Simulizi : Dar To Mumbai
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mhm Priyanka huyu miss mumbai au mwingine?" Mzovu akauliza.
"Duuh! Kama ni yule kweli huna bahati" kabla sijajibu Steve akadakia.
"Ni huyo huyo, mrembo wa mumbai"
Kila mmoja akaishiwa na nguvu na kujilaza sehemu yake kusikia nimesema kuwa namuhitaji Priyanka ambaye ni msichana wa kwanza kumuona nilivyotua tu Mumbai, kutokana na umaarufu wa binti huyo, uwezo wake wa kifedha hamna aliyeamini wala kunisapoti katika harakati zangu.
"Nea, Priyanka ni kama nyota za angani kwa sasa, utaishia kuzingalia jinsi zinavyong'aa na kupendeza lakini usiwe na uwezo wa kuzikarbia na kuzigusa hata kwa dakika moja".
Regy ambaye ndiye aliyenipokea na kukubali kuishi nae, akanipa maneno yale ni wazi kabisa swala la kumpata Priyanka lilikuwa kama ndoto za mchana na wala hamna katika kundi letu aliyetaka nijiweke hatarini kwa kulisaka penzi la binti yule.
"Mnaweza endelea na harakati zenu, lakini kama nilivyokwisha sema awali tofauti na Priyanka sitoweza ruhusu moyo wangu kuwa kwa msichana yeyote yule" nikasema kwa msisitizo na rafiki zangu wakacheka na kunitakia kila la heri japo waliamini kitu nikitakacho hakitawezekana.
Siku iliyofata nikaamua niingie zangu town kucheki nguo kidogo maana toka niingie Mumbai sijawahi kununua nguo, nikaingia kwenye maduka makubwa ila nikashindwa tu bei zake nikajikuta nikitoka na kuongea na mlinzi
"Namastey (habari)"
"Namaskar (Nzuri)",
"Samahani, naona salio langu halitoshi kununua chochote hapa, Je unaeza kunielekeza sehemu yeyote yenye nguo za bei nafuu!"
Wakati naongea vile na mlinzi nikasikia sauti ambayo kiukweli ilinikaaa akilini mwangu. Nikajikuta naishindwa kuendelea kuuliza, nikageuka kumtazama nikakuta yupo na mwanaume wakiwa wameshikana mikono, nikajishangaa kuona naumizwa na ukaribu wao, akaniangalia kisha akaendelea na shughuli zake, mlinzi akanielekeza, nami pasipo kupoteza muda nikaelekea nilipoelekezwa.
************************
"Wewe kwangu ni pumzi, furaha na dunia, ninapokuwa mbali nawewe nahisi kuchanganyikiwa, eeh binti mwenye uzuri wa malaika, sikiliza kilio changu. Asubuhi Njema. ~ by X".
Priyanka anakutana na ujumbe ule katika kabati lake, akausoma na kuangaza huku na huko asimuone aliyeuleta, anapogeuza nyuma anaona umeandikwa Canteen 13.30, anaangaza tena lakini asione mtu anaingia darasani na kuendelea na vipindi.
Baada ya vipindi vya asubuhi Priyanka akiwa na wenzake akaelekea canteen kwa ajili ya kupata chakula cha mchana kama ilivyokawaida ndoto za wanaume wengi ni kupata nafasi walau ya kuongea machache na mlimbwende yule, kitendo cha yeye kufika canteen na kuagiza chakula tayari baadhi ya wanaume watanashati wa chuo wakafika kila mtu akionesha mikogo yake mbele ya mrembo huyo wa Mumbai, Chakula kikaletwa kikiwa na ujumbe.
"Napenda kila kitu toka kwako, jinsi uongeavyo na namna unavyotabasamu kwa hakika unanichizisha~ by X" akapogeuza ujumbe ule na akakutana na maneno mengine "home garden 21.00" akagutuka na kuangalia saa yake akagundua ni saa 13.33 kwa hiyo ujumbe ulikuja sawa na muda elekezi wa asubuhi. Akutaka kuongea kitu wakati anaendelea kula nami nikaona ngoja nikapate msosi lakini kila nilipoangaza meza zote zikawa zimejaa ni meza ya Priyanka pekee ndiyo haikuwa imejaa, nikaagiza chakula kisha nikasogea na kukaa, nikasalimia hamna aliyeitikia nami nikajifanya chizi tuu, chakula kikaja nami nikaanza kula.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hivi wewe kikongwe kwanini unapenda kunifatafata"
"Nikufate wewe nyuki?"
"Nyuki? Unamaana gani kusema hivyo?" Priyanka akaamaki kidogo.
"Kuna msemo unaosema fata nyuki ule asali, kwa hiyo ndiyo nimeuliza wewe nyuki?”.
"Mhmh! laiti ungejua unavyonitia kichefu chefu usingenikaribia hata kwa sentimita chache!"
"Na laiti ungejua ulivyo mbaya usingekuwa na maringo hivyo!"
Nikamjibu huku nikicheka na kumkata jicho la wizi nione atakuwa vipi. Daah! Kama maneno yangekuwa yanarudi baada ya kuongea basi ningeyarudisha maana kilichotokea baada ya hapo ni hatari mno. Nikaona sura ya mrembo yule ikibadilika kwa hasira mno, haikutokea hata siku moja kuambiwa maneno kama yale niliyomwambia mimi, akanikazia macho nami nikaendelea kula msosi dakika 3 nyingi, vikaja vidume mbavu kweli nikabebwa juu juu nisijue wapi ninapopelekwa, Nilipokuja kukaa sawa nikajikuta katikati ya njemba hizo,
"Kwani kuna nini mbona sielewi?" nikauliza lakini hamna aliyenijibu, nikanyanyuka nikajikuta narudi chini kwa baada ya kupigwa kofi zito.
"Sikia wewe mwanaharamu, nampenda sana Priyanka na hamna aliyewahi kumdhalilisha kama ulivyofanya wewe, nakuonya usirudie tena, iwe mwanzo na mwisho"
Akasema jamaa mmoja hivi kwa kumuangalia ni mtanashati tena mwenye kwenda na wakati, nikajiangalia mimi nikamwangalia tena yule jamaa nikajikuta najicheka kimoyo moyo, nikawa mpole zaidi, kisha wale jamaa wakaniruhusu niende nami bila kuchelewa nikasepa kwa haraka zaidi.
Siku ilikuwa ngumu sana kwa Priyanka kila akifikilia maneno niliyomwambia mchana moyo wake ulimuuma mno, basi kwakuwa alikuwa akiishi na rafiki zake akatoka hadi sehemu ilipo bustani akakaa kwenye moja ya bembea zilizopo sehemu hiyo wakati akiwa bado katika dimbwi la mawazo akaona bahasha inapepea na upepo akaifata na kuifungua
"Wewe ni mzuri zaidi ya neno uzuri, unavutia nyakati zote ukicheka na hata ukilia, chozi lako ni la thamani sana kwanini uliangushe kwa mtu asiyejua thamani ya chozi ilo" . Usiku mwema malkia wa moyo wangu ~ by X” ujumbe ule ulimfanya miss Priyanka atabasamu walau kusahau yaliyotokea mchana.
*****************************
Kufika chumbani nikakuta rafiki zangu wamekaa roho juu wakashangaa kuniona nimechakazwa kidogo kwa kipigo kile nilichopata, ikabidi niwasimulie kila kitu, wakanicheka mno lakini mwisho wa siku kila mmoja akanambia nizime ndoto za kuwa na Priyanka la sivyo nitarudi maiti wakati mwingine.
"Ebhna eenh ziara imepelekwa mbele, mpaka tumalize mitihani" Mzovu akaongea.
"Kwa hiyo baada ya wiki mbili ndio safari ila ni sawa walivyofanya hivi maana hadi dakika hii kila mrembo ninaye mwingia wamoto!" alisema Steve.
"Mwenzenu mimi ukapela nauacha” Regy akaongea na kuteka akili zetu,
"Mhm kaka ushapata koloni nini?" nikauliza.
"Ndio! Unakumbuka siku ile pale mgahawani kuna mrembo nilikuwa naongea nae".
"Aah! Yule cheupe! Dimpozi aaaah namjua!" nikajibu.
“Sasa yule ndiyo shemeji yenu”, basi ikawa burudani nikasahau maumivu niliyopata kutokana na kichapo cha wale jamaa.
**********************
Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo Priyanka alivyozidi kupenda jumbe za mr.X. Kila siku akawa akipokea jumbe zile zenye msisimko wa aina yake, akajikuta taratibu akianza kumpenda mr.X. kazi ikawa kumtambua huyo mr.X ni nani..?
Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo Priyanka alivyozidi kupenda jumbe za mr.X. Kila siku akawa akipokea jumbe zile zenye msisimko wa aina yake, akajikuta taratibu akianza kumpenda mr.X. kazi ikawa kumtambua huyo mr.X ni nani, ikabidi awashirikishe rafiki zake kuhusu hilo kila mmoja akawa anashangaa na wote wakajikuta wakitamani kumjua uyo mr.X, ikiwa ana ujumbe mzuri vile jee vipi kuhusu muonekano wake, kila mmoja akajaribu kuvuta picha juu ya huyo mtu anayejiita mr. X. Siku moja Priyanka akaamua aache ujumbe kwa mr.X, endapo ataleta ujumbe wake basi akutane na ujumbe kuwa anahitaji sana kuonana naye.
Siku na muda alioupanga Priyanka kuonana na mr.X ikawa imefika, nami katika siku hiyo hiyo nikaona bora nitamfute mrembo huyo walau niombe radhi kwa kilichotokea, katika pita pita zangu nikaona amekaa sehemu ya peke yake hakuwa na rafiki wala mtu yeyote yule, nikaona hiyo ndiyo nafasi yangu ya kuondoa kinyongo chake kwangu, nikasogea hadi alipokaa alivyoniona akashtuka mno, mimi sikuwa nafahamu chochote juu ya mpango wake basi bila kupoteza muda nikamsalimu na kwenda moja kwa moja kwenye lengo la kufika pale, nikaona anavuta pumzi ndefu kisha akanijibu
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Naomba usiniharibie siku, kuna mtu muhimu sana namsubili hapa, hivyo tafadhali naomba uende!".
Nikastaajabu kidogo kwani muda aliotumia kunieleza hayo yote ungetosha kwa yeye kuniambia kuwa kama tofauti zimeisha au la,
"Sawa nitaondoka lakini ujanijibu kama umenisamehe au la?" kabla sijamalizia sentesi yangu nikajikuta namwagiwa sharubati na yule mdada, ukweli nilichukia mno.
"Iwe mwanzo na mwisho kunifatilia, popote utakaponiona fanya kama hunijui" nikatamani nimzibue kofi ila nikajiona mjinga sana kuomba radhi, ikabidi niwe mnyonge Zaidi na nikaondoka eneo lile.
"Kama ilivyo kwa mwenye kiu kuitaji maji au mwenye njaa kuitaji chakula kushibisha tumbo lake, ndivyo ilivyo kwangu mimi kuhitaji kukuona kuiridhisha nafsi yangu, lakini nasikitika muda ulipowadia nilifika eneo la tukio, lakini nilipotaka kusogea nikakuta unaongea na mwanaume mwengine, nafsi ilikaangika sana, sikua na jinsi zaidi ya kurudi nlipotoka kwa unyonge zaidi ~ X".
Priyanka akajikuta machozi yakimlenga kukosa kuonana na mr. X kwa sababu yangu, chuki ikaongezeka mara dufu juu yangu, popote tulipokutana lazima anianzishie balaa ikafika kipindi ikabidi nimkwepe ukweli sikuwa na uwezo wa kushindana naye kivyovyote ingawa yeye ni wakike namimi ni wakiume. Nikajiapiza kuwa lazima siku moja atakuwa wangu.
Baada ya kumaliza mitihani siku ya picnic ikawadia huku rafiki zangu wakiwa tayari washapata wasichana wa kuwa nao, kila mmoja na kampani wake, tukapaki vitu kwenye mabegi tayari kwa safari, njiani ilikuwa burudani sana ucheshi wa hapa na pale ulifanya safari yetu kuchangamka. Tukafika mahali gari moja ikapata tatizo hivyo ikabidi waliokuwa kwenye lile gari wahamishiwe kwenye magari mengine, nikasikia nikiitwa jina langu na kuambiwa nipande gari jingine nikagoma sababu siwezi kuacha marafiki zangu. tukaamishiwa wote kwenye gari nyingine ilikuwa bahati kwa rafiki zangu sababu tulipopelekwa ndimo walimo wale warembo wao jamaa walifurahi mno, kwa upande wangu ilikuwa kama balaa tuu maana baada ya kupanda, nikashuudia Priyanka nae akipanda kwenye gari ilo ilo tena sehemu niliyokaa naye akaja kukaa hapo hapo.
Hatukusemeshana wala kusalimia ilikuwa kama filamu vile huku rafiki zangu wakishangilia yaani ilimradi tuu fujo safari ilinoga kwao kwangu ilikuwa kama mzigo. Uvumilivu ukanishinda ikabidi nivunje ukimya
"Excuse me miss....! (Samahani bibiye)"
"What do you want? (Unataka nini?)",
"Kwanini unanichukia?" nikauliza.
Akanisonya kisha akaendelea na mambo yake, wakati tukio lile linaendelea rafiki zangu wakawa wameona basi wakanicheka mno hadi nikakereeka, nikatoka ile sehemu ambayo nilikaa na yule mrembo na kwenda kukaa nyuma kabisa ya gari. Safari ikazidi kukolea tukafika sehemu moja yenye muinuko mkali, gari ikazima na kushindwa kupanda, wakati huo magari ya wenzetu yalishatangulia hivyo ikabidi tushuke na kuanza kutembea kwa mguu sababu hapakuwa mbali sana na eneo la tukio. Njiani stori zikaendelea huku tukikatisha vijipori vidogo vidogo hatimaye tukatokea kwenye daraja kubwa sana na refu kwenda chini, wengi wakashindwa kuvuka hasa hasa wasichana maana ukiangalia chini unahisi kizunguzungu. Mimi nikawa wa mwisho kabisaa nikiangalia watu wanavyohaha kuvuka, ikabidi kila mtu abebe msalaba wake walio wapenzi ikabidi washikane mikono ili wavuke.
Miss Priyanka akawa muoga zaidi kuvuka akajikuta wenzake wakimpita na kubaki mwenyewe, basi nilipokaribia ikabidi aniombe msaada nikamuangalia kisha nikacheka kimoyomoyo, nikamwambia afunge macho naye akatii nikamnyanyua kwa mikono yangu na kuanza kuvuka naye, akaning'ang'ania kama ruba kuhofu labda naweza kumuangusha, nikamfikisha salama upande wa pili kisha nikamwambia shuka akagoma, nikamwambia afungue macho akajikuta yupo upande wa pili akashuka nikamkabidhi begi lake na kuendelea na safari wakati wenzetu wakiwa wametutangulia kidogo, sikutaka kumsemesha chochote, nikawa kimya ikafika mahali akaniita.
"Nea...!"
Hakika mwili wote ulihisi kupigwa na shoti, kwani ni mara ya kwanza kwa mrembo yule kulitamka jina langu, nikasimama na kumtazama.
"Thank you (akhsante)" akanambia, sikumjibu kitu nikaendelea na safari, akaniita tena
"Mbona unaroho ngumu hivyo, mtu anakushukuru hata kumjibu unashindwa".
"Unataka nikujibuje!?"
"Mpumbavu wee kukushukuru usione kama nakushobokea, kwanza naweza kukuajili unibebe na nikakulipa kiasi chochote kile!" akasema Priyanka huku akiwa amekasirika.
"Sawa bosi, nahitaji malipo yangu kwa kazi niliyoifanya!" nikamjibu huku nikiwa nimekereka mno.
"How much (kiasi gani?)"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Rupia 3000, na naziitaji sasa hivi"
"Hapa sina hiko kiasi cha pesa labda tukirudi"
Nikabwaga begi chini nikamyanyua kwa hasira, nikavuka kwenye daraja kwa haraka haraka nikamwacha alipokuwa mwanzo,
"Uwa sifanyi kazi za bure, si unapesa eenh! na umaarufu juu, ita pesa zako zikubebe kwa heri" Nikamwacha nakuanza kuondoka pale kunifata akashindwa kukaa akaogopa, akajikuta machozi yakimdondoka akaniita nikageuka nikarudi kumsikiliza
"Tafadhali usiniache hapa, niko radhi kufanya lolote utakalo!"
Kauli ile ikanifanya nifikiri kwa muda kidogo, kisha nikamtazama usoni na kumwambia
"Sawa nimekubali ila kwa masharti",
"Sema lolote Nea"
"Pretend to be my girl friend for a month (tujifanye kuwa wapenzi kwa mwezi mmoja)"
"What!? Do you think am cheap (unahisi mimi ni mlaini ivyoo?!" akahamaki.
"Hapana Priyanka, wee kubali tuu".
"I can’t (siwezi)" akajibu.
"Basi tufanye tuu kwa hizi siku 5 tutakazokuwa huku alafu zikiisha basi", nikaendelea kubembeleza japo shida yake ila kwangu nilitaka kuwaonesha rafiki zangu ata niwe vipi lazima na mimi niwe na msichana mrembo Zaidi ya wote.
"Kwa hiyo unataka kutumia udhaifu huu kupata unachotaka??"
"Hapana! Yaani ni kama tunaigiza tuu ila hamna mabusu, kukumbatiana wala sex" Nikamjibu basi akaangalia juu na kufikiri kisha akasema.
"Nea nimekubali lakini uthithubutu kuvuka mipaka".
Mhmhmh! Haya makubaliano ndio hayo unafikiri nini kitafata hasa baada ya chuo kizima kuwaona wapo karibu na nini kitatokea baada ya siku hizo 5 kuisha.! Usikose sehemu ya 10 ya simulizi hii ya kusisimua itakayokujia siku ya jumatatu muda na wakati kama huu….
"Sitofanya kinyume na makubaliano",
Tukakubaliana pale kuanzia muda huo akawa wangu wa ubani, nikajihisi mshindi kwa kiwango kikubwa sana, nikafikiria jinsi nitakavyoshangaza kadamnasi ya chuo, moyo ukajawa na furaha mno japo yalikuwa mapenzi ya siku 5 sikujali sana, tukashikana mikono na kuelekea wenzetu walipo huku tukipiga stori za hapa na pale. kwakuwa Priyanka alikuwa anashikiria taji la mrembo wa Mumbai hivyo kwa namna ya pekee akapewa nafasi ya kufungua zile shamrashamra za ziara, watu wote wakawa wakimsubiria mrembo yule afike ili mambo yaanze, kila mmoja aliduwaza baada ya kuona wawili sisi tunasogea eneo lile tukiwa tumeshikana mikono, nikatupa jicho kwa rafiki zangu Mzovu, Regy na Steve nao wakawa wameduwaa wasikiamini kile wanachokishuhudia, tulipofika tukaachiana mikono yeye akaelekea eneo alilotakiwa kuwa, nami nikajisogeza kwa jamaa zangu.
"Ebhana eenh! Ushafanya mazuri nini?"
"Asee mtoto anaonekana kashakuelewa yule!"
"Mhmh Nea tuambizane tayari nini?"
Zilikuwa kauli za rafiki zangu ambao wakajikuta wakiniuliza maswali mfululizo nikawa sina la kuwajibu zaidi ya kutabasamu tuu.
Priyanka akafungua rasmi shughuli zile hivyo kila mwanafunzi akapata fursa ya kuburudika na rafiki au mpenzi wake, watu wakajigawa kimakundi makundi wakatengeneza mahema baadae burudani zikaendelea. Usiku watu wakatengeneza fire camp ivyo wanaoimba sawa, wanaocheza karata, wanaopiga stori yaani kila aina ya burudani ikawepo. Mimi na rafiki zangu tukajitenga kidogo tukachochea kuni zetu na kuanza kupiga stori mara baada ya muda mfupi kila mtu akaacha kuongea na kuduwaa nami nikageuka ili nione wanachokishangaa, nikamuona Priyanka akija tulipokaa, mapigo ya moyo yakaongeza kasi nikatamani ata nikimbie, niliogopa rafiki zangu wanaeza kushtukia mchezo nikaibika ila nikapiga moyo konde na kutulia.
"Excuse me! can i join u? (Samahani! Naweza ungana nanyi?)"
"Ofcourse yes! (bila shaka ndio)" nikamkaribisha, mwanzoni hakuwa huru na sisi ila kadri muda ulovyozidi kwenda ndivyo alivyozidi kutuzoea, baada ya muda rafiki zangu wakaniaga na kwenda kwenye mahema kupumzika nikabaki na mwanamke anayechanganya akili yangu.
"Priya..!" nikaita nae akanitazama
"Uwezi kuutambua mbalamwezi pasipo mwanga wake na kama ilivyo kwa nyuki kuitaji maua ili kutengeneza asali, ndivyo hivyo ilivyo kwa mtu mume kuitaji mtu mke kwa ajili ya upendo".
Nikasema maneno hayo huku nikimtazama usoni ghafla nikaona anaanza kubadilika na kuhema kwa kasi mno, sikujua nini kimemkuta akaniuliza.
"Wewe ni nani?" nikacheka kidogo kisha nikamshika mkono akanitoa kwa nguvu akanambia
"Usinikaribie!"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kama umependa basi penda tuu mmoja, si vyema kumpenda kila mtu na kuruhusu kila mtu autawale moyo wako".
nikaona mwanadada huyo anatokwa na machozi akazidi kunishangaza nikamuuliza vipi akasema
"Mr. X"
"Mr. X amefanya nini na ni nani?"
"Nea acha nikapumzike naona sipo sawa tutaonana kesho" nikaridhia ikabidi nimsindikize hadi karibu na hema lake nje kukawa na rafiki zake ambao kiukweli hawanipendagi hata kidogo basi nikamgeuza Priyanka na kutaka kumkisi mbele ya wale rafiki zake.
Akashtuka akanipiga kibao, nikabaki kucheka
"Mhm Priya si tunaigiza ka nakukiss tuu" akasonya kisha akaondoka,
"mhm! umeanza lini kudate na yule kikongwe?" Christine mmoja kati ya rafiki zake akauliza, "that’s none of your busness (haikuhusu)" akamjibu
"lakini Priya!! Hadhi yako haikuruhusu kuwa na yule kinyago"
Christine akaendelea kuongea lakini Priyanka alishaingia ndani wala hakutaka sikiliza sababu ukweli wote anaujua yeye.
Siku iliyofatia tukaingia msituni kuangalia vivutio vilivyomo umo, kama kawaida mkataba wangu na mrembo yule ukaendelea swala ambalo lilizidi kuwa gumzo kwa wengi, vidume vyenye uwezo wao kiuchumi, vikazidi kuumiza kichwa kwanini binti yule aamue kuwa na mimi wakati wao wakijiangalia wamenizidi kila kitu,taratibu nikaanza kuliona bifu likizuka kubaguliwa kukaja juu lakini nashukuru mara zote Priyanka alikuwa upande wangu. Tukafika sehemu moja ya mto watu wakapenda waogelee basi nami kwa nafasi iyo nikakaa na mwanamke ambaye naweza kusema ni wa maisha yangu ukweli nilikuwa nafuraha sana,
"Nea kuna kitu kinanchanganya mno?” Priya akasema huku akintazama, nikamuuliza
"kitu gani iko mpenzi?"
"Nea maneno yako nahisi si mageni kwangu, naona kama nilishayazoea kuyasikia japo kwa lugha nyingine"
"Mhm! Sijakuelewa?"
"Nea je inawezekana kumpenda mtu ambaye hujawahi kumuona wala kuisikia sauti yake?", nikaangua kicheko mno kisha nkamuuliza
“Utampendaje mtu usiyejua anamuonekano gani au ata kujua tabia yake?". “Mhm! ata sijielewi yaani?"
Maongezi yale yalizidi kuninyong'onyeza, nikahisi nafasi ya kuushinda moyo wa binti yule ni ndogo kwani yaonesha tayari kuna mtu anampenda.
*****************************************
Baada ya mizunguko ya kutwa nzima jioni tukakaa wote sehemu moja mbele likaandaliwa jukwaa kila mmoja akapata nafasi ya kuonesha alichokuwa nacho, ikafika nafasi ya miss mumbai kupandwa jukwaani na kuonesha uwezo wake. Sikuamini kile nilichokisikia toka kwa binti yule, aliimba nyimbo moja ya mapenzi na yenye msisimko wa hali ya juu, ukweli nami nikashindwa jizua nikamfata huko huko jukwaani watu wakashangaa nini nataka fanya ila niliwaduwaza zaidi baada ya kuungana na Priyanka kwenye kuimba mashairi, mimi sikuwa najua ka yeye anajua kuimba pia yeye hakujua kama mimi sivumi lakini nimo, hakika ilikuwa ni bonge la shoo kwa usiku huo kwani hakuna aliyetegemea ilo kutokea. Baada ya kushuka jukwaani pongezi za hapa na pale zilikuwa za kumwaga. Nikamvuta Priyanka pembeni na kumpa pongezi zake naye bila hiyana akanirudishia pongezi zile, Christine pamoja na rafiki wengine wa Priya hawakupendezwa na hilo hata kidogo, siku hiyo hatukukaa muda mrefu tukaagana kama ilivyo kawaida nikamsindikiza kisha nikawa narudi zangu lilipo hema langu, wakati nakaribia kufika nikasikia sauti ikiniita
"Nea!”
Ikabidi nisimame na kumsubili huyo aliyeniita, sikuwa namfahamu jina ila kwa sura hakuwa mgeni machoni pangu
"Mhm samahani kaka angu naomba niulize una uhusiano gani na Priyanka?"
"Kwanini umeuliza?"
"Mhm Nea nahisi umjui vizuri Priyanka na familia yake?"
"Unamaanisha nini?"CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Baba yake Priyanka ni mfanyabiashara mkubwa tena wa kimataifa alafu mbaya zaidi Priyanka ni mchumba wa mtu na huyo mchumba wake ni mtu hatari sana" alisema huyo dada, nikakuna kichwa, zile habari zilinitisha lakini sikuwa tayari kughairi mpango wangu.
“Asante kwa taarifa, unaitwa nani?"
"Naitwa Aider!"
"Okey nice to meet you (Nafurahi kukufahamu)"
"Nice to meet you too (Nafurahi pia)" akajibu kisha akarudi alipotoka nami nikaendelea na safari yangu.
***************************************
"Mhm jamaa yangu naona unakuwa maarufu siku hizi ata muda wa kupiga stori nasi huna kabisaa” Mzovu aliongea pindi nilipofika tu sehemu walipokuwa wanaota moto.
"Hongera baba naona umekamua kinoma na shemeji jukwaani" Steve akajazia nikavuta pumzi kidogo kisha nikasema.
"Jamani eenh mimi nipo pamoja nanyi ila si mnajua nguvu ya mapenzi, ila msinitupe Priyanka ndiye mwanamke nnayempenda"
Rafiki zangu wakanitia moyo nikaingia zangu kulala, kabla sijapitiwa na usingizi nikawa nafikilia yale maneno aliyoniambia Aider nikayapuuzia nikaona hayana ishu siku zenyewe zimebaki 3 mkataba uishe.
Siku hiyo nililala kupita kawaida wenzangu wakawa wameamka na kuendelea na shughuli zao mimi bado niliendelea kuvuta shuka, nikashtushwa na kofi la mguuni nilipoangalia nikakuta ni Priyanka.
"Wee umeingiaje humu?"
"Amka bhana sitokuongezea siku sababu umechelewa mwenyewe!",
"Sasa mbona unyanyuki tuondoke!"
"Wewe ni chizi nini nitanyanyuka vipi wakati upo hapa!",
"Eenh sasa unaogopa nini si uvae, kwani mimi si ni mpenzi wako!"
"Eenh sasa unaogopa nini si uvae, kwani mimi si ni mpenzi wako!" Priyanka akaongea namimi nikajifanya chizi nikata vaa nguo mbele yake akapiga kelele.
"Weee subiri mimi natania!" akatoka nje basi nikacheka nikabadili nguo nikatoka njee nikaenda kwenye bafu la kizushi lilikuwapo eneo lile kuweka mwili safi kisha nkarudi hemani kuvaa vizuri.
"Unajua nini Priya! Mimi leo sijisikii kwenda popote yaani?"
"Twende wenzangu wananisubiri" akaendelea kuongea.
"Kweli mimi sitanii we nenda tutaonana jioni mkirudi..!" nikamuacha aende.
Ukweli siku hiyo mwili ulikuwa mzito sana sikutaka kwenda popote zaidi ya kuwa eneo ilo, nikaenda hadi jikoni siku iyo ilikuwa zamu ya rafiki zangu kuandaa msosi kwa wote ikabidi niungane nao watu wakaondoka sisi huku jikoni vituko vikaanza hamna aliyekuwa anajua kupika vyakula vya kihindi ukizingatia waliokuwa jikoni siku hiyo wote wabongo,
"Ebhna eenh sasa leo tunafanyaje kuhusu msosi?" Mzovu akauliza
"Tuwapikieni ugali na mrenda ujue kitambo kweli msosi huo" Steve akadakia.
"Wee jamaa huku amna unga wala huo mlenda zaidi ya pisholi ili na nyama hizi" Regy akasema, mimi nikaingilia kati nikawaambia.
"Niachieni usukani nifanye mazuri jikoni leo tunapika kinyumbani lazima wajilambe" kwa pamoja tukakubaliana maandalizi ya kupika yakaanza, wakati naosha nyama nikashangaa kumuona Priyanka amekuja jikoni.
"Nilikuahidi kutokuwa mbali nawe, sikueza endelea na safari wakati wee hupo huku"
Nilifurai mno na rafiki zangu wakaanza shangilia basi ikawa burudani sikujali hadhi yake nikamvika aplon na kumkaribisha jikoni.
"Nea katika maisha yangu sijawahi kupika na wala sijui".
Nikamwangalia nikamwambia usijali kwangu utajua kila kitu, mapishi yakaendelea huku utani wa hapa na pale ukitawala kwa kila aliyemuona Priyanka eneo lile hakuamini kuwa mrembo yule ataweza zifanya kazi zile, msosi ukaiva tukapack kwenye
kila kikontena cha mtu na kuvihifadhi sehemu iliyostahili.
Sisi tukatangulia kula na kuosha vyombo na ni katika wakati huo huo wanafunzi wenzetu wakawa wanarejea na wote wakapigwa na butwaa kuona miss Mumbai akifanya shughuli zile. Christine akawa wa kwanza kuja na kumchukua rafiki yake,
"Priya! Priya! Unahisi ni sahihi kwa wewe kuyafanya yote haya?)" Christine akamuuliza.
"Its my decision (ni uamuzi wangu)".CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Wewe sio bure lazima kuna kitu atakuwa amekufanyia yule kikongwe" Christine akajikuta akipokea kofi baada ya kutamka ile kauli ya kwamba mimi ni kikongwe.
"Whats wrong with you Priya!? are you slap me because of that good for nothing boy? (nini kimekukuta Priya! Yaani unanipiga kwa sababu ya yule hoe hae wako)" Christine akazidi kuhoji huku akionesha kutopendezwa na kitendo cha Priyanka.
"Christine! Acha kufatilia mambo yangu binafsi)" Priyanka akahamaki mno kwa kitendo cha kufatiliwa hadi maisha yake binafsi.
"Priya wewe ni mchumba wa mtu, na hadi sasa kuna watu wamewapiga picha na zishamfikia Rohit"
Christine akaongea huku akimuhurumia rafiki yake, Priya akaishiwa nguvu na kukaa chini aliposikia kauli ya rafikiye, akaogopa asijue nini la kufanya ikabidi amuelezee Christine kila kitu ata juu ya yale makubaliano.
"Mhm kwa hiyo leo ndiyo siku ya 3, imeisha na mmebakiza siku 2?" Christine akauliza na Priya akamjibu kwa kutingisha kichwa.
"sawa basi leo iwe mwisho kuonana nae, mengine niachie mimi". Priya akakubaliana na rafiki yake kisha akaingia kwenye hema Lake.
********************************
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment