Search This Blog

Sunday, July 10, 2022

KISASI NDANI YA NAFSI YANGU - 5

 







    Simulizi : Kisasi Ndani Ya Nafsi Yangu

    Sehemu Ya Tano (5)



    Siku ya tatu tangu nilipotoka kuishi maisha ya gerezani.Sikutaka kurudi tena kwenye nyumba ile, kurudi tena Sumbi kutanilea matatizo, nikaamua kwenda kutafuta mbele kwa mbele.Nikaongoza mpaka mbeya mjini. Macho nayafumba na kufumbua, kifua kinapanda na kushuka njaa imeniandama pasipo kitu tumboni. Nikaamua kuanza kujishughulisha ili nipate angalau mlo mmoja kwa siku.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikaanza kazi ya kukusanya takataka majumbani mwa watu kisha uenda kuzitupa kwenye majalala makubwa yaliyopo maeneo hayo, nilipitia kila nyumba asubuhi na mapema kuchua takataka hizo ili kujipatia angalau shilingi mia tano ili nipate cha kuingiza mfukoni. Niliendelea kuwa na hali duni, kuishi katika mazingira magumu ya mjini, nikipata chakula nakula nikikosa nalala.Ikiwa mwezi mmoja umepita tangu nitoke gerezani,huku nikiendelea kufanya shughuli zangu kuzoa taka na kuzibua vyoo, ikawa vigumu kuyazoea maisha ya uraiani, nilipigania hivyo hivyo nikiamini ipo siku mungu atayafuta machozi na kusahau kisasi ndani ya nafsi yangu.Siku moja nikiwa kwenye mizunguko ya kuokota chupa, ghafla nilisikia sauti kutoka kwa mtu akiita jina langu “Fred!” nilipogeuka nyuma sikuamini macho yangu, nilipomuona Shangazi Zuwena, Moyo wangu ukaanza kwenda kasi, nikaisi kupatwa na homa, muda huo huo tumbo likaanza kuniuma. Sasa alikuwa mtu mzima, na nywele nyeupe zikiwa zimemchomoza kichwani mwake. Alikuja mpaka pale nilipokuwa nimesimama, aliponisogelea karibu zaidi na kutabasamu.Nikaamua kuondoka, maana niliona nisije kumfanya kitu kibaya nikarudi tena gerezani.Shangazi alinishika begani na kunitaka nimsikilize kisha akaniambia,

    “Fred, mwanangu najua nimekukosea sana, naomba unisamehe, kisha unisikilize”Shangazi Zuwena aliniambia,

    “Nikusikilize nini?”Nilimjibu

    “Kwanza nakuomba unisamehe sana mwanangu”aliomba msamaha,

    “Nikusamehe kwa lipi shangazi?”nilimwuliza

    “Nilikutesa sana mwanangu, nikakufukuza nyumbani,tena nyumba yako ambayo uliachiwa urithi na wazazi wako”Shangazi alisema huku akiangua kilio,

    “Kwa hiyo,si umeamua mwenyewe kunifukuza?Nilimwuliza huku nikiwa na hasira

    “Punguza hasira Fred mwanangu, rudi nyumbani nikukabidhi nyumba yako”,

    “Hapana shangazi nenda kaendelee kuishi peke yako”nilimwambia,

    “Hapana nipo chini ya miguu yako, nisamehee mwanangu”Shangazi aliendelea kunibembeleza.

    Nilimuhurumia sana Shangazi Zuwena,huku nikifikiria hatima ya maisha yake,jinsi alivyokuwa.nilimsamehe shangazi bila pingamizi nikaomba na kumshukuru mungu kurejea tena nyumbani Busale kisha tukakumbatiana kwa pamoja.Nilikumbuka shida ninayoipata kuzulula mjini.Pale pale nikamwambia Shangazi” nipo tayari unipeleke nyumbani kwani hapa unaponiona sina pa kulala,siku zote nalala vichocholoni au kwenye magenge makubwa ya watu wa mnadani,nipo tu natangatanga mjini bila msaada wowote,nashukuru sana Shangazi kwa Kunisaidia...

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Niliongozana na shangazi mpaka kijijini Busale, tulitumia saa moja kufika nyumbani, nilishangaa sana kuona nyumba yetu imebadilishwa, ikawa nyumba ya kisasa, kulikuwa ni kuzuri kiliko nilivyokuacha. Shangazi Zuwena alikarabati nyumba na kujengea fensi huku vyumba vikiwa vimeongezeka badala ya vyumba vine sasa vimekuwa vyumba sita na sebule kubwa iliyosheheni thamani za kisasa kabisa.Shangazi alinikaribisha na kuingia ndani. Nilipoingia tu Sebuleni kulikuwa kumebadilika sana, nilifurahi kuona nyumba yetu ikiwa katika muonekano mzuri, shauku ikanishika kutaka kujua shangazi amepa wapi pesa mpaka kubadilisha nyumba kiasi kile.Baada ya kukaa, nikamwuliza Shangazi.

    “Shangazi pesa zote za kujengea nyumba hii umezipata wapi mpaka ukafanikisha nyumba hii kupendeza kiasi hiki?”

    “Fred Mwanangu si unakumbuka kazi zangu za ujasiliamali, maisha yangu nimeyabadilisha mwenyewe na pia naishi peke yangu katika nyumba hii tangu mlipoondoka wewe na Mjomba ako”, Shangazi alisema kisha akaendelea,

    “Kipi kile wakati Mjomba wako amefariki nimesikia taarifa zake, pia msibani nilikuja ila wewe sijakuona na pia pole kwa matatizo yaliyokukuta.Nimeumia sana moyoni mwangu juu yako, sasa kuanzia leo urithi wa mali hizi zote zitakuwa zako,hata kama nimegalamia kiasi gani kupendezesha hii nyumba mimi sijali, kwa sababu ni urithi toka kwa wazazi wako,nimefurahi sana kukuona Mwanangu.Kuna kipindi nilikuwa nakuja gerezani kukuona lakini ilishindikana sababu waliniambia ulijiandikisha hukuwa na ndugu.



    Ila nilipata taarifa muda wa kifungo chako kilikuwa karibuni kumalizika hivyo kila siku nikawa nahesabu siku,miezi hatimaye mwaka na nusu sasa.Moja kwa moja nikajua utakuwa umeshatoka gerezani, hivyo nikaanza harakati za kukutafuta kila kijiji hatimaye nikakutana na mtu alinipambia amekuona maeneo ya Kyela Mjini,ndio nikaamua kuzunguka maeneo hayo na kukuona.Nilikutafuta sana mwanangu bila mafanikio hatimaye mungu ni mwema siku zote nikakutana nawe kyela.Nilimsukuru kwa mara nyingine tena kwa kubadilika kitabia,nikamtana shangazi anisimulie jinsi ilivyotokea naye pila hiyana akaanza kunisimuliza jinsi gani hapo kabla alivyomfanyia Anko Mashaka visa vya kusikitisha,alinisimulia kila kitu mwanzo mpaka mwisho ,ukitaka kujua alivyonisimulia shangazi ni kwamba.

    *******

    “Nataka uniambie shida yako”

    “Nataka huyu mtu usimuue ila ninachoitajiapatwe na ugonjwa wowote ule”

    “Sawa je hupo tayari kumuona akiumwa ugonjwa huo?”

    “Ndio Mtaalamu Nipo tayari, ninachoitaji asinijue kabisa ikiwezekana muweke ndondocha

    “Aisee! Ugonjwa unaoutaka unaweza kutekelezeka ndani ya siku moja tu”Yule mganga alisema

    “Sawa Mtaalamu nakungoja wewe nataka hawe ndondocha kabisa hasiyeweza kufanya kitu chochote,

    “Hapa umefika mama, sema kila kitu lakini sio kwa mambo yetu ni kiboko yake”Mganga alijinadi

    “Nashukuru mtaalamu

    “Haya niambie huyu jamaa jina lake nani......nani yako? Mtaalamu huyo alisema

    “Anaitwa Mashaka ni mume wangu”

    “Mmmh! Mumeo?”Mganga aliuliza

    “Tumegombana siku nyingi sana na ndio maana sina mahusiano nae naona ananijazia mzigo”

    “Sawa basi usiwe na shaka kazi yako itafanyika sasa hivi weka shilingi.elfu themanini ndani ya kikapu hicho”AliwekaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa nakupa dawa hii uifiche vizuri inatakiwa usiingie upepo hata kidogo, matumizi yake ni kwamba unapokuwa unampelekea chai au uji unachota kidogo unakuloga na kuchanganya pamoja na uji huo unampa anakunywa”

    “Akishakunywa inakuwaje?”

    “Yaani utaona matokeo yake akishakunywa anachanganyikiwa anabadilika na kuwa ulivyotaka”

    “Sawa Babu Mtaalamu nashukuru”

    “Shaka ondoa ukiona bado yupo vizuri basi njoo nikubadilishie dawa nyingine lakini naamini hii itamfaa maana ni kiboko ya mazezeta”

    “Naam, mtaalam ahsante sana”

    Ilikuwa ndio siku niliyoenda kwa mganga wa kienyeji huko kijijini cha Butogwa nilikuwa na shauku ya kutaka kukudhurumu mari zako Mwanagu ila yote hayo yalitokana na umaskini niliokuwa nao.Nilivyopewa hiyo dawa nilirejea nyumbani moja kwa moja na kuificha ndani,nilikuwa na mawazo sana juu ya kumpa Mume wangu Mashaka dawa hiyo.Kuna kipindi upande mwingine wa mawazo yangu yaliniambia kitendo ninachokifanya kilikuwa cha kinyama kabisa lakini sikuisikiliza sauti hiyo bali nilifuata vile mawazo yangu yaliyokuwa yakiniambia lazima nifanye haraka iwezekanavyo kuhakikisha siku hiyo hiyo usiku nichanganye na kumpa dawa hiyo anywe .



    Hakika ilikuwa ni mtihani mkubwa sana pale nilipokuwa nikimtaka Bwana Mashaka anywe uji wenye dawa hiyo.Mashaka alikuwa mgumu wala hakukubali hata kidogo kupokea kikombe hicho chenye uji na mchanganyiko wa dawa hiyo yenye unga unga mweusi kama masizi ya mkaa.Sijui kama alijua uji huo ulikuwa na madhara kwake ukweli ulikuwa hivyo kama mtu yoyote angejalibu kuunywa uji huo basi angeambulia kuumwa ugongwa wa ajabu ajabu.

    Wakati nikiwa nimeshikilia kikombe chenye uji huo nilimsogelea karibu yake na kuanza kunywesha kwa lazima lakini Mashaka alikuwa na nguvu sana kunizuia mkono wangu kukipeleka kikombe mdomoni mwake.Nilipoona inashindikana nikajidai kukitoa nje kikombe hicho ukweli ilikuwa nimekenda kukiweka kwenye kabati nikasubilia alale kwanza ndio nijue namna ya kuupitisha kooni mwake uji huo japo lipite funda moja tu mdomoni lingetosha kabisa kumaliza kazi yangu...



    Nikajifanya kulala kitandani naye akajizoa zoa pale kitini kisha akajilaza kitandani,punde akapitiwa na usingizi mzito,nilimuacha alale vizuri kwanza na usingizi kumkolea ndipo nianze kazi nilipohakikisha hayupo kabisa kwenye dunia hii nilitoka kitandani na kufuata kikombe chenye uji huo kisha nikaanza kunyata taratibu kufuata kitanda,nilipokifikia nikakiweka kikombe chini ya kitanda kisha nikaanza kumgeuza ili aweze kulala chali.Ilishindikana kila nilipokuwa nikimlaza alikuwa akijigeuza geuza baada ya kujitaidi sana kumuweka vizuri hatimaye alilala chali nami bila kupoteza muda nikainama uvunguni na kuchukua kikombe hicho na kunywesha funda la kwanza,la pili nikamuona akijitingisha na kujigeza pale kitandani.Nikaona nisilazimishe sana bora tu nisubilie hata kesho nitamalizia kikombe hicho maana pia nikaona inatosha.Nikawaza Mtaalamu mwenye aliniambia kidogo tu umpumbaza ila utakapomalizia ndio kabisa uwendawazimu unamkuta na kumvaa kihalali nikaona nimuache nimalizie kazi hiyo kesho yake.

    Niliamka asubuhi na mapema ninyi mkiwa bado mmelala, nikaona sasa muda huu ndio mwafaka kumalizia kazi yangu niliyopewa na mganga huyo.Moyo wangu ulikuwa katili sana kila nilipomuangalia Mashaka ikiwa amelala kitandani nilizidi kumchukia, nikajiapia lazima nifanye kitu ili siku hiyo.Nikatoka kitandani ghafla na kukimbilia jikoni, nikachukua chupa na kumimina uji kwenye kikombe kisha nikaifuata dawa na kurejea ndani huku nikitembea mwendo wa kinyonga mpaka chumbani.Nilimkuta Mashaka ameamka na kukaa kitandani,nilichofanya kwa wakati huo kuichanganya dawa katika kikombe kilichokuwa na uji kisha nikamfuata na kumtaka anywe. Lakini alionekana kama hakunisikia muda wote alikuwa ameduwaa na kuzubaa, nilistuka Ghafla kumuona akiwa katika hali hiyo hapohapo mawazo yakanijia kumbe jana nilimpa kidogo ndio maana leo amebadilika, hama kweli dawa hiyo ilikuwa kiboko yake kama alivyosema Mtaalam kule Ndaga. Nilipokuwa namchunguza nilimuona kama ajielewi elewi hapo nikapata wazo nimnyweshe tu uji huo, punde nikafanya hivyo nikahakikisha anakunywa penda si kupenda.



    Nilimnywesha kwa lazima maana alikuwa mgumu kweli kufungua mdomo wake,nilimshika kwa nguvu zangu zote kuahakikisha anamaliza kikombe chote kwa hilo nilifanikiwa kwa asilimia mia moja alikunywa penda si kupenda ikawa vuta nikuvute lakini sikumuachia mpaka alipomaliza na kuhakikisha sasa dawa imeshachanganya nikamuhacha akiwa anagalagala chini nikatoka ili kuwai kuificha dawa hiyo.Wakati nilipokuwa natoka asubuhi hiyo ndipo nilipokutana mlangoni ukiwa umekaa chini ya mlango huo,nikajua moja kwa moja kwamba lazima utakuwa umesikia kila kitu tulivyokuwa tunabuluzana ili nikamilishe kazi yangu kiukweli nilifanikisha hilo.

    Nakuomba msamaha wako mwanangu nakili kweli nimekosa sana tena sana,ila msamaha wako ndio tiba yangu Fred Mwanangu.Aliongea shangazi japo moyoni nilikuwa na dukuduku la kisasi ndani ya nafsi yangu nikaona nimsamehe tu kwa vile amekili makosa yake basi nikamwachia mungu. Shangazi hakuishia hapo alizidi kuniambia na kunifanya niwe mtu mwenye mawazo sana kuhusiana na simulizi hiyo aliniacha mdomo wazi macho nimemkodolea kodoo kwa mshangao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku zilivyozidi kwenda ndivyo nilivyokuwa nabadilika kitabia nilijiona kabisa kama nimebadilika na kuwa mtu mwenye roho mbaya mno,hata majirani pia waliniona muda wote kuwa mwenye kisilani nisiyekuwa na muda wa kucheka na mtu.Hata pale nilipokuwa nakupiga na kukunyanyasa haikuwa kawaida yangu,na wala sikujua kama nimefanyiwa kitu na yule mganga alikuwa amenifanyia madawa yake sasa akanifanya nisahau fadhira na kuendelea kufanya maovo ndani ya familia yangu.Baada ya kuwafukuza nilikaa nyumbani peke yangu kuna muda akili inanirudia na kujilaumu kwa nini nimetenda kitendo furani,bora tu nisingefanya na nikapata baraka lakini kuna muda mawazo ya ajabu yananiingia akilini mwangu na kuniambia kitendo nilichokifanya hakikuwa kizuri kutokana na madhala kadha wa kadha.Nikaja kugundua baadae kabisa alipokuja Kaka yangu kutoka nyumbani Kyela anayeitwa Abdul,mgeni huyo alikuja baada ya kusikia taarifa zangu kwamba nimewafukuza ninyi nyumbani na taarifa nyingi zilienea sikuwa na maelewana mazuri na majirani zangu.Kaka yangu ikabidi afike nyumbani kunionya lakini alipofika pale cha kushangaza alishtuka kunikuta katika hali kama aliyonikuta nayo mtu yoyote yule angekuwa mbele yangu angeshindwa kujua kama nilikuwa Zuwena yule uliyekuwa unamjua wewe kipindi kilichopita.Kiukweli muonekano wangu ulikuwa kama ugonjwa na muda wowote ningeweza kulala kitandani na kuhitaji msaada,nilikuwa nimekonda na kukondeana japokuwa sikuwa mgonjwa kama alivyodhani.Mwili wangu ulikuwa nimekondeana sana unene wote niliokuwa nao umeteketea hata shepu niliyokuwa nimejaaliwa sasa ilipotea kabisa na kubaki kimbaumbau.

    Abdul alikuwa kijana mdogo sana ni wa pili kuzaliwa katika familia yetu kutoka kaka yangu mkubwa anayefuatiwa ndio yeye,siku aliyokuja na kunikuta katika hali hiyo hakulidhika alitaka kujua kisa na mkasa.Aliniuliza kama nilijiisi kuumwa lakini nilimjibu sikuwa mgonjwa nilijiona nipo kawaida japokuwa nilikuwa kweli nimekwisha.Aliniuliza kwa nini sikuwa na maelewano mazuri na majirani,sikumjibu badala yake nilimwangalia tu bila kupepesa.

    Abdul alipata mashaka juu ya hali aliyonikuta nayo,moja kwa moja akajua kwamba nilikuwa na tatizo tena kubwa linalohitaji kutatuliwa,akawaza zaidi alipofikilia kwamba na majirani hatuna mahusiano mazuri akajua ya kwamba kati ya hao majirani zangu kuna mmoja wapo alikuwa mbaya wangu,ndiye aliyesababisha na ikiwezekana kunifanyia kitendo cha kishirikina ili kunikomoa kutokana na dharau nilizokuwa nazo.Abduli akawaza na kuwazua mwisho alinitaka nijiandae ili tutoke sehemu tukaongee,kiukweli sikumuelewa maana kama kuongea nyumbani palitosha maana tulikuwa mimi nay eye kama ana maongezi ambayo hakuhitaji mtu kusikiliza basi nyumbani pangefaa pia lakini Kaka hakusikiliza aliitaji nijiandae tutoke.Nilijiuliza sana anataka tutoke twende wapi? Saa sita yoye hii si tuzungumze tu hapa hapa, nilijiuliza yote hayo bila kupata jibu mwishowe nikaamua kukubali tu niende kumsikiliza, anapotaka tukaongelee nitajua huku huko, nikainuka na kuelekea chumbani kujiandaa.......





    Tulitoka na kuelekea barabarani mbele kidogo kabla hatujafika kituoni ilikuja pikipika na kupaki jirani yetu , kaka akanitaka nipande ili tuwai nami bila kinyongo nikajipakina na kaka nae akajipakia safari ya kuelekea huko anapopajua yeye ilianza mara moja.Baada ya mwendo mrefu kidogo ikiwa mwenye pikipiki na Kaka wakielekezana naomna ya kufika eneo ilo bila kusumbuana.Baada ya nusu saa tulifika mbele ya barabara kuu inayokwenda kyela na Ipinda ,Dereva akakata njia inayokwenda kanisa la T.A.G.Mbele kidogo tulikuta kibao chenye mshale kilichoandikwa Tanzania Assemblies of God Sumbi.Tukasimamia mbele ya kanisa moja kubwa juu ya kanisa ilo kulikuwa na msalaba mkubwa uliochongwa vizuri,kaka alimlipa mwenye boda boda kisha tukapanda ngazi na kuelekea ulipo mlango wa kuingilia kanisani na kuingia ndani,ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kufika na kuindia ndani ya ukumbi huo wa kanisa.Sikushangaza wala sikuteteleka kabisa kuuliza kwa nini kaka alinileta hapo,tulichofanya kwa wakati huo tulivyowaona waumini hao wakiwemo wengi wao walituangalia pia kuna wale waliokuwa wakinong’onezana kisa sisi kuingia ndani.Mchungaji Elias alipotuona alitukaribisha nasi tukaitikia na kukaa katika vitu vilivyokuwa wazi.Kumbe kaka alifahamiana vizuri na mchungaji huyo aliniambia kwamba waliomaga pamoja shule ya sekondari ,kwa hiyo kwenda pale kulikuwa na ahadi waliyopatana.Nilimuona mchungaji akija haraka nilipokuwa nimekaa na kuanza kunishika kichwa changu na kuniomba,nilimsikia mchungaji huyo akiongea maneno nisiyokuwa nikiyaelewa maana aliongea haraka haraka mpaka nikawa najihisi kizunguzungu na kuanguka chini kama mzigo sikujua tena kilichokuwa kinaendelea kwa wakati huo.Kaka alikuja kunisaidia nilikuja kustuka baadae pale nikiwa nimekaa kitandani,nilipoangalia vizuri kumbukumbu zikanirudia nilipomuona Kaka Abdul akiwa amenikalia pembea yangu,akili zikanirudia nikakumbuaka kilichotokea na kumshukuru mungu maana yeye ndiye muweza wa yote.Baada ya kukaa sawa mchungaji alinitaka niwasimulie ilivyokuwa,nikawaeleza kilichotokea nivyokuwa nimekwenda kwa mganga na kupata dawa kumpa Mashaka ili nimpumbaze kisha kumuweka msukule,alichoniambia mchungaji ni kwamba mganga yule baada ya kunipa dawa hiyo atakuwa amenifanyia kitu na mimi ikiwezekana alitaka kuniua kabisa kutokana na Waganga wengi kuwa na mizimu mingi anaweza kukugawia hata mmoja akakutesa na kukukondesha ndio itakuwa wewe sasa umefanyiwa hivyo.

    “Kwanza unajisikiaje?”Mchungaji aliniambia

    “Najisukia nafuu tu nashukuru sana”nilimjubuCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hashukuriwe bwana wetu yesu kristo”Alisema mchungaji

    “Amina!

    “Pole sana kwa matatizo yaliyo kukuta”mchungaji aliongeza

    “Ahsante mchungaji, nimeamini kweli yupo mungu msemaji wa mwisho”

    “Hakika, unachotakiwa sasa kumfuata Bwana yesu kristo aliye hai”

    “Sawa mchungaji, nitakuwa pamoja nanyi”

    “Amina karibu sana tumsifu bwana”

    ”Amina”

    Baada ya maongezi hayo nilimshukuru sana kaka nilijiona mwili wangu ukiwa mwepesi sasa,maana nilijiona kama umebeba mzigo mzito sasa nilikuwa nimeshautua na kuuweka chini.Mchungaji alinisihi niwe naudhulia bila kukosa vipindi vyote kanisani ,alinitaka nibadilike ili niwe mwana wa mungu nipokelewe na nisamehewe makosa yangu yote niliyoyatenda,hapo nilifaulu vema na mpaka sasa nimeokoka na kuwa mkiristo kwa jina la Zabibu ninasali katika kanisa la mchungaji Elias vipindi vyote na ratiba zote za kanisani hazinikosi sasa nimeokoka kabisa nimekuwa namuhamini mwana wa Mungu Yesu Kristo aliye hai.Ninamshukuru yeye kwa kuweza kutukutanisha mimi na wewe mwanangu nisamehe yote niliyokosea.

    *******

    Wakati shangazi Zuwena anaonge maneno hayo,nilikuwa mbali kimawazo, nililia sana,kama Anko Mashaka angelikuwa hai tungekuwa wote nyumbani sasa,nilimkumbuka sana Musa na Asha ila sikuwa na jinsi Maana imeshatokea,nikainua mikono yangu juu na kumshukuru mungu. Nilishusha pumzi ndefu kisha nikafuta machozi kwa shati langu kuukuu na kuanza kumuadithia shangazi kila kitu kilichonitokea katika maisha yangu, tangu alipotufukuza nyumbani na Anko Mashaka, mpaka Asha livyomuua Anko kisha nami kumua Musa na dadaye Asha hatimaye nikafungwa jela .Shangazi alisikitika sana kwa mara ya kwanza nikayaona machozi ya shangazi yakichuluzika mashavuni mwake nikamsihi kunyamaza maana

    yameshapita nae akatulia.Nikamuona shangazi akinipigia magoti miguuni mwangu na kuniomba naitaji msamaha kwa mara nyingine tena,”Nisamehe sana Fred,najua Mimi ndio chanzo cha yote,nimekatisha masomo yako na kusababisha kupelekea wewe kufanya mauaji,nimejiona mkosefu mbele ya mungu,najua mungu ataniukumu mimi na sio wewe Fred.Tafadhali naitaji msamaha wako kwani ndio kinga yangu mbele ya mungu.”Shangazi alisema huku akiendelea kulia.Nilimshika mkono shangazi na kumnyanyua, kisha tukakumbatiana kwa huzuni tele.Nikamwambia “Wewe ni shangazi yangu na ndio ndugu pekee katika maisha yangu, umenisaidia sana nikiwa mdogo mpaka sasa umenitafuta na kukili makosa yako, nami sina budi kukusamehe Shangazi yangu.Yote yaliyopita tumwachie Mungu kwani ndio msemaji wa mwisho, nakupenda sana shangazi yangu.”Nilipomaliza kusema maneno hayo, shangazi alifurahi Sana kisha wote Kwa pamoja tulikumbatiana tena Kwa furaha.......





    Siku iliyofuata nilishida ndani,nikifikiria safari ya maisha yangu niliyotokea mpaka hapa nilipo,sina budi kumshukuru mungu,nikiwa mtu mwenye mawazo shangazi aliingia ndani na kunipa habari ambazo zilinishandaza japo upande mwingine ulinifurahisha.alichoniambia shangazi ni kwamba ni “wiki ijayo kutakuwa na sherehe hapa nyumbani,sherehe hiyo kwa ajiri yako ya kukupa pole na pongezi ,kutokana na umri wako kuwa mdogo lakini changamoto ulizopitia ni kubwa sana.hapo hapo tunaonganisha sherehe hiyo pamoja na siku yako ya kuzaliwa,hivyo basi jiandae mwanangu kwa ajiri ya shughuli hiyo,kuwa na amani ndani ya moyo wako”.nilimkubalia shangazi huku machozi yakinilengalenga kwa furaha

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sherehe ilianza siku mbili kabla ya siku ambayo ningefikisha umri wa miaka Arobaini na tano.Vifijo na ndelemo zilitanda kwenye kijiji cha Busale,wakati wote huo nilikuwa ndani chumbani nikingojea siku yangu ya kufikisha miaka thelathini na tano ifike nitoke nje.Shangazi alikuwa na shauku ya kunitoa na kunipongeaza mapema.shangazi hakuona sababu ya kungojea kesho yake ifike.Siku ya sherehe ilipofika Shangazi akanitaka nitoke nje ili nijumuike na wageni waalikwa.nilitoka nje vifijo na vigelegele vilitawala, kwa shangwe na ndelemo huku machozi yakinitoka.Siku hiyo shangazi alinunua ng’ombe mzima,watu walikula,kunywa mpaka wakasanza.Nilifurahi sana kumuona shangazi akiwa na upendo juu yangu. Nikaanza kucheza na na wageni mbalimbali.

    Siku hiyo nilikuwa nimependaza ,wasichana walinisifia kila mmoja wao alitaka kukaa karibu yangu.Muda ulipofika wa kucheza,nilitoka na kujumuika na wageni waalikwa.vifijo viliongezeka,kadri muda ulivyozidi kwenda ndio mori ya kucheza ilivyoongezaka.



    vigelegele vikaongezeka na sauti za wasichana zikawakauka kwa kushangilia.wakati huo macho yangu yalitua na kuganda kwa Msichana mmoja mrembo sana.Alikuwa mweupe,mrefu,mwenye tabasamu pana,aliyevalia gauni ya kitenge.nilivutiwa nae sana,nikamwangalia kwa muda mrefu sana bila kupepesa macho.Nilivyokutana nae karibu nikajifanya kuangalia pembeni.

    Baada ya muda wa shughuli kuisha,nilikuwa na wakati mgumu kumfuata Yule msichana.wakati wageni wakiaga na kuondoka nilijifanya kutembea tembea ili kumzugia Yule msichana.Mara tulipishana na ule dada akageuza shingo yake,tukakutanana uso kwa uso.Alikuwa na tabasamu pana sana.tulijikuta sote tukasimama.“Si vibaya tukisalimiana” Yule msichana aliniambi akitabasamu.Sikuwai kupata mshtuko wa moyo kama wakati huo.nikaisi kupigwa shoti ya umeme baada ya kusikia sauti tabu ya Yule mdada.sikumbuki kama nilimjibu au nimemjibu ila nami niliendelea kutabasamu.

    “Habari yako?”Yule mdada akanisalimia

    “Safi, mzima wewe?”Nikaitika tukapeana mikono

    “Mimi naitwa Rosemary, sijui mwenzangu?”

    “Fred.”anikamwambia

    “Unaishi hapa si ndio?”

    “Ndio, sijui wewe unaishi wapi? Nilimwuliza

    “Naishi Kyela mjini”

    “Asante nimefurahi kukutana na wewe”

    “Hata Mimi pia, ingawa nataka kukuambia jambo litalokushangaza”

    “Niambie ndugu, nakusikiliza”

    “Katika maisha yangu naitaji kuwa na mke.nimekuona wewe nadhani itakuwa sahihi kwa mahamuzi yangu kukuoa wewe!”

    “Kwa nini?”Aliuniuliza

    “Utaratibu tu, moyo wangu umekuchangua wewe uwe mke na mama wa familia yangu”

    “Kwahiyo ina maana unataka kunioa?”Aliniuliza

    “Ndio Rosemary, niamini! Nilimwambia kwa msisitizo



    Tuliongea mambo mengi mwisho tukaafikiana na Rose akakubali ombi langu,tuakaaga na kisha akaondoka.Ukweli nilimpenda sana Rose,mwendo wake pekee ulinichanganya sana.Ndoto zangu za kuoa zimekamilika kwa msichana Rose ilitosha kabisa kuutesa moyo wangu.Rose hakuwa na tatizo kwenye suala ilo, alikuwa tayari kuwa kuanza maisha na kuwa mke wangu.Wakati anaondoka akanikabithi namba zake za simu ili nimpigie tuwasiliane na kujadili ndoa vizuri.Nilibaki na mzigo wa mawazo mengi ,niliwaza sana kuhusu Rose.kwa kiasi kikubwa kabisa bila ya kuwa na wasiwasi nilikuwa na uhakika na hisia zake kwangu,Rose angekuwa mwanamke wa maisha yangu yote.Wakati nikiwa kwenye mawazo,Shangazi alikuja na kukaa karibu yangu,akiniuliza ninachowaza nami sikuwa na jinsi nikaamua kumueleza ukweli.Shangazi alicheka sana nilipomwambia kuhusu kumpenda kwangu Rose kisha akanitaka nisiwe na shaka,anaijuia vizuri familia yake.nilifurahi sana kusikia Shangazi anaijua familia yake kisha nikwambia shanga “Nampenda sana Yule binti,naitaji awe mke wa maisha yangu”shangazi aliniambia yeye atalishughulikia ilo swala,atahakikisha kila kitu kinakwenda sawa mpaka nimuoe Rose....



    Usiku ulipofika nikiwa zangu kitandani,kichwa changu kikiwa juu yam to,miguu nimeinyoosha kitandani,macho yangu yaki darini.Mawazo yakanijia kumtafuta Rose,nikachukua simu yangu na kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Rose.Katika ujumbe wangu nilimtaka kesho yake aje nyumbani alikubali.Siku iliyofuata alifika nyumbani bila kukosa,nilifurahi sana kumuona Rose.Tuliongea mambo mengi sana,tukapanga na kupangua kuhusu mustakabali wa maisha yetu,hakika Rose alikuwa mwepesi sana kuelewa,nilimueleza kila kitu kuhusu maisha yangu,alisikitika sana kisha akanipa pole na kunitaka niwe na amani,ya nyuma yamepita ningange yajayo.Ilipoitimu saa kumi jioni Rose aliaga nyumbani kisha akaondoka.

    ******* CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya miezi miwili Mzee Ramso na Bwana Peter walikuwa nyumbani,hawa ndio wazee aliowatuma Shangazi kwa Mzee Gonza kupeleka Barua.Bwana Peter ndio alikuwa mshenga,Mzee Ramso msindikizaji tu.Siku hiyo sura zao zilionyesha furaha tele ikionyesha kwamba walichokifuatilia kwa Mzee Gonza kilikuwa wamefanikiwa kwa majibu yakulidhisha.

    “Haya niambieni wazee wangu, vipi mtoto amekubaliwa au amekataliwa? Shangazi aliwauliza, baada ya kukaa

    “Kijana amekubaliwa, Mama Shaka ondoa”Mzee Ramso alisema

    “Daaah! Mungu mkubwa hatimaye Napata mke sasa”nilidaki huku nikinyoosha mikono yangu

    “Hongera mwanangu,ila inabidi ujipange kidogo,maana usije fanya masihara Fred”Shangazi alisema

    “Nimekuelewa Shangazi nitafanya hivyo, maana Nina shauku ya kuwa na Rose”nilimwambia shangazi huku nikicheka cheka kwa aibu,

    “Vipi mwanangu, lakini malengo yako yapo vizuri maana vijana wa siku hizi wakiona sikumbili tatu wanaacha”Bwana Peter alisema,

    “Yes! Nimejipanga kila kitu Mzee wangu nipo tayari kumchukua mke ata kesho”nilisema kwa pamoja tukaangua kicheko.



    Baada ya siku mbili kupita taarifa zilifikishwa kwa Mzee Gonza,mahali ikatolewa na taratibu nyingine zikaendelea.Shangazi hakuwa na muda wa kupotea akachapisha kadi chapu chapu kisha jamaa na marafiki wakaalikwa.Alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha anaungana na Majirani katika tukio ilo muhimu katika maisha yangu kufunga ndoa na Rose.Nilifurahi sana maana nilimuoa mwanamke wa maisha yangu nimpendae.Baada ya wiki moja tukafunga ndoa katika kanisa la mbeya luthelin charch,siku hiyo watu walikuwa wengi kanisani kuliko siku zote za ibada.Mabibi na Mabwana walifurika kutoa pongezi kwa kujana wao mpenda,Muda mwingi Shangazi alikuwa mwenye furaha tele.Muda wa kutoa zawadi ulipowadia Shangazi alinizawadia funguo za geti,watu walishangaa sana wakaanza kucheka nilimuona shangazi akichukua mic na kuongea “Mabibi na Mabwana najua nimewashangazi kumpa kijana wangu Fuguo ya geti.niwaambie kwamba funguo nilizompa za fremu ya biashara,nimemjengea fred nyumba yenye fremu tano,yeye ataamua kama atapangisha au kuzifungulia biashara yeye mwenyewe,namalizia kumwambia mwanangu nampenda sana Fred”Shangazi alimaliza,zikasikika ndelemo na vifijo.Baada ya kufunga ndoa na Rose,tulikwenda moja kwa moja nyumbani kulipokuwa na tafrija fupi ya kutupongeza kwa hatua hiyo niliyofikia.



    Harufu ya manukato katika chumba hicho, kilichokuwa na mwanga wa taa langi ya blue hafifu.kilikuwa chumba cha maharusi kilichotengenezwa na kupamba marashi ya unguja.Chumba hicho kilichokuwa na urembo wa urimbo kilivutia sana na kuwa burudani ya aina yake.Nilikuwa nimelala kitandani na Mke wangu kipenzi Rosemary katika chumba hicho kilichotayarishwa na Shangazi.tukiwa tumepumzika nikaanzisha maongezi,

    “Nimefurahi sana,Rose kuwa na wewe katika siku hii muhimu kwetu”

    “Hata mimi pia nimefurahi sana Fred kuwa na wewe”Rose alisema

    “Nadhani napaswa kukueleza jambo moja katika siku hii ya leo”

    “Niambie mpenzi nakusikiliza”

    “Moyo wangu umekufa na kuoza juu yako, nimekuchagua wewe uwe malkia wangu Rose”Nilimwambia

    “Asante Mume wangu kipenzi”

    “Naitaji tuzae watoto tuwe na familia yetu”nilimwambia Rose kwa msisitizo.

    “Usijali Mume wangu kipenzi”alijibu

    “Nakupenda Sana Mke wangu “nilimwambie huku nikimtazama machoni

    “Nakupenda pia Mume”

    “Mwaa!”

    “Mwaa!”

    Baada ya kumaliza harusi kwa amani na upendo,tukaendeelea kuishi maisha ya furaha nikiwa nyumbani na Shangazi.Mke wangu alikuwa kipenzi cha kila mtu,alikuwa mcheshi na mchangamfua wa kila alie mbele yake.Hakika nilimshukuru mungu kupata mke aliye mwema kwa kila jambo.Ilipofikia miaka miwili ndani ya ndoa,Mke wangu Bi.Rose alipata ujauzito wa kwanza.ilipofika miezi tisa alijifungua mtoto wa kike,tulifurahi sana hasa shangazi akaomba mtoto tumuita kwa jina lake Zuwena .mpaka sasa mtoto wangu wa kwanza anaitwa Zuwena anayesoma dalasa la saba katika shule ya msingi Tumaini.Baaya ya miaka miwili ulipata mtoto wa pili,akiwa wa kiume tukamuita Frankie.kwa sasa ana umri wa miaka saba akiwa darasa la kwanza katika shule anayosoma dadayake.Mimi na Mke wangu Rose tumefanikiwa kufungua miladi mbalimbali kuhusiana na kilimo cha matikiti maji.Katika Maisha yangu napenda sana amani lakini mpaka hivi sasa nikikumbua historia ya Maisha yangu nilikotokea machozi unitoka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Huo ndio ukawa mwisho wa maisha ya mateso kwangu na kilio kilikuwa kawaida kwangu ila sasa furaha imechukua nafasi yake.Kwanza napenda kushukuru Shangazi yangu kipenzi Bi.Zuwena amenisaidia mambo menngi sana bila kumsahau Mke wangu kipenzi Bi.Rosemary kwa upendo aliokuwa nao juu yangu japo alinitenda mabaya ila sina budi kumshukuru mungu pia Nawakumbuka rafiki zangu wapendwa waliotangulia mbele za haki, Musa na Dadaye Asha nimejifunza vitu vingi sana kupitia kwao,kisasi ndani ya nafsi yangu.Namalizaa kusema nawapenda sana watu wote waliotoa michango yao katika harakati za maisha yangu.



    TAMATI.



0 comments:

Post a Comment

Blog