Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

DAR TO MUMBAI - 5

 







    Simulizi : Dar To Mumbai

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku iliyofata siku muona kipenzi cha roho yangu kutwa nzima ivyo ikabidi jioni niende kwake nikamkuta mnyonge sana, nikamsogelea na kumchumu kama ilivyo kawaida yetu kila tunapoonana

    "Vipi mpenzi mboni huko ivyo, alafu ata darasani hukuingia leo!" nikamtupia swali baada ya kusalimiana, hakujibu kitu zaidi ya kusema kuwa yupo sawa tuu. Nikamuuliza amekula akanijibu kuwa hakula chochote ikabidi niingie jikoni nikamfanyia mazuri pale baada ya nusu saa msosi ukawa mezani, nikamkaribisha tukala pamoja lakini muda wote alikuwa akinitazama sana usoni

    nikaligundua hilo kwa haraka nikauliza

    "Honey! Nakuona wa tofauti sana leo, umekuwa mnyonge, huna raha nini tatizo?". Akanitazama kisha akasema

    "Hivi Nea unanipenda kweli?".

    Nikajikuta nacheka sana wala sikutegemea kama atauliza swali hilo.

    "Priya mimi sijui niseme nini kuthibitisha nakupenda lakini vitendo vyangu ni ushaidi tosha kuwa nakupenda na kuthamini kuliko kitu chochote kile" nikamsogelea na kumruhusu aegame kwenye kifua change.

    "Hivi Nea, Vanessa ni nani yako?" ilo swali likanishtua sana nikajikuta najiuma uma kwa kuwa sikuwa na jibu wala mimi mwenyewe sikujua Vanessa ni nani kwangu.

    "Vanessa ni mwanafunzi mwenzetu" nikamjibu, akanitazama kisha akasema "tangu lini umeanza niongopea?"

    "Aaah! Priya kukuongopea vipi mpenzi",

    "Unajifanya ujui eenh?"



    Kwa kweli ilikuwa mtihani mkubwa sana kwangu kujua nini Priyanka anamaanisha, baada ya kuona amerizika na majibu yangu ikabidi niage na kuondoka, kufika chumbani nikawasha simu nikakuta meseji imeingia kuangalia namba mpya ila nilivyoisoma vizuri nikagundua kuwa ni Vanessa, kwa kuwa nilimuahidi kumsaidia juu ya tatizo lake hivyo nikamjibu na akaomba tukutane. Nikatoka usiku huo kwenda sehemu aliyonielekeza, nikamkuta amekaa na jamaa ambaye sikuwa namfahamu, niliposegea jamaa akabadilika na kuanza kunishambulia kwa matusi huku akinikunja akitaka nipiga nikavumilia kwa kuwa sikuwa na sababu ya kurudisha mapigo. Jamaa akaendelea kunishambulia na hata kuanza kunipiga huku akidai kuwa nina mahusiano na mchumba wake ambaye ni Vanessa, uvumilivu ukanishinda nami nikajibu mashambulizi nilimdhibiti vilivyo jamaa. Nikamchukua Vanessa na kumtaka aondoke eneo lile, ajabu yule binti akanikumbatia huku akiniomba radhi kwa kile kilichotokea nikamtuliza na kumwambia asijali, wakati naondoka nikagundua kuwa sina simu nimeiangusha nikajisachi na Vanessa akaniuliza kulikoni, nikamwambia nimeangusha simu tukarudi wote eneo lile tukataitafuta hatimaye Vanessa akaipata na kunikabidhi nikaagana naye na kurejea nyumbani, nikakuta rafiki zangu wamelala hivyo nami nikaingia bafuni kuoga kisha nikajibwaga kitandani na usingizi ukanichukua.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ********************



    Siku iliyofata nilihisi mwili kuuma sana, nikawa najisikia vibaya mno nikashindwa kwenda chuo, nikabaki tu ndani nimelala kutwa nzima, jioni Priya akaja ninapoishi, akanikuta na hali mbaya akagundua kuwa sikula kitu toka asubuhi, akanipashia maji ya moto na kunitaka nikaoge, kisha akaingia jikoni, nilivyotoka kuoga nikaanza kuona mwili mwepesi akanikaribisha chakula tukala pamoja huku tukilishana kwa mahaba, wakati hayo yanaendelea simu ikaita nikamwambia Priya apokee aliposoma jina ni Vanessa, akaipokea



    "Hallo...!"



    Simu ikakatwa, nikamuuliza vipi akajibu simu imekata nikamwambia achana nayo, akaanza kuipekuwa ile simu akaingia moja kwa moja inbox akakuta meseji akaanza kusoma moja baada ya nyingine sikuwa na hofu juu ya hilo kwa kuwa niliamini hamna baya nililofanya, kadri alivyozidi kusoma ndivyo sura yake ikazidi badilika, machozi yakaanza mtiririka nikashtuka kuona hiyo hali ikabidi nimsogelee kuona kitu gani kinamliza, akanionesha meseji nikahisi nami mwili wote kufa ganzi.



    Yalikuwa ni mazungumzo ya kimapenzi kati yangu na Vanessa, Priya alilia mno kwa nini nmemfanyia vile nami nikabaki kushangaa kwani sijawahi mimi kuongea na Vanessa chochote kuhusu mapenzi, sasa ni nani aliyetumia simu yangu kuchati na Vanessa kuhusu mambo yale yakimapenzi moyo uliuma mno, sikujua nifanye nini ili Priya aamini kuwa hamna lolote kati yangu na Vanessa, nikajitahidi kumuelewesha lakini sikuambulia kitu, akatoka huku akiwa na hasira nyingi akaelekea kwake, nikajitahidi tena na tena lakini haikufaa kitu. Ikabidi niombe msaada kwa rafiki zake nayo pia haikufaa kwani Christine hakutaka hata nisikia nikawaelezea maswahiba zangu nao wakabaki wameduwaa, ila walau wakanitia moyo kuwa watanisaidia.



    Siku zikazidi kukatika nikaiona dunia chungu darasa sikulitamani, uvumilivu ukanishinda nikaamua niende hadi anapoishi sikumkuta nikaambia yupo kwa mama yake nikaenda hadi huko, kufika mlinzi akanizua lakini nikaingia kimabavu hadi ndani nikamuita Priya kwa nguvu zote akatokea huku akiwa bado na hasira, machozi yakanitoka kama mtoto mdogo nikamtazama na kumwambia

    "Priyah kwanini wanipa adhabu kubwa kiasi hiki" hakuongea kitu zaidi ya kulia tuu.

    "Priya nakupenda mno na sijawahi kukusaliti na haitotokea kukusaliti katika maisha yangu".

    "Nea nilikuuliza kwa utaratibu Vanessa ni nani yako lakini ukawa tu unazunguka zunguka kujibu, heshima na mapenzi niliyokupa leo unakuja kunichanganya na yule, aah Nea!” Priya aliongea huku akiendelea kulia.

    "Nea kuanzia leo mimi naona uendelee na Vanessa na uniache na maisha yangu". Nikahisi nguvu kuniisha nikajikuta nakaa chini bila kupenda

    "Lakini Priya, hamna chochote kati yangu na Vanessa!!"

    Akanipiga kibao cha nguvu akasogea hadi kwenye kabati akavuta bahasha akaifungua asee nilichokiona hapo mungu mwenyewe anajua, zilikuwa picha nilizopigwa nikiwa na vanessa kuanzia siku namsaidia kufanya maswali, pia ile siku namfuta machozi na kumkubatia hadi ile siku napigana kumtetea, daah kweli nimewezwa kwa picha nililochezewa sikuwa na namna ya kujitetea nikawa mnyonge zaidi nikasimama na kumsogelea.

    "Priya unahaki ya kuamua hayo ila ipo siku utaujua ukweli, jua nakupenda sana tena sana"



    Nikamsogelea Zaidi na kumbusu kisha nikaondoka, wakati naondoka nikakutana na mzee wake uso kwa uso ghafla nikakumbuka ile kauli kuwa,

    "Siku utakayouvunja moyo wa binti yangu sitokuacha mzima."

    Nikaogopa mno japo sikuwa na hatia ila nina uhakika angenifanya vibaya endapo akindua mambo si sawa kwa binti yake, mzee aliponiona akanichangamkia sana kidogo hofu ikaondoka nami nikajifanya kama vile hakuna kitu kilichotokea.

    "Leo nina kazi kubwa sana mwanangu naomba uambatane nami ukanisaidie"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akasema baba yake Priyanka, nikageuka kumtazama Priya nae akanitazama kisha nikamgeukia baba mkwe na kukubaliana nae, mzee akafurahi sana akaingia ndani akachukua brifkesi akanikabidhi kisha tukaingia kwenye gari na safari ikaanza, tukatoka nje kidogo ya mji kufika mahali flani mzee akanambia nikafanye makabidhiano ya brifkesi hile nami nitapewa nyingine akanielekeza baadhi ya ishara ambazo nikifika nitumie ili niweze kutambuliwa nami nikafanya kama mzee alivyoniagiza tukabadilishana na nikarudi na brifkesi nyingine mzee akafurahi zaidi.

    "Wewe unafaa kumuoa mwanangu sababu unaonekana unaweza kurithi shughuli zangu nikistaafu" akanipongeza nami nikabaki kutabasamu tu.





    Siku zikazidi kuyoyoma hukua baba yake Priya akionesha kuniamini na kunitumia katika shughuli zake nyingi, name taratibu nikajikuta nazoea. Nakumbuka Siku moja baba yake Priyanka akanipa mzigo mwingine niusafirishe nje ya mji wa Mumbai, nikakubali na kuungana na vijana wengine. Safari ikaanza ila kilichonishtua ni zile njia tulizokuwa tukipita, hatukupita kwenye barabara kuu zaidi tulipita njia za panya, barabara za vumbi wakati mwingine tukaingia porini, Safari iliendelea hatimaye tukatokea sehemu moja ya daraja kubwa hapo nikashtuka kuona tunavamiwa na askari huku milio ya risasi ikilindima nikabaki nimeduwaa wale vijana wakaja wakanizunguka huku wakisema

    "Mkuu hali imechafuka tukimbie!!"



    Nikaendelea kushangaa kwanini naitwa mimi mkuu sikupata jibu kwa wakati huo, tukakimbia na kuingia kwenye jumba moja kubwa sana. Hadi apo kwangu kila kitu kilikuwa kama ndoto, wakawasha tv kuona nini kinaendelea huko nje, ajabu kukawa na taarifa za gaidi Abdulrazak kareem kutoroka wakati jeshi la polisi lilivyokuwa likishambulia wafanya biashara haramu, wakahaidi kufanya msako hadi kulitia mkononi gaidi hilo. Wakazima Tv na kunambia mkuu hapa tena hapafai itabidi tuondoke, nikaona upuuzi huo nikachukua simu na kumpigia baba yake na Priya kumueleza kila kitu akawa anacheka tu, kabla sijaendelea kuongea nikasikia kishindo kikubwa kwenye mlango.



    Kilikuwa kikosi maalumu cha kupambana na magaidi kikavamia na kutuweka kati, wenzangu wakarudi nyuma na kuanza kushambulia lakini hawakufua dafu mbele ya maaskari wale ambao walionekana kujipanga vilivyo, walimalizwa wote na nikaamuliwa ninyanyue mikono juu, nikatii amri wakaanza nisogelea kwa tahadhari kubwa, taa zikawashwa kwenye jengo lile kukawa na bidhaa na silaha nyingi za magendo nikabaki nimeduwaa tuu sikuwa nafahamu juu ya yale, wakati mikono ipo juu simu ikawa inaita japo haikutoa mlio ila niliisikia ikitetema, nikaamua nishushe mkono na kuitoa mfukoni, lakini kabla sijaifikisha sikioni risasi kadhaa zishaushambulia mwili wangu nikahisi mwili kushikwa ganzi macho yakaanza kuwa mazito, nikabebwa haraka haraka hadi nje nikapakiwa kwenye gari ya wagonjwa. Kabla gari halijaondolewa nikashuhudia jengo lile likilipuka na maaskari wote waliokuwamo humo wakiteketea kasoro wale walioambatana nami. Jengo likaendelea kulipuka na moto ukawa mkali sana ikabidi waondoe gari kwa haraka sana. Baada ya hapo sikujua kilichoendelea teena siku nafumbua macho nikajikuta nipo gerezani.



    *********************************



    Nea akamalizia simulizi yake huku machozi yakimtoka, Pooja naye akamtazama Nea kwa masikitiko makubwa mno,

    "Hiyo ndiyo sababu hata ulipoonesha mapenzi kwangu sikuwa tayari, Japo wengi husema mapenzi ni furaha na faraja kwangu imekuwa kinyume hadi leo nipo huku sijui kama Priyanka yu hai au la, na hata kama akiwa hai lazma atakuwa ameshaolewa",

    "Pole sana Nea" Pooja akamkumbatia Nea na kumfariji.

    "Kwa hiyo haikutokea hata siku moja ukamwona baba yake Priyanka?" Pooja akauliza.

    "Alikuja gerezani akiambatana na yule mwanaume ambaye ndiye aliyekuwa mchumba wake na Priyanka, wakanicheka sana na baba yake priya akanambia kuwa “nilitaka ufe kabisa sikuwa napenda uingie katika maisha ya binti yangu ila inaonesha mungu yupo upande wako, lakini bado lazima nitimize kusudio langu" na yule jamaa akanambia nisione vizuri ujue vimegharamiwa".



    Pooja hakutaka kuuliza zaidi sababu jua lilishazama hivyo akamwambia Nea waanze safari ya kurudi nyumbani. Siku iliyofata Nea akapelekwa mahakamani kesi ikasomwa na Pooja akapeleka ushahidi wa sauti na video, kumbe Pooja hakuwa binti wa bwana jela kama Nea alivyozani ila alikuwa ni askari mpelelezi aliyeitaji kujua ukweli wote juu ya kilichomsibu Nea, na kwanini majaribio ya kumuangamiza yatokee mara kadhaa, hivyo ukweli ukawa wazi na Nea akaachiwa huru, Mchakato wa kuwatia nguvuni waarifu wa ukweli ukaanza.

    "Pooja siwezi kurudi nchini kwetu hadi nihakikishe wale wote walionifanyia ubaya wanalipa”

    "Nea miaka 8 imepita sasa, mambo yamebadilika, ila nitakusaidia kwa nitakapoweza".

    "Sina sehemu ya kuishi kwa kipindi hiki".

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pooja akamchukua Nea hadi Mumbai, Mazingira ya jiji lile yalibadilika mno, miundo mbinu iliboreshwa zaidi tofauti na ilivyokuwa awali wazo la kumtafuta Priyanka likaibuka kwenye ubongo wa Nea, ila akahofu itakuwaje endapo atakuta ameolewa na ana familia, akawaza atawapata vipi marafiki zake Steve, Mzovu na Regy ambao bila shaka watakuwa wamesharudi Tanzania. Kila alilofikiria akaliona gumu, akatamani kusamehe yote na kuanza maisha mapya, lakini hakuwa amani ya moyo hasa kwa yule aliyempenda, akawaza pia kuhusu bibi yake kwa kipindi hiki cha miaka 8, atakuwa anaishi bado au la? Hakupata jibu kwa siku hiyo kichwa kilikuwa kizito kwa mawazo akaamua kulala akiamini atakapo amka atakuwa na majibu ya maswali yake.



    *************************



    Siku iliyofata akaamua kwenda kwa kina Priyanka, akafika na kuulizia jibu alilopata liliuhuzunisha moyo wake, waliama muda mrefu uliopita. Akazunguka huku na huko lakini hakupata habari zake. Akurudi tu nyumbani kufika akamkuta Pooja akiwa anaangalia taarifa ya habari

    "Vipi za huko utokako?".

    "Mhm si nzuri sana na wala si mbaya sana".

    "Hukufanikiwa?",

    "Nimetafuta kila sehemu niliyoijua lakini sikupata habari yeyote kuhusu Priyanka wala familia yake!"

    "Je umefika chuoni?" aliuliza Pooja na hapo mawazo yakafunguka na tumaini jipya likaanza kuchanua ndani ya mtima wake

    "Asee! Pooja sikwenda ila kesho lazima niende", Pooja akamkaribisha mezani akala hatimaye usiku ukawa mzito na mwili ukaitaji kupumzika.



    *************************



    "Najua kila kitu kuhusu wewe kwa iyo usijali, na pole sana kwa yote yaliyokukuta" ilikuwa kauli ya mkuu wa chuo baada ya Nea kujitambulisha na kumuelezea shida yake, moyo ukatulia,

    "Sina taarifa juu ya alipo Priyanka, ila wazazi wake wote walifariki kwenye ajari ya gari, lakini wakati wenzako wanahitimu kuna kitu wakanipa nikihifadhi wakiamini ipo siku utafika hapa chuo" Mkuu wa chuo akatoa bahasha ndogo iliyofungwa vizuri na kumkabidhi Nea.



    "Hiko tu ndicho ninachokijua".



    Akashukuru na kurudi nyumbani, alipofika akafungua ile bahasha na kukuta kuna flash disk, akaitoa na kusogea kwenye kompyuta iliyopo hapo ndani, akaichomeka baada ya muda mfupi ikafungua, Moyo ulihisi kulipuka kwa kile nilichokiona.



    "Nea pindi utakaposoma haya jua sipo duniani, nisamehe kwa yale niliyokufanyia, Mpango wa kukuachanisha na Priyanka ulifanywa na Christine huku akipewa nguvu kubwa na Rajesh pamoja na baba yake Priyanka. Ile siku nilivyoomba unisaidie kufanya maswali ilikuwa tu njia ya kuanza kutengeneza mazingira ya kuwa karibu nawewe, hata siku nilipokutumia ujumbe ukaja kwa haraka nikaigiza kulia ili unikumbatie tu, lengo lilikuwa kuruhusu watu wapige picha zilizoonesha kuwa kweli mimi na wewe tuna mahusiano, siku uliyopigana kwa ajili yangu pia yote yale nilipanga na picha zilipigwa kumfikishia Priyanka, Nea ni katika siku ile uliyepigana nikafanikiwa kuichukua simu yako na kujitumia meseji za kimapenzi."



    Nea hakuweza kuendelea kusoma roho ilimuuma sana, akahisi kushikwa na hasira mno, hakuwa mtumiaji wa kilevi ila siku hiyo alikunywa, Baada ya kuona kichwa kimekaa sawa akaendelea kusoma huku glasi ya mvinyo ikiwa pembeni.



    “Mpango wa wewe kuonekana gaidi uliandaliwa na baba yake Priyanka, kwani hakupenda uwe na binti yake, Rafiki zako walijitahidi sana kufatilia kesi yako ili wakuokoe lakini kwa bahati mbaya wote waliingia mikononi mwa Rajesh na kufanyiwa mauaji ya kikatili sana".



    Alipofika apo hakuweza zuia machozi kudondoka, alilia kama mtoto mdogo, akakumbuka upendo na utani wao roho ilimuuma zaidi, akajitahidi kuendelea kusoma ajue hatima ya yote ila akahisi kupigiliwa msumari wa moto kwenye kidonda kibichi pindi aliposoma sentensi iliyofata,

    "Rajesh alifanikiwa kumuoa Priyanka".



    Moyo ukaenda kasi sana, hakutaka kuendelea tena kusoma, akazima kompyuta na kutoa ile flash, hamu ya kubaki Mumbai ikamuisha, akawaza jinsi ya kurudi Tanzania, Pooja akarudi akamkuta Nea akiwa amelewa hata alivyoviongea hakuvielewa, Daah pombe sio chai kila alivyomtazama Pooja akawa anamuona kama Priyanka, hisia kali za mapenzi zikaamka juu yake, akajikuta anamkumbatia kwa nguvu mno kisha akaanza kumbusu, Pooja akasita kidogo na kusema.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nea are you sure about this (unakielewa unachotaka kukifanya?)",

    "Ndio nakielewa, Priya ameolewa na sijui atakuwa na watoto wangapi sasa hivi, kama si wawili basi hata watatu". Nea akajikuta machozi yakianza kumdondoka huku akiwa bado amemkumbatia Pooja.

    "Rafiki zangu wote wamekufa, wamewaua Steve, Regy na Mzovu, sitowaona tena" Nea alizidi kuongea huku huzuni kubwa ikiwa imeufunika moyo wake, Pooja alielewa masumbuko na mataabiko yaliyo kwenye moyo wa Nea.

    "Pooja wewe si unanipenda, basi kaa nami usiniache kamwe, lakini acha kwanza nirudi kwetu alafu nitakuja huku kwa ajili yako", Nea aliendelea kuongea mengi katika hali ile ya ulevi mwisho wa yote mambo yakawa mambo usiku ukapita.



    **********************



    Nea akawa wa kwanza kuamka na kujikuta kwenye mazingira tofauti, alipoangalia pembeni akamkuta Pooja akiwa bado amelala moyo ulilipuka kwa hofu hakukumbuka chochote kilichoendelea usiku uliopita.



    Ikabidi aamke na kutaka kuondoka chumbani humo lakini alipotaka nyanyuka akajikuta mtupu hapo nguvu zikamwishia ikabidi amwamshe Pooja.

    "Pooja mboni sielewi, nini kilitokea?" Pooja hakujibu kitu zaidi ya kumwangalia Nea kwa tabasamu zito,

    "Nea nakupenda".

    "Kwa hiyo inamaana toka usiku wa jana, nimelala hapa?",

    "Ndiyo..!"

    "Na tulifanya nini usiku huo?"

    "Tulifanya vyote kama mtu na mpenzi wake", daah Nea akabaki ameduwaa,

    "Nilikubali kufanya nawe kila kitu sababu nakupenda zaidi ya chochote kile, na nikahisi hii ndio ilikuwa nafasi niliyoisubiri kwa miaka mingi, tafadhari usinifikirie vibaya ni mapenzi tuu yaliyonisukuma kukubali yote, hata ivyo jiandae leo saa 1 kamili usiku utapanda ndege ya kurejea kwenu ukifika huko kama utahisi kuniitaji nitakuja"



    Akaongea Pooja kisha akambusu Nea, Nea akawa kama aelewi elewi hivi ila akabaki kumshukuru Pooja kwa yote na kwwenda kujiandaa kwa ajiri ya safari yake.



    **********************



    Akafika katika jiji la Dar-es-salaam, saa 4 usiku kwa kuwa hakuwa anayakumbuka vizuri mazingira ya nyumbani kwao, ukizingatia ni muda mrefu umepita ikabidi aende kulala hotelini, hakuwa na shida ya kifedha kwani Pooja alimpa kiasi kikubwa sana cha pesa.



    Kesho yake akaingia mtaani ili aone kama ataweza kukumbuka alipo bibi yake, kwa kuuliza uliza akajikuta amefika, ila kilichomshangaza zaidi palipo kuwa na kale kajumba chao kibovu, kulijengwa nyumba kubwa sana tena ya kifahari, hata majirani wengi nyumba zao hazikuwepo hapo ivyo akajua ni wazi kabisa hata bibi yake, hawezi kuwa eneo hilo. Akaulizia kwa mjumbe mzee Mreme akaambiwa mjumbe alishafariki miaka 3 iliyopita, akaenda kwenye nyumba ile ya kifahari akiamini mmiliki wa ile nyumba, anaweza kujua wapi walipoelekea waliomuuzia eneo.



    Aponyeza kengele, geti likafunguliwa na mlinzi,

    “Habari ya kazi ndugu”

    “Nzuri tu! Nikusaidie nini?”

    “Samahani naweza kuonana na mwenye nyumba”

    “Wewe sema shida yako nitaifikisha”

    “Shida yangu ninataka kujua watu waliokuwa wakiishi hapa wameenda wapi, maana nilijaribu kuulizia sehemu nyingine lakini sikupata majibu ya kuridhisha”

    Mlinzi akachukua simu na kumpigia bosi wake kisha, akamruhusu Nea kuingia, Akavuta hatua fupi fupi huku akiishangaa mandhari ya nyumba ile, wakati akikaribia mlangoni akashtuka kusikia,

    "Nea! Nea! Nea...!" kitoto cha kiume kikampita na kuelekea alipoitwa, mlango ukafunguliwa, alipotazama akabaki kuduwaa, alikuwa ni Priyanka mwanamke anayempenda kuliko maisha yake, hakuamini akahisi kama anaota, Priyanka akasogea, akamkumbatia na kuanza kulia, wakati amemkumbatia hakuamini kumuona bibi yake akija upande ule, akajikuta akimtoa Priyanka na kwenda kumlaki bibi naiyepotezana nae kwa zaidi ya miaka 8, kwa kweli ilikuwa furaha kubwa sana kati yao.

    "Nea wakati upo gerezani, nikagundua nimebeba ujauzito wako, hivyo sikuweza kuolewa na mwanaume yeyote baadae nikagundua kuwa haukua na hatia roho iliniuma sana, nilijiona msaliti, nikaamua nije huku na kumtafuta bibi yako kwa msaada wa rafiki zako nikampata nikanunua nyumba zote za hapa na kujenga hii"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nea akashtuka aliposiki Priyanka akiwataja rafiki zake, akamuuliza ina maana hawakufa lakini kabla hajanimjibu, rafiki zake wote watatu wakawa wamefika akashangaa sana, asielewe ilikuaje hadi wao kuwa hai akati aliambiwa walishafariki,

    “Najua ulidhani kuwa tuliuawa, sisi ni wajanja wa mjini tulifanikiwa kuwa toroka kabla hawajatudhuru” Steve akasema

    "Nea......!" Regy akaita,

    “Naam” Nea akaitika

    “Si Nea wewe ila mtoto wako, tuliamua kumpa jina lako”

    Nea alifurahi Zaidi na kumnyanyua mtoto wake ambae hakuwa na shaka kwani alifanana nae sana. Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwao.



    Maisha mapya yakaanza, Nea akamjurisha Pooja na Kumtaka radhi kwani asingeweza kujenga mahusiano nae, kwa pamoja wakafanikiwa kufungua kampuni kubwa sana iliyojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa Filamu. Kampuni hiyo iliwapa umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi na kuyafanya maisha yao yawe bora siku zote.



    MWISHO





0 comments:

Post a Comment

Blog