Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

UPENDO WANGU - 3

 







    Simulizi : Upendo Wangu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ikiwa yohana ametumwa kumfuata semeni lakini pia alipewa onyo na mzee rashidi, kuficha suala la ndoa kama mzee Rashidi alivyomtaka asisema yohana nae hakuwaambia,si mgalu wala mama semeni hakika hawakujua mpango uliopangwa kuhusu mtoto wao kuolewa.Walipo maliza maongezi dada na kaka yake mgalu (mjumbe) walitoka ili kumpa tamko la mwisho Yohana.

    Walipomaliza maongezi Walitoka nje walimkuta msichana kakaa kwenye kiti cha mgeni na mgeni kasimama, wakati wamepigwa bumbuazi Yohana alidakia kumtaalifu mama mwenye nyumba kama Yule msichana alikuwa mgeni kaja kwake, kwa iyo amsikilize shida yake Mama Semeni amsikilize

    huyo ndio mgeni? ‘’ndio sababu iliyokufanya ukampa kiti,tulichokupa ukae"mara punde tu wote wakacheka,muda huo huo, mgalu aliaga nakumkabidhi yona kwa mama semeni akamwacha Yohana akishangaa walikuwa anacheka, akaamua kusimamisha ucheshi unaenda pale na kumpa maelezo Yohana kwa kumtaka Semeni aje karibu kwa kuwa t alisimama karibu na Yohana ‘’huyu ndiye Semeni uliyeambiwa,alikuwa katoka tu na safari zake ndio analudi’’Yohana alichoka kwa kustaajabu na kutoa tabasamu la kinafki kwani kama Semeni atasema yaliyotokea kabla ya hawajajuana itakuwa aibu kwake na kuonekana kijana. baada ya utambulisho mama alimwita Semeni wakaongee ndani.

    Hawakuchukua muda mrefu walitoka na kutoa jibu kwani haikuwa shida mama yake kumwambia mtoto haende kwa baba yake , Semeni hana tatizo na baba yake ,Semeni anampenda baba yake ila kule kugumu sababu ya mama wa kufikia. Yohana alipewa jibu ili kumchukua semeni,alimtaka aje amchukue baada ya wiki au atakuja mwenyewe semeni, Yohana hakusita ila alitaka kumtaalifu mzee mwenyewe Rashidi. baada ya yohana kuongea na mzee Rshidi kwa upande Wa pili mzee rashid alimtaka Yohana ampe simu Semeni ili aongee NSW aliponaliza, akiwaambia mjumbe na mama Semeni mzee Rashidi amekubari nimsubili hapo mpaka hiyo wiki moja ipite ndio wataondoka pamoja mama semeni na kaka yake walikubaliana,halikuwa tatizo ila mahali pa kulala mgeni ndio tatizo,mgalu alikataa kwake sababu ana chumba kimoja.Nao waikuwa wanalala kila mtu na chumba chake ila walikuwa na sebule moja tu wakakubaliana mgeni alale kwenye kochi sebuleni,Mjumbe aliondoka na kuludi kwake na kumtakia siku njema kila mmoja.

    Usiku ulipofika baada ya kula chakula cha jioni Semeni alimwonesha Yohana pa kulala,Ilikuwa usiku mrefu sana kwa Yohana kwani hakuwa na mazoea ya kulala kwenye makochi kama yale pia na mbu ndio tatizo kubwa sana iliyofanya atafute usingizi kwa tabu sana kwani alishindwa kulala,Asubuhi kulipokucha Yohana alichelewa kuamka na alipoamka alimkuta Semeni anamwangalia huku amesimama,Baada ya kujiana hali Yohana alimuuliza kwanini unaniangalia hivyo Semeni alijibu hajawai kuona mwanaume anaependa kulala kama yeye halikuwa jibu zuri kwa Yohana ilimbidi kunyamaza tu,Semeni alimwambia Yohana kama mama yake ameshatoka kwenda shamba na yeye anakwenda kukamua maziwa ya ng’ombe kwa ajili ya chai

    Yohana akutaka kuwa nyuma akaomba kama anaweza kumsaidia ili waende wote sababu atakuwa peke yake sebuleni hapo.Semeni alimkubalia na wakaenda wote zizini, walipofika Semeni aliingia kwenye zizi na kukamua ng’ombe aliyekuwa tayari ametayalishwa kwa kukamuliwa na mtayalishaji wa ng’ombe hao ambaye ni kibarua tu.Yohana alimwona ng’ombe mwengine alietayalishwa na kumwambia Semeni amruhusu aende kukamua maziwa Semeni alimuuliza kama ataweza alipojibu ndio Semeni akamruhusu.Mpaka Semeni anamaliza ng’ombe watatu Yohana alikuwa na mmoja na mwili mzima ulikuwa umejaa Kinyesi cha ng’ombe,Semeni alipomuona Yohana akamcheka na kumtaka warudi ndani mara moja akakoge na kubadilisha nguo.Wakati yohana anakoga na kubadilisha nguo tayari na mama Semeni karudi kutoka shamba.

    Ulipofika wa kuandaa chakula cha mchana mama Semeni alimtaka Semeni akakamate kuku kwa ajili ya chakula cha mchana,kabla Semeni ajajibu chochote Yohana nae alitaka kwenda kumsaidia,Wakaenda wote hadi kwenye mabanda ya kuku Yohana alipoona Semeni anasumbuka kukunja kanga ili aingie kukamata kuku aliomba yeye aingie na aambiwe yupi anatakiwa kukamatwa alipoingia ilimchua muda wa dakika 45 bila ya kumpata kuku Mama Semeni alikuja na kumkuta Semeni anamcheka Yohana jinsi anavyokamata kuku kwa mbwembe na baada ya kukamata kuku ambaye siye anayetakiwa mama Semeni alimwambia huyo huyo anatosha sababu alimwonea huruma jinsi alivyokuwa anakimbia hovyo kumkamata kuku yule ,Yohana alisimama huku mwili wake ukiwa na mavumbi na Semeni alikuwa hana mbavu kwa kumcheka Yohana.

    Siku ya pili Yohana aliwai kuamka ili kupinga na kauli ya Semeni kwamba mwanaume uwai kuamka,siku hiyo aliwai kweli kuamka,Mama Semeni alipoamka alimkuta Yohana yupo nje ameshaamka alishangaa na kish kuuliza

    "mbona mapema baba"?CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hamna mama,napenda kamka mapema tu"yohana akamjibu

    "Sawa basi pumzika"! Mama semeni alimwambia,

    Yohana akutaka mama Semeni ajue sababu ya kuamka mapema,akajibu nataka nikapajue shamba na nikusaidie kulima kidogo,Mama Semeni alicheka na kumtaka aendelee kupumzika tu.ila Yohana alikazia kwenda,mama semeni hakuwa na pingamizi alimkubalia wakaenda shambani pamoja walipofika mama alimkabidhi jembe na kumfundisha jinsi ya kulima yohana alijalibu hatimaye akaweza kulima. Mama semeni na yohana Walipomaliza kulima Waliludi na kumkuta Semeni ameshaandaa chai walikunywa na kupumzika .Ilifika mchana aliitajika kuku tena kwa chakula cha mchana na Yohana alijitolea kwenda kumchukua bandani haikuwa kazi ngumu kwa siku hiyo, kwani alipata maelekezo kutoka kwa mama Semeni jinsi ya kumkamata kuku yule.

    Siku zilisogea huku Yohana akiwa na ukalibu na kila mtu pale nyumbani pia alikuwa msaada mkubwa pale nyumbani kwa mama semeni,Mama Semeni alimpenda Yohana kutokana na ukalimu, ucheshi kwa jumla na tabia yake, Semeni alimpenda pia kwani alishaanza kumweka moyoni Yohana japokuwa hakujionesha.

    Hatimaye Siku ya kuondoka ilifika Yohana na Semeni walifunga mizigo yao kwa ajiri ya safari ya kuja kwa mzee Rashidi ,kabla ya kuondoka,Mama Semeni alimtaka Yohana waongee pembeni kwani kuna kitu alitaka kumwambia,yohana alikubali kisha wakasogea pembeni Mama Semeni alianza

    ‘’Yohana samahani kukabidhi majukumu au mzigo usioutarajia

    ’' hapana mama bila samahani "yohana alijibu

    "Najua Semeni anaenda kwa baba yake, ila mimi namkabidhi kwako umlinde na umwangalie, furaha yake ndio mboni yangu na moyo wangu pia mama semeni aliendelea kumwambia

    ’’usijali mama nitayafanyia kazi maneno yako"

    " usichukulie kiraisi hivyo, kwani namjua mzee Rashidi kutakuwa na kitu si bule,hawezi kumwita Semeni namna hii,lolote litakalo tokea mwanangu Semeni akilizika nalo sitakuwa na dosali nalo ila likienda kombo wewe ndiye msahada kwake,ndio maana nakukabidhi mwanangu" mama semeni alimsihi yohana .

    Yohana alikuwa kwenye wakati mgumu kukubaliana na hilo ila akuwa na la kufanya aliamua kukubali "sawa mama nimekuelewa ‘

    " nataka uwe mkwe wangu ’’mama semeni aliendelea kumwambia,

    "una maana gani mama,sijaelewa? Yohana alimuliza mama semeni huku akiwa ametoa macho pima.

    ‘’usijali mwanangu,nendeni mtachelewa usafiri’’

    "Sawa ! Yohana alimjibu huku akiwa na maswali kibao kichwani mwake,akitafakari kwa maneno yale.

    Saa nne asubuhi Yohana na Semeni walianza safari, kuelekea nyumbani kwa mzee Rashidi, njiani nzima ukimya uliwatawala, Yohana alimuogopa mtoto wa bosi wake, upande wa Semeni yeye hakutaka kuonekana mwenye maneno mengi kwa Yohana .........

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Baada ya safari ndefu,iliyochukua takribani Masaa kumi na mbili,hatimaye walipofika jijini arusha.yohana na semeni waliposhika tu kutoka kwenye basi kituoni pale,walimkuta Mzee Rashidi anawasubili ilikuwa furaha kwa Semeni kumuona baba yake,kwani muda mrefu ulipita bila kuonana,mzee rashidi alimkumbatia na kumbusu mwanae mashavuni.

    Mzee rashid hakutaka kupoteza muda walipanda gari kuelekea nyumbani,nyumbani kulikuwa kama kustukizwa kufika kwa Semeni kwani hamna mtu aliyejua zaidi za Mzee na Yohana.ilikuwa ngumu kwa mama Amina kukubali ujio wa Semeni lakini hakuwa na namna,Yohana aliakikisha kila kitu cha Semeni kipo salama na yupo kwenye furaha.Yohana alianza kuaga ili aende kupumzika nyumbani kwake,Mzee Rashidi alikubaliana na yohana na kumwambia watakutana kesho kwa maongezi zaidi.

    Semeni alimwomba baba yake amsindikize Yohana hadi nje ya nyumba,Mzee alikubali ila Yohana aliona wazi kuwa alikubali kwa shingo upande.Semeni na Yohana waliongozana hadi nje ya nyumba, huku Semeni akimtaka Yohana awe anakuja kumsalimia mara kwa mara na kumshukuru kwa upendo aloufanya kwake na familia yake akiwa kule kijijini, Yohana alimshukuru na kukumbatiana Kipindi chote Semeni na Yohana wanaongea Mzee Rashidi alikuwa anawachungulia kupitia dirishani,semeni na yohana waliagana na kisha yohana akaondoka.

    Semeni aliporudi ndani,alimkuta baba yake amebadilika si kama mara ya kwanza alivyomuacha alipotoka na yohana.

    Siku iliyofuata Yohana aliamkia kazini, kutokana na mrundikano wa kazi siku hiyo hakutokea kabisa kwa mzee Rashidi,huku nyumbani kwa mzee Rashidi Semeni alimwuliza sana baba yake, Yohana kwanini siku hiyo hakuonekana nyumbani hapo,lakini baba yake hakumpa jibu la uhakika. Mzee Rashidi hakutaka kumwambia mapema mwanae kitu alichomwita pale.

    Siku iliyofua,asubuhi na mapema Mzee Rashidi aliaga nyumbani, akidai kuna mtu anaenda kuongea nae ila hakumtaja jina huyo mtu ,alitoka na kuelekea moja kwa moja hadi ofisini kwake kuongea na Yohana ,alipofika alimkuta Yohana anamalizia kazi zake.Mzee Rashidi hakusita kuanza maongezi hapo hapo ofisini, alimwuliza kwa kumtega

    "safari yako ilikuwaje na uliishi vipi na akina Semeni?"

    "haikuwa ngumu kufika kwani nilifuata maelezo yote uliyonipa na pia tuliishi kwa amani na upendo kwa muda huo mfupi"

    "Nakusifu sana, umefanya vizuri ila nataka kujua kitu kimoja, una mahusiano yoyote yanayoendelea kati yako na semeni" mzee rashidi aliuliza

    " hapana" yohana alijibu

    "Niambie ukweli,jana nimekuona mlivyo agana wakati anaondoka",Yohana alishtuka kisha akamjibu

    "Sina mahusino yoyote,Semeni ni kama dada yangu na siwezi fanya kitu kama hicho",

    Japo kwa kauli hiyo Mzee Rashidi hakulizika na kumtaka yohana akae mbali na mwanae kwani atamfanyia kitu kibaya hatoweza kukisahau katika maisha yake,Yohana alikubali huku akiwa na mshangao kwani haikuwai kutokea hata siku moja mzee huyo kuongea nae akiwa kwenye hari ya hasira kama hile.

    Mzee rashidi alimuaga yohana kisha akaondoka,huku akimtaka aje nyumbani Semeni anamulizia na kumsisitiza ayaeke akilini maneno aliyomwambia Yohana alikubali na kuakikishia atayafanyia kazi pia atakuja ili ajue nini Semeni anachmulizia.

    Baada ya muda Mzee alifika nyumbani kwa na kumwambia mwanae Semeni kwamba Yohana hatoweza kuja leo kwani àna kazi nyingi, atakuwa anamalizia ila kwa leo atakuja kwa chakula cha usiku,semeni alifurahi kusikia vile kwani, taarifa ile ilikuwa faraja kwake, alionyesha furaha ya wazi kwa baba yake,hata baba yake aliduwaa ila alishindwa kumuliza mwanae kilichomfurahisha.

    Siku iliyofuata majira jioni,semeni alivaa gauni lefu rangi ya bluu,hakika alipendeza na kuvutia,hata baba yake alipomwona alimuuliza kisa cha kupendeza usiku ule lakini semeni alimjibu kua hakuna sababu yoyote ila ameamua kufanya hivyo. Ilipotimia saa mbili za usiku, yohana alifika nyumbani kwa mzee rashidi,alikalibishwa na kuketi sambamba mzee rashidi. Yohana akiwa kwenye maongezi na bosi wake gafla semeni alifika pale sebleni akitokea chumbani kwake,yohana alipomuona moyo wake ukapiga paa!huku akijikuta akimshangaa semeni alivyokua amependa kwani hakuwai kumiona semeni katika mpendezo hule,alijikuta moyo wake ukienda mbio mithili ya mtu aliyekimbizwa na simba polini,hisia nazo zikaanza kumpanda yohana akajikuta anamtamani semeni,yohana alikuwa mbali kimawazo aligutushwa na sauti ya mzee rashidi akimwambia mwanae

    "Umependeza leo semeni"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ahsante baba angu!"semeni alijibu

    Semeni hapo hapo akauliza

    " heti kaka yohana,unaonaje nawe?"

    Yohana yeye alikua kwenye amaki,aliposikia swali lile kutoka kwa semeni,alimwangalia mzee rashidi kisha akamjibu semeni

    "Kweli wewe ni mrembo na kupendeza ni kawaida yako,ila kwa usiku huu umependeza sana"wote kwa pamoja walicheka na kisha semeni alienda kukaa kwenye kochi alikokaa yohana,baba yake itarajia mwanae ataenda kukaa kochi alilokalia yeye lakini haikuwa hivyo.

    Semeni alianza kumuongelesha na kumuuliza maswali, ulikuwa mtihani mkubwa kwa yohana,alijua wazi baba mtu hapendezwi ukaribu wao,ila kwa wakati huo hakuwa na jinsi.

    Muda wa chakula ulipofika wote walielekea mezani,yohana akajaribu kumkwepa semeni lakini ilishindikana semeni alikaa karibu nae yohana alikuwa na wakati mgumu sana.

    Wakati wakiwa wanakula mzee rashidi alimwambia mwanae kesho ana mazungumzo nae muhimu,wataongea wakiwa wawili,semeni alikubali.walipomaliza kula yohana hakutaka kubaki nyumbani pale kwani hali ilikuwa mbaya kwake sababu ya semeni.baada muda yohana aliaga na mzee rashidi alimsindikiza ila semeni alimtaka baba yake apumzike yeye amsindikize,mzee rashidi alikubali kwa shingo upande . yohana na semeni walitoka mpaka nje kisha semeni akamuuliza

    " mbona upo hivyo yohana una nini leo ?

    " hapana sina tatizo ,nipo sawa!" Yohana alimjibu

    "Mbona naona sivyo nilivyokuzoea? Semeni alimuuliza

    "Uchovu tu wazi nyingi za offisi!

    "Pole sana yohan"semeni alimwambia

    "Naomba niende nikapumzike,najiisi vibaya"yohana alimwambia

    "Sawa tutaonana kesho"

    Wakati wanaagana semeni alitaka kumkumbatia lakini yohana akakwepa na kumnyooshea mkono kwa ishara ya kuagana .kitendo kile kilimchanganya semeni akaisi kuna kitu kinaendelea kwani sio kawaida yohana kukataa kumkumbatia,muda wote huo mzee rashidi aliwachungulia ili ajue nini kinaendelea.

    Siku iliyofuata mzee rashidi alimchukua mwanae wakaenda kutembea mbali kidogo na nyumbani,walipofika uko mzee rashidi alianzisha mazungumzo,akaamua kumwambia alichomuitia na kilichomfanya amtoe kwa mama yake kumleta pale.habari ile haikuwa nzuri kwa semeni,kwanza hakujua nani mhusika na pia hakupenda kuingia kwenye mahusiano na mtu hasiyemjua,mzee rashidi alikuwa na kazi ya ziada kumbembeza mwanae akubali,kwani hana jinsi washaafikiana na rafiki yake,semeni alihoji kuhusu huyo mhusika ila majibu yaliyotoka kwa baba yake yalionekana yana manufaa yao binafsi kwa biashara zao.

    Mwishowe semeni hakukubaliana na hilo na kumuomba baba yake amrudishe nyumbani,baba yake alimtaka awe na muda wa kufikiri ili aweze kupata jibu sahihi,semeni aliitikia tu ili kumlidhisha baba yake.

    Mzee rashidi hakuwa na jinsi aliamua kumrudisha mwanae nyumbani,baada ya mwendo mrefu uliochukua kama saa nzima wakiwa njiani,hatimaye kuwasili nyumbani....................

    ..

    Baada ya kushuka tu kutoka kwenye gari na baba yake,semeni alienda moja kwa moja mpaka chumbani kwao,alimkuta mdogo wake amina amelala,alimwamsha kisha akamwambia

    " naomba unijulishe yohana anaishi wapi?

    "Naweza nikampigia simu ili muongee!

    "Hapana yohana hawezi kukubali labda uongee nae wewe!"semeni alimwambia mdogo wake

    " sawa ngoja nimpigie niongee nae kisha ntakupa jibu

    Amina alichukua simu yake kisha akampigia yohana,kisha simu upande Wa pili ilisikika

    " hallowCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hallow bro yona mzima? Amina alisikika

    " safi kabisa sister,nambie" yohana alimjibu

    " salama, sasa yona naitaji kuonana na wewe ,nina maongezi muhimu sana "

    " mmmh amina ishu gani tena sister? Yohana aliuliza kwa mashaka

    "Ni ishu ya kawaida yohana "

    "Poa basi tukutane club maisha pale saa mbili hivi nitakuwa nishamaliza ishu zangu nitaonganisha kufika hapo"yohana alimwambia amina

    " Sawa basi,poa! Amina alijibu kisha akakata simu.

    Amina alipomaliza kuongea na simu alimgeukia dada yake kisha akamwambi jinsi alikubaliana kukutana na yohana,kisha akamtaka wajiandae kwa safari hiyo.

    Saa mbili na dakika kumi,semeni na amina waliwasiri club maisha walipokubiana kukutana na yohana,walitafuta sehemu iliyotulia kisha wakakaa Mara muda huo huo yohana nae alifika pale,alistuka kumkuta na semeni eneo lile,yohana akutaka kujionesha alijikaza na kuwafuta walipokuwa wamekaa amina na ndugu yake.

    Baada ya kusalimiana,amina akaanzisha mazungumzo

    "Kaka yohana,samahani sana kwa kukusumbua!"

    "Wala hakuna shida sister,nakusikiliza" yohana alijibu

    "Mimi binafsi sina tatizo ila dada semeni ndio mwenye shida na wewe!"amina alimwambia

    "Sawa" yohana alijibu kwa mkato

    "Sasa mimi natoka kidogo,niwaache muongee"amina alisema kisha alinyanyuka na kukaa mbali kidogo na walipokaa wao.

    Yohana alimwangalia semeni Kisha akamwambia

    "Haya Bi .semeni niambie kuna tatizo gani limekupata?"

    "Hakuna tatizo ila nataka kujua ukweli kuhusu baba kuniitaji?semeni alimuuliza yohana

    "Mimi sifahamu chochote,kwani Luna nini?yohana alijifanya hajui

    "Baba anataka niolewe na manase,mtoto wa rafiki yake,na ameniambia kwamba wewe pia unajua ila ukutaka kusema ukweli ulipokuja nyumbani!"semeni alimwambia yohana

    "Hapana mi nilikua sifahamu,ndio kwanza nasikia kwako!"

    "Siniongopee! Embu niambie ulikua hujui au unajua? Semeni alimuuliza

    "Sawa nafahamu" yohana alimjibu huku akiinamisha kichwa chake chini kwa aibu,

    Semeni alibadilika gafla kisha akaendelea kumuuliza

    "Kwa nini nilipokuuliza kabla sijakwambia ukweli,ulikataa?

    "Ni amri ya bosi semeni ndio iliyonifanya nisiseme kwa wakati ule!" Yohana alijitetea

    "Unajua kwanini nilikiwa mwepesi kukubari kuja huku?"

    "Samahani semeni!"

    "Unajua kiasi gani moyo wangu umeutia kidonda"semeni alimwambia yohana huku machozi yakimtoka machoni mwake,kweli alikuwa ameumia kiasi gani moyo wake umeingia kidonda alilia kwa uchungu,yohana alimwonea huruma akamsogelea na kumbembeleza,semeni hakutaka kumbembelezwa kwa wakati huo,kwa hasira akanyanyuka kitini na kutaka kuondoka.kabla semeni hajaiga hatua tatu mbele aligeuka nyuma na kumuangalia yohana aliyekua amekaa pale kitini akimuangalia yeye kisha akamwambia CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Umenikatisha furaha ya maisha yangu,siwezi kuolewa na mtu nisiyekuwa na mapenzi nae,nakulaumu sana wewe ni mmoja wapo uliyesababisha yote haya"semeni alisema uku akiondoka eneo lile. Amina alimuona dada yake akiondoka huku akili,alimfuata kisha semeni akamtaka waondoke eneo lile,amini akutaka kumsikiza Dada yake kwa wakati huo ,akaanza kumbembeleza na kumtaka amueleze kilichotokea mpaka akawa katika hali ile,semeni hakusita akamueleza yote yaliyokea,alimueleza mpaka hisia zake kwa yohana tangu alipokwenda kijijini kwao mpaka walipo sasa,semeni hakumfucha kitu mdogo wake.amina alimpa pole Dada yake kumwahidi atashirikiana nae kwa maamuzi yoyote atakayochukua pia atatoa msaada pale utakapoitajika,semeni alifurahi sana kusikia hivyo,akamshukuru mdogo wake kisha wakakumbatiana kwa furaha.

    Siku mbili baadae,mzee rashidi alimtaka mwanae ampe jibu,semeni hakusita kutoa jibu,alimwambia baba yake kauli ile ile, hatoweza kuolewa na manase,haikuwa taarifa nzuri kwa baba yake,hakutaka kukubaliana na mwanae hata kidogo,mzee Rashidi alimng'ang'aniza semeni bila mafanikio.

    Baada ya kuona semeni kashikilia msimamo wake,mzee rashidi akamwambia mwanae " utake usitake ndoa ipo pale pale lazima uolewe na manese".mzee rashidi alitoka pale sebleni na kumuache semeni akilia kwa uchungu ,hakujua cha kufanya kwa wakati huo. Amina kwa wakati huo alikuw ndani,alipotoka alimkuta dada yake Analia pale sebuleni alimchukua na kumpeleka chumbani kwao,kisha kumtaka anyamaze

    "Nyamaza dada,usilie unatakiwa usubili,siku ya kukutana na mhusika mwenyewe!"

    "Lakini mdogo wangu,mimi nampenda yohana pekee si mwingine!semeni alisema

    "Sawa dada,lakini sibiri ukiongea nae manase anaweza kukuelewa!" Amina alimueleza dada yake.

    " sawa nimekuelewa amina"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog