Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

DAR TO MUMBAI - 4

 







    Simulizi : Dar To Mumbai

    Sehemu Ya Nne (4)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Siku ya nne, nikaamka mapema sana kwa kuwa nilijua siku ndiyo zinaishia nikapanga kumueleza vitu vingi sana miss Priyanka, nikaenda hadi sehemu tunayokutanaga nikamsubili sana lakini hakutokea, muda ukazidi kwenda wenzangu wakawa washaenda matembezi. Kiutani utani nikajikuta nikianza onja maumivu ya mapenzi, niliumia mno nikaamua kwenda kwenye hema lake, nikamkuta anasoma kitabu flani cha hadithi

    "Kwanini umenitelekeza leo?" hakunijibu kitu akaendelea kusoma, nikamuuliza tena kwa mara ya pili lakini hakujibu, nikamnyang'anya kitabu.

    "Kwanini umevunja makubaliano?"

    "Nea samahani! Piga hesabu kwa muda uliobakia nitakulipa ila siwezi tena kuendeleza makubaliano"



    Moyo uliuma sana kwangu ilikuwa kama msiba mbali na kumpenda tayari nilishaanza kumzoea, nilitamani kujua sababu lakini akanambia ni maamuzi yake, basi nikaona isiwe shida maana kisicho riziki hakiliki, nikanyanyuka bila kusema neno na kwa mara ya kwanza nikahisi chozi kunidondoka sababu ya kupenda, nikawa mnyonge zaidi wakati natoka akaniita.

    "Nea.! Ujaniambia kiasi cha pesa unachonidai",

    "Thamani ya mtu haiwezi kulinganishwa na kitu, mtu atabaki kuwa mtu na kitu kitabaki, kuwa kitu, huwezi kufidia upendo na thamani uliyonayo juu yangu kwa kutumia kitu, nitakuwa sehemu tunayokutanaga kila siku, kama unajua thamani yangu utafika, usipofika sitokusumbua tena naapa" niliongea kwa uchungu kisha nikaondoka, maneno yale yalimwingia vilivyo Priyanka. Uamuzi ukawa juu yake,kama kusuka au kunyoa.



    Muda ukasogea nami nikajisogeza eneo la tukio huku nikifikiri kama atafika au hatofika. Nikakaa sana lakini hakutokea nikasuburi tena na tena lakini sikusikia hata arufu yake, nikakubali matokeo na kuamua kuondoka eneo lile wakati naondoka nikakutana nae ana kwa ana kumbe nae alifika muda mrefu akawa akinitazama na kutaka kujua nini nitafanya endapo hatofika. Moyo ulishtuka mno nikajikuta nikimkumbatia na kutotamani muachia, kwa mara ya kwanza nikaona muitikio chanya toka kwake, tofauti na ilivyokuwa awali alikuwa hataki ata nimguse nikahisi moyo wangu kuchanua na kupendeza tena. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Priya! kwanini ulitaka nitelekeza jangwani, wakati unajua wewe ndiye pekee unayenipa tumaini la kuishi"

    "Nea nahisi kuchanganyikiwa Nea, sijielewi"

    "Moyo wako unasemaje?"

    "Nea nimekuwa nawe kwa siku 4 sasa, lakini nahisi kukufahamu kwa zaidi ya hizo siku, tuachane na hayo nipo hapa kukamilisha deni langu na kesho ni siku ya mwisho!"

    Priyanka akasema huku akiwa ameishika mikono yangu, mawazo yakanipeleka mbali nikahisi kushindana na nafsi yangu, nikatamani kumueleza lililo moyoni mwangu lakini nikahofu anaweza kuchukia na asinipe nafasi tena ya kuwa karibu nae.

    "Kwa hiyo hatuwezi kuwa karibu baada ya kesho?"

    "Ndiyo mkataba wetu utakuwa umeisha na sitokuwa na sababu ya kuwa karibu na wewe" akanijibu,

    "Priyanka!"

    "Nea!"

    "Kwa siku hizi zote tulizokuwa pamoja hukuhisi chochote moyoni mwako juu yangu?" nikauliza.

    "Sijahisi wala kufikiria chochote juu yako zaidi ya kuwa mtumwa kutimiza masharti ya mkataba"



    Jibu lake liliuhuzunisha mtima wangu, nikahisi kama tamthilia vile itawezekana vipi mtu niliyekuwa nae kwa siku 4 mfululizo asiwe na fikra wala kutokumbuka lolote toka kwangu, nikahisi mpango mzima umebuma sikuwa na la kuendelea kuongea nikaamua tuishie hapo kwa siku hiyo nikaagana naye akaondoka nami kuendelea kubaki eneo ilo huku nikifikiri nitaimaliza vipi siku iliyobaki.



    ************************************



    "Samahani Christine, Priyanka yupo?" Regy akauliza.

    "Wewe wanini usiku huu!" akajibu.

    "Tunataka tujue tuu maana Nea, hatujamuona hadi muda huu kwa hiyo tulifikiri labda yupo naye"

    Christine akawaangalia akatoa kicheko cha kebehi kisha akawajibu

    "Mhm kwa hiyo Priyanka amekuwa mlinzi wa Nea!"

    "Sisi tunajua ni marafiki kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa Priyanka kujua Nea alipo ndio maana tumekuja kumuuliza"





    Christine akasonya kisha akaingia kwenye hema lake bila kusema neno,

    "Asee huyu manzi angekuwa bongo kashachezea kichapo saa hizi, anamajibu ya kisolo kichizi" Mzovu akasema.

    "Oyah mi naanzisha tifu hapa, huyu mtoto wa kike hawezi kutujibu kiajabu akaondoka tunamwangalia", steve akasema, wakaanza piga piga lile hema hadi wote wakaamka na kutoka nje.

    "Mboni mnatufanyia fujo usiku huu?" Priyanka kwa hasira akawauliza rafiki zangu.

    "Eenh! Wewe ndiye tuliyekuwa tukikuhitaji, tuambie ndugu yetu yuko wapi hadi muda huu hatujamuona!"

    "Nea hajaonekana?” Priyanka alishtuka kusikia hivyo.

    "iIlo jibu si swali, sisi tunafahamu wewe ndiye uliyekuwa naye" Mzovu akasema.

    Priyanka akarudi hemani akavaa sweta na kuwaambia nifateni, maswahiba zangu bila kusita wakaungana na kuanza kunisaka.



    *********************************



    Baada ya Priyanka kuondoka nikahisi moyo wangu kujawa na ganzi, sikutamani kurejea walipo wenzangu nikatoka eneo lile na kusonga mbele zaidi usiku ule hadi nilipokutana na nyumba ambayo haikukaliwa na watu kwa muda mrefu, nikaingia na kutafuta tafuta kuni kisha nikakoka moto na kukaa huku nikiendelea kuwaza na kuwazua juu ya Priyanka, moyo uliuma mno maswali kadhaa yakatiririka kwenye ubongo wangu nikajikuta nikichukuliwa na usingizi mzito.



    "Nea! Nea! Nea!", nikiwa usingizini nikahisi kwa mbali kuitwa, katika hali ya uchovu nikafungua macho yangu kuona nani aliyekuwa akiniita, alikuwa mwanamke ninayempenda kuliko kitu chochote duniani namaanisha Priyanka akiwa na rafiki zake pamoja na maswahiba zangu, nikainuka kichovu na kuketi.

    "Kwanini umetuweka roho juu jamaa yangu?" Regy akauliza.

    "Mimi nilijua Priyanka kashakutoa kafara, nilitaka muanzishia kisanga" Steve akadakia na wote tukajikuta tunacheka.

    "Samahanini jamani, nilijikuta nikitamani kumalizia usiku huu sehemu tofauti na nilipozoea kuwa, katika kuzunguka nikajikuta nimefika hapa, na nyie mmepajuaje hapa?"

    "Ebhna eenh! Priyah ndiye aliyetusaidia hadi kufika hapa”



    Nikamtazama mrembo yule kisha nikamshukuru.

    Wote wakajikuta wakivutiwa na sehemu ile wazo la kurudi walipo wenzetu likatoka tukaongeza kuni na kuuzunguka moto jumla yetu tulikuwa 8 wasichana wanne na wavulana wanne, tukapiga stori za hapa na pale, muda wote nikawa kimya hadi nilipoona wote wameanza kuchoka.

    "Naomba niwasimulie kisa cha mfalme upepo"

    "upepo!"

    "Ndiyo! Mfalme upepo!" kila mmoja akajivuta na kukaa sawa tayari kusikia simulizi hiyo.



    "Mfalme upepo alikuwa na binti yake mrembo sana, wavulana wengi toka karibu kila falme za dunia, wakaitaji kumuoa binti upepo, kila mmoja alionesha ufahari wake mbele ya binti huyo, lakini hamna aliyefanikiwa kuuiba moyo wake. Siku moja binti mfalme alikuwa akisafiri kwenda upande wa kaskazini ya falme ya baba yake, njiani punda wake akapata na matatizo akashindwa kwenda alipotazama huku na huko akamuona kijana mmoja ambaye anatoka katika familia ya kimasikini, alipomuona akamuomba ampeleke kaskazini na kuahidi kulipa fadhila pindi arudipo katika ufalme wa baba yake, lakini kijana yule alikataa kata kata na kumwambia binti mfalme ninachoitaji toka kwako ni urafiki tuu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari ya kutoka hapo alipo hadi kufika kanda ya kaskazini ya ufalme wa baba yake inachukua siku 5, basi binti mfalme akakubali na kwa pamoja wakaongozana, njiani wakazoeana na wakajikuta wakipendana sana. Siku moja kabla ya kufika binti mfalme akamwambia yule kijana waweza niacha hapa huko mbele nitafika mwenyewe, kijana akatii matakwa ya binti mfalme, akamsogelea kisha akamwambia,

    "Will you marry me!?(Je utakubali nikuoe..?)"

    "Yes i will (ndiyo)" Binti mfalme kwa furaha kuu akaitikia.

    Wakakumbatiana na bila hiyana kijana akampa busu motomoto na huo ndio ukawa mwanzo wa mapenzi yao.

    "No no no!!!! Nea haijaishia ivyo"



    Alisema Priyanka ambaye kwa asilimia 95 stori ilimuhusu, wote wakashangaa Priyanka ameijuaje stori ile, Nea akamtazama Priya kisha akacheka akajiegeza chini na kuwaachia kila mmoja aifikilie stori ile huku akivuta usingizi. Ghafla hali ya hewa ikabadilika mvua ikaanza kunyesha, radi na ngurumo nzito zikazidi kuwatia hofu hasa wasichana, ikabidi wote tuwe pamoja na kwa mara nyingine nikaridhishwa na ukaribu wa Priya ambao kiukweli ulifanya nijihisi faraja moyoni.

    "Nea kwa nini umeongopa?" Priya akaniuliza kwa sauti ya chini kuogopa kuwasumbua wengine ambao walishalala.

    "Nimeongopaje?”

    “Umesema binti mfalme alimkubalia yule kijana amuoe na akamkisi wakati si kweli"

    "Priyanka nikwambie kitu"

    "Ndiyo niambie"

    “wewe ni mzuri zaidi ya neno uzuri, unapendeza nyakati zote ukicheka na hata ukilia....." kabla sijaendelea akashtuka na kuniangalia

    "Nea are you mr.X (Nea wewe ni mr. X)?"

    "Yes i am (ndiyo mimi ndiye)" nikajibu, akanipiga kofi zito ambalo lilinishtua mno.

    "Kwanini unacheza na hisia zangu Mr. X sasa nimejua lengo lako na kamwe huwezi kufanikiwa kwaheri".

    Katika siku nilioharibu siku iyo ndiyo nilikologa niliamini nikimwambia kuwa mimi ndiye mr. X niliyemfanyia yote yale, ataweka moyo wake juu yangu lakini haikuwa hivyo, akahisi nina nia mbaya nae nikajilaumu mno. Priya hakujali mvua akatoka nje kwa kasi huku akilia nami nikatoka kwa kasi kumfatilia nikaogopa uenda baya laweza kumkuta nikamkuta amesimama chini ya mti akilia sana.

    "Am sorry Priya! (Nisamehe Priya)" nikasema lakini akaendelea kulia huku akisema.

    "Why Nea? Why....! (Kwanini lakini?)"

    Mvua ikazidi kupiga kwa kasi hasira za mwanadada yule zikazidi kuongezeka akachukua kipande cha mti na kuanza kunipiga nacho, nikakidaka akaendelea kunipiga makofi mfululizo nikamtuliza na kumwambia.

    “I love you! (Nakupenda)"



    Akanikata jicho la hasira nilipotamka hilo neno, akaniongezea makofi mfululizo nikamsogeza hadi kwenye mti na kumbusu kwa nguvu, mwanzoni alinisukuma lakini kadri muda ulivyoenda joto la hasi na chanya lilipanda akatulia.



    Fahamu zetu zikahama wala hakuna aliyeelewa kilichokuwa kikiendelea katika dunia ya kawaida, nikashtuka baada ya kusikia watu wakikohoa kutazama nikawaona maswahiba zangu. Hapo fahamu zikanirudia nikaona haya mno Priya nae hakuamini kama ingefika siku ningembusu vile, kila mtu akabaki ameduwaa, Priya akaondoka kurudi walipo wakina Christine bila kusema neno huku nyuma nikabaki na rafiki zangu wakaanza shangilia na kutoa sifa za kijinga.



    "Duuh! Nea weee ni noumah, mtoto mkali vile leo duuuh aaaah!" njia nzima rafiki zangu wakawa wanashangilia utafikiri labda wametoka kwenye mechi.



    Siku ikapita asubuhi ikaingia, kila nilipomuangalia Priya roho iliniuma zaidi nikakumbuka kilochotokea usiku nikawa sina namna zaidi ya kukubali matokeo, safari ya kurejea chuo ikaanza nikakaa gari moja na Priya lakini tukawa kama hatufahamiani vile, akawa akipiga stori za hapa na pale na wenzie mara acheke mara anune, vyote vilikuwa kheri maana vilionesha dhairi uzuri aliokuwa nao. Tukafika chuo na kushuka, yeye akatangulia nami nikafata ile nashuka chini natazama alipo, roho iliniuma zaidi alikuwa ni mchumba wake amekuja kumpokea wakakumbatiana kwa zaidi ya dakika sikuweza kustahimili kuwa eneo lile nikaondoka zangu.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ebhana eeenh! Mboni kama sielewi elewi, imekuaje tena lile lijamaa likamkumbatia shemeji yetu?! " Steve akauliza.

    "Alafu kweli asee yaani jamaa mubashara mbele za watu" mzovu akaunganishia.

    "Jamani kiukweli mimi nililazmisha kuwa na Priyanka ila yule ndiye mwenye mali kwa hiyo kuanzia leo, tusahau kuhusu yeye".

    "Mhmh! Mimi sijaelewa bado, jana nimekukuta umemshikilia mtoto unampa mabusu mazito", Regy akasema kwa mshangao.

    Ikabidi niwasimulie kila kitu kuanzia mr.X hadi mapenzi yale ya mkataba wa siku 5, wote walishangaa mno wakanitia moyo na kukubaliana nami.



    Masomo yakaanza kwa kasi nikahama sehemu niliyokua nikikaa awali kwa kutotaka kuwa karibu na Priyanka, wiki ikakatika bila mawasiliano yeyote, moyoni mwangu nikaanza kukubali matokeo. Siku moja nikiwa natoka zangu darasani naenda mtaani, nikamwona Christine nikataka kumpita akaniita nikasimama kumsikiliza.



    "Nea ninashida naomba msaada wako" alisema Christine.

    "Shida gani?"

    "its about Priyanka (kuhusu Priyanaka)”

    "Amefanya nini Priyanka?"

    "Hana raha, amekuwa akikutaja wewe kila mara na wakati mwingine anajisahau na kumuuita mchumba wake jina lako"

    "Kwa hiyo unaitaji mimi nifanye nini?" nikauliza.

    "Priya anahitaji kukuona kabla hajaolewa”

    "Priya anaolewa?" nikauliza kama vile sikusikia alichosema Christine.

    "Ndiyo anaolewa na anaomba kukutana na wewe leo saa 3 usiku"



    Akanilekeza sehemu ya kukutana naye basi nami kwa roho moja nikakubali na kuendelea na safari yangu kabla sijafika mbali zaidi akaniita tena nikasimama kumsikiliza.

    “Aah! Nea samahani nimesahau kitu" alisema na nikamtazama na kumruhusu aseme.

    “Amesema uje peke yako"

    "Sawa".

    Nilivyofika geto nikawapa stori nzima maswahiba zangu, sikua na imani na Christine hata kidogo nikahisi kama anataka kuniuza hivi, lakini wakanipa moyo na kunambia nikasikilize wito.



    ***********************************



    "Kwanza nikushukuru kwa kipindi hiki kifupi ulichofahamiana na binti kiukweli amebadilika sana, hakuwa mtu wa kupika wala kufanya kazi yeyote, matumizi yake kwa wiki ni ghali mno" Alisema mama yake Priyanka ambaye nilionana nae badala ya Priyanka mwenyewe.

    "Ukweli binti yangu anakupenda na hilo halipingiki kabisa, lakini nakuomba tuu mwache Priya aolewe na mwanaume ambaye ni chaguo la familia yetu"

    "Sawa mama, mimi nimekuelewa yeye aolewe tuu mimi sina tatizo" nikamjibu yule mama japo moyoni iliniuma sana.

    "Priya hawezi kubali kuolewa bila wewe kutamka kuwa haumuitaji"



    Hilo likanitisha zaidi nitaanzia wapi kumwambia simpendi mwanamke niliyeangaika kuwa nae nikashindwa kumweka mikononi mwangu japo nipo naye moyoni, ulikuwa mtihani mzito sana na wala sikuwa tayari kuonana na Priyanka hasa baada ya kugundua kuwa naye amenipenda.

    "Mama! Nimemruhusu aolewe"



    Mama yake Priyah akafurahi akanambia niende nyumbani kwake siku inayofata nikayamalize kwa Priya. Siku iliyofata nikaenda kama nilivyoahidi jana kufika nikabonyeza kengele, mlinzi akafungua geti baada ya kumuelezea kuwa nahitaji kuonana na mama yake Priyanka akaniruhusu, nikaendelea kupiga hatua hadi nilipoifikia nyumba hiyo ya kifahari sana napo nikabonyeza kengele mlango kufunguliwa nikahisi kupigwa shoti na kama kuzimia hivi. Ikawa ni uso kwa uso na Priyanka, nikaisi miguu mizito, sikuelewa niingie au nirudi,ata yeye mwenyewe akawa ameduwaa hakutegemea kama naweza kufika kwao

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nea...!"

    "Naam"

    "Umefata nini hapa?"

    "Mama yako anahitaji kuongea na mimi na ameniomba nije hapa"

    "Sawa karibu" nikaingia japo kiuoga nikakaa kusubiri mama yake na Priyah aje.

    "Nea! Bahati mbaya mama ametoka ila atarudi muda si mrefu”

    Nikatazama saa vizuri nikajua kuwa nipo sahihi na muda ambao nilikubaliana na mama yake Priyanka, nikawa najiuliza kwanini atoke wakati nilikubaliana nae nitakuja muda huo. Nikiwa bado nayawaza hayo nikashtushwa na Priyanka

    "Nea samahani kwa kuukatili moyo wako, sikujua ni kiasi gani inauma kumkosa mtu unaempenda"

    "Unamaana gani?" nikamuuliza kana kwamba sikuwa naelewa nini kinaendelea ndani ya mtima wa mrembo Yule.

    "Nilikuwa kipofu nisione mwanga wenye thamani halisi ya kupendwa, nikawa mbinafsi kutojali kile unachohisi kwangu, lakini kwa kipindi ambacho nimekukosa hali si shwari kwangu, Nea nimejifunza vingi toka kwako na sioni haya kukwambia nakupenda tena sana"



    Nikahisi mwili wote ukisisimka ukweli nampenda sana Priyanka lakini itakuaje juu ya kile alichoniambia mama yake kuwa familia tayari ilishamchagua mtu wa kumuoa Priya, nikabaki kimya nisijue lipi sahihi la kusema.

    "Nea! Sema kitu tafadhali"

    Bado nikashindwa kuongea sauti ya mama Priya ikawa inashindana na nafsi, je nifate alichosema mama Priyah au nifate nini moyo wangu kinahitaji.

    "Priyah! Nakupenda tena sana tuu, lakini nahisi kuna upinzani mkubwa kwenye mapenzi yetu"

    "Nea! I don't care, what i need is to be with you for the rest of my life (sijali, ninachotaka ni kuwa na wewe katika siku zote za uhai wangu)"



    Baada ya kusikia jibu hilo sikuweza kujizuia tena zaidi ya kumsogelea na kumkumbatia kwa nguvu mno,

    "Priyanka sitaki nikupoteze,nipo tayari kwa lolote"



    Machozi ya faraja yakanitoka, Priyah nae akuweza zuia machozi yake wote kwa pamoja tukajikuta tukilia, nililia zaidi hasa nilivyokuwa nikikumbuka msoto nilioupitia hadi leo hii mrembo huyo kuwa mikononi mwangu. Tukashtushwa na hatua za mtu ambaye alikuwa akija tulipo. Tukaachiana kuangalia ni nani anayetukaribia, alikuwa ni mama ake Priyanka alionekana mwenye hasira sana, nilipomtazama vizuri macho yake yalikuwa mekundu kama vile mtu aliyekuwa akilia kwa muda mrefu

    "No! Priyah this can not be real (hapana Priyah hili haliwezekani)"

    "Mamy please! I love him (tafadhali mama, nampenda sana)",





    "Priyah what should i do, you belong to someone else, so please end with him now, (Priyah mimi sina la kufanya wewe ni mchumba wa mtu kwa sasa, achana na huyo tafadhali".

    "Mama! Siwezi kuishi bila ya yeye, naomba uelewe na kuheshimu hisia zangu"

    Yalikuwa majibizano kati ya Priya na mama yake, mama hakutaka uhusiano wetu uendelee sababu Priyah tayari alishachumbia na muda si mrefu alitakiwa aolewe, ikabidi niingilie kati majibizano yale na kumuweka wazi mama Priyah kuwa sikuwa tayari kumpoteza binti yake mama hakuwa na la kusema zaidi ya kutoa machozi na kunitaka niondoke kabla baba yake priyah ajarudi.



    *********************************



    Mapenzi yalianza kushamiri kwa kasi mno hakukuwa na kificho kati yetu, maisha tuliyafanya kuwa rahisi sana, tukazoeana na kupendana zaidi kadri ya siku zilivyosogea. Kutokana na umaharufu wa Priyah uhusiano wetu ukachukua sura mpya katika vyombo vya habari, wapo waliouponda sababu ya ubaguzi wa utaifa na rangi, wapo waliosapoti kwa kuwa nguvu ya mapenzi haina kikomo na huweza tokea kwa mtu yeyote bila kujali dini wala utaifa. Kwangu ilikuwa ni zaidi ya neno furaha.

    "Nea tukishaoana utapenda nikuzalie watoto wangapi?",

    "12 tu wananitosha!!!", CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nini!! Hao 12 mbili nawazaa mimi wote au kuna mwingine atanisaidia?"

    "Mhm mwingine ataniharibia, wote utawazaa wewe!"

    “Mhm! Honey! You cant be seriously"

    "Am serious my love, si unajua mumeo nina vipaji vingi, nataka wanangu warithi, alafu nilishindwa kuwa padri mtoto mmoja itabidi atimize hilo"

    "Hahaha! Nea wewe uwe padri mhmh! Ila mpeni watoto 12 ni wengi nitazeeka haraka"

    "Usijali kipenzi utazaa mara ya kwanza 6 mara ya pili 6!"

    "Aaaaaah! Nea kumbe hunipendi eeenh!"

    "Nakupenda sana mpenzi"



    Ilikuwa ni moja ya siku za faraja sana katika maisha yangu, tuliongea mengi sana kuhusu maisha yetu ya baadae.

    Mapenzi yangu na Priya yakawa kivutio mbele ya macho ya wengi, kila mwanaume aliitamani kuwa sehemu yangu na kila mwanamke alitamani kuwa sehemu ya Priyah, Wengi wanafikiri kuwa mapenzi si rafiki wa elimu, wapo wenye mtazamo ambao naweza kuuita hasi kuwa ukichanganya mapenzi na masomo basi kuna asilimia kubwa ya kufanya vibaya, lakini kwa upande wetu haikuwa ivyo tulikuwa vinara kwa kila somo basi watu kila wakatupachika jina la Prinea.



    *************************************



    "Christine i need your help! (Christine nahitaji msaada wako)",

    "Mhm on what? (msaada wa nini?)".

    "Nitakulipa chochote utakacho, watenganishe Nea na Priya".

    "Hapana Rajesh, Priya ni zaid ya rafiki kwangu, siwezi mfanyia kitu kama iko",

    "Christine siku zote rafiki mwema umtakia mema rafikiye, kama una upendo wa kweli kwa rafiki yako kwanini umekubali awe na yule nyani?" alisema Rajesh lakini christine hakuwa na jibu.

    "Fanya kama nilivyosema" Rajesh akaondoka huku akimuacha Christine njia panda asijue la kufanya.



    **********************



    "Samahani Nea!" Ilikuwa sauti ya mtoto wa kike ambae sikuwa namfahamu, siku hiyo baada ya vipindi niliamua kubaki darasani kufanya baadhi ya maswali ambayo tuliachiwa siku iyo. Nikaacha nilichokuwa nafanya na kumsikiliza shida yake.

    "Nimekwama baadhi ya maswali,naomba msaada wako tafadhali" akanambia msichana yule mwenye asili ya mabara mawili asia na afrika, nikamtazama machoni ili kujua kile ndicho kilichomleta au kuna mengine, nikaona ana hofu kuu moyoni mwake sikujua imetokana na nini, sikujichosha kufikiria sana nikaamua tufanye maswali Kwa pamoja, haikuchukua muda tukamaliza, akanishukuru na kuondoka.



    Nikamalizia kazi yangu na kuanza safari ya kurudi nyumbani, njiani nikakutana na gari la kifahari sana likiwa limepaki nilipolikaribia, mlango ukafungulia nikajikuta navutwa ndani sikujua kilichoendelea, niliporejewa nafahamu nikajikuta kwenye kiwanda kikubwa mno sikuona mlango wa kuingilia wala kutokea na wala sikujua ni sehemu gani.

    "Nea usiogope! Sisi hatuna uadui na wewe ila jua kuwa vizuri vina gharama, unampenda sana binti yangu Priya naye anakupenda kiasi kwamba hawezi sikia lolote nimuambialo"

    Nilihisi mwili wote kufa ganzi hasa baada ya kugundua yule aliye mbele yangu ni baba wa mwanamke nimpendaye.

    "Ni kweli nampenda binti yako na sikumpendea umaarufu wala uwezo wa kifedha toka familia yake, nimempenda kama alivyo na sitaki kumpoteza" Mzee akacheka sana na wote waliomo mle wakacheka mno, sikujua nini kinawafuraisha

    "Nimependa ujasiri wako na nadhani hujanifahamu vizuri, nakuacha endelea na binti yangu maana siwezi kukuadhibu kwa kumpenda naye kukupenda ila siku utakayo uvunja moyo wa binti yangu, sitokuacha mzima"

    Mzee akaongea hayo walau kidogo moyo wangu ukafarijika nikiwa na imani kuwa haitotokea siku nikamsaliti

    Priya wangu.



    ***********************



    Nilivyorudi geto sikusimulia kitu, japo nilikuwa na furaha sana swala hilo liliwapa maswali mengi rafiki zangu wakatamani kujua nini kikichojiri hadi kuwa na furaha kiasi iko. Mzovu akanipa kikaratasi chenye ujumbe kusoma jina la mtumaji ni Vanessa sikuwa namfahamu nikaamua kusoma ndani, nlipoanza kusoma tuu nkaanza shikwa na mshangao.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sikukimalizia ikabidi nitoke ndani kwa haraka bila kusema naenda wapi, mapigo ya moyo yalienda mbio mno nikafika eneo ambalo ujumbe ulinitaka nifike nikakuta Vanessa analia mno, nikamsogelea

    "Whats wrong with you? (Una shida gani?)". Akaendelea kulia kwa nguvu, akazidi nichanganya nikatamani ka nimpige kofi atulie lakini nikaona si njia sahihi.

    "Hey Van calm down and tell me what the hell is going on! (Tulia basi Van embu niambie nini kinaendelea)".

    "Nea i broke up with my boyfriend, b'se he thought am dating you, he saw us that day when you helped me to solve those questions (nimeachana na mpenzi wangu sababu anahisi nina uhusiano na wewe alituona ile siku uliyokuwa ukinisaidia kufanya yale maswali)".

    Nilichukia mno nikajua amefiwa au amekutwa na tatizo gani kubwa hadi kuniweka roho juu, akaendelea kulia nikamkaribia Zaidi na kumwambia,

    "Crying is not a solution, tell me where can i find him, i will make everything clear (hatutofikia muafaka kama utaendelea kulia nielekeze alipo na nitajaribu kumuelewesha)".

    "Nea am not sure if he will agree to meet you, sababu ana hasira mno mwache kwa sasa" akaongea Vanessa huku machozi yakizidi mtoka, nikatoa leso yangu na kumfuta machozi kisha nikamkumbatia na kumsihi asiendelee kulia kila kitu kitakuwa sawa.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog