Search This Blog

Friday, July 15, 2022

VIGANJA MASHAVUNI MWANGU - 5

 







    Simulizi : Viganja Mashavuni Mwangu

    Sehemu Ya Tano (5)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Patricia alikuwa msichana mrembo aliyekuwa akiishi katika Jiji la Lyon nchini Ufaransa. Alikuwa msichana mwenye mchanganyiko wa rangi, sura ya kitoto na kila alipokuwa akitabasamu au kucheka vishimo vilionekana mashavuni mwake kitu kilichomfanya kuonekana mzuri maradufu.

    Katika kipini ambacho alikuwa na mapacha walioungana kwenye ndege alikuwa akitoka Dubai kuelekea nchini Marekani. Walikutana ndani ya ndege na kuzungumza na Walter, kwa jinsi alivyokuwa akiwaona kila siku katika mitandao ya kijamii na hata magazeti, kitendo cha kuonana nao na kuzungumza pamoja kilimchanga.

    Alifurahi na mwisho wa siku kupiga nao picha. Hakutaka kuondoka pasipo kuwaomba namba ya simu, alipoomba, mtu wa kwanza kabisa kutoa alikuwa Walker. Alichukulia kila kitu kuwa kawaida japokuwa kwa upande mwingine alijiona kuwa mtu mwenye bahati kubwa mno.

    Aliwajua masupastaa, walikuwa watu waliojiona, walioishi maisha yao ambapo hawakuwa radhi kutoa namba zao za simu. Kwa Walker, alishangaa, ilikuwaje mwanaume huyo awe mwepesi kumpa namba ya simu, kuweka ukaribu kitu ambacho kilionekana kuwa kama ndoto katika maisha yake.

    Njia nzima alikuwa akijibaraguza kwa Walker, walikuwa wakizungumza mambo mengi huku Walter akiwa amechuna kabisa, yeye alikuwa bize na Catherine aliyekuwa katika upande mwingine kabisa.

    Ndege ilipofika Marekani, akateremka huku akimwambia Walker kwamba kesho yake alitakiwa kuondoka kuelekea Ufaransa alipokuwa akisoma ambapo huko ndipo alipokuwa akiyaendesha maisha yake.

    Kitendo cha kubadilishana namba za simu kikawafanya kuwasiliana mara kwa mara. Walker alijua kuzungumza na mwanamke, alijua kusifia, alijua kubembeleza kitu kilichomfanya Patricia kujiona kama malkia wa mbingu aliyeshushwa duniani kwa bahati mbaya.

    “Unajua kama wewe ni mzuri sana?” aliuliza Walker kwenye simu.

    “Mmh! Mimi?”

    “Ndiyo! U mzuri sana. Kama ungekuwa gari, basi wewe ungekuwa Lamborghini au Ferrari,” alisema Walker.

    “Mmh! Una maneno wewe!”

    “Kweli tena. Nilipokuona kwa mara ya kwanza, moyo wangu ulibabaika, nilishindwa kukuangalia mara mbili. U mzuri sana, unapokasirika, uzuri wako haupotei, unapokuwa kimya, bado u mzuri mno, unapokasirika, uzuri wako unazidi kuonekana maradufu. Patricia, hivi ulizaliwa muda gani?” aliuliza Walker baada ya maneno mengi yalimfanya msichana huyo kutabasamu kila wakati.

    “Hahah! Unanichekesha!”

    “Sidhani kama ulizaliwa hospitalini! Nahisi ulizaliwa supamaketi, tena karibu kabisa na friji lililokuwa na chokolate. U mrembo sana, sina mtu wa kukufananisha nawe,” aliendelea kusema Walker huku akichukua maneno mengi kutoka katika Kitabu cha Romeo And Juliet kilichoandikwa na mwandishi wa Kiingereza, William Shakespear.

    “Walker! Hujakutana na wazuri!”

    “Nimekutana nao, ila moyo wangu umekukubali zaidi wewe! Unajua kutabasamu, unajua kuringa, unajua kupetika, kwa kifupi wewe ni malkia wa nyuki, acha kidume niwe mtafuta maua.”

    “Hahah! Nashukuru sana!”

    “Hebu rudia tena! Nataka niisikie sauti hiyo tena!” alisema Walker huku akitoa kicheko cha mbali kabisa.

    “Kwani sauti yangu ipoje?”

    “Hebu rudi kwanza. Kidogo tu!”

    “Niambie kwanza ikoje!”

    “Jamaniiiii! Rudi basi mpenzi! Rudia basiiiii...”

    “Nashukuru!”

    “Patricia, nimekwambia una sauti nzuri sana, kwa sauti yako ina uwezo wa kulifungua daraja la London, kwa sauti yako ina uwezo wa kuufanya mnara wa Eifel jijini Paris ukapinda na hata kuanguka,” alisema Walker.

    “Hahah! Utanifanya nisikie aibu!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hakuna bwana! Unajua nashindwa kuvumilia, nashindwa kuongea lolote lile. Nahitaji nikuchore, picha moja matata sana,” alisema Walker.

    “Kweli?”

    “Haswaa! Nitakuchora. Haiwezekana nikutane na msichana mrembo kama wewe halafu niache kumchora. Patricia, ninakupenda mno!” alisema Walker huku simu ikiendelea kuwa sikioni mwake, Waltr alishindwa kuzungumza lolote lile kwani kwa jinsi ndugu yake alivyokuwa akiendeshwa kwa nguvu kubwa ya mapenzi, hata kwake ilikuwa hivyohivyo.

    Walizungumza mengi, Patricia akajisikia raha moyoni mwake, alipenda kupendwa, alijihisi kuwa msichana aliyekuwa na bahati kubwa mno maishani mwake.

    Hakutaka iwe siri, alichokifanya ni kuwaambia wazazi wake kwamba alipata mwanaume wa kweli na alipowaambia kuhusu mwanaume huyo, wao wenyewe hawakuamini. Walimfahamu Walker, alikuwa mwanaume mzuri wa sura japokuwa alikuwa ameungana na ndugu yake, Walter. Walijisikia fahari mno na kumsisitizia kwamba kitu cha kwanza kabisa alitakiwa kusoma na kuhakikisha anapata digrii yake ya kwanza ya mambo ya uchumi.

    Walker hakutaka kuchelewa, bado penzi lilikuwa changa na alikuwa na presha kubwa, alichokifanya ni kumchora msichana huyo na picha yake kumtumia katika barua pepe. Patricia alipoipata, hakuamini macho yake, aliishangaa kwani kwa jinsi ilivyoonekana, ilikuwa kama si picha ya kuchorwa.

    Kwa jinsi alivyokuwa na furaha, akaanza kububujikwa na machozi na kumpigia simu Walker na kuanza kuzungumza naye. Moyo wake ulijisikia furaha mno, walizungumza kana kwamba hawakuwahi kuzungumza kabla.

    “Nakuja Marekani!” alisema Patricia huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Unasemaje?”

    “Nakuja Marekani! Siwezi kuvumilia!” alisema msichana huyo.

    “Mmh! Mbona ghafla hivyo?”

    “Najua! Nina hamu ya kukuona, siwezi kubaki Ufaransa, naomba nije, tena kesho!”

    “Kesho?”

    “Ndiyo!”

    Huo ndiyo ulikuwa uamuzi wake, moyo wake ulichanganyikiwa, hakutaka kusikia kitu chochote kile, kitu pekee alichokitaka muda huo ni kumuona mwanaume huyo tu. Hakutaka kubaki Ufaransa, alichokifanya siku iliyofuata ni kupanda ndege kuelekea Marekani.

    Njiani, moyo wake ulikuwa na mawazo tele, alikuwa na kiu ya kumuona mwanaume huyo kwa mara nyingine tena. Baada ya saa kadhaa ndege ikatua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK na kuteremka. Akampigia simu na kumwambia kwamba alikuwa amekwishafika.

    “Mbona sikuoni mpenzi?” aliuliza Patricia.

    “Nimekuja kusaini mkataba wa American Got Talent! Umekwishafika?”

    “Ndiyo!”

    “Chukua teksi! Nimekwishakuchukulia chumba katika Hoteli ya Caspean Ville! Chumba namba 79. Ukifika hapo chukua ufunguo, nimekwishaacha maagizo. Nitakuja mpenzi nikimaliza kazi ya huku!” alisema Walker.

    “Sawa. Nashukuru! Utanikuta huko.”

    “Haina shida. Nakupenda mpenzi!”

    “Nakupenda pia!”

    Patricia hakutaka kubaki mahali hapo, alichokifanya ni kuchukua teksi na kuanza kuondoka mahali hapo huku akionekana kuwa na furaha tele. Wakati gari likiwa limeingia katika Barabara ya St. Louis IV, ghafla honi nyingi zikaanza kusikika, dereva alikuwa amejisahau kuzembe kabisa, hakuangalia vizuri taa zilizokuwa zikiwaka na hivyo kuingia katika barabara hiyo iliyokuwa ikiruhusu magari yaliyokuwa yakikimbia kuanzia kasi ya 100 mpaka 150. Ni mlio mmoja mkubwa ndiyo uliosikika mahali hapo.

    “Puuuuuuuu!” Teksi ile ikagongwa, ikaruka angani, ikabingirika mara tano, watu wakashika vichwa, ilipotua chini, damu tu ndizo zilizokuwa zikionekana kwenye lami. Patricia akatulia kwenye kiti kama alivyokuwa huku akitokwa na damu mfululizo.



    Hakukuwa na siku ambayo Walker alikuwa na hamu ya kuzungumza na Patricia kama siku hiyo. Wakati wakiwa kwenye mkutano kwa ajili ya kusaini mkataba huo ambao ungewafanya kuwa majaji katika Shindano la American Got Talent, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria msichana huyo mrembo.

    Wakati mwingine alitamani asimame na kuondoka, aliona kila kitu kikiendelea taratibu sana, alitamani yeye ndiye angekuwa msimamizi wa mkutano huo mdogo ambao angeamua ni muda gani walitakiwa kuondoka humo ndani.

    Muda ulizidi kwenda mbele, baada ya dakika kadhaa, akapokea notification ya CNN ambayo ilimwambia kwamba kulikuwa na ajali mbaya iliyokuwa imetokea katika Barabara ya St. Louis.

    Hilo wala halikumtisha, kwake, lilionekana kuwa jambo la kawaida akaendelea kukaa kwenye kikao mpaka kilipokwisha ambapo kitu cha kwanza kabisa akachukua simu yake na kumpigia Patricia ambaye alimwambia atangulie hotelini.

    Simu ikaanza kuita pasipo kupokelewa, hilo halikumtia hofu sana kwani alihisi kwamba msichana huyo alikuwa bafuni akioga hivyo kusubiri zaidi na baada ya dakika kadhaa kumpigia tena. Majibu hayakubadilika, yaliendelea kuwa vilevile kwamba simu haikupokelewa.

    Hilo likaanza kumtia hofu, akaanza kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea huko alipokuwa. Alichokifanya ni kupiga simu katika hoteli aliyomuwekea chumba kwa lengo la kusikia kama msichana huyo alikuwa amefika humo au la.

    “Hajafika,” sauti na msihana upande wa pili ilisikika.

    “Hajafika?”

    “Ndiyo!”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hilo likamchanganya zaidi, likamfanya kuipiga simu ya msichana huyo zaidi lakini majibu yalikuwa yaleyale kwamba simu haikupokelewa kitu kilichomfanya kuwa na hofu kubwa.

    Akamwambia Walter kile kilichokuwa kikiendelea, jinsi alivyokuwa na hofu kwamba inawezekana kulikuwa na jambo baya limemtokea mpenzi wake kwani kila alipokuwa akimpigia simu haikuwa ikipokelewa kitu ambacho hakikuwa kawaida kabisa.

    “Sidhani kama kuna jambo baya limetokea. Au amelala hotelini baada ya kuchoka na safari,” alisema Walter manano ambayo aliamini kwamba yangemfariji ndugu yake huyo.

    “Walter! Nahisi kuna tatizo!” alisema Walker.

    “Hakuna tatizo! Usihofu braza, hakuna kitu chochote kile, niamini!” alisema Walter.

    Japokuwa alifarijiwa vya kutosha lakini Walker hakufarijika, bado moyo wake ulimwambia kwamba kulikuwa na kitu cha hatari kilichokuwa kimetokea. Hakuacha kumpigia simu, kuna kipindi kila alipokuwa akipiga simu, haikuwa ikiita, ilionyesha kabisa ilikuwa imezima.

    Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Wakati akiendelea kuwa katika hali ya mawazo huku akiwa hajui ni kitu kilimtokea Patricia mpaka kuamua kuzima simu, akasikia tena mlio kwenye simu yake kuonyesha kwamba kulikuwa na notification ilikuwa imeingia. Haraka sana akaifungua, ilitoka katika akaunti ya CNN ambayo ilionyesha kwamba jina la mtu aliyekuwa amepata ajali hatimaye alijulikana kwa jina baada ya kupatikana kwa vitambulisho vyake kwenye gari.

    “Ni Patricia...” alisema Walker huku akiwa ameshutuka.

    Akahisi kama moyo wake ukipigwa ganzi, hakuamini kile alichokuwa amekiona, msichana aliyekuwa akimpenda kwa moyo wote, aliyemuona kuwa kila kitu katika maisha yake alikuwa amepata ajali mbaya ya gari.

    Hakukukalika tena, machozi yanaanza kumtoka na kububujika mashavuni mwake, hakutaka kubaki mahali hapo, akamwambia Walter kwamba ni lazima waelekee hospitalini kwani Patricia alipata ajali mbaya ya gari.

    Kazi ya Walter ilikuwa ni kumbembeleza ndugu yake huyo, alimuonea huruma, alikuwa akibubujikwa na machozi tu kitu kilichomfanya kuumia mno moyoni mwake kwani hakupenda kumuona Walker akiwa kwenye hali hiyo, ila kwa kuwa alimpenda sana Patricia, hakuwa na jinsi.

    Wakaondoka mpaka katika Hospitali ya St. Monica iliyokuwa hapohapo New York. Walipofika, kama kawaida watu wakaanza kuwazunguka, kila mtu alitaka kusainiwa kitabu na nguo zake kwani kitendo cha kukutana na watu maarufu kama hao lilikuwa jambo moja adimu sana.

    Wakatembea pasipo kuzungumza na mtu yeyote mpaka walipofika katika chumba walichoambiwa wasubiri. Muda wote huo Walker alikuwa akilia, moyo wake ulimuuma, hakuamini kama msichana aliyekuwa akimpenda kwa moyo wote alikuwa hoi hospitalini hapo.

    Madaktari walikuwa bize wakihangaika na hali yake, walimtibu kwa nguvu zote kuhakikisha kwamba msichana huyo anapata nafuu na kurudi katika hali yake ya kawaida. Muda ulizidi kwenda mpaka baada ya saa tatu ndipo mlango ukafunguliwa na kuchukuliwa kupelekwa katika ofisi ya daktari.

    Huko, wakapewa taarifa ambazo hazikuwa nzuri, Patricia alikuwa ameumia vibaya mno, ubongo wake ulipata ufa huku uti wa mgongo ukiwa umevunjika mara moja hali iliyomaanisha kwamba hata kama angerudiwa na fahamu, angepooza mwili mzima.

    “Unasemaje?” aliuliza Walker huku akimwangalia daktari.

    “Hatoweza kusimama! Amepooza mwili mzima. Cha msingi tumuombe Mungu tu,” alisema daktari maneno yaliyomfanya Walker kulia mno.

    Walter akaanza kumbembeleza ndugu yake aliyekuwa ameumia sana, alilia kama mtoto, hakubembelezeka wala kunyamaza, kitendo cha Patricia kupata matatizo hayo kilimfanya kuumia moyoni mwake na kujiona kwamba yeye ndiye alikuwa sababu kubwa ya msichana huyo kupata matatizo hayo kwani pasipo kumwambia kwamba aelekee nchini Marekani, asingepata ajali hiyo.

    “Pole sana Walker! Huu si mwisho wa Patricia,” alisema Walter huku akimpigapiga ndugu yake huyo mgongoni kama njia ya kumfariji.

    Daktari alinyamaza, mbali na taarifa hiyo pia alikuwa na taarifa nyingine kuhusu msichana huyo, taarifa ambayo aliamini ingekuwa mbaya zaidi, kila alipotaka kuwaambia, alinyamaza kwani kama kwa taarifa hiyo tu Walker alilia hivyo, ingekuwaje kama angempa taarifa nyingine ambayo aliamini ingemuumiza zaidi?

    Hakutaka kunyamaza, ilikuwa ni lazima kumwambia ukweli juu ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Akawaambia kwamba mbali na tatizo hilo, pia kitendo cha ubongo wake kupata ufa uliufanya kutikisika na kupata tatizo jingine ambalo lingeonekana kuwa la hatari kama lilivyokuwa lile la kupooza.

    “Kitu gani?” aliuliza Walter.

    “Hatoweza kukumbuka kitu chochote kile. Kumbukumbu zake zimefutika, zimekuwa kama za mtoto aliyezaliwa leo. Yaani hatoweza kumfahamu mtu yeyote yule, hatowafahamu wazazi wake, hatowafahamu nyie, hatokumbuka kitu chochote kile, ila yote hayo yatatokea kama tu atarudiwa na fahamu,” alisema daktari aneno yaliyomfanya Walker kulia zaidi.

    Huo ndiyo ulikuwa ukweli wenyewe, hakukuwa na kilichobadilika, msichana Patricia alikuwa kimya kitandani, uti wa mgongo ulivunjika na mbaya zaidi alipata matatizo kichwani yalioupelekea fuvu lake kupata ufa na ubongo kutikisika.

    Yalikuwa ni maumivu makali kwa Walker, hakuamini kama kweli mpenzi wake angepatwa na tatizo kama hilo. Hakuacha kulia, alibembelezwa lakini hakubembelezeka, alihisi kama huo ndiyo ungekuwa mwisho wa msichana huyo mrembo aliyekuwa akimpenda kwa moyo wake wote.

    Baada ya kuzungumza na daktari, wakatoka na kuelekea nje ya chumba ambacho Patricia alikuwa amelazwa kwa ajili ya mapumziko baada ya kufanyiwa upasuaji. Wakatulia hapo, hakukuwa na mtu aliyewasogelea kwani kwa jinsi walivyoonekana, haukuwa muda mzuri wa kuomba kupiga nao picha au kuomba kusainiwa vitabu vyao.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Edmund alikuwa akitafutwa kila kona, watu waliangalia mitaani, kila mtu waliyekuwa wakimtia hofu kwamba alikuwa yeye walimchukua. Hawakujua mahali jamaa huyo alipokuwa, japokuwa matangazo yalibandikwa kila kona lakini bado mwanaume huyo hakuonekana.

    Hilo likawapa wasiwasi watu wengi na kuhisi kwamba inawezekana mwanaume huyo akawa amepotea sehemu fulani na hivyo alitakiwa kutafutwa kwa nguvu zote. Walipambana, walimtafuta lakini matokeo yaliendelea kuwa yaleyale kwamba hakuonekana sehemu yoyote ile.

    Baada ya kuona kuwa wasingefanikiwa, M16 wakaamua kuanza kumtafuta kupitia simu yake, waliamini kwamba huko alipokuwa ilikuwa ni lazima kuwasiliana na familia yake hivyo kufanya hivyo.

    Walipomtafuta kwa kutumia simu yake, waliona kabisa kwamba jamaa alikuwa akiondoka kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Walimfuatilia kwa nguvu zote, waliona akiondoka Uingereza na kuingia Wales, hawakutaka kubaki nyuma, wakawasiliana na polisi wa huko na kuwaambia uwezekano wa kumkamata Edmund.

    Wakati akiwa ameondoka katika sehemu ya kuchezea watoto, dakika tatu mbele polisi wakafika mahali hapo na kuanza kuangalia kila kona, waliamini kwamba alikuwa hapo lakini kitu cha ajabu kabisa hawakuweza kumuona.

    Kifaa cha GPS ndicho kilichokuwa msaada kwao, wakaanza kuangalia ili kuona kama alikuwa mahali hapo amejificha au la, walipoangalia, wakaona kwamba alikuwa amekwishaondoka mahali hapo na kuanza kumfuatilia kwa kutumia kifaa hicho.

    Hilo lilifanyika kwa nguvu kubwa, wakafanikiwa kuifikia nyumba ambayo alikuwepo, kifaa kile kiliwaonyeshea kwamba Edmund alikuwa ndani ya nyumba hiyo na hivyo kuanza kuelekea humo.

    Walipoufungua mlango, Mzee Vonn akatoka, kitu cha kwanza wakamuweka chini ya ulinzi na kuingia ndani ambapo huko, pamoja na kumtafuta sana, wakamkosa kabisa.

    “Yupo wapi?” aliuliza polisi mmoja.

    “Sijui! GPS inaonyesha yupo humu. Mungu wangu! Kumbe ameacha simu na yeye kukimbia,” alisema polisi mmoja huku akishangaa.

    Waliifuatilia simu hiyo kwa kipindi kirefu, waliamini kwamba wangempata lakini mwisho wa siku waliweza kuipata simu na Edmund hakuwepo mahali hapo. Walichanganyikiwa, wakatoka ndani, wakamtafuta hata kwa nje na sehemu nyingine lakini hawakufanikiwa kumpata.

    ****

    Japokuwa Edmund alikaribishwa kwa upendo mkubwa ndani ya nyumba ya Bwana Vonn lakini moyo wake haukuwa na amani hata kidogo. Alimwangalia mzee huyo, alionekana kuwa na furaha mno kwa yeye kuwa hapo na hakuona dalili zozote za mzee huyo kumkamata au kumfanyia mchezo mchafu wowote ule.

    Akapelekwa chumbani kwake na kutulia huko. Usingizi haukuja, alijaribu kulala lakini usingizi ulikataa kabisa kitu kilichomfanya kuwa na hofu kwamba inawezekana kungekuwa na kitu kibaya ambacho kingemtokea mahali hapo.

    Akatulia chumbani, muda ulizidi kwenda, usingizi ukakata na kutulia kitandani. Macho yakeyalikuwa dirishani, alikuwa akiangalia nje kuona kama kungekuwa na mtu yeyote ambaye angefika nyumbani hapo.

    Muda ulizidi kwenda, baada ya dakika kadhaa akasikia muungurumo wa gari kutoka nje, haraka sana akainuka na kuangalia nje, alichokiona ni gari kubwa lililoandikwa SWAT ubavuni, gari ambalo alifahamu kabisa kwamba lilikuwa ni la polisi waliokuwa na silaha nzito.

    Hakutaka kujiuliza sababu ya watu hao kufika mahali hapo, akajua kwamba walifika hapo kwa kuwa walikuwa wakimtaka yeye, hivyo akasimama na kuanza kufikiria ni kwa jinsi gani angeweza kuondoka nyumbani hapo pasipo kuonekana.

    “Ni lazima niondoke!” alijisemea.

    Wakati hajajua hata kitu gani alitakiwa kufanya, akasikia mlango wa sebuleni ukifunguliwa, hakutaka kujiuliza, alijua dhahiri kwamba huyo alikuwa Vonn ambaye bila shaka ndiye aliyewaita polisi hao kwa kuwa yeye alikuwemo ndani ya nyumba hiyo.

    Kwa haraka sana akachomoka chumbani, akaelekea jikoni, huko, akakuta mlango mwingine wa kutoka nje, hakutaka kujiuliza, akaufungua taratibu na kuangalia kama kulikuwa na mtu.

    Polisi walionekana kufanya uzembe mmoja tu, ni kweli walifika nyumbani hapo, mtu wao alikuwa ndani lakini uzembe waliokuwa wameufanya ni kutokuizunguka nyumba ile. Kitendo cha kumpata Vonn pale mlangoni walikuwa na uhakika kwamba Edmund alikuwa ndani na hivyo kuingia.

    Hakukuwa na mtu, waliangalia kila kona, kabatini, chini ya kitanda na sehemu nyingine lakini hawakufanikiwa kumuona mtu yeyote yule.

    Wakati wao wakiangalia huku na kule, Edmund alikuwa mbali kabisa na nyumba hiyo, alikuwa akikimbia kwa mwendo wa kasi, kubaki ndani ya nyumba hiyo kulimaanisha kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake.

    Alikimbia mpaka sehemu moja aliyokuta nyumba kubwa iliyokuwa imezungushiwa fensi kubwa huku kwa pembeni kukiwa na mti. Alichokifanya ni kuufuata mti na kuupanda na kutulia huko, sehemu ambayo aliamini kwamba ingekuwa salama mpaka asubuhi yake ambapo angeamua ni kitu gani angetakiwa kufanya.

    Kwake, alijiona kutokuwa na rafiki, aliamini kwamba inawezekana Mark alimfanyia ujanja ili akamatwe na kuvuna kiasi cha pesa kilichokuwa kimewekwa au mjomba wake, Vonn aliingiwa na tamaa na hivyo kutaka kumkamatisha na kuvuna kiasi hicho cha pesa.

    Hakutakiwa kumwamini mtu yeyote yule kwa kipindi hicho. Alihitajika kupambana na hali yake mpaka kuona kwamba anafanikiwa kuwakimbia polisi hao kwa maisha yake yote.

    Macho yake hayakutoka kule ilipokuwa nyumba ya Bwana Vonn, alikuwa akiiangalia kwa kuyaweka majani pembeni. Akaona mzee huyo akichukuliwa na kupakizwa ndani ya gari kisha kuondoka mahali hapo huku polisi wengine wakibaki kuhakikisha kwamba hatoki kama tu alikuwa ndani amejificha.

    *** CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Walker alitia huruma, moyo wake ulikuwa ukimfikiria mpenzi wake, Patricia, alimpenda, kwake, msichana huyo alikuwa kila kitu. Bado hakuamini taarifa za madaktari kwamba mpenzi wake asingeweza kukumbuka kitu chochote wala kusimama kama ilivyokuwa zamani, wakati mwingine alihisi kwamba alikuwa kwenye ndoto mbaya na ya kusisimua ambapo baada ya muda fulani angeshtuka na kujikuta akiwa kitandani.

    Kama kulia, alilia sana lakini hakukuwa na kitu kilichobadilika. Siku ziliendelea kukatika, kila siku alikwenda hospitalini hapo akiwa na pacha wake, Walter. Alihitaji kumuona mpenzi wake kitu ambacho baada ya siku tatu kuukatika, madaktari wakawaruhusu kuwaona.

    Macho yake yalipotua kwa msichana huyo aliyekuwa kitandani hoi, hakuamini, alimsogelea na kumwangalia vizuri, hakuonekana kama alikuwa mzima, alionekana kama mfu kitandani pale. Alilia zaidi, akamsogelea na kumkumbatia.

    Alijiona kuwa kwenye wakati mgumu, alijihukumu kwamba yeye ndiye aliyesababisha hayo yote kwani bila yeye Patricia asingesafiri mpaka nchini Marekani na kupata ajali hiyo.

    “Patty! Wake up and talk to me,” Patty! Amka na uzungumze nami) alisema Walker huku akiendelea kulia.

    Siku hiyo ilikuwa kimya, siku ziliendelea kukatika huku kila siku wakifika mahali hapo. Kwenye magazeti, mitandao ya kijamii na sehemu nyingine kila kona walikuwa wakiwazungumzia watu wao. Kila mmoja alimuonea huruma Walker, kwa jinsi alivyokuwa na pacha wake walipaswa kupata fulana maisha yao yote lakini kitu cha ajabu kabisa kilichokuwa kikiendelea kilikuwa ni maumivu makali.

    Baasa ya siku kumi na sita kupita ndipo Patricia akayafumbua macho yake na watu wa kwanza kabisa kuwaona walikuwa mapacha hao hata kabla ya wazazi wake.

    “Patricia! Hatimaye umeamka,” alisema Walker huku akitabsamu.

    Msichana huyo alinyamaza, hakukumbuka kitu chochote kile, alikuwa akiwashangaa, hakujua watu hao walikuwa wakina nani na walihitaji nini kutoka kwake.

    Wazazi wake waliokuwa na nyuso za furaha hasa baada ya kumuona akiwa amefumbua macho wakamsogelea na kumwangalia, hata nao pia, Patricia hakuwa akiwakumbuka, alibaki akiwashangaa tu.

    “Nyie ni wakina nani? Nipo wapi hapa?” aliuliza Patricia huku akimwangalia kila mmoja.

    Swali hilo likawapa maumivu makali zaidi mioyoni mwao, hawakuamini walichokuwa wamekisikia kutoka kwa binti yao, alikuwa amepoteza kumbukumbu zake zote na kitandani pale hakuwa akikumbuka kitu chochote kile.

    Patricia alipojaribu kunyanyuka kitandani pale, alishindwa kabisa, akahisi mwili wake ukiwa umekufa ganzi, hakujua ni kitu gani kilichokuwa kimetokea kitu kilichompelekea kuwauliza watu wale waliokuwa mbele yake kwamba ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka kuwa hivyo.

    Hakukuwa na mtu aliyemjibu kitu chochote kile, msichana huyo aliendelea kushangaa na hata wakati mwingine kulia. Daktari akaingia, alipomuona yupo katika hali hiyo, akawaomba watoke chumbani humo kwani mgonjwa alitakiwa kupumzika zaidi kitu ambacho hakikuwa tatizo lolote lile, wakatoka chumbani humo.

    Nje, Walker akaanza kulia, aliumia mno moyoni mwake. Alibaki nje ya chumba kile akiuangalia mlango wa kuingia ndani. Alimwambia Mungu kwamba mtu aliyekuwa akimuhitaji kwa kipindi hicho alikuwa msichana wake tu, hakuhitaji pesa, hakuhitaji umaarufu, kwake, Patricia alionekana kuwa kila kitu.

    Alimuomba Mungu afanye muujiza lakini hilo halikuwezekana, msichana Patricia akaendelea kuwa kitandani pale huku akiendelea kushangaa sababu za kutokusimama na hata watu wale waliokuwa chumbani mule, kilichokuwa kikiendelea, hakukielewa kabisa.



    Naseku hakuwa na raha hata kidogo, kila alipokuwa akiwaangalia watoto wake alikuwa akilia tu. Walikuwa na umaarufu mkubwa, pesa nyingi lakini kitu cha ajabu kabisa maisha waliyokuwa wakipitia, yaliwapa maumivu makubwa mno.

    Walter na Walker walikuwa watu wa huzuni tu, kila siku walikuwa wakipitia majanga mbalimba, kama walinusurika katika janga hili, kesho walikuwa wakitumbukia katika janga jingine kabisa. Hayo yalikuwa maisha yao, ni kama walikuwa wamezoea kumbe kwa jinsi walivyokuwa hawakutakiwa kabisa kupita katika maisha waliyokuwa wakipitia kila siku.

    Yeye na mumewe, Cassian walikuwa na mtoto mwingine, Esta ambaye kipindi hicho alikuwa chuo kikuu lakini bado tu hawakuonekana kufurahia kabisa, walikuwa wakimuomba Mungu ili kila kitu walichokuwa wakipitia watoto wao hao yaishe ili waishi maisha ya amani na furaha kama ilivyokuwa zamani.

    Machozi hayakuacha kutiririka mashavuni mwake, kila siku viganja vyake vilikuwa mashavuni akifuta machozi yaliyokuwa yakitiririka kila alipokuwa akiwaangalia watoto wake waliokuwa kwenye matatizo makubwa.

    Walker hakuacha kulia, mpenzi wake aliyafumbua macho yake lakini hakuwa na furaha hata kidogo, alisahauliwa, msichana huyo hakukumbuka kitu chochote kile na kila alipokuwa akiwaangalia, alibaki akishangaa.

    Hawakuacha kufika hospitalini hapo, Patricia aliendelea kuwa kitandani na hata pale alipopata nafuu, alichukuliwa na kuwekwa kwenye kiti cha walemavu kwani hakuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile katika kiti kile alichokuwepo.

    Walker na Walter ndiyo waliokuwa na kazi ya kumpeleka huku na kule, walihuzunika, wakati mwingine walikuwa wakilia, kwa Walker, alitumia nafasi hiyo kuzungumza naye maneno mengi na hata kumkumbusha yaliyopita lakini msichana huyo hakuwa akikumbuka kitu chochote kile.

    “Mimi nilikuwa nasoma?” aliuliza Patricia huku akishangaa.

    “Ndiyo! Ulikuwa nchini Ufaransa ukiishi na wazazi wako. Unakumbuka?’ aliuliza Walker huku akimwangalia msichana huyo.

    “Hapana! Sikuwahi kuishi Ufaransa hata siku moja.”

    “Unamkumbuka Annie?”

    “Ndiye nani?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Rafiki yako chuoni!”

    “Kwani mimi nimewahi kusoma?”

    “Ndiyo! Tena ulikuwa na akili sana darasani,” alisema Walker.

    Hakukumbuka kitu chochote kile, kila kitu alichokuwa akiambiwa kilionekana kuwa kipya katika maisha yake. Walker na mwenzake walijaribu kumkumbusha kila kitu kilichotokea lakini hakukumbuka kabisa.

    Wazazi wake nao walikuwa wakilia tu, waliumia, hawakuamini kama binti yao angepitia maisha kama aliyokuwa akipitia. Ubongo ulicheza na uti wa mgongo kuvunjika, yalikuwa ni matatizo makubwa yaliyowafanya kulia kila siku.

    Siku zikaendelea kukatika, baada ya miezi tisa, Walker na Walter wakaanza kujisikia hali ya tofauti vichwani mwao. Walikuwa wakipata maumivu makali ya kichwa kiasi kwamba wakati mwingine walihisi kama walibeba vitu vizito na kupoteza fahamu.

    Lilikuwa tatizo kubwa lililowatesa kupita kawaida, Naseku na mumewe walishangaa, watoto wao hawakuwahi kupata tatizo kaka hilo, hawakujua kilichokuwa kimetokea hivyo kuwachukua na kuwapeleka hospitalini.

    “Tatizo limeanza lini?” aliuliza daktari huku akiwaangalia.

    “Ni ghafla sana, hatujui tatizo nini!” alijibu Cassian huku akimwangalia daktari.

    Kilichofanyika ni vipimo, wakaangalia vichwani mwao, walihisi kwamba inawezekana fuvu la kichwa lilikuwa limepata majeraha hivyo kuangalia. Huko hawakugundua kitu, iliwashangaza, hakukuwa na tatizo lolote lile sasa kwa nini walikuwa wakizimia mara kwa mara.

    Kilichofuata kilikuwa ni kuangalia mishipa na misuli yao pale ilipokuwa ikiwaunganisha vichwani. Hapo ndipo wakagundua kwamba walikuwa wameharibu mishipa na misuli kwa kuwa tu walikuwa wakitumia nguvu kubwa mno katika kufikiria na kulia hivyo mishipa mingi kulegea na kutanuka hali iliyoonyesha kwamba hali ingekuwa mbaya zaidi katika maisha yao kama hali hiyo ingeendelea.

    “Tatizo kubwa ni nini?” aliuliza Cassian, Naseku hakuzungumza chochote kile, kazi yake ilikuwa ni kulia tu.

    “Misuli na mishipa yao ina tatizo hasa katika sehemu hii waliyoungana, kuna tatizo kubwa la kuvimba na kusinyaa,” alijibu daktari huku akiwaangalia wazazi hao.

    Lilikuwa pigo kubwa kwao, kitendo cha kufikiria sana na kuhuzunika ndicho kilikuwa sababu kubwa ya wao kuwa katika hali hiyo. Wakalazwa hosipitalini. Kila mtu duniani akajua kile kilichotokea, watu wengi wakaanza kutuma salamu zao za pole kwa mapacha hao ambao walilazwa katika chumba maalumu huku madaktari wakiendelea kuwahudumia.

    Hakukuwa na mtu aliyeruhusiwa kuingia ndani ya chumba hicho zaidi ya manesi na madaktari ambao walikuwa kwa ajili ya kuwatibu tu. Siku ziliendelea kukatika huku wakiwa humo. Tatizo lile likaanza kukua na mwisho wa siku kuanza kutoka damu katika masikio yao na madaktari walipowapima, wakaonekana kuwa na tatizo jingine kabisa, mishipa na misuli iliyokuwa imevimba ilianza kuchanika.

    “Nini?” aliuliza daktari mmoja huku akionekana kuchanganyikiwa.

    “Ndiyo hivyo! Tatizo kubwa ni kuungana kwao, haya mengi hujitokeza mara chache sana, ni wawili kati ya watu elfu kumi. Chanzo kikubwa kabisa ni kuungana kwao,” alisema daktari ambaye alikuwa ametoka kuwachukua vipimo.

    Ilikuwa taarifa mbaya ambayo hawakujua ni kwa namna gani walitakiwa kuwaambia wazazi wao. Pale katika kichwa ambapo waliungana kulipitia mishipa mingi ya damu na misuli kiasi kwamba hata ilipokuwa imevimba, ilikuwa rahisi kuchanika kwa kuwa tu ilikuwa imebanana sana na tena ilikuwa mingi kupita kawaida.

    “Watakufa! Kama kweli tatizo limefikia hapa, watakufa,” alisema daktari mmoja huku akiwaangalia wenzake, kidogo akaonekana kukata tamaa, hakukuwa na mgonjwa aliyekuwa akichanika mishipa na misuli halafu akapona.

    ****

    Edmund aliendelea kukaa kwenye mti mpaka asubuhi. Mwili wake ulichoka, hakulala usiku mzima, alikuwa na hofu kwa kuona kwamba angekamatwa na polisi. Akateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea barabarani.

    Siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti, kila alipokuwa akipita, hakukuwa na watu wengi kama ilivyokuwa siku nyingine hasa katika nchi hizo zilizokuwa zikitawaliwa na Malkia Elizabeth.

    Alitembea kwa mwendo wa taratibu, uso wake ulikuwa chini, mawazo mengi yalimtawala na hakutaka kabisa kugundulika alionekana kuwa mnyonge kupita kawaida, alijuta, hakujua kama kuna siku angekuja kuishi katika maisha aliyokuwa akiishi kipindi hicho.

    Alitembea mpaka alipofika katika kituo cha daladala ambapo hapo akatulia. Akaanza kuyafikiria maisha yake yaliyopita, japokuwa yalikuwa kwa kipindi kifupi sana hasa baada ya kutaka kuwaua mapacha walioungana lakini aliona kama ulikuwa mwaka mzima kwa jinsi alivyokuwa.

    Wakati akiwa hapo, watoto wanne wakaletwa mahali hapo huku wakiwa wamevaa sare za shule na kusubiri hapo huku wakiwa na wanawake watu wazima wawili. Walimsalimia lakini mawazo ya Edmund hayakuwa hapo kabisa, alikuwa akifikiria mbali, maisha yake yalimchanganya kupita kawaida.

    Hawakutaka kushughulika naye, wakasubiri gari la shule ambalo lilifika hapo baada ya dakika kadhaa na kuwaingiza watoto wale na kuondoka. Edmund hakusimama, bado kichwa chake kilikuwa kimechanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, alikuwa na njaa, mwili ulichoka na hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kula.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati akiwa amekaa mahali hapo, kwa mbali akaliona lile gari la wanafunzi likaanza kurudi mahali hapo. Hakuliona, kichwa chake kilikuwa mbali kabisa, gari lile likasimama karibu naye, polisi wawili waliokuwa na bunduki mikononi mwao wakateremka na kumuweka chini ya ulinzi kwa kutaka aweke mikono yake kichwani.

    Hakufanya hivyo, alikuwa akibubujikwa na machozi mfululizo na muda wote alihisi kama alikuwa akienda kufa kwa jinsi maisha aliyokuwa amepitia yalivyomchanganya.

    Alibaki akiwa kama mtu aliyeganda, hakutingishika, kichwa alikiinamisha kidogo na hakuonekana kujua kitu chochote kilichokuwa kikiendelea. Kama kuzunguka huku na kule, alifanya hivyo kwa kipindi kirefu sana, akachoka, ilikuwa ni bora kukamatwa na polisi akapumzike lakini si kuendelea kuzurura kama alivyokuwa akifanya.

    “Hands on your head,” (mikono kichwani mwako) alisema polisi mmoja huku akiwa amemnyooshea bastola lakini Edmund hakufanya hivyo.

    Wakamsogelea na kumfunga pingu, hakufanya kitu chochote zaidi ya kulia, moyo wake ulibadilika na kuumia mno, hakuyapenda maisha yake, aliyachukia na kitu pekee alichokuwa akikihitaji kilikuwa ni kupumzika tu.

    Kitendo cha kukamatwa, watu wakaanza kujaa na kutaka kujua kilichokuwa kimeendelea, dereva wa gari lile la wanafunzi ambaye ndiye aliyetoa taarifa kwa polisi hao baada ya kumuona katika kituo hicho akaambiwa kwamba gari hilo lilihitajika kumpeleka Edmund mpaka kituoni jambo ambalo halikushindikana kabisa.

    Akachukuliwa, akapakizwa ndani ya gari huku akilia. Hakuzungumza kitu chochote kile, alikuwa kimya, watu waliogundua kwamba yule alikuwa Edmund, wakapigiana simu na kuwaambia wenzao kwamba hatimaye Edmund alikuwa amekamatwa, ili kuonyesha ushahidi, mpaka picha wakawatumia.

    “Una uhakika ni yeye?” aliuliza jamaa mmoja kwenye simu.

    “Ngoja nikutumie picha uone!”



    Hakukuwa na kitu kilichobadilika, Walter na Walker waliendelea kuwa katika hali ileile, walikuwa kitandani huku wakiwa kwenye hali mbaya. Madaktari walikuwa wakihangaika kuhakikisha wanarudi katika hali zao za kawaida lakini hilo lilishindikana kabisa.

    Damu zilizidi kuwatoka, mishipa ilipasuka hali iliyowafanya kuwa katika hali mbaya zaidi. Wazazi wao walikuwa wakilia, hawakuwa wakiamini kama mwisho wa kila kitu ungekuwa namna hiyo.

    Vyombo vya habari viliendelea kutangaza kwamba watu hao walikuwa na dalili ndogo sana za kupona na kurudi katika hali kama zamani kwani hakukuwa na mtu ambaye mishipa yake ilipasuka halafu akapona.

    Kipindi hicho ni kama dunia ilikuwa kimya, ilikuwa ikiomboleza kwa kile kilichokuwa kikiendelea. Kwenye mitandao ya kijamii, magazetini na hata mitaani watu walikuwa wakiwazungumzia wawili hao na jinsi walivyokuwa na nafasi ndogo ya kuweza kupona na kurudi katika hali zao kama walivyokuwa zamani.

    “Wanakufa!” alisema mwanaume mmoja alipokuwa akiziangalia picha za mapacha hao waliokuwa hawajitambui katika kitanda kikubwa walicholalia.

    “Ila nina uhakika Mungu atawaponya!” alisema mwanamke aliyekuwa pembeni yake, macho yake yalikuwa mekundu, japokuwa hawakuwa ndugu zake lakini alishindwa kujizuia, alikuwa amelia sana kwa ajili ya watu hao.

    Watu wakaendelea kujazana hospitalini walipokuwa, kila mmoja alitaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea. Wengi waliokuwa mahali hapo walionekana kukata tamaa, walijua kabisa kwamba baada ya saa chache zijazo wawili hao wangefariki dunia na kwenda kuanza maisha mapya baada ya kifo.

    Naseku alilia sana, aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu zaidi ya mara tatu, alikuwa na uchungu mno, moyo wake ulimuuma na kila alipokuwa akiwaangalia watoto wake, alisikia kitu chenye ncha kali kikiuchoma moyo wake.

    Aliomboleza, mtu pekee aliyekuwa akimfariji kwa kipindi hicho alikuwa mume wake, Cassian. Kila alipokuwa akibembezwa, hakubembelezeka kwani alijua kabisa kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wa kila kitu, watoto wake wangekufa palepale hospitalini walipokuwa.

    Madaktari hawakuacha kuhangaika, walifanya kila liwezekanalo kuokoa maisha ya mapacha hao. Kila mtu aliwatumainia, wao ndiyo ulikuwa msaada wa mwisho waliokuwanao kipindi hicho, yaani wao ndiyo waliokuwa wameshililia uhai wa mapacha hao, wao ndyo wangeamua kama watu hao walitakiwa kufa au kuendelea kuishi.

    Hawakuwa na mategemeo yoyote ya mapacha hao kupona, damu zilizokuwa zikiwatoka baada ya mishipa kuchanika ziliendelea kusambaa miilini mwao na hivyo kuwafanya kuwa kwenye hali mbaya zaidi.

    Ilipofika tarehe 2/09/2016 majira ya saa 2:36 usiku ndiyo muda ambao Walter na Walker wakafariki dunia katika kitanda walichokuwepo.

    Hiyo ilikuwa habari ya mshtuko, madaktari ambao walilitambua hilo wakaishiwa nguvu, hawakujua ni kwa namna gani wangeweza kuwaambia wazazi wao juu ya kile kilichokuwa kimetokea kwani kwa kipindi chote ambacho watoto hao walikuwa mahututi nyuso zao zilionekana kuwa kwenye maumivu makali, ingekuwaje kama wangewaambia kuwa walifariki dunia?

    “Tutaitoaje miili hii na wakati wazazi wao wapo hapo nje?” aliuliza daktari mmoja.

    “Labda tukawatoe!”“Tukawatoe? Tutaanzaje?”“Subiri! Nakwenda kuwachukua na kuwaambia twende kwa daktari kuongea nao. Wakati nimetoka nao, nyie watoeni haraka sana muwapeleke katika chumba maalumu kwanza,” alisema daktari mwingine.

    “Sawa.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakakubaliana, hakukuwa na muda wa kupoteza, hapohapo daktari yule akatoka, akaanza kuzungumza nao na kuwaambia kwamba walitakiwa kuzungumza nao katika ofisi yake hivyo awafuate.

    “Wanaendeleaje?’ aliuliza Naseku huku akimwangalia daktari.

    “Wanaendelea salama! Twendeni,” alisema daktari.

    Wakasimama na kuanza kuondoka, walipiga hatua fupifupi huku kila mmoja akiwa na mawazo tele. Daktari alikuwa akiwaza ni kwa namna gani angeweza kuwaambia wazazi hao kile kilichokuwa kikiendelea kwani kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, hawakuwa radhi kupokea taarifa kwamba watoto wao walikuwa wamefariki dunia.

    Wakaondoka katika korido ile, haraka sana madaktari wale waliokuwa wamebaki ndani ya chumba kile walipoona wameondoka, wakaanza kuitoa miili ile iliyokuwa kitandani na kuipeleka katika chumba kingine.

    Wakati Naseku na mumewe akipiga hatua, akajipekua, hakuwa na simu, alikuwa ameisahau pale alipokuwa amekaa kwani aliondoka kwa kushtukiza sana. Hakutaka kuendelea na safari ya kuelekea huko, akamwambia mumewe kwamba alisahau simu na hivyo kuirudia.

    Alipofika katika korido ile, macho yake yakatua katika kitanda kikubwa kilichokuwa kikitolewa katika chumba kilekile walichokuwa watoto wake huku kikiwa kimefunikwa na shuka kubwa la kijani.

    Moyo wa Naseku ukapiga paaa! Hakuamini alichokuwa akikiona, madaktari walipomuona, wakashikwa na hofu na kujua kwamba ile siri waliyokuwa wameitunza ilibumburuka. Haraka sana Naseku akaanza kupiga hatua za harakaharaka kuelekea kule wapokuwa wale madaktari, tayari akili yake ilimwambia kwamba wale walikuwa watoto wake, na kama walikuwa wamefunikwa shuka la kijani ilimaanisha kwamba walifariki dunia.

    Hata kabla hajafika, madaktari wakamzuia, hakutakiwa kuangalia kile kilichokuwa kimefunikwa, hapo ndipo akaanza kulia. Alilia kama mtoto, alipiga kelele kiasi kwamba watu wengine wakafika kuona nini kilikuwa kikiendelea. Alilia kwa ajili ya watoto wake, alilia kwa kuwa walikuwa watu muhimu sana katika maisha yake.

    “Walter...Walker...kwa nini mmekufa? Kwa nini mmetuacha...mbona hamkusema kama mtakufa...nitaishi vipi mimi....nitaishi vipi bila nyie wananngu?” alilia Naseku kama mtoto huku madaktari wakiwa wamemzuia pande zote, hakuchukua muda mrefu, akaanguka kama mzigo, akapoteza fahamu na hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo.

    ***

    Hali haikuweza kubadilika kwa Patricia, aliendelea kuwa vilevile kama alivyokuwa. Hakuweza kukumbuka kitu chochote kile, kila alipokuwa akitembelewa na watu alikuwa akiwashangaa, hakujua walikuwa wakina nani na wakati mwingine alijiuliza sababu ya kuwa hospitalini hapo lakini akakosa jibu.

    Wazazi wake waliendelea kuhuzunika, hakukuwa na kipindi kigumu walichokuwa wakipitia kama kipindi hicho. Hakukuwa na kilichobadilika, mbaya zaidi wakati wakiendelea kumsubiri binti yao arudiwe katika hali ya kawaida, wakasikia kwamba Walter na Walker walikuwa wamefariki dunia.

    Ilikuwa ni habari mbaya, ilikuwa ni zaidi ya kuchomwa na msumali wa moto mioyoni mwao, hawakuamini kile kilichokuwa kimetokea kwani mbali na pacha mmoja kutoka kimapenzi na binti yao, walikuwa wakiwapenda kupita kawaia.

    Dunia ikashtuka, hakukuwa na aliyeamini kwamba mapacha hao walikuwa wamefariki dunia, kila mtu alikuwa akilia, wengi wakaelekea hospitalini hapo na kuweka mashada ya maua na picha mbalimbali katika eneo ambalo waliruhusiwa kufanya hivyo.

    Hakukuwa na mtu aliyeamini kama wasingeweza kuwaona watu hao tena, vile vipaji vya kipekee walivyokuwanavyo wasingeweza kuviona au kusikia tena. Watu maarufu wakatuma salamu za rambirambi katika mitandao ya kijamii na wengine kwenda huko na kuwatia moyo wazazi wao waliokuwa watu wa kulia kila wakati, tena mpaka muda huo, Naseku alikuwa amepoteza fahamu zaidi ya mara nne, yote ilikuwa ni kwa sababu ya kuumizwa na msiba mzito aliokuwa ameupata.

    Baada ya siku mbili, mapacha hao wakapelekwa katika Kanisa la St. John lililokuwa haohapo New York na kuagwa sura ya mwisho kabla ya kupelekwa nchini Tanzania tayari kwa maziko.

    “Hivi ni kweli wamekufa?” aliuliza mwanamke mmoja, macho yake yalikuwa yamevimba huku mashavu yakiwa yamelowanishwa kwa machozi.

    “Yaani siamini! Kweli mapacha hawa wamekufa?” aliuliza mwanamke mwingine, naye hakuwa ameamini kile kilichokuwa kimetokea.

    Siku iliyofuatwa taratibu za kuwasafirisha mapacha hao zikafanyika na hivyo kupelekwa nchini Tanzania. Ndani ya ndege ilikuwa ni huzuni tele, kila wakati Naseku alipokuwa akiliona jeneza la watoto wake alikuwa akilia kwa uchungu, hakuwa akiamini kwamba mwisho wa kila kitu ungekuwa namna ile.

    Zaidi ya watu elfu kumi na tano walikuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwa ajili ya kuipokea miili hiyo. Watu wengi waliokuwa mahali hapo walikuwa na fulana zilizokuwa na picha za mapacha hao huku wengine wakiwa na maua kama njia mojawapo ya kuomboleza kwa kile kilichotokea.

    Ndege ilipotua, watu wakateremka, jeneza likashushwa, watu wakaanza kulia kwa sauti, kila mmoja alitaka kuligusa jeneza hilo ambalo lilipakizwa na kuanza kupelekwa katika uwanja wa taifa ambapo huko watu walitakiwa kuaga na kisha kuelekea kanisani, kufanyiwa ibada na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.

    Kila kitu kilichotakiwa kufanywa, kilifanywa na ilipofika majira ya saa kumi jioni, tayari msafara ukaanza kuelekea katika makaburi hayo na hivyo mapacha hao kuzikwa huko.

    Ilikuwa ni huzuni, mapacha waliokuwa wameipatia Tanzania umaarufu walifariki, kila mmoja alihuzunika, japokuwa walikuwa wameondoka lakini kwenye akaunti yao waliacha utajiri mkubwa ambao wazazi wao wakaamua kutumia asilimia kumi ya utajiri huo kwa ajili ya kuwasaidia watoto waliokuwa kwenye matatizo mbalimbali.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa msichana Patricia, aliendelea kuwa kwenye hali hiyohiyo kwa muda wa miaka mitano. Alikuwa akitibiwa kwa nguvu zote, pingili za mgongo wake ambazo ziliachia zikaanza kurudi na miaka miwili mbele, akafanikiwa kusimama na kuanza kutembea ila kumbukumbu zake hazikuweza kurudi tena.

    Ubongo wake ulikuwa kama umeathiriwa, hakujua kilichotokea, hakujua kama aliwahi kuwa na mwanaume aliyekuwa akimpenda kwa moyo wake wote. Wazazi walijitahidi kumpeleka katika hospitali mbalimbali lakini kote huko waliambiwa kwamba binti yao asingeweza kukumbuka kitu chochote mpaka kifo chake.

    Maisha yake yakaanza upya, akaanza kutengeneza urafiki na watu wengine, hata alipokuwa akiziona picha za Walter na Walker hakuwa akikumbuka kitu chochote kile, kwake, watu hao walionekana kuwa wageni kabisa ambao aliwaona mara kadhaa walipokuwa wakimfuata hospitalini kumuona.

    Naseku hakuwa na furaha, alikuwa mtu wa huzuni, kila alipokuwa akiziona picha za watoto wake, alikuwa akilia, machozi yalitiririka mashavuni mwake na kuyafuta kwa kutumia viganja vyake.

    Hakikubadilika kitu, kwa mtoto mmoja waliyekuwa naye, Esta, wakaendelea kumlea na baada ya miaka minne, akaolewa na kufanikiwa kujifungua watoto mapacha wa kiume ambao kwa kuwaenzi ndugu zake, akaamua kuwaita Walter na Walker.



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog