Simulizi : Sipendi Ujinga Mimi
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya dakika 15, mzee Bang’ala akatoka na kuwatazama wanawake wale, akamkazia macho kila mmoja ila alipofika kwa mama Ashura akashangaa sana. Mama Ashura nae akamkazia macho yule babu jambo lililomfanya mama Salehe kuingiwa na hofu. Walitazamana kwa sekunde kadhaa kisha kwa pamoja wakaangua kicheko,
“Hahahaha! Umekuwa mkomavu sasa,” alisema mganga.
“Eenh! Nimeyazingatia masharti yako ndio maana nadunda hadi leo,” mama Ashura akajibu.
“Naona umeniletea mgeni leo”
“Ndio babu, huyu ni rafiki yangu anamatatizo sana atakueleza mwenyewe”
“Hahahha matatizo! Hamna nilishindwalo chini ya jua, suburini kidogo,” alisema mzee Bang’ala na kuingia ndani.
“Mhmhm! Mama Ashuu, sikuwezi shoga yangu”
“Kwa nini?”
“Si nilikuwa nakuona unavyomtazama mzee wa watu nikabaki sielewi elewei”
“Aah! Mambo ya kawaida tuu haya shosti”
“Inaonekana umezoana sana naye”
“Yeah! Mimi ni mteja wake wa siku nyingi”
“Mhmh! Yaani si kwa kutazamana kule kwa kweli”
“Hahaha! Jamani mama Salehe mhmhmhm!”
“Ila anaonekana kazi anaiweza, naamini tatizo langu atalitatua”
“Shaka ondoa hapa ndipo kwa mzee Bang’ala”
Wakaendelea kuongea huku wakiendelea kusubili wito wa mganga, baada ya muda mfupi wakaitwa na kuingia ndani, mganga akawasha udi na ubani kisha akaanza kuongea maneno yasiyoeleweka akafumbua macho na kumtazama mama Ashura ambaye alijawa na aibu nyingi. Mama Salehe akawatazama tena akawa aelewi nini kinachoendelea baina ya wale wawili, kisha mganga akamtaka mama Ashura atoke nje ili aweze kubaki na mama Salehe kwa ajili ya kukamilisha dawa, mama Ashura bila kusita akanyanyuka na kumuacha shoga yake akiwa na woga mwingi.
“Nimeyaona matatizo yako jee! Wataka tufanye nini juu ya mbaya wako”
“Yaani mganga huyu mama Juma nataka umlambishe mchanga au awe chizi tuu”
“Hahahahaha! Hainashida mwanadamu mizimu itatimiza hitaji la moyo wako”
“Tawile babu” mganga akaendelea na ibada yake, kisha akamkabidhi mama Salehe dawa.
“Hakikisha unainyunyiza hii kwenye nguo zake, akiwa ameanika”
“Tawile babu”
“Weka fungu la mizimu na uende” Mama Salehe akafanya kama alivyoagizwa na mganga kisha akaenda alipo shoga yake.
“Mhmh! Mwenzangu nimefanikisha ila wewe na huyu babu sio bure”
“Huhuhu! Shoga sipendagi ujinga mimi”.
“Mhmh ndio hata kwa huyu mzee, akikufia kifuani jee”
“Shosti stori ndefu si unajua baba Ashuu toka apate ajali hawezi tena shughuli, katika kuangaika angaika nikafika kwa mahabuba Ba’ngala na mambo yakawa mambo ndiyo ivyooo tena”
“Mhmhm! Makubwaa…..!”
“Tuachane na hayo kama umefanikisha twende,” akasema mama Ashura na safari ya kurudi nyumbani ikaanza.
***********************
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kama bahati mama Salehe alifika na kukuta mama Juma amefua na kuanika nguo zake nje usiku huo kwa kuwa anakosa muda wakati wa mchana kutokana na shughuli zake. Bila kuchelewa mama Salehe akaangaza huku na huko na baada ya kuona usalama upo akasogelea nguo za mama Salehe na kunyunyuzia ile dawa aliyopewa na mganga kisha akanawa mikono na kuingia ndani kulala.
“Mhmh! Wewe mama Juma njoo uanue nguo zako na sie tuanike zetu,” alisema Upendo aliyetoa nguo zake kwa ajili ya kufua.
“Bado hazijakauka vizuri acha zishike joto kidogo”
“Mama Juma naona mambo siyo mabaya siku hizi viwalo vipya kibao, kweli utaki ujinga tutakoma mwaka huu,” alisema Upendo.
“Hamna mambo ya kawaida tuu hayo”
“Alafu iyo blauzi ya bluu umenunua shilingi ngapi nimeipenda ghafla”
“Hiyo nilimbana mmachinga mmoja hivi akaniachia kwa elfu tatu”
“Jamani nzuri mno, hii nikiavaa na ile suruali yangu daah! Lazima kitu apagawe,” Upendo akaongea huku akiisogelea ile blauzi ya mama Juma.
“Conso shosti njoo uone, kama itanipendeza nimpore mama Juma,” Upendo akamuita shoga yake aliyekuwa akifanya usafi chumbani kwake.
“Nakuja shosti”
Maongezi yale yakamshtua sana mama Salehe, akaanza kuhisi mpango wake utafeli, ikabidi atoke nje haraka sana, alipofika akashikwa na butwaa baada ya kuona Upendo ameishika ile blauzi na kuanza kuvaa.
“Yaani vibinti vya siku hizi kwa kudandia nguo za watu, mta vaa visivyovalika mfyuuu!” akasema mama Salehe.
“Bibi eenh! Niache mie nipendeze”
“Acha kuvaa nguo hiyo ya mama Juma”
“Eeenh! Ugomvi wenu mie haunihusu”
Upendo akavaa ile nguo, mama Salehe akatumbua macho kama kabanwa na mlango kwani alijua nini kitatokea ndani ya muda mfupi ujao, bila kupoteza muda akaondoka haraka kuelekea kwa shoga yake mama Ashura.
“Mhmhm! Vipi tena mbona hai hai asubuhi yote hii hata chai sijapika”
“Mwenzangu nimekosea masharti”
“Nini?”
“Nimeharibu dawa”
“Mama Salehe usitake kunichanganya”
“Kweli shoga yangu, nimefata maagizo yote ya mzee Bang’ala ila aliyevaa nguo ni Upendo sio mama Juma, sijui itakuaje?”
“Mhmh! Basi usipaniki shoga yangu twende tukaangalie nini kitakachotokea”
Wakatoka mbio mbio hadi nyumbani kwa mama Salehe lakini walishangaa kukuta hamna baya lolote lililotokea, Upendo alikuwa bado kaivaa ile nguo na anaongea na kucheka kabisa.
“Inamaana mzee Bang’ala kaniongopea?”
“Mhmh! Labda kwakuwa yule sio mkusudiwa ngoja nirudi nyumbani”
Mama Ashura akaondoka na kumuacha mama Salehe akiwa hana Amani huku hofu kuu ikimtawala, akaingia ndani kuendelea na usafi. Haikupita dakika tano Upendo akasikika akipiga yowe la kuomba msaada, mama Salehe akajikuta anatoka ndani kama mshale alichokishuhudia hakuamini macho yake, Upendo baada ya kuivua ile blauzi akaanza kuwashwa mwili mzima na ndani ya muda mfupi akawa amevimba na kutisha mno, hamna aliyeweza kumtazama mara mbili.
“Upendo shoga yangu nini kimekukuta mbona ulikuwa mzima muda huu tuu,” alisema Conso huku akilia asijue amsaidie vipi rafiki yake.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nisaidie Conso nakufa mwenzio,” akasema Upendo huku akiwa kwenye maumivu makali.
“Jamani Upendo vumilia ngoja tufanye mpango wa kumuwaisha hospitali,” akaongea mama Juma na kuchukua simu yake kumpigia dereva wa bajaji.
Mama Salehe ikabidi atimue mbio kwenda kwa mama Ashura na kumtaarifu kilichotokea, ikabidi waje wote harakaharaka, Mama Ashura akafikiri kwa haraka kisha akamvuta pembeni shoga yake.
“Kweli mambo yameharibika na anabahati kweli yule mwanaharamu, sasa shoga yangu hapa lazima tumtupie lawama mama Juma kuwa yeye ndiye aliyemfanya vile Upendo”
“Daah! Asante sana mama Ashuu umenipa wazo zuri sana na lazima aone joto ya jua leo”
Wakatoka walipokuwa na kurejea alipo Upendo, Conso na mama Juma.
“Mhmhm! Maskini Upendo umefanya nini hadi kuwa katika hali hiyo”
“Hakufanya lolote! Zaidi ya kujaribu ile blauzi ya mama Juma na alipoivua tuu ndiyo hali ikaanza kubadirika,” akajibu Conso.
“Mama Juma naona uchawi wako unavuka mipaka, umemuua mwanangu nikakuvumilia sasa umeona haitoshi unataka kumuua msichana wa watu asiye na hatia,” alisema mama Salehe.
“Mhmh! Wewe mama Salehe unazungumza nini?”
“Ndiyo kwani nani hajui kama wewe ni kigagula mfyuuu!” alidakia mama Ashura.
“Mbona siwaelewi, tusaidianeni tumpeleke mgonjwa hospitali”
Kauli iyo ikamfanya mama Salehe akumbuke maneno ya mganga kuwa pindi mbaya wake baada ya kudhurika na dawa kama atapelekwa hospitali na akatumia dawa yeyote ya kizungu basi ndio utakuwa mwisho wa maisha yake.
“Hapana huyu kalogwa na mama Juma unajua kila kitu, sasa tunaomba umponeshe asipopona nawewe lazima ufe,” akasema mama Salehe.
Conso hakuweza kuongea lolote machozi yakawa yanmtoka kumwona rafiki yake akiwa katika hali ile, dereva wa bajaji akafika, mama Juma akaomba wasaidiane kumpeleka hospitali lakini mama Ashura na mama Salehe hawakuwa tayari, majirani kadhaa wakafika baada ya kuusikia mzozo ule wote wakamuhurumia sana Upendo.
“Jamani tumuwaisheni hospitali asije pata tatizo Zaidi hapa nyumbani,” alisema mama Juma. Majirani wakajitokeza na kumpakia Upendo ndani ya bajaji, dereva akaendesha kwa mwendo wa kasi na kumpeleka hospitali ya Plan, daktari alivyoona tuu hali ya upendo ikabidi awape rufaa kwenda hospitali ya mkoa Amana.
Safari ya kwenda Amana ikaanza huku Upendo akiwa hajitambui, Conso akawa mtu wa kulia mama Juma akamuweka Upendo miguuni mwake. Wakafika Amana, manesi wakampokea na kwa haraka wakampeleka chumba cha daktari, daktari akaduwaza na hali ile ya kuvimba mwili, baada ya Conso na mama Juma kutoa maelezo ya muda mfupi kabla ya hali ile kutokea, daktari akagundua kuwa uenda Upendo ameingiwa na sumu, akachukua dawa kwa ajili ya kumchoma sindano ili apunguze makali ya sumu iliyo mwilini mwa Upendo kisha vipimo vingine viendelee. Daktari akamchoma sindano upendo na kumuweka mapumziko, ndani ya muda mfupi uvimbe ukaanza kupungua jambo ambalo liliwapa faraja mama Juma na Conso.
Baada ya muda mchache kupita daktari akamfanyia tena vipimo Upendo kisha akawaambia,
“Mgonjwa wenu anaendelea vizuri ila sitoweza kumruhusu kwa sasa hadi nitakapokuja kumtazama jioni”
Mama Juma na Conso wakaridhia maneno ya daktari na hawakuwa na maswali mengine, kwa kuwa Upendo hakuwa amekula kitu toka asubuhi ikabidi mama Juma atoke nje ya hospitali na kwenda kumtafutia chakula Upendo ambaye alionekana kurejewa na hali yake ya kawaida.
********************
Baada ya Upendo kupelekwa hospitali mama Salehe akaenda moja kwa moja kwa shoga yake kipenzi mama Ashura. Alikosa amani na hofu kuu ikamjaa moyoni.
“Mhmh! Shoga usihofu wala nini hayo ni mambo ya kawaida tuu”
“Mhmh! Mambo ya kawaida kivipi shoga yangu, motto wa watu anakufa bila kosa lolote,” alisema mama Salehe.
“Kosa ni kiherehere chake cha kudandia mambo yasiyomuhusu mwache alambe mchanga na itakuwa funzo kwa wajinga wengine,” alisema mama Ashura.
“Sasa shoga yangu tunafanyaje hapa maana mimi moja haikai wala mbili haikai”
“Ondoa hofu shoga! Mzigo wote huu ataubeba mpinzani wako,” alisema mama Ashura.
“Huhuhuhu! Hapo tuu ndipo ninapokupendea shoga yangu wewe!”
“Sipendi ujinga mimi,” alisema mama Ashura.
“Haya shoga yangu tujiandae twende tukamuone huyo mgonjwa huko hospitali,” alisema mama Salehe.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************************
Mama Juma alifanikiwa kupata chakula na kuingia nacho chumba cha mapumziko ambapo Upendo alikuemo. Wakati huo pia baadhi ya ndugu wa upendo wakawa wamewasili na kushirikiana katika kumuuguza Upendo. Mama Juma akatoa chakula na kumkabidhi dada yake upendo, akakipokea na kusogea alipo mdogo wake kisha akamuinua na kumkalisha. Kabla hajaanza kula mama Ashura na mama Salehe nao wakawa wamefika. Upendo alifarijika mno kuona watu wakimjali kiasi kile akapata nguvu ya kula.
Dakika kumi ishirini baadae hali ya Upendo ikabadilika ghafla, ule uvimbe ukarudi tena na safari hii ukazidi kuliko ule wa mwanzo, kila mmoja akashangaa ikabidi daktari aitwe lakini kabla hajafanya lolote Upendo akakata kauli na kupoteza maisha papo hapo. Hakuana aliyeamini tukio hilo, mama Juma akachanganyikiwa, dada yake upendo akapoteza fahamu. Vilio vikatanda huku mama Ashura na mama Salehe nao wakalia tena kwa uchungu mno.
“Jamani Upendo umetuachaje hivi!” alisema Conso.
“Ooh! Nini kimekukuta mbona ulikuwa mzima muda si mrefu jamani,” mama Salehe akasema.
“Wakina mama embu nyamazeni, hii ni kazi ya Mungu na ni vyema mkaenda kufanya taratibu zingine kwa ajili ya kuuhifadhi mwili wa marehemu,” daktari akasema.
Wakatoka nje na kumwacha daktari pekee chumbani mle. Vilio viliendelea kutawala mama Salehe akamuangalia mama Juma kwa jicho kali kisha akamwambia,
“Wewe mama Juma ifike mahali umuogope Mungu, binti wa watu anakosa gani hadi umuue?”
Kauli ile ikazua tafrani ya aina yake wote wakamgeukia mama Juma, ndugu zake upendo wakahamaki na kutaka kumpiga mama Juma. Watu waliokuwa eneo hilo wakasaidia kumtete mama Juma na kumtaka aondoke eneo hilo,
“Damu ya Upendo haiwezi kupotea hivi hivi! Tutahakikisha nawewe unalipa kwa hili,” alisema mmoja kati ya ndugu zake Upendo.
Mama Juma alijawa na simanzi nzito akawa anatembea huku aelewi wapi anaelekea, kifo cha Upendo kilimuuma mno.
Taarifa zilifika mtaani watu wote walihuzunika na kumlaani mama Juma, vijana wa kiume waliomzoea Upendo nao hawakukbali wakapanga wampige mama Juma popote watakapo muona. Mipango ya chini chini ikasukwa jamii yote ikaona kuwa mama Juma astahili kabisa kuwepo mazingira hayo.
****************
Siku hiyo mama Juma alitembea mno na kujikuta akiingia mtaani kwake majira ya saa tatu usiku, mama Juma alishangaa kidogo kuona mtaa umepooza kwani haikuwa kawaida. Ila akafikiri kuwa uenda watu wameenda msibani, akapiga hatua ndefu lakini kabla hajakaribia nyumbani akajikuta amezungukwa na vijana wapatao 10 walioshika fimbo. Akawatazama na kuwasalimu lakini hamna aliyeitikia, mama Juma akahisi hatari iliyopo mbele yake.
“Wewe mama leo ndiyo mwisho wa uchawi wako,” alisema kijana mmoja.
Kabla mama Juma hajasema kitu tayari akaanza kushambuliwa kwa bakora, alijitahidi kujitetea lakini hamna aliyesikia. Walimpiga sana mama Juma na hatimaye akaanguka chini hakuwa na nguvu ya kujisogea wala ufanya lolote.
“Oyah! Kashaisha huyu twendeni!”
Kabla hawajaenda popote wakahisi miguu yao mizito hawakuweza kwenda popote, upepo mkali ukavuma na kuwachanganya vijana wale papo hapo kila mmoja akashangaa kuona damu zikiwatoka puani, mdomoni na masikioni.
Mama Juma alishuhudia hilo akashangaa mno, kukatokea viumbe vya ajabu vilivyo na haiba ya kibinadamu lakini vyenyewe vilitisha mno. Vikawasogelea vijana wale na kuwapiga kichwani mmoja baada ya mwingine, mama Juma hakuelewa nguvu ameitolea wapi ila akajikuta akisimama na kutimua mbio.
Siku iliyofata vilio vilisikika katika mtaa huo watu hawakuelewa nini hasa chanzo cha hayo yote, mama Juma akazidi kuchukiwa na kila mtu. Serikali ya mtaa ikabidi iingilie kati swala hilo mama Juma akashikiliwa na vyombo vya dola lakini hata hivyo wakamuachia kwa kukosekana ushahidi ambao ungemueka hatiani. Watu wote wakakata ushirikiano na mama Juma wakiamini kuwa yeye ndiye mbaya wao.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
BAADA YA MIEZI MIWILI
Matukio ya ajabu hayakukoma ndani ya nyumba ya mzee Kobelo, vita baridi viliendelea baina ya mama Salehe na mama Juma, watu hawa hawakuchangamana hata kidogo, jambo lolote baya linapotokea mama Salehe anaamini ni kazi ya mama Juma. Mama Salehe aliendelea na kampeni za kumsema vibaya mama Juma na kufanya baadhi ya wapangaji kujitenga kabisa naye.
Usiku mmoja mama Juma alijisikia vibaya na haikuwa bahati kwani baba Juma siku iyo aliingia kazini usiku, hivyo akawa hana wa kumsaidia. Kadri ya muda ulivyozidi kwenda ndivyo hali yake ilivyozidi kuwa mbaya akahisi kuishiwa nguvu huku Juma ambaye ni mdogo sana mwenye umri wa miaka 3 akilia asijue la kufanya juu ya mama yake. Juma alijaribu kufanya kila aliloweza kumsaidia mama yake lakini kwa akili zake za utoto hakuweza, ikabidi atoke nje kuomba msaada, mtu wa kwanza kumuona ni mama Salehe hakujali tofauti iliyopo kati ya mama huyo na mama yake akamfata na kumuelezea hali ya mama yake lakini mama Salehe akacheka kwa dharau na kumsonya kisha akaingia ndani kwake,
“Mama Salehe, njoo umuone mama yangu tafadhali”
“Wewe mtoto koma tena ukomaye kama huyo mama yako kakutuma basi mambie safari hii amechemka, msyuuuu!” alijibu mama Salehe.
Juma akaachana na mama Salehe akagonga mlango wa pili, ukafunguliwa na walipoona kuwa ni Juma aliyegonga wakafunga mlango kwa haraka na hamna aliyejishughulisha kumsikiliza. Wakati hayo yanaendelea Mdidi naye ndiyo akawa anarudi toka kwenye shughuli zake, akashangazwa na hali ile hasa baada ya kuona Juma Analia sana, akamsogelea na kumuhoji kwa upole.
“Kipi kinachokuliza mdogo wangu?”
Juma aliposikia ile kauli akamkumbatia Mdidi kwa nguvu huku machozi yakiendelea kumtoka,
“Usilie sasa embu nieleze kinachokusibu”
“Kaka tafadhali msaidie mama yangu”
“Mama yako anashida gani?”
“Twende ukamuone”
Mdidi akaongozana na Juma hadi kilipochumba chao na kuingia ndani, hali aliyoikuta hakuamini macho yake, mama Juma akawa chini akipigania uhai wake, Mdidi aliumia sana.
“Kwanini hukuomba msaada kwa wengine?” akauliza kwa hasira.
“Kila niliyejaribu kumfata hakutaka kunisikia”
Mdidi alimuhurumia sana Juma katika hali yake ya utoto kukutana na magumu kama yale ni wazi yatamuathiri sana kisaikolojia. Mdidi akajitahidi kumyanyua mama Juma pale chini na kutoka naye hadi nje, akaangalia milango ya wapangaji waliojifanya kuwa hawana wanachokielewa, alipoangalia saa yake akagundua ndiyo kwanza ilikuwa saa 3.30 usiku akashangaa mno watu kujifanya wamelala muda huo. Akamtoa hadi nje kabisa ya nyumba na kwa bahati nzuri akakutana na bajaji iliyowazi, akaikodi na kumkimbiza hospitali. Hali ilizidi kuwa mbaya kwani pamoja na kufika hospitali hakupewa huduma kwa haraka. Mdidi alichukia Zaidi na kuamua kuingia chumba cha daktari lakini kwa bahati mbaya daktari hakuepo ikabidi awafate manesi.
“Kwanini mmekosa roho ya kibinadamu wakati ninyi ni binadamu, mnawezaje kumuacha mgonjwa katika hali ile bila kufanya lolote,” aliongea Mdidi kwa hasira sana.
Manesi wakamuangalia bila kujibu lolote, wakati akiendelea kutafakari la kufanya Juma akamfata huku akilia, Mdidi alivyoona ivyo ikabidi atimue mbio hadi alipo mama Juma, alipomgusa akagundua mapigo yamoyo yameshuka sana, Mdidi akajikuta akitokwa na machozi asijue la kufanya, akawarudia tena manesi.
“Mgonjwa huyu akifa leo, sitowaacha lazima niwashtaki,” aliongea kwa hasira huku akipiga piga meza na kuwafanya manesi waogope sana.
Wakati huo huo daktari akawa kashafika kwa haraka wakampeleka katika chumba cha dharula ikabidi wafanye CPR ili kushtua mapigo ya moyo, wakayashtua Zaidi ya mara tatu Mungu mkubwa yakarudi katika hali ya kawaida. Daktari akamtaka Mdidi atulie hili aendelee na kazi yake. Mdidi akamchukua Juma na kukaa naye kwenye benchi kusubili taarifa ya daktari. Baada ya muda mfupi daktari akamuita,
“Una uhusiano gani na mgonjwa?”
“Mpangaji mwenzangu”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ana mume au anaishi mwenyewe?”
“Dokta sidhani kama naweza kukupa majibu sahihi ya maswali utakayoniuliza, naomba usubili nifanye na mawasiliano na mumewe au yeye mwenyewe akiamka atakupa majibu sahihi”
Daktari akakubalina na Mdidi, akamuacha aende. Mdidi akambeba Juma aliyepitiwa na usingizi kisha akatoka nje na kukodi bajaji iliyomrudisha nyumbani, kwa kuwa hakuwa na namba ya simu ya baba Juma, ikamlazimu ampigie baba mwenye nyumba ili aweze kupata mawasiliano na baba Juma. Akafanikisha kutoa taarifa kisha akaenda bafuni na kurudi ndani walau kuupumzisha mwili. Usingizi haukuja kwa haraka akafikiri sana kuhusu maisha ya nyumba hiyo akautazama mtaa mzima akabaki akisikitika asijue la kufanya.
Asubuhi na mapema Mdidi akadamka na kujiandaa kwenda hospitali, alipomtazama Juma akagundua kuwa bado amechoka, akaamua kumuacha na kuanza kwenda lakini kabla hata hajatoka nje simu yake ikaita, kuiangalia akakuta ni baba Juma akaipokea.
“Habari ya asubuhi Mdidi”
“Salama kaka sijui wewe”
“Mimi mzima wa afya, vipi Juma ameamkaje?”
“Naona amechoka sana kutokana na hali ya jana bado amelala, ila mimi natoka nyumbani nakuja hospitali”
“Nashukuru sana ndugu yangu na usisumbuke hapa ninavyoongea mama Juma anaendelea vizuri na muda si mrefu ataruhusiwa kurudi nyumbani”
Mdidi alifurahishwa na taarifa ile, ikabidi arudi ndani kwake na kujitupa kitandani kisha akaendelea kufikiri juu ya matukio yanayotokea katika nyumba hiyo na mtaa kiujumla.
“Hivi kweli uchawi upo kama watu wa mtaa huu wanavyoamini, uchawi ni nini? Na mchawi ni mtu wa aina gani? Je mama Juma kweli ni mchawi, kamuua Salehe ili afaidike nini? Kamuua Upendo ili apate nini? Kaua vijana 10 kwani yeye hatokufa,” Mdidi aliendelea kujiuliza na kujipa majibu mwenyewe japo hayakuweza kumridhisha.
“Jamii hii ujinga umewapofusha, kwanini watu wanashindwa kufikiri kwa upana? Kwanini wameshikiria Imani potofu, Je ni kweli mafanikio ya mtu huja kwa kafara kama wao wanavyodhani! Kwani mtu ukijituma katika unachofanya hauwezi fanikiwa?. Nifanye nini kuiokoa jamii hii, watoto zao hawafanyi vizuri mashuleni na hata waliobahatika kufanya vizuri hawapati ushirikiano wa kutosha, ooh! Mungu nifanye nini?” Mdidi alizidi kuzama katika dimbwi la mawazo akajikuta akiwa katika dunia ya peke yake huku akishindana na nafsi yake katika kufanya maamuzi.
Muda ukaenda kwa kasi sana Mdidi akapitiwa na usingizi mzito, alishtusha na joto la mchana akaamka na kutazama pembeni hakumuona Juma, ikabidi atoke nje na kukuta mlango wa mama Juma upo wazi bila kusita akabisha hodi na Juma akatoka,
“Karibu kaka!”
“Ooh! Juma upo na nani?”
“Nipo na baba ila ameenda dukani”
“Mama yuko wapi?”
“Hakurudi hapa alichukuliwa na mamkubwa wa Kimara”
“Ayah! Asante kwa taarifa”
Mdidi akamshukuru Juma kisha akageuza kuelekea chumbani kwake lakini kabla hajaingia ndani Juma akamuita,
“Kaka!”
Mdidi akageuka na kumtazama Juma kisha akatabasamu,
“Mama yangu si mtu mbaya kama wakina Yusufu wanavyosema, siku hizi hawataki hata kucheza na mimi,” alisema Juma
“Ni kweli mama yako ni mtu mwema na hana ubaya wowote, usihuzunike wakikutenga hivi karibu wataelewa tuu wema wako na utakuwa na marafiki wengi sana”
“Kweli kaka!”
“Ndio!”
“Ila mama Salehe anamtesa sana mama yangu”
“Usiseme na usifikirie ivyo, kila mtu ana mapungufu yake kwa iyo mchukulie mama Salehe kama alivyo wala usimchukie sawa!”
“Kwanini wewe tu ndiye upo upande wetu!”
“Hahahahah! Juma si nishakwamabia kuwa nyie ni watu wema”
Wakaongea mengi huku Mdidi akizidi kumjenga Juma kwa maneno yenye hekima na busara.
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********************
Jioni ya siku hiyo Mdidi akaamua aingie mtaani hili atafute majibu ya maswali ambayo kwa hakika yalimuumiza kichwa, akafika kwenye kijiwe kimoja cha muuza viazi au maarufu kama kwa Yahaya machipsi, kwa kuwa hakuwa na ratiba za kupika siku iyo akaona ni vyema aagize viazi,
“Habari braza!”
“Njema tuu, vipi nikuwekee zege, vikavu, mishkaki au hawa kuku wasiokuwa na baba”
“Duuh! Kuku wasiokuwa na baba?”
“Inaonekana mgeni wewe?”
“Ni kweli braza”
“Basi usijali wenyeji tupo, kaa kwenye benchi nikufanyie mazuri”
“Poa fanya basi na mishikaki”
Mdidi Akaka huku akiendelea kusubili oda yake itoke, wateja walikuwa wengi na iyo ilimpa nafasi ya mdidi kusikia nini kinachopendwa kuzungumzwa,
“Oyah! Yahaya angalia relini”
“Kuna nini tena?”
“Yule mzee nuksi anapita”
“Apite huko huko asisogee huku”
“Hahaha! Unaogopa utafunga biashara bila kupenda eenh!”
“Aah! Wazee kama wale nuksi wewe si unaona mambo yote yaliyotokea kwenye nyumba ya mzee Kobelo sababu ni yeye”
“Ila yuko fiti mzee naona kampika mama Juma vilivyo haguswi hovyo”
Stori zile zilimgusa moja kwa moja Mdidi, akili yake ikaanza kufunguka na akahitaji kujua Zaidi yule mzee ni nani na kwanini ahusishwe na matatizo yaliyotokea?
“Braza eenh! Toka nimefika nasikia sikia tuu stori za ajabu ajabu mara mama Juma, mara huyo mzee kwani nini shida Zaidi”
“Daah! Kweli wewe mgeni asee, Musa eenh geuza viazi hivyo” alisema Yahaya huku akikaa sawa kumdadavulia Mdidi kilichojili.
“Siku kadhaa kulikuwa na ugomvi kati ya mama Salehe na mama Juma, alafu yule mzee alitokea kuamulia lakini mama Salehe na baadhi ya watu walimjibu vibaya, asee kilichotokea jioni yake ni noma”
“Mhmh! Nini kilitokea”
“Bhana wee! Usiombe wewe sikia tuu, hali ya hewa siku hiyo ilibadirika watu tukajua leo gharika itatokea ila haikuwa hivyo jioni hivi, Salehe akafa na daktari hakujua ugonjwa, basi mwisho wa picha mama Juma ndiyo akagundulika muhusika”
“Mhmh! Kaka na wewe unaamini kweli mama Juma alimuua Salehe?”
“Aah! Kabisa yaani mama Juma na yule kikongwe inaonekana wanafahamiana na yule mzee mwanga kweli kweli kila mmoja anajua habari zake, alafu baada ya kifo cha Salehe biashara zake zikashamiri na kujenga kashaanza”
“Hahahaha! Je ulishawahi kushuhudia uchawi wake kwa macho yako,” Mdidi akauliza.
“Aah! Hapana mimi nasikia sikia tuu, ila kushuhudia hata siku moja sijawahi, alafu mbona unauliza maswali kama vile polisi”
“Hamna mimi ni mtu wa kawaida ila broo kumbe hata wewe mchawi”
“Nini?”
“Wewe pia mchawi japo sijui umemua nani?”
“Daah! Dogo naona sasa wanishushia heshima”
“Hapana kwa maelezo yako tuu inaonesha wewe mchawi, kama mama Juma anapata wateja wengi kwenye biashara yake je vipi kuhusu wewe, una wateja wengi je na wewe ni mchawi au umetoa kafara?”
“Aah! Wewe mchawi Mungu peke yake, akiamua iwe itakuwa na akiamua isiwe hata ufurukute vipi haitokuwa, mimi nina maneno mwengi ndio maana wateja wanapenda kuja kwangu hata ivyo wewe mwenyewe si unaona chipsi zina viwango vya kimataifa,” alijibu Yahaya.
Mdidi alicheka sana swala ambalo lilimshangaza kidogo Yahaya na watu wachache waliokuepo eneo hilo.
“Vipi mbona wacheka”
“Nimefurahi tuu”CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kilichokufuraisha ni nini?”
Mdidi akamgeukia jamaa mwengine ambaye walikaa kwenye benchi moja wote wakisubilia zamu yao ifike wahudumiwe, pia akamtazama msichana ambaye alikaa pembeni kidogo yao kisha akawaambia,
“Kama Yahaya machipsi anaamini kuwa mchawi ni Mungu pekee, na mafanikio ya biashara yake yametokana na jitihada zake binafsi na kudra za mwenyezi Mungu, je! Vipi kuhusu mama Juma hakuwahi kufanya jitihada au hakuwai kumuomba Mungu amsaidie?”
“Daah! Kweli asee kwa hili Yahaya umebugi inawezekana tunamuhisi mtu vibaya”
“Nyie ndio hamna akili kabisa, kwani mmesahau ile jioni ambapo vijana 10 walifariki ghafla baada ya kumvamia mama Juma?” aliongea yule msichana ambaye anatambulika kwa jina la Aisha.
“Umeuliza vyema dada yangu hongera kwa hilo lakini je ulimuona mama Juma akiwavamia wale vijana na kuwadhuru kwa namna moja au nyingine?”
“Hapana sikumuona”
“Sasa umepata wapi ujasiri wa kusema kuwa mama Juma ndiye muhusika”
“Daah! Kaka wewe kweli mwanafalsafa mimi naitwa Jumbe maarufu kama Jumbe mikoba, kitaa kizima kinaelewa kazi yangu nikiwa uwanjani sipendi Ujinga” alisema yule kijana ambaye alikaa benchi moja na Mdidi huku akionesha kukubali sana maneno ya Mdidi.
“Naitwa Mdidi, ni mgeni maeneo haya”
Mdidi akakabidhiwa chipsi zake ikabidi awaage na kuondoka, lakini kabla hajafika mbali Yahaya akamuita.
“Mdidi eenh! Nimejifunza vitu vingi kutoka kwako leo, uwe unakuja tujadili mambo mawili matatu, maana naona leo watu wote walikuwa wanasikiliza hoja zako”
“Hahahah! Usijali kaka nitakuja tuu”
Mdidi akaondoka na kuacha gumzo huku nyuma,
“Tatizo Yahaya unaongea sana ila huna hoja, leo umekutana na mbabe wako,” alisema Aisha.
“Daah! Huyu jamaa anaitikadi kali kwa maswali yale asee sizani kama hata demu anaye”
“Kwanini asiwe naye wakati yeye ni mwanaume”
“Mhmhm! Hata akiwa naye labda sio wa mtaa huu”
“Kwa hiyo Yahaya umetudharau wasichana wa mtaa huu kuwa hatuwezi kuwa na yule jamaa”
“Hamna atakayeweza na nyie mshazoea kupiga mizinga mara bebi nipe hela ya saluni, mara lotion imeisha mara sijui kuna shughuli ya Fatuma naomba hela ya sare, kwa yule jamaa mjipange”
“Huhuhuhu! Pole wee! Mwanamke siku zote akitaka kitu atakipata tuu”
“Ila sio kwa wewe! Ata ufanyaje huwezi kuwa na yule jamaa”
“Jamani mbona wanidharau ivyo”
Yahaya akendelea kumtania Aisha na kuwafanya wateja wengine kufurahi kutokana na vituko vya hapa na pale.
*******************
Siku iliyofuata Mdidi akaamua afunge safari hadi mtaa wa 8 ambapo yule Mzee anaesadikiwa kuwa ni mchawi anaishi. Haikuwa rahisi kwa Mdidi kufahamu ni nyumba gani hasa ni makazi ya mzee Yule. Wazo la kuuliza likamjia lakini swali ni kwamba atamuulizia kwa jina lipi? Na ata akisema anamuulizia mzee mmoja je mtaa huo unawazee wangapi watu watawezaje kumuelekeza kwa yule mzee aliyemkusudia, baada ya kuwaza sana akaamua atoe kitambulisho kwenye begi alilobeba na kuvaa shingoni kisha akatoa faili moja na kulishika mkononi.
“Nitapita kwa wazee wote haijalishi watakuwa wangapi lakini naamini nitampata yule niliyemkusudia,” alisema Mdidi kwa sauti ya chini ambayo haikuweza kusikika kwa yeyote aliye karibu na mazingira hayo.
Mdidi alipojiridhisha kuwa yupo mtaa wa 8 akaangaza huku na huko ili aone mtu wa kumuuliza na kwa bahati akakuta vijana wawili wakiwa wanachimba shimo, akawasogelea na kuwasabahi.
“Habari zenu!”
“Salama tuu sijui wewe!”
“Kwangu kwema! Poleni na kazi”
“Aah! Tushapoa si unajua Mungu alishasema wanaume tutakula kwa jasho”
“Ni kweli ndugu! Ila nina shida kidogo naomba niwaulize”
“Kuna mzee namuulizia nimeelekezwa anakaa mitaa hii”
“Mzee yupi tena?”
Swali likawa gumu sana kwa Mdidi kwani hakuwa anajua lolote juu ya mzee huyo Zaidi ya ile sifa ya uchawi iliyompa umaarufu kule mtaani kwake, akajiuliza awaambie mzee mmoja mchawi ila akaona si vyema, akafikiri tena kisha akawatazama na kuwaambia.
“Mzee mmoja maarufu sana”
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘Aah! Mzee Kilonda”
Mdidi hakusema ndiyo wala hapana sababu hakujua hata jina la huyo Mzee, akabaki akiwatazama wale vijana kwa tabasamu ili wasigundue shaka alilonalo moyoni,
“Kwa mzee Kilonda si mbali sana na hapa, nyoosha nah ii njia mbele utakuta mti wa mwembe kata kulia kisha hesabu nyumba 3 alafu uliza”
“Sawa akhsanteni sana”
“Karibu tena”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment