IMEANDIKWA NA : TATU KIONDO
*********************************************************************************
Sehemu Ya Kwanza (1)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa siku ya jumapili majira ya jioni, Ahmed alikuwa amembeba mtoto wake Baraka, wakati huo alikuwa na umri wa miezi mitano.Bwana Ahmed alimtazama mtoto wake miguu yake ilivyokuwa, akajaribu kumsimamisha lakini akaona hali isiyokuwa ya kawaida kwa mtoto huyo, akaanza kugundua kitu kisicho cha kawaida, mara alimuona Baraka akijikunja miguu na kuanza kulia Bwana Ahmed alipata mshangao akafanya kama vile anataka kumnyoosha miguu, bado Baraka akuonyesha dalili za kunyooka kwa miguu. Hofu na mashaka ikamjia, alimuangalia mtoto wake kwa makini kisha akaona tatizo kwenye miguu ya Baraka. Ahmed akaamua kumuita mkewe
“Mama Baraka’’
“Labeka’’
“Hebu njoo mara moja”
“Nakuja mume’’ Bi Mwasi alimjibu mume wake
“Hebu sogea karibu umwangalie mtoto…..”
“Ana nini, tena?”Bi mwasi aliuliza kwa mshangao na kuonyesha wasiwasi kwa wito huo.Bi Mwasi alimsogelea taratibu, huku akiwa na hofu moyoni, mwili ukimtetemeka mithili ya mtu aliyekimbizwa na simba polini.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mke wangu, hebu mwangalie mtoto wetu vizuri, naona ananitia wasiwasi”.
“Wasiwasi gani tena”Bi.Mwasi aliendelea kutaharuki.
“Ninahisi kama miguu yake imepinda’’
“Hee! Kwani unamwonaje?”Bi.Mwasi aliendelea kuhoji
“Kwa kumuangalia tu hivi hivi huwezi kujua mpaka umchunguze nilikuwa namsimamisha lakini hasimami vizuri, angalia miguu yake ilivyokuwa kama imegeuka pembeni”Bwana Ahmed alimwambia mkewe.
Bila kuongeza neno Bi.Mwasi alimchukuwa Baraka kutoka mikononi mwa baba yake na kumbeba. Alimsimamisha miguu ikawa imegeukia upande mwingine yaani haikanyagi unyayoni Kama kawaida ila yeye anakanyagia mwishoni mwa unyayo, Alimsimamisha tena na tena lakini Baraka hakusimama vizuri.
Akaamua kumlaza chali na kumnyoosha miguu yake kisha kumwangalia mara mbili mbili, kuanzia miguu mpaka mapajani nae akagundua kutokaa sawa miguu ya Baraka.Mara pale pale Bi.Mwasi akaangua kilio kikubwa kama mtu aliyepokea taarifa za msiba, akaona furaha yake imeyeyuka kwani alikuwa anampenda sana mtoto wake kuliko kitu kingine chochote.
“Mungu wangu, imekuwaje kwani mume wangu? Bi.Mwasi aliuliza baada ya kumchunguza
“Kwa kweli nimemsimamisha nikaona miguu imekaa upande, sio kawaida kwa watoto kusimama hivi mke wangu”Bwana Ahmed alisisitiza
“Hee! Si mkosi huu tena jamani”Mwasi alisema wa huzuni
“Usilie kwanza mke wangu”
“Hapana mwanangu jamani,”Mwasi alijibu huku akiendelea kulia
“Sasa inabidi mtoto tumpeleke hospitali”
“Sawa mume wangu”Mwasi aliitikia kwa unyonge uliojaa simanzi, huku akijifuta machozi kutumia ncha ya upande wa kanga yake aliyokuwa amevaa.
Mwasi alijifuta machozi na kuelekea jikoni kumalizia kupika chakula cha jioni,Huku akimuacha Baraka kwa Bada yake.Pale nje Ahmed aliendelea kumchunguza Baraka kwa kumnyoosha nyoosha kiwingo cha miguu.Baada ya muda Mwasi alimaliza kupika chakula cha usiku kisha akapika uji wa Baraka na kuuweka kwenye chupa,uji huo wenye mchanganyiko wa ulezi na kalanga.Baada ya hapo walikula chakula na Mtoto wao mkubwa Tausi.Siku ya pili ilikuwa Jumatatu Mwasi aliamka asubuhi na mapema, akamkogesha mwanae na yeye kujiandaa kisha wakajumuika pamoja mezani kupata kifungua kinywa.Muda si muda walimaliza kupata cha Asubuhi kisha kwa pamoja wakaanza safari ya kuelekea hospital na Mume wake Ahmed.Katika mji huo si kawaida kwa wanaume kuongozana na kuwasindikiza wake zao kuwapeleka watoto hospital.Mara chache sana wanaume uonekana wakiwa na wake zao hospital.Mara nyingi ujaa wanawake hasa sehemu ya kiliniki ya watoto.
Mwasi na Mumewe Ahmed walitembea kwa miguu mpaka kituo cha daladala Buguruni sheli,kisha wakapanda daladala inayokwenda mwenge,Baada ya mwendo wa nusu saa walifika na kushukia Hospitali ya Amana.Amana ni hospital ya wilaya Temeke, iliyopo mkoa Dar es salaam.Walipofika walienda moja kwa moja kwa Daktari wa mifupa, siku hiyo wagonjwa walikuwa wengi. Bwana Ahmed na Mkewe nao wakapanga foleni na kusubili waingie kwa Daktari.Baada ya muda zamu yao ilifika wakaingia kwa Daktari.
“Habari yako, Daktari?”Mwasi akaanza kumsalimia
“Nzuri Mama, karibu sana”Daktari aliwakaribisha
“Ahsante,”Ahmed aliitikia
“Mtoto anasumbuliwa na nini?”
“Ana tatizo!”Mwasi alisema kwa ufupi
“Tatizo gani?”
“Miguu Daktari, naomba umuangalie alivyo,miguu yake haipo sawa sawa!”Bi.Mwasi alisema.........
Baada ya hapo Daktari aliinuka na kumuangalia mtoto kwa umakini huku akimnyoosha nyoosha miguu, Daktari hakutaka kujiridhisha akamfanyia uchunguzi wa kutosha pamoja na kumpiga picha ya utla sound ili kujia tatizo. Mwishowe akapata jibu kweli miguu ya mtoto huyo haipo sawa imepinda yaani kuwa na matege kama watu wanavyoita.Alikuwa na matatizo ya mifupa hivyo imepelekea kupooza kwa misuli iliyounga Magoti na kiwiko cha miguu yote miwili kukosa nguvu ya kusimama sawa.Baada ya vipimo hivyo Daktari aliwageukia na kuwaambia ukweli kuhusu tatizo linalomkaabili mtoto wao, aliwaeleza na kuwajulisha kuwa hatoweza kutembea vizuri kwani sehemu ya kiwiko cha miguu yake hakina uwezo wa kukaza ili iweze kusimamisha miguu kama kawaida. Hivyo miguu yake inaonekana kuwa mifupi kutokana na muonekano wake,pia Miguu yake kukosa uwezo wa kutembea umbali mrefu, hivyo hakuna dawa wala tiba inayousiana na hali hiyo kwani amezaliwa akiwa na tatizo hilo.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huu mtihani sasa, Lakini hatuna jinsi kukubali”Ahmed alisema kwa unyonge mara tu daktari alipomaliza kuwaeleza.
“Mi nashauri mumtunze mtoto wenu vizuri mumpe haki zote muhimu, sawasawa na watoto wengine pia atakapoanza kutembea basi Mumzoeshe kufanya mazoezi yatakayomfanya miguu yake kuchangamka na hali yake”Daktari alishauri
“Daktari unahisi hali hii imesababishwa na nini?”Ahmed alitaka kujua
“Unajua tatizo la mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu linajulikana kama Birth Defect,hivyo mtoto alikubwa na tatizo linaloitwa “orthopaedic birth defects hili ni tatizo ambalo utokea pindi mtoto anapokuwa anaendelea kukua pindi akiwa tumboni,mifupa na misuli huathiriwa na kupelekea mtoto kuzaliwa na ulemavu.Sababu nyingi zinapelekea kutokea tatizo ilo ni kurithi vinasaba visivyo vya kawaida kutoka kwa wazazi wake,sumu ambazo usababisha mtoto kuwa hivyo pamoja na unywaji pombe,utumiaji wa madawa ya kulevya,uvutaji wa sigara,kutumia dawa kwa muda mrefu au kutokana na chemical ambazo mama anazivuta pindi awapo mjamzito”Daktari alijibu kwa kirefu.
“Ahsante sana daktari tunashukuru kwa kutujulisha”Mwasi alishukuru Daktari huku wakiwa wima tayari kwa safari
“Sawa karibuni sana, msipuuze kumpa malezi mema mtoto wenu.Atakapokuwa mkubwa atafanya kila kitu mwenyewe”Daktari alisema
Siku zilikatika,wiki zikapita miezi ikateketea,Baraka akaendelea kukua kidogo kidogo na hali yake hiyo hiyo.Ahmed na Mkewe walikubaliana na hali ya mtoto wao.Walimpenda na kumtunza,Ahmed alimnunulia Baraka,miwani,kofia kubwa ya kujikinga na Jua,Tausi mtoto wa kwanza wa Ahmed alipenda kukaa karibu na mdogo wake Baraka ,walicheza na kufurahi pamoja alionyesha mapenzi ya huruma kwa mdogo wake.Baraka alipofikisha umri wa miaka mitano, Ahmed na mkewe walimkataza kutoka nje mwenyewe, ata pale alipojalibu kunyanyuka alikatazwa na kutakiwa kukaa pale pale. Ahmed na Mkewe walipuuza maelezo waliyopewa na daktari, badala yake wakaanza kumtesa Mtoto wao. “Wee Baraka! Tulia hapo hapo usiondoke! Usije ukanitafutia matatizo mengine mtu mwenye Albino wakikuona watakuchukua,hujui kutembea vizuri unafikili utakimbiaje si wanakubeba juu juu tu”kila wakati Mwasi alisikika akimsema mtoto wake,Kuashiria huruma aliyokuwa nayo kwa mtoto wake asije akauwawa na kukatwa viungo.Wakati mwingine Baraka alikuwa analia kwa uchungu sababu alichoka muda mwingi kukaa ndani peke yake bila kutolewa wala kunyanyuliwa.
Siku moja mama yake alimuacha peke yake ndani, dada yake Tausi alikwenda shuleni hivyo siku hiyo alibaki pekee nyumbani.Baraka akiwa anajisikia haja aliona bora atoke nje akajisaidie, alijikokota pale kwenye kiti alichokuwa amekaa na kuinuka.Wakati Baraka akiwa anapiga hatua mbili mbele alijikwaa na kuanguka chini kama mzigo.”Puu”Maskini Baraka hakuweza kunyanyuka, alilala pale pale alipoangukia kila alipokuwa akijitaidi kuinuka alishindwa kwani hakuwa na nguvu za kumuwezesha kuinuka.Mama yake aliporejea, alimkuta Baraka amelala chini.“Jamani mwanangu umefanya nini sasa, yaani nikitoka mara moja tu na wewe unaanza kunyanyuka, mtu mwenyewe unaijua hali uliyonayo mwanangu utulie, utakuja kupata matatizo mengine tena”.Mwasi aliendelea kumsema mtoto wake huku akimnyanyua na kumlaza kitandani, Baraka alilia na kumtaka mama yake yake msamehe.Baraka anapenda atolewe nje lakini mama yake alikataa kumtoa, ata pale dada yake Tausi anapojalibu kumtoa Mama yake uwa mkali na kuamuru mara moja Baraka akakae ndani.
*******
Ilikuwa saa nane mchana sauti na vifijo ziliposikika kutoka nyumbani kwa Bi.Mwasi .Majirani walikuwa na furaha kubwa, furaha hiyo ilitokana Mwasi au mama Tausi alipojifungua mtoto mwingine wa kiume.Majirani hao waliingia ndani na kumpongeza kwa kusema”Hongera jirani kwa kupata Baba.Bi Mwasi aliwashukuru majirani zake kisha wakakumbatiana kwa furaha, Wakati wote huo Mumewe alikuwa hajafika kutoka kazini.
Pamoja na kwamba majirani walifurahi sana lakini Bi.mwasi alikuwa amezidi kwa furaha,Meno yote thelathini na mbili yanaonekana meupe.Wakati wote huo majirani wakifurahi,Mkunga alikuwa katika pilika pilika za kumshafishaMtoto.Hata hivyo mtoto huyo alikwishasafishwa na wakunga wa kituo cha afya Amana,ambako Mwasi alikwenda kujifungua.Pamoja na furaha zote zilizokuwemo ndani ,mkunga hakuonekana na furaha hata kidogo.Uso wake ulikuwa umekunjika,yeye ndiye aliyekuwa amemchunguza na kumbadilisha nguo mtoto huyo alizokuwa amevalishwa kule hospitalini.Hata Mwasi mwenyewe alikuwa hajamuona katika ukamilifu wake....
Wakati furaha zinaendelea, Ghafra Bwana Ahmed aliingia ndani akitokea kazini kwake, akapigwa na mshangao.Mara alisikika akisema “Jamani,kuna nini hapa ?,naona watu wamefurahi furaha isiyo na kifani’’aliongea huku akicheka cheka mpaka meno yake yote yalionekana “Bwana hongera,leo umepata mtoto wa kiume,ndiyo maana na sisi majirani tume furahi mpe jina mtoto Baba’’majirani walimwambia kwa pamoja huku wakiwa na nyuso zenye furaha .Bila kujua siri aliyoiona mkunga Bwana Ahmed alivyoyasikia maneno hayo alifurahi sana siku hiyo furaha yake yote ilionekana machoni mwa majirani hao,alianza kurukaruka huku na kule kisha akisema “Ama kweli mungu akiamua kukupa atakupa kwa wakati wake,kinachotakiwa usikate tama, siku zote hamtupi mja wake,hasipokupa leo basi kesho atakupa”. Maneno ya Bwana Ahmed yalikuwa na maana yake kwani yalitoka ndani ya moyo mwake ambapo sasa alikuwa amepata mabadiliko yalitoka katika majonzi na kuingia kwenye furaha.Iliwachukua miaka saba toka kumpata mtoto tausi hawakupata tena mtoto mwingine walimaliza waganga na waganguzi bila mafanikio pia makanisani na msikitini walikwenda Bi.Mwasi kuombewa labda ana majini. Pamoja na hayo yote kufanyika, mtoto wa pili aligoma kutokea, Mambo ya waganga kushindikana Bi.Mwasi na Bwana Ahmed walikata tamaa ya kupata mtoto mwingine.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya miaka mingi kupita wakiwa hawana dalili ya kupata mtoto mwingine,walimwachia mungu itakavyokuwa na kuomba sana wajaaliwe.Siku moja Bi.mwasi na Mumewe wakiwa sebleni wamejipumzisha huku wakisikiliza redio iliyokuwa katika sebule hiyo,punde walisikia kipindi cha afya ya jamii kikitangazwa.Katika kipindi hicho daktari alizungumzia tiba ambayo inaweza kumfanya mwanamke asiyekuwa na tatizo, kukaa muda mrefu huweza kuzaa tena .Bi.mwasi aliamua kusikiliza ushauri wa daktari, kesho yake akaamua kwenda hospitali ile iliyotajwa katika kipindi hicho na alipofika akaonana na daktari wa matatizo ya wanawake.Daktari huyo alimfanyia vipimo na kumpatia matibabu.Kuanzia hapo Bi.Mwasi na Bwana Ahmedi wakajenga matumaini makubwa ya kupata mtoto ,baada ya kuhangaika kwa waganga wa jadi na sehemu mbalimbali ili kupata mtoto mwingine.Siku hiyo ndio maana Bwana Ahmedi alikuwa hashikiki kwa furaha.Wakati wote Bi.Mwasi alipokuwa mjamzito,Bwana Ahmed alimtuza sana mkewe.Alimkataza kubeba mizigo mizito na wakati mwingine aliingia jikoni kupika mwenyewe.
”Hii ni bahati yangu niliyopewa na mungu, sasa mtoto nitamwita Baraka Ahmed’’Bwana Ahmedi alisikika akisema huku akiwa na Furaha tele kuona familia yake ameongezeka.Baada ya kufikiri kwa muda mfupi.Furaha za bwana Ahmedi nazo zilikuwa hazijui mkunga aliyokuwa na siri nzito.Hii ilitokana na hata majirani walikuwa bado hawajamuona mtoto tokea vidoleni hadi utosini.Mara nyingi wazazi wakijifungua huridhika kuambiwa na madaktari kuwa umejifungua mtoto wa kiume au wakike.
Mara nyingi, hawawatazami kwa makini pindi wanapojifungua,ndio maana wakati mwingine watoto wao wakabadilishwa au kuibiwa bila wao kujua .Kwa uzoefu wake mkunga Yule wa kienyeji amekwishajua kinachoendelea kwa mtoto Yule.Hakika kwa kumtazama ghafla mtu asingejua kilichomsibu mtoto huyo maana rangi ya ngozi yake ilikuwa ya ajabu,nyeupe si nyeupe,sijui ilikuwa rangi gani?.Siku zilikatika Kama mwezi angani hatimaye Baraka alikuwa vizuri, mama yake alimlea vema Baraka akapendeza na kuwa mwenye afya tele.Siku moja majira ya jioni Bi.Mwasi alimwangalia mtoto wake na kugundua hali isiyo ya kawaida ngozi yake ilikuwa nyeupe isiyo badilika, akamwangalia machoni akaona Baraka muda mwingi akiwa anachezesha macho yake, wala mboni ya macho yake haikutulia sehemu moja yalipepesa kila upande.Bi.Mwasi aliogopa alikuwa hajui kinamchomsumbua mwanae.
Siku ya pili Bi mwasi alimfuata mkunga nyumbani kwake akiwa na mwanae mgongoni,alipofika pale mkunga alimkaribisha kisha Bi.Mwasi aliomba amwangalie mwanae kilichomsibu.Mkunga alimweleza Bi.Mwasi hali halisi ilivyokuwa tangu siku ya kwanza mtoto huyo alipozaliwa akiwa na ulemavu wa ngozi.Bi.Mwasi hakuwa na jinsi alikubali maelezo ya mkunga na kurejea nyumbani.Bi.Mwasi alimueleza Bwana Ahmed kuhusu Baraka kuwa Albino,Mumewe alichanganyikiwa,pia hakuwa na jinsi mwishowe wakakubaliana kumlea na kumtunza vema mtoto wao.Wiki ikapita Bwana Ahmed na mkewe wakaizoea hali ya mtoto wao waliendelea kuwa karibu nae, Mama yake alikuwa anamnyonyesha kila wakati hakupenda kumpa mziwa ya ng’ombe ya nayotengenezwa viwandani, Ahmed nae alikataa mwanae kupewa maziwa hayo mara kwa mara.Mama yake alimpa kwa nadra sana maziwa ya kopo kwa sababu hayana ubora kwa afya ya mtoto wake.Baraka aliendelea kukuwa na kuwa mwenye afya bora, Bwana Ahmed alipenda sana kumchukuwa mwanae hasa wakati wa jioni na kucheza nae huku akimbembeleza.
********
Mara nyingi watoto wanapenda kucheza,hupenda kuruka huku,mara waruke hapa na waruke kule.Ukifuatilia michezo yao kwa mara nyingi,utaona ina sehemu katika Nyanja za Sanaa,lakini hayo yote yalikosekana kwa Bahati sababu ya ulemavu wake wa ngozi na miguu.Baraka alikuwa mnyonge akawa mwenye kulia muda mwingi alikosa furaha,akapotelewa nguvu na uchangamfu sababu ya ulemavu ule. Ijapokuwa alikuwa mzuri wa sura, rangi yake ilikuwa maji ya kunde wenye shingo ndefu,
alikuwa mtoto wa pili na wakiume pekee katika familia ya Ahmed na mkewe Mwasi.Lililomkosesha furaha Baraka ni kukosa ushirikiano kutoka kwa familia yake,kwa sabau ya ulemavu aliokuwa nao Dadaye Tausi pekee ndie aliyekuwa msaada kwake.
Baraka alijiona mtu mwenye mkosi wakati wate alionekana mwenye mawazo wazazi wake walichukulia kuwa mlemavu ni kukosa akili na kushindwa kufanya kazi.Walimwangalia kwa huruma na kumwona ni mtu wa kusaidiwa muda wote.Hawakumpeleka tena hospitali kama daktari alivyowashauri,pia hawakujishughulisha na mtoto wao kumsihi kufanya mazoezi maalum kwa ajiri ya kumuwezesha miguu na viungo vyake vifanye kazi vizuri.Wazazi wake walimuona si mtu kamili katika familia,walimkosesha haki nyingi za msingi,utadhani ni mfu ndani ya nyumba yao.Mtoto Baraka alijiona kama mzigo ndani ya nyumba,hakuwa na furaha wakati wote alijiinamia peke yake kulia ndio ikawa sehemu ya maisha yake.......
Baada ya kufikia umri wa miaka kumi,Baraka alianza kutamani kwenda shule.Hisia hizo za kwenda shule ziliibuliwa na dada yake Tausi, kwani muda alipokuwa anatoka shuleni akimletea vitabu vya watoto na kumfundisha kusoma na kuandika.Barakaalifurahi sana anapokuwa anafundishwa na dada yake,sasa akatamani kwenda shuleni kusoma.Kuna wakati Tausi umuachia kitabu ,Baraka alisoma mwenyewe bila kukosea,alisoma kwa ustadi mkubwa ,ukimwona alipokuwa anasoma utadhani amewai kwenda shule yote ni juhudi za dada yake Tausi kumfundisha.Siku moja Tausi alikuwa anamfundisha Baraka,Mama yao alikuja na kuwakuta wakisoma kwa ufasaha.Mwasi hakufurahishwa na kitendo hicho akamfukuza Tausi na kumtaka hasiingie tena katika chumba hicho,kisha akamfungia ndani kwa kufuri.Siku hiyo Baraka alilia sana kumuomba mama yake hamtoa nje,lakini Mama yake alikataa na kuogopa endapo mtoto wake akaenda shule na dadaye atakuja kuuawa.Alimfungia ndani bila kumtoa nje Bahati akawa maisha yake ndani.Kipindi chote anapokuwa ndani,mama yeke umpelekea chakula na maji,ata alipotaka kwenda kujisahidia ugonga mlango au kupiga kelele kisha Baba,Mama au Tausi kwenda kumfungulia na kumsaidia mpaka Msalani kisha umrudisha ndani na kumlaza kitandani au kuendelea kukaa katika kiti chake.
“Jamani maisha gani haya, nimefungiwa kama mfungwa magereza kwa nini Mama hataki kunitoa nje? Angalau nipate hewa,”Baraka aliuliza siku moja baada ya kupelekwa msalani,
“Usijali kaka ipo siku utakuwa huru”Tausi alimjibu
“Dada, dada nataka unitoe nje”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Baraka mdogo wangu, namuogopa mama atanipiga”
“Kwa nini mama hataki kunitoa nje”Baraka aliuliza
“Sijui kwa sababu gani”Tausi alimjibu
“Baraka Baba unataka nini?”Sauti ya mama yeke ilisikika akitoka chumbani kwake
“Mama Nataka unitoe nje”Barakaalimwambia
“Tukutoe nje, Nje utaiona wapi mwanangu na wewe ulemavu ukitoka utakwenda wapi? Mama yake alimwuliza
“Nitakaa hapo hapo nje Mama”Baraka alijibu kwa upole
“Sawa mwananngu nitakutoa usijali ila kumbuka ukitoka nje wapiti njia na majirani watakuona mwanangu na kukuteka, unaona wenzako Albino wanavyokatwa viungo vyao? Mama yake alimwambia.
Baraka akaanza kulia, kwikwi ilimkaba kooni alitamka maneno na kumwambia mama yake “Mimi Albino mlemavu niliyekuwa na miguu yenye uwezo wa kusimama, nitashindwaje kucheza na wenzangu” Bi.Mwasi hakumjibu wala hakujali alichozungumza Baraka, alitoka na kuendelea na majukumu yake alimuacha mtoto wake akilia kwa uchungu.Bwana Ahmed hakushughulika na chochote kuhusu Mtoto Barakazaidi ya kushinda kazini kutwa nzima, akirudi nyumbani usiku anamkuta Baraka ameshalala.
Siku moja majirani wa Bi.Mwasi walikuwa wanaulizana kuhusu kutomuona mtoto Baraka.Katika mjadala huo alikuwepo Mama Juma.Maongezi ya majirani hao kila mmoja akiongea anavyojua yeye kumteta na kutetea kumlaumu Mwasi.Kati ya majirani hao kulikuwa makini na wenye utu ni Mama Juma Pekee ni jirani wa muda mrefu usaidiaana kwa hali na mali.Mama Juma ana mtoto mmoja ambaye anayejulikana kama Juma Kimenya,Mama Juma ni mwenyekiti wa kijiji cha Busale, anapenda sana kuelimisha jamii kuhusiana na mambo mbali mbali kama vile Maradhi,elimu na umuhimu wa chakula.Siku hiyo Mama Juma alikuwa amekaa na wenzake akisubili muda wa kikundi chao kufika,ndio hapo maongezi hayo yalipoanzia walitamba na kutambiana ,mawazo mengi kichwanni akimuwaza Baraka mtoto wa Bi Mwasi.Mama yake umfungia bila wasi wasi kumbe nje majira wengi walimwulizia na kumfuatilia mwenendo wote mtoto Baraka.
“Siku hizi Baraka hatolewi nje?”Mama Juma alianzisha mazungumzo
“Mwenzangu ata Mimi simuoni kabisa siku hizi”Bi.Fatma alisema
“Sijui kwa nini mama yake anamfanyia hivyo”Mama Juma alisema
“Naona labda anasikia aibu kuwa na mtoto Albino mlemavu”Bi.Salma alisema
“Labda kweli anaona atachekwa, au anaogopa Albino atauwawa maana mauwaji yameshamili”
“Unaona hee! Aibu hiyo kuzaa mtoto mlemavu”Bi.Magret alisema
“Bora tu amfungie ndani, maana Kachinjwa bure mtoto Albino”Bi.Salma alisema
“Mmmh haya tutaona mwisho wake”Mama Juma aliwaambia
“Kweli tutaona sijui itakuwaje”Bi.pili nae alidakiaCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*******
Siku moja jirani yake mama Juma aliamua kulivalia njuga suala la mtoto Baraka,alikwenda nyumbani kwa Mwasi alipofika pale aliwakuta , Bi.Mwasi alimkalibisha na kumpa kigoda akakaa.Kwani alikwishapata taarifa kutoka kwa majirani wenzake kuhusu mtoto huyo mwenye matatizo ya ulemavu ndio maana mama yake umfungia ndani bila kumtoa nje.Lakini siku hiyo akaamua kumwendea nyumbani kwake ili kumwambia ukweli kuhusiana na aliyoyasikia. Baada ya Bi.Mwasi na Mama Juma kusalimiana wakaanza mazungumzo
“Baraka mbona simuoni siku hizi anaumwa au?”
“Kwanini? Mwasi aliuliza
“Maana simuoni kutoka nje”mama Juma akauliza
“Haumwi yupo ndani tu”mwasi alijibu
“Umemfungia hee!”Mama Juma alimwambia
“Bibi wee! Mtoto Albino, mlemavu hata uwezo wa kutembea vizuri hana, nje atatokaje?”
“Lakini Mama Bahati, unajua unamuumiza mtoto”
“Shoga ya nyumbani kwangu niachie mwenyewe, wewe hayakuhusu”Mwasi alisema kwa hamaki
“Sawa, lakini kumbuka ninayokwambia unamuumiza mtoto”Mama Juma alisema huku akiondoka.
Mara nyingi watoto walimwita Tausi atoke na Baraka ili wacheze pamoja,lakini mama yake alikataa na kumkalipia Tausi, pale anapojalibu kumtoa nje na kuwafukuza watoto huku akiwashikia fimbo kutaka kuwachapa.Maisha ya Baraka yalikuwa magumu sana kutokana na kutokupata nafasi ya kutoka nje,pia kupata mazoezi ya viungo vyake.Zaidi mtoto Baraka alikuwa Albino mwenye ulemavu,lakini alipata ugonjwa mwingine.Alianza kupooza mwili wake ,mikono yake ikakosa uwezo wa kukamata kitu kizito,masikio yake nayo yakakosa uwezo wa kusikia vizuri.Alibaki kama mzigo husiokuwa na mbebaji ndani ya nyumba.Yote ilisababishwa na kukosa kushirikiana kwa namna moja ama nyingine na watoto wenzake.Baraka alifungiwa tu ndani bila msaada wowote kutoka kwa wazazi wake.
Baraka alikuwa na wakati mgumu sana jinsi alivyokuwa akiendelea kukua siku hadi siku ndivyo akili yake ilivyozidi kutanuka kiali.Siku moja wakati Mwasi na Mumewe akiwa hawapo,Mama Juma alikuja nyumbani kwa Mama Baraka na kubisha hodi,Tausi alitoka ndani na kufungua mlango alimkuta mgongaji ni Mama Juma,Tausi alimkalibisha na kuingia ndani...
Mama Juma alikuwa na madhumuni yake kufika nyumbani pale alitaka kumuona Baraka,Tausi alimuonyesha chumba alichokuwepo , bila Baraka kupoteza muda akaenda chumba alichoonyeshwa.Alipiga hatua mbili mbele akakifikia chumba hicho na kubisha hodi,Sauti kutoka ndani ikasikika Baraka akimtaka aingie Mama Juma bila hujizi alizama ndani.Alipoingi tu alishangaa na kuhamaki kumwona Bahati amekondeana na kudhoofika mwili wake ukiwa na mapele makubwa kutokana na kulala muda mrefu, huku nzi wamejazana mwilini mwake. Baraka alimsalimia kisha Mama Juma akaitikia na kumwambia.
“Baraka wewe upendi kutoka nje?”
“Napenda sana lakini mama hataki nitoke nje” Baraka alijibu
“Kwanini sasa hakukataze kutoka “Mama Juma alimwuliza
“Amesema Mimi mlemavu siwezi kucheza na watoto wenzangu” Baraka alisema huku yakianza kumtoka
“Kwa hiyo Mama yako ndio anakufungia ndani?”Mama Juma alizidi kumhoji
“Ndio amesema nilivyo Albino nikitoka nje tu, watanichinja na kunikatakata” Baraka alijibu kwa unyonge huma machozi yakiendelea kumtoka,
“Sawa naenda, nitakuja siku nyingine kukuona,”Mama Juma alimwambia
“Ahsante Mama, Karibu”
Mama Juma aliaga na kuondoka, kichwani mwake akiwa mtu mwenye mawazo lukuki “Hee! Makubwa haya si ubaguzi huu, unamfungia mtoto wako ndani sababu ni Albino na ulemavu haiwezekani lazima tupige vita ubaguzi huu naona sasa ushakuwa ulimbukeni”Alijisemea moyoni Mama Juma huku akifuata njia inayoelekea nyumbani kwake,hakujali hata Mvua iliyokuwa ikinyesha kwa wakati huo, aliona bora kujitesa kuliko kuendelea kukaa katika chumba hicho kilichokuwa kikitoa harufu mbaya.Baada ya muda Mama Baraka alireje kutoka sokoni, wakati yupo mlangoni kabla ya kuingia ndani alisikia harufu ya kinyesi ikitokea chumbani kwa Baraka hakutaka kuuliza akaingia na kuingia katika chumba hicho.Akaanza kulalamika na kusema
“Jamani mambo yanazidi kualibika shetani anazidi kutuingilia humu ndani, naona sasa huyu mtoto matatizo matupu”Baraka alisikia kelele za mamaye hivyo akanywea na kujiinaia chini.
“Hee! Baba mbona umefanya haja kubwa ndani kwa nini lakini?”
“Nimebanwa mama, Dada Tausi hayupo”alimjibu
“Hukuweza ata kupiga kelele?”Mama yake alimwuliza
“Naogopa majirani watasikia, wewe si umesema nisitoke nje?”
“Wewe mchafu sana!”Mama yake alibwataCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mama Ninakwambia unitoe nje hutaki kwanini mama?”Alimwoji mama yake
“Hutoki popote unataka nini nje wakati wewe hutembei”
“Nataka niende kwa kina Juma kucheza” Baraka alimwambia
“Hebu nitokee mie! Mchezo gani utaouweza kuucheza hapo na wewe miguu mibovu”mama yake alisema kwa ukali.Maneno hayo yalikuwa makali kama ncha ya kisu yalimkatisha tamaa Baraka, ilimfanya kunyamaza kimya na kijiinamia huku akiendelea kulia.
Mvua ilikuwa inanyesha,radi zinalika na hali ya hewa ilifanya kama giza hivi,Lakini hali hiyo haikumfanya na kumkera Mama Juma alitembea kwa mwendo wa kukazana kama vile alikuwa anafukuza kitu.Jambo alilokuwa nalo moyoni mwake lilikuwa kubwa mno lilimuuma na kumkereketa rohoni mwake.Ijapokuwa kutoka nyumbani kwake anapoishi hadi kufikia kwa Mama Baraka ni umbali uliochukua hatua kumi tu,lakini mama Juma siku hiyo aliona hafiki,alitamani akimbie alihisi kwa mwendo wa haraka haraka tu angechelewa kufika.Aliendelea na safari yake baada ya muda akafika na kubisha hodi.
“Hodi! Hodi! Wenyewe “Mama Juma alibisha hodi alipofika chini ya mlango wa Mama Baraka
“Karibu!”Mwasi alijibu kisha akafungua mlango na kumkaribisha ndani
“Vipi jirani naona umekasilika “Mama Juma aliuliza baada ya kumuona Mama Baraka amekunja sura yake,
“Mwenzangu malezi haya yashanifika shingoni”
“Kwa nini?”Mama Juma aliuliza
“Ungeona anavyochafua ndani! Wala usingeuliza,”Bi.Mwasi alisema.
Mama Juma alijifanya kama kushangaa hivi.akaweka mikono yake mdomoni, kisha akaishusha na kutamka.
“Lakini Mama Baraka yote hayo unayataka, Mwache mtoto akacheze na wenzake, unamfanya mtoto kama mnyama, kuwa na matatizo ya ulemavu si sababu ya kumfungia ndani”
“Mwenzangu mimi namhurumia sana mwanangu, Baraka ni mlemavu nimeamua kumfungia ndani asije kupata matatizo kama wenzake wanavyo uawa ,maana miguu yake tatizo anasimama kwa shida vipi na kucheza hataweza kweli.Si wenzake watamnyanyasa na kumuonea”Mama Baraka aliongea huku akiwa amefadhaika na maneno yake.
“Sikiliza Shoga yangu kaa utafakari sana hiyo huruma imepitiliza, unazidi kumuumiza mtoto kwanza anaweza kucheza na wenzake, kufanya kazi ndogondogo kama kuchota maji,kufua nguo zake mchangamshe mapema kwa vile bado mtoto”Mama Juma alimwambia
“Shoga tafadhali usinisimange, leo kwangu kesho kwako”Mama Baraka alisema
“Kwa nini unasema hivyo shoga?”
“Ndio!Mtoto Albino,alafu unaniambia atafanya hili,ooh!atafanya lile!atafanyaje wakati mtoto hata kusimama vizuri hawezi,bora uende tu usiniongezee majonzi bure.Kweli mtoto ni majaliwa ya mwenyezi mungu,lakini akiwa na kasolo ni mtihani”Bi.Mwasi alisema kwa kejeri.......
Mama Juma alipomuona Shoga yake amekwishahamaki, akainuka ili aende zake na kuepusha ugomvi.Wakati Mama Juma anaondoka aligeuka na kumwambia maneno ambayo ni nuru kwake, kwamba ni vizuri akayatafakari maneno aliyomwambia na kuyachukulia hatua ili mtoto wake Baraka awe huru.Baada ya mama Juma kuondoka tu, punde si punde Bwana Ahmed alirejea akiwa akitokea kazini huku mkononi akiwa ameshikilia kifuko kidogo cha Rambo.Alipofika nyumbani alimkuta mkewe anasafisha chumba cha Baraka. Mama Baraka alipomuona Mumewe alienda na kumpokea, kisha wakasalimiana na Bwana Ahmed akaanzisha mazungumzo na utani wa hapa na pale.
“Heee! Naona leo mke wangu umeamua kupiga deki au ndio siku ya Jumamosi ya usafi wa Magufuli”Ahmed alimchokoza mkeweCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hebu nipishe mie.Nionee huruma kwanza sababu ya mtoto wako”Bi.Mwasi alijibu
“Amefanya nini au amejikojolea tena”Bwana Ahmed alihamaki
“Afadhali angalikojo kuliko alivyofanya, kajisaidia aja kubwa kabisa ndani”
“Heee! Kwani alivyokuwa anajisikia aja hakumwita dada yake Tausi ampeleke msalani?
“Tausi alikuwa hayupo, nimemtuma kwa jirani, nami nilikuwa sokoni alibaki ndani pekee ndio akaamua kufanya mambo yake hapa.Yaani nimechoka ningekuwa na mtu wa kumpa ningalimpa”Bi.Mwasi alisema
Bwana Ahmed hakuongeza neno, akaamua kukaa kwenye kiti pale sebuleni na kuwasha radio yake akaendelea kuburudika.
*******
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment