Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

KISASI NDANI YA NAFSI YANGU - 3

 







    Simulizi : Kisasi Ndani Ya Nafsi Yangu

    Sehemu Ya Tatu (3)

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku iliyofuata ilikuwa ni sikukuu kusherehekea kuanza kwa mwaka mpya.wakubwa kwa watoto walikuwa furahani walivaa na kupendeza wengine walikwenda beach na kwengineko kufurahi niliingia chumbani na kumkuta Anko akiwa amelala nilimwamsha na kumsalia nae akaitika kisha akanieleza kuhusu funguo alizonipa jana yake aliambia “fungu nilizokupa za upande wa kulia wa kabati lile,akinyoosha mkono ukifungua utakuta kadi mbili za bank,najua zinaweza kutusaidia baadae, nimeona nikukabidhi kutokana na hali yangu kama unavyoniona si wakupona leo wala kesho,shangazi yako ni mtu mbaya sana,amenifanyia mambo ya kishirikina.hakikisha kadi hizo hasizione ziwe mikononi mwako. Anko aliniambia mambo mengi sana, mengine sikuwai kuyasikia kutoka kwa wazazi wangu.Nilijifunza kitu kutoka kwa maneno ya anko nikamuaga na kutoka .Siku hiyo ikawanafasi nzuri kwangu kuondoka nyumbani, nilimuaga Anko Mashaka,kisha Shangazi nakwenda kwa rafiki yangu Musa, aliniruhusu mani nikaongoza njia kuelekea kwa musa,ilichukua nusu saa kufika mtaani wanapoishi Musa na dadaye,nikaifikia nyumba yao na kubisha hodi,dakika sifuri mlango ukafunguliwa Asha akatoka na kunikaribisha nami nikajitoma ndani,nilipoingia sebuleni nikamkuta Musa akiwa amekaa kwenye viti chakavu vilivyokuwemo mle ndani.Musa aliponiona aliachia tabasamu na kunikalibisha kwa bashasha kisha nami nikaka kitini. Baada ya salamu nilimtaka tuongee pembeni, musa hakuwa na kinyongo alinikaribisha chumbani mwake kwa ajiri ya maongezi hayo.

    “Musa!, mwenzako nipo kwenye matatizo”nilianza kumwambia

    “Matatizo gani tena rafiki yangu?”Musa alinijibu akiwa amenikazia macho

    “Tangia wazazi wangu walipofariki sina amani kabisa”niliendelea kumwambia

    “Niambie rafiki yangu,kwanini huna amani?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Shangazi Musa! Ananichukia amejawa na roho mbaya”

    “Unasema kweli bwana?”Musa alisema kwa mshangao

    “Ndio musa sikufichi kitu, kila siku tunagombana mpaka imefikia kipindi anataka tuondoke nyumbani Mimi na Anko sasa tutakwenda wapi wakati ile ndio nyumba yetu”nilimwambia.

    “Pole Sana Fred”Musa aliniambia huku akiwa na huzuni

    “Sijui nifanye nini rafiki yangu ili niendelee kushikiria na kulinda mali zangu ingawa sijui chochote Anko ndiye ameachiwa kila kitu kuhusiana na urithi huo”Niliendelea kumwambia

    “Aisee! Pole Sana Fred, sasa una mawazo au hatua gani uliyochukua kurudisha amani katika nyumba yenu?”Musa aliniuliza

    “Sijui la kufanya rafiki yangu, ndio maana nimekuja kwako unipe ushauri”nilimjibu

    “sina cha kukushauri Fred, wewe ni mwanaume simama imara pigania haki yako utaipata.Hali ya maisha yetu unayaua,tumeangaika mpaka tumefanikwa kuishi katika nyumba yetu,hatukutaka kuishi na ndugu yeyote sababu ndio kama hizo,tukipata tunakula tukikosa tunalala Mimi na dada yangu tumezoea”Musa aliniambia. Tuliongea mambo mengi, musa alinishauri nivumilie ili nipate kuchunguza mwenendo wa shangazi Zuwena.Baada ya maongezi hayo, Musa alinitaka nisiwe na wasi wasi akaniahidi kuwa pamoja nami pindi ninapoitaji msaada kutoka kwake, basi yupo tayari kunisaidia.ilipofika jioni niliaga na kurejea nyumbani..........



    Wakati nikiwa njiani narudi nyumbani niliwaza mambo mengi, nitawezaje kuondoka nyumbani ikiwa Anko hajiwezi kutembea wala kuzungumza vizuri, tutakwenda wapi sasa nilifikilia kuhusu pesa nilizoambiwa na Anko, kwamba wazazi wangu wameacha pesa zaidi ya milioni ishirini zilizopo Bank. Muda wowote na wakati wowote nikiitaji pesa,basi nifuate benki.Nilichokuwa natakiwa kuchukua pesa hizo haraka iwezekanavyo kabla bank aijafanya mabadiliko yoyote,kutokana na kifo cha wahusika wa akaunti hiyo.Niliwaza yote hayo nikiwa njiani kurudi nyumbani.

    Baada ya mwendo wa nusu saa nilifika nyumbani na kumkuta Anko Mashaka akiwa nje amelowana maji, nilishangaa na kumsogelea karibu kisha nikamwuliza kilichomsibu nae bila shaka akaniambia yaliyomkuta “nilikuwa nimelala kitandani nilipoamka nikamtaka shangazi yako aje kunisaidia kunipeleka msalani, lakini cha ajabu alinitoa mpaka nje akanikalisha chini,kisha aliingia tena ndani,safari hii akatoka na maji na kunimwagia bila sababu”.nilimsikiliza Anko kwa makini sikuwa na huamuzi tena maana nimeshazoea visa vya shangazi,nikamwangalia Anko jinsi alivyokuwa akitetemeka pale nje nikamwonea huruma.Siku hiyo nilijisikia vibaya sana jinsi muda ulivyokuwa ukienda nikiwa nimezubaa pale nje nikapata wazo ghafla nikanyanyuka haraka kisha nikamsaidia kumuinua na kumkurudi ndani, nilimbadilisha nguo kisha nikampa uji na kumlaza pale kitandani nae akanishukuru na kunitaka nikapumzike.Kabla sijaagana nae nilimuuliza kama Shangazi yupo,Anko akanijibu kwa kukiweka kidole mdomoni na kusema shiiip! Nikanywea kama kuku aliyemwagiwa maji ,sikujua kama shangazi yupo nyumbani kwa wakati huo,niliangaza macho yangu huku na kule kweli nilimuona akiwa jikoni,sikutaka kuongea zaidi nikaamua kwenda chumbani kwangu na kujitupa kitandani,kama ilivyo ada ya uchovu nikapitiwa na usingizi nikalala fofofo.

    ilipofikia saa mbili usiku nilishtuliwa na sauti ya shangazi akigonga mlango wa chumba changu,nilitoka na kwenda kumsikiliza.Alichoniambia kilinifanya nimjibu huku nikimtazama kitetemeshi si kitetemishi,hofu si hofu.hata sijui wapi mawazo yangu na maneno yangu yalikopotelea.nikayaelekeza macho sakafuni.nikajaribu kifunua kinywa changu nikaona kimekomelewa kama milango ya safina ya Nuhu.ulimi ulikuwa mzito kama nanga.nikajaribu kusema mwenyewe sikusikia hitakuwa wao walionisikiliza,nikaketi chini nimefura kwa hasira uso sina pa kuuweka.Shanzazi akinitaka nikaoshe vyombo ambavyo sikuvitumia wala kupikia.Nilitoka huku hasira zimenikamata wakati wote nikiwa na majonzi dhidi ya wazazi wangu, pia alimuonea huruma sana.

    Baada ya siku kadhaa nikaanza kuhisi hali isiyo ya kawaida Nyumbani, Anko alikuwa mtu hasiyejielewa, muda mwingi anaongea peke yake, kitu ambacho hakieleweki amekuwa Kama chizi.Nilikuwa kwenye wakati mgumu Sana kuwa karibu na Anko.Siku zinavyozidi kwenda ndivyo hali inazidi kuwa mbaya ikafika kipindi Anko akawa ulimwengu mwengine wa umwendawazimu aliyeweuka (chizi).Shangazi hakumjali wala kumsikitikia Anko kwa ugonjwa ule. Siku moja nilipoamua kumwambia ukweli Shangazi,

    “Shangazi, yaani wewe humuonei huruma anko anavyoteseka?

    “Mwendawazimu Yule! Unataka nimfanye nini?” shangazi aliniuliza kwa ukali?

    “Anko anaumwa, kumhuduma hutaki, unazidi kumtesa kabisa.jinsi alivyo unamuona kinyaa ata Kumgusa hutaki kama sio mumeo”nilimwambia,

    “Weee! Ishia hapo hapo. Na bado nitaakikisha mpaka mnaondoka ndani ya nyumba hii”shangazi alizidi kuuchuma moyo wangu,CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hee! Shanganzi unatufanyia sisi hivyo, Kama sio ndugu zako? Nilimhoji pasipo kupepesa

    “Sasa unatakaje? Hivi hujui Kama mnaniwekea mzigo nyumbani kwangu”shangazi alisema huku amenikazia macho. Nikawa sina cha kumjibu nikanywea Kama ndizi mkunguni.

    Nilishindwa kuendelea, nikaamua kwenda chumba cha stoo ambapo Anko Mashaka ndio alipofungiwa.Shangazi alimuona mchafu, vurugu zilikuwa sehemu ya maisha yake, hakumpenda wala kumpa huduma yoyote akaona bora akae nae mbali......





    ********

    Mwezi August Mwaka 1990, Majira ya asubuhi na mapema nilichukua kadi yangu ya benki na kutoka kuelekea moja kwa moja mpaka kyela, nilipofika nikakuta foleni nami nikapanga msitari kusubili zamu yangu.Ilipofika zamu yangu nikaingia na kuzitoa pesa zote kiasi cha shilingi Milioni Ishirini.Niliamua kuzipeleka kwa rafiki yangu aniwekee kwa muda,najua zitanisaidia iwapo shangazi atanifukuza nyumbani,nitaweza kutafuta maisha kwa pesa hizo.Wakati nipo njiani kuelekea kwa Musa niliwaza mambo mengi sana,kuhusu pesa zile nilipanga kununua nyumba pamoja na maitaji mengine,sikutaka kuzipeleka nyumbani,niliofia shangazi akiziona anaweza kuzichukua,nilijiona mshindi siku hiyo kwa maamuzi yangu. Baada ya mwendo wa nusu saa nikafika nyumbani kwa Musa, nilimkuta Musa yupo nje amekaa kwenye ti mmoja mrefu uliokuwa na kimvuli kizuri amekaa kwenye mkeka.

    Musa alipomuona alinikalibisha kisha nikaa karibu yake katika mkeka huo kisha tukasalimiana na nikamweleza shida yangu naye akanitaka kumueleza kila kitu kuchimba na kuchimbua kuhusiana na Pesa hizo Musa alishangaa sana nilipomwambia kwamba pesa zilikuwa za wazazi wangu kisha akaniuliza “pesa kiasi chote hiki nimezibeba kwenye mfuko wa bahasha tu bila kuwa na tahadhali yoyote ?”,nikamwambia sikuwa na namna ya kuzificha pesa hizo maana sikuwa na sehemu nyingine kuzihifadhi hivyo nikaona nizipitishe kwake.Nikamtaka aniwekee vizuri mpaka pale nitakapokuja kuzichukua naye nitamgawia fungu lake,Musa hakusita alizipokea na kusema “Niamini Rafiki yangu pesa zako utazikuta kama

    ulivyoziacha, hakuna mtu yeyote atakaye zigusa, nilifurahi sana kusikia hivyo kisha nikaendelea kumwambia,

    “Nakuamini rafiki yangu, ndio maana nimekuja kwako uniwekee”,

    “Usijali Fred pesa utazikuta,si umezihesabu lakini?Musa alinitupia swali

    “Ndio nimezihesabu, zipo Milioni ishirini na tano”nilimjibu huku nikimwangalia usoni kwa udadisi

    “Sawa nitakuifadhia vizuri”Musa alinijibu

    “Nakutegemea Sana Rafiki, husitumie hata shilingi mia, nikija kuzichukua ndio nitakupa na wewe kiasi cha pesa rafiki yangu”nilimwambia.Muda si mrefu nilimalizana na Musa kisha nikaagana nae na kurudi nyumbani.



    Ilikuwa siku ya jumamosi majira ya asubuhi na mapema, nilikwenda nyumbani kwa Musa.Nilipofika sikuamini macho yangu,niliamua kusogea karibu na nyumba ile,ilikuwa yapita siku nyingi mwezi mmoja ukafikia sikuwa na mawasiliano yoyote na Musa mpaka pale siku hiyo nilipoamua kwenda kumsalimia nilichanganyikiwa kwakweli sikuelewa kinachoendea,kuona ujenzi ukiendelea maeneo yale.Mafundi na makandalasi wakiwa makini kwa kazi yao,vifusi vya mchanga na kokoto nyingi zikiwepo kando ya eneo ilo,kilichonishangaza zaidi nyumba yao haikuwepo mahali pale nikaisi kizunguzungu nikaketi kando ya kifusi cha kokoto.Nikiwa nafikiria jinsi gani nitawapata wenyeji wangu, nilipata wazo kuwafuata watu waliyokuwepo eneo lile na kuwauliza,

    “Habari zenu?”niliwasalimu

    “Salama! Karibu”mmoja wapo alinijibu

    “Samahani ndugu zangu, mwenye nyumba hii yupo wapi? Niliwauliza

    “Hata hatufahamu kijana, sisi tumekabidhiwa kazi na Mtu mmoja ila Jina lake Hatumfahamu!”

    “Yupo vipi huyo jamaa? Niliwauliza

    “Mrefu kidogo, mweupe mtu mzima mzima hivi”alinijibu mmoja wapo

    “Aisee! Ina maana Musa amehama hapa? Atakuwa ameamia wapi?”Niliuliza maswali mfululizo

    “Hatujui Kijana labda ukaulize kwa jirani yake pale nyumba ya pili”

    Niliondoka bila kuaga nikiwaacha wakijiuliza maswali mengi juu yangu, sikuwajali nikaongoza moja kwa moja mpaka nyumba mmoja wapo iliyopo jirani na kubisha hodi, baada ya muda alitoka Mama wa makamo nikamsalimi nae akaitikia. Kisha nikamwambia shida yangu.Alichoniambia Yule Mama nilijiisi kuchanganyikiwa, mapigo ya moyo yakaongezeka nikashindwa kujizuia machozi yakanidondoka.Alichoniambia Yule Mama ni kwamba Musa na dadaye Asha wameamia makazi mapya katika kijiji cha Sumbi na kununua nyumba ya kifahari.Sikutaka kuendelea kumsikiliza Yule mama, nilimuaga na kuondoka.Kijiji cha sumbi ni kitongoji cha wilaya ya kyela kilichopo jilani na kijiji cha busale,nakifahamu vizuri kijiji cha Sumbi kwa matukio mbalimbali ya unyanyasaji.Mauwaji ya kutisha yanayofanyia katika kijiji hicho hasa nyakati za mavuno,watu wengi wanapokuwa mashambani urejea mapema nyumbani ili kuepuka na ualifu.

    Siku iliyofuata niliondoka mapema nyumbani kuelekea kijiji cha Sumbi, nilipanda boda boda mpaka kijiji hapo, nipofika nikauliza kwa wanakijiji kama wanamfahamu Musa na Asha. Walikuwa wameamia kijijini pale, wengi wao hawakumfahamu Musa na dadaye,nilipata wakati mgumu kuwaelezea maumbile yao,kila nilipokutana na mtu nilimuuliza majibu yalikuwa yale yale hawakumfahamu.Safari ile ilinichosha sana mwili ukaanza kunyong’onyea njaa nayo ikiniyoyoma,nikajipa matumaini kuendelea na safari,nilipokuwa njiani nikaona kibanda cha mama ntilie nikaongoza ili kujipatia chakula,nilipofika nikamkuta dada mmoja akiwaudumia wateja nami nikaagiza ugali kwa samaki,nililetewa na kuanza kula. Wakati naendelea kula Gafla moyo wangu ukapiga paa! Sikuamini macho yangu nilichokiona kilinipa kiwewe, nikafikiri labda naota nilipojichunguza nikajua sio ndoto bali ni ukweli, sikujali wala kufikilia tena njaa niliyokuwa nayo iliishia pale pale.Kwa mara ya kwanza nilimuona Musa Akiingia ndani ya kibanda kile. Musa alikuwa amependeza na kunawili,nikajikuta nikiinuka na kumfuata,nilipofika pale nikamgusa begani nae akageuza shingo tukawa tunaangaliana uso kwa uso.Nilimwona Musa akijizoazoa pale alipokaa na kusimama,sikutaka kupoteza muda nikaanzisha mazungumzo.......



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Musa habari yako?”

    “Salama!”Alijibu kwa mashaka

    “Vipi rafiki yangu mbona Kama haupo sawa”nilimuuliza

    “Hapana nipo sawa “alijibu

    “Sawa! Naomba tuongee pembeni kama inawezekana nipeleke nyumbani unapoishi sasa”

    “Sawa twende nyumbani”Musa aliniambia

    Hakuna aliyefikiria chakula kwa wakati huo, kila mmoja alikuwa na mawazo yake, hasa kutokana na taharuki iliyokuwa kati yetu.Ujio wangu mlimchanganya sana Musa hakuelewa nimefikaje mahali pale, maana alijua fika nimefuata pesa zangu baada ya kumkosa Busale.

    Baada ya mwendo wa nusa saa tulifika kwenye nyumba ya kifahali iliyokuwa kando ya kanisa kuu la k.k.t dayosisi ya Sumbi.Ilikuwa nyumba mpya yenye ukuta mrefu iliyozungushiwa nyaya kwa usalama wa nyumba hiyo.Musa aligonga geti la nyumba hiyo baada ya muda nilimuona Asha akifungua Mlango wa nyumba hiyo kisha Musa akanikaribisha tukaingia ndani.nilipoingia tu sebuleni nilikutana na televisheni kubwa iliyokuwa ukutani,friji ikiwa pembeni ya mlango wa kuingilia sebuleni, kiyoyozi kikali kikiwa kinayoyoma katika sebule hiyo,hakika ilikuwa nyumba nzuri inayovutia.



    Nikashikwa na tamaa ya mali zile nikageuka mzima mzima na kumuangalia musa kisha nikamuambia kwa hasira“Musa nimekuja kuchukua pesa zangu, nimeshapata kiwanja nataka kujenga nyumba”,Musa alijifanya kama hajasikia badala ya kunijibu nikamuona akijiinamia chini na machozi kumtoka.kwakweli sikumuelewa nikaisi kama kuna jambo ananificha ,nikamsogelea na kumtaka aniambie kinachomliza lakini Musa aliendelea kulia,woga ukaniingia hasira zote zakaishia pale,nilimsihi kunyamaza ili tuongee bila shaka Musa alinisikiliza na kunyamaza.Sikutaka kukubaliana na Masikio yangu,nilichokisikia kutoka kwa musa kunitoa machozi na kuumiza moyo wangu,nilijongea na kutulia kama maji mtungini,mtu niliyemuamini amenigeuka nikakumbuka msemo usemao Akufahaye kwa dhiki ndio rafiki,kumbe nilikuwa najidanganya Musa hakuwa rafiki wa kweli bali alikuwa rafiki mnafiki,siku hiyo nilimwona Musa msaliti binadamu aliyevaa ngozi ya chui,hakika niliumia moyoni mwangu.

    “Pesa tumezifanyia biashara hivyo basi tutarudisha baada ya wiki moja”,

    “Kwanini hukuniambia Musa kama pesa zangu mmezifanyia biashara?”Nilimwuliza huku nikitetemeka

    “Sikuwa na haja ya kukwambia mapema kwa sababu wewe ni kama ndugu yangu”Musa alinijibu

    “Hukunifanyia vizuri rafiki yangu, mmeuza nyumba yenu busale na kuamia Sumbi bila taarifa, gari na mna maisha mazuri, haiwezekani na mimi mnipe pesa japo kidogo”nilimwambia Musa huku nikiwa na hasira

    “Samahani niliyokosea, kiukweli nipe wiki moja, pesa zako nitakurudishia kama zilivyokuwa”Musa alijitete,

    “Sawa, kama umeamua kunidhurumu, mungu anajua”nilimwambia musa huku machozi yakinitoka.

    Niliondoka kwa Musa nikiwa mtu aliyekosa amani, niliwaza mambo mengi kuhusiana na pesa nilizompa aniwekee sasa yeye ameamua kuzitumia,kichwa kilikuwa kizito kutokana na mawazo mengi kuhusu hatima ya maisha yangu na Anko Mashaka.Baada ya mwendo wa boda boda uliotumia nusu saa kufika busale niliongoza moja kwa moja mpaka nyumbani, nilimkuta Shangazi yupo nje ya nyumba yetu huku akiwa na hasira.Nilihamaki kisha kumsogelea karibu Anko Mashaka aliyekuwa amekaa pembeni na kumnyanyua.Hali yake ilikuwa mbaya, alikuwa mtu ambaye aeleweki ni nikaisi kitu kinachoendelea kati yake na Shangazi.Nilimsalimia lakini hakuitika, nilijiuliza sijui sababu ya sauti yangu kuwa ya kwikwi au alichukizwa na safari zangu mfululizo sikupata jibu sahihi.nikamchukua Anko na kumuaingiza ndani,kabla sijafika mlango mkubwa,Shanzazi akaniwai kunishika mkono na kunitaka nisimame,sikuelewa madhumuni ya shangazi mpaka kufanya hivyo, nilipata wakati mgumu kumshawishi shangazi nimuingize Anko ndani alikataa.nilipoona hivyo, nikaamua kamuuliza kwa jazba.

    “Shangazi vipi mbona umetuzuia kuingia ndani”nilimwuliza

    “Uingie ndani kufanya nini?”Alinijibu kwa kejeli

    “Anko akapumzike ndani”nilimjibu

    “Nataka muondoke hapa nyumbani kwangu, kama kuna kitu nimesahau niambie nikuletee”Shangazi alinijibu

    “Hee! Shangazi unatufukuza sisi kweli”nilishangaa

    “Ndio hivyo naomba muondoke mapema maana nyumba hii imeshanunuliwa”alizidi kuniandama.

    “Haiwezekani! Tutaishi wapi sasa?”Nilimwambia kwa kujiamini

    “Naenda dukani nikirudi nisiwakute”Shangazi alisema bila chembe ya mzaha na kufuga mlango kisha akaondoka zake.

    Hapo sasa nikaamini kweli Shangazi ametugeuka na kutuona hatufai, amesahau fadhila na kuiuza nyumba yetu bila kutushirikisha.Nilisononeka moyoni machozi yakilowanisha mashavu yangu, nilimfuata Anko alipokaa na kumshika mkono kisha tukaanza safari ya kuondoka huku nikiwa sijuie niende wapi.Tukiwa njiani nikapata wazo kwenda tena kwa Musa ata kama ameniambia hana pesa basi nitamuomba niishi nyumbani kwake kwa muda mpaka atakapopata pesa zangu nami nitajua sehemu ya kuishi.......

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******

    Nilipoondoka huku nyuma Musa alichukua pesa hizo na kuzificha chumbani kwake, ile anatoka tu chumbani kwake alikutana uso kwa uso na dada yake akirudi toka sokoni. Baada ya muda ukimya ulitawala kati yao.Musa akaamua kuvunja ukimya huo, akamweleza dadaye Asha kuhusu pesa nilizompelekea kuhifadhi.Asha alimshangaa Sana, akapata kigugumizi cha ghafla hakashindwa kuzungumza akakaa kimya kwa muda bila kumjibu kakaye.Mawazo tele kichwani akawaza na kuwazua akaona utajiri mbele yake, hakutaka kuwa masikini tena, sasa muda wa kuvaa,kula na kupendeza vizuri umewadia akazifikilia pesa hizo kisha akajisemea mawazoni,”lazima nizipate pesa hizo haiwezekani kuziacha hivi hivi. Akapata wakati mgumu, akaamua kumwambia nduguye,

    “Hiyo ni bahati husiitupe!”

    “Dada si nimekuambia pesa za watu, hiyo bahati hitoke wapi? Musa alimjibu dadaye pasi na mashaka juu

    “Husiwe mshamba!, pesa alizokupa Fred ni nyingi mno, unaweza ukafanya biashara na kuingiza faida kubwa zaidi ya pesa hizo,unaweza kuwa na maisha mazuri, unajenga au unanunua nyumba, magari ya kifahali na kila kitu ndani.Sisi tunaishi katika kijumba kibovu kama hiki,mvua ikinyesha usiku hatulali maji mpaka ndani”Asha alizidi kumshawishi ndugu yake,

    “Lakini dada naogopa na sitaki, kuzitumia pesa za watu naogopa lawama,”Musa alijitetea

    “Kama unaogopa nipe hizo pesa nibadilishe maisha yetu, unamuonea huruma Fred wakati wewe unaishi maisha mabovu, unaangaika huko kiwandani msahara wenyewe elfu thelathini”Asha alishadadia,

    “Hapana dada siwezi kukupa pesa za watu!”Musa alishikilia msimamo wake,

    “Nipe hizo pesa nimekwambia!, nitahakikisha kila kitu kinakwenda sawa, usiwe na wasiwasi, huu utajiri wa bure kaka yangu,ushamba wote uliokuwa nao utakwisha”Asha alimwambia.



    Baada ya ushawishi huo, hatimaye Musa aliafiki na kwenda chumbani kwake kuchukua pesa zote na kumkabidhi nduguye.Asha alizipokea pesa hizo kwa bashasha kisha akamuambia ndugu yake “Usiwe na wasi wasi pesa zimefika mikono salama tufurahie maisha yetu kwa upendo”.Musa aliudhunika sana moyoni kumdhurumu rafiki yake Fred, aliona maamuzi aliyofanya dadaye si sahihi ata kidogo. Akapiga moyo konde kusubili kitakachotokea kama kweli pesa za Fred zitarudishwa kutukana na biashara watayoifanya. Baada ya wiki mbili kupita Asha alimpata dalali wa kuuza na kununua nyumba, mtu huyo aliwafanyia mpango mpaka kufanikiwa kuiuza nyumba waliokuwa wanaishi kwa milioni kumi kisha kupitia dalali huyo pia kununua nyumba yenye thamani ya milioni kumi maeneo ya Kijiji cha Sumbi. .

    Baada ya kukamilisha taratibu za ununuzi wa nyumba hiyo,Musa na dadaye waliamia makazi mapya kwa furaha na fanaka,hawakumfikiria Fred.Waliishi pekee kwa amani na upendo,Musa alijiona mkosaji mbele ya mungu,kuchukua pesa za rafikie bila idhini yake kulimuumiza sana, ingawa hakuwa na namna kubaki na lake rohoni.Ikawa mwanzo wa maisha mazuri kwa musa na dadaye Asha.Ndugu hao walinidhulumu na kuchukua pesa zangu bila mwenyewe kujua kinachoendelea.Siku zilizidi kwenda hatimaye mwezi kukatika Musa na dadaye waliendelea kuishi raha mustarehe katika nyumba ya kifahari,walikula vizuri,kulala vizuri kila kitu kwao kilikuwa kipya.Pesa ziliwachanganya,waliishi kwa raha bila wasiwasi.

    Siku zinavyozidi kwenda ndivyo Maisha yao yanavyobadilika, Asha akawa mlevi kupindukia, akaanza kuzitumia pesa kwa fujo, kitu chochote kinachopita mbele ya macho yake yeye ununua wala hakuona umuhimu wa kutunza fedha hizo, usiku uchukuzana na waume zake kwenda club kunywa pombe, akirudi nyumbani ufanya fujo na kumpiga kaka yake. Hali hiyo ilimuumiza sana Musa ingawa hakujua afanye nini wakati huo, alimwogopa sana dadaye japo

    yeye alikuwa mkubwa lakini Asha alimshinda kwa nguvu kuliko maalifa.alipotezea na kumuachia dadaye afanye anavyotaka, Musa alikosa amani kutokana na wasiwasi kuhusu pesa za rafikiye Fred , je mwenyewe akizitaka hatamjibu nini,alijua amefanya makosa makubwa sana kumkubalia dadaye kuzitumia pesa za rafikiye,aliwaza na kujiuliza sana Musa kuhusina na pesa hizo.

    *******

    Baada ya kufukuzwa nyumbani ,Sikufahamu sehemu nikayokwenda kwa wakati huo nilikaa njiani huku nikifikiria hatima ya maisha yangu.Nitawezaje kuishi nikiwa sina pesa nikachoka zaidi nilipomuangali Anko Mashaka, maskini akiwa hana hili wala lile akichezea mchanga kama mtoto,nikajiinamia chini huku machozi kunibubujika.Nadhani nilisinzia nikiwa bado nimekaa kwenye kigogo cha mti pale njiani.Nilipoamka sikumuona Anko nikahamaki na kumtafuta huku na huko nikamuona amekaa mita chache kutoka pale,nilimfuata na kuondoka nae kuelekea Sumbi.Niliifuata barabara kuu mpaka nyumbani kwa Musa,nikafika na kubisha hodi,Akatoka Asha na kunikaribisha ndani,nami nikaingia moja kwa moja mpaka sebuleni.Nikamkuta Musa amekaa,aliponiona alishangaa kwa ujio wangu, kwa tahadhari akaketi kitini nami nikafuata.niliumia sana moyoni niliitaji kusaidiwa angalau sehemu ya kulala siku hiyo,ili niweze kuishi pamoja na Anko Mashaka, ambaye ni mgonjwa.Sebuleni tulikuwa watu watatu yaani mimi,Musa na Asha tukiwa tumekaa,tulipomaliza kusalimiana, Asha alitoka na kuendelea na kazi zake.Siku hiyo kichwa kiliuma sababu nilikuwa na mawazo mengi mno, Nilishindwa kuvumilia, sikutaka kuwa mjinga tena nikamgeukia Musa na kumwambia.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Musa Rafiki yangu, Nina matatizo makubwa sana”Nilimwambia

    “Matatizo gani tena? Aliniuliza kama mtu ambaye hajui kinachoendelea

    “Shangazi ametufukuza nyumbani”nilimwambia,

    “Pole sana rafiki yangu,ilikuwaje?”Aliniuliza kwa mshangao

    “Basi tu maamuzi yake, amesema ameshauza nyumba”nilimwambia

    “Aisee! Pole Sana Fred, kwa hiyo umechukua hatua gani rafiki?”Aliniuliza

    “Hakuna hatua yoyote niliyochukua”nilimjibu

    “Kwa hiyo utaishi vipi?”Aliniuliza

    “Nimekuja kwako unisaidie, naomba pesa japo kidogo niweze kupanga chumba”nilimwambia,

    “Nikusaidiaje rafiki yangu?” Musa aliniuliza

    “Naomba kuishi hapa kwa muda, maana sina pa kwenda”nilimwambia, musa alijifikilia kisha akajibu................







    “Sawa basi nitakusaidia kukaa hapa nyumbani mpaka utakapokuwa sawa”

    “Nashukuru sana Musa, ila nimekuja na Anko Mashaka nimemwacha nje”nilimwambia

    “Aina tatizo kamlete tutaishi nae pia”Musa alisema

    Niliondoka nikiwa na furaha moyoni kukubaliwa na kupata makazi ya kuishi katika nyumba ya kifahali nilitoka moja kwa mmoja mpaka kwenye kibanda kibovu, kilichopo nje ya nyumba hiyo, sikutaka kuangaika wakati wa kuongea na Musa. Nilifika kwenye kibanda hicho na pale kumchukua Anko na kuingia nae ndani. Musa alishtuka alipomwona Anko Mashaka, akaniuliza “huyu ndie Anko Mashaka?”nilimjibu “ndio yeye”,Musa hakuamini alimsogelea na kuanza kumsemesha Anko hakujibu badala yake alimshika shika Musa huku udenda ukimtoka,Musa hakuendelea tena kumgusa,alirudi nyuma kuchukua mabegi yetu na kunitaka nimfuate kumsaidia Anko kuingia chumbani kisha Musa aliniambia,

    “Fred Mbona Anko Mashaka hayupo sawa, ataweza kweli kukaa humu ndani akimuona kwenye hali hii sijui kama atakubali kuishi nae”Musa alisema,

    “Sikiliza rafiki yangu huyu ni Anko wangu naomba umkubalie tuishi pamoja, pia mwambie dada Asha akubali”nilimwambia,

    “Sawa nitamwambia, lakini sijui Kama hatakubali”musa aliendelea kuniogopesha.

    “Sawa kama hajakubali basi nitatafuta pa kwenda lakini naomba unisaidie ndugu yangu

    “ Usijali karibu sana”



    Tulipomaliza maongezi hayo Musa alinitaka nimfuate ili kunionyesha chumba ambacho nitalala nikiwa pamoja na Anko Mashaka,bila kusita nilimfuata.Tulifika kwenye chumba ambacho ndani yake kuna kitanda na television, musa alinikabizi funguo za chumba hicho kisha akaniambia “Hiki ndio kitakuwa chumba cha makazi yako siku zote utakazokuwa nyumbani hapa pamoja na na Anko Mashaka.Nilifurahi sana kusikia hivyo na kumwambia Musa “nashukuru sana rafiki yangu kwa Msaada wako,Musa alijibu “husiwe na wasiwasi nitakusaidia kwa kila jambo wakati wote utakaoishi hapa nyumbani”, tulikubaliana kwa pamoja tukakumbatiana.

    Ilikuwa yafikia saa tatu za usiku tukiwa sebuleni tunaangalia televisheni, Asha aliingia akiwa amelewa hakuna aliyemsemesha kila mtu alikuwa kimya macho kwa wakati huo, alipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kwake.Wakati tukiwa tunaendelea na maongezi ikasikika sauti ya Asha akimtaka Musa ampelekee soda, Musa aliona taabu kunyanyuka, akanyamaza kimya na kujifanya hajasikia.Asha alirudia tena kuita safari hii ikiwa kwa jazba, Musa aliamua kumuuliza dadaye kwa dharau na kejeli,

    “Unasemaje, naona unatupigia kelele?”

    “Nimekwambia niletee maji Asha alimjibu kwa kejeli



    “Nimechoka njoo uchukue mwenyewe, wakati umepita sasa hivi hapa kwa nini hujachukua kabisa”Musa alimjibu dadaye.

    “Najisikia vibaya ndio maana nikaomba uniletee”Asha alisema

    “Nani kakwambia unywe pombe zako huko?”Musa alimjibu.

    Maneno hayo yalimuuza Asha, hivyo alitoka mpaka sebleni na kuanza kumpa kichapo nduguye, nilishuhudia Asha anavyomkunja na kumpiga mateke kwa ngumi kakaye bila huruma,Nguvu zilimuishia Musa nikaamua kuingilia kati na kuwaamulia.Musa akajikuta mikononi mwangu, alipoona hivyo akaamua kuepusha shari na kukimbilia nje,huku akimuacha Asha akiwa na hasira.

    ********CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Musa akiwa amekaa sebuleni alikuwa ameshika tama, akiwa na mawazo lukuki kichwani mwake Wakati najiandaa kutoka chumbani kwangu nilimuona Asha akitokea chumbani kwake nakujumuika na kakaye sebuleni.Musa alivunja ukimya na kuanza kuongea,Sikutaka kwenda tena pale sebuleni nikajibanza pale pale mlango kusikiliza mazungumzo yao,nikamsikia Musa akimwambia nduguye kuhusu kuwa na wageni nyumbani, alimueleza kwa upole kila kitu kilichonitokea. Kuhusu uwepo ugeni ndani ya nyumba yao,

    “Dada hivi ninavyokwambia Fred na Mjomba wake wamekuja kuniomba msaada,

    “Msaada wa nini?Asha aliuliza kwa dhalau

    “Si kuhusu matatizo yake,kwani wewe hujui?” musa alimuuliza

    “Hapana sifahamu”Asha alimjibu

    “Basi nitakueleza baadae, kwa sasa anaomba tuwapokee na kuishi hapa, nyumbani kwao wamefukuzwa”,

    “Unasemaje yaani aje kuishi humu ndani?Asha alihamaki

    “Ndio dada, yeye pamoja na Anko Mashaka”Musa alimjibu,

    “Kwa hiyo wewe umewakubali hee!”Asha alisema

    “Ndio, sikuwa na sababu ya kuwakatalia”musa alimjibu

    “Sikiliza wewe, ujui Kama wanatuongezea mzigo humu ndani?

    “Hapana dada sio vizuri, kumbuka kwamba yeye ndio aliyetufanya kuwa hapa!”Musa alipomwambia hivyo dadaye akanywea na kuishusha sauti yake.......



    “Sawa Kama umewakalibisha amna neno,

    “Sawa dada nashukuru kukuona na wewe umewakubalia”

    “Alipoulizia kuhusu pesa zake, ulimjibu vipi?”Asha alimwuliza kwa mashaka nduguye

    “Nilimwambia tumefungua biashara, ndani ya mwezi huu tutampa pesa zake”Musa alijibu kwa kujiamini

    “Safi sana mtoto una akili wewe”Asha alimsifu nduguye

    “Sawa ila kuwa makini na hizo pombe unazokunywa, usiwatese unatakiwa uwaonyeshe upendo na ukalimu”Musa alimwambia dadaye.

    Wakati wanaongea yote hayo si Musa wala Asha hakuna aliyefahamu kama nilikuwa nawasikiliza maana hawakuniona nilipokuwa nimesimama.Baada ya kumaliza maongezi yao, nilimuona Musa anakuja usawa wa chumba nilichowemo, nikaruka kama mshale na kuzama ndani. Sekunde kadhaa nikasikia mtu akibisha hodi katika chumba hicho, nilitoka na kwenda kufungua mlango nikakutana uso kwa uso na Musa, nikamkaribisha ndani nae akaingia.Wakati huo Anko Mashaka akiwa bado amelala, hivyo hali ilikuwa tulivu katika chumba hicho. Tulisalimiana kisha Musa akaanza kunieleza walivyoongea na dada yake kwamba amekubali Mimi kuishi nyumbani kwao na kupata ninachokitaka.Sikutaka kuonesha chuki za wazi wazi niliachia tabasamu pana ili kuonyesha furaha usoni mwangu.kisha nikamwambia “nifurahi sana kusikia hivyo nawaombea kwa mungu awabariki sana, “usijali wewe ni rafiki yangu nitakusaidia kwa lolote”musa alinijibu.Sikujisikia kuendelea kuongea nae maana nilikuwa na dukuduku moyoni mwangu,badala yake nikajifanya kwenda msalani musa aliponiona naelekea msalani aliaga na kutoka.Aliniacha kwenye wakati mgumu sana,nilijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.Nikaaanza kumchukia Musa nikaona yeye ndio chanzo cha mateso ninayopitia nilishindwa kuelewa nichukue mahamuzi gani ili kuondokana na mateso hayo.

    **********

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog