Simulizi : Sikutegemea
Sehemu Ya Tatu (3)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hivi unajua kitu chochote kuhusiana na mahoteli yaliokuwepo katika kisiwa hichi" nilimuuliza Mzee Robert. "Mwanangu hayo si mahoteli tu bali kuna mambo yanafanyika hapo na ni mabaya kuliko ubaya wenyewe. Hapo watu hukutana kwa ajili ya kufanya ibada, na kwa mwaka hukutana mara mbili. Kama uliwahi kusikia kuwa kuna watu wanaabidu mashetani basi hawa ni miongoni mwao. Na katika ibada zao hutoa kafara kubwa sana ya damu na kula nyama za watu, isitoshe kila baada ya miezi sita kuna meli maalumu inayopita nchi mbali mbali na kukusanya watu kwa ajili ya ibada zao".
Baada ya kunambia nilihisi mapigo yangu ya moyo kuongezeka kwa kasi, nilianza kujuta kwanini nilimuacha Latifa. Nilishindwa kujizuia kabisa na machozi yalitengeza michirizi mashavuni kwangu. "Kijana vipi mbona unalia" aliniuliza, "nimewakumbuka wenzangu ambao wapo mikononi mwa hao wapumbavu sijui hatima yao itakuwa nini" nilimjibu kiunyonge. "Ipo nji ya kujua kama wenzako wako hai au tayari washatolewa kafara" aliniambia na mimi nikafungua masikio kumsikiliza.
"Swali je utaweza kutumia hio njia maana inataka moyo kweli kweli" aliniuliza, "nimeshateseka vya kutosha, na hio njia nina imani nitaiweza" nilijibu kwa ujasiri. "Sawa, hiyo njia ni bomba la kupitishia maji taka. Ninaposema maji taka nakusudia maji ya chooni, hivyo unatakiwa utambue kuwa vinyesi ndio vinapita katika njia hio. Ukifanikiwa kupita mpaka juu basi utakuwa umekamilisha hatua ya kwanza. Hatua ya pili ni kutafuta mtu wa kuua ili upate nguo za kuvaa kwa ajili ya kuzunguka ndani ya mahoteli hayo. Ukifanisha hatua hizo mbili basi kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kuwaona marafiki zako kama watakua hai".
Nilihuna kwanza maana ilikuwa ni shughuli pevu lakini pia hakukua na uhakika kama nitawakauta wako hai. Hata akili yangu ilinambia kuwa bado wako hai hivyo ni vizuri kama ningerudisha fadhila zao kwa kuwasaidia. Kama kawaida yangu niliamua kufanya maamuzi magumu, lakini kabla sijaenda huko nilimuomba mzee Robert anipeleke kwenye hiyo boti kwanza ili niangalie kama kuna uwezekano wa kuitumia kutorokea kisiwani hapo.
Alikubali na kunikabidhi vijana kadhaa kwa ajili ya kunisindikiza, siku ya pili mapema safari ilianza. Ukisikia kuna watu wanamapafu ya farasi wala si uongo, maana hao jamaa niliopewa walikuwa wanakimbia kweli kweli japo si kasi kubwa. Ilibidi nijikaze kiume maana safari hiyo ilikuwa yangu na kwaaajili yangu. Tulikimbia kwa muda mrefu sana zaidi ya nusu siku mpaka tulipofika upande wa pili wa kisiwa. Kwa kweli nilihisi mapafua yanawaka moto, lakini kwa wenzangu ilikuwa tofauti kabisa wao hawakuonesha kabisa dalili za kuchoka.
Tulipofika nilikaa chini kwanza kuvuta pumzi, wale wengine walikuwa wakiangaza huku na kule na hapo ndio nikashtuka kuwa nilipewa walinzi. Maana hata kwa jinsi walivyokuwa wakikagua eneo hilo, baada ya mapumziko mafupi nilisimama na kuelekea ilipokuwa boti hiyo ambayo tayari ilishakuwa na kutu. Nijilikuta nikitabasamu baada kugundua kuwa boti hiyo ilikuwa na zile mashine za kawaida kama za mashua za wavuvi. Zile zinazowashwa kwa kutumia kamba kama jenereta, haikuwa kubwa sana. Kwa makadirio ya haraka ilikuwa na uwezo wakuchukua watu kumi ambao wangekaa kwa amani kabisa.
Baada ya kukagua ndani nilirudi nje na kufungua sehemu ya mafuta katika zile mashine ili kuangalia kama yamo. Ama kweli Mungu humpa mja wake pale asipotegemea, mafuta yalikuwemo tena mengi tu. Tatizo lilikuja kwenye kuwasha sasa, zile waya za kuwashia zilikuwa zimekatika kabisa. Nilikaa kitako nikafikia nini cha kufanya lakini sikupata jibu, baada kuona nimeishiwa kabisa mawazo niliwafuata wale wengine na kujaribu kuwaambia kitu. Mwanzo ilikuwa shida kunielewa kutokana na kupishana lakini walinielewa nilichokuwa nakitaka, nilikuwa nataka kamba ngumu.
Basi mmoja wao aliingia msituni na baada muda kidogo alirudi vitu kama kamba lakini zilitokana na miti. Nilizichukua na kurudi nazo katika boti, nilipofika nilizifungua mashine zote kwa ajili ya kuzifunga kamba hizo nijaribu zari kama zitawaka. Nilifanya utukutu nnao jua mwenyewe kwa sababu sikua na kifaa maalum cha kuwashia. Nilijaribu mara nyingi sana kuwasha lakini hazikukubali, "Mungu wangu mimi nimekoma na nikiokoka katika hili janga sitakaa nirudie tena upuuzi, hata kufikiria pia sitothubutu" nilijisemea moyoni huku nikilengwa na machozi.
Hiyo ilikuwa ni sawa una njaa na chakula kipo mbele yako lakini unashindwa kula, baada ya mapumzikoa mafupi nilianza kujaribu bahati yangu tena. Mungu si asumani baada ya majaribio kadhaa mashine ziliitika na kupata uhai, yaani siwezi kuelezea furaha niliopata baada mashine hizo kuwaka. "Laiti wangelikuwepo wenzangu basi saa hivi tungekuwa tushauwacha ufukwe" nilijisemea moyoni kisha nikazima mashine hizo na kuweka kila kitu sawa kwa ajili ya kutoroka.
Baada ya kukamilisha kila kitu nilirudi walipo wale wengine na kuwaonesha ishara kuwa tuondoke. Safari ilianza tena lakini wakati huu hatukukimbia kutokana na kiza kilikuwa tayari kimeshatanda. Tulitembea kwa mwendo wa haraka lakini kwa umakini wa hali ya juu, tulifika sehemu wale jamaa wakasimama haraka na kutoleana ishara. Hapo kila mtu alitoa kisu chake, vizu hivyo havikuwa vile nilivyovizoea bali vilikuwa ni mawe yaliochongwa vizuri. Mmoja alinifuata na kunipa ishara nipande kwenye mti, hapo sasa akili yangu ikanambia kuwa kulikuwa na hatari mbele yetu.
Sikuwa mbishi nilisogea kwenye mti uliokuwa karibu na kupanda huku nikitetemeka, nikiwa juu ya mti kwa mbali niliona vitu kama macho yakisogea walipo wale jama waliokuwepo chini. Cha ajabu wao wala hawakutetereka kabisa, walikuwa makini sana huku wakizunguka zunguka. Ghafla alitokea chui mweusi kwenye kiza na kumrukia mmoja wao, lakini alikuwa mwepesi sana maana aliinama ghafla na chui alipita juu. Yaani maisha yangu yalikuwa kama ndoto maana kila kitu nilichokuwa naona kwenye filamu za kizungu siku hiyo kilikuwa kinatokea kweli.
Kitu kingine kilichoniacha mdomo wazi ni pale walipoanza kuimba huku wakirukaruka na kujipiga makofi mapajani. Yule alitoa mngurumo na kumrukia mmoja wao, lakini huyu yeye hakumkwepa. Alifanya kama kumdaka hivi na kugeuka nae kwa nguvu na kumbamiza chini, aisee hii mijitu ilikuwa na nguvu. Wengine nao walifuata kwa juu na kumkita chui huyo visu kadhaa shingoni na miguuni. Ama kweli siku hiyo chui alikuwa ameingiza choo cha kike maana alichokutana nacho ni bora hata asingefikiria kuwadhuru watu hao.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa katika hali ya kushangaa juu ya mti nilihisi kitu cha baridi kikipinda nyuma yangu, ila kabla sijafanya kitu nilishangaa nimerushwa kwa nguvu. Kitendo cha kugusa tu ardhi nilijikuta tayari nimeshviringwa na nyoka. Tena si nyoka tu bali ni joka maana likuwa kubwa kweli kweli, ukweli niliishiwa nguvu na kujikuata nikisalimu amri kumuacha mdudu huyo afanye yake amalize. Ghafla yule nyoka alijizongoa kutoka mwili wangu na kutoa mlio mkali, mmoja wa wale jamaa kumbe alifika na kumchoma kisu kwa nguvu. Na baada ya hapo alimrukia na kumkita kisu kwenye kichwa, mbona nyoka alikuwa mpole.
Ama kweli Mungu huumpa mwanadamu uwezo wa kumudu mazingira aliokuwepo, maana kama yule chui na nyoka wangetokea Dar ingekuwa ni hadithi nyingine. Maana watu tungepoteana kama kundi la nyumbu lililotawanywa na simba lakini si kwa watu hao niliokutana nao huko. Baada ya purukushani zote hizo walibeba miili ya nyoka na chui na safari iliendelea, tulifika kule kijijini karibu na alfajiri tena. Wanakijiji walitupokea kwa shwangwe, walifurahia sana kuletwa kwa nyama zile mbili amazo moja wapo ilitaka kuchukua maisha yangu.
"Jamaa wanasema yule nyoka ni windo lako" Mzee Robert alininong'oneza, "ah wapi alitaka kunifanya chakula" nilijibu huku nikitabasamu. "Pole kijana haya ndio maisha ya huku, ukikutana na mnyama umuue au akuue lakini hakuna kukimbia" alinieleza huku akizidi kutabasamu kisha akaendelea "vipi umefanikiwa". "Ndio boti ni nzima japo si sana lakini huenda ikasaidia" nilimjibu, tuliendelea mazunumzo mengine na hasa tulizungumizia suala zima la kupenya ndani ya hoteli zile kwa ajili ya kuwaokoa wenzangu kama bado wangekuwa hai. Siku iliisha na nilipumzika kwa ajili ya kazi nzito ya siku ya pili japo nilikuwa naipeleka kwenye mdomo wa mamba.
Siku iliofuata mapema niliamka na kuanza maandalizi ya safari, mzee Robert alinikabidhi kisu pamoja na kamba ngumu sana. "Kijana najua hujawahi kuuwa lakini njia pekee ya wewe kuweza kuishi ndani ya maeno yale ni kuwa kama mgeni au mwanajeshi, kwa hiyo atakae jitokeza ni halali yako" aliniambia maneno hayo ambayo yalipenya sawia kabisa ndani ya ubongo wangu. "Kama ukifanikiwa kutoka, pitia njia ile ile ulioingilia lakini usije hapa kijijini. Nitakupa vijana ambao watakuonesha mto mkubwa unaoelekea upande wa pili wa kisiwa hichi. Basi ukifanikisha kazi hiyo na kutoka rukeni katika mti huo, na utakupeleka mpaka baharini ilipo hiyo boti" alizidi kunipa maelezo.
"Mzee wangu naomba unisaidie kitu kimoja, mimi sijui umbali kutoka katika kisiwa hichi mpaka nchi kavu. Hivyo ningeomba unisaidie kunipelekea chakula katika ile boti ambacho kitanisaidia kwa siku kadhaa" niliomba nae alinikubalia na papo hapo akaagiza asakari wake ambao aliwaamini sana. Baada ya maongezi hayo mafupi niliga na kuanza safari yangu yenye matumaini finyu sana. Nikiwa vijana kadhaa tulitembea mpaka katika huo mto aliosema mzee Robert kukariri vizuri njia za kufika hapo. Kisha tulielekea mpaka katika hilo bomba la maji taka, kama mtu ungekuwa na roho nyepesi basi uhakika ungegeuza na kuondoka.
Maana ile harufu tu iliokuwepo eneo hilo ilikuwa ni yakutapisha, niliwaaga wale vijana na kuanza kupanda ngazi maalum iliokuwepo pembeni. Nahisi ile ngazi ilikuwa inatumika kufanya marekebisho ya bomba endapo lingeharibika. Nilipofika karibu na bomba hili wala siku jiuliza mara mbili niliingia na kuanza kutembea. Yaani nilifuta kabisa wazo la kuwa nilikuwa natembea kwenye maji yalioyajaa vinyesi japo harufu ilinitesa sana. Baada ya mwendo kidogo nilifika sehemu kuna ngazi ya kuelekea juu, nilipanda ngazi hiyo mpaka juu kabisa ambako kulikuwa na mfuniko ambao haukukaza.
Niliusukuma kwa nguvu na kutoka, ama kweli bahati ilikuwa yangu maana hakukuwa na mtu yeyote eneo hilo pia lilikuwa mbali kidogo na upeo wa macho ya watu. Nahisi sehemu ile ni sehemu ya kuingilia kwenye chember zile kutokea juu, basi nilitafuta sehemu nikajificha kwa ajili ya kusubiri mtu wa kuuwa japo nilikuwa nikitetemeka kweli kweli. Miguu yangu ilikuwa na utando wa brown hivi ukichanganja na weusi na kijani kibichi. Nzi nao hawakua mbali kuafanya sherehe kwenye miguu yangu.
Nilisubiri sana na hatimae nafasi ilifika, nilimuona mtu mmoja akija upande ule niliokuwa nimejificha na kwa bahati nzuri alikuwa anakuja peke yake. Nilikaa tayari kwa ajili ya kutekeleza lile jambo lililoitwa mauaji. Alipita sehemu niliopo bila kunishtukia, nilitoka kwa kasi sana na kwa kutumia kamba ngumu niliopewa. Nilimpishia shingoni na kwa kutumia nguvu zangu zote niliivuta mpaka alipoacha kupapatua na kutoa pumzi ya mwisho ndio nikamuachia huku siamini kama kweli nimeuwa.
Nilimvuta na kuingia nae sehemu nilikuwa nimejificha, kila kitu na kuvichukua mimi, tatizo sasa lilikuwa ni kupata sehemu ya kuoga. Maana sehemu niliopo hakukuwa na choo kabisa, hapo likanijia wazo nielekee kule alipokuwa anaelekea yule jamaa niliemuua. Kwa mwendo wa taratibu nilitembea na kwa umakini wa hali ya juu sana. Kila nilivyozidi kutembea nilisikia kelele za watu, hata hivyo sikufuata njia kwa sababu ilikuwa hatari badala yake nilipita ndani ya vinyaka kama kichehche. Mungu mkubwa kumbe ndani ya vichaka hivyo kulikuwa na mabomba ya mvua. Kweli Mungu hamtupi mja wake, nilosogea kwenye mamomba hayo na kuanza kuoga. Nilijisugua sana maana nilikuwa na nongo kweli kweli ukichanganya na mavi ndio kabisa. Nilioga mpaka nilipohakikisha nimetakata, nilivaa zile nguo nyingine pamoja na kila kitu nilichomvua mpaka mpaka viatu japo vilikuwa vikinibana kweli kweli.
Nilipohakikisha kuwa naonekana kama wao, niliondoka sehemu hiyo ili nijaribu kujichanganya na watu. Wakati natembea niliingiza mkono katika mfuko wa nyuma wa suruali ile nilioiba na kukuta pochi. Niliitoa na kuifungua ili kuangalia kama kuna kitu kinaweza kunisaidia, kwa bahati nzuri nilikuta kadi maalum ya kufugulia mlango ikiwa na nambari ya chumba pamoja na nambari ya hoteli kilipokuwepo chumba hicho. Nilitabasamu kidogo na kukaza kuelekea katika hoteli ambayo namba yake ilikuwa kwenye kadi ile.
Nilipishana na watu wengi sana tena wakubwa wakubwa na wazito katika nchi zao, "kumbe nao wamo katika huu mchezo" nilijisemea moyoni huku nikizidi kukazana. Nilifika katika hoteli hiyo na bila kuongea kitu niliingia kwenye lifti na kuelekea juu. Sikupata shida kwa sababu hata gorofa kilipokuwepo chumba hicho ilikuwa imetajwa kwenye ile kadi. Bahati nyingine nilioipata ni kwamba mpaka nafika katika gorofa husika hakuingia mtu mwengine katika lifti hiyo.
Iliposimama nilitoka na kuelekea moja kwa moja mpaka katka chumba kile na kuingia, nilifanya yote hayo bila ya kuwa na wasiwasi wowote maana nilielewa kuwa kama ningejifanya nina wasiwasi basi ingekuwa rahisi kushtukiwa. Nilipoingia ndani ya chumba hicho sikulaza damu, niliingia chooni na kuanza kuonga tena kwa sabuni ilik kutioa harufu ya kinyesi iliobakia mwilini mwangu. Baada ya kumaliza kuoga nilirudi chumbani na kuelekea kwenye kabati na kufungua. Nilitoa kaptula kubwa kiasi nne na kuzivaa zote kisha nikatoa na suruali pana kidogo nikamalizia juu.
Najua utakuwa unajiuliza nimewezaje kuingia mpaka ndani ya hoteli hii bila kushtukiwa ukiachilia mbali kujishtukia mwenyewe. Mambo yaliokuwa yanafanyika katika sehemu ile yalikuwa ni siri hivyo hakukutakiwa kuwepo na kit chochote ambacho kingeweka kumbukumbu ya matukio ya huko. Na hilo ndilo lililonisaidia mimi mpaka kuingia katika chumba kile bila kushtukiwa. Nilibana katika chumba hicho hadi kiza kilipoanza kuingia na njaa ilikuwa ikinisumbua lakini sikutaka kula hata chakula kilichopikwa katika hoteli hiyo.
Kiza kilipoanza kuimeza siku sasa, nilitoka na kuelekea nje kwa ajili ya kuanza msako wa wenzangu. Nilizunguka sana bila mafanikio yeyote yale maana palikuwa pakubwa sana, mwisho niliona isiwe tabu nikamtafuta muhusuika mmoja na kumuuliza. "Wapi nitapata viijana kama watatu hivi wapya kabisa ambao hawajaonekana na wengi" nilimuuliza huku nikitabasamu. Ukichangaya na ndevu zangu nyingi zilizojaa kidevuni nilionekana mtu mkubwa tu. Yule mhudumu alitabasamu na kuniambia nimfuate nami sikuweka ajizi nikafanya hivyo.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulitembea kama dakika mbili hivi mpaka katika mabanda fulani ivi ambako kulikuwa na vijana wengi. Nilijifanya kutabasamu ili kumtoa wasiwasi huku nikitingisha kichwa, alinipeleka mpaka kwenye banda moja hivi ambalo lilikuwa na watu kama sita hivi. "Mkuu hawa hapa ndio bidhaa mpya lakini wanauzwa bei ghali sana kutokana na kuwa wametupa sana shida" aliniambia. "Usijali" nilimjibu huku nikijaribu kukaza macho ili kuangaliza kama kina Louise wapo miongoni mwao. Nilimuona Latifa akiwa kajikunyata katika pembe ya banda hilo huku akilia, Loise na Linda walikuwa na kazi ya kumnyamazisha . "Naomba unitole yule binti anaelia na hao wenzake wawili wanaomnyamazisha, watafaa sana kwa kazi yangu" niliongea kwa sauti nzito sana.
Jamaa aliitika na kutoka nje, baada ya dakika kidogo alirudi na askari wawili na kuwaambia wafungue lile banda. Baada kuwaambia hivyo alinigeukia mimi na kunitajia bei, bila kusita nilitoa pochi mfukoni na kutoa karatasi kadhaa zilizoandikwa kiasi cha pesa. Hiyo ni sifa nyingine ndani ya hoteli hio walikuwa hawatumii pesa kama zinavyotumika sehemu nyingine. Bali wanabadilisha pesa na kukupa karatasi maalum ambazo zinatumika katika kufanyia kila kitu. Nilimkabidhi kiasi alichotaja na kuwaomba wale askari wanifuate. Tulitoka eneo hilo ikiwa bado kina Louise hawajanishtukia, "Mkuu huko saa hivi ni hatari" aliongea askari mmoja.
"Lakini huku ndio pazuri kwa kazi ninayotaka kuifanya kabla ya kwenda kutoa kafara" nilijibu kwa ukakamvu japo nilihisi haja kubwa ikitaka kutoka maana hao askari walikuwa na mitutu. Na ingetokea kama wangenishtukia basi ningetolea kafara mimi. Tulitembea mpaka ili sehemu yenue chember nilipoingilia mwanzo, kwa mbele kidogo kulikuwa na vichaka na ndipo nilipokuwa nakusudia kuwatenda askari hao.
Nilipofika sehemu na kujiridhisa kuwa pako salama na naweza kutekeleza jambo nililokusidia. Nilisogea mpaka karibu na Louise kisha nikamnong'oneza kitu lakini nilimminya mkono ili asije akashtuka na kuharibu mipango yangu. Baada ya hapo niliwaamuru wale askari wawafungue pingu, mwanzo walisita lakini nililazimisha huku nikiwahakikishia kuwa yoyote atakae leta ujinga basi nitamnyonga kwa mikono yangu.
Basi wale askari waliwafungua pingu kisha nikawaambia waniachie uhuru wao wakae mbali kidogo. Louise alifanya kile nilichomnong'oneza kuwa awashike waschana wote wawili mikono ili wasikimbie. Baada ya askari kufika mbali kidogo na eneo nililopo, ndipo nikasogea karibu na kina Lousie. "Latifa na Linda msiogope, ni mimi Adam" niliongea kwa chini, Latifa alibaki amekodoa macho tu asiamini kwa kweli nilikuwa mbele yake. Nilitoa kisu na kumkabidhi Louise kisha mimi nikatoa ile kamba na kuishika vizuri mkononi.
"Njia ya kutorokea ipo pale walipo wale askari, ili tufanikiwe ni lazima tuwauwe" niliongea kwa sauti ya chini huku nikimchezea shingo Latifa ili wale askari wasije wakshtukia. Lakini kabla sijataka kuwaambia kile nilichokusudia, niliwaona askari wakiongea kitu na baada ya hapo mmoja alianza kuja uoande wangu. "Kuna nini" nilimuuliza huku nikikaza kamba mkononi, "yule mwenzangu ameona maiti pale kichakani hivyo niko hapa kukusindikiza tuondoke" alinijibu. Nilijifanya kama nimemuelewa na kumsogelea ila nilipomkaribi tu niliishika kamba yangu kwa mikono miwili na kwa kasi ya hali ya juu nilimzunguka na kumtia kabari ya kamba. Louise nae hakuwa nyuma alimsukumia kisu cha shingo kwa nguvu sana.
Baada ya tukio hilo niliwapa ishara wanifuate, na kwa sababu yule askari mwingine alikuwa ameelekea kule ulipo mwili hakuona tukio lililotokea. Tulipokaribia na ile sehemu waliokuwepo mwanzo niliwapa ishara wajifiche kisha nikamuonesha mkono Louise. Mkono huo niliupitisha shingoni nae alielewa anatakiwa afanye nini. Baada ya hilo nilitoka haraka huku nikiomba msaada, yule askari alikuja mbio na kunishika. "Mkuu kuna tatizo gani" aliniuliza, ila kabla sijamjibu Louise alimtokea kwa nyuma na kumkita kisu shingoni. Kwa sababu mimi nilikuwa mbele yake nilimzuia na kumshusha chini taratibu kabisa.
Kwa mwendo wa haraka nilianzakutembea huku nikiwafanyia ishara wenzangu wanifuate, nilifika pale kwenye mfuniko wa chemba na kuufunua kisha nikawapa ishara waingie nao wakatii bil kujali harufu iliokuwa ikitoka katika chemba hiyo. Mimi niliingia mwisho na kuurudishia mfuniko huo kisha nikapita mbele na kuongoza njia. Nilitembea kwa mwendo wa haraka huku wao wakinifuata kwa nyuma mpaka sehemu ambayo maji machafu yalikuwa yanamwagika. Nilitangulia mimi kushuka katika ngazi zilizokuwa pembeni kidogo na tobo hilo.
Tulipofika chini tu nilianza kutimua huku wao wakinifuata kwa kasi nyuma, sikujali kama walikuwa uchi wa mnyama kabisa. Lakini hata wao wenyewe walisaha kabisa kama walikuwa hawana nguo mwilini. Wakati tunakimbia tulianza kusikia ving'ora kwa mbali kutoka katika mahoteli yale. Mimi havikunitisha kabisa isipokuwa viliniongezea ari ya kukimbia. Nilifuata njia ile ile nilioelekezwa mpaka kufika katika mto ambao ulikuwa unaelekea uoande wa pili wa kisiwa ambako ndiko kulikuwa na usafiri wa kuondokea kisiwani hapo.
"Jamani tukikimbilia msituni hawa jamaa watatukamata, hivyo njia rahisi ya kuwatoroka ni..." hata sikumalizia kuongea Latifa alinipa kama mshale kuruka ndani ya maji. Wengine walifuata punde tu baada ya yeye kupita na mimi nikawa mtu wa mwisho. Kutokana na kasi ya maji ya mto huo, tulipelekwa kasi sana huku mimi nikiomba tusijie tukakutana na maji. Maji hayo yaliendelea kutupeleka mpela mpela na kwa bahati nzuri tulipata gogo ambalo lilikuwa kama mtumbwi wetu.
Baada ya mwendo wa muda mrefu hatimae tulifika ufukweni, tulitoka kwenye maji na kisha nikawapa ishara wanifuate. Lakini waliingiwa na wasiwasi kadiri tulivyokuwa tunasogea sehemu ilipo ile boti, na wasiwasi huo ulitokana na kuwepo kwa wanajamii wale walionisaidia. Hata hivyo niliwatoa wasi wasi kabisa na kuwaambia kuwa wale watu ni rafiki. "Poleni vijana" Mzee Robert aliongea punde tu baada ya sisi kufika. "Asante mzee wangu, vipi kila kitu kimekamilika" nilimuuliza huku nikihema.
"Ndio kila kitu kama ulivyosema" alinijibu na baada ya hapo nikawapa ishara wenzangu waingie ndani ya boti. Mimi niliingia mwisho baada ya kumuaga mzee Robert, "nakutakia safari njema" aliongea mzee huyo na kuwageukia watu wake kisha akwapa ishara waondoke eneo hilo. Nilipoingia tu nilisogea kwenye mashine na kuanza kuziamsha. Ziligoma mara kadhaa lakini baada ya majaribio kama matano hivi zilikubali na kurudiwa uhai. Nilizishusha mashine hizo kwenye maji na kwa sababu zote zilikuwa zimeungwa sehemu mojoa hivyo sikupata tabu ya kuzimilika.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilivuta mafuta kwa nguvu kama vile naendesha pikipiki yangu ya bodaboda, nazo zilitii kwa kishindo na kuanza safari yenye matumaini hafifu. Mpaka tunakiacha kisiwa sikuoana dalili zozote za watu ufukweni, hapo niliamini kuwa walikuwa wakitutafuta ufukweni. Baada ya kuhakikisha tumeshaakiacha kisiwa mbali mno nilisimamisha boti na kuwaangalia wenzangu ambao walikuwa wakiona aibu kutokana na kutokuwa na nguo. Nilivua ile suruali na kuiweka pembeni kisha nikavua kaptula tatu nilizokuwa nimevaa na kumkabidhi kila mmoja moja na mimi nikabakiwa na moja.
Baada ya hapo niliichana vibande viwili ile suruali na kuwakabidhi Latifa na Linda ili wasitiri vifua vyao ambavyo vilikuwa wazi muda wote. "Poleni jamani kwa yaliowakuta" niliongea baada kila mmoja kutulia. "Mbona hatuendelei na safari" badala ya kunijibu wote waliniuliza swali hilo kwa pamoja. "Mimi sijui hapa tulipo ni wapi hivyo nasubiria kiza kiingia ili nitumie nyota kupata upande wa kuelekea" niliwajibu kwa utaratibu. Wote walishusha pumzi na kuniangaliwa kwa makini, Latifa alinisogelea na kinitandika kibao. "hicho ni kwa sababu ya kunitisha kule hotelini" aliongea kama mtu aliekasirika.
Ila kabla sijaongea kitu, alinikumbatia kwa nguvu huku akinipiga mabusu yasio na idadi maalum. Lakini kati ya mabusu yote aliokuwa akinipiga, moja lilifika mdomoni na kilichofuata ilikuwa ni kingine kabisa. Baada ya kuridhika na kubadilisha mate huko alirudi nyuma na kuniangalia huku machozi yakimtoka. "Hivi umeponaje ponaje maana niliwasikia wale askari wakisema umeanguka bondeni tena mto uliokuwa unapita huko chini ulikuwa na mamba si mchezo" Louise aliniuliza. "Ndugu yangu wee ni rehema za Mungu tu ndio zilizoniweka hai" niljibu na kuwaeleza kila kilichotokea mpaka mwisho.
"Na ulijuaje kama turakuwa hatuna nguo" swali hilo lilitoka kwa Linda. "Wakati naelekea kule hotelini baada ya kuiba hizi nguo, nilikutana na askari kadha waliokuwa wakitembea pamoja na mateka ambao walikuwa uchi kabisa. Hivyo nikajiaminisha kuwa ukifikishwa pale hotelini, uanvuliwa nguo zote na utu pia. nikiwa na maana kuwa unaishi kama mnyama anaesubiria kuchinjwa tu. Na hilo ndilo lililpnifanya mpaka niva kaptula za ziada nikiamini kuwa hata nyie mtakuwa kama wengiene tu waliokamatwa" nilijibu kwa upana zaidi.
"Maisha ya ile sehemu sitakaa katika maisha yangu nikayasahau hata siku moja" aliongea Lousie na kuendela "yaani mtu unanunua binaadamu mwenzako kama unanunua ng'ombe tu, halafu eti anakufanya chochote kile anachotaka bila kujali jinsia. Hivi kweli binaadamu unadiriki kumla nyama bianaadamu mwenzio, ama kweli dunia imefika mwisho wake" alimaliza kuongea huku machozi yakimtoka. "Sasa unalia nini wakati tumeshawachomoka" nilimuuliza, "Si unamkubuka Akinola" aliniambia, "ndio si yule jamaa kutoka Nigeria" nilimjibu. "Sasa siku ile tuliokamatwa, yeye ndio siku aliokuwa anachinjwa.
Tulipofikishwa pale mahotelini tuliwekwa makusudi tushuhudie mwenzetu anavyogeuzwa nyama, tena aliemnunua alikuwa ni mtu wa huko huko Nigeria. Halafu alikuwa akifurahi sana na furaha yake ilizidi baada kupewa kikombe kilichojaa damu na kunywa".
Tuliendelea kuongea mambo mengi tu mpaka kiza kilipoanza kuingia, nilinyanyua kibuyu kimoja miongoni mwa vibuyu kadhaa vilivyomo katika boti hiyo na kunywa maji. Baada ya kumaliza kunywa maji nilioliokota kipande kimoja cha nyama na kula, lakini wenzangu walikuwa wakiniangalia tu. "Jamani karibuni kula jamani" niliwaribisha, "hiyo nyama ni ya kiumbe gani" Latifa aliniuliz. Sikutaka kuwaambia kama nyama ni ya chui ama nyoka, niliwajibu tu kuwa nyama ile ni ya mnyama wa msituni tu. Japo walikuwa na mashaka nayo lakini kutokana na njaa kila mtu alinyanyua kipande kimoja na kuanza kukishambulia.
Tulipomaliza kula nyama tuliongezea na matunda kwa juu, halafu tukapumzika kidogo kabla ya kuanza na safari. "Jamani tuombe Mungu tu bahari isije ikachafuka" niliongea huku nikianza kuvuta mafuta taratibu na boti hiyo ikatii na kuanza kukata mawimbi. Kwa taaluma niliopewa na kaka pamoja na marafiki zake wengine wakati navua, nilitumia nyota kama njia ya kupata muelekeo wangu. Kutoka na na uchovu wenzangu wote walipitiwa na usingizi, mimi japo nilikuwa nimechoka sana lakini nilijitahidi nisilale. Maana kama nahoza ningelala si ningezamisha boti, nilivuta mafuta kwa muda mrefu sana lakini sikubahatika kuona hata dalili ya kisiwa.
Ulifika wakati nikawa nimechoka sana, hivyo nilisimamisha boti na kushusha nanga ili na mimi nisinzie kidogo maana nilikuwa nahisi kuchanganyikiwa. Nikiwa usingizi nilihisi kama kitu kikinitambalia kichwani, haafu kilifuatiwa na kijiraha fulani hivi. Nilivyoshtuka kumbe alikuwa Latifa akinichezea nywele, sikutaka kuongea kitu bali niliivuta miguu yake na kuinyoosha kisha nikalala mapajani mwake na kuendeleza usingizi wangu.
Nikuja kushtuka tena baada kuhisi matone matone ya maji yakinipiga usoni, nilipofungua macho niligundua kuwa mvua ilikuwa inanyesha. Moja kwa moja nilifahamu kuwa ikiwa mvua hiyo itaambatana na upepo basi hali itakuwa mbaya. Niliinuka na kuelekea kwenye vikabati vidogo katika boti hiyo na kuanza kuvifungua. Vilikuwa vigumu kutokana na kushika kutu lakini nilipambana navyo hadi vikaunguka. Na kweli nilichokuwa nakitafuta nilikipata, yalikuwepo makoti matatu ya kuokolea maisha. Niliyatoa na kumkabidhi kila mmoja wao koti moja na kuwaambia wavae, "wewe mbona huna koti" Louise aliniuliza.
"Usiwe na wasiwasi na mimi, ntajua cha kufanya" nilijibu huku nikielwa fika kuwa ilikitokea la kutoa basi ndio itakuwa nitolee tena. Nilitoa pia na kamba moja ndefu kisha nikawapa na kuwaambia wajifungue kiunoni kila mmoja wao. Na mimi nikajifunga kisha nikarudi kwenye sehemi za mashine na kuwasha ili kujaribu kuepuka na shari ilioko mbele yetu. Nilifanya hivyo nikiamini kuna sehemu hali itakuwa shwari. "Jamani hii mvua kama mnavyoiyona inadalili za kuja na upepo, na likitokea hilo basi maisha yetu yatakuwa hatarini sana" niliongea kwa msisitizo. "Hivyo lolote litakalotekea msije mkathubutu kujifungua hiyo kamba maana ndio njia pekee ya kutuweka pamoja hata kama tutakufa" nilimalizia kisha nikaanza kuvuta mafuta na taratibu tukaanza kukata maji tena.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kinyume na nilivyotegemea, mvua ile haikunyesha tena bali kulikuwa na upepo wa wastani uliokuwa baridi kali sana. Ilibidi nisitishe safari maana huko nilipokuwa naelekea ndiko upepo ulipokuwa mkali zaidi. "Mbona umesimamisha" Latifa aliniuliza, "huko tunapoelekea ndio kuna mkali zaidi ni bora tuishie hapa kwanza mpaka pale upepo utakapoacha kupuliza" niliwaeleza na wote wakanielewa. Wakati tunasubiria upepo ukate tulianza kupiga soga za huku na kule, kila mtu alikumbushia maisha yake huko alipotoka.
Baada muda kupita upepo ulikata kabisa na bahari ikatulia kama kapeti, sasa baridi ndio ilikuwa imepamba moto. Maana tulianza kutetemeka kama wagonjwa, kadri muda ulivyoenda ndivyo baridi ilivozidi kuwa kali. Mwisho kabisa baada kuoana hali mbaya ilibidi tujikunyate wote sehemu moja kama watoto wa paka. Hata hivyo haikusaidi kitu, na ilifika wakati nikahisi mpaka vidole vinataka kuganda. Baada hali kuzidi kuwa mbaya Latifa alinisogelea na kunikumbatia kwa nguvu, "hata kama tutakufa nataka tufe pamoja" alininong,oneza maneno hayo masikioni mwangu. "Usijali hatuwezi kufa saa hivi, Mungu yu pamoja nasi kama ameweza kutuokoa kutoa huko tulipotoka basi na hapa atatuokoa kwa mapenzi yake" nilimjibu.
Hata sijui alifikiria nini mtoto wa kike, taratibu alianza kunichokonoa kwa kuingiza mikono yake katika kaptula yangu. Nilijitahidi kumzuia huku nikimuambia kuwa huo si wakati wa kufanya mambo hayo lakini hakusikia hata kidogo. Aliendelea na mchezo wake huo, lakini kadri muda uliovyokwenda mapigo ya moyo yaliongezeka. Na unajua kama mapigo ya moyo yakiongezeka, damu inazidi kusukumwa kwa wingi na kupelekea joto la mwili kuongezeka kwa kiwango kadhaa.
Hako kamchezo kalinoga na kujikuta tukihamia ulimwengu mwingine kabisa na kusahau kama tupo katika hali ya kifo cha muda wowote ule. Huko kamchezo kalipohamia ndiko joto lilipopanda na kuichemsha miili yetu, pia tulisahau kabisa kama kulikuwa na watu wengine katika chombo hicho. Ama kweli mapenzi asali ya roho, tuliendelea na mchezo huo mbaya mpaka pale tulipofikia mshindo mkuu lakini hakuna hata mmoja aliemuachia mwenzake. Usingiz ulitupitia tukiwa katika halia hiyo hiyo ya kukumbatiana.
"Adam, Adam amka kaka kimenuka" nilimsikia Louise akiniamsha, nilifungua macho kiuvivu na hapo ndio nikagindu kuwa bahari ilikuwa imechafuka. Nilimuamsha Latifa ambae bado alikuwa amelala na kumwambia avae vizuri na kuvaa koti la kuokolea maisha. Tulifanya kama tulivyofanya mchana, tulijifunga kamba vizuri. Kisha nikaangalia angani kama ningepata ishara yoyote ya tunapoelekea. Baada kuona wingu zito limetanda nilikata tamaa kabisa ya kuona kile nilichokuwa nakitafuta.
Hata hivyo nilivuta mafuta na kuanza tena safari, wakati huu nilijitahidi kukwepa mawimbi makali kutokana na kuwa boti yenyewe ilikuwa ndogo na mbovu kidogo. Ukichnganya kiza, upepo na mvua ilioanza kunyesha matumaini ya kuokoka yalikuwa madogo sana. Milijitihadi kadri ya uwezo wangu kutumia mbinu nilizofundishwa na watu niliokutana nao wakatu wa kazi yangu yangu ya uvuvi lakini hali ilizidi kuwa mbaya. Maana hata mawimbi yalizidi kuwa makubwa na makali zaidi kila muda ulivyoyoma.
Ghafla lilikuja wimbi moja kubwa sana kulipigia boti kwa pembeni na kulipindua na wote tulirusha lakini kwa bahati mbaya kamba ile tuliokuwa tumijifunga ilganda katika chuma kimoja katika boti ile. Kamba hiyo ilianza kunibana sana, hilo lilitokana na kuwa wenzangu walikuwa na maboya na mimi nilikuwa sina. Hivyo maji yaliwapelekea juu lakini haikuwenzekana kutokana na mimi kuganda. Na hilo ndilo lilipelekea kubanwa sana, mwisho niliona kama ningeendela hivyo basi ingenisababishia madhara hivyo niliona boara nijifungue tu.
Baada ya kufanya hivyo nilipata afueni na kuanza kuogelea ili kuibuka maana muda wote nilikuwa chini kwenye maji. Nilipotokeza juu sikuwaona wenzangu, wakati huo huo mawimbi hayakuacha kunisulubu. Nilijaribu kuoambana nayo lakini wapi, yalinizidi nguvu na kunafanya kama mpira wa kona. Kila wimbi lilipiga linavotaka, hata hivyo sikukata tamaa niliendelea kupambana nayo lakini mwisho nguvu zilianza kuniishia. Hapo ndio niliona kuwa kifo changu kimefika, hivyo nilion hakuna haja ya kuendelea kupambana na jeshi hilo la Mungu.
Nilijielegeza na kufunga macho maana hakukuwa na njia nyingine zaidi ya kukubali matokeo. Taratibu pumzi ilianza kuniishia huku vikombe kadhaa vya maji vikitafuta njia yake na kuingia mdomoni. Nguvu ziliendelea kuuacha mwili wangu huku viungo vikasaliti kutoa ushirikiano, haukupita hata muda macho yalipoteza nuru na kuingia katika usingizi mzito au kama wanavyouita kupoteza fahamu. Sikujua nini kiliendelea maana ulimwengu ulikuwa tayari umetwaliwa na kiza kizito kilichoashira dalili zote za kifo.
Nikiwa katika usingizi huo mzito nilihisi kama kitu kikinigonga gonga, nilijaribu kufungua macho ili niangalie makazi yangu baada ya kufa. Nilishtuka baada kuona sura ya mtoto ikiwa inaniangalia kwa mshangao, japo mwangaza uliniumiza ulipoingia machoni lakini nilijahidi kutafumbua hivyo hivyo kibishi. Yule mtoto alipoona nimemkodolea machoa alikimbia huku akiita "mama", baada ya dakika kidogo aliingia mwanamke kijana kidogo.
"Unajisikiaje" aliniuliza huku akitabasamu, "hapa ni wapi" sikumjibu bali na mimi nilimuuliza swali. "Hapa ni Jamaica" alinijibu, "jamaica"nilisema kwa nguvu kidogo huku nikionekana kutoamini kile nilichokisikia. Hilo nalo liliingia katika mambo ambayo siku ya tegemea katika maisha yangu, kwa obama kugeuka msituni, kukutana na mtanzania anaieshi miongoni mwa wanajamii ya misituni na sasa Jamaica. Nilifunga tena macho ili kujua kama naota au ni kweli, lakini nilipoyafungua hakukubadilika kitu.
"Wewe endelea kupumzika" aliongea yule mwanamke kisha akainuka na kuondoka, ama kweli katika maisha yangu sikutegemea kabisa kama ipo siku nitafika Jamaica hata kwa bahati mbaya. Niliendelea kulala pale kitandani nilipokuwa nimelala bila fahamu huku nikiwakmbka wenzangu ambao sijui hatima yao ilikuwa nini. Nilijikuta machozi yakinitoka bila kupenda, na yalizidi kila nilipomkumbuka Latifa. Mwanamke amabe ametokea kuuteka moyo wangu ndani ya kipindi kifupi nilichokaa nae na kunifanya kuwa bwege mtozeni.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini ndio limeshatokea japo nilimlaumu Mungu kwanini ameniacha hai na kuwachukua wale wote ninaowapenda. Kwa kweli lilikuwa pigo kubwa sana kwangu, nilijiona mtu nisie na bahati hata kidogo. Lakini pia nilifahamu kuwa Mungu ananiadhibu kwa kukosa shukurani kwa kile alichonipa na kuwa kinanipatia riziki kila siku inayopita. Nililia mpaka machozi yakawa hayatoki tena, ndipo niliamua kunyamaza. Hapa subiri nikuwambie kitu kidogo, ukiwa umekwazika halafu ukatamani kulia wewe lia tu. Hata kama ukahisi kupiga kelele wewe piga tu maana ukifanya hivyo utapata afadhali kidogo.
Baada kilio cha muda mrefu, kwa kujizoa zoa niliinuka na kukaa kitako kitandani, na haukupita muda yule mwanamke alikuja tena akiwa na sahani ya chakula. yaani alipokiweka tu chini sikusubiri hata maji ya kunawa, nilikivamia na kuanza kula kama ndama wa ng'mbe ambae hakupewa ziwa na mamaake kwa muda mrefu. Yule mwanamke alijaribu kuniambia nile taratibu nisije nikapaliwa lakini ilikuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gita ukitegemea aimbe mziki labda kulia "meee". Nilikula mpaka nilipohisi tumbo limerdhika ndio nikapunguza kasi, nilimuangalia yule mwanamke ambae nilimuona akinishangaa sana.
"Asante kwa ukarimu wako" baada ya kushiba nikamshukuru, "Unaitwa nani" aliniuliza. "Jina langu ni Adam" nilimjibu huku nikitabasamu. "Adam, mimi naitwa Delilah na huyu ni mwanangu anaitwa Noah" na yeye alijitambulisha. "Nashkuru kukufahmu" niliongea huku nikikaa sawa maana sasa hata kukaa ilikuwa shida kutokana na tumbo kujaa sana. "Hivi ilikuaje mpaka nikakukuta ufukweni juzi" aliniuliza, "ah ni hadithi ndefu sana" nilimjibu na kumsimulia kila kitu tokea mwanzo hadi mwisho.
Alisikitika sana kuona mwanaume mzima nimekimbia kwetu eti kisa kuna matatizo, "mwanaume wa kweli hayakimbii matatizo bali anayavaa na kupambana nayo kiume zaidi mpaka kieleweke" aliniambia maneno hayo ambayo yalikuwa kama msumari moyoni. Maneno hayo yalindhalilisha sana, hakuishia hapo tu "unashindwa hata na baadhi ya wanawawake, anakuwa na maisha magumu lakini hakati tamaa. Leo atauza machungwa, kesho atauza ndizi, kesho kutwa atauza mboga za majani ili mradu asikose kitu cha kupitisha siku. Wewe rijali mzima, una nguvu za kutosha unadiriki kukimbia eti kisa uanatafuta maisha mazuri. Unakimbia nchini kwako ambako una uhuru wa kutembea bila kutiliwa mashaka unakwenda katika nchi ambayo kila mtu anakuona kama kinyago. Halafu bado unatembea kifua mbele unajiita mwanaume uliokamilika, hayo si maisha kakaangu".
Hapo ndio akawa amenimaliza kabisa maana nilijiona bwege kuliko watu wote duniani, nilitamani hata kutoa machozi lakini niliona aibu. Matatizo nieyataka mwenye halafu nilie kwa kweli ingekuwa aibu kubwa sana. Basi baada ya maongezi hayo nilitoka nje kidogo kuona mji, ilikuwa jioni tena na kiza kilikuwa kimeshaanza kuchukua nafasi yake. Kila mtu alikuwa akichakarika kumalizia siku kwa ajili ya kwenda kupumzika. Nikiwa hapo nje niliona bahari na ilikuwa imetulia sana, picha ya Latifa ilinijia kichwani ikiambatana na picha marafiki zangu wakubwa sana katika shida Louise na Linda.
Hata sijui walikuwa katika hali gani, ima waliokoka kutoka katika hali ile ya hatari au wamekufa. Kisha niliangalia angani "kweli Mungu umeamua kuniadhibu" nilijisemea moyoni, asikwambie mtu hakuna adhabu kali katika hii dunia kama kuona kila mtu wako wa karibu na unaempenda anatoweka. Kwanza niliwapoteza wazazi wangu wawili, kisha nikampoteza kakaangu kwa kukimbia vitimbi vya shemeji yangu. Kabla hata sijapoa vizuri nikamkimbia rafiki yangu kipenzi Frank alienitoa mbali sana, tokea mbulula tu na mgeni wa jiji na kunipa maisha. Alipoteza muda wake na nguvu zake kunifundisha kuendesha pikipiki. Kipindi hicho ilikaribia afukuzwe kazi kazi kwa kupeleka hesabu dogo kwa bosi wake lakini hakuacha kunipa mafunzo.
Nilikula kupitia jasho lake, hivi utu wangu niliupeleka wapi mimi. Mtu aliejitoa kwa hali na mali kunisaidia lakini nimemsaliti kwa kumkimbia. Mbali na Frank, watu niliokutana nao kisiwani baada ya kutoroka na kuzoeana na kwa muda mfupi tu nao pia wakatoweka. Mungu hakunitupa alinibakisha na marafiki wenye upendo na amani. Kumbe Mungu alikuwa akinionjesha tu furaha ya kuwa karibu na watu wanaokujali, halafu anipe maumivu ya kuwaona wakitoweka mbele ya macho kama nilivyowafanyia wengine.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Machozi yalianza kutengeneza njia katika mashavu yangu, kilio cha chini kwa chini kilishika nafasi yake kikiambatana na kwikwi. Nilihisi jeraha kubwa sana moyoni na kama lingekuwa sehemu ya nje ya mwili basi lingeonekana kiasi gani linavuja damu. Nililia sana mpaka machozi yalikata kutoka nikawa naliza kilio kikavu tu. Baada ya kuridhika na kulia niliamua kurudi ndani, "vipi umefurahia upepo wa bahari" Delila aliniuliza nilipoingia ndani. "Ndio nahisi afadhali kidogo sasa" nilijibu huku nikikaa kwenye kigoda.
"Samahani hivi kuna uwezekano wowote wa kupata njia ya kurudi Tanzania" nilimuuliza baad kimya cha sekunde kadhaa. "Kwa njia za kawaida sidhani kama ipo maana wewe huna hata passport hapo ulipo" alinijibu. Huo nao ulikuwa mtihani mwengine, hata uwezo wa kurudi Tanzania sikuwa nao kabisa. "Lakini kuna meli moja kubwa sana ya mizigo huwa inafanya safari zake mpaka nchini Tanzania" aliniambia lakini moyo wangu ulipiga "paa" hasa baada kusikia neno meli. Neno meli ndipo matatizo yangu yalipoanzia.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment