Simulizi : Darkness Of Comfort (Giza Lenye Faraja)
Sehemu Ya Nne (4)
Watoa vifusi walikuwa wakiendelea na kazi yao ya kutoa vifusi kama kawaida, miili ya watu waliokufa iliendelea kutolewa huku kukionekana kutokuwa na majeruhi wengine waliokuwa wamebakia.
Hali ilitisha mno, hakukuwa na mtu aliyevumilia, wengi walihuzunika lakini kuna wengine ambao walikuwa wakilia tu, mioyo yao iliumia kupita kawaida.
Wakati wanaendelea kutoa vifusi hivyo, ghafla, watu fulani ambao walikuja na gari la serikali mahali hapo wakaonekana kushtuka, mbali na miili ambayo walikuwa wakiendelea kuitoa katika vifusi hivyo, kulikuwa na mwili wa mtu mmoja, kwa kumwangalia alionekana kama mtu aliyekata roho lakini kwa mbali, mikono yake ilikuwa ikichezacheza.
Walichokifanya watu wale ni kupiga kelele za kuwaita wenzao, walipokuja, wakasaidiana kukitoa kifusi hicho, mtoto aliyekuwa na miaka kumi na saba, akatolewa huku akiwa anahema kwa mbali sana kwani hata waliposikiliza mapigo yake ya moyo, yalikuwa yakidunda kwa mbali mno.
“他死了” (anakufa) alisema mtu mmoja, mmoja wa waokoaji wa watu wale waliokuwa wakitoa vifusi.
“讓他走” (tumpelekeni hospitali) alisema jamaa mwingine.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakukuwa na muda wa kupoteza, siku hiyo, hawakuwa wametoa majeruhi hata mmoja, kila waliyekuwa wakimtoa, alikuwa amekwishakufa. Toka siku iliyopita ambapo tetemeko kubwa la ardhi lilikuwa limetokea, ni watu wachache ndiyo waliokuwa wamenusurika kufa, ila wengi walikuwa wamepoteza maisha.
Wakamchukua Richard na kuondoka naye kuelekea hospitali, bado mapigo yake ya moyo yaliendelea kuwa chini mno, kila aliyekuwa akimwangalia mtoto huyo, ilionekana dhahiri kwamba muda wowote ule ungeweza kukata roho.
Mara baada ya kumfikisha katika hospitali ya Jiji la Yunnan, machela ikaletwa, akapakizwa na kuanza kupelekwa katika chumba maalumu kwa ajili ya kuanza tiba.
Alikuwa kijana mweusi, walimkuta katika kifusi cha nyumba ya serikali iliyoanguka, nyumba ambayo ilikuwa ikikaliwa na watu masikini ndani ya jiji hilo.
Kitu cha kwanza kabisa, ili kuyarudisha mapigo yake ya moyo, wakamuwekea dripu yenye dawa maalumu ya kuyarudisha mapigo yake ya moyo katika hali ya kawaida. Katika kila kitu kilichokuwa kikifanyika, Richard alikuwa kimya, hakujua kitu gani kilichokuwa kikiendelea mahali hapo.
****
“Hakuna fedha,” ilisikia sauti ya Pong, kila mmoja akashtuka.
“Unasemaje?” aliuliza bwana Tai Peng huku akisogea karibu zaidi, alitaka kuhakikisha kile alichokuwa ameambiwa.
Alionekana kuchanganyikiwa, maneno aliyosema Pong kwamba ndani ya akaunti ya mzee Walusanga hakukuwa na fedha yoyote ile ilimchanganya. Alipomsogelea Pong, akaanza kuangalia vizuri kwenye kompyuta kwani alihisi kwamba hata kwenye ile televisheni hakuwa akiona vizuri.
Kile alichokuwa amekizungumza Pong ndicho kilichokuwa kimetokea, akaunti ya mzee Walusanga haikuwa na fedha hata dola moja. Zilikwenda wapi? Au zilihamishwa, hakukuwa na mtu mwingine? Hakuna aliyejua.
“Unanitania,” alisema bwana Tai Peng, alionekana kuchanganyikiwa.
“Hakuna kitu, nahisi zilihamishwa,” alisema Pong.
“Unaweza kuangalia ‘bank statement’ ya akaunti tujue zilihamishwa kwenda akaunti gani?” aliuliza bwana Tai Peng, kichwa chake kilichanganyikiwa kabisa.
“Hakuna tatizo.”
Kama ilivyokuwa kawaida, yake, Pong akaanza kazi yake ya kuangalia ni akaunti gani fedha hizo zilikuwa zimehamishiwa.
Kazi haikuwa nyepesi hata mara moja, bado vidole vyake vilikuwa vikiendelea kubonyeza vitufe vya kompyuta yake ya mapajani (laptop). Hata yeye mwenyewe alionekana kuchanganyikiwa, kuingia ndani ya akaunti ile na kukuta hakukuwa na fedha yoyote na wakati aliambiwa kwamba mtu huyo alikuwa bilionea, kulimchanganya.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Umepata nini?” aliuliza bwana Tai Peng.
“Fedha zake hazikuamishwa ila zilitolewa,” alijibu Pong.
“Nani alizitoa?”
“Sijajua, hilo ndiyo la kufuatilia huko benki,” alisema Pong.
Bwana Tai Peng hakutaka kubaki kimya alichokifanya ni kuwatuma vijana wake waelekee Benki ya Chinesse na kuuliza ni nani alikuwa amezitoa fedha hizo kutoka katika akaunti hiyo.
Baada ya dakika kadhaa, vijana hao walikuwa katika benki hiyo ambapo wakaomba kuonana na meneja kwa kuwaambia kwamba walikuwa vijana kutoka kwa bwana Tai Peng.
Kitu alichokifanya meneja yule ni kupiga simu kwa bwana Tai Peng ambaye akathibitisha kwa wale walikuwa vijana wake na hivyo kuwaruhusu kuingia ndani. Swali aliloulizwa ni moja tu, ni nani aliyekuwa amekuja kuchukua fedha za mzee Walusanga Ndaki.
“Alikuja yeye mwenyewe kama wiki mbili zilizopita,” alijibu meneja.
“Alikuwa peke yake?”
“Kifamilia, alikuja peke yake, ila mbali na hapo, alikuja na mwanasheria wake,” alisema meneja.
“Kwa hiyo walizichukua hizo fedha?”
“Ndiyo. Ila walipoelekea baada ya hapo, hatujui, labda atafutwe mwanasheria wake,” alisema meneja.
“Mwanasheria wake ni nani?”
“Pei Pei Young,” alijibu meneja.
“Huyu mwanasheria maarufu ninayemfahamu?”
“Ndiye huyohuyo.”
“Sawa. Hakuna tatizo. Mpaka nyumbani kwake tunapafahamu. Asante sana,” alisema kijana mmoja na kisha kutoka ndani ya ofisi ya meneja huyo.
***
Taarifa zilipomfikia bwana Tai Peng, moja kwa moja akawatuma vijana wake wengine kwa mwanasheria wa mzee Walusanga, Pei Pei Young aliyekuwa akiishi katika Mtaa wa Wun-Wen uliokuwa pembezoni mwa jiji la Chixiong.
Vijana wale wakajipanga vilivyo, wakachukua bunduki zao na kuanza safari ya kuelekea Wun-Wen. Walipofika huko, hawakutaka kupoteza muda, wakaelekea katika sehemu iliyokuwa na nyumba kubwa na ya kifahari ya mwanasheria huyo.
Walipofika, kwa sababu ilikuwa usiku, kitu cha kwanza kabisa, wakawazimisha walinzi na kuanza kuusogelea mlango wa kuingia ndani huku wakiwa wamekwishaambiwa kwamba mwanasheria huyo na familia yake walikuwa ndani ya nyumba hiyo. Mlango haukuwa na kitasa bali kulikuwa na kimashine kidogo kilichokuwa na vitufe kadhaa kama kalkuleta ambacho hutumika kuingiza namba za siri na mlango kufunguka.
Hapo, wakaonekana kuwa kwenye hali ngumu, hawakuzifahamu namba za kuufungulia mlango huo wa chuma ambao pia haukuwa rahisi kupigwa na kung’oka, walichokifanya ni kuzunguka upande wa pili mpaka kwenye dirisha moja dogo la choo, hapo ndipo walipotaka kupatumia kuingilia ndani.
Wakaanza kubebana na kuvivunja vioo vya madirisha hayo na kupenya ndani. Tofauti na hali ya kawaida, nyumba nzima ilikuwa kimya kitu kilichoonyesha kwamba inawezekana walinzi walikuwa wamewadanganya kwamba mwanasheria Pei Pei alikuwepo ndani ya nyumba hiyo na familia yake, wakawarudia walinzi.
“Mmetudanganya!” alisema jamaa mmoja.
“Wapo ndani. Hakuna mtu aliyetoka,” alisema mlinzi mmoja.
“Mnatutania sasa,” alisema jamaa mmoja, usoni alikuwa amevaa kinyago kama wenzake.
“Kweli tena.”
Hakukuwa na kingine cha kuuliza, alichokifanya ni kuchukua bunduki yake na kummiminia mlinzi mmoja, damu zikaruka na kubaki kimya mahali hapo. Akageukiwa mlinzi mwingine.
“Tuambie ukweli, Pei Pei yupo wapi?”
“Sijui, alikuwa ndani,” alisema mlinzi yule huku akitetemeka kwa hofu, tayari kifo kilikuwa mlangoni.
“Unatutania.”
“Kweli, alikuwa ndani,” alisema mlinzi yule.
Hawakutaka kushughulika naye sana, walichokifanya ni kurudi tena ndani ya nyumba ile na kuanza kumtafuta. Walikwenda kwenye kila chumba na kila sehemu huku wakihakikisha kwamba hakukuwa na handaki.
“Mmemuona?” aliuliza jamaa mmoja.
“Hapana. Ila tuna wasiwasi.”
“Wasiwasi wa nini?”
“Tumesikia minong’ono ndani ya chumba kimoja ambacho kimefungwa, bila shaka wapo huko. Twendeni,” alisema jamaa mmoja na kuanza kuelekea katika sehemu iliyokuwa chumba kile.
Walipoufikia mlango, wakakishika kitasa na kuanza kuufungua, mlango ulikuwa mgumu kufunguka, hawakutaka kukata tamaa, waliendelea kuufungua mlango ule na walipoona kwamba unakuwa mgumu kufunguka, wakaanza kuumiminia risasi mfululizo, sauti za watu waliokuwa ndani ya chumba kile zikaanza kusikika.
“Wapo ndani,” alisema jamaa mmoja na kuendelea kuumiminia risasi mlango ule, wala haukuchukua muda, ukafunguka na kuingia ndani. Mwanasheria, Pei Pei alikuwa amepiga magoti chini huku akilia kama mtoto, mbali na yeye, pembeni mwake kulikuwa na familia yake ambao wote walikuwa wakilia.
“Umetusumbua sana mpumbavu wewe,” alisema jamaa mmoja na kumshika Pei Pei na kuanza kutoka naye nje. Alikuwa akimburuza tu bila kujali kitu chochote kile. Pei Pei akakiona kifo mbele yake.
Ingawa alijua fika mahali fedha zilipokuwa, usiku wa siku hiyo alijiahidi kwamba asingeweza kutoa siri, fedha zile aliambiwa kwamba ni za Richard, alikuwa tayari kuuawa lakini si kuusema ukweli.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
TULIPOTOKA
Mara baada ya kujikusanyia fedha nyingi na kuwa mtu mweusi wa kwanza kuwa tajiri nchini China, mzee Walusanga Ndaki anajikuta akiingia katika matatizo na tajiri wa China aitaye Tai Peng.
Wivu na tamaa ya kutaka kumiliki fedha za mzee Walusanga ndiyo unaompelekea tajiri huyo wa China kumuua mzee Walusanga na mkewe, bi Diana kwa ajili ya kujichukulia fedha hizo.
Huku kila kitu kikiwa kimekamilika, anakuja kugundua kwamba mtoto wa mzee huyo, Richard hakufa hivyo anaagiza vijana wake wamtafute kwani bila kumpata ingekuwa kazi bure kwa kuona kwamba inawezekana fedha hizo alizokuwa akitaka kuzichukua zikachukuliwa na mtoto huyo.
Huku akiwa amewatuma vijana wake kumtafuta na kumuua Richard, anaamua kumuita mtaalamu wa kompyuta kwa ajili ya kuzihamisha fedha za mzee Walusanga na kuziweka katika akaunti yake, cha kushangaza, mtaalamu huyo anapoingia katika akaunti ya mzee Walusanga, hawakuti fedha zozote zile.
Haishii hapo, anawatuma vijana wake waende benki kuangalia ni nani alikwenda kuchukua fedha hizo, ripoti anayopewa ni kwamba mzee Walusanga alikwenda na mwanasheria wake, Pei Pei na kuzichukua fedha hivyo, anachoamuru, Pei Pei atafutwe na kueleza ukweli ambapo vijana hao wanakwenda nyumbani kwa mwanasheria huyo, wanamchukua yeye na familia yake na kuwapeleka chumbani huku wakiwaburuza, kitu wanachokitaka ni kuambiwa mahali fedha zilipo.
Upande wa pili, msichana Shu Yan ambaye ni rafiki mkubwa Richard, haelewi mahali alipokuwa rafiki yake huyo. Mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa ni siku ile ambayo tetemeko la ardhi lilitokea katika Jiji la Yuannan. Baada ya hapo, ametembea sehemu nyingi kumtafuta rafiki yake huyo lakini hakufanikiwa kumpata. Kinachomjia kichwani ni kuona kwamba rafiki yake huyo alikuwa amekufa.
SONGA NAYO..
Richard alikuja kupata fahamu baada ya masaa matano kupita. Aliposhtuka tu kutoka katika usingizi huo, macho yake yakaanza kuangalia huku na kule, alikuwa ndani ya ukumbi mkubwa ambapo kulikuwa na vitanda vingi, kote huko kulikuwa na watu waliokuwa wamelala.
Kitu kingine ambacho alikiona mahali hapo ilikuwa ni dripu ya maji aliyokuwa amewekewa huku mdomo na pua yake vikiwa vimefunikwa na chombo maalumu cha kumsaidia kupata hewa safi kitandani hapo.
Japokuwa alijiuliza sana juu ya mahali alipokuwa lakini mwisho wa siku alikuwa na jibu moja tu kwamba mahali alipokuwepo palikuwa ni hospitali na kitu pekee alichokukuwa akikikumbuka ni kwamba mara ya mwisho kabisa alikuwa ndani ya jengo moja la ghorofa walilokuwa wakilitumia kwa kulala usiku, baadae, tetemeko la ardhi likatokea na jengo lile kuanza kuanguka, baada ya hapo, hakujua kile kilichokuwa kimeendelea zaidi ya kujikuta ndani ya chumba hicho.
Mwili wake ulikuwa umefungwa bandeji kitu kilichoonyesha kwamba alikuwa na majeraha makubwa mwilini. Akajitahidi kuinuka kitandani pale lakini akashindwa kufanya hivyo zaidi ya kusikia mwili ukimuuma tu.
Kumbukumbu zake zikaendelea kujirudisha kama mkanda wa filamu, akaanza kumkumbuka rafiki yake kipenzi, Shu Yan ambaye mpaka katika kipindi hicho hakujua alikuwa mahali gani, alitamani kuwauliza madaktari au manesi juu ya rafiki yake huyo, lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyetokea mahali hapo zaidi ya wale wagonjwa wenzake ambao wote walionekana kuwa kwenye hali mbaya.
Wala hazikupita dakika nyingi, nesi mmoja akaingia ndani ya chumba hicho, kwa haraka, akaichomoa ile mashine ya oksijeni iliyokuwa imepachikwa puani na mdomoni mwake na kumuita nesi yule.
“Hautakiwi kuitoa hii,” alisema nesi yule huku akianza kuirudishia mashine ile.
“Subiri kwanza. Hapa ni wapi?”
“Hospitali.”
“Hospitali gani?”
“Shwai Phei.”
“Nani alinileta hapa?” aliuliza Richard.
“Subiri kwanza. Weka hiyo mashine, nitakujibu maswali yako baadae,” alisema nesi yule na kuirudisha mashine ile kwa Richard.
Kichwa chake kilikuwa kwenye mawazo mengi juu ya rafiki yake, Shu Yan, hakujua kama alikuwa hai au naye alikuwa amekufa baada ya tetemeko lile la ardhi ambalo lilisababisha nyumba ile waliyokuwa wakiishi kuanguka.
Aliendelea kukaa hospitalini hapo zaidi, kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo majeruhi wengi wa tetemeko lile walivyokuwa wakiletwa. Japokuwa alijiona kuwa na majeraha makubwa lakini kuna kipindi kingine alimshukuru Mungu kwani watu waliokuwa wakiletwa walikuwa zaidi yake.
Hakuwa na ndugu wala rafiki, aliendelea kukaa ndani ya hospitali ile huku hata chakula alichokuwa akila ni kile kilichokuwa kikiletwa maalumu kwa wagonjwa ambao hawakuwa na ndugu wala marafiki ambao walikuja kuwaona.
Hiyo ilikuwa siku ya kwanza, alitegemea kuona Shu Yan akija mahali hapo kama alikuwa hai lakini hakuweza kufika, siku ya pili ilipoingia na kuona kimya, hapo ndipo alipogundua kwamba inawezekana rafiki yake huyo alikuwa amekufa katika tetemeko lile.
“Shu Yan upo wapi? Kama upo hai njoo nikuone na kama ulifariki, naomba nijue sehemu uliyozikwa,” alisema Richard huku machozi yakianza kumbubujika mashavuni mwake.
Ilipofika siku ya tatu, nesi yule ambaye mara kwa mara alikuwa akija kumuona akaingia ndani ya chumba hicho, aliwaacha wagonjwa wote na kwa mwendo wa harakaharaka akaanza kusogea kule alipolazwa Richard.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mkononi alikuwa na picha ya kijana huyo, uso wake ulikuwa ukionyesha furaha kubwa kitu kilichomshangaza sana Richard kwani siku hiyo alionekana kuwa tofauti na siku nyingine.
Alipomfikia, tabasamu pana likaongezeka usoni mwake, bado Richard alikuwa akishangaa, hakuwa akielewa ni kitu gani kilichokuwa kikiendelea moyoni mwa nesi yule.
“Kuna nini?” aliuliza Richard huku akionekana kuwa na maswali mengi yasiyo na majibu.
“Huyu ni nani?” aliuliza nesi yule, alikuwa akimuonyeshea picha yake.
“Mmmh! Ni mimi. Umeipata wapi picha yangu?” aliuliza Richard huku akionekana kushtuka.
“Ndugu zako wanakuja kukuona, ilikuwa imebandikwa sehemu zote hapa mjini” alisema nesi yule.
“Ndugu zangu! Ndugu gani? Sina ndugu hapa China, wazazi wangu walifariki,” alisema Ricard.
“Mmmh! Inawezekana vipi? Mbona wao wanakufahamu vilivyo. Bado unaonekana haujakaa sawa, tulia kwanza,” alisema nesi yule.
“Kweli nesi, sina ndugu.”
Nesi hakuonekana kushtuka, bado uso wake ulikuwa wenye furaha kubwa, kitu alichokuwa akitaka ni kuwaona ndugu wa Richard wakifika mahali hapo kwani kwa maelezo yaliyoendana na ile picha yalisema kwamba walikuwa wakimtafuta Richard aliyepotea baada ya tetemeko la ardhi kutokea na kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwake, angepewa dola elfu kumi.
“Nisubiri, nadhani watakuwa wamekwishafika,” alisema nesi yule na kuondoka mahali hapo kwa mwendo wa kasi.
Richard akabaki akijiuliza maswali mfululizo, hakuelewa kile kilichokuwa kinaendelea, kuambiwa kwamba ndugu zake walikuwa wakimtafuta tena kwa kubandika picha zake barabarani kilimshtua.
Hofu ikamshika moyoni mwake, akaanza kuhisi kwamba ndugu hao ambao walizisambaza picha zake, hawakuwa ndugu kama walivyojitambulisha bali walikuwa ni walewale vijana ambao mwezi uliopita walikuwa wamemkamata na kutaka kumuingiza ndani ya gari.
“Hapana, sina ndugu hapa China, wazazi wangu walikwishakufa kitambo,” alisema Richard huku akikisumbua kichwa chake juu ya kitu gani alitakiwa kukifanya mahali hapo kwani tayari aliona kwamba kama angesema akutane na hao watu waliojitambulisha kama ndugu zake, ni lazima angeuawa tu.
Mara mlango ukaanza kufunguliwa! Mapigo yake ya moyo yakawa juu.
****
Mwanasheria Pei Pei na familia yake wakawekwa sakafuni, japokuwa mke wake na watoto wake wawili walikuwa wakilia lakini watu wale hawakutaka kujali. Mikono yao ilikuwa imeshika bunduki, walionekana kuwa na roho mbaya kiasi kwamba wangeweza kuwaua muda huohuo endapo wasingepewa ushirikiano waliokuwa wakiutaka.
Pei Pei alijua kila kitu kilichokuwa kikitokea, alijua fika kwamba watu hao walikuwa wametumwa na wabaya kwa ajili ya zile fedha ambazo alikuwa amezitoa benki na kuzificha kwa ajili ya mtoto wa bilionea Walusanga.
“Tuambie kitu kimoja tu. Fedha zipo wapi?” alisema jamaa mmoja, kwa sauti aliyoitoa, hakuonekana kuwa na masihala hata kidogo.
“Fedha zipi?” aliuliza Pei Pei.
“Paaaaa…” kilisikika kibao kizto kutoka kwa jamaa mmoja, akaanguka chini.
“Tuambie fedha zipo wapi?”
“Fedha zipi?” aliuliza tena, jamaa akakoki bunduki yake.
“Una sekunde thelathini za kutuambia mahali fedha zilipo,” jamaa yule alisema huku akiikoki bunduki yake na kumnyooshea mtoto wake mmoja.
Huo ulikuwa mtihani mgumu kwa Pei Pei, hakujua ni kitu gani alichotakiwa kukifanya. Fedha ambazo alizitoa benki na mzee Walusanga alikuwa amezificha sehemu kwa kuwa katika kipindi ambacho mzee huyo alikuwa akitishiwa, alijua kwamba angeweza kuuawa na hivyo fedha zake kuchukuliwa.
Alikabidhiwa na kuambiwa kwamba ilikuwa ni lazima afanye juu chini kama Richard hatokufa, basi fedha hizo akabidhiwe yeye na kama ikitokea amekufa basi fedha hizo zipelekwe kwa watoto yatima na watu wenye matatizo mbalimbali barani Afrika hasa katika nchi ya Tanzania.
Kitendo cha kulazimishwa aseme mahali fedha zilipo lilikuwa suala gumu kwake lakini pia alipoona kwamba mtoto wake amenyooshewa bunduki tayari kwa kuuawa, huo ukawa mtihani mwingine mkubwa.
Kuna sauti mbili moyoni mwake zikaanza kushindana, kuna moja ilimwambia kwamba ni lazima aseme mahali fedha zilipokuwa ili kuiokoa familia yake lakini kuna sauti nyingine ilimwambia hakutakiwa kufanya hivyo kwani fedha zile hazikuwa za watu wale, fedha zilikuwa za Richard ambaye mpaka katika kipindi hicho hakujua yupo wapi.
“Sijajua mnazungumzia fedha zipi,” alisema Pei Pei huku akianza kulia.
“Paaaaa….” Mlio wa risasi ukasikika mahali hapo, mtoto wake mmoja akaanguka chini, damu zilikuwa zikimtoka kifuani na kuanza kuhangaika pale chini, mara akatulia tuli.
Yalikuwa ni zaidi ya maumivu moyoni mwake, machozi yaliyokuwa yakimbubujika yakaongezeka zaidi, mke wake, akaushika mwili wa mtoto wake na kuupakata huku akianza kulia kwa uchungu.
Ilikuwa ni moja ya picha yenye kuhuzunisha sana, damu zilizokuwa zimetapaa mahali hapo zilionyesha ni kwa jinsi gani watu wale walivyokuwa na roho mbaya. Hasira kali ikamkaba, akatamani kuwarukia vijana wale na kuanza kupambana nao kama mwanaume ila kila alipokuwa akiziangalia bunduki zile, akaamua kutulia.
“Mbona mnaniuliza familia yangu, naomba msifanye hivyo, nitawapa kiasi chochote cha fedha,” alisema Pei Pei huku akiomba kwa kuikutaniha mikono yake na huku akiwa amepiga magoti.
“Hatutaki fedha zako, tunataka fedha zile mlizozitoa benki,” alisema jamaa yule.
“Fedha zipi? Benki ipi? Sijui chochote kile,” alisema Pei Pei huku akilia kama mtoto, japokuwa alikuwa akidanganya, kama watu wale wangekuwa na huruma, wangeyaamini maneno yake.
“Una sekunde thelathini za kutuambia mahali fedha zilipo,” alisema jamaa yule huku akiikoki bunduki yake na kumnyooshea mtoto mmoja wa Pei Pei.
“Una sekunde kumi tu….una sekunde tisa…una sekunde nane…una sekunde saba….” alisema jamaa yule huku akiendelea kuzihesabu sekunde zilizobakia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mambo yameharibika! Tetemeko kubwa la ardhi linatokea nchini China katika Jimbo la Yunaan, watu wengi wanakufa na wengine kujeruhiwa. Miongoni mwa watu waliojeruhiwa viabaya, yupo mtoto wa bilionea mkubwa aliyeuawa na bilionea wa Kichina, Tai Peng.
Baada ya kuchukuliwa majeruhi, Richard anapelekwa hospitalini ambapo baada ya muda nesi anaingia na kumwambia kwamba kuna ndugu zake wamefika mahali hapo kuja kumuona. Anashtuka kwa kuona kwamba hana ndugu, je hao walikuwa wakina nani?
Upande wa pili, wakili Pei Pei ambaye alichukua fedha benki na bilionea, mzee Walusanga anachukuliwa yeye na familia yake na watu wasiojulikana na kupelekwa sebuleni, hapo, wanataka kujua kitu kimoja tu, mahali pesa hizo zilipokuwa.
Pei Pei hataki kusema kitu, yupo radhi kufa lakini si kuongea ukweli. Huku akiwa amegoma kabisa, mtoto wake wa kwanza anapigwa risasi, anaambiwa aseme fedha zilipo, anagoma, hivyo mtoto wake wa pili kuelekezewa bunduki. Ili kumuokoa mtoto wake, anatakiwa kusema ukweli mahali fedha zilipo.
SONGA NAYO…
Wakili Pei Pei alibaki akitetemeka, machozi yalikuwa yakimbubujika huku moyo wake ukidunda kupita kawaida. Wakati huo, watu hao walikuwa mahali hapo kwa kutaka kujua kitu kimoja tu, sehemu ambapo alikuwa amezihifadhi fedha alizozitoa benki na mzee Walusanga.
Sauti ya yule mtu ikiwa inahesabu ilisikika vilivyo masikioni mwake, tayari mtoto wake mmoja alikuwa amepigwa risasi na sasa hivi walitaka kumpiga risasi mtoto wake mwingine endao tu asingeweza kusema ukweli juu ya mahali fedha zilipokuwa.
Moyo wake haukutaka kabisa kuitaja sehemu hiyo, alibaki kimya huku akiendelea kutetemeka, moyoni alikuwa akimuomba Mungu amuepushie mbali tukio hilo la mauaji lakini kwa wakati huo, aliyasikia maombi yake yakigonga ukuta na kumrudia, hayakusikika kwa Mungu hata chembe.
“Paaaaa….” Ilisikika sauti ya risasi, akayainua macho yake na kumwangalia mtoto wake, alitaka kufahamu kama alipigwa risasi au la. Alichokiona hakuamini, mtoto wake wa pili naye alikuwa chini huku damu zikimtoka kifuani, alikuwa amepigwa risasi moja katika sehemu ambayo wala hakukuwa na nafasi ya kupona tena.
“Noooooo!!!!” alisema Pei Pei kwa hasira.
Alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa, kile alichokuwa amekiona kilikuwa ni kitu kilichomuuma mno. Alibaki akilia tu, ghafla akajikuta akisimama na kumvama yule mtu aliyekuwa na bunduki kwa lengo la kutaka kupambana naye.
Kwa wakati huo hakutaka kuogopa, hakujali kama watu wale walikuwa na bunduki au la, kitu pekee alichokuwa akitaka kukifanya ni kupambana na watu hao tu. Japokuwa alikuwa na nguvu za ajabu ambazo hakujua zilitoka wapi lakini alishindwa kupambana nao, akajikuta akipigwa na kitako cha bunduki na kudondoka chini.
“Tunahitaji kujua mahali fedha zilipo,”alisema jamaa yule huku akiikoki bunduki yake, kwa wakati huu, alitaka kumuua mke wake pia.
Huo ukawa mtihani mgumu kwa Pei Pei, hakujua ni kitu gani alitakiwa kukifanya. Tayari aliwapoteza watoto wake wawili ndani ya dakika tano tu, hiyo ikaonekana kutokutosha, pia watu hao walitaka kumuua na mke wake aliyekuwa akimpenda.
Ni kweli alijua mahali fedha zilipokuwa, alijua kila kitu lakini moyo wake haukuwa radhi kuzungumza kitu chochote kile. Yeye mwenyewe alijishangaa, moyo wake ulikuwa tayari kuipoteza familia yake lakini hakuwa radhi kusema mahali fedha zile zilipokuwa.
“Nisamehe mke wangu,” alisema Pei Pei huku akilia, alimwambia mkewe wa uchungu mkubwa moyoni mwake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jamaa yule hakunyamaza, aliendelea kuhesabu zaidi, alianzia kumi kushuka chini. Katika kila namba aliyokuwa akiitaja, Pei Pei hakusema kitu, alikuwa kimya huku akiendelea kulia kama mtoto. Ilipofika moja tu, mlio wa risasi ukasikika mahali pale na mke wake kudondoka chini na damu kuanza kumtoka.
Ilikuwa moja ya picha mbaya ambazo aliwahi kuziona katika maisha yake, hakuamini kwamba ndani ya kipindi kifupi angeweza kuipoteza familia yake kwa ajili ya kuzilinda fedha alizopewa ambazo hata hazikuwa zake, upendo wake mkubwa kwa usiku wa siku hiyo ukamponza na kujikuta katika maumivu makali.
Roho ya Pei Pei ilionekana kuwa ya kishujaa, watu wale hawakuamini kama mtu alikuwa tayari kuiona familia yake ikiuawa lakini si kusema mahali fedha zilipokuwa. Alichokifanya jamaa yule mara baada ya kuona Pei Pei hakusema kitu, akachukua bunduki yake, akaikoki na kumuelekezea Pei Pei.
“Zamu yako imefika. Tuambie mahali fedha zilipo,” alisema jamaa yule.
“Nipo tayari kuteswa, nipo tayari kuuawa kama ilivyouawa familia yangu, ila sitokuwa tayari kusema mahali fedha zilipo. Kama mnataka kuniua, sawa, niueni nikaungane na familia yangu huko ilipo,” alisema Pei Pei kijasiri mpaka kuwafanya watu wale kushangaa.
“Kumi…tisa…nane….saba….” alihesabu jamaa yule lakini bado Pei Pei hakutaka kuufungua mdomo wake kutaja mahali fedha zilipokuwa, alikuwa tayari kuuawa mahali hapo.
“Nyie niueni tu,” alisema Pei Pei.
Familia yake yote ilikuwa imeuawa, hakuona kama kulikuwa na sababu ya kuendelea kuishi tena, angeishi vipi na wakati familia yake nzima ilikuwa imepigwa risasi, kwake, hayo yalikuwa ni zaidi ya maumivu, hakukuwa na kitu kilichomuuma duniani kama kuona familia yake ikiuawa, tena mbele ya macho yake.
Jamaa yule alipomaliza kuhesabu, akabonyeza kitufe cha bunduki, bahati nzuri kwa Pei Pei na bahati mbaya kwa mpigaji yule wa risasi, haikutoka risasi yoyote ile, risasi zote zilikuwa zimekwisha.
“Nini tena? Muue tusepe zetu,” alisema jamaa mmoja.
“Hakuna kitu.”
“Unasemaje?”
“Risasi zimekwisha.”
“Hapana. Haiwezekani.”
Alichokifanya jamaa yule ni kuifungua risasi yake, hakukuwa na risasi yoyote ile, yaani pamoja na kujiandaa kuja ndani ya nyumba hiyo, hawakuwa wamebeba risasi nyingi kitu kilichoonekana kuwa kama uzembe mkubwa.
“Yaani ni lazima afe hata iweje,” alisema jamaa yule.
“Kwa hiyo tumuue vipi?”
“Tumechome moto ndani ya nyumba hii.”
“Mmmh!”
“Haina jinsi, tufanye hivyo,” alisema jamaa yule.
Huo ndiyo mpango waliokuwa wameafikia kwamba ilikuwa ni lazima Pei Pei achomwe moto ndani ya nyumba yake. Walichokifanya ni kumfunga kamba mikono yake na kisha kuelekea nje ambapo wakachukua dumu la mafuta ya petroli lililokuwa garini na kuanza kuimwagia nyumba ile kuanzia ndani mpaka nje.
“Piga kiberiti,” alisema jamaa mmoja na mwingine kukiwasha kiberiti, kilichofuata, ni mlipuko kubwa na nyumba ile kuanza kuteketezwa kwa moto.
****
Bado Richard alikuwa akitetemeka kitandani pale, nesi aliyeondoka ambaye alisema kwamba kulikuwa na ndugu zake waliokuja kumuona alimtisha, kijasho chembamba kiliendelea kumtoka, huku akiwa kwenye hali hiyo, mara mlango ukafunguliwa.
Mtu aliyeingia, alikuwa nesi mwingine, alipomuona tu akiwa amefumbua macho yake, tabasamu kubwa likautawala uso wake, akaanza kumsogelea na kuanza kuyapima mapigo yake ya moyo.
“Moyo wako unakwenda kasi sana, kuna nini?” aliuliza nesi yule.
“Nataka kuondoka kurudi nyumbani, tena sasa hivi,” alisema Richard huku akionekana kumaanisha kile alichokuwa akikiongea.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Uondoke kurudi nyumbani! Hapana, subiri kwanza bado haujawa sawa,” alisema nesi yule huku akiiweka mashine ile ya kusikilizia mapigo ya moyo shingoni mwake.
Richard hakutaka kuongea kitu chochote, ili asifikiriwe vibaya, akajifanya kuwa mpole. Nesi yule alipomaliza kazi zake ndani ya chumba hicho kikubwa, akaondoka zake.
Richard hakutaka kuendelea kubaki ndani ya chumba hicho, alichokifanya ni kuchomoa sindano zote za dripu alizokuwa amechomwa na kisha kutoka itandani pale. Kitu pekee kilichokuja kichwani mwake wakati huo ni kuondoka kuelekea mitaani na kwenda kumtafuta rafiki yake, Shu Yan.
Hatua zake kuufuata mlango wa nyuma zilikuwa ni za harakaharaka, hakutaka kutembea taratibu kwa kuhisi kwamba watu wale waliojitambulisha kama ndugu zao wangefika na kumchukua kitu ambacho hakutaka kitokee.
Huku akiwa ameukaribia ule mlango wa nyuma, mlango wa mbele ukafunguliwa, alipogeuka nyuma na kuangalia, nesi yule aliingia na wanaume watatu, kwa jinsi walivyoonekana, walionekana kuwa watu hatari.
“Yupo wapi?” aliuliza jamaa mmoja kwa sauti kubwa, hakujali kama sehemu waliyokuwepo ilikuwa ni hospitalini na wagonjwa walikuwa wengi.
“Alikuwa hapa,” alijibu nesi yule huku akikishika kitanda alichokuwa amelazwa Richard.
“Yupo wapi?” alirudia swali lile, wakati huu akaitoa bunduki yake, nesi akashtuka zaidi.
“Alikuwa hapa,” alijibu nesi yule huku akitetemeka.
Wakiwa bado wanaangalia huku na kule, kwa mbali wakamuona Richard, walimfahamu vilivyo, alikuwa kijana mwenye ngozi nyeusi, walipomuona tu, hapohapo wakaanza kumfuata, alichokifanya Richard ni kuufungua mlango ule wa nyuma na kisha kuanza kukimbia, watu wale wakaanza kumkimbiza, wagonjwa na nesi, wote wakapigwa na butwaa.
Tayari hatari ilikuwa mbele yake, alikuwa akikimbia kwa kasi huku akifungua mlango huu na kuufunga, aliufungua huu na kuufunga. Japokuwa alikuwa akijisikia uchovu mwilini mwake lakini hakutaka kujali, aliendelea kupiga hatua kwa kasi, alipofika nje, akaongeza mwendo na kukimbia zaidi.
“Simamaaaaaa,” ilisikika sauti ya mlinzi mmoja wa getini, alikuwa ameshika bunduki, alionekana kuwa na wasiwasi na Richard.
Wakati anasema hayo, walinzi wenzake wawili nao wakatokea, kama alivyokuwa amefanya mwenzao, nao wakachukua bunduki zao na kumnyooshea Richard ambaye alibaki akitetemeka.
“Wanakuja kuniua,” alisema Richard huku akitetemeka.
“Nani anakuja kukuua?” aliuliza mlinzi mmoja.
Hata kabla Richard hakujibu swali hilo, mlango ule ukafunguliwa na wanaume watatu waliokuwa na bunduki wakatokea. Kwanza kitedo cha kumuona Richard amesimama mbele yao kama hatua thelathini kiliwashangaza, kitu pekee kilichowashtua, kilikuwa ni uwepo wa walinzi waliokuwa wameshika bunduki na kumnyooshea Richard.
Ghafla, wakaona bunduki za walinzi wale zikianza kuwaelekezea wao, walichokifanya, ni kuanza kurushiana risasi mahali hapo. Ilikuwa ni lazima kufanya hivyo, kumpata Richard halikuwa jambo jepesi, walihitajika kumwaga damu kwanza.
“Paaaaa….paaaaa….paaaaa” milio ya risasi ikaanza kusikika mahali hapo. Eneo la hospitalini likaonekana kuwa uwanja wa vita, kwa jinsi hali ilivyoonekana, ilikuwa ni sawa na filamu za kina Anord na Rambo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment