Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

SAFARI NDEFU KUELEKEA KABURINI - 2

 





    Simulizi : Safari Ndefu Kuelekea Kaburini

    Sehemu Ya Pili (2)



    Martin hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo, usiku hakukulalika hata kidogo, muda wote alikuwa akionekana kuwa na mawazo tu. Kitendo cha Patricia kumkatalia kuingia katika mahusiano pamoja nae kulionekana kumuumiza kupita kawaida kwani kila siku ndoto zake zilikuwa ni kuwa katika mahusiano na msichana huyo mrembo.

    Kila wakati alikuwa akiichukua simu yake na kisha kuliangalia jina la Patricia, alitamani sana kumpigia lakini kila alipokuwa akifikiria jinsi ambavyo msichana huyo alivyokuwa akikataa kuwa katika mahusiano pamoja nae alikosa nguvu za kumpigia. Hakujua ni kwa namna gani ambavyo angeumia hapo baadae kama tu Patricia angekubali kuingia katika mahusiano pamoja nae.

    Kila alipokuwa akijiuliza, alikosa jibu kabisa. Alikuwa tayari kuyapata maumivu yoyote yale ambayo yangetokea hapo baadae lakini ili mladi tu akubaliwe kuingia katika mahusiano na msichana yule ambaye alikuwa ametokea kumpenda kupita kawaida. Kichwa chake bado kilikuwa kikifikiria namna ya maumivu ambayo angeyapata baadae lakini alikosa jibu ni aina gani ya maumivu ambayo angeyapata.

    Akaanza kujifikiria labda Patricia alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mvulana mwingine lakini hakuweza kukubaliana na hilo. Muda mwingi alikuwa pamoja na Patricia, je kama alikuwa na mwanaume, huyo mwanaume alikuwa wapi na alikuwa akiwasiliana nae vipi? Wazo hilo likaonekana kutokuwa na nguvu kichwani mwake jambo lililomfanya kuachana nalo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akaanza kufikiria kwamba labda Patricia alikuwa ameathirika lakini napo wazo hilo likaonekana kutokumuingilia akilini. Kila siku Patricia alikuwa akinawili zaidi na zaidi, je huo UKIMWI alikuwa ameupata wapi na wakati kuna kipindi alimwambia ukweli kwamba alikuwa msichana bikira, msichana ambaye hakuwahi kukutana kimwili na mwanaume yeyote yule.

    Kila kitu ambacho alikuwa akikifikiria mahali hapo alikosa jibu kabisa, hakuelewa ni sababu zipi ambazo zilimfanya Patricia kutotaka kuingia katika mahusiano pamoja nae. Alijiona kuwa na kila sababu za kulalamika na kumlazimisha Patricia kuingia katika mahusiano pamoja nae.

    Usiku ulionekana kuwa mgumu kwake, usingizi ambao alikuwa nao ukapotea kabisa, mawazo yake yalikuwa kwa Patricia tu, alitamani akubaliane na Patricia kwamba wasiingie katika mahusiano lakini jambo hilo likaonekana kuwa gumu kwake.

    Moyo wake tayari ukaanza kupatwa na wasiwasi kwamba kuna siku Patricia angekuja kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mvulana mwingine jambo ambalo lingemfanya kuumia zaidi maishani mwake. Hakutaka kuliona jambo hilo likitokea katika maisha yake, alitamani kuwa na Patricia katika maisha yake yote.

    Kichwa chake kikaanza kufikiria tena muziki, nyimbo ambazo zilikuwa zikija kichwani mwake ni zile ambazo zilikuwa na majonzi ya kuachwa na kukataliwa kuwa katika mahusiano. Martin alikuwa na kila sababu za kuandika aina hizo za nyimbo kutokana na kile ambacho alikuwa akikipitia kwa wakati huo.

    ******

    Hali ambayo ilikuwa ikitokea kwa Martin ilikuwa ni hali ile ile ambayo ilikuwa ikimtokea Patricia. Muda wote alikuwa akimfikiria Martin, ni kweli kwamba alitamani kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na Martin lakini bado moyo wake ulikuwa ukiogopa kumuumiza.

    Alimpenda sana Martin hivyo hakuwa radhi kumuumiza, alipenda sana kumuona mvulana huyo akiishi katika maisha ya furaha, hakutaka yeye kuwa moja ya sababu ambayo ingemfanya Martin kutokuishi katika maisha ya furaha na amani, alikuwa akifanya kila liwezekanalo ili kumfurahisha Martin hasa katika kipindi cha baadae na si katika kipindi hicho.

    *****

    Mwaka ukakatika na hatimae kuingia kidato cha nne. Urafiki wao bado ulikuwa ukiendelea kama kawaida huku katika kipindi hiki ukiwa umezidi zaidi na zaidi. Bado walikuwa wakiendelea kusaidiana kwa kila kitu. Wanafunzi wote shuleni walikuwa wakiufahamu uhusiano huo kwamba watu hao walikuwa wapenzi.

    Hapo ndipo mambo yalipoanza kubadilika. Martin na Patricia wakaanza kuishi maisha kama wapenzi. Wakaanza kunyonyana midomo na kuanza kutomasana hasa katika kipindi ambacho walikuwa ndani ya gari. Miili yao ilikuwa ikizidi kuwaka tamaa ya kufanya ngono katika maisha yao. Kila mmoja akawa na hamu ya kuuona mwili wa mwenzake, siku ambayo walitaka jambo hilo lifanyike ikapangwa na kila mtu kuisubiria kwa hamu.

    Siku ikafika. Gari aina ya Harrier nyeusi ilisimama katika eneo la hoteli ya Mtanzania. Patricia na Martin wakateremka na moja kwa moja kuelekea mapokezini na kisha kuchukua chumba. Walipoingia chumbani tu, wakaanza kukumbatiana, mabusu mfululizo yakaanza kupigwa jambo ambalo likawafanya kuanza kusaidiana kuvuana nguo.

    Ni ndani ya dakika moja, wote walikuwa watupu. Martin akaanza kufanya mambo yake, japokuwa ndio kwanza ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya kile ambacho alikuwa akikifanya lakini akaonekana kuwa kama mjuzi. Patricia alikuwa akilalamika tu pale kitandani jambo ambalo lilikuwa likimpa Martin nguvu ya kuendelea kufanya kile ambacho alikuwa akikifanya.

    “Sijawahiiii....” Yalikuwa maneno ambayo yalisikika kutoka kwa Patricia.

    Ni kweli. Patricia hakuwa amekutana kimwili na mvulana yeyote katika maisha yake, alikuwa bikira. Martin ndiye alikuwa mwanaume wa kwanza kuyaona matiti yake, alikuwa ndiye mwanaume wa kwanza kuyaona mapaja yake mazuri na pia alikuwa mwanaume wa kwanza kumvua nguo yake ya ndani.

    Harufu nzuri ya manukato ambayo alikuwa akinukia Patricia mwilini mwake ndiyo ambayo ilimfanya Martin kuchanganyikiwa zaidi na zaidi. Alifanya kila awezalo kumlainisha Patricia mpaka pale ambapo wakaanza kuvunja amri ya sita mahali pale.

    Patricia alikuwa akipiga kelele za maumivu chini ya kitovu lakini Martin hakuonekana kumuacha, bado alikuwa akiendelea na shughuli yake. Damu zikaanza kuonekana, moyo wa Martin ukaanza kuogopa lakini alipokumbuka kwamba jambo hilo hutokea kwa msichana yeyote ambaye alikuwa akifanya kitendo kile kwa mara ya kwanza, hofu ikamtoka na kuendelea.

    Kitendo kile kilichukua saa moja, kila mmoja alikuwa amechoka, wakabaki wakiangaliana tu. Wakainuka na kuelekea bafuni ambako wakaoga na kisha kuondoka hotelini hapo. Hiyo ndio ilikuwa siku ya kwanza kwa wao kukutana kimwili. Hawakuishia hapo, kila siku walikuwa wakiendelea kufanya zaidi na zaidi. Walifanya ngono kila sehemu ambayo waliiona kustahili kufanyiwa mapenzi.

    Patricia akazidi kunawili zaidi na zaidi, urembo wake ukazidi kuongezeka zaidi na zaidi, hipsi zake zikaanza kutanuka huku mwili wake ukizidi kutamanisha zaidi na zaidi kwa kila mvulana ambaye alikuwa akimwangalia.

    Wakaendelea kusoma, juhudi zao za kusoma zikaogezeka zaidi na zaidi mpaka pale ambapo wakaja kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne. Walipomaliza, wakapata uhuru wa kukaa nyumbani, ukaribu wao ukazidi zaidi na zaidi lakini huku Patricia akionekana kuwa mpweke zaidi. Kila siku Martin alikuwa na kazi ya kumuuliza Patricia sababu ambayo ilikuwa imemfanya kuwa katika hali ile lakini Patricia hakuwa radhi kuzungumza.

    “Lakini kwa nini Patricia? Kwa nini unakuwa hivyo?” Martin aliuliza.

    “Usijali Martin. Nipo salama” Patricia alijibu kiunyonge.

    “Sasa kwa nini upo hivyo? Una mimba?”

    “Hapana”

    “Sasa tatizo nini?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Usijali. Achana na hayo”

    “Sawa. Uko tayari kwa sasa kuwa mpenzi wangu?” Martin alimuuliza Patricia swali ambao likamuongezea majonzi zaidi.

    Martin akaonekana kubadilia, katika maisha yake hakutamani kumuona Patricia akiwa katika hali ile, majonzi ambayo alikuwa nayo yalionekana kumsikitisha. Akamsogelea na kumkumbatia. Patricia akaanza kulia, alilia sana kama mtu ambaye alikuwa amefiwa na mtu ampendae.

    “Uko tayari?”

    “Hapana Martin” Patricia alijibu.

    “Lakini kwa nini?”

    “Sitaki kukuumiza. Najua utaumia tu”

    “Nitaumia? Kivipi?”

    Patricia hakujibu swali hilo, alibaki kimya huku akimwangalia Martin usoni. Macho ya Martin tayari yakaanza kuonyesha wasiwasi mkubwa jambo ambalo lilimfanya Patricia kuonekana kuwa na majonzi zaidi na zaidi. Wakakumbatiana tena na kisha kuanza kupiga stori nyingine.

    Muda ulikuwa umekwenda sana na hivyo Patricia kuaga mahali hapo. Wote kwa pamoja wakaanza kupiga hatua kulifuata gari lile, walipolifikia, Patricia akasimama kwa nje, akamshika mikono Martin na kisha kuuinamisha uso wake chini.

    Siku hiyo Patricia alionekana kuwa na majonzi kuliko siku zote, machozi yalikuwa yakimtoka muda wote, alionekana kuumia kupita kawaida. Akamvuta Martin kwake na kumkumbatia. Siku ilionekana kuwa ya majonzi kwa Patricia jambo ambao lilimchanganya sana Martin.

    “Mbona unaonekana hivyo?” Martin alimuuliza Patricia ambaye wala hakujibu chochote. Wakakumbatiana tena. Yaani ulikuwa ni muda wa kukumbatiana wakati wote.

    Patricia akatoka kifuani mwa Martin na kisha kuufungua mlango wa gari na kutoa boksi moja ambalo lilikuwa limerembwa na lilionekana kuwa na zawadi fulani ndani yake. Akamkabidhi Martin ambaye alikuwa akitetemeka kwa hofu kwani tayari alikuwa amekwishaona mabadiliko fulani.

    “Asante. Ila kuna nini?” Martin aliuliza huku akitaka kufungua.

    “Usifungue. Utafungua chumbani kwako katika kipindi ambacho nitakuwa nimeondoka” Patricia alimwambia Martin ambaye akatii.

    Patricia akamkumbatia tena Martin na kisha kuingia garini ambako akaliwasha na kuondoka mahali hapo huku ikiwa imetimia saa tano kasoro usiku. Martin akaonekana kuwa na kimuemue, akaondoka mahali hapo na kuelekea chumbani kwake, akakaa kitandani na kuanza kulifungua boksi lile.

    Mwili wake ulikuwa ukitetemeka, hali ambayo aliionyesha Patricia tayari ilionekana kumtia wasiwasi moyoni. Kijasho chembamba kikaanza kumtoka huku akizidi kutetemeka zaidi na zaidi. Kitu cha kwanza ambacho alikuwa amekutana nacho katika boksi lile ilikuwa ni karatasi ambayo akaifungua kwa haraka haraka na kukutana na mwandiko mzuri. Hakutaka kupoteza muda, akaanza kuisoma barua ile ambayo ilionekana kuanza kumtia wasiwasi. Kadri ambavyo alivyokuwa akisoma na ndivyo ambavyo wasiwasi ukazidi kumshika zaidi na zaidi, alipomaliza kuisoma tu, machozi yalikuwa yakimtoka, kila alipokuwa akijaribu kuyafuta, yalikuwa yakimtoka zaidi na zaidi.

    “Patricia......Patricia....” Martin alijikuta akiita kwa uchungu, akasimama na kuanza kwenda nje huku akionekana kuchanganyikiwa.

    Barua ile tayari ikaonekana kumchanganya, akaanza kukimbia kuelekea nyumbani kwa kina Patricia, japokuwa alikuwa akikaa Mwananyamala na Patricia alikuwa akikaa Mikocheni B lakini hakuonekana kujali, alikuwa akikimbia kwa kasi kuelekea nyumbani kwa kina Patricia huku akionekana kuchanganyikiwa.

    Barua ile ambayo alikuwa ameisoma, ilikuwa imeandikwa hivi.



    Kwako Martin.



    Najua kwamba utachanganyikiwa sana kile ambacho utakisoma katika karatasi hii lakini naomba uamini kwamba huu ndio ukweli wenyewe ambao umenifanya mimi kutotaka kuingia katika mahusiano pamoja na wewe. Naomba ujipe nguvu ya kusoma mpaka pale ambapo utamaliza kuisoma barua hii ambayo itakushtua sana na kukufanya kutokuwa na furaha kabisa.

    Najua kwamba umetokea kunipenda sana ila sidhani kama ulikuwa ukinipenda kama ambavyo nilitokea kukupenda Martin. Tumekuwa marafiki kwa muda mrefu sana, tukazoeana mpaka kufikia hatua ya kufanya kila kitu ambacho wapenzi wanastahili kukifanya hasa wanapokuwa faragha. Naomba uamini kitu kimoja Martin kwamba sisi hatukuwa wapenzi bali tulikuwa marafiki wa kawaida kama wengine.

    Huu ni muda wangu wa kukwambia kwamba sitoweza kuwa pamoja nawe tena kwa sababu moja kubwa kwamba ninahama nchini Tanzania na kuhamia nchini Marekani ambako nitakwenda kuishi na baba yangu mzazi, mzee Thomson.

    Maisha yangu yataanza nchini Marekani na kumalizia nchini humo bila ya kuwa na ndoto zozote za kurudi nchini Tanzania. Najua kwamba umeshtuka sana Martin ila naomba ujipe nguvu moyoni mwako. Kila siku ulikuwa ukinitaka niingie katika mahusiano pamoja nawe ila nilikuwa nikikataa kila siku, na hii ndio ilikuwa sababu kubwa.

    Kamwe nisingeweza kuingia katika mahusiano na wakati nilikuwa na mikakati ya kuondoka nchini Tanzania. Ningeweza vipi kuingia kwenye mahusiano na wakati nilikuwa na muda mchache wa kuishi nchini Tanzania? Najua ungeumia sana hata zaidi ya unavyoumia kwa sasa endapo tu ningekuwa mpenzi wako Martin.

    Sikutaka kukuaga Martin kwa sababu sikutaka kukuona ukiwa na majonzi, sikutaka kukuona ukilia kwa ajili yangu na wakati nilikuwa ninatimiza ahadi ambayo nilimuahidi baba yangu ya kuishi pamoja nae mara nitakapomaliza kidato cha nne. Sikutaka kuyaona machozi yako, sikutaka kuisikia sauti yako ya kilio chako masikioni mwangu.

    Najua kwamba maisha yako yatategemea zaidi muziki, naomba ufanye muziki Martin na achana na masomo kwani naamini kama utaingia kwenye masomo hautofanya vizuri kwa kuwa tu utakuwa kwenye hali ya mawazo mengi.. Nakuomba uendelee na muziki kwani nyimbo zako nzuri natumaini zitakufanya kupata mashabiki wengi watakaokupenda na kuvutiwa nawe.

    Katika boksi hili nimekuwekea kadi yangu ya benki ambayo ina kiasi cha zaidi ya milioni kumi na tano. Naomba uzitumie fedha hizo katika kuyaendeleza maisha yako huku nami nikikutumia kiasi cha zaidi ya milioni tatu kila mwezi katika akaunti hiyo hiyo. Usijali kuhusu kuitumia kadi yangu, kabla sijaondoka, kila dokumenti nimebadilisha na kuliandika jina lako kama mmiliki wa akaunti hiyo.

    Nakupenda sana Martin ila haina jinsi, inanipasa kuondoka kuanza maisha na baba yangu mbali nawe. Najua tutaweza kuonana, ila katika kipindi hicho nadhani utakuwa tayari una familia yako na mimi pia nitakuwa na familia yangu. Kama utaweza, naomba unitoe moyoni mwako, na kama kutatokea msichana ambaye atatamani kuwa nawe, naomba umkubalie tu ila kama utakuwa na uhakika kwamba hatokuja kukuumiza maishani mwako.

    Najua kuna wengi watakupenda kwa kuwa naamini utakuwa supastaa ila itakupasa kuwa makini Martin kwa kuamini kwamba si kila anayekupenda atakuwa na mapenzi ya dhati kwako kama niliyo nayo. Pamoja na hayo, nitafanya kila liwezekanalo maishani mwangu kukununulia nyumba nzuri ya kuishi nchini Tanzania. Nafikiri baada ya mwaka mmoja, nitahitaji utafute nyumba nzuri ambayo itakuwa na hadhi kubwa ya kuishi kwa mtu kama wewe nami nitakununulia kwa kukutumia kiasi hicho cha fedha.

    Natumaini baba yangu atanisaidia kufanikisha kila kitu ambacho ninakuahidi kwa sababu ana uwezo mkubwa kifedha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Usiku wa leo ndio nitapanda ndege kuelekea nchini Marekani. Mama amekwishanipelekea mabegi yangu uwanja wa ndege na ni mimi tu ndiye ninayesubiriwa. Nakuomba Martin jipe moyo wa ushujaa, nakuomba ujipe moyo kwamba utampata msichana mzuri na atakayekupenda zaidi yangu.

    Nakutakia maisha mema, naomba uniagie kwa mama na umwambie kuhusu mapenzi mazito niliyo nayo juu yako. Nakupenda Martin.



    Ni mimi

    Patricia Thomson.



    ******



    Bado Martin alikuwa akikimbia kwa kasi kuelekea nyumbani kwa kina Patricia huku jasho likimtoka. Machozi yalikuwa yakimtoka muda wote, bado alikuwa akilia kwa uchungu. Kasi ambayo alikuwa akiitumia ilionekana kumshangaza kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia mahali pale.

    “Ungeniambia Patricia....ungeniambia Patricia” Martin alikuwa akijisemea huku akizidi kukimbia kuelekea Mikocheni B huku tayari akiwa amekwishafika Sayansi, Kijitonyama.



    Martin aliingia katika eneo la nyumba ya kina Patricia huku saa yake ikimwambia kwamba tayari ilikuwa saa sita usiku. Alikuwa akihema kupita kawaida. Sauti mbalimbali za mbwa ambazo zilikuwa zikisikika masikioni mwake zilikuwa zikimtia wasiwasi. Akaanza kumfuata mlinzi na kuanza kuongea nae.

    Muda wote Martin alionekana kutokuwa na furaha moyoni mwake, alikuwa akiongea kwa uchungu jambo ambalo lilimfanya hata yule mlinzi kumshangaa. Hali ambayo alikuwa nayo Martin alikuwa akitia huruma kupita kawaida, uso wake ulikuwa katika majonzi makubwa.

    “Nadhani ndege yenyewe itakuwa imekwishapaa kwani ratiba yake ilikuwa saa sita na nusu” Mlinzi alimwambia Martin ambaye akaangalia saa yake na kukuta kwamba tayari ilikuwa saa sita na dakika ishirini na saba.

    Martin akakaa chini, machozi bado yalikuwa yakimtoka kupita kawaida. Moyo wake ulikuwa katika maumivu makali kuliko kipindi chochote katika maisha yake. Kama ambavyo alitabiri Patricia ndivyo ambavyo ilivyotokea, Martin alikuwa ameumia kupita kawaida. Hakutaka kuondoka mahali hapo siku hiyo, alichokifanya ni kumsubiri mama yake Patricia, Bi Beatrice.

    Zilipita dakika hamsini, gari aina ya Harrier ambalo alikuwa ameondoka nalo Patricia likaanza kulisogelea geti la nyumba ile na kisha kuanza kupiga honi. Mlinzi akaanza kulifuata geti lile na kisha kulifungua na gari kupita. Bi Beatrice akateremka, macho yake yakatua usoni mwa Martin ambaye alikuwa amelia vya kutosha.

    Bi Beatrice akamsogelea Martin na kisha kumkumbatia. Moyo wake ulifahamu ni kwa kiasi gani Martin alikuwa ameumia moyoni mwake kutokana na kitendo cha Patricia kuondoka nchini huku akimuaga katika hatua za mwisho kabisa.

    “Nyamaza Martin.....Nyamaza mwanangu” Bi Beatrice alimbembeleza Martin ambaye alikuwa akiendelea kulia.

    Martin hakunyamaza, tukio ambalo lilikuwa limetokea lilionekana kumuumiza kuliko matukio yoyote ambayo yalikuwa yametokea katika maisha yake. Alimpenda sana Patricia zaidi ya msichana yeyote katika dunia hii, aliona kuwa na haki za kuishi na Patricia katika kipindi chote cha maisha yake ambacho angeishi katika dunia hii.

    Bi Beatrice akamchukua Martin na kwenda nae ndani na kisha kukaa nae kochini. Muda wote Martin alikuwa akionekana kuwa na huzuni, machozi kwake hayakukauka hata kidogo. Bado alikuwa akimhitaji Patricia wake ambaye alikuwa ameondoka kuelekea nchini Marekani kuishi na baba yake.

    Bi Beatrice hakutaka kumchelewesha Martin, alichokifanya ni kumpakiza kwenye gari lake na kurudisha nyumbani kwao huku ikiwa imetimia saa nane kasoro usiku. Ndani ya gari, Martin hakuongea kitu chochote kile, muda wote macho yake yalikuwa yakiangalia nje.

    Alipofika nyumbani kwao, akateremka na kumuaga Bi Beatrice na kisha kuanza kuelekea chumbani kwake. Mama yake hakuwa amelala, muda wote alikuwa macho akimsubiria Martin ambaye hakuwa amejua ameelekea mahali gani.

    “Mbona unaonekana hivyo?” Mama yake, Bi Evadia alimuuliza.

    Martin hakutoa jibu lolote lile, akaanza kupiga hatua kuelekea chumbani kwake na kisha kujitupa kitandani. Bi Evadia hakuonekana kuridhika, akaanza kupiga hatua kumfuata chumbani kule na kumuuliza swali lile lile zaidi ya mara tatu.

    “Patricia ameondoka” Martin alimwambia mama yake.

    “Usijali. Kesho si atarudi tena”

    “Hapana mama. Hawezi. Ameondoka kuelekea nchini Marekani. Hatorudi tena” Martin alimwambia mama yake huku machozi yakianza kumtoka tena.

    Bi Evadia akaonekana kushtushwa na maneno yale, akakataa kuamini kwamba kile ambacho alikuwa amekizungumzia Martin kilikuwa na ukweli wowote ule. Alichokifanya Martin ni kuichukua ile barua na kumgawia mama yake.

    “Fedha si kitu kwangu. Muhimu kwangu ni mapenzi yake tu” Martin alijisemea.

    *****

    Patricia alikuwa akiendesha gari kuelekea uwanja wa ndege, uso wake ulikuwa na majonzi makubwa huku muda wote macho yake yakitoa machozi. Moyo wake ulikuwa ukimuuma kupita kawaida, kitendo cha kuondoka nchini Tanzania kuelekea nchini Marekani huku akimuacha Martin nchini Tanzania.

    Moyoni hakupenda kabisa kuondoka lakini hakuwa na jinsi, kwa wakati huo alikuwa na wajibu wote wa kutekeleza ahadi ambayo alikuwa amemuahidi baba yake, Bwana Thomson ya kwenda kuishi nchini Marekani

    Kichwani alikuwa na mawazo tele, bado machozi yalikuwa yakiendelea kumtoka. Alichokifanya baada ya kufika Boma ni kulipaki gari pembeni na kuegemea usukani wa gari lake. Kilio cha sauti kikaanza kusikika kutoka kwake. Alikaa katika eneo hilo kwa dakika kadhaa na ndipo alipoamua kuendelea na safari yake.

    Akafika uwanja wa ndege na kuingia katika eneo la uwanja huo ambako akaanza kumtafuta mama yake. Wala hakuchukua sekunde zaidi ya thelathini, akamkuta ndani akiwa anamsubiri. Patricia hakuonekana kuwa na furaha kabisa, bado hali ya majonzi ilikuwa ikionekana usoni mwake.

    Akamsogelea mama yake na kumkumbatia. Bi Beatrice akapata wakati mgumu wa kuanza kumbembeleza Patricia. Kadri alivyokuwa akibembelezwa na ndivyo ambavyo alizidi kulia zaidi na zaidi. Muda mwingi Patricia alikuwa akilitaja jina la Martin, mwanaume ambaye alikuwa ametokea kuuteka moyo wake kupita kawaida.

    Tangazo likatolewa kwamba abiria wote ambao walikuwa wakielekea nchini Marekani kwa kutumia ndege ya shirika la American Airways walikuwa wakihitajika. Beatrice akamkubatia tena mama yake na kisha kuchukua mabegi yake mawili ambayo akayapeleka sehemu ya uchunguzi huku yeye akitangulia ndani ya ndege na mabegi yake kuchukuliwa na wahusika wa mizigo.

    Patricia akaingia ndani ya ndege, akachukua nafasi isiyokuwa na mtu na kisha kutulia, Bado majonzi yalikuwa mengi moyoni mwake, hakuonekana kuwa na furaha hata kidogo. Abiria wakazidi kuingia ndani ya ndege ile mpaka idadi ya abiria mia na hamsini kutimia na kisha abiria wote kutakiwa kufunga mikanda.

    Hilo ndilo lilikuwa tukio ambalo liliuchoma moyo wa Patricia kuliko matukio yote ambayo alikuwa amepitia katika maisha yake kabla ya hapo. Akabaki akiangalia dirishani, mianga ya taa ilikuwa ikionekana kwa mbali machoni mwake, majonzi ambayo alikuwa nayo yalizidi kuongezeka zaidi na zaidi kwani aliamini kwamba wala asingeweza kumuona Martin katika kipindi chote cha maisha yake japokuwa wangezidi kuwasiliana kwa kutumia simu.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******

    Ndege ya shirika la ndege la American Airways ilikuwa ikitua katika uwanja wa ndege wa John F Kennedy uliokuwa katika jiji la New York nchini Marekani. Ndege ile ikaanza kutembea katika ardhi ya nchi hiyo mpaka pale iliposimama na abiria kuanza kuteremka.

    Macho ya Patricia yalikuwa yakiangalia katika kila upande katika uwanja ule, maghorofa yalikuwa yakionekana kwa mbali huku hali ya hewa ya kiubaridi kikiwa kinaupiga mwili wake. Patricia pamoja na abiria wengine wakaanza kutembea kuelekea katika jengo la uwanja ule na kisha kuchukua mabegi yao mara tu yalipomalizwa kuchunguzwa.

    Patricia akayachukua mabegi yake mawili na kisha kuanza kupiga hatua kuelekea nje. Ghafla macho yake yakagongana na macho ya mwanaume mmoja ambaye alikuwa na ndevu aina ya mustachi, akamsogelea na kumkumbatia, alikuwa baba yake, Bwana Thomson.

    Ilikuwa ni furaha kwa Patricia, ingawa katika kipindi kilichopita alikuwa na huzuni kwa kuwa alikuwa ameondoka nchini Tanzania lakini muda huo kidogo furaha ikaonekana kurudi japokuwa haikurudi kwa asilimia mia moja.

    Bwana Thomson pamoja na binti yake, Patricia wakaanza kupiga hatua kuelekea nje ya jengo lile huku mabegi yakibebwa na kijana mmoja ambaye alionekana kuwa mfanyakazi wa Bwana Thomson. Walipofika nje, gari zuri na la gharama, Mc Lloyd lilikuwa likiwasubiri, mizigo ikapakiwa na kisha safari ya kuelekea katika mtaa wa kitajiri wa Frankline Square kuanza.

    Muda mwingi macho ya Patricia yalikuwa yakiangalia nje, mandhari mazuri ya jiji la New York yalionekana kumvutia kupita kawaida. Moyoni alikuwa akifurahia muda wote, kuingia nchini Marekani huku akiwana baba yake kulionekana kumfariji kupita kawaida.

    Dereva akachukua barabara ya St’ Peters na kunyooka moja kwa moja kama umbali wa kilometa tatu na kisha kuchukua barabara ya magari yaendayo kasi ya Smallville. Gari lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi kupita kawaida, barabara ilionekana kuwa bize muda wote, magari yalikuwa yakiendeshwa kwa kasi ya zaidi kilometa 200 kwa saa.

    Walitumia muda wa dakika kumi na ndipo wakachukua barabara ya Rangers Park ambayo ilikuwa ikitumiwa sana na watu waliokuwa wakielekea katika jengo la kampuni ya kutengeneza majarida ya Cow Boy. Walitumia muda wa dakika mbili na ndipo wakaingia katika mtaa wa Frankline Square, mtaa ambao ulikuwa ukikaliwa na watu matajiri wakiwemo wafanyabiashara wakubwa, wacheza filamu, wanamichezo na watu wengine wengi.

    Gari likaanza kusogea katika geti la nyumba moja iliyozungushiwa ukuta mkubwa na geti lile kujifungua. Gari likaanza kupita kuingia ndani. Kamera nyingi zilikuwa zikionekana ndani ya eneo lile huku zikizunguka katika kila upande kuhakikisha usalama ndani ya nyumba hiyo.

    Patricia akabaki akiwa ameduwaa tu, hakuamini kama hapa duniani kulikuwa na nyumba kubwa na nzuri kama ile. Bwawa kubwa la kuogelea, sehemu ya kupaki magari, sehemu iliyokuwa na mbuga ya wanyama, sehemu iliyokuwa na kiwanja cha mpira wa kikapu vilikuwa baadhi ya vitu vilivyokuwa vikionekana katika eneo la nyumba ile.

    Hapo ndipo ambapo maisha ya Patricia yalitakiwa kuanzia. Moyoni mwake alitamani kumuita Martin na kisha kuishi nae ndani ya jumba hio la kifahari lakini kitu kama hicho kilionekana kuwa kama ndoto maishani mwake.

    “I missed you my only daughter (Nilikukumbuka binti yangu pekee)” Bwana Thomson alimwambia Patricia huku akionekana kuwa na furaha.

    Muda wote Bwana Thomson alikuwa akionekana kuwa na furaha. Patricia ndiye alikuwa binti yake pekee ambaye alikuwa akimpenda katika maisha yake, yeye ndiye alikuwa binti na mtoto pekee katika maisha yake. Alimthamini Patricia, alikuwa tayari kupoteza kitu chochote lakini si kumpoteza Patricia.

    Baada ya wiki moja Patricia alitakiwa kuanza chuo. Bwana Thomson hakutaka mwanae akae hostel, alikuwa akitamani muda wote amuone. Alichokifanya ni kumpeleka katika chuo cha St’ Mariana ambacho kilikuwa kinachukua watoto wa watu wenye fedha tu na watu ambao walikuwa maarufu nchini Marekani.

    Patricia akaanza katika chuo hicho huku akisoma na kurudi nyumbani kwao. Masomo ya Biashara ambayo alikuwa akiyachukua hayakuonekana kuwa magumu kwake kitu ambacho kilimfanya kuyafurahia kupita kiasi.

    Mambo yakaanza kuonekana kubadilika. Uzuri ambao alikuwa nao Patricia ukaanza kumvutia kila mwanaume ambaye alikuwa akimwangalia chuoni hapo. Kila mvulana akatamani kuwa pamoja nae, uso wake na mchanganyiko wake wa rangi vilikuwa vitu ambavyo vilimvutia kila mtu.

    Wavulana wakaanza kuanzisha ukaribu na Patricia, Patricia akazoeleka lakini kila alipokuwa akitongozwa na wavulana mbalimbali wala hakuwa radhi kuwakubalia. Bado kichwani mwake kulikuwa na mwanaume mmoja, moyo wake haukutaka kumsahau mvulana huyu. Alimpenda na alitamani aje kuishi nae hapo baadae lakini aliona kitu hicho kutokuwezekana kwa kuwa hakuwa na ndoto zozote za kurudi nchini Tanzania.

    Uzuri wa Patricia ukaanza kuwa gumzo, wanachuo ambao walikuwa wakisoma chuoni hapo wakaanza kupeleka taarifa kwa wanachuo wa vyuo vingine jambo ambalo liliwafanya watu wengi kufika chuoni hapo. Uzuri wa Patricia ulionekana kumshinda hata Sandra Manucho, msichana aiyekuwa akivuma ambaye alikuwa na asili ya Mexico.

    Katika kipindi hiho gumzo kubwa lilikuwa ni Patricia. Wavulana mbalimbali wakaanza kupiga nae picha na kuziweka kwenye kompyuta zao na simu zao. Patricia hakukubalika na wavulana tu, bali hata wasichana walikuwa wakiukubali uzuri wake. Kwa mara ya kwanza msichana Sandra akaonekana kushtuka mara tu alipouona uzuri wa Patricia, hakuamini kama kweli kulikuwa na msichana mzuri namna ile.

    Ndani ya miezi miwili, sifa za uzuri wa Patricia zikaanza kuenea taratibu mpaka kufika katika jengo la kampuni ya kutengeneza majarida ya Cow Boy. Meneja wa kampuni hiyo akaanza kufanya jitihada za haraka haraka za kumpata Patricia kwa ajili ya kuandikisha nae mkataba kwa ajili ya kuzitoa picha zake katika kava la mbele katika majarida yake kwa kuona kwamba angeingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na uzuri aliokuwa nao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bwana Smith hakutulia garini, muda wote macho yake yalikuwa yakiiangalia picha ya Patricia ambayo alikuwa ametumiwa kwenye simu yake. Katika kipindi hicho alikuwa katika mwendo wa kasi kuelekea katika chuo cha St’ Mariana kwa ajili ya kuonana na Patricia na kisha kuweka nae mkataba. Japokuwa kazi ya kuandikishiana mikataba halikuwa jukumu lake lakini uzuri wa Patricia ukamfanya kujipa jukumu hilo.

    Gari likaanza kuingia katika eneo la chuo hicho, ni picha za Patricia ndizo ambazo zilikuwa zikionekana mbele yake huku zikiwa zimebandikwa katika sehemu mbalimbali huku maneno yaliyosomeka ‘MISS ST’ MARIANA’ yakisomeka katika kila picha aliyoiona.

    “I have to see her (Inanibidi nimuone)” Bwana Smith alisema huku akianza kupiga hatua kuelekea katika ofisi za chuo hicho huku mawazo yake yakimfikiria Patricia na namna ambavyo angetengeneza fedha kupitia msichana huyo kutokana na uzuri aliokuwa nao.



    Bwana Smith akafika katika ofisi ile na kuanza kuanza kuongea na professa Mickey. Akalielezea lengo la yeye kuwa mahali hapo. Professa Mickey akaonekana kushtuka, macho yake yakaonyesha msangao ambao ukamfanya Bwana Smith kushindwa kuelewa sababu ambayo ilisababisha hali ile usoni mwa Profesa.

    “Kuna nini?” Bwana Smith aliuliza.

    “Mnanishangaza sana”

    “Kwa nini?”

    “Wewe ni mkurugenzi wa jarida la kumi kuja kumuulizia. Naomba uende kwenye darasa lile kule utakutana nae pamoja na wenzako” Profesa alimwambia.

    Bwana Smith hakutaka kubaki ndani ya ofisi ile, kwa haraka haraka huku akionekana kuwa na haraka akaanza kupiga hatua kuelekea katika darasa ambalo alikuwa ameelekezwa. Mpaka kufika kipindi hicho tayari akaona kwamba kulikuwa an upinzani mkubwa ambao ulikuwa ukimkabili kutoka kwa majarida mengine ambayo yalikuwa yakitaka kufanya kazi na Patricia.

    Akaingia darasani, watu zaidi ya ishirini walikuwa wamemzunguka Paticia ambaye alikuwa amekaa katika kati yao. Bwana Smith akawasogelea na kukivuta kiti kukaa pamoja nae. Bado watu wale ambao walikuwa wametoka katika majarida mbalimbali walikuwa wakimlazimisha Patricia kuingia nao mkataba wa kufanya nae kazi.

    Tayari sura na umbo la Patricia likaonekana kuwa faida, fedha zilionekana waziwazi kwa mtu yeyote ambaye angeshinda kumsainisha mkataba Patricia ambaye alikuwa akionekana kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha.

    “150000000$ per year(Dola milioni kumi na tano kwa mwaka)” Mkurugenzi wa jarida la Mississippi alimwambia Patricia.

    “I will pay you 20000000$ Per year (Nitakulipa dola milioni ishirni kwa mwaka)” Mkurugenzi wa kampuni ya jarida la Washington Daily alimambia Patricia.

    Ubishi ulikuwa mkubwa mahali hapo, kila mtu alikuwa akizidisha madau makubwa kama njia mojawapo ya kuweza kumsainisha mkataba Patricia. Wenyewe ka wenyewe walikuwa wakiendelea kubishana. Malipo ya dola milioni moja yakafika lakini hakukuwa na mtu ambaye alionekana kushinda. Madau yakaongezwa zaidi na zaidi mpaka kufika dola milioni tano, na hapo ndipo Bwana Smith akashinda huku akiwa amewaacha vibaya wenzake.

    Patricia hakuwa na jinsi, kiasi ambacho alikuwa ameahidiwa kukipata kwa mwaka kilikuwa kiasi kikubwa sana ambacho kilikuwa ni zaidi ya Bilioni mia moja kwa mwaka. Mawazo yake yalikuwa kwa Martin tu. Yeye alikuwa amezaliwa katika familia iliyokuwa na fedha, hakuona umuhimu wa kuendelea kuhitaji fedha, kila fedha ambazo angekuwa akiingiza katika maisha yake, basi aliona fedha zile kuwa mali ya Martin ambaye alikuwa akiishi maisha ya dhiki nchini Tanzania.

    Mkataba ukaandikishwa na moja kwa moja Patricia kuanza kazi. Mategemeo ambayo yalikuwa yametegemewa ndio ambayo yalitokea. Kwa mara ya kwanza picha za Patricia zilipoanza kutoewa kwenye majarida ya Cow Boy, majarida yakanunuliwa kupita kawaida.

    Sura ya Patricia ikaonekana kumvutia kila mtu ambaye alikuwa akiiangalia, urembo wake ulionekana kuwa mkubwa machoni mwa watu. Watu wengi wakashindwa kuvumilia, hawakuamini kama duniani kulikuwa na msichana mrembo namna ile jambo ambalo liliwafanya kuanza kuelekea katika chuo cha St’ Marianna kwa ajili ya kumuona msichana huyo mrembo.

    Kila siku wanaume walikuwa wakimiminika chuoni hapo kwa ajili ya kumuona msichana ambaye alikuwa akivutia sana. Kila mmoja alikuwa na kiu ya kumuona msichana huyo ambaye alionekana kuwa na uzuri wa ajabu. Walipofika chuoni hapo, walimuona Patricia ambaye alionekana kuwachanganya kupita kawaida.

    Huo ndio ukawa mwanzo wa umaarufu wa Patricia, asilimia zaidi ya themanini nchini Marekani wakamfahamu Patricia ambaye uzuri wake ulikuwa ukizidi kuongezeka zaidi na zaidi. Wanaume hawakuisha kujigonga, kila siku walikuwa wakimtaka Patricia kwa ajili ya kuanzisha mahusiano pamoja nae.

    Patricia hakuonekana kuwa mwepesi kuwakubali. Bado akili yake na moyo wake katika kipindi hicho alikuwa akimfikiria mwanaume ambaye alikuwa amemtoa bikira yake, Martin. Kitendo cha kumkubalia mvulana mwingine ilionyesha dhahiri kwamba alikuwa radhi kumsaiti Martin.

    Miezi ikaendelea kukatika na hatimae mwaka mmoja kukatika. Uzuri wa Patricia ukaonekana kumteka kila mwanaume nchini Marekani. Majarida ya Cow Boy bado yalikuwa ykiuza sana kutokana na picha mbalimbali za Patricia ambazo zilikuwa zikionekana katika ukurasa wa mbele kabisa.

    Patricia akafanikiwa kuingia mikataba na makampuni mbalimbali kama Pepsi, makampuni ya pafyumu pamoja na vinywaji vingine. Patricia aliendelea kulishika soko la Marekani na duniani kwa ujumla mpaka pale ambapo alifuatwa kwa ajili ya kushiriki katika filamu ya BLOWN JEANS. Akasaini mkataba mnono wa kushiriki katika filamu hiyo, mkataba ambao uligharimu zaidi ya dola milioni nane mara tu atakapomaliza kurekodi filamu hiyo.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha ya Patricia yakawa yamebadilika kabisa, utajiri ambao alikuwa akiumiliki kwa wakati huo ulikuwa ni zaidi ya dola bilioni themanini. Akanunua nyumba kubwa ya kifahari, magari ya kifahari pamoja na kuanzisha biashara zake nyingi ambazo zilikuwa zikimuongezea kiasi kikubwa cha fedha.

    Bado fedha zilikuwa zikiendelea kuingia katika akaunti yake kila siku. Ingawa katika kipindi hicho kichwa chake kilikuwa kimemsahau Martin lakini kamwe hakuweza kuzisahahu ahadi ambazo alikuwa amempa. Kila mwezi alikuwa akimtumia kiasi kile cha fedha huku mwaka ulipokwisha akiwa amemtumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kununulia nyumba nchini Tanzania.

    Maisha yaliendelea zaidi na zaidi mpaka pale ambapo Patricia akaingia katika mahusiano na mchezaji wa mpira wa kikapu wa timu ya Chicago Bulls, Banana Kelvin. Uhusiano huo ukatangazwa sana kuwa uhusiano ambao ulikuwa ukivutia kuliko uhusiano zote kwa wakati huo.

    Patricia alikuwa akionekana kuwa na furaha, sehemu nyingi ambazo alikuwepo, alikuwa pamoja na Banana ambaye alikuwa akimpenda sana katika kipindi hicho. Walikuwa wakitembea sehemu nyingi duniani kwa ajili ya kuhudhuria matamasha mengi pamoja na sherehe mbalimbali. Kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Patricia, jina la Banana likakua zaidi na kuwa mwanamichezo ambaye alikuwa akijulikana sana.

    Banana ndiye ambaye alikuwa akitumia kiasi kikubwa cha fedha. Hakutaka kabisa Patricia atumie fedha alizokuwa akiziingiza katika biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya pamoja na mikataba mingi aliyokuwa akiingiza. Banana ndiye alikuwa kila kitu, alikuwa akimnunulia Patricia vitu mbalimbali vya thamani.

    Mwaka wa pili ukakatika, Patricia akaendelea kung’aa zaidi na zaidi, akazidi kuingiza fedha nyingi kuliko wasichana wote duniani. Jina lake likazidi kukua huku uhusiano na Banana ukiwa umeendelea zaidi na zaidi mpaka kufikia hatua ambayo wakaamua kutangaza kwamba walikuwa mbioni kufunga ndoa jambo ambao liliwafurahisha watu wengi duniani.

    ********

    Martin bado alikuwa akiendelea na maisha yake. Kiasi cha fedha ambacho alikuwa ameachiwa na Patricia kikamfanya kwenda kupanga vyumba viwili vilivyokuwa na hadhi na kisha fedha nyingine kuziingiza katika kazi yake ya muziki. Kila siku alikuwa mtu wa kuandika nyimbo mbalimbali na kisha kuanza kurekodi nyimbo moja baada ya nyingine.

    Nyimbo zake zilikuwa zikivutia lakini si watu wote ambao walikuwa wakizisikia kutokana na ubaguzi ambao ulikuwa ukifanywa na madj mbalimbali waliokuwa katika vitu vya redio. Hapo ndipo Martin alipoanza kuhonga, hakuona kama kulikuwa na njia nyingine ambayo ingemfanya kusikika zaidi ya hiyo.

    Nyimbo zake zikaanza kusikka zaidi na zaidi masikioni mwa Watanzania. Kutokana na nyimbo zake kuonekana kuwa nzuri, akaanza kujizolea mashabiki mbalimbali. Akaanza kuhalikwa kwenye matamasha mbalimbali. Jina lake likaanza kukua hatua kwa hatu.

    Fedha ambazo alikuwa akiwahonga madj zikaonekana kuanza kurudi, akawa miongoni mwa wasanii chipukizi ambao walikuwa wametoka hivi karibuni. Martin hakutaka kuishia hapo, alichokifanya ni kuanza kutoa video ambazo zilikuwa kwenye ubora mkubwa ambazo zilimfanya kukubalika kupita kawaisa

    Akazidi kualikwa zaidi na zaidi, akaanza kuitwa sehemu mbalimbali nje ya Tanzania, ingawa mara ya kwanza alikuwa akiimba jukwaani na kulipwa laki tano lakini baadae akaanza kulipwa mpaka kiasi cha shilingi milioni moja.

    Martin hakumsahau mama yake, akampangishia nyumba nzima huku nae akiendelea na harakati zake za kufanya muziki. Maisha yakaonekana kubadilika kwa Martin, mafanikio yakaonekana kumfuata kwa haraka sana kiasi ambacho wengine wakawa na mashaka kwamba alikuwa amejiunga na dini imuabudio shetani ya Freemason.

    Martin ambaye alikuwa akilitumia jina la MAPAC JNR akazidi kuwa maarufu zaidi na zaidi na kuwa miongoni mwa wasanii ambao walikuwa wakiingiza kiasi kikubwa cha fedha. Kila matamasha ambayo yalikuwa yakifanyika nchini Tanzania, Martin au Mapat Jnr alikuwa akiitwa na kuimba. Tayari akaonekana kuwa kipenzi cha Watanzania, nyimbo zake zilikuwa zikisikika mara kwa mara katika vituo mbalimbali vya redio.

    Ni ndani ya miezi saba tu, Martin akawa msanii mkubwa na kuongoza kwa malipo makubwa nchini Tanzania. Maisha yake yakabadilika kabisa, vituo mbalimbali vya redio vikaanza kumuita na kufanya nae mahojiao.

    Watanzania wengi walikuwa wakihitaji kufahamu ni kwa namna gani ambavyo alikuwa amefanya mpaka kupata mafanikio makubwa namna ile tena kwa haraka kupita kawaida. Martin akaamua kwenda katika kituo cha Flavour Tv na kuanza kufanyiwa mahojiano.

    Watanzania wengi walikuwa wamekusanyika katika televisheni zao tayari kwa kumuona Martin ambaye alionekana kuwa na mvuto kwa watu wengi katika kipindi hicho. Kule kuonekana moja kwa moja kwenye televisheni, kila mtu akaonekana kufarijika, kuonekana kwake kwenye televisheni kulionekana kumfurahisha kila mtu.

    “Hebu tupe historia ya maisha yako Mapac” Mtangazaji ambaye alikuwa akimhoji Martin katika kipindi maalumu alimwambia Martin.

    “Nilizaliwa miaka ishirini na mbili iliyopita na kusoma katika shule ya Salma Kikwete pale Kijitonyama. Maisha yangu katika kipindi hicho yalikuwa ni maisha ya shida sana, shuleni nilikuwa mwanafunzi ambaye nilikuwa mchafu kuliko wanafunzi wengine. Sidhani kama nilifikisha siku zaidi ya mia moja kuvaa viatu shuleni, yaani muda mwingi shuleni nilikuwa nikivaa kandambili tu” Martin alimwambia mtangazaji kauli ambayo iimshtua kila aliyekuwa akiangalia.

    “Mmh! Ulimaliza shule mwaka gani?”

    “Nilimaliza mwaka jana. Kwa hiyo haya maisha ambayo niliyapitia yalikuwa kama miaka mitatu iliyopita. Nilikuwa nikiuchukia sana umasikini na nilikuwa tayari kujitoa kwa ajili ya kupigana na umasikini huu kwa kuwa tu niliuchukia. Kiukweli watanzania msifikiri kwamba nilifaulu mitihani. Nilifeli sana na hata mtihani wa kidat cha nne nilifeli vibaya kwa kupata daraja la sifuri, yaani hapa hata cheti sina” Matin alimwambia mtangazaji.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pole sana”

    “Asante”

    “Sasa kwa nini uliamua kujiita Mapac Jnr?”

    “Jina hili ni muunganiko mwa majina mawili. Ma ni kifupi cha jina langu Martin na Pac ni kifupi cha jina la msichana Patricia na Jnr ni neno ambalo linaonesha kwamba mimi ni kijana mdogo” Martin alimwambia mtangazaji.

    “Kwa hiyo una msichana anayeitwa Patricia?”

    “Hapana. Yeye ni rafiki yangu ambaye alinisaidi sana toka nilipokuwa shuleni. Nilikuwa kwenye maisha ya kimasikini sana lakini uzuri ulikuwa kwamba yeye alikuwa na uwezo wa kifedha jambo ambalo lilimfanya kunisaidi kwa kila kitu. Alininunulia nguo, viatu na kila kitu nilichokua nikikihitaji. Yaani aliyabadilisha maisha yangu mpaka ya mama yangu mpaka pale alipoondoka kuelekea nchini Marekani” Martin alijibu.

    “Nimepata picha sasa. Huyu msichana likuwa akikupenda kama rafiki tu?”

    “Ndio”

    “Kwa hiyo hamkuwahi kuwa wapenzi?”

    “Ndio”

    “Sawa. Kwa hiyo huwa unawasiliana nae?”

    “Hapana japokuwa huwa ananionyeshea upendo mkubwa wa kunitumia fedha. Yaani maisha yangu hayategemei muziki. Hata kama nisingekuwa mwanamuziki, bado maisha yangu yangekuwa hivi isipokuwa umaarufu tu. Nilijiingiza kwenye muziki kwa kuwa ulikuwa damuni tu” Martin alijibu.

    “Kwa hiyo una ndoto za kuwa na msichana huyo baadae?”

    “Bado nina kiu ya kuwa nae kwa kuwa ninampenda sana. Naamini kuna siku nitasafiri na kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kumuona tu” Martin alijibu.

    “Kwa hiyo wasichana ambao mara kwa mara wanatokea kwenye magazeti ya udaku kuwa wanakutaka waache kujitangaza kwa kuwa kuna msichana unampenda?”

    “Yeah! Ikibidi waache tu. Ninampenda sana Patricia, ninampenda sana, tena sana tu” Martin alijibu.

    Hayo ndio yalikuwa maisha yake, mara kwa mara alikuwa akiitwa katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni na kufanyiwa mahojiano, Bado alikuwa akisisitiza kwamba Patricia alikuwa msichana ambaye alikuwa akimpenda sana kuliko msichana yeyote yule katika maisha yake.

    “Nitaendelea kumpenda na kumhitaji milele” Martin alisema huku tayari akiwa ametangazwa na kuwa msanii aliyekuwa na uwzo mkubwa kifedha kuliko mwanamuziki yeyote nchini Tanzania.



    Je nini kitaendelea?

    Je nini kitaendelea katika maisha ya Martin na Patricia?

    Je Patricia ataweza kufunga ndoa na Banana kama walivyopanga?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog