Search This Blog

Friday, July 15, 2022

JULIETH - 1

 





    IMEANDIKWA NA : ZULFA HUSSEIN



    *********************************************************************************



    Simulizi : Julieth

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    “Krii,kriiii, krii, krii,” sauti kali ya simu ya mkononi ilikuwa ikiita kwa kasi, ilirudia rudia kuita kwa kasi bila kukoma, mtu aliyekuwa anakoroma katika kitanda, hakuwa na dalili ya kuamka kwa wito wa simu ile ya mkononi.

    .CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mpigaji wa simu ile hakuchoka, ni wazi alikuwa na shida muhimu na mmiliki wa simu ile, aliendelea kupiga ile simu ilihali mmiliki akiwa amezama kabisa katika usingizi mzito wa pono.

    Yapata saa tisa za usiku, joto lilikuwa kali ndani ya chumba hiki ambacho ndani yake kulikuwa na mwanamke aliyelala fofo akiwa mtupu, huku mwili wake ukiwa umeloa mijasho itokanayo na joto kali lililokuwa likifukuta mule ndani.

    Ilikuwa ni chumba kidogo, ambacho hakikuwa na vitu vingi vya thamani, ungeweza kuona kitanda cha tano kwa sita, meza ndogo, stuli mbili za kukalia,kiruninga kidogo aina ya sony na beseni lililo beba vyomba vingi vya plastiki.

    Katika kuta za chumba kile, kulikuwa na mapicha ya wasaniii wa ughaibuni wa muziki aina ya hihop, hadi hapo ungeweza kuhisi mwenyeji wa chumba hiki alikuwa ni kijana, lakini sio kijana tu bali ni kijana wa kileo mwenye mapenzi na muziki.

    Simu ile iliendelea kuita pasina kupokelewa na binti aliyekuwa amelala chali kihasara huku akiwa kama alivyo kuja duniani.

    Simu ilikatika na katika kioo cha simu ilionyesha missed call kumi na nne.

    Binti yule alizidi kukoroma. Huku mwili wake wenye shepu ya kuvutia ukiwa bado umeloea katika bahari ya usingizi..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini wakati huo huo, nje ya nyumba ile kulikuwa na mtu aliyekuwa akimwaga mafuta ya petroli kuzunguka nyumba ile ya chumba kimoja, ambayo ndani yake alikuwa amelala msichana yule aliye uchi wa mnyama.

    Jamaa aliyekuwa akimwaga mafuta yale ya petrol alionekana ni mtu mwenye hasira na donge kubwa kifuani mwake, alidhamilia kabisa kuua mtu, hakuwa na utani na kile alicho kuwa akikifanya.

    Hatua hamsini kulikuwa na kijana aliyekuwa akihaha huku na kule kama kuku mwenye kutaka kutaga, alikuwa akipiga simu yake kila mara, lakini alionekana kutopata majibu kutoka upande wa pili, na kadri alivyokuwa akikosa majibu ya kupokelewa kwa simu yake ndivyo alivyo zidi kuwa na wahka mkubwa mno.

    Muda huo yule jamaa aliyekuwa akimwaga mafuta ya petrol alikuwa amekwisha maliza zoezi lake, sasa alitoa kiberiti cha gesi na kuwasha moto.

    Jamaa aliyekuwa umbali mdogo alipo ona lile tukio alitoa ukulele mdogo wa fadhaa huku mikono yake akishika kichwa chake. Macho yamemtoka pomoni.

    Moto mkubwa ulilipuka ghafla, na kijumba kile cha chumba kimoja kikashika moto, jamaa aliyekuwa mita hamsini alipagawa vibaya mno, alihaha huku na kule, alitamni akimbie eneo lile lenye kuwaka moto, lakini alikuwa mwingi mno wa hofu.

    Binti aliye kuwa ndani amelala uchi akiwa ameloea katika usingizi wa pono hakujua nini kiinaenda kutokea katika maisha yake.

    Moshi mwingi na mzito ulizagaa ndani ya chumba,

    Sasa binti yule ikawa hapati pumzi, hewa aliyo kuwa anavuta ikawa nzito iliyochanganyikana na moshi mzito kabisa.

    Alikohoa hovyo huku akifumbua macho kwa shida, nguvu zikiwa hazipo mwilini mwake, moto ulikuwa umekamata katika godoro na chandarua, alijisukuma kwa shida, huku moto mkali ukimuunguza vibaya katika mapaja na kifua chake kilichokuwa hakijastiliwa na nguo yoyote.

    Alijisukuma kutoka pale katika kitanda kilicho kuwa kimeshika moto vibaya na kujivuta mlangoni, alishika kitasa cha mlango na kuuvuta mlango kwa nguvu, lakini mlango haukufunguka, ulikuwa umefungwa kwa nje.

    Wakati huo huo mbao iliyokuwa imeshikilia kenchi za paa ilipolomoka na kumtwanga kichwani kwa nguvu, binti alidondoka chini huku mbao za paa zilizo kuwa zimeshika moto kisawasawa zikimwangukia juu ya mgongo wake ulio kuwa mtupu!.

    Alitoa sauti kali ya maumivu ya kuungua moto, huku akisukuma kwa viganja vyake laini mbao zile zilizo kuwa juu ya nyama ya mgongo wake wenye ngozi ya rangi ya chokleti na kugeuka kuwa na donda kubwa lililo acha nyama nyekundu iliyo tokana na kuunguzwa na moto ule.

    Hata viganja vyake vilipogusa mbao zile zilizo kuwa zikiwaka moto, alishia kupiga ukulele mkali wa kuunguzwa na moto japo alifanikiwa kusukuma ubao ule,

    Tayari hata mlango pia ulikuwa umekwisha shika moto mkali wa petrol.

    Binti akajitahidi kusimama, lakini wapi, kabla hata hajasimama kwa uzuri, ukuta wa kijumba kile ulipolomoka na yeye kufunikwa ndani ya kifusi chenye kuwaka moto wa chini kwa chini.

    Sasa aliungua kama tofali la kuchoma.

    Majirani wa eneo lile lenye kufahamika kama, Keko Magurumbasi walijazana pembeni mwa kijumba kile alicho kuwa akishii kijana mwenye kufahamika kwa jina la Chuse boy, jitahdada za kuuzimisha moto ule kwa maji hazikuzaa matunda hata tone.

    Wakati huo Mtu mwwenye kuitwa Chuse boy ama unaweza kufupisha ukamwita Chuse, aliendelea kusimama mita hamsini, akiwa ni mwenye kuchnganyikiwa kupita kiasi, alishuhudia kijumba alicho kuwa akishii kikipolomoka chote na binti aliyekuwa ndani mwake akiteketea kwa moto huku majirani wakishindwa kabisa kuudhibiti moto.

    Kila mtu usiku ule alikuwa akiulizia juu ya uhai wa Chuse, hakuna aliye jua kama kijana huyo alikuwa ndani ya chumba kile ama laa!

    Ilikuwa ni saa tisa na nusu usiku..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jamaa aliyekuwa ametia moto nyumba ile alikuwa amejichanganya na mashuhuda wa sakata lile huku na yeye akijifanya kutojua chanzo cha moto ule, dakika ishilini badae, aliondoka maeneo yale ya Keko magurumbasi baada ya kushuhudia kijumba kile kikipolomko na kuridhika kwa kutokuwepo kwa uhai kwa viumbe waliokuwa ndani. Jambo moja tu ambalo hakulijua, aliyeungua ndani alikuwa ni mtu mmoja pekee ilihali moyo wake ukiamini ameteketeza watu wawili ndani ya chumba.

    Alitembea taratibu kutoka kule mabondeni uswahilini, na kutembea kwa hadhali kubwa, kisha akashika njia ya ngazi ngazi zilizo jengwa mahususi kwa wakazi wa mabondeni, alipandisha na kutokea katika kiwanda cha mkate, hapo akapita kichochoro kilefu na kutokea katika sheli kubwa ya mafuta aliko kuwa amepaki gari lake dogo la Nisani patrol, akaingia na kuliondoa taratibu eneo lile.

    Sasa ilikuwa ni saa kumi kamili usiku.

    Aliingia katika barabara ya keko, na kunyooka na njia ya karume magomeni. Ambako njia hii ilimpeleka hadi makumbusho na kunyooka na njia ya Tegeta.

    Dakika ishilini na tisa zilimtosha kumfikisha mbezi beach ya jogoo, alingiza gari lake katika jumba la kifahari, nyumba ambayo bindamu yeyote wa jangwa la sahala, angetamani kuishi katika makazi yale.

    Alingia katika sebule kubwa lililosheheni kila aina ya fenicha, hapo hakukaa alipitiliza hadi chumbani mwake.

    Nyumba nzima ilikuwa kimya.

    Ndani ya chumba nadhifu, jamaa alisimaa akiwa amevua shati lake anahema, huku macho yake yakiwa mekundu na yenye hasira kali, alitizama picha kubwa iliyo mwonyesha binti mrembo aliyempenda zaidi ya kitu chochote,.sasa roho yake ilipata amani,alijiona ni kiumbe aliye punguza mzigo mkubwa mno maishani mwake.mtu yule alikuwa ni mtu mwenye hasira za ajabu mno



    Picha ilimwonyesha binti mzuri, mwenye sura ya duara, na macho ya kuvutia midomo,mashavu na uso wake kwa ujumla mwanume yeyote asingeacha kutamani kuwa tulizo la moyo wake. Kifua chake kilikuwa kidogo kilicho beba maziwa madogo kama maembe,kiuno kizuri na miguu yenye kufanana na chupa za bia ya Serengeti, binti alikuwa mrefu wa futi sita kimo ambacho angeweza kabisa kushiriki katika mashindano ya mwanamke wa urembo.

    Jamaa litizama picha ile ambayo nayo ilikuwa ikimtizama kwa tabasamu, akaibusu huku machozi yakimtoka na hata wakati anafanya tendo lile kumbukumbu lukuki zilipita katika kichwa



    .*********

    Katika darasa la journalism department ndani ya chuo cha DSJ, masomo yalikuwa yakiendelea kama kawaida, ndani ya chumba kikubwa cha darasa kilicho na hewa ya kutosha na kutoka katika mashine za AC, kila mwanafunzi alipenda hali ya hewa na mazingira yale.

    Kiasi cha wanafunzi ishirini na ushee waliokuwa ndani ya darasa hili wakiendelea na masomo, kiti cha nyuma kabisa aliketi mtu mwenye kuitwa Chacha, ni kijana kutoka musoma, alikuwa amejiinamia mbele ya meza yake ndogo yeye akiendelea kuuchapa usingizi.

    Siyo kwamba alikuwa labda hakulala usiku wa kuamkia siku hii, lahashaa.

    Chai nzito aliyokunywa katika kibanda cha mama ntile asabuhi hii, na hewa nzuri iliyokuwa ikitoka katika mashine zilizo fungwa mule ndani ndio zilizo mfanya alewe usingizi darasani.

    Lakini haikuwa hilo pekee lililochangia kulala, pia mwalimu aliyekuwa akifundisha somo la P.R {Public Relation and Advertisingi} hakuwa ni mpenzi kabisa wa somo hilo.

    Katika kozi hii ya miaka mitatu ngazi ya diploma aliyokuwa akichukua katika chuo hiki ni somo hili ambalo hakuwa akilipenda wala kuvutiwa nalo.

    Alilala na hakuna aliyemwamsha.

    Kiasi cha nusu saa alihisi kuguswa na kutikiswa katika mabega yake na vidole laini huku halufu nzuri ya manukato ikisambaa puani mwake. Alishituka na kuinua kichwa, hapao macho yake yaliyo toka katika usingizi na midomo iliyo tapakaa udenda uliyokuwa ukichuruzika wakati akiwa amelala ukamwagika chini.

    Alijipangusa mimate ilisambaa mdomoni mwake huku akikapua kapua kope za macho yake mbele ya mtu aliye mwamsha..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Binti mrembo mwenye sifa zote za kuwa miongoni mwa wanawake warembo alikuwa amesimama mbele yake akimtizama kwa tabasamu la mbali.

    “Mambo Chacha” binti alisalimia kwa sauti nyororo na yenye mvuto, jamaa aliguna kabla ya kuitikia, swali kuu kichwani mwake ikiwa ni mtu huyu mgeni mwenye kufaa kuwa malkia wa urembo kajuaje jina langu mimi, ilihali leo ndio mara ya kwanza namtia machoni.

    “Sorry nahitaji kiti hicho” binti aliongeza tena, jamaaa alitizama pembeni yake na aliona kuwa kulikuwa na kiti ambacho aliweka mizigo yake, vitabu na laptop ndogo.

    “Ooh! Samahni chukua tu”

    Alisema na kutoa mizigo yake na kumpatia kiti kile.

    Binti aliketi mkabala na Chacha eneo la nyuma kabisa ya darasa. Alikuwa ni mwanafunzi mgeni, ndani ya darasa lile.

    Wakati huo kipindi cha P.R kilikuwa kinaelekea ukingoni, Chacha hakulala tena, usingizi uliyeyuka ghafla.

    Kichwa chake kikaingiliwa na fikra mpya, sura ya msichana mgeni aliyeketi pembeni yake.



    Mwalimu aliyekuwa akiendelea kufundisha darasa lile lililosheheni watu wazima ambao wengi wao walikuwa tayari wana ajira zao na maisha yao, hakukuwa na bugudha kwa wanafunzi aiana ya akina Chacha. Aseme nini wakati kila mtu ndani ya chumba kile alikuwa ni mtu mzima na mwenye akili timamu zenye kujua nini anatakiwa kufanya.

    Hapakuwa na maongezi kati ya chacha na binti yule ambaye hakumjua jina lake, udhaifu wa Chacha ukiwa kutokuwa mzungumzaji mbele ya watoto wazuri, kama wasemavyo vijana wa leo, alikuwa mwoga na mtu asiye jiamini mbele mwanamke mzuri, japo tangu afike katika jiji la Dar es salama aliona wanawake wengi warembo, lakini moyo wake ulikiri kuwa binti huyu mgeni aliye pembeni yake ni funga kazi, alimuhusudu kweli kweli. Lakini hakuja aanze vpi kusema naye.

    Hadithi ya maisha ya Chacha huko musoma ilikuwa ni fupi

    Huku kwao Musoma alikotoka Chacha, alifahamika kama kijana jasiri na asiye ogopa lolote, alikuwa ni miongoni mwa vijana wachache katika kijiji cha Makutano aliye tajiri wa ng’ombe pengine kuliko kijana mwingine wa lika lake.

    Utajiri huu ulitokana na jambo kuu moja.

    Katika jamii za kabila la kikulya ilikuwa ikikabiliwa na tatizo kubwa la wizi wa ng’ombe kutoka koo moja hadi nyingne.

    Kuliwa na mapambono makali na vita kubwa miaka hiyo, katika koo hasa za waryochonka na wangurimi.

    Watu waliuuwana kwa mapanga.

    Familia zilisambaratika.

    Lakini pia watu walipatwa na ulemavu wa kudumu katika miili yao.

    Mwanzoni mwa miaka ya 1996 hadi 1999 hali ilikuwa tete mno.

    Ni hapo ambapo mashujaa wa koo hizi walio fanikiwa kuiba ama kukomboa n’ombe zao walinufaika kwa kiwango kikubwa. Chacha wakati huo akiwa na umri wa miaka kumi na sita tu, alikuwa ni miongoni mwa vijana wachache wenye kumiliki ng’ombe nyingi. Kabla ya migogoro hiyo kuzimwa na serikali ya awamu ya tatu.

    Wakati huo chacha alihitimu darasa la saba, lakini hata hivyo alifeli vibaya mno kutokna na kutumia muda mwingi katika makabiliano ya vita za kiukoo kuliko masomo.

    Hilo halikumpa tabu kijana yule ambaye wazee wake walimtaka aoe na aanze rasmi maisha ya kiutu uzima. Jambo lililoshangaza watu wengi ni pale kijana huyo alipo uza ng’ombe wawili katika mnada, na pesa aliyo ipata kuielekeza katika shule za sekondari za kulipia.

    Bado uwezo wake darasani ulikuwa mbovu kabisa, kutokana na kutokuwa na maandalizi mazuri tangu akiwa msingi,

    Lakini mahaba ya kijana huyo kuwa miongoni mwa watu wachache wasomi katika kijiji, hakusita kununua mitihani kwa gaharama yoyote ile..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hilo lilimfanya apande vidato bila kuwa na uwezo stahiki, na hata alivyo fika kidato cha nne Chacha alikuwa na mtandao mkubwa wa watu wenye uwezo wa kumvujishia mitihani.

    Alifanya mtihani wake wa mwisho akiwa na majibu ya ya mtihani aliovujishiwa, na mwisho alifaulu vizuri na kujiunga na kidato cha tano katika shule ya Mara sekondari.

    Huko alisoma miaka miwili, na katika mtihani wa mwisho alifeli vibaya mno kwani huko hapakuwa na mtu aliye mpa majibu ya mtihani kama ilivyo kuwa katika kijiji chake.

    Lakini mtu huyu hakukata tamaa, kwa kutumia vyeti vizuri vya kidato cha nne

    Alituma maombi ya kusoma katika chuo cha habari na mawasiliano DSJ kilicho jijini Dar.

    Siku chache badae alikubaliwa kusoma katika chuo hiki katika ngazi ya cheti.

    Alisoma mwaka mmoja na kuunganisha katika ngazi nyingine ya diploma. Hapa ndipo hali ilipo kuwa tete tena, kichwa chake kilikuwa kizito mno kuelewa masomo yale ambayo yalikuwa na uwanja mkubwa zaidi kuliko yale ya ngazi ya cheti. hakika

    Chacha alipenda elimu, lakini elimu ilimwendea kombo.

    ***

    Akiwa bado hajui kwa namna gani anzishe mazungumzo na binti yule mrembo, alishtuka alipoitwa tena jina lake na msichana yule.

    “Chacha” sauti nyororo ilipenya ndani kabisa ya ngoma za masikio yake.

    “Naam”

    Aliitikia upesi upesi, swali kuu bado likiwa ni vipi mtu huyu kamjua.

    “Kuna haja ya kuniazima vitabu vyako ili nicopy some notes ambazo mmekwisha soma hadi sasa” alisema binti.

    “Ooh! Haina neno, hilo umepata, wewe ni mgeni?” alijibu uchangamfu ukiwa usoni mwake.

    “Ndio, naitwa Jullieth Charles”

    “Asante mie Chacha Mabula”

    “Najua, nimeambiwa pale” alijibu binti huku akisonta kwa jamaa aliyekuwa mita mbili ambaye alimwambia jina la Chacha.

    “Alaa! safi, karibu sana, mtu wa wapi wewe Jullieth?” Chacha aliuliza huku akijitia uchangamfu zaidi.

    “Hapahapa mjini, naishi osterbay ” alisema Jullieth.

    “Ooh, mimi mwenyeji wa Mara huko musoma, ila hapa naishi huko gongo la mboto eneo moja linaitwa Kitunda.”

    “Asante Chacha nashukuru kukufahamu”

    “Mimi pia Jullieth”

    Walipeana mikono, lakini baada ya hapo walizungumza mambo mengi tu ya kawaida, huku Chacha akiwa mwenyeji mkuu wa Jullieth chuoni pale.

    Kila mvulana katika chuo kile aliyemwona Jullieth alikili moyoni kuwa amekutana na msichana mzuri.

    Lakini aliye jisikia vizuri katika wanaume wengi walio ishia kula kwa macho alikuwa ni Chacha, kwanza binti mrembo alikuwa karibu zaidi na yeye kuliko mtu yeyote chuoni pale, pili ni hatua ya kuwa na namba za simu za msichana yule aliyezoeana nae ghafla siku ile na hata kupena namba, aliamini hiyo ni fursa pekee itakayo mfanya achukue point tatu muhimu mbele ya masharobalo wa chuo kile,

    Hata baada ya vipindi vya dasani kuisha, waliagawana kwa miadi ya kukutana tena kesho chuoni pale.

    Jioni ya siku hiyo, Chacha alikuwa ndani ya chumba kidogo alicho kuwa amepanga huko kitunda.

    Bado ubongo wake haukuwa na kitu kingine zaidi ya taswira ya sura ya Jullieth.

    Pengine ungepata bahati ya kuona ndani ya kifua cha mtu yule, ungeweza kuona namna jina ‘Jullieth’ lilivyo kuwa limetapaka kwenye mishipa ya damu ya yule mtu. Joto kali la jiji halikuwa kitu kumzuia mtu yule kuwa ndani ya chumba chake jioni hii, chumba ambacho hakikuwa na panga boi labda lenye kupungza hewa nzito ya chumba kile.

    Hadi magharibi inaingia, mionzi dhaifu ya jua la jioni ikiwa inaelekea kuzama kabisa. Chacha alistushwa na sauti kali ya muadhini aliyekuwa akinadi swala kule musikitini, alijinyanyua kutoka katika kitanda na mahala alipo kuwa amelala chali kwa muda mrefu. Akili yake sasa ikiwa na uimara kidogo, sasa aligundua likuwa amezama katika bahari ya mawazo dhidi ya mwana mke wa urembo.

    Alijizoa kivivu na kuelekea bafuni,.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akiwa bafuni simu yake ya tecko iliita hadi ikakatika, dakika moja tena simu iliita tena na hadi ikakatika.

    Mara ya tatu simu iliita tena, wakati huo Chacha alikuwa ndio anatoka bafuni, aliiwahi simu na kutizama jina la mpigaji wa simu ile, moyo wake ulilipuka huku tumbo likipata joto furaha ikimtamba katika kifua chake baada ya kuona mpigaji wa simu ile, alikuwa Jullieth, bahati iliyoje. Alijikuta akitetemeka viganja vya mikono yake, bila kuelewa vipi anakuwa na hali ile. alijiweka sawa huku akitoa mguno katika namna ya kukwangua koo lake ili apokeapo simu ile kusiwe na mikwaruzo kooni, sauti yake isikike kwa uzuri katika masikio ya binti mrembo.

    Alibonyeza kitufe cha kushoto ambacho kiliruhusu kupokea simu ile, lakini wakati anafanya hivyo tayari na simu ile ilikuwa imeita katika kiwango cha kutosha.

    Ilikatika.



    “Ayaaaaaah” Chacha alipiga ukulele wa fadhaa, akijilaumu kwa kuchelewa kwake kupokea simu ile ya mrembo.

    upesi aliibonyeza sehemu imeandikwa Dialled Calls na kuipiga ile namba,

    samahani, salio lako halitoshi kupiga simu hii sauti ilitoka katika simu yake,

    “AAAAAGH, nini hiii!!” aliajilaumu tena kwa sauti.

    Alitizama mezani na kuona noti ya shilingi elfu tano, alitoka na taulo lake, mwilini akiwa na maji, alitoka nje na kupita katika kibalaza walicho kaa akina mama wengi na watoto, kila mtu alibaki akimshangaa vipi mtu yule amekumbwa na wazimu gani,

    Jamaaa hakujali, alikimbia hadi katika duka la mangi na kununua vocha, hakukumbuka hata chenji, alirudi ndani na kujaza zile namba za vocha, akili yake ilikuwa ikifanya kazi katika jambo moja tu, kuwasiliana na Jullieth.

    Baada ya kuingiza namba za vocha, sasa alipiga tena namba zile na kuweka simu sikioni akiwa makini kusikiliza upande wa pili.

    Simu ilikaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha sauti nyingine ikatokea katika spika za simu yake,

    “Samahani mtumiaji wa simu unayo mtafuta hapatikani kwa sasa jaribu tena….” “AAAAGH blood Coward nini hiki” hawa watu wa mitandao ni makum..{tusi} mtu kanipigia sasa hivi simu, mara hii eti hapatikani tena haya si mambo ya .. {tusi}”

    Alipiga tena na tena, lakini mambo yalibaki kuwa vile vile namba ile ilkuwa haipatikani, jamaa alinyong’onyea, hakujua mrembo yule alikuwa na shida gani na yeye, sasa vipi tena azime simu yake mara hii, hakujua.

    Usiku wa siku hii, baada ya chakula cha usiku hakuapata hata lepe la usingi, ungetazama katika simu yake katika sehemu yenye kusomeka dialed calls ungeona namba ya Jullieth ilipigwa mara hamsini na kidogo. Kwa hakika Mapenzi yalimzidi nguvu Chacha.

    Kitandani hakulala, alikuwa akijigeuza geuza huku na kule, taswira ya sura ya Jullieth ikimjia kichwani mwake, aliliona tabasamu mulua la binti yule, alikumbukua mguso laini wa dada yule, lakini pia aliikosa sauti nyororo ya malkia yule, alitamni kukuche upesi ili kesho asubuhi akutane na mrembo huyu mwenye kuumiza moyo wake.

    Ilikuwa ni kwa mara ya kwanza katika maisha yake kuhisi kumpenda mwanamke. Japo hili halina maana kuwa Chacha alikuwa mshamba katika ulimwengu wa mapenzi, aliwahi kuwa na mahusiano na mabinti wengi, ambao alishiriki nao kingono kwa nyakati tofauti, badhi yao walimpenda lakini yeye hakuwahi kuwa na pendo la kweli kwa mwanamke..CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zaidi ni kuwa, wanawake wengi ambao alifanikiwa kuwavua nguo zao za ndani, hapakuwa na hata mmoja aliyegusa japo nyayo za urembo wa mwanamke huyu aliye mtokea leo katika chuo.

    Alimfikilia mno Jullieth, hakuwa mwanamke wa kawaida japo alikuwa viungo kama vya bindamu wengine.

    Alifikilia mabo mengi kuhusu urembo wa binti yule, ambalo lilikuwa likimsumbua ni vipi anaweza kuwashinda vipopa wa mjini wenye pesa zao na maisha ya kifahari mbele ya malikia yule.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog