Simulizi : Dar To Mumbai
Sehemu Ya Pili (2)
Siku ya siku ikafika, wakapaki vyakula na kuingia kwenye gari tayari kwa safari. Walitumia masaa mawili hatimaye wakapaki gari na kuanza kupanda kamlima mwishowe wakatokea sehemu moja nzuri sana, iliyopambwa kwa ukijani, mawe na maji yanayotiririka mtoni, sauti za ndege zilinogesha vyema sehemu ile.
"Twende tukakae pale" Pooja akamuelekeza Nea.
Kwa pamoja wakaelekea Wakakaa na kuanza kuongea hili na lile, Pooja akatoa chakula na wakaanza kula na kuendelea kupiga stori, ukweli ilikuwa ni siku ya furaha sana kwa Nea kuwepo katika mazingira yale, mawazo yakahama na kwenda mbali sana wala hakusikia lolote Pooja alilolisema, akashtushwa baada ya kushikwa bega.
"Mhm! Unawaza nini?" CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Pooja umekuwa mwema sana kwangu, umekuwa ukinionesha upendo na kunijali bila kuangalia mapungufu yangu, ukweli katika dunia hii hamna mfungwa anayetendewa hivi kama unavyonitendea wewe, nashukuru sana tena sana".
"Nea binadamu wote tuna haki sawa chini ya jua, hivyo ni wajibu kumsaidia mtu kama nina uwezo wa kumsaidia" Pooja akaongea huku akimminya minya mkono Nea.
"Pooja nataka nikuambie siri ya moyo wangu, ambayo ni chanzo cha yote haya hadi leo mimi kuwa hapa".
Pooja akajiweka sawa kusikiliza nini anataka kuambiwa, Nea akamtazama Pooja kisha akataka kusema kitu lakini akasita, na Pooja naye akamtazama Nea kwa makini zaidi akisubilia kuambiwa.
"Hata sijui nianzie wapi?" alisema Nea.
“Popote tuu anza”
Baada ya kumaliza kidato cha 6 nlikuwa na ndoto za kuendelea elimu ya juu na nilitamani sana kuwa mtaalamu wa "Mult-media and animation" ambapo kwa bahati mbaya nikakosa chuo nchini kwetu Tanzania,h ivyo ikaniradhimu nisubiri hadi mwaka unaofatiwa kwa kuwa sikutaka kupoteza muda ndipo nikatuma maombi katika chuo kikuu cha Mumbai chini ya usimamizi na udhamini wa serikali ya India, Majibu yalivyotoka nikawa mmoja kati ya watu 10 ambao walifanya vizuri, hivyo kustahili udhamini wa kujiunga na chuo hiko kikubwa kabisa nchini India na duniani kwa ujumla.
Siku zikayoyoma hatimaye tiketi za ndege na fomu yenye maelezo ya kujiunga zikatumwa, kwenda kuangalia kama nami nimo, kwa bahati mbaya sikuwemo kati ya zile tiketi 5 ambazo zimefika, Nikawa nawaza sana kwanini mimi niliyeshika nafasi ya kwanza nikose kipaumbele cha kwanza na wenzangu ambao nimewazidi kupata hiyo nafasi, ata hivyo walitutia moyo kwa sisi ambao tumekosa kwa mara ya kwanza kuna awamu ya pili pia, hivyo tuwe na subira.
Siku, wiki, hatimaye mwezi ukakatika ndipo chaguzi ya awamu ya pili na ya mwisho ilipotoka sikuwa na shaka kwani niliamini kabisa kwa asilimia zote lazima nitapata nafasi ya kwenda kutimiza ndoto zangu. Nilipoingia mtandaoni kuangalia majina yaliyotoka, haikuwa kama nilivyotegemea kwani jina langu halikuwepo, moyo ukanienda mbio sana nikaanza kulia kwa Mungu wangu kipi nilichokosea kikubwa hadi kukosa fursa ambazo niliamini kwa kiasi kikubwa zitanisaidia katika kuyabadili maisha yangu. Bibi yangu kipenzi akawa akinitia nguvu kila siku, wale wenzangu wakaniaga na kwenda zao kusoma. Maisha ya mtaani yakawa magumu mno, ila hivyo hivyo nikawa napambana ili mradi tuu bibi yangu kipenzi aweze kula.
Siku moja nikiwa mjini katika mihangaiko yangu, ikanyesha mvua kubwa mno ambayo ilimfanya kila mmoja atafute pa kujificha ili asilowe kwa mvua ile, katika tafuta tafuta yangu nikaona kiuwazi ambacho watu wengi walikuwa wamesimama wakiogopa kunyeshewa na mvua ile, nami nikajibanza mvua ikanyesha sana huku radi ikipiga kwa nguvu na kufanya walio na roho nyepesi kuanza kuogopa . Kwa upande wangu sikuifurahia kabisa ile mvua kwani hadi muda huo sikuwa nimeingiza hata sh.10, mawazo yakarudi kwa bibi yangu nikaifikilia nyumba yetu ile ambayo mvua ikinyesha inakuwa kama chujio, sikuwa na la kufanya zaidi ya kuomba mungu tuu madhara yasiwe makubwa. Nikiwa katika dimbwi lile la mawazo nikaona watu wakianza kusukumana kuangalia vizuri nikaona kuna mama wa makamo akiwa ameshikwa na mbavu, kiasi kwamba hawezi hata kupumua, nikagundua hatari ambayo inaweza mkuta mama yule kama msaada wa haraka haujatoka, hali ikazidi kuwa mbaya kwa mama yule kila niliyefikiria anaweza kutoa msaada hakufanya hivyo, zaidi ya taratibu kuondoka eneo lile, ikabidi nisogee na kuanza kuwaomba msaada.
"Jamani tusaidianeni kumfikisha huyu hospitali la sivyo atakufa hapa.."
kila mtu aliniangalia lakini hamna aliyethubutu kunisaidia, ikabidi niite tax iliyokaribu na kusaidiana na yule dereva wa tax tukamwingiza yule mama kwenye tax, nikaomba msaada kwa wamama wakanipa kitenge na nikamfunika vizuri yule mama kisha kumuhimiza dereva wa tax awahi hospitalini, hali ya mama yule ambaye sikuwa na mfahamu hata jina ikazidi kuwa mbaya zaidi kiasi kilichonifanya nizidi kuogopa, mvua ile ikafanya barabara kufunga na magari kushindwa kabisa kutembea ivyo kukawa na ugumu kwa gari ile kupenya. Namsifu sana dereva wa tax ambaye alijitahidi hatimaye tukafika hospitali, kwa haraka haraka nikaomba msaada, manesi wakamchukua na kumpeleka kwa daktari, muda wote nilikuwa nje kusubili taarifa ya daktari, sikuwa na pesa ya kumlipa mwenye bajaji nikajitahidi kumuelewesha lakini hakunielewa, nikavuta pochi ya yule mama, moyo ulidunda mno nilichokiona mle.
Kulikuwa na maburungutu matano ya pesa, ambayo sikujua idadi ya pesa iliyokuwa katika kila burungutu, ikabidi nichomoe noti ya shilingi elfu kumi na kumkabidhi dereva kisha akaondoka. Daktari akatoka nikanyanyuka kwa haraka.
"Vipi daktari hali ya mgonjwa?".
"Una uhusiano gani na mgonjwa?"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikawa nashindwa kujielezea swala ambalo likamfanya daktari atie shaka juu yangu, lakini nikaamua kumwambia kila kitu kilichotokea, daktari akanielewa, akasema nisijali mgonjwa yupo katika mikono salama ivyo naweza kuendelea na shughuli zangu, basi nikaridhika kwa maneno ya daktari nikaondoka kurejea nyumbani, mawazo tele yalinijaa nikawaza ntapeleka nini nyumbani wakati mfukoni sina hata senti. Wakati nikiendelea kufikilia hayo nikakumbuka kuwa nina pochi ya yule mama yenye pesa na vitambulisho vyake muhimu, moyo ukanienda mbio nikafungua begi langu kuhakikisha kuwa vitu vyote vipo sawa, nikajiridhisha na kuendelea na safari, wakati nikiendelea kupiga hatua ndefu nikasimama kwenye mgahawa mmoja baada ya kuona watu kadhaa wamesimama, nikajisogeza vizuri kutazama kile kinachowafanya wale watu kukusanyika pale, nikagundua ilikuwa ni taarifa ya habari za saa, taarifa kuu ilikuwa juu ya mvua kubwa ilivyoathiri shughuli za watu, kilichonishangaza zaidi ni kuripotiwa kutekwa kwa mke wa meneja wa kampuni moja ya usafirishaji, inasemekana alitekwa na vijana wawili na kisha kutelekezwa hospitali huku pochi lake likiwa na kiasi cha shilingi milioni150 pamoja na vito vya thamani likiwa limechukuliwa na vijana hao, nikaona daktari akihojiwa na kuelezea jinsi alivyompokea mgonjwa yule akanielezea na mimi jinsi nilivyo niliogopa sana begi nikaliona zito sikujua kama kuna vito vya thamani mbali na kiasi kile kikubwa cha pesa, taratibu nikaanza kuondoka huku nikitamani kurudi hospitali kujieleza lakni nilishikwa nauoga ikabidi nirudi nyumbani kwa haraka Zaidi. Nikafika sehemu moja ya wazi nikakutana na genge la wahuni, nikataka kuwakwepa lakini wakanizuia.
"Oyah dogo acha dharau, mbona usalimii" aliongea mmoja wa wahuni wale, kwa kumuangalia alikuwa amejazia mwili kiasi kwamba akisema anipige ngumi moja tu na nilivyo mwembamba hivi basi nahisi kaburi lingenihusu, nikakaa kimya huku nikishika begi langu vizuri.
"Alafu ilo begi lina nini embu tulione" muhuni mwingine akaongea huyu alikuwa na sura ngumu mno iliyojaa makovu kila sehemu, kwa kumtazama hakunipa amani ya moyo hata kidogo. Nilitamani nigeuke nikimbie lakini hali ile ya matope ingenizuia nisifike popote. Moyo ukadunda zaidi na yule muhuni mwenye sura ngumu akawa akinisogelea, akanifikia na kuanza kufungua begi lakini kabla hajafungua vizuri akasikika mmoja kati yao akisema.
"Oyah masela kisanga hiko, mambo si mambo tupoteeeni"
Wakaanza kukimbia hovyo, mimi nikabaki nimeduwaa, maaskari walokuwa wakizunguka mitaani wakanikamata na kunivika pingu huku wakifikiri mimi ni mmoja katika genge lile la wahuni.
"Wewe utatusaidia kutuambia wenzio wapo wapi". Alisema mmoja kati ya maafande wale, nikawa mpole zaidi nikajiuliza ni mkosi gani ule niliokutana nao, wakati wakinambia nikasikia taarifa iliyonishtua toka kwenye simu zao za upepo. Taarifa juu ya mama mmoja, kutekwa na kutelekezwa hospitali baada ya kunyang'anwa kila kitu zikawafikia maaskari wale, moyo ukaenda mbio Zaidi.
"Embu muache huyo aende zake tutawashughulikia siku nyingine" akaongea askari mmoja ambaye alionekana kuwa ni mkuu wa msafara ule.
Nikaachiwa na kuanza kuondoka huku mwili ukiwa unatetemeka sana, nilipofika kichochoroni tu nikaanza kutimua mbio kali sana, huku nikiamini muda wowote nitafatwa, Mungu mkubwa, nikafika nyumbani salama nikamkuta bibi akiwa amejawa na wasiwasi mno. Nikamueleza bibi kila kilichotokea na akahuzunika na kunishauri nijisalimishe kituo cha polisi kwa kuwa sikufanya tukio lolote la kiharifu, nikakubaliana na wazo la bibi.
Nikasubiri hadi kiza kilivyoingia, nikabadili mavazi na kuvaa tofauti kidogo kiasi kwamba haikuwa rahisi kwa watu walionizoea kunitambua, nikakata vichochoro kwa tahadhari kubwa mno huku nikiwa nimerishikilia begi kwa uangalifu mkubwa, nikajifikiria mara mbili mbili kwenda kituo cha polisi na mzigo wa thamani vile, moyo ukasita nikavuta simu na kupiga namba ya meneja ambaye ni mume wa yule mama aliyelazwa hospitali. Nikamuelezea ilivyokuwa akaniuliza nilipo nikamtajia akasema nimsubili hapo nisiende popote, nikakubali. Kadri dakika zilivyokatika mwili ndivyo ulivyozidi kunisisimka nikahisi hatari mbele yangu, ikabidi nipande juu ya mti uliopo pembeni kidogo na sehemu niliyotakiwa kuwepo. Baada ya dakika 5 ikafika gari aina ya Noah nyeusi, wakashuka watu walioficha nyuso zao na kuanza kuangaza huku na huko, niliogopa sana sikujua mzigo huu una thamani kubwa kiasi gani hadi watu wausake vile, waliangaza tena na tena lakini hawakuona kitu, wakati nashangaa hayo simu yangu ikaita kutazama ni namba ya yule meneja, hisia mbaya zikanijia juu yake nikakata simu na kuizima kabisa, baada ya muda wale watu wakaondoka nami nikasubili kitambo kidogo kisha nikaondoka. Wazo la kutaka kumiliki vile vtu vya thamani likanijia lakini kauli ya bibi ikanijia akilini mwangu na kubadili lile wazo, nikaamua liwalo na liwe acha niende kituo cha polisi nikashuka mtini na kuanza safari ya kituoni lakini kabla sijasogea karibu zaidi nikaliona lile gari lililokuja kunitafuta muda ule. Moyo ukadunda nikahisi pia hata pale polisi hamna usalama.
Nikasogea sehemu yenye huduma ya simu za umma, nikapiga namba ya yule meneja, nikamwambia
"Kuna watu wanafatilia simu yako na kila tunachoongea wanakisikia hivyo fanya uwezavyo tuonane na mkeo akiwepo" CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikamtajia mahali pa kukutana na muda, akakubali na kukata simu. Sikuweza kurudi nyumbani usiku huo kwa kuhofia kuwa watu walishafatilia simu yangu na kujua ninapoishi hivyo ingekuwa matatizo zaidi. Pia sikuweza kulala kwenye nyumba ya wageni kwa kuhofu kupoteza mzigo ule, ikabidi nikae macho hadi kulipokucha. Nikawahi kufika eneo la tukio saa nne kabla ya muda tuliopanga, nikaa juu kabisaa sehemu niliyoweza kuona kila kitu kilichoendelea chini. Baada ya saa 3 nikaona Noah ile ile ya jana ikifika eneo ilo na vipande vya wanaume wakishuka na kukaa kila mmoja sehemu yake, moyo ulishtuka zaidi pale nilipoona gari nyingine nyeupe ikiingia. Alikuwa ni meneja pamoja na mkewe niliweza kumtambua mkewe kwa haraka zaidi, wakakaa katika moja ya viti vilivyo hotelini pale mimi nikiwa juu nikatazama namna ya kuwafikia ikawa ngumu sana, ikabidi nimwite muhudumu mmoja wa kiume na kuomba mavazi yake akanipa nikayavaa nikachukua vifaa nakuanza kuelekea walipo walengwa wangu, nikafika nikawapa menu wakaiangalia kisha nikaangalia huko na huko na kugundua kuwa wale watu wanatutazama hivyo nikajitambulisha kwa haraka na kuwaambia mimi ndiye muhusika ila pale si mahali salama kuna watu wanawafatilia nikaahidi kuwakabidhi mzigo wao sehemu salama, wakakubali nikaondoka na kuleta vinywaji wakati nawafungulia nikawambia,
"Endeleeni kukaa hapa kwa saa moja zaidi, baada ya hapo ondokeni na mzigo wenu mtaupata"
Nikarudi ghorofani nikampa mavazi yule muhudumu nikapita upande wa pili na kuanza safari ya kwenda nyumbani kwa Meneja, nilipofika nikagonga hodi nkafunguliwa na mlinzi nikajieleza kuwa mimi ni mgeni wao hivyo nikakaribisha sebuleni kuwasubili warudi, baada ya saa moja na nusu wakawa wamefika wakiongozana na maaskari kadhaa, nikawekwa chini ya ulinzi nikiambiwa nisifanye lolote nikajikuta nikicheka sana, hadi wakashangaa na kufikiri kuwa labda naanziwa na uchizi, Nikatoa begi na kukabidhi kila kitu chao na kuwaambia
"mlizani kuwa mimi ni muharifu hata kuniwinda kama simba awindavyo swala, msifanye nijutie na kuogopa kufanya wema hata kwa wengine, mzigo wenu upo kama nilivyoukuta ila nmepunguza elfu 30 siku nliyokodi tax kumpeleka mama hospitali na mizunguko ya leo kuhakikisha mali yenu ipo salama" niliongea kwa uchungu na hasira mno, nikamgeukia yule mama na kumuuliza.
"Ulifikilia nini hadi kusingizia kuwa umetekwa na kunyang'anywa kila ulichonacho, kwanini hukusema ulishikwa na pumu na kusaidiwa kufikwa hospitalini?"
Yule mama machozi yakamtoka na kuanza kuomba radhi, akaelezea kuwa kuna watu walikuwa wakimfatilia sana, kila alipopita na wao wanamfata, akaamua apaki gari na kuanza kutembea kwa miguu huku akijichanganya kwa watu akiamini atasalimika, ghafla mvua ikanyesha kwa hiyo ile hofu ukichanganya na hali ya hewa akajikuta akibanwa mbavu na kupoteza fahamu, alipoamka alijikuta hospitali na alipotazama vitu vyake hakuwa navyo ivyo iyo ikawa sababu kuu ya kuamini kuwa alitekwa. Nilimtazama yule mama kwa hasira mno sababu ya kutokufikili kwake angesababisha mimi nipoteze maisha, nikawa sina la kuongea nikakabidhi mzigo wao na kunyanyuka kutaka kuondoka lakini yule mumewe akaniambia
"Kijana umetusaidia sana, naomba tulipe fadhila, sema chochote utakacho tutakupa".
"Batilisheni taarifa zilizotoka awali".
************************
Nikarudi nyumbani nikiwa nmechoka sana, bibi akanitazama na kunipongeza kwa kazi nzuri nikatabasamu akanisogezea ugali na mlenda, bila kusita nikaanza kuufakamia kwani nlikuwa na njaa sana, wakati naendelea kula simu ikaita kuangalia ni namba mpya moyo ukashtuka nikaanza ogopa nikahisi ni wale wale nini.
"Bila shaka naongea na Nea mdidi, uliomba udhamini wa kwenda kusoma nchini India, tiketi yako imefika naomba kesho asubuhi ufike ofisini kwetu kwa maelezo zaidi".
Moyo ulijawa na furaha kubwa mno chakula chote nikakiacha hadi bibi akashangaa nimekuaje nikajikuta nikimkumbatia kwa furaha sana, nikamueleza juu ya simu niliyoipokea bibi nae akafurahi mno.
***********************
Nilikamilisha taratibu zote zilizostahili hatimaye nami kwa mara ya kwanza nikakwea pipa. Safari ilikuwa ndefu lakini niliifurahia sana kwangu ilikuwa ni zaidi ya utalii, muda ukasogea kwa kasi hatimaye ndege ikatua katika uwanja wa ndege wa kimataifa uliopo Mumbai, taratibu nikashuka kwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza kufika ikabidi nifate abilia wenzangu ili nijue pakutokea uwanjani hapo, kila niliyemtazama hakuna alieonesha moyo ata wa kuulizwa, nikachukua begi hatimaye nikawa nje kabisa ya uwanja nikaangaza huku na huko sikuona wa kumuuliza, nikasogea hadi sehemu zilipo tax,
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Excuse me! Am new here, and am heading to Mumbai university, do you know where exactly that place is? (Samahani! Mimi ni mgeni hapa, naelekea chuo kikuu cha mumbai, je wajua kilipo?)". Kabla hajanijibu nikasikia sauti ya mdada aliye mle kwenye gari
"Dereva, nachelewa twende tafadhari" nikamwangalia mdada yule kisha nikamwambia,
"Wewe ni kiziwi?" yule dada akashusha kioo na kunipa fursa ya kumtazama vizuri, kwa kweli yule dada ni mzuri na mwenye kuvutia mno,
"Pardon!" akasema kama vile hakusikia nilichomwambia dereva.
"Youngman! This lady also going the same place, you asked for! (Kijana huyu mwanadada pia anaelekea huko unapopaulizia)"
Dereva akajibu nikamwagalia mrembo yule baada ya dereva kusema kuwa hata mdada huyo anaenda sehemu ninayoenda mimi, nikamuomba tuungane wote kwenye safari akakubali ila akanambia kwa kuwa usiku ulishaingia sina budi nilale hotelini kisha kesho mapema ndiyo niingie chuo kwa taratibu nyingne, nikakubaliana nae akanipa maelekezo, nikaenda hotelini nae akaendelea na safari yake. Kutokana na uchovu wa safari nikajikuta nikipitiwa na usingizi baada ya kufikiri mambo mawili matatu hasa kuhusu maisha mapya ambayo naenda kuyaanza katika chuo kikuu cha mumbai. Asubuhi nikaamka baada ya kifungua kinywa nikakodi tax iliyonipeleka moja kwa moja chuoni. Daah mazingira yalikuwa mazuri mno, kila mtu alikuwa bize na shughuli yake, Nikaona watu wa kila aina watanashati na warembo wakutosha, yaani ata kama ningeambiwa nichague mchumba kwa wakati ule nisingeweza, sababu kila baada ya dakika mbili nikawa nakutana na warembo zaidi ya wale niliopata kuwaona awali. Nikafanya taratibu zote nikapewa ratiba nilivyoangalia nikagundua kuwa nina kipindi baada ya nusu saa, kwakuwa nilikosa hosteli ikabidi niifadhi vitu vyangu kwa mmoja wa wanafunzi ambao kwa siku hiyo nimemzoea.
"Excuse me Sir, may i come in? (Samahani mwalimu naweza kuingia?)"
"Excuse me Sir, may i come in? (Samahani mwalimu naweza kuingia?)"
"Are you new here? (Wewe ni mgeni hapa?)".
"Yes sir, (ndiyo mwalimu)"
"Owky get in, (sawa karibu)"
"Thank you sir"
Nikaingia darasani shughuli ikawa kupata nafasi ya kukaa, nikajikuta nimesimama nisijue upande upi wa kuelekea, mwalimu akaomba umakini kidogo kisha akasema
"Jamani huyu ni mgeni na anaitaji ushirikiano wenu, nani aliye tayari kuwa mwenyeji wake?"
Kila mtu akainamisha kichwa chini kuonesha kutovutiwa na ujio wangu pale class, sikushangaa jambo lile la kubaguliwa sababu nilishajua ilo toka mwanzo,
"Inaonesha hamna ukarimu kwa mgeni, sasa nachagua mwenyewe mtu wa kuwa nae karbu" mkufunzi akasema huku akiangaza kila pande ya darasa kisha akasema tena.
"Kijana nenda kakae pale nyuma"
Nikatembea taratibu hadi sehemu niliyoelekezwa, darasa lote likazuka minong'ono sikujua ni ya nini na wala sikujiangaisha kuuliza, kipindi kikaendelea sikuelewa kitu kabisaa, kila nilivyojaribu kusikiliza kwa umakini nilitoka kapa. Kipindi likazidi kukolea, mkufunzi akaanza kuuliza maswali, mimi nikawa kimya muda wote sikuwa na la kujibu. Baada ya dakika 120 kipindi kikaisha mkufunzi akatoka darasani, ikanilazimu nisogee kwa mwanafunzi mwenzangu aliye pembeni yangu.
"Ebhana eeh! Mimi sijaambulia kitu, toka kipindi kinaanza hadi mkufunzi anatoka sijaelewa chochote, nisaidie kunielekeza ya nyuma"
"Wewe kikongwe usinizoee!" alijibbu huku akiniangalia kwa dharau sana.
Akachukua begi lake na kuondoka, nilijisikia vibaya mno, nikatoka darasani nikarudi kule niliipoacha begi kisha nikaingia mtaani kutafuta chumba cha kupanga, maisha ya India hayana tofauti sana na ya kwetu Tanzania, kuna maeneo ambayo yanafanana sana, naeza kupaita uswahilini kama ilivyo Buguruni, Vingunguti, Tandale na maeneo mengine. Wakati natoka nikakutana na jamaa fulani nilipovuta kumbukumbu nikagundua kuwa huyu jamaa nilikutana nae kipindi nafanya majaribio ya kuweza kuja huku, aliponiona nae akatabasamu
"Habari yako?" nikamsalimu.
"Safi sijui wewe!",
"Nzuri asee", CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Vipi mbona begi mkononi?",
"Daah! Kaka majanga tuu, Nimeingia leo hapa chuo, nikafanya taratbu zote, sasa nikakosa pa kukaa hivyo nikashauriwa nitafute chumba mtaani"
Nikamwelezea yule jamaa ambaye nikahisi ni kama ndugu yangu wa damu sababu wote ni watanzania na tupo katika ardhi ya watu, nikaweka tumaini kubwa kuwa ataweza kunisaidia. Jamaa ambaye hadi muda huo sikumuuliza jina na wala yeye hakuniuliza lakini tukawa kama tunafahamiana vizuri. Akanitazama kisha akasema,
"Japo tumetokea nchi moja, nasikitika kukwambia kuwa Si rahisi kwa mgeni kama wewe kuaminika hata kukodishwa chumba, ila usijali utakaa na mimi nipo na wenzangu wawili kwa iyo tutaishi pamoja".
Nikavuta pumzi ndefu na kushukuru sana sikutegemea lile, tukaongozana hadi ilipo nyumba akanikaribisha chumbani kwake, na ndio ukawa mwanzo wa maisha mapya tukatambuana majina,
"Mimi naitwa Reginald, na huyu chalii hapa anaitwa Mzovu na huyu mwingine Steve, jamani huyu ni jamaa yetu toka bongo anaitwa Nea" basi tulifurahi kutambuana ule upweke nilokuwa nao mwanzo ukanitoka nikajihisi nipo nyumbani kabisa.
Regy yeye alikuwa akisoma kozi ninayosoma mimi ila yeye alinitangulia mwaka mmoja, Mzovu yeye anasomea Information technology (IT), wakati steve akiwa amejikita kwenye computer science, katika kozi zote hizo kukawa na baadhi ya masomo ambayo wanasoma pamoja ila wote walikuwa mwaka wa pili wakati mimi ndio kwanza naanza, Ukweli nilikuwa nimechelewa sana nikawa na pengo la mwezi mzima toka wenzangu waanze kusoma.
Siku iliyofata kama kawaida nikaingia darasani nikawahi na kukaa sehemu niliyokaa jana sikumsemesha mtu baada ya kugundua kuwa wanaubaguzi baada ya muda akaja msichana mwenye asili ya kihindi, kuingia kwake darasani kulifanya watu wote wanyamaze huku baadhi ya wavulana wakitoa macho ya kumuhusudu, sikumfatilia sana nikaendelea kupitia notsi ambazo nilipewa na Regy
"Excuse me! Old man, (Samahani kikongwe)"
“Naitwa Nea na si kikongwe" Nilimjibu huku nikimtazama machoni.
"Hainiusu ninachotaka kujua kuwa nani aliyekupa ruhusa ya kukaa karibu nami" yule mdada akaongea kwa ukali na dharau ya juu, nilivyomtazama nikagundua kuwa ni yule mrembo niliyeonana nae siku ile niliyofka katka jiji la Mumbai Sikumjibu neno, nikasikia jamaa yangu aliyepembeni akanambia.
"Asee huna bahati, hamnaga anayemzingua huyo binti, mbali na kushikiria taji la miss mumbai, pia kwao wako njema kipesa"
"Wote tunalipa ada na michango mengine kwa usawa, sina haja ya kuogopa".
Wakati mzozo ukiendelea mwalimu akaingia darasani, tukakaa tayari kwa kipindi, mwalimu hakufundisha badala yake akaacha zoezi na kuamuru watu wajichague watatu watatu, kila niliyeomba kuwa nae akanikatalia, ikabidi nifanye mwenyewe zoezi lile na kukusanya.
Mambo yakachanganya nikajikuta nikishika mkia kwa kila zoezi lililotolewa, hali hiyo ikanifanya nidharilike na kukashifiwa mno. Ikabidi nimfate kila mwalimu nikajielezea na walimu wakanielewa na wakanipa dodoso ya kila somo hivyo ikawa rahisi kwangu kujua kilichofundishwa, kinachofundishwa na kitakachofundisha. Nikarudi na zile dodoso geto nikaamua nijipe siku tatu ya kutohudhulia vipindi ili nijivute, kwa msaada wa maswahiba zangu Regy, Mzovu na Steve nikajikuta nikiiva ndani ya siku hizo tatu,na kwa kuwa siku iliyofatia ilikuwa ni wikiendi nikaamua nikaze ili niwatangulie kidogo wenzangu mambo hayakuwa magumu kwani kila nilipokwama nikavutwa na maswahiba zangu. Maisha yakabadilika kwa kasi nami nikajikuta nanyanyuka kwenye matokeo hatimaye nikafanikiwa kushika nafasi ile ya kwanza.
****************************
Siku moja kukaandaliwa picnic (ziara) pale chuo, hivyo kwa kila mwanachuo ilikuwa ni nafasi ya kwenda kutembea katika moja ya vivutio ambavyo vitahitimishwa na tamasha kubwa la muziki na kutoa fursa kwa wanafunzi wote kuburudika. Maandilizi yakaanza kila mwanachuo akawa katika maandalizi yake kuhakikisha kuwa anaifurahia ziara hiyo, mambo yalikuwa tofauti kwa upande wangu na wale rafiki zangu watatu ambao wote tulikuwa tupo tupo hatuna watu.
"Oyah wazee huku kujifanya waguumu, kutatuua asee, wenzetu wanaenda kula raha sisi tutabaki kuwaangalia tuu" mzovu akawa wakwanza kuvunja ukimya jioni hiyo tukiwa katika sehemu yetu ya kusoma.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ila ni kweli! Mimi nishaanza harakati hivi karibuni tuu kitaeleweka" Steve akasema.
"Oyah Nea vipi wewe unamchakato gani maana bado siku 3 tuu?" Regy akauliza.
"Jamani eenh mimi kuna mtu moja tuu hapa chuo kama kuanzisha uhusiano naye basi huyo" nikasema na Kila mtu akanitolea jicho la shauku kutaka kujua ni nani huyo ninayemzungumzia.
"Duuh! Kumbe na wewe ni mzee wa kimyakimya, si tunafikiri upo kizembe kumbe ushafanya mazuri na unatuchora tuu hapa". Alisema Regy.
"Nifanye mazuri wapi mi naishia kumwangalia kwenye mabango na hata darasani akija kazi kunizodoa hata fursa ya kuongea nae sijapata".
"Mhm! nani huyo tuambie ikiwezekana tukufanyie mchakato umpate" Steve akaongea wengine wote wakaunga mkono kauli ya Steve, nikajikuta nacheka sana kwani ni wazi hakuna awezaye kunisaidia.
"Kiukweli namkubali sana Priyanka, tofauti na huyo sioni mwingine". Jamaa zangu wakashtuka mno nilipolitaja lile jina.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment