Simulizi : Jela Ni Haki Yangu
Sehemu Ya Nne (4)
" toa huo mfuko wa juu "
" jamani hakuna kitu ni mahindi tu na maharage " alijitetea
" poa endeleeni na safari , kuna gaidi linacheza na akiri zetu ,!"
Walitoka eneo hilo wakiwa hawamini kama wangepita salama kutokana na kuhisiwa kama walikuwa na kitu kibaya
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" asanteni sana na mungu awatangulie ila ninaomba msaada mmoja mniazime Nguo zenu !" aliongea mmoja wa abilia
" sheria na kanuni za kanisa letu ,haziruhusu msaada tuliokupa unatosha" waliwasha gari na kuondoka wakimuacha mtu huyo
******
Rambo aliendelea kupunga mkono hewani kuashilia gari hilo lisimame lilokuwa linakuja kwa kasi ya ajabu , kutokana na umakini wa dereva yule aliweza kumuona Rambo hivyo akawa amepunguza gari mwendo kabla ya kusimama
" vipi ww "
" nipeni msaada naelekea dar ,"
" na huku " ilibidi Rambo atoe maelezo ya kiongo kwamba aliachwa na basi na hakuwa na nauli alijenge picha halisi ya tukio " gari halina nafasi ila chukua hii itakusaidia Kwa ajili ya nauli " dereva alitoa. noti mbili za elfu kumi kumi na kumkabidhi Rambo kisha aliwasha gari na kuondoka
" lakini mbona huyo jamaa kama yule anaetafutwa"
" hapana duniani wawili wawili itakuwa umemtazama vibaya yalikuwa ni mazungumzo kati dreva na nesi wake .
Rambo hakuta kubaki barabarani haraka haraka alirudi kichakani humo na kuipanga vizuri hakiri yake
" Boss unajua siku moja inaweza ikatokea mmoja wetu akabaki peke yake !"
" oyaaaa acha maswala ya kitwana hapa jisemee mwenywe Mimi sifi hadi kieleweke " aliongea Peter aliekuwa amekaa juu ya jiwe
" ila kweli !". " Dan acha kuunga mkono hujui ,". " ukiwa na njaa unaweza kula hata mizizi ya miti kutokana na kukabwa na njaa " ilikuwa kumbukumbu iyopita ndani ya kichwa chake siku tatu nyuma .
Aliumia sana pindi alipowakumbuka vijana wake hasa hasa Dan bingwa wa kutabili na Mzee wa mabomu , kutokana na njaa yaliyokuwa nayo alifakamia mizizi ya miti iliyokuwa hapo na kuifanya chakula huku akiwa ameivuta sura Kwa uchungu na maumivu yaliyochanganyikana na uchungu wa mizizi hiyo .
" yaaani mwanagu usije ukakata tamaa , na kumuacha huyu fala akaendelea kuumiza wanainchi komaaa hadi mwisho "
" katika point zote ulizosema hiyo ndo point , sio kuongea mipumba pumba " aliongea Carlos aliekuwa bize na kitafuna mirugi
" pigana!! pigana!! mwanaume daima hashindwi , komaaa mwanangu " Dan aliendelea kuongea huku akimpiga piga Rambo kifuani
Shit !!," alilopoka Rambo neno hilo baada ya kutoka katika lindi la mawazo hayo , " lazima afe , amechangia kuua hata vijana wangu hapana !" aliongea Kwa hasira huku akipiga piga mti uliokuepo hapo kwa hasira , hakujali maumivu yaliyokuwa akiyasikia kutka jeraha lake
Aliendelea kuwa eneo hilo akiusubili usiku aweze kuondoka , akiwa bado eneo hilo na kigiza kilikuwa kimeanza ghafla alisikia nyayo za mtu akija eneo hilo , haraka alisimama kumtazama
" ooooh! sister " Rambo aliongea na kumfanya sister astuke sana na kutoka kukimbia " ninashida nahitaji mnipeleke huko mnakokwenda " alianza kujieleza huku akiwa amepiga magoti
" oky twende kwenye gari nikazungumze na wenzangu " aliongea sister huyo alieelekea eneo hilo Kwa lengo la kujisaidia alijikuta haja ikipotea
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" sawa lakini kwanini unataka tukuweke kwenye Chakula " sister Magdarena alizungumza baada ya kusikia ombi la Rambo " nyie mficheni humo humo tunachelewa " walikubaliana na ombi la Rambo na safari ikaanza huku Rambo akiwa ndani ya mahindi na kufananani na mzigo hiyo .
Waliweza kupita vituo vingi bila kikaguliwa na hata walipokutana na Coplo Mwita Rambo alikuwa humo , Mwita alipuuzia kufungua majunia yote , hivyo wakawa wamesafili nae hadi mbagala akiwa hajui pa kuanzia .
Hadi kunakaribia kupambazuka raisi wa nchi ya Busoga alikuwa macho akikodolea TV yake , mda mwingine aliwasumbua sana viongozi wa ngazi za juu hususani wazili wa ulizi na usalama alipata shida hadi ilifikia kipindi akawa amemzimia simu
" hili litoto ni la nani kati ya wote niliotembea nao , ...mmmh!!!, na linanijua kweli sura mbaya kichizi mama yake ni yupi!?," alikuwa mheshimiwa Robson akizungumza na picha ya Rambo iliyokuwa mbele yake , huku machozi ya hasira yakijichora katika mashavu yake , ambayo yalikuwa manene kiasi kutokana na kutapanya Mali za wananchi waliokuwa wakilala njaa , kukosa huduma muhimu za jamii na memgi .
"nitaliua iwe isiwe lazima life maana nadhani linajua hata siri zangu , matoto mengine hayana hata adabu kwa baba zao". Aliendelea kukiadhibu kichwa chake pamoja na hakiri yake kutokana na mrundikano wa mawazo mia mia
" eeeeeh wacha niongee na Maja!" alipata wazo " haraka alinyanyuka na kutoka eneo hilo na kuifaata compyuta yake na kuanza kusarch sarch kisha alifanikiwa kuliona jina la Maja raia wa urusi jambazi na mwizi hatari .
Bahati nzuri alikuta yuko online
" Mr Ganga Majaaa, habari za usiku huu " ilikuwa SMS ya Robson iliyotumwa kwa Maja na kusubili jibu kutoka kwake
" ndio mwanaume vipi hulali !???" nae alijibu ila Kwa lugha ya kingereza na kumfanya Robson kutoa meno yote nje baada ya kuiona sms hiyo juu ya kioo cha compyuta yake , hakuta kupoteza mda ilibidi amweleze nia yake na kipi alikuwa akihitaji kutoka kwake.
" hahaha !, hiko ni kitu kidogo sana kwangu so huyo gaidi yuko wapi !?,"
" Nimesikia amekimbilia Tanzania nchi jirani na yangu " alizidi kutoa maelezo huku moyo wake ukiwa umeanza kupata furaha ya ajabu
" oky nipe mda wa kufanya mambo yangu nimchunguze yupo eneo gani nitakujibu masaa sita baadae" alitoa jibu hilo na kufanya Robson aangue kicheko cha furaha
" oyaaaa uko wapi nawewe twende tukale matunda ya nchi"
" fasta mheshimiwa nipo Jisangu club vipi nije " yalikuwa ni maongezi kati ya raisi wa nchi hiyo na makamo wake ambao matendo yao na matumizi yao ya lugha hayakufanania na heshima zao .
Hakuwa na mda wa kupoteza aliingia chumbani kwake alionga na kuondoka huku akimuaga mke wake kuwa alikuwa amepata dharula ya ghafla sana na yenye umuhimu , laiti angejua angelia sana .
" bwana mkubwa hebu niambie umefikia wapi !?" aliuliza baada ya kukaa ndani ya chumba alichokuwemo makamo huyo ambaye mambo yake alikuwa akiyafanya kwa siri sana na hata Robson alikuwa hivyo , hawakuacha kuwa na wasichana zaidi ya mmoja huku meza zikiwa zimejaa aina tofauti tofauti za vinywaji
" huyu lazima akwishe tu ninampango mzuri sana " aliongea huku akizingusha mikono yake katika kiuno cha mwanamke aliekuwa hapo
" kiaje ???"
" nimeongea na mpelelezi toka urusi anakuja kufatilia swala hilo na ni jamaa mzuri sana " alitoa maneno ya kiongo kutokana na kutomwamini hata yeye " basi sawa "
Saa kumi na mbili asubuhi walitoka ndani humo na kila mtu alielekea kwake wakiwa wameacha maelekezo Kwa mabausa wao kuwaua wanawake walio nao ili wasitoe siri kutokana na tabia ya baadhi ya wanawake kutokutunza siri , na isitoshe waliogopa kunadiwa na vidada hivyo .
******
Historia ya Maja ama Ganga Maja kama alivypenda kujiita ,Maja alizaliwa nchini marekani baada ya wazazi wake kuchukuliwa kitumwa na wamarekani kwenda kulima mashamba ya miwa huko ,
Aliishi Marekani Kwa mateso sana kutokana na kuwa peke yake kwani wazazi wake waliuliwa na wazungu hao baada ya kuzidiwa na mateso hivyo wakawa wamegoma hali iliyosababisha wamarekani hao kuwapiga risasi na kumfanya Ganga Maja kuwa yatima akiwa na miaka Tisa .Uyatima wake na udogo wake haukuwafanya wamarekani hao kusitisha mateso na manyanyaso Kwa Maja hali iliyopelekea atoroke shambani humo na kuzama mitaani alikoishi Kwa mateso na manyanyaso kutoka Kwa polisi wa kimatekani pamoja na raia
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maisha ya mtaani yalimfundisha tabia tofauti tofauti zikiwemo za kuiba , kivuta bagi pamoja na kuuza madawa ya kulevya na hata mda mwingine alitumiwa kama begi la kusafirishia madawa hayo ambapo alikuwa akichanwa tumbo lake na kujazwa uga kisha anasafilishwa hadi Africa akiwa ndani ya jeneza kama maiti ,
Huku akiwa amedugwa madawa ya usingizi ndani ya jeneza.
Kutokana na umasikini na miundo mibovu ya usalama katika viwaja vya ndege vya Africa Maja aliweza kuingizwa Africa na kupata chake maana kila safari alikuwa akipewa asilimia thelasini na tano ya mauzo yaliyopatikana huku huduma zingine zikiwa juu yao yakiwemo marazi , usafiri na matibabu , japo alikuwa anapunjika sana .
Maja alifanya kazi hiyo hadi alipompindua boss wake raia wa marekani Kwa kumuua kisha alihamia nchini kwao akiwa tajiri mkubwa sana na muuzaji mzuri Wa madawa , jambazi sugu asie na huruma .
Kwa kuwa ilikuwa usiku na ni Mgeni wa mji ule Rambo hakuwa mjanja Kwa lolote zaidi ya kununua mavazi yatakayo mfanya kupoteza muonekano wake , kisha alipiga hatu hadi kituo cha daladala cha rangitatu na kutulia hapo huku akiwa anatathimini jinsi ya kutoka humo salama ,.
Hakupenda kuongea na mtu kwa hofu ya kukamatwa maana kila kona ama nyuma machapisho ya kutafutwa kwake yalikuwa yamebandikwa .
Siku iliyofuata alielekea kariakoo alikokuwaga amepata historia yake kutoka kwa Carlos .
Kutokana na kuwa mzoefu katika wizi hakuweza kupoteza mda alianza mara moja kukwapua kwa wadada ama vijana ili tu apate nauli ya kumpeleka Somali kujifua tena Kwa ujio mpya .
Wiki tatu alikuwa ameshapata pesa kuw wa ajili ya nauli hivyo akawa anajiandaa kwa safari " oyaaaa!, mala ya mwisho kushika laki tano ni lini mwanaaa!?"
" mmmmh !, sijui kwani vipi !?"
" lipo dili hapa tamu kishenzi , tukifanikisha tumeula "yalikuwa ni mazungumzo kati ya Hasan na Husen vijana waliokuwa wakiishi mtaani kwa kazi ya kupora , kuvuta bagi na kila aina ya uchafu " unamcheki yule jamaa alieagusha pale ndo anaetafutwa na siafu pamoja na wababe"
" eeeeh!!" Husen alishangaa huku akinyanyuka na kukaa kitako " kweli !??, twende msimbazi wangu " teyari alikuwa ameshasimama
" Dogo tulia huyo jamaa sio wa kupaparukia , ni mshari kinoma anacheza na miguu ya kuku kama mpira sie wenyewe ni wazee wa viwembe na visu , wangu tutaenda kesho na lazima aende mmoja sio kukurupuka atachoma kariakoo yote!" Ilibidi Hasan amueleshe Husen aliekuwa ameshawakwa na tamaa ya pesa .
Baada ya kupambazuka hawakuta kupoteza mda Husen alielekea kituo cha polis na Hasan alibaki akimuwinda winda Rambo kila alikokwenda , Siku hiyo ndo ilikuwa ya Rambo kuondoka Tanzania hivyo alitafuta sehemu ya huduma za kujisafisha na baada ya hapo alianza safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere huku nyuma akiwa anafatiliwa na Hasan pamoja na Husen aliekuwa ndani ya gari la polisi nao wakielekea huko .
******
Maja ama Ganga hakutaka kupoteza mda usiku huo huo alizama katika chumba chake cha mitambo na kukaa katika moja ya kiti akitazamana na compyuta aliwasha na kuanza kuitafuta Tanzania dakika tatu teyari alikuwa ameshaipata , kisha aliitafuta Dar es salama , na baadae mbagala hakuishia hapo aliweka jina la Rambo akiwa ameambatanisha na picha yake haikuchukua mda akawa amempata Rambo alitoa tabasamu kutokana na uwezo wa mitambo yake ya kisasa
" he is a simple person( ni mtu rahisi sana )" alizungumza hayo akiwa anatoka ndani ya chumba hicho kilichokuwa na mitambo ya kuonesha dunia nzima CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" mtu wako ameshaingia Tanzania na sasa yuko kariakoo"
" what!!? ( nini !!?)"
" yaah!!, usishangae na nikijitu kidogo sana kwangu " aliongea Maja Kwa kujiamini huku akilainisha koo lake na wisky " so utatusaidieaje !?" Robson aliuliza Kwa haraka sana " nimesha mseti kila anachofanya nakiona na wiki tatu zijazo nitakuwa Africa hasa hasa Tanzania hivyo nanyi mjiandae.
" kesho muwe Tanzania asubhi sana nimemuona akikata tiketi ya ndege nadhani anataka kutoroka nami naanza safari sasa kwa ndege yangu " alikuwa Maja akizungumza na raisi wa nchi ya Busoga huku akiwa anajiandaa kwa safari .
Saa mbili za asubhi alikuwa akitua katika uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere huku akiwa anafatilia kila kitu kilichokuwa kinaendelea upande wa Rambo toka alipoanza safari yake ya kutoka kariakoo , namna alivyo kuwa akingia ndani ya uwanja huo kufuata taratbu zote , pia hakuwa nyuma kimazungumzo na wanajeshi wa Busoga waliokuwa teyari uwanjani hapo wakifuata maelekezo yake .
Rambo hakutaka kupoteza mda baada ya taratibu zote kukamilika alianza kupita hatua kuelekea ndani ya ndege lakini kabla hajaingia alishangaa kuona wanajeshi wakija upande wake , aligeuka haraka kurudi ilikotoka lakini nako alikutana na askari waliokuwa na siraha mikononi wakija eneo alilokuepo kulia Maja na vijana wake wawili , hivyo akawa amewekwa katikati asijue la kufanya
Dakika mbili ulisikika mlio wa helkopita iliyokuwa ikitafuta uelekeo wa kutua , hata kabla ya kutua vyema waliruka vijana saba na kuanza kukimbia kuelekea ndani ya uwanja huo.
Al- kida lilikuwa kundi kubwa sana lilokuwa limetapakaa karibia nusu dunia na lilikuwa likifanya kazi Kwa kushilikiana kila kona na kufanya liwe imara sana ,
Kutafutwa Kwa Rambo ambaye ni kijana wa kundi hilo kulifanya Al- kida wa somalia kuja kumuokoa maana taarifa ilikuwa imezagaa pande zote za kundi hilo , .walifatilia ni wapi alikokuwa na walipongundua hawakuwa na mda Wa kupoteza walisafiri moja Kwa moja hàdi Tanzania na bahati ilikuwa kwao siku hiyo hiyo walibahatika kumuona Rambo akiwa katika harakati za kukamatwa tena.
Wepesi wa miili yao pamoja na mavazi waliokuwa wamevaa hayakufanya wajulikane mapema hivyo waliweza kupita na kuingia ndani bila wasi wasi , askari waliokuepo getini walifikilia ni moja ya watu waliokuwa wameambatana na Maja .
******
Hali ilikuwa ya kutisha eneo lote la uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere jijini dar es salaam , wanajeshi walikuwa wametapakaa eneo lote si wa Tanzania pekee bali hata wa nchi ya Busongo ,achilia mbali jambazi wa kimataifa Maja na vijana wake , wananchi waliokuwa eneo hilo walibaki na sitofahamu wengine walianza kukimbia kuondoka eneo hilo na hata huduma zilizokuwa zikifanyika hapo zilianza kudorola macho na masikio ya watu yalikuwa yakifatilia tukio hilo la ghafla .
Rambo hakuweza kukimbia ama kufanya lolote alibaki ameganda kama maziwa mgando , roho ilianza kulia taratibu hasa alipotathimini picha ya gereza na mateso ya mahabusu ilianza kuonekana katika hakili yake , alijiona kama sisimizi mbele ya tembo japo aliamini ipo siku jela ingekuwa haki yake lakini iwe ameshakamilisha malengo yake ,
" wacha nipambane nao siwezi kukamatwa kipuuzi namna hii " aliwaza huku akijitayarisha kuwashambulia japo hakuwa na siraha yeyote zaidi ya kalamu
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" tafadhali tunakuomba ujisalimishe mwenyewe hatutaki tutumie nguvu " aliongea Maja kwa lugha ya kingereza hali iliyowashitua askari wa Tanzania ambao hawakumjua , " mimi ni mpelelezi toka urusi " alisema Maja huku akitoa kitambulisho " wapi !" Rambo alitamka hivyo na kuanza kukimbia kuelekea upande wa kushoto lakini mbio zake hazikuzaa matunda alipigwa risasi ya mguu iliyompelekea kudondoka huku akiachilia kilio cha maumivu , nao wanajeshi hawakuwa mbali walimkamata na kuanza kumvuta kuelekea nje.
" tafadhali tunamhitaji mtu huyo " mmoja wa wale vijana saba walioshuka kwenye helkopita aliongea huku akiwa amewalenga na siraha
" wewe nani " Maja aliuliza huku nae akiwa na siraha .
" hutakiwi kuj..." hata kabla yajamalizia sentesi yake walianza kuwashambulia akina Maja na wanajeshi , nao hawakuwa nyuma walianza kuwarushia risasi hivyo ikawa vita kati ya kundi la kigaidi la Al- kida pamoja na wanajeshi Wa Tanzania , Busoga pamoja na Maja ambao walikuwa kitu kimoja ,
" Twende " alimuaru mwanajeshi aliekuwa namvuta Rambo ambaye alikuwa amegoma kuondoka kutokana na kuona ukombozi umefika
Al- kida walikuwa wepesi katika kuruka na hata mapigano ya hewani walikuwa wazuri , mili yao ilikuwa membamba lakini yenye nguvu , istoshe walikuwa wamevaa vifaa vya kuzuia risasi hivyo hawakutetereka walizidi kuwashambulia na kusababisha mauaji mengi kwa wanajeshi na hata Maja mwenyewe alipigwa risasi ya bega akawa ametulia chini .
" hello angalia kule wanamtorosha !" Rasta aliongea huku akinyosha kidole kisha alianza kukimbia kama umeme akifuatiwa na Brown , lakini kabla hajafikia walimuona Rambo akitupiwa kama mzigo ndani ya deffender na safari ikaanza , Rasta hakutaka kupoteza mda aliipiga risasi tairi za deffender na kufanya liyumbe kabla ya kudondoka , Rambo aliekuwa makini sana aliona hali hiyo hivyo akawa ameruka ndani ya gari kabla halijadondo na Brown akawa amekamata na kuanza kukimbia kuelekea usawa wa helkopita .
Japo Rambo alikuwa ameumia mguu hakuwa nyuma kitka kukimbia huku wakiendelea kurushia risasi kila kona , .
" ingia ! ingiaaaa !!" Rasi alizungumza kwa sauti ya juu yenye maumivu makali kutokana na kupigwa risasi ya miguu , wengine walianza kumvuta Rambo aliekuwa hawezi kupanda ngazi za helkopita hiyo , dakika tatu walikuwa wamefanikiwa kuingia wote na helkopita ikaanza kunyanyuka taratibu lakini haikufika mbali ikawa imepigwa risasi katika matairi na kuanza kupoteza mwelekeo kabla ya kudondoka huku tairi zake zikianza kutoka Moshi .
Hali ya sintofahamu iliendelea kutanda eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius kambarage Nyerere kati ya pande zote mbili wanajeshi wa Tanzania na wale wa Busoga kutokana na kile walichokiona , macho yao na mioyo yao haikuamini kama vijana wale waliweza kuwazidi ujanja wanajeshi wa pande zote
" fuc**** you, i will kill them i swear upon am ..am( msh*** wew , nitawaua wote nahapa mi.)" Maja alikuwa akiongea kwa uchungu na maneno yasiyo ya maana baada ya kuziduka kutoka katika mshituko aliokuwa ameupata wa kupigwa risasi " take me to hospital now( nipeleke hospitali sasa hivi )" alizidi kumuamrisha kijana wake aliekuwa akimsaidia kunyanyuka pale chini huku nusu ya mwili wote ukiwa umetapakaa damu na kumfanya aonekane vibaya
" watu wa huku ni wazembe sana "
" yaaah! kweli hata mie nimegundua hilo (black person a fake ) mtu mweusi ni hafai )" walizidi kuongea huku wakipiga hatua za kutoka nje , wakipita miili ya wanajeshi waliokuwa wamepoteza maisha yao " we need to talk before u go some where ( tunataka kuongea nawe kabla hujaenda popote )CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" heey!! man get serious in this critical condition am not reader for it , go away stup***( heee!!!!, hebu kuwa makini Kwa hali hii baya siko tayari Kwa hilo toka mpu***) yalikuwa ni mazungumzo kati ya Maja na mkuu wa polisi kada ya Dar es salam bwana kova ambaye alikuwa amemtilia wasiwasi Maja toka alipomuona.
" inatakiwa uwe mwelewa kila nchi ina taratibu zake hivyo uko chini yetu "alizidi kuongea mheshimiwa Kova na kumfanya Maja kuendelea kuwaka na kutoa maneno machafu sana lakini hayakumzuia yeye kusitisha zoezi lake .
Safari ya kuelekea kituo cha polisi cha msimbazi ikaanza mala moja huku baadhi ya wananchi wakisaidizana na wanajeshi na askari polisi kuondoa miili na majeruhi , wengine walikuwa wakiifatiria helkopita ya Al- kida .
Baada ya kufika kituo cha polisi mahojiano kati ya Maja na wananchi wa Busoga yalianza mala moja huku jeshi la polisi likijazia lawama kubwa Kwa nchi ya Busoga kuingiza mtu bila kibali ama kutoa taarifa , mwishowe mwafaka ulifikia wa Tanzania kusamehe yote na kuendelea kusaidizana huku Maja akipelekwa hospitali ya Regency kilomita chache kutoka hapo .
MISSION NCHINI BUSOGA.
Taarifa za kutoroshwa kwa gaidi Rambo master na magaidi wenzake zilikuwa zimepamba moto kila kona , kila kituo cha radio mjini humo kilikuwa kizungumzia swala hilo hilo ,. Robson ambaye ni raisi wa nchi hiyo alikuwa amechanganyikiwa hakuamini kama Maja angeshindwa kumkamata Rambo ukizingatia na matukio makubwa aliyowahi kuyafanya huko nyuma ya kuteka mtoto wa raisi wa awamu ya kumi wa kimarekani ili tu atende haki Kwa warusi waliokuwa wakinyanyasika humo , sio hilo tu bali kupitisha madawa ya kulevya katika nchi mbali mbali hivyo hakuamini , aliendelea kufikicha macho yake kana kwamba alitoka usingizini na hata mda mwingine alijifinya ili agundue kama alikuwa akiota lakini ulikuwa ukweli halisi wala si ndoto .
" je tutafanyaje kuhusu huyu gaidi ??" aliuliza baada kuitisha kikao cha dharula ndani ya ikulu ya nchi hiyo wakiwa katika chumba cha mkutano
" Kwa kuwa nchi yetu haijafungamana na upande wowote tuombe msaada " yalikuwa ni mazungumzo yaliyochukua masaa zaidi ya matatu na mwafaka uliopatikana ni kuomba msaada kwa umoja Wa kimataifa
" lakini hata kama watatusaidia na Mimi nitafanya upelelezi wangu wa chini chini na lazima nimkamate kabla ya wao " Robson aliongea peke yake akiwa anatoka katika chumba cha mkutano ilionesha dhahili alikuwa amechanganyikiwa , hakupoteza mda aliingia katika chumba chake cha siri na kuanza kuongea na Maja
" Maja mbona umeshindwa kumkamata!??" " watu wako ulionipa ni wazembe sana " nae alimrushia mpira lakini moyoni alikiri kuwa alizidiwa ujanja
" uko wapi mida hii ?"
" naelekea airport narudi nyumbani sitaki kuwa humu tena ila kumbuka ahadi yangu "
" oky " alijibu Kwa upole baada ya kusikia maneno ya ahadi waliokuwa wamekubaliana ya kuleta madawa ya kulevya kwani malipo hakuweza kuyamudu.
Mili ya wanajeshi waliofariki Tanzania ilifikishwa siku hiyo hiyo na kuongeza simazi sana Kwa wananchi wa nchi hiyo hasa hasa zile familia zilizokuwa zimepoteza wapendwa wao.
******
Helkopita aliendelea kuyumba yumba huku ikitafuta uelekeo wanajeshi nao hawakuchoka kurusha risasi ambazo zilikuwa zikianza kupotelea hewani kutokana umakini wa rubani wake kuwa makini na alikuwa mzoefu sana ,
" yes tupo hewani ila matairi yanaendelea kuwaka moto na unaelekea kwenye ijini " aliongea rubani huyo na makao makuu ya kikundi hicho ambacho teyari kilikuwa kimeshatuma watu wa kutoka msaada.
Wanajeshi wa Busoga nao walichukua helkopita na kuanza kuwafatilia lakini walijikuta wakipoteza mwelekeo baada ya kuchengana na kuanza kuzunguka hewani bila mafanikio yeyote
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
" ndio tuko upande wa magharibi fanyeni haraka " walizidi kuchanganyikiwa baada ya moto kuzidi kasi hakukuwa na maelewano ndani humo , wakiwa katika hali ya kukata tamaa kutokana na moto , Moshi mkali na helkopita kuanza kuyumba tena ndipo helkopita nyingine kubwa iliyokuwa imejaa vijana wa kisomalia ilifika eneo hilo na kuanza kutoka msaada Kwa kurusha kifaa kilichoenda kuishikilia Kwa juu helkopita ya kina Rambo iliyokuwa imeanza kushuka chini .
Hapo hapo walishusha kamba zaidi ya kumi ambazo akina Rambo walianza kuzikwea na kufanikiwa kutoka salama wakiiacha helkopita ikilipuka Kwa kishindo kikubwa hali iliyosababisha hata ndege waliokuepo eneo hilo kushituka.
" haha haha !" Kilikuwa ni kicheko cha furaha cha wanajeshi waliokuwa wamewafatilia akina Rambo baada ya kuiona helkopita ikiteketea moto na waliamini Al- kida wote wameteketea Kwa moto polini humo .
Japo Kwa mbali waliweza kuiona helkopita ikipaa kwa kasi sana hawakujali walipuuzia na kuamini Al- kida wote wameteketea .
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment