na mumewe walionyesha furaha ya wazi kwa mtoto wao kukubali kumaliza masomo yake,waliwashukuru walimu hao kwa juhudi walizozionyesha juu ya Baraka.Baada ya walimu hao kufanikiwa kumshawishi Baraka na kukubali kesho yake atafika shuleni,waliaga na kuondoka huku Ahmed na Mkewe waliwasindikiza kwa maongezi ya hapa na pale........
Siku ya jumanne ilikuwa yenye furaha ,vigelegele,ndelemo na vifijo vilisikika kutoka shule ya msingi uhuru mchanganyiko.Walimu na wanafunzi walikuwa wenye furaha mno.Juma,Benson,Sadiki,Shamila na wengineo walionekana wakikimbia huku na kule ya kila pembe wakishangilia.Hata wale walemavu wengine Kipofu,Kinziwi,Bubu na Albino walionekana siku hiyo kuwa na furaha.Furaha hiyo ilionekana pale Baraka mtoto mwenye uremavu wa ngozi Albino kuonekana akiletwa shuleni na mama yake,kila mwanafunzi alitamani amfuate,lakini walimwogopa Bi.Mwasi.Juma alijitokeza na kumpokea Baraka kisha akamsindikiza kuelekea Darasa.hatimaye Baraka akaendelea na masomo yake kama kawaida,akisubilia wiki moja ipite afanye mtihani wa mwisho.
Walimu walimpenda sana Baraka walimshirikisha kwa kila jambo linalofanyika kama wanafunzi wengine.Alifurahi sana kuona hali hiyo ikiendelea ,wanafunzi wengi walimfuata Baraka pale wanapokwama katika masomo,uwasaidia na kuwafundisha wenzake jinsi yeye alivyoelewa yote hayo yametokea kipindi Baraka akiwa mwishoni kumaliza elimu ya msingi.Baraka alisoma kwa utulivu,bila kusumbuliwa na kitu chochote,Benson na Sadiki walijenga urafiki nae,maana yeye hakuwa na kinyongo na mtu alishasamehe hivyo ilikuwa bahati ilioje kupendwa na watu wote katika shule hiyo.
*****
Ilikuwa siku moja majira ya jioni Tausi alipokuja kuchukuliwa na shangazi yake Bi.Moza anayeishi Songea.Siku hiyo Bi.Mwasi alikuwa na majonzi tele kutenganishwa na mtoto wake ,hasa akimuona kuwa ni msaada mkubwa kwake ,hata pale anapokuwa hayupo basi Tausi ufanya kazi zote .Hata Baraka aliona sasa nguzo yake aliyokuwa akiitegemea sasa imedondoka kwani alikuwa akimtegemea kwa kila jambo hasa msaada wake wa kumuwezesha kwenda shuleni asubuhi uongozana sasa leo dada yake anaondoka atakwenda na nani.Bahati alilia pale muda wa Bi.Moza kuondoka akiwa na Tausi,aliona kama hawataonana tena lakini Bwana Ahmed hakuwa na tatizo na Tausi aliafiki ili amfuate shangazi yake kwenda kuendelea na masomo ya sekondari songea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bi.Moza na Tausi waliondoka kuelekea stend ya mkoa ubungo ili kuwai usafiri utaochukua masaa kadhaa kufika mjini songea.Tausi alifurahi sana kuona kwamba ndoto zake za kuendelea kusoma sasa zimetimia na kufikia tamati kwa shangazi yake kwani alimpenda sana shangazi yake huyo.Baada ya muda Bwana Ahmed na Bi.Mwasi waliwasindikiza mpaka stand ubungo kisha wakapanda gari Tausi na Shangazi yake mpaka mjini songea.Walifika siku ya pili yake na kupokelewa na wenyeji ambao ni watoto wa bi moza.Tausi aliendelea na masomo katika shule ya sekondari Songea Girls iliyopo nje kidogo ya mji wa songea.
Ilikuwa siku ya jumamosi majira ya saa tatu asubuhi, upepo ulikuwa unavuma kwa kasi ya ajabu kutoka mashariku kwenda magharibi.Shule ya msingi Uhuru mchanganyiko ilikuwa imefurika wazazi na wanafunzi pamoja na wakazi wa maeneo hayo,wakiwa mamekaa juu ya viti vyao.Waalimu na wanafunzi walikuwa makini kuwasubiri wageni waalikwa,kutoka katika kitengo cha umoja wa walemavu kinachojiusisha na masuala ya kukemea unyanyasaji kwa watoto wenye ulemavu.Katika hafla hiyo mwalimu mkuu aliamua kuunganisha pamoja na sherehe ya kuwaanga wanafunzi wanaomaliza Darasa la saba.Ilikuwa sherehe ya Furaha sana hasa kwa wanafunzi hao wanaomaliza elimu yao ya msingi, katika sherehe hiyo kulikuwa na mgeni rasmi ambaye alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Ilala, baadhi ya wanafunzi na wazazi walikuwa wakiburudika mziki mwanana uliokuwa ukipiga katika hafra hiyo.Punde wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali walifika na kujumuika pamoja, walicheza na kufurahi.Muda wa hotuba ulipofika wageni waalikwa walikuwa tayari kuzungumza na wanafunzi wote na wazazi pamoja na waalimu.
Baada ya wanafunzi na wazazi kukaa na kutulia kwenye viti vyao,Mwalimu mkuu alisimama na kuwakalibisha wageni hao kwa furaha kisha Baraka akapanda jukwaani na kusoma risala kwa ajiri ya wageni hao.Risala hiyo ilipoisha alipanda jukwaani mkuu wa kitengo cha kupambana na unyanyasaji wa walemavu Bwana Nyilenda,mtaalamu huyo alieleza kuhusiana na elimu ya walemavu ni elimu ambayo hushirikisha aina mbali mbali za masuala ya ulemavu,elimu hii inamfanya mtu aweze kuwapenda na kuwasaidia walemavu kwa hali na mali.Mfano Mbunge wa Lindi Mjini Salum Baru’ani ni jibu lingine kwa wale wenye mtizamo hasi juu ya watu wenye ulemavu hususan wa ngozi “Albino”. Baada ya mauaji ya kupindukia kwa watu wenye ulemavu wa ngozi wananchi wa Jimbo la Lindi Mjini waliudhihirishia umma wa watanzania kuwa wana imani na watu wenye ulemavu wa ngozi na kumpa ridhaa kuwa mwakilishi wao katika chombo muhimu cha kutunga sheria.Kwa kuzingatia mfano huo ni muhimu jamii ikubali kuwa ulemavu sio Mjungu wala mateso ,wapo watu wenye viungo vyote, rangi sawa, akili sawa, elimu kubwa lakini hawajaonyesha mchango wowote katika jamii na hawana ulemavu wowote.Hali hii inadhihirisha kuwa ulemavu ni mtazamo hasi ndani ya jamii na sio upungufu wa viungo unaomfanya awe au asiwe na mchango katika jamii .Kama ulemavu ni ukosefu wa viungo ni vizuri kila mtu katika jamii aelewe kuwa ni mlemavu mtarajiwa aidha kwa ugonjwa au kwa usafiri ambapo ajali imekuwa ikizalisha walemavu wa viungo ambao pengine ni kati ya wale waliokuwa na kiburi isiyo na kifani ya kuwanyanyapaa watu wenye ulemavu.
Ni ukweli usiofichika kuwa kundi ilo la walemavu limesahaulika na jamii na hata serikali, na kusababisha kukosa huduma muhimu za kijamiia, kisiasa na kiuchumi kwa kiwango kikubwa. Taarifa za utafiti wa walemavu Tanzania uliofanywa na Taasisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) unaonyesha kuwa walemavu ni asilimia 7.8 kiasi sawa kwa wanaume na wanawake. Kundi hili si kubwa kiasi cha serikali kushindwa kulihudumia na kulipa mahitaji yanayostahili......
Lakini kutokana na ufisadi na ubinafsi uliojaa katika taasisi husika watu hawa hujikuta wakikumbukwa pale tu, linapotokea tukio au janga kama vile mauaji ya maalbino. Ukosefu wa huduma mbalimbali za jamii kwa watu wenye ulemavu, kunawafanya waathirike kisaikolojia na wengi wao kukata tamaa.Shirika la Afya Duniani (WHO), linakadiria katika nchi nyingi duniani kiwango cha ulemavu ni kati ya asilimia 10 hadi 12.16,Agalabu utafiti wa NBS mwaka 2008 ulionyesha kuwa aina na idadi ya walemavu kwa asilimia ni macho milioni 1.2 sawa na asilimia 4, matatizo ya kutembea 956,669 (3) uziwi 600,000 (2) albino 8,193 kiasi ambacho kinawezekana ikawa ni zaidi ya hiyo kwa sasa.Mtaalamu huyo aliongeza kwa kirefu kisha akaendelea kufafanua.Pia, utafiti ulionesha kuwa, watoto walio na umri wa chini ya miaka 15, ni asilimia 50 kati ya hao walizaliwa na ulemavu au waliupata kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja.Kwa watu wazima asilimia 12 walisema walizaliwa na ulemavu huo na asilimia 14 walitaja baridi yabisi kama chanzo cha ulemavu walionao huku asilimia sita wanaamini kuwa uchawi ndiyo chanzo cha ulemavu walionao, wakati ulemavu mwingine ambao utafiti huo haukutaja unasababishwa na ukatili majumbani ‘Domestic violence’ ambayo hufanywa aidha na wanaume au wanamke.Pia, visiwani Bi. Asha Alfani ambaye ni mlemavu wa macho aliupata kutokana na kipigo kwa Shangazi yake.
Matokeo mengine ya utafiti yanaonyesha kuwa viwango vya ulemavu ni vikubwa kwa maeneo ya vijijini kwa asilimia 9.4 sawa na watu milioni 2.9 ukilinganishia na maeneo ya mijini ambao ni asilimia 7.3 sawa na watu 560,000 huku kiwango cha ulemavu ni kikubwa kwa Tanzania bara kwa asilimia tisa sawa na watu milioni 4.4 kuliko Tanzania Zanzibar asilimia 7 sawa na watu 55,355.17.
Aidha tafiti kadhaa zilizofanywa katika baadhi ya Tanzania bara na Tanzania Zanzibar, zilibaini kuwa watu wenye ulemavu hawapati fursa sawa katika kupata haki ya elimu kutokana na mila na fikra potofu kuwa kuwasomesha watoto wenye ulemavu ni uharibifu wa rasilimali. Tafiti hizo zinaonyesha kuwepo uhaba mkubwa wa vifaa vya kufundishia katika shule yenu, walibaini uhaba mkubwa wa vitabu na vifaa vingine vya kufundishia watu wasiona, na vifaa rafiki kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. Matokeo ya utafiti kuhusu watu wenye ulemavu Tanzania ya mwaka 2008, yanaonyesha kuwa ni watoto 4 tu kati ya 10 wenye umri kati ya miaka 7 na 13 ndio wanaopata elimu ya msingi na wanaopata elimu ya sekondari ni asilimia 5.Kwa mujibu wa matokeo hayo waliopata elimu ya juu ni chini ya asilimia moja na asilimia 48 ya watu wenye ulemavu hawajui kusoma wala kuandika ukilinganisha na asilimia 25 ya wale wasiokuwa na ulemavu.Alipofika hapo Mtaalamu Nyilenda alichukua maji ya uwai akapiga funda moja kisha akaendelea tena.
Katika masuala ya ajira watu wenye ulemavu wanaendelea kunyanyapaliwa na kufanya wabaki nyuma licha ya katiba kutoa fursa ya wao kupata haki ya kufanya kazi sawa na watu wengine.Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria ya watu wenye ulemavu (2010) Sera ya Taifa ya Watu wenye Ulemavu (2004), na mkataba wa Kimataifa wa Haki za watu wenye ulemavu (ambao Tanzania umeuridhia) vinasisitiza haki sawa ya ajira kwa watu wenye ulemavu.Pamoja na kuwepo kwa sheria, mikataba hiyo,bado hali ya ajira kwa watu wenye ulemavu ni duni.Elimu hii uweza kumsaidia mtu aliyepo nyumbani,hospitali ata mashuleni na sehemu zote zilizoizunguka jamii yetu.Mtaalamu huyo aliendelea kuwasihi wazazi kutowabagua watoto wenye ulemavu na,wapendwe na kuishi nao kwa upole na kuwatendea mema,watoto walemavu wathaminiwe.Mtaalamu huyo alifika mbali zaidi na kueleza athari za kutowatendea wema walemavu,alisema wanafunzi wengi wanatoloka shuleni kwa sababu ya kutodhaminiwa,maana ukata tamaa mapema na kuacha shule kwa sababu ya mateso wanayoyapata. Uchunguzi umebaini kuwa, baadhi ya sababu zinazofanya watoto wenye ulemavu wakose elimu ni pamoja na wazazi kuwaficha watoto hao nyumbani, miundombinu hisiyo rafiki katika shule mbalimbali na ukosefu wa vifaa vya kufundishi na kutokuwepo kwa walimu wa kutosha wa kuwafundisha watoto wenye ulemavuMwisho nawaomba wazazi na waalimu kuishi vema na watoto hawa wenye ulemavu.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati mtaalamu huyo alipokuwa anahutubia,waalimu na wanafunzi walitulia tuli kumsikiliza kwa umakini.Mwalimu Aisha nae alikuwepo siku hiyo,alijilaumu sana na kujutia katika moyo wake,aliona mkosaji mbele ya walemavu,alitaka kwenda mbele ili kuomba msamaha kwa wanafunzi hao,lakini aliogopa kwenda kutokana na umati wa watu waliofurika katika hafla hiyo,aliona kabisa ataumbuka na kupata fedhea.Wanafunzi Benson na Sadiki walikuwa wamekaa karibu kabisa na kiti alichokuwa amekaa Baraka na Juma,Sadiki alimshika mkono Baraka na kumtaka wamalize tofauti zao hapo hapo,Baraka hakuona Sababu ya kuendelea kuwachukia wanafunzi wenzake alikubali mkono huo kwa moyo wake wote kisha Benson nae alimsogeLea Baraka kisha wakakumbatiana kwa furaha.Juma alifurahi sana kuona Sadiki na Benson kukubali makosa yao kisha akawaambia “Rafiki wa kweli ni Yule akupendaye kwa dhiki, Juma kuanzia sasa Baraka atakuwa rafiki yetu kwa shida na raha”Baraka alifurahi sana kusikia maneno hayo kutoka kwa maadui zake wa muda mrefu sasa wamegeuka kuwa marafiki.Siku hiyo walicheza na kufurahi pamoja,Licha ya kumaliza pamoja darasa la saba Benson na Sadiki walimpatia Baraka zawadi mbalimbali kuonyesha upendo kwake.....
Baada ya kuhutubia Mwalimu mkuu aliwashukuru wataalamu hao kwa kazi kubwa ya kutoa elimu kwa wazazi na wanafunzi kwa ujumla.Wataalamu hao pamoja na taasisi nzima walishukuru wazazi na wanafunzi kusikiliza hotuba hiyo kisha wakagawa Baiskeli za walemavu shuleni hapo.Mwalimu Mkuu aliwataka kuwa na tabia ya kupita vijijini na kuelimisha jamii kuhusu haki za walemavu walikubaliana nae watalifanyia kazi wazo lake kisha wakaondoka.
Wakati wageni walipoondoka,wanafunzi na wazazi waliendelea na Mahafali kwa ajili ya darasa la saba,siku hiyo shule ya uhuru ilionekana kung’ara tena wenye nuru mbele yake,watoto walicheza kwa furaha wenye ulemavu na wasio walemavu wote walikumbatiana kwa furaha.Siku hiyo shule nzima sura zao zilionyesha furaha tele moyoni mwao.Wakati sherehe ikiendelea,muda wa kugawa zawadi ukawadia,wazazi na walimu waliwapatia zawadi wahitimu wa darasa la saba,Bwana Ahmed na mkewe walimpatia zawadi mbalimbali mtoto wao,Mwalimu Aisha nae alimpatia zawadi ya Begi kubwa la nguo na vitu vingine vingi,pia Baraka alifurahi sana siku hiyo,haikuwa na mfano kwake ilikuwa ya kipekee kabisa.
Ilikuwa Juma la mwisho kabla ya kuingia katika mitihani mwalimu Rehema anayefundisha Kiswahili alifanya mashindano, aliwataka wanafunzi kutunga methali na vitendawili vitano.Wanafunzi wote walishindwa lakini Baraka alishinda kwa kutunga methali tano kwa wakati mmoja.Mwalimu Rehema alifurahi sana na kumpa Baraka soda ya kopo.Ilikuwa yapata Wiki sasa tangu Baraka arejee shuleni,mitihani ya darasa la saba tayari ilikuwa inaandaliwa,walimu walionekana kukosa nafasi za kupumzika kwa ajili ya kutayarisha wanafunzi wao katika mitihani hiyo.Waalimu walianza kuwatangazia wanafunzi kwamba siku inayofuata kufanyika mitihani ya darasa la saba .Wanafunzi walikaa kwa umakini kusubili mitihani hiyo.
Siku iliyofuata wanafunzi walifanya mtihani wa darasa la saba, Baraka alikaa kiti cha mbele kutokana na herufi yake kuwa juu, hivyo walikaa mbalimbali na Juma.Wanafunzi hao walifanya mitihani yao kwa amani, wasimamizi walikuwa makini kuwachunguza kila mtu aliogopa kumsaidia mwenzake Baraka alifanya kwa uwezo wake bila bugudha yoyote.Siku mbili mbele wanafunzi hao walimaliza mitihani yao waliagana na walimu wao kisha wakarejea nyumbani wakiwa na matumaini ya matokeo vizuri mitihani hiyo.
*******
Baada ya miezi mitatu kupita matokeo ya darasa la saba yalitangaza,wanafunzi walisikilizia majina yao,wenye magazeti walisoma,redio walisikiliza,mitandaoni waliangalia ili kujua kama majina yametangaza.Ilikuwa kazi bule majina hayakusikika wala kuonekana mpaka pale alipobandikwa Shuleni ndio kila mtu alikwenda kuangalia jina lake.Siku hiyo Baraka na Juma walipofika shuleni kwao na kuona majina yao ,kwa bahati nzuri wakiwepo katika orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.Walifurahi sana ,walirudi nyumbani wakiwa na amani tele kuendelea na masomo.Meno yote thelathini na mbili yalionekana kinywani mwao.
Walipofika nyumbani Baraka hakutaka kuficha alimwambia mama yeke furaha aliyokuwa nayo.Bi.Mwasi alishangaa ghafla alimrukia mwanae na kumkumbatia,kelele za Baraka zilifika mpaka nyumba ya jirani.Mama Juma alisikia kelele hizo alitoka na kuelekea nyumbani kwa Bi.Mwasi ,alimkuta Baraka na Mamaye wakiwa na furaha ,alishangaa maana hakuelewa kelele zile zimetokana na nini.........
alimsogerea Bi.Mwasi na kumtaka kumweleza kinaga ubaga kilichomsibu mpaka akawa katika hali hiyo Bi.Mwasi alimweleza ilivyokuwa.Muda huo huo ilisikika sauti kutoka upande wa pili kilikua kilio,wote walishangaa na kugeuka nyuma walimwona Shamila akilia kwa uchungu,mama yake alimfuata na kumwuliza kilichomsibu,akamweleza mama yeke kwamba amefeli mtihani wa darasa la saba.Bi.Mwasi,Juma na Baraka walimtuliza Shamila kisha wakamtaka awe na amani yawezekana matokeo yaweza toka tena awamu ya pili jina lake litakuwepo.Shamila alivyosikia hivyo akanyamaza na kuwapongeza wenzake kwa kuingia sekondari.Baada ya maongezi yao Mama Shamila aliaga kisha wakaondoka na Juma kukatisha nyumbani kwao.
Ilikuwa siku ya Jumapili majira ya saa kumi jioni,walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchanganyiko walionekana wakiwa na furaha,Furaha hiyo ilitokana na kufaulu kwa daraja zuri kwa wanafunzi wa shule hiyo akiwemo Baraka kuingia kidato cha kwanza.Wanafunzi hao walialikwa baada ya kumaliza mitihani yao,basi atakaye faulu atakuja hapa shuleni ili aweze kupokea zawadi yake.Sherehe ilifanyika siku hiyo kukiwa na michezo mbalimbali kama ngoma na mashairi,Baraka alishiriki kikamilifu katika sherehe hiyo,wanafunzi na wazazi walikula wakanywa mpaka wakasanza.Baraka alionyesha furaha ya ajabu siku hiyo,alicheza na kuimba jukwaani huku akitumia ujuzi wake kuwafurahisha waalikwa,Juma nae alitunga mashairi ya hali ya juu sana,wenzake walimshangilia kila alipogani ubeti wa shairi lake.Sherehe hiyo iliyoandaliwa na mwalimu Njaidi ilipendekeza hafla hiyo fupi iliyochukua masaa sita kufurahi,wanafunzi walikuwepo wachache na wengine hawakuwepo,muda wa mwisho kabla sherehe kumalizika wanafunzi walimbeba Baraka juu juu kwa furaha. Siku hiyo Bi Mwasi na Mumewe walikuwepo katika shughuli hiyo pia walimfuata mtoto wao na kumkumbatia kwa furaha walimu nao walimpongeza Baraka wakasikika wakisema jambo husilolijua ni kama usiku wa giza“hama kweli walemavu wanaweza”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya mwezi mmoja kupita Mwalimu Njaidi aliitekereza ahadi aliyoitoa kumsomesha Baraka iwapo atafaulu,sasa akaanza kufuatilia shule aliyochaguliwa kwenda kusoma Baraka.Shule ya sekondari kibasila ndio shule ambayo amechaguliwa kuanza kidato cha kwanza,Mwalimu gama alipoakikisha kila kitu kikiwa tayari Baraka akapelekwa kulipoti shuleni hapo.Hatimaye siku iliyofuata Baraka akaanza masomo.Alianza kwa taabu kutokana na kutokuwa na rafiki anayemjua ,baada ya siku mbili tatu Juma nae akaaanza katika shule hiyo na darasa likawa moja.wakajikuta kwenye wakati mgumu kujenga urafiki na wanafunzi wengine,walijitenda peke yao ,kila kitu walifanya kama wao,hawakupenda kumshirikisha mtu.Siku zinavyozidi kwenda ndivyo ukaribu wao na wanafunzi wengine wanavyokuwa,walijikuta wanaomba hiki mara wanauliza ili yote hayo yakaanza kujenga mazoea na wanafunzi wenzake.
Ilikuwa imefika miaka miwili sasa tangu Baraka kuanza masomo ya sekondari kwa wakati huo alikuwa kidato cha pili shule ya sekondari kibasila,alishayazoea mazingira ya shuleni hapo,wazazi wake na mwalimu Njaidi walijitaidi kadri ya uwezo wao,kumpatia malezi bora,alipata kila anachokiitaji,alipendwa na kila mtu si nyumbani wala shuleni.Baraka alikuwa anaongoza darasani tangu kidato cha kwanza mpaka sasa kidato cha pili bado anashika nafasi ya kwanza au ikikosekana nafasi ya pili.Juma yeye alikuwa katika kumi bora hakuwai kuvuka wala kushuka katika nafasi ya sita.Wanafunzi wengine walikuwa na chuki za wazi juu yao, Baraka na Juma hawakujali waliendelea kukazana katika masomo yao maana hayo yote walishayapitia shule ya msingi.
Siku moja Baraka akiwa peke yake anakwenda shuleni, Ghafla akiwa njiani alihisi hali isiyo ya kawaida akaona Kama kimvuli za mtu kikimfuata akasimama.Aligeuka nyuma ili kuangalia, alishangaa kumuona wanaume mrefu mwembamba wala hakumtambua alimwangalia kwa muda Yule bwana akaanza kumsukuma huku akiwa amemshika mkono wa kulia kwa nguvu zake zote. Baraka akawa anagoma kwenda akaogopa kuuawa akaamua kujipigania kupambana na mtu huyo ikawa vuta nikuvute , akaona sasa nguvu zikimwishia akapiga kelele ili kuomba msaada.Watu waliokuwepo kando ya Barabara waliona mtiti huo waanza kujitokeza kwa wingi na wakaenda kumsaidia Baraka , ghafla Yule jamaa alimwachia Baraka kisha akaanza kukimbilia upande wa pili na kutokomea kusikojulikana,Baraka alijisikia afadhali baada ya mtu huyo kumwachia, watu walimtafuta bila mafanikio.Baadhi ya watu wakamwuliza Baraka kilichomsibu mpaka kupelekea jamaa Yule kukimbia.
“Vipi wewe kuna tatizo gani limetokea?”Mama Mmoja wa makamo alimwuliza
“Yule Jamaa alikuwa anataka kuniteka”Baraka alijibu
“Aisee! Pole kijana”Yule mama alimpa pole
“Ahsante sana nyote, kukosa ninyi ningelikuwa ameshanichukua sasa”Baraka alisema
“Je hunamjua au? Mkaka mwingine alimwuliza
“Hapana simfahamu hata sura yakesijawai kuiona.
Watu wote walijawa na hudhuni wa hali ya juu kumsikitikia mtoto Baraka wengi wao waliongea na kumlaumu kutembea peke yake kwani kuna hatarisha maisha hasa kipindi hicho Albino wengi wanauliwa na wengine kukatwa mikono kwa miguu.Baraka hakuwajali maongezi yao aliwashukuru kisha akaondoka kuelekea shuleni.Aliondoka huku akiwa mtu mwenye mawazo mengi, mashaka na majutio ya kuondoko bila kumsubili Juma, baada ya mwendo mfupi alifika shuleni salama salmini.Alipofika tu alimtafuta Juma na alipomuona alimwambia kilichomtokea akiwa njiani,Juma alimpa pole mwenzake na kumtoa wasiwasi yeye yupo siku zote kwa ajili ya kumlinda.
Wiki ilipita miezi nayo ikasogea hatimaye kipindi cha mitihani ya kidato cha pili ikawadia.Baraka na Juma wakafanya mtihani huo kwa furaha na amani, siku hiyo ilikuwa ya muhimu kwao hasa kuwa na matumaini ya kuingia kidato cha tatu.Siku ya mwisho kumaliza mitihani hiyo Baraka na Juma walirudi nyumbani.Juma siku hiyo hakutaka kupitia kwa Baraka aliunganisha moja kwa moja mpaka kwao.
Baraka yeye alipoachana na Juma alifika nyumbani na kumkuta mama yake akilalamika kichwa kumuuma, alichukua dawa aina ya panadol na kumpatia akameza ili kutuliza maumivu. muda ulikuwa ukizidi kwenda ndivyo Bi.Mwasi alizidi kulalamika maumivu ya kichwa aligalagala na kupiga kelele,Baraka alipoona mama yake akizidiwa alitoka nje kuomba msaada.Ile anatoka tu alikutana uso kwa uso na Baba yake,bila kuchelewa alimwambia babaye kuwa mama hajielewi,anapiga kelele mara nyingi akiwa akilalamika kichwa kinamuuma.Bwana Ahmed aliposikia maneno hayo hakujali chochote kilichopo mbele yake, mawazo yote yalikuwa kwa mkewe aliingia ndani moja kwa moja na kumkuta mkewe akiugulia maumivu.Bwana Ahmed alimsogelea karibu na kumwuliza kilicho msibu mpaka akawa katika hali hiyo,Bi.Mwasi alimweleza kuwa ni maumivu makali anayapata kichwani.Hakutaka kuendelea kumwoji mkewe alimbeba juu juu na kumpeleka hospitali.Njia nzima Bi.Mwasi alilalamika maumivu anayoyapata,alilia kama mtoto mdogo Walipofika tu manesi na wakunga walimpokea Bi mwasi na kupatia matibabu.Siku hiyo Bi. Mwasi hakuruhusiwa kutoka badala yake alitakiwa kulala kwa muda wa wiki mbili hospitalini hapo.Baraka akiwa amejiinamia nje ya hospitali Ghafla alimuona baba yake akimfuata pale alipokuwa amekaa kisha akamwuliza kilichotokea, ambapo alimweleza kulichomsibu Mama yake kuwa na Marelia kali sana iliyopelekea kulazwa ili kuwa chini ya uangalizi wa daktari, mpaka pale atakapopata nafuu ndio tutarudi nae nyumbani.
Kesho yake Asubuhi na Mapema Baraka na Baba yake walikwenda tena hospitali,walipofika wodini hawakumuona mgonjwa wao.Bwana Ahmed alichanganyikiwa alitembea na kuzunguka wodi nzima akimtafuta mkewe lakini hakumwona ,hata pale walipojalibu kuulizia wagonjwa waliokuwepo pia walisema hawajui alipoelekea.Waliamua kwenda kuulizia mapokezi ambapo walipata taarifa kamili ,habari hizo zilikuwa za kuhuzunisha Baraka alijiisi mwili wake ukiishiwa nguvu.Taarifa hizo zilikuwa zikitoka kwa Dokta mmoja wa kike hospitalini pale ni kwamba Mgonjwa wao aliyekuwa amelazwa jana yake alikuwa amefariki dunia.Bahati hakuamini masikio yake aliisi kama yupo ndotoni , kwani maneno hayo yalimwumiza vilivyo na kuumiza moyo wake vibaya sana.Bwana Ahmed nae alikaa chini kabisa pale pale mapokezi, aliiisi mwili mzima umepata ganzi punde akaanza kulia ni pale manesi walipomwakikishia kuwa mwili wa Bi.Mwasi upo mochwali tayari umeshaifadhiwa kilichobaki ni utaratibu wa mazishi tu basi.Hawakuwa na jinsi waliwasiliana na ndugu na marafiki wakaanza kukusanyika nyumbani kwake.Siku iliyofuata Mazishi ya Bi.Mwasi yakafanyika nyumbani kwake Buguruni.Marafiki walikuwa na kazi ya ziada kumbembeleza kijana Baraka kwani ilikuwa pigo kubwa kuondokea na mama yake kipenzi,aliyemzaa na kumlea katika misingi bora leo hii anamuacha akiwa hana mlezi,Baba pekee hatoweza hata kidogo aliona bado hajakamilika.Hakika Baraka alikuwa katika wakati mgumu sana kuamini kama kweli mama yake kipenzi amefariki.Juma na Mama yake walikuwa katika mstari wa mbele kuakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika mazishi ya Bi.Mwasi.Juma alikuwa na kazi ya ziada kumbembeleza rafikiye kipenzi Baraka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment