Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

DARKNESS OF COMFORT (GIZA LENYE FARAJA) - 5

 





    Simulizi : Darkness Of Comfort (Giza Lenye Faraja)

    Sehemu Ya Tano (5)



    Nyumba ilikuwa ikiteketea, majirani waliokuwa wamelala ndani ya nyumba zao wakaamka na kuanza kutoka nje, kile alichokiona hawakuweza kuamini, nyumba kubwa na ya kifahari ilikuwa ikiteketezwa kwa moto.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kitu cha kwanza kilichokuja katika vichwa vyao ni kuhusu wakili Pei Pei na familia yake. Kadiri walivyokuwa wakijiuliza ni kitu gani walitakiwa kukifanya na ndivyo ambavyo moto ule uliendelea kuongezeka zaidi kitu kilichowapelekea kuwapigia simu kitengo cha zimamoto ambao walifika mahali hapo ndani ya dakika chache.

    “Mmmh! Kitu gani kilitokea?” aliuliza jamaa mmoja huku watu wa zimamoto wakiendelea kuuzima moto ule.

    “Hata mimi sifahamu. Nahisi kuna tatizo,” alisema jamaa mwingine.

    Hakukuwa na mtu aliyefahamu kilichokuwa kimetokea, walinzi wa mlangoni wa nyumba hiyo hawakuwa wakionekana, kila walipokuwa wakijaribu kuwatafuta, bado hawakuwapata.

    Mara baada ya moto kuzimika, hawakutaka kuingia ndani kwani bado kulikuwa na joto kali. Walisubiri kwa takribani dakika ishirini na ndipo baadhi ya polisi waliofika mahali hapo na watu wa zimamoto wakaingia.

    “Hii si shoti ya umeme kama nilivyofikiri, nadhani kuna mtu ameichoma moto nyumba hii,” alisema polisi mmoja.

    “Hata mimi nahisi hivyohivyo, harufu kali ya ptroli inaeleza kila kitu. Sasa ni nani amefanya hivi?” aliuliza polisi mmoja kwa sauti ya chini huku akiwa ameshika tochi iliyokuwa ikimulika huku na kule.

    “Sijajua. Hebu kwanza tuwatafute wahusika wa nyumba hii,” alisema polisi yule wa kwanza.

    Walichokifanya ni kuingia ndani ya kila chumba kwa ajili ya kuwatafuta wenyeji wa nyumba ile yaani wakili Pei Pei na familia yake. Hakukuwa na kitu kilichokuwa kimesalia, kila kitu kiliteketezwa na moto ule mkubwa.

    Walizunguka katika kila chumba, hawakufanikiwa kumuona mtu yeyote yule ila waliporudi sebuleni kwa mara ya pili, wakafanikiwa kuiona miili ya watu watatu ikiwa sakafuni, miwili ilikuwa ni ya watoto na mmoja ukiwa ni wa mtu mzima, tena alikuwa mwanamke.

    “Mungu wangu!” alisema polisi mmoja, kile alichokuwa akikiona mbele yake haikuweza kuaminika.

    Miili ilikuwa imeunguzwa vibaya na moto ule, halikuwa jambo jepesi kugundua watu wale walikuwa ni wakina nani kwa kuwaangalia mara moja tu. Bado ilikuwa ikitoa moshi huku ikiwa imekauka mno.

    Kilichofanyika ni kuitoa miili ile ndani ya nyumba ile kwa kutumia mifuko mikubwa ya nailoni na kuipeleka nje. Kila mtu aliyeiona, alishika kichwa chake kwa masikitiko makubwa, hawakuamini kile walichokuwa wakikiona.

    Wala haukuchukua muda mrefu, mkuu wa polisi wa Jimbo la Yunaan akafika mahali hapo, yeye mwenyewe alionekana kuchanganyikiwa mara baada ya kuiona nyumba ya wakili mkubwa nchini China ikiwa imeteketezwa kwa moto.

    Alichokifanya ni kuwafuata baadhi ya majirani waliokuwa pembeni, lengo lake kubwa lilikuwa ni kuwauliza maswali kadhaa.

    “Nini kilitokea?” aliuliza mkuu wa polisi, Li Yeng.

    “Nadhani kuna mtu amehusika katika mauaji haya,” alijibu jirani mmoja.

    “Kwa nini unahisi hivyo?”

    “Nilianza kusikia milio ya risasi, ilikuwa mitatu, nilishtuka lakini kabla sijafanya lolote ndani ya nyumba yangu, nikaiona nyumba hii ikiteketea kwa moto,” alisema jamaa huyo.

    “Una muda gani hujawahi kumuona Pei Pei?”

    “Kama wiki moja hivi.”

    “Unahisi yeye ndiye aliyeua?”

    “Sijui. Kwani yeye hajafa?” aliuliza jamaa yule.

    “Asante kwa ushirikiano wako.”

    Miili yote iliyokuwa imetolewa ndani ya nyumba hiyo, mwili wa wakili Pei Pei haukuwepo kitu kilichozua maswali mengi kwamba alikuwepo sehemu gani. Maelezo kutoka kwa baadhi ya majirani yakachukuliwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Yunaan.

    Kila mtu aliyeyasoma maelezo hayo aligundua kwamba kulikuwa na kitu ambacho kilitokea kabla ya nyumba hiyo kuchomwa moto, na mtu wa kwanza ambaye alishukiwa katika madai hayo alikuwa mmiliki wa nyumba hiyo, bwana Pei Pei.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama nyumba ilikuwa imepigwa shoti ya umeme, kwa nini kulikuwa na harufu ya mafuta ya petroli? Na kama nyumba ilikuwa imeteketea kwa bahati mbaya, kwa nini dakika chache kabla ya nyumba kuteketea kwa moto kulisikika milio ya risasi?

    Mbali na maswali hayo, kulikuwa na swali ambalo lilimtatiza kila mmoja. Kama wakili Pei Pei hakuwa akihusika na mauaji ya familia yake, mbona ndani ya nyumba hakuwepo na wakati gari lake lilikuwepo? Kila swali walilokuwa wakijiuliza, jibu lililokuja ni kwamba Pei Pei ndiye alikuwa muuaji wa familia hiyo.

    ****

    Kamba zilikuwa zimekaza mikono yake, kila alipokuwa akijaribu kujifungua, alishindwakabisa kuzifungua. Watu wale waliokuwa wameiteketeza familia yake wakatoka nje na kisha kuwasha moto nyumba ile.

    Wakili Pei Pei alijitahidi kujifungua kamba zile ili aweze kukimbia lakini alishindwa kufanya hivyo kwani zilikuwa zimefungwa vilivyo. Moto ukaingia ndani na kuanza kuteketezwa, ulipomkaribia, akawa hana jinsi, akatulia na kuanza kusali sala zake za mwisho tayari kabisa kwa kuteketezwa kwa moto huo.

    Mbele ya macho yake, akaiona miili ya watoto wake na mkewe ikianza kuteketezwa kwa moto ule. Moyo wake ulimuuma lakini hakuwa na jinsi, kila kitu kilichokuwa kikitokea alijiona kama yupo ndotoni ambapo baada ya muda mfupi angeshtuka kutoka usingizini na kujikuta akiwa kitandani.

    Hiyo haikuwa ndoto, kila kitu kilichokuwa kikitokea, kilikuwa ni maisha halisi, miili ya familia yake ikaendelea kuteketezwa na moto ule na kuhamia kwake, akaanza kuteketezwa na yeye pia.

    Alipiga kelele kwa maumivu makali huku akijaribu kuomba msaada lakini sauti yake haikuweza kutoka kabisa. Mwili wake ukaendelea kuunguzwa kwa moto ule.

    “Nisaidieniiiiiiii…..” alipiga kelele Pei Pei lakini bado moto ule uliendelea kumuunguza.

    Hakutaka tena kuendelea kuomba msaada tu, aliona kwamba kwa hatua aliyokuwa amefikia sasa alitakiwa kupambana kwa nguvu zake kuhakikisha kwamba anajiokoa kutoka katika moto ule na si kuendelea kuteketea.

    Kitu cha kwanza, huku akiendelea kuteketea, akazipeleka kamba zile katika moto mkali, kamba zikaanza kuteketea na mwisho wa siku kukatika. Asilimia sitini ya mwili wake ulikuwa umeteketezwa kwa moto, miguu yake, tumbo na sehemu za usoni zote hizo zilikuwa zimeunguzwa vibaya.

    Pei Pei hakutaka kukaa hapo, huku akiwa kwenye maumivu makali akaanza kukimbilia jikoni ambapo hakukuwa na moto kabisa na kisha kujimwagia maji kwa kuamini kwamba angeweza kuyapunguza maumivu makali ya moto ule, alipomalizia, akaufungua mlango na kutokomea zake.

    Kwa jinsi alivyokuwa ameunguzwa na moto ule, ilikuwa ni vigumu kugundua kwamba mtu huyo alikuwa wakili Pei Pei, nusu ya sura yake iliunguzwa vibaya huku miguu yake na tumbo lake vikiwa vimeteketezwa vibaya mno.

    ****

    Kwa sababu ilikuwa usiku sana, hakukuwa na mtu aliyeweza kumgundua, hakuwa na msaada mahali hapo, japokuwa alikuwa akitembea kwa maumivu makali lakini alijitahidi kupiga hatua na kuelekea barabarani.

    Alipoifikia, akaanza kutembea pembezoni mwa barabara huku akiwa kwenye aumivu makali. Ilikuwa ni usiku sana na alitamani gari lipite ili aombe lifti lakini kwa bahati mbaya kwa upande wake, hakukuwa na gari yoyote ile iliyopita.

    Safari yake hiyo ilichukua zaidi ya dakika arobaini na ndipo akafika katika nyumba moja kubwa na ya kifahari, hapo palikuwa ni nyumbani kwa rafiki wake wa siku nyingi, mzee Alexander, mwanaume Mzungu kutoka nchini Marekani, alikuwa wakili kama alivyokuwa.

    “Wewe nani?” aliuliza bwana Alexander, alishindwa kumtambua Pei Pei mara moja kwa kumwangalia.

    “Pei Pei.”

    “Hapana. Eeeeh! Nini kimetokea tena?” aliuliza Alexander huku akionekana kushangaa.

    “Nisaidie kwanza, nimepata tatizo,” alisema Pei Pei huku akiingia ndani.

    Kwa sababu ilikuwa ni usiku sana, akamuamsha mkewe, bi Amanda ambaye alifika hapo na kuanza kumwangalia Pei Pei. Kwa jinsi alivyoonekana, ilikuwa ngumu mno kumgundua, mwili wake ulikuwa umeungua kwa kiasi kikubwa sana, hatua ya kwanza kabisa kufanyika ilikuwa ni kumpatia huduma ya kwanza kwa kumpaka asali na dawa nyingine ambazo zilionekana kufaa kwa vidonda alivyokuwa navyo.

    Muda wote, Pei Pei alikuwa akilia kwa maumivu, kadiri alivyokuwa akipakwa asali na ndivyo ambavyo alilia kama mtoto mdogo. Ngozi yake ya nje ilikuwa imebanduka kwa kiasi kikubwa, aliposhikwa hapa, alilia, aliposhikwa pale, alilia, yaani kila aliposhikwa, alilia kwa maumivu makali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bado risasi ziliendelea kusikika katika eneo zima la hospitali, watu walikuwa wakikimbia huku na kule kuyaokoa maisha yao. Katika kipindi chote hicho, Richard alikuwa amelala chini kifudifudi huku mikono yake ikiwa kichwani.

    Wala hazikupita dakika nyingi polisi wakatokea mahali hapo na kuanza kushirikiana na walinzi wale kuwashambulia watekaji wale kutoka kwa bwana Tai Peng. Mapambano hayo ya kurushiana risasi yalidumu kwa zaidi ya dakika ishirini, vijana wale wakaonekana kuzidiwa hasa mara baada ya risasi walizokuwa nazo kuisha. Hiyo ikaonekana kuwa hatari kwao, kuisha kwa risasi zile kulimaanisha kwamba wangeweza kukamatwa na hivyo kufikishwa mbele ya sheria na kushtakiwa kwa kile kilichokuwa kimetokea hospitalini hapo.

    “Tujisalimishe,” alishauri kijana mmoja.

    “Hapana. Hapa ni kukimbia tu,” alisema mwingine.

    Hilo lilionekana kuwa wazo zuri, walichokifanya ni kuanza kukimbia. Japokuwa polisi wale waliendelea kuwarushia risasi lakini hakukuwa na mtu yeyote iliyompata.

    Richard hakutaka kubaki mahali hapo, bado maisha yake yalionekana kuwa kwenye hali ya hatari, alichokifanya, tena huku akiwa mwenye hofu nyingi ni kuinuka na kuanza kukimbia.

    Akaingia mtaani, hakutaka kusimama, bado aliendelea kukimbia kwa lengo la kuyaokoa maisha yake. Hakujua mahali alipokuwa akielekea, hakuwa na sehemu yoyote ile, kitu alichokuwa akikitaka ni kuondoka tu.

    Maisha yake yalikuwa na misukosuko mingi, hakujua ni nani alikuwa nyuma ya kila mpango wa kumuua. Hakujua sababu wala hakujua kama watu hao waliokuwa wakitaka kumuua ndiyo waliowaua wazazi wake.

    Alikimbia mpaka Gou Nux, hii ilikuwa sehemu pekee iliyokuwa ikitumiwa na vijana wengi Jijini Yunaan kwa kucheza michezo ya kamari. Alipofika hapo, hakutaka kuwafuata vijana waliokuwa wamejikusanya sehemu tofautitofauti kwa kutengeneza makundi, alisogea pembeni kabisa na kutulia juu ya mbao na kuanza kufikiria misukosuko kadhaa aliyokutana nayo.

    Aliiona dunia ikiwa imemuelemea, hakuwa na tumaini lolote lile mahali hapo, kila alipokuwa akikaa na kufukiria njia alizokuwa akizipitia, moyo ulimuuma na alibubujika machozi mashavuni mwake.

    “Mungu nisaidie, peke yangu sitoweza, na kama unaona ni jambo jema kuwafuata wazazi wangu, naomba ulifanikishe hilo haraka,” alisema Richard huku akionekana kukata tamaa kabisa.

    Hapo ndipo mawazo juu ya msichana aliyekuwa naye karibu ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa, Shu Yan yakamjia kichwani mwake, alijiona kupata nguvu mpya ya kutaka kuondoka na kwenda kumtafuta msichana huyo ambaye mpaka katika kipindi hicho hakujua kama alikuwa hai au naye alikufa katika jengo lile lililodondoka.

    Safari yake ikaanza, alikuwa akielekea kule kulipokuwa na jengo lile walilolitumia kwa ajili ya kusogezea siku zao, alijua kwamba lilikuwa limeanguka lakini lengo la kwenda huko, alitaka kuona kama angeweza kusikia kuhusu mwili wa msichana huyo.

    Alipofika, ni vifusi tu ndiyo vilikuwa vimekusanywa sehemu mbalimbali, alijaribu kuangalia huku na kule kwa kutegemea kwamba angeweza kumuona Shu Yan, hakuweza kufanikiwa.

    “Shu Yan upo wapi? Au na wewe ulikufa kama wengine?” alijiuliza Richard bila kupata jibu.

    Alichokifanya ni kuulizia kuhusu sehemu walipokuwa wamepelekwa majeruhi na miili ya watu waliokufa katika tetemeko hilo walipopelekwa, hilo wala halikuwa tatizo, akaambiwa mahali majeruhi na miili ilipopelekwa na kuanza kwenda huko.

    Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi, sala ya kimoyomoyo ilikuwa ikiendelea moyoni mwake, hakutaka kusikia kwamba Shu Yan alikufa katika jengo lile lililodondoka na hata kama ilitokea na yeye kujeruhiwa, alimuomba Mungu asiwe amepatwa na majeraha makubwa yatakayomfanya kushindwa kufanya chochote kile.

    “Nimekuja kumuona rafiki yangu,” alisema Richard mara baada ya kufika katika zahanati ndogo ya muda iliyojengwa kwa maturubai kwa ajili ya watu walioathirika na tetemeko hilo.

    “Anaitwa nani?”

    “Shu Yan.”

    “Ana miaka mingapi?”

    “Kumi na sita.”

    “Anaishi wapi?”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Alikuwa akiishi katika jengo la serikali.”

    “Sawa. Nisubiri hapahapa.”

    Nesi Yule akaondoka, Richard akabaki benchini na kumsubiria. Idadi ya watu bado ilikuwa kubwa mahali hapo, wapo watu waliokuwa wameumia vibaya mpaka bandeji walizokuwa wamefungwa kuwa na madoa ya damu. Kila alipokuwa akiwaangalia, alimshukuru Mungu kwa kumlinda.

    “Nimerudi,” alisema nesi baada ya kumrudia Richard.

    “Vipi?”

    “Sijamuona mtu huyo.”

    “Hapana. Umeangalia vizuri?”

    “Ndiyo. Una uhakika ni majeruhi?”

    “Hapana. Sina uhakika sana. Lakini nilihisi ameletwa mahali hapa,” alisema Richard.

    “Nenda kajaribu kuangalia katika hospitali ya jiji, inaelekea alifariki na mwili wake kupelekwa huko,” alisema nesi yule.

    Richard hakutaka kuendelea kukaa mahali hapo, alichokifanya ni kuondoka huku akionekana kuwa na mawazo lukuki. Wala hakuchukua muda mrefu, akafika katika hospitali hiyo ambapo aliulizia kwamba anamtafuta ndugu yake na kupelekwa katika chumba kilichokuwa na maiti za watu waliofariki katika tetemeko lile.

    Huku akiwa na hofu, akaanza kuangalia ndani ya chumba hicho kwa kutumia msaada wa mhusika wa chumba kile. Alifunguliwa droo moja baada ya nyingine lakini mpaka wanafika mwisho, hakuweza kuiona maiti ya Shu Yan, akachanganyikiwa zaidi.

    “Yupo wapi? Yaani kotekote hayupo, atakuwa wapi sasa?” alijiuliza Richard bila kupata jibu.

    ****

    Pei Pei hakutaka kutoka ndani ya nyumba ya wakili mwenzake wa Kizungu, Alexander, aliendelea kubaki ndani ya nyumba hiyo huku matibabu yakiendelea kila siku. Mwili wake uliharibiwa kwa kiasi kikubwa, madawa makali aliyokuwa akiyatumia ndiyo ambayo kwa kiasi kikubwa yakaanza kuleta nafuu mwilini mwake.

    Daktari ambaye alikuwa mtaalamu wa kutibu majeraha ya ngozi hasa inapokuwa imeunguzwa kwa moto, kila siku alikuwa akifika ndani ya nyumba hiyo na kumtibia Pei Pei ambaye kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele na ndivyo hali yake ilizidi kutengemaa.

    Bado mawazo yake juu ya familia yake hayakumuisha, kila siku moyo wake ulikuwa ukimuuma mno kila alipokumbuka familia yake ambayo iliuawa ndani ya nyumba yake tena mbele ya macho yake.

    Moyo wake ukajawa na maumivu makali, akajiahidi kisasi kwa kila mtu ambaye alihusika katika uteketezaji wa familia yake aliyokuwa akiipenda kwa moyo wa dhati. Kila alipokuwa akikaa, hakusita kuyazungumzia maumivu makubwa aliyoyapata mara baada ya kuiona familia hiyo ikiuawa.

    “Ninataka kuondoka, bado kuna kazi ya kufanya,” alisema Pei Pei.

    “Hapana. Subiri kwanza, bado haujawa vizuri,” alisema Alexander.

    “Najua, lakini kuna mtu nahitaji kumuona kabla hawajamuua.”

    “Mtu gani?”

    “Mtoto wa mteja wangu, anaitwa Richard.”

    “Yupo wapi?”

    “Sijajua. Kama nilivyotaka kuuawa mimi na hata huyo pia anatakiwa auawe. Ninahofia kwamba wanaweza kumpata na kumuua. Naomba niondoke niingie mitaani kumtafuta,” alisema Pei Pei.

    “Haiwezekani. Bado haujapona.”

    “Alex, ninashukuru kwa kila kitu, naomba uniruhusu niondoke. Bado nina safari ndefu mno, naomba uniruhusu tu, bila kufanya hivi atauawa kabla sijampa kile ambacho baba yake ametaka nimpe,” alisema Pei Pei, wakati mwingine alikuwa akiugulia maumivu, bado mwili wake ulikuwa na maumivu na majeraha kadhaa ya kuunguzwa kwa moto.

    “Hilo ni jambo lisilowezekana, hata kama umeomba lakini hapana, hauwezi kutoka humu mpaka upone kabisa,” alisema Alexander.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huo ndiyo uamuzi uliokuwa umefikiwa, lilikuwa jambo gumu kwa Alexander kumruhusu Pei Pei kwenda mitaani kumtafuta mtu aliyekuwa akitaka kumtafuta na wakati hali yake kiafya haikuwa nzuri.

    Alijitahidi kumlinda na kumjali kwa kumletea dokta ndani ya nyumba hiyo. Alipewa dawa nyingi ambazo zilimfanya kutengemaa na kuanza kurudi katika hali yake ya kawaida.

    Mwezi mmoja ulipotimia huku akiendelea kuwa ndani ya nyumba hiyo, Pei Pei hakutaka kukubali, kila alipokuwa akilala, aliona maono kwamba Richard alikuwa akitafutwa na watu kwa ajili ya kuuawa, kwake, alijiona kuwa mkombozi pekee wa motto huyo.

    “Ni lazima nitoroke, siwezi kukaa ndani ya nyumba hii, ni lazima nimtafute Richard nimpe fedha zake,” alisema Pei Pei, siku hiyo alidhamiria kutoroka ndani ya nyumba hiyo.



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog