Simulizi : Upendo Wangu
Sehemu Ya Nne (4)
Amina alifanikiwa kumtuliza dada yake kisha walikubaliana kusubili wahusika watakapokuja waeleze ukweli kwamba semeni hakuwa tayari kuolew na manase.
Ilikuwa siku ya alhamisi,majira ya saa 12:30 mchana,ni siku ambayo wageni walifika nyumbani kwa mzee rashidi, kwa ajiri ya kutambulishwa kisha kupanga siku ya kuja kuoa.muda ulivyozidi kwenda ndio wageni mbalimbali walivyozidi kuongezeka,wageni wake kwa waume walipendeza na kua na furaha wakiongea maongezi ya hapa na pale wengine wakiendelea kucheza musiki uliokuwa unasikika pale sebuleni.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Semeni na mdogo wake walikuwa wapo chumbani,Amina alimtaka dada yake kuwa na furaha.muda ulifika bi harusi mtakajiwa kutoka ili kutambulishwa kwa wageni waalikwa.baada ya muda mchache semeni alitoka chumbani mwao akija na amina walifika sebuleni kujumuika na wageni ,mzee rashid alipomuona mwanae akiwa na furaha,aliachia tabasamu kisha akaanza kuwatambulisha wageni waalikwa,kisha alimgeukia mwanae na kumtambulisha kijana mhuoaji,semeni aliachia tabasamu mwanana akamuacha hoi kijana manase,huku akionesha uchangamfu kwa kijana yule bila kujua yaliyopo moyoni mwake.semeni aliwapa mikono wageni,upande wa mhuoaji akiwepo baba Wa mhuoaji mzee mubaraka,semeni muda wote alionesha furaha hakutaka kumuabisha baba yake mbele ya wageni wale.manase alijisifu kupata mke kama semeni na waliongea na kuahidiana mambo mengi bila manase kujua kinachoendelea kati ya mzee rashidi na mwanae. Wakati shughuli ikiendelea semeni na manase walikuwa wakiongea mambo mbalimbali
" semeni wewe ni msichana mzuri sana"manase alisema
"Asante nashukuru,ata mimi nimekupanda kijana mtanashati kama wewe"semeni alimjibu
"Nimefurahi sana kisikia hivyo,
"Nashukuru pia"semeni alisema ila ukweli ulibaki ndani ya moyo wake,hakumpenda hata kidogo kijana hiyo,ila hakutaka kumualibia baba yake,muda wote semeni aliendelea kujitengenezea tabasamu feki huku moyoni mwake akijiraumu kukubali kuwa karibu na manese.
Wageni waliendelea kuburudika na kupata vinywaji vya kila aina,ilikuwa sherehe ya aina yake. Hatimaye muda Wa chakula ulipofika,wageni wakiwa foleni kuchukua chakula,yohana nae alifika nyumbani hapo,akawa anasalimiana na wageni semeni alipomuona yohana furaha yake yote ikayeyuka,akajikuta mapigo ya moyo wake yakienda kasi,nguvu zikimuishi,akajikuta anakaa kiti kilicho karibu yake,amina alipomuona dada yake yupo kwenye hali hiyo akamfuata kisha akamwambia
"Vipi dada?"
" nipo vizuri tu" semeni alimjibu
"Kweli,nakuona kama haupo sawa?amina aliendelea kumdadisi
"Hapana!"
"Changamka dada,watu wote hapa wanakuangalia wewe!"
Semeni alikubali kwa kutingisha kichwa kuonesha kukubaliana na hilo,alijikaza kisha akanyanyuka na kujumuika na wegeni.
Baada ya wageni kumaliza kula, waliaga na kuondoka,wakiwa ndio wanatoka semeni alimshika mkono manase kisha alimbusu mashavuni mwake,manase alifurahi ila kwa yohana ilikuwa sivyo ulikuwa mwiba kwa uliochoma ndani ya moyo wake,kinywaji kilimpalia na kisha kukohoa mfululizo,amina alipoona hivyo alimfuata yohana kisha akamvutia pembeni na kumuliza
"Yohana! Uko sawa kweli?"
" hamna nipo sawa mbona!"yohana alimjibu huku akiwa anakooa kwa fujo
" unampenda kweli dada yangu ?"
Yohana hakumjibu amina,badala yake alimuaga na kutoka,alipofika nje alimkuta semeni na manase wakiwa wamekumbatiana,yohana hakutaka kubaki pale tena kwani alishaingiwa nakinyongo,moyo wake uliumia kupita kiasi.baadae wageni wote wakaondoka,mzee rashidi na semeni nao wakaingia ndani, kisha mazee rashidi alimpongeza semeni na kumwambia jinsi alivyovutiwa na muonekano wake kwa wagen.....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Semeni hakutaka kuzungumza sana na baba yake,aliamua kumuaga Kisha akaingia chumbani mwao,alimkuta amina akimsubili kwa hamu,amina alianza kumuuliza dada yake
" vipi ,unamuonaje manase,upo tayari kuolewa nae?
"Msema kweli ni mpenzi wa mungu,kijana Wa watu mzuri,anavutia" semeni alijibu
"Kwa hiyo upo tayari,kuwa mkewe?
"Hapana sipo tayari,moyo wangu umempenda yohana"
Amina alijifikilia kumwambia dada yake ila aliona atamchanganya,akaamua kunyamaza,kisha semeni akaendelea
"Sitaki kuwa tofauti na baba,sina budi kuondoka hapa ikishindikana nitajiua kwani mapenzi yangu ypte yapo kwa yohana"semeni aliendelea
"Hapana dada usifanye hivyo" amina alimsii dada yake
"Naona thamani yangu kwa baba imeisha"
Amina alijifikilia akaona anaweza kumpoteza dada yake,aliona vema amwambie kilichotokea kwa yohana,wakati yeye alipowasindikiza wageni,yohana aliondoka huku akiwa na uchungu moyo mwake kwa kitendo alichofanya,semeni akafurahi kusikia hivyo moja kwa moja akajua kumbe yohana nae anampenda,akajipa moyo ipo siku watakuwa pamoja.
Siku iliyofuata amina alikwenda ofisini kwa yohana,alimkuta yohana akiwa na kazi nyingi,alimuomba waongee,yohana hakuwa na jinsi alimsikiliza amina.
"Jana nilikuuliza kama unampenda semeni,lakini ukunijibu?"
"Sasa unataka nikujibu vipi?yohana aliamaki
"Niambie tu kama unampenda dada yangu?"
" semeni ni dada yangu,kama ilivyo kwako sina sina nia nyingine kwake!" Yohana alijibu
"Naomba uniambie ukweli yohana,maana dada yangu anakupenda sana" amini alizidi kumkandamiza yohana
"Kuna kitu moyoni mwako,ila unaficha kumwambia semeni kwa sababu unamuogopa mzee!"
"Nilikuwa najisikia vibaya tu sikua na tatizo lolote"yohana alijitetea
"Sawa,nimekuja hapa kwa ajiri ya kukusaidia kama unaitaji kuwa na dada yangu!"amina alimwambia
Maneno ya amina yalimwingia Pima yohana yalienda sawa sawa na kuchoma ndani ya moyo wake,kisha alimtaka amsikilize,
"Naomba unisikilize kwa makini!" Yohana alisema
" sawa nipo kwa ajiri yako!" Amina alimjibu
"Mafanikio yangu yametokana na mzee,ninamuheshimu kama baba yangu na sipo tayari kumkosea"yohana alimwambia
"Sawa nakuelewa,lakini vipi kuhusu Dada?"
"Kiukweli moyo wangu upo kwenye mateso makubwa sana kumkosa semeni"yohana alisema
"Sasa yohana wewe ni mwanaume,maamuzi ni yako"
Amina alimshika bega yohana kisha akaendelea kumwambia
" najua una mapenzi ya dhati kwa semeni,pambana,jipiganie semeni awe wako,usimogope mzee!"
"Nimekuelewa amina,tangu siku ya kwanza kukutana na semeni moyo wangu ulikufa juu yake,nampenda sana semeni"yohana alisema
Amina alifurahi kusikia hivyo,aliachia tabasamu pana lililopendezesha sura yake,yohana alimtaka amina wasichukue maamuzi magumu,amina alimuakikishia hakuna baya litakalotokea kisha waliagana na amina akaondoka kuelekea nyumbani huku akiwa na furaha.
Alipofika nyumbani alimkuta semeni akimsubiri kwa hamu,alipofika tu amina akamsimulia kila kitu dada yake,semeni alifurahi sana kwa taarifa ile,akamuambia mdogo wake lazima aondoke siku inayofuata atajua yeye pa kwenda na si kubaki pale nyumbani,amina alijifikilia kisha akamuambia dada yakeCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mimi nimepata wazo"
"Wazo gani mdogo wangu,nisaidie" semeni alimwambia
"Kesho nitaanza kupeleka baadhi ya nguo zako kwa shoga angu"amina alisema
"Wazo zuri mdogo wangu,alafu inakuwaje?"semeni aliuliza
"Nitakutorosha na nitaongea na yohana tutapanga pa kufikia"
" mmh! Sawa mie sina neno"semeni alimjibu mdogo wake.
Amina na semeni walielewana kisha kila mmoja akaendelea na shughuli zake.
Siku iliyofuata walisubiri mpaka baba yao alipotoka kisha amina akajiandaa na kutoka,alifika kwenye kolido alikutana na mama yake,akamsalimia kisha akamuaga anakwenda kwa rafiki yake jane,mama yake hakuwa na mashaka nae alimruhusu kisha wakaagana amina akaondoka.
Jeni rafiki yake amina,walisoma pamoja shule ya sekondari,Jeni na amina walipenda sana kupelekea urafiki wao ukawa mkubwa,walisaidiana kwenye shida na raha ata wazazi wao pia walifahamiana kutokana na ukaribu huo amina na jane walishibana kwa kila kitu.
Baada ya mwendo mrefu,alitumia kama nusu saa amina alifika nyumbani kwa kina jeni,alibisha hodi mama jeni alitoka na kumfungulia mlango amina akaingia ndani,Jeni alipomuona amina alimpokea mzigo wake kisha akamkaribisha chumbani kwake,amina alikaa kitandani kisha waanza mazungumzo.
"Jeni,kama nilivyokwambia kuhusu ile ishu yetu"amina alimwambia Jeni
" sawa nimekuelewa,shoga angu usiwe na wasi nitampokea bila kinyongo dada yako"Jeni alimjibu
"Semeni nitakapomtoa nyumbani nitamleta hapa"amina alimwambia
"Sawa nimekuelewa,atakuja saa ngapi?
Leo usiku nadhani tutafanikisha ilo,si unajua zimebaki siku tatu tu wafunge ndoa!"amina alisema
" daaa!,kumbe siku zimefika ?"
"Umeona hee!siku zimeisha shoga,amina alimjibu Shoga ake.
Amina na jeni walikubaliana mipango yao ya kumsafirisha semeni ili hasiolewe na manase bila kupenda,walikua tayari kwa lolote kumsaidia semeni bila kumshirikisha yohana,baada ya muda amina aliaga na kuondoka.
Alipofika alimtaka dada yake ajiandae kesho itakapofika usiku safari itaanza,semeni alikuwa muoga alimkubalia ndugu yake bila kujua atakapotoka kwa jane atakwenda wapi.siku hiyo semeni hakulala alitafakari jinsi safari yake ya kutoroshwa na ndugu yake itakavyokua,aliutafuta usingizi bila mafanikio alipiga moyo konde lazima aondoke mikononi mwa baba yake mpenda pesa bila utu.
Siku ya pili ilipofika semeni akajiandaa kwa safari ya kutoroka bila mama yake wala baba yake kujua mpango walioupanga watoto wao.hatimaye masaa yakapita na jua likazama kuashiria usiku umeingia,semeni akiwa tayari kwa safari ya kutoroka ,amina nae akaanza kuzunguka huku na kule kujua usalama Wa kutoka ndani ya nyumba ile.
Ilipoitimu saa saba usiku,watu wakiwa wamelala,amina alinyata mpaka usawa wa mlango wa kuingilia chumbani kwa wazazi wake,akatega sikio lake akasikia wakikoroma kuashiria wameshalala,nae akarudi chumbani kwao fasta na kukuta simu yake ina message aliichukua na kusoma akakuta ujumbe kutoka kwa Jeni ukisomeka hivi "sisi tupo nje tunawasubiri!"amina akamshtua fasta semeni na kumtaka watoke safari imeanza,wakati semeni akiwa amesimama tayari kwa safari,amina alichukua mito na nguo akafunika kwa shuka ikionekana kama mtu amelala kisha wakanyata na kufungua mlango wakatoka,walipofika getini semeni alijificha kwenye bustani ya mauwa,amina akamwita mlinzi aende kumsaidia chumbani kwake,mlinzi alikuwa kwenye wakati mgumu sana alipomwangalia amini jinsi alivyoumbika mtoto mashaallah alijisemea moyoni mlinzi yule,walipoingia ndani amina akamtaka amshushie begi kubwa LA nguo lilokuwa juu ya kabati chumbani mle bila kumuamsha dada yake aliyekuwa amelala pale kitandani,akimuonesha ile mito alioifunikipa pale kitandani,mlinzi akafanya kama alivyoagiza,alipolishusha lile begi amina akamtaka atoke mara moja chumbani kwake,mlinzi aliondoka.
Semeni alipoona mlinzi ameingia ndani akatoka,alipofika nje alimkuta jane kwenye gari naye akajipakia wakaondoka.
Kesho yake asubuhi semeni hakuonekana mpaka muda wa chai bado hawakutokea semeni wa amina,mzee rashidi alipatwa na wasiwasi,alimwambia mkewe akawaangalie chumbani mwao,mama amina alipokwenda chumbani mule alimkuta amina peke yake ila semeni hakuwepo,alimsalimia mwanae kisha akamwambia baba yake anamuitaji,amina alienda sebuleni na kumkuta baba yake,alimsalimia kisha nae akajumuika katika meza ile.baada ya muda mzee rashidi akamuuliza mwanae.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mbona umekuja peke yako,dada yako yupo wapi?"
"Nimeamka sijamuona,nikajua kawai kuamka"amina alimjibu
"Hapana,hatujamuona bado"mzee rashidi alisema
"Hatakuwa amekwenda wapi asubuhi hii huyu mtoto" mama amina alisema
Mzee rashidi alimuita msichana wa kazi kisha akamtaka azunguke kila chumba kumtafuta semeni,yule mdada wa kazi alifanya kama bosi wake alivyomweleza,alikagua kila chumba,alizunguka kila upande lakini hakumuona semeni ,alipoona hakuna dalili ya semeni kuwepo ndani mule akaenda kumwambia bosi wake jibu lile lile kwamba semeni hakuwepo.
Mzee rashidi alichanganyikiwa,akamtaka mlinzi aitwe,mlinzi alipofika pale sebuleni,mzee rashid akaanza kumuuliza kama alimuona semeni kutoka getini.
"Haya baba niambie,hukumuona semeni kutoka getini?"mzee rashid alimuuliza mlinzi
"Hapana baba sikumuona tangu jana semeni"mlinzi alijibu
"Sasa atakuwa ametokaje humu ndani?"
"Mimi sijui bosi"
"Kwa hiyo unanitania hee?,semeni ataondokaje bila kupita getini?"mzee rashid alisema kwa ukali,hali iliyompelekea mlinzi kuanza kutetemeka.
Wakati mzee rashidi akiongea hayo,amina alijua kila kitu akabaki akimwangalia na kumuonea huruma mlinzi aliyekuwa akitetereka,gafra mzee rashid alichukua funguo za gari kisha akatoka bila kuaga,hapa sasa kazi imeanza alijisema moyoni amina kisha nae akatoka...............
Yohana akiwa nyumbani kwake,akijiandaa kutoka,alisikia mlango ukigongwa,akaenda kufungua hamad uso kwa uso na mzee rashid akiwa na polisi,yohana akawakaribisha ndani,bila kusita wakaingia,mzee rashid akaanza kumtaka yohana amtoe semeni.
" yohana nipo hapa,sitaki kupoteza muda naomba umtoe semeni"
"Mzee mbona sijui kinachoendelea"?yohana alimjibu
"Narudia tena mtoe semeni ndani haraka iwezekanavyo!" Mzee rashid sasa aliongea kwa ukali.
"Semeni hayupo humu,sijamuona tangu nitoke katika sherehe yake nieleze kilichotokea!"yohana alijibu
"Semeni ametoroka tangu jana haonekani,atakuwa amekuja kwako"
"Semeni hajawai kufika hapa ata siku moja,sasa hatafikaje wakati hapajui"yohana alijitetea
"Basi tutakagua humu ndani,kikipatikana chochote cha semeni kesi itakuwa juu yako!"
"Sawa ,hakuna tatizo kagueni tu"yohana aliwaambia.
Mzee rashidi hakutaka kuendelea kubishana na yohana badara yake akawaambia polisi wafanye kazi yao.polisi wale walianza kukagua chumba kizima walienda uku na kule hawakufanikiwa kupata kitu chochote kinachousiana na semeni,mzee akataka yohana awekwe ndani lakini polisi wale wakakataa maana hawakuwa na udhibitisho wowote unaomuhusu kukamatwa kwake. Mzee rashid hakuwa na jinsi ikabidi aondoke huku akiwa amefura kwa hasira,polisi nao wakaondoka.
Yohana akabaki akiwa amechanganyikiwa kwa hukumu ile ya mzee rashid pili kumkosa kipenzi cha moyo wake semeni,akaamua kumpigia simu amina,ambapo walipanga wakutane sehemu,siku hiyo yohana alijiisi kuumwa kutokana na msongo Wa mawazo juu ya alipo semeni.amina alipomaliza kuongea na yohana mara akamsikia baba yake kija huku anaongea peke yake,alipomwangali aliisi mzee rashid amelewa,amina alimuuliza habari za hatokako baba yake akamjibu hakuna mafanikio yaliyopatika kumtafuta semeni ila taarifa ipo polisi wanaendelea na uchunguzi.
Ilipofika saa 10 jioni amina na yohana walifika walipopanga kukutana,yohana alikuwa na hamu kubwa kutaka kujua alipokwenda semeni,
"Amina naomba uniambie alipo semeni"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mbona una wasi wasi sana,embu punguza jazba!"amina alimwambia
" sio jazba,nataka kujua semeni amekwenda wapi?"
"Utapajua tu baadae"amina alimjibu kwa mkato
" unajua kiasi gani nampenda semeni,istoshe mama yake alinikabidhi mikononi mwangu,lolote litakalompata mimi ndio nitabeba lawama"yohana alilalamika
"Kumbe unampenda sana dada angu,kwanini hukumwambia ukweli kama unampenda?"amina alimuuliza
"Najua yote ni makosa yangu ila kwa sasa nipo tayari kwa lolote!"yohana alisema
"Sawa ila naomba utulie kwa sasa,mimi najua alipo semeni,hivyo nitakujulisha muda ukifika" amina alimwambia
Yohana alikubaliana na amina kwa shingo upande,kisha wakaaga na kila mmoja akaondoka kivyake.
Mzee rashidi akiwa sebuleni huku macho yake yakiwa kwenye runinga,kichwa chake kiliwaka moto kwa mawazo kibao huku moyoni akiwa na hofu kubwa kuhusiana na mtoto wake semeni,mawazo yakamjia mzee rashidi bila kupoteza muda akampigia simu mzee muba wakapanga kukutana sehemu.
Baada ya muda mzee rashidi akajiandaa na kutoka, ili kuonana na mzee muba.
Mzee rashidi alipofika pale,alimkuta mzee muba akiwa na mtoto wake wakimsubili,aliwasalimia kisha nae akaketi kwenye kiti kilichokuwa kwenye meza hile,mzee rashid alimtaka manase awapishe waongee,manase akakubali kisha akaenda kukaa jilani na walipokaa wao.
Mzee rashidi akaanza kumuambia mzee muba kila kitu jinsi ilivyotokea mpaka semeni kupotea.mzee rashidi bila kutarajia alimshuhudia mzee muba akimtukana na kumkereli kwa maneno mengi na kumwambia amefanya makusudi ila amualibie sherehe ya mwanae, sababu ameshaharika watu kibao, sasa leo itakuwaje!,lilikuwa pigo tena pigo kubwa sana kwa mzee muba istoshe amepokea michango cha harusi kutoka kwa ndugu na jamaa.
Gafla manase alimuona baba yake katika hali hile akaamua kwenda pale walipokuwa wamekaa,alipofika akawauliza kilichotoke bila kusita mzee muba akamueleza mwanae kilichotokea kwa mzee rashidi,nanase alisikitika sana kisha akawataka washirikiane kumtafuta semeni,
"Naomba wazee wangu tumtafute semeni mpaka atakapopatikana ili tufunge ndoa yetu!"manase akasema
" sawa nimekuelewa mwanangu "mzee rashidi alijibu
"Yaani mzee mwezangu,ulichokifanya kama umetuvua nguo adharani,tunataka shughuli iwe pale pale" mzee muba alisema
"Sawa nimewaelewa,nitahakikisha semeni anapatikana leo"mzee rashidi alisema.
Baada ya makubaliano ya kushirikiana kumtafuta semeni ,wakaanza kuwapataarifa waalifu wote ndugu na jamaa, kupotea kwa sameni,habari zilisambaa kwa kasi kama moto wa kifuu,semeni akaaza kutafutwa kwa udi na uvumba,karibia jiji lote la arusha kuenea taarifa zinazosema binti wa tajiri rashid atoweka nyumbani.
Siku ya jumatatu ilikuwa yenye shughuli nyingi wa wakazi wa arusha,yohana akiwa anakwenda kazini njiani aliwakuta vijana wawili wakisoma gazeti la sani lenye maandishi makubwa juu yake yaliyosomeka mtoto wa tajiri rashid atoweka nyumbani,ilikuwa taarifa iliyomshtua yohana,hakuyaamini macho yake,akaamua kumpigia simu amina akamwambi.
"Hallow"simu upande wa pili ilisikakika
" hallow yohana,vipi kwema?"
"Kwema kiasi!"yohana alijibu
" mbona asubuhi,asubuhi hii kuna tatizo"simu upande wa pili ilisikika
"Ndio tatizo lipo,wakati naenda kazini nikakutana na watu wakisoma gazeti lenye tangazo la kupotea kwa semeni"yohana alisemaCHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Heeeh! Mpaka kwenye gazeti tena?"
"Ndio!sasa inachotakiwa semeni asafirishwe mbali na mji wa arusha,maana ili tatizo limeshakua kubwa" yohana alisisitiza
"Sasa tutampeleka wapi?"
"Popote pale lakini husiwe mji huu"
"Niambie basi kama wapi panafaa?"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment