Search This Blog

Friday, July 15, 2022

MY X GIRLFRIEND - 1

 





    IMEANDIKWA NA : HUSSEIN O. MOLITO



    *********************************************************************************



    Simulizi : My X Girlfriend

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Mungu ameujaalia mkoa huu kwa kuwa na milima kila sehemu na miti yenye majani ya rangi ya kijani kibichi. Ameupa ardhi yenye rutuba iliyoweza kuzalisha mazao mbali mbali, pia amawapa mito japokuwa kasoro yao ni moja kubwa na ndio jina livumalo hususani ukiitaja kasoro hiyo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nauzungumzia mji kasoro bahari. Si mwengine na mji wa Morogoro.



    Huko aliishi mzee kambi na mtoto wake wa pekee Aisha. Hiyo ni kutokana na kumpoteza mke wake na kuamua kuishi hivyo huku akiridhika kumlea mtoto wake huyo wa kike aliyeachwa na mama yake akiwa na umri wa miaka sita tu.



    Maisha sio mazuri kwa upande wa kipato, ila furaha ya familia hiyo ilizika mapengo yote ya umasikini walionao.



    Aisha alikua kwa kasi na kupelekwa shule na baba yake alipofikisha umri wa miaka saba.

    Kichwa cha msichana huyo kiliwafurahisha sana walimu wake kutokana na uwezo wa darasani aliokuwa nao.



    Alishika nafasi ya kwanza kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la sita ambapo aliachishwa shule na baba yake mkubwa baada ya baba yake mzazi kupooza viungo kuanzia kiunoi kushuka chini.



    Walimu na wanafunzi wenzake walisikitishwa na hatua hiyo, lakini hawakuwa na la kuamua japokuwa waliamini kuwa angemaliza darasa la saba, basi lazima angefaulu tena kwa kiwango kikubwa.



    Kazi ya kumuhudumuia baba yake aliachiwa peke yake. Hadi kuna vitu vingine kama kumsafisha pindi baba yake alipojisaidia aliifanya yeye mtoto wa kike huku ndugu zake wakiwa wanakuja kwa nadra sana kuwatembelea.



    Mzee kambi alikua analia kila siku na kumuomba mungu amchukue ili mtoto wake asipate yale mateso aliyokuwa anayapata juu yake.



    Siku moja Shani alitumwa na baba yake aende akamtafutie ndulele kwa kua alikuwa anashida nazo.



    Kwakua walikua wanaishi mbali kidogo na shamba lao, ilimchukua dakika ishirini kwenda na kurudi baadae baada ya dakika zipatazo arobaini na tano toka alipotoka pale.



    “baba…babaaaaaaaaaaaaa’



    Alilia kwa uchungu Aisha baada ya kumuona baba yake amekata roho baada ya kujichoma na kisu alichokua anakitumia kummenyea baba yake machungwa.

    Kilio kilikua zaidi na majirani walikisikia kilio kile na kukusanyika eneo la tukio. Waliungana na yule mtoto na wengine wakimpooza mazito yaliyo mkuta.



    Baada ya mazishi ya mzee Kambi, baba mkubwa wa Aisha alichukua jukumu la kumlea mtoto huyo.



    Ukurasa mpya wa mateso kutoka kwa mama yake mkubwa na baba yake huyo ulifunguliwa baada tu ya arobaini ya mzee kambi.



    Aligeuzwa mfanyakazi wa ndani kwenye nyumba ya marehemu wazazi wake, alichota maji, kufua nguo za watu wote mule ndani na kila kazi zihusiayo na ile familia basi aliifanya yeye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Maisha ya tabu,dhiki,mateso na msoto ndio uliomkuza Aisha. Ugumu wa maisha na kutafutiwa wanaume kwa ajili ya kuolewa kinguvu ndio vitu vilivyomchosha Aisha na kuamua kutoroka nyumbani kwao na kukimbilia kijiji cha pili.



    Huko alipata hifadhi na mama mmoja baada ya kumuhadithia kila kitu kilichohusu maisha yake. Kwa imani ya yule mama, alimkaribisha na kuanza kuishi naye kama mtoto wake.



    Uzuri uliofunikwa na shida miaka mingi iliyopita, ulianza kuonekana taratibu kama kijua cha asubuhi kichomozapo. Hali iliyofanya vidume vya kijiji hicho kumtolea macho.



    Alinawiri vizuri kutokana na matunzo ya yule mama ambaye alifaidika naye kutokana na yeye alivyokuwa anajituma.



    Aisha alipotimiza miaka ishirini na moja, alifanikiwa kumpata ampendaye pale kijijini. Alianzisha uhusiano na mvulana huyo wa kwanza katika maisha yake kwa makubaliano ya kutofanya mapenzi mpaka ndoa.



    Kutokana na uelewa na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo ZAKARIA, alikubaliana na Aisha na mapenzi yao yalinoga bila kushiriki kitendo hicho.



    Kila mahali walikuwa wote na walipendezana kwa hali. Hakaka walikuwa kivutia kwa kila mahali wapitapo.



    Baada ya mwaka mmoja toka waanzishe uhusiano wa kimapenzi, Zakaria aliitwa na kaka yake Dar-es-salaam kwa ajili ya kufanya kazi kutokana na kupata nafasi aliyokuwa anamuahidi kila siku.



    Kwa majonzi makubwa, Zakaria alimuambia kua anaenda kutafuta maisha na yakikaa sawa basi atakuja kumchukua.



    Wote walilia sana na kupeana ahadi ya kuishi pamoja tena kivyovyote vile. Dhakaria aliondoka na kumuacha Aisha peke yake.



    Baada ya miezi sita kupita, mama mlezi wa Aisha aligongwa na nyoka alipokuwa Shambani na kupoteza maisha.

    Lilikua ni zaidi ya pigo kwa Aisha ambaye hakuwa na mtegemezi mwengine pale kijijini zaidi ya yule mama pake yake.



    Alilia sana na baadae uamuzi wa kwenda kumtafuta mpenzi wake mjini Dar-es-salaam ulimjia.



    Hela za pole alizozipata ndizo alizozitumia kwenda nazo Dar bila kujua ni wapi afikiapo, atakapolala wala chakula atakachokula kwa siku zote atakazokuwa mjini. Yote hayo hakuyawaza zaidi ya kuamini kuwa akifika huko ataonana na mwanaume wa ndoto zake. ZAKARIA

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safari ya Dar ilianza kwa taratibu huku Aisha akiwa na matumaini makubwa ya kuonana na mpenzi wake. Hakujua ukubwa wa jiji hili ni tofauti na vijiji vyao. Pia hakujua kuwa mioyo ya watu wa huku pia ni tofauti na watu wa huko kutokana na mchanganyiko mkubwa wa makabila na tabia pia.



    Masaa matano baadae toka alipotoka kwao, alifika Dar kwa mara ya kwanza. Alishangaa sana kuona maghorofa na wingi wa watu waliokuwa wakishuka na kuingia kwenye jiji hili.



    Akiwa na begi lake la nguo, alianza kuhagaika huku na huko na kuuliza watu juu ya Zakaria.

    “namtafuta mpenzi wangu anaitwa Zakaria Kamonalelo. Sijui unamjua?” aliuliza Aisha baada ya kutembea mwendo mrefu bila kumuona mpenzi wake.



    “wewe dada umechanganyikiwa?.. huyo mpenzi wako sura yake ipo kwenye shilingi mpaka kila mtu amfahamu?... una wazimu wewe.” Aliongea dada mmoja aliyekuwa na rafiki yake na kusababisha kicheko kati yao.



    Aisha alizunguka mpaka usiku bila ya mafanikio. Usiku ulipokuwa mkubwa, hakujua ni wapi anaweza kupata hifadhi, alitembea huku na huko na kukuta wakina dada wakiwa wamejipanga wakiuza miili yao maeneo ya shekilango.



    Alistaajabu kuwaona madada wale waliokuwa wamevaa nusu uchi, aliamua kufungua mkoba wake na kutoa khanga kadhaa na kuwapelekea.



    “wewe dada una wazimu nini??... wewe wa wapi wewe?..hebu nitolee takataka zako hapa. Muangalieni huyu jamani amekuja kutufunga hela.” Aliongea dada poa mmoja baada ya kumuona Aisha amekuja kuwapa khanga.



    “we mwenyewe si unamuona alivyo, ametuka Kimbiji leo hii.” Alongea dada poa mwengine na kuwafanya wenzake kuangua kicheko.



    Aisha aliamua kurudisha khanga zake kwenye begi lake na kwenda kukaa pembeni kabisa.

    Kutokana na kuzunguka muda mrefu, uchovu aliokuwa nao uliishinda njaa na kupitiwa na usingizi mzito pale pale alipokaa.



    Kwa kudra za Mwenyezi Mungu palikucha salama. Aisha aliamka asubuhi hiyo huku akiwa hana dira yoyote ya kuelekea. Aliamka na njaa ya ajabu sana, lakini akiangalia salio lake halikumuwezesha kununua chochote hapa mjini.



    Aliamua kutembea huku na huko bila kuchoka kumuulizia mpenzi wake huyo ambaye hakupata majibu yaliyomridhisha. Zaidi alipata majibu ya kumkatisha tamaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mpaka mchana uliingia bila ya Aisha kutia kitu chochote kinywani mwake. Mpaka kichwa pamoja na tumbo vilianza kumuuma kutokana na njaa aliyokuwa nayo. Aliamua kukaa chini na kujiinamia huku akiugulia maumivu aliyokuwa nayo.



    “umepatwa na nini dada?”



    Ilisikika sauti ya kiume iliyomfanya Aisha anyanyue kichwa chake pale alipojiinamia na kumtazama mtu aliyemsemesha kwa tabu kutokana na maumivu aliyokuwa anayasikia muda huo.



    “kicha kinaniuma na tumbo pia, ila vyote hivyo vimesababishwa na njaa kaka yangu.” Aliongea Aisha na kumuangalia yle mtu aliyekuja kumuangalia.



    “pole sana.”

    Aliongea yule kaka na kuingiza mkono mfukoni na kutoa waleti yake na kutoa noti moja ya shilingi elfu tano na kumkabidhi Aisha.

    Ilikuwa kama ndoto kwa aisha kutokana na kuijua thamani ya hela aliyopewa.

    “ahsante sana kaka yangu.” Alishukuru Aisha.

    “usijali,” aliongea yule kaka na kuondoka zake.



    Hatua tano tu alizopiga yule kaka toka aondoke pale alipokuwa amekaa Aisha, alishtushwa na kishindo kikubwa kilichotokea nyuma yake. Aligeuka haraka na alichokiona hakukitarajia. Alimkuta Aisha ameanguka chini na kuzimia. Aliruda pale na kuamua kukodisha taksi iliyowapeleka kwenye hospitali ya magomeni usalama.



    Huko alipokelewa na manesi waliokuwa nje na kumuwekea dripu ya maji.

    Nusu saa baadae, Aisha alirejewa na fahamu na kuanza kuangaza huku na huko na kumkuta kijana aliyemuokata akiwa pale. Yule kijana alipomuna Aisha anamuangalia, alimuita daktari ambaye alifika pale na kumkagua.



    Baada ya hapo alipewa chakula ambacho alikishambulia kwa kasi na kukimaliza haraka.

    Baada ya daktari kuridhika na hali ya mgonjwa, Aisha aliruhusiwa kurudi nyumbani.



    “wewe ni mkazi wa wapi hapa Dar?” aliuliza yule kaka ambaye alimsaidia Aisha.

    “mi nimkazi wa Morogoro, hapa Dar nimekuja kumtafuta mpenzi wangu tu.” Aliongea Aisha na kumuangalia yule kaka.



    “amekupa anuani yake au namba ya simu?” aliuliza yule kaka.

    “sina anuani wala namba yake.” Aliongea Aisha na kumfanya yule kaka aliyemsaidia kupigwa na butwaa.



    “sasa utampataje huyo mpenzi wako?” aliuliza yule kama na kumfanya Aisha kujiinamia kwa muda.

    “ni imani tu ndio niliyojiwekea kuwa nitampata.” Aliongea Aisha na kumfanya yule kaka aelewe kwa kina kitu kilichomsukuma binti huyo kutoka kijijini kwao na kuja huku Dar bila kuangalia madhara yatakayompata.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “bila shaka huna pa kufikia hapa mjini?” aliuliza swali yule kaka ili mradi ahakikishe kitu alichokiwaza kutokana na maelezo ya Aisha.

    “ndio.” Alijibu Aisha.



    “sawa, mi nitakupa hifadhi nyumbani kwangu. Hapo utakaa mpaka utakapofanikiwa kumpata huyo mpenzi wako.” Aliongea yule kaka na kumfanya Aisha afurahi.



    Yule kaka aliyemsaidia Aisha alikodi taksi na kupelekwa nyumbani kwake maeneo ya magomeni moroco ndogo.



    Huko Aisha alikutana na mdogo wake wa kiume na huyo kaka ambaye walikuwa wanaishi wawili tu humo ndani.



    “nimeongeza familia mdogo wangu Mack. Huyu ni dada yetu wa hiyari, atajitambulisha mwenyewe. Nimemleta hapa ili tusaidiane maswala ya hapa ndani, si unajua nyumba bila mwanamke haijakamilika?” aliongea yule kaka kwa utani na kufanya kicheko kilichodumu kwa sekunde kadhaa kutokea baina yao.



    “sawa kaka Jack. Enhee, dada unaitwa nani?” aliuliza mdogo wake na Jackson ambaye alionekana machachari kuliko kaka yake.



    “naitwa Aisha.” Alijibu Aisha kwa aibu kidogo.

    “wooooh..Aisha, Mack, Jack sasa ni familia moja. Karibu sana dada yangu.” Aliongea Mack na kufanya wacheke tena.

    “mzoee tu mdogo wangu. Anaongea sana huyu.” Aliongea Jack na kunyanyuka alipokaa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Aisha, hapa ndio nyumbani. Jisikie huru sana. Twende nikakuonyeshe chumba utakachokuwa unalala. Ili kama unajisikia uchovu uende ukalale hata muda huu.” Aliongea Jack na Aisha alimfuata na kupewa chumba ambacho kilikuwa na kitanda pamoja na kabati la nguo tu.



    “nitachonga Dressing Table kwa ajili yako. Jisikie huru Aisha.” Aliongea kaka huyo na kumuacha Aisha mule ndani.



    Alikaa Aisha kwenye kitanda hicho na kushangaa kwa jinsi kilivyoluwa kinabonyea. Alipojaribu kulala, alikuta kinadinya ndinya na kumpa raha ya kulala. Alijikuta anatabasamu peke yake na kumshukuru mungu kwa kusaidiwa na kijana yule alionyesha kuwa na nia nzuri kwake



    Usingizi ulimchukua na kulala kwa masaa kadhaa. Alshtushwa na mtu aliyekuja kumuita kwa ajili ya kula chakula cha usiku.

    “ulichoka sana eeh.. maana umelala muda mrefu?” aliuliza Jack walipokuwa kwenye meza ya chakula.

    “ni kweli. Nilikuwa na uchovu wa maana. Yaani sijui hata kama nitapata usingizi usiku huu kwa jinsi nilivyolala muda mrefu.” Aliongea Aisha na wote wakamuangalia dada huyo kwa pamoja.



    “unaonaje kama ukituhadithia ilivyokuwa mpaka ukaja huku Dar kumtafuta huyo mpenzi wako.” Aliongea Mack baada ya kumaliza kula.

    “mimi mzawa wa morogoro. Ni mpogoro halisi kutoka kwa baba na mama yangu ambao wote kwa sasa ni marehemu.” Alianza kuhadithia Aisha huku wote wakiwa makini kumsikiliza.

    “pole sana.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kipengele hicho cha kufiwa na wazazi wote wawili kiliwagusa moyoni na wote wakatjikuta wanongea maneno hayo kwa pamoja.



    “baada ya kifo cha baba yangu mpenzi, hapo ndipo nilichukuliwa na baba yangu mkubwa na kuanza kuishi nae pale nyumbani kwetu kama mlezi wangu na mali zangu. Mwanzo wa mateso ulianzia hapo. Kazi zote nilizifanya mimi. Niliteswa na kupigwa mara kwa mara hata wakati mwengine niliunguzwa na moto na mama yangu mkubwa. Uzalendo ulinishinda na kuamua kutoroka pale nyumbani. Nilikimbilia kijiji cha pili, huko nilikutana na mama mmoja aliyekuwa mkulima. Hakika namshukuru sana kwa kukubali kunipokea na kunilea kama mwanae wa kumzaa. Mpaka na fika kwa huyo mama, sikuwahi kuwa na mpenzi kabla, ila baadae nilipokuwa najitambua, nilikuwa na mvulana ambaye tulikua tunapendana sana. Hakuna ambaye alikuwa hatujui pale kijijini kuwa sisi tulikuwa wapenzi. Kwa bahati nzuri au mbaya, mpenzi wangu aliitwa na kaka yake anayeishi huku Dar, alikuwa amemtafutia kazi huku mjini na ndipo mpenzi wangu aliponiaga na kuja huku kwa huyo kaka yake. Nilivumilia sana kwakua nilikua namuamini kupita maelezo, ila mwaka mmoja baadae yule mama aliyekuwa ananilea aliaga dunia na kuniacha mimi mpweke nisiye na msaada wowote pale kijijini kwao. Ndipo nilipoamua kuja huku Dar kwa ajili ya kumtafuta mpenzi wangu.”



    Aisha aliwahadithia stori ya maisha yak e na kusababisha wamuonee huruma kwa msoto alioupitia.



    Baada ya kusikiliza stori hiyo, kila mtu aliingia chumbani kwake na kutafuta usingizi ulipo.

    Asubuhi Jack aliamka na kumpatia Aisha kiasi cha shilingi elfu kumi kwa ajili ya nauli ya kuzunguka hapa mjini kwa ajili ya kazi yake ya kumtafuta huyo mpenzi wake aliyemteka hisia na aliyekuwa na ndoto naye nyingi kuliko mwanaume yeyote hapa duniani.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alitoka asubuhi Aisha kwa msaada wa Mack aliyekuwa anampeleka kila sehemu anayotaka kwenda na kumsaidia kumuulizia mtu huyo ambaye hawakuwa na hata picha yake.



    Walirudi jioni bila mafanikio. Jack aliwapa moyo na kuwaambia watafanikiwa tu kwakua mungu yupo na atawakutanisha tu.



    Zoezi la kuenda pamoja na Mack lilichukua muda wa mwezi mmoja na baadae Aisha aliananza kwenda mwenyewe kwa sababu alishalizoea jiji na kila sehemu alipajua kwa muda mfupi.



    Zoezi hilo lilichukua muda wa mwaka mzima bila kuonana na Zakaria.

    Aliheshimiwa mule ndani kama dada yao wa tumbo moja. Mpaka kupita muda huo tayari Aisha alishachoka kumtafuta mpenzi wake huyo. Aliamini kuwa ukubwa wa jiji hili, kuna uwezekano asionane nae kabisa katika maisha yake.



    “vipi dada, mbona siku hizi huendi kumtafuta shemeji, wiki ya pili leo hii hujatoka kabisa?” aliuliza Mack baada ya kumuona Aisha kila siku wakishinda wote, na hata kama akitoka basi humkuta akirudi.

    “ah!.. nimechoka kumtafuta Mack.” Aliongea Aisha na kumuangalia Mack ambaye walizoeana sana kuliko kaka yake ambaye alikua yupo bize na kazi kwa muda. Na akirudi huwa amechoka hivyo kutumia mud mfupi sana kuwa karibu nay eye.



    Muonekano wa Asha ulibadilika sana kutokana na kukaa mjini kwa kipindi kirefu. Licha ya uzuri halisi wa mrembo huyo, lakini aina ya nguo za kisasa, kucha za bandia, kope na ma wigi ya Brazil ndio ulioubadilisha kabisa muonekano wake na kuwa wakuvutia zaidi. Alipendeza sana kutokana na shooping za mara kwa mara alizokuwa anapigwa na Jack. Hata mule ndani walikubali kuwa uzuri wa yule dada yao wa hiyari ulifunikwa na shida tu, ila kiukweli alikuwa mzuri sema alikosa tu huduma.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kadri siku zinavyozidi kwenda, Aisha aliendelea kuvutia sana na kuwafanya wanaume wengi aliokuwa anakutana nao njiani au popote kutupa ndoano zao ili wajaribu bahati zao kwake.

    Hakuna aliyefanikiwa kwa binti huyo aliyejiwekea msimamo mkali kwa kutokubali kuvua nguo yake ya ndani kwa mvulana yoyote mpaka afunge naye ndoa.



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog