Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

DAR TO MUMBAI - 1

 







    IMEANDIKWA NA : NEA MAKALA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Dar To Mumbai

    Sehemu Ya Kwanza (1)

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku zote kesho uandaliwa na leo, kama ukiitumia vyema leo yako basi hautokuwa na shaka kwa kesho uliyoiandaa leo, Mapenzi ni kama upepo na mwanadamu ni tiara, mapenzi yanaweza mpeperusha mwanadamu popote yapendavyo, kama ilivyo kwa tiara kupeperushwa na upepo, mapenzi yana uezo wa kubadili na kuzima kabisa ndoto zako, nakumbuka bibi alishawahi nambia kuwa



    “Usitegemee raha au furaha pindi tu uingiapo kwenye ulimwengu wa mapenzi, na kama ukihisi umependa basi uandae moyo wako kuumizwa na katika kiwango kile kile ulichopenda ndivyo ilivyo kwa moyo wako kuumia pale bahati itakapotoka upande wako”.



    Maneno hayo yakawa yanajirudia sana akilini mwa kijana mmoja ambae ni mfungwa katika jera moja iliyopo pembezoni kabisa mwa jiji la Delhi, afya ya mfungwa huyo ilidhoofika sana, kwani ni kwa muda mrefu alikuwa amefungiwa katika chumba kisichokuwa na mwanga hata kidogo kutokana na makosa aliyoyafanya, hakuelewa usiku upi na mchana ni upi, wala hakuweza tambua ni kwa muda gani amekuwa katika chumba kile.



    Kwa mara ya kwanza mlango wa chumba alichofungiwa kijana huyo mwenye asili ya kiafrika, unafunguliwa na anatolewa nje ya chumba kile, kwa kumtazama unaeza fikiri kuwa ni kikongwe cha miaka 70 ila ni kijana mdogo ambae ata miaka 30 hajafika,

    "Kutokana na mahusiano mazuri tuliyo nayo kati ya taifa letu na ardhi ya nyumbani kwenu, tunakupunguzia adhabu kuanzia sasa utatumikia kifungo chako ukiwa katika sero ya kawaida"

    Bwana jela aliwambia yule mfungwa wa kiafrika mwenye namba 117,

    "Ranjit embu mpeleke huyu hospitali, akikisha anafanyiwa vipimo vyote na kurudishwa hapa",

    “Sawa mkuu” ,



    Bwana jera akatoa agizo kwa mmoja ya askari wake nae akatii.

    Baada ya mfungwa yule kufikishwa hospitali, daktari akaanza kumfanyia vipimo, huku akimuulza maswali kadhaa, lakini muda wote alikaa kimya asijibu lolote,



    "Mbona wewe si kiziwi wala bubu, kwanini hujibu ninavyokuuliza?"

    Daktari akaongea huku akimkazia macho mfungwa, lakini asipate ushirikiano wowote,

    "Abdulrazak Kareem, mfungwa namba 117 Kwa makosa ya kigaidi na biashara haramu, naongea na wewe!" CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Daktari ambaye pia ni askari akajikuta akiongea kwa ukali kwa kutaja jina na makosa ya mfungwa anayemfanyia vipimo, baada ya miaka mingi kupita leo akili ya mfungwa ikafunguka na hakuamini kile alichokisikia toka kwa daktari, akalishangaa zaidi jina lile aliloitwa kwani alilifahamu kupitia vyombo vya habari akawa anajiulza zaidi imekuaje yeye kuitwa vile.



    "Abdulrazak Kareem! Kesi ya kigaidi na biashara haramu!?”

    Mfungwa alishangazwa Sana japo alikuwa akitumikia kifungo kile hakuwa akijua ni makosa yapi hasa yalomweka hatiani.

    “Kweli maisha hubadilika kama upepo, leo unaeza tokea kaskazini na kesho kusini, ndani ya ardhi hii ngeni utu na wema wangu umevikwa ngozi ya simba, kila anitazamaye anaona taswira ya uadui na hatari ninayoweza msababishia, ivyo kunishambulia pasipo kujua kuwa mimi ni kondoo niliyevikwa gamba la nyoka yule mwenye sumu kali"

    Kwa huzuni kubwa akajikuta akiyatamka maneno hayo pasipo daktari kusikia.



    Maisha ndani ya selo mpya yakawa magumu sana kwa upande wake, kutokana na upole na unyonge aliokuwa akiuonesha, wafungwa wenzake na baadhi ya maaskari jela wakawa wanamaswali mengi juu ya tuhuma alizobeba, Vitendo vya kibaguzi vikazidi kushamiri juu yake akawa hana wa kuongea nae wala wakucheka nae muda wote akawa kimya na wakati mwingine machozi yakiwa rafiki.

    "Hii ndio jela wee sokwe, usikae kimama humu utaolewa"

    alisikika mfungwa mwingine akimkamshifu Abdul, lakini Abdul akamtazama akawa hana la kumfanya akaendelea na mambo yake.



    Kengele ikalia kuashiria ni wakati wa kwenda kula, akiwa kwenye foleni ya chakula mzee mmoja ambaye kwa mtazamo alionekana kuwa amekuwapo gerezani pale kwa muda mrefu akamsogelea Abdul sehemu alipo kisha akamnong'oneza

    "ukishachukua chakula njoo meza ya mwisho kabisa nina mazungumzo na wewe"

    Abdul akaitikia na kufanya kama alivyoambiwa,

    "Naitwa Ahmed Patel, nina uraia wa Pakistani na India, huna haja ya kujitambulisha sababu habari zako hamna asiyezijua"

    Mzee Ahmed akaongea na kuzidi kumchanganya Abdul, ambaye maisha yake yote ya jela hadi siku iyo anakutana na mzee Ahmed hakufikiria kuwa anaweza kuwa maarufu kiasi kile hata kwa wafungwa waliomtangulia gerezani,

    "unahitaji nini toka kwangu?"

    Abdul akaulza, mzee Ahmed akacheka sana kisha akamjibu,

    "nipo katika gereza hili kwa zaidi ya miaka 20 sasa, mimi sihitaji msaada wowote, ila wewe ndiye muhitaji"

    Abdul akamtazama kwa makini yule mzee kisha akamuuliza tena,

    "Inaonesha unafahamu vingi kuhusu mimi"

    Kabla ajaendelea mzee Ahmed akamkatisha na kumwambia,

    "wakati walioupanga juu yako umewadia na kesho kabla jua halijazama utakuwa mwisho wako, jiandae, pambana ukiweza"

    Mzee Ahmed akanyanyuka na kumuacha Abdul akiwa bado kwenye sintofahamu.



    Usiku ukawa mrefu sana kwa Abdul kauli ya mfungwa mwenzie ikawa ikijirudia sana, akahisi usalama wake ndani ya gereza umekuwa mdogo mno, akatamani apate nafasi ili aweze kutoroka lakini akabaki kushindana na nafsi yake.

    "leo ni siku ya kwenda shamba kufanya kazi, na wafungwa nitakao wataja watahusika katika safari ya leo, Angalizo ole wake atakayethubutu kutoroka! Kitakachomkuta hatokaa akasahau katika maisha yake"

    kwa mikwara mizito bwana jela akazungumza kisha majina yakatajwa Abdul akiwa miongoni mwao, safari ikaanza huku kukiwa na ulinzi mkali mbele zikatangulia gari zikiwa na maaskari wenye silaha, kati kukawa na gari la wafungwa nyuma likisindikizwa na magari mengine ya maaskari, safari ikaendelea hadi kufka sehemu moja ya daraja gari zikapunguza mwendo mwishowe yakasimama kabisa, walipotazama kuona nini kilichosababisha magari kusimama kabla ya kufika waendapo,wakaona magogo yamepangwa kuzuia njia yaani hamna gari yeyote kupita.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maaskari kadhaa wakashuka kwenye magari yale yaliyotangulia, wakaenda kuangalia nini hasa kimetokea lakini hatua chache kabla ya kulifikia daraja milio ya risasi ikasikika hapo hapo maaskari wakaanguka chini, kundi la watu wasiojulikana wakiwa wamevalia kininja wakaanza kushambulia magari ya maaskari kwa silaha nzito, mapigano yakawa makali mno, huku hofu kubwa ikiwa imewatawala baadhi ya wafungwa waliokuwamo kwenye gari na wengine wakionesha kuishangilia ile hali wakiamini siku ya ukombozi wao imefka, Abdul akajawa na hofu akayakumbuka maneno aliyoambiwa na mzee Ahmed kuwa kabla ya jua alijazama watakuwa washatimiza walilopanga, hakuamini kuwa kifo chake kitakuwa cha namna ile, akatamani afanye namna yeyote ajiokoe lakini hakuweza fanya lolote kwa kuwa pingu zilizuia miguu na mikono yake barabara, wafungwa waliokuwa ndani ya gari wakafanikiwa kuvunja mlango na kuanza kukimbia, Abdul aliitambua hatari ya kuendelea kukaa ndani ya gari, idadi kubwa ya maaskari walipoteza maisha na wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya mno, Abdul katika kuhangaika ili atoke akaona wale watu wakilisogelea gari alilokuwepo yeye, kisha wakapeana ishara ambayo Abdul hakuielewa inamaana gani, ghafla alisikia mlipuko mkubwa ukitokea katika gari alilokuwemo, moto ukashika hewa ikawa nzito, kifua kikambana, kiza kikatawala macho yake na akaanguka.



    Nchi ikazizima juu ya tukio lile, vyombo vya habari vikawa vinaripoti moja kwa moja huku ikionesha picha ya baadhi ya wafungwa ambao inasadikika kuwa wametoroka.

    Wakati hayo yakiendelea katika moja ya kasino zilizopo jijini Delhi kukawa na kikundi cha watu ambao wanaonekana wakiwa na furaha wakinywa na kushangilia,

    "Kazi iliyokuwa ikitusumbua kwa miaka 3 sasa imekamilika, hivyo haina budi tufurahi"

    Aliongea mmoja kati ya wale waliokuwepo katika furaha hiyo huku wakigongeana cheers, Waliendelea kuburudika kwa kunywa na kucheza muziki uliokuwa ukisikika eneo hilo.



    ************************************



    Siku zikasogea, hatimaye wiki miezi nayo ikakatika, Abdul akafungua macho na kuangaza huku na huko, mazingira yalikuwa mapya sana kwake akajaribu kuvuta taswira ya kilichomkuta hakukumbuka kitu, wakati akijigeuza pale kitandani mwili haukuwa na nguvu kabisaa, akatokea msichana mmoja mrembo sana, akasogea hadi pale alipolala Abdul,

    "Wow! Dady mgonjwa ameamka!"

    Mrembo yule akatoa taarifa kwa sauti ambayo ilimfanya baba yake atoke alipotoka na kuja kutazama kile binti yake alichosema kama kina ukweli, mzee alipofika akashusha pumzi ndefu sana.

    "Binti yangu amekuwa akikuuguza kwa miezi mitano sasa, hatimaye leo umerejewa na fahamu, twamshukuru mungu kwa hilo" mzee akaongea huku akimtazama Abdul vyema.

    "Nadhani unanikumbuka, mimi ni yule bwana jela, mara ya mwisho mlivamia mkiwa njiani kuelekea shambani, tokea hapo ukawa hujitambui, tukakuchukua na kukupeleka hospitali, hata hivyo hakukuwa salama kwako hivyo kitengo cha siri kabisa kimeamua kikulete huku. Utakapopona utatueleza kwa nini wenzio walitaka kukuangamiza au kuna jambo ambalo unalo na hujalisema bado..!"



    Mzee yule ambaye ni bwana jela akajikuta anamuulza maswali Abdul, ambaye ndiye kwanza ameamka toka usingizi mzito, lakini binti yake akamzuia na kumsihi baba amuache mgonjwa apumzike wakati ukifika ataongea yote, mzee anakubali na kutoka chumbani lakini kabla ajatoka kabisa akageuka na kumwambia binti yake

    "Pooja! take care (Pooja! Kuwa makini)"

    "Okey dady! Love you, (Sawa baba! Nakupenda)"

    Abdul akapata nafasi ya kulisikia jina la mtu aliyekuwa anamsaidia kwa mara ya kwanza, akamtazama vizuri na akagundua kuwa yule mdada ni mrembo kuliko neno lenyewe mrembo. Roho yake ikasuuzika kwani kwa zaidi ya miaka minne hakuwahi kusikia sauti wala kuwa karibu kabisa na msichana yeyote, ukizingatia dunia inamuona kuwa gaidi na muuaji asiyefaa kwa lolote.

    "Asante sana Pooja, sikuwahi kufikiria kuwa kuna watu wachache wenye utu katika dunia hii, kukutana na ninyi naona ni kama bahati ya mtende kuota jangwani” Abdul akaongea huku akionesha kushukuru zaidi kwa kile alichotendewa na mwanadada Pooja sambamba na baba yake.

    "Abdul usijali......!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pooja alivyotamka lile jina Abdul akabadilika machozi yakamtiririka swala ambalo likamshtua sana Pooja na kutaka kujua kulikoni,

    "jina langu ni Nea, naomba usiniite kwa jina la Abdul tafadhari”.

    Pooja alishtuka mno akawaza itakuaje mtu anayemfahamu kwa Jina la Abdulrazak Kareem leo analikataa ilo jina na kutaka kuitwa Nea.

    "Kwani Abdulrazak si jina lako halisi?" aliuliza Pooja.

    “Abdulrazak hana tofauti na simba mwenye njaa kali, tena aliye mawindoni, chochote kitakachotokea mbele yake ni halali kwake, bila kujali kuwa kinamanufaa au la".

    "Una maana gani kusema hivyo?".

    "Jina huakisi uasilia wa maisha ya kitu, kadri siku zitakavyosogea utajua nini nakimaanisha leo" alisema Nea na Pooja akaridhia japo kwa shingo upande.



    ************************************



    Siku zikaenda kwa kasi mno huku Afya ya Nea ikizidi kuimarika maradufu, ukaribu kati yake na Pooja nao ukaongezeka naweza kusema kwa asilimia karibu 90, Pooja hakuamini kuwa kijana yule ni mtu hatari, ingawa baba yake alishamuonya mara kadhaa juu ya kijana huyo. Pooja akajikuta akimpenda Nea ambaye hakuonekana kuwa na mawazo yoyote ya kimapenzi juu ya mrembo huyo, alimueshimu na kumchukulia kama dada yake japo kulikua na utofauti wa utaifa Nea ni Mtanzania na Pooja ni muhindi.



    Usiku wakati wakiwa mezani wakila chakula cha jioni, Nea akagundua kitu tofauti kwa Pooja kila alipomtazama akaogopa sana, hakutamani kabisaa mrembo yule kujenga hisia za kimapenzi kwake. Wakati wakiendelea kupata chakula simu ikaita, Pooja akanyanyuka na kuipokea, akaongea kwa sekunde kadhaa kisha akarejea mezani huku akiwa na furaha mno, Nea akaigundua furaha ile ya Pooja akamuuliza.

    "Nini kimekufurahisha?"

    "harudi leo",

    ”Nani?”

    "Dady..!"

    Nea akamshangaa sana, Pooja kwa nini hafuraishwe na kutokurudi kwa baba yake siku iyo,

    "Nahisi leo nitatimiza haja ya moyo wangu" kwa macho malegevu zaidi Pooja anamwambia Nea, amabaye tayari alishaelewa nini Pooja anakihitaji toka kwake.

    "Usiku mwema Pooja, naenda kulala"

    Nea akamuaga Pooja na kwenda chumbani kwake, Pooja hakukubali akamfata, bila hodi akaingia chumbani kwa Nea,

    "What do you want from me? (Unahitaji nini toka kwangu?)" Nea akauliza huku akionesha kuchukizwa na kitendo kile cha pooja.

    "Don’t be mad Nea..!(Usichukie!)"huku akivuta hatua zake hadi kitandani alipokaa.

    "Nea..! Hum Tumse Pyar Hai (Nakupenda Nea)" alisema Pooja na kumfanya Nea kushtuka zaidi.

    "Pooja mapenzi hayana nafasi katika maisha yangu, isitoshe mimi ni mfungwa tu”.

    Nea akamjibu Pooja lakini mwanadada yule alishaanza kumuweka Nea katika wakati mgumu kwa kujaribu kumtomasa tomasa.

    "Naomba nipe hifadhi ndani ya moyo wako, unifikilie mimi katika fahamu zako, niote walau kidogo nipende na unifanye niwe wako," alisema Pooja huku tayari lipsi zake zikiwa zimeungana na za Nea.

    Kwa kiasi kikubwa Pooja aliamini kuwa amefanikiwa kutimiza haja ya moyo wake, lakini kabla hawajafika popote Nea akahisi maumivu ya tumbo, hali ya kuugulia ikamshtua Pooja na kusitisha alichotaka kukifanya, Nea aliugulia na kuanza kugalagala kwa maumivu.

    "Po-o-ja tu-mbo, linauma sana"



    Pooja akaanza kuchanganyikiwa mtu aliyekuwa mzima muda mfupi uliopita sasa anadai kuwa na maumivu ya tumbo.

    "Nea imekuaje?”

    "Hata sijui ila linauma sana, tafadhali naomba nitafutie dawa naweza kufa hapa”.

    Pooja hakuwa na maswali Zaidi akatoka kwa haraka kwenda kumletea Dawa. Baada ya muda mfupi akarejea na kumkuta Nea akiwa amejilaza sakafuni.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nea dawa hizi amka umeze"

    Nea akusema kitu zaidi ya kutoa machozi,

    "Jamani linauma sana kwani, jikaze wewe mtoto wa kiume, meza hizi litapoa"

    "Samahani sana Pooja"

    “Samahani ya nini?"

    "Siumwi na tumbo, niko mzima kabisaa"



    Pooja alichukia mno aliposikia kauli ile akampiga kofi Nea, hasira zikampanda akamsogelea na kumwongeza makofi mengine, kisha akatoka chumbani mule kwa hasira. Nea akanyanyua mikono juu kwani ni wazi bila kufanya drama ile angejikuta amefanya kosa jingine, ambalo lingeweza kugharimu zaidi maisha yake, ukizingatia yeye bado ni mfungwa na yule binti ni mtoto wa bwana jela.



    Asubuhi na mapema kama kawaida yake Nea aliamka na kuanza kufanya mazoezi ya kuuweka sawa mwili wake lakini alihisi tofauti siku hiyo kwani Pooja hakuwa sehemu hiyo ya mazoezi kama alivyozoea, akajua labda tuu ni hasira za kilichotokea jana. Akafanya mazoezi kisha akaingia bafuni, baadae akakuta kifungua kinywa kipo mezani hivyo akajongea na kula lakini Aligundua kuwa amemkosea sana Pooja, ila kuingia kwenye mapenzi tena kwake lilikuwa swala gumu sana. Akamtafuta Pooja lakini hakumuona akatoka na kukaa nje, kwenye moja ya bustani zilizopo kwenye eneo hilo. Akazama katika dimbwi la mawazo akitafakari zaidi juu ya hatima yake katika nchi hiyo ya kigeni, lakini akashtushwa baada ya kuhisi kushikwa bega alipogeuka akakuta ni pooja akiwa ameshika kisu, ujio ule wa Pooja haukuonesha kuwa wa heri kabisa.



    “Nea..! Nataka uniambie unanipenda au hunipendi"

    Nea akamtazama Vizuri Pooja akashindwa kusema lolote, Pooja hakujichelewesha akajichoma kisu kwenye mapaja yake, Nea alishtuka mno.

    "Nea umeuiba moyo wangu, kila nifanyalo ni kwa ajili yako ila sawa, isiwe tabu najua hunipendi na wala sikulazimishi unipende acha iwe hivi"



    Pooja akajichoma kisu cha tumbo, Nea alikurupuka aliposimama na kukishika kile kisu kuzuia Pooja asiendelee kujichoma, wakati hayo yakiendelea gari la polisi likaingia, kutazama akawa ni baba yake Pooja, mzee alipotupa jicho hakuamini kile alichokishuhudia mtoto wake wapekee Poooja.

    Nea aliilaumu sana nafsi yake, alijua kuwa Pooja anampenda lakini kutokana na moyo wake kuwa mgumu hakutaka kumsikiliza mrembo yule, hali ya Pooja ikawa mbaya zaidi.



    "Mkamateni...! Ranjit ita ambulance"

    Baba ake Pooja alitoa amri kwa maaskari aliye ongozana nao, akili ikamruka kabisa hakuamini, Nea anaeza mfanyia kitendo cha kikatili vile.

    "Kweli jasiri haachi asili, wema wote tuliokutendea leo unadiriki kumuua binti yangu, sitokuacha mzima naapa"

    Baba Pooja alifoka na kuamuru askari wampe kipigo kitakatifu Nea, maskini hakupewa nafasi ya kujitetea kila akijaribu kuongea alichoambulia ni kipigo tuu.

    "Muingizeni kwenye gari, Mpelekeni sehemu yetu ya kazi" Baba Pooja akatoa agizo jingine na askari wake wakatii.

    Pooja hakawa ajitambui kabisa kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kujishambulia kwa kisu, Baba yake akawa analia kama mtoto huku akimlaani sana Nea.

    "Nisamehe mwanangu, najua sikufanya sahihi kukuacha na gaidi yule nakuhakikishia nitalipa kwa hiki alichokufanyia".

    Baba Pooja akaongea huku machozi yakimtoka akiamini kuwa Nea ndiye aliyekusudia kumuua binti yake. Hakujua kuwa binti yake aliamua kujiangamiza mwenyewe baada ya kuona hana nafasi kwa Nea. Kipigo na maneno ya maudhi yaliendelea kumiminika kwa Nea.



    "Wewe mwanaharamu, omba tu yule binti awe mzima, asipoamka basi jua maisha yako nawe ndiyo yamefikia mwisho"

    Walimpiga mno hadi akapoteza fahamu, Wakamwagia maji ya baridi na kumuacha. Baada ya muda kupita, Nea akazinduka, mwili ukawa unamuuma sana, akanyanyua kichwa chake na kuitazama mbingu machozi yakamtoka kisha akasema,

    "Eeh! Mungu najua mimi ni mwenye dhambi na ninastahili adhabu, lakini tafadhali naomba unusuru maisha Pooja" CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kabla ajaendelea zaidi na sala, akasikia wale maaskari wakija tena kwa kasi, huku wakiongea.

    "Yaani huyu dogo leo atakiona cha mtema kuni, bora Pooja angekuwa mzima labda mkuu angefikiria kumpunguzia adhabu lakini ndio hivyo tena Pooja amefariki basi hamna jinsi nae lazima alambe mchanga"



    Walizungumza wale maaskari Nea aliposikia akahisi kuishiwa na nguvu machozi yakamtoka akalia kwa uchungu mno, akatamani ardhi ipasuke ajitumbukize humo, lakini haikuwa hivyo.

    "Embu tuondolee usanii wako hapa, nahisi sasa umefurahi, kusudio lako limetimia na Pooja amefariki"

    Maaskari wakaongea huku wakimpiga vibao vya usoni, wakamfungua na kumpakia kwenye gari kisha wakatokomea nae sehemu isiyojulikana, muda wote wa safari Nea alikua amefungwa kitambaa usoni hakuona wapi anaelekea.Baada ya muda gari likasimama akashushwa kwenye gari akakokotwa hadi mahala flani kisha wakamfungua kitambaa, alishangaa kujikuta katikati ya nyika, mbele yake kukiwa na watu asiowafahamu, akatokea baba yake Pooja na kumwambia,

    "Ningekusamehe yote, lakini swala la kumuua binti yangu sitokuacha ukipumua, wakati wako sasa unaweza kukimbia ukiweza ili kujikoa"



    Baba Pooja akasema kwa hasira mno kisha akaanza kuhesabu

    "1....2.....3....shoot"

    Nea akanyanyuka alipokaa pale chini na kuanza kutimua mbio lakini hakufika mbali risasi zisizo na idadi zikaushambulia mwili wake.

    Akahisi mwili umekufa ganzi, taratibu akaanguka chini na papo hapo akaamka kutoka usingizini. Asee kumbe ni ndoto ambaye Nea ameiota baada ya Usiku ule kukosana na Pooja, mapigo ya moyo yakaenda kasi mno, akaitafakari ile ndoto vizuri asipate jibu inamaana gani.



    "Itabidi nimwambie ukweli Pooja kwanini sitaki kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi, kama sitofanya hivi mapema haya niliyoota yanaweza tokea"

    Nea akajisemea mwenyewe kisha akatoka hadi sebuleni akamkuta Pooja mezani.

    "Namastey, (habari yako)".

    "Namaskar (Nzuri)," Pooja akaitikia kisha akainuka na kuondoka.

    "Pooja!"

    "Sema"

    "Am sorry for what happened last night (samahani kwa kilichotokea usiku)".

    "Never mention, i deserve it (usijali, nilistahili)" akaendelea na safari yake. Nea akafikiri zaidi akainuka na kumfata hadi chumbani kwake.

    "Nikusaidie nini?"

    "i have something to tell you (kuna kitu nataka nikwambie)"

    "What is it?, (kitu gani)"

    "It’s about me (ni kuhusu mimi)"

    “Najua kila kitu kuhusu wewe"

    "Kwa hiyo unajua kuwa mimi....".

    "Yeah, najua kuwa wewe ni Abdulrazak Kareem, mfungwa namba 117 kwa makosa ya kigaidi na biashara haramu," Pooja akasema kwa hasira mno.

    "Haven’t you seen the good side of me? (je ujaona wema wangu?)"

    "No! (Sijaona)"

    Nea hakuendelea tena kuongea akageuka na kuvuta hatua ndefu kuelekea nje ya chumba kile cha Pooja, alikata tamaa kabisaa kwani tukio moja tuu lilibadili kabisa muonekane wake hata Pooja sasa akaamini kuwa yeye ni Abdulrazak Kareem ila anajifanya kujiita Nea kupoteza lengo.

    "Moyo wa gaidi ni sawa na chuma, ambacho huweza kusababisha maumivu kwa kitu chochote lakini chenyewe kisiumie, Nea ujui ni kiasi gani nateseka juu yako"

    Maneno yale yakawa yakijirudia kichwani mwake, alihisi Pooja kuujua ukweli kungemsaidia sana lakini haikuwa kama alivyotegemea kwani Pooja alikataa kata kata kumsikiliza. Wakati akiendelea kuwaza akasikia kelele za kuomba msaada, akafatilia zilipokuwa zinatokea akagundua kuwa ni Pooja. Akatafuta huku na huko akamkuta Pooja ameanguka chini, akamsogelea na kumuuliza



    "Nini kimekukuta?",

    "Haikuhusu niache!" Pooja akajibu, Nea ikabidi acheke kwanza,

    "Sasa wewe umeteua mguu huwezi tembea bila msaada wangu",

    "Nimekwambia sitaki niache bora nikae hapa kuliko kusaidiwa na gaidi kama wewe" Pooja akajibu kwa kumdhiaki Nea. CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sawa kama uhitaji msaada wangu mimi naenda," Nea akaanza kuondoka.

    "No! Usiniache hapa mwenyewe tafadhali!!"

    Nea akageuka na kucheka kisha akasogea hadi alipo Pooja na kumbeba mikononi mwake, Wakati wanatembea Pooja hakutoa macho yake usoni mwa Nea, akaendelea kumtazama hadi alipomfikisha ndani na kumuweka kitandani, Nea akachukua dawa na kumchua Pooja.

    "Nea..!" Pooja akaita na Nea akanyanyua shingo na kumtazama mrembo huyo.

    "Am sorry for everything (samahani kwa yote niliyokufanyia)". Pooja akamtaka radhi Nea kwa maneno aliyomtolea, lakini jamaa akatabasamu na kumwambia asijali ni vitu vya kawaida, Maelewano baina yao yakarudi upya.

    "Nea japo huna ruhusa ya kutoka nakutembea kama raia wengine, naomba mwishoni mwa wiki hii nibebe dhamana na kwenda nawe mahali flani hivi!" Pooja akamwambia Nea ambaye hakutegemea hata siku moja kama itatokea nafasi ya yeye kutoka, ukizingatia eneo lote lile lilikuwa na ulinzi mkali masaa 24, akaitika kwa kichwa kuonesha kukubaliana na Pooja.



    **************************



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog