Simulizi : Julieth
Sehemu Ya Pili (2)
Kuna wakati akili yake ilimwambia amfutilie mbali binti yule ambaye hakuwa saizi yeka na badala yake, endeleze mahusiano yake na Salma binti mwenye muenekano wa kawaida asiye na mvuto wa kushtua, Ila mwenye tabia na maadili mema na penzi la kweli kwake. Ni nadra sana kumkuta binti aliyekulia uswahilini katika jiji la Dar akiwa na umri wa miaka kumi na tisa, ama Ishilini akiwa bikra.! Lakini ni Chacha aliye ipasua bikra ile kwa binti yule mkazi wa Kitunda..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliyafikilia hayo pia, lakini moyo wake ulikataa kabisa, msukumo mkubwa wa moyo uliishinda akili yake, moyo ulimwambia, ni budi apambane kumpata Jullieth binti ambaye hutochoka kuyatizama macho yake, mwanamke ambaye hutochoka kitizama shepu yake, msichana ambae ungehitaji kuipapasa ngozi laini isiyo tokana cosmetics cream, kama wasemavyo kwa kimombo, kuliko kuhangaika na mwana mke ambaye kamwe huwezi kupata furaha ya maisha ya kimahusano asilani, kwa kuishi na mtu ambaye moyo hauja mlidhia.
Saa sita usiku ndipo usingizi ulipo mpitia bwana Chacha, moyoni akiwa na nadhiri ya kupambana kwa gharama yoyote ilimuladi Jullieth awe wake maishani.
Siku ya pili, alidamka asubuhi na mapema, kuliko kawaida, alijitayarisha na kuelekea stendi ambako alipanda basi hadi chuo.
Hadi saa mbili kamili muda rasmi wa vipindi kuanza, Julliet hakuwa ametokea, katika darasa.
jamaa alikuwa roho juu, mawazo yake hayakuwa katika masomo tena, macho yake muda wote yalikuwa katika mlango wa darasa akitegemea kuona kiwiliwili cha mrembo yule kikijichoma ndani muda wowote, lakini wapi. Muda ulizidi kuyoyoma bila Jullieth kutokea…
kwa mtu aliye kuwa anamjua Chacha vema ni wazi angeweza kuona mabadiliko makubwa kwa kijana huyu siku hii.
Macho yalimwiva pumzi zikawa zinamtoka taratibu huku donge kubwa likuwa limemkaba kooni.
“Vipi mrembo yule hadi wasaa ule hajatokea,. Kakumbwa na kitu gani tena.. hajui kama nimekwisha zama katika bahari yenye kina kirefu,” alijiuliza. nguvu ya pendo ilikuwa inanguvu kuliko akili yake..
Sasa pumziko iliingia ambapo wanachuo wengi walitoka katika madarasa na kwenda katika migahawa kupata stafutahi, bado Jullieth hakuwa ametokea.
Ilikuwa ni siku mbaya kwa chacha pengine kuliko siku yoyote. Aliishia kuegemeza kichwa chake katika meza ndogo huku nafsi yake ikikumbwa na simanzi kubwa, na hata ingetokea ukamuuliza vipi awe na hali ya hasira kutokana na hali ile, bado asingekuwa na jibu lenye mantiki juu ya hasira yake, kinywa chake kikiwa kikavu macho yamemwiva, hakupata hata hamu ya kula,.
“Juliieth kwanini unanitesa kiasi hiki wewe mwanamke kwanini aagh” alisema kwa sauti ndogo akiwa ameinamia katika meza.
“Chacha vipi mkuu, una nini leo wewe” Masawe aliyekuwa hatua chache alihoji baada ya kusikia akiongea peke yake huku akiwa kajinamia.
“Ooh!. naumwa mkuu” alijibu huku ajibaraguza kushika kichwa na kukunja uso wake kwa maumivu.
“Pole sana, ni vema ukaenda kucheki dawa duka la madawa hapo nje kaka”
“Ooh yeah! Ni kweli” alijibu na kunyanyua mizigo yake na kuondoka katika darasa. Chacha hakuona uzuri wa siku hii kabisa, asingeweza kukaa chuoni pale muda ule ilihali akiwa katika hali ile.
Alizipiga hatua kukiacha chuo na kuelekea stend ya mabasi.
Hapakuwa mbali kutokea pale hadi katika mabasi ya gongo la mboto, alijichoma katika UDA lililokuwa halina abiria wengi na kuketi siti ya mbele kabisa karibu na dereva.
Akiwa katika gari nafsi yake ilikuwa ikimsuta kwa kujingiza katika penzi la mwanamke wa mjini aliyekutana nae siku moja pasina kumwelewe kiundani na kumpenda, ambapo mwisho wake akiishia kupata maumivu makali ya moyo..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Gari liliondoka na kushika njia ya buguruni ambayo ilikuwa na msururu mlefu wa magari foleni kubwa iliyo anzia katika mataa ya Tazara barabara ya nyerere, ilifanya lile UDA ligande sehemu moja kwa muda mrefu
Gari liliondoka katika mwendo wa kunyata kiasi cha saa nzima gari lilikuwa ndio kwanza linawasiri katika makutano ya mataa ya Tazara ambako bahati nzuri askari aliye kuwa akiongoza magari aliruhusu magari ya usawa wao yapite na sasa wakawa wanavuka mataa ya Tazara na kushika njia ya Nyerere tayari kwa mwendo kuelekea gongo la mboto.
Jamaa alikuwa amelowea katika usingizi, moyo wake akiwa ameweka nadhiri ya kumtoa kabisa Jullieth katika fikra zake.
Kwani katika kipindi kifupi,.alijkuta anapatwa na maradhi mabaya mno madhila ya kumpenda mtu asiye eleweka.
Alistushwa na konda aliyekuwa akidai nauli., na hapo aliona alikuwa amefika uwanja wa mwalimu Nyerere, kutokea pale pia kulikuwa na foleni na magari yalisimama huku magari ya viongozi wa nchi hii, yaliyokuwa uwanja wa ndege yakiruhusiwa kwanza kuingia barabarani kabla ya magari mengine kuruhusiwa.
Chacha aliingiza mkono mfukoni na Alitoa noti moja na kuumpa konda. Wakati tendo hilo linafanyika, wakati huo huo simu yake iliiita kwa vurugu, alitoa mfukoni na kutizama mpigaji wa simu ile.
Ghafla mwili wake uliingia ubaridi, moyo ukimlipuka. Na kujikuta akipata nguvu za ghafla.
Alikuwa ni Jullieth.
Upesi alipokea simu ile Na kuweka sikioni.
“Heloow”
Mambo Chacha sauti nyororo ya kike ilitokea katika spika za simu yake, alikuwa ni Jullieth.
“Poa Jullieth uko wapi?” aliuliza Chacha moyo wake ukimwenda mbio.
“Jamani Chacha I’m sorry nilipata dharula kidogo” Alisema Jullieth pumzi nyepesi zikitoka puani mwake zilizo penye moja kwa moja katika masikio ya Chacha.
Jamaa alivuta pumzi nyingi na kuzishushua kwa mkupuo, kifua chake kiakapanda juu na kushuka chini pindi alipo vuta pumzi na kuzishusha chini.
Moyo wake ukiingiwa na ubaridi wa ghafla, donge na huzuni alivyo kuwa navyo vikayeyeuka ghafla, ikawa ni kama mtu aliye katika milima ya theluji ya baridi kali, alibaki ameduwaa hata asitie neno midomo yake ikijenga tabasamu murua, ukimya wa nukta kadhaa ukampitia hadi alipostuliwa na sauti nyororo ya Jullieth kwa mara nyingine.
“Mbona kimya Chacha”
“Tuko pamoja Jullieth, uko wapi sasa?”
“Niko airport Chacha”
Airport!!. Aliuliza kwa mshangao.
“Ndio nipo airport,jana nilipiga sana simu yako lakini hakukuwa na majibu,.lakini leo pia, nimekupigia simu, pengine simu hii ni yamwisho kwako” alisema Jullieth kwa kituo, na kunyamaza kidogo ili maneno yale yamwingie vema yule mtu.
Na kweli upande wa pili Chacha alikunja uso aliposikia maneno yale malaini kutoka katika kinywa cha mrembo aliyetokea kumuhusudu vibaya mno. Mistari katika paji lake la uso ilijichora na kuwa mithili ya mkeka wa kizaramo.
“What are you talking Jullieth?” nimekufamu jana tu chacha, lakini sikjui ni kitu gani kina zungumza ndani ya moyo wangu,lakini kwa sasa acha niseme hivi, kuna mahala katika dunia naenda, ambako naamnini nitaishi huko maisha yangu yote,”
Sauti ya huzuni ya mwanamke wa urembo ilisema, na kuingia kabisa na kugonga ngoma za masikio ya Chacha. Mwili wake ukagubikwa na misisimko ya ajabu kutokana na sentesi za yule malkia wa urembo.
“Wewe..weee..unaongea nini wee..mbona sikuelewi mwanamke..wewe” Chacha alilalama haraka haraka, akikosa utulivu.
“Upo chuo Chacha?” badala ya kujibu Jullieth alimtupia swali katika hali ya utulivu mkubwa.
“Yes..oooh no.. nipo.. katika UDA.. sasa sikiliza jullieth siko mbali na uwanja wa ndege nashuka sasa hivi nakuja kukuona.”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alisema Chacha akikosa utulivu mkubwa, na wakati huo huo magari ya upande wao yakaruhusiwa kwa kuondoka, “kondaaa kondaaa shusha hapa hapa nishusheni” alilapiga kelele ndani ya gari kama mtu aliyepatwa na wazimu, simu yake ikiwa bado ipo sikioni macho yake yakiwa upande ule wa kushoto wa uwanja wa ndege.
“Wewe hapa hakuna kituo unataka tupate matatizo kwa matrafiki sasa hivi.” Konda alimjibu huku dereva na yeye akiliondoa gari kwa kasi zaidi.
“Ooh shiiit blood fool nini hii jamani” Chacha alilalalama kwa mahamaniko.
“Sio sisi ni sheria mjomba”. Konda alimjibu.
Wakati huo huo sauti ya Jullieth ilisikika tena katika simu.
“Chacha usihangaike ndugu, labda siku moja tutaonana japo ni ngumu sana,.ona Chacha, ni dakika kumi na mbili tu zimesalia kabla ya ndege kuondoka,. Huwezi kuniwahi,,.” Alisema Kwa upole, na hata alifika hapo alisita, akahema kidogo kisha akendelea kusema kwa sauti ile ile ya utulivu na upole,. “ naenda Spain madridi.. ni kwamume wangu,.lakini hata hivyo…iko hivi…ilove you Chacha and…” kabla ya kumalizia simu ilikatika, jamaa alibaki ameganda kama mtu aliye pigwa na shoti ya umeme wa voti mia saba,.maneno ya Julieth yalijurudia rudia akilini mwake,.ghafla alistuka na kuona alikuwa ameganda huku gari likizidi kujisukuma kwa kasi na kuwa mbali na uwanja wa ndege alipagawa, alitizama katika simu yake na kuona ilikuwa imezima, na hapo akakumbuka simu yake ilikuwa imekwisha chaji.
“AAAAAGHAA NISHUSHEE” alipiga makelele katika gari kama mtu aliye pandwa na majini. Abilia na hata dereva na konda wake walistuka mno, hali iliyo lazimu dereva kusogeza gari ukingoni mwa barabara na kumshusha.
“Shuka bhana maana hayo maruhani yako yasije kutujeruhi humu katika gari,.” Alisema konda.
Jamaaa alitoka mbio kurudi nyuma katika uwanja wa ndege, dakika zilizo kuwa zimebakia ni dakika tano tu toka zile kumi na mbili alizo kuwa ameambiwa na mrembo yule.
Alipitia katika kibanda cha simu na kununua betri la simu lililokuwa na angalau chaji kidogo kisha akampigia Jullieth.
Simu iliita kidogo tu, na ikapokelewa upesi, “mbona ulikata simu Chacha?”
No ..sikukata simu ilizima chaji.. sasa mimi niko njiani nakuja sasa hivi anagalau nikuone Jullieth nakupenda pia,.tena mimi zaidi yako jullieth wangu” alisema Chacha huku akihema, na hata hapo alikuwa akikimbia kwa kasi kama yupo katika mbio kali za malathoni.
Jullieth hakujibu alikuwa kimya akimsikiliza mwanaume yule aliyepatwa na wazimu wa pendo.
“Its four minuts only remain Chacha.. please mie naingia sasa katika chumba cha wasafiri tayari kwa kuondoka its too late” alisema Jullieth tena kwa unyonge, Na hapo chacha aliongeza kasi ya kukimbia mno.
Upande wa pili wa barabara aliona kuna stendi ya bodaboda, aliona kuchukua usafiri huo ndio njia pekee ya kumuwahisha ndani ya uwanja wa mwalimu Nyerere akiwa ni mwenye wahka bila kutizama kulia wala kushoto alingia katikati ya barabara, bila kuwa makini na magari yaliyokuwa yakienda kasi,
Lilikuwa ni kosa kubwa.
Gari dogo la Toyota landcrueser lililo kuwa kasi, lilishindwa kabisa kuzuia breki zake hata taili za gari hilo zisipande juu ya kiuno cha Chacha.
Paaaaa.,kishindo kikubwa kilisikika. Hakuna kilicho salia.*****
Ukavu wa koo ulikuwa ulimfanya kinywa chake kiwe kikavu na kufanya apatwe na kiu cha maji, taratibu kope za macho ya Chacha zilifunguka macho yake hayakuwa na nguvu yaliona ukungu, huku sura ya mwanadada mrembo ikiwa mbele yake., masikio yake yalisikia sauti za ndege wakiimba kwa mfumo mzuri wenye kupendeza.
Alimtizama yule mwanamke mrembo, tabasamu hafifu likamtoka, kwa sauti isiyo na nguvu akaita “Ju..lli…eth”. akajaribu kunyanyua mkono kumshika Jullieth lakini mkono wake ulikuwa mzito ajabu.
Jullieth alimsogelea na kumwinua kidogo pasina kusema neno kisha akalaza kichwa cha Chacha juu ya kifua chake kidogo kilicho beba matiti yaliyosimama wima.
Machozi yakamtoka Jullieth..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nisamehe Chacha..haikuwa dhamira yangu kukuumiza. Nilitaka tu kujua kiwango cha hisia zako kwangu niwie radhi,” alisema Jullieth kwa sauti ya kilio huku akiwa amemkumbatia kwa nguvu.
“Kivipi Jullieth kwani nimepatwa na nni?” aliuliza Chacha huku akijisukuma kando kidogo ya Jullieth na kutizamana macho kwa macho.
“Nimekusababishia matatizo”
“Bado sijakuelewa Jullieth?”
“Nilitaka kujua kwa kiwango gani unanipenda hata nikakuongopea kuwa nasafiri, hilo likapelekea wewe kupata ajali mbaya ya gari baada ya kujaribu kuja kuniaga uwanja wa ndege”
“Uwiii Mungu wangu weee..! kumbe Jullieth ulikuwa unanifanyia masikhara!! Khaa!.” alisema Chacha kwa mahamaniko makubwa.
“Samahani Chacha.. sikuwa na dhamira ya wewe upate ajali,.ule ulikuwa ni utani tu mpenzi ambao mwisho umeleta madhara haya”
Alisema Jullieth kwa mahamaniko..Chacha alilia kwa fadhaa kuliko kawaida mguu wake wa kulia ulikuwa umevunjika kabisa na kukatwa huku kiuno cheke kikipata madhara makubwa mno yaliyo mfanya aishii kwa kukaaa katika baiskeli ya magurudumu matatu kwa miaka mingi mno.*****
Kila kitu katika maisha ya Chacha kilibadilika kama masikhara, ile ndoto yake ya kuwa miongoni mwa vijana wachache wasomi kutoka katika kijiji chao ilibaki kuwa historia ambayo haikutimia tena.
Alikuwa akiishi yeye na Jullieth huko kitunda katika nyumba aliyokuwa amepanga kwa kipindi kirefu tangu akiwa angalia anasoma katika chuo cha DSJ.
Mahusiano yake na Jullieth yalikuwa kwa kasi mno.
Kitendo cha Chacha kupata ulemavu wa maisha kutokana na utani wa kimapenzi kutoka kwa Jullieth ilifanya mwanamke huyo moyo wake kuzimika kabisa kwa Chacha.
Jullieth ndiye alikuwa nguzo muhimu kwenye maisha ya Chacha, ni Jullieth ndiye aliyejua chakula kinapatikana vipi, pia ni Jullieth aliyejua kodi ya chumba inalipwa vipi, lakini pia ni Jullieth aliyejua hata Mavazi ya Chacha yanatoka wapi.
Chacha alikuwa mtu wa kwenye baiskeli la magaurudumu ya mataili matatu kutwa kucha isipokuwa wakati wa kulala tu.
Nguvu ya moyo ulio penda ulimfanya Jullieth kutoona adha yoyote juu ya matunzo kwa mpenzi wake.
Maisha yao yalitawaliwa na tabasamu na vicheko siku zote.
Kiasi cha mika mitatu kupita hatimae Jullieth alimaliza shahada ya uandishi wa habari,.kisha akaajiliwa katika kituo maarufu cha Tv hapa nchini kama mwandishi mtangazaji wa vipindi vya burudani.
Uwezo, kipaji na sura nzuri ya mvuto aliyokuwa nayo Jullieth ilimfanya kuwa maarufu taratibu,.kadri siku zilivyo zidi kwenda mbele ndivyo jina lake lilivyo zidi kukua,.
Kila mtu alipenda kumtizama Jullieth, kila mtu alipenda kumsikiliza, umaarufu wake ukaongezeka zaidi na kujikuta kila anako pita watu walimnyooshea vidole..
Pamoja na umaarufu wake kuwa mkubwa lakini jina lake halikuendana na maisha yake. Alilipwa pesa kiduchu katika kampuni ile ya matangazo.
Pesa ambayo hakumwezesha kabisa kuishi katika namna ya hadhi ya jina lake..
Siku zote alienda kazini kwa daradara zile za gongo la mboto hadi makumbusho ambako ilimlazimu kupanda daradara jingine lililompeleka Kawe mahala ambapo ndipo kazini kwake..
Changamoto zilikuwa nyingi mno kwake.. vijembe vya makonda na hata abiria juu ya mtu maarufu kama yeye kugombania usafiri ule ilikuwa ni fedheha kubwa mno kwake..
Kuna wakati aliona umaarufu ni mzigo mkubwa mno ambao alishindwa kwa nmna gani autuwe.. umaarufu ulimnyima uhuru kabisa wa kuishi maisha yake ya kawaida kama binadamu wengine...umaarufu ulimfanya awe mnyonge mno...CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hii baada ya kuteremka katika kituo cha CCM Kawe, alitembea taratibu hadi ofisini. Baada ya kusaini kwenye daftari la wafanya kazi alijichoma katika ofisi yake, aliketi akiwa mnyonge kabisa.
Ikiwa ni siku mpya kabisa ya juma tatu bado hakuona raha ya kufanya kazi siku hii,.kichwa chake kiligubikwa na taswira ya matukio lukuki yaliyo kuwa yakimtokea huko barabarani alipokuwa akigombania mabasi asubuhi ajapo kazini na kuondoka.
Ni matukio mengi aliyapita, lakini alionekana dhahili hili la leo liligusa sehemu mbaya kabisa kwenye akili yake.
Alikusanya mikono pamoja na kuikunja kifuani kwake na kulaza kichwa chake juu ya meza ndogo iliyobeba computure na makablasha mengine lukuki.
Fikra zake zikarudi ndani ya basi la UDA.
Alimkumbuka konda wa basi lile alivyo mjia na kumtaka alipe nauli…alifungua mkoba wake uliokuwa ameukumbatia katika kwapa lake ili atoe pochi iliyokuwa na pesa..lakini alistuka baada ya kukuta pochi halimo na akakumbuka mara moja kuwa alikuwa amesahau ndani..
“Samahani konda nimeshau pochi ya pesa nyumbani kwangu” alimwambia kwa sauti ya chini yenye mahaniko makubwa.
“Niniiii?..wewe anti usilete shobo zako za kisister duu.. sisi hapa hatuuzi sura..tumetumwa pesa na siyo vinginevyo haya lipa changu upesi” konda alipayuka kwa ukali macho kayatoa kama kinyonga.
“Jamani kaka yangu, niwie radhi kweli nimeshau pesa nyumbani tafadhali ndugu…”
“Acha zako wewe,. Usilete urembo wa kwenye video hapa ukafikili kuna mtu atakae kubabaikia hata usilipe nauli mshamba wewe..”
“Please brother..”
Hakuna cha please hapa.. wee demu vipi wewe..hicho kingereza chako cha please..please sijui nini vile.. peleka huko kwenye videoni kwenu..sio kwenye hili basi.eti supar star..supar star bongo!!. Leta pesa hapa.
Konda alizidi kukoroma kwa hasira abiria wote walikuwa zwii’ kimyaa wakisikiliza na kutizama kisanga kile cha aina yake..bahati nzuri jamaa aliye kuwa ameketi kiti kimoja na Jullieth alitoa noti ya elfu tano na kumpa konda kisha akamtaka akate nauli ya watu wawali yanii yeye na Jullieth.
Hiyo ndiyo ikawa pona pona ya tatizo lile la yeye na konda.
Yote hayo yalipita kwenye kichwa chake akiwa ameinama chini mule ofisini mwake.. alimua meno kwa hasira na kupiga ngumi ndogo katika meza huku akiachia msonyo mkali.
“Vipi wee supar star una nini leo?” Haji mfanya kazi mwenzie aliyekuwa akihusika na mambo ya video production alihoji kwa utani akiwa mbele yake.
“Aagh vipi Haji umefika saa ngapi hapa?”
Dakika nyingi tu niko mbele yako nakushangaa ulivyo zama kwenye bahari ya mawazo, kuna nini tena”
“Hamna kitu Haji matatizo tu ya dunia”
“Au shemeji kisha kuvuruga huko nyumbani?” alisema Haji kwa dhihaka akiachia cheko dogo.
“Sema haji unashida gani asubuhi hii leo?”
Aisee, program manager anakuita kidogo ofisini kwake.” Alisema Haji akiwa siliasi kidogo.
Julliet alitafakari kwa nukta kadhaa wito ule, akijaribu kubashiri sababu ya kuitwa na maneja asubuhi ile kisha akasimama upesi na kuongoza ofisini kwa meneja.
Kijana maji ya kunde, mrefu wastani mwenye sura ya duara iliyosadifiwa na pua iliyochongoka kama mtusi, alikuwa ameketi mbele ya meza ndogo iliyobeba kumputure kubwa aina ya mark na mafaili kadhaa pale mezani.
Jullieth aliketi mbele ya kiti cha wageni kisha akatega sikio kumsikiliza yule bosi wake, wakati huo akiwa amejikita katika kubofya bofya keybord ya komputure ile kubwa.
Sekunde kumi na tano badae alimgeukia Jullieth paji lake la uso likiwa limetengeneza mikunjo kiasi na macho kayatumbua..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kuna mabadiliko kidogo ya kiofisi Jullieth.” Alisema yule meneja akiwa bado anamtizama usoni kwa macho yake makaubwa na makali.
“Kitengo chako cha kazi kinafanyiwa mabadiliko kidogo, wewe utaondolewa pale na kuwekwa mtu mwingine.” Alisema tena na kukohoa kidogo huku sekunde kadhaa zikipita kimya ili yale maneno yamwingie vizuri Jullieth.
“Na sasa hauto onekana tena hewani badala yake utakuwa upande wa…” alikohoa huku akiziba mdomo kwa viganja vyake. Akameza funda la mate kisha akendelea.
“Utakuwa upande wa news analysis haya ni maamuzi ya ofisi, kwa hiyo jiandae kwa ajili ya hilo, kesho asubuhi unatakiwa uhamie kitengo hicho.
Alisema yule meneja sasa akiegemea kiti chake cha kuzunguka kwa madaha akijitikisa tikisa pale kitini.
“Kwanini imekuwa hivyo lakini mkuu?”
“Aah ukiniuliza swali hilo nitapata wakati mgumu kukujibu kwakuwa majibu yake hata mie sina”.
Alisema tena meneja aliyefahamika kama Robert.
Jullieth alishusha pumzi ndefu, moyo ukatanda huzuni kidogo akabaki akitizama kushoto mwa ofisi ile ambapo kulikuwa na picha kubwa ya kiongozi mkuu wan nchi.. siyo kwamba mawazo yake yalikuwa katika ile picha ya mkuu wa nchi..lahasha, moyo wake ulizongwa na mfadhaiko mkubwa wa kutothaminika kabisa katika kampuni ile..
Ni kweli kampuni ilikuwa ikimlipa mshahara kiduchu.. lakini umaarufu aliokuwa nao kutokana na kuonekana katika kipindi maarufu cha tv, kwa upande wa pili ulikuwa na faida nyingi kwake..kwanza aliweza kupata upendeleo mwingi katika sehemu mbalimbali kutokana na kujulikana kwake, pili aliweza kuaminika popote pale ilipo tokea ikawa na tatizo na kutokana na maisha yake ya kijungu jiko aliweza kupata msaaada kwa wepesi.. mfano mzuri ni sekeseke la asabuhi kati yake na konda wa basi.
Alipo fikilia yote haya aliona sasa kila kitu kinaenda kuyeyuka kama mshumaa hofu, huzuni, na donge zito moyoni ilimwenea. Alijinyanyua taratibu katika kiti mule ofisini na kuanza kuondoka taratibu,. Robert aliendelea kubofya koputer yake pasina kumjali kabisa mwanamke yule.
Alishika kitasa cha mlango na kuvuta..
“Julliet” Robert aliita mara baada ya kugusa kitasa cha mlango.
“Abeee”
“Dakika mbili tafadhali”
Alirejea kinyonge na kuketi tena katika kiti..Robert aliendelea kubofya bofya pasina kumtizama usoni akasema. “mbona unaonekana mnyonge sana mrembo?”
Aliuliza, tabasamu jepesi likiwa kinywani mwake macho yake yakiendelea kuangalia kazi zake alizokuwa akizichapa katika computer.
“Ulidhani nitafurahia habari hizi Bosi?” alijibu.
“Kwa kiasi gani umefadhaika?” Robert aliendelea kumtupia maswali ya dhihaka.
“Kwakweli nashindwa..sijui nisemeje”
“Pole sana mrembo lakini una nafasi ya pili ya kubadili hali hiyo.. pengine utarejeshwa katika kitengo na labda hata saraly lako litapanda kidogo.. unaonaje hilo kisura?”
“Itakuwa sherehe kubwa kwangu”
“Very Nice.. kwahiyo uko tayari niset mambo na kila kitu kiende kama nilivyo ongea?”
“Unafikili nina sababu ya kukataa juu ya hilo bosi?..utakuwa ni malaika wa ukombozi kwenye maisha yangu fanya hivyo”
“Kweli Jullieth?”
“Bosi unaniuliza nini aagh!!.. mie naona unakawia nisaide kwa hilo tafadhali bosi”
wangu”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijibu Juliieth kwa wahaka mkubwa macho yake yakionesha uhitaji dhahili wa swala hilo
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment