Simulizi : Julieth
Sehemu Ya Tatu (3)
“Ulikuwa unalipwa bei gani jullieth?” aliuliza Robert kwa utulivu sasa akiwa ameacha kubofya bofya na akawa anamtizama Jullieth machoni.
“Laki mbili na ishirini”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tobaa yaillah..!! laki mbili na ishirini? yanii na urembo wote huo unalipwa laki mbili na ishirini!!. Hivi wewe Jullieth Wee billgate huwa humsomi speech zake? Alisha sema,kuzaliwa maiskini sio dhambi ila kufa masikini ni dhambi kubwa utalipwaje pesa kidogo hivyo halafu ulidhike mwanamke?.. hiyo ni dhambi mama.”
Robert alisema kwa kulalama zaidi..
Sasa alisimama katika kiti alichokuwa ameketi na kuzunga upande ule aliokuwa ameketi Jullieth kisha akaketi juu ya mkono wa sofa pembeni mwa Jullieth.
“Nataka nibadilishe maisha yako lakini kwa sharti moja tu jepesi.”
Alisema Robert kwa utulivu akimpindisha mkono wake na kuupandisha juu ya bega Jullieth.
Kengele ya hatari iligonga katika kichwa cha Jullieth..
‘Rushwa ya ngono inataka kutokea’..
Ndio kitu pekee kilicho tambaa katika akili yake wasaa ule…hata ule mkono wa ulipotua begani mwake alijikuta akirejea katika huzuni yake ile ya awali..kwani katu asingekuwa tayari kutoa mwili wake sadaka ndani ya ofisi ile kwa ajili ya mshahara na kitengo cha kazi katika kampuni..
“Sharti gani hilo jepesi bosi..?” aliuliza Jullieth akijitengeneza vizuri pale sofani wasiwasi ukiwa mwingi usoni mwake.
“Good question mwanamke..jambo moja tu jepesi..” alisema Robert huku akipapasa taratibu bega la Jullieth.
“nataka unifanyie jambo moja dogo..” alisema Robert na kutoa simu yake ya mkononi na kupiga namba Fulani kisha akaweka simu sikioni..dakika kadhaa simu upande wa pili iliita kwa muda kidogo kisha ikapokelewa na sauti ya mwanamke.
“Hellow”
Sauti ya upande wa pili izungumza ajabu Robert hakujibu kitu zaidi alikata simu kisha akamgeukia Jullieth.
“Nataka ufanye jambo moja..nahitaji umtambie mwanmke huyu katika simu kuwa mie ni wako na katu huwezi kuniacha”
Alisema Robert..Jullieth alishangaa alimwona mwanume yule kama punguani..vitu gani vya kipuuzi anamtaka avifanye, na kwanini vitu hivyo vilivyo vya kipuuzi ndio iwe kazi yake..jambo hilo la kipuuzi lina umuhimu gani kwa huyu mwanaume?. ‘Mtambie huyu mwanamke umwambie kuwa mie ni wako na huwezi kuniacha’
Khaaa!.
Jullieth aliyawaza ndani ya dakika moja.
“Nafikili Sijakuelewa vizuri” alisema Jullieth.
“Sikia Jullieth,iko hivi..”.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Robert alirudia tena kutoa maelekezo. “kuna mwanamke ni mpenzi wangu..nampenda mno, ni mrembo na anapendwa na wanaume wengi sana hapa jijini actually anajijua kuwa yeye ni mzuri hivyo anatumia nafasi hiyo kunisumbua na kunitesa sana kimapenzi, sasa nataka kumwonyesha kuwa hata mimi niko vizuri, napendwa na nagombaniwa vilevile..ninacho taka umpigie simu na umchimbe mkwara mkali juu yangu mie.”
Alisema Robert.
“Sasa hapo unatengeneza penzi au unabomoa bosi”
“Fanya kazi ninavyo kuagiza mwanamke” alisema Robert kwa ukali kidogo..
“Haina shaka, unauhakika ni hilo tu au kuna jingine.?”
“Hakuna zaidi ya hilo mrembo.” Alijibu Robert,.sasa akawa anapiga tena ile namba.
Simu iliinza kuita,.kisha akamkabidhi Jullieth simu. “Zungumza nae” alisema haraka haraka.
Simu iliita kwa muda kidogo kisha ikapokolewa na sauti nyepesi ya mwanamke
“Hellow”
“Nisikilize wewe mwanamke” Jullieth alinza sanaaa ya maigizo.
“Wewe nani kwanza” mzunguzaji wa upande wa pili alisema kwa wahaka kidogo.
“Ooh.. unaogea na mrs Robert nimekupigia simu kukueleza maneno machache lakini mazito..upo bibi?”
“Mwenye simu yuko wapi?”
“Sikia wee kizabizabina,.mwenye simu kalala kachoka kwa shughuri pevu ya malovee niliyo mpatia..nataka nikwambie kuwa kuanzia leo sitaki nione namba yako katika simu ya mahabuba wangu Robert na siyo hilo tu, pia kaa mbali na Shabab wangu.. kama itatokea nikagundua bado unaleta shobo zako za kike kwa mwanaume wangu..nafikili hapo ndipo utakaponijua kama mie mtoto wa kisambaa au wakingazinja nyang’au wewe”
“Wewe nani unaezungumza” mzungumzaji wa upande wa pili aliongea kwa mahamaniko makubwa.
“Wewe una matatizo ya masikio ama? Niseme mara ngapi kuwa mie ubavu wake na Robert” alijibu Jullieth,.Robert aliyekuwa pembeni ndani ya ofisi akamwonyesha dole gumba ishara ya kuwa alikuwa akifurahishwa na namna mazungumzo yalivyo kuwa yakiendelea baina yao wawili.
“Hivi kweli Robert anafikia hatua ya kunichanganya na machangudoa mie!. We kahaba nimesema mpe simu huyo mwanaume” alisema mzungumzaji wa upande wa pili kwa hasira.
“Alaa!. Sasa nataka kukuonyesha kuwa mie nimefundwa nikafundika namna ya kumshughurikia mwanaume..we si unajitia jeuli huyu mwanaume leo huto mwona hadi nitakapo amua mwenyewe..na hili penzi la kichangudoa ndio haswaa linampagawisha bwana wako kama hujajua hilo.. chukua hilo la bure..” alisema Jullieth kisha akakata simu.
Hapo hapo Robert alimrukia na kumkumbatia kwa furaha.. “safii Jullieth ume-crooning vizuri sana.” Jullieth alibaki kimya akimwona bosi wake kama mtu aliyepatwa na wazimu Fulani utokanao mapenzi..
“Unajua farasi unae mjua hakutishii mwendo, hapa sasa kazi iliyobaki ni yangu” alisema Robert kwa furaha.
“Pole sana bosi wangu,ila naona kama nimelivuruga kabisa penzi lenu”
“Hujavuruga hata kidogo, hapo sasa ndio umeliboresha penzi Jullieth”
“Kivipi bosi”
“Unajua katika maisha ya kimapenzi huwezi jua thamani ya mtu hadi utakapo kumbwa na hali tete moyoni, hapo ndipo nguvu ya pendo inapo jidhihirisha moyoni mwako” alisema Robert, na wakati huo huo ile simu iliita. Mpigaji akiwa ni yule mwanamke wake.
“Unaona sasa, huko aliko kiroho kinamwenda mbio”
Alisema Robert huku akitabasamu, simu iliita bila kuipokea kisha akaizima kabisa simu yake.
Badaaa ya kufanya tendo lile ambalo kwa Jullieth lilionekana ni upuuzi, Robert alimuhakikishia kuendelea kubaki katika kitengo chake ndani ya kampuni, lakini pia, mshahara wake kupanda mara mbili zaidi..
Ilikuwa ni ushindi mkubwa kwa Jullieth kwani aliona maisha yake yamebadilika ghafla kwa mtihani wa kumwua mende kwa kumkanyaga..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kweli katika kampuni Jullieth alibaki katika kitendgo huku akipata malupulupu lukuki kila alipo ingia ofisini.
Vilevile, ajabu ni kuwa penzi la Robert na mpenzi wake ambaye badae Jullieth alikuja kumfahamu kuwa anaitwa Penina lilichanua na kumea kama uyoga.
Ama kweli ‘MAPENZI YAMELOGWA’ kama alivyo andika yule mwandishi katika muswada wake..
Hili lilimstajabisha Jullieth na kuamini maneno ya Robert kuwa “katika maisha ya kimapenzi huwezi jua thamani ya mtu hadi utakapo kumbwa na hali tete moyoni, hapo ndipo nguvu ya pendo inapo jidhihirisha moyoni mwako”
Maisha yaliendelea kama kawaida japo walau kidogo hali ikiwa nzuri kwa Jullieth ambapo toka atengeneze penzi la bosi wake huyo alikuwa akipata fursa nyingi za kipato ndani ya kampuni na hata nje ya kampuni urafiki wake na Robert ukiwa mkubwa siri ya mipango iliyofanywa siku za nyuma ikibaki vifuani mwao.
Laikini pia pendo lake kwa Chacha ambaye hakuwa na uwezo wa kusimama lilikomaa mno moyoni mwake.
Kiasi cha miezi minne ilikatika toka kisanga cha Kule ofisini kati yake na Robert na mchumba wa bosi wake kutokea.. alisahau kila kitu..kitu ambacho hakujua ni makubwa ambayo yangekuja kutokea katika maisha yake kutokana na tukio lile..*****
Siku ya alhamisi, kulikuwa na msururu mrefu wa magari katika barabara ya Nyerere, jua lilikuwa kali joto likiwa la kiwango cha juu katika jiji la dar.
Askari wa barabarani alikuwa akiruhusu magari ya upande mmoja kwa muda mrefu, hususani yale yaliyo tokea uwanja wa ndege,
Magari yaliyo tokea mjini, buguruni na temeke yalikuwa yameganda katika barabara kwa muda mrefu huku kukiwa na msururu mkubwa.
Jullieth alikuwa katika bajaji akitokea kawe akipita ubungo, lakini hakuweza kuendelea mbele kutokana na mlundikano wa magari eneo la Tabata relini foleni iliyokuwa imeanzia Tazara.
Mlundo wa magari njiani hapakuwa na upenyo walau wa kupenyaza bajaji.
Yeye na dereva bajaji walisalimu amri ilibidi watulie tu hadi magari yatakapo ruhusiwa.
Dakika kumi na mbili zilikatika foleni ikawa inakwenda kwa mwendo wa kunyata.
Dakika hiyo hiyo simu ya Jullieth aliita kwa kasi, alitoa katika mkoba na kutizama mpigaji alikuwa ni nani.
ilikuwa ni namba ngeni.
Alibonyeza kitufe cha kupokelea na kuiweka simu sikioni.
“Yes hellow.”
“Unaongea na Eric Zabareta naongea na Jullieth Charles”
“Yes ndio mie”
Vema..kwa sasa upo Tabata relini kaskazini magharibi mwa Tazara,upo ndani ya bajaji ndogo ya rangi ya buluu umevaa suruali ya jinsi raba nyeupe na kitopu cheupe, unatumia simu Tecno A5 uongo au ni kweli? Mzungumzaji wa upande wa pili alizungumza kwa mpangilio kama msomaji wa habari katika redio.
Jullieth alipatwa na mikunjo usoni mwake,akiwa na vitendawili lukuki dhidi ya mtu yule wa ajabu.
“Unashida gani na wewe ni nani?” Jullieth aliuliza.
“Utanifahamu muda mfupi ujao lililo la muhimu kwako ni kutulia hivyo hivyo ndani ya bajaji hiyo hadi utakapo fikishwa eneo hili.”
“Whaat!.”
Jullieth alitahayari kwa hamaki..lakini wakati huohuo mtu mmoja alitokeza nyuma ya Toyota nyeupe iliyokuwa ukingoni mwa bajaji ile na kujisokemeza ndani ya ile bajaji na kuketi nyuma kwa abiria alipokuwa ameketi Jullieth..CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jullieth akiwa bado amepachika simu katika sikio lake alichia yowe dogo la mstuko lakini kwa kitendo cha haraka mno yule jamaa alitoa bastola ndogo iliyokuwa imevishwa bomba la chuma mbele ya mdomo ambapo kilitumika kwa kuzuia sauti.
“Ole wako upige kelele namwaga utumbo wako sasa hivi” jamaa alisema kwa kitisho macho makali ameyatoa kwa Jullieth yule dereva bajaji alivuta krachi na kuvuta mafuta akipandisha tuta la upande wa pili wa barabara..wakati yule mvamizi akiwa ameipachika ile bastola ubavuni mwa Jullieth.
Ala!. Kumbe na huyu dereva yupo pamoja na huyu baradhuli!.
Wakati Jullieth akiwaza hilo tayari yule dereva alikwisha iingiza bajaji katika bustani iliyo kando ya barabara na kuiondoa kwa kasi huku akichukua uelekeo wa ubungo.
Yule mvamizi aliendelea kudidmiza kwa nguvu mdomo wa bastola katika ubavu wa Jullieth. Jasho lilimtoka binti yule hata siku moja hakuwahi kutegemea kuwa ipo siku ataelekezewa mwilini mwake silaha hiyo hatari.
Dereva yule aliondoa kwa kasi bajaji na kuingiza katika barabara,.hatua kumi kabla ya kuyafikia mataa alikata kushoto kama aningia ilipo mitambo ya umeme songas kisha akachepuka katika kinjia kidogo kilicho mpeleka hadi katika barabara ya rami, sasa akachukua uelekeo wa ubungo maziwa safari yake ikaishia mbele ya nyumba ya kifahari.
Akajitoma ndani ya ngome ya nyumba ile.
Ilikuwa ni moja ya nyumba za kisasa katika viunga vya ubungo maziwa.
Jamaa aliyekuwa amekandamiza mdomo wa bastola katika ubavu wa Jullieth alimtaka kutelemka.
Jullieth aliyekuwa akihema kwa hofu huku jasho likimtoka kama kwamba ametoka katika mbio za marathoni aliteremka huku akiwa anatetemeka kama yupo katika milima ya theruji.
“Jamani mimi kosa langu nini?” alisema kwa hofu.
Jamaa hakujibu zaidi ya kuangaza huku na kule kisha akingiza mfukoni na kutoa noti za shilingi elfu arobaini na kuumpa yule dereva bajaji.,
“Chuse boy kazi nzuri hakikisha simu yako inakuwa hewani ili badae uje uchukue maiti ya huyu demu ukaitupe huko ufukweni” jamaa alisema kwa kunong’ona,.maneno yale yalipenya katika masikio ya Jullieth na hapo alijikuta anajikojolea pasina kutegemea.
“Poa kama kawa man, mie sina longolongo” alijibu dereva bajaji huku akiachia tabasamu pana kwa kupata elfu arobaini za haraka haraka.
“Haya wee kamalaya songa huko..” jamaa alisema huku akimsukuma Jullieth kwa mbele upande zilipo kuwa nagzi za kupandisha kuingia ndani ya jumba lile la kifahari.
“Jamani lakini kwani unashida gani na mimi wewe mkaka” Jullieth alisema kwa mahamaniko.
Na mara hiyo hiyo jamaa aliachia kofi kali la uso lililomfanya Jullieth atoe yowe la mstuko na uchungu.
“Shenzi taipu!!. songa mbele huko unaleta pozi mbele ya chizi nitakupasua…oooh!.” Jamaa alikoroma kwa ukali.
Binti alipepesuka huku akiona nyota mbili mbili mbele yake.
Jamaa alimwongoza Jullieth hadi katika sebule kubwa ndani ya nyumba ile, sebule ilikuwa na vitu vyote thamani kila pembe.
Kama ungepata bahati ya kuona madhali ya sebule ile ungeona masofa ya kisasa ya rangi ya kijivu, runinga kubwa ya kisasa{flat screen} iliyobadnikwa katika ukuta, meza ndogo ya kioo iliyo kuwa katika ya sebule lakini pia chini kulikuwa na zulia kubwa la manyoya ya sufi ya kupendeza.
Yule jamaa alimsukumiza Jullieth katikati ya sebule, yowe jingine la mstuko lilimtoka Jullieth kabla ya kujikuta akienda mzima mzima na kujibwaga katika zulia...CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hata alipo inua macho yenye hofu kubwa alimwona jamaa akiwa amekamata bastola mkononi mwake huku akimtizama kwa dharau.
“Wewe shida yako nini kwangu?” aliuliza Jullieth kwa hofu.
“sijakuleta hapa kunihoji maswali kahaba wewe funga bakuli lako”
“Lakini jamani mie sina ubaya na mtu kwanini madhila haya unifanyie eeh?” Alisema kwa mahamaniko makubwa.
“Kaa hapo” jamaa alisema kwa sauti ya kawaida akimwonyesha sofa aketi.
Jullieth alibaki amesimama kwa sekunde kadhaa akiwa haelewi afuate agizo la yule mtekaji wake ama laa!. Lakini mwisho aliamua kuketi katika sofa akiwa makini mno na yule jamaa.
“Sikiliza Jullieth Charles” jamaa alianza kuongea kwa pozi akiwa tayari ameketi katika sofa lililokuwa likiangaliana na pale alipokuwa amekaa Jullieth.
“Kuna mambo mawili hapa unayo takiwa kuchagua..alisema yule mtu dharau ikiwa kubwa usoni mwake..akabadilisha mkao na kuketi mtindo wa kukunja nne kwa miguu yake mikono yake ikipangusa pangusa bastola iliyokuwa imeelekea kwa Jullieth.
“Mambo mawili mrembo…kufa au kucheza picha la ngono”
“Whaaaat!!”
“Hujasikia ama? Nimesema uchague kufa ama kucheza picha la ngono”
“Wewe mkaka vipi una wazimu!.mie nimekukosea nini hata utake kunipa adhabu kubwa hivyo!”
Alisema Jullieth kwa mshangao mwingi uliochanganyikana na hofu.
“Wewe kahaba unataka nizungumze kinyamwezi ndio unielewe blood fool” jamaa alikoroma kwa hasira macho yake yakiwa makali mbele ya Jullieth.
“una nini lakini brother?” Jullieth aliuliza akimtizama jamaa kama kwamba amemwona kichaa aliyeshikilia lungu mbele yake.
“Doniii!” yule mtu alipaza sauti kuita na mara hiyo hiyo sauti ya kumwitikia kutokea moja chumba katika ile nyumba ilisikika.
“Kuja hapa na wenzio”
Sekunde tano zilizofuata njemba wawili wenye miili iliyo shiba zilitokeza katika sebule lile wakiwa vidali wazi na bukta fupi, ni kama walitoka katika mazoezi fulani ndani ya nyumba ile.
“Ndio Raja” jamaa waliitikia wito na hapo Jullieth akapata kujua jina la mtekaji wake anaitwa Raja.
“Fanyeni kazi yenu iliyo waitieni” Alisema Raja, wale jamaa walimgeukia Jullieth na kumtizama kwa jicho la uchu wa ngono, mihemko ya kiwazimu ya mapenzi ikawavaa, wakasogea katika sofa alilokuwa ameketi Jullieth.
Jamaa alisogeza uso wake karibu na shingo ya Jullieth kisha ikawa ni kama anamnusa nusa mwili wa yule binti huku mkono wa kulia ukiwa unashika shika nywele za binti yule.
Jullieth alitetemeka kwa hofu, dalili ya kubakwa na wale watu ikawa waziwazi, aliachia kofi kali lililombatiza katika uso jamaa aliyekuwa akinusa shingo yake.
Jamaa alitoa mguno wa mstuko maumivu makali ya kibao yakafukuta katika shavu lake.
Jamaaa wa pili alimuwahi Jullieth na kumshika miguu yake kisha kwa nguvu akmvuta kwa mbele, Jullith aliachia ukulele wa hofu huku akijikuta akianguka chali katika lile sofa.
Wakati huohuo jamaa aliyepigwa kibao alisimama kama mbogo na kumvaa Jullieth pale katika sofa na kumkaba shingoni huku akimtandika vibao vikali mashavuni.
.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment