Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

NISAMEHE GRACE - 4

 





    Simulizi : Nisamehe Grace

    Sehemu Ya Nne (4)



    Baada ya Mama yake na Grace kuondoka Mahakamani na Kufika nyumbani Mama yake na Grace hakuitaji kabisa kusubiri. Alichofanya alifanya Maandalizi na Safari ya kuelekea Kijiji cha Himo ilianza. Kule Himo Moshi Kilimanjaro ndiko kulikuwa na Mganga wa kipare ambaye Mama yake na Grace alikuwa anamfahamu sana.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kutoka ashura user river hadi Moshi mjini mama yake na Halima alitumia Muda wa Dakika arobain na tano tu. Alipofika Moshi Mjini alisimama na kushuka kwenda Duka moja kununua Maji ili aweze kuendelea na Safari yake. Wakati Akiwa kwenye Duka lile ndipo Goodlucky aliweza kumuona. Goodlucky alipomuona yule mama alishituka sana na kushindwa kuelewa huyu mama kafika saa ngapi kwenye hili eneo maana siyo Muda taarifa alipewa na Afande Sophia kuwa Frank amehukumiwa Jela Miaka kumi pia wazazi wa Grace walikuwepo wote na Walionekana kufurahishwa na lile tukio. Sasa kitendo cha Ghafla kumuona mama yake na Grace kwa kweli kilimshitua mbaya Goodluck. Kitu cha kwanza ambacho alikifanya Goodlucky ni kupanga kumfatilia Ili Kujua yule Mama alikuja Moshi kwa lengo Gani. Mama yake na Grace alipoenda kupanda kwenye gari na kuondoka tayari na Good alishapata Tax ambayo alimuomba Dreva aifatilie Gari ya mama yake na Grace inapoenda ili kuweza kujua huyu mama alikuwa anaenda wapi. Waliifatilia ile Gari hadi walifika kijiji cha Himo kuna sehemu Mama yake na Grace alipaki Gari na kuanza kutembea kwa Mguu. Hata kina Goodluck na wenyewe walipaki Gari na Kumfatilia Mama yake na Grace kwa Miguu. Safari ya mama Grace ilienda kuishi kwenye nyumba moja hivi ambae ilikuwa vigumu kuamini kama ilikuwa kwa Mganga. "Unaweza ukawa unapafahamu hapa ndugu yangu"Good alimuuliza kijana Dreva tax ambae alimuomba kwa muda ule washirikiane kumchunguza huyu mama. "Napafahamu sana ndugu yangu, huyu ni Mganga ambae anajulikana sana. Hivyo kama huyu ni mama yako naomba umzuie maana huyu Mganga anawafanya watu kuwa matajiri kupitia kuua watu au kuwafanya kuwa machizi"Aliongea yule Dreva tax maneno ambayo yalimshitua kidogo Good. Good aliposikia kuwa pale ilikuwa kwa Mganga basi ilibidi kusogea maana hata wasingemuhisi vibaya wangejua naye amekuja kutibiwa tu. "Nahitaji Mwanangu asimwaze tena Frank na aolewe na Mwanaume ambaye ninamtaka mimi. Huyu siyo Mwingine bali ni Shawali"Aliongea mama yake na Grace maneno yalimfanya Goodlucky kushituka. "Haina Shida mama yangu mtoto wako tayari ameshaolewa. Nakupa hii hapa hirizi naomba ukaweke kwenye kitanda cha mwanao. Baada ya siku mbili mambo yako yatakuwa tayari. Huyo mtoto wako atamchukia huyo frank kama mavi. Nashangaa kazi ilikuwa rahisi sana ungeshakuja zamani haya yote yasingekusumbua"Aliongea yule Mganga. Kwa kweli yale Maneno ya Mganga yalizidi kumchanganya Goodluck. Kwa kasi ya Ajabu alichukua simu yake haraka huku akisogea eneo lile ambapo alikuwepo mganga ili ampigie Simu Grace na kumwambia Juu ya Ubaya wa mama yake. Kilichozidi kumpa Pressure Good ni namba ya grace kutokupatikana. Ile hali ilizidi kumtia wasiwasi good na kuhisi sasa Frank anaenda kumkosa Grace maana manemo ambayo aliongea Mganga huenda yalikuwa ya kweli. Baada ya Grace simu yake kutokupatikana Goodlucky aliamua kuondoka mwenyewe hadi Arusha kwenda Kumjulisha Grace. Kwa kweli Good hakuwa tayari kumuona Grace akiolewa na mtu mwingine. Kama yeye alishamkosa alikuwa anahitaji yule mtu aliyemsababishia matatizo ndio amuoe ila siyo Shawali. Alichofanya ni kumwambia Dreva tax waondoke kwa kasi ya Ajabu. Dreva alimuelewa Goodluck na wote waliondoka kwa kasi mbaya. Wakati wakiwa Wametoka barabara ya himo na kufika njia panda ya Barabara inayoenda Makondeko kwa bahati mbaya Gari yao Tairi ya nyuma ilipasuka kisha iliyumba na kwenda kupinduka na kuviringita mara mbili.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Baada ya Gari ambayo Goodlucky alikuwepo kupinduka na kuviringita Mara mbili hakuna ambaye alipoteza maisha zaidi ya Wote kuumia. Uzuri sehemu ambayo walikuwa wamepatia Ajali ilikuwa Mjini hivyo Mara baada ya kupata Ajali walichukuliwa na Kukimbizwa Hospitali ya Makondeko na Kuendelea na Huduma. Wakati wamepelekwa Hospitalini kwa Kweli Good alikuwa hajitambui kabsa maana alikuwa amejipigiza vibaya kichwani hadi kupelekea kuzimia hivyo tayari jinsi ya kumuokoa Grace kutoka kwa mama yake ambaye alienda kuchukua Dawa ili kwenda kumwekea na Grace kumchukia Frank tayari ilikuwa imeshindikana. Ilichukua Kama Muda Wa Siku Mbili Ndipo Good alipatwa na Fahamu Muda ule tayari hata na Suzani Pamoja na Aisha tayari walishapata Taarifa na walikuwa kwa Goodlucky. "Jamani naombeni niondoke sasa hivi nahitaji kwenda Kumuokoa Grace. Nahitaji kwenda Kumuokoa Grace maana mama yake alimuendea kwa Mganga ili amchukie Frank alafu aolewe na Shawali. Pia huyu Dreva Tax yukoje mbona Sasa anakuja kunilaza Hospitalini wakati Mimi nilimwambia kabsa anipeleke stendi ya Mabasi yanaoenda Arusha ili nimuwahi mama yake na Grace"Aliongea Goodlucky huku akiwa Anaamka. Yeye hakuwa Anajua kabsa kama tangu apate ajali tayari zilikuwa zimeshapita siku mbili hivyo tayari alikuwa ameshachelewa. Goodlucky alipojitutumua ili aamke ndipo Sasa alihisi Mguu wake wa kulia Kama Hauna Nguvu hivi alipotupa macho ili Kuangalia ndipo alipokutana na muhogo Mkubwa ukiwa Umezunguka Mguu wake. "Goodlucky naomba tulia maana Unasiku mbili tangia upate Ajali ya Gari hujalejewa na fahamu. Hivyo naomba utulie maana umevunjika mguu na Dactari Kasema ulale hadi yeye atakapokuja kukuona"Yalikuwa ni Maneno ya Aisha ambayo yalimshitua Good na kukumbuka kila kitu ambacho kilitokea. "Aisha mbona Sasa tumechelewa, nakwambia tumechelewa tayari Frank ameshamkosa Grace"Aliongea Goodlucky huku akiwa ametumbua Macho. Yale Maneno kwa kweli yalimshitua Sana Suzani na Aisha na kumuulizia Anamaana Gani Good kuongea hivyo. Goodlucky hakuwa na Jinsi huku akiwa anaonekana kama Mtu aliyekuwa amekata tamaa aliwaelezea Aisha na Suzani kuanzia Mwanzo hadi Mwisho. ............................................................... Maisha ya Gerezani kwa Frank kwa kweli yalikuwa ya upweke sana. Muda wote alikuwa mtu wa kulia na kumuwaza Grace tu. Kitu ambacho kilizidi kumshanga hadi Alimaliza Mwezi Mmoja hakuna Mtu hata Mmoja ambaye alikuwa anamfahamu alikuja kumuona. Ilikuwa hakuna cha baba, mama wala rafiki yeyote ambaye alikuja kumuona. Sasa yeye kuhusu Ndugu na Rafiki kuto kuja kumuona alikuwa hata haumii ila kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza ni Grace kutokuja kumuona. Ile Hali kwa kweli ilimuuma Sana Frank hadi kufikia kuwaza kutoroka Jera ili kwenda Kumuona Grace. Ingawa zilipita siku nyingi bila mtu yeyote kutokea lakini Frank hakuchoka kumuomba Mungu alihisi iposiku tu Grace atakuja kumsalimia. Upande Mwingine alihisi huenda Mimba yake imeshakuwa kubwa inamfanya awe na Wakati Mgumu Sana kuweza kuja Sehemu ambayo alikuwepo. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Yale Maelezo ambayo Goodlucky aliwaambia Suzan na Aisha yaliwashitua na kuamua kumpigia Simu Grace kumjulisha juu ya ile hali ingawa walikuwa wanajua tayari walikuwa wameshachelewa. Aisha alichukua Simu yake haraka haraka na kuangalia namba ya Simu ya Grace na kuipiga. Simu iliita kwa Muda kisha mtu aliikata bila kupokea. Aisha alipoona vile alirudia tena kupiga ndipo ilipokelewa. "Grace mimi Aisha vipi lakini Hali ya Frank Gerezani uliwahi kwenda kumuona hata Siku Moja"Aliongea Aisha ili kumpima Grace maana kama kweli angekuwa ameshalishwa madawa tayari angegundua tu. "Frank ndio nani na wewe ulionipigia simu ni nani, unaanza tu vipi Grace umeenda kumuona frank tangu afungwe. Nikamuone frank ili iweje, mtu ambaye alinisaliti na kutembea na wewe malaya usiyekuwa na haya leo hii nikamuone mwache aozee Jela mimi wala sina Muda mchafu wa kwenda kumuangalia Frank. Baada ya kuniuliza unampango gani wa kuhakikisha Frank anahukumiwa upya kifungo cha Maisha Jela wewe unaniulizia Upumbavu. Wewe si unampenda Sana Frank hadi ulifikia kuja kufanya Mapenzi kwenye chumba changu, basi nakuruhusu nenda kamtoe alafu muoane mimi mwenzako wala Sina Time kabsa na huyo malaya"Yalikuwa ni maneno ya Grace akimjibu Aisha. Yale maneno kwa kweli yalimfanya aisha hadi machozi yalianza kumtoka maana kwa dalili ile tayari walishamkosa Grace. Baada ya aisha kushindwa kuongea neno lolote ndipo Goodlucky aliomba simu ili yeye mwenyewe aongee na Grace. "Grace unaongea na Goodlucky nakuomba tafadhari usifanye hivyo. Kumbuka Frank anakupenda sana na wewe ndio sababu iliyofanya Frank hadi sasa kuwekwa jela. Mama yako mbaya najua kakuwekea madawa kwenye kitanda chako ili umchukie frank"Aliongea Good kwa huruma. "Goodlucky masuala ya mama kuniwekea Dawa hayo wewe hayakuhusu. Huyo ni mama yangu aliyenizaa na kunilea hivyo anauchungu na mimi acha afanye kile ambacho anakitaka. Labda mimi Goodlucky acha nikushukuru kwa kunipa mimba ambayo imepelekea hadi kuachana na Frank na Hatimae naenda kuwa mke wa mtu maarufu sana. Ndio siyo Muda naenda kuolewa na Shawali huoni kama nitakuwa mke wa mtu mwenye pesa. Hii ni bahati ya aina yake na wewe ndio msababishaji mkubwa. Hivyo kama ndoa yangu itafungwa wewe nitakupa zawadi kubwa sana maana wewe ndio ulifanya hadi mpango wa kuolewa na Frank kusitishwa. Asante Sana Goodlucky na Mungu akujalie"Aliongea Grace na kukata Simu .



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yale Maneno ya Grace kwa kweli yalimchanganya vibaya Sana Goodlucky. Kwa maneno ambayo alikuwa anaongea Grace Goodlucky aligundua tayari alikuwa ameshachelewa na tayari Dawa ambazo mama yake na Grace alikuwa ameshazifanyia kazi. Baada ya Grace kukata Simu bado Goodlucky hakulizika alimpigia simu tena ili kuweza kuongea naye kwa mara nyingine tena. "Good vipi Mbona unanisumbua Sana hivi au unataka kunidanganya tena uje kunibaka kwa mara ya pili siyo. Hebu niache Bwana Najiandaa hapa nataka kwenda kwa Mpenzi wangu Shawali kuna kitu anahitaji kwenda kunifanyia. Unajua wewe ulifanya mapenzi na Mimi mara moja tu tena kwa haraka haraka na kunipa mimba. Sasa tangu nipate mimba hakuna mtu ambae ananikuna na wakati wewe ulishachokoza kaupele ambacho kalikuwa kanawashwa. Acha niende kwa shawali Mpenzi wangu ambae nimepangiwa na Mungu ili akanikune. Hata hivyo wakati ananikuna atakuwa amekusaidia na wewe mtoto wako kutoka akiwa na Afya nzuri. Maana mimi ninadamu yako pia tumboni. Nakuomba tafadhari usiendelee kunisumbua niache nifanye ninayojua na ukiendelea kunisumbua basi nitatoa hiki kitakataka chako tumboni alafu na Frank naenda kumuua na siyo kumfunga tena"Aliongea Grace kwa sauti ya kujiamini. Yale Maneno ya Grace kwa kweli yalimfanya Aisha na Goodlucky hadi kuanza kulia. Hata siku Moja hawakuamini Kama Grace angekuja kuongea Maneno kama yale. Yale Maneno yalimchoma Sana Aisha na kuamua kumuondolea Simu Goodlucky ili kuongea na Grace. "Grace rafiki yangu Tafadhari nakuomba usiwe hivyo, tafadhari nakuomba nisikilize mimi mwenyewe naweza kukusaidia. Kwa nini unataka kusubutu kutembea na Mwanaume ambaye ndio amemfanya mpenzi wako Frank kukaa jela bila hatia. Tafadhari nakuomba Grace fikilia kuhusu frank anavyoteseka Gerezani bila hatia"Aliongea Aisha huku machozi yakiwa yanamtoka. Yale Maneno aisha aliyoongea yalionekana kumpa raha sana Grace na kumfanya acheke kwa sauti. "Aisha mimi sina alama yeyote kwenye Mwili wangu ambao inaonyesha mimi mpenzi wangu ni Frank. Pia wakati naumbwa sikupewa maelekezo kuwa Mume wangu atakuwa Frank. Hivyo naomba fanya kama nilivyokwambia Mwanzo nenda kamtoe Frank Gerezani kisha akuoe mimi sina shinda na yeye naolewa na shawari. Alafu nakushangaa sana wewe si ulikuja kwangu ukihitaji tukamsaidie frank kushinda kesi na kutoka jela. Ulivyoona tu Afande Joshua kafa na wewe ulikimbia si jui woga gani huo. Au wewe ndio ulimuua Afande Joshua ili Frank asitoke Jela maana ulihofia uenda akitoka Jela ataniona. Acha kutokujiamini mimi Frank simtaki tena kamtoe tu Jeka ili umuoe."Aliongea Grace huku akicheka. Yale maneno ya Grace kwa kweli yalizidi kumpandishia Hasira Good. "Grace mimi ni mojawapo ya Wanaume ambae nilikuwa nakupenda sana. Niliamua hadi kukubaka ili niweze kutuliza moyo wangu. Kwa kweli niliamua kuachana na wewe ili kumwachia rafiki yangu frank ambae nilimuumiza bila kutegemea akuoe. Sasa siwezi kuwa tayari kukuona unaolewa na shawari. Nipo tayari kumuua huyo mwanaume ili wewe uolewe na Frank na Ukijifanya unajua hata wewe Utakufa Grace"Aliongea Goodlucky huku machozi yakiwa yanatoka na kukata simu. "Nataka nikaonane na Grace sasa hivi ili yeye aniambie kama hamtaki Frank. Tena nahitaji kwenda kumuona na huyu Shawali wake nimwambie kabsa kama anataka kuishi akae mbali na Grace"Aliongea Good huku akiwa amechanganyikiwa na kwenda chumbani kwake kujiandaa ili kumfuata Grace kwake





    Ile hali ya Frank kuwepo Jela alafu hakuna Mtu yeyote ambaye alitokea kuja kumuona ilizidi kumchanganya mbaya na kumfanya kuwa mtu wa mawazo sana. Alijiuliza Grace ambaye alikuwa anamlilia kipindi amehukumiwa kwenda Jela na Kumuhaidi kuwa atakuja kumuona yukwapi. Pia upande Mwingine aliumia Sana Maana hata ndugu zake ikiambatana na wazazi wake hakuna hata Mmoja ambae alikuja kumuona. Frank alimaliza Muda wa Mwaka Mmoja jela lakini hakuna mtu yeyote ambae alikuja kumuona. Ile hali ilimfanya Frank hata Afya yake kuzoroteka sana kwa Ajili ya Mawazo. Kitu ambacho aliamua Frank kupanga ni kuweza Kutoroka Gerezani kwa kweli hakuwa tayari kuona mtu ambaye alikuwa anampenda na ndie ambayo alimleta hata Gerezani anachukuliwa na Mtu Mwingine. Hakuna kitu Kingine ambacho alikuwa amekipania Frank kama kutoroka Gerezani. Kule Gerezani Frank alikuwa Anaisha Maisha ya kawaida Sana kuliko Wafungwa wengine maana hata kazi ambazo alikuwa anazifanya zilikuwa za kawaida sana kama kufanya Usafi kwenye nyumba za Askari Magereza. Hata kulala Frank hakuwa analala kwenye vyumba vya Magareza bali alikuwa analala ofisini kwa Mkuu wa Gereza. Mle Gerezani Frank alikuwa anashangazwa na ile Hudumu nzuri ambayo alikuwa anapatiwa kuliko wafungwa wote. Kwa Haraka alihisi lazima kuna mtu ambaye alikuwa anaongea na Askari wale ili kuhakikisha kuwa anapatiwa Huduma nzuri. Kweli kile ambacho alikuwa anakiwaza Frank kilikuwa kipo Sahihi. Yale mambo yote yalikuwa yamefanywa na Mzee Ramadhani. Mzee Ramadhani ambaye alikuwa baba yake na Shawali alikuwa na Mpango wa kumtoa Frank Jela. Frank alipokaa Mwezi Mmoja tu alikuwa ni mtu wa kwanza kwenda kuongea na Mkuu wa jela namna ya kumtoa Frank. Mkuu wa Jela alimwambia kuwa Frank kessi yake imesimamiwa na Vigogo na kweli hana hatia lakini kumtoa kirahisi itakuwa kazi. Ambacho aliambiwa Mzee Ramadhani ni Kusubilia yule mtu aliyekuwa anagombania Mpenzi na Frank amuoe mke wake na Frank ndipo wao itakuwa Rahisi kumtoa frank. Mzee Ramadhani alipoambiwa vile aliamua kukubali ila aliwapa Afande pesa na kuwaambia wahakikishe kuwa Frank hateswi jela wala kufanya kazi ngumu huku akiwaambia Frank alikuwa ndugu yake. Mzee Ramadhani yeye alikuwa Hajui kabsa kama Frank alikuwa anagombania Mke na Mtoto wake Shawali. Alikuwa Hajui kama Shawali ndio ambae alihakikisha anampeleke frank Gerezani. Mzee Ramadhani yeye alikuwa Anamuomba Mungu yule mtu ambaye alikuwa anataka kumuoa Grace amuoe mapema ili Amtoe Frank Gerezani. Kila Muda alikuwa anawaulizia afande kama yule mtu alishamuoa Grace ili yeye CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/akamtoe Frank lakini aliambiwa bado na hiyo ndio ilikuwa Sababu ya Frank kukaa sana Gerezani. Frank kwa kuwa alikuwa Huru sana aliamua kutumia huo Uhuru wake kuweza kutoroka Gerezani. Alipanga Atakaa Gerezani Mwezi Mmoja tu akisubulia kama hakuna mtu ambaye angekuja Kumuona basi angetoroka. Upande wa wazazi wake na Frank wao walikuwa wanaongea na mzee Ramadhani maana yeye ndio aliwaambia waache kabsa ile kazi ataishughulikia yeye.mzee Ramadhani alibaini kama ndugu watakuwa waenda kwa wingi kumuona frank ndio wangefanya wale waliokuwa wamemfunga Frank kuzidi kuhakikisha wanamfanyia unyama frank. Hivyo Mzee Ramadhani aliwaambia wala wasiende kumuona Frank yeye ndio anamaliza mchezo. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Baada ya Goodlucky kupata Ajali ya Gari na kupelekwa hospitalini kisha siku ya pili kurudiwa na Fahamu wakaongea na Grace na Grace kuamua kuwapotezea hawakuwa na jinsi waliamua kuachana naye na kuwaza mbinu nyingine ya kumtoa Frank Gerezani na hatimae watatumia mbinu nyingine kumpata Grace. siku tatu Goodlucky alikaa hospitalini na Baadae waliruhusiwa kurudi nyumbani. Muda ule Wote goodulucky pamoja na Aisha walishaacha kwenda hata shuleni maana walikuwa Walimu. miezi Mitatu mbele tayari Goodlucky alishapona Mguu wake kabsa. Ilikuwa Siku ya Juma tatu ambapo Goodlucky aliamua kumpigia Grace simu ili kumwambia kuwa anataka kumpitia ili kwenda kumuona Frank Gerezani. Frank alikuwa Anamwambia Grace vile ili kumpima kama kweli Grace mama yake alishamfanyia yale mambo na kweli alishamsahau kabsa Frank. "Goodlucky nakuomba tafadhari sitaki uniambie kitu chochote kuhusu Frank. Mimi muda huu najiandaa kwa ajili ya ndoa yangu na Shawali leo hii unaniambia upuzi kama huu. Wewe nenda kamuone Mwenyewe Frank tena Umwambie asiniwaze kabsa mimi maana nitamuua. Kama Huamini hiki ambacho Nakiongea leo Shawali anaenda kunitambulisha kwa baba yake njoo ushuhudie"Yalikuwa ni Maneno Ya Grace ambayo yalimfanya Good kuchukia mbaya. " Aisha nahitaji kwenda Kumuona Grace sasa hivi, nahitaji kwenda kumsitisha asiende kutambulishwa. Siwezi kukubali kuona Grace akiolewa na mtu Mwingine"Aliongea Goodlucky na kuamka kuelekea chumbani kwake. Aisha alibaini kuwa Goodlucky amepaniki hivyo anaweza kupeleka Mambo vibaya na kuharibu. "Goodlucky Unatakiwa kutulia na Kutimia akili ili haya mambo yafanikiwe. Kumbuka kuwa Sisi Afande mkuu wa jeshi la Polisi Arusha anajua tumeshakufa hivyo wakituona bado wazima inaweza kusababisha kuanza kutafutwa na kushindwa kufanya kitu chetu. Kama Grace tayari dawa zimempitia wewe huitajiki Kumlaumu nenda na wewe kwa yule yule Mganga ili kuweza kumuoakoa Grace"Aliongea Aisha Maneno ambayo Goodlucky aliona yanafaa



     Yale Maneno ya Aisha Kumwambia Goodlucky kuwa hapaswi kumlaumu Sana Grace maana pale zinazofanya kazi ni dawa hivyo na yeye anatakiwa kwenda kwa Mganga kama Yalimshitua hivi Good na kuhisi kama yanaukweli hivi ndani yake. "Aisha nahisi Umeongea ni ukweli lazima niende kwa Mganga ili kuhakikisha ile dawa inayomteka akili Grace aiondowe. Unajua Siwezi kukubali bora ningemuoa mimi Grace ila siyo Shawali. Mwanamke huyu Tumeteseka naye hadi sasa tunaelekea kufukuzwa kazi kwa ajili yake leo mtu from no where aje amchukue kizembe mama yangu mzazi haiwezi tokea labda niwe maiti"Aliongea Goodlucky kwa Hasira na kutoka Nje. Muda ule Kweli Goodlucky alikuwa Amepania kwenda kwa Mganga maana si alikuwa anapajua. Alipotoka nje alienda hadi kituo cha Tax na Kukodi tax tayari kwa kuanza Safari ya kuelekea kwa Mganga. Afande Sophia wao walikuwa wanaendelea na Uchunguzi wa Hali ya Juu sana na kwa siri kubwa ili Kuhakikisha kuwa wanapata ushaidi wowote Ambao Wangeupeleka Mahakamani na Kuhakikisha Afande Rama pamoja na Mkuu wa jeshi la polisi Arusha wanakamatwa. Tayari pale walikuwa na picha za tukio za kutekwa kwa Suzana mke wake na Afande Joshua, Aisha pamoja na Goodlucky na kwenda kutupiwa kwenye shimo. Pia Suzana Goodlucky na Aisha wao ndio walikuwa Wanamjua Afande aliyemua Afande Joshua. Kitendo cha Mkuu wa kituo kuuawa na Afande wenzake kisa tamaa ya Pesa kilimuuzi sana Afande Sophia. Kama Wao kwa wao Muda ule walikuwa wanauana na kushindwa kutetea haki za watu ilikuwa kitu cha kipuzi. Ambacho alikuwa anakitaka ni Kuhakikisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Arusha anafungwa ili kumthibitishia kuwa Sheria ni Msumeno hata ukiwa wakwako basi unakata tu. Muda ule Sophia alipanga kwenda Hadi Moshi kisha anaenda kumrudisha Mama Suzani kwake ili kumuwekea Ulinzi na yule ndio ambae angemuonyesha mtu aliyemuua Afande Joshua na kuanza naye. Safari ya kutoka Makondeko hadi Himo ambako alikuwa anakaa yule Mganga ambaye alimpa Mama Grace dawa na kumfanya grace kumchukia Frank iliwachukua kama nusu saa tu maana haikuwa mbali sana. Alipofika Moja kwa Moja alienda hadi Kwa Mganga na bahati nzuri alimkuta. Alipofika alimuelezea Maganga kila kitu na lengo la kutaka ampe dawa ambayo ingemrudisha Grace kwenye hali yake na kawaida. "Mwanangu mbona umechelewa sana kama Ungeliniambia siku hiyo hiyo ningekusaidia. Ila Sasa hivi umechelewa maana Dawa tayari imeshafanya kazi pia hadi ni mtibu na Dawa kuacha kufanya kazi siyo chini ya mwaka mmoja. Sasa huo mwaka mmoja tayari tutakuwa tumechelewa maana tayari watu watakuwa wameona maana tayari Huyu mama hata kadi ya Harusi Amenipa"Aliongea Mganga Maneno yaliyomfanya Good lucky kuchoka. "Mganga wewe Naomba nisaidie hivyo hivyo naombaTengeneza hata wakija kuona waachane itakuwa vizuri tu maana sitaki huyu mbwa amuoe huyu Mwanamke wakati hajamwangaikia"Aliongea Good kwa hasira. Mganga kwa kweli hakuwa na jinsi zaidi ya kumwambia Good yeye aondoke atalifanyia kazi. Mganga kwa kweli hata yeye ile tabia alikuwa hapendi maana hata yeye alishawahi kuondolewa mwanamke anayempenda kwa ajili hakuwa na pesa hivyo kile kitendo kilimuuma Sana. Hiyo ndio sababu iliyomfanya hadi kumwambia babu yake amfundishe Uganga ili kumrudisha mke wake pamoja na kuwasaidia wale wanaondolewa wanawake kama yeye. Baada ya Goodlucky kutoka himo kwa Mganga alipanga Sasa kwenda Hadi Arusha kwenda kumzuia Grace asifanye hivyo. Wakati Goodlucky akiwa Safarini kuelekea Arusha kule Grace ndio alikuwa anajiandaa kwa ajili ya shawali kuja kumchukua na Kumpeleka kwa baba yake kwenda kumtambulisha.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Kwa shawali kwa kweli alikuwa na Furaha ya ajabu sana maana alimpata mwanamke kirahisi ambaye alikuwa anamtaka ingawa hakujua kuna kitu mama yake na Grace kakifanya. Muda wa saa Sita tayari Gari ya kifahari ilikuwa imepaki kwa Mzee mambo baba yake na Grace ili kumchukua Grace kumpeleka kwa Mzee Ramadhani kutambulishwa. Mzee Ramadhani Huku naye alikuwa na Furaha mbaya maana alikuwa na hamu ya Kumjua mkwe. Mbaya zaidi alimwalika hata Mzee Oska ambaye alikuwa baba yake na Frank. Mzee Ramadhani yeye hakujua kama Mwanamke ambaye alikuwa analetwa ni yule wa Frank. Kutoka kwa Mzee Mambo Shawali alimchukua Grace na kwenda naye hadi nyumbani kwao. Alipofika nyumbani yeye ndio alikuwa wa kwanza kuingia. Alipoingia sebureni kwa kweli alishituka kidogo alipomuona baba yake na frank naye yupo maana alijua Mzee anamfahamu Grace hata Mpango mzima aliyoucheza anaweza akawa anaujua. Yaye alikuwa anajua Mdingi wake ndio hajua. Hakuwa na kitu cha kufanya tena zaidi alimkaribisha Grace ili kuingia Ndani. Grace alipoingia ndani kwa kweli Mzee Ramadhani alishituka sana hasa alipomuona Mwanamke ambaye alishawahi kuja kutambulishwa kwake na Frank kuwa wataoana ndio ambaye alikuwa anakuja kutambulishwa kwa Muda ule. "Shawali bwana na wewe kwa kutufanyi Surprise inamaana Umeamua kumtanguliza kwanza Mshenga wako ndio afuate mpenzi wako. Tuna mambo mengi sana mwambie mkwe wangu aingie nimuone bwana mambo ya washenga baadae"Aliongea Mzee ramadhani huku akicheka maana yeye alijua Grace huenda yupo pale kama Mshenga na mwanamke ambaye Shawali alikuwa anamleta alikuwa yupo nyuma. "Baba bwana hebu na wewe acha kuleta utani, huyu ndio mwanamke wangu ambaye namuona. Huyu ndio atakuletea Wajukuu baba yangu tena usiwe na Wasi wasi kabsa na wala mimi sikudanganyi"Aliongea Shawali maneno yaliyomfanya mzee Ramadhani hadi kuanza kuona kizuzungu.-





     Kwa kweli Mzee Ramadhani alishituka Sana hakutegemea hata Siku moja kama Mtoto wake Mke ambaye alikuwa anamwambia anataka kumuoa alikuwa ni Mke wa Frank. "Mkuu kuhusu Swala la kumtoa Frank hapa kwa sasa bado Gumu. Hii Kesi imeshikiliwa na Mtoto wa kigogo ambaye mimi siwezi kukutajia Kigogo gani pia yule mtoto wa Kigogo wanashirikiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa Arusha. Hivyo kama Mimi nitakurusu nitakuwa natafuta kifo tu au Kukosa kazi. Afande Joshua alikuwa mtu ambaye alikuwa anahitaji kumtoa Frank maana yeye alikuwa anajua Uhalisia kabsa kama Frank hana Kosa lakini si unaona kilichomtokea amekufa na kuiacha Familia yake. Natamani sana hata Mimi kumtoa Frank ila Subiri kwanza. Subiri kwanza Mzee Yule Mtoto wa Kigogo amuoe Grace mke ambaye wanagombania na Frank ndipo Sasa Makali yatakuwa yamepungua Tutamtoa Frank Gerezani. Najua kabsa kuwa frank hana hatia hata robo ila siwezi kumtoka kwa kuwa bado napenda kazi yangu pia napenda kuendelea kuishi mzee wangu"Mzee Ramadhani alikumbuka Maneno ambayo aliambiwa na Mkuu wa Magereza wakati anaenda kuomba Msaada ili Frank atalowe ndio alizidi kuchoka kabsa. Kumbe mtoto wa Kigogo ambaye alikuwa anashirikiana na Mkuu wa jeshi la Polisi kufanya Maovu alikuwa ni Mwanae. Mzee Ramadhani kwa kweli hadi Machozi yalianza kumtoka maana yeye alikuwa ni mzee wa dini swala tano ilikuwa kila Siku lakini kumbe Mtoto wake alikuwa anatumia pesa zake kuwadhurumu haki watu wenye kipato cha chini. Pia alizidi kushangaa Mtoto wake ambae Muda mwingi walikuwa wanashinda wote msikitini kuswali kumbe alikuwa anafanya mambo ya kinyama vile. "Shawali Mwanangu imanaana wewe ndio ambae ulikuwa unagombania Mpenzi na Mwanangu hadi umempeleka Jela. Shawali kwa nini unamfanyia hivi Mwanangu. Frank aliniambia kweli yeye hajafanya kitu chochote wala hajamuua Afande Joshua ila kuna mtoto wa mtu mwenye pesa anamfanyia hivi kumbe ni wewe shawali. Mbona mimi baba yako anapesa lakini ni rafiki yangu sana hajawahi kunifanyia hivyo"Aliongea Baba yake na frank hadi machozi yalikuwa yanamtoka. "Mzee Oska unaongea nini wewe, mwanangu amechagua mwanamke acha amuoe. Mwanangu hawezi kufanya mambo kama haya na huyu mke ni halali yake. Kama ulikuwa umekuja hapa kwa nia mbaya kwa kumchafua Mwanangu tafadhari nakuomba toka nyumbani kwangu. Nakuomba toka ndani kwangu maana unaongea maneno ya kumchonganisha Mwanangu. Mwanangu mtu wa Mungu muda wote nashinda naye Msikitini lini atapata muda wa kufanya mambo ya kinyama kama hayo. Unataka kuniambia mwanangu hajui kama hayo mambo ya kinyama hadi ayafanye. Wewe Juma Njoo hapa nakuomba mtoe huyu mzee mpakie kwenye Gari mpeleke stendi arudi kwao Sanya Juu naona anaakuja kuongea mambo ambayo hayapo hapa"Aliongea Mzee Ramadhani kwa Hasira. Muda ule Mzee Raamadhani kwa kweli alikuwa ameamua kutumia akili ya kuzaliwa. Aliona Bora ajifanya kama anamkoromea Mzee Oska ili Mwanae asishitukie maana alikuwa anataka kumfanyia kitu ambacho angeamini kama mzee ramadhani hapendi upumbavu. "Mzee Ramadhani mimi nitatoka kwenye nyumba yako wala usiwe na wasiwasi kabsa hiki ambacho Mwanao amemfanyia Mwanangu Mungu atamlipa tu tena Malipo yapo hapa hapa duniani. Pia Mwanangu Grace mwanaume mwema kamwe hawezi toka kwenye Familia ya kitajiri tu hata kwenye Familia za kimasikini kama za Mzee Oska wapo. Mwanangu alikupenda sana na wewe bila shaka utakuwa umesababisha mwanangu kufika gerezani ila mimi nakutakia ndoa njema mwanangu"Aliongea Mzee Oska huku akiamka kwenye kiti tayari kwa kutoka nje. Kweli juma alienda akamchukua mzee Oska na kumtoa nje. Kwa kweli ilikuwa inasikitisha Mzee Oska alikuwa anatoka nje anamwangalia Shawali hadi machozi yalikuwa yanamtoka. Grace yeye alipomuona mzee Oska Machozi yakiwa yanatoka yeye alikuwa anatabasamu maana dawa zilikuwa zimemkolea na alikuwa anamuona shawali Kama Mungu. "Mwanangu naomba nyie kaeni na Ngoja nihakikishe huyu Mwanaharamu anaondoka kabsa hapa kwangu maana anatuchafulia vitu ambavyo tumepanga bure. Anaongea mambo ya kijinga wakati anajua kabsa kuwa hivi vitu wewe huwezi kufanya. yeye kama mtoto wake alishindwa kumuoa Grace mwanangu kamuona acha Amuoe Hivyo Ndivyo Mungu alivyopanga. Leo hii nimemwalika kwa ajili ya kuja kufuraahia Utambulisho wa Mwanangu kumtambulisha mke wake Mwenza ambae amejaliwa na Mungu alafu anakuja kutuharibia. Mwanangu wewe usiwe na wasi wasi kama huyu mke ni halali kwako utamuoa"Aliongea Mzee Ramadhani na kutoka nje. Lengo la Mzee Ramadhani kutoka Nje alikuwa ananaenda kumwambia Mtumishi wake Juma kuwa amepeleke Mzee Oska sehemu alafu wakamsubilie kule ili aje kumuelewesha Vizuri. Baada ya kumpa maelezo Juma Mzee Ramadhani alirudi hadi ndani na Sherehe ya Shawali kumtambulisha Mkewe Iliendelea



     Sherehe ya Shawali Kumtambulisha Mpenzi wake Grace ilikuwa ndogo lakini ilikuwa ya Aina yake na ilikuwa imehudhuliwa na watu muhimu. Yani mwenye pesa siku zote siyo Mwenzako maana sisi kwenda kumtambulisha mchumba wako huwa tumezoea unaenda kwa wazazi wako unaweeleza inapita. Lakini kwa ukoo wa Pesa wa Ramadhani kwanza alikuwepo Shehe mkuu wa Mkoa wa Arusha ndio ambaye alipanga kuja kuomba Dua. Pia kwa kuwa Ukoo wa Mzee Ramadhani ulikuwa wa Kidini zaidi na Mashekhe mbali mbali walikuwa Wamekusanyika. "Kwa kweli Mimi namshukuru Mungu kwa kunipatia Mke mwema ambaye nimemtafuta kihaki na..."Aliongea Shawali lakini hata kabla ya kumaliza Maneno yake alipaliwa hali iyomfanya mzee Ramadhani kubaini kile ambacho alikuwa anakiongea kilikuwa cha Uongo. "Jamani watu wananisema nini? maana nimepaliwa wakati naongea hii huenda ni uzuri wa mke wangu unawafanya watu waniongelee huenda mashekhe humu humu ndani"Aliongea Shawali na kufanya Mashekhe walikuwepo pale kucheka. "Huyu ni Mke halali kabsa ambae mimi nimemtafuta mwenyewe wala haya Maneno mzee wangu aliyosema siyo ya kweli ndugu zangu waislamu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mimi siwezi kufanya kama mzee huyu anavyosema kumnyanganya Frank mwanamke wakati Frank mwenyewe baba yake wanaurafiki mkubwa na Baba yangu. Mimi nilimfuata Grace na kumueleza kuwa nataka kumuoa akanikubalia. Sasa haya Maswala ya kusema nimemuondolea mtu sijui yametoka wapi haya"Aliongea Shawali kwa urefu na Mashekhe kwa kweli walimpongeza kwa kupata mke. "Kama baba yako alivyosema Shawali kama usiwe na wasi wasi kabsa. Kama huyu Mke umechangua kwa haki na unaimani Mungu ndie kakujalia basi ndoa yako itakamilika vizuri kabsa. Hayo Maswala ya kusema eti umemuondolea mke kijana frank hiyo mimi sijui. Ila kama mke huyu ni wa haki kwako basi Utamuo na kama siyo wahaki basi hiyo ndoa lazima Mungu ataipinga tu. Hata kama tukajidaidi kuilazimsha basi itakuwa ndoa ya balaa sana hata mkioana."Aliongea Shekhe Mkuu wa Arusha. Yale Maneno ya Shekhe kwa kweli yalimshitua Shawali maana alijua fika kuwa yule mke hadi kumpata pale alikuwa amefanya dhambi kubwa sana. Alifikia hadi kuua lengo ampate Mke. Alimpeleka kijana wa watu Gerezani ilikumpaata Grace hivyo yale Maneno yalimchoma sana maana yalikuwa yanapingana vikubwa. Shekhe Mkuu wa Arusha aliongea yale Maneno Makusi maana Duku duku alikuwa alishaanza kuzipata. Maana yule binti Grace alikuwa anafahamu kuwa Mume wake alikuwa ni Frank hata Kadi ya Ndoa yeye alikuwa amepewa na pia hata kwenye Matangazo ya Tv aliona. "Lazima nikumalize wewe Mzee Oska maana wewe ndio umesababisha hadi watu wamepunguza uaminifu na mimi, lazima nikuue tu hakuna namna nyingine maana unaweza kuwa kipingamizi kikubwa kwenye ndaoa yangu. Nitakuua wewe kisha nitaenda kumuua na Frank ili sasa Grace awe huru kabsa"Aliwaza Shawali kichwani haya Maneno hasa baada ya Shekhe Mkuu kukataa kuomba Dua kwa ajili ya kubariki utambulisho wa Shawali na kumtupia shekhe mwingine kuomba Dua. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Kutoka Moshi Mjini hadi Arusha maaeneo ya Usa river Goodlucky alitumia Nusu saa tu tayali alikuwa Ameshafika maana alikuwa amepanda basi kubwa ambalo lilikuwa linakimbia sana. Aliposhuka Usa river moja kwa moja alienda kwa kina Grace kwenda kumuona Grace. "Mama Nimekuja kumuona Grace yupo"Aliongea Goodlucky. "Bwana Jitambulishe kwanza wewe nani na Grace nani yako unakuja tu kumuona bila kujitambulisha. "Naitwa Goodlucky ni rafiki yake na Frank pia Grace ni rafiki yangu"Aliongea Goodluky kwa Makusi maana alijua fika mama yake na Grace anamchukia Frank. "Pumbavu sana wewe mtoto anza na shikamoo mama kisha sema mimi Goodlucky siyo mpaka rafiki yake na frank. Wewe huna shida kwangu maana nasikia ndio ulimpa mimba Grace na kufanya waachane na Frank. Asante kwa hilo pia Asante kwa kunipatia Mjukuu pia nahisi mjukuu wangu atakuwa handsome maana kasura kidogo hata wewe kapo. Ila sema nitakesha nikiomba Mjukuu wangu asifuate Umasikini wa baba yake maana hata ndevu umeshindwa kunyoa na mwili mzima unanuka Jasho. Wakati naongea naomba kaa sambamba na mimi ili hiyo harufu isinipate mbona Mkwe wangu Shawali muda wote huwa ananukia Harufu nzuri. Kweli unakosa hata elfu tano ya kununulia kansa blanka ya kulipoteza hilo liharufu. Tuachane na hayo , Grace Bwana ameenda kutambulishwa Rasmi kwa ukoo wa watu wanaonukia pesa kama mke tarajali wa Shawali. Mbona unakodoa macho ulifikilia Mtoto wangu angeolewa na watu vibudu kama kina frank au wewe. Nilimzaa kwa Uchungu Grace wangu na nilimtunza ili aje kuolewa na watu wenye pesa"Aliongea Mama yake na Grace huku akifatisha na mikono utafikilia yupo kwenye shoo. "Nashukuru sana Mungu aliponijalia kupata mama muelewa tofauti na wewe kama ningelikuwa na mama kama wewe singekuwa na muda wa kuwepo duniani maana ningekuchinja bure. Ila naumia sana kwa Mungu kumpa Grace mama taira kama huyu. Mama anayejali pesa kuliko utu wa watu. Mama anayemdhurumu mtoto wake haki na kumlazimisha kuolewa na mtu ambaye hampendi. Labda mama Grace nikwambia kitu kimoja tu ambacho kitakusaidia. Umri wako wewe umeshaenda ulitakiwa kufanya mambo mazuri ambayo yangekutengenezea njia ya kwenda peponi ila nashanga unajisafinyia njia ya kwenda motoni. Eti Mama wa Grace, Mama Gani ambaye anasubutu Kuandaaa kilio bandia ili kumfunga kijana wa watu. Mama Gani ambaye Hana Huruma na Mwanae hadi ana mwendea kwa Mganga mtoto wake. Mbona wewe mama yako hakuenda kwa Waganga ili kukudhuia ulipompenda mzee mambo. Ila nitakusifia kidogo kwa kumzaa Binti mzuri na kumlea kwa Malezi Bora hadi anafikisha miaka ishirini alikuwa bikra. Tunampenda sana Grace wako na mimi nimeenda kwa Mganga kuhakisha kuwa Grace hawezi kuolewa na shawali na kama Ikishindikana lazima Grace tumuue tu ili wewe umkose mtoto na baadae uende motoni vizuri nazani umenielewa mama yangu mpumbavu"Aliongea Goodlucky Maneno yaliyomfanya Mama Grace kubaki amemkodolea macho Goodlucky



    Kwa kweli yale Maneno ambayo aliongea Goodlucky huku akiwa yupo silius mbaya yalimuogopesha sasa mama yake na Grace. Kumbe wakati Frank akiwa anaongea Mzee Mambo naye alikuwepo ndani hivyo alikuwa anamsikiliza. "Huyo nani ambaye anaongea kibabe hapa ndani kwangu,Kijana hebu nakuomba ondoka hapa Maswala ya Grace tuachie sisi maana ndio tunaojua Uchungu wa Mtoto. Wakati namzaa Grace sikumbandika Mkataba Mgongoni kuwa ataolewa na Frank bali Mwanaume yeyote ambaye Grace angemchagua angekuwa halali yake. Sasa wewe ambae unajifanya Unajua kuchagua Mume Sahihi zaa Wako alafu umlee akue ndio ukamuozesha kwa Frank. Unatutishia Utamuua wapi bhana kabla hujamuua Grace wewe ndio utakuwa wakawanza kufa. Alafu huna hata shukrani mwanangu umempa mimba hadi sasa amekuzalia mjukuu hutaki hata kuja kumuona, hutoi hata matumizi lakini bado huna shukrani mwanaume gani wewe mpumbavu"Aliongea Baba yake na Grace Mzee mambo alipofika sehemu ambayo Goodlucky alikuwa Amesimama. "Mungu wangu mimi nilifikili Mama yake tu na Grace atakuwa taira kumbe hata baba. Bila shaka mzee na wewe mke wako tayari amekushikilia maana huyu Mama kwa Wataalamu mbaya. Ila nyinyi mmemzaa Grace lakini hawezi kuolewa sehemu ambayo nyinyi mnataka. Sasa hivi Nageuka kama Baba mzazi wa Grace na nitahakikisha na mimi anaolewa sehemu ninapotaka. Mkileta Ujinga atakufa alafu nyinyi mtabaki matasa maana mtoto mwenyewe mnaye huyu huyu Mmoja alafu mnaletea Ujinga hamnijui mimi. Ndio mtabaki matasa kweli maana hata Mjukuu wenu nitamchukua"Aliongea Goodlucky na kutoka kwa Kina Grace kwa kasi. Alipotoka kwa Grace Moja kwa moja aliamua kwenda kwa kina Shawali CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/akamwambie Ukweli kabsa kuwa huyu Siyo mke wake. Kutoka kwa Grace hadi kwa Mzee Ramadhani haikuwa mbali sana ukifikilia alikuwa Amekodi na Boda boda. Alipofika aliweza kuingia kwenye nyumba ya kina Shawali bila tatizo lolote maana hata Mlinzi alijua ni moja ya watu ambae walialikwa kuja kushuhudia Jinsi Shawali alipokuwa anamtambulisha mke wake. Hata Alipofika ndani aliweza kukaa bila mtu kumshitukia Shawali alimuona lakini yeye alikuwa hamfahamu kama yule ndio Goodlucky. Grace yeye alimuona ila wala hakuwa na shida wala kushituka aliona kama kitu cha kawaida tu. Wakati Shawali akiwa anajinadi kama huyu ni mke wake wa haki wala hajamuondolea mtu yeye alikuwepo tu pale anamsikiliza. Hata baba yake na Frank mzee Oska akiwa anaondolewa baada ya kulizusha Goodlucky alikuwa yupo tu anawasikilizia. Baada ya watu wote kuonge ndipo na Goodlucky uvumilivu ulimshinda aliamua kuongea machache maana maneno ambayo aliongea shekhe wa Mkoa wa Arusha yalimgusa sana. "Ndugu zangu na mimi ninaneno moja ambalo nahitaji kuchangia kwenye hii ndoa ya kinafiki ambayo najua kamwe haiwezi kufanyikiwa. Na kama hii ndoa itafosiwa ili kukamilika lazima mtu Mmoja afe" Aliongea Gooducky baada ya kupewa nafasi na watu wote walikuwepo pale waligeuka huku wakiwa wanamshangaa na kusikiliza kwa Makini. "Ndio nasema hii ndoa ya kinafiki ninaama yangu maana Mwanamke hajakubali kutoka moyoni kalazimishwa na mama yake kwa kumwendea kwa Mtaalamu. Mume anayeoa analazimisha maana amempeleka kijana wa watu Jela bila hatia lengo eti yeye amuoe huyu Mwanamke. Siyo kumpeleka Jela Frank tu bali Amesubutu hadi kumuua Afande wa watu kwa kumtumia Majambazi baada ya Kumuona yule Afande anampango wa kumtoa Frank Magerezani. Mzee Ramadhani nasikitika sana wewe mzee unayehishima kwa Roho nzuri lakini Mwanao anakuwa anati..."Aliongea Goodulcky lakini hata hajamaliza kuongea alishangaa mzee ramadhani anaanza kufoka na kusema atolewe nje. "Naombeni toeni na hii takataka nje mtoeni kabsa hivi hawa watu wametumwa kuja kuharibu ndoa ya Mwanangu. Shawali Mwanangu ndoa Ngumu sana hivyo Changamoto kama hizo lazima uzipitie ila usijari baba yako yupo bega kwa bega na wewe"Aliongea Mzee Ramadhani. Kitu ambacho alikuwa anakitaka mzee Ramadhani ni kuhakikisha Mwanae asigundue kama hata baba yake ameshitukia mchongo. Shawali yeye aliposikia na Good kafokewa yeye alifurahi sana hakujua kama Mzee alikuwa anamsoma na kumpangia kufanyia kitu cha kinyama ambacho kingemtia aibu. Mzee Ramadhani alipomtoa Goodlucky ndani alimkabidhi tena mfanyakazi wake Juma na kumwambia ampeleke hadi kwa mzee Oska atawakuta huko ili waweze kuongea. Baada ya Utambulisho ambao ulijawa na maswali mengi kwisha shawali waliondoka na Mpenzi wake Grace huku wakiwa na raha mbaya. "Baby Najua ni Frank tu anafanya hivi, kawatuma watu wake lakini wameshindwa. Sasa twende tumkute huko huko Gerezani kumwambia kuwa watu wake aliyowatuma wameshindwa"Aliongea Grace huku akiwa anamlalia Shawali. Yale Maneno ya Grace kwa kweli yalimfanya shawali kufurahi sana na kugeuza gari kuelekea Magereza. Shawali pia alishangaa sana mwanamke ambaye alikuwa hamtaki na alikuwa anamlilia Frank Gerezani leo hampendi Frank anampenda yeye. Maneno ya Goodlucky kuwe Mama yake na Grace alimwendea Grace kwa Waganga nayo yalimfurahisha maana aliona yule mama alimsaidia vyakutosha. Mwende wa Nusu saa tayari walikuwa wameshafika Gerezani na kwenda kuomba kituoni waongee na Frank. Gerezani Frank bado alikuwa anakaa kwa hara tu na hii kazi alikuwa anafanya baba yake na Shawali mzee Ramadhani. Frank alipokuja na kumuona yule ambaye alikuja kumuona alikuwa ni Grace kwa kweli alifurahi sana na kumshukuru mungu. Alipoangalia kwa makini tena alishituka sana alipomuona na mbaya wake akiwa pembeni mwa Grace. Kwa haraka haraka alihisi labda shawali naye alikuwa amekuja kumuomba msamaha. "Mpenzi wangu upo kwa kweli siamini macho yangu vipi upo mzima. Mbona mpenzi wangu umemaliza siku nyingi bila kuja kuniona kuna tatizo gani vipi ulijifungua Salama maana Mwaka sasa"Aliongea Frank mambo mengi huku akiwa haamini kama yule ambaye alikuwepo pale alikuwa ni Grace. "Ndio Frank Mimi nimejifungua Salama na sasa hivi mtoto karibia anataka kuanza kutembea. Lakini wewe haina haja ya kumuulizia yule mtoto maana uliikataa ile mimba wakuulizia hali ya mtoto ni Good lucky na Shawali. Hata hivyo siyo hicho ambacho kimenileta hapa kilichonileta hapa ni kukutarifu wale watu ambae unawatuma kuja kufelisha ndoa yetu na Shawali wameshindwa. Ndio tena waambie wajiandae kufa maana wanafanya vitu kinyume na oda yetu. Alafu hata wewe umenifanyia kosa sana kuniita mimu mpenzi wako maana umeamua kuniabisha mbele ya Mpenzi wangu shawali. Hivyo kwa kuniita mpenzi wangu mbele ya mume wangu shawali ni kosa kubwa sana ambalo linafanana na kubaka. Hivyo na wewe Jiandae kufa maana nikikuacha utaniita tena. Baby hebu naomba Mwambie lini utakuja kumuua huyu malaya"Aliongea Grace kumwambia Frank kisha alimbusu Shawali mbele ya Frank. "Baby mimi nakusikiliza wewe hata ukisema hapa hapa nimuue mimi naua tu na wala siwezi kufanywa kitu chochote. Pesa zitatumika kuwazima Afande wa chache hapa Gerezani na kesi tutaangalia mfungwa Mmoja anatupiwa"Aliongea Shawali huku akiwa anamwangalia Frank kwa Dharau. "Ok basi huyu nakuomba Muue baada ya kumuua baba yake pamoja na Goodlucky. Ukishamaliza kazi ya kuwaua wale watu ndio Utammalizia na huyu kenge"Aliongea Grace na kuanza kuondoka. Kwa kweli yale Maneno ya Grace yalimchanganya Frank na kushindwa kuelewa kuna nini kinaendelea hadi kimemfanya Grace kumgeuka hivi.



    Bado Frank alikuwa haamini kabsa Mwanamke ambaye alimpenda na kukaa naye kwenye mahusiano karibia miaka kumi upendo wao ukizidi kuongezeka leo hii yule yule alikuwa na Mpango wa Kumuua. "Shawali Naomba Usimguse baba yangu Mwache kama Alivyo, Kama Ukimgusa baba yangu kwa kweli kitu ambacho nitakufanyia hadi Dunia itashituka. Umeshamchukua mpenzi wangu haya Ponda naye Raha ila kwa baba Yangu Kaa mbali. Umemuua Afande Joshua sijafanya kitu lakini mzee wangu naomba Mwache kama alivyo"Aliongea Frank huku akiwa anatetemeka mbaya. Yale Maneno ambayo Frank aliongea wala Shawali hayakumshitua zaidi alimgeukia na kuanza kumcheka. "Unaogopa kuona baba yako Atakufa, Acha Ujinga wako sasa unafikilia kama mzee wako ananiharibia Njia yangu unafikilia nitampa zawadi Gani zaidi ya kifo. Sasa naenda kumuua baba yako ili unifanyie kile kitu CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/kibaya alafu Dunia ishituke"Aliongea Shawali kisha hakutaka tena Kupoteza Muda wa kuendelea kukaa Pale Magerezani na kuondoka. Kwenye kichwa cha Shawali kweli yeye ambacho alikuwa Amekipanga ni kuwaua hawa Watu watu. Yeye alijua kama Atamtuliza Goodlucky, Mzee Oska na Mwanae Frank basi ndoa yake ya kumuoa Grace ingepita bila utata wowote. Bado Hakujua kama Mzee wake naye alikuwa anajua na alikuwa na Mpango mbaya juu ya Mwanae. Hakujua kama Kuna Afande Mwingine Anaitwa Sophia alikuwa kwenye operation Kabambe ya Kuhakikisha watu wote waliohusika na kifo cha Afande Joshua wanakamatwa. Baada ya Kumaliza Kikao cha Kumtambulisha Grace kwa Ukoo wa Mzee Ramadhani na Grace wakiwa na Shawali kuondoka ndipo walimuachia Upenyo na Mzee Ramadhani kwenda kuongea na Mzee Oska pamoja na Goodlucky. "Ndugu zangu mimi najua kama Mwanangu ni mbaya tena Mnyama lakini mlitakiwa kufanya hiki kitu kwa Siri sana. Mnatakiwa Msiongee kwani hata mimi kuna kitu ambacho nahitaji kumfanyia Mwanangu ambacho kitakuwa cha aibu kwake pia kumpeleka Gerezani. Mimi nahitaji ndoa kama kawaida tutaendelea kuandaa ila naenda kufanya Mishe zangu na Frank kutoka Pale Gerezani akishatoka kwenye siku ya Harusi atakuwepo na yeye Frank ndio ambae atamuoa Grace wala siyo Mwanangu shawali Maovu yote aliyofanya yatagundulika na kukamatwa"Aliongea Mzee Ramadhani baada ya kukutana na Goodlucky. "Mzee Wazo lako ni zuri lakini pia lina Ugumu wake. Sawa unataka kwenye hiyo Ndoa Frank ndio ambae ataoa lakini ataoaje wakati Grace yeye atakuwa hamtaki. Mama yake na Grace wamemuendea Mwanae kwa Mganga hivyo anamchukia vibaya mno Frank"Aliongea Goodlucky kumwambia yule Mzee. "Swala la Grace kumchukia Frank hilo Achana nalo sisi tunaangalia Moyo wa Grace si ulikuwa unampenda Frank tutamuozesha hata kwa Nguvu alafu mambo Mengine yanafuata. Tusiwe Waongeaji Sana Muda huu tunatakiwa Kuondoka tukamuone Frank kwa Mara ya kwanza tangia Afungwe ili tupange namna ya kumtoa Pale"Aliongea Mzee Ramadhani na wote walikubaliana maana hawakuwa na Muda wa kuendelea kupoteza waliondoka kuelekea Gerezani kumuona Frank. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Gari aina ya MURANO ilikuwa kwenye Mwendo kasi wa Hatari. Ndani ya ile Gari kulikuwepo na Afande Sophia ambaye alikuwa na Kisasi cha kuhakikisha watu wote ambao walimfanyia Unyama mkuu mwenzake wa kituo Joshua wanakamatwa. Tayari alikuwa anajua kabsa watu ambae walikuwa Wameshiriki ila alikuwa anahitaji Ushaidi wa kutosha wa Kukamilisha Kesi ya Kumpeleka Mkuu wa Jeshi la Polisi mahakani na kufungwa. Gari yake mpya ambayo ilikuwa haijamaliza hata Mwezi tangia ainunue ilikuwa inatesa sana Barabara. Kichwa chake kilikuwa kimevurugika kuona Watu ambae wamewekwa kutetea haki za binadamu ndio wale wanawatesa. Tena wanatesa innocenty people tena Masikini ambae hawana kitu. Tayari Sophia alikuwa Amewasiliana na Suzani pamoja na Aisha kwa kuwarudisha Arusha ili Kuja kumalizia kazi yake. Alijua kupitia Suzani ambaye alikuwa Mpenzi wake na Afande Joshua atafahamu mtu ambaye alihusika na kifo cha afande Joshua. Pia kupitia Aisha na Suzani Angetumia kama Mtego kuwakamata Wahusika wengine ambao wanashirikiana na wakuu wale. Alijua Watu waliomua Afande Joshua wakiwaona Suzani bado wazima wakati waliwateka na kuwapeleka kwenye shimo watashituka na kutaka kuwaua tena ili kuficha siri yao hapo ndipo sasa angeweka mitego yake na kuwakamata. Kwa Mwendo ambao Gari ya Afande Sophia ilikuwa inakimbia Muda wa Nusu saa tayari alikuwa Moshi mjini. Alipofika Moshi mjini alinyoosha Moja kwa Moja hadi Makondeko ambako alielekezwa. Alipofika kwa kina Aisha aliwachukua na Safari ya kurudi Arusha tena ilianza. Wakati Mzee Ramadhani wakiwa wanaenda Magerezani walipishana njiani na Kina Shawali wakiwa wanarudi ila sema Mzee Ramadhani aliwaona ila Mwanao alikuwa hajamuona. Walienda Moja kwa Moja hadi kituo cha polisi na kwenda Kumuona Frank. Kumbe wakati wakiwa Wanaingia kuna Afande Mmoja alikuwepo pale Magarezani naye alikuwepo wakati wa kumuua Afande Joshua na yeye akishirikiana na Wenzake ndio ambae waliwapeleke Goodlucky kwenye shimo. Hivyo alipomuona Goodlucky akiwa Mzima alishituka sana maana yeye alihisi kuwa amekufa. Frank kwa kweli Alipomuona baba yake pamoja na Goodlucky wamekuja kumtembelea Alifurahi sana. "Baba na wewe umeshanisaliti kama Grace maana mwaka sasa sijakuona hata Hukuwa unakuja kunisalimia. Goodlucky kwa Nini ulikuwa kimya hivi hebu niambie kuna kitu gani kimemkuta grace hadi kanisaliti"Aliongea Frank huku hadi machozi yakiwa yanamtoka. "Frank wazazi wako hawajakusaliti ila mimi ndio niliwaambia kuwa wasije kukutembelea mara kwa mara maana hawa watu wangejua huenda wanataka kukutoa. Ila mimi ndio nilikuwa nafanya mambo huku ndio maana ulikuwa unakaa kwa raha humu ndani. Sasa mimi ninampango wa kukutoa hapa na wewe ndio utamuoa Grace na wala siyo Mwanangu shawali. Lazima umuoe Grace hata kama hakutaki. Najua utauliza kwa nini Grace amebadilika wakati mahakamani alikuwa anakulilia. Mama yake Grace alienda kwa Mganga na kwenda kumzindika ampende mwanangu hivyo alifanikiwa. Hivyo wewe usimchukie Grace kwa kuwa hana Hatia"Aliongea Mzee Ramadhani.





     Kwa kweli yale Maneno ya Mzee Ramadhani yalimshangaza Sana Frank. Kweli Frank alipokumbuka hata Majibu ambayo Grace alikuwa anampa akifikilia na jinsi alivyokuwa anamlilia Mahakamani alibaini kweli mama yake atakuwa Amemwendea kwa Mganga Grace. "Sasa Goodlucky kwa nini na wewe Usiende kwa Mganga ili Grace arudiwe na Fahamu zake. Hivi Unajua ni kiasi gani nampenda mke wangu. Goodlucky wewe ndio uliyembaka mke wangu hadi tukapelekeana kufika huku sasa mimi nilishakusamehe lakini kwa nini umeshindwa kwenda na wewe kwa Mganga ili mke wangu awe kwenye hali ya kawaida"Aliongea Frank huku akiwa amechanganyikiwa. Yale Maneo ya Frank kwa kweli yaliwafanya wazee wote Mzee Ramadhani na Oska kubaki wakiwa wanamwangalia Good maana walikuwa Hawajui kama Good ndio aliyempa mimba Grace na kufelisha ndoa yao. "Frank hayo mambo tulishayamaliza na tayari umeshanisame. Grace Amejifungua Mtoto wa kiume na Jina nitamwita Frank kama njia ya kukuthamini kwa msamaha ulionipa. Sawa nitamwita tu hivyo ingawa sijawahi kumuona tangia alivyozaliwa. Pamoja na hayo Frank mimi nilienda hadi kwa Mganga na hadi wakati anapewa dawa nilikuwa nasikiliza alitakiwa kuziweka kwenye kitanda. Ambacho nilifanya mimi ni kumpigia simu Grace kumtaarifu lakini bahati mbaya akawa hapatikani. Nikaamua kuondoka pale kwa Mganga na kumuacha Mama Grace pale ili niende hadi kwa Grace nikamwambie lakini bahati mbaya tax ambayo nilipanda ilipata ajali na nimejikuta kwenye fahamu siku mbili mbele na tayari nilikuwa nimeshachelewa. Baada ya kupona nilienda tena kwa Mganga kumueleza ila aliniambia nimechelewa. Pia amenisaidia kwa kuondoa lile zindiko baada ya mwaka ndio Grace akili yake itarudi sasa huo muda tayari grace atakuwa ameolewa"Aliongea Goodlucky kwa kina na Frank alimuelewa. "Ok sawa nimekuelewa ambacho nimepanga mimi nahitaji kuachana na Grace na nitafute Mwanamke mwingine nikitoka Jela. Sioni haja ya kugombania mwanamke mmoja wakati wengine wapo kibao. Ila Goodlucky naomba kuwa makini na umlinde baba yangu maana wanataka kumuua. Pia Mzee Ramadhani wewe mwache Shawali amuoe tu Grace na Mwambie asimuue baba yangu kama alivyosema maana tayari mke nimemwachia. Shawali kaja hapa na Grace wamesema eti niliwatuma baba yangu na Good kuja kuharibi ndoa yao na sasa wataniua na mimi pamoja na Baba yangu. Mzee Ramadhani kamwambia Shawali Aje aniue mimi lakini wazee wangu awaache maana hawana hatia"Aliongea Frank huku hadi machozi yakiwa yanamtoka. "Frank nakwambia baba yako hatakufa na Grace lazima umuoe. Mwanamke huyu umesota naye sana hata tukimwachia Shawali itakuwa siyo vizuri. Hakuna kurudi nyuma ni ubabe ubabe uzuri mzee Ramadhani anatusapoti hivyo lazima umuoe Grace na Shawali lazima afungwe"Aliongea Good naye kwa hasira. "Frank mimi ndio nimemzaa Shawali na nimesema Grace utamuoa wewe na hakuna mtu ambaye atakufa tena. Chamuhimu huku Gerezani utakuwa kwenye wakati Mgumu. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Nitaongea na Mkuu wa Gereza ili utoroke na hiyo siku atawaweka askari wake ili hata ukitoroka pasiwepo na watu wa kukuzuia. Ukishatoroka utakuja kukaa kwangu hadi siku ya Harusi ndipo utatoka. Siwezi kukubali mtoto wangu akatumia wizi kuoa mke ambaye siyo sahihi"Aliongea Mzee Ramadhani. Hiyo Siku kwa kweli waliongea Vitu Vingi sana na hatimae walimuacha Frank na kuondoka huku wakiwa na imani kuwa kazi yao itafanikiwa Vizuri. Wakati Mzee Ramadhani wakiwa wanaongea na Frank yule Afande tayari alishampigia Mkuu wa Jeshi la Polisi na kumpa taarifa kuwa wale watu ambae walienda kuwatupia kwenye shimo mmoja hajafa na amemuona yupo kituoni. Yale maneno ya yule Afande kwa kweli yalimshitua Mkuu wa Jeshi la Polisi na kuhisi huenda wote hata Mke wake na Afande anaweza akawa hajafa kitu ambacho kitaleta hatari kubwa. Ambacho alikifanya Afande Mkuu wa Jeshi la Polisi Bwana Sikujua ni Kuagiza watu wake kwenda Hadi nyumbanI Kwa Marehemu Afande Joshua kuchunguza kama mke wake na Afande Joshua atakuwa Mzima. Kwa bahati mbaya wakati Afande waliotumwa na Afande Sikujua mkuu wa jeshi la Polisi kwenda kuchunguza nyumba ya Afande joshua na kuangalia mke wake kama yupo ndio Siku na Afande Sophia alikuwa anarudi na na Mke wake na Marehemu Joshua. Walipofika tu nyumbani hata kabla ya kuingia ndani afande walifika na kukutana ana kwa Ana na Suzani. Wale Afande wala hawakumfanya kitu chochote zaidi walisema wapo wanachunguza kuhusu kifo cha Joshua kisha baada ya Muda waliondoka. Pia wale afande Walimuona Sophia lakini hawakujua kama na Sophia alikuwa ni adui yao "Hawa Watu wametumwa na Kama wamejua wewe ni mzima lazima watakuwa na plan za kukuua sasa hapa ndio kazi yetu inaanza kuwa rahisi. Kitu cha kwanza twende chumbani ambako utakuwa unalala tutategesha camera chumba kizima. Pia nitakuwekea ulinzi wa kufa mtu maana lazima watakuja kukuua. Sasa wakija kukuua ndipo tutawakamata na Kazi itaanza"Aliongea Afande Sophia huku wakiwa wanaingia ndani.





    Walipoingia ndani afande Sophia alikuwa yupo full alitoa Mkoba wake na kuanza kufunga Camera taratibu tena kwenye sehemu ambayo itachukua matukio yote vizuri. Alifunga camera tatu vizuri na kuziweka On. "Sasa kinachotakiwa wewe hakikisha hutoki kwenye hiki chumba muda wote ili kama watakuja hili tukio lifanyike huku. Hawatakuua ila tunataka kuchukua Ushahidi tu na pia kupitia hizi Camera na mimi nitategesha kwenye compyuta zangu ofisini chochote nitakuwa naona. Hivyo nikiona kama hawa watu wameingia baada ya Maongezi nitawapigia Simu Afande wangu wa Ulinzi ambae nawaleta siyo Muda na kuwafungia Humu humu ndani kwenye chumba kingine ndio watakuja kukuokoa. Aisha wewe hakikisha huyu mtu asitoke kwenye hiki chumba maana tukio likitokea nje ya chumba hiki mimi sitaweza kuona na mwenzako atauawa bila kupata ushaidi wowote. Wewe kila kitu mletee hapa hata kunya mwanadalie ndoo anyee humu maana hatujui saa wala dakika hawa wapumbavu watakuja"Aliongea Afande Sophia maneno yaliwafanya wote kukubaliana na ile plan kwani ilionekana kuwa inafaa. Baada ya Maongezi Afande Sophia aliondoka Moja kwa Moja hadi Kwenye kituo chake cha kazi kambi ya pili. Alipofika kule aliangalia compyuter zake na kutegesha kweli ziliungana vizuri na kubahatika kuona kila kitu ambacho kilikuwa kinaendelea kwenye chumba cha suzani. Baada ya kuhakikisha mambo yalienda vizuri aliwaita Afande wake wa kazi ambao alikuwa anawaamini na kuanza kuwaelezea. "Huyu mama ndio ambae Mume wake alikuwa Mkuu wa kituo cha Majengo na aliuawa na afande wenzetu kama nilivyowaelezaga. Sasa baada ya Mwaka kupita ndio kazi tunainza hivi, huyu mama sasa hivi anaatafutwa kuuawa maana wanajua kama anajua siri ya kifo cha mume wake na Anajua mtu ambaye alimuua mume wake. Nimetegesha hizi Camera na kuunganisha na hii Compyuter ili kuweza kuona tukio zima ambavyo litaenda. Hivyo Afande kumi nawapeleka Sasa hivi hadi kwenye hiyo nyumba na mtaenda kukaa chumbani kingine. Nyinyi mtakaa hapo hadi hii misheni ikamilike. Hata Kama itamaliza Mwaka hamtatoka maana nauhakika hawa Watu lazima watakuja kumuua. Siku wakija mimi nitaona kupitia huku na nitawashitua mkawakamate. Tukifanyikisha kuwakamata hawa watu tukacheza mchezo mzuri na mkuu wa jeshi la polisi kufungwa sisi lazima tutapanda vyeo na kuwa watu wakubwa hivyo hii ndio nafasi na siyo ya kuichezea."Aliongea Afande Sophia na Afande wote walikubali na kushangilia kuona walikuwa na mkuu mpenda haki na anayetumia akili ya kuzaliwa. Muda huo huo Sophia akiwa na Afande wake kumi waliondoka kuelekea kwa kina suzani. Njiani walinunua na vinywaji pamoja na chakula ambacho watakuwa wanakula huko. Walipofika walionyeshwa chumba ambacho kilikuwa karibu tu na chumba ambacho alikuwepo Suzani na kuingia. Aisha yeye ndio alipewa Jukumu la kuwapikia wale Afande kumi. Muda ule kwa kweli Aisha alishasahau kabsa kama alikuwa Mwalimu. Alijitoa kusaidia maisha ya frank. Baada ya mambo kuenda Safi Sophia naye alirudi hadi kituoni na kukaa kwenye compyuter yake na alitakiwa Muda wote awe pale maana yeye ndio angewapa taarifa Afande kama wale watu ambae wangiingia mle kumuua Grace wangeshafika. Hata kula kwa kweli chakula alimpigia tu mwanae awe anamletea pale. Baada ya wale Askari waliotumwa kwenda kupeleleza nyumba ya Afande Joshua na kukuta Suzani yupo walimpelekea Majibu mkuu wao. Yale Majibu yalimchanganya sana Mkuu wa jeshi la Polisi Arusha bwana Sikujua. Hiyo hiyo Siku alimwita Shawali na Kupanga Namna ya kumuua Suzan pamoja na Goodlucky. "Kwanza kabsa idadi ya watu ambao inatakiwa wauawe hadi sasa wapo watano na siyo watatu tena. Hawa watu tukiwauwa basi kuhusu harusi yangu itakuwa safi sana na kuhusu kuogopa siri itatoboka itakuwa hakuna tena. Ndio sasa hivi siyo Goodlucky, Suzani na iasha tu wanatakiwa kuuawa sasa hivi na Frank pamoja na baba yake lazima tuwauewe. Sasa hapa tutapiga Ndege wawili kwa wakati Mmoja na kama tukifanyikiwa hii kazi kila mmoja milioni tano nitamuingizia kwenye Acount yake. Afande Koboko wewe ndio ulihusika na kifo cha afande Joshua hivyo mambo yatakuwa Magumu maana huyu mama anakujua. Hivyo wewe utaongozana na wenzako kesho kutwa utaenda kumuua yule mama tena mchana kabsa maana hakuna ambaye watawashitukia maana nyinyi ni Polisi. Mimi pamoja na afande watatu tu ambao mtanipa watatosha Sana kwenda kumuua Goodlucky pamoja na Mzee Oska maana CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Goodlucky wapo na Mzee Oska. Tayari ninakazi rahisi ya kuweza kuwapata kirahisi na kuwamaliza kimya kimya. Nikishawauwa hawa watu basi moja kwa moja naenda kummaliza Frank. Yani wewe mkuu usiguse kitu subilia tu kusikilizia Kazi ambayo tunaenda kuikamilisha kisha ndoa inafuata"Aliongea shawali na kila Mmoja aliafika hawakuwa na Muda wa kuendelea kuongea zaidi walitawanyika huku wakipanga keshokutwa saa sita kazi ya kuanza kuua inatakiwa kuanza. Siku hiyo Afande Sophia alikesha bila kulala tukio lile wala halikufanyika. Siku ya pili yake naye aliweza kukaa hadi saa kumi usiku lakini hakuna kitu ambacho kiliendelea. Hatima usingizi ulimpitia na kulala maana kukaa siku mbili bila kulala ilikuwa kazi ngumu sana. Siyo yeye tu hata Afande huku siku hiyo usiku mapema tu saa tano wao walikuwa wameshalala. Siku Moja kabla ya tukio kufanyika shawali tayari alishapanga mbinu za kuweza kuwapata Goodlucky. Ambacho alikipanga ni kwenda kuiba simu ya Baba yake na kuweza kuwasiliana nao na kuwaambia waonane sehemu. Alijua kupitia simu ya baba yake mzee Oska lazima angekubali kuonana na mzee Ramadhani maana walikuwa marafiki sana. Kweli kesho yake Mida ya Saa nne Shawali alimuotea baba yake alipoenda kuoga akachukua simu yake na kumpigia simu mzee Oska. Mzee Oska na uzee wake maskini wa Mungu wala hata hakuweza kubaini kama ile sauti haikuwa ya Mzee Ramadhani. Hivyo alivyoambiwa wakutane kwenye hotel ya Mileniuam iliyo usa river yeye wala hakukataa kabsa zaidi alimwambia Goodlucky ajiandae waondoke. Upande wa Afande Koboko na yeye tayari alikuwa na team ya watu watano walikuwa wapo kwenye Gari kuelekea kwenda kummaliza suzani bila kujua kama kulikuwa na Mtego hatari umewekwa.





    Kaboko alikuwa anaenda kwenye tukio huku akiwa na hasira mbaya alikuwa anahitaji kuhakikisha anamuua kabsa Suzani ili kufuta ushaidi kabsa ambao alihisi yule mama akiutoa basi atakuwa Matatizoni. Wakati Koboko akiwa anaenda kummaliza Suzani pamoja na Aisha huku nako Mkali wa pesa Bwana Shawali alikuwa anaenda kuonana na Mzee Oska baba yake na Frank pamoja na Goodlucky anawamaliza kisha anaenda kumuua na Frank. Wote wakiwa wapo safarini huku nako tayari Afande sophia alikuwa ameshaamka na macho yalikuwa kwenye compyuter hivyo Koboko muda ule alikuwa hana bahati labda mwenzake Shawali. Tayari Sophia alishawaamsha Afande wake na kuambia wakae sawa ingawa hakujua kama tukio lingetokea muda ule ingawa yeye kama machale tu yalimcheza na kuwapigia Afande wake na kuwaambia wakae sawa. Mzee Ramadhani baada ya kutoka bafuni kuoga na kwenda hadi chumbani kwake akavaa vizuri na kurudi sebureni alikuta simu yake kama imehama sehemu ambayo alikuwa ameweka. Alipoangalia simu yake ndipo alikuta kuna namba imepigiwa na mbaya zaidi ilikuwa ya mzee Oska. Kwa kuwa mle ndani kulikuwa na Mwanae tu wasiwasi ulianza kumjia. Kwa kasi ya Ajabu Mzee Ramadhani alipiga Simu kwa mzee Oska kumuuliza kama kuna mtu alikuwa amempigia bahati mbaya hakuwa anapakitana kumbe mzee Oska naye alikuwa yupo Safarini kuja arusha kuonana na mzee ramadhani bila kujua hakuwa mzee Ramadhani. Baada ya Mzee Ramadhani kupiga simu kwa Mzee Oska na kutompata hewani aliamua kumpandia Mwanae na kumuulizia kwa nini ametumia simu yake kumpigia mzee Oska "Baba utanisamehe kweli kutumia Simu yako bila Ruhusa. Nimeamua kumpigia Mzee Oska na kumuomba tuonane nimwelekeze kuwa mimi sihusiki kufungwa kwa Frank. Si unakumbuka baba kuwa mzee Oska aliondoka huku akiwa na hasira. Simu yangu ilikuwa haina vocha ndio maana nimtumia yakwako"Aliongea Shawali kumwambia baba yake hasa alipopigiwa simu. Yale Majibu ya Shawali kwa kweli yalimshitua baba yake maana kwa mtoto wake alivyo na pesa ilikuwa siyo kawaida kukosa vocha. Alikumbuka na Maneno ambayo Frank alimwambia kuwa baba yake anataka kuuawa na Shawali ndio alizidi kuchanganyikiwa. Alihisi tayari mwanae alikuwa anaenda kumuua Mzee wa watu bila hatia. Mzee ramadhani alirudia tena kupiga simu lakini simu ilikuwa haipatikani. Koboko hakuwa na kazi ngumu hivyo aliweza kwenda hadi nyumbani kwa Afande bila kushitukiwa alipofika aligonga na Aisha ndio alimfungulia. Aisha alipomwangalia Afande Koboko alishituka sana Maana alimfahamu ndio Afande ambaye alimchoma kisu Joshua hadi kumuua bila huruma. "Unashituka nini nimekuja kumaliza kazi yangu ya kuwaua. Ila kwa kuwa wewe ni mtu wa kwanza kuniona naweza nikakupa angalau miezi mingine mitatu ya kuweza kuwa hai ila kama utafanya haya yafuatayo. Nahitaji unipeleke sehemu ambao yupo Suzani haraka"Aliongea Afande Koboko huku akimsindikiza na kibao Aisha. Kile kibao kwa kweli kilikuwa cha Aina yake ambacho hadi Afande kiliwaashitua na Kuhisi sasa tayari inawezekana kazi inahitaji kuanza. Kwa kweli Aisha alipoambiwa vile alishukuru Mungu na kuwaongoza moja kwa Moja Afande hadi kwenye chumba cha Suzani maana kule ndiko alihisi kuna Pona pona yake. Walipoingia tu chumbani Afande Sophia aliwaona na kuhisi tayari kazi yake imekamilika. Hivyo kwa Haraka aliwapigia Simu Afande wenzake na kuwaambia tayari wauaji ambao ni askari wameshaingia ndani hivyo atawajulisha muda wa kwenda kuvamia ila kwa sasa walitakiwa kutulia kwanza hadi awajulishe. Tena uzuri ambacho alikifurahi Afande Sophia wale Askari wote walikuwa Hawana Bunduki koboko tu ndio alikuwa na Bunduki. Suzani alipomuona Koboko kwa kweli hadi Machozi yalianza kumtoka maana alikumbuka jinsi Koboko alivyamua mume wake hasira. "Inamaana Baada ya kumuua Mume wangu Bado hujatosheka tu unakuja kuniua na mimi. Wewe ni Afande Gani sasa ambae unauwa watu wasiokuwa na hatia. Tambua kama Mungu hapendi maana hata ulipotutupia kwenye shimo bado tulitoka wazima"Aliongea Suzani huku Machozi yakiwa yanamtoka. Yale Maneno ya Suzani yalimfanya afande Sophia kushituka huku pembeni akiwa anafurahi maana tayari alikuwa ameshamjua mtu ambaye alikuwa amemuua Afande Joshua. Ambacho alikuwa anakiomba Muda ule yule mtu kuthibitisha tu kama kweli alimua. " Sasa kama mume wako amekufa wewe utabakije huku duniani. Huoni mume wako huko atakuwa Mpweke hivyo lazimfa nikuue Suzani umfuate Mume wako. Kweli mimi ndio nilimuua Afande Joshua kwa kuwa hadi CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Mkuu wa Jeshi la polisi arusha alimwambia aache kufatilia Kesi ya Frank ni ya watu wakubwa lakini bado hakutaka. Afande Rama naomba Kagueni kwenye hiki chumba cha Afande joshua kama kuna ushaidi wowote aliacha mlete hapa "Aliongea Afande koboko. Alipoongea vile yale maneno sasa ndio sophia alifurahi zaidi na kuwambia Afande wake wakavamie na kuwakamata wote. "Sawa Mimi nitakufa kwani nahamu kweli ya kwenda kumuona mume wangu. Ila kabla sijafa nakuomba nipe fair kidogo tu ya kuweza kunijibu maswali yangu. Kabla hujaniua naomba niambie kwanza ni nani ambaye alikupa oda ya kumuua mume wangu. Maana wewe mume wangu haja kukosea wala hujamkea lazima kutakuwa na mtu kakutuma"Aliongea Suzani lengo kuzidi kumchelewesha Afande koboko asimuue na awahiwe na wale afande wa Sophia. "Wewe Mwanamke bwana Jasiri sana na ulipaswa kuwa mke wa afande kweli. Kweli mimi nimepewa oda na hiyo oda imetoka kwa mkuu wangu afande Sikujua. Pia mdhanimi mkuu wa kifo cha mume wako ni shawali yeye ndio amemwaga pesa za kuhakikisha mume wako anakufa lakini hata hivy.."Aliongea Koboko hata kabla hajamalizia alishanga Afande wakiwa wanakuja na Mmoja alifyatua risasi lakini Koboko aliwahi aliruka na Kumshika Suzani na ile risasi ilienda kumpiga Suzan





     Baada ya Askari Kumkosa Afande Koboko Risasi kisha kumpiga Suzani Waliona Sasa Wanawakati Mgumu wa kuweza Kumkamata Koboko maana kwa Jinsi ambavyo alikwepa Ile Risasi na kumtega Suzani alionekana alikuwa na Utalaamu wa kiaina. Ambacho aliamua Afande MUSSA ambaye ndie alikuwa Kiongozi wa lile kundi ni kutumia akili ya kuzaliwa. Kwanza Walikuwa na Inshara yao hatari ya kubadilisha missioni pindi tu wanapoona ile ya kwanza imefell. Kwanza alikanyaka chini kwa kishindo Inshara ya kuwaambia wenzao Misheni inabadirika. Kitendo cha Kukanyaga chini Wale afande wenzake walielewa na kushusha Silaha zao chini kisha Kukanyaga na wao chini na kutoa Salute kusubiri Mpango wa Faster ambao Ungetolewa na Afande Mussa kuhakikisha wanamkamata Afande Koboko bila kusababisha kifo. Walipokanyaka na kutoa Salute taayari walimpunguzia Plesha Afande Koboko maana aliona kama ametolewa heshima kumbe wenzao ile ilikuwa ni njia ya Kubadilisha Misioni kwa tayari walikuwa wameshapanga kama Wakifell njia ya kubadilisha missioni ingekuwa ile. "Afande Koboko Samahani Bwana kidogo tukushambulie. Hii kazi ambayo unaifanya imegundulika kuna Afande wengine wanahitaji kuja kukukamata hivyo Afande Mkuu wa Arusha Ametuongezea Sisi Kuhakikisha unakuwa Salama Mkuu wangu"Aliongea Afande Mussa huku akisogea ndani ya kile chumba. "Afande Koboko aliposikia yale Maneno ilibidi Kumwachia Suzani ambaye Muda ule alikuwa amepigwa Risasi na bahati nzuri ilikuwa imempiga begani. Aliamini kabsa kweli Wale wanaweza kuwa Watu ambae Wametumwa na Mkuu wake kwani ilikuwa vigumu kugundulika kama alikuwa kwenye misheni za kwenda kuwauwa suzani na Aisha. "Pumbavu wakati Mwingine mnapokuja njoeni kimachale na Msipende kufyatua Risasi ovya. Sasa hapa nisingekuwa Makini si mgeniua Bure. Vipi mkuu amesema Tuendelee na Misioni ya kuwaua hawa mabiti au tuache"Aliongea Afande koboko huku Akishusha Silaha yake na kuirudisha kiunoni kama ilivyokuwa mwanzo. Kitendo cha kurudisha Silaha yake ndipo alikosea maana Ghafla Afande Mussa alimuibukia na kumpelekea Ngumi lakini Afande Koboko alikuwa Mwepesi alipangua ile Ngumu na kumtandika Teke Afande Mussa hadi alienda kumuangukia Suzani na wote walienda chini. Walipoanguka chini faster afande koboko alianza kutoa Pisto ili kukiwasha lakini nani angemruhusu kutoa pisto. Afande Mwingie aliruka kwa Utaalamu wa hali ya juu na kumpiga teke la kifuani Afande Koboko na kuanza kuyumba huku akihangaika kuchomoa Pisto. Kabla hajaanguka chini tayari alikuwa ameshachomoa ile pisto, alipochomoa Pisto tayari Afande Mussa alishaamka alimuwahi na kurusha teke ambalo lilienda kupiga Mkono wa Afande Koboko ambae ulikuwa Umeshikilia ile Pisto na Pisto ilianguka pembeni. Afande Koboko alipopigwa na Silaha yake ikaangukia Pembeni aliona sasa ni muda wa kupambana Mkono kwa mkono lakini hata kabla ya kuanza aliweka chini ya ulinzi na Afande Wengine huku na watu wake kitambo waalikuwa chini ya Ulinzi maana wao wala hawakusumbua maana ilikuwa Rahisi kuwakamata walikuwa hawana Silaha. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Afande Sophia alipowambia Vijana wake wakavamie na yeye aliona hana Muda wa kuendelea kukaa pale zaidi awahi kwenye tukio maana alikuwa na kitu cha kwenda kukifanya mara tu ya koboko kukamatwa. Kwa Mwendo wa Kasi alitoka Ofisini kwake na kwenda kupanda Gari yake na kuliondoa kwa kasi. Alipofika Usa river mara aliona Gari ikimpita kwa kasi na ndani alimuona Shawali akiwa na Afande Rama. Alipoona lile Gari Machale yalimcheza na kuamua kulifatilia kwanza ili akasome mchezo kitu Gani kilikuwa kinaendelea. Alilifatilia lile Gari kwa Umakini wa hali ya juu hadi lilienda kuingia kwenye Hoteli ya Mileniamu. Ile Gari ilipoingia kwenye ile hoteli na yeye aliingiza Gari lake kwenye ile hotel na kusubilia kuona Shawali alikuwa na Mishe Gani kwenye ile Hotel. Wakati Afande Sophia akiwa yupo Pale huku akiwa Makini wazo lilimwijia kutoa Camera yake na kuamua kuchukua kila tukio ambalo lingeendelea hilo lingemsaidia katika Upelelezi wake.alipotoa tu Camera yake na kuiwasha tayari kwa kuanza kuchukua Tukio Aliwaona Mzee Oska wakiwa na Goodlucky wanatoka ndani ya Hoteli alafu wanaenda kwenye Gari ya Shawali. Alitamani Kumuita Goodlucky lakini Upande wa Moyo Mwingine ulikataa. "Mzee Ramadhani rafiki yangu, ina maana unataka kuniambia Sasa hivi umezeeka Sana hadi Unashindwa kushuka kwenye Gari hadi tukufuate huko..."Aliongea Mzee Oska lakini hata kabla hajamalizia Walitokea watu Watano ambao walifunika nyuso zao na kuwaweka chini ya ulinzi Mzee Oska pamoja na Goodlucky kisha walipeleka hadi kwenye Gari ya Shawali na kuondoka kwa kasi. Tukio lile lilikuwa limefanyika kwa Kasi sana hata Pale Hotelini hakuna ambaye aliona ukifikilia na ile Hotel hapakuwa na watu. Sofia alipoona vile alijua Moja kwa Moja Hawa watu watakuwa kwenye hatari hivyo alitoa Bastora yake ikakaa flesh na kuamua kulifatilia Lile Gari tena kwa Umakini bila wao kujua kama Wanafatiliwa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Afande Sophia alikuwa analifatilia lile Gari kwa Umakini wa hali Juu kuhakikisha hawezi kushitukiwa huku akiwa amewasha Camera yake na kuchukua Tukio zima ambalo lilikuwa linaendelea. Gari zilikimbia Kama Muda wa Nusu Saa tayari walishatoka kwenye Mji wa Arusha na walikuwa sehemu ambayo haikuwa na Makazi ya Watu. Walipofika kule Shawali alisimamisha Gari na Kuwashusha Goodlucky na Mzee Oska. "Mlikuwa Mnajifanya Mnajua Sana Kuongea nyie Sasa leo nimewakamate. Nitawaua Mimi Mwenyewe kwa Mikono yangu ili Muiache Hii Dunia watu wafanye kama vile wanavyotaka. Hamuwezi Hata Siku moja kushindana Na tajiri"Aliongea Shawali huku Akiwa anaweka Bastora yake Sawa tayari kwa kutaka kuanza kazi. Muda ule Afande Sophia na yeye alikuwa ameshafika karibu na Eneo la tukio na hata Yale Maneno ya Shawali ambayo alikuwa Anaongea alikuwa anayasikia. Upande Mwingine alianza kujilaumu kutembea kwenye Gari peke yake kwani angekuwa na Afande wenzake ilikuwa rahisi kuvamia Siku ile. Hivyo kwa Kuwa alikuwa peke yake ilikuwa Vigumu kupambana na Watu watano ambao tena mbaya zaidi Wengine walikuwa ni Afande wenye uwezo wa Juu kutumia Bastora. Alichoamua ni Kuumiza Kichwa tu kuwaza ni Mbinu gani anaweza kutumia ili Kuhakikisha kuwa anawaokoa mzee Oska na Goodlucky. "Ulichoongea Kijana ni kweli kuwa leo utatuua Je Unauhakika na hicho ambacho Unakiongea? Maana mimi kwa kweli leo naona siyo Dalili ya kufa kabsa. Hivi unafikili Watu wanakufa Kizembe tu siwezi kufa mimi hata Kidogo Muda wangu bado"Aliongea Mzee Oska huku akiwa Anamwangalia shawali. Mzee Oska kwa kweli alikuwa hana wasiwasi kabsa hadi Shawali alianza kuogopa na kuhisi huenda kuna Mtu alikuwa yupo Karibu yao nini. "Wewe Mzee Unashangaza kweli, ila Kabla Sijakuu nataka Ufahamu kuwa baba yangu siyo yeye ambaye aliwapigia simu kuwaambia Mkutane Milennium. Hivyo kufa kwenu baba yangu hana hatia ila mimi ndio nilichukua Simu yake na kukupigia maana Nilijua baba yangu ni Rafiki yako sana akikuita lazima Uje tu. Sasa Mimi nahisi huu ndio Muda wenu wa Kufa, Naanza na wewe Mzee kwani unajifanya kihelehele sana"Aliongea Shawali huku tayari alikuwa Ameshatoa Pisto na ameielekeza kwa Mzee Oska. Cha Ajabu Oska hata alivyoelekezwa ile Pisto yeye alikuwa anacheka tu tena Baada ya Shawali kumnyoshea Bastora ndio Furaha kama iliongezeka zaidi. Afande Sophia alipoona shawali kamnyoshea Mzee Oska alibaini siyo Muda atampiga kitu ambacho alikuwa Hapendi. alichofanya alianza kukimbia kuelekea Kwa Shawali huku akisema usimpige Mpango umeharibika. Yale Maneno ambayo alikuwa anaongea Sophia Yalimfanya Shawali kushituka na kuacha kumpiga kwanza Risasi na kuja kumsikiliza yule Afande wa kike ambae alikuwa anakuja huku akipiga Kelele alikuwa anataka kuja kumwambia nini. "Jamani nani Shawali hapa, afande Mkuu wa Arusha kanituma niwaambie Msitishe kile ambacho mnataka kukifanya maana Afande Koboko walipoenda Kule wenyewe wamekamatwa. Kumbe wakati mnapanga hizi Misheni kuna Askari wengine walikuwa wanavujisha Siri. Hivyo inaeleweka kama nyinyi mko huko kuwaua hawa hivyo kama watakufa utakuwa kwenye hatia kubwa sana maana ushaidi upo wakati unasema unataka kuwauwa hawa. Sasa ili kuonyesha kama kile kwenye video ni Uongo basi usiwaue hawa"Aliongea Afande Sophia Kumdanganya Shawali huku akipumua haraka haraka. Kile ambacho alikibuni afande Sophia na kukiongea kwa kweli kilienda na tukio zima ambalo walijadili mkuu wa jeshi la polisi pamoja na shawali. "Nilikwambia mimi siwezi kufa kizembe Yani sijaona hata Harufu ya kifo changu alafu nife wewe pumbafu nini. Alafu eti niuliwe na mtoto laini kama wewe thubutu wewe bado hujafikia Umri wa kumtolea mtu kama mimi roho kasome kwanza"Aliongea Mzee Oska kwa Dharau. Yale Maneno ya Mzee Oska yalimuumiza Sana Shawali. Hata Hivyo bado hakutaka Kuamini Moja kwa Moja hivyo aliamua kutoa Simu yake ili Ampigie Mkuu wa Jeshi la Polisi arusha kumuuliza kama kweli inshu imeharibika. Sophia alipoona Shawali katoa Simu aliona atamuharibia Dili tena. Alichofanya alimsogelea shawali kisha kwa kasi ya ajabu alimuondelea Pisto yake na kumpiga teke takatifu hadi Simu ilianguka Pembeni. Haraka haraka alimuwahi na kwenda kumkaba Shawali shingoni. "Nyie wapuzi Mliobakia Shusheni bastora chini. Yani Afande Wazima badala kufanya kazi kama mlivyoapa leo hii mnafanya kazi kwa kuwaonea Raia kisa pesa. Sasa shusheni Bastora zenu chini kabla sijasambaratisha kichwa cha huyu Mbwa wenuna nyinyi kukosa Kazi"Aliongea Sophia. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Mzee Ramadhani alipopiga Simu yake kwa Mzee Oska na kuona hapatikani alijua Moja kwa moja kuwa wapo kwenye hatari sana. Alikumbuka Frank alivyosema kuwa Shawali anataka kumuua Baba yake alafu amuue na yeye. Mzee Ramadhani alipokumbuka yale Maneno alibaini tayari Mzee Oska kamkosa hivyo ambacho alitaka kukifanya ni kwenda kumuokoa Frank. Kwa kasi Ya Ajabu alitoka ndani na kwenda kupanda Gari na kuanza kuelekea Magerezani. Huko Magarezani alikuwa Anajuana Sana na Mkuu wa Gereza. "Nahitaji Huyu Kijana leo atolewe mara moja, Leo ndio Siku yake ya Kufa na baba yake tayari ameshauawa hapa ninavyokwambia hivyo naomba fanya kila linalowezekana Frank atolewe"Aliongea Mzee Ramadhani alipofika kwa Mkuu wa Gereza ila kujua kama mzze Oska kule alishaokolewa na Afande Sophia. "Mzee nilikwambia huyu Mtu kutolewa itakuwa Vigumu sana maana Wakuu wanamwangalia huyu. Ila mimi nitakusaidia nitakupa huyu mtu utaondoka naye na Sisi huku tutatangaza kuwa ametoroka. Afande ambao leo wapo Doria ni watu wangu wa Nguvu hivyo hii siri tutaificha. Tutasema huyu Mfungwa ametoroka kumbe wewe ndio umemchukua na wewe nakuomba muweke sehemu nzuri huyu kijana maana huko wakiumuona itakuwa Rahisi kumuua"Aliongea Mkuu wa Gereza na baada ya kuelewana Alienda akamtoa Frank na Kumkabidhi kwa Mzee Ramdhani, Mzee Ramadhani alimchukua Frank akampakia kwenye Gari na kuondoka naye.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

     Mzee Ramadhani alikuwa anakimbiza Gari kwa Kasi sana kuelekea nyumbani kwake. Ambacho alikuwa amekipanga Mzee Ramadhani ni kwenda kumuweka Frank ndani Nyumbani kwake huko alihisi angekuwa yupo Salama Maana hakuna Mtu ambaye Angemuona. "Frank Nisamehe Sana nimechelewa kukutoa na nimeshindwa kumlinda baba yako. Nisamehe Sana Frank maana Hapa ninapoonga Sizani kama Mzee Oska atakuwa Mzima. Mwanangu niliyomzaa Amenizidi kete hivyo alienda kuonana na baba yako amuue na ndipo aje Kukuua na wewe"Aliongea Mzee Ramadhani huku hadi machozi yalikuwa yanamtoka. "Mzee Ramadhani wewe usijali kama baba yangu atakuwa amekufa hicho wala kisikuumize kichwa. Chamuhimu naomba ndoa ambayo Shawali anataka kumuoa Grace ipeleke Mbele ili mimi nifunge hiyo Ndoa na Grace. Tafadhari usiicheleweshe na mimi nisije kufa kama baba yangu"Aliongea Frank huku akiwa kawaida sana wala hakushituka alipoambiwa baba yake kafa. Yale Majibu ya Frank kwa kweli yalimshitua Mzee Ramadhani. Alishindwa kuelewa kwa Nini Frank wala Hajashituka alipoambiwa kuwa baba yake Amekufa. "Frank mimi nimekuelewa hata mimi nahitaji kumaliza huu Mchezo mapema Sana, kama nitachelewesha huenda nitasababisha Watu wengi sana kufa. Lakini Frank mbona unanishangaza nakuambia kuhusu baba yako kufa lakini wala hata hujashituka"Aliongea Mzee Ramadhani na kumuuliza Frank swali maana alishangazwa kidogo. Mtu unampa Ujumbe wa kufiwa tena Kufiwa na baba yake anakuwa kawaida tu. "Mzee Ramadhani ulipokuja kuniona kituoni na mzee Wangu mimi nilikwambiaje, nilikwambia Shawali anahitaji kumuua Mzee Wangu pamoja na Mimi. Kwa kuwa nilikuwa Gerezani nilijua Moja kwa Moja mzee Wangu lazima afe. Hivyo Unaponiona nipo kawaida taayari Msiba wa baba yangu mimi nilishalia"Alijibu Frank kwa Uchungu sana. Siyo kwamba Frank alikuwa Haumii alikuwa anaumia vibaya mno ili kuna kitu ambacho alikipanga Kuja kufanya kwenye Harusi. Kama Grace ambaye alikuwa anampenda na amesababisha kwenda Jela Muda ule alikuwa hampendi kutoka na Dawa ambazo alipewa aliona hakuna Haja ya kuendelea Kugombania Mwanamke hapa Duniani. Frank Kuna kitu ambacho alipanga kuja kukifanya kwenye hiyo Harusi wala hakuwa na Wasi wasi. Mzee Ramadhani walipofika nyumbani kwake alimchukua frank na kumpeleka chumba ambacho kilikuwa karibu na chumba chake na alikuwa na uhakika hakuna mtu ambaye anaingia mle maana kilikuwa chumba chake ambacho alikuwa analala siku zingine kama hataki kulala na mke wake ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Afande Sophia alipomkaba Shawali na kuwaambia Wale Afande washushe Bunduki zao chini, wale Afande wala hawakubisha maana kama boss wao alikuwa ametekwa walikuwa hawana Jinsi. "Sasa nisikilizeni kwa Makini nyinyi pigeni magoti hapa chini wewe Goodlucky kusanya Bunduki zao ondoka na Mzee Oska kapandeni Gari yangu ile kule barabarani. Nyinyi Pigeni Magoti hivi hivi hadi na mimi nifike kwenye lile Gari niingie ndio nitamwacha na mtu wenu ila kama Mtu ataamka hapa nasambaratisha kichwa chake pamoja na hiki kichwa cha Boss wenu"Aliongea Afande Sophia. "Afande hawa watu walikuwa wanataka kuniua hadi mimi. Mimi niliwaambia wenyewe ni dhaifu kamwe hawawezi kumuua Mzee Shupavu kama mimi. Ili niwaonyeshe kama wao ni Dhaifu Hizo Bunduki zao acha nikusanye mimi"Aliongea Mzee Oska na kusogea hadi sehemu ambayo kulikuwa na Bunduki na kukusanya huku akiwa anawacheka wale Afande. "Shawali Mimi naondoka bwana, tena Naondoka mzima tutaonana kwenye Harusi yako labda hapo ndio utaniua huenda nitakuwa nimevimbiwa ubwabwa ila siyo hapa"Aliongea Mzee Oska na kuanza kuondoka na Good. Sophia naye alianza kusogea na Shawali. Walisogea hadi akafika kwenye Gari yake na muda ule wale Afande bado walikuwa wamepiga Magoti. "Shawali leo siwezi kukukamata bado namalizia upelelezi wangu hivyo nitakuja siku nyingine" aliongea Afande sophia huku akisogea karibu kabsa na Gari yake. Alipofika karibu na Gari yake alimuachia Shawali na kumtandika Ngumu kama tatu hivi ambazo zilimfanya hadi alianza kuyumba. Wakati Shawali akiwa anasikilizia maumivu ya zile ngumi ndio Afande Sophia alitumia ule Mwanya alipanda kwenye Gari na kuliondoa kwa kasi ya ajabu. Hadi Shawali Maumivu ya ngumi yanaisha tayari Afande sophia alikuwa ameshapotea. "Amka Fanyeni haraka misheni ya Kwanza tumefeli sasa tunatakiwa kufanya Misheni ya pili. Najua mnajua kama tulikuwa na kazi mbili kazi ya kwanza ilikuwa kushirikiana kuwamaliza Mzee oska na Goodlucky. Hiyo nazani Tumefelly sasa Inafuata Misheni ya Pili ya kwenda kumuua Frank. Hiyo nafanya Mimi peke yangu hivyo panda kwenye Gari nitaenda kuwaacha sehemu mimi naenda Gerezani kumaliza kazi"Aliongea Shawali. Muda wa Dakika Kumi tayari Shawali alishafika Majengo Arusha Maana alikuwa anakimbiza Gari kama hana akili vile. Alipofika Majengo aliwashusha Afande kisha alianza Safari ya kwenda gerezani kwenda kumuua Frank. "Mkuu nahitaji kumuona mfungwa Anajulikana kama Frank Oska nahitaji kuongea naye tafadhari maana nahisi kama alionewa vile nahitaji kumsaidia"Aliongea Shawali alipofika kwa Mkuu wa Magereza. Shawali yeye hakujua kama yule Mkuu wa Gereza alikuwa anamfahamu. "Mungu wangu yani baraka zinakuja za kijana wa watu kutetewa na yeye ndio hayupo. Yule Kijana Frank Oska kwa kweli anaatafutwa na Jeshi la Polisi maana leo Asubuhi Ametoroka Gerezani. Yeye anampango wa kumuua binti Flani anaitwa Grace. Hivyo wewe kama unamjua huyo Mwanamke hebu nenda kamsubilie huko lazima aje alafu utatujulisha sisi"Mkuu wa Gereza alimwambia Shawali ili kumkata kabsa asimuulize kitu. Maana alijua kama ataambiwa yule mtu anaenda kumuua Grace na yeye alikuwa anampenda Grace basi angeondoka ghafla. Kile ambacho alikuwa anakiwaza Afande ndicho ambacho kilitokea maana Shawali alipoambiwa vile alitoka Nduki kwenye Ofisi ya Mkuu wa Gereza tena bila hata kuaga na kwenda kupanda kwenye Gari na kuondoa Gari kwa kasi kwenda kumuangalia Grace na Kumlinda ili asije kuuawa na FrankCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Shawali alikuwa anakimbiza Gari kutoka pale kituoni mbaya. Ambacho alikuwa anakitaka ni kwenda Moja kwa Moja hadi kwa Grace na kwenda kumchukua ili asije kuuawa na Frank kama alivyoambiwa na Mkuu wa Gereza. Akiwa Ndani ya Gari alikuwa anajilaumu Sana maana tayari Misheni zake zote zilikuwa zimeharibika tena Mbaya zaidi kuna Afande wa kike ambaye alikuwa Hamjui alimwambia kuwa anahitaji kuja kumkamata. "Lazima Niongee na baba yangu niweze kumuoa Grace haraka sana maana nahisi upinzani unakuwa mkubwa. Baada ya kumuoa Grace ndipo sasa nitamtafuta huyu Afande wakike namuua, namtafuta Frank namuua alafu namalizia na Mzee Oska pamoja na Goodlucky"Aliongea Shawali kwa hasira huku akipiga Gari yake. kile ambacho alikuwa anakiongea shawali cha Harusi yake kuwaishwa ndicho ambacho na mzee Ramadhani alikuwa Anakitaka kama alivyoambiwa na Frank. Mwendo ambao alikuwa anakimbiza Shawali Gari alitumia Dakika Kumi tu tayari alikuwa ameshafika kwa Kina Grace. Alipofika kwa Kina Grace hata Salamu hakutoa kitu cha kwanza ilikuwa kumuulizia Grace. "Mama Samahani kwa kutokuwasalimia maana nilikuwa na Wasiwasi juu ya Grace. Mama Kwa taarifa Frank ameshatoroka Gerezani na Anampango wa kumuua Grace. Ambacho nakihitaji Mimi nataka Grace tuende wote nyumbani kwetu au nimwekee Ulinzi alafu Harusi pia Tutasogeza siku inatakiwa kufanyika wiki inayokujaa hii siku ya Juma tano. Ndio Hakuna kitu ambacho kitachelewesha wala kusumbua maana Kadi mlikuwa Hamjagawa hivyo anzeni Kugawa ili Harusi iwe Juma tano ya wiki inayokuja. Nahitaji kumuoa Grace Mapema ili nimlinde maana ndio Mwenye moyo wangu"Aliongea Shawali baada ya Kumuona Grace alikuwepo. Yale Maneno ya Shawali kuwaambia wazazi wake na Grace kuwa Frank ametoroka Gerezani yaliwashitua zaidi. "Baba mimi nimekuelewa ila Mwanangu kuanza kukaa kwako wakati bado hujamuoa ni Kinyume na Maadili wewe fanya haraka umuoe tu maana kweli Mwanangu yupo kwenye wakati mgumu atakufa. Hata Goodlucky ambaye ndio Kijana aliyezaa na Mwanangu alikuja hapa na kuongea mambo mengi sana. Pia Amesema hawezi kukubali wewe umuoe Grace hivyo lazima wenyewe wamchukue na ikishindikana basi watamuua. Hivyo Mwanangu hebu wewe fanya haraka huo mpango maana sasa hivi hata mtu akigonga geti mioyo inaanza kwenda mbio. Kama ulivyosema wewe Ongeza Walinzi hapa ili wamlinde Mpenzi wako"Aliongea Mama yake na Grace. Baada ya Maongezi mengi hatimae Shawali aliondoka kurudi nyumbani kwake. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Afande Sophia baada ya kuwatoroka Shawali alikuwa anakimbiza Gari kwa Mwendo kasi kuelekea Arusha Majengo ambako yalikuwepo Makazi ya marehemu Afande Joshua. Huko alijua tayari wabaya wake walikuwepo walishakamatwa. Moyoni Afande Sophia alikuwa na Furaha sana Maana Upelelezi wake ulikuwa unaenda Vizuri sana. Hadi pale ambapo alikuwa amefikia alikuwa na uwezo wa kupeleka Kesi Mahakamani na kushinda. Ila yeye bado hakuwa na Haraka alitaka kukamilisha Ushaidi kabsa ili hata kwenye ile kesi washitakiwa washindwe hata kutafuta mawakili. Ambacho alikuwa anakitaka hadi Mkuu wa Jeshi la Polisi na yeye amchukue kabsa video akiwa anaongea kama amehusika katika kumuua afande Joshua. Maana pale kama angepeleka Mahakani angelikuwa na Uwezo wa Kukaa na Kusema hawa Vijana wameamua kumchafua. Kule kwenye nyumba ya Suzani tayari Afande Koboko walishawekwa chini ya ulinzi hawakuwa na Ujanja tena. Afande kumi ambaye walipelekwa na Sophia wakiongozwa na Afande Mussa walikuwa siyo watu wa mchezo. Ingawa Suzani alikuwa amepigwa risasi begani lakini walisubiri kwanza hadi Mkuu wake Aje ndipo wamepeleke Hospitalini. Ambacho walikifanya kwa Muda ule walimfunga na kamba Mkononi ili kuzuia damu isiendelee kutoka. "Mama wewe unaonekana Jasiri sana umewaweza Afande watano umetumia akili nyingi za kuzaliwa. Asante sana kwa kuokoa maisha yangy ukija Sanya Juu itakuchinjia Ng'ombe unywe supu"Aliongea Mzee Oska kuanzisha maongezi maana walikuwa kimya. Afande Sophia na Goodlucky walikuwa wanafahamiana maana afande sophia ndio ambaye aliwatoa Goodlucky kwenye shimo siku ile walivyotekwa na kutupiwa mle. Waliendelea na Mazungumzo ya hapa na pale hadi walifika kwa Suzani na kuingia hadi ndani. Walipoingia ndani Goodlucky alibaki akiwa anashangaa kumuona Afande Koboko ambaye alimchoma kisu afande Joshua alikuwa chini ya ulinzi. "Huyu mtu siyo wa kumuweka chini ya ulinzi mnatakiwa kumuua. Huyu ndio ambaye alimuua Afande Joshua kwa kumchoma kisu tena mimi mwenyewe kwa macho yangu nilimuona. Suzani hivi kweli umesahau kama Huyu mtu ndio ambaye alikuulia mume wako alafu unasimama naye hapa. Aisha unataka kuniambia huyu mtu umesahau kama alimua afande Joshua kesi ikaenda kwa frank alafu na sisi alienda kututupia Shimoni na fande Sophia ndio alikuja kutuokoa. Kama nyinyi mmeshindwa kumuua basi mimi lazima nimuue"Aliongea Goodlucky kwa hasira hadi machozi yalikuwa yanamtoka. Yale maneno ambayo aliongea Good yalimfurahisha Afande Sophia maana yalizidi kusafisha ushaidi wake. Alipotoka kuchukua Bastora ili kwenda kumaliza Afande Sophia alimzuia. "Goodlucky tulia punguza Hasira huyu Afande hana hatia kabsa na tunatakiwa tumsafishe maana anatumwa. Mimi nitampa kazi moja na ndio ambayo itamtoa kwenye hii hatia. Labda Afande Koboko kabla sijakwambia kazi yangu unaweza kukubali kufanya"Aliongea Afande Sophia. "Wewe mwanamke wewe bado mdogo sana kwangu na huwezi kunituma kufanya kazi hata siku moja. Hamna ushaidi wa kunifunga mimi na tena nafanya kazi na watu wakubwa hivyo mmeshindwa" aliongea afande koboko wa dharau. "Mimi nilijua wewe Afande Mpumbavu unaweza kutugeuka hivyo ndio maana wewe afande mpumbavu tulikuweka mitego ya kipumbavu kukunasa. Najua utafanya tu kazi yangu ingawa umeonyesha Dharau kubwa"Aliongea Afande Sophia kwa kujiamini na kumsogelea afande CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/Koboko na kumpiga busu kumuonyesha kuwa yeye ni mchumba kwenye kazi zile. Baada ya kumchumu alianza kutoa camera zake ambazo alikuwa amezitegesha. Alipotoa alisave zile video kisha aliwasha tena na kumpelekea Afande Koboko kuangalia. Afande Koboko aliangalia kuanzia mwanzo hadi mwisho Jinsi alivyokuwa anaropoka kama Amemuua Afande Joshua hadi alibaki akiwa anashangaa. "Jamani naombeni Mnisamehe mimi nipo tayari kufanya kazi yenu yeyote ile ili tu msinifanyie kitu kibaya"Aliongea Afande Koboko huku akiwa anatetemeka. "Mimi nilishakwambia hadi Mwanzo kuwa sikufanyi kitu kibaya maana wewe unatumwa kufanya hii kazi pia ni mchumba tu kwangu. Nilikwambia tu kuna kazi nahitaji unifanyie wala usiwe na wasiwasi hii video mimi nitaifuta na nitakutetea hautafungwa ila naomba unifanyie kazi moja tu. Nahitaji kumfunga Mkuu wa jeshi la Polisi arusha ila Ushaidi bado haujakamilika. Nikipeleka hii mahakani nitakufunga na wewe. Hivyo mimi nakupa Camera utaitegesha na kumchukua Mkuu wa Jeshi la Polisi wakati wanaongelea jinsi walivyomuua Afande Joshua. Ukichukua hiyo Video na kuniletea wewe utakuwa huru"Aliongea Afande Sophia



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog