Simulizi : Jela Ni Haki Yangu
Sehemu Ya Tatu (3)
" sikieni nyote " alianza kuzungumza Rambo huku akiwa amesimama na kujilinganisha wima na mti uliokuwa eneo hilo na kuwafanya wenzie waliokuwa wamesimama katika miti kutega masikio yao vyema ,
"kinachotakiwa wote tuwe makini sana maana hizi ndege zinazunguka zunguka eneo hili hivyo tujikate kate na tujifunge kwa majani ya miti ili kupoteza uhalisia wetu na ikitokea ndege imekukalibia lala chini ama itengue kama utaweza " aliongea Rambo na wote walifaata maelezo hayo ikawa ni kutekeleza tu , CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndege nazo zilizidisha kasi ya kuzunguka zunguka eneo lote hasa hasa lilokuwa limetanda moto baadae zilipotea na hali ikawa shwari eneo lote na kuwafanya magaidi hao kuendelea na safari ya kuupanda mlima haraka iwezekanavyo .
Wakiwa wamekaribia kufika mpakani ghafla kwa mbele yao waliweza kuona kwatumia kiona mbali , kundi kubwa la wanajeshi na askari likija kwa kasi sana kufumba na kufumbua helkopita zilianza tena kuzunguzunguka eneo hilo safari hii zilikuwa zimeshuka chini zaidi na kuwasha taa maana eneo lote lilikuwa giza tupu kwao kutokana na wingi wa miti mikubwa iliyokuwa imesogamana , victor aliekuwa amelala kifudi fudi akiwa hajui hili wala lile alistukia helkopita ikisimama nyuma yake na wanajeshi watatu walianza kupiga hatua kuelekea eneo hilo kwa kasi " tueleze wenzio wako wapi !?" mmoja wa wanajeshi alimhoji huku akimpiga na kitako cha bunduki kisogoni , " sijui"
Alijibu Kwa kifupi na kejeli baada ya kuona ishara ya Rambo aliekuwa mita chache eneo hilo akiseti mashine yake ya kulipua kila kitu ,
" hutaki kusema "
" nini nita...." kabla hajamalizia sentesi yake alishangaa kuona yule mwanajeshi akilushwa hewani na helkopita ikiwaka moto hapo hapo Rambo alimkamata mmoja wa wanajeshi aliekuwa amezubaa , lilikuwa ni tukio la kushitukiza sana na la dakika tatu tu Rambo akawa amemuokoa victor kwa staili hiyo na kumteka mwanajeshi aliekuwa akitetema baada ya kuona sura ya Rambo kijana hatari sana , mwembamba wa mwili lakini machachari , walianza kumvuta kutoka eneo hilo kabla ya kusogelewa na helkopita zilizokuwa zinatoa msaada kwa ile iliyokuwa inateketea moto " wale paleeeeeeee!" mmoja wa wanajeshi aliongea huku akinyosha kidole chake kuelekea eneo hilo , mvua za risasi zilianza kunyesha kuelekea huko na moja ilimpiga victor mgongoni na kuanguka chini , kuona vile Rambo alimtwanga shaba yule mwanajeshi japo alikuwa amemteka kwa lengo la kumhoji , alifanya hivyo baada ya kuona victor amepigwa risasi ,kisha alijificha chini ya mti uliokuwa mkubwa sana na kufanania nao kutokana na weusi wa nguo zake na majani aliyokuwa amejifunga funga .
" huyu msh***zi atakuwa eneo hili tu wacha tumtafute "
" hapana tusipoteze mda tumuwahisheni kwanza mkuu hospitali na tutoe taarifa idala ya ulizi tuongezewe watu leo hii lazima tuwakamate wote " yalikuwa mazungumzo ya wanajeshi waliokuwa eneo hilo ambalo Rambo aliyasikia yote na hata kuwaona .
*******
Moto ulizidi kusamba eneo lote walilikuepo wanajeshi na mbwa wote hakukuwa na kusaidiana kila mtu alihaha kivyake hata helkopita zilipofika eneo hilo hazikuweza kuambulia chochote zaidi ya masalia ya wanajeshi hao " sasa imekuwaje ?"
mmoja wao aliuliza " coplo Mhina alinipigia simu na kudai tuje na helkopita kwani walikuwa wamewakaribia "
" heeeee!!!! nini hiki aliongea mwenzao na wote waliziruhusu shingo zao kugeukia upande huo " hilo bomu na ni hatari sana tuondokeni haraka kabla ya kulipuka " walirudi ndani ya helkopita zao na kuondoka eneo hilo dakika tatu ulisikika mlipuko .
" nyie niwanajeshi mliopitia mafunzo ya jeshi , na mkahapa kufa na kupona sasa mmeshindwaje kuja na wajinga hao na istoshe taarifa mlikuwa nazo hata eneo coplo Mhina aliwaelekezeni wapi waliko " aliongea mkuu wa jeshi Mr Njawi huku jasho jembamba likitirika mwilini , macho alikuwa ameyatoa hakutulia kitini hapo mala asimame mala atembe hakika alikuwa amechanganyikiwa .
" nawapa dakika tatu muwe , mmepotea hapa wengine mkapitie mpaka wa Tanzani ili pawe na wepesi Wa kuyakama " alitoa maelekezo hayo na kitoka katika chumba hiko akiubamiza mlango " paaaa!" .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wanajeshi walirudi tena msituni humo Kwa nia ya kuwakamata magaidi hao Napo Rambo ameanza Kwa kuwafyatua mmoja baada ya mwingine .
" mnaenda wapi !?" '" tunaingia humo msituni kuna magaidi wameingia "
" hayo magaidi yakutoka wapi tuje tuyalipue !"
" Al- kida " alidakia askari usalama aliekuwa mpakani hapo kwa lengo la kuzuia magaidi hao , na kufanya maongezi kati ya mwanajeshi wa busonga na Tanzania kukatishwa
" aaaaah ! si yale ya kutoka nchini Somalia !?" " eeeeh!!!!!!hayo hayo "
" duuuuh! poleni sana na hatutoweza kuwaruhusu mpitie tena huku Tanzania ni nchi ya amani sana hatutaki mtuchafurie nchi yetu " mwanajeshi wa Tanzania alizidi kuongea maneno yaliyowakera wale wanajeshi na kufanya kuanza kuingia mstuni humo wakiwa na hasira sana " linajifanya linaipenda nchi yake wakati hata wao linaweza kutokea la kutokea " aliongea mkuu wa msafara upande huo .
Walienda Kwa mwendo wa tahadhali sana kitokana na kujua njama za Al- kida kila hatua waliyokuwa wakipiga waliichunguza sana , mavazi waliokuwa wameyavaa yaliwazuia kuonekana virahisi sana hivyo wakawa wanatumia darubini kutazama mwelekeo na bahati njia ilikuwa nzuri hivyo walipanda mlima huo vizuri huku wakichunguza kila kona na kufanikiwa kuwaona Al- kida kiurahisi
" tujigaweni wengine mpitie huko wengine kule na sie hapa tuwazunguke "
" poa " wote walitii na kuchukua hatua walitawanyika kwa kunyata na hata mda mwingine walitambaa kama nyoka wakielekea eneo hilo " wote mikono juu mkigaidi nawapasua vichwa vyenu mala moja " mkuu wa msafara alitoa amri hiyo baada ya kuwafikia vijana watatu wa Rambo peter , Daniel na Denis waliokuwa bize na kuvuta sigara pamoja na kunywa pombe huku siraha zao zikiwa pembeni
Hawakuwa na ubishi zaidi ya kutii amri walikamatwa na kufungwa kamba na safari ya kutoka msituni ikaanza
" semeni wenzenu wako wapi !?" " hatujui " peter alijibu kwa kifupi na kumtemea mate mmoja wa wanajeshi hao hali iliyosababisha kuanza kushushiwa kichapo cha maana na mateso ya hali ya juu Kwa wote lakini hakuna alieweza kuongea ama kuelekeza ," hili la kuua tuu!" hata kabla hajamalizia neno lake alimpiga risasi ya kichwa peter na kuanguka hapo hapo
" haya nanyi semeni la sivyo nitawasambaratisha na ninyiiiiii!" mwanajeshi huyo aliongea Kwa sauti sana huku hasira zikianza kumtawala , akiwapiga kila sehemu na kufanya miili yao kulowa damu , hakuwa na huruma kama kuua kwake ilikuwa kazi rahisi sana .
Carlos aliekuwa juu ya mti eneo hilo hilo alikuwa akiona kila kitu na kufanya hasira yake iongezeke , alichukua mtambo wake wa kusambaratisha kila kitu na kuwaweka wote sehemu moja kisha aliseti mtambo huo na kuvuta kitufu cha kutokea shabaha na sauti kubwa ilisikika na kufanya wanajeshi wote pamoja na akina Dani kupoteza maisha yao hapo hapo
" mtanisamehe Daniel na Denis najua lazima mgeusema ukweli " aliongea hayo akiwa anashuka mtini na safari ya kumtafuta Rambo ikaanza akitumia Radio call iliyokuwa na uwezo wa kuzuia maongezi hayo kufika Kwa wengine waliokuwa nazo za tofauti .
******
Rambo alisubuli wanajeshi wote waondoke eneo hilo kisha nae alianza kupiga hatua kutoka eneo hilo baada ya kuhakikisha wote wameondoka na kujithilisha kuwa victor alikuwa amefariki aliumia sana lakini hakuwa na jinsi CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"nipo huku " Rambo aliongea kupitia radio call aliyokuwa nayo haraka haraka Carlos alielekea eneo hilo
" vipi wengine wako wapi !"
Ilibidi Carlos aelezee kila kitu hali iliyomuumiza sana Rambo hasa hasa alipomkumbuka Denis Mzee wa mabomu wanaume alitoa chozi lilochanganyikana na kamasi nyepesi nyepesi " so tumebaki wawili tu ?"
" ndio boss " .
Kwakuwa usiku ulikuwa umeanza kuingia na walijiaminisha kuwa wapo salama walishuka mtoni kuoga na kulala huko huko ili kuisubili kesho , wakiwa usingizini mala walistukia wamevamiwa na watu watano wakiwa wamevalia nguo za kianajeshi
" kueni wapole na siraha zenu ziwe chini hakuna kutisika " mmoja wao alisema huku mwingine akiinama kuchukua siraha ya Carlos iliyokuwa pembeni yao , kitndo kilichomkera Rambo kuona siraha hiyo imara ikichukuliwa kirahisi rahisi , alinyosha mkono wake na kuchukua bastora yake aliyokuwa nayo kiunoni na kuanza kurusha risasi za hovyo huku mkono mwingine akinyanga'nyana na mwanajeshi huyo ile mashine hatari , lakini mwingine alimpiga shaba ya kifua upande wa kulia na kuangukia mtoni , huku akitoa sauti ya uchungu " yalaaaa!!", mto uliokuwa mkubwa sana na wenye mamba na majabari makubwa achilia mbali kasi kubwa ya maji.
"Nawe nakumalizia" mwingine alimuua Carlos kisha walitoa taarifa ya msaada Kwa wanajeshi wa majini kuja kumfatiria Rambo waliokuwa wakimuhitaji sana awe hai ama la .
******
Baada ya wanajeshi hao kulejea mjini mission na habari mbaya ya kifo cha msaidizi wa jeshi na taarifa za kuuliwa Kwa wanajeshi wake , kikao cha haraka haraka kiliitishwa kikishirikisha viongozi wote wa ngazi ya juu akiwemo balozi wa Tanzania madomTeddy na mkuu Wa jeshi la wananchi BUSOGA ( J WB)Mr Njawi pamoja na mpelelezi wa serikali Mr Steven akiwemo na amri jeshi mkuu mheshimiwa Robson raisi Wa nchi ya BUSOGA .
Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kuhitaji msaada wa jeshi la Tanzania , kwakuwa Tanzania ilikuwa nchi isiyokuwa na kinyongo na nchi yeyote ilikubali kutoa msaada Wa wanajeshi watano baada ya balozi Wa Tanzania madom Teddy kuongea na raisi wake mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete hivyo wanajeshi hao wakaianza kazi hiyo usiku wakiongozwa na Mr Njawi na kufanikiwa kuwakamata Al- kida waliokuwa wamesalia .
Maji yalikuwa mengi sana yakienda kwa kasi ya hali ya juu, lakini hayakuweza kumzamisha kutokana na mafunzo ya kivita ndani ya maji aliyokuwa ameyapita nchini Somali makao makuu ya Al- kida , hivyo aliweza kuogerea kufuata mkondo wake , japo hakujua ni wapi alikokuwa anaelekea, Rambo aliendelea kuogerea , mda mwingine aliweza kujipigiza katika majabari makubwa yaliyokuwemo humo na hata alikoswa koswa sana kukamatwa na mamba pindi alipowavamia eneo walilokuepo.
Maumivu ya risasi aliyokuwa amepigwa sehemu ya kifua kwa juu karibia na bega hakuyasikia tena kutokana na gazi iliyokuwa imesababishwa na maji baridi ya mto huo , hivyo aliweza kuogerela bila shida , hakujua nini kilitokea kwa Carlos japo mda mwingine alitamani kurudi na kumtafuta Carlos lakini roho nyingine ilikataa , hadi kunaelekea kupambazuka alikuwa bado ndani ya maji na alikuwa ametembea umbali mrefu , CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" nyie yule pale sio mtu !
" yuko wapi !?" aliuliza mmoja wa wanawake waliokuwa wakiteka maji mtoni hapo asubhi sana , japo palikuwa na kigiza giza flani lakini mboni za macho yao ziliwaruhusu kuona vizuri baadhi ya vitu " twendeni tukamuone " wote watatu walianza kupiga hatu kuelekea upande aliokuwepo Rambo ambaye hadi mda huo alikuwa nusu mwili majini na nusu mwili mchangani , Kwa mbali sana aliweza kusikia kama sauti za watu wakizungumza eneo hilo lakini hakuweza kuongea ama kufanya chochote kutokana na kuzidiwa na baridi na hata nguvu zilikuwa zimemwishia
" masikin " mmoja wa wale wanawake aliongea neno hilo kwa hudhuni na uchungu baada ya kumuona Rambo akiwa katika hali mbaya , haraka haraka walianza kumvuta kutoka ndani ya maji huku mwingine alikimbia kuelekea kijijini kutoa taarifa , kwa kuwa hakukuwa mbali sana dakika chache tu wanakijiji walikuwa wamefurika eneo hilo , wanaume walijitolea kumbeba msobe msobe hadi nyumbani Kwa mwenyekiti huku huduma ya kumtibu ikiendelea , Kwa kuwa hakuwa katika hali mbaya sana aliweza kujitolea risasi yeye mwenyewe japo aliumia sana na kufanya watu wamshangae sana
" huku ni wapi ?
" mtwara Tanzania ?" alijibu mwenyeji wake na kumfanya Rambo astuke sana hakutegemea kama angejikuta eneo hilo , lakini moyoni alishkru kuwa salama , japo wakazi wa kijiji kile walitaka kujua nini chanzo cha yeye kuwa pale aliwadanganya kuwa alitekwa na majambazi ambao walimchukuria kila kitu na kumtupia majini , walimhurumia sana na roho ya huruma iliwaingia hivyo waliitisha mkutano asubhi hiyo hiyo , kikao cha kimchangia nauri Kwa ajiri ya kurundi nchini kwao ,.
Rambo hakutaka kubaki pale kwani alihisi mda wowote angeweza kukamatwa ,saa 2: 30 alianza safari ya kutoka kijijini hapo hadi mtwara mjini akisindikizwa Kwa baiskeri na kijana mmoja , japo alikuwa akihisi maumivu ya hali ya juu sana kutokana na kidonda alichopigwa na risasi jana yake eneo la juu kabisa katika kifua chake lakini alijikaza kiume na kujivika sura ya uzima , alifika mtwara mjini na kubahatika kupata basi lilokuwa likielekea Dar es salama moja kwa moja alifuata utaratibu kisha aliingia ndani ya basi aina ya SUPER DAR na kusubili safari ianze huku akiwa na mawazo lukuki ya kulipiza kisasi .
Kumbukumbu ya maneno aliyoyasema katika kaburi la mama yake yalianza kuzunguka katika kichwa chake na kusababisha aanze kulia taratibu.
******
" Eeeeh!, coplo Marwa anaongea hapa !" ulisikika upande wa pili wa radio call
" tunahitaji watu wanatakao ogelea mtoni humu , kumfatiria huyu gaidi "
" bwana Machota mida hii haitawezekana mpaka kesho asubuhi maana sasa kuna giza na isitoshe huo mto una mamba wa kutosha hebu ongea nao waeleze hivyo " aliongea mwanajeshi aliekuwa zamu siku hiyo .
" daaah ! inawezekana jamaa halijafa hebu tulifatilie Kwa kupitia kando kando "
" hapana Njawi zoezi hili lifanyike kesho " japo hakuridhika na majibu hayo hakuwa na jinsi ilibidi akubaliane nao maana hata huo msaada wa kesho walikuwa wakiuhitaji sana , hivyo walirundi ndani ya helkopita iliyokuwa mita chache kutoka hapo wakiwa na wazo la kumtafuta Rambo kesho yake.
Wanajeshi walikuwa wamefurika eneo lote la mto huo wakimtafuta Rambo Kwa udi na uvumba huku wengine wakiwa ndani ya maji , hadi inafika saa tatu na nusu walikuwa hawajampata na walikuwa wametembea umbali mrefu sana , japo wanajeshi Wa Tanzania walikuwa wameanza kukata tamaa na baadhi yao walianza kuondoka eneo hilo wakipitia ndani ya vijiji.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" masikini watu wanaroho mbaya sana , yaani mtu anahangaika kutafuta wen yewe wanataka kuchukua kirahisi rahisi tu" " eti yaani baba wa watu walitaka kum...., hiyo nchi ni mbaya sana" , yalikuwa mazungumzo ya akina mama waliokuwa wakielekea shambani ambayo yaliweza kupenya ndani ya ngoma za masikio za wanajeshi waliokuepo eneo hilo , hali iliyosababisha kuvutiwa na maongezi hayo , iliwaladhimu kuulizia , Kwa kuwa walikuwa hawajui chochote walijikuta wakielezea kila kitu na kuwafanya wanajeshi hao kutoa taarifa Kwa mwenzao.
" ameondoka saa ngapi !?"
" asubhi sana ila mnaweza mkampata maana hata kijana aliempeleka bado hajarudi" alizungumza mwenyekiti Wakijiji hicho baada ya kuelezwa ukweli wote
Wanajeshi hao hawakuwa na mda Wakupoteza walirudi ndani ya helkopita zao na safari ya kuelekea mtwra mjini ikaanza Mara moja huku wakiwa wametoa taarifa Kwa jeshi la polisi na amri ya kukagua kila gari lilokuwa linatoka humo,.
Helkopita zilichukua dakika tano tu kufika mtwara mjini hata kabla hazijatua vizuri chini teyari wanajeshi karibia wote walikuwa wapo chini huku siraha zao zikiwa mikononi hakika ilikuwa kama kamchezo ka kuigiza kila mtu aliekuepo hapo alitumbua macho yake na kuiruhusu akili yake kuwaza nini hiko ,
Haraka haraka walianza kukagua kila gari kubwa ama dogo wakiongozwa na mkuu wa jeshi la Busoga mr Njawi na wengine waliokuwa wakimfahamu , jeshi la polisi nalo halikuwa nyuma lilihakikisha nanapatikana , haikuishia hapo walitoa machapisho ya picha yake katika vikaratasi na kuvibandika kila kona ya mji ule vikiwa na maandishi meusi yaliyosomeka " GAIDI HUYU NI HATARI SANA ANATAFUTWA, ZAWADI NONO ITATOLEWA KWA ATAKAYE FANIKISHA KUKAMATWA"
Yalikuwa maandishi makubwa sana na yenye kuoneka kwa kila mtu , ambayo yaliandikwa chini ya picha ya sura yake na kufanya kasi ya utafutaji kuongezeka , taarifa ziliendelea kusambaa hadi jijini Dar es salama kukafanya askari na hata wanajeshi kutanda barabarani wakiwa na kazi ya ukaguzi achilia mbali picha ya sura ya Rambo wakiwa nazo mikononi
" hebu wote shukeni chini naanza na dereva kisha kila mtu apite mmoja mmoja , wenye mashungi mtoe na wenye kofia nao hivyo hivyo !" aliongea askari aliekuwa akikagua basi lilokuwa likielekea Dar aina ya SUPER DAR , kwakua ilikuwa ni sheria hakuna aliebisha japo baadhi ya wanawake waliokuwa wamefunga walianza kunung'unika nung' unika mioyoni mwao kuwa hawatendewi haki maana kilikuwa kipindi cha Ramadhani hivyo kutolewa nguo zao na kuonewa na wanaume ilikuwa ni kitu kibaya sana katika imani zao lakini hawakuwa na nguvu za kupinga hilo , hadi watu wote wanaisha ndani ya basi hilo Rambo hakupatikana wakawa wameliruhusu kuendelea na safari yake.
" Eeeeeh coplo marwa niambie !"
" kuna basi la SUPER DAR linakuja huko inasemekana huyo gaidi ndo amepanda humo hakikisheni mnakagua vizuri na ikiwezekana muangalie hadi chini ya viti!, aliongea mkuu wa jeshi la Busoga
" kumbe sio Marwa bwana Njawi hilo basi limepita hapa kama dakika kumi hivi ila hakuemo huyo gaidi "
" aaaaash!!, mlifanya ukaguzi mzuri kweli ?"
" duuuuh! sio sana lakini usijali wacha niwasiliane na bwana Mwita ambae yupo kituo kinachofuata huyo jambazi lazima akamatwe tu" , baada ya kumaliza kuingea na bwana Njawi alimpatia taatifa hiyo coplo mwita aliekuwa kituo kingine kilomita tano tu kutoka hapo nae akawa amewaeleza wezake .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" acha ukaidi paki hapo haraka " coplo Mwita kutoka mkoa wa Mara kijiji cha Loylia aliongea huku akiwa ameshikilia sawa sawa silaha yake mkononi , alitoa amri ya abilia wote kutoka mmoja mmoja huku akisaidizana na wanajeshi wenzake pamoja na polisi " wewe hebu toa hiyo kofia "
" aaaah ! kichwa kibovu na kinauma siwezi " alizungumza mmoja wa abilia aliekuwa wa mwisho kutoka humo , huku kichwa chake amekiruhusu kutazama aridhi , kitendo cha yeye kukataa kutii amri hiyo kiliwafanya wanajeshi na askari wote kumzunguka
" jamani mimi sie !" alilalamika kwa sauti ya kigonjwa kigonjwa baada ya kuvuliwa kwa nguvu kofia yake , walimkagua kagua na kufananisha fananisha na picha ile lakini hakuwa Rambo , haraka haraka walingia ndani ya basi hilo na kuanza kukagua kila sehemu hadi juu ya gari hilo lakini hakukuwa na Rambo wala harufu yake wote walisitajabu na kuona kazi ni ngumu japo walidhani ni nyepesi sana , walitoa taarifa kwa wenzao nao hawakuamini hivyo wakawa wameriluhusu basi hilo kuendelea na safari na ukaguzi katika vituo vingine.
******
Rambo alikuwa amekaa siti ya tatu toka mwisho upande wa dereva huku akiwa na mawazo lukuki yaliyokuwa yakipita kichwani mwake kama matangazo ya taarifa ama biashara yapitavyo katika television chini kabisa , roho ilikuwa ikimuuma sana kupoteza nafasi ya kulipiza kisasi , akiwa katika lindi la mawazo huku basi likiwa linatembea alishangaa kuona sura yake katika karatasi la mmoja wa abilia alieingia humo kituo kimoja baada ya kutoka stendi , mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi huku miguu ikimtetemeka , haraka sana alikiinamisha kichwa chake katika kiti huku uso wake akiufunika kwa gazeti alilokuwa ameazima ,
Akiwa katika hali hiyo alishangaa kuona basi hilo likisimama na idadi kubwa ya wanajeshi na askari polisi wakiwamuru abilia wote washuke , Rambo aliendelea kubaki pale pale hadi walipokaribia kuisha haraka haraka alizama chini ya uvungu wa kiti na kutulia , hadi zoezi linakamilika alikuwa chini ya viti na bahati nzuri askari hao hawakuingia ndani kukagua akawa amepita kwa namna hiyo kituo cha kwanza , baada ya kutoka hapo mita chache alinyanyuka huku akiwa ameshika tumbo akiashilia kuumwa " dereva tumbo , tumbo nataka nikajisaidie "
" aaaah ! , acha maswala ya kis*** e, tumesima hapo tu , tutasima huko mbele !, dereva huyo aliongea bila hata kumtazama usoni
" nisaidie mshikaji " safari hii alikuwa amekaa chini akiendelea kujinyonga nyonga " jamani msaidie atatuhalibia hali ya hewa humu!!!" zilikuwa sauti za abilia ndo zilizomshawishi dereva yule kusimamisha gari na Rambo alishuka akiwa katka hali hiyo hiyo " dakika tano tu , na uache kula hovyo hovyo " aliongea dereva kwa sauti na kufanya baadhi ya abilia kuangua kicheko.
Rambo alizunguka nyuma ya basi hilo na kuzama katika kichaka na kutulia humo , japo alikuwa akisikia honi za basi hilo hakuthubutu kutoka , ilibidi basi liondoke na kumuacha Rambo akiwa hapo ,
Nusu saa kupita alisikia mlio wa gari la wagonjwa mahutihuti likija eneo haraka haraka alitoka humo na kuelekea barabarani , alifika na kulala katikati huku mkono mmoja akipunga hewani kuashilia lisimame .
Rambo alizunguka nyuma ya basi hilo na kuzama kichakani huku akisubilia nini kitafuatia , aliendelea kuwa humo hadi basi lilipoondoka baada ya kumsubili Kwa mda mrefu na isitoshe dereva alipiga honi za kutosha . Nusu saa kupita alisikia mlio wa gari la wagonjwa mahututi haraka alitoka kichakani humo na kuelekea barabarani na kulala .
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Twende pamoja...
Ukaguzi ulikuwa mkali sana na ulizidi kuogeza kasi hasa hasa Kwa wanajeshi Wa Tanzania ambao hawakutaka kumpa nafasi gaidi huyo hatari waliekuwa wamesikia story yake kuwa akiamua kuchafua nchi ni dakika kumi tu, lakini alichokifanya ni kikubwa sana hivyo hawakupenda gaidi huyo aingie Dar kirahisi rahisi .
Hakuna gari iliyopita bila kukaguriwa walihakikisha wanashusha watu wote na kukagua, kila sehemu inakaguliwa hata pale palipoonekana binadamu hawezi kukaa.
" huyu gaidi hatari sana haonekani !"
" jitahidini sana apatikane hadi ubungo napo mwepo , bila kusahau chalize, madafu, mbezi na kimara , na hata ikiwezekana na vituo vyote vikaguliwe , kila gari huko nalo mlikague hakikisheni anapatikana leo hii hii"aliongea mkuu wa majeshi waTanzania baada ya kupewa taarifa na wakubwa wa jeshi waliokuepo katika msako huo
Mji wa Dar es salaam na Mtwara ulikuwa umetapakaa wanajeshi hakika ilikuwa kama vita , wananchi watembea Kwa miguu walizuiwa kupita barabara ya morogoro road hali iliyoleta taflani Kwa wakazi wa mji ule
" pipiii pipiii!, pipiii, " ulikuwa ni mlio wa gari la wagonjwa lilokuwa likiomba njia ili limuwahishe mgonjwa aliekuwa katika hali mbaya
" paki gari hapo shelhe "
" jamani tunawagonjwa wenye hali mbaya sana hivyo kuendelea kukaa hapa kunaweza kuathili maisha yao " aliongea dereva huyo huku akiwa anasereresha gari lake pole pole
" fungueni tuwasarch fasta ni dakika mbili tu "
" itakuwa ngumu Afande kama hamuamini fatanen na sisi huko muhimbili ila hapa no " shelhe yule aliongea huku akitia gia na kuondoka hadi anafika kimara mwisho alikuwa amepitia msuko suko wa nguvu , hakupata shida kutoka hapo hadi muhimbili na kuwashusha wagonjwa wake .ambapo maaskari waliokuwa wamefatana nae walimkagua kila mgonjwa lakini Rambo hakuwemo walizidi kuchoka akiri zao.
Hali ya mheshimiwa Robson raisi Busoga ilikuwa mbaya , alijihisi maumivu makali ndani ya moyo wake achilia mbali plesha ya kupanda na kushuka na kichwa kumgonga sana japo alijitahidi sana kunywa maji ya kutosha na dawa za kipunguza maumivu lakini hakufanikiwa kila mda alikuwa akibadili Chanel za TV angalau aweze kukutana na tangazo lolote la kukamatwa Kwa Rambo lakini haikuwa hivyo , simu yake ilikuwa bize mda wote alikuwa akizungumza na watu wake kuhusiana na swala hilo , hadi unaingia usiku hakuwa amepata taarifa yeyote kuhusiana na kukamatwa Kwa Rambo .
" nyie masister hebu pakini hapo gari lenu " aliongea coplo Mwita ambaye alikuwa kituo kimojawapo njiani humo usiku huo , sauti hiyo iliwafanya wote watetemeke na mapigo ya moyo yakienda mbio maana huko nyuma walipita bila wasiwasi na hakuna aliewashakia kutokana na heshima hiyo ila walipokutana na Mwita jamaa kutoka rolya Mkoani Mara hakujali cha usisita
Mikono ya dereva ilishindwa kupaki vyema gari hilo na kuhisi likimdhinda lakini alifanikiwa .
" jamani sisi ni watumishi wa mungu hatuna kitu kibaya "
" nani kakwambia kuwa wengine watumishi wa shetani"
" tena ninyi ndo wachafu sana mnatumia dini kigezo cha kufichia maovu yenu " coplo Mwita alizungumza huku akifungua mlango wa gari " haya wote chini " alitoa amri na masister hao walianza kushuka mmoja mmoja lakini wakiwa na woga mkubwa
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" Haraka acheni kulegeza miguu !" aliongea coplo Mwita huku akiwamlika Kwa kuruzi yake kubwa aliyokuwa nayo " mnaenda wapi usiku huu !?"
" tumetoka kuchukua chakula cha wanafunzi mtwara na tunaenda Dar es salama " aliongea mmoja wa masister aliefahamika kwa jina la sister Magdarena , msaidizi wa shule ya st marry iliyoko Mbagala.
" kiko wapi hich Chakula !?" aliuliza huku akizunguka nyuma ya gari hilo kumfuata sister magdarena aliekuwa ametangulia
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment